bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,095
A PLACE WITH NO NAME.
(Sehemu isiyo na Jina)
SEHEMU YA (1)
Mtunzi........hemed mayugu
UTANGULIZI.
Ni Hadithi nzuri iliyoandikwa na Jumanne katika
kitabu chake alichokitoa mwishoni mwa mwaka wa
elfu mbili na kumi na Moja, ni hadithi ambayo watu
wengi waliipenda, hasa vijana wengi wa Tanzania na
hata watu kutoka inchi za Jirani kama Kenya na
Uganda. Vijana wengi waliyoisoma hadithi hii wengi
wao walitokwa na machozi pia wengine wakifurahi
kutokana na visa vilivyo mkuta Jumanne. Kutokana
na matukio kuwa mazito mengine ya ajabu watu
wengi walithubutu kumtafuta Jumanne kupitia simu
na wengine wakituma ujumbe kwa barua pepe
ilimradi tu wapate uhakika juu ya alichokuwa
amekiandika. Wengi walikuwa hawaamini kama ni
kweli alifika eneo hilo, alikutana na visa alivyokuwa
ameviandika kwenye kitabu chake cha A place with
no name, Eneo hilo lipo? Majawabu yake yalikuwa
ya kweli kwani hata ndugu zake walithibitisha hilo
pale walipojumuika naye kwenye vyombo vya habari
ili kuwambia watu kuusu sehemu ambayo aliishi
miezi kadhaa kisha akatokako kwa msaada wa Mtu
wa uko aliko Kuwa. Nyuma ya hilo Jumanne alikuwa
na Siri nzito ambayo hakupaswa kabisa kuisema
kwa Mwanadamu yeyote ambaye anaishi katika
ulimwengu huu baada ya kufanikiwa kutoka katika
sehemu isiyo na jina. Jumanne alionywa na mtu
aliyemsaidia kutoka katika ulimwengu wa ajabu,
ulimwengu ambao alikuwa aamini kama upo katika
uso wa Dunia. Kutokana na kukeleketwa na siri
ambayo hakupaswa kuisema kwa mtu yeyote
Jumanne alishindwa kuvumilia akajikuta anaisema
Siri hiyo nzito. Je nini kilimkuta Jumanne baada ya
kuisema siri ambayo hakupaswa kabisa kukifumbua
kinywa chake kwa ajili ya kuitoa siri hiyo, na ni Siri
gani hiyo, na aliyemwambia asiitoe siri hiyo ni nani,
je viumbe waliyokutana naye walikuwa wa aina gani.
Soma hadithi ya maisha ya Jumanne mwenyewe
akielezea ukweli wa maisha yake katika kitabu
chake cha A place with no Name, kisha Mimi
nitakuendelezea ni nini ambacho kilimkuta Jumanne
baada ya kuitoa siri nzito ambayo alikatazwa asiitoe
kutoka kwa ndugu zake. Hadithi yake inaanza hivi.
""Kwa jina naitwa JUMANNE A. MWAKYOMA Ni
mzaliwa wa mkoa mpya wa RUNGWE. Kwa
wasiojua rungwe ilikuwa wilaya ya mkoa wa mbeya
na ndio ilikuwa makao makuu ya wilaya. Lakini Kwa
sasa ni Mkoa mpya katika mikoa 30 ya Tanzania
pia mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu cha Mbeya
university of science mwaka wa tatu. Hii ni simulizi
inayo nihusu. Isome na ukimaliza kusoma uwache
comment pia share na like page yetu. Ku-like page
bofya Link/maandishi ya bluu hapo Chini.
Nakumbuka ilikuwa tarehe 6/8/2012. Ni siku
ambayo kamwe sitoisahau,
Ilikuwa ni siku ambayo niliaga nyumbani kwenda
kutarii kwenye vivutio vya mkoa wetu wa rungwe.
kama mnavyojua mkowa wetu unavivutio vingi vingi
na vya maajabu yake kama mlima Rungwe, bwawa
la mungu, na ziwa ngozi na vingine vingi.
Siku hio Nakumbuka nilichukua begi langu la
mgongoni nikaweka karanga kama robo, zilikuwa
zimekaangwa, maji ya kunywa pamoja na soda ya
chupa (fanta) niliaga nyumbani na kuondoka
kuelekea polini nia yangu ilikuwa ni kwenda kuliona
ziwa NGOZI, ziwa ambalo watu wanaliogopa
wakirihusisha na imani za kishirikina. Na
inasemekana ziwa ilo ukiingia kuoga utoki, wewe
utaishi huko huko.
Nilifanikiwa kufika sehemu ya ziwa hilo salama japo
ziwa hilo limezungukwa na msitu ambao si wa
kawaida pamoja na milima labda ndo maana watu
wanaogopa, nilipata kuliona ziwa hilo, ni ziwa
dogodogo unaweza kusema bwawa kubwa lakini
ndio hivyo lenyewe ni ziwa. Nilikaa kama masaa
mawili pale kando ya ziwa lile huku nikitafuna
karanga zangu nikishushia na soda. Mazingira ya
pale kwangu yalinivutia kwasababu ilikuwa na upepo
mwanana.
Nilimaliza kula vizuri nikakusanya vitu vyangu na
kurudisha kwenye begi ili nipate kuondoka pale
nirudi nyumbani. Kabla sijatoka pale nilikumbuka
kuwa nina camera ya digital. Hapo nilipata wazo la
kupiga picha eneo hilo ili nipate kumbukumbu na
ushahidi tosha. baada ya hapo niliamka kuondoka
lakini nikakumbuka kuwa sijachukua maji ya ziwa
hilo ili niwe na ushahidi zaidi wa kuwambia watu
waamini Kama nimefika au raha. Nilimwaga maji
yangu ya kunywa kisha nikasogea na kuteka maji ya
ziwa lile, kipindi nateka maji hayo begi langu
nilikuwa nimeliacha pembeni. Nilipo maliza kuteka
maji kugeuka nyuma sikuliona begi langu, nilibaki
nimezubaa Kwa muda huku nikijiuliza Nani
kalichukuwa begi langu na wakati nilikuwa peke
yangu. nikiwa bado najiuliza tena hofu nayo ikiwa
ishaniingia, ghafra Giza nene lilitanda maeneo hayo
ya ziwa ngozi, nilishikwa na uoga ghafra, uoga
wangu uliongezeka zaidi giza lile lilipozidi kuwa
nene, pale nikagundua ndio wakati wangu wa kufa,
niliisi kizunguzungu kwa muda wa sekunde kadhaa
kisha nikaanguka chini, toka hapo sikujua nini tena
kiliendelea.
Baadaye niliisi mtu ananiita kuniamsha kutoka
kwenye usingizi mzito, niliamka lakini nilijikuta
kwenye mji mmoja mdogo wenye nyumba tatu
kubwa Kweli kweli, halafu watu wakiwa wengiii, pia
eneo hilo likiwa limezungukwa na miti mingi
mikubwa na cha kushangaza watu wote walikuwa
awaniangalii wala awataki kusema na Mimi kila mtu
alikuwa Amenyamaza..........
.ITAENDELEA.