Shunie
JF-Expert Member
- Aug 14, 2016
- 157,076
- 463,978
- Thread starter
- #61
48
“Hakuna tatizo. Kuna sehemu nataka twende, huko, kuna dawa zangu hatari sana, haijalishi kama ni wa Magharibi au wapi,” alisema mzee Majoka.
Kidogo mzee Hamisi na Maliki wakashusha pumzi kwa furaha, tayari walijiona kushinda juu ya kile kilichokuwa kikiwatatiza, kitendo cha mzee huyo kusema kwamba hakukuwa na uchawi wowote uliokuwa ukimshinda, kukawafariji na kuona kwamba waliukaribia ushindi.
Alichokifanya mzee Majoka ni kuinuka, akaenda chumbani kwake na kujiandaa tayari kwa safari ya kuelekea porini ambapo huko ndipo kulipokuwa na madawa yake ambayo alikuwa akiyategemea kwa kufanya kazi kubwa.
“Umeona?”
“Nimeona, huyu kiboko,” alisema mzee Hamisi.
Hakukuwa na haja ya kuona matukio aliyoyafanya, maneno ya kuudharau uchawi wa Magharibi tu kulimpa uhakika kwamba angeweza kupambana na Ramadhani. Mzee Majoka alichukua dakika ishirini kujiandaa, baada ya hapo, mlango ukafunguliwa.
“Twendeni,” alisema mzee Majoka, mzee Hamisi na Maliki wakashtuka.
Hilo ndilo tukio la kwanza alilolifanya, alitaka kuwaonyeshea kwamba alikuwa kiboko ya wachawi wote, alifungua mlango na kuingia chumbani, alipotoka, hakuwa akionekana, kitu walichokiona mzee Maliki na Hamisi ni mlango kufunguka lakini hakukuwa na mtu na ghafla wakasikia sauti ikiwaambia waondoke.
Walishtuka mno, sauti waliisikia, ilikuwa ni ya mzee Majoka, ila mwenyewe yupo wapi? Kila walipoangalia, hakukuwa na mtu yeyote yule, wakazidi kuogopa kwa kuona uchawi wa huyo mzee ulikuwa balaa.
“Mmmh!” aliguna mzee Hamisi.
Hapohapo mzee Majoka akatokea na kuanza kucheka.
Alicheka kwa sauti kubwa, wazee wale wawili walikuwa wakiogopa. Si kwamba hawakujua kwamba mchawi alikuwa na uwezo wa kupotea, ila kwa mchana, kwao ilikuwa ni kitu kingine cha ajabu.
Mara nyingi sana wachawi walikuwa wakipotea nyakati za usiku na si mchana na ndiyo maana wengi wanaoshikwa mchana huwa wanashindwa kupotea. Leo hii walikutana na mchawi aliyekuwa na nguvu ya kupotea hata mchana, hiyo ilitosha kuonyesha kwamba mzee Majoka alikuwa moto wa kuotea mbali.