Simulizi: Safari Yangu Kuzimu

Shunie

JF-Expert Member
Aug 14, 2016
153,016
454,028
Mtunzi: Nyemo Chilongani

Sehemu ya 01

Nilisimama juu ya mlima mmoja mkubwa, mawingu yalitanda angani huku radi zikianza kupiga mfululizo hali iliyoonyesha muda wowote ule mvua kubwa ingenyesha.

Nilikuwa nikiogopa sana, pembeni ya mlima ule mkubwa ambao sikujua nilifikaje, kulikuwa na miti mingi iliyosababisha giza kuwa kubwa kitu kilichoniongezea hofu nzito moyoni mwangu.

Sikuwa na msaada wowote mahali hapo, nilijaribu kuangalia huku na kule nikiamini ningeweza kupata msaada lakini hakukuwa na mtu yeyote. Wakati nikijiuliza nilifikaje hapo, ghafla nikaanza kusikia vishindo vikubwa vikija kule nilipokuwa. Sikujua vilikuwa vishindo vya nani, nikabaki nikitetemeka kwani nilijua huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yangu.

Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka sana, nilitamani kukimbia kutoka mlimani hapo lakini kitu cha ajabu, sikuweza kukimbia, miguu ilikuwa mizito kuinuka, hivyo nikabaki nikiwa nimesimama tu.

Ghafla, nikawaona watu zaidi ya ishirini wakija mbele yangu, walikuwa ni binadamu wa kawaida ila walikuwa na muonekano wenye kutisha sana. Walikuwa watupu, viunoni walivaa vitu kama ukili, nyuso zao hazikuwa zikionekana vizuri.

Walikuwa wakinisogelea huku wakicheza wimbo ambao sikujua ulitoka wapi. Walikuwa wakiniangalia huku wakichekacheka kama watu wasiokuwa na akili fulani. Walitisha, nilitamani kuyafumba macho ili nisiweze kuwatazama lakini nilipotaka kufanya hivyo, nilishindwa pia.

Nikabaki nikiwa nimesimama, dakika ziliendelea kwenda mbele, cha ajabu, idadi hiyo ya watu haikuishia ishirini tu bali iliendelea kuongezeka mpaka wakafika watu zaidi ya sitini.

Baada ya dakika kama thelathini hivi, nikawaona watu kadhaa wakija pale niliposimama huku wakiwa wameshika beseni kubwa, nilipochungulia ndani, niliona damu nzito za watu, zilikuwa mbichi kabisa na kila aliyekuwa akizingalia, alionekana kuzitamani.

“Umeshawahi kunywa damu wewe?” aliniuliza mwanamke mmoja mtu mzima, alikuwa na umri usiopungua miaka sabini, alikuwa hajiwezi lakini ndiye aliyeonekana kucheza kwa nguvu kuliko wote mahali hapo.

“Sijawahi kunywa damu, na siwezi kunywa,” nilisema kwa sauti tena kwa kujiamini sana.
Screenshot_20230116_034753_OGInsta%2B.jpg
 
Sehemu ya O2

“Hahaha....hahaha...hahaha...” niliwasikia watu wale wakicheka tena kwa nguvu kiasi kwamba nikahisi ngoma za masikio yangu zilitaka kupasuka.

“Utakunywa tu, tena hadi nyama utakula,” alisema mwanamke yule na hapohapo kuanza kuwaita watu wengine ambao walikuwa na sinia kubwa, lilikuwa limejaza nyama za watu na pia walikuwa na jagi kubwa, hilo lilikuwa na damu nyingi.

“Mlisheni naye ashibe, anaonekana ana njaa kali,” alisema mwanamke yule, hapohapo watu watatu wakanishika na kuanza kunilisha nyama zile na damu ile kinguvu.
***

Nilishtuka kutoka usingizini, jasho lilinitiririka mno, mapigo ya moyo yalikuwa yakidunda kupita kawaida huku mwili wangu ukisisimka sana. Niliangalia saa yangu ya ukutani, ilionyesha tayari ilikuwa saa tisa usiku, nilipochungulia nje, giza totoro lilitawala.

Nikakaa kitandani, picha kamili ya ndoto ile ikaanza kunijia kichwani mwangu, nilikumbuka kila kitu kilichonitokea ndotoni kuanzia wale watu walivyonifuata na kuanza kunilisha nyama zile.

Huku nikiwa sifahamu kilichotokea, mara macho yangu yakaanza kuwa mazito, sikufahamu nini kilichosababisha, lakini ghafla nikajikuta nikiwa pembeni ya bahari moja kubwa, sijui kama ilikuwa ni Hindi, Pasifiki au bahari gani.

Nilijiuliza maswali mengi lakini sikupata jibu, sikujua sababu iliyonifanya niwe mahali pale, nilihisi kabisa inawezekana ilikuwa ndoto nyingine na hivyo kuamua kujing’ata lakini sikushtuka kuashiria ile haikuwa ndoto bali ni kitu halisi kilichokuwa kikitokea.

Huku nikiwa ninajiuliza maswali, ghafla kwa mbele nikamuona mwanamke mmoja aliyesimama juu ya maji, alivalia gauni refu jeupe, alikuwa na nywele ndefu mpaka mgongoni, miguu yake haikuwa kama yetu, ilikuwa ni kwato za ng’ombe, alininyooshea kidole na kuanza kuniita.

Kiukweli niliogopa, sikutaka kumfuata lakini ghafla nikajikuta nikianza kupiga hatua kumfuata huku nikiwa na hofu kubwa moyoni. Sikuzama kwenye maji yale, na mimi nilikuwa natembea juujuu mpaka nilipomfikia.

Alikuwa msichana mrembo mno, kwa kumwangalia harakaharaka ungeweza kusema alistahili kuwa mrembo wa dunia, alikuwa akitabasamu tu.

“Hujambo Michael,” alinisalimia.
“Sijambo, wewe nani?” nilimuuliza huku nikitetemeka, sikutaka hata aniguse.
 
Sehemu ya O3

“Ninatwa Yusnath.”
“Ndiye nani?”
“Mimi ni msichana mrembo kuliko wote duniani na kuzimu, nimekuleta kwa ajili ya kukuonyesha mambo fulani hivi,” aliniambia huku tukiwa tumesimama juu ya bahari.

“Mambo gani?” niliuliza kwa kuhamaki.
“Mambo yanayofanywa na watu kisiri. Upo tayari tuondoke?”
“Hapana, unataka twende wapi?”
“Kuzimu.”

“Kuzimu?” niliuliza kwa mshtuko.
“Ndiyo!”
“Kuna nini?”
“Kuna siri kubwa sana zimejificha, nataka nikuonyeshe watu wanaofanya mambo mabaya huku nyie mkiwaamini. Upo tayari?” aliniuliza.

Sikuwa tayari lakini kilichonishangaza, eti nikakubaliana naye bila tatizo lolote. Mara ghafla, kwa mbali nikaliona wimbi moja kubwa likija kule tulipokuwa, naweza kusema ukubwa wake ulikuwa ni sawa na jengo lililokuwa na ghorofa sita, niliogopa sana, nikataka kukimbia kuelekea ufukweni.

Mwanamke yule akanishika mkono, akaning’ang’ania nisimkimbie, nikaanza kupiga kelele huku wimbi lile likiendelea kutufuata pale tulipokuwa.

Wala hazikuchukua dakika nyingi, wimbi lile likatupiga, tukaanza kuzama, nikaanza kupiga kelele za kuomba msaada, ghafla nikajikuta nimetokea sehemu nyingine kabisa, ulikuwa mji mwingine ambao kwa kuuangalia harakaharaka.

Ulikuwa na majengo mengi yaliyonifanya kujiuliza, ilikuwaje kuhusu ile bahari? Mbona hatukuwa baharini tena?
“Karibu kuzimu tuanze kazi,” aliniambia Yusnath, nikapigwa na butwaa baada ya kusikia pale nilipokuwa palikuwa ni kuzimu.

Sikuamini! Hakukuwa na watu, eneo zima lilikuwa kimya kabisa hali iliyonifanya kuogopa sana. Yusnath akaniambia nimfuate, nikafanya hivyo.

Ardhi yao haikuwa kama hii yetu yenye mchanga, yao ilikuwa ni kama changarawe, ukitembea pekupeku ni lazima uumie nyayo zako.

Tulitembea huku nikiangalia huku na kule kana kwamba nilikuwa nikimtafuta mtu fulani.

Hakukuwa na mazingira mazuri hata kidogo na kila hatua niliyokuwa nikipiga, nilitamani kurudi duniani, yaani kwa jinsi mazingira ya kule yalivyokuwa, sikuwa na hamu ya kuendelea kukaa.

Tulitembea kwa mwendo wa taratibu na kuingia sehemu moja hivi. Ilikuwa ni sehemu yenye viumbe vingi mno. Kwa mbali walionekana kuwa kama binadamu lakini ukweli ni kwamba hawakuwa binadamu.
 
Sehemu ya O4

Maumbo yao yalitisha mno, hawakuwa na vichwa kama hivi vyetu, vichwa vyao vilikuwa ni vya wanyama.

Kuna wengine walikuwa na vichwa vya paka, macho makubwa mithili ya machungwa, vichwani walikuwa na mapembe lakini cha kushangaza, miguu yao ilikuwa kwato za ng’ombe.

Ukiachana na hao, kulikuwa na viumbe vingine vilivyokuwa na vichwa vya ng’ombe, walitembea huku miguu yao ikiwa mikubwa mno na mgongoni walikuwa na mabawa yaliyoonekana kuchoka.

Kila nilipowaangalia, waliniogopesha mpaka kipindi kingine kuyapeleka macho yangu pembeni kabisa. Kila tulipopita, kulikuwa na majagi makubwa yaliyokuwa na damu ndani yake.

Duniani watu waliendelea kufa kwa ajali na kule kuzimu damu ziliendelea kukusanywa kama kawaida. Tulitembea mpaka kwenye jumba moja kubwa, lilionekana kuwa zuri lakini kwa nje kulisimikwa mafuvu ya watu na sehemu nyingine kuwa na miguu ya binadamu.
“Unaiona hii?” aliniuliza huku akiiangalia ile miguu ya watu.

“Naiona.”
“Hii ilikuwa miguu ya maiti, ngoja nikuonyeshe kitu,” aliniambia na ghafla kukatokea kitu kama televisheni na kuanza kutazama kile alichotaka nikitazame.

Nililiona kundi kubwa la watu, ilikuwa ni usiku sana, walisimama sehemu moja ambayo kwa haraka sana niligundua ni makaburini.

Kulikuwa na makaburi ya kila aina, sehemu nyingine majeneza yalikuwa nje huku sanda zikitundikwa juu ya makaburi, tena sanda nyingine zikiwa na damu mbichi kabisa.

Niligundua kulikuwa na maiti ambazo zilichukuliwa pindi tu zilipozikwa na ndiyo maana damu zile mbichi ziliendelea kuwepo.

Hapo, katikati ya watu kulikuwa na mtoto mmoja, alionekana kuwa na sura ya kipole lakini Yusnath akaniambia huyo ndiye alikuwa malkia huko duniani, yaani wachawi wote wa Tanzania walimuabudu yeye.

Kazi kubwa iliyokuwa ikifanyika mahali hapo ni kufukua makaburi tu. Maiti zilihitajika kwa nguvu zote kwa ajili ya nyama ambayo huliwa kila inapofika siku ya Alhamisi ambayo kwao kule kuzimu huwa ni siku ya sherehe.
 
Sehemu ya O5

Ufukuaji wa makaburi yale haukuwa wa kawaida, yaani kulikuwa na mwanamke anasimama juu ya kaburi huku akiwa mtupu, anacheza kwa kukatika viuno huku wakati mwingine akikaa juu ya kaburi na kuanza kuyasugua makalio yake hapo kaburini na ghafla kaburi linaanza kujifukua lenyewe.

Kuna maiti nyingine zilikuwa zikija juu huku zikiwa na sanda tu na nyingine zikiwa na suti.

Zilikuwa maiti hizihizi ambazo zilizikwa hivi karibuni au kama hakukuwa na maiti mbichi, zoezi la kwenda mochwari huanza mara moja.

Zile maiti zinapotolewa na kuonekana zimeanza kukauka, zoezi la kwenda mochwari huanza mara moja. Siku hiyo, hakukuwa na maiti iliyokauka, nyingi zilikuwa mbichi hivyo kuzichukua na kuziweka juu ya kaburi.

Mambo yote yaliyokuwa yakitokea nilikuwa nayaangalia kwa macho yangu. Nilikuwa nikiogopa na kusisimka mwili lakini sikuwa na jinsi, kwa wakati huo nilitakiwa kuangalia kila kitu kilichokuwa kikitokea usiku huo.

“Unamuona yule mtoto?”
“Ndiyo! Amefanya nini?”
“Yule ndiye kiongozi wenu duniani, yeye ndiye anayepanga ratiba ya kuyashughulikia makanisa na misikiti, yeye ndiye mpangaji wa kila kitu,” aliniambia Yusnath.

“Anaishi wapi?”
“Duniani.”
“Sehemu gani?”
“Hahaha! Hahaha! Hahaha!” alicheka Yusnath, ghafla, na mimi nikajikuta nikiwa nimesimama katikati ya makaburi, nilikuwa nimezungukwa na watu wengi waliokuwa watupu kabisa, sijui kama waliniona au la, lakini niliwasikia wakianza kucheka kwa pamoja.

Nilipogeuka na kuangalia pembeni yangu, kulikuwa na maiti moja ya mwanamke mjauzito, ghafla, ikafumbua macho na kuanza kuniangalia.
“Nisaidieeee....nisaidieeee....” ilisema maiti ya mwanamke yule, nilitamani kuzimia.

Nilibaki nikitetemeka tu, sikuamini kile nilichokuwa nikikiona, maiti kuongea, tena ikiniomba msaada makaburini, hakika niliogopa mno.

Maiti ile haikunyamaza, bado iliendelea kuniomba msaada huku wachawi wengine wakibaki wakicheka tu.

Sikujua ni msaada wa aina gani aliokuwa akiuomba kwani mimi nilikuwa mgeni mahali pale, hivyo sikujua ni kwa namna gani ningeweza kumsaidia, na kubwa zaidi, mimi mwenyewe nilihitaji msaada wa kutolewa huko.
 
nikajua wewe shunie ndo umeandika uzi umeenda kuzimu! Yangekuwa si mambo madogo haya ingekuwa ni hivyo kweli ningeomba jf wakubadili na jina wakuite mzimulilo!.

wacha tusome simulizi
 
Sehemu ya O6

Wala hazikupita sekunde nyingi, nikaanza kujisikia kuwa kwenye hali ya tofauti kabisa, baridi kali likaanza kunipiga makaburini pale. Sikuelewa ni kitu gani kilikuwa kikiendelea kwani hakukuwa na siku ambayo nilihisi baridi kali kama siku hiyo usiku.

Nilikwishawahi kukaa Mbeya, Iringa na hata Arusha lakini sikuwahi kusikia baridi kama nililokuwa nikilisikia makaburini hapo, kulijaa mauzauza mengi yaliyonifanya niogope mno na kujiona kama nilikuwa sehemu moja iliyonifanya nihisi muda wowote ule kuanzia sasa ningekufa.

Huku nikihisi baridi kali kiasi cha kujishika vilivyo kwa staili ya kuipitisha mikono kifuani mwangu, ghafla nikaanza kusikia sauti za watoto wakilia kwa sauti za juu kabisa. Sikujua watoto hao walikuwa wapi zaidi ya kusikia sauti hizo pale kaburini.

Nilianza kuangalia huku na kule ili kuona ni wapi watoto hao walipokuwa, baada ya sekunde kama ishirini nikawaona wanawake kama kumi wakisogea pale kaburini huku wakiwa wamewabeba watoto waliokuwa kwenye sanda, wanawake hao walikuwa kama walivyozaliwa.

“Hao ni watoto kutoka mahospitalini, wazazi wao waliwazaa lakini wameonekana wamekufa. Kiukweli, hawajafa bali tunawachukua hasa tunapokuwa na uhitaji wa kula nyama,” aliniambia mwanamke yule kwa sauti ya juu.

Hapa nikagundua kitu kwa kipindi chote nilichokuwa hapo makaburini, hakukuwa na mtu aliyekuwa akiniona zaidi ya ile maiti tu na ndiyo maana aliposema anahitaji msaada, wale wachawi wengine walicheka tu kwa kuona kama alikuwa akiongea peke yake.

Niliwaonea huruma watoto wale waliokuwa wakilia tu, mbali na hao, nikawaonea huruma wanawake waliowazaa watoto hao na kuona wamekufa na wakati ukweli hawakufa zaidi ya kuchukuliwa na kupelekwa kwa ajili ya kuliwa nyama tu.

“Lete sinia,” alisema mwanamke mmoja, alionekana kuwa kiongozi chini ya yule mtoto mdogo. Sinia likaletwa.
.
.

Itaendelea.
 
Tulia kijana na urudi kitandani kulala ukumbatie mto
Unamatusi mazito sana nawe usiku huu umekosa wa kukumbatia mpaka ututishe na mambo ya kuzimu..? Si vizuri mdada kama wewe kujiita pisi halafu kutuletea stori za kuzimu itakuwa we ni jamaa fulani tu hivi la kitaa..😅
 
O7

Ndani ya sinia lile kulikuwa na kisu kikali kilichofungwa kitambaa chekundu. Hakikuwa kisafi, japokuwa ilikuwa ni usiku na mahali pale kulikuwa na giza lakini niliona damu zilizoganda zikiwa katika kisu kile hali iliyoonyesha kilitumika sana kukata nyama za watoto makaburini hapo.

Kwa macho yangu nikashuhudia watoto wale wakichinjwa na mwanamke yule. Hakuwa na huruma, alianza kumchinja mtoto wa kwanza huku kila damu ilipotoka, alikinga mdomo wake na kuanza kunywa.

Niliumia zaidi, kitendo kilichokuwa kikiendelea makaburini hapo kilinitisha zaidi, kuna kipindi sikutaka kabisa kuangalia zaidi ya kutaka kuyafumba macho yangu. Nilipojaribu kufanya hivyo, sikuweza, macho yangu yaliendelea kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea.
“Imetosha, naomba unitoe hapa,” nilimwambia Yusnath.

“Bado, kuna mengi ningependa uyafahamu hapa makaburini na kuzimu, kuwa mvumilivu,” alisema mwanamke yule.

Ndugu yangu, makaburini kunatisha, usione unapita nyakati za mchana basi ukajua hata usiku huwa hivyohivyo tu. Huwa ninawashangaa hata wezi wanaokwenda makaburini nyakati za usiku na kufukua makaburi kwa ajili ya kuchukua vitu alivyozikwa navyo maiti.

Kwa kile nilichokiona usiku ule, kilikuwa ni cha kutisha mno. Baada ya kuhakikisha watoto wpote wamechinjwa, mwanamke yule akaanza kuwakatakata vipande.

Wachawi wengine wakaanza kuzigombania nyama zile kama tunavyogombania vitu fulani kwenye minada hasa masokoni.

Kila aliyefanikiwa kuzipata nyama zile, alizitafuna harakaharaka kama mtu aliyeambiwa asiungefanya hivyo basi angepokonywa.

Ilikuwa kama sherehe kwao, wakaanza kuzila zile nyama huku wengine wakijilamba kuonyesha zilikuwa tamu mno. Niliendelea kusimama mahali pale mpaka walipomaliza na ndipo mwanamke yule aliyekuwa akicheza kama alivyozaliwa akalifuata kaburi moja na kuanza kucheza huku akiyasugua makalio yake katika kaburi lile.

Kama lilivyokuwa kaburi la kwanza, na lile likaanza kujifukua na baada ya dakika kadhaa, moshi mzito ukaanza kufuka na maiti moja kutoka huku ikiwa na sanda. Alipoifunua, ilikuwa maiti ya mwanaume mmoja, alionekana kuwa mzee kama wa miaka sitini.
 
O8

Wachawi wale wakaanza kucheka sana, walicheka huku vicheko vyao vikiwa kero masikioni mwangu kwani sikufurahia kabisa kile walichokuwa wakikifanya makaburini pale.

Walipoona maiti imetoka ndani ya lile kaburi, wakaiweka pembeni na mwanamke yule aliyekuwa na kisu kusogea na kuanza kumkata tumbo mpaka alipohakikisha umetoka, akauchukua na kuanza kuutafuna huku wenzake wakimwangalia kwa matamanio makubwa.

Katika hili ngoja nikwambie kitu kimoja. Si maiti zote zinazozikwa huwa na viungo vilivyokamilika, kwa mfano maiti hii ya huyu mzee, haikuwa na sehemu za siri, nahisi zilikatwa tangu ilipokuwa mochwari ambapo biashara ya viungo vya maiti hufanyika mara kwa mara.

Nilijiuliza kama wachawi wale walihitaji kuitafuna maiti yote au la kwani hawakuonekana kutosheka, yule mwanamke mchovumchovu alipokuwa akikata kipande na kula, kilichofuata alikikata na kuwapa wenzake ambao walivipokea kwa shangwe na kuanza kula.

“Nataka niondoke,” nilisema huku nikiwa sitaki kuendelea kuwa mahali hapo.
“Subiri kwanza,” aliniambiaYusnath.
“Nisubiri nini sasa? Sitaki kuangalia zaidi,” nilimwambia huku nikionekana kukasirika.

“Hutaki kumuona mkuu wa makaburini?”
“Mkuu wa makaburini?”
“Ndiyo! Kila sehemu huwa kuna mkuu wake, subiri, muda si mrefu atafika mahali hapa, usiogope,” aliniambia Yusnath.

Kilichonishangaza ni pale ambapo ghafla hali ikabadilika na kuanza kuwa na hamu ya kumuona huyo mkuu wa makaburini ambaye kwa kweli sikutaka kumuona kwa kuwa niliamini anatisha.

Nilijifikiria kuhusu huyo mkuu wa makaburuni aliyetarajiwa kufika mahali hapo, sikujua aliwaje na alifanana vipi. Wachawi wale waliokuwa makaburini pale waliendelea kula nyama za watu.

Zilipita kama dakika mbili hivi, ghafla wachawi wale waliokuwa wakizungumza yao huku wakisherehekea kwa kula nyama zile nikawaona wakikaa kimya na kiviinamisha vichwa vyao chini kama ishara ya kutoa heshima fulani.

Nikaanza kusikia tena baridi kama nililolisikia kipindi cha nyuma. Kwa wakati huu, baridi lile liliambatana na upepo mkali huku nikisikia majani ya miti yakivuma vuuu vuuu muda wote.
 
O9

Mara nikaanza kusikia milio mikubwa kama ngurumo za radi makaburini pale huku kwa mbali kukiwa kama na tetemeko la ardhi. Kiukweli niliogopa lakini nikajua ndiyo kwanza yule mkuu wa makaburini alikuwa akifika mahali hapo, nilichokifanya ni kusubiri ili na mimi nimuone kwa macho yangu.

Kwa mbali nikaanza kumuona mtu akija, alionekana kuwa na mwili mkubwa kama walivyo wacheza mpira wa kikapu wa Marekani.

Alikuwa amejazajaza. Alipokuwa kwa mbali nilimuona kuwa binadamu wa kawaida kwa sababu ya giza lakini mara aliposogea kule walipokuwa wale wachawi ndipo nikagundua hakuwa binadamu wa kawaida.

Mwili wake ulikuwa na manyoya mengi kama simba, miguu ilifanana na miguu ya sokwe, hakuwa na uso wa binadamu, alikuwa na uso wa mbweha huku kichwani akiwa na mapembe makubwa mithili ya urefu wa chupa ya soda na masikio makubwa kama sahani ya chakula.

Jitu lile la ajabu lilipokuwa likitembea, bado wachawi waliviinamisha vichwa vyao chini kama kumpa heshima yake, lilitembea mpaka mbele kabisa, juu ya kaburi moja ambalo kwa juu kulikuwa na sinia jingine lililokuwa na nyama na jagi lenye damu za watu kisha kuanza kula.

Hakuwa akitafuna kama binadamu wa kawaida wanapotafuta vitu bali alikuwa akitafuna kana kwamba alitafuta kitu kigumu tena alichotakiwa kukimaliza kwa haraka sana.

Nilishindwa kuvumilia kubaki mahali hapo kwani kila nilipoliangalia lile jitu la kutisha, mwili wangu ulisisimka tu. Nikamwambia Yusnath tuondoke mahali hapo.

“Umeridhika?” aliniuliza.
“Ndiyo! Naomba tuondoke,” nilimwambia.
Akaunyoosha mkono wake, ghafla pale nilipokuwa nikaanza kuvutwa lakini sikukiona kile kilichokuwa kikinivuta.

Nilipelekwa mpaka kule alipokuwa Yusnath na aliponishika mkono tu, tukapotea na kuibukia kule mlimani.

Pale mlimani hatukukaa sana, akaniambia niyafumbe macho yangu kwani sehemu tuliyokuwa tukienda ilikuwa na watu wengi lakini hiyo njia ambayo tulitakiwa kuipita ilikuwa na mauzauza mengi ambayo hakutaka niyaone. Hilo halikuwa tatizo, nikayafumba macho yangu.
 
nimecheka sana kwamba me jamaaa me nipo lindo nalinda ndio maana unaniona
Lindo la kulindwa na mdada kweli..? Nyie ndio huwa mnasababisha majambazi tubadili mission zetu unakuta misson ilikuwa kuiba ila ghafla tu inakuwa ya kubaka! Unyama sana
 
1O

Ghafla tukaibukia sehemu ambayo ilikuwa na watu wengi mbele yetu, watu wale walikuwa wameviinamisha vichwa vyao, walikuwa wengi zaidi ya watu elfu moja. Nikaanza kujiuliza walikuwa mahali pale wanafanya nini.

“Hawa ni wenzako kutoka duniani ambao wamefika hapa kwa ajili ya kumuabudu mkuu wetu,” alinijibu Yusnath japokuwa swali lile nilijiuliza moyoni mwangu na sikujua alijuaje kama nilijiuliza vile.
“Kuna ninaowafahamu?”
“Wapo wengi tu, unataka kuwaona?”
“Ndiyo!”
“Basi subiri!”

Niliendelea kusubiri, nikawa na kiu kubwa ya kutaka kuwaona hao watu waliokuwa mahali hapo ambapo Yusnath aliniambia kulikuwa na wengine niliokuwa nikiwafahamu kabisa.

Nilisubiri mpaka baada ya dakika kadhaa, nikasikia muungurumo mkubwa mithili ya simba, Yusnath akaniambia nifumbe macho kwani yule aliyekuwa akija ndiye alikuwa kiongozi wao, yaani shetani mkuu.

Kwanza nikajifanya kupinga kimoyomoyo kwani nilihisi kutokana na mahali hapo kuwa usiku basi Yusnath asingeweza kuona kama macho yangu hayakufumbwa bali nilikuwa naangalia kisirisiri tu.

Muungurumo ule uliendelea kusikika na mara kule ambapo Yusnath aliponaimbia ndiyo ingekuwa njia ya shetani kufika mahali hapo kukaanza kufuka moshi mzito, tena ulikuwa ukifuka kwa kasi kubwa.

Nilibaki nikiangalia tu, ghafla nikaanza kuyaona macho yangu yakiwa mazito. Nilijitahidi sana kuyaacha wazi ili nimuone shetani lakini ikashindikana, nikashtukia yakiwa yamefumba kabisa kitu kilichonifanya nikubaliane nacho.

Nikasikia kishindo kikubwa cha mtu aliyekuwa akitembea, kishindo kile hakikuwa cha kawaida hata kidogo na alikuwa akitembea kuelekea kule kulipokuwa na watu wengi waliokuwa wameinamisha vichwa kama ishara ya kumuabudu.

Sikujua alikuwa akifanya nini, ila baada ya dakika kama kumi, nikaambiwa niyafumbue macho yangu, nikafanya hivyo.

Yule shetani hakuwepo tena, alikuwa amekwishaondoka na nilipowaangalia wale watu ambao waliyainua macho yao, sikuamini kabisa kama watu hao ningeweza kuwakuta mahali hapo.
 
Lindo la kulindwa na mdada kweli..? Nyie ndio huwa mnasababisha majambazi tubadili mission zetu unakuta misson ilikuwa kuiba ila ghafla tu inakuwa ya kubaka! Unyama sana
niacheee
 
11

Mtu wa kwanza kabisa kumuona, aliitwa Fabian Joseph. Huyu alikuwa mchungaji wa kanisa fulani hivi lililokuwa maarufu sana huku duniani nchini Tanzania. Waumini wengi walikwenda kwake kuabudu, aliponya wagonjwa kwa kuwapaka mafuta ambayo kwake alisema aliyatoa Israel.

Viwete walitembea, hakufanya hivyo tu bali kulikuwa na miujiza mingi aliyokuwa akitokea kanisani kwake. Leo hii, mchungaji huyo ambaye alijiita mtume, naye alikuwepo huko kuzimu akipewa nguvu.

Hebu ngoja nikwambie vizuri kuhusu huyu mchungaji.
.
.
Je, nini kitaendelea?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom