Simulizi: Safari Yangu Kuzimu

Simulizi: Safari Yangu Kuzimu

77.

Alizidi kuyatamka maneno yale, alipoona kwamba hayatoshi tu, akaanza kuchukua karatasi zenye maneno yale, akachukua na unga fulani kisha kuuweka katika karatasi ile na kuanza kumpulizia Ramadhani kitu kilichomchanganya vilivyo, hapohapo akaanguka chini na mapovu kuanza kumtoka mdomoni na puani.

Huo ulikuwa ushindi mkubwa ambao hakutarajia kuupata kabla, mtu ambaye alimsumbua kwa kipindi klirefu, leo hii, tena usiku huu alikuwa hoi pale chini. Kwake, hiyo iliendelea kuwa furaha, kubwa, alichokifanya ni kupotea, na ghafla akaibukia katika uwanja wa wachawi wenzake, wote waliomuona, wakaanza kutetemeka akiwemo mkubwa wao.

Nguvu alizokuja nazo mzee Hamisi zilikuwa kubwa mno, uwanjani hapo walikuwa na kiongozi wao lakini naye alipomuona mzee Hamisi akiingia, akajikuta akitetemeka, hofu ikamjaa na mwisho wa siku, wote kwa pamoja akiwemo yeye kiongozi wakapiga magoti chini kama ishara ya kumpa heshima.

Huo nao ukawa ushindi mkubwa, kule kuzimu alipokwenda, alipewa nguvu za ajabu ambazo hakuamini kama angeweza kuzipata katika maisha yake.

Huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kila kitu, mzee Hamisi akawa kiongozi wa wachawi lakini huyohuyo ndiye alikuwa hakosi msikitini. Alikuwa mtu wa swala tano, aliheshimika mno pasipo watu kujua kwamba mtu huyo alikuwa mkubwa wa wachawi na alikuwa na nguvu mno za kichawi.

Hiyo ndiyo stori ya mzee Hamisi niliyotaka kukupa, alikuwa miongoni mwa watu niliokutana nao kule kuzimu. Walikuwa watu wengi sana, wote hao walikuwa wakimuabudu shetani ambaye alikuwa mbele yao.

Ukiachana na mzee Hamisi, yule mchungaji na mwanasiasa ambao wote niliwapeni sifa zao, kulikuwa na msichana mmoja hivi, msichana mrembo kwa kumwangalia, aliyekuwa na figa matata sana, naye huo alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa humo.

Kwa kumwangalia, mwanaume yeyote aliye rijali asingeweza kumuacha, alivutia, alikuwa na umbo namba nane, sura nyembamba na kifuani alionekana kama msichana aliyetoka kuvunja ungo siku si nyingi.

Sikuwa nikimfahamu, sikuwahi kumuona kabla lakini Yusnath aliniambia kwamba msichana huyo aliitwa Esta.
 
78.

Naweza kusema kwamba nchi ya Tanzania ilikuwa ikifanya mashindano ya walimbwende kila mwaka, niliwahi kuwaona wengi wakiwemo Wema Sepetu, Irena Uwoya na wengine wengi lakini kwa uzuri aliokuwa nao Esta ilikuwa ni balaa.
“Huyu msichana ni nani?” nilimuuliza Yusnath.

“Anaitwa Esta.”
“Anakaa wapi?”
“Anaishi Ilala.”
“Naye anaabudu hapa?”
“Ndiyo!”

“Yupo kitengo gani?”
“Huyu ni kwa ajili ya kuua tu na kuwalaghai watu. Huyu ni msichana mbaya sana ambaye ombea kukutana na simba lakini si msichana huyu,” alisema Yusnath.

“Mmmh!”
“Ndiyo hivyo!”
“Ooppss!”
“Nikwambie kingine?”
“Kipi?”
“Huyu msichana si binadamu!”
“Unasemaje?”

“Ni jini!”
“Hebu niambie vizuri kwanza,” nilimwambia Yusnath.
“Usijali, kuna mengi nitakwambia kuhusu Esta na namna anavyofanya kazi zake,” aliniambia Yusnath.

“Sawa. Ningependa kusikia mengi.”
“Usihofu! Ushawahi kusikia kuhusu jini Maimuna?”

“Ndiyo! Nasikia ni msichana mzuri mno!”
“Basi ndiye huyu!”
“Ndiye yule tuliyekutana naye kule mwanzo?”

“Unaposikia jini Maimuna, hayupo mmoja, wapo wengi, tena wote warembo!”
“Duuh! Hebu niambie kuhusu Maimuna, ningependa kusikia mengi sana!”

Wala usijali! Njoo huku,” aliniambia na kunipeleka pembeni, kulikuwa na viti kadhaa, nikatulia hapo, baadaye akaniambia twende kwenye ule mlima mkubwa, tukapaa mpaka tulipofika huko.

Kama kawaida ile televisheni kubwa ikawashwa, nilikuwa hapo kwa ajili ya kuona yale yaliyokuwa yakimhusu jini Maimuna tu. Akaanza kazi.

***
Nilimuona msichana akiwa amesimama barabarani, ilikuwa usiku sana, kama saa nane hivi. Alikuwa msichana mrembo, alivalia kiheshima sana, alivutia mno, nywele zake ndefu zilifika mgongoni, alipendeza mno, kadiri nilivyokuwa nikimwangalia, hata mimi nilimpenda sana.

Uso wake ulijawa na tabasamu kila wakati, hakuwa Mswahili, alikuwa msichana mwenye mchanganyiko wa rangi ambaye ningeweza kumuita Chotara.

Sikujua msichana huyu alikuwa nani, alikuwa akifanya nini mahali pale, ila kila nilipomwangalia, hakika nikajisemea kwamba hakukuwa na mwanamke mrembo kama alivyokuwa.
 
79.

Mwanzo nilifikiri alikuwa akijiuza barabarani pale, lakini haikuwa hivyo, sidhani kama kungekuwa na mwanamke aliyekuwa akijiuza huku akiwa amevalia gauni refu, lililofika unyayoni kama alivyovaa msichana yule.

Magari yalipita, kila aliyepita na gari lake, alipokaribia mahali aliposimama msichana yule, alipunguza kasi ya gari lake na kumtupia macho.

Msichana yule aliendelea kusimama mpaka nilipomuona jamaa mmoja akienda upande ule aliokuwepo, kwanza akampita huku akimwangalia, alipofika kama hatua nne mbele, akaona haiwezekani, akaanza kupiga hatua kumrudia.

Kumbuka haya yote nilikuwa nikiyaona kwenye ile televisheni kubwa ya kichawi, baada ya kumuona msichana huyu kule kuzimu huku akiitwa kwa jina la Maimuna, hapo ndipo nilipoanza kuonyeshewa maisha yake, yaani kwetu sisi hujulikana kama Jini Maimuna, yaani jini ambaye hutumia sana mvuto wake kukamata wanaume.

Kabla ya kuzungumza chochote kile, mwanaume yule akaupamba uso wake kwa tabasamu pana, alijitahidi kuonyesha uchangamfu usoni mwake lakini msichana yule akabaki akimshangaa, mshangao uliomfanya aonekane mzuri zaidi.

“Mambo vipi mrembo!” alisalimia jamaa yule.
“Salama.”
“Mbona upo hapa usiku-usiku, huogopi vibaka na wabakaji?’ aliuliza jamaa yule.
“Niogope nini sasa?”
“Au mfanyabiashara tufanye biashara ya chapchap?”

“Wewe kaka, umeniona mimi malaya?”
“Hapana. Ila nimeuliza tu, ila kama haupo kama ninavyofikiria, naomba unisamehe,” alisema jamaa yule.

Maimuna hakuongea chochote, alibaki kimya huku akipiga hatua kwenda nyuma zaidi. Kumuacha ilihitaji roho ngumu mno, jamaa yule hakutaka kukubali, mvuto wa msichana yule ulimpagawisha sana, hivyo akaona iwe isiwe ilikuwa ni lazima kumchukua usiku huo.

Jamaa alijielezeaelezea wee, mwisho wa siku akakubaliana naye, ila kwa sharti moja tu kwamba hakuwa tayari kwenda nyumbani kwa mwanaume huyo au gesti, kama alitaka, basi usiku huohuo, sehemu yoyote isipokuwa zile sehemu alizozitaja, na baada ya hapo, wasijuane, jamaa akakubaliana naye.
 
80.

Wakasogea pembeni kidogo, kutokana na usiku kuwa mkubwa, hakukuwa na watu kabisa, ni magari tu ndiyo yaliyokuwa yakipita. Walisogea nyumba mpaka walipofika sehemu iliyokuwa na mitimiti, hapo ndipo walipoamua kumalizia haja zao.

Kuwa na Chotara, mrembo, anayevutia, kulimpagawisha sana jamaa yule, akachojoa nguo zake harakaharka mithili ya mtu aliyetaka kwenda sehemu fulani, baada ya hapo, akalipandisha gauni la msichana yule, akaishusha nguo ya ndani na kisha kumlaza chini na kwenda juu yake.

Baada ya dakika kadhaa ni sauti za mahaba tu ndizo zilizokuwa zikisikika, wala hazikupita hata dakika mbili, ghafla nikamuona jamaa yule akianza kukakamaa mwili, akaanza kutokwa na mapovu mdomoni yaliyochanganyikana na damu, baada ya hapo, akatulia palepale kifuani.

Jini Maimuna akasimama, macho yake yalikuwa mekundu mno, meno yake yakabadilika na kuwa kama ya ngiri, akamwangalia kijana yule, mwili wake ukakauka, baada ya kuona kwamba amekufa, akanyoosha mikono juu kisha kupotea.
***

“Dada! Una kampani yoyote?”
“Kampani ya nini?”
“Utakaporudi nyumbani!”
“Hapana! Kwani nini?”
“Wewe unaishi wapi?”
“Naishi Ilala!”

“Waooo! Mimi naishi Magomeni Mikumi. Naweza japo kukupa lifti manake nipo alone tu, nina usafiri mzuri tu.”
“Sawa! Ila mpaka muziki uishe!”
“Haina noma.”

Yalikuwa ni mazungumzo ya watu wawili, alikuwa kijana mmoja aliyeonekana mstaarabu sana lakini uso wake ungekufanya kugundua kwamba alikuwa mlevi, alikuwa akizungumza na msichana mmoja mrembo sana katika klabu ya Usiku ya Maisha.

Kulikuwa na disko, watu walijazana mno, kila aliyecheza, alijitahidi kuonyesha umahili mkubwa, msichana huyo ambaye alikaa peke yake, alikuwa kimya.

Wanaume wengi walikuwa wakimmezea mate mrembo, kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka kuzungumza naye lakini hakukuwa na aliyemsogelea zaidi ya kijana huyo tu.

“Mimi naondoka!”
“Poa! Twende tu!
Wakachukuana na kisha kuelekea garini. Mwanaume yule alijiona kupata lakini ukweli ni kwamba alipatikana yeye.

Alionekana kuwa mchangamfu mno, kuopoa msichana mzuri kama yule klabu, kulimfurahisha na kujiona mtu mwenye bahati sana.
 
81.

Gari likawashwa na kuanza safari ya kuelekea huko Ilala. Njiani, walizungumza mengi. Kijana yule alionekana kuwa na presha kubwa, alijiona kama angemkosa msichana yule au ule ndiyo ungekuwa mwisho wa kuonana naye, hivyo akaanza kutupia ndoano yake.

Kweli ikanasa, walipofika karibu na Mkwajuni, Kinondoni, jamaa akaegesha gari pembeni, akahamia kiti cha nyuma na kisha kumvuta msichana yule kulekule.

Hakukuwa kilichoendelea zaidi ya kuanza kushikana hapa na pale na mwisho wa siku wote kujikuta wakiwa watupu, kilichofauata ni kuanza kufanya ngono.

Kama ilivyokuwa kwa jamaa yule wa jana ndivyo ilivyotokea hata kwa huyu, akiwa kifuani mwa msichana yule, akaanza kukakamaa mwili wake, mapovu yaliyochanganyikana na damu yakaanza kumtoka mdomoni mwake, kilichofuata, akafariki dunia na kisha yule Jini Maimuna kupotea mulemule garini.

***
Tetesi zikaanza kusikika ndani ya jiji la Dar es Salaam kwamba kulikuwa na mwanamke aliyekuwa akiua watu nyakati za usiku, alikuwa msichana mrembo kwa kumwangalia lakini urembo wake ule ndiyo uliowamaliza wanaume wengi.

Watu wengi walipuuzia na hivyo kuendelea kupukutika mitaani. Wengi waliogopa lakini hakukuwa na mtu aliyethubutu kuacha kumchukua msichana mrembo kama alivyokuwa Maimuna ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kupeleka damu kule kuzimu.

Ndani ya miezi miwili, tayari wanaume kumi na nne walikuwa wameuawa na miili yao kukutwa ikiwa imekakamaa.

Miongoni mwa majini yote yaliyokuwa na roho mbaya, Maimuna alikuwa na roho ya kikatili, hakuwa na huruma hata kidogo kitu kilichompelekea kukusanya kiasi kikubwa cha damu na kukipeleka kuzimu.

Ndugu yangu! Unaposikia kuhusu majini, usitegemee kila jini atakuja huku akiwa kwenye utisho mkubwa, kwa hapa Tanzania, hasa mitaani kuna majini wengi mno wanaokatiza huku wakiwa katika maumbo ya kibinadamu, ni vigumu kuwajua.
 
82.

Niliendelea kubaki kuzimu kwa muda zaidi, mpaka hapo nilionyeshwa watu watatu au wanne ambao walikuwa na kazi kubwa ya kuhakikisha kazi ya Mungu aiendi sawa huku duniani na kwa kiasi kikubwa walikuwa wamefanikiwa kwani kama alivyotaka shetani ndivyo kile kilichokuwa kikiendelea kilivyofanyika.

“Tunataka kuondoka,” aliniambia Yusnath.
“Kwenda wapi?”
“Kwako!”
“Wapi?”
“Duniani!”
“Kwani tushamaliza?”

“Ndiyo! Sikutaka kukuonyeshea mengi kwa huyu Maimuna kwani bado anaendelea na kazi kubwa huko duniani, cha msingi, kuwa makini na wasichana warembo wa usiku wa manane,” aliniambia Yusnath.

“Sawa. Ila hukuniambia lengo la kunileta huku usiku huu.”
“Nilitaka kukuonyeshea haya, upate kuwaambia na wenzako wawe makini.”
“Mmmh!”

“Nini?”
“Wewe ni jini au binadamu?”
“Unanionaje?”
“Sijui nijibu nini, ila unaonekana kuwasaidia wanadamu, unanishangaza,” nilimwambia Yusnath ambaye alicheka sana, naweza kusema kwamba kicheko chake kilikuwa cha ajabu mno, kilinishtua sana, hapohapo akapotea, na mimi kujikuta nikiwa nimelala kitandani, yaani usiku uleule aliokuwa amenichukua, nikajiuliza sasa mbona siku haikubadilika na wakati nilitumia siku nyingi? Sikupata jibu.

Asubuhi nilipoamka, nikayabadilisha maisha yangu, kwanza sikutaka kumuamini mtu yeyote, leo hii ninapowasikia wachungaji wakijisifia sana kwamba wanatenda miujiza, huwa ninawachukia kwa kuamini miujiza anafanya Mungu peke yake na si binadamu.
 
83.

Ninaposikia kwamba maalbino wanauawa, najua wanasiasa wenye roho mbaya wapo kazini wakifanya mambo yao ya kikatili.

Ndugu yangu! Katika ulimwengu huu kuna mambo mengi sana hutokea, mengine yanaweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu ila mengine ni vigumu sana.

Tunachotakiwa ni kuishi katika misingi ya Mungu, wale wa kwenda kanisani, waende, na wale wa kwenda msikitini pia waende japokuwa hatutakiwi kuwaamini hata viongozi wetu kwani wengi wao huchukua nguvu kutoka kuzimu.

Hiyo ilikuwa safari yangu ya kwanza na ya mwisho kwenda kuzimu, ni miaka ishirini imepita, sikuwahi kuchukuliwa tena na kupelekwa huko mpaka leo hii ambapo nimemkabidhi Mungu maisha yangu na kuwa mchungaji katika Kanisa la Praise And Worship hapa jijini Dar.

Yusnath hakunitokea tena, na sikutaka kusikia kitu chochote kile kutoka kwake. Nilichokuwa najaribu kukwambia ni kwamba shetani yupo kazini, unapojikwaa tu, anatokea kwa ajili ya kukuchukua na kukutumikisha maisha yako yote.

Sisi kama watoto wa Mungu! Yatupasa tumwangalie Baba yetu ambaye ni Mungu na kuachana na uovu wote wa dunia hii.

MWISHO.
 
83.

Ninaposikia kwamba maalbino wanauawa, najua wanasiasa wenye roho mbaya wapo kazini wakifanya mambo yao ya kikatili.

Ndugu yangu! Katika ulimwengu huu kuna mambo mengi sana hutokea, mengine yanaweza kuonekana kwa macho ya kibinadamu ila mengine ni vigumu sana.

Tunachotakiwa ni kuishi katika misingi ya Mungu, wale wa kwenda kanisani, waende, na wale wa kwenda msikitini pia waende japokuwa hatutakiwi kuwaamini hata viongozi wetu kwani wengi wao huchukua nguvu kutoka kuzimu.

Hiyo ilikuwa safari yangu ya kwanza na ya mwisho kwenda kuzimu, ni miaka ishirini imepita, sikuwahi kuchukuliwa tena na kupelekwa huko mpaka leo hii ambapo nimemkabidhi Mungu maisha yangu na kuwa mchungaji katika Kanisa la Praise And Worship hapa jijini Dar.

Yusnath hakunitokea tena, na sikutaka kusikia kitu chochote kile kutoka kwake. Nilichokuwa najaribu kukwambia ni kwamba shetani yupo kazini, unapojikwaa tu, anatokea kwa ajili ya kukuchukua na kukutumikisha maisha yako yote.

Sisi kama watoto wa Mungu! Yatupasa tumwangalie Baba yetu ambaye ni Mungu na kuachana na uovu wote wa dunia hii.

MWISHO.
Baadae nikimaliza kazi nashuka nao
 
Shunnie naomba uache tabia ya kuiba hadithi zangu na kuposti huku. Naomba tu uache kabla hatujafika mbali dada angu.
 
Mtunzi: Nyemo Chilongani

Sehemu ya 01

Nilisimama juu ya mlima mmoja mkubwa, mawingu yalitanda angani huku radi zikianza kupiga mfululizo hali iliyoonyesha muda wowote ule mvua kubwa ingenyesha.

Nilikuwa nikiogopa sana, pembeni ya mlima ule mkubwa ambao sikujua nilifikaje, kulikuwa na miti mingi iliyosababisha giza kuwa kubwa kitu kilichoniongezea hofu nzito moyoni mwangu.

Sikuwa na msaada wowote mahali hapo, nilijaribu kuangalia huku na kule nikiamini ningeweza kupata msaada lakini hakukuwa na mtu yeyote. Wakati nikijiuliza nilifikaje hapo, ghafla nikaanza kusikia vishindo vikubwa vikija kule nilipokuwa. Sikujua vilikuwa vishindo vya nani, nikabaki nikitetemeka kwani nilijua huo ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yangu.

Mwili wangu ulikuwa ukitetemeka sana, nilitamani kukimbia kutoka mlimani hapo lakini kitu cha ajabu, sikuweza kukimbia, miguu ilikuwa mizito kuinuka, hivyo nikabaki nikiwa nimesimama tu.

Ghafla, nikawaona watu zaidi ya ishirini wakija mbele yangu, walikuwa ni binadamu wa kawaida ila walikuwa na muonekano wenye kutisha sana. Walikuwa watupu, viunoni walivaa vitu kama ukili, nyuso zao hazikuwa zikionekana vizuri.

Walikuwa wakinisogelea huku wakicheza wimbo ambao sikujua ulitoka wapi. Walikuwa wakiniangalia huku wakichekacheka kama watu wasiokuwa na akili fulani. Walitisha, nilitamani kuyafumba macho ili nisiweze kuwatazama lakini nilipotaka kufanya hivyo, nilishindwa pia.

Nikabaki nikiwa nimesimama, dakika ziliendelea kwenda mbele, cha ajabu, idadi hiyo ya watu haikuishia ishirini tu bali iliendelea kuongezeka mpaka wakafika watu zaidi ya sitini.

Baada ya dakika kama thelathini hivi, nikawaona watu kadhaa wakija pale niliposimama huku wakiwa wameshika beseni kubwa, nilipochungulia ndani, niliona damu nzito za watu, zilikuwa mbichi kabisa na kila aliyekuwa akizingalia, alionekana kuzitamani.

“Umeshawahi kunywa damu wewe?” aliniuliza mwanamke mmoja mtu mzima, alikuwa na umri usiopungua miaka sabini, alikuwa hajiwezi lakini ndiye aliyeonekana kucheza kwa nguvu kuliko wote mahali hapo.

“Sijawahi kunywa damu, na siwezi kunywa,” nilisema kwa sauti tena kwa kujiamini sana.View attachment 2482889

Kazi nzuri
L
 
76.

Usiku wa siku hiyo ndiyo ulikuwa wa kazi, mzee Hamisi alimchukia mno Ramadhani, na hakupenda hata kidogo. Aliamini mtu huyo ndiye aliyesababisha vyote vilivyotokea katika maisha yake vikiwemo vifo vya watu aliowapenda mno maishani mwake.

Siku hiyo alitulia chumbani kwake, hakutaka kuwasha taa yenye mwanga mkali, ilikuwa ni taa iliyokuwa na mwanga hafifu sana wa rangi nyekundu, alijifunika shuka jeusi tii huku ndani yake akiwa na karatasi iliyokuwa na maneno ambayo aliweza kuyatamka yeye tu kwa kuyasoma.

Chumba kizima kilinukia ubani tu, sauti yake ilisikika kwa chini sana. Ulikuwa ni usiku wa manane ambapo alitaka kufanya kazi yake ili kummaliza Ramadhani aliyeonekana kuwa nuksi kwa kile alichokuwa akikifanya.

Baada ya dakika kadhaa kelele zikaanza kusikika ndani ya chumba hicho, hakutaka kunyamaza aliendelea kuyazungumza maneno yale mpaka akajiona akianza kupaa juu chumbani mule na kuelea angani kitu ambacho hakikuwahi kutokea kabla.

Harufu ya ubani ule ikaongezeka zaidi, akaongeza kasi ya kuzungumza maneno yale, mara zile tunguli zilizokuwa ndani ya chumba kile zikaanza kuvunjikavunjika kuonyesha kwamba yale aliyokuwa akiyafanya chumbani mule yalikuwa na nguvu zaidi.

Ghafla, akajikuta akipotea, alipokuja kuibuka, akajikuta ndani ya chumba cha Ramadhani, wakabaki wakiangaliana tu kwani naye Ramadhani alijua kwamba mtu huyo angefika nyumbani hapo usiku huo.

“Nilijua tu ungekuja...hahaha...” alisema Ramadhani na kuanza kucheka.
Kilichofuata ni kuanza kupimana nguvu za kichawi.

Walibaki wakiangalia huku kila mmoja akianza kuzungumza maneno yake yenye nguvu tena kwa haraka mno kwani ndiyo yalikuwa maneno yenye nguvu ambayo mara nyingi huyatumia.

Ghafla, taa iliyokuwa ikiwaka, ikapasuka, vyombo vilivyokuwa kabatini vikaanza kuanguka kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea ndani ya chumba hicho tu.

Hawakuacha kuzungumza maneno ya ajabu, ghafla, Ramadhani akaanza kuzidiwa, akaanza kuzunguka huku na kule chumbani mule.

Mzee Hamisi hakutaka kunyamaza, tayari aliona huo ulikuwa nusu ya ushindi wake na alitaka kupambana mpaka pale atakapouona ushindi wenyewe.
Nitarudi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom