Simulizi: Safari Yangu Kuzimu

Simulizi: Safari Yangu Kuzimu

12

Kanisa lilianza kama utani, nakumbuka kipindi kile kulikuwa na washirika kama wanne, watu wengi waliokuwa wakipita karibu na kanisa lile, walishangaa ilikuwaje mchungaji awe na nguvu ya kutoa huduma na wakati watu walikuwa wachache sana.

Watu tulipuuzia, mchungaji yule ambaye alipenda sana kujiita mtume akaanza kuchapisha matangazo na kuyabandika mitaani kwamba alikuwa akiponya magonjwa mbalimbali, wanawake waliokuwa tasa waliitwa pia kwa ajili ya kuwekewa mikono na kupokea uponyaji.

Hilo halikuwafanya watu kulisogelea kanisa lile kwani kitu walichohitaji ni kuona miujiza ili waamini. Baada ya mwezi mmoja, watu walewale wanne waliokuwa ndani ya kanisa lile wakaanza kuwaambia watu wengine kwamba kulikuwa na miujiza ilikuwa ikitendeka hivyo watu wawapeleke wagonjwa kwa mchungaji yule.

Kama unavyojua binadamu kuna kitu kujaribu. Kuna mwanamke aliyekuwa akiishi karibu na mtaa uliokuwa na kanisa lile, miaka nenda rudi alikuwa na kibiongo. Watu walimuonea huruma lakini baada ya kusikia kile kilichozungumziwa kuhusu mchungaji na miujiza aliyotarajiwa kuitoa, mwanamke yule akaingia.

Sijui nini kilitokea kanisani lakini siku moja baadae nilipomuona mwanamke yule, hakuwa na kibiongo. Hapo ndipo watu walipoanza kuamini kwamba ile miujiza iliyokuwa ikitangazwa kweli ilikuwa ikifanyika, kanisa likaanza kujaza watu.

“Nilifahamu hilo tu, hebu niambie kingine nisichokijua,” nilimwambia Yusnath.
“Subiri,” aliniambia na kunipeleka sehemu iliyokuwa na kitu kikubwa kama televisheni na kuanza kunionyeshea maisha halisi ya mchungaji yule.

Lile kanisa halikuwa kanisa kama tulivyokuwa tukiliona, lilikuwa pango kubwa ambalo lilikuwa na muonekanao wa kichwa cha paka, mlangoni kulikuwa na miti mikubwa iliyokuwa imesimikwa huku juu yake kukiwa na mafuvu mawili ya binadamu na mafuvu mengine ya mnyama nisiyemfahamu.

Mlangoni hapo kulikuwa na mtungi mkubwa wa damu, kila mshirika aliyekuwa akiingia kanisa, ilikuwa ni lazima kuinama mlangoni kisha kuingia. Unapoinama pale mlangoni, unauinamia ule mtungi bila kujua na katika hali ambayo sikuifahamu, kuna kiasi kidogo cha damu unachangia katika mtungi ule.
 
13

Unajiona kwamba umevaa nguo lakini unapouvuka mlango wa kuingia kanisani, nguo zako zinaachwa mlangoni na wewe kuingia mtupu.

Kanisani mule hakukuwa na washirika tu bali kulikuwa na viumbe vingine vya ajabu ambavyo kazi zao zilikuwa zilezile za kuwavuta watu. Viumbe hivyo vya ajabu havikuwa ndani ya kanisa tu bali vilikuwepo mpaka pale nje.

Ushawahi kupita nje ya kanisa fulani, unasikia kuwa na hamu ya ghafla kuingia kanisani humo kwa ajili ya kuabudu? Yaani moyo wako unasisimka na kutamani zaidi uingie. Ndugu yangu, hiyo inakuwa ni kazi ya hivyo viumbe vya ajabu ambavyo husimama nje na kukuvuta wewe.

Nilimuona mchungaji yule akiwaombea watu, mkononi alikuwa na kitambaa cheupe, kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwapiga watu na kile kitambaa ambacho Yusnath aliniambia kwamba kilikuwa chao na walimpa kwa ajili ya kufanyia kazi hiyo.

Mtu anapopigwa na kitambaa kile, kwanza akili yake inachanganyikiwa, hakuna kitu kingine anachokipenda zaidi ya kuingia kanisani humo na huwa mtumwa wa moja kwa moja.

Mambo niliyokuwa nikiyaona ndani ya kanisa lile yalinishtua sana. Pembeni ya kiti cha mchungaji kulikuwa na joka kubwa, kazi yake ilikuwa ni kukaa hapohapo huku akiwaangalia washirika.

Ukiachana na joka lile, kulikuwa na joka jingine ambalo lilikuwa likitembea huku na kule, kazi yake kubwa ilikuwa ni kuwatemea watu mate ambayo Yusnath aliniambia kwamba mara unapotemewa mate yale, hata kama kuna mtu atakuja na kukwambia yule mchungaji ni mchawi, mzinzi, huwezi kuamini na unaweza kugombana na mtoa taarifa.

“Kumbeeee....” nilisema.
“Kumbe nini?”
“Nilipokuwa nikipita nje ya kanisa lake nilitamani kuingia,” nilimwambia.
“Hiyo ndiyo kazi ya vile viumbe, kuwavuta nyie tu.”

“Sawa. Kuna kingine?”
Hakutaka kuniambia hivihivi tu, alitaka kunionyeshea kila kitu kupitia televisheni ile.

Nilimuona mchungaji akichukua mafuta fulani hivi, alijipaka mikononi, alipokuwa akimuona mshirika mwanamke mzuri, alikuwa akimfuata na kumpaka mafuta yale na kumwambia kwamba yalitoka kwa Mungu kumbe hakuna lolote lile.
 
14

Baada ya kupakwa mafuta yale, akili ya msichana huyo inachanganyikiwa, muda mwingi anamuwaza mchungaji na mwisho wa siku kulala naye kitanda kimoja.

Kila nilichokiangalia, kilinifanya nichukie, nilikuwa mkristo, lakini sikuwa mtu wa kwenda kanisani lakini yale yaliyokuwa yakifanywa kwa baadhi ya makanisa likiwepo lile la mchungaji huyu, lilinisikitisha sana.

“Unajua watu wanaponywa vipi magonjwa yao?” aliniuliza Yusnath.
“Hapana! Inakuwaje?”
“Njoo huku,” aliniambia, akanishika mkono na kuanza kuelekea katika chumba kimoja.

Kilikuwa kikitisha sana, kulikuwa na maiti nyingi zilizokuwa zimetobolewatobolewa, sikujua za nini lakini nyingine zilivarishwa sanda nyeupe kabisa zisizokuwa na doa hata kidogo.

Chumbani mule kulikuwa na milio ya ajabu, wakati mwingine ilisikika milio ya paka na bundi, kila nilipoisikia, niliogopa sana. Yusnath hakutaka kujali, aliendelea kunishika mkono na kuelekea mbele zaidi huku sakafuni kukiwa na damu nyingi zilizokuwa zikinuka mno.

Tukafika sehemu moja iliyokuwa na uwanja mkubwa, sikujua kama ilikuwa makaburini au la, alichoniambia ni kwamba nisimame imara, nikatii, akaniambia kwamba kuna mambo mengine ya mtume huyo nitayaona, nikamwambia hakuna tatizo, hivyo nikaanza kusubiri huku mwili ukinisisimka mno kwani sehemu ile ilitisha sana.
***

Nilianza kuyaona mambo kama mtu anavyoona maono au kuota ndoto fulani hivi. Nilimuona mchungaji yule akiwa amevalia vazi la ajabu sana, lilionekana kuwa kama kaniki fulani nyeusi tii, uso wake ulikuwa tofauti kabisa kwani ulipakwa na vitu ambavyo vilionekana kama masizi.

Alitisha sana, nilimkazia macho kumwangalia kwa umakini kile alichokuwa akikifanya. Alikuwa amesimama katikati ya uwanja wa makaburi mawili, moja lilikuwa la mtoto mdogo na jingine likiwa na mtu aliyekuwa na ulemavu wa ngozi (albino).

Mchungaji yule alikuwa akizungumza maneno nisiyoyaelewa huku akichezacheza wimbo ambao sikuwa nikiusikia. Kuna kitu fulani kikaibuka ghafla juu ya kaburi lile la mtoto aliyekuwa na miaka minne kabla ya kufariki.
 
15

Nilikitolea macho kile kitu, sikuweza kukifahamu lakini alipokichukua na kukifunga mkononi mwake, nikagundua kwamba ilikuwa ni hirizi iliyofungwa kwa kitambaa chekundu.

Mchungaji yule aliendelea kukaa pale makaburini huku akizungukazunguka huku na kule, ghafla, likaja kundi la wachawi wengi, walikuwa na muonekano kama aliokuwa nao yeye, walimfuata na kuanza kuzungumza naye maneno mengi ambayo sikuweza kuyasikia.

Miongoni mwa watu wale waliokuwa wamemfuata, alikuwepo mtu ambaye nilimfahamu sana kwa sura, hakuwa mgeni kabisa machoni mwangu, alikuwa mchungaji mwingine ambaye naye nitakupa stori yake hapo baadae nikimalizana na hawa watu niliowaona kule kuzimu.

“Ninataka kuwa na washirika wengi zaidi,” nilimsikia mtume yule akisema kwa sauti ya juu huku wengine wakimsikiliza.
“Kingine?” aliuliza mchungaji yule.

“Ninataka niwe na mvuto mkubwa,” alisema mtume.
“Hakuna tatizo, subiri.”
Aliposema hivyo, watu wote wakainamisha vichwa vyao chini akiwemo huyo mtume mwenyewe.

Ghafla nikaanza kuona moshi mkubwa ukianza kufuka kutoka katika sehemu iliyokuwa na giza totoro, nilibaki nikiangalia na sikutaka kuyaamisha macho yangu.

Mara akatokea mzee fulani, alionekana kuwa dhaifu na mwendo wake ulionyesha aliumia mguu. Kwa kumwangalia tu, isingekupa wakati mgumu kugundua kwamba mzee yule alikuwa mchawi.

Alimsogelea mchungaji yule huku akiwa ameshika tunguli moja kubwa ambayo kwa juu aliifunga kwa kitambaa cheusi. Alipomfikia, akamwambia apige magoti, mchungaji akatii na kumuwekea tunguli ile kichwani mwake.

Alizungumza maneno ambayo nayo sikuyaelewa na mwisho wa siku kumgawia kisu mtume yule na kumwambia akichomeke kaburini, katika lile kaburi la mtoto mdogo, akafanya hivyo.

“Ninataka utoe kafara,” alisema mzee yule.
“Hakuna tatizo, nipo tayari bwana wangu,” alisema mchungaji.
“Chukua hii tunguli, kuna damu ndani yake, nyunyizia katika kaburi hilo.”
 
16

Sauti ya mzee yule haikuwa ya kawaida, alikuwa akizungumza huku ikisikika kuwa na utetemeshi mkubwa, mtume yule akachukua tunguli ile na kufanya kama alivyoagizwa.

Sikuwa nimejua kabla kama ndani yake kulikuwa na damu, akaanza kunyunyizia katika kisu kile kilichochomekwa kaburini, nikaanza kusikia sauti kutoka ndani ya kaburi lile.

“Unatoa kafaraaaaaaaaaaaaa....” niliisikia sauti hiyo vilivyo kabisa.
“Ndiyo bwana wangu.”
“Tunahitaji damu kutoka kanisani kwako.”
“Nipo tayari kutoa.”

“Chukua hicho kisu, ujikate na damu unyunyizie kaburini,” ilisikika sauti kutoka ndani ya kaburi lile.

Alichokifanya mchungaji ni kuchukua kisu kile na kufanya kama alivyotakiwa kufanya.

Damu yake ilipoangukia juu ya kaburi lile, wachawi wengine waliokuwa kaburini pale wakaanza kucheka kwa furaha kwani waliamini kwamba kila kitu kilikuwa kikifanyika.
.
.
Je, nini kitaendelea?
 
17

Baada ya tukio hilo la ajabu, nikaanza kuyaona maono mengine, nikatolewa kaburini na kuonyeshwa nikiwa ndani ya kanisa.

Taarifa zikaanza kuzagaa kwamba kulikuwa na msiba uliokuwa umetokea usiku uliopita, mshirika mmoja wa kanisa hilo alikuwa amefariki dunia katika kifo cha kutatanisha sana akiwa anachota maji.

Kwanza nikashangaa, sikujua chanzo cha kifo cha huyo mtu ila Yusnath alinikumbusha kwamba ile kafara iliyokuwa imetolewa kule makaburini, ilikuwa ni ya huyo mtu aliyekuwa amefariki dunia.

“Unasemaje?”
“Hiyo ndiyo kafara yenyewe. Kanisa hili limesimama kwa ajili ya makafara yanayotolewa kila leo,” alisema Yusnath huku akinitaka niendelee kuangalia kile kitakachoendelea kutokea kanisani.

Ndugu zangu! Kanisa linapokuwa halina nguvu za Mungu watu wengi wanaingia, tena wale wenye nguvu za aina tofautitofauti.

Kanisa lile halikuwa na washirika wa kawaida tu, bali washirika wengine waliingia wakiwa watupu kabisa tena wengine wakiwa na hirizi mikononi mwao.

Wachawi kwa kawaida huwanga usiku lakini ndani ya lile kanisa, mpaka mchana wakawa wanawanga.

Mchungaji huyo alipokuwa akisimama na kuhubiri, watu wengine walikuwa wakipigwa na pepo la uchovu na kujikuta wakianza kusinzia.

Hilo ndilo pepo kubwa lililowekwa kanisani, pepo la usingizi lilishika kasi zaidi kiasi kwamba hakukuwa na mtu yeyote aliyeelewa.

“Unamuona mchungaji alivyo?” aliniuliza Yusnath, nikayahamishia macho yangu kwa mchungaji.

“Mmmh!”
“Unaona nini?”
“Naona joka likihubiri...mhh! Mchungaji yupo wapi?” niliuliza huku nikiwa nimestaajabu sana.

“Hiki ndicho kinachotokea, si kila siku anahubiri mchungaji, wakati mwingine mtu anayehubiri huwa ni jini kutoka kuzimu, ila huwezi kujua hilo kama wewe si mmoja wetu,” alisema Yusnath.

“Ni kwa makanisa yote?”
“Hapana. Makanisa mengine yana Mungu wa kweli, hata kuyasogelea tunaogopa kwa kuwa tunaungua sana kila tunaposogea, ila haya yenye wafuasi wetu, ni rahisi kuingia kwa kuwa ni watu wetu. Na ndiyo makanisa yenye watu wengi zaidi kwani kazi yetu kubwa ni kuwavutia kanisani,” alisema Yusnath.

“Sasa mchungaji yupo wapi?”
“Swali zuri sana, ngoja nikuonyeshee,” alisema Yusnath.
 
18

Mara baada ya kuliona joka lile likiendelea kuhubiri kanisani pale, Yusnath akaamua kunichukua na kunipeleka sehemu ambayo sikujua ni wapi, sehemu ambayo nilijua kwamba ndipo kulipokuwa na yule mtume.

Safari hiyo wala haikuchukua muda mrefu, tulifika sehemu moja, ilikuwa porini sana, ilikuwa chini ya mti mmoja mkubwa wa mbuyu, chini ya ule mti kulikuwa na kitambaa kikubwa chekundu kilifungwa huku kukiwa na tunguli nyingi.

Ukiachana na hivyo, kulikuwa na michirizi mingi ya damu ambayo yote hiyo ilinifanya kuona kwamba sehemu ile haikuwa ya kawaida hata kidogo. Hakukuwa na mtu yeyote yule, sehemu ilikuwa kimya na ni upepo tu ndiyo uliokuwa ukisikika mahali hapo.
“Mchungaji yupo wapi?” nilimuuliza Yusnath.

“Subiri! Utamuona tu,” aliniambia.
Wala hazikupita sekunde nyingi, ghafla nikamuona paka mmoja mkubwa akija pale mbuyuni.

Paka huyu hakuwa wa kawaida kabisa, alikuwa na umbo la paka lakini uso wake ulikuwa ni wa binadamu.

Najua unaweza kushtuka kwamba ilikuwaje lakini hivyo ndivyo nilivyokuwa nikimuona. Mkononi mwake alivaa hirizi moja kubwa iliyokuwa na pembe nne ambayo ilikuwa nyeusi tii na kiunoni mwake alivaa ushanga mkubwa ambapo kila alipokuwa akitembea, ushanga ule ulikuwa ukiburuzika chini.

“Huyu ni nani?” niliuliza.
Hata kabla sijajibiwa swali langu, ghafla paka yule akaanza kuwa mkubwa, nilishtuka sana na ilikuwa kidogo tu nikimbie. Kadiri alivyokuwa akikua na ndivyo alivyobadilika na kuwa binadamu kamili.

Kila kitu kilichokuwa kikiendelea nilihisi kama naangalia filamu moja ya Kinaigeria, sikuwahi kuyaona mambo hayo kwa macho yangu mawili.

Alipokuwa mtu kamili, nikapigwa na bumbuwazi baada ya kugundua kwamba paka yule alikuwa ndiye yule mchungaji wa kule kanisani.

“Mungu wangu!” nilisema kwa mshtuko huku nikishika mdomo wangu.
“Usishangae.”

“Lazima nishangae, sikuwa nikitarajia kuona hili.”

“Huyu ndiye mchungaji, wakati joka likiendelea kuhubiri kanisani, yeye yupo huku,” aliniambia Yusnath huku akiniangalia usoni, tena kwa kunikazia macho.
“Huku anafanya nini?”
 
19

“Amekuja kuomba nguvu za kuliendesha kanisa. Ngoja nikwambie kitu kimoja,” aliniambia.

“Kitu gani?”
“Makanisa mengi yanayofunguliwa huwa na nguvu kutoka huku, wachungaji wapo kifedha zaidi na si kama zamani na ndiyo maana tunapata nguvu ya kufanya mambo yetu tupendavyo,” aliniambia, nikajifikiria, nikagundua kwamba lile alilokuwa akilizungumza, lilikuwa kweli kabisa.

“Kwa hiyo naye huyu ni mchawi?”
“Ndiyo! Ila mtu akipata nguvu zaidi, wakati mwingine anakuwa na uwezo wa kugeuka jini,” aliniambia, nikashtuka.
“Unasemaje?”

“Ndiyo hivyo! Huyu mchungaji ni mchawi wa kawaida sana, ila anasomea masomo maalumu, akimaliza, atakuwa na uamuzi wa kuchukua nguvu za kijini pia,” aliniambia, niliendelea kushangaa.

Wakati akiendelea kuniambia mambo mengi, nikashtukia kuona paka wengine wakija mahali pale, walikuwa wa rangi tofautitofauti, walikuwa wekundu, weupe na weusi na muonekano wao ulikuwa uleule.

Waliposogea mahali pale karibu na mchungaji yule, akawapulizia unga fulani na hapohapo paka wale wakaanza kubadilika maumbo yao na kuwa binadamu.

Niliwafahamu vilivyo, mmoja alikuwa mke wa mchungaji, mwingine alikuwa mchungaji msaidizi na mwingine alikuwa mwalimu wa kwaya.
“Mmmh!”
 
20

“Usishangae, hivi ndivyo tunavyofanya kazi yetu.”
“Naomba niulize swali.”
“Endelea.”

“Kama hawa wamekuja huku, kule kanisani wamebaki wakina nani?” niliuliza huku nikiwa na hamu ya kutaka kujua.
“Twende ukaone,” aliniambia na kisha kuyafumba macho yangu, nilipoyafumbua tu, tulikuwa kanisani.

Watu walikuwa bize na ibada, wakati joka lile lililokuwa na muonekano wa mchungaji likiendelea kuhubiri, watu wengi kanisani pale walikuwa wamesinzia kwani ile ilikuwa moja ya kazi ya kule kuzimu.

Sikutaka kujali sana, nilichokifanya ni kuyapeleka macho yangu na kuangalia kule ambapo mke wa mtu alipokuwa akikaa, sikuona mtu zaidi ya paka mkubwa mithili ya binadamu alikuwa amekaa huku lile joka likiendelea kuhubiri kama kawaida.

Nilishtuka, hakukuwa na mtu yeyote kanisani aliyekuwa akiliona hilo, nikayapeleka macho yangu hata kwa watu wengine wale waliokwenda chini ya ule mbuyu kule porini, nao walikuwa na muonekano uleule, walikuwa paka wenye maumbo makubwa mno. Nilibaki na mshangao uliojawa na hofu kubwa.
 
21

Uchawi upo ndugu yangu, tena umejaa sana katika nyumba za ibada. Kwa kile nilichokiona kwa mchungaji yule kiliyafumbua macho yangu na kuona kwamba hakukuwa na mtu aliyetakiwa kuaminika katika dunia hii.

Niliyoyaona yalitosha sana na hivyo kumwambia Yusnath kwamba alitakiwa kunitoa mahali pale na kunipeleka kule tulipotoka ili niweze kuwaona watu wengine, hilo halikuwa tatizo, akaniambia nifumbe macho, nikafanya hivyo na nilipofumbua tu, tayari tulikuwa tumefika.

Kwenye kundi lile la watu waliokuwa wamepiga magoti akiwemo mchungaji yule aliyependa kujiita mtume, kulikuwa na mtu mwingine ambaye nilimfahamu sana, alikuwa mwanasiasa mkubwa ambaye alipendwa na watu wengi.

Nilimwangalia, sikuamini kama na yeye alikuwa mahali pale, uso wangu ulionyesha kutokukubaliana na kile nilichokuwa nikikiona hivyo nikamuuliza Yusnath kama yule niliyekuwa nikimuona ndiye yule niliyekuwa nikimfahamu au macho yangu yalichanganya? Akaniambia ndiye mwenyewe.

Huyu alikuwa mwanasiasa mmoja mkubwa anayejulikana kwa jina la Abuzael John. Alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa wakitikisa sana Tanzania kutokana na umahiri wake katika kuteka akili za watu mara anaposimama jukwaani na kuzungumza.

Huyu naye alikuwa kule kuzimu akimuabudu shetani kitu kilichonishangaza sana. Yusnath alijua jinsi nilivyochanganyikiwa mara baada ya kumuona mtu huyo mahali hapo, hivyo alivyotaka kukifanya ni kunionyeshea maisha ya huyo mtu.

“Nataka nikuonyeshe maisha ya huyu mwanasiasa,” aliniambia.
“Sawa, hakuna tatizo.”

Kama kawaida akaniambia nifumbe macho, nilipofumbua baada ya sekunde kadhaa, tulitokea katika ule mlima wa kutisha ambapo mbele yetu kulikuwa na televisheni kubwa, ikawashwa na kuanza kumuona Abuzael akiwa ofisini kwake.

“Unataka kuona nini?” aliniuliza Yusnath.
“Nione jinsi anavyofanya kazi zake za kishirikina,” nilimjibu.
“Hakuna tatizo.

Subiri.”
Yusnath akafumba macho, sikujua alikuwa akifanya nini kwani alikaa kimya kwa muda fulani kisha kufumbua, nilipoyapeleka macho yangu katika televisheni ile, nikaona Abuzael akiwa sehemu moja iliyokuwa na msitu mnene.
 
22

Hapohapo Yusnath akanichukua na kuwa kule alipokuwa mwanasiasa yule yaani kila kitu alichokuwa akikifanya ni kama nilikuwa pembeni yake. Nilimuona akitembea huku akionekana kuwa na mawazo mno, alionekana kutokuwa na furaha hata kidogo.

Alitembea kwa mwendo wa taratibu sana, alipokuwa akielekea, sikuwa nikipafahamu. Alizidi kupiga hatua mpaka katika kijumba fulani kidogo kilichokuwa kimetengenezwa kwa udongo na nje ya nyumba ile kulikuwa na fimbo kubwa iliyokuwa imesimikwa.

Alichokifanya Abuzael ni kugeuka nyuma, akavua suruali yake na kuyaacha makalio nje kisha kuingia ndani ya nyumba ile kinyumenyume. Mpaka hapo nikapata jibu kwamba pale alipokuwa kulikuwa kwa mganga, hivyo na mimi nikaingia huku nikitaka kujua alikwenda kufanya nini.

Kilio chake kikubwa kwa mganga yule kilikuwa ni kupata ubunge tu. Aliongea huku akilalamika kwamba hakuwa akipendwa na watu wa jimboni kwake, wengi walimchukia na kumuahidi kwamba iwe isiwe asingeweza kurudi tena bungeni, yaani kipindi kile cha karibia na uchaguzi ndiyo ungekuwa wakati wake wa mwisho kuingia bungeni kule.

Alionekana kuhitaji sana msaada kwani hata uongeaji wake ulionyesha hilo. Mganga yule alimwangalia tu, kwa mtazamo alioutumia kipindi kile, ulionyesha kumuonea huruma mno.
“Ninataka ulete mkono wa albino,” alisema mganga yule huku akimkazia macho.

“Unasemaje?”
“Nadhani umenisikia, ukifanikiwa, utapata ubunge,” alisema mganga yule.
Abuzael alionekana kuwa na mawazo mno, hitaji alilopewa lilikuwa kubwa lakini hakuwa na jinsi, alitakiwa kufanya kama alivyoambiwa afanye.

Alimuamini sana mganga yule, nahisi ndiye aliyekuwa akimfanyia kazi zake katika kipindi alichokuwa akigombania kila uchaguzi na ndiyo maana alidumu sana katika ngazi ya ubunge.
 
23

Baada ya kuambiwa hivyo, mganga akamwambia ainuke na amfuate kule alipotaka kwenda, akamchukua na kuelekea naye porini zaidi.

Walitembea huku kila mmoja akiwa kimya, kwa Abuzael alionekana kuwa mwingi wa mawazo, bado kichwa chake kilikuwa kikifikiria ni kwa namna gani angeweza kupata nafasi ile ambayo alikuwa akiililia kila siku.

Walitembea mpaka walipofika katika mti mmoja mkubwa. Katika mti ule, kulikuwa na tunguli nne zilizokuwa zimefungwa vitambaa vyekundu huku kukiwa na kitambaa kikubwa kilichokuwa na rangi nyeusi, kilifanana na kaniki.

“Subiri tuite nguvu zaidi ili upewe dawa ya kufanya kutokugundulika,” alimwambia mganga yule na kuanza kuzungumza maneno yasiyoeleweka.

Katika kila kitu kilichokuwa kikiendelea, niligundua kwamba watu walikuwa radhi kufanya jambo lolote lile lakini mwisho wa siku wafanikiwe maishani mwao. Mbunge huyu alionekana kuwa na uchu wa madaraka, hakutaka kuwa mwananchi wa kawaida.

Alichekwa sana jimboni kwake, watu walisema hafai hata kidogo hivyo kuamua kumfuata mganga huyo aliyempa sharti ambalo kwangu lilikuwa kubwa ila kwake, nahisi halikuwa kubwa sana.

Aliendelea kubaki kimya huku mganga yule kiendelea kuzungumza maneno yasiyoeleweka, ghafla nikaanza kuona moshi mkubwa na mzito ukifuka kutoka katika kitambaa kile. Nikaogopa.
.
.
Je, nini kitaendelea?
 
24

Sikujua ni kitu gani kilikuwa kinaendelea mahali pale kwani kufuka moshi kwa kitambaa kile kulizidi kuniongezea hofu zaidi. Niliendelea kumwangalia mzee yule huku macho yangu wakati mwingine yakikiangalia kitambaa chake.

Ghafla nikaona kitu kama sura za watu zikitokea katika kitambaa kile. Mganga yule aliendelea kuzungumza maneno yasiyoeleweka na baada ya dakika chache, nikaona kitu kama kisu kikitokea chini ya mti ule mkubwa, kilikuwa kisu chenye makali pande zote na kilifungwa kwa kitambaa cheusi.

“Chukua hicho kisu,” alisema na hivyo mbunge yule kuchukua kisu kile.
“Unachotakiwa ni kutumia kukatia viungo vya albino kwa kisu hiki,” alimwambia.
“Ooppss...!”

“Pia nitakupa dawa ambayo utawaambia watu wote watakaohusika kuwateka albino wasionekana kirahisi, yaani wawe wanapoteapotea machoni mwa watu. Na kazi yote itakayofanyika, ni lazima uwepo,” alisema mganga yule.

Mzee yule mwanasiasa akapewa maelekezo yote aliyotakiwa kufanya mara baada ya kutoka mahali pale. Nilibaki nikimwangalia, watu walimchukulia kuwa mtu mpole na mara nyingi vyombo vya habari vilimpamba kwamba tangu nchi ipate uhuru hakukuwa na mtu aliyekuwa mpole bungeni kama yeye.

Watu hawakujua kama nyuma ya pazia mzee huyo alikuwa mtu mbaya. Mara baada ya kukabidhiwa kila kitu, akaondoka mahali hapo.

Hatukuishia hapo, Yusnath akaanza kunionyeshea mambo mengine ya huyu mzee, tayari alikuwa amewaita vijana wake na kuwapa maagizo kwamba alihitajika albino kwa ajili ya kumkata kiungo chochote kwa ajili ya kazi maalumu hivyo vijana wale wakaondoka kwa ajili ya kufanya kazi.

Ikaonyesha upande mwingine kwamba tayari vijana wale walikuwa mitaani katika mishemishe zao za kumvizia albino mmoja wa kiume kwa ajili ya kufanya kile walichokuwa wameagizwa.

Walikuwa wakijipitisha sana katika nyumba aliyokuwa akiishi albino huyo, baada ya dakika kadhaa alipotoka nje, wakajipaka unga maalumu ambao walipewa na yule mzee na mmoja wao kumfuata mtoto yule.

“We mtoto njoo,” alisema jamaa mmoja.
“Shikamoo kaka,” alisalimia mtoto yule.
“Marahabaaa....hujambo?”
“Sijambo.”
 
25

“Hebu twende huku,” alisema mwanaume yule.
Ndugu yangu, kila kitu kilichokuwa kikitokea nilikuwa nakifuatilia kwa macho yangu. Ule unga ambao alioupaka kijana yule na wenzake ulikuwa na mvuto fulani wa kichawi ambapo hata mtu gani angeambiwa amfuate, asingeweza kukataa.

Mbali na hivyo, hata kama wewe ungekuwa mahali hapo na kuwauona wakiondoka na mtoto huyo wala usingekuwa na hofu hata kidogo.

Walimchukua na kuanza kuondoka naye. Hakuonekana kuwa na wasiwasi hata kidogo, uchawi aliofanyiwa ulimfanya kuwaona watu wote kuwa ndugu zake kama walivyokuwa watu wengine, hivyo akaanza kutangulizana nao.

Walikwenda mpaka kwenye moja ya magari waliyokuja nayo na kuondoka naye. Moyoni nilihuzunika lakini Yusnath akaniambia kwamba nisihuzunike kwani kama ningefanya hivyo basi asingeendelea kunionyeshea mambo mengi zaidi.

“Usihuzunike...” aliniambia.
“Sasa nifanye nini kama naumia?”
“Fanya vyovyote lakini usihuzunike, kuna mengi nitakuonyesha,” aliniambia.

Kabla ya kuona kile kilichotokea mara nyingi albino walipokuwa wakichukuliwa, niliwalalamikia polisi kwamba ilikuwaje mpaka hao watu wasikamatwe? Lakini siku hiyo ndiyo nikagundua kwamba ushirikina unatumika sana.

Waliondoka na yule mtoto mpaka katika mkoa aliokuwa akitokea yule mzee na huko ndipo walipomwambia mzigo alioutaka ulikwishaletwa mahali hapo.
“Hakuna cha zaidi, fanyeni kazi,” alisema.
“Lakini na wewe si utakuwepo au?”
“Ndiyo! Ni lazima nishuhudie,” alisema na kisha kuelekea huko.

Ndugu yangu, naweza kukwambia kwamba katika dunia hii tuna watu wenye roho mbaya mno.

Madaraka yanatafutwa kwa nguvu sana, watu wanauawa kinyama kwa sababu ya fedha na vyeo. Ninachokuhadithia hapa, si kwamba nimehadithiwa bali ninakwambia kilichotokea na kukishuhudia kwa macho yangu.

Mpaka muda huo niliwaona watu wawili, mchungaji na mwanasiasa. Yusnath aliniambia kulikuwa na watu wa aina mbalimbali ambao duniani waliheshimika sana, hivyo sikutakiwa kuwa na haraka kwani angeniambia mmoja baada ya mwingine.

Baada ya kupelekwa alipokuwa yule mtoto, akaanza kukatwa mkono huku akiwa amefumbwa macho kwa kutumia kitambaa kizito ili asiweze kumuona mzee yule.
 
26

Alilia kwa maumivu makali, hakukuwa na mtu aliyemuonea huruma, walikuwa hapo kwa ajili ya pesa, walikuwa tayari kufanya kitu chochote kile lakini mwisho wa siku wapate kile walichokuwa wakikitaka.

Baada ya kuukata mkono wake na kuuweka pembeni huku damu zikimtoka mfululizo, wakamuacha apumzike na kusubiri hatua nyingine ya kuendelea kuchukua viungo vyake.
“Kuna chochote kinahitajika?” aliuliza kijana mmoja.

“Ndiyo! Tunahitaji miguu pia, unajua hawa watu ni mali sana, nikipata viungo vyote, nitavuiuza kwa wenzangu wengine,” alisema mzee yule na hivyo kuanza kuikata miguu ya mtoto yule.

Kila nilivyokuwa nikiangalia, mwili ulinisisimka mno, wakati mwingine nilitamani nisiendelee kuangalia picha ile ya kutisha kwani niliogopa mno lakini Yusnath aliendelea kunisisitizia kwamba nilitakiwa kuangalia kila kitu kilichokuwa kikiendelea mahali hapo.


***
Niliyoyaona, yalitosha kabisa, sikutaka kuendelea kuona zaidi kuhusu maisha ya mwanasiasa huyu bali kitu nilichokifahamu ni kwamba mwanasiasa huyo alikuwa mtu mbaya, katili ambaye hakutakiwa kupendwa hata kidogo.


Walimkata viungo vilivyobakia kitu kilichopelekea kifo cha yule mtoto, moyo wangu uliumia sana lakini sikuwa na jinsi, sikujua ni kwa jinsi gani ningeweza kumsaidia kwani nilichokuwa nikikiona pale hakikuwa kitu kilichokuwa kikitokea wakati huo, ni kama kilirekodiwa.
 
27

Nilimwambia Yusnath kwamba ninahitaji anitoe hapo na kama kulikuwa na mtu mwingine wa kumuona basi afanye hivyo, akanichukua na kunirudisha kulekule kuzimu, mtu ambaye alitaka kunionyeshea aliyekuwa mahali hapo ni mwanaume mmoja mwenye ndevu nyingi nyeupe.

Kwa kumwangalia usoni, hakuwa mpole lakini inawezekana alikuwa mkali hasa wakati wa kuongea. Nilimwangalia mzee yule, nilihisi niliwahi kumuona mahali fulani kwani hakuwa mgeni machoni mwangu, kila nilipomwangalia, nilihisi kwamba niliwahi kumuona sehemu japokuwa sikupakumbuka.

“Huyu ni mtu mwenye heshima kubwa, unamfahamu?”
“Hapana! Ila sura yake si ngeni machoni mwangu.”
“Anaishi Manzese Midizini,” aliniambia Yusnath.

Hapo ndipo nilipata kumbukumbu juu ya mtu huyu aliyekuwa amesimama mbele yangu. Niliweza kumgundua kwamba alikuwa shehe mkubwa aliyepewa cheo kikubwa na kusimamia msikiti mmoja maeneo ya Manzese. Kama ilivyokuwa kwa mchungaji yule aliyepita, hata huyu shehe naye alikuwa kule kuzimu.

Nilihuzunika sana, viongozi hawa wa dini hizi mbili walipewa majukumu makubwa ya kuwafanya watu kwenda peponi lakini mwisho wa siku, nao walikuwa kule kuzimu wakiendelea kumuabudu yule shetani.

Mzee huyu, kila siku ya Ijumaa alisimama mbele ya waumini wa dini hiyo na kuwasisitizia watu kwamba walitakiwa kumswalia Mungu. Ndugu zangu, kila nilichokiona kule kuzimu kilinisikitisha na kuona kwamba dunia ilipokuwa ikielekea si pazuri hata kidogo.

Sikutaka kujali sana, nilimwambia Yusnath kwamba nilitaka kuangalia maisha ya mzee huyo kama nilivyoyaona maisha ya mchungaji na mwanasiasa yule, hapo ndipo aliponichukua na kunipeleka kule kulipokuwa na televisheni.

Huko, nilimuona mzee yule akiwa amesimama sehemu moja iliyokuwa na giza totoro, alivalia kanzu yake kubwa na macho yake aliyapeleka juu huku akiongea maneno yasiyoeleweka. Nilijaribu kumwangalia mikononi nikagundua kwamba alikuwa na hirizi moja kubwa iliyofungwa na kitambaa chekundu.

Ilikuwa ni saa nane na nusu usiku. Yusnath akaniambia kwamba alikuwa akijiandaa kwa ajili ya kwenda kuswalisha. Alikaa katika hali ile kwa dakika kadhaa, ghafla nikaanza kusikia sauti za miungurumo, ilifanana na ile ya radi.
 
28

Huku nikiendelea kuangalia kila kitu kilichokuwa kikitokea, ghafla nikamuona mwanamke mmoja akija mbele yake. Alikuwa mzuri sana, naweza kusema kwamba sikuwahi kumuona mwanamke mwenye sura nzuri kama aliyokuwa nayo huyo.

Alimsogelea mzee yule aliyeyapeleka macho yake juu na kumshika ndevu zake. Ghafla, nikaanza kuona vitu kama shotishoti vikiiingia mwilini mwake kupitia ndevu zake zile.

“Ndiyo nini ile?” niliuliza.
“Anaingiziwa nguvu ili aendee kuwapoteza watu wengi zaidi duniani,” alinijibu Yusnath.

Sikiliza ndugu yangu, nilipelekwa kuzimu kwa kuwa kulikuwa na baadhi ya vitu nilitakiwa kuonyeshwa, nilitaka kufahamu mengi sana hivyo akaanza kuniambia mambo mengine kuhusu huyu mzee.

Heshima kubwa aliyokuwa nayo duniani ilionekana si kitu, alikuwa akisifiwa kutokana na ukarimu wake mkubwa lakini ukweli ni kwamba huyu mzee hakuwa lolote lile. Watu wengi walimheshimu, walimuita katika sherehe za Maulidi mbalimbali huku akipewa sifa kubwa lakini mtu huyo hakuwa kama watu walivyomfikiria.

Alikuwa mtu hatari ambaye kazi yake kubwa ilikuwa ni kuviua vyuo vya madrasa vingi kama moja ya njia zake za kuweza kusimamisha kazi zao.

Hiyo ndiyo ilikuwa kazi yake ambayo aliifanya mara kwa mara. Vyuo hivyo viliongezeka lakini hakukuwa na maendeleo yoyote yale. Ukiachana na hivyo, kulikuwa na misikiti mingi ambayo ilikuwa na kusudio la kuendelea zaidi lakini shehe huyu alikuwa na kazi moja ya kuhakikisha misikiti haikui zaidi.

Alisababisha roho chafu kwa watu wengine misikitini, unapoona watu wanagombana wenyewe kwa wenyewe, ilikuwa ni kazi ya huyu mtu. Hapo ndipo nilipoamini kwamba shetani alikuwa bize kuhakikisha kwamba kila kitu kinakwenda sawa kwa upande wake.

Migogoro mingi, majivuno na vitu vingine misikitini vilisababishwa na huyu mzee. Fedha zake zilitumika kujenga matabaka na kufanya vitu vingine.

Alipomaliza kupewa nguvu na mwanamke yule mrembo, nikamuona akiondoka mahali hapo, kuja kuonyeshwa, nilimuona akiwa amesimama katika uwanja mmoja mkubwa wa wazi, ulikuwa ni uwanja wa mpira wa miguu lakini sikujua ulikuwa maeneo gani.
 
29

Mzee yule alisimama akiwa mtupu huku mkononi akiwa na tunguli moja kubwa iliyofungwa kitambaa chekundu. Alikuwa akizungumza maneno ya ajabuajabu, mbali na ule mkono aliokuwa ameshika tunguli, mkono mwingine ulikuwa umeshika kuku mwekundu ambaye akamuweka chini kuanza kumchinja.

“Kwa nini anachinja kuku mahali hapa? Naye anahitaji kunywa damu?” nilimuuliza Yusnath.
“Hapana.”
“Sasa kwa nini anafanya hivyo?”
“Anatafuta nguvu ya ziada ya kusonga mbele.”

“Sasa kupitia kuku?”
“Ngoja nikwambie kitu, hakuna kitu chenye nguvu duniani kama kutoa kafara ya damu. Kitu kinapowekwa kwa kutumia damu huwa na nguvu sana.

Mtu anapotaka kuua kwa kutumia damu, kazi hufanyika kwa haraka sana, mtu anapotaka mafanikio kwa kutumia damu, hufanyika kwa haraka zaidi ya kitu chochote kile,” aliniambia Yusnath.

Niliwahi kusikia hilo kipindi cha nyuma kwamba kafara ya damu huwa na nguvu na hata Yusnath alivyokuwa akiniambia, nilikubaliana naye kwa asilimia mia moja kwamba huo ndiyo ulikuwa ukweli wenyewe.

Mbali na hayo aliyokuwa akiyafanya, mzee huyu alikuwa akifuga majini nyumbani kwake. Mambo mengi aliyokuwa akiyafanya, alielekezwa na majini hayo aliyokuwanayo.

Hakuwa mzee wa kuchezewa, alichokifanya Yusnath alitaka kunionyeshea roho mbaya ya huyu mzee. Ghafla nilimuona akiwa amesimama nje ya nyumba yake, aliangalia kitu ambacho sikukiona, uso wake ulikunjwa kwa hasira na hakutoa tabasamu hata kidogo.

Sikujua aliangalia nini lakini alionekana kuchukizwa na kitu fulani hivi. Huku nikiendelea kumwangalia, ghafla nikamuona kijana mmoja akija kule alipokuwa, alikuwa amekasirika na mkononi mwake alikuwa na panga.

“Wewe mzee nitakuua,” alisema kijana huyo huku akisimama, alionekana kuwa na hasira mno. Kila alipoongea, alimnyooshea panga lile.

“Na wewe nitakuua, tena kuwa makini kijana,” alisema mzee yule, hakuonekana kuogopa kitu chochote kile.

Kwa kuwa walikuwa wakiongea kwa sauti kubwa, watu waliokuwa pembeni waliposikia wakaanza kusogea kule walipokuwa na hatimaye vita vya maneno kuanza kuzuka mahali hapo, kila mtu alimpaa mwenzake vitisho vya kuuana tu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom