NimekaribiaKaribu mkuu
Day, mtihani kweli kweliSEHEMU YA 66
Kwa jinsi alivyoniambia niingie ilionekana kuwa rahisi sana, wala sikuogopa, nilihisi kwamba hakukuwa na mtu, nilipozama tu, macho yangu yakatua kwa wazee wawili, nahisi walikuwa wazazi wao, walikaa kibarazani kwenye viti wakipunga upepo, nilipoingia tu, wakayapeleka macho kwangu na kuniangalia.
Nilishtuka mno, kijasho chembamba kikaanza kunitoka, nilitamani kukimbia lakini nilishindwa kabisa.
Mzee huyo alikuwa akiniangalia huku akionekana kuhitaji kufahamu ni kitu gani nilikuwa nakihitaji nyumbani hapo.
Nikapiga moyo konde, nikawasogelea, nikawasalimia kwa heshima kubwa na kuwaambia kwamba nilikuja kumuona Esta.
“Wewe ni nani?” aliniuliza.
“Nasoma naye!” “Unasoma naye wapi?”
“Ardhi!”
“Unamjua Esta?” aliniuliza kwa ukali kidogo.
“Namjua!”
“Sawa. Stela! Kawaite dada zako,” alisema mzee yule.
Tayari nilijua kulikuwa na balaa hapo, yule mtoto akaingia ndani kwenda kuwaita. Nilibaki pale nje na wazazi wao huku nikiwa na hofu mno ila uso wangu ulikuwa kwenye tabasamu pana.
Baada ya dakika moja, yule mtoto akarudi na hao dada zake, nilipowaangalia moyo ukapiga paa. Yaani kama duniani kulikuwa na mapacha waliokuwa wanafanana basi hawa walikuwa balaa.
Walifanana, walikuwa wazuri kiasi kwamba nilichanganyikiwa.
Kilichotokea sasa, sikujua yule msichana ambaye nilikutana naye nje alikuwa yupi kwani hata nguo alikuwa amebadilisha.
Niliwaangalia kwa makini lakini sikumgundua kabisa, nikabaki nikishangaa.
“Aya mchukue huyo Esta uongee naye, si umesema unasoma naye,” aliniambia yule mzee kwa sauti ya kutaka kunikomoa, mtu mzima nikaloa, halafu watu wenyewe nilivyokuwa nikiwaangalia, wote walikuwa wakinishangaa.
Yaani ghafla nilitamani tu ardhi ipasuke nitumbukie ndani, au niwe mchawi, nipotee na nitokezee nyumbani kwangu kwani hata huyo Esta sikumjua ni yupi kati ya wale wawili waliosimama mbele yangu. *
*
*
Je, nini kiliendelea?
Noma sanamkuuNitaropoka Tu 'easta Lecture Wetu Amefariki', Huyo Atakayeshtuka Ndo Esta Mwenyewe
Nitaropoka Tu 'easta Lecture Wetu Amefariki', Huyo Atakayeshtuka Ndo Esta Mwenyewe
Ndo mmeanzaKhaaaa
Toka lini ww na story
Hahaaaahaaa...dahh!nimecheka hapo alipoambiwa aondoke nae estaSEHEMU YA 66
Kwa jinsi alivyoniambia niingie ilionekana kuwa rahisi sana, wala sikuogopa, nilihisi kwamba hakukuwa na mtu, nilipozama tu, macho yangu yakatua kwa wazee wawili, nahisi walikuwa wazazi wao, walikaa kibarazani kwenye viti wakipunga upepo, nilipoingia tu, wakayapeleka macho kwangu na kuniangalia.
Nilishtuka mno, kijasho chembamba kikaanza kunitoka, nilitamani kukimbia lakini nilishindwa kabisa.
Mzee huyo alikuwa akiniangalia huku akionekana kuhitaji kufahamu ni kitu gani nilikuwa nakihitaji nyumbani hapo.
Nikapiga moyo konde, nikawasogelea, nikawasalimia kwa heshima kubwa na kuwaambia kwamba nilikuja kumuona Esta.
“Wewe ni nani?” aliniuliza.
“Nasoma naye!” “Unasoma naye wapi?”
“Ardhi!”
“Unamjua Esta?” aliniuliza kwa ukali kidogo.
“Namjua!”
“Sawa. Stela! Kawaite dada zako,” alisema mzee yule.
Tayari nilijua kulikuwa na balaa hapo, yule mtoto akaingia ndani kwenda kuwaita. Nilibaki pale nje na wazazi wao huku nikiwa na hofu mno ila uso wangu ulikuwa kwenye tabasamu pana.
Baada ya dakika moja, yule mtoto akarudi na hao dada zake, nilipowaangalia moyo ukapiga paa. Yaani kama duniani kulikuwa na mapacha waliokuwa wanafanana basi hawa walikuwa balaa.
Walifanana, walikuwa wazuri kiasi kwamba nilichanganyikiwa.
Kilichotokea sasa, sikujua yule msichana ambaye nilikutana naye nje alikuwa yupi kwani hata nguo alikuwa amebadilisha.
Niliwaangalia kwa makini lakini sikumgundua kabisa, nikabaki nikishangaa.
“Aya mchukue huyo Esta uongee naye, si umesema unasoma naye,” aliniambia yule mzee kwa sauti ya kutaka kunikomoa, mtu mzima nikaloa, halafu watu wenyewe nilivyokuwa nikiwaangalia, wote walikuwa wakinishangaa.
Yaani ghafla nilitamani tu ardhi ipasuke nitumbukie ndani, au niwe mchawi, nipotee na nitokezee nyumbani kwangu kwani hata huyo Esta sikumjua ni yupi kati ya wale wawili waliosimama mbele yangu. *
*
*
Je, nini kiliendelea?
I Simulizi Very Mbaya Ishaniboa
naogopa kuibiwaJamani kwa nn sasa umemficha
huo mdomo wako kwangu unaingia mara 200Eeenh mm tena kibao kinanigeukia