Simulizi: Namtaka mpenzi wangu arudi

Simulizi: Namtaka mpenzi wangu arudi

SEHEMU YA 31

Hilo lilimpagawisha mno Dickson, alichanganyikiwa, hakuamini kama msichana huyo alimfanyia michezo hiyo ambayo alizoea kuiona katika filamu za kikubwa tu.

Hakuwa amewahi kutembea na mwanamke wa uswahilini, alizoea kutembea na wanawake wa ushuani ambao hawakuwa wakijua lolote lile, hawakujua jinsi ya kumpagawisha mwanaume faragha, hawakujua kufanya chochote zaidi ya kuwa gogo tu kitandani.

Amina alilijua hilo, alimfanyia utundu hapo kwenye kiti mpaka Dickson akachanganyikiwa, akili ikamruka na kuhisi kama alikuwa kwenye ulimwengu mwingine kabisa.

“Nakupenda mpenzi!” alisema Amina, tena alimwambia hilo sikioni kabisa huku akimpulizia na pumzi yake katikati ya sikio.
“Oooh! Aishiiiiii,” alijikuta Dickson akitoa sauti ya mhemko.

Hawakutaka kuchelewa, hapohapo akamchukua msichana huyo na kuelekea naye chumbani, walipofika, akamlaza kitandani na kuanza kuuchezea mwili wake.
“Subiri kwanza!” alisema Amina.
“Kuna nini?” aliuliza Dickson.

“Chini kumelowa!”
“Unamaanisha nini?”
“Nipo kwenye siku zangu. Leo ndiyo siku ya mwisho!” alisema Amina.

Dickson hakutaka kukubali, alitaka kuhakikisha kile alichoambiwa, Amina hakuwa na presha, akavua nguo zake na kumuonyeshea kile kilichokuwa kikiendelea huku akiwa amepaka tomato iliyokuwa na muonekano kama wa damu.

“Kwa hiyo?”
“Leo ndiyo inaisha! Naomba tufanye kesho bebi,” alisema Amina.
Dickson alichanganyikiwa lakini hakuwa na jinsi, akakubaliana naye, humo chumbani akabaki akiliangalia wowowo la Amina mpaka aliporidhika na msichana huyo kuondoka.

Walibaki wakiwasiliana kama kawaida, baada ya kumaliza, akampigia simu Linda na kumwambia kilichotokea.
“Wewe mwanamke kiboko! Hebu tuonane kwanza nikugawie kamera yenyewe.

Halafu hakikisha sasa hivi chumba unalipia wewe, chagua hoteli ya mbali kidogo, utategesha kamera, wakati akiingia, uanze kurekodi, hakikisha hiyo kamera inafichwa, mkianza kufanya mapenzi jifanye kama hutaki ili awe katika hali ya kukulazimisha, sawa?” alisema Linda.

“Sawa!”
“Nataka nimkomeshe huyu mpumbavu. Hawezi kuniacha kijingajinga,” alisema Linda na kukata simu. Wakapanga muda wa kuonana, wakaonana na kumkabidhi kamera hiyo. Kazi ikabaki kwa Amina kufanya kazi aliyokuwa amepewa.

Itaendelea
 
SEHEMU YA 32

Nandy hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alizoea sana kupokea simu kila wakati kutoka kwa mpenzi wake, Dickson na kumjulia hali lakini siku moja tu mambo yalikuwa ni tofauti kabisa. Alisubiri kuanzia asubuhi mpaka mchana lakini hakukuwa na simu yoyote iliyoingia kutoka kwa kijana huyo.

Alichanganyikiwa, alimpigia simu lakini kitu cha ajabu kabisa simu yake haikuwa ikipokelewa. Hakujua ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, aliogopa na kuhisi kwamba inawezekana mpenzi wake huyo alikuwa amepata tatizo.

Nyumbani hakukukalika, akaondoka kuelekea nyumbani kwa akina Dickson, alipofika huko, akamkuta mama yake, Natasha na kumuuliza kilichokuwa kikiendelea. Kama ilivyokuwa kwa Nandy, hata na yeye hakujua kitu chochote kile, akajaribu kumpigia simu mtoto wake huyo lakini matokeo yalikuwa kama ya Nandy kwamba simu haikupokelewa.

Wakahisi kulikuwa na tatizo, akawapigia marafiki zake chuoni, hao ndiyo waliomwambia kwamba hakukuwa na tatizo lolote lile na inawezekana kwamba simu alikuwa ameiacha hosteli na ndiyo maana hakuwa akipokea.
“Mna uhakika hakuna lolote baya huko?” aliuliza Natasha.

“Hakuna mama! Dickson yupo safi tu, aliondoka hapa kama dakika ishirini zilizopita,” alisema kijana aliyekuwa akiongea naye kwenye simu.
“Na alikuwa na simu yake?”
“Hapana! Nahisi aliiacha hosteli. Hutakiwi kuhofia lolote mama, Dickson yupo salama kabisa,” alisema kijana huyo.

Hilo kidogo likamfanya mama yake kushusha presha na kumwambia Nandy kwamba hakukuwa na jambo baya lolote lile kwani Dickson alikuwa salama kabisa na kuhusu kutokupokea simu zao iliwezekana aliisahau simu yake hosteli.

Wakati Nandy akipiga simu si kwamba Dickson hakuiona, aliiona, mawazo yake hayakuwa kwa msichana huyo kipindi hicho, moyo wake ulichanganyikiwa na wowowo la Amina, aliiacha simu hiyo kwani kama angeipokea ilimaanisha kuwa angechanganya vitu viwili kwa wakati mmoja.

Hata mama yake alipokuwa akipiga, alihisi kabisa kwamba baada ya Nandy kutokupokea simu zake alikwenda nyumbani kwao na mama yake kujaribu kumpigia, hivyo alichokifanya hata naye hakumpokelea.
 
SEHEMU YA 33

Hiyo ilikuwa siku ya kwanza na hata ile iliyofuata ambayo ndiyo ilikuwa ni kuonana na Linda, hakupokea simu yoyote ile. Wakakutana hotelini na kuagana, siku ya tatu pia ambayo ndiyo ilikuwa ya kufanya ngono, hakutaka kumpigia simu Nandy, hakuwasiliana naye kwa siku mbili mfululizo lakini moyo wake wala haukujishtukia, kwake aliona kila kitu kipo sawa kabisa.

Amina akampigia simu na kumwambia kwamba walitakiwa kuonana katika Hoteli ya Las Vegas iliyokuwa Sinza, jiji Dar es Salaam, hilo halikuwa tatizo kwa Dickson, hata kama hakuwa akiifahamu hoteli hiyo alihisi kabisa kwamba angeelekezwa mpaka kufika huko.

Muda ulipofika, hakutaka kuchelewa, haraka sana akaingia ndani ya gari na kuelekea katika hoteli hiyo ambapo baada ya dakika ishirini, akafika na kulipaki gari sehemu ya maegesho na kuelekea ndani ambapo baada ya kusema kwamba kulikuwa na mteja wake na kumtaja jina, Amina akapigiwa simu na kuambiwa aelekee katika chumba hicho.

Amina alifika mapema kabisa mahali hapo huku akiwa na mkuba wake, akaomba chumba na kuambiwa kwamba vyumba viivyobaki vilikuwa vya shilingi elfu hamsini kwa usiku mmoja, hilo halikuwa tatizo, akalipia na kupewa ufunguo, akaanza kuelekea huko.

Pale mapokezi, kulikuwa na wanaume kadhaa waliokuwa wamekaa, Amina alivyoingia, kwanza kwa uzuri wake, aliwadatisha na hata alipogeuka na kuwaonyeshea wowowo lake, kila mmoja udenda ukamtoka.

Hawakuamini kama kungekuwa na mwanamke nchini Tanzania aliyekuwa na wowowo kama lake, alidatisha, alionekana kuwa mtamu, kila mwanaume alichanganyikiwa na kubaki wakimtumbulia macho huku mioyoni mwao wakimuonea wivu mwanaume aliyekuwa akienda kulala naye chumbani.

Amina alijua kuwatega wanaume, alijua kabisa kwamba pale mapokezini wale wanaume walikuwa hoi, alichokifanya ni kujishembendua, kulitingishatingisha kitu kilichoonekana kuwapagawisha zaidi.

Akaelekea chumbani, alipofika, akachukua mkoba wake, akaufungua na kutoa kamera ndogo, ilikuwa imekwishachajiwa na ndani kulikuwa na kadi kabisa. Akaelekea kwenye kabati, akafungua mlango wa kabati hilo la kuwekea mataulo na kuiweka kamera ile na kumpigia simu Dickson.
 
SEHEMU YA 34

Wakati alipopigiwa simu kuonyesha kwamba tayari Dickson alifika, akaiwasha kamera hiyo na kuanza kurekodi. Mahali ilipokuwa, ilikuwa ni vigumu sana kwa mtu kuweza kuiona, baada ya dakika mbili, mlango ukaanza kugongwa, alipofungua macho yake yakatua kwa mwanaume huyo.

Kwa jinsi alivyokuwa amevaa taulo, Dickson alichanganyikiwa, alimwangalia kwa nyuma, wowowo lake lilikuwa likicheza na wakati mwingine kama lilitaka kudondoka.

Akamchukua na kumpeleka kitandani, pale, wakaanza kuongea, kichwa cha Dickson kilikuwa kikifikiria ngono tu, alitamani kumlalia Amina na kuanza kufanya naye mapenzi. Walizungumza kwa dakika chache, Dickson akashindwa kuvumilia, akaanza kumshika Amina huku na kule.

Kwa kuwa ulikuwa ni mchezo, akaanza kujikatalisha, kila alipoguswa, alikataa lakini Dickson akashindwa kumuacha. Amina alijua kuigiza, alikuwa akijifanya kukataa kataa lakini Dickson hakutaka kumuacha.

“Bebi! Nifikishe kileleni kwanza,” alisema Amina huku akimwangalia Dickson, mikono yake ni kama ilikuwa ikiendelea kukataa kufanya mapenzi na mwanaume huyo.

“Kivipi?” “Nipige vibao, nipige vibao shavuni, humo ndipo zilipokuwa,” Alisema Amina huku akiendelea kumzuia Dickson kumtoa taulo lile.

Hilo halikuwa geni kwa Dickson, aliwahi kukutana na wanawake ambao walikuwa na stimu kila kona, wengine videleni, wengine mikononi, wengine sikioni, hata alipoambiwa kwamba ampige vibao vya shavu akaanza kumpiga.

Amina aliumia lakini hakuwa na jinsi, hilo ndilo lilikuwa lengo lake, alipopigwa, akaacha kumzuia, akajilaza na kumwachia Dickson afanye lolote lile alilolitaka.
Walifanya huku Amina akiendelea kujifanya kama anakataa, siku hiyo hakuonyesha ushirikiano wowote ule kwa kuwa kamera ilikuwa ikiendelea kuchukua video.

Dickson alipomaliza, akaondoka na kwenda kuoga na huku nyuma Amina akaichukua kamera na kuizima.
Hiyo ilikuwa siku ya kwanza, akamfuata Linda na kumwambia kwamba alifanikiwa na hivyo kumpa ile kamera na kumuonyeshea jinsi ilivyokuwa.

“Safi sana! Chukua hii,” alisema Linda huku akimpa bahasha ya kaki iliyokuwa na pesa.
 
SEHEMU YA 35

Walimalizana na kila mtu kuondoka zake. Kwa Amina, hakutaka kumuacha Dickson, kwake, mwanaume huyo alikuwa mzuri kupita kawaida. Alipoachana na Linda, haraka sana akamtafuta Dickson na kuanza kuongea naye.

“Upo wapi?” aliuliza Amina.
“Njiani naelekea chuo.” “Naomba utafute chumba, nataka kuja kukuonyeshea ushirikiano mpaka ushangae,” alisema Amina.

“Kweli?”
“Niamini!”
Japokuwa alikuwa akielekea chuo, akakata kona na kuanza kutafuta hoteli. Hakuchukua muda akaipata moja na kuchukua chumba na kumuelekeza Amina kwenda kule.

Alipofika, akamuulizia na kuruhusiwa. Muda huo ndiyo walifanya mapenzi ambayo Amina alikuwa akiyataka, alimvuruga Dickson kiasi kwamba hakuona kama kungekuwa na mwanamke mwingine wa kumtenganisha na Amina kwani alijua kuzichezea nyonga zake kupita kawaida.

Walipomaliza, wakapumzika, siku hiyo Dickson hakurudi chuo, akabaki hotelini na msichana huyo mpaka siku iliyofuata.
Kwa usiku mzima, Nandy alikuwa akipiga simu lakini hakuwa akipokea, aliiangalia tu na kuipuuzia lakini kwa wakati huo mtu aliyekuwa akimfikiria alikuwa Amina tu.

Asubuhi ya siku hiyo, wakarudia tena, mchana, wakafanya tena na kisha kuagana. Moyo wake ukaridhika, kufanya mapenzi na msichana huyo kulimfanya kujisikia furaha kupita kawaida.

Ilipofika saa kumi na mbili jioni, Nandy akampigia tena simu. Kitendo cha kuiona namba ile, moyo wake ukapiga paaa! Hakuamini kama zilipita siku tatu hakuwa amepokea simu ya msichana huyo, akajisikia hukumu nzito moyoni mwake, maumivu aliyoyasikia yalimshangaza, akabaki akitetemeka, hapohapo akaipokea.

“Dickson!” aliita Nandy, sauti yake haikuwa vigumu kugundua kwamba alikuwa amechanganyikiwa.
“Ndiyo mpenzi!”
“Mbona nimekupigia sana simu na hukuwa ukipokea? Kuna nini?” aliuliza Nandy.
“Nani? Mimi?”

“Dickson! Kwani naongea na nani hapa?”
“Niliibiwa simu!”
“Uliibiwa simu? Unanidanganya!”
“Sikudanganyi! Niliibiwa simu mpenzi!”
“Unanidanganya Dickson, unanidanganya,” alisema Nandy na kukata simu.

Dickson alichanganyikiwa mno, moyoni mwake kukawa kunasikika sauti zaidi ya moja zikimlaumu kwa kumwambia kwamba alifanya kosa kubwa mno kumsaliti Nandy ambaye alijitolea kwa mapenzi ya dhati kuwa naye.
 
SEHEMU YA 36

Dickson alikuwa akitetemeka, kijasho chembamba kikaanza kumtoka. Ilikuwa ni lazima kuonana na Nandy kwani aliamini kwamba endapo asingeonana naye basi hali ingekuwa mbaya zaidi.

Akaondoka hosteli na kuelekea nyumbani kwa akina Nandy, alipofika, akapaki gari lake na kuingia ndani. Akamkuta Nandy akiwa peke yake, alikuwa kwenye meza ya kujisomea huku akisoma Biblia.

Machozi yalikuwa yakimtoka na kutiririka mashavuni mwake. Alijiona akipitia katika kipindi kigumu kupita kawaida. Akaanza kuyasikia maumivu ya mapenzi ambayo alizoea kuyasikia yakizungumziwa na watu wengine.

Alitamani kujiua, alitamani kuondoka nyumbani na kukimbilia sehemu ambayo kusingekuwa na mtu yeyote yule ambaye angempata.

Dickson akamsogelea mahali pale, akamkumbatia. Japokuwa Nandy alikuwa na hasira, moyo wake ulikata tamaa, akajikuta akiitanua mikono yake na kumkumbatia Dickson huku akilia kama mtoto mdogo.

“Naomba unisamehe mpenzi,” alisema Dickson, naye kwa jinsi moyo ulivyokuwa ukiuma kwa kumsaliti msichana huyo mrembo, akajikuta akianza kulia.
“Why are you doing this to me?” (kwa nini unanifanyia hivi?) aliuliza Nandy.

“I am sorry! Forgive me hubby,” (Samahani! Nisamehe mpenzi) alisema Dickson.
Alimuahidi mpenzi wake huyo kwamba kamwe asingemuumiza, asingemdanganya, kitendo cha kuvunja ahadi yake kiliufanya moyo wake kuwa na maumivu makali kupita kawaida.

Aliendelea kumuomba msamaha lakini hakumwambia ni msamaha kwa jambo gani baya alilokuwa amelifanya. Waliendelea kukumbatiana kwa dakika kadhaa, wakaachiana.

“Kulikuwa na nini?” aliuliza Nandy huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Simu yangu iliibiwa chuoni, kwa siku mbili, leo ndiyo nimeletewa baada ya jamaa kuiiba halafu akawa hajaizima, hivyo nilitumia GPS kuitafuta mpaka kufanikiwa,” alisema Dickson, japokuwa alikuwa akidanganya lakini ilikuwa ni vigumu kugundua kama alikuwa akidanganya.

“Nandy! Ninakupenda mpenzi! Ninataka nikuoe, ninataka uwe mke wangu! Naomba uniahidi kitu kimoja, utakuwa tayari tuoane na kuishi pamoja?” aliuliza Dickson.

“Ndiyo! Nakupenda pia mpenzi,” alisema Nandy ambaye alionekana hajiwezi kwa mwanaume huyo.
 
SEHEMU YA 37

Wakakumbatiana tena. Moyo wa Nandy ulikuwa na furaha kupita kawaida. Huku wakiwa katika hali hiyo, simu ya Dickson ikaanza kuita, akaichukua simu hiyo, macho yake yakakutana na namba ngeni, akaipokea, akashtuka alipoisikia sauti ya Linda.

“Dicky! Ninahitaji kuonana nawe! Kuna jambo nataka tuzungumze,” alisema Linda.
“Jambo gani?”
“Kuhusu kesi yako!”
“Kesi yangu! Kesi gani?” aliuliza Dickson huku akionekana kushtuka.
“Kesi ya ubakaji!”

“Hebu subiri kwanza!” alisema Dickson, akakata simu na kumwangalia Nandy huku akionekana kuogopa.
“Kuna nini bebi?” aliuliza Nandy.
“Kuna tatizo!”
“Tatizo gani?”

“Kuhusu kesi ya simu hii! Hebu subiri nikalimalize hili tatizo,” alisema Dickson huku akionekana kushtuka.
Hakutaka kubaki mahali hapo, kile alichoambiwa kilimchanganya mno.

Akamuaga Nandy na kuondoka mahali hapo, akaingia ndani ya gari na kupotea.
Njiani alikuwa na mawazo, hakujua ishu ya ubakaji aliyokuwa ameizungumzia Linda, alipofika njiani, akasimamisha gari na kumpigia simu Linda.

“Nimebaka! Nimembaka nani?” aliuliza Dickson.
“Kuna msichana anakufungulia kesi, umembaka hotelini!”
“Yupi?”

“Subiri,” alisema Linda, hapohapo akamtumia video waliyokuwa wamefanya mapenzi kwa mara ya kwanza.
Kwa jinsi ilivyoonekana, ilikuwa ni rahisi kuonekana kama alikuwa akimbaka, kwa jinsi Amina alivyokuwa akijifanya kukataa kufanya mapenzi, kwa jinsi alivyokuwa akimpiga vibao, ilionekana kama alikuwa akilazimisha penzi na mbaya zaidi video hiyo ilitolewa sauti.

“Mungu wangu! Amina!” Alisema Dickson kwa mshtuko, alipojaribu kumpigia simu msichana huyo, haikuwa ikipatikana na wakati akijiuliza kuhusu jambo hilo, akatumiwa ujumbe mfupi na Linda uliosomeka: “Nitahakikisha mpaka unafungwa gerezani miaka thelathini ushike adabu ya kuwadhalilisha wanawake kingono”
Dickson akaogopa.

Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 38

Mapigo ya moyo wa Dickson yalikuwa juu, hakuamini kile alichokiangalia kwamba alikuwa na msichana chumbani na kuanza kumbaka. Hapo ndipo alipogundua kuwa siku ya kwanza Amina kumpigia simu hakumpigia kwa bahati mbaya na kumuulizia rafiki yake, Ashura bali alipiga kwa makusudi na alimjua kabisa mtu aliyekuwa akimpigia.

Alipigwa na butwaa, kila alipokuwa akiiangalia video ile alionekana kabisa alikuwa akimbaka Amina kwani hakutulia, ni kama alikuwa akimzuia kufanya kitendo kile, tena na vile vibao alivyokuwa amempiga ndiyo kabisa vilimchanganya.

Hakutaka kuliacha suala hilo hewani, akampigia simu Amina, msichana huyo alipopokea tu, kitu cha kwanza kilikuwa ni kumshutumu kwa kile alichokifanya kwamba hakikuwa cha uungwana kwani walikubaliana na hakumbaka kama video zile zilivyoonyesha.

“Amina! Mimi nilikubaka wewe?” aliuliza Dickson huku akionekana kuchanganyikiwa.
“Nani?”
“Si naongea na wewe,” alisema Dickson huku akionekana kuwa na hasira kupita kawaida.

Amina hakujibu swali hilo, akakata simu. Dickson hakukubalia, akampigia tena, haikupokelewa, hakukoma, alimpigia zaidi na zaidi, haikupokelewa na mbaya zaidi simu ikazimwa.

Hiyo ndiyo ikaonekana kuwa sababu kwa Linda kuanza kumsumbua Dickson, alimwambia kwamba amekwisha kwani ile video angeipeleka polisi na ingetumika kuwa kama ushahidi kwa kile kilichotokea.

Dickson akaanza kuomba msamaha kwani aliamini kwamba kama Linda angeipeleka video ile katika kituo cha polisi na msichana huyo kupelekwa kituoni, basi kesi ingekuwa kubwa na angeweza kufungwa gerezani.

“Linda, unataka nini kwangu?” aliuliza Dickson, alionekana kuchanganyikiwa.
“Kwa nini umenisaliti?” aliuliza Linda.
“Sikukusaliti!”
“Kumbe umefanyaje?”

“Mbona nipo kawaida tu mpenzi! Sijakusaliti!” alisema Dickson.
“Nataka unijibu swali moja, unanipenda?”

Dickson akaa kimya kwa sekunde kadhaa, hilo lilikuwa swali gumu sana kumjibu msichana huyo. Moyoni mwake, hakuwepo kabisa lakini alihisi kabisa kwamba kama angemwambia ukweli kuwa hakuwa akimpenda basi video ile ingefika katika kituo cha polisi na hivyo kupelekwa mahakamani.
 
SEHEMU YA 39

Hakuwa na jinsi, ni kama alikamatwa na kufungwa sehemu, swali hilo likajibika kirahisi sana kwamba kweli alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati na hakukuwa na mwanamke mwingine zaidi yake.

“Nakupenda,” alijibu Dickson, jibu ambalo lilionekana kama kulazimishwa.
“Nataka unioe,” alisema Linda.
“Unasemaje?”
“Si umesema unanipenda, nataka unioe,” alisema Linda.
“Linda!”

“Basi subiri niipeleke hii video polisi halafu wao utajua cha kuwaeleza,” alisema Linda.
Dickson akatishika, moyo wake uliogopa, hakukuwa na kitu alichokuwa akikiogopa kama gereza. Alimuomba sana msamaha Linda na kumwambia kwamba angefanya lolote lile lakini kile kilichokuwa kimetokea kiendelee kuwa siri na ikiwezekana baada ya harusi video zifutwe.

Walizungumza mambo mengi, japokuwa Dickson hakuwa akipenda kuzungumza na msichana huyo lakini hakuwa na jinsi, alikubaliana naye ingawa moyo wake haukuwa kwa msichana huyo hata kidogo.

Kuanzia muda huo Dickson hakuwa na furaha tena, moyo wake ulikuwa na huzuni tele, aliamini kwamba kila kitu kilichokuwa kimetokea kilikuwa kimepangwa, hakutaka kukubali, ilikuwa ni lazima kuzungumza na Amina amwambie ni kitu gani kilikuwa kikiendelea, alipompigia simu msichana huyo, akaambiwa kwamba namba ilikuwa imefungiwa.

Akawa na mawazo tele, tamaa zake zilimkosesha furaha, tamaa zake zilimfanya kujuta kwani kwa kile kilichotokea kilikuwa ni kitu kibaya, cha kipumbavu ambacho alijiahidi hatokuja kukifanya tena maishani mwake.
Alipokutana na Nandy, hakumwambia ukweli, alikuwa mnyonge mno na msichana huyo alipomuuliza, alimwambia kwamba alikuwa akiumwa lakini hakukuwa na jambo baya lolote lile.

Linda alikisumbua kichwa chake, hakumpenda, msichana ambaye alitamani kumuoa maishani mwake hakukuwa na mwingine zaidi ya Nandy ambaye aliamini kwamba alikuwa akimpenda kwa moyo wa dhati.

Siku zikakatika, Linda hakutaka mambo hayo yaishe, akamwambia Dickson kwamba alitaka kuonana naye, kweli wakaonana na kuanza kuzungumza. Ni kama Dickson alikuwa ametegwa, kila alichoambiwa alikuwa akikubaliana na msichana huyo kwa sababu tu alikuwa na kitu ambacho kingehatarisha maisha yake.
 
SEHEMU YA 40

Video zile ziliendelea kutumika kama silaha ya kulipata penzi la mwanaume huyo. Hakutaka kuishia hapo, alichokifanya ni kwenda kuwalipa polisi kiasi kikubwa cha pesa na kuwaambia kwamba walitakiwa kujifanya kama wanafahamu kuhusu Dickson na hivyo kutakiwa kumkamata.

Hilo likafanyika, siku moja Dickson akiwa chuoni alifuatwa na polisi na kuanza kuzungumza nao. Ilikuwa vigumu kugundua kama polisi hao walikuwa wametumwa, walizungumza na Dickson na kumwambia kuhusu kilichokuwa kikiendelea.

Kijana huyo akaogopa, mapigo yake ya moyo yalikuwa yakidunda kwa nguvu na kuona kabisa kwamba huo ndiyo ungekuwa mwisho wake. Wakamchukua, wakamfunga pingu na kuondoka naye.

Njiani walikuwa wakizungumza naye, Dickson alilia, macho yake yalikuwa mekundu, hakuamini kama alikuwa akienda polisi na mwisho wa siku kufungwa gerezani kwa kesi ya kubaka.
Aliomba msamaha sana lakini hakukuwa na mtu aliyemsikiliza.

Walichukua dakika kadhaa wakafika polisi na kumuweka rumande. Humo ndani alikuwa mtu wa kulia tu, hakuamini kile alichokuwa akipitia kwamba mwisho wa siku alikuwa njiani kwenda gerezani, moyo wake ulimuuma, aliendelea kuomba msamaha mpaka pale alipoambiwa kwamba alitakiwa kutolewa kwa kuwa kuna mtu alikuja kumuwekea dhamana.

Hakujua ni mtu gani, akatoka mahabusu na kwenda kaunta, macho yake yakagongana na macho ya Linda aliyekuwa kwenye sura ya huruma, akamsogelea na kumkumbatia.

Kitendo cha kukaa kwa saa mbili tu mahabusu alichanganyikiwa, aliiona dunia kuwa mpya kabisa, maisha ya mahabusu hayakuwa mchezo, yalimvuruga na kupata picha ya maisha ya gerezani kama tu angekwenda huko.

“Hii ni kesi kubwa sana Dickson, ila nitaizima baada ya kufunga ndoa,” alisema Linda huku akimwangalia mwanaume huyo.
“Kweli?”
 
Hili li dikson ni lifala kwa nn lisirekodi mazungumzo yake na Linda?..poor Nandy !..good job shunie!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom