Simulizi: Namchukia Mama Yangu

Aisee story tamu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tuendelee eeee, naiona harufu ya mimba kutoka
 
Huku mambo bado ndo maana huwa napenda nikute imeisha
 
Sehemu ya 20

Pia sikutaka kumzuia kwa vile nilikuwa naye kwangu kwa wiki moja na nusu kitu ambacho kilikuwa hakijatokea, siku za nyuma alikuwa akilala mara mojamoja na kuondoka siku ya pili.
***
Ilikuwa ajabu baada ya mzee Sambi kuondoka ilipita wiki bila kufika kwangu kitu ambacho hakikuwa kawaida yake. Baada ya wiki moja ndipo alikuja. Vilevile sikutaka kumuuliza niliamini ni mihangaiko pia nilizingatia ni mume wa mtu.

Siku aliyokuja tulikutana kimwili usiku majira ya saa tano aliondoka kwenda kwake. Nilala vizuri mpaka asubuhi wakati huo nilikuwa nalala na msichana wa kazi kwa ajili ya msaada wa usiku.

Siku ya pili nilipoamka nilipokwenda kuoga nilishtuka kukuta kwenye nguo ya ndani kuna damu kidogo. Haikunishtua sana japokuwa nilijiuliza damu ile inatokana na nini.
Sikutaka kukaa kimya nilimjulisha mzee kuhusiana na hali niliyojikuta asubuhi.

“Mmh! Au jana nimetumia sana nguvu?”
“Walaa, kawaida, mbona nipo sawa tu ila kilichonishtua ni damu kidogo kwenye nguo ya ndani.”
“Unasikia mabadiliko yoyote mwilini?”
“Nipo sawa.”

“Fanya hivi fika hospitali mara moja mi nitakuja baadaye ila nijulishe maendeleo yako.”
“Hakuna tatizo.”
“Basi fanya hivyo.”

Baada ya kuzungumza na mzee wangu nilioga na kumpigia dereva aliyekuwa akisaidia kunipeleka popote kwa vile nilikuwa sijajua vizuri gari pia hali yangu ya ujauzito.

Baada ya kufika nilimweleza anipeleke hospitali. Sele alinipeleka mpaka hospitali ya Madona iliyopo Tabata Aroma. Nilipofika nilimweleza daktari hali niliyokutana nayo asubuhi ambaye alishtuka sana.

Lakini baada ya kunifanyia vipimo ilionesha hakukuwa na athari zozote kwenye ujauzito wangu.

Alinipa dawa na kunieleza nisifanye kazi yoyote ngumu kwa kipindi kile. Nilimshukuru Mungu kukuta ujauzito wangu upo salama. Jioni alipokuja mzee Sambi nilimweleza niliyo elezwa hospitali kuhusu ujauzito wangu.
“Nina wasiwasi jana labda nilitumia nguvu bila kujua.”

“Mmh! Labda, sasa tutafanyaje?”
“Itabidi tuvumilie mpaka hali itakapokuwa sawa.”

Tulikubaliana kutokutana kimwili kwa kipindi kile. Kwa vile muda wake wa kuwepo kwangu uliisha saa nne usiku aliondoka. Kama kawaida niliendelea kulala na msichana wangu wa kazi ambaye alikuwa mtu muhimu sana kwangu hasa kwa kipindi kile.

Siku ya pili nilipoamka kabla ya yote niliangalia nguo yangu ya ndani na kukuta tena damu kidogo. Lakini ya siku ile ilizidi kidogo ya jana yake.

Nilishtuka sana na kumpigia simu daktari mmoja shoga yangu aliyekuwa serikalini pia alikuwa akifanya kwenye hospitali ya ‘private’ ambaye tulianza naye urafiki nilipokuwa dukani.

Baada ya kuita kwa muda ilipokelewa upande wa pili, nilimweleza hali yangu, naye alishtuka baada ya kumweleza mi’ ni mjamzito lakini natoka damu kidogo hasa usiku nikilala na ninapoamka asubuhi hukuta hali ile.

“Unataka kuniambia baada ya kuiona hiyo damu huendelea kutoka kama upo kwenye siku zako?”

“Hapana, ikitoka mara moja basi mpaka siku ya pili asubuhi kitu ambacho sikielewi.”
“Unasema ya leo imezidi kidogo tofauti na ya jana?”

“Ndiyo.”
“Mmh! Itakuwa nini? Mtu uwe na ujauzito damu zitoke, kuna kitu chochote ulichokifanya ambacho kinaweza kusababisha hali hiyo?”
“Juzi usiku nakumbuka nilikutana kimwili na mwenzangu.”
“Hamkutumia nguvu katika tendo?”
“Wala kawaida tu.”

“Tumbo unalisikiaje?”
“Lipo kawaida tu.”
“Haliumi?”
“Haliumi.”
“Hebu njoo hospitali mara moja tufanye uchunguzi wa kina.”

“Sawa nakuja.”
Nilikata simu na kumueleza msichana wangu wa kazi hali iliyonitokea, ambaye jana yake sikumweleza ile hali. Baada ya kumweleza alishtuka.

“Dada kuwa makini damu itatoka vipi ikiwa tayari una ujauzito, tumbo linauma?” naye aliniuliza kama daktari.

“Walaa.”
“Sasa kitakuwa nini?”
“Hata najua naona maluweluwe tu.”
“Unasema jana ulikwenda hospitali na kusema hakuna tatizo, basi hebu isikilizie hali na leo kama itazidi basi urudi hospitali,” alinipa ushauri.

“Hapana kuna daktari wangu mmoja alinieleza niende leo.”
“Dada kama kurudi si ungerudi kwa daktari aliyekutibu jana kuliko kubadili daktari?”
“Siyo mbaya siendi kwenye tiba bali kufanya uchunguzi wa kina ili kujua hali hii inasababishwa na nini.”

“Kama ni hivyo hakuna tatizo.”
“Wacha nimjulishe shemeji yako”
“Bado hujamwambia?”
“Bado nilitaka kwanza kupata maelezo ya kitaalamu kwa vile ilinitisha.

Kwa vile natoka nitampigia na Sele aje anichukue.”
Nilimpigia simu mzee Sambi na kumweleza hali iliyonitokea asubuhi alishtuka na kunieleza nirudi hospitali.
“duh! Sasa ni nini hicho?”
“Yaani hata mwenyewe nashangaa.”

“Tumbo linauma?”
“Lipo kawaida.”
“Basi ungerudi Madona.”
“Nakwenda kwa Dokta Hindu.”
“Si mbaya inabidi afanye vipimo vya kina ili tujue tatizo nini na tiba yake ifanyike haraka.”

“Sawa mpenzi.”
Nilikata simu na kumpigia dereva anifuate asubuhi ile. Nilikwenda kuoga na kujiandaa kwenda hospitali. Baada ya kufungua kinywa nilielekea kwa dokta Hindu aliyekuwa mtaalamu wa magonjwa ya wanawake.

Nilisahau kuwaeleza kitu kimoja kuhusu da’ Suzy wakati huo alikuwa amepata bwana na kuamua kuacha kazi pale super market. Kitu kingine kilichosababisha aache kazi kilikuwa ugomvi kati yake na Meneja Emma bwana yake wa zamani waliyeachana.

Kutokana na habari nilizopewa Meneja Emma baada kujua da’ Suzy ana bwana mwingine tena mwenye uwezo ambaye alikuwa akimpitia baada ya kazi kama mwanzo wangu na mzee Sambi roho ilimuuma.

Kitendo kile kilimuumiza sana Emma na kutaka kutumia ubosi wake kurudisha uhusiano wa zamani kitu kilichosababisha usumbufu kwa da’ Suzy na kuamua kuacha kazi.

Hata baada ya kuacha kazi bado aliendelea kupata usumbufu toka kwa Emma wa kupigiwa simu bila kuzingatia yupo wapi na nani. Pia alikuwa akimtumia ujumbe wa vitisho kitu kilichosababisha kubadili namba yake ya simu ambayo mimi sikuwa nayo.

Taarifa hizo nakumbuka nilipewa na mmoja ya wasichana tuliokuwa tunafanya kazi pamoja aliyekuwa akiendelea na kazi.

Kwa kipindi kile sikuwa na shida naye kwa vile nilijua ana namba yangu lazima angenipigia na kunipa michapo mizima. Niliamini alichokifanya kilikuwa na maslahi kwake.

Baada ya dereva kuja alinichukua na kunipeleka hospitali. Nilipofika nilikuta wagonjwa wengi nilisubiri kwa saa nzima ndipo nilipopata nafasi ya kuonana na dokta Hindu.
 
Mmh jmn nini tena nlipata furaha kama mimba ninayo mie!

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…