Simulizi: Namchukia Mama Yangu


[emoji122][emoji122]
 
Mnaofuatilia hadithi hii bila kucomment chochote like hapa tujuane!

Tumpe moyo mwandishi kwamba tupo pamoja nae!!

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Nimecheka mama tena wanaosoma kimya kimya wapo wengi mnooo

Ngoja siku uone kuna arosto humu watakavyoibuka unajiuliza hawa walikuwa wapi
 
Sehemu ya 24

Moyoni niliwaza mengi baada ya kupina nami lazima nilipe kisasi kama alivyonifanyia. Baada ya tiba ile niliweza kukaa peke yangu baada ya wiki, nilishangaa mama kumsifia mama Amina, kwangu sikuona kigeni sana japokuwa nililetwa nusu mfu lakini haikuwa na tofauti na kwa mganga wa kwanza.

Niliendelea kukaa kwa mama Amina kwa kutumia dawa za kunywa na kufusha. Kila siku nilichuliwa sehemu zote zilizo kufa ganzi kama miguu ambayo ilikuwa haina nguvu.

Baada ya wiki moja nyingine niliweza kunyanyuka na kutembea kwa kushikwa. Niliendelea kutumia dawa ya kuchua na kunywa na kuweza kutembea mwenyewe japo kwa shida.

Pamoja na kutolewa kwenye umauti bado sikuwa na imani ya kurudia hali yangu ya zamani. Baada ya afya yangu kuimarika niliruhusiwa kuondoka lakini baada ya kupata kinga.

Niliweza kutembea lakini miguu bado ilikuwa haijakaa vizuri. Nilijiuliza yatakirudia ya mwanzo japo kulikuwa na tofauti na mganga wa mwanzo kwa kiasi kikubwa.

Niliendelea kutumia dawa ya kuchua kwa ajili yakuondoa ganzi miguuni ambayo iliondoka taratibu. Lakini ajabu muda wote sikumuona mzee Sambi.

Nilimuuza mama ambaye alinieleza niachane naye kama kila kitu kimekwenda vizuri.
“Lakini mama mtu niliyekuwa naishi naye kama mume na alikuwa mstari wa mbele katika matatizo yangu apotee ghafla lazima kutakuwa na kitu.”

“Sasa sisi tutajuaje, tulitakiwa kukuuliza wewe kwa vile baada ya siku ile ambayo ulisema ulimbana kuhusu yule mwanamke aliyekuja kwako kuwa ni mkewe alipoondoka hatujamuona tena.

“Ilitakiwa utumbie baada ya mazungumzo yale kuna kitu gani kingine kilitokea.”
“Mbona yalikuwa mazunguzo ya kawaida wala hakukuwa na kitu chochote kibaya.”

“Ndiyo maana nasema uachane naye, kama hamjakosana ameondoka akijua wewe ni mgonjwa. Hivi leo upo hivi nimuone nitamfukuza kama mbwa.”

“Lakini mama lazima nijue sababu.”
“Kama hakukwambia, mimi nitajuaje?”
“Mamaa ina maana naye anaweza kuondoka kana Beka?” kauli ya mama ilinishtua sana.

“Kwani Beka ulimfukuza?”
“Sijamfukuza, lakini aliniachia fumbo zito.”
“Fumbo gani?”

“Kwamba wewe unajua, lakini wewe umekataa. Kabla sijapata jibu inawezekana mzee Sambi naye kakimbia!”
“Hata akikimbia wewe umepungukiwa nini, hukutibiwa?”

“Nimetibiwa.”
“Sasa tatizo nini?”
“Mama hawezi kuondoka hivihivi lazima kuna sababu.”
“Mwaija mi nitajuaje, wewe ndiyo unanihusu wengine sijui chochote.”

“Mama sasa hivi sikubali lazima nijue sababu ya mzee Sambi kupotea ghafla tena kipindi cha matatizo mazito ambayo kwa upande mwingine ameyasababisha yeye.”

“Mwanangu wanaume wa sasa wanakupenda kwenye uzima yakikukuta unakula wewe na familia yako.”

“Mmh! Nitajua tu.”
“Utajua, lakini sasa hivi endelea kwanza kuimarisha afya yako. Sambi si muhimu kama afya yako ila sitaki kumuona kwa vile alikusudia kukuua.”

“Kivipi?”
“Mkewe aliyofanya madogo?”
“Sawa, lakini akija naomba usimfukuze ili aniambie sababu ya kunikimbia.”
“Hiyo mtajuana lakini kwangu sitaki kumuona.”

“Sawa, lakini kila kitu kitakuwa wazi.”
Kwa vile bado nilikuwa nahitaji msaada wa familia yangu kutokana na hali yangu kutengemaa taratibu sikuweza kurudi kwangu, niliendelea kukaa nyumbani.

Kwa vile muda ule kodi nayo ilikuwa imekaribia kwisha niliwatuma watu kuhamisha vitu vyangu vyote na kuvirudisha nyumbani.

Kichwa changu kilikuwa kizito kuhusu kutoweka mzee Sambi bila taarifa. Pamoja na kujua mkewe ndiye mbaya wangu niliamini bado nikuwa nahitaji msaada wake.

Da’ Suzy ambaye alikuwa amekuja kwa muda Dar baada ya kuhamia Mwanza na mumewe. Alinieleza alivyonikuta siku aliyokuja kunitembelea.

“Mwaija Mungu mkubwa,” alisema huku akiniangalia kwa jicho la siamini.
“Kwa nini?”

“Nilivyokukuta siku ya kwanza na leo hii tunaongea hivi naamini Mungu mkubwa na Mungu yupo pia mama Amina mganga.”
“Kwani ilikuwaje?”

“Baada ya kufika Dar nilikuwa na hamu ya kuonana na wewe kipenzi changu japo niliondoka bila kukuaga na kubadili namba kwa ajili ya Emma.”

“Taarifa niliisikia.”
“Basi niliamua kuishi bila mawasiliano na mtu yeyote zaidi ya ndugu zangu. Baada ya kufika nilishinda siku moja na siku ya pili ndipo nilipokuja kwako ambako sikukuta mtu na ilionekana hakuna dalili za kuwepo .

Niliamua nije kwenu kukuulizia ndipo nilipofika na kukutana na mshtuko. Nilikuwa watu wamekusanyika kwenu, nilipouliza niliambiwa umefariki.

Nilishindwa kuamini niliingia mpaka ndani na kushangaa kukuta watu wakijadiliana kuhusu hali yako. Wapo waliosema umekufa lakini mzee mmoja alikataa na kusema hujafa kwa vile kwa muda wote bado mwili wako ulikuwa na joto.

Walisema wasubiri siku mbili kama hali yako itabakia hivyo basi wakuzike. Mungu alinifungua akili ghafla ya kumkumbuka mama Amina.

Nilimpigia simu na kumwelezea hali yako, aliniambia nimpe muda kidogo. Baada ya muda alinipigia na kunieleza kuwa wewe ni mzima ila kilichotumwa kilikuwa katika hatika ya mwisho kukutoa uhai wako,” mmh! Zilikuwa habari zilizofanya nihisi mwili kusisimka.

Nilitulia nikimsikiliza da’ Suzy macho yamenitoka pima mkono shavuni kama akinihadithia mkasa wa kusikitisha wa mtu mwingine lakini ulikuwa wangu kwa vile yote yale yalipotokea sikuwa na fahamu nilikuwa nusu mfu.

Nimeamini katika maisha kama hujafa hujaumbika na kisemwacho kipo. Habari zilizokuwa zinanihusu nilisimuliwa na mtu mwingine nami kuwa msikilizaji kama mtu mwingine.

Da’ Suzy aliendelea kunisimulia mkasa wangu mzito baada ya kuyaonja mauti na kuamini bila yeye ningezikwa ningali hai.

“Basi mdogo wangu baada ya kumuomba msaada wake wa haraka mama Amina, alitoa masharti tukubebe tukupeleke kwake kwa vile kwenu isingewezekana.”
Kauli ile ilinishtua na kujiuliza kwa sababu gani tiba yangu isingewezekana nyumbani kwetu?

“Basi nilimweleza mama na kina dada kuhusu kukupeleka Mbagala kwa mama Amina walikataa kwa vile ilionesha familia yako ilikuwa imeisha kata tamaa na wewe kuwa hai.
“ Kuna kipindi waliniambia maiti hii uipelekea wapi, nikuache ili mwili upoe waweze kukuzika.

Niliwakatalia kuwa wewe si maiti bali upo hai na kuwahakikisha ukipata tiba unapona. Kwa kweli ushindani ulikuwa mkubwa na kujikuta nikiangua kilio kulilia ili nikupelekea kwa mama Amina.

Walinikubalia huku nikipewa masharti kama umekufa basi mwili nitaurudisha mwenyewe bila kuwashirikisha. Huwezi kuamini Mwaija hali niliyokuona nayo ilinipa ujasiri wa ajabu na kukuchukua mpaka kwa mama Amina.

Nilipokufikisha nilishtuka kumuona hata mama Amina naye akishtuka baada ya kukuona jinsi ulivyokuwa. Mwaija ulikuwa ufu kabisa mdogo wangu na kuniuliza.
“Mmh! Wewe mbona kama mgonjwa ameisha kufa?”

“Yupo hivi siku ya pili leo na ulipo angalia yupo hivihivi.”
“Mmh! Ipo kazi.”
Tulikuingiza ndani na haraka alianza kazi ya kukutibu ikiwa kupakwa mafusho ambayo alisema yalipunguza nguvu ya mdudu aliyekuwa amekushika.

Alichukua dawa ya majani na kukuwekea puani na kutueleza baada ya muda utapiga chafya ndipo. Na kweli ilichukua nusu saa ulipiga chafya ndipo mama Amina alipokuja ndani kukuangalia na kurudia akasema amerudiwa na fahamu.

Mama yako hakuamini alikuwa na hamu ya kukuona. Tuliingia na kumsaidia mama Amina kukunywesha uji.

Hali uliyokuwa nayo pamoja na mama Amina kutupa moyo bado sikuamini kama ningeweza leo kuongea na wewe hivi kweli Mungu mkubwa,” da’ Suzy alinisimulia kwa uchungu mpaka machozi yalimtoka.
Maelezo ya da’ Suzy aliusisimua mwili wangu na kujiuliza mateso kama yale mpaka lini. Moyo iliniuma lakini nilishindwa nifanye nini.

Nilimshukuru da’ Suzy kwa ujio wake kwa kuamini kama asingetokea basi nilikuwa nazikwa hai. Pia nilimshukuru kwa kujitolea kwa hali na mali kuhakikisha afya yangu inaimarika ikiwa pamoja na kunipeleka kwa mama Amina.

Kutokana na moyo wa utu ilibidi apitishe muda wake wa kuondoka ili kuhakikisha anakuwa na mimi mpaka muda ule. Siku za mwanzo kuwa kwa mama Amina nilikuwa na da Suzy pamoja na ndugu zangu.

Aliendelea kunipa moyo na kunihakikishia matatizo yanayonikabili yataisha na kurudi kwenye hali yangu.

“Da Suzy kwa nini kila maisha yangu yakianza kuwa mazuri napata matatizo makubwa? Unafikiri lini nitayafurahia maisha kama wengine?”

“Mdogo wangu kila kitu chenye mwanzo hakikosi mwisho, ipo siku utasahau yote haya yatakuwa simulizi kwa wanao.”

“Mmh! Sina uhakika wa kupata mtoto kwani kila tatizo huanzia kwenye ujauzito.”
“Mwaija hili umelitaka mwenyewe, mama Amina alikueleza urudi lakini kwa kiburi chako ukaona ulielezwa mambo ya kitoto,” da’ Suzy alinilaumu.

“Dadaa, niliogopa kumshirikisha mzee Sambi kuwa ujauzito wangu umetokana na kutumia mitishamba. Kingine muda mwingi alikuwa karibu yangu na wewe ukaondoka ghafla nikakosa mtu wa kunisukuma kwenda kwa mama Amina.”

“Umeelezwa matatizo yako unafanya mchezo, Mwaija wewe si mtoto mdogo dunia ya leo bila kuhangaika unakufa unajiona.”
“Unajua mpaka sasa sielewi kabisa.”

“Kitu gani?”
“Alivyoondoka mzee Sambi hana tofauti na mume wangu Beka.”
“Mwaija kwa nini usimweleze mama Amina nina imani atakusaidia.”
“Sawa, itabidi nikifuata dawa ya kuchua nitamweleza.”

“Vipi kwanza miguu?”
“Sijambo, sasa hivi naweza hata kukimbia. Sijui mama Amina nimpe zawadi gani.”
“Yeyote, mbona yule mama hana tamaa za kijinga.”

Baada ya wiki da’ Suzy aliondoka kuelekea Mwanza. Nilimtakia safari njema na kumuombea kila lenye heri limtangulie na kumuepusha na kila la shari. Niliamini sikuwa na uwezo wa kumlipa yote aliyonifanyia bali Mungu peke yake.

Nami hali yangu ilitengemaa na kuweza kufanya kitu chochote bila msaada wa mtu. Nilitoka siku moja bila kumtaarifu mtu na kwenda saiti kuangalia nyumba yangu japokuwa mama alinikataza niachane na kila kitu cha mzee Sambi.

Nilipanda daladala hadi Mwenge na kuunganisha kuelekea Bunju. Nilipofika kwa mbali niliona jumba limependeza likiwa limekamilika.

Uzio ulikuwa umeisha jengwa na kuwekwa geti la chuma. Nilisogea mpaka pale getini, bahati nzuri mlango mdogo wa geti la kuingilia ulikuwa wazi.

Niliingia ndani, nilipotupa macho kwa mbele nilishtuka kumuona mzee Sambi na mkewe wa mwanaume mwingine akiwa na mkewe wakizungumza.
 
Dah! Mzee Sambi amegeuka
 
Mwee...story nzuri sna asante shunie

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…