X_INTELLIGENCE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2014
- 10,737
- 14,896
Story: NAJUTA KUKUTOA KAFARA MWANANGU NO.1
Mtunzi: EDDY MHANDO
NB: (majina yaliyotumiwa humu hayahusiani na maisha halisi ya wenye majina hayo)
Naitwa mshana jr
Katika maisha yangu nilitamani sana kuwa na maisha mazuri sikuyapenda yale maisha niliyokulia kule kijijini kwetu kwedizando, handeni mkoani Tanga, nilitamani siku moja na mimi niishi maisha kama wanayoishi wakina Obama wa Bongo kenyata obo kikwete na wengine wengi waliofanikiwa...nilitamani kuwa na nyumba nzuri na gari la kifahari niliichoka sana baiskeri yangu niliyorithishwa na mzee GENTAMYCINE ....
Nilizunguka sana kutafuta maisha kila kazi niliyofanya haikuzaa matunda, wadogo zangu niliowapita walizidi kujiimarisha wakanipita kiuchumi, nilihudhunika sana niliposhindwa kuyakabiri maisha hadi kufikia hatua ya kusaidiwa na wadogo zangu.
Nilimuomba Mungu lakini ni kama Mungu alifunga milango ya baraka kwangu, shida ziliniandama nikaichukia siku iliyonileta duniani.
Niliamua kuondoka mbali kabisa na nyumba, niliona pengine pale kijijini kuna watu wamenifanyia ulozi ili nisifanikiwe, kwakuwa sikuwa na kiasi chochote cha fedha niliamua kuiuza baiskeli yangu, nilimuuzia Vladimirovich Putin Ndipo nilipo pata nauli....lakini sikuwa najua wapi nielekee, nilibeba begi langu dogo bila kuaga mtu alfajiri ile nilidamka nikawahi stend nilipanda gari lililo nipeleka Tanga mjini, ambako nilikuta kuna roli linaenda kigoma dereva wa lile roli alikubari kuongozana nami huko waendapo...safari ilikuwa ndefu hatimaye tulifika...sikuwa na ndugu kigoma nililanda landa mithiri ya yatima aliyekosa wa kumsaidia,
hatimaye nilikutana na Shunie Moyo wangu ulinidunda sana nilipomuona Shunie , Uzuri wake wa asili ulinifanya nisahau shida zangu kwa muda, tulisalimiana na katika mazungumzo yangu mimi na Shunie Ilinibidi nimuweke wazi kuwa sina pakwenda, sikumficha juu ya safari yangu kutoka Tanga hadi Kigoma... Shunie Alinionea huruma akaniambia kuwa anaishi peke yake na anacho chumba kimoja kwaajiri ya wageni hivyo atanisaidia kwa kuishi hapo kwake hadi hapo nitakapo jiimarisha kiuchumi...
Tulikaa kwa amani sana pale nyumbani kwa Shunie Upendo ulitawala nyumba ile, niliamua kuungana na wenzangu kuvua samaki, hivyo nilikuwa navua samaki na kuwauza, sio siri biashara ya samaki ilinisaidia sana,
Kadri siku zilivyozidi kwenda nilijikuta navutiwa sana kimapenzi na Shunie NiliShindwa kabisa kutoa hisia zangu kwake, kumbe ata Shunie Alikuwa akinipenda sana,
Siku moja nilirudi nyumbani nilimkuta Shunie Amekaa tulisalimiana kisha Shunie Alianza mitego ya kiunamke nilishindwa kuvumilia, punde wote presha zikatupanda tukajikuta tunachezesha viuno, kujibu mashambulizi huyu akipeleka juu mwingine chini, yule akipeleka juu yule anapeleka chini, tulifanya kitendo hicho pasipo kutegemea na hapo ndipo uhusiano kati yangu mimi mshana jr Na Shunie Ulipo zaliwa...
Kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzie Shunie Alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya utafiti wa madawa ya asili hivyo kutokana na mimi kujua dawa mbali mbali za asili Shunie Aliniunganisha kwenye kazi zao nika ajiriwa, furaha yetu ilizidi sana pale tulipo bahatika kupata mtoto wetu wa kwanza ambaye tulimwita Sakayo,
Nilimpenda sana mwanangu Sakayo Hata Shunie Alimpenda sana Sakayo Mtoto wetu...
Kutokana na kipato kikubwa tulichokuwa tunakipata tulinunua nyumba ya kifahari pamoja na gari la kutembelea, sio siri maisha yalitunyookea sana.
Kwakuwa nilikaa zaidi ya miaka 6 kule kigoma niliamua kurudi nyumbani Tanga kuwasalimia nilimuaga mke wangu Shunie Na tukaahidiana kuwa nikirudi tutaandaa utaratibu wa kuoana, nilichukua gari letu nikaondoka nalo, niliendesha hadi nyumbani kijijini kwetu, nilikuta kijiji chetu kimeendelea sana zile nyumba za nyasi na udongo zilikuwa za kuhesabu, nilipatwa na uchungu sana kwani miongoni mwa nyumba chache za udongo na nyasi zilizo baki pale kijijini nyumba yetu pia ilikuwepo tena mbaya zaidi ilikuwa ni kama imetegeshwa inangoja mtu mwenye nguvu aisukume ianguke, niliona aibu kusimamisha gari langu pale lakini sikuwa na jinsi nilishuka kwenye gari. Mama yangu cocochanel Ambaye umri ulikuwa umemtupa mkono alitoka huku akijikongoja kunifuata alipiga vigere gere vya furaha, mama alishindwa kujizuia machozi yalimtiririka kwenye mabonde ya mashavu usoni mwake, ndugu zangu walikuja tulifurahi niliwapa zawadi nilizotoka nazo Kigoma, baba naye alikuja tulizungumza mengi akanilaumu kwa kitendo changu cha kuondoka bila kuaga, alisema kuwa pindi nilipo toweka walijua nimesha kufa, baba aliniambia kuwa itanibidi niende kwa MziziMkavu Ambaye ni mganga pale kijijini aende akausafishe mwili wangu kiganga kwani wao walisha lia wakanyamaza, hivyo ni lazima nikasafishwe kuondoa mkosi wa misiba...
Sikuwa na jinsi nilienda kuonana na MziziMkavu Na alikuwa mzizimkavu kweli kwenye kilinge chake cha uganga palikuwa panatisha, kulikuwa na mapembe kadhaa ya wanyama yaliyokuwa na madawa ya kiganga ndani yake, MziziMkavu Alifanya uganga wake kisha akaniambia kuwa ili nidumu kwenye utajiri na utajiri wangu uongezeke kuna jambo rahisi na gumu natakiwa kukubari kulifanya, jambo hilo litanifanya nizidi kuwa tajiri......
Itaendeleaaaaaaa usikose kufuatilia Simulizi hii ya kusisimua
Ndugu zangu poleni sana kwa kusubiri hadithi kwa mu...da mrefu bila muendelezo....kiukweli najifunza uandishi na kazi ya uandishi inatumia akili tena akili nyingi...kutokana na harakati za maisha nimejikuta nashindwa kuendeleza muendelezo wa hii story....ila naomba niwahaidi kuwa kuanzia wiki ijayo nitawaletea hii story hadi mwisho....nawapenda sana na asanteni sana .

Story:NAJUTA KUMTOA KAFARA MTOTO WANGU NO.2
Mtunzi: eddy mhando
NB: (majina yaliyotumika humu hayana uhusiano wowote na maisha harisi ya watu wenye majina hayo)
Ilipoishia........
Sikuwa na jinsi nilienda kuonana na MziziMkavu Na alikuwa mzizimkavu kweli, kwenye kilinge chake cha uganga palikuwa panatisha, kulikuwa na mapembe kadhaa ya wanyama yaliyokuwa na madawa ya kiganga ndani yake, MziziMkavu Alifanya uganga wake kisha akaniambia kuwa ili nidumu kwenye utajiri na utajiri wangu uongezeke kuna jambo rahisi na gumu natakiwa kukubari kulifanya, jambo hilo litanifanya nizidi kuwa tajiri......
Kiukweli siku penda niwe masikini, nilitamani niwe tajiri zaidi na zaidi, MziziMkavu Alinipa dawa za kuoga na za kuchoma akaniambia kuwa niende nyumbani kisha kesho nirudi nikiwa na jibu je napenda kubaki kwenye utajiri, mkubwa zaidi ya huu ama lah, niliondoka. njiani nilikutana na mzee GENTAMYCINE alikuwa anakokota baiskeli tena ile ile yangu niliyomuuziaga, mzee huyu ni mtunzaji sana wa mali, tulisalimiana tukaongea mengi sana ndipo GENTAMYCINE Alipo nisimulia kisa kimoja, kuwa yeye aliwahi kufanya kazi kwenye moja ya kampuni kubwa sana ya viatu, katika kampuni hiyo alikuwa meneja, alifanya kazi hiyo kwa juhudi zote, lakini kutokana na imani za kishirikina za baadhi ya wafanyakazi wenzake walio chini yake wakadhani kuwa GENTAMYCINE Atakuwa ameenda kwa waganga ili apendwe sana pale kiwandani, hapo ndipo vituko vilipoanza kumuandama GENTAMYCINE Alianza kuchukiwa na wafanyakazi wenzake, ikawa kama mkosi umemuingia mambo yalimvurugikia hatimaye alifukuzwa kazi, kurudi nyumbani ambako alikuwa anaishi na Sky Eclat Kama mke wake, alikuta Sky Eclat Ameondoka nyumbani kachukua kila kitu kuanzia sturi hadi vitanda, hakuacha ata mashuka, mzee GENTAMYCINE Aliamua kurudi kijijini kuanza maisha upya vile vile aliamua kumrudia Mungu,
GENTAMYCINE Alinisisitiza sana kumcha mwenyezi Mungu, akaniambia kuwa Mwenyezi Mungu huwa anajibu maombi ya kila mtu amuombaye, tofauti huwa ni muda tu wa kujibiwa...
Mazungumzo yale kati yangu mimi mshana jr Na mzee GENTAMYCINE Yalinivutia sana lakini hayakuweza kubadilisha msimamo wangu wa kurudi kwa Mganga MziziMkavu ili akanipe dawa za kunifanya niwe tajiri maradufu, hatimaye GENTAMYCINE Alifika anakoenda mimi nikaendelea na safari, nilipofika nyumbani nilichukua maji nikaenda bafuni kuoga, bafu lile lilikuwa bafu la kijijini si kama lile la mjini, ndani ya lile bafu kulikuwa na choo humo humo....nilichukuwa ile dawa niliyopewa na GENTAMYCINE Nikaiweka kwenye maji yangu ya kuoga kisha nikaanza kuyaoga yale maji, kiukweli nilishituka sana nilipokuwa najimwagia yale maji mwili wangu ulikuwa kama unapigwa na shoti, lakini nilijikaza nikaendelea kuoga.
Siku hiyo nilishinda pale pale kijijini kwetu, Fdt Alikuja kunisalimia huyu alikuwa rafiki yangu ambaye tulisoma wote shule ya msingi, Fdt alinieleza ugumu wa maisha anayopitia alinisimulia jinsi alivyompa mimba miss chagga , alisema kuwa anampenda sana miss chagga Lakini hana uwezo wa kumudu kuishi naye hivyo Fdt Aliniomba nimsaidie kumtafutia ajira, baada ya story za hapa na pale Fdt Aliniaga nikatoa pochi nikampatia noti kadhaa za elfu kumi, Fdt Alinishukuru sana kisha akaondoka,
Baba baba, ilikuwa ni sauti ya kike ikiita kutoka sehemu isiyojurikana kule porini, sauti ile iliendelea kuita kwa ukali kuliko ile ya mwanzo babaaaa, babaaaa, babaaa nilijitahidi kutafuta hatimaye niligundua sauti ile ilikuwa inatokea kwenye shimo, nililisogerea lile shimo lilikuwa refu nilipochungulia sikuamini macho yangu nilimuona mwanangu Sakayo Akiwa amefungwa mguu na mkono ndani ya lile shimo, sikuwa na uwezi wa kumuokoa maana ili nimuokoe ilikuwa ni lazima niingie mule shimoni nimfungue kamba alizofungwa kisha ndipo atoke...nilihudhunika nisijue cha kufanya kisha ilitokea sauti kali nzito iliyoambatana na radi ikisema "MWANAO Sakayo NDIE ALIYEBEBA UTAJIRI WAKO, MIAKA YA MBELE ATAFUNGWA HIVI NA HAKUNA WA KUWEZA KUMFUNGUA, ILA HAKIKISHA HILI LINAFANYIKA LASIVYO UTAJIRI WAKO UTAPUKUTIKA, ghafra ndege mkubwa alitokea kaingia mule shimoni na kwa kasi ya ajabu akambeba Sakayo Na kutokomea naye kusikojurikana....nilishituka kumbe nilikuwa naota
Ndoto hii ilinitesa sana, nikajiapiza kuwa nikienda kwa mganga MziziMkavu Nitamuhadithia hii ndito, kulipokucha nilienda kilingeni kwa MziziMkavu Nilimkuta amekaa tukasilimiana kisha akaniambia kuwa nadhani ujumbe wake nimeupata, nilishangaa sana....nikajiuliza ni ujumbe upi huo na Maana kwenye kumbukumbu zangu ikumbuki kama mganga MziziMkavu alikuwa anaMiliki simu.....
Ni kama MziziMkavu Alijua mshituko niliokuwa nao. Akaniambia kuwa usiku wa leo tulikuwa wote na tumeongea...yale niliyosikia ndiyo makubariano yenyewe. Bado nilibaki kwenye mshangao.......
Itaendelea.....
Story: NAJUTA KUMTOA KAFARA MTOTO WANGU NO.3
Mtunzi: EDDY MHANDO
NB. (majina yaliyotumika humu hayana uhusiano wowote na maisha harisi ya wenye majina hayo)
Ilipoishia.....
Ni kama MziziMkavu Alijua mshituko niliokuwa nao. Akaniambia kuwa usiku wa leo tulikuwa wote na tumeongea...yale niliyosikia ndiyo makubariano yenyewe. Bado nilibaki kwenye mshangao.......
Sikujua mimi na MziziMkavu Tulikuwa wote wapi maana usiku sikutembea kabisa nilikuwa tu nyumbani...
MziziMkavu Akasema "mizimu yangu iliongea na wewe kwa njia ya ndoto, ile ndoto uliyokuwa unaota haikuwa ndoto, ili uulinde utajiri wako, uzidi kuwa tajiri, inabidi umtoe kafara mtoto wako, mtoto wako hatokufa ila tutamfunga...."
Maneno ya MziziMkavu Yalinichanganya na kuniogipesha, nilikuwa na mtoto mmoja tu Sakayo Nilikuwa nampenda sana mwanangu Sakayo Leo mganga anataka tumtoe ili nizidi kuwa tajiri...nilibaki njia panda utajiri naupenda, sikupenda kuishi maisha ya nyuma, yenye manyanyaso simanzi, kulala na njaa ama kuishi mithiri ya omba omba....nilitamani kuishi kifalme, niendeshwe, niwe na watu wanao nitumikia....
Sikuwa na jinsi nilikubariana na MziziMkavu Akaniambia nipeleke mbuzi mwekundu, sanda na baadhi ya dawa alisema atazitafuta yeye mwenyewe....
Nilimfuata miss chagga Ambaye alikuwa mfugaji maarufu wa mbuzi na ng'ombe, nikamuomba aniuzie mbuzi. miss chagga Aliniambia kuwa kwa muda ule Nokia83 Ambaye ni mchungaji wa mifugo ya miss chagga Bado hajarudisha mifugo kutoka malishoni hivyo nisubiri pindi mifugo itakaporejea nije nichukue mbuzi wangu, nilimlipa miss chagga Kisha nikaondoka.
Nilimkumbuka sana mke wangu Shunie nilichukua simu yangu Nikampigia simu iliita kisha akapokea akasema
"halo mume wangu nimekukumbuka sana"
Nikamjibu
"ata mimi nimekukumbuka sana mke wangu" Shunie Akaendelea
" Sakayo Mtoto wetu anakulilia sana"
nikamjibu
"mwambie Sakayo Baba nitarudi muda si mrefu babu na bibi yake wanamsalimia sana"
Tulizungumza mengi na Shunie Laiti kama Shunie Angejua nililokuwa napanga kufanya juu ya mtoto wetu Sakayo Asingenipenda kamwe...
Jioni ilipofika nilienda kwa miss chagga Kuchukua mbuzi wangu ili nimpeleke kwa mganga MziziMkavu Kama nilivyo ahidiana naye
Nilichukua yule mbuzi, nikaenda kwa MziziMkavu Nilimkuta anafanya mambo yake ya uganga...akanikaribisha kisha akasema kazi yetu tutaifanya usiku, MziziMkavu alinipa shuka jeusi...akaniambia nijifunge hilo shuka kama wavaavyo wamasai.
Mida ilipotimia MziziMkavu Akiongozana nmsaidizi wake anaeitwa dab pamoja na mimi tuliongozana hadi katikati ya milima fulani hivi, huku tukiwa na yule Mbuzi...nilishanga kukuta sehemu maalum imeandaliwa, huko juu ya mlima porini, Daby Alimchukua mbuzi akamfunga vitanzi mguuni n mkononi.... mshana jr Nilibaki nashangaa tu, MziziMkavu Alichukua tunguli yake kubwa iliyovilingishwa shanga akawa anaongea maneno huku anavuruga dawa iliyopo kwenye hiyo tunguli yake...tulifanya ule uganga kule porini hadi alfajiri...kisha tulimuacha yule mbuzi kule kule kisha mimi , Daby Na MziziMkavu Tuliondoka...kule porini MziziMkavu Akaniambiaa kazi imesha ish mambo yaliyobaki atafanya yeye mwenyewe,
Ila alinisisitiza kuwa kamwe nisitoe msaada wowote kumsaidia...mtoto wangu Sakayo
Vile vile MziziMkavu Aliniambia kuwa nisimrudie tena mke wangu Shunie .... Maneno ya mganga yaliumiza sana moyo wangu kwani, ni kama alizamilia kunitenganisha na familia yangu...
MziziMkavu Akamalizia kuwa niki kiuka hayo aliyonieleza kitakachonipata nisimfuate
Itaendeleaaaa......