Simulizi; Najuta kumtoa kafara mtoto wangu

Story: NAJUTA KUKUTOA KAFARA MWANANGU NO.1
Mtunzi: EDDY MHANDO
NB: (majina yaliyotumiwa humu hayahusiani na maisha halisi ya wenye majina hayo)

Naitwa mshana jr
Katika maisha yangu nilitamani sana kuwa na maisha mazuri sikuyapenda yale maisha niliyokulia kule kijijini kwetu kwedizando, handeni mkoani Tanga, nilitamani siku moja na mimi niishi maisha kama wanayoishi wakina Obama wa Bongo kenyata obo kikwete na wengine wengi waliofanikiwa...nilitamani kuwa na nyumba nzuri na gari la kifahari niliichoka sana baiskeri yangu niliyorithishwa na mzee GENTAMYCINE ....

Nilizunguka sana kutafuta maisha kila kazi niliyofanya haikuzaa matunda, wadogo zangu niliowapita walizidi kujiimarisha wakanipita kiuchumi, nilihudhunika sana niliposhindwa kuyakabiri maisha hadi kufikia hatua ya kusaidiwa na wadogo zangu.

Nilimuomba Mungu lakini ni kama Mungu alifunga milango ya baraka kwangu, shida ziliniandama nikaichukia siku iliyonileta duniani.

Niliamua kuondoka mbali kabisa na nyumba, niliona pengine pale kijijini kuna watu wamenifanyia ulozi ili nisifanikiwe, kwakuwa sikuwa na kiasi chochote cha fedha niliamua kuiuza baiskeli yangu, nilimuuzia Vladimirovich Putin Ndipo nilipo pata nauli....lakini sikuwa najua wapi nielekee, nilibeba begi langu dogo bila kuaga mtu alfajiri ile nilidamka nikawahi stend nilipanda gari lililo nipeleka Tanga mjini, ambako nilikuta kuna roli linaenda kigoma dereva wa lile roli alikubari kuongozana nami huko waendapo...safari ilikuwa ndefu hatimaye tulifika...sikuwa na ndugu kigoma nililanda landa mithiri ya yatima aliyekosa wa kumsaidia,
hatimaye nilikutana na Shunie Moyo wangu ulinidunda sana nilipomuona Shunie , Uzuri wake wa asili ulinifanya nisahau shida zangu kwa muda, tulisalimiana na katika mazungumzo yangu mimi na Shunie Ilinibidi nimuweke wazi kuwa sina pakwenda, sikumficha juu ya safari yangu kutoka Tanga hadi Kigoma... Shunie Alinionea huruma akaniambia kuwa anaishi peke yake na anacho chumba kimoja kwaajiri ya wageni hivyo atanisaidia kwa kuishi hapo kwake hadi hapo nitakapo jiimarisha kiuchumi...

Tulikaa kwa amani sana pale nyumbani kwa Shunie Upendo ulitawala nyumba ile, niliamua kuungana na wenzangu kuvua samaki, hivyo nilikuwa navua samaki na kuwauza, sio siri biashara ya samaki ilinisaidia sana,

Kadri siku zilivyozidi kwenda nilijikuta navutiwa sana kimapenzi na Shunie NiliShindwa kabisa kutoa hisia zangu kwake, kumbe ata Shunie Alikuwa akinipenda sana,
Siku moja nilirudi nyumbani nilimkuta Shunie Amekaa tulisalimiana kisha Shunie Alianza mitego ya kiunamke nilishindwa kuvumilia, punde wote presha zikatupanda tukajikuta tunachezesha viuno, kujibu mashambulizi huyu akipeleka juu mwingine chini, yule akipeleka juu yule anapeleka chini, tulifanya kitendo hicho pasipo kutegemea na hapo ndipo uhusiano kati yangu mimi mshana jr Na Shunie Ulipo zaliwa...

Kila mmoja alifurahia uwepo wa mwenzie Shunie Alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya utafiti wa madawa ya asili hivyo kutokana na mimi kujua dawa mbali mbali za asili Shunie Aliniunganisha kwenye kazi zao nika ajiriwa, furaha yetu ilizidi sana pale tulipo bahatika kupata mtoto wetu wa kwanza ambaye tulimwita Sakayo,

Nilimpenda sana mwanangu Sakayo Hata Shunie Alimpenda sana Sakayo Mtoto wetu...
Kutokana na kipato kikubwa tulichokuwa tunakipata tulinunua nyumba ya kifahari pamoja na gari la kutembelea, sio siri maisha yalitunyookea sana.

Kwakuwa nilikaa zaidi ya miaka 6 kule kigoma niliamua kurudi nyumbani Tanga kuwasalimia nilimuaga mke wangu Shunie Na tukaahidiana kuwa nikirudi tutaandaa utaratibu wa kuoana, nilichukua gari letu nikaondoka nalo, niliendesha hadi nyumbani kijijini kwetu, nilikuta kijiji chetu kimeendelea sana zile nyumba za nyasi na udongo zilikuwa za kuhesabu, nilipatwa na uchungu sana kwani miongoni mwa nyumba chache za udongo na nyasi zilizo baki pale kijijini nyumba yetu pia ilikuwepo tena mbaya zaidi ilikuwa ni kama imetegeshwa inangoja mtu mwenye nguvu aisukume ianguke, niliona aibu kusimamisha gari langu pale lakini sikuwa na jinsi nilishuka kwenye gari. Mama yangu cocochanel Ambaye umri ulikuwa umemtupa mkono alitoka huku akijikongoja kunifuata alipiga vigere gere vya furaha, mama alishindwa kujizuia machozi yalimtiririka kwenye mabonde ya mashavu usoni mwake, ndugu zangu walikuja tulifurahi niliwapa zawadi nilizotoka nazo Kigoma, baba naye alikuja tulizungumza mengi akanilaumu kwa kitendo changu cha kuondoka bila kuaga, alisema kuwa pindi nilipo toweka walijua nimesha kufa, baba aliniambia kuwa itanibidi niende kwa MziziMkavu Ambaye ni mganga pale kijijini aende akausafishe mwili wangu kiganga kwani wao walisha lia wakanyamaza, hivyo ni lazima nikasafishwe kuondoa mkosi wa misiba...

Sikuwa na jinsi nilienda kuonana na MziziMkavu Na alikuwa mzizimkavu kweli kwenye kilinge chake cha uganga palikuwa panatisha, kulikuwa na mapembe kadhaa ya wanyama yaliyokuwa na madawa ya kiganga ndani yake, MziziMkavu Alifanya uganga wake kisha akaniambia kuwa ili nidumu kwenye utajiri na utajiri wangu uongezeke kuna jambo rahisi na gumu natakiwa kukubari kulifanya, jambo hilo litanifanya nizidi kuwa tajiri......

Itaendeleaaaaaaa usikose kufuatilia Simulizi hii ya kusisimua
Story nzuri sana sehemu ijayo nistue kwa kunitag kwa koment
 
Inabidi ujifunze hata kuandika Jina la Hadith lenye mvuto au ushawishi wa mtu kutaka kujua ndani kuna nini. Mimi nmeshaona hiyo title najua mwishoni hiyo hadith itaishaje. Yaani hainishawishi kuisoma coz tayari kichwa cha hadith kimeshamaliza hadith kabla sijasoma.

Mimi nakushauri uepuke majina ambayo yanahitimisha hadith.mfano: asiyesikia la mkuu, najuta kumuua mke wangu n.k
 
Inabidi ujifunze hata kuandika Jina la Hadith lenye mvuto au ushawishi wa mtu kutaka kujua ndani kuna nini. Mimi nmeshaona hiyo title najua mwishoni hiyo hadith itaishaje. Yaani hainishawishi kuisoma coz tayari kichwa cha hadith kimeshamaliza hadith kabla sijasoma.

Mimi nakushauri uepuke majina ambayo yanahitimisha hadith.mfano: asiyesikia la mkuu, najuta kumuua mke wangu n.k
Asante bado...najifunza...hope...next time...itakuwa poa...zaidi
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom