ng'ombo
JF-Expert Member
- Dec 1, 2014
- 418
- 619
Mwanamke mmoja alikuwa akifanya kazi katika kiwanda cha kusindika nyama. Siku moja baada ya kumaliza kazi zake pale kiwandani alienda katika chumba chenye freezer (Cold Room) ambako nyama zilikuwa zikihifadhiwa kukagua kama zimeifadhiwa vizuri. kwa bahati mbaya wakati yupo kwenye hicho chumba cha ubaridi mlango ulijifunga na kijilock kwa nje na hakukuwa na msaada wa kuweza kuufungua mpaka kuwepo mtu wa nje.
Ingawa alilia na kupiga kelele za kuomba msaada wa kufungiliwa lakini kelele hizo hazikuwa rahisi kusikika nje ya hicho chumba kidogo, na wafanyakazi wengi pale kiwandani walikuwa washaondoka.
Masaa machache baadae akiwa katika hali mbaya ya kukaribia kukata roho kutokana na baridi kali ya hicho chumba, Ghafla yule mlinzi wa getini alifika na kufungua mlango wa Cold Room alimokuwamo yule mwanamke. Na baadae baada ya kutolewa na kupata nafuu alipata wasaa wa kumuuliza yule mlinzi ilikuwaje akafungua mlango wa Cold Room wakati ilikuwa si ratiba yake na vile vile si kazi yake?.
Maelezo ya yule mlinzi yalikuwa hivi ''nimefanya kazi hapa kiwandani kwa zaidi ya miaka 20 sasa, mamia ya wafanyakazi wanatoka na kuingia kiwandani lakini wewe peke yako kati ya wote ndio uliyekuwa ukithubutu kunisalimia asubuhi na kuniaga kila jioni unapoondoka hapa kiwandani, wengine wananichukulia kama mtu nisiye na thamani labda ni kutokana na hii kazi yangu hii ya ulinzi.
Leo ulipokuja kazini asubuhi ulinisalimia kama kawaida ya tabia yako ya kunijulia hali ''uliniambia habari za asubuhi na tukafurahi kwa dakika mbili tatu, lakini baada ya muda wa kazi kuisha sijapata salaam yako ya kunitakia jioni njema na kubaki salama nilipitiwa na wasiwasi hivyo nilichukua uamuzi wa kuanza kukutafuta kwa kuanzia nilianzia humu ndani kuangalia kama upo.
Kwa kutokukuona kwako jioni baada ya muda wa kazi kuisha nikagundua tu lazima kuna baya litakuwa limekupata na ndipo nilipokukuta kwenye hiki chumba cha barafu.
FUNZO
Ishi vizuru na kila mtu, mheshimu kila mtu wakubwa kwa wadogo. Hauwezi kujua siku utakapopata tatizo ni nani atakusaidia.