SIMULIZI: Mwalimu wa zamu

SIMULIZI: Mwalimu wa zamu

Xav Emmanuel

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2018
Posts
215
Reaction score
316
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

*********
Simulizi hii ni mwanga kwa kuendeleza Imani ya kumwabudu mungu aliye kweli.. pia ni ni funzo kwa watu ambao wanaacha tamaduni zao kwa kuzizarau au kwa namna moja au nyingine.
Pia haya ni baadhi tu ya mambo ambayo waalimu wanakutana nayo katika taaluma zao. Pengine si walimu tu, hata madaktari, na wengineo.
Tuungane katika simulizi hii fupi ya Mwalimu wa Zamu kupata funzo… Funzo la Maisha.
Karibu.
**********

SEHEMU: 01
Ilikuwa ni alfajiri ya mapema ambapo viungo vya mwili viliendelea kukumbushana majukumu yake, mdomo haukuacha kabisa kupanuka kuashiria unaitaji kupumua kwa nguvu zote, kupumua huko hukumbusha pia mikono kuwa inaitajika kusimama kwa ukakamavu na kuinuka, tena kwa kukunja ngumi huku mwingine ukienda kushoto na mwingine kwenda kulia. Kiuno nacho hakikuwa mbali katika kubinuka ili kuendana na kasi ya mdomo, mikono na miguu.

“Alhamdullilah!”, swala fupi ikatoka kinywani mwangu kuashilia sipo mbali sana Mungu. Hakuna aliyekosea kusema kuwa mimi ni Muislam tena Muislam aliyekomaa kwa kuangalia tu jina langu.

“Yusuph Athumani” Jina hili linamaanisha Baba Muislam, Mama Muislam; Nilitabasamu.

Baada ya muda nikaupa ubongo nafasi ngeni ya kutabasamu kwa kukumbuka baadhi ya kumbukumbu wakati nipo chuo, na maandalizi yote ya safari kutoka Dodoma hadi Songea. Ubongo nao haukuitupa nafasi hiyo kwa kutaja neno UDOM; kila baada ya nukta.

Kuna mda nilikaa kushangaa kwa nini neno hilo limekuwa mzizi katika mawazo yangu, lakini kushangaa huko kulijibiwa vizuri na ubongo. “University of Dodoma” Ubongo ukaishia kunijibu hivyo na kutoweka.

Nilikumbuka kuwa hata safari hiyo ya kutoka Dodoma kwenda Songea ilikuwa ni sababu ya neno UDOM. Ni kweli kabisa nilikua nimetumwa kufanya moja ya majukumu ya mafunzo yangu ya ualimu. Yaani mafunzo ya ufundishaji wa vitendo.

Basi harakati za hapa na pale zikaendelea, hatimaye nikafanikiwa kumaliza kila kitu kwa kujiandaa, angali sehemu ambayo ilikuwako shule nilikua bado siijui vizuri, lakini jina na maeneo ilipo nilishaelekezwa tayari, kilichobaki ni kuchoma tu pesa kwa dereva bodaboda kunifikisha sehemu husika.

“Naenda Ruvuma Sekondari”, nilitoa maelezo hayo na sikuulizwa kitu zaidi ya kupanda na safari ikaanza, dakika tano tu nilifika eneo la shule.

Nilipokelewa kwa shangwe na vumbi la kutosha, lote lilitaka kung’ang’ania mwili wangu. Miti iliyolala ikasimama na kunionea huruma, barabara nayo ikatanuka kwa kiasi chake kuacha njia kubwa ya mimi kupita.

Nilihisi furaha kupitiliza kwa baadhi ya salamu nyingi kutoka kwa wanafunzi, nyingi zikiwa za lugha ya Kiswahili, hizo nilivunga kuitikia, ila za lugha ngeni nilipatwa na shauku ya kuzijulia hali,

“Good Morning! how are you?”. Huku uso wa bashasha uliojaa nizamu ya ugeni ukisogea machoni mwa wanafunzi.

Nilitulia sehemu ambayo juu ya jengo hilo kuliandikwa neno UTAWALA. Ndio nilisimama hapo, niende wapi mimi kuku mgeni?. Nilikuwa mimi na begi langu lililosheheni makatasi ya kulipo sehemu ya kazi.

Nilitulia kama dakika sita hivi bila kutikisika, kwani nilizubaa kuangalia wanafunzu ambao wengi wao walivaa hijabu zao nyeupe ‘pee’ na kuendelea na shughuli zao za usafi. Walikuwa bize kweli kufanya usafi huku wengine wakikata majani, wengine kufagia na wengine kumwagilia maua.

“Eti kaka samahani!, kwa tunaofika leo utaratibu upoje?”, sauti nyepesi ilinishitua katika dimbwi la mawazo na kukaa sawa kama askari aliye fanyiwa ziara ya kushitukiza na mkuu wake wa kazi. Alikuwa ni mwanamke.

“ah ah… khoonho konhooo” nilikohoa kidogo kwa kujiweka sawa kisha kujibu.

“Sijajua!, kwa maana na mimi naripoti leo!” nilijibu huku macho yangu yakiendelea kuchambua uzuri wa mwanamke yule mgeni katika mboni yangu. Alikuwa na asili yake kwa kweli.

“Mmmh!, Oky!. ko nawe wa TP e?, Chuo gani mwalimu?”. Maswali mengine yakafuata kutoka kwa mwanamke yule ambaye naye alikuwa mgeni kama mimi.

“Yahp, natokea huko Dodoma, Chuo Kikuu cha Dodoma”. Nilijibu, nikikuna kichwa kidogo na kumtazama.

“Oh wow!, aya sawaa, mi wa UD..!” hakumalizia kauli yake akapokea salamu ya mwanafunzi na mazungumzo mengine yakaendelea, wakaongezeka na waalimu wengine saba na kuwa jumla yetu kufikia waalimu tisa tulioripoti siku hiyo.

Walimu walioajiliwa shule hiyo walitupokea vizuri kwani walijua kwa majuma machache tutakayo kuwa shuleni hapo, tutakuwa tunawapunguzia baadhi ya majukumu ya ufundishaji, na uhudumu shule.

Tulipokelewa na mkuu wa shule pamoja na makamu wake na kufanyiwa semina fupi inayohusu mienendo na falsafa za shule hiyo. Hakuna alichotuficha mkuu wa shule, alituambia yote japo mengine alitubinya, aliyasema kwa hofu.

“Wazazi wa watoto ni wakali kweli…….., mjitahidi kulinda hasira zenu……..” mkuu wa shule licha ya kuongea mambo mengi sana ya kujenga lakini alikomea sehemu hii kwa malizia maneno hayo mawili ambayo hakuyatolea ufafanuzi zaidi ya kuongea kimkato tu na kumkaribisha mwalimu mkuu msaidizi.

“Kama nilivyojitambulisha mwanzo, Mwalimu Kunambi Michael ndio jina langu, yote yameshaongelewa na mkuu, nategemea utekelezaji tu.”, mwalimu huyu alikuwa na ushawishi wa maneno wa aina yake, aliongea kisomi bila kipindapinda. Alikuwa mwepesi wa kutumia lugha.

Baada ya kumalizika kwa semina tukakabidhiwa waalimu wa masomo na majukumu ya hapa na pale yakiendelea. Tukawa rasmi waalimu wanafunzi kwa mafunzo ya vitendo.

***********
Labda kabla sijaendelea kusimulia ndugu wasikilizaji, hii ni simulizi iliyojaa visa vingi ndugu zangu, iliyo na lengo ya kuelimisha uma kuwa si kila sehemu ya kuingia kichwa kichwa, maana kila sehemu kuna utamaduni na mienendo yake iliyolenga kuimalisha jamii hiyo katika kila mipaka……..

INAENDELEA….
KUMBUKA:
Baadhi ya matukio, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo….
FB_IMG_1587754989713.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU (02)
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

***********
Labda kabla sijaendelea kusimulia ndugu wasikilizaji, hii ni simulizi iliyojaa visa vingi ndugu zangu, iliyo na lengo ya kuelimisha uma kuwa si kila sehemu ya kuingia kichwa kichwa, maana kila sehemu kuna utamaduni na mienendo yake iliyolenga kuimalisha jamii hiyo katika kila mipaka……..

SEHEMU: 02
Mimi Yusuph ambaye nilichagua shule hii ya Ruvuma sekondari kufanyia mafunzo yangu ya ualimu niwapo mwaka wa kwanza tu.

Sijaona sababu za kuchagua shule hii, labda ni mipango ya mwenyezi Mungu tu ili nioneshe ushuhuda huu niliokumbana nao. Nilikuja kwa mapendo mazito sana, nilipenda kazi yangu, nilimpenda kila mtu, nilipendwa sana japo nilipendwa kwa wakati ambao si sahihi. Niliteseka sana, nimeteseka ndugu wasikilizaji…

********
Niliishi shuleni hapo kwa wiki zipatazo mbili bila tatizo la aina yoyote, nilipata ‘support’ kubwa na baadhi ya waalimu tuliofika pamoja; wiki hiyo ya pili waliongezeka waalimu wengine saba kutoka chuo kikuu cha Mwalimu Nyerere Momorial Accademy na kufikia idadi ya waalimu kumi na sita tuliokuja kufanya mafunzo yetu ya vitendo shuleni hapo, ikawa ni timu kutoka Chuo kikuu Dar Es Salaam (UDSM), Chuo kikuu Dodoma (UDOM), na Mwalimu Nyerere.

Jambo ambalo liliniumiza kupita yote ni kuwa kumi kati waalimu wanafunzi tuliokuja, walihifahamu vizuri shule, wengine kati ya hao kumi walikuwa wahitimu wa mwaka wa masomo wa 2015 shuleni hapo, jambo jema zaidi walikua wanatoa vionjo tu vya historia ya shule hiyo lakini kamwe hawakuwai kutoa SIRI.

Eeeeh!! Ni siri ndugu wasikilizaji kwa maana sifa tu zilikuwa kedekede zaidi ya kuelezwa hatari ya shule hiyo, nilinufaika kwa uchache japo mengi nilikuwa siyafahamu. walikuwa wanaficha.

“Kipindi tunasoma sisi, ilikuwa bata sana, hakuna aliyevunja sheria waalimu. Shule ilikua poa sana. Sio kama kipindi hiki wanafunzi wamekaa kishamba sana… aaahg!!. Ila kuna wakalii ohoo!” Mwalimu Kussa alikazia kauli ya Mwalimu Banda ambae alianzisha gumzo zito kuhusu mambo yaliyopo shuleni hapo.

“Nakubali mwalimu, hata mimi nakumbuka tukio ambalo lilikua gumzo ni moja tu lile la jamaa… nani huyu… aggghh!! Jafari Lunje. Eeh Lunje. Hahahaha huyu jamaa we acha tu, kuchafuka sio jambo la kushangaza ukipata bahati ya kukutana naye, kwanza kubali kuchafuka.” Mwalimu Luoga akachangia huku akionyesha sura ya mashaka usoni kwake, kwani aliongea kwa sauti ndogo iliyopelekea chembe ya uoga.

Kwa kufanya vile kwake ilikua ni vita vya moyo kwa kuwa hakuwa na tamaduni ya kuongea sanaa ila akiongea lazima ardhi Iteteme. Basi Ijumaa hiyo ikaisha kama ilivyoanza.
------

Ndugu wasikilizaji wiki iliyoaanza juma tatu ya pili ya mwezi wanane, nilikabidhiwa zamu kama mwalimu msaidizi wa zamu ya wiki hiyo hadi ijumaa ya mwisho ya wiki, na hapa sifa mbaya ya jina la T.O.D (Teacher On Duty: (Mwalimu wa Zamu) iliibuka.

Zilikua siku saba tu. Lakini zilitawala miaka yangu yote ishilini na moja. Huwezi amini nawaambia, miaka ishilini na moja ni michache sana kuliko uwingi wa siku saba nilizo kumbana nazo.

“Anaitwa Mwalimu Yusuphu, mtakua naye na waalimu wengine wawili wiki hii, si mnamwona lakini?”

“Ndiyoooooo!”. Mwalimu wa zamu iliyopita, aliuliza umati wa wanafunzi na wote kuitikia kwa kishindo hasa kidato cha kwanza ambapo walinizoea na ucheshi wangu wakati niwapo darasani kuwafundisha.

Kwangu mimi ualimu ulikuwa kama kipaji. Nilifanya kwa nizamu kubwa sana. Laiti kama kungekuwa na kipimo cha utendaji kazi basi Assessor wangu angukua either Waziri wa Elimu au Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Nilisogea mbele ili kuweza kuonekana kwa urahisi zaidi, kwani kulikuwako na waalimu wengine warefu zaidi yangu.

“”Konho Konhooh”, nilistua kidogo kwa kukohoa na kuanza kutoa salamu kwa wanafunzi na waalimu wa pale. Lakini cha kushangaza hakuna neno hata moja lililotoka kinywani mwangu.

Kinywa kilikuwa kizito utadhani kuna mtu alinibana kwa kutotaka kuropoka ushahidi juu ya kesi yake. Nilipotaka kulazimisha kuongea nikaanza kukohoa kwa nguvu sana.

Kwa sasa haikuwa tena kama mwanzo, nilikohoa mfululizo mno bila kuacha, nikaona aibu kwa kusogea nyuma taratibu lakini cha kushangaza hakuna hata mmoja alieonyesha kushituka na hali yangu.

“Mpeni ushirikiano wa kutosha, kama mlionionesha mimi katika wiki yangu!” nilimsikia Mwalimu Yule akiendelea kusisisitiza wanipe ushilikiano wa kutosha.

Sasa ni ushilikiano gani huu ambao walinionesha mimi?, inamaana hata waalimu wengine nao wanapewa ushirika kama huu?. Au nini hasa kosa ambalo nafanya hadi nakuja kujutia namna hii?. Kweli nilipewa ushilikiano kwa wiki nzima.

Kwa kipindi kama hiki hata kama ulikua hujafikia hatua ya kutambaa, ndugu msikilizaji nakuambia utatembea na hatimaye utakimbia.. au kufikia umri wa balehe wakati bado mchanga. “Dunia Hadaa…. ”

ITAENDELEA…..
Mwalimu Yusuphu anakabidhiwa zamu, kuiongoza shule kwa takribani siku saba za wiki. Siku ya kwanza tu anakutana na vibwenzo vya kutoweza kuongea katika mkusanyiko wa wanafunzi. Endelea katika sehemu ya pili kujua Majanga ambayo yamekuta Mwalimu Yusuphu katika wiki yake hiyo.

KUMBUKA:
Baadhi ya matukio, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU (03)
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

ILIPOISHIA…
“Mpeni ushilikiano wa kutosha, kama mlionionesha mimi katika wiki yangu!” nilimsikia Mwalimu Yule akiendelea kusisisitiza wanipe ushirikiano wa kutosha.

Sasa ni ushilikiano gani huu ambao wananionesha mimi?, inamaana hata waalimu wengine nao wanapewa ushitika kama huu?. Au nini hasa kosa ambalo nafanya hadi nakuja kujutia namna hii?. Kweli nilipewa ushirikiano kwa wiki nzima.

Kwa kipindi kama hiki hata kama ulikua hujafikia hatua ya kutambaa, ndugu msikilizaji nakuambia utatembea na hatimaye utakimbia.. au kufikia umri wa balehe wakati bado mtoto. “Dunia Hadaa…. ”

SEHEMU: 03
Nakumbuka tu wanafunzi walipiga makofi na kutawanyika. Baada ya kupotea kwa wanafunzi hao niliacha kabisa kukohoa, nilijikokongoja kufuata msafara wa waalimu waliokuwa wanaelekea ofisini baada ya kutawanyika.

“Mwalimu.. kumbe wewe ni jasiri e?”. Madamu mmoja ambaye hakuwa na sifa ya kuongea ongea ovyo ofisini alinishika bega na kuniuma sikio.

“Jasiri? Ah ila inategemea na sehemu gani upo na nini unafanya. Hicho ndio kipimo cha ujasiri sasa.” Nikajikakamua kutoka katika kifungo cha Malkia Yule wa sauti, alikuwa ni Madam Komba.

“Yaani kwanza sikutegemea kama utafanya kitu kama kile, hivi unajua umetuchelewesha sana?, mi na kipindi sa hizi, nisipomaliza utanilipa mda wangu”. Mwalimu Yule aliendelea kulalamika huku akitoa mkono wake begani kwangu na kuuchezesha katika tumbo lake ambalo linaonyesha kwa mda mfupi ujao litaongeza idadi ya watu duniani.

Sikuelewa hata nini cha kuuliza, nini cha kuacha. Nikaingia ofisini na kuketi, sikumwelewa hata kidogo.

“Mwalimu hii zamu itakua moto sana, You Killed!” Mwalimu Banda nae hakuacha vituko vyake, alijaribu kuchekesha kila mtu na alifanikiwa, ni kweli alifanikiwa kwani kila mtu alicheka hadi nikaona aibu na mimi nikaanza kucheka.

Hapo nikaweka uhuru kwa kila mtu kunivamia kwa kauli yake, wapo waliosema nilikua na sifa sana, wapo waliosema kuwa maisha yangu ya kijanja, eti najifanya tu kuwa mpole. Wengine wakaponda hata chuo nachotoka kwamba hicho ndicho walichonituma.

Nilikua sijui nini kinaendelea kwani nilibaki kimya tu. Namuuliza nani wakati kila mtu anajua kila kitu!, si naweza onekama nimechanganyikiwa.

Nilitulia chini na kuwaza kwa kutafakari nimefanya nini hadi yote hayo yatokee,

Nikipo kaa tu nilihisi hali tofauti ya mwili kama mtu aliyeogeleshwa baharini kwa masaa mengi na kutolewa. Niliinua kichwa juu kwenye kiti kile nikiendelea kuwaza na hatimaye usingizi mzito ulishika hatamu.

“hahahahahaha, hahahahahaha, hahahahahaha.. hahahaha” zilikua sauti za vicheko ambazo zilianza kwa sauti ndogo sana, ni kama watu wawili au watutu hivi walikua wakipokezana kucheka, kadri muda ulivyozidi kwenda ndipo vicheko hivyo vilizidi kuongezeka na kuwa kama watu zaidi ya sabani au themanini kasoro hivi walikuwa wakicheka huku wakipishana, walifanya mchezo huo kwa mda mrefu mno hadi kichwa kikaanza kuuma.

Nilitaka kujitoa katika tukio lile lakini tayari nilikuwa nimefungwa kamba mikono na miguu yote, nilishindwa kujikwamua na kuendelea kuangaika tu bila mafanikio.

Nilipoangaika kwa muda mrefu sauti zile ziliacha kwa pamoja na kimya kilitanda. Nikawa nagumia kwa nguvu kwa kuomba msaada, sauti niliyoitoa kwa muda huo ilikuwa kubwa mno…

“Mwalimu, Mwalimu Jaman vipi Kuna tatizo gani! Oh pole e ni njozi, tulia kwanza”. Mbele yangu alikuwa Madam Prica ambaye ndiye pekee alikuwako ofisini, sikujua wengine walienda wapi.

Kwa hali ile nilianza kutetemeka na kutafuta sehemu ambayo mkoba wangu upo kuangalia kama nilikumbuka kubeba msaafu siku hiyo.

Niliingiza mkono na kutoa. Hora!!, nilikutana na makatasi tu niliyokosea Scheme Work yangu. Nilihema kwa nguvu huku Madam akiendelea tu kusikitika kwa kunionea huruma.

“Madamu, inaweza kuwa sa ngapi mda hu”. Nikazuga kwa kuuliza kana kwamba hakuna kilichotoke.

“Oh kamuda kamekwenda kidogo, na me nilikua nakusubili wewe tu nirudi zangu nyumbaniii. Sa Kumi kasoro dakika tatu hiii” aliongea kwa mapozi huku akiangalia saa yake ya mkononi na kukusanya vitu vyake.

Nilichoka sana, kwani sikujua hata siku imeishaje, yaani kulala tu kidogo siku imeisha?

“Hmmm, hata kengele sikuisikia? Na mimi ni mwalimu wa zamu! Oh shit! Mambo gani haya, huu ni uzembe asee” nilijisemea mwenyewe huku nikiambatana na Madam Prisca kutoka ofisini, ili kumpisha mfunga milango ya Ofisi na madarasa afanye kazi yake.

“Da!, Mwalimu yani kila nikikumbuka siku ya leo, sipati picha imeanzaje wala imeishaje. Yaani sielewi: sielewi”. Nilijieleza japo kwa ufupi na kusubili jibu kutoka upande wa pili.

“Hahahaha ile ya asubuhi sijui ni Hotuba sijui ni nini hata, Leo ofisini tumekesha kusurgest majina tofauti ya manemo yako leo asubuhi, hahahaha”. Madam nae akaibua maada yake iliyomsaidia kupanua japo midomo yake na kucheka kwa pozi….

ITAENDELEA……
Ndio kwanza mwalimu anatokea na maluweluwe asiyoyaelewa. Mara, maisha yake yanaanza kuwa magumu katika simo tu ya zamu yake. amelala na kuita mdoto ambayo haina kichwa wala miguu.. fuatana nami ktk siku nyingne sita zilizobaki...

KUMBUKA:
Baadhi ya matukio, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU (04)
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

ILIPOISHIA…
“Da!, Mwalimu yani kila nikikumbuka siku ya leo, sipati picha imeanzaje wala imeishaje. Yaani sielewi: sielewi”. Nilijieleza japo kwa ufupi na kusubili jibu kutoka upande wa pili.

“Hahahaha ile ya asubuhi sijui ni Hotuba sijui ni nini hata, Leo ofisini tumekesha kusurgest majina tofauti ya manemo yako leo asubuhi, hahahaha”. Madam nae akaibua maada yake iliyomsaidia kupanua japo midomo yake na kucheka kwa pozi….

SEHEMU: 04

“Niliongea sana e?” nilihoji. Kwa kutaka kujua nini kilifanyika asubuhi ambacho wengi wanakiongelea na mimi sikijui.

“Weeeh! umetukalisha sisi zaidi ya dakika kumi na tano. Unajitambulisha tu, humalizi, au kisa Chuo chenu kipo Mji mkuu nini?” hakujibu swali vizuri akashushia na kinywaji cha matusi malaini kuelekeza kwenye chuo chetu.

Basi hakuna lililoeleweka hadi tunaachana, nikapita kushoto na kuacha akipanda bodaboda kuelekea kwao.

Siku hiyo hakuna kilichoeleweka hata nilipofika nyumbani, nilikua ni mtu wa kulala tu na kujiziuka, kwa kuwa nilikaa mwenyewe basi ilikua rahisi kwa kujiliwaza na kaswida ili kupandisha imani yangu, wakati nawaza mauza uza niliyoyapata kwa siku nzima. Na siku ikaisha kwa juma wa tatu kuwakalibisha juma wa nne…

Kama ilivyo kawaida kwa siku ya nne ya juma, kijua hakikuacha kuchomoza kivivu maeneo ya shule ya Ruvuma sekondari, rangi yake iliangaza vyema idadi kubwa ya hijabu nyeupe zilizopo kichwani mwa wanafunzi. Bado shule iliitii ile hali ya nizamu kwa kila mwanafunzi kufanya jukumu lake, niliangaika sana kupita kila sehemu kusimamia usafi, sikujali kama nilikua peke yangu siku hiyo, nilihakikisha kila kona inakua safi, sio choo tu hata katika vijisehemu ambavyo vinatunza vumbi kwa muda.

Siku hiyo ilikuwa ni siku yenye ucheshi na hamasa kubwa sana moyoni, kwa vile kazi ya ualimu niliipenda basi sikusita katika kuifanya kwa moyo, niliangaika huku na kule; pale na hapa, lakini idadi ya maeneo ya sehemu ya shule hiyo ilikua kubwa, cha ajabu ni kuwa kila nikiangalia simu yangu kuona saa nakuta ni saa moja na dakika kumi. Napiga moyo konde kuendelea kusimamia usafi.

Kila mwanafunzi alionenekana kuonesha ushilikiano wa maana, hakuna aliyeleta kikwazo!. Bado saa yangu ya mkononi na simu yangu ziliambatana katika kutaja majira ya mida hile. Bado ilikuwa ni sa moja na dakika kumi na tano. Aisee nilichoka, nikakaa kwanza chini na kuangalia jinsi wanafunzi walivyotii nizamu kwa kuendela kufanya usafi.

“Ah!! hapana!!, yaani mbona kama lisaa la nne sasa nafanya usafi tu simalizi?, kila nikiangalia mda saa moja, kila nikiangalia sa moja hmmm! Ila inaweza kuwa kweli, mbona waalimu wengine bado hawajafika……. Aloo we, Mwanafunzi!! Mwambie Timekeper agonge kengele” nilipaza sauti kwa kuagiza moja ya mwanafunzi aliye karibu yangu huku hatua zangu zikielekea sehemu ya mstalini kwaajili ya kuwapeleka tu watoto darasani maana kama mimi nilichoka na sikufanya usafi vipi kwao?.

Dakika mbili kila mtu alikaa katika mstari kusikiliza wito, nilisimama vyema kwa kuwaweka sawa kusikiliza matangazo.

Sikujua waalimu wenzangu walitokea wapi lakini walijaa mahali pale. Wengi wakiwa wameshikwa na butwaa, wengine vifaa vya kufundishia. Baada ya Kwata mbili tatu kiongozi akanikaribisha mwalimu wa zamu kutoa neno, lakini sikua na lolote lile zaidi ya kutangaza kama kuna mwalimu yeyote Yule anatangazo basi alitoe.

“Teachers! Anyone have announcement please?”. Nililopoka, tena nililopoka kwa sauti kubwa sana ya kiingeleza, haikuombwa kurudia, nilihamaki tu kila mwanafunzi alianza kucheka tena kwa sauti kubwa, walicheka sana na hatimaye waalimu wengine walipokea kicheko hicho huku wale wazoefu wakitawanyika kwa kwenda kuendelea na majukumu yao.

Nilipagawa sana kuona mambo kama hayo yanatokea, hasira zilinishika sana, lakini nikawa mpole tu kwani wanasema “hasira hasara” kwa bahati nzuri Mkuu wa shule naye alikua anasogea taratibu sehemu ya tukio. Kabla hajakalibia nilimkimbilia kwanza kumpokea wakati waalimu wengine tayari wameshatawanyika na kubaki wanafunzi ambao bado walikuwa wanacheka.

“Mwalimu, kuna nini tena mbona kushtuana, kuna tatizo?” Mwalimu Mkuu alihoji uku akiweka sawa shati lake mikononi.

“hamna Mkuu ni kengele tu ya kawaida, watoto wamechoka na usafi umeisha sa bora tu wakasome, nje hawana kazi tena!” nilijitetea.

“wakasome?, kwani walikua wapi kabla?” swali lile lilinitatanisha kidogo, kabla sijajibu akatoa Amri kwa wanafunzi kwenda darasani, kisha akanigeukia na kuanza kuongozana nae kuelekea ofisini.

“Mwalimu siku hizi kengele hatupigipigi tu kila mda, shule inawenyewe hii!” aliongea huku akinipigapiga mgongoni. Nilichoka sana kwa kweli. Nilitaka kuuliza lakini ukubwa ukaingilia kati ‘nikafunika kombe ili mwanaharamu apite’….

ITAENDELEA…

KUMBUKA:
Baadhi ya matukio, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU (05)
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

ILIPOISHIA…
“wakasome?, kwani walikua wapi kabla?” swali lile lilinitatanisha kidogo, kabla sijajibu akatoa Amri kwa wanafunzi kwenda darasani, kisha akanigeukia na kuanza kuongozana nae kuelekea ofisini.

“Mwalimu siku hizi kengele hatupigipigi tu kila mda, shule inawenyewe hii!” aliongea huku akinipigapiga mgongoni. Nilichoka sana kwa kweli. Nilitaka kuuliza lakini ukubwa ukaingilia kati ‘nikafunika kombe ili mwanaharamu apite’….

SEHEMU: 05

“Sawa mkuu” tuliachana kila mtu akienda ofisini, nilikua na mawazo sana kwani hadi mda huo hakuna kitu nilichokielewa.

Wakati napanda ngazi ya kuelekea ofisini nilitoa simu yangu kwa kuangalia jumbe fupi, baada ya kutoa Lock nikakutana na Pop-notification ya ujumbe kutoka namba ngeni.

Nilipandisha macho yangu juu ya ujumbe ule na kukutana na tarakimu kubwa nne zilizoonyesha saa kwa ufaha, 13:28. Nilisimama na kuganda mlangoni. Kichwa kikawa kizito ghafla kwa kuanza kuitafakari saa hile kwamba ni kweli au ndo masaa ya kizungu yalikuwa yananichanganya.!.

“Naomba kupita Baba!” sauti nzito ya Mwanamke ilisisika, niligeuka kwa kumpisha alikuwa ni Mama Mpoli.

mama ambaye analeta chakula cha mchana kila siku za juma, alikua amebeba ndoo mbili na beseni kichwani kama kawaida yake akileta chakula mda wa mchana, ni kweli ilikuwa sa saba ndugu wasikilizaji.

Hapo ndipo nikahisi kufa. Nilichoka jamani, sijui kama nitakuja kuchoka kama nilivyochoka siku hiyo. Nilitamani nikae chini kabisa ya sakafu. Mawazo yakazidi hadi kichwa kikawa kinauma, sikujiskia njaa wala hamu ya kula; masikio yalikuwa yameziba kabisa.

Msikilizaji hata ungekuwa wewe usingeamini kabisa lakini ni kweli kabisa yani hiyo hali ilinitokea mimi. Kwa haraka haraka ilikuwa ni kwamba nilifanya usafi kwa muda usiozidi na kupungua masaa nane. Alafu kumbe kengele niliyoipiga iliwatoa walimu katika vipindi. Sasa usafi wa masaa yote hayo nilikuwa nafanya na nani?. Maana nilikuja saa kumi na mbili asubuhi. nikapagawa.

Nikawa najiuliza hiki naacha; kinakuja hiki kinapita; linafika hili linakwenda kwa kweli sikuwa sawa; nilichanganyikiwa. Nilishukuru Mungu siku hiyo ikapita na ikafika siku kiboko yake. Ilijaa maajabu zaidi ya iliyopita…..

------

Ilikuwa ni jumatano angavu ambayo anga lilikasilika, kila jambo lilienda mlama siku hiyo, nakumbuka saa nne asubuhi tu nilishikwa mkono na Madamu Haule na kutoka nje ya ofisi. alikua naye Mwalimu mwenzangu tuliokuja katika mafunzo.

Nilijalibu kuhoji tunaenda wapi lakini sikupata jibu. Alinishika mkono kwa nguvu na kuongoza njia, tulipita madarasa ya kidato channe, cha tatu na hatimaye cha pili na hadi kidato cha kwanza, bado mwendo ukiwa mkali na hakuna neno lilizungumzwa na Mwalimu huyo zaidi ya kunishika mkono kwa nguvu na kunipeleka sehemu nisiyoijua.

Tuliongozana hadi kufikia kwenye kiwanja cha mpira wa miguu, hapo akasimama na kugeuka kuniangalia, akakutana na swali lilelile “Tunaenda wapi Mwalimu”, kwa kuwa tulizoea kila siku maksihara akatabasamu tu kidogo akanishika tena mkono na kuendelea na safari bila kuongea chochote.

Kwa sasa tulikuwa tunakalibia poli kubwa lilikuwa linaziba shule kwa kuacha mpaka kati ya shule na nyumba za wanakijiji., nashangaa tulitembea sana hadi nikaanza kuchukia.

Nikaanza kusimama kwa kutotaka kusogea mbele, nilitaka kujikwamua kutoka mikononi mwake lakini sikuweza, alikuwa amenizidi nguvu tayari, janja yote ilishia mashavuni mwake kwa kugeuka kutabasamu na kunivuta kuendelea na safari.

Nakumbuka toka hapo tulipo tulitembea tena kwa dakika hadi kumi hivi, tukayaacha majani makubwa na kutokea katika dimbwi la miti mingi na mikubwa iliyoota bila kuacha nafasi.

Nikaanza kuogopa kwani kwa jinsi sehemu ilivyo ilikuwa ni msitu kabisa, sidhani kama kuna aina ya misitu kama hiyo mkoa huu wa Ruvuma….

ITAENDELEA….

KUMBUKA:
Baadhi ya, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo….

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU (06)
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

ILIPOISHIA…

Nakumbuka toka hapo tulipo tulitembea tena kwa dakika hadi kumi hivi, tukayaacha majani makubwa na kutokea katika dimbwi la miti mingi na mikubwa iliyoota bila kuacha nafasi.

Nikaanza kuogopa kwani kwa jinsi sehemu ilivyo ilikuwa ni msitu kabisa, sidhani kama kuna aina ya misitu kama hiyo mkoa huu wa Ruvuma….

SEHEMU: 6

Hapo nikakasilika na kuchukua maamuzi mkononi, nikasimama ghafla na kujariibu kujitoa katika mikono yake, Yes! Niliweza, nilijitoa katika mikono yake. Hapo hakugeuka tena kama alivyokuwa anafanya mwanzo, wala hakugeuka nyuma kabisa,

Aliangalia mbele tu huku mimi nikiwa nyuma yake, kwa kuwa nilimzoea sikuona shida, nikataka kuongea lakini sikupata nafasi hali kama hile ya mdomo kuwa mzito ilinirudia tena. Sikuongea chochote.

Ghafla eneo hilo lilianza kutanda mvuke ambao ulikua unaenea kama moshi hivi, nilichokiona kutoka kwa Madam Haule ni nyele zake za kichwani kuongezeka ukubwa na kuwa ndefu sana, kwa makadilio zilikalibia kufika sehemu yake ya magoti; zilirefuka mno.

hapo hofu ikaanza kunitanda na kuanza kutetemeka, hadi wakati huo sikupata mda wala nafasi ya kuongea chochote, mwili nao ulikuwa mzito haswa kiasi kwamba nilishindwa kukaa wala kukimbia, nilijikuta tu nimesimama.

Mvuke ulikuwa mkubwa kiasi kwamba tulishindwa kuonana, sikumwona tena Madam Haule, msitu ulikuwa kimya sana kiasi kwamba hakuna ndege wala majani yaliyotikisika.

Nilitetemeka kwa kasi kama yale majenereta ya hospitali kuu ya Muhimbili kitengo cha moyo. Sikujua ni jasho au maji yaliyolowanisha mwili wangu; nilikuwa nimelowa.

Punde zilianza sikika sauti za kuniita zikianza kwa upole, zilianza taratibu lakini baadae zilianza kukinzana..

“Yusuphu!” sauti ya kwanza niliitambua inafanana na Mwalimu Kasembe, nilitaka kupiga kelele za kuomba msaada lakini nilishindwa, bado nilikuwa bubu, ni machozi tu na jasho ndio vilihamaki mwili wangu.

Ikasikika nyingine kutoka upande wa kulia “Yusuphu!” hii ilikuwa inafanana na Mwalimu Luoga kabisa kwa asilimia zote, sijakaa sawa ikasikika nyingine “Yusuphu”, nikaganda kutafakari sauti hii ilikuwa ya nani kabla sijapata jibu ikasikika nyingine ya Mwalimu “Choroko”, baada ya hapo sauti zote zikawa zinajirudia rudia kama wanashindana kuniita sasa.

“Yusuph, Yusuph, Yus, Yusuphu, Yu, Yusuph, Yu….” Zilikuwa sauti za wale wale, zilinichanganya na kichwa kuanza kuuma.

Nilishindwa kuelewa nini nifanye; niliganda tu pasipo uwezo wa kunyanyua kiungo chochote cha mwili wangu; nilishindwa, hapo hapo sauti hizo zikaanza kuambatana na vicheko vya watoto ambao umri wao ulikuwa ni miaka mitano au sita hivi, sauti hizo zilianza kuchanganya na kuafuatiwa na za watu wazima.

“Msaadaaaaaa!”. Oh my God!, sauti hatimaye ikatoka na kunga kubwa, huku mwangi hukijirudia, ghafla nikashangaa mwili unakuwa mwepesi ghafla na nguvu kunijia, ukungu nao ukatoweka ghafla na kuniachia njia ya kukimbilia, bado nilikuwa mwenyewe, Sikumuona tena Madam Haule; ambaye niliamini alinitelekeza.

Asee!! nilikimbia sana, nilikimbia huku moyo ukijionya kwa kufika sehemu hatari ya namna hiyo, nilikimbia sana kiasi kwamba hata huyo mnae mwamini kuwa ndio mkiza upepo nambari moja wa dunia sijui “Hussein Bolt” hawezi kufua dafu, hizi zilikua ni mbio za ushindi wa maisha. sio mbio za kutangaza taifa na kupata medali, nilikimbia sana ndugu wasikilizaji, nilikimbia bila kuangalia nyuma au la.

Kigiza nacho kikaangaza machoni mwangu, ghafla nguvu nazo zikaanza kuniisha, mwendo ukapungua na hatimaye kusimama kabisa, nikayumba kama mara mbili hivi na kuanguka chini Puuuh! Kama mzigo wa maindi,

ukungu ule wa mwanzo ukaja tena kwa kasi, safari hii ulikuwa mzito sana tofauti na ule wa mwanzo na kunifanya nishindwe kupata pumzi sawasawa. Nilizimia: Nilizimia ndugu wasikilizaji. Nilizimia jamani. Sikujua nini kilifuata baada ya kupoteza fahamu.
----

Nilikuja kuamka nipo kitandani kwangu nikiwa nimelala chali, nikiwa tumbo wazi na bukta tu ikifunika sehemu zangu za utupu, niliinua kichwa na kuanza kujikagua, nilikutana na baadhi ya majani mabichi kifuani, chale kadhaa maeneo ya kifua na ukingo wa tumbo.

Nilihamaki sana na kupatwa na maluweluwe ya hapa na pale, nilianza kuwa na roho ngumu ya kuanza kuzoea mauzauza hayo, nilitoka kitandani kufuata kioo kikubwa kilichopo ukutani, nilijichungulia mgongoni japo kwa wiziwizi lakini nilifanikiwa kujiona, hakukuwa na chale wala majani, ila kulikuwa na rangi nyeusi tofauti na rangi iliyopo upande wa mbele wa mwili wangu. Pumzi ndefu nilishusha na kuanza kutamka baadhi ya maneno.

“Ewe Allah! Naomba ni…” sikumalizia simu ya mkononi ikaita, tena ikaita kwa sauti kubwa, cha kuchangaza simu ilikuwa karibu yangu juu ya meza tu,

nikachungulia nani anapiga alfajiri hili na kukutana na jina la Mtima wangu. “Mama”, nikatabasamu kwa kusahau shida zote zilizopitia, nikapokea…

ITAENDELEA…

KUMBUKA:
Baadhi ya, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo…

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU (07)
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

ILIPOISHIA…

Nilihamaki sana na kupatwa na maluweluwe ya hapa na pale, nilianza kuwa na roho ngumu ya kuanza kuzoea mauzauza hayo, nilitoka kitandani kufuata kioo kikubwa kilichopo ukutani,

Nilijichungulia mgongoni japo kwa wiziwizi lakini nilifanikiwa kujiona, hakukuwa na chale wala majani, ila kulikuwa na rangi nyeusi tofauti na rangi iliyopo upande wa mbele wa mwili wangu. Pumzi ndefu nilishusha na kuanza kutamka baadhi ya maneno.

“Ewe Allah! Naomba ni…” sikumalizia simu ya mkononi ikaita, tena ikaita kwa sauti kubwa, cha kuchangaza simu ilikuwa karibu yangu juu ya meza tu, nikachungulia nani anapiga alfajiri hili na kukutana na jina la Mtima wangu. “Mama”, nikatabasamu kwa kusahau shida zote zilizopitia, nikapokea…

SEHEMU: 07

“Aloo!, Ee mimi mzima,.. Ndio mzima,... Mama e mimi mzima kabisa wa afya, naaam.... hamna mama, Sa kama nimekufa ndo ningepokea simu?, ah! Usijali Mama..” simu nayo haukuisha utamu, ikakata, nikajaribu kupiga haikupatikana.

Nilijua ni mtandao wa sehemu alipo kwani hakukua na huduma nzuri za mtandao hadi aanze yeye kupiga.

Zilikua ni taarifa kutoka kwa Mama yangu mzazi kuwa Ameniota et nimefariki.. ndio dababu haswa ya kupiga simu asubuhi hiyo.

Nikapiga moyo konde na kuanza kujiandaa kuelekea shule, nikasahau kabisa kumrudia Muumba wangu kwa kumalizia dua niliyoianza. Nikavaa kibishi na kuanza safari ya kwenda Shule.

Kikukweli ndugu msikilizaji, sikuanza kuwa na hofu tena kwani nilianza kuzoea mauzauza hayo. Sijui nini kilinisukuma kuzoea hali hiyo.

Basi nilifika shule japo kwa kuchelewa, siku hii ya Alhamisi nilichelewa shule lakini hakuna kilichohalibika, kila kitu kilienda sawa, yamkini nikaanza kuwaogopa baadhi ya waalimu walionitokea katika tukio la jana yake,

Sikuwapa ushilikiano hata kidogo, hasa hasa huyu Madam Haule na roho yake ilivyo mbaya, siku nyingine nikizembea atanipeleka baharini, na jinsi nilivyo mzembe kuogelea sijui nini kitatokea..

Siku hii niliamua kutoka kabisa ofisini na kushinda madarasani, nilikua nazunguka tu kutoka darasa hili kwenda lingine kupiga stori na wanafunzi.

Nikiwa napita darasa moja la kidato cha tatu niliitwa na Mwalimu moja kusaidia kuchapa. Sikuwai kuthubutu kuchapa katika maisha yangu lakini sijui kijana huyu aitwae tamaa ilitokea wapi; nilikuwa na hamu ya kupiga watoto wa watu, miguu ikawa miepesi mno kukimbilia tenda hiyo.

Nikavuta kiboko kilichopo karibu, nikaanza na wakwanza, alikuwa wa kiume, nikamlamba mbili akaenda kukaa, wa pili alikuwa wa kike, alikuwa msumbufu sana katika kupigwa;

Alinipa shida sana hadi kumpiga kiboko kimoja, kiboko chenyewe hakikuingia sawasawa hata, lakini nilimwona machozi yanamtoka na kuanza kuishiwa nguvu huku bado akinyoosha mkono kumalizia idadi yake, nilivaa roho ngumu kweli kwa kuinua mkono wangu kumalizia adhabu ya kiboko cha pili, sikutilia hata maanani hapi yake aliyoanza kubadilika. nilijua tu mapozi ya watoto wa kike pindi waadhibiwapo : sasa unadhani hata nilifanikiwa kumchapa kiboko kingine? ndugu msikilizaji sikuweza kufanya hivyo.

Naaaam! Alilegea tu na kuanguka chini. nakili kuwa kile kiboko cha kwanza ndio kilimyima nguvu. nikaanza kumgusa gusa kwa kumuamsha. hakuamka. alikuwa amezimia. amezimia kwa kiboko komoja tu.

Alizimia yule mtoto ndugu wasilikizaji. Basi nikaomba wasichana kadhaa kumbeba na kumpeleka sehemu yenye hewa na huduma nyingine za kumuamsha zikaendelea.

Walitumia kila kitu, mashati, daftari, kanga vitenge vya waalimu, maji... lakini bado hakuamka.

Nikagharamia pesa zangu za mkononi kwa zoezi la kumpeleka hospitali ya mkoa. alipelekwa huko na alidumu huko kwa muda wa masaa matatu tu. Nikaja kupewa taarifa kuwa mwanafunzi yule amefariki dunia!. amekufa.

Daa! Hakuna kitu kibaya kama hiki!, nimeua, naiweka wapi mimi sura yangu, nakimbilia wapi mimi, e! kuua! We sikia tu kwenye bomba, nilikuwa na hali mbaya: sikumbuki kama nilikumbuka kuna choo siku hiyo, maana kila haja nilidhani inapitiliza tu sio ndogo ndogo hata zile haja kubwa.

Basi hadi kufika sa nane nilikuwa sina amani kabisa nikawa nasubiri sheria za shule, chuo na nchi zinihukumu, nilifunga mikono yangu nyuma kwa kukata tamaa.

Hatimaye kengele ya kutawanyika ikagonga kwa nguvu na tangazo la waalimu wote kukusanyika na wanafunzi likafuata. Baada ya kimya kirefu alipanda jukwaani Mwalimu mkuu na kuanza kutoa tangazo ambalo lilikuwa lazima litolewa.

Tangazo ambalo lilikuwa ni la kuendelea kupasua na kucharanga moyo wangu. Tangazo la Kuua

“Ndugu, makamu mkuu wa shule, waalimu, wafanyakazi na wanafunzi wengine, tumepokea kwa masikitiko makubwa taarifa ya kumpoteza moja ya mwanafunzi wetu aliyekuwa anasoma kidato cha tatu mkondo C, kutokana na taarifa tulizopokea toka hospitali ya mkoa zinasemaa…” akasita kuongea kidogo na kugeuka nyuma kuwaangalia waalimu.

Alipitisha macho yake kwa kila mwalimu na mwisho kugongana macho na mimi, tendo ambalo sio la kawaida ni kuwa mwalimu huyo aliachia tu tabasamu mbele yangu na kufungua dayari yake ndogo iliyojaa mkononi mwake.

Presha inilikuwa nayo mwanzo ilizidi kuongezeka hadi kufikia 270/120 kama ningekuwa magurudumu basi ningepasuka kabisa yani, akageuza sura yake kwa umati wa wanafunzi na kuendelea kuongea

“..Ah! kutokana na majibu kutoka hospitali ni kwamba marehemu alifariki ghafla mara baada ya kuanguka kutoka kitandani!, ripoti inasema kuwa mgonjwa alikua anasumbuliwa na Pumu na ilimuanza masaa nane kabla hajapelekwa hospitali, baada ya kupelekwa hospitali na jitihada kutoka kwa madaktari zikagonga mwamba mara baada ya mgonjwa huyo kuanguka mda wa mapumziko alipokuwa anasubiri kupata dozi yake ya mwisho.” Hapo akaacha na kumwita mwalimu mkuu msaidizi.

Nilipigwa na butwaa kwa kushangazwa na taarifa zile, sikuwa na uhakika kwamba ni ripoti kweli za daktari au ni ripoti iliyoingiliwa kati na wakuu wale wa shule?, akamuuma sikio mwalimu mkuu msaidizi na kisha kumalizia kuongea…

ITAENDELEA…
Mwalimu amebakiza siku moja tu ya ijumaa na taatifa kifo bado ikimnyima nguvu.... fuatana nami katika tamati ya sehemu inayofuta ya mkasa huu..


KUMBUKA:
Baadhi ya, sehemu na watu katika simulizi hii ni ya kweli. Lakini simulizi ni ya kutungwa na haina uhusiano wowote hule kati ya matukio mengi ya humu na uhalisia wa sehemu yenyewe. Karibu katika mwendelezo…
 
SIMULIZI FUPI: MWALIMU WA ZAMU
MTUNZI: XAVERY LUOGA *AUTHOR XAV*
Namba: 0672493994
==================================

ILIPOISHIA…

Nilipigwa na butwaa kwa kushangazwa na taarifa zile, sikuwa na uhakika kwamba ni ripoti kweli za daktari au ni ripoti iliyoingiliwa kati na wakuu wale wa shule?, akamuuma sikio mwalimu mkuu msaidizi na kisha kumalizia…

SEHEMU: 08

“Mazishi yatafanyika nyumbani kwao mkoa wa Njombe siku ya alhamisi ijayo, na maiti itasafilishwa siku ya jumatatu asubuhi. Mwili huo utaagwa na baadhi ya waalimu na wanafunzi hospitalini, utaratibu mwingine mtatangaziwa…. Raha ya milele humpe e bwana na mwanga wa milele umwangazie, astarehe kwa Amani”.

“Amina” shule ikaitikia kwa masikitiko makubwa na taratibu nyingne zikaendelea hadi kurudishwa kwa wanafunzi. Waalimu nao tukatawanyika kuelekea majumbani kwetu. sikupata kuamini tukio lile.

Kila siku ilikuwa mpya kwangu, matatizo yalinifanya nikomae kimaisha, nilikuwa nimeanza kuzoea ndugu msikilizaji, kwa siku zilizobaki chozi lilikuwa halitoki, kwa maana nimeshazoea. Nitalia mara ngapi?.

Basi siku ya ijumaa siku ya mwisho kabisa katika Zamu yangu shuleni hapo, ilikua ni siku ambayo jua lilikuwa ni kali kisasi, ahsubuhi iliisha kimazabe na mchana kukalibia.

Wakati nipo ofisini nilipata ujumbe mfupi kutoka kwa Mwalimu mwenzangu. Mwalimu Kusa. Ujumbe huo ulisomeka vyema kabisa katika simu yangu.

“Da! Unamatatizo sana Mwalimu wangu. Kuna mda naitaji kukusaidia lakini nashindwa kwa kuwa utanifikilia vibaya sana, lakini kama utakuwa tayari nakuomba nikusaidie.” Baada ya ujumbe huo niliangaza huku na huko ofisi nzima sikumuona.

Nikatoka nje na kumwona amekaa katika kizingiti kilicho karibu na kidato cha tatu, nilimsogelea na kuitaji msaada wake, mambo yalinikalia kooni, yalishanishinda kwa kweli.

“Mwalimu unasiku moja tu imebaki leo, tunaweza kukupoteza!” Mwalimu alianza kwa kunitisha ili iwe rahisi kunishawishi.

“Hmm! Kwanini mwalimu?” nilihoji.

“Kwa sababu kwanza unamaliza zamu ijumaa, ambayo ni leo, na bado nyota yako ipo kwao na leo ni siku nzuri kwao ya kukuhitaji!” aliongea huku akionyesha sura ya huruma na kuniangalia usoni.

“Mwalimu sielewi mimi, kwanini unasema hivyo?”

“Ni hivii… kwanza nyota yako imependwa na watu wabaya, pili wakabadilisha zamu, zamu hii ilibidi iwe yangu lakini nashangaa ukatajwa wewe, kuna watu wabaya wanataka kukupoteza. Mimi kuna mtu ananisaidia sana na ndiyo anayeniambia kila kitu. Kwa hatari iliyopo mbele nakushauli nifuate mwalimu. Tunaenda kwa mtaalamu.”

“Mtaalamu?... Mganga??” nilishituka.

“Ni kwaajili yako lakini, nimeamua kukusaidia” aliishia hapo na kusubili jibu la hapana au ndiyo.

Kwa kweli shughuli za waganga nilizisikia tu kwa bongo muvi na wengi wa waganga walikuwa ni matapeli tu, hawakuwa na msaada wowote ule, na hadi nipo hapo sijawai fikilia neno mganga katika kichwa changu. Kwa kuwa nilihaidiwa kusaidiwa basi sikua na budi kusaidiwa.

“Ndiyo mwalimu, naomba twende, tena mda huu kama hutakuwa free. Naenda omba ruhusu kule chini au vipi mwalimu?” nikamtupia swali ambalo hakulijibu, akanyunyuka na kuongoza njia kwenda ofisini.

Mimi nilifanya kama nilivyo mwambia na ruhusa haikuwa na pingamizi lolote, niliomba naenda hospitali, najiskia vibaya. Nikaungana na Mwalimu kusa na safari ya kwa mtaalamu ikawadia.

Tulitembea maeneo ya vichaka na hatukukawia tulifika kwa mtaalamu, kabla hata hatujaingia, tukiwa tu mlangoni tukasimamishwa.

Tukaamuliwa kwanza kuvua viatu na kusimama wima. Tukasimama kwa dakika kama mbili hivi na kumwacha mtaalamu aungurume kwanza.

Matukio kama haya nilishayazoea kwenye movi kwa hivyo ilikuwa kawaida tu.

Baada ya hapo tukaruhusiwa kuingia, mimi nilikuwa mgeni sikusema chochote kile zaidi kumwacha Mwalimu mwenzangu akamilishe mambo.

“Kijana! Unanyota kali sana! Wameichukuwa!!, una kazi nzito mbele kijana wangu, lakini kitu cha kukuambia ni kuwa yote uliyokutana nayo ni hadithi tu, hakuna la kweli hata moja” akaishia apo na kuanza kucheka kwa nguvu. Kisha akaendelea.

“Yaani unafuatwa kila sehemu, hata hapa umekuja nao, ndio maana nikakusimamisha kwa mda mrefu nipambane nao kwanza. Hahahahahahaha! Tatizo ni kubwa sana, mwalimu unafanya usafi hadi saa nane! Hahahahahaha, mwalimu jana tu umetoka kuua mtu!! Hahahahahahahaha.” Vilikuwa ni vicheko tu vya mtaalamu Yule, nikaanza kuweka imani yangu kwake kwa kila alisemalo ni kweli tu.

“Kijana kila lililo kutokea sio la kweli, ila yalikuwa ni maandalizi tu kuanza kukuchukua, wameanza na nyota yako, leo wanataka kukumalizia na wewe, vizuri umewahi.

Kijana maisha ya shule yanendelea kama kawaida vitu unavyovifanya na kuviona unavifanya ukiwa peke yako, wengine hawavioni, mfano ulipogonga kengele siku ile, walimu walikuwa kwenye vipindi wanafundisha, lakini wewe unaona wanafunzi wapo nje wanafanya usafi.

Hahahahahahaha! Watu ni wabaya sana, mda mwingine watu wabaya wanatumia rafiki zako wa karibu kukuharibia, mfano Mwanamke aliyekupeleka msituni hakuwa yeye unayemdhania, ila alitumika kama kivuli tu kukutesa!!!. Hahahahaha kijana Ruvuma hakuna msitu kama ule, pale ulikuwa Nchini msumbiji.

Ulikwenda na kurudi kwa masaa kadhaa tu. Hahahahahahahahahaa hahahahahaha, Yusuph, Yusuph, wacha nikupe dawa leo ya kukuzuia wasikuone, kesho tutafanya matibabu ya kurudisha nyota yako.

Lakini kitu cha mwisho ambacho inabidi ukitambue kwamba ukienda mkoa wa watu kuna tamaduni tofauti, kuna misingi tofauti, kuna imani tofauti, dunia ya sasa sio dunia ile ya zamani kwa sasa hivi kila mtu anakinga, dunia imehalibika sana kila mtu anamtafuta mtu dhaifu amuonee, kinga ni muhimu sana, nitakuchanja kwa kukulinda, nitakupa kinga ya muda mrefu..” mganga aliongea na kumaliza yote, akanipa dawa ya kuoga na kunywa asubui. Nikamshukuru kwa msaada,

kilitutoka kiasi cha elfu tatu tu kwa tiba hile ya siku ya kwanza, tukaondoka kwenda shuleni kwa kuwa bado muda wa kazi uliendelea.

Nilipofika tu mlango wa ofisi, nilikutana na Mwalimu Catherine ambaye mkononi mwake alishika kitabu kitakatifu cha Mungu. Alinishika begani na kutabasamu kidogo, hapo akaniita kando na kuanza kuzungumza na mimi.

“Yesu amenituma nikukomboe! Naomba tuzame katika maombi kwa maana imani ya kweli bado inaishi katika roho yako!”, nikaanza kuwaza kama kuna sherti kutoka kwa mganga lililosema siruhusiwi kuombewa: hakuna. Nikakubali.

“Sasa sikia, tutatoka hapa na Madamu na Prisca, moja kwa moja hadi katika vyumba vya dini, tutaunganisha madhehebu yote na kuanza maombi.” Aliongea huku hakiwa hana hata chembe ya kicheko mashavuni. nikakubali.

Kwa kuwa ulikuwa ni muda wa dini basi tukaelekea kiwanjani maana watu walikuwa ni wengi sana, haya yalikuwa ni maombi ya mwaka mzima ambayo hayajawai kotokea, madhehebu yote yaliungana kwa imani na kila mtu aliomba, tena maombi ya imani, kuzuia na kupinga kila baya.

Maonbi yalisikika kila pande nilikuwa bado nipo chini nimepiga magoti na kuendelea kusuburi miujiza ya Allah tu. Takribani robo saa bado sikuhisi chochote, lakini kadri mda ulivyozidi kwenda nilianza kuona kizunguzungu na mwishowe nikazimia.

Nilikuja kuzinduka nipo hospitali ya mkoa… ni jana tu hapa ndugu wasikilizaji. Jana ndio nimeamka, nasikia nimekaa huku kwa siku tatu bila kuzinduka. Ndugu wasikilizaji mliokuwa hapa, hii ni hadithi ambayo imenitokea mimi.

Nashukuru sana waalimu wenzangu kwa kunisaidia kunitoa katika fungu la shetani. Hadi sasa naona kila kitu kipo sawa, hata ule weusi na chanjo zilizopo mwilini mwangu zimeshaisha na kutoweka kabisa. Nashukuru sana kwa kuja kunijulia hali na kusikiliza japo kwa uchache mkasa huu.

Nawashauli tu kwamba ni sharti Usiache kumwamini muumba wako, binadamu hana msaada wowote utakapoanguka.

Cheki sasa hata Yule mtaalamu ambaye alihaidi kunisaidia; Mwalimu kussa amenipa siri kuwa amefariki siku ya pili yake tu. Hakuna mweza zaidi ya Mungu Baba.

“Simulizi hii imetungwa na Xav Emmanuel Luoga @Author_Xav.

Natoa shukran zangu kwa wasomaji wa simulizi hii kuanzia mwanzo hadi mwisho. Niwakaribishe katika simulizi nyingine zinazokuja.
Kwa maoni ushari na msaada wowote usisite kuwasiliana name kupitia 0672493994
AHSANTENI.”

*****MWISHO****



Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom