Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

the_legend

JF-Expert Member
Joined
Jan 14, 2019
Posts
1,612
Reaction score
7,110
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA KWANZA

Erick Amuona Lucia Kwa Mara Ya kwanza

“Amani ya Kristu iwe nawe” “Iwe nawe pia” walikuwa ni Eric na Lucia wakipeana mikono ya amani katikati ya ibada ya mkesha wa Noeli Parokia ya Mavurunza Kimara Jijini Dar es salaam. Padre Masunga alisisitiza waumini wapeane mikono ya amani kwa kumaanisha na kuwa kama kuna mtu anajua ana chuki na mwenzake basi ni wakati wa kuombana msamaha kwani haitakuwa na maana waumini kusherehekea kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo huku wakiwa na chuki na visasi na majirani zao. Padre Masunga alisisitiza kuwa waumini wasalimiane kwa kujuliana hali tena kwa tabasamu.

Lucia, msichana mrembo sana mzuri kwa sura na umbo alikuwa akisalimiana na Eric kijana mtanashati tena mseminari. Lucia alikuwa na nywele ndefu za rangi ya blond, macho yake yalijaa kope nyingi utadhani ameongezea na za bandia alikuwa hawezi kumtazama mtu usoni kwa sekunde tatu kwa jinsi alivyojaa haiba na aibu.Alikuwa ni mrefu na mwenye umbo la wastani lakini cha mno kuhusu Lucia aliweza sana kujua kuvaa na kujipamba ilikuwa ni kawaida sana yeye kupita na kila mtu wa kike na wa kiume kumwangalia na kumpenda.Hakika alivutia sana kwa macho.

Eric alimpa mkono wa amani Lucia na ghafla alijikuta moyo wake unakwenda mbio kwa jinsi mkono wa Lucia ulivyokuwa laini. Lucia alimtazama machoni Eric kwa kuibia kisha aliangalia chini kwa aibu kama kawaida yake. Eric aliendelea kuushika mkono wa Lucia bila kuuachia, haikuwa kawaida kwani mtu hutakiwa kumshika mkono na baada ya kusalimiana hutakiwa kumwachia na kumsalimia mtu mwingine. Lucia alikuwa amekaa dawati la nyuma ya Eric.Baada ya sekunde kadhaa Eric aliuachia ule mkono wa Lucia na kuendelea kusalimia waumini wengine. Kisha ibada ikaendelea.

Ibada iliendelea huku akili ya Eric ikiwa imehama. Eric alikuwa ni mwanafunzi wa seminari kubwa ya Kipalapala Tabora. Alikuwa akiendelea na masomo yake ya upadre na sasa alikuwa likizo. Katika maisha yake Eric hakuwa amewahi kukutana na mwanamke kimwili. Ni kijana alielelewa kwenye familia yenye maadili sana na hakika hakuwahi kuwa na mahusiano na mwanamke ya kimapenzi japo mara nyingi alikuwa akiingia kwenye vishawishi hivyo. Eric siku zote aliamini padre hutakiwa kuwa mtakatifu na kuwa kwa kazi ile ya uchungaji anayoitaka ambayo hairuhusu kuoa alijitahidi sana kutojiingiza kwenye mahusiano ya kingono.

Ibada ilikuwa ikiendelea lakini Eric akili yake haikuwa pale. Alishindwa kuelewa nini kinatokea akilini mwake, inakuwaje anashindwa kuzingatia ibada mara tu baada ya kumuona Lucia.Wakati hayo yakiendelea Lucia nae alikuwa akitafakari kuhusu Eric kumng’ang’ania mkono wake bila kumsemesha chochote. Hakuwa akimjua Eric na kama ni mwanafunzi wa u padre lakini nae akili haikumtulia.

Ilipofika muda wa watu kwenda kupokea sakramenti Eric aliwahi sana ili aweze kurudi mapema na kukaa kumtazama Lucia. Wakati Lucia akiwa anarudi ndipo Eric aliweza kumtazama vizuri na kwa umakini. Mapigo ya moyo ya Eric yalikuwa yakienda kwa kasi sana. Lucia nae bila kujua alimtupia macho Eric na kujikuta anapoteza hatua na kutaka kudondoka. Eric hakuweza kujizuia alichukua karatasi iliyokuwa ndani ya misale yake (Kitabu kinachoonyesha masomo ya siku hiyo) akaandika “Naitwa Eric ningependa kuongea nawe baada ya Ibada kama hutojali.Asante” alipomaliza alikikunja na kutafakari namna ya kumpa Lucia alieketi nafasi ya nyuma yake.

Wakati akitafakari ulikuwa umefika muda wa kutoa sadaka ya pili hivyo vikapu vya sadaka vilikuwa vikipita kwenye viti unaweka sadaka halafu unampa mwenzako nae akimaliza anampa mwengine hivyo hivyo. Eric akaona hapo ndio muda wa kupenyeza ujumbe wake.Alipokipokea kikapu akaweka sadaka kisha badala ya kumpa wa pembeni yake yeye akageuka akampa Lucia kikapu lakini mkono mmoja akiwa ameshika kile kikaratasi akamshikisha Lucia vyote. Haraka Lucia akang’amua kuwa ule ujumbe ulikuwa wake hivyo akaweka sadaka kwenye kikapu na kumpa wa pembeni yake na kubaki na ule ujumbe. Baada ya dakika kadhaa kupita kwa siri Lucia alifungua kile kikaratasi na kusoma ule ujumbe. Mapigo ya moyo yalimwenda mbio kwani alianza kuhisi nini kitafuata na yeye hakuwa akimjua mwanaume mpaka umri ule. Lucia ndio kwanza alikuwa amejiunga na Chuo kikuu mwaka wa kwanza shahada ya Sheria.

Wakati hayo yakiendelea padre Masunga alisimama na kutoa tangazo kuwa katika ibada ile wapo vijana waliopo seminari wanaosomea u padre na angependa waumini wawafaham kwani ndio mapadre wao wa kesho. Vijana watatu walisimama lakini Eric hakusimama. Hakusimama kwa makusudi kwani kwa anachotaka kuongea na Lucia hakutaka kabisa Lucia ajue kama yeye anasomea u padre. “Nilimwona Eric hapa amekaa wapi mbona simwoni kusimama” alikuwa ni padre Masunga akimwita Eric asimame huku akizungusha shingo kumtafuta alipokaa. Haraka Eric alisimama kwa aibu. Waumini waliwapigia makofi na kisha walikaa.

Baada ya ibada Eric alihitajika kwenda kuonana na padre lakini yeye alitoka haraka ili amuwahi Lucia pale nje. Alipofika nje alimwona Lucia akiwa anatoka nje ya kanisa na alianza kumsogelea ili amsalimie lakini alipomkaribia Lucia alimkwepa na hakupokea mkono wake aliokuwa ameunyoosha tayari kumsalimia Lucia. Eric aligeuka na kumuona Lucia akiingia ndani ya Land Rover Discovery series 4 likiendeshwa na baba yake kisha likaondoka. “Eric padre anakutafuta” ilikuwa ni sauti ya Stanley rafiki wa Eric na mseminari mwenzake ikimwita kumtaarifu kuwa padre Masunga ana mwita Sakrestia (Chumba wanachotumia padre kujiandaa kabla na baada ya ibada). Eric alishtuka na kuanza kukimbia kuelekea sakrestia.

the Legend☆
 
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA PILI

Askofu Aharibu Mipango Ya Erick

“Eric mbona leo upo waruwaru sana” Padre Masunga alimuuliza Eric baada ya kuingia Sakrestia. Eric alijiuma uma meno pale kisha padre Masunga akaendelea na alichowaitia. Aliwaambia vijana wote kuwa siku ya tarehe 26‘boxing day’ ilikuwa wana ratiba ya kwenda kutembelea sehemu za wahitaji. Aliwaambia kuwa yeye mwenyewe akiongozana na Alex na Kido wataelekea hospitali ya wagonjwa wa saratani Ocean Road na hivyo yeye Eric ataungana na timu ya jimbo wakiongozwa na Mhashamu Baba Askofu Kengele kuwatembelea kituo cha watoto yatima Kurasini. Baada ya kukubaliana hayo walitawanyika.

***************************

Siku ya tarehe 25 sikukuu ya Noel ilikuwa ya shamra sana kwa upande wa Lucia. Lucia akiwa na familia yake walisherehekea sana. Familia ya Lucia ilikuwa ni ya uwezo kimapato. Baba yake akiwa mchumi mwandamizi wa benki ya dunia tawi la Tanzania mama yake alikuwa wakili wa mahakama kuu hivyo hata Lucia kuamua kusoma masomo ya sheria ni kutokana na hamasa aliyoipata kwa mamaye. Mbali ya uwezo huo kifedha lakini familia ya Lucia ilikuwa ni moja ya familia iliyojaa ibada na hofu ya Mungu.Kina Lucia akiwa na mdogo wake wa kiume Jonathan walilelewa kimaadili sana na maadili yaliwaingia haswa.

Suala la Eric kumpa kile kikaratasi Lucia tena kanisani na baadae kugundua ni mwanafunzi wa upadre kilimchanganya Lucia akili. Japo hakuwahi kukutana na mwanaume kimwili lakini haikupindisha ukweli kuwa aliwafahamu na kufahamu mbinu zao. Alijua fika suala analotaka kuambiwa na Eric na hivyo alianza kulikataa akilini lakini kadiri alivyokuwa akilikataa ndivyo lilivyozidi kumsonga mawazo.Picha ya muonekano wa Eric haikumtoka akilini kuna wakati alijikuta akitazama eneo moja kwa muda mrefu mpaka ashtuliwe. Mama yake alimuuliza nini kinamsibu kwanini anaonekana hayupo sawa lakini Lucia hakuwa tayari kumwambia. Hata Lucia hakuelewa ni kwanini Eric amemganda kwenye akili tofauti na mamia kwa maelfu ya wavulana aliowahi kuwaona.

*********************************

Tarahe 26 iliwadia na kama ratiba ilivyopangwa PadreMasunga na vijana wawili walielekea hospitali ya Ocean Road na Eric aliwahi makazi ya Askofu Kurasini ili kuungana na vijana wenzake wa seminari waliopangwa kumsindikiza mhashamu kutembelea kituo cha watoto yatima pale Kurasini.

Eric na wenzake wakiambatana na baba Askofu Kengele waliwasili kituoni na kuanza kuongea na watoto mbalimbali wakiwagawia zawadi za sikukuu ya Noel. Mbali na wao walikuwepo na wageni wengine mbalimbali waliokuwa wametenga siku hiyo kutembelea wahitaji.

Wakiwa wanazunguka huku na huku wakiongea na watoto Eric hakuamini alichoona mbele yake. Alimwona msichana mrembo akiwa kwenye vazi la kigauni cha sinderera na viatu vyenye mchuchumio mrefu ila wa wastani. Msichana yule alikuwa amechuchumaa akiongea na mtoto mdogo mweye umri kama wa miaka miwili hivi halafu akamnyanyua akambeba. Eric alipotazama vizuri aligundua alikuwa ni Lucia. Lucia na mama yake waliamua kuitumia siku hiyo kutembelea kituo kile cha watoto yatima na kuwagawia zawadi.

Eric aliwaacha vijana wenzake aliokuwa amesimama nao na kupiga hatua kumfuata Lucia. Alifika na kumgusa bega, Lucia aligeuka na kuonekana kushtuka. “Mambo” Eric alitoa salamu kwa sauti ya chini sana huku tabasamu likiwa limejaa mdomoni. “Hi” Lucia alijibu. Lucia alionekana kutetemeka, kwa wakati ule hakuelewa afanye nini, je amkimbie Eric au ajidai hamfaham au afanye nini. Alizungusha kichwa kuangalia kama mama yake anamwona ila akakuta yupo na watoto anawagawia pipi.

“Mbona juzi usiku uliondoka nami niliomba kukuona?” Eric alimuuliza Lucia. “Baba alikuwa akinisubiri nje nisingeweza kusimama” Lucia alionekana kujibu bila kujielewa. Alishakuwa nje ya control . Eric akiwa msomi wa saikolojia kama moja ya masomo wanayofundishwa seminarini alijua namna ya kucheza na akili ya Lucia, kwa wakati ule alitumia mbinu ambayo vijana wa mjini wangeiita attacking from the end yaani unaongea na mtu kana kwamba mlishakubaliana jambo fulani. Lucia alikuwa akiingia mkenge bila kujua. Eric hakuwa mtaalamu wa kutongoza hivyo hata yeye alijivika ujasiri siku ile. Alisahau kama yeye ni mseminari tena mwenye kujitayarisha kuweka nadhiri ya umaskini, useja(kutooa) na utii.Alisahau kama pale alikuwa ameongozana na baba Askofu. Lucia alimvuruga akili.

“Naitwa Eric, sijui wewe unaitwa nani” Eric aliuliza, “Lucia” Lucia alijibu huku akitabasamu kwa kujilazimisha .“Lucia naweza kupata namba yako?” Eric aliongea kwa utaratibu lakini huku akimkazia Lucia macho. Lucia alichukua simu ya Eric na kuandika kisha Eric akaondoka.

Hakika Eric alipoondoka Lucia alipumua kwa nguvu na aligundua viganja vyake vililoa jasho. Ilikuwa ni dhahiri picha,sura,sauti na mwonekano wa Eric vilimwingia Lucia akilini. Eric aliondoka moja kwa moja mpaka chooni akafika na kujifungia kisha alihema kwa nguvu. Alikuwa ni kama mtu alietoka kufanya mazoezi fulani ya viungo. Hakuamini kama ameipata namba ya Lucia.Alijaribu kuipiga pale pale na iliita. “Helow” sauti tamu na nyororo ya Lucia ilipokea .“Eric hapa” Eric alijibu, “Am,,,am,,,sawa” Lucia aliishiwa maneno. “Tunaweza kuchat leo usiku?” Eric alimwambia Lucia. “Yes” Lucia alijibu kwa upole na Eric akamshukuru na kukata simu.Akatoka.

********************************

Baada ya shughuli kwisha wote walitawanyika na wale waseminari walirudi pamoja na baba Askofu mpaka kwenye makazi ya Askofu kwa ajili ya kupata chakula cha mchana. Baada ya chakula cha mchana walichokula nae pamoja waliaga ili kila mmoja arudi parokiani kwake lakini Eric alishangaa baba Askofu kumwita na kumwambia “Elige unum”(Maneno ya kilatini yenye kumtaka mtu achague moja). Eric alishtuka na kabla ya kujibu chochote. Baba Askofu alimwambia kuwa siku ile asingeondoka na kuwa atabaki nae pale kurasini.

Kwa taratibu za kawaida Padre ni mtu asie na makao, makao yake ni popote kwa maelekezo ya Askofu wake. Hivyo ilikuwa jambo la kawaida sana Eric kubaki pale na kumtaarifu tu paroko wake na labda alipofikia kuwa asingerudi na kuwa Askofu amemuhitaji abaki kwenye makazi yake. Askofu alimwambia atoe taarifa na kisha baada ya hapo alimwambia azime simu na kuicha kwenye moja ya kikapu pale sebuleni maana tayari ilishafika saa kumi na mbili kengele zilishaanza kulia na walitakiwa wasali sala ya Angelus kisha waingie kwenye masifu ya jioni.

Hakuna kipindi kigumu Eric alipitia kama kile maana alijua ana ahadi ya kuchati na Lucia.Hakuna sala hata moja ilipanda siku ile. Mawazo,akili na moyo vyote vilikuwa vinamuwaza Lucia. Wakiwa wamefunga macho Askofu alimwomba Eric aongoze sala lakini kadiri alivyomwita alimwona Eric ameinamisha kichwa chini bila jibu. Aliita tena Eric akabaki kimya.

******************************

the Legend☆
 
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA TATU

Eric Aingia Kwenye Kumi Na Nane Za Askofu Kengele

Jioni ya siku ile Lucia alikuwa akisubiri kwa hamu kupigiwa simu na Eric au hata kuona akimtumia ujumbe mfupi. Kama ilivyo hulka ya mtoto wa kike tena mwenye haiba na malezi bora, alijionea aibu kuanza kumtafuta yeye. Alidhani kwa kufanya hivyo ni kujishushia utu wake kama mwanamke kutokana na tamaduni alizolelewa za ki Afrika. Lucia alisubiri sana na hatimaye subira ikageuka hasira.

Aliwaza sana ni kwanini Eric alimdanganya, au alikuwa akimpima? Alianza kujisikia vibaya kuwa sasa Eric anaesomea upadre labda alikuwa akifanya majaribio fulani yanayohusiana na masomo yao.

Alimchukia na kujiapiza kamwe kutopokea simu wala kujibu ujumbe wake. Tena alijisemea moyoni kuwa hata akimuona atakuwa akimkwepa. Kwa ufupi alikasirika na hakutaka kusikia jambo lolote kuhusu Eric.

Masikini Lucia hakujua hasira ile ni kwa sababu moyo ulishampenda kijana Eric na hivyo ulikasirika ni kwanini umemdanganya. Hakika, penzi la Eric lilianza kuzama kwa Lucia bila hata kutamkwa.

Lucia alionekana mnyonge jioni ile na mama yake alipomuuliza kulikoni mbona tangu kutoka kituo cha watoto yatima anaonekana mnyonge namna ile? Alikosa jibu na kusingizia uchovu tu wa kawaida. Alikuwa akishika simu kutaka kuanza yeye kumtafuta Eric lakini moyo unamkatalia, alizidi kuugua ndani kwa ndani.

****************************

Baada ya Askofu Kengele kuona Eric hajibu alimwomba Sista Kadadaa aongoze masifu ya jioni na baada ya muda Eric alionekana kama kushtuka na kuungana nao kusali.

Baada ya masifu kuisha Askofu aliomba kuongea na Eric kabla ya kuelekea kupata chakula cha jioni. Maongezi ya Askofu Kengele yalijikita katika kusisitiza nadhiri ambazo Eric anakwenda kuziapa siku za usoni. Alimwambia juu ya nadhiri ya useja na usafi lakini nadhiri ya utii na umaskini. Lakini alikadhia haswa ya nadhiri ya useja.

Haya ni mafunzo wanayofundishwa seminarini lakini Askofu aliyarudia kana kwamba Eric hayafahamu. Alichokuwa anakifanya Askofu tungeweza kukiitaMultiple targets attacking kama tungekuwa vitani, yaani unapiga tageti nyingi kwa wakati mmoja na kumwacha adui hoi asijue achomokee wapi.

Ni dhahiri Askofu Kengele alikuwa akifuatilia nyendo za Eric pale kituoni Kurasini na kwa uzoefu wake wa saikolojia alijua kinachoendelea akilini mwake. Aliamua kumsaidia. Usoni, Eric alionekana kuelewa lakini akilini hakuna kilichoeleweka. Lucia aliiteka serikali ya akili yake.

“Eric unadhani Upadre ni wito wako na kuwa utauweza?” hili ni swali kutoka kwa Askofu lililorudisha sawa akili ya Eric. Ni swali lililoshtusha sana hasa ukizingatia linatoka kwa Askofu. Kwa utaratibu wa kanisa Askofu ana uwezo wa kusema neno moja tu kuwa “Hastahili” na upadre wa Eric akausikia kwenye bomba maisha yake yote.

Eric alishtuka sana. Hakutaka kuamini wala kutaka kusikia neno ‘hastahili’likitamkwa na kinywa cha Askofu. Aliwaza inakuwaje Lucia anataka kuharibu jambo alilolipenda toka utotoni mwake, alilolihangaikia na kulisomea maisha yake yote na sasa yupo hatua za mwisho.

“Baba, ndiyo, upadre ni wito wangu na nitauweza kwa uwezo wa Mungu”, Eric alijibu kwa unyenyekevu mkubwa huku akimwangalia Askofu kwa amcho ya huruma.

“Elige unum”, Askofu Kengele alirudia tena maneno yale ya kilatini yenye kumtaka mtu achague moja. Baada ya hayo alimwalika Eric chakula na kisha kuagana kila mmoja kuingia chumbani kwake.

*************************

Kipalapala ni moja ya Seminari kubwa kabisa ya Kanisa Katoliki. Seminari hii ipo Jimbo Kuu Katoliki Tabora na jina lake halisi ni Seminari Kubwa ya Mtakatifu Paulo. Ilianzishwa mnano mwaka 1923 na shirika la mapadri lijulikanalo kamaWhite Fathers. Ni kati ya seminari kuu tatu za kimajimbo, au kwa kingereza ikijulikana kama ’Inter-diocesan regional seminaries’. Nchini Tanzania ipo Kipalapala, nyingine ipo Peramiho na ile ya Mtakatifu Karoli Lwanga, Segerea.

Kipalapala ni moja ya seminari iliyotoa mapadri wa kikatoliki wasomi na wajuvi katika nyanja ya Imani, Falsafa na Elimu ya Ufahamu. Mfano, itamchukua mtu miaka minne kusoma masomo ya Theolojia ili kufuzu na kupewa daraja la upadri, achilia mbali masomo mengine ya kitaaluma na utambuzi kama vile Saikolojia, Sosholojia na Falsafa.

Mtu kufikia hatua ya kuingia katika seminari hii ni maana kuwa tayari umeshakata shauri na kuwa yu tayari kimwili na kiakili kulitumikia kanisa.

Ni katika seminari hii Eric ndiyo alikuwa akisoma na sasa akiwa amebakiza miaka miwili kuhitimu. Eric, mmoja wa wanafunzi mahiri kwa wakati ule alikuwa katika kipimo kikubwa cha kuamua kulitumikia kanisa ama kuitikia wito mwingine wa ndoa.

****************************

Eric usiku ule hakulala. Ilikuwa shida kwake kidogo kupata usingizi. Alijawa mawazo sana kuwa Lucia atamwelewa tena kweli? Hamu ya kuongea na Lucia ilimzidi. Simu alikuwa amezima na kuiacha kwenye kikapu pale sebuleni kwa maelekezo ya Askofu.

Alijigaragaza pale kitandani lakini wapi. Aliamua atoke akaichukue simu kwa siri, aiwashe angalau amtumie ujumbe mfupi tu maneno Lucia kisha aizime airudishe. Hakutaka kugombana wala kujulikana na Askofu. Maneno ya Askofu kuwa achague moja aliyoambiwa mara mbili yalimwingia kichwani. Alijua yatakapomtoka Askofu kwa mara ya tatu basi kitakachofuata ni hatari kwa mustakabali wa wito wake.

Aliwakumbuka watu kadhaa ambao kwa mwaka wa 30 sasa wameishia kuitwa ma Brothers pasi kuwa ma padre kamili kwa sababu tu walikosea mahali fulani fulani na hivyo kubakia kwenye jamii ya watumishi wa kanisa bila kuoa lakini pia bila kupewa u padre.Hakutaka hali hiyo imkute.

***************************

Kengele alikuwa ni askofu mkimya, ila mwenye roho ya ukali wa sirisiri. Ni askofu ambaye aliweza kuwafungia kutoa huduma mapadri wengi kama adhabu ya utovu wa nidhamu. Aghalabu wapo mapadri wawili ambao alihakikisha wanafutiwa kabisa haki ya kuhudumu kanisa katoliki na Papa Benedict XVI kwa sababu tu ya utovu wa nidhamu na kutoelewana ane. Hakuna padri ambae hamwogopi Askofu Kengele. Hata wanaoishi naye hapo kwenye makazi yake wanamuogopa kweli kweli.

Japo ana mapungufu yake hayo lakini ni Askofu anayependa sana maendeleo, kwani ni chini ya awamu yake tangu akabidhiwe jimbo amewezesha kufanikisha ujenzi wa vyuo vya ufundi na vya Elimu ya juu, hospitali iliyofanywa na serikali kuwa ya rufaa, shule nyingi kuanzia za awali mpaka za kidato cha tano na sita.

Ni yeye aliwezesha kufungua kituo cha redio, runinga na gazeti la kanisa. Tena ni yeye amewezesha kupanua uenezi Injili jimboni kwa kufungua vigango vingi zaidi kuwahi kutokea. Hakika ni ngumu kuliongelea kanisa katoliki na maendeleo makubwa bila kumtaja Askofu Kengele.

Mbali na hayo yote pia Askofu Kengele ni mpenda ibada sana. Kama hana ziara popote basi kila siku jioni utamkuta kanisa kuu la Jimbo akiabudu Ekaristi takatifu. Ni askofu aliyependa kufunga na kusali novena. Lakini la zaidi ni namna ambayo kila siku saa sita usiku lazima aamke na kusali novena ya Bikira Maria.

*******************************

Baada ya kuona usingizi hauji Eric alikata shauri kuwa atatoka aende kuichukua simu na kuwasiliana na Lucia japo kwa sekunde kadhaa kisha airudishe simu yake kwenye kikapu. Taratibu Eric alitoka kwenye chumba alichokuwa amelala upande wa kushoto mwa makazi yale ya Askofu kisha akaambatana na korido kwa kunyata akielekea sebuleni.

Alipita mlango unaokatiza kuelekea kwenye ngazi zinazoelekea ghorofani ambapo hulala masista kisha akapita kwenye korido ndogo inayoelekea kwenye chumba cha askofu halafu akakatiza kulia ili kuelekea sebuleni.

Eric alifika sebuleni na haraka huku akitetemeka alikijongea kikapu alichokuwa ameweka simu yake. Katika hali ya mshangao hakuikuta ile simu na akiwa ameshangaa ni nani ameichukua ama kuihamisha alisikia kutoka nyuma yake “Ninayo hapa”. Eric alipogeuka alikuta ni Askofu Kengele akiwa amesimama akimtazama.

**********************************

Upadri ni wito huyu erick huyu kazi ipo
 
Eric upadri hana
 
Upadri ni wito huyu erick huyu kazi ipo
Hahahaa, kweli Shunie, ndo maana wengi wanaendaga seminari ndogo kusoma o level au advance, ila ikifika suala la kwenda seminari kuu wanakimbia. Upadri wito

the Legend☆
 
Hahaha, ni ngumu Shunie To be honest nlipitia seminari pia(o level + advance), ila baada ya kumaliza advance sikwenda seminari kuu, nkaenda zangu chuo. Ila nakumbuka wakati naanza form one huko seminari nlikua na wito balaa

the Legend☆
Hahhaha huo wito ungeendelea nao tu ujue
 
Back
Top Bottom