Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Simulizi: Mtoto wa Baba Paroko

Hahhaha huo wito ungeendelea nao tu ujue
Ha ha ha, nlijipima nkaona hapana, ngoja niingie duniani. Uzuri ni kwamba huwa hawalazimishi, ilikua tukikaribia kumaliza four na six tunaitwa kwa Baba wa Kiroho (spiritual director) tena mmoja mmoja afu unaulizwa unataka kuendelea na seminari au vipi. Ila hata ambao hatukuendelea bado kuna misingi flani ilijengeka ndani yetu ambayo ni ngumu kupotea, na huwa inatusaidia sana maishani

the Legend☆
 
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA NNE
Cc. Shunie instanbul lovelovelove kuku mweus

Eric Akabidhiwa Barua Na Askofu. Aleta Majonzi Makubwa Kwa Mkuu Wake Wa Seminari

“Baba nisamehe. Nisamehe na sitarudia tena’’, Eric alikuwa akilia kama mtoto mdogo. Alilia huku amepiga magoti akimwomba askofu Kengele amsamehe. Kwa muda wote huo, Askofu Kengele alimkodolea Eric macho bila kusema chochote.

Askofu Kengele alikuwa na hasira kwa wakati ule. Alimtafakari Eric ni kwa namna gani hana adabu wala utii. Aliwaza kama kwa wakati ule tu hakuweza kutii jambo dogo kama lile la kutoshika simu wala kuwasiliana na Lucia tena agizo kutoka kwake yeye askofu, Je, akipata upadri si ndo kiburi kitamjaa kabisa? Alikasirika sana.

“Quid tibi ego dicam?” (Nilikwambia nini?), Askofu Kengele aliuliza kwa utaratibu. Lugha ya kilatini ni lugha muhimu kwenye kanisa. Ni lugha ambayo seminari hutumika sana kwa mawasiliano na angalau hakuna padri anayehitimu masomo ya utumishi bila kuifahamu japo kwa uchache. Mseminari kuijua lugha hii ni sawa na mwanasayansi wa viumbe hai kufahamu majina ya viumbe na makundi yake.

Kwenye misheni za kanisa, mathalani kwenye jumuiya za viongozi wa kanisa kuongeleshwa kilatini ni alama ya umakini na umuhimu wa jambo hilo. Yaani kiongozi akikukanya kwa lugha hii ni ishara kuwa amefikia kiwango cha mwisho cha kukuvumilia na sasa lolote laweza kutokea. Askofu Kengele alimuuliza Eric kwa kilatini.

“Parce mihi Pater”, (Nisamehe baba), Eric aliendelea kulia akiwa amepiga magoti. Alielewa mwisho wa wito wake wa kutaka kuwa mtumishi wa kanisa kama padri unaishia pale, au kwa kiasi kikubwa upo mikononi mwa Askofu Kengele. Alimwelewa vyema askofu Kengele.

Eric alikuwa akimuwaza sana mama yake ambaye alimwambia furaha yake kubwa ni kumuona akiwa padri. Mama yake Eric alikuwa akiugua kansa ya damu na alimwambia mwanae kama anataka aishi maisha yenye baraka, amani na mafanikio makubwa basi amtumikie Mungu madhabahuni kwa kuwa padri. Mama yake Eric alikuwa akisubiri kumuona akiwa padri, alimwambia kuwa ni hilo tu analisubiri ili afe. Hakika Eric alikuwa akifikiria hilo machozi yanazidi kumtiririka sana.

“Proverbiorum XXIX Quod non: I dicit?” (Mithali 29:1 inasemaje?), Askofu Kengele alimuuliza Eric kwa sauti ya upole akitaka arejee kitabu cha Mithali sura ya 29 mstari wa 1.

“Viro qui corripientem dura cervice contemnit, repentinus ei superveniet interitus, et eum sanitas non sequetur” (Aonywaye mara nyingi akashupaza shingo, atavunjika na wala hatapata dawa), Eric alijibu huku akibubujikwa na machozi kuonesha kujutia kitendo alichofanya

Baada ya Eric kumaliza tu kumjibu, askofu Kengele aliingiza mkono kwenye joho alilokuwa amevaa la rangi ya zambarau ambalo kikanisa huitwa ‘cassock’na kuibuka na bahasha nyeupe iliyoandikwa upande mmoja maneno ya kilatiniquod dominus noster jesus muneris in yenye maana, ‘Katika kumtumikia Bwana Yesu’ na upande wa pili kulikuwa na maneno yaliyosomeka de secreto, yaani Siri.

Eric alipoona bahasha ile alizidi kulia. Kawaida inatakiwa aipokee mkononi mwake na akitoka hapo anahitajika asafiri moja kwa moja kuelekea Tabora kuiepeleka kwa mkuu wake wa seminari. Padre Mapunda ndio ambae ni mkuu wa seminari ya Kipalapala. Mkuu wa seminari hujulikana kama rector

Askofu Kengele alimwamrisha Eric aipokee ile barua ambayo alikwisha iandaa tangu hajaingia kulala. Alishajua na kumwona Eric ni mkaidi hivyo alishaandaa hukumu yake kabisa. Mkono mmoja akiwa ameishika ile bahasha ambayo Eric asingetakiwa kuifungua hata kwa namna gani mpaka imfikie mkuu wake wa seminari, mkono mwingine alishika kibunda cha pesa za nauli.

Eric alitakiwa kupanda gari pindi kukipambazuka tayari kwa safari ya moja kwa moja kwenda Tabora bila kupita popote wala kuaga popote. Askofu Kengele alipanga kupiga simu seminarini kesho yake asubuhi.

Eric kwa unyonge sana alipokea ile bahasha na zile hela na askofu aliondoka na kuingia chumbani kwake. Eric nae aliingia kwenye chumba chake na kulia sana. Hakuamini kama ndoto zake zimeishia hapo na sababu kubwa ni Lucia.

****************************************

Siku ya tarehe 27 ilikuwa ni siku ndefu na ngumu sana kwa Lucia. Lucia alikuwa akijitahidi kujisahaulisha kuhusu Eric lakini alishindwa. Yani kadiri anavyojitahidi kutomfikiria na kadiri Eric asivyomtafuta Lucia ndio Lucia anavyozidi kumpenda na kumfikiria.

Lucia siku hiyo hakutaka kutoka chumbani kwake, picha ya Eric ilikuwa ikijivinjari akilini mwake. Waswahili husema mapenzi upofu, japo hawakuwahi kutamkiana lolote lakini thubutu, moyo wa Lucia ulizama kwa Eric. Alishindwa kujizuia alianza kumpigia tena Eric.

Simu ya Eric iliita. Eric alikuwa kwenye basi akielekea Tabora. Wakati simu ikiita aliitazama huku akitetemeka. Eric alikuwa na hamu zote za kuipokea angalau amwambie tu Lucia kilichotokea au amjulie hali lakini pembeni alikuwa na barua ambayo amepewa aipeleke kwa mkuu wake wa seminari na chanzo cha yote ni Lucia.

Simu ya Lucia ilivyokuwa ikiita mawazo mengi yalipita kichwani mwa Eric, aliwaza hivi ni nguvu gani haswa Lucia anayo inayomtesa namna hiyo kwa wakati ule. Mbona alishaona wasichana wa kila aina na hawakuweza kumsumbua iweje Lucia anafanya maisha yake yanabadilika kiasi kile? Hakuelewa.

Simu ya Lucia ilizidi kuita na mwishowe Eric alimua kukata simu na kuizima. Alifanya hivyo huku machozi yakimtoka. Lucia alipoona Eric amekata simu alichanganyikiwa.

****************************************

Safari kutoka Dar mpaka Tabora ilimchukua Eric siku mbili. Eric aliona kama imemchukua masaa mawili kwa jinsi alivyokuwa hataki afike seminarini. Alijua kufika seminarini ni kwenda kuhalalishiwa kwa kauli kuwa si mmoja wa waseminari tena kwa tamko la askofu Kengele.

Barua ile ilibeba ujumbe mzito wa mustakabali wa wito wa Eric na alilitambua hilo. Alihuzunika sana.

Eric aliwasili seminarini na tayari padre Mapunda alikuwa na taarifa za ujio wake. Eric aliingia na kumkuta padri Mapunda ametoka kwenye masifu ya jioni kwani aliingia mishale ya saa moja hivi usiku.

“Tumsifu Yesu Kristu Baba”, Eric alisalimia huku akitaka aanze kulia nakuomba msamaha.

“Milele amina Eric. Umefanya nini?Umenisikitisha sana”, Padre Mapunda alimjibu Eric kwa sauti nzito sana na yenye mikwaruzo. Waseminari wamezoea kumwita Padri Mapunda chap chap kwa jinsi anavyoendesha mambo yake, huwa ni mtu yupo resi muda wote na asiependa kutumia muda mwingi kwenye jambo moja.

“Una mzigo wangu kutoka kwa Mhashamu Baba Askofu Kengele siyo? Haya ulete”, Padre Mapunda alimwambia Eric ampe ile bahasha. Aliipokea na kuifungua na kuanza kuisoma.

Kadiri alivyokuwa akiisoma alikuwa akinyanyua macho na kumtazama Eric tena huku akiwa amekunja ndita. Barua ile nzima iliandikwa kilatini kama lugha rasmi ya mawasiliano kwa matukio kama yale.

Ilionekana wazi kilichoandikwa kule kilimsikitisha sana Padri Mapunda kwani ni yeye aliyeonekana macho kubadilika rangi na kuanza kupata wekundu. Padri Mapunda alimpenda sana Eric lakini sasa neno la Askofu halihojiwi.

“Eric tangu mkiwa seminari ndogo mnafundishwa Utii kama moja ya jambo muhimu kabisa kwa wito wetu huu, why have you done this for God’s sake?” Kawaida ya uharaka ilimwisha Padre Mapunda, alimuuliza Eric kwa sauri ya upole mkuu na iliyojaa simanzi sana. Eric tayari alikuwa ameshapiga magoti akiomba msamaha.

“Quid est enim non mutata “, Padre Mapunda aliyatamka maneno hayo ya kilatini kwa sauti kama yalivyoandikwa mwisho kabisa mwa ile barua ya askofu Kengele. Maneno hayo yalimaanisha ‘Kilichoandikwa kimeandikwa’.

************************************************

the Legend☆
 
Mtoto wa Baba Paroko : SEHEMU YA TANO

Cc. Shunie instanbul lovelovelove kuku mweus

Barua Ya Askofu Kengele Yasababisha Simanzi Nzito. Mama Wa Eric Asababisha Sintofahamu

Eric ni kijana alielelewa na mama yake na wajomba. Alilelewa kwa taabu sana hata kuna wakati mama yake alikuwa akipata msaada wa kusomeshewa Eric kutoka shirika la kusaidia watoto wa wasiojiweza linalofadhiliwa na Jaques Laurento tajiri mmoja wa Kifaransa. Msaada huu aliupata baada ya kuwa akifanya kazi za usafi katika ofisi za shirika hilo zilizopo Masaki jijini Dar Es Salaam.

Mama yake Eric alieitwa MariaClara Alphonce alipata uja uzito wa Eric akiwa na miaka 19. Ni ujauzito ule uliosababisha afukuzwe na baba yake huko Sengerema na kukimbilia Dar kwani baba yake alitishia kumuua kwa kusema alimdhalilisha sana.

Baba yake MariaClara yaani mze Alphonce Mabula alikuwa ni katekista wa kanisa katoliki Jimbo la Sengerema Parokia ya Nyagawa. Ni yule mzee asiekosa ibada hata ziwe 12 kwa siku. Mzee Alphonce alitambulika pia kwa ukali uliopitiliza tena asie na masihara.

Aliongoza kwa kuwasema mabinti wa wazazi wenzake kuwa wana tabia mbaya na kuwalaumu wazazi wenzie kwa malezi mabovu ya mabinti zao. MariaClara alipopata ujauzito ilikuwa ni aibu isiyomithilika kwa mzee Mabula. Kwanza mamake MariaClara alikula kipigo cha mbwa koko ktoka kwa mumewe mzee Mabula kwa kuambiwa alikuwa wapi wakati binti yao akifanya ‘uchafu’. Alimpiga sana.

MariaClara yaani mamake na Eric alipoona kichapo kile alikimbia nyumbani na hakurudi tena. Mamake alimtumia salamu kuwa akimbilie Dar kwa mjomba wake aliekuwa akifanya biashara ya kuuza ng’ombe kutoka Sengerema kwenda Dar. MariaClara kwa kusaidiwa na mjomba wake mwingine aliekuwepo kule Sengerema alifanikiwa kwenda Dar na kuanza maisha huko.

Haikuwa rahisi kwani alipofika tu kitu cha kwanza mke wa mjomba wake alichotaka kujua ni ile mimba ni ya nani na nani atamlea huyo mtoto akizaliwa. MariaClara hakutaka kusema mimba amepewa na nani. Katu hakusema. Hata mjomba wake alipomuuliza MariaClara alidanganya kuwa mtoto yule alipewa na utingo wa moja ya malori yaliyokuwa yakienda kusweka ng’obe kule kijijini.

Alipoulizwa jina alidanganya, sasa kwa sababu mjomba wake ni mfanyabiashara hiyo ya ng’ombe alijaribu kuchunguza kwenye malori yanayokwenda kusweka ng’ombe Sengerema lakini hakuweza kumjua huyo utingo. Siri ya baba wa Eric alibaki nayo mamake Eric yaani MariaClara.

Ni katika mazingira yale MariaClara aliilea mimba ya Eric kwa taabu sana. Alianza kufanya kazi ndogo ndogo za kumuingizia kipato mpaka akajifungua na baada ya kupumzika aliendelea na kazi mbalimbali. Kazi kama za mama ntilie, usafi wa majumbani, kuuza genge ni shughuli zilizomlea Eric.

Katika makuzi ya Eric kila wakati mamake alimkumbusha kuwa hataki chochote kutoka kwa mwanae ila amuone akihudumu madhabahuni kama padre.

Katika ukuaji wa Eric MariaClara alimwambia mwanae huyo kuwa babake alifariki na kuwa Eric hana baba. MariaClara alijitahidi sana na kwa uwezo wote kumlea Eric katika mazingira na tamaduni za dini na maadili na hakika hilo alifanikiwa sana. Eric alikuwa ni aina ya kijana asietiliwa shaka hata kidogo.

Japo MariaClara alikimbia kwao kumwogopa baba yake lakini ilifikia hatua baba yake yaani mzee Alphonce alielewa kuwa wakati mwingine watoto hukengeuka na hivyo alimsamehe binti yake na kumtaka arudi nyumbani lakini MariaClara alikataa.

Kipigo alichoshuhudia mama yake akipigwa na babake kilimuumiza akili sana. Alimchukia sana baba yake kiasi kwamba hata mzee Alphonce alipokuja kuugua sana hakwenda kumtazama. Mama yake alimsihi sana aende lakini Maria alikataa. Maria alikuwa anaweza kwenda Sengerema na kushukia kwa wajomba zake na mama yake kwenda kuonana nae hapo lakini kwa miaka 10 tangu akimbie nyumbani katu hakuwahi kurudi.

Wakati wa kifo cha mzee Alphonce Mabula kila ndugu alimsihi Maria aende kumzika baba yake lakini Maria alishikilia msimamo wake kuwa yule si baba yake kwa kitendo alichomfanyia. Mzee Alphonce alizikwa.

Ni baada ya kukaa na kujitafakari sana ndipo Maria alipogundua alifanya makosa. Hasa baada ya malezi ya Eric kuchanganya na kuona uchungu anaoupata pale Eric anapofanya jambo kinyume na alichomfundisha. Aligundua baba yake alipatwa hasira kutokana na kitendo chake cha kubeba ujauzito huku yeye akiwa kinara wa kufundisha watoto wa wengine na mzee muheshimiwa pale parokiani.

Roho ilimuuma sana baada ya kugundua kuwa hata Eric hamjui babu yake na wao kuzaliwa wasichana watupu ilikuwa ni fahari sana kwa mzee Mabula kama angemjua Eric kama mzaliwa wa kwanza wa kiume kwake.

Ni katika hali hiyo Maria aliamua kurudi kijijini baada ya miaka 3 toka babake afariki na kufika kwenye kaburi la babake na kuomba msamaha huku akilia sana.

Alimwahidi babake kuwa ni kwa sababu hiyo atahakikisha Eric sio tu anakuwa mpenda dini kama yeye mzee Mabula bali atakuwa padre kama ambavyo yeye baba yao alitaka sana mtoto wa kiume ili awe padre. Maria alilia sana kaburini mwa mzee Mabula siku zile.

MariaClara tangu kuzaliwa kwa Eric alimpa jina la Nyagabona yaani jina la ukoo wa mama yake, ndio kusema Eric alijulikana kama Eric Nyagabona na hata baada ya ndugu kuuliza sana baba wa Eric mwisho walichoka wakakaa kimya na maisha yakaendelea.

****************************

Baada ya padre Mapunda kumaliza kuisoma ile barua ya askofu macho yaligeuka kuwa mekundu. Alisikitika sana, alimwangalia Eric kama dakika tatu hivi bila kuongea jambo.

Eric alikuwa ni miongoni mwa waseminari wenye akili sana. Alijituma, alikuwa na uelewa mkubwa wa mambo na katika vijana padre Mapunda alikuwa akijivunia katika seminari yake ile basi Eric asingekosa kwenye tatu bora.

Padre Mapunda hakuona sababu hasa ya Eric kusimamishwa masomo na askofu Kengele lakini kwa mujibu wa kanisa na taratibu utovu wa Utii ni kosa kubwa sana kwa kanisa. Ni sawa na jeshini mkubwa amwambie mdogo‘Mbeleee tembea’ halafu yule mdogo abaki amesimama anamwangalia tu. Yani askari kama huyu ataondolewa hapo haraka kwa sababu ipo siku mtakuwa kwenye uwanja wa vita umwambie apige adui risasi halafu atakugomea tena ili awe salama atakupiga wewe unaempa amri usije ukaamrisha mwingine ampige na kumuua. Ni watu hatari sana wanaokosa utii kwa mamlaka.

Ni kwa muktadha huo Eric kwa askofu Kengele alikuwa ni mtu hatari kwa kanisa na alistahili adhabu kali tena haraka kabla hajageuka kuwa bomu kubwa zaidi. Askofu Kengele aliwaza wale mapadre wanaofanya mambo kinyuma na maagizo halafu wanajizolea umaarufu na kuungwa mkono matokeo yake hata akisimamishwa anayumbisha parokia ama jimbo kwa wengine kumfuata ama kuhama kanisa kwa kuliona halina haki. Askofu Kengele aliona ni bora wakawa wanadhibiti watu wa namna hii katika hatua hizi za chini na ndio maana kwake ukosefu wa utii ni mbaya kuliko jambo lingie lolote.

Padre Mapunda hakuwa na la kuficha, alimwambia Eric kuwa barua ile imemwelekeza kumsimamisha masomo mpaka hapo askofu Kengele atakapoamua vinginevyo na kwa muda huo ampange Parokia ya Kwedizinga huko Tanga kama sehemu yake ya kuangaliziwa na mafunzo.

Askofu Kengele alisema atawasiliana na askofu Shemsika wa jimbo katoliki Tanga ili afanye maandalizi hayo.

Taarifa ile ilimuumiza sana Eric, alilia sana. Uchungu ule ulitokana na ukweli kwamba ukipelekwa kwenye uangalizi kama vile basi kuna mawili ni aidha unaishia huko na upadre utausikia bombani au yawezekana kweli askofu akakukumbuka na kukurudisha kumalizia masomo. Vyote viwili kwa Eric vilikuwa ni vichungu. Alilia kama mtoto mdogo alienyang’anywa titi la mama wakati ana njaa kali.

************************

Baada ya Eric na padre Mapunda kubembelezana Eric aliomba ampigie simu mama yake kumtaarifu, kwa wakati ule hata wazo kuwa kuna kiumbe kinaitwa Lucia halikuwepo. Lucia kwa wakati ule alipotea kabisa kwenye mawazo ya Eric na sasa alikuwa akipigania wito wake.

Eric alishika simu huku akitetemeka, alijua taarifa ile ina matokeo mawili. Moja ni kumfanya mama yake afariki kwa mshtuko ama kumfanya awe kichaa. Yaani MariaClara na kutaka Eric awe padre kulishamtengenezea addictionyaani ndio kitu pekee kilikuwa kikimpa matumaini ya kuishi kwa wakati ule.

Padre Mapunda alimwambia Eric kama anadhani taarifa ile itasababisha sintofahamu kwa mama yake basi amuachie yeye ndio ataangalia namna ya kuongea nae. Japo padre Mapunda hajawahi kuongea na mamake Eric na wala hamfaham ila taarifa za kuugua kwake anazifahamu kwa sababu ya ruhusa za mara kwa mara Eric alizokuwa akiomba kwenda kumtazama.

Eric aliomba aongee mamake mwenyewe.

“Shikamoo mama”, Eric alisalimia na mara baada ya maongezi mawili matatu Eric alianza kumweleza mama yake kilichotokea. Alimweleza huku akibubujikwa na machozi.

“Nisamehe mama nimekuangusha ila najua bado Mungu ananiita kumtumikia mama”, Eric alikuwa akiongea kwa uchungu uliochanganyika na kwikwi ya kilio huku akimtia moyo mama yake. Ilikuwa ni ngumu kuamini kuwa Eric alikuwa ni kijana wa umri wa miaka 30 kwa jinsi alivyokuwa akilia.Mama yake alikuwa akisikiliza kwa makini huku kukisikika sauti ya kwikwi pia.

“Mama” Eric aliita baada ya kuona hakuna neno mama yake anajibu.

“Mama”, Eric aliita tena.

“Eric mpe simu Padre Mapunda”, MariaClara mamake Eric alimwambia Eric ampe ile simu padre Mapunda mkuu wake wa Seminari.

Eric alishangaa iweje mamake ameomba ombi lile. Katika miaka mitatu ya Eric kukaa seminari kuu ya Kipalapala mamake hakuwahi ongea na padre Mapunda. Kwanza alishangaa hata jina amelijuaje maana hakumbuki hata siku moja kuongelea mkuu wao wa seminari.

“Padre, mama anaomba kuongea na wewe”, Eric alimwambia padre Mapunda huku akimpa simu.

“Tumsifu Yesu Kristu mama”, Padre Mapunda alimsalimia mamake Eric kwa sauti ya upole na masikitiko.

“Milele amina Kapalata”, mamake Eric alimjibu padre Mapunda na kutulia kimya.

Hakika kama kuna kitu padre Mapunda kilimshtua basi ni kusikia mtu anamwita kwa jina la Kapalata. Jina hilo ni jina lake alilokuwa akilitumia utotoni tena alilopewa na babu yake mzaa mama yaani mzee Kapalata aliyekuwa Msukuma. Mara ya mwisho kuitwa jina hilo ni kama miaka 30 iliyopita.Isitoshe, si jina alilowahi kulitumia kabisa na aliitwa kwa nadra sana tena hasa na babu yake huyo ambae alishafariki. Alishtuka sana.

“Naongea na nani?”,padre Mapunda aliuliza kwa mshangao uliomfanya hata Eric ashangae.

“Unaongea na MariaClara mama wa huyo mwanao hapo Eric”, mamake Eric alijibu tena kiufupi na kutulia.

Padre Mapunda alikata simu haraka huku akiwa ametoa macho kama mjusi aliebanwa na mlango wa korido za mahakama huku akimtazama Eric na mapigo ya moyo kiongezeka kwa kasi ya pikipiki ya msafara wa Rais.

****************************

Usiache Kufuatilia Sehemu Ya Sita Ya Simulizi Hii.

Dah
 
Amina. Tuko pamoja Shunie. Sahivi nahamia kwako kusoma simulizi zako, sijazimaliza bado

the Legend☆
Kuna viporo huko mtunzi kaibiwa simu kama ya Gloria hiyo nyingine ndio nimepost leo

Hivi mwanzo ulikua unatumia I'd gani eti samahani lakini
 
Ha ha, bila samahani. To be honest with you sijawahi kua na id nyingine huku jf(but that doesn't mean sikua mfuatiliaji wa jf). Hii ni id yangu ya kwanza na bila shaka itakua ya mwisho pia. Asante kwa kuuliza Shunie

Asante mkuu nimekuelewa nimeona una uenyeji ndio mana nikakuuliza
 
Ha ha. Najua kwanini uliuliza vile mkuu. Actually i have been following jf(via web) for years, that is exactly why umeona nipo familiar nayo

the Legend☆
 
Back
Top Bottom