Simulizi: Mpaka Kieleweke

SEHEMU YA 44



Mara kikaonekana kichwa cha Magugi kikielea hewani kama kiliundwa kwa moshi kikiongea, ?hakuna hata mmoja kati yenu mwenye akili kunizidi, Sauda nilikuona kama ni msaliti wala sikukosea kukuhukumu kifo, wewe mzee Mikausho ukaleta hila zako za kudai Sauda hakuwa na hatia lakini nilikuona kama unaongopa, na niliona chote ulichokifanya, bado haikutosha ukaamua kumuua mtumishi wangu muaminifu na kuniletea muuaji, hivi mlidhani mimi ni mjinga kiasi hicho?? alihoji Magugi ambaye alionekana kuzijua hila zetu mapema tu. ?dawa zako hazina nguvu mbele yangu kijana, na mwisho wako umefika, na kama ulitaka kuuju ufunguo wa mlango wa Muifufu leo umekutana nao, huu ndo ufunguo wangu na leo utaitoa roho yako? alisema Magugi akinionesha yule mwnamke ambaye alikuwa ametuteka. ?Tunu endelea na kazi yako, nataka Sauda na mzee Mikausho watangulie kufa kisha wengine wafuate maana wao ndio viongozi wa usaliti huu? kilisema kichwa kile cha Magugi kisha kikatoweka. Hofu ilitawala sana, kila mtu alikuwa akiongea neno lake kujaribu kumsihi mwanamke yule asiye na macho asituue, mwanamke yule alionekana kuwa na hisia za hali ya juu kwani aliweza kujua kila kitu kilipo bila kuona, pengine angekuwa anategemea macho asingetuona kama wale waliotupita baada ya kujipaka yale mafuta. Tunu akanyanyua mkono wake juu sana na mwili wa Sauda ukafuata mkono ule kwa kuinuka juu sana kisha akafanya kama kamrusha na mwili wake ukapigizwa kwenye miti kwa kasi kubwa na Sauda akatua chini kama mzoga,na kutuli tulii! alionekana kama viungo vingi vya mwili wake vilikuwa vimevunjika, ikafuata zamu ya mzee Mikausho ambaye naye kilimkuta kama kilicho mkuta Sauda, hofu ikatanda, hakuna aliyejua nani atafuata!. Ilikuwa ni zamu ya Hisham, akapigizwa kwenye miti huko naye akatua chini na kutulia. Nikapata wazo la ghafla na kutoa lile yai la bundi ambalo lilikuwa limebaki kwenye mkoba na kumuonesha yule mwanamke.?kama ukituruhusu kuondoka nitakupa yai hili?nilisema na mwanamke yule akasita kuendelea na zoezi lake,akawa kama anasikilizia kujua nilikuwa namuonesha nini maana hakuwa na macho, alikuwa anatumia hisia tu. ?tufungulie mlango tuondoke kisha nakupa? nilimwambia mwanamke yule ambaye alionekana kuvutiwa na nilichokuwa nimekishika. ?niwaachie wangapi?? alianza kujadili biashara mwanamke yule. ?sote tuliobakia, nilisema kwa kujiamini? lakini mwanamke yule akawausha mbali vijana wale watatu, wakajigonga kwenye miti kama ilivyokuwa kwa Sauda, mzee Mikausho na Hisham. Sasa nilikuwa nimebaki na mke wangu na yule binti wa hakimu tu. ?kwa yai hilo moja naweza kuwaachia ninyi watatu tu? alisema mwanamke yule huku akitutua chini polepole kabisa. Nilisikitika sana kuwapoteza wote ambao tulikuwa tumepambana pamoja kwenye harakati za kutoroka Muifufu lakini sikuwa na namna. Ikanibidi kuikubali hofa ile ya sisi watatu, ?nipe hilo yai haraka, hatuna muda? alisema yule mwanamke kwa sauti ya kuamisha, nikaingiwa na mashaka kidigo, itakuwaje kama nitampa anachokitaka kisha akaendela na zoezi la kutuua? Niijiuliza. ?tutajuaje kam kweli tukikupa yai hili utatuachia tuondoke?? nilimuuliza kuonesha wasiwasi wangu. Yule mwanamke kabaki kimya, hakutoa jibu lolote ndani ya sekunde kama 20, kisha akazungumza ?mnanichelewesha? ilikuwa ni kama hakusikia swali langu. Nikafikiri kwa kina na kuona sikuwa na chaguo lingine, nikaamua kumuamini mwanamke yule na kumkabidhi lile yai.





Baada ya kupoke yai lile, Tunu akaifanya mikono yake kama natanua kitu na ikaonekana ukifanyika upenyo ambao ulitosha mtu kupita, ?haya nendeni haraka? alisema Tunu kwa sauti yake ile ya kuamrisha, tukajikongoja kwa mwendo ule ule wa polepole kutokana na ugonjwa wa mke wangu na uchovu wa mimba wa yule binti hakimu, bwana Tago. Tukapenya kwenye ile njia, mke wangu akitangulia na kufuatiwa na binti wa bwana Tago kisha mimi nikafuata kabla Tunu naye hajapenya na kupotela kusikojulikana.



Hewa ya duniani ilikuwa safi sana, na ilikonekana kama ni mida ya alfajiri, ilhali kule tuliacha ikiwa ni usiku. Nilijisikia faraja sana kurudi kwenye aridhi niliyoizoea nikiwa na mke wangu, moyo wangu ulijwa na furaha ya hali ya juu, nikakumbatiana na mke wangu kwa bashasha, fuaha yetu haikuwa na mfano wake, hata binti yule wa bwana Tago naye alishindwa kuzizuia hisia zake, akatusogelea na kutukumbatia kwa pamoja huku akibubujikwa na machozi ya furaha. Nikawataka tutoke eneo lile ambalo nilikuwa sijalitambua bado. Mavazi yetu yalikuwa ya kizamanizamani, hayakufanana kabisa na dunia ya leo, kama mtu angetuona angedhani tumetokea kwenye kiiji ambacho chakina maendeleo hata kidogo.
 
SEHEMU YA 45



Tukatembea hatua chache na kukutana na barabara ya vumbi ambayo niliitambua, nikaamua kuchukua njia ambayo ilitupeleka moja kwa moja kwenye nyumba ya kulala wageni ambapo tulichukua vyumba viwili vilivyokuwa vinatazamana, mimi na mke wangu tukachukua chumba kimoja na kingine kikawa kwaajili ya yule binti wa bwana Tago. ?inabidi ulipie kabisa mzee? alisema kijana ambaye alikuwa msimamizi wa nyumba ile ya kulala wageni. Kweli ni kwamba sikuwa pesa yoyote, na wala sikujua pa kupata pesa ?sisi ni wasafiri, na kwa sasa nimeishiwa kabisa pesa, wacha tuwapatie vyumba hawa wapumzike kisha mimi nikatafute sehemu ya kutoa pesa kwenye simu kisha tutamalizana bwana mkubwa? niliongea kwa kujiamini kabisa na bwana yule akakubali na kutukabidhi funguo za vyumba.



Tulipofika chumbani nikaoga haraka na kumtaka mke wangu aningojee kidogo nitoke kwaajili ya kwenda kuangalia usalama kisha nitawarudi,mke wangu akakubali japo ilikuwa kwa shingo upande, hakutaka nitoke mbele ya mboni za macho yake, alihitaji sana kupata muda wa kutosha wa sisi kuwa pamoja, kama ilivyokuwa kwangu pia.



Safari yangu ilinichukua mpaka eneo la mahakamani, nilikuwa nimekwenda kumtafuta bwana Tago, nilijua kuwa ilikuwa mmapema sana kwa yeye kuwepo kazini lakini nilijua pale naweza kupata hata mawasiliano yake.



?samahani bwana, namuulizia muheshimiwa Tago, sijui naweza kumpataje? nilimsemesha bwana ambaye bila shaka alikuwa ni mlinzi. ?sasa wewe unategemea atakuja kazini jumamosi hii ofisi ya baba yake nini?? alihoji mlinzi yule na kufumbua macho, kumbe ilikuwa ni siku ya jumamos. ?naweza kupata namba yake ya simu?? niliuliza. ?nenda kasome pale kwenye ubao, nadhani namba yake ipo pale? alinijibu mlinzi yule nami nikaenda kwenye ubao wa matangazo, kweli nikakuta namba mabimabli za viongozi wa mahakama, akiwem bwana Tago. Nikanakili namba ile kichwani, kwani sinaga mgogoro na namba.



?samahani bwana, unaweza kuniazima simu yako?? nilimrudia yule mlinzi na kumuomba anisaidie simu yake ili niweze kumtafuta bwana Tago kwani sikuwa na simu. ?nitakuazimaje simu yangu na mimi sikujui bwana?, siku hizi matapeli wamekuwa wengi, hakuna kuaminiana mjini? alisema milinzi yule kwa nyodo. Muonekano wangu ulikuwa wa hovyo sana, hivyo hata mimi sikutegemea kuheshimiwa na mtu yeyote ndani ya sare ile ya watumishi wa Magugi ambayo ilionekana kuwa manguo ya fukara eneo hili. ?mimi sio tapeli ndugu yangu, muheshimiwa hakimu ni ndugu yangu, nimetokea mbali sana kuja kumtafuta yeye, tusaidiane kama wanaume? maneno yangu yakamuingia mlinzi yule ambaye alinikabidhi simu yake ?usiongee sana, sina dakika za kutosha? alisema. ?unaongea na Abubakar Saire, naomba unipigie? nilisema maneno hayo baada ya simu kuwa imepokelewa,kisha nikaikata. ?duuh! Wewe mzungu kwelikweli, sasa atakuwa amekuelewa?? alisema mlinzi yule ambaye alonekana kufurahia dakika zake kutotumika sana, kabla sijamjibu simu ikaita na mimi nikaipokea. Bwana Tago hakuamini kama alichokisikia kilikuwa sahihi ?umesema wewe ni bwana Abubakar Saire?? alihakikisha bwana Tago na jibu likabaki kuwa ndio. ?uko wapi ndugu yangu?? aliuliza kwa shauku baada ya kuthibitisha kweli nilikuwa mimi. ?niko hapa mahakamani, sikuwa na namna nyingine ya kukupata? nilimjibu, akanitaka nimsubiri hapohapo mahakamani. Nikamrudishia mlinzi yule simu yake na kumshukuru kisha tukaendelea kuzungumza hili na lile nikiwa namsubiri bwana Tago ambaye alifika ndani ya dakika 10, nikamueleza kwa kifupi juu ya safari yangu na mafanikio ambayo niliyafikia. Bwana Tago alifuahi sana. Tukaingia kwenye gari lake na safari ya kwenda kwenye ile nyumba ya wageni ikaanza, tukafika na kuingia ndani ambapo nilimpeleka kwana Tago kwenye chumba alichokuwemo binti yake wakaonana na kukumbatiana huku wakilia kwa furaha. Nikawaacha wakiendelea kuongea nami nikarudi kwa mke wangu.



Baada ya kama robo saa bwana Tago akaniita na kutaka tutoke mara moja, tukaenda mpaka benki ambapo alitoa pesa na kunikabidhi kiasi ambacho harakaharaka niliona hakikupungua milioni moja ?bwana sina cha kukulipa kwa wema ulionifanyia, najua utakuwa unaanza upya mambo yako, pokea kiasi hiki kwa kuanzia ila ukikwama popote usiache kuniambia? alisema bwana yule nami sikuwa na budi kupokea pesa zile maana ni kweli kuwa sikujua naanzia wapi.



Bwana Tago akaniudisha mpaka pale kwenye nyumba ya wageni ambapo alimchukua binti yake na kulipia pesa ambayo tulikuwa tunadaiwa wakaondoka.



Nami nikamchukua mke wangu mpaka kwenye duka moja kubwa la nguo, tukanunua mpya na kubadilisha zile za kizamani, tukanunua na nyingine kadhaa za kuanzia maisha, tukapitia na kwenye duka la simu na kununua visimu vidogo tu viwili, kisha tukaenda nyumbani kwetu ambapo tulikua hatujakanyaga bado. Nyumba ilikuwa na vumbi sana, kutokana na kutotumika kwa muda, tukafikia kufanya usafi tukisaidiana maana mke wangu pia hakuwa na maumivu ya tumbo tena, kisha tukapumzika huku tukipata wasaa wa kupanga namna ya kuyaanza upya maisha yetu. Usiku wa siku hiyo pia tukawasiliana na wazazi wangu na pia wa mke wangu na kuwaelezea kilichotokea, wote walifuahi na kututaka kwenda nyumbani. Tukawajibu kuwa tutakwenda ila tuliitaji kidogo muda wa kuwa pamoja.
 
SEHEMU YA 46

Tulichelewa sana kulala siku hiyo kwani kila mmoja alikuwa na hamu na mwenzie na tuliona kama kulala haukuwa na umuhimu mkubwa kama kuwa pamoja. Lakini kama ilivyo ada usingizi ukifika kulala kunafuata ukiwa unataka ama hutaki. Mke wangu alikuwa ameshapitiwa na usingizi lakini mimi nilikuwa bado sijalala vizuri, nikashangaa kuona upepo mkali mule chumbani, kwa mwanga wa taa ambayo haikuwa imezimwa niliona vitu visivyokuwa na uzito wa kutosha vikiamishwa kwenye nafasi viliyokuwa vimewekwa kutokana na upepo ule, mara kwenye kona moja ya chumba kile alionekana mtu akiwa amechuchumaa. Haikunichukua muda kugundua kuwa mtu yule aikuwa ni Mnaro, ingawa alionekana kuwa na hasira sana, moja kwa moja nikajua hasira zile zilitokana na kipenzi chake Sauda kufia Muifufu, sikufanikiwa kumleta kama ambavyo tulikubaiana. ?Nilikwambia kama atatoka mtu mmoja awe ni Sauda wangu,lakini mmekuja watatu ila Sauda mmemuacha akiwa marehemu? aliongea kwa ukali Mnaro huku akibubujikwa na machozi. ?mimi nimefanya kila kitu ndugu yangu lakini haikuwa bahati, hata mimi inaniuma kuona tumemuacha Sauda nyuma na msaada aliotupatia, nilitamani sana tuwe tunafurahia pamoja wakati huu? nijithidi kujieleza lakini Mnaro hakuonekana kunielewa.



?nilikupa zana zote za kuwawezesha kutka salama, lakini nyingine hukutumia, kama ungeitumi ile fimbo kumchapa Tunu, Sauda angekufa saa ngapi??alihoji Mnaro ambaye ilionekana kama alishuhudia kila kitu kilivyoenda. Nikweli sikuwa nimetumia fimbo aliyonipa Mnaro, lakini mazingira hayakuruhusu mimi kumchapa Tunu na fimbo ile huku nikiwa naelea hewani, ningewezaje? Niliwaza lakini sikuona umuhimu wa kumshirikisha Mnao mawazo yale kwani alionekana kama alikuwa amekuja amejiandaa kutoelewa.



?Magugi hawezi kumuua Sauda wangu na yeye akabaki akiishi kwa furaha, ni lazima na yeye afe. Jianda kwa safari nyingine ya Muifufu? alisema Mnaro baada ya kuniona niko kimya. ?safari ya Muifufu???? kwakweli siwezi kurudi huko tena? nilisema. ?utarudi tu huna ujanja, ukinitaka unajua namna ya kunipata? alisema Mnaro na kutoweka akikiacha chumba kile kikiwa kwenye mvurugiko wa hali ya juu.





Muda wote huu mke wangu alikuwa amelala, hakushtuka hata kidogo pamoja na Mnaro kuongea kwa sauti kubwa sana, hata zile vurugu zake za maupepo hazikusumbua usingizi wake, nadhani ulikuwa ni uchawi wa Mnaro kutaka mimi tu ndo nisikie maongezi yake ndio maana alingoja mpaka mke wangu alale ndio aje.



Asubuhi tuliamka mida ya saa tatu, mke wangu alitangulia kuamka kisha kaniamsha haraka baada ya kushangazwa na hali ya chumba kwani wakati analala chumba kilikuwa katika mpangilio wake, hakukuwa na namna ikanibidi kumthimulia yaliyojili baada ya kupotea kwake, nikamuelezea msaada ambao alinipa Mnaro mpaka kufanikisha zoezi lile pamoja na mkataba wetu wa kuhakikisha namejeshea Sauda katika maisha yake, kisha nikamuelezea ujio wa Mnaro usiku na malalamiko aliyokujanayo. ?mmh! Kurudi tena Muifufu ni kwenda kufa, usithubutu? alisema mke wangu baada ya maelezo yangu marefu. ?nilimueleza waziwazi Mnaro kuwa siko tayari kurudi Muifufu lakini cha ajabu alisema ni lazima nitarudi na akanitaka kumtafuta nikimuhitaji, yani ni kama ana uhakika kuwa mimi nitataka kurudi huko? nilieza. ?huyu atatusumbua sana, unaonaje tukiama hii nyumba?? mke wangu alitoa ushauri wake ambao ulionesha waziwazi kuwa maelezo yangu hayakutosheleza kumuonesha Mnaro alikuwa na nguvu kiasi gani. ?hatuwezi kumkimbia mke wangu, akitutaka atatufuata popote tutakapokuwepo? nilijaribu kumuelewesha mke wangu ambaye ainielewa. ?ila cha msingi ni kuwa tuko pamoja na sitoruhusu tena tutengane? nilijaribu kumfariji.
 
kXcpEDcj7uugjqDqn8AHrQ-320-80.jpg
 
SEHEMU YA 47

Tukaendelea na maisha yetu kama kawaida lakini watu walikuwa wanatushangaa sana tulipokuwa tukipita mitaani tukiwa tumeongozana kama ambavyo tulikuwa tumezoea kufanya, nadhani hii ilitokana na watu hawa kujua kuwa mke wangu alikuwa amepotea, walikuwa wakishangaa kaudije wakati watu wengi sana kwenye eneo lile walikwishaga potea na hawakuwahi kurudi. Wakati mwingine watu walitusimamisha na kujaribu kuhoji maswali mbalimbali lakini hatukuwa tukipenda kuliongelea swala lili.



Siku kama ya nne toka tulipotoroka Muifufu alitujia nyumbani mzee wa kama miaka 70 akiwa na mkewe na wakatuelezea juu ya kupotea kwa binti yao miaka saba iliyopita, mazingira ya kupotea kwake yalifanana sana na yale ya kupotea kwa mke wangu, wazee wale wakataka kujua namna gani nilimpata mke wangu ili na wao waweze kuitumia njia hiyo kumpata binti yao. ?mzee maneno yanayosemwa ni mengi lakini mengi sio ya kweli, mke wangu kweli alipotea lakini yeye alitekwa na mjambazi na walinipigia simu wakitaka pesa ili wamuachie hivyo nikatafuta pesa na kuwapa nao wakamuachia? nilidanganya ili kuwatoa njiani wazee wale. ?kweli majambazi wanaweza kumteka mtu kisha wakamvua nguo na kuziacha?? alihoji mzee yule, swali ambalo kwakweli lilikuwa gumu. ?ndio maana nikakwambia kuwa maneno yanayosemwa ni mengi ila mengi sio ya ukweli, sio kweli kama nguo za mke wangu zilibaki? nilijitetea na wazee wale wakakubali na kuondoka japo hawakuonesha kuniamini.



Maisha yetu yalianza kuwa magumu ghafla sana, sisi tulikuwa tunapeda maisha ya utulivu lakini sasa maisha yetu yalikuwa yanaangaliwa na kila mtu, wengine wakitutaka msaada ambao waliamini tunaweza kuwapa ila tulikuwa wachoyo wa kusaidia.



Mwisho tukafikia uamuzi wa kusafiri kidogo kwenda kuwaona wazazi wangu, mpaka tukirudi vuguvugu lile litakuwa limetulia.



Maisha nyumbani kwa wazazi wangu yalikuwa rahisi, hakukuwa na tabu kama ambazo tulizikimbia kule kwangu kwani huku hawakuwa wakijua juu ya janga ambalo liltukuta.



Maisha yakaendelea mpaka siku ambapo tulipanga safari mimi na mke wangu kwenda kumuona rafiki yangu Max ambaye nilikuwa sijaonana naye muda mrefu. Nakumbuka nilisikia kama muwasho fulani mgongoni nikawa najikuna huku najiandaa kwaajili ya safari yetu. Mara baada ya kuvaa fulana nyepesi ya ndani, kabla sijavaa shati mke wangu akashtushwa na alichokiona mgongoni mwangu ?heee! Mbona kama una damu mgongoni?? aliuliza mke wangu huku akinisogelea na kuifunua fulana ile, akakutana na kidonda ambacho hakikujulikana kimetoka wapi, mke wangu akapatwa na wasiwasi mkubwa na akanisaidia na mimi kukiona kidonda kile kwa msaada wa kioo. Haraka sana nikakumbuka kuu ya kiapo changu kule mlima Kalingisi, niliahidiwa kupata jeraha mgongoni na jeraha hilo lisingepona mpaka nitakapotekeleza ahadi ya kumuua Magugi, pia nilipaswa kufanya haraka kwani niliambiwa kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo jeraha hilo linazidi kuwa kubwa na lingefikia hata kunitoa uhai. Japo jeraha lile halikuwa na maumivu, nilipatwa na wasiwasi mkubwa, maisha yangu yaikuwa yapo mashakani.



Nilimwelezea mke wangu asili ya jeraha lile kwa kifupi, tukakubaliana kutafuta wataalamu wa tiba za asili (waganga) ili waweze kutusaidia. Wengi wa waganga hao walikuwa waongo, ?hili jeraha limetokana na jini ambalo umetupiwa na jiani yako ambaye hapendi mafanikio yako?alisema mganga mmoja ambaye moja kwa moja tulimuona ni muongo na kupuuza maelekezo yake.
 
SEHEMU YA 48

Mganga mwingine akatuambia ?kuna afiki yako ambaye mliwahi kugombana zamani sana lakini mkaja kupatana, mwenzio alibaki na kinyongo , akakuendea kwa mganga ukalogwa? huyu naye alikuwa muogo mwingine, tulihangaika sana kwa waganga wakati jeraha langu lilizidi kukua, sasa likaanza kuuma na kutoa harufu mbaya, lakini hatukukata tamaa ya kuhangaika, kila tulipoambiwa kuna mtaalamu mzuri sisi tulikwenda, tulikwenda mpaka kwenye maombi lakini hakukuwa na mafanikio



?inaonekana wewe uliwekeana kiapo na mtu kisha ukakivunja, na hii ni laana ya kiapo hicho? alisema mganga mmoja ambaye tulipelekwa na rafiki yangu kujaibu kama anaweza kutusaidia,mganga huyu nilimdharau mara tu baada ya kumuona kutokana na umri wake mdogo, mara nyingi waganga huwa wazee lakini huyu alikuwa kijana mdogo tu. ?enhee, tunawezaje kulitibu hilo tatizo?? niliuliza kwa shauku baadaya kuona huyu mganga wa leo alikuwa wa kweli. ?tiba pekee iliyopo ni kufanya ambacho uliapa kukifanya kisha ukamuombe msamaha huyo mliyeapizana kwa kujaribu kukiuka kiapo, kama akikusamehe basi utapoana. Nilijawa na simanzi baada ya maelezo hayo, kwani yalikuwa yakimanisha nirudi Muifufu, nikamuga mganga yule na kurrudi nyumbani kwa msaada wa rafiki yangu na baba ambaye tulikuwa tumeendanae kwa mganga yule.



?Jamani nimewahita hapa kwaajili ya kuongelea afya yangu? nilianza kuongea kwenye kikao ambacho niliwaita ndugu zangu na mke wangu. ?ugonwa huu umetusumbua sana na naona unaleta umasikini nyumbani maana kila kinachopatikana kinatumika kutibia ugonjwa huu usiopona, sasa imetosha. Sote tunajua dawa ya ugonjwa huu nikurudi Muifufu, kwanini tunajidanganya na ukweli tunao? Sasa nimeamua kuwa nitarudi Muifufu kujaribu kupata tiba ya ugonjwa huu, kama nitakufa basi itakuwa mepangwa hivyo? nilimaliza maneno yale ambayo niliyatoa kwa uchungu sana, baadhi ya ndugu zangu hawakuweza kujizuia kutoa machozi baada ya maelezo yale, wengi walona ni kama walikwisha nipoteza. Afya yangu ilikuwa imedhohofu sana, nilikuwa nimekonda mno na ngozi yangu ilifanya mabakamabaka, pia nilikuwa na kikohozi kisichosikia dawa, ukichangia na lile donda la mgongoni ambalo lilikaribia kutapakaa mwili mzima, hata mimi nilijiona ni kama mfu aliye hai.



Ndugu zangu wakabishana sana baada ya maelezo yangu, wengine wakiona lilikuwa wazo zuri kwenda kutafuta tiba huku wengine wakiona kwenda huko ni kujiua kabla ya siku zangu za kufa kufika. ?bora aendelee kuwa hapa hata kama akifa tutamzika kiheshima kuliko kujipeleka kufia mbali ambapo hatutoona hata mwili wake? alishauri baba yangu mdogo ambaye alikuwpo kwenye kikao kile.



?mimi nafikiri ni bora kufa ukipmbana kuliko kukaa kukingojea kifo? alishauri mdogo wangu na mke wangu akamuunga mkono, ?anachokisema shemeji ni sawa ila anahitaji mtu wa kwendanae maana hali yake ya afya sio nzuri, mimi nitakwendanae? alisema mke wangu na kuzua mzozo, wengine wakisema aende huku wengine wakikataa ?lazima aende, kwani mwenzie si alipata matatizo haya kwaajili ya kwenda kmsaidia yeye? Kwanini na yeye asimsaidie sasa?? alisema dada yangu ambaye hakuwahi kuwa na mapenzi ya dhati kwa wifi yake huyu. Mabishano ya hapa na pale yakaendelea lakini mimi nikajihisi mwili wangu ukiishiwa nguvu, hata mabishano yale nikawa nayasikia kwa mbali kama vile nilikuwa ndotoni, mara nikaanguka chini kama mzoga na sikujua nini kiliendelea tena.







Fahamu zangu zilipokuja kurudi nikajikuta nikiwa nimelala kitandani ndani ya kajumba cha udogo, chumba kilikuwa kidogo na chenye makolokolo mengi sana.
 
SEHEMU YA 49

Ilionekana hakuwa usiku ila kulikuwa na kagiza kutokana na mwanga kuingia kwa taabu ndani ya kachumba kale. Afya yangu haikuwa mbaya sana kama ilivyokuwa wakati nilipopoteza fahamu, kwani sikuwa na maumivu makali ambayo nilikwa nikiyahisi kabla, pia kile kikohozi kilichokuwa nami muda wote kilikuwa kimeniachia, nikajaribu kupapasa mgongoni kuona kama lile jeraha lilikuwepo nikakuta lipo, lakini lilikuwa dogo sana tofauti na lilivyokuwa limefikia.



Nilitumia dakika kadhaa kufikiria nini kilikuwa kimetokea na kunusuru maisha yangu, nikajiuliza pale palikuwa wapi, mwisho nikaamua kujiaminisha kuwa itakuwa ndugu zangu walifanikiwa kupata mganga wa kweli, na pale palikuwa kwa mganga. Nikaamka na kutoka ndani ya kachumba kale, na mwisho nje ya nyumaba ile ndogo, macho yangu yakapokelewa na pori kubwa, kajumba kale kalikuwa kamezungukwa na pori pande zote, hakukuwa na nyumba nyingine wala mtu ambaye nilimuona, lakini kwa mbali nilisikia sauti ya kama mti unakatwa na watu wakiongea, nikaamua kufuata sauti hizo. Nikiwa kwa mbali kabla sijafikia sauti zile zilipokuwa zinatokea niliweza kuona kulikuwa na watu wawili, mwanamke na mwanaume na walionekana kuwa wanafanya kazi fulani, nilipozidi kusogea zaidi nikagundua kuwa yule mwanamke alikuwa mke wangu na yule mwanaume alikuwa Mnaro, Mnaro alikuwa akifua magome ya mti mmoja mkubwa kwa kutumia panga huku mke wangu akiokota magome yaliyokuwa yanaanguka chini na kuweka kwenye ungo ambao ulikuwa pembeni ya mti ule. Sasa nikawa nimewafikia nao wakaniona, mke wangu akaacha alichokuwa anakifanya na kunijia kwa mwendo wa haraka na kunikumbatia kwa furaha, alionekana kufurahia sana kuona nikiwa nimezinduka, sikujua nilikuwa katika hali ile ya kupoteza fahamu kwa muda gani. Mnaro yeye alinipuuza na kuendelea na kazi yake kama vile hakuniona, nadhani bado alikuwa na hasira kutokana na mimi kutofanikiwa kuokoa maisha ya mpenzi wake Sauda na kumtoosha Muifufu. Tuliachiana kwanza na mke wangu nikamsogelea Mnaro na kumsalimia, akaitikia lakini kama mtu ambaye ana kinyongo na mimi, niliona aikuwa na haki ya kukasirika maana hata kama ni mimi ingeniuma mke wangu kufia Muifufu, hivyo nikaamua kumvumilia nikijua alihitaji muda kuamua kunisamehe. Basi nami nikaanza kushiriki ile kazi japo sikujua walikuwa wakifua magome yale kwaajili ya nini, wakati naanza mke wangu alijaribu kunizuia akidai hali yangu ya afya bado haikuwa nzuri lakini Mnaro akamtaka aniache nifanye kazi ile kwani hali yangu iliuhusu na nilikuwa nikpaswa kufanya mazoezi ili kuendelea kuimarisha afya yangu.



Tuliporudi nyumbani pale kwa Mnaro mke wangu akawasha moto wa kuni, akayaweka magome yale ndani ya sufuria yenye maji kisha akayabandika. Tulikaa tukiongea japo waongeaji sana walikuwa mimi na mke wangu, Mnaro alikuwa kimya akisikiliza zaidi na wakati mwingine kujifanya kama anatabasamu, ila hakuwa muongeaji.



Mke wangu akanielezea kuwa baada ya kupoteza fahamu pale kwenye kikao walijaribu kunipeleka hospital na kwawaganga bila mafanikio, maombi pia ya dini zote hayakuzaa matunda. Mwisho wakaamua kuniacha nyumbani tu kungojea mauti yangu, ?kwakweli tulikata tamaa, tulijua tumeshakupoteza tayari? alisema mke wangu na kufikia hapa akashindwa kuzuia kilio, nami nikafanya kazi ya kumbembeleza, ambayo ilifanikiwa kisha akaendelea kunithimulia kuwa nikiwa nina wiki ya pili toka niwe katika hali ile ya kutokuwa na fahamu,
 
SEHEMU YA 50

Mnaro akawaendea na kuwaambia kuwa alikuwa na uwezo ya kunisaidia lakini alitaka kuondoka na mimi na ataenda kunitibia ambako angejua yeye lakini ningerudi nikiwa mzima, ndugu zangu wakamkatali naye akaondoka, lakini usiku wa siku hiyo akaja katika chumba ambacho nilikuwemo, na mke wangu alikuwemo akilala na mimi, akamshawishi mke wangu kumruhusu anichukue akanitibu, ?kwakweli hata mimi nilikuwa naogopa sana kumkabidhi kuondoka na wewe, maana baada ya kujitambulisha nilijua yeye ni nani maana ulikuwa umenielezea uwezo wake mara kadhaa, sikujua kama alikuwa na nia ya kukusaidia au kukulipizia kisasi maana najua ana hasira na wewe? alelezea mke wangu, lakini baadae ikambidi kujaribu kwakuwa hakukuwa na namna nyingine ya mimi kupona, pia alikuwa anaujua uwezo wake, na alijua fika kuwa kama angeamua kufanya maamuzi ya kunichukua hakuna ambaye angeweza kumzuia, ?hivyo niliweza kufanya ni kumsihi tu na mimi nije, nashukuru akanikubalia? . Kutoka kwenye maelezo haya ya mke wangu, nikajikuta nimegundua kuwa nilikuwa katika hali ile ya kupoteza fahamu kwa muda mrefu maana ujio wa Mnaro tu ulitokea wiki ya pili baada ya kuwa katika hali ile, ?inamaana nimekuwa katika kutojifahamu kwa muda gani?? niliuliza na mke wangu akaniambia nilikaa katika hali ile kwa mwezi mmoja na siku nne. Nilishangaa sana, kumbe nilikuwa katika hali ya nusu ufu kwa muda wote huo, mimi nilona ilikuwa ni kama jana tu.



Baadae baada ya giza kuwa limeingia Mnaro akamuomba mke wangu amuachie nafasi tuongee kidogo, jambo ambalo alitii. ?sina chuki yoyote niliyonayo juu yako, hasira zangu zote zipo kwa Magigi, yeye ndiye aliyenitenganisha muda wote huo na Sauda, na niyeye aliyeuhukua uhai wake? alianzisha mzungumzo Mnaro, nikashukuru sana kusikia kuwa hakuwa katika ugomvi na mimi maana balaa lake nalijua, sikutaka awe adui yangu hata kidogo. ?ndani ya muda mfupi tutapaswa kufanya safari ya kwenda Muifufu, inabidi tujiandae? aliongezea Mnaro na kuishtua nafsi yangu, mimi nilidhani kwakuwa afya yangu imerudi kuwa nzima basi sikuwa na haja tena ya kukifuata kifo Muifufu. ?lakini mimi sina tena haja ya kwenda Muifufu, maana nimepona tayari? nilimjibu Mnaro ambaye aliniangalia kwa macho makali sana. ?unadhani umepoana wewe? Wewe dawa yako ni kulipa ahadi uliyowekeana na jamii ya watu wa milima Kalingisi, ugojwa uliokupata unasehemu tatu,sehemu ya kwanza ndio hii ambayo tumefanikiwa kuitibu, sehemu ya pili mwili wako wate huo utavuka ngozi, ndo maana tunaandaa dawa ile, sehemu ya tatu ni kifo, hakuna ambaye anaweza kuzui isipokuwa kifo cha Magugi, sote tunataka jambo moja, lazima tushirikiane ili kulifanikisha? alisema Mnaro, maneno yake yakanitisha sana. ?sasa kama niko tayari kwenda Muifufu na kumuua Magugi, kuna haja gani ya kuniandalia dawa,maana hiyo sehemu ya tatu ya ugonjwa huo haitonikuta. ?hili eneo langu nimelizindika sana, halionekani kwa macho ya kawaida wala ya mchawi, hata ubaya wa Muifufu na mlima Kalingisi hauwezi kuingia kwenye himaya hii, ndio maana nimeweza kukutibia huku na umepona, kwenye dunia ya kawaida wewe ungekuwa mfu sasahivi? aliweka kituo kidogo kisha akaendelea. ?kama ungeweza kubaki kwenye eneo hili tu, ugonjwa wako ungepona kabisa lakini maandalizi ya safari hii yatatutaka kwenda safari ya mbali ambapo hutokuwa na kinga yoyote, ndo maana tunaandaa dawa ile ambayo itakuwa ikipunguza makali ya ugonjwa, nasi tutapaswa kumaliza haraka kilichotupeleka huko kabla nguvu ya dawa haijazidiwa na ugon jwa? alielezea vizuri Mnaro,
 
SEHEMU YA 51

nilichanganyikiwa kuona jambo hili lilikuwa bado bichi namna ile, mimi nilidhani hatimaye sasa nilikuwa naelekea kupata amani baada ya afya yangu kurudi. ?hiyo safari ni yakwenda wapi na kufanya nini?? niliuliza. ?ni safari ya kwenda kwenye ufalme wa uchawi kutafuta nguvu ambayo itamuondosha Magugi na utawala wake kufumba na kufumbua tu? alielezea Mnaro. ?Na huko kwenye ufalme wa uchawi ni wapi?? niliuliza kwa shauku baada ya kuona kuna matumaini kwenye safari hiyo. ?ni ujinini, chini ya bahari? alijibu Mnaro.







?unamanisha nini?? nilimuuliza kijana yule ambaye kwenye macho yangu nilimuona kama mtu wa kawaida tu,sikuona kama alifanana na majini, maana nilikuwa nimewahi kuonana na majini na sura zao tu zilitosha kuonesha kuwa walikuwa majini. ?usijali mimi nimemuelewa na nitakuelewesha? alijibu Mnaro haraka haraka, alionekana kukwepa mimi kupewa jibu na kijana yule, sikujua kwanini. ?sasa unatusaidiaje?? aliuliza Mnaro. ?mtapelekwa kwa huyo ndugu yangu,yeye ndo anaweza kuamua kuwasaidia ama kutowasaidia, mimi sina msaada wowote kwenu? alijibu kijana yule kisha akamuita mtumishi wake na kumtaka atupeleke kwa huyo ndugu yake. ?inamaana yule kijana naye ni jini?? nilimuuliza Mnaro wakati tuko njiani kuelekea kwa huyo ambaye tuliambiwa ndiye aliyekuwa na uwezo wa kutupa msaada. ?itakuwa? alijibu Mnaro, jibu lake lilionesha kuwa hata yeye hakuwa na uhakika. ?mbona anaonekana mtu wa kawaida tu?? niliuliza. ?marehemu mzee Mnsuri alikuwa ni jini, alioa wanakwake wanne ambao watatu kati yao walikuwa majini akini mmoja wao ambaye ndiye aliyekuwa wa mwisho alikuwa ni mwanadamu, na huyo ndiye alimzaa Musa,ndio maana unamuona ana sura ya mwandamu, ilitokana na mama yeke? alituelezea mtu yule ambaye alikuwa anatuelekeza, nilishangaa kuona mtu yule ametusikia maana aikuwa ametutangulia hatua chache na tulikuwa tunaogea kwa sauti ya chini sana kuepuka asitusikie. ?kwahiyo na wewe wazazi wako ni mchanganyiko wa jini na mwanadamu?? nilimuuliza mtu yule ambaye naye alikuwa na sura ya kawaida tu. ?hapana, mimi ni jini, ila bosi wetu anatutaka kuja na sura ambayo haitowaogopesha wageni endapo wageni hao ni wandamu, hivyo hii sio sura yangu ila nimeichukua kwaajili yenu? alijibu jini yule, kisha akaendelea ?ukikutana na jini lazima utauona utofauti kwenye sura yake,labda awe na mchanganyiko na mwanadamu au awe ameamua kujivika sura ya binadamu, japo mwili wako wenyewe pia unaweza kuhisi kuwa mtu uliyekutana naye ni jini hata kama sura yake ni ya kibinadamu?alielezea vizuri jini yule, akawa amenijuza jambo jipya, sikuwa nikijua kabla kama jini na mwanadamu wanaweza kuzaa mtoto. ?kwahiyo huku kuna wanadamu wengi tu walioolewa na majini?? nilihoji ili kupata kulielewa vizuri swala hili. ?wapo wachache sana ambao wanaishi huku, wengi wako hukohuko duniani, na wengi wao wala hawajui kama wana ndoa na majini, kwani mahusiano yao hufanyika mwanadamu huyo anapokuwa usingizini,lakini atakapozaa mtoto lazima atchukuliwa na kuletwa ujinini kwani sio kazi nyepesi kwa mwanadamu kulea mtoto wa jini? alielezea jini yule. ?sasa hao wazazi wa kibinadamu huwa wanakubali watoto wao wahamishiwe ujinini?? niliendelea kupeleleza, muda wote Mnaro alikuwa kimya kama vile hakuwa akisikia yale maongezi. ?mwanadamu huwa hajui kinachoendelea, kama jini ni mwanamke mwanadamu huwa hana hata habari juu ya mimba hiyo ila kama jini ni mwanaume mwanamke huwa anajua fika kama ana mimba ila mimba hizi husemekana zieharibikia mwishoni, kumbe huwa mtoto amechukuliwa na kuja kulelewa ujinini? alisema jini yule. Tukawa tumeingia kwenye eneo ambalo lilikuwa tofauti sana na eneo lile tulilotoka, eneo lile lilikuwa chafu sana na majumba yalikuwa ya kizamani mno na hayakupangika vizuri, hata hali ya hewa ya huko haikuwa nzuri, pumzi iikuwa nzito sana kutokana na harufu ya uvundo. ?mwenyeji wenu anapaikana kwenye jumba lile pale, mimi narudia hapa? alisema jini yule ambaye hakusubiri jibu letu, akageuka na kuanza safari ya kurudi.
 
SEHEMU YA 52



Tukatembea polepole mpaka kwenye jumba lile kubwa lakini chakavu, tukapanda ngazi ambazo zilikuwa nyingi na kuufikia mlango ambao ulikuwa juu sana, wakati tunajiandaa kugonga mlango ule ukafunguka wenyewe na Mnaro akaingia bila kuwaza mara mbili, nami nikalazimika kumfuata kwani eneo lile lilitisha sana na sikutamani kubaki popote pekeyangu. Ndani ya jumba lile tulikutana na holi kubwa sana, kulikuwa na giza kubwa na kimya cha kutisha. Mara ule mlango nyuma yetu ukajibamiza kwanguvu sana, tulipoguka tukakuta umejifunga, giza likazidi kuwa la hali ya juu maana ule mwanga mdogo uliokuwa unaingia kupitia mlango ule nao ukakatika. Giza lilikuwa kali kiasi kwamba sikuweza hata kumuona Mnaro ambaye alikuwa pembeni yangu tu. Nilikuwa na maswali mengi ya kuuliza lakini sikutaka sauti yangu isikike maana nilona kama tulikuwa katika hali ya hatari.



Mara ikasikika sauti kama ya mluzi, ikaenda ikipanda mpaka ikawa kali sana ya kuumuza masikio, mpaka ikanibidi kuziba masikio yangu kwa viganja vya mikono yangu. Kisha mule ndani kukapatikana mwanga, nikaanaza macho yangu kuona mwanga ule ulikuwa unatoka wapi, nkagundua kuwa kulikuwa na vitu kama mishumaa kwenye pembe za kuta za holi lile na mwanga ule ulitokea hapo, kitu cha ajabu ni kuwa Mnaro alikuwa ameanguka chini, alionekana kama mtu ambaye kafa au kazimia kwani hakuwa akitingishika hata kidogo, uoga ukanitawala,nikachuchumaa na kuanza kumtingisha ili aamke, lakini sikuwa natoa sauti yoyote, niliona ingekuwa ni kumjuza adui juu ya eneo ambalo tulikuwepo. ?achana naye, hawezi kukusikia? alisema sauti nzito, nikatizama ilipotokea na kuona kuwa kulikuwa na mtu ambaye sura yake haikuonekana vizuri kuokana na uhafifu wa mwanga ndani ya chumba kile. ?samahani mkuu, hatukuja kwa nia mbaya, tunomba utusikilize shida yetu? niliongea kwa kunyeyekea maana sikujua nini kilikuwa kimeandaliwa kwaajili yangu, baada ya kuona kilichompata Mnaro. Mtu yule akasogea karibu zaidi na kunifanya niione vizuri sura yake, alikuwa na sura ya kutisha sana, baada ya kuiona sura hiyo mara moja tu sikutaka kuiona tena, nikaangalia pembeni lakini nikutana nayo huko pia, nikaangalia chini lakini bado niliiiona, nikafumba macho lakini huko nako nikaikuta. ?huna haja ya kunielezea chochote, kwani mimi najua kila kitu, nisikilize mimi nikuelezee wewe ambacho hukijui? alisema kiumbe yule wa kutisha, ?najua mnahitaji msaada ili muende kwenye safari ya mapambano, nitawapa msaada na mtashinda, ila amacho hujui ni kuwa huyu mwenzio ana hasira sana na wewe juu ya kosa ambalo uliwahi kumfanyia na mpaka sasa uko hai kwakuwa anakutegemea kutimiza malengo yake. Baada ya kufanikiwa atakutoa uhai wako kulipiza kisasi chake? aliweka kituo bwana yule, akanitizama kisha akauliza ?unataka hili lisitokee??, nami nikjibu haraka haraka ?ndio, naomba unisaidie tafadhali?. Mara mkononi mwa bwana yule kikatokea kisu na akanikabidhi, kisha akasema ?wakati wako ni huu na hakuna mwingine, kama unataka hilo lisitokee mchome bwana huyo kwa kisu hicho, atakuwa marehemu na wewe nitakusaidia kushinda vita iliyoko mbele yako? nikabaki nikiwa nimeshika kisu kile huku nikitetemeka, nilikuwa na uamuzi mgumu sana wa kufanya. Je, ni kweli Mnaro alikuwa bado ana hasira na mimi? Je kumuua lilikuwa jambo sahihi kulifanya? Au ndo maana yule kijana aliyeagiza tuletwe kwa huyu ndugu yake alisema mmoja wetu ana muishilio mbaya?, nilijiuliza maswali mengi lakini sikuwa na jibu la hata moja kati ya maswali hayo.



?wewe bwana unataka msaada wangu au huutaki?? alihoji bwana yule, swali lake likanishtua kutoka kwenye lindi la mawazo. ?ninataka sana msaada wako mkuu? nilijibu harakaharaka baada ya kuona kulikuwa na hatihati a kupoteza msaada ule. ?basi fanya haraka nilichokuagiza? alisema bwana yule kwa sauti ya kuamuru.
 
SEHEMU YA 53









?samahani mkuu, huyu bwana ni kweli nilimkosea,anayo haki ya kuwa na hasira na mimi, na kama kuniua ndicho kitu pekee kitakchoweza kupoza hasira zake basi niko tayari aniue, kwani hata mimi sina amani juu ya kilichotekea kwa mpenzi wake na najutia sana kutofanikiwa kumuokoa? nilijielezea baada ya kufikiria vizuri na kugundua kuwa kile ndicho ambacho nafsi yangu litaka. Baada ya kumaliza kusema maneno yale nilishangaa kile kisu kikiniponyoka na kumuangukia Mnaro ambaye alikuwa amelala pale chini, nikaogopa sana kwa kudhani kuwa kilitaka kumuua lakini kilimgonga kwenye paji la uso kwa mpini wake na kumshtua Mnaro ambaye aliamka kama mtu ambaye alikuwa anatokea kwenye usingizi mzito. ?vizuri, nyote mmefanikiwa kufaulu jaribio la umoja umlionao, umoja wenu ndio utakaowapa ushindi, lazima kila mmoja awe tayari kuyatoa maisha yake kwaajili ya mwenzie? alisema bwana yule mwenye sura ya kutisha ambaye nilianza kuizioea sura yake. Maneno yake yakanifanya kujua kuwa kumbe lile lilikuwa jaribio na Mnaro pia alipata lake japo sikujua lake lilikuwaje wala sikujua alilipata mda gani, ila nilijua tu naye alifaulu kama ambavyo ilikuwa kwangu. ?nitawasaidia, na mtashinda ila msaada huo una gharama kubwa sana? alisema bwana yule. ?tuko tayari kulipia gharama yoyote ili hili jambo lifanikiwe? alisema Mnaro huku akiniangalia mimi kama ambaye alinitaka kutopinga maneno yake. ?mna uhakika na hilo?? aliuliza bwana yule na Mnaro akajibu haraka haraka, ?ndio? . ?mbona anaitikia mmoja? Na wewe uko tayari?? aliniuliza bwana yule. ?ndio, niko tayari kwa lolote? nilijibu kwa upole. ?sawa, gharama hii ni uhai wa mmoja wenu? alielezea bwana yule. ?sijaelewa, yani uhai wa mmoja kivipi?? nilihoji uoga ukianza kuniingia tena. ?kwenye hiyo vita yenu mtafanikiwa ila mmoja wenu atapoteza maisha, hiyo ndo gharama ya msaada wangu, kama mnaukubali au mnaukataa mnijibu sasa maana ukianza haurudi nyuma? alisema bwana yule, tukatazamana na kukubaliana kwa vichwa, kisha tukamwambia bwana yule kuwa tulikuwa tuko tayari kwa hilo,pia tukamtaka atuambie ni maisha ya nani kati yetu yangepotea. ?hilo litabaki kuwa fumbo, siku ikifika mtajua? alisema bwana yule nasi tukakubaliana naye.



Bwana yule alitutoa kitaka holi lile lenye mwanga hafifu na kutupeleka nje, tukatembea tukimfuata nyuma mpaka maeneo ya porini, huko akatuambia alikuwa tayari kutenda kazi ambayo ilikuwa imetupeleka kule, na kazi yenyewe ilikuwa kutupatia nguvu ambazo zingeweza kuuangusha utawala wa Magugi. Kabla bwana yule hajafanya chochote, nilijihisi kuwashwa mwili mzima, nikaanza kujikuna lakini haikusaidia, nikona kucha zangu hazikutosha nikachukua mchanga na kuanza kusugulia maeneo mbayo yalikuwa yakiniwasha, nikasugu kwanguvu mpaka damu ikawa inatoka. Mnaro akakimbilia kibegi chake na kuoa chupa ya dawa ambayo tuliiandaa kabla ya safari ya ujinini na kunipa, nikaipokea na kuinywa haraka, muwsho ule ukakoma hapohapo.



?uwezekano wa kuzuia ugonjwa wako upo, ila sio busara kuvunja kiapo ambacho ulikiweka wewe mwenyewe ukiwa na akili timamu? alisema yule bwana ambaye bila shaka alikuwa ni jini. Ngozi yangu ilikuwa imerudi kwenye hali yake, japo ilikuwa imeacha vijeraha vidogovidogo kwenye maeneo ambayo nilisugua sana.



?nitawapa nguvu za aina mbili, mkizitumia kwa ushirikiano nguvu hizo hamuwezi kuzidiwa na mchawi yeyote wa kibinadamu? alisema bwana yule. ?wewe nitakupa upanga wa radi, upanga huo unauwezo wa kukata chochote unachotaka kutokea umbali wowote? alinimbia mimi na kisha akamgeukia Mnaro, ?wewe nitajaza nguvu mikono yako, itaweza kufungua mlango wowote, itaweza kunyanyua chochote bila hata kukigusa na itaweza kuzuia mashambulizi yote ya kichawi? alimaliza kuelezea, tukamuelewa, maelezo haya juu ya nguvu alizotaka kumpa Mnaro yalinifanya kuona kuwa nguvu hizo zilifanana na zile za Tunu, yule mwanamke ambaye nilimuhonga lile yai la mbuni akatufungulia mlango wa Muifufu wakati tunatoroka. Akatutaka kupiga magoti tukielekea upande mmoja, yeye akaja nyuma yetu na kutushika vichwani huku akisema maneno ambayo sikuyajua maana yake, ila yalisikika kama maneno ya kiarabu, miili yetu ikaanza kutetemeka kama tulikuwa tumenaswa na shoti ya umeme, ndani ya seunde chache nikajikuta nimepoteza fahamu.
 
SEHEMU YA 54

Nilipokuja kuzinduka nilijikuta katika maeneo ambayo yalikuwa tofauti na maeneo ambayo tulikuwa wakati napoteza fahamu, pembeni yangu kulikuwa na panga kubwa sana, nikalishika na kuanza kulishangaa. Panga hili lilifnana sana na mapanga ambayo huonekana kwenye sinema za wachina yakitumika kama silaha. Kwa mbali nilimuona Mnaro, nikasogea karibu na kuona kuwa alikuwa aking'oa miti mikubwa sana kwa kutumia mikono yake japo alikuwa mbali na miti hiyo, mkono yake tu ilitosha kuielekeza miti kung'oka nayo ikatii. Baada ya kuwa ameung'oa mbuyu mkubwa Mnaro aliunyanyua juu sana kwa mikonyo yake, nami nikaamua kulijaribu panga lile, nikafanya kama naukata mti ule kutokea pale pale nilipokuwa, nikashangaa kuona mti ule ukikatika palepale ambapo nililenga, hii ilikuwa ni silaha kwelikweli. Mnaro aliona nilichokuwa nimekifanya, akaniijia akiwa na tabasamu, nilishangaa kwani muda mrefu ulikuwa umepita bila kuona tabasamu la Mnaro. ?Magugi ameisha? alisema baada ya kunifikia. Mapaka muda huo nilikuwa nimeshagundua kuwa lile lilikuwa pori la kule kwa Mnaro.



Tulikubaliana kuipitisha sehemu ya siku hiyo iliyobaki lakini kesho yake asubuhi na mapema tudamkie kwenye safari ya Muifufu kwaajili ya kwenda kumsambaratisha Magugi. ?kwenye jaribio lako wewe uliona nini?? aliniuiza Mnaro wakati tunapiga story tukiwa tumepumzika. Nikamuelezea kila ambacho nilikiona, kisha nikmtaka na yeye kunielezea ambacho alikiona, ?niliiona siku ambayo Sauda alipoteza maisha, nikakuona wewe ukiwa makini sana kuokoa maisha ya mkeo lakini ukimuacha Sauda apotee japo ulikuwa na nafasi ya kumsaidi. Nilipatwa na hasira sana, na nikapewa kisu kukuua ili kuipiza kisasi ila nikakuhurumia kwa kuwa bado una kila sababu ya kuishi, pia ulijitahidi kufanya ila Magugu alikuzidi ujanja? alisema Magugi. ?mmoja wetu atakufa kesho? nilimkumbusha Mnaro juu ya hili maana hakuonesha kuliwaza hata kidogo. ?Mimi namjua ambaye atakufa kesho kati yetu? alisema Mnaro. ?nani?? nikauliza lakini ni wazi kuna jibu sikutaka kulisikia hata kama ndio ukweli. ?wewe? alinijibu Mnaro, jibu ambalo sikutaka kabisa kulisikia.







"umejuaje kama ni mimi"? niliuliza kwa wasiwasi. "kwakuwa siku zote waoga ndio hufa haraka katika vita" alisema Mnaro, akaniacha kushusha pumzi ya kujionea nafuu maana nilidhani labda Mnaro alikuwa ananipa majibu ambayo alikuwa ana uhakika nayo.



Baada ya kuliwaza hili la kuwa huenda kesho ya siku hiyo ningekufa, nikaamua kuwa ilikuwa lazima nikaonane na mke wangu ili angalau nipate kumuona kwa mara ya mwisho, maana sikujua nini kingetokea kesho yake. Nikamuelezea Mnaro adhma yangu, Mnaro akanionya kuwa mke wangu asingeniruhusu kuondoka kama angejua kuna hatihati ya kufa huko tuendako. "hakuna haja ya kumjuza juu ya hilo" nilijibu kwa kifupi na kumtaka Mnaro kunipeleka usiku utakapoingia.



Mke wangu alikuwa usingizini wakati nimeingia mule chumbani, nikamuamsha polepole, akaamka na kufurahi kukuta ni mimi, pia akanilaumu sana kwa kumtoroka, "nakupenda sana mke wangu, pamoja na mtoto wetu aliyemo humo tumboni, siwezi kuruhusu uende kwenye safairi hizo za hatari maana kama nitakufa nikijua nimewaachia uhai, nitakufa nikitabasamu ila kitakuwa kifo cha maumivu kama kitawajumuisha na nyie" nilisema kwa hisia sana, hata mke wangu akakosa cha kusema, akanikumbtia kwa nguvu sana. "tafadhali nambie sasa yameisha" alinambia mke wangu ambaye kwakweli alikuwa amechoshwa na mauzauza yale ambayo yalituvamia na kutibua maisha yetu ya furaha ambayo ndio kwanza tulikuwa tumeyaanza. "hapana, bado kidogo sana, safari imekuwa ya mafanikio na inatuhakikishia kulimaliza hili hivi karibuni" nilimjibu kwakifupi. "najua sipaswi kung'ang'ania tena kwenda na wewe, wala sipaswi kukuzuia, ila angalau usinitoroke tena, ukienda uniage" alisema mke wangu, maneno yeke yaliniumiza ila nikajikaza na kufanya kama lilikuwa jambo la kawaida. "angalia vizuri unayoyaona ili siku mwanangu akikua umwambie namna gani ninawapenda na niko tayari kufanya chochote kwaajili yenu" nilimwambia mke wangu jambo ambalo nilitaka amwambie mwanangu endapo atakuwa na kukuta baba yake ni marehemu, ila sikutaka mke wangu alijue hilo kwa sasa. "hakika nitamwambia" alijibu mke wangu ambaye hauweza kutegua fumbo lile. Tuliendelea kuongea hili na lile mpaka mke wangu alipopitiwa na usingizi. Kisha nikaamka na kuanza safari ya kurudi kwa Mnaro, nikimuacha akiwa usingizini, nilikuwa nakumbuka sana hitaji lake la kutaka kumuaga kabla sijaondoka ila nilikuwa najua kuwa nisingeweza kuagana naye, na kama ningethubutuat angefanikiwa kujua kuwa huko tunakokwenda hakukuwa salama. Nikaondoka kwa kupenya ukutani na kurudi kwa Mnaro.
 
SEHEMU YA 55



Mida ya safari yatu ilipofika tulienda mpaka maeneo yale ambayo kuna mlango wa Muifufu, kwa kutumi mikono yake Mnaro akafanya kama anatanua kitu, na kweli kukaonekana uwazi ambapo alinitaka kupita, kisha na yeye akafuata kabla hapajajifunga tena. "mpaka sasa Magugi ameshajua kama nimeingia Muifufu, hivyo kuwa tayari kwa mapambano" alisema Mnaro nami nikalishika vizuri panga langu, tukaanza safari katikati ya pori tukiutafuta mji wa Muifufu. Tofauti na mara ya kwanza safari hii tulikuwa na nguo zetu, tofauti na ambavyo nilikuwa nikijua kuwa mtu akiingia Muifufu lazima nguo na vyote alivyokuwanavyo kabla vibaki nje. "mbona leo tumebaki na nguo zetu?" nilimuuliza Mnaro. "hata mimi sijui, labda ndo manufaa ya safari ya ujinini" alijibu Mnaro, tukaendelea na safari. Tulipokuwa tumetoka eneo la pori na kuanza kuingia eneo la mji ilisikika suti kubwa, sauti ile ilikuwa haitofautiani sana na na sauti ya honi ya meli ambayo inalia karibu na masikio ya msikilizaji. "hao wanaitana kwaaajili yetu, jiandae" alisema Mnaro. Baada ya dakika kama kumi lilionekna kundi kubwa la watu mbele yetu, wakikimbia kuja upande wetu, Mnaro akawakusanya kwa mkono wake na kuwatupa mbali, huku tukiendelea kwenda. Mbele kidogo tukaona mawe mkubwa sana yakitupwa kuja upande wetu, Mnaro akayazuia yakabaki yakielea hewani, tukamuona mrushaji wa mawe yale akiendelea kuyarusha, lilikuwa ni limtu kubwa sana ambalo lilionekana kuwa na nguvu nyingi mno, kwa kutumia upanga wangu nikakata mkono wake wa kushoto ambao alikuwa anautumia kurushia mawe, lakini likaanza kurusha na mkono wa kulia, kanibidi kuukata na huo. Jitu lile ambalo lilionekana kuwa na hasira likatimua mbio kutufuata, Mnaro akalitandika na yale mawe ambayo lilikuwa linarusha na kulibwaga chini baada ya sehemu kubwa ya mawe yale makubwa kulipata kichwani. Basi mwendo wetu ukawa wa kukutana na vikwazo njiani lakini tulivimudu. Tulipambana na wachawi wazee vijana, mpaka watoto wengine walisikitisha sana kuwaua kwani niliona kama hawakuwa na hatia maana walichokuwa wanakifanya ni kutokana na maamrisho ya Magugi, wengine hata akili zao hazikuwa sawa, lakini ilikuwa ni lazima kuwazuia kama sisi ulitaka kutimiza lengo letu na njia ya kuwazuia ilikuwa ni kuwauwa tu kwani maneno yetu yasingeweza kusikilizwa.



Tukaenda mwendo huo wa kupambana na vikwazo mbalimbali mpaka kwa Magugi, leo tena nyumba haikuwepo. "tayari ameificha nyumba, utafanyaje sasa" niliuliza kwa kukata tamaa. "fumba macho yako" alisema Mnaro ambaye nilipomtazama niligundua kuwa yakweke yalikuwa yamefumbwa tayari, nimi nikafanya hivyo na kushangaa naiona nyumba ya Magugi vizuri tu. Tukaenda moja kwa moja na kuingia mpaka ndani ambapo tulimkuta Magugi akiwa amekaa kwenye kiti chake na pembeni yake alikuwepo yule jini ambaye husimama pembeni yake siku zote, sikujua namna gani yeye aliacha kuonekna msaliti maana Magugi alidai kuujua mpango wetu wote wa kutoroka Muifufu, sasa kwanini huyu bado anamuamini ikiwa pia alinisaidia, nilijiuliza. "washughulikie wapumbavu hawa" aliamuru Magugi, jini yule akatembea kuelekea upande wetu, Mnaro akaandaa mikono yake kupambana naye lakini nikamzuia, jini yule akatuvuka na kutoka akituacha tumfanye Magugi chochote ambacho tungependa kumfanya. "mbio za sakafuni huishia ukingoni, leo ndo mwisho wa ufalme wako" alisema Mnaro, akaunyoosha mkono wake na kumkaba Magugi kamnyanyua miguu yake ikabaki ikining'ia kisha akamtembea naye akimtoa nje katika hali hiyo. Huko nje kulikuwa na watu wengi ambao walionekana kama walikuja kwaajili ya kupambana ila muonekano wa Magugi ukawafanya wakashikwa na bumbuwazi, wakabaki kuwa watazamaji tu. Mnaro akambwaga Magugi chini pale uwanjani, akasimama na kutaka kukimbia, alikuwa anachekesha maana alikuwa ni mzee na hakuwa na uwezo huo wa kukimbia. Manaro akamnyanyua na kumsogeza mpaka kwake,kisha akamkaba shingo kwa mikono yake kabisa, mara Magugi akatoa kisu kidogo na kumchomanacho Mnaro shingoni, Mnaro akayumba na kumuachia Magugi ambaye alijiandaa kumjeruhi tena kwa kisu chake, nikawahi na kukata mkono wa Magugi, japo nilikuwa mbali hilo liliwezekana kwa msaada wa panga lile la ajabu sumu iliyopo kwenye hiki kisu ni kali sana, huwezi kupona tunakufa wote, alisema Magugi kumwambia Mnaro amabye alikuwa ameshika shingo yake kuzuia damu iliyokuwa inachuruzika, nikajisikia hasira sana na kukata shingo ya Magugi, kichwa chake kikadondoka chini. Nikenda kumtizama Mnaro ambaye nguvu zake zilionekana kumpunga kila muda ulivyozidi kwenda. "yule mmoja wetu ambaye anakufa leo ni mimi" alisema Mnaro, nikakosa hata cha kujibu. Twende haraka nikakufungulie mlango, usije ukabaki huku.



Mwendo wetu wa polepole ukatufikisha mahali ambapo Mnaro hakuweza kutembea tena, akasimama na kuniangalia kisha akatabasamu na kusema "nakuonea wivu sana, wewe unapata kila ambacho unakitaka na hata usichokitaka, umemtaka mkeo umempata, umetaka maisha yako umeyapata, mwisho umepata na kumuua Magugi, jambo ambalo hukuwa hukulitaka ila mimi niliyeliaka sana nimelikosa pia". Nilikuwa namuonea huruma sana Mnaro, mwisho wake haukuwa wa kupendeza ila sikuwa na chakufanya, hata cha kusema tu nilikikosa pia, machozi yaliyokuwa yakinichuruzika yalitosha kuelezea hisia zangu. "siwezi kuendelea, hii sumu ni kali kweli, kimbia haraka nikufungulie mlango kabla sijakata roho" alisema Mnaro nami nikaamua kukimbia kuelekea ulipo mlango, ambapo hapakuwa mbali na pale alipokwamia Mnaro, akajikaza na kuutanua mlango, lakini nguvu zikawa zinamuishia na mlangu unaanza kujibana polepole, nikakaza mwendo na kufnikiwa kupita na baada ya hapo ukajibana kwa kasi, nadhani ndipo Mnaro alipoaga dunia.



Maisha yangu yalirudi kuwa kawaid, nina furaha nikiwa na mke wangu na mtoto wetu wa kiume ambaye tumemuita Mnaro, sasahivi ana mimba ya mtoto wa kike nadhani huyu tutamiita Sauda. Famila yetu imejikita kwenye uchamungu, kwani nimegundua kuwa chamungu ni silaha kubwa dhidi ya nguvu za giza.



Mwisho
BURE SERIES
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom