Simulizi: Mpaka Kieleweke

SEHEMU YA 31

Nikavaa nguo na kutoka nnje ya nyumba ile ambapo nilimkuta yule mzee mwenye nyumba ile akiwa amekaa kwenye kiti cha mbao huku pembeni yake akiwepo binti mwenye afya mbovu sana akitwanga kitu ambacho sikukijua kwenye kinu! kwa mbali niliona watu wengine kila mmoja akiwa na kazi yake!...

ujio wangu pale nnje ulionesha kuwashitua watu wote waliokuwepo eneo lile wakawa wanasogea mmoja baada ya mwingine wakiwa wameshikwa na bumbuwazi!..

"ungepumzika kwanza afya yako itengemae, kaa hapa" alisema mzee yule huku akinipisha kiti ambacho alikuwa amekalia yeye! "hapana mzee, kaa tu! mimi niko sawa" nilijibu huku nikionekana kuwa na utimamu wa kutosha wa mwili, nikasogea na kukaa chini karibu na kile kiti chake "nadhani hamnijui, ningependa kwanza mnitambue kabla ya kukijua ambacho kimenileta kwenye mjini wenu" nilianza kujieleza lakini kabla sijafika mbali mzee yule alinikatisha "tunajua kila kitu kuhusu wewe, wewe ndiye ambaye hujui mengine kutuhusu! ila leo tutakueleza" alizungumza mzee yule nami nikakaa sawa kumsikiliza "najua unafahamu historia iliyopo kati ya wakazi wa mji huu na bwana Magugi.." Alianza kuzungumza nami nikakubali kwa kichwa kisha akaanza kuelezea kama sio yeye alieanza kwa kusema kuwa anajua kama naijua historia ile!..

akanielezea kila kitu kama ambavyo nilielezewa awali, lakini yeye alielezea mpaka maisha yalivyokuwa upande wa pili wa mlima baada ya kufika kwao "maisha hayakuwa mazuri kabisa, tulikuta ni eneo kame na lisilo na rutuba, hakukuwa na chochote cha kutuendeshea maisha zaidi ya ambavyo tulikuja navyo! Magugi alikuwa ametudanganya..

baada ya chakula kubaki kidogo, ilitubidi kukitoa chote kwa vijana kumi ili wao wapate nguvu na kwenda kutafuta kingi kwaajili ya wengine lakini walitakiwa kuwa makini wasiingie eneo la Muifufu na kuvunja mwiko tuliokuwa nao, vijana wale wakaenda na kufanya kazi ambayo waliagizwa, wakatafuta sana bila kupata chochote, mwishowe wakashauriana kuwa ni bora waingie Muifufu kuliko kuacha watu wote wa huku kijijini wafe na njaa!. kukatokea mabishano makili, wengine wakikubaliana na wazo hilo huku wengine wakipinga, hatimaye uamuzi ukaafikiwa kwamba kila mmoja afanye ambalo yeye aliona ni sahihi, hivyo vijana wanne wakarudi kijijini huku sita wakielekea eneo la Muifufu kutafuta chakula kwaajili ya waliobaki kwenye kijiji hiki wakiwa na hali mbaya sana kutokana na njaa...







"...basi wale vijana ambao waliamua kuvuka mpaka wa mlima kalingisi na kuingia eneo la Muifufu walilaanika na kugeuka kuwa Masokwe ambao wamekuokota na kukuleta hapa" alimaliza kunielezea mzee yule, nikashusha pumzi ndefu iliyoambatana na mshangao mkubwa juu ya historia ya sokwe ambao walinibeba kutoka mlimani mpaka pale kijijini "hivyo inamaana sokwe wale wanauwezo wa kutambua mambo?" niliuliza baada ya kushangazwa na kitendo cha sokwe wale kunipeleka pale nyumbani.

"ujio wako ulitabiriwa zamani sana na marehemu mzee Jafari ambaye alikuwa kiongozi wetu wakati huo na alikuwa na maono ya mbali, jamii hii imekuwa ikiishi maisha ya shida sana huku wakingojea ujio wako, hata masokwe wale wanatambua juu ya ujio wako ndio maana mara baada ya kukutambua walikuleta hapa haraka" alifafanua mzee yule namimi nikatumia nafasi ile kuwaelezea historia yangu yote ambayo inasababisha niwe pale na msaada ambao niliuhitaji sana kutoka kwao..

"kama ambavyo nimekueleza, sisi huwa hatuvunji ahadi, nadhani mpaka sasa unajua ubaya ambao unafuatia iwapo tutavunja kiapo ambacho tulikiweka. Kukusaidia kumuangusha Magugi bado ni kuvunja kiapo kwa maana tuliahidiana kutoshughulika na maisha yake kama akituacha tukaondoka Muifufu bila kutudhuru" aliongea mzee yule maneno ambayo yalielekea kunikwamisha, mapigo ya moyo yaka badilika ghafla na akili yangu ikawa inafanya kazi harakaharaka kujaribu kubuni namna ya kuwavutia watu wale ili kuungana nami katika kuuangusha utawala wa Magugi!..

"lakini tumekuwa tukiishi maisha ya kubahatisha kwa miaka mingi sana, jambo ambalo linatishia kutoweka kabisa kwa jamii hii, maana watu wanakufa kwa njaa. Tunahangaika sana kutafuta chakula na maji lakini tunapata kidogo sana kiasi cha kutoweza kututosheleza. Huu ni wakati wa kufanya maamuzi magumu na kuiweka hatma yetu mikononi mwako" aliongea tena mzee yule safari hii akiyarudisha matumaini yangu kwa kasi sana.

"sisi tutakusaidi ila ni lazima na wewe utusaidie. Kwakuwa nguvu kubwa ya Magugi ni msaada wa majini ambao ni sisi tulimtengenezea, basi tutaipunguza nguvu hiyo bila yeye kujua, baada ya hapo utafanya ambacho unataka kufanya ila malipo yetu sisi ni kifo cha Magugi ambacho kitavunja kiapo kilichopo kati yetu na yeye hata laana ambayo itatupata kwa kuvunja kiapo hicho itafutika papohapo" alielezea mzee yule nami nikamuelewa vizuri sana na kumsihi anisaidie na nitahakikisha maisha ya Magugi yanafikia mwisho kama malipo yangu kwao.
 
SEHEMU YA 32

"huu ni uamuzi mgumu sana tunafanya, hivyo itatupasa kukuapisha na wewe kama hutotenda kama ambavyo tumekubaliana basi hutokuwa na maisha marefu" alionya mzee yule.

"mzee wangu mimi nimetoka kote huko mpaka huku kwaajili ya kuhakikisha Magugi anakufa, bila kufa kwake hakuna mafanikio yoyote ambayo nitayapata ndani ya safari hii" nilijitahidi kumshawishi mzee yule ambaye hakuonekana kujishughulisha sana na maneno yangu baadala yake akaendelea kutoa maelezo yake.. "tutaapizana kiapo hapa na kisha tutakukata kidogo kwa kisu mgogoni kwako ambapo pataweka kakidonda kadogo tu lakini kidonda hicho kitaanza kukua siku hadi siku iwapo utaondoka Muifufu bila kumuua Magugi, kidonda hicho hakitopona kwa dawa yoyote zaidi ya kufa kwa Magugi na kama hilo halitotekelezeka basi kitafikia kutoa ushai wako mara baada ya kutapakaa mwili mzima" alitoa maelezo ya kutisha sana mzee yule na kunifanya kujiuliza mara mbilimbili kama niko tayari kuingia kwenye kiapo cha aina ile, lakini bado nilijikuta sina njia nyingine ya kufanikiwa zaidi ya kukubaliana na masharti yale magumu".

"niko tayari kwa lolote, lazima Magugi afe",

Nilijibu kwa ujasili mkubwa. Mzee yule akanitaka kupumzika hukua akiahidi kuwa usiku wa siku hiyo tutafanya taratibu zote za kiapo kisha asubuhi ya kesho yake nitafanya safari ya kwenda Muifufu kukamilisha zoezi lililopo mbele yangu!..

Niliwatazama watu wale nikawaonea huruma sana, afya zao zilikuwa dhaifu na kumbe chanzo ni njaa ambayo imesababishwa na ukatili wa Magugi, niliingia ndani nikaenda kwenye chumba ambacho nilijikuta baada ya kuzinduka na kuchukua fuko lile kubwa ambalo lilikuwa na nyama bado na maji kidogo nikatoka na kuwapati watoto wadogo ambao nilikuwa nawaona pale wakiwa na afya isiyo ya kuridhisha "hawa wananyonya, hawali chakula" nilishangazwa na kauli ile ambayo ilitoka kwa mwanamke mmojawapo pale kwa maana umri wao ulitosheleza kuwa wameanza kula "huku kwetu mtoto hunyonya mpaka hapo maziwa yatakapoisha kwa mama yake, chakula tunachopata huwa hakitoshi hivyo ni bora ale mama ili aweze kumnyonyesha mtoto, wote wapate" alifafanua yule mzee nikasikitishwa sana na ugumu wa maisha ya watu wale. Nikamkabidhi mwanamke yule mzigo ule ili yeye apange matumizi mazuri kwa maana niligundua kuwa pamoja na udogo wake kilikuwa na maana kubwa kwa watu wale...



Nikabaki nikiongea hili na lile na mzee yule huku akinithimulia mambo mengi ya zamani na jinsi ambavyo anayatamani tena maisha ya dunia ya kawaida ambayo yalikuwa mazuri na mepesi sana hata anajutia kuwa kwake mchani na hatimaye kuangukia Muifufu...

"lakini mzee mimi ninavyoelewa ni kuwa watu wote ambao walikimbia dunia ya kawaida na kujificha Muifufu hawakuweza kuzaliana tena, mbona huku mna watoto?" niliuliza swali na mzee akanijibu "watu wa Muifufu pia wanaweza kuwa na maisha tofauti kama watengwa kama ambavyo tulitengwa sisi, laana ya kutozaliana tuliipata kwa umoja ule, kwakuwa sisi sio sehemu yao tena, laana ile haituhusu tena" alifafanua mzee yule, nikamuelewa na kuendelea na habari nyingine mpaka kiza kilipoingia ambapo watu walianza kukusanyika kwenye uwanja wa nyumba ile na kulipotulia nikaitwa na kukalishwa kwenye kiti ambacho kilikuwepo katikati ya watu wale wakiwa wamekizunguka na kufanya mduara, mzee yule akaja na kuanza kusema maneno huku akinitaka kumfuatisha "mimi Abubakar Saire, ninaahidi kutekeleza makubaliano ambayo tumewekeana na kama nisipotekeleza basi kiapo hichi kiishi na mimi mpaka kitakaponitoa uhai wangu" yalisemwa maneno hayo huku nikifuatisha mpaka tukamaliza kisha akazunguka nyuma yangu na kunichanja na kitu chenye ncha kali mgongoni, hayakuwa maumivu makali kama ambavyo nilitegemea, na hapo kazi ikawa imemalizika. Watu wale wakaanza kuondoka huku kila mmoja wao akipita mbele yangu na kunipa mkono huku wakitoa maneno ya kunitakia mafanikio.



Asubuhi siku iliyofuata nikaongea na mzee yule na kumuuliza juu ya utekelezaji wa kazi ambayo wao walipaswa kuifanya.. "kila kitu kitakuwa sawa wakati unaingia Muifufu wewe kuwa tayari kwa safari" alisema mzee yule na safari ya kurudi Muifufu ikawa tayari, nikaondoka kijijini pale nikisindikizwa na wakazi wa kijiji kile mpaka mlimani kisha wakarudi na kuniacha nikipanda mlima ule...





safari ya kupanda mlima ilikuwa na changamoto kama ile ambayo nilikuwanayo wakati wa kuja mlima Kalingisi ingawa safari hii kidogo kulikuwa na unafuu uliotokana na kuijua safari yenyewe tofauti na safari ya kwanza ambapo sikuwa nikijua nilikuwa nakwenda katika safari ya aina gani!..
 
SEHEMU YA 33

ugumu wa safari hii ulinikuta mchana wa kwenye saa sita ambapo nilipatwa na kiu ya hali ya juu lakini sikuwa na maji ya kunywa, nilikuwa nimetokwa na jasho jingi sana nadhani sasa yalihitajika maji mwilini kufidia yaliyopotea, lakini ndo hivyo tena, sikuwa na maji hivyo ikanibidi kupambana kiume na safari ile mpaka majira ya saa kumi za jioni ambapo hali ilikuwa mbaya zaidi nikajikuta nikishindwa hata kunyanyua hatua moja ya ziada, hata macho hayakutaka kufanya kazi yake tena na kizunguzungu kikanitawala. Jambo pekee ambalo nilimudu kulifanya ni kukaa chini polepole lakini kabla sijafika chini kabisa nikashindwa kuutawala mwili wangu na kujikuta nikianguka na kupoteza fahamu...

nilipokuja kuzinduka nilijikuta katika mazingira ambayo niliyatambua, hapa ndipo ambapo wenyeji wangu wa Muifufu waliniachia nikaendelea na safari na wao wakarudi Muifufu wakati waliponisindikiza. Hii ni ndoto au hali halisi? nimewezaje kuvuka shughuli nzito ya kupanda na kushuka kwenye mlima ule nikiwa katika hali ya kutojifahamu? nilijiuliza lakini sikupata majibu na kuamua kuachana na jambo lile kwani akili yangu pia ilikuwa imechoka na haikutaka kufikiria zaidi. Nikapata nguvu na kusimama na kujitahidi kutembea kuelekea Muifufu. Hali ya mwili wangu bado ilikuwa dhaifu lakini kutokana na matumaini mapya niliyoyapata nikamudu vizuri kutembea ingawa haikuwa rahisi.

Sasa nakwenda wapi? sijui pa kumpata Sauda na mfadhili wangu bwana Mkude tayari alikuwa ameteketezwa kwa moto pamoja na mkewe na nyumba yao vile vile, nakwenda kufikia wapi?.. nilijiuliza na kuamua kuwa niende kwenye lile shamba ambalo nilimkuta Sauda akiwa na watu ambao walinisindikiza.

Pengine naweza kuwakuta, ila hata nisipowakuta nijificha hukohuko na kuwasubiri kuliko kunasa mikononi mwa Magugi, niliwaza nikiendelea kujikongoja.

Kwa mbali nililiona shamba likiwa na watu wawili waliovalia sare kama ambazo walivaa wale ambao walinisindikiza, nikazidi kujivuta kuelekea walipo ila kwa taadhari wasije wakaniona kwamaana sikuwa nimejua kama walikuwa salama kwangu ama laa!..

Nilipofika kwenye eneo la kuweza kuwatambua watu wale nikapata amani na kuwafuata moja kwa moja!..

walikuwa vijana wale ambao walinisindikiza wakati naelekea mlima Kalingisi..

Nilipowafikia nikajibwaga chini kama mzigo, sikutaka tena kufanya chochote kutokana na uchovu ulioambatana na njaa na kiu ya muda mrefu, mdomo wangu ulikuwa umekauka sana, hata mate hayakuwepo kinywani.

Mmoja wa vijana wale akasogea mpaka ambapo kulikuwa na vitu vyao, akachukua kibuyu na kujanacho pale nilipo na kuanza kuninywesha maji..

katika maisha yangu yote sikuwahi kuona maji yakiwa matamu namna ile, nilikunywa haraka haraka ndani ya muda mfupi yakawa yameisha ndani ya kibuyu nami nikajiachia na kulala chali pale chini shambani, nilikuwa nimechoka sana.

Vijana wale wakakusanya vitu vyao harakaharaka na kuja kunichukua wakinitaka tuondoke, wakaninyanua, nikasimama kisha wakaniweka katikati yao huku mikondo yangu ikiwa mabegani mwao kunirahisishia kutembea. Ama kweli maji ni uhai, nilikuwa na nafuu kubwa kiasi cha kuwataka mabwana wale waniache nitembee mwenyewe, jambo ambalo walikubali nami nikalifanya na kufanikiwa. Tukaenda tukizama zaidi kwenye mashamba na hatimaye tukakutana na kajumba kadogo katikati ya shamba la mahindi..

tukaingia ndani ya nyumba ile, nikaenda moja kwa moja na kujilaza kwenye kitanda ambacho kilikuwemo kwenye Kijumba kile na kupitiwa na usingizi...

Baada ya muda mfupi niliamshwa na vijana wale, walikuwa wameandaa chakula, tukala pamoja ingawa mimi nilionekana kula zaidi kuliko wenzangu ambao walimaliza mapema na kuniacha nikiendelea kula harakaharaka kama mtu ambaye sikuwahi kuona chakula kabla mpaka ambapo nilishiba na kuamua kupumzika huku nikiwataka vijana wale kumfikishia Sauda taarifa za kwamba mimi nilikuwa pale, vijana wale wakanitaka kupumzika huku wakiniambia swala lile niwaachie wao. Nikaendelea kupumzika nikiwaacha wao wakiendelea na mambo mengine..

Nilipoamka giza lilikuwa limeingia tayari, nikatoka nnje na kumkuta mmoja wa vijana wale akiwa busy kukusanya kuni kutoka huko mashambani na kuleta pale nyumbani "bwana, mbona Sauda hakuja? unajua sio salama mimi kuendelea kuwepo hapa bila muongozo wake" nilimsemesha bwana yule ambaye alikuja mpaka pale nilipokuwa nimesimama akanitaka kukaa chini naye akakaa kisha mazungumzo yakaanza "bwana kuna jambo unapaswa kulifahamu juu ya bi.Sauda" alianza kuelezea bwana yule na moyo wangu ukapiga paaah!, nikiona dalili ya kuwepo kwa habari mbaya kutokana na utulivu aliouonesha bwana yule kwenye kunipatia habari hizo.. "nini kimetokea?" niliuliza na bwana yule akaanza kunielezea "mpaka wakati huu tunaoongea bi. Sauda amekamatwa na bwana Magugi na hukumu yake inategemewa kutolewa kesho" alielezea kijana yule nikapatwa na mshituko mkubwa sana, sikutegemea jambo lile kutokea kabisa, Sauda ndiye aliyekuwa kiongozi wa mipango yote, kukamatwa kwake nilikuona kama kukwama kwa kila kitu.
 
15032762_940334169444393_761982921131658668_n.jpg
 
SEHEMU YA 34

"ilikuwaje mpaka akakamatwa?" niliuliza na kijana yule akatoa maelezo "wapelelezi wa Magugi wamekuwa wakimfuatilia mwenendo wake na kugundua kuwa amekuwa akitoka nyumbani kwake mara kwa mara hata usiku mwingi hivyo wakamfikishia taarifa hizo Magugi ambaye alipata mashaka juu yake na kuamuru akamatwe. Tulipotoka kukusindikiza wewe tukakuta habari za kukamatwa kwake na bwana Magugi ameahidi kutoa hukumu kesho baada ya kujua ukweli juu ya mwenendo wa Sauda" alimaliza kuelezea kijana yule, nikafikiria kwa muda kisha kumuuliza tena kijana yule "unadhani Magugi ataweza kuugundua ukweli?" kijana yule akanijibu "yani baada ya kukamatwa kwake tu sisi tulikata tamaa ya kuwanaye tena, Magugi akiutaka ukweli huwa haukosi" nikatulia na kufikiria kwa muda kisha kumuuliza tena kijana yule.. "kwanini ninyi mmejitolea kumfuata Sauda hata kumsaliti Magugi ikiwa mnajua hatari iliyopo ikiwa mtakamatwa?"...

"ni kwakuwa sisi tunaujua ukweli ambao watu wengi wa Muifufu hawaujui, ukweli ambao tumeupata kwa msaada wa Sauda na kuamua kuanzisha harakati za chinichini za kuwakomboa watu wote" alijieleza vizuri, lakini nilikuwa na maswali mengine ya kumuuliza.. "ni watu wangapi ambao mmejitolea kuwepo upande wetu mpaka sasa?" niliuliza, naye akanijibu "siijui idadi kamili lakini tuko wengiwengi kidogo, Sauda amekuwa akihakikisha tunakuwa na mtu kila sehemu, amekuwa pia akichagua wananchi ambao anawaona wanaweza kufaa iwapo wataujua ukweli na kuanza nao taratibu mwisho kuwarudishia kumbukumbu ambazo Magugi alizifuta vichani mwao, na kujaribu kuwaondoa hofu ambayo wamekuwa wakiishi nayo juu ya Magugi ambapo baadhi hufanikiwa ila ambao hawafanikiwi hua wanauwawa kwa maana wanakuwa wamepata siri ambazo wanaweza kuzitoa na kusababisha matatizo" alimaliza kunielezea nami nikauliza "je hakuna mtu wa karibu kidogo na Magugi ambaye yuko upande wetu?" kijana yule akanijibu "hapana ingawa Sauda aliwahi kumshawishi mshauri mkuu wa Magugi ambaye ni Mjomba wake lakini alikataa na mipango ya kumuua haikufanikiwa lakini hakuwahi kusema chochote, nadhani kwakuwa alikuwa karibu sana na Mnaro na alimpenda sana"

alielezea kijana yule na moja kwa moja nikapata hamu ya kutaka kuonana na mtu huyo "nawezaje kuonana na huyo mjomba wake?" kijana yule akanielezea "labda umfuate kwake kwa maana huwa sio mtu wa kutoka sana" alinielezea kijana yule nami nikamtaka anipeleke kwa huyo mtu naye akawa tayari.

Tukaenda mpaka kwenye nyumba moja kubwa ambayo haikuwa mbali sana na pale tulipokuwepo, tukakaribishwa na mwanamke wa makamo ambaye nilitambulishwa kuwa alikuwa mtoto wa mzee ambae tulikwenda kumuona pale "mmh! mzee amelala tayari" alielezea mwanamke yule baada ya kuambiwa kuwa tulikuwepo pale kwaajili ya kuonana na baba yake..

"ni suala la haraka sanaa, tunaomba utuamshie" nilieleze lakini mwanamke yule alionekana kutaka kupinga, lakini aliponyanyua kinywa chake tu kutaka kuongea mimi nikamuwahi "tafadhali tusaidie, ni jambo la uhai au kifo" nilisema huku nikimkazia macho nikiamini udhaifu wa wanawake utanifaa na kweli, hakuongeza neno zaidi ya kuelelea kumuamsha baba yake!...

Baada ya dakika kama tano alikuja mzee ambaye umri wake haukutofautiana sana na Magugi.

"kuna nini cha kuniamshia usikuusiku mabwana?" alisema bwana yule huku akikaa kutusikiliza.

Sikutaka kupoteza muda, nikamuelezea bwana yule juu ya ujio wangu..

"Mnaro alinitaka kukuona wewe ikiwa nitakwama popote, alisema wewe ni tegemezi kubwa kwake" niliongezea uongo kwakuwa mpaka wakati huo nilikuwa nikiamini kuwa mzee yule alikuwa na upendo kwa Mnaro ndio maana hakutoa taarifa kwa Magugi juu ya mwenendo wa Sauda hata baada ya kujua vizuri ambacho Sauda anakipanga kukabiliana na Magugi.

"sasa kijana unataka mimi nikusaidieje?" aliniuliza mzee yule kwa upole kabisa.

"mimi nataka kujua tu ni namna gani tunaweza kumuokoa Sauda kutoka kwenye kifo ambacho kiko mbele yake" nilijieleza, mzee yule akanitizama kwa utulivu, kisha akaongea "nilimuonya sana Sauda lakini hakutaka kusikia, jambo ambalo mnataka kufanya ni jambo la hatari sana, yani ninyi mmeamua kukitafuta kifo kwa jitihada zote hizo? kijana wangu, amini kuwa Sauda tumempoteza na urudi ukamwambie huyo Mnaro akae hukohuko aliko habari za huku azisahau kabisa kwaajili ya usalama wenu nyote" aliongea mzee yule akionesha waziwazi kutoamini kama Magugi anashindika...

"mzee wangu mpaka kuwepo hapa nimepoteza vingi sana, siwezi kurudi bila mafanikio ni bora kufa nikitafuta kufanikiwa" nilimjibu mzee yule nikionesha kutokuwa na nia ya kukata tamaa..

"sasa kama ninyi hamuhofii maisha yenu basi niachieni yakwangu, mimi siko tayari kufa hata kidogo" alijibu mzee yule.

Kufikia hapo nikaona kama sina kingine cha kumwambia mzee yule. "wakati mwingine jamii huwataka watu fulani kujitolea kwaajili ya usalama wa wengine wote hata kama kufanya hivyo ni kujiweka mashakani" hatimaye nilipata cha kusema na mzee yule akawa kimya, kama ambaye alikosa cha kusema.
 
SEHEMU YA 35

"sawa mzee wangu, sisi tunaondoka ila tunaomba kama huwezi kutusaidia basi angalau usijaribu kutuzuia" niliongea nikisimama kujiandaa kuondoka.. "safari ya mlima kalingisi ilikuwa na mafanikio?"

aliuliza mzee yule, nikashangaa kuona kuwa alikuwa akijua juu ya safari ile. Ikanibidi kukaa tena na kumuelezea juu ya safari ile.

"Magugi hakufanikiwa kupata majibu juu ya ukweli wa habari alizozipata kuhusu Sauda kutoka kwa majini wake kama ambavyo amekuwa akipata kabla, pengine ndiyo matunda ya safari ya mlima Kalingisi" Alizungumza mzee yule na kisha akaongeza "Magugi ameamua kuwa kesho atamtumia mtabiri wake wa siku nyingi, mzee Mikausho ili amwambie hatua ambazo atapaswa kuchukua juu ya Sauda, mnaweza kwenda, huo ndo msaada pekee ambao naweza kuwapa" alimaliza kuelezea mzee yule nami sikutaka kuendelea kuwa kero, nikaaga na kuondoka na kijana yule.

"unapafahamu kwa mzee Mikausho?" nilimuuliza kijana yule naye akakiri kupajua, na safari ya kwenda huko ikaanza mara moja...





njiani kote nilikuwa nikiwaza nakwenda kuongea nini na mzee Mikausho, jibu la swali hilo lilionekana kuwa mbali sana kwa wakati huo lakini bado ilikuwa lazima niende kwa maana kutokwenda ilikuwa ni kuruhusu kifo cha Sauda na kisha mipango yote kuvurugika. “haya ni mayai ya bundi wa zamani sana, mayai haya ni muhimu sana kwenye shughuli za uchai.. mchawi yuko tayari kufanya jambo lolote lililo ndani ya uwezo wake iwapo mayai haya yatakuwa malipo” maelezo yale ya Mnaro yalipita ghafla kichwani mwangu kama vile kuna mtu alikuwa akinielezea.



“inatubidi kurudi kwanza mpaka nyumbani kabla ya kwenda kwa mzee Mikausho” Nilimuelezea kijana yule, akaonesha kushangazwa na wazo lile hata akauliza “kwanini turudi kwanza nyumbani? unajua ni karibia saa tano sasa?” ilikuwa lazima kurudi nyumbani kwa maana sikuwa na ule mkoba alionipa Mnaro na sasa niliamini kuwa kuna kitu muhimu sana kwa wakati ule kiko ndani ya mkoba ule.. “ni bora kufanya mambo polepole lakini kwa usahihi kuliko kuwa na haraka isiyo na mafanikio, turudi” nilisema kwa msisitizo na kijana yule akawa mtiifu na safari ya kurudi penye makazi yetu ikaanza.. “vijana wa umri wangu huku Muifufu hawajui kama kuna maisha mengine ambayo yaliwastahili na sio haya” alivunja ukimya kijana yule na kuanzisha mazungumzo tukiwa katika safari ya kuelekea nyumbani.. “watu ambao walikuja Muifufu kwa hiari yao wote ni watu wazima kwa sasa, sisi mama zetu walipewa adhabu ya kuja huku kwakuwa walikuwa na mimba zetu matumboni mwao” alielezea kijana yule akionesha kuumizwa sana na hali ile.. niliuona uchu wa kuyataka maisha ya dunia ya kawaida ambao alikuwanao waziwazi kijana yule.



“umewahi kumuona mama yako?” nilimuuliza kijana yule jambo ambalo lilionekana kumuongezea machungu “mama yangu na wanawake wengine wote ambao huporwa maisha yao na kuletwa Muifufu kwaajili ya kujifungua watoto wao ili kuijaza Muifufu hufa mwezi mmoja baada ya kujifungua!.. hivyo mama yangu alinilea kwa mwezi mmoja tu kabla ya kufariki kwake” alieliza kijana yule. “mwisho wa Magugi umekaribia, ni lazima aadhibiwe kwa uonevu ambao amekuwa akiufanya” nilisema kumfariji kijana yule..

“sitokuwa na furaha maishani mwangu mpaka ambapo nitayatoa maisha ya Magugi kwa mikono yangu mwenyewe” alisema kijana yule akiongea kwa usongo wa hali ya juu huku aking’ata mengo yake kwanguvu kuonesha hasira alizokuwanazo”, sasa nikaamua kubadilisha mada kwa maana niliona mada ile ilikuwa ikimuumiza sana kijana yule.. “unajua mpaka sasa sikujui jina lako, unaitwa nani?” niliuza ili kubadili mada.



“naitwa Hisham” alijibu kwa kifupi kijana yule.. “Hisham unaweza kuwa unajua ambapo wanawake wajawazito huwekwa baada ya kukamatwa na kuletwa Muifufu?” Niliuliza tena nikilenga kujua alipo mke wangu kwa maana nilihitaji sana kumuona..

“kuna jumba moja kubwa sana, huwa wanahifadhiwa humo wakipewa huduma zote ili wawe na afya njema na kujifungua salama” alielezea kijana yule nami nikapata hamu kubwa ya kufika kwenye jumba hilo..

“tumalizane kwanza na hili, kesho utanipeleka kwenye hilo jumba”. Tulikuwa tumefika pale nyumbani, nikaingia ndani na kuchukua ule mkoba wa Mnaro na kutokanao kisha safari ya kwenda kwa mzee Mikausho ikaanza tena.





ulikuwa ni mwenda wa kama dakika ishirini tukawa tumefika kwenye nyumba moja kubwa na kubisha hodi kwa kama dakika tatu bila majibu "bila shaka watakuwa wamelala tayari" alisema Hisham!.. "lazima tuongee naye, hata kama amelala lazima tuhakikishe anaamka" tukaendelea kugonga mlango ule, mara tukasikia ukifunguliwa.. "shikamoo mzee Mikausho" Hisham alimsalimia mzee ambaye alikuwa amefungua mlango akiwa na taa ya chemli mkononi mwake.
 
SEHEMU YA 36

"marahaba Hisham" aliitikia mzee yule. Inaonekana mzee Mikausho na Hisham walikuwa wakifahamiana vizuri tu.. "shikamoo mzee" na mimi nikasalimia, mzee Mikausho akaitikia na kugeuza kurudi ndani "karibuni vijana" mzee Mikausho alikuwa mzee sana, hata mwendo wake ulikuwa wa kuinama.

Tukaingia ndani mzee Mikausho akiwa ametangulia huku sisi tukimfuatia nyuma yake.

Tukaishia sebuleni ambapo tulikaa na mzee Mikausho akafungua maongezi "watu ambao tunaelewa nini kinaendelea Muifufu ni wachache mno, ni ambao akili zetu ziliacha zikiwa nzima kwa sababu maalum" aliongea mzee Mikausho na kunifanya nijue kuwa alikuwa ana kitu ambacho anafahamu juu ya ujio wetu. "mimi niliachwa kuwa sawa kwaajili ya uwezo wangu wa kutabiri mambo yajayo pamoja na kuganga magonjwa mbalimbali" alisita kuongea mzee yule, akatulazama kwa zamu kisha akasema akiniangalia mimi "tuna mengi ya kuongea, lakini hatuna muda, sasa nipatie mzigo ambao umeniletea" alisema mzee yule akiniacha mdomo wazi, aliwezaje kujua kama nilileta kitu kwaajili ya kumpa?..

"inatupasa kuongea kwanza na kukubaliana kabla ya kukupatia huo mzigo" nilionesha nia yangu ya kufanya makubaliano kabla ya kutoa malipo ya jambo ambalo alipaswa kulifanya..

"mimi ndiye nisemaye nini kinafanyika, sio wewe! nipatie huo mzigo haraka na muende mkalale" alisema kwa kufoka mzee yule nami nikatii haraka sana!, nikatoa yai moja la bundi na kumkabidhi..

"haya nendeni mkalale, niachieni mimi jambo hili" aliamuru mzee yule mimi na Hisham tukatazamana na kusimama, tukatembea kuelekea ulipo mlango wa kutokea huku mzee Mikausho akitufuata kwa nyuma kutusindikiza. Hisham ambaye ndiye aliyekuwa mbele akafungua mlango na kutangulia nnje mimi nikifuatia.. "hongera sana kwa kazi nzuri kule Mlima Kalingisi, umenirahisishia sana" alisema mzee yule huku akifunga mlango nasi tukaendelea na safari ya kwenda nyumbani ambapo tulifika na kupumzika..

Asubuhi niliamka mapema na kumkumbusha Hisham juu ya safari ya kwenda ambapo wanahifadhiwa wajawazito pengine ningemuona mke wangu.

"sasa inabidi ungoje nikaongee na ambao wana zamu ya kupeleka kuni au maji leo niwaombe watuachie sisi kazi hiyo, pia nikakutafutie sare kama hizi zangu maana bila kuvaa hizi utashtukiwa haraka sana" alisema Hisham nami nikamkubalia, akaondoka akiniacha nikichimba mihogo ambayo ilikuwa imepandwa pale nyumbani kwaajili ya kuandaa kifungua kinywa..

Baada ya muda Hisham alirudi akiwa ameongozana na kijana mwingine ambaye nilimtambua moja kwa moja kuwa ni mwenzie ambaye walinisindikaza naye wakati nakwenda Mlima Kalingisi, na hata jana yake niliwakuta pamoja pale shamba nikitokea Mlima Kalingisi.

Walikuwa wambeba mabegani mwao madumu mawili ya majini yakiwa yameunganishwa na mti mgumu dumu moja likiwa mbele na lingine likiwa nyuma ya mti ule ambao ulikaa begani vizuri.

Vijana wale wakanywa chai kwa mihogo niliyokuwa nimeandaa kisha nikapewa sare na kuzivaa na ikapangwa safari ya mimi na Hisham kuelekea mtoni kuchukua maji na kisha kuyapelekea kwenye lile jumba ambalo alikuwepo mke wangu..

Kazi ya kubeba maji yale ilikuwa ngumu sana, ule mti ulikuwa ukiumiza mabega vibaya, ni bora maji yale ningeyabeba mikononi kawaida kwa maana nimewahi kubeba mara nyingi tu lakini aina hii ya ubebaji ilikuwa mpaya kabisa. Tulifika kwenye jumba lile nikiwa hoi, tukamimina maji kwenye moja ya mapipa makubwa yaliyokuwepo kwenye eneo ambalo kwa harakaharaka lilionekana kuwa la jikoni, kisha tukaelekea kwenye eneo ambalo lilikuwa na uwanja mkubwa sana watu wengi wakiendelea na shughuli zao, mara nikapishana na binti ambaye niliitambua sura yake haraka, nikaingiza mkono mfukoni na kutoa picha ambayo nilikuwa nimekwenda nayo na kujaribu kufananisha sura ambayo ilikuwepo kwenye picha na ile ambayo niliiona pale, hakika huyu alikuwa ni Regina, binti yake bwana Waisaka (yule hakimu ambaye alinitaka kuhakikisha ninatoka Muifufu nikiwa na binti yake).

Sikutaka kupoteza muda sana kwa binti yule, jambo la maana ni kuwa nilikuwa nimejua alipo, sasa kazi ya kumtafuta mke wangu ikaendelea!, Hisham alikuwa amenipotea baada ya mimi kuwa makini na picha ile kujaribu kuifananisha na mtu ambaye nilimuona..

Nikaendelea kuangalia bila mafanikio, lakini mara Hisham akanijia kwa kasi "njoo huku nimemuona"

alinieleza kwa kunong'ona huku yeye akigeuka na kutangulia nami nikamfuata haraka mpaka eneo ambalo lilikuwa limejitenda, nikamkuta mke wangu akiwa amekaa juu ya ngozi ya mnyama chini ya mti wa kivuli. Hisham akaniacha pale na kupotela ambapo sikupajua.

Nilimtazama kwa mbali kwa dakika kama tatu, kisha nikaamua kusogea mpaka pale alipokuwa amekaa, mke wangu alinitizama usoni lakini hakuonesha mshtuko wowote jambo ambalo lilinishangaza. "habari yako dada?" nilimsalimia mke wangu kama watu ambao hatujuani, naye akaitikia "nzuri tu kaka, sijui wewe"...

hali ile iliniumiza sana, mke wangu alikuwa hanijui kabisa kama ambavyo nilikuwa nimetahadharishwa kabla..
 
SEHEMU YA 37

"sijui unaitwa nani dada yangu?" niliuliza kujaribu kuona alikuwa hajitambui kwa kiasi gani.. "mimi naitwa Victoria, wengi wanapenda kuniita Vicky, alijibu mke wangu huku akiachia lile tabasamu lake zuri ambalo nilipenda kuliona usoni mwake siku zote.

Roho iliniuma sana, nikatamani kumrudisha mke wangu kwenye himaya yangu wakati huohuo lakini nikakumbuka kuwa sikuwa na lakufanya zaidi ya kuyafanya mambo kwa kasi ambayo mambo yenyewe yalitaka kwendanayo ili nisije nikaharibu kila kitu.

"yani wewe baadala ya kwenda kufuata maji unaleta umalaya hapa?" nilishtuliwa na sauti iliyotoka nyuma yangu, nikageuka na kukutana na mtu mwenye mwili mkubwa na ana jicho moja, nikabaki nimesimama nikimshangaa bila kusema neno lolote! "kwenda kachukue madumu ukalete maji" liliamuru jitu lile kubwa na mimi nikaondoka haraka eneo lile huku yeye akifuata nyuma yangu "watu wengine mnatafutaga kufa tu, unaingia hadi anga za mzee? mzee ana mpango naye yule" alisema kimzaha bwana yule nami nikajifanya kama ambaye sikuwa nikiyatilia maanani maneno yale, kumbe nilikuwa nikiyasikiliza kwa makini sana. Nikaenda mpaka eneo la jikoni ambako nilimkuta Hisham akichukua madumu yake na mimi nikachukua yangu, kisha tukatoka "fanyeni kinachowaleta humu mabwana, acheni ujinga" alitusindikiza na maneno bwana yule, nadhani alikuwa mlinzi , sisi tukaendelea na safari ya kwenda nnje bila kusema lolote.

"mzee ana mpangonaye yule? inamaana ni kweli Magugi anataka kumuoa mke wangu?" nilizungumza kwa sauti baada ya kuwa tumetoka kabisa kwenye lile jengo..

"ndivyo inavyosemekana, Magugi ana mpango wa kumuoa mkeo" alichangia Hisham..

"lakini si ulisema wanawake wale huwa wanauwawa baada ya kujifungua?" niliuliza.

"ni kweli, lakini sidhani kama sheria hiyo itatekelezeka kwa mwanamke ambaye anampenda" alijibu Hisham.

"hilo halitotokea kamwe, labda ayatoe maisha yangu kwanza" nilisema na safari yetu ikaendelea. Sikuwa nikitamani kwenda tena kwenye shughuli ile ya kuchota maji kwa maana lengo la safari ile lilikuwa limetimia tayari..

"sasa warudishie wale mabwana kazi yao waendeleenayo, mimi nakwenda kupumzika bwana" niliagiza na Hisham akaelekea kwenye utekelezaji wa hilo na kuniacha nikielekea nyumbani kupumzika.

Nilifika nyumbani, nikazunguka nyuma ya nyuma na kuoga, maana hakukuwa na choo wala bafu kwenye nyumba ile.

Nilipomaliza kuoga nikakaa pale nnje nikingojea maji yakauke mwilini ili niende kulala, lakini mara nilimuona Hisham akija mbio...

"watu wanakusanyika kwenye uwanja wa kwa Magugi, Inasemekana hukumu ya bi. Sauda inatolewa" habari ile ilikuwa yakushtua sana kwangu kwani nilikuwa naamini kuwa swala lile lilikuwa limeisha..

"inamaana mzee Mikausho amefanya uhuni?" niliuliza swali ambalo hakuwepo mwenye jibu lake pale, huku nikiingia ndani kuchukua shati na kutoka kwa kwasi nikiongozana na Hisham..







Tulikwenda moja kwa moja mpaka kwenye uwanja mkubwa mbele ya nyumba ambayo niliikumbuka kuwa ilikuwa ile nyumba ya Magugi, ingawa sikufanikiwa kupaona niliporudi tena.

Kwenye uwanja ule kulikuwa kumekusanyika watu wengi mno na mara nikamuona Sauda akiletwa mbele ya umati ule akiwa chini ya ulinzi wa wanaume wawili walioonekana waziwazi kuwa wakatili hasa, minong'ono ikatawala wakati akisogezwa mbele ya umati ule.

Baada ya watu wale kumfikisha ambapo walikusudia walimsukuma akaanguka chini na kutulia magoti, kisha mzee Magugi mwenyewe akasimama kutoka katika kiti cha thamani alichokuwa amekalia akinyoosha mkono wake wa kulia juu kuashiria kuunyamazisha umati ule uliokuwa umezi disha minong'ono, kimya cha kutisha kikatokea mara moja na Magugi akaanza kuzungumza.

"leo tuko hapa kushuhudia kuwa sheria ni msumeno!" alianza kuongea Magugi ambaye alikuwa na sauti iliyojaa ukali na ukosefu wa huruma.. "hakuna mtu hata mmoja ambaye anaweza kuwa juu ya sheria zangu na mfano mtauona muda mfupi ujao. Huyu mwanamke ni msaliti, amekuwa akifanya mambo mengi nyuma ya mgongo wangu akidhani haonekani ila serikali yangu ina mkono mrefu sana" Aliendelea kuongea Magugi akiwa amesimama hatua chache mbele ya kiti chake huku viti vya nyuma yake vikiwa vimekaliwa na watu wengine sita, niliweza kuwa tambua watu wawili tu kati ya sita ambao walikuwa wamekaa kwenye viti vilivyokuwa pale mbele!, walikuwa ni wazee ambao niliwatembelea majumbani mwao usiku kutaka msaada wa kuokoa maisha ya Sauda, hasira zangu zilikuwa juu ya mzee Mikausho ambaye aliahidi kutoa msaada lakini sasa alikuwa amekaa pale mbele kushuhudia kifo cha mwanamke ambaye aliahidi kumlinda. Kama wamefikia kuamua kumuua Sauda bila shaka ni ushauri wa mzee Mikausho, kwani utabiri wake ndio ambao ulikuwa ukisubiriwa ili kuamua Sauda aadhibiwe ama laah, kwa maana Magugi hakuwa na uhakika juu ya hili.
 
SEHEMU YA 38

"ili iwe fundisho kwa wengine, ninaku hukumu kifo cha kukatwa kichwa kwa upanga" alitamka Magugi, umati ule ukalipuka kwa kelele za kushangilia, ama kweli akili za watu wale hazikuwa sawa, siku zote walikuwa upande wa Magugi na kuona kila uamuzi wake ulikuwa sahihi. "hatuwezi kuruhusu Sauda afe!, inatupasa kufanya kitu" nilimwambia Hisham kwa sauti ya kunong'ona ikiwa na wasiwasi mwingi ndani yake.. "wewe ni mtu muhimu sana kaka, ukombozi wa Muifufu unakutegemea! tumia busara kwenye maamuzi ama utakata matumaini yote tuliyonayo, huu sio wakati wa kukata tamaa" alisema Hisham, maneno yake yakionesha ukakamavu wa hali ya juu. Nilimuele wa sana Hisham na kuamua kuwa mvumilivu na kushuhudia Sauda akifa bila msaada wowote kwani hata kama ningeamua kutoa msaada, ni nini ningefanya mbele ya watu wote wale? nikaamua kuwa mpole.

Wakati huu watu wale waliomleta Sauda walimburuza mpaka kwenye meza ndogo iliyokuwepo pale mbele wakaifunga mikono y ake kwa kamba ambazo zilishikanishwa vizuri kwenye meza ile huku paji lake la uso likigusa kwenye meza ile na kuacha sehemu ya nyuma ya shingo ikiwa tayari kwa kukatwa!..

Mtu mrefu sana aliyekuwa amevaa kinyago cha kuficha sura yake akasogea mpaka pale walipokuwa amefungwa Sauda akiwa na panga refu sana, maalumu kwaajili ya kuchinjia. Mtu yule alikuwa amesimama kama ambaye anangoja amri ya kutekeleza tukio lile la kinyama!.. umati wote ulikuwa ukipiga kelele nyingi huku zikisikika kauli za kuchochea kitendo kile kifanyike haraka!, hakika watu wale hawakuwa na huruma hata chembe. Magugi akanyoosha mkon o wake kuwanyamazisha kwa mara nyingine na watu wale wakatii.. "KATAAA" aliamuru Magugi na mtu yule akanyanyua panga juu kwa kasi tayari kwa kulishusha shingoni mwa Sauda!....

Niliishiwa nguvu mwili mzima ukawa ukinitetemeka na jasho jingi likinitoka.

Kabla panga lile halijashuka kulitokea tukio la ajabu sana..

ilitokea radi ambayo ilikwenda moja kwa moja na kupiga kwenye lile panga na kufuatiwa na kishindo kikubwa sana! panga lile likaponyoka mkononi mwa bwana yule na kuanguka mbali..

watu wote wakawa kimya wakishangaa kilichotokea.. "mfungueni, hana hatia" alisimama na kusema mzee Mikausho, kisha akaendelea "siku zote palipo ukweli, uongo hujitenga! mwanamke huyu hana hatia ndio maana mizimu ya mababu imezuia adhabu hii na kuipinga ni kukaribisha matatizo makubwa" alielezea mzee Mikausho.

"mfungueni" Magugi aliamuru baada ya kuona jambo lile halikuwa limetekelezeka baada ya maeleze ya mzee Mikausho.

Sauda akafunguliwa na kunyanyuliwa akasaidiwa kutembea kuelekea ndani ya jumba la Magugi, Magugi mwenyewe akifuata kwa nyuma.

"tawanyikeni, tutawajuza ambacho kitaendelea" alizungumza mmoja wa wazee ambao walikuwa wamekaa kwenye viti pale mbele kisha wazee wale wakaanza kuingia kwenye jumba la Magugi h uku watu wakitawanyika..

"mimi sio mtu wa kuvunja ahadi. Nimeona jinsi ambavyo umekuwa ukiteswa na dhana ya kuwa nimefanya usaliti" alisema mzee Mikausho ambaye alikuja mpaka ambapo nilikuwa nimesimama.. "kilichotokea hapa ni kazi ya la bundi ambalo ulinipa, kupitia yai hilo pia nitahakikisha nakuwa wa kuaminiwa na Magugi na watu wote wa Muifufu, kisha kazi itakuwa rahisi sana" alisema mzee yule kisha naye akaelekea kwenye jumba lile la Magugi. Nami nikaona sikuwa na sababu nyingine ya kunibakisha eneo lile, hivyo nikamtaka Hisham tuondoke.

Tukarudi kwenye makazi yetu tukiwa na matumaini mapya, moyo wangu ulikuwa ukimshukuru sana Mungu kwa kunusuru maisha ya Sauda.

Siku hiyo ilikwenda ikiwa tulivu mpaka giza lilipoanza kuingia ambapo nilimtaka Hisham tutoke kidogo ili nipate kuiona Muifufu inakuwaje usiku.

Tukatoka na kutembea huku na huko nikiona mambo mengi ya ajabu.

Watu wa Muifufu walikuwa ni wachawi sana na kwao halikuwa jambo la kuficha kama ambavyo uchawi umekuwa ukifichwa kwenye maisha ya dunia ya kawaida..

Watu wa Muifufu walikuwa wakifanya kazi nyingi usiku kuliko mchana, tena kwa njia za kichawi.

Nikafikia kutamani na wachawi wa dunia yetu wangekuwa kama hawa, wanatumia uchawi wao kufanyia kazi zao lakini sio kuleteana matatizo.

Niliona pia wachawi wakiendesha wanyama mbalimbali kama vyombo vya usafiri, wanyama wengine hata sikuwa nikiwajua, wengine walitisha sana hata kushindwa kuvumilia na kushtuka waziwazi wanapotokea mbele yangu.. ingawa Hisham alikuwa akinitaka kuvumilia kwa maana kushtuka kwangu kunaweza kusababisha kugundulika kuwa mimi sikuwa mwenyeji wa Muifufu kwa maana wanyama wale hawakuogopwa hata na watoto..

Nilichoshwa na safari ile kumwambia Hisham turudi nyumbani.

Tulipofika nyumbani tukamkuta yule kijana mwingine ambaye alinisindikiza pamoja na Hisham wakati wa safari ya kwenda mlima Kalingisi "nimewasubiria kwa muda sana, Sauda anataka kuonana na wewe" alinieleza kijana yule, akanitaka kufuatana naye nami nikafanya hivyo.
 
SEHEMU YA 39

Tukaenda tukipita njia ambayo inakwenda kwa Magugi lakini kwa mara nyingine tulipofika eneo lile sikuiona nyumba ya Magugi..

"hapa si ndipo ilipokuwa nyumba ya Magugi? mbona haipo tena?" safari hii nilimuuliza kijana yule ambaye nilikuwa nimeongozana naye, naye akanijibu, "nyumba ya Magugi imefanyiwa zindiko la kumkinga na wabaya wake, hivyo ukiwa na nia mbaya naye kuwezi kuiona nyumba yake" alizungumza kijana yule. "lakini mbona mchana niliiona?" niliuliza baada ya kushindwa kuzielewa kanuni ambazo alikuwa akinikaririsha kijana yule."kwasababu ni yeye aliyeitisha mkutano" alijibu kwa kifupi kijana yule tukawa tumefika kwenye nyumba ndogo lakini nzuri, tukaingia moja kwa moja ndani na kukaa kwenye viti, baada ya dakika kama tatu Sauda alikuja, akajumuika nasi na mazungumzo yakaanza."hongera kwa safari ya mlima Kalingisi, imekuwa ya mafanikio na imetusaidia sana. Sasa tunaweza hatu kutumia uchawi ambao tunaujua kufanya mambo ambayo yako kinyume na Magugi bila hofu ya kukamatwa, lakini pia umefanya jambo la maana sana kumleta mzee Mikausho upande wetu, kwani ni mtu muhimu sana kwa sasa, Magugi anamuamini na kumsikiliza sana" alipongeza Sauda nami nikashukuru.. "asante pia kwa kuokoa

maisha yangu, kama sio jitihada zako ningekuwa nimekufa" alisema Sauda, akionesha hisia kali zilizokaribia kumtoa machozi.. "usijali, ilikuwa lazima uishi ili tuweze kufanikisha zoezi ambalo limenileta huku, siwezi kukwama kwenye kumuokoa mke wangu" niliongea kwa msisitizo.

"kwa msaada ulionipa leo, nitahakikisha mkeo anarudi duniani kwa gharama yoyote" alisema Sauda nami nikashukuru.

Sasa kazi imebaki ndogo tu, inatupasa kuiba ufunguo wa Kufungua mlango wa Muifufu kurudi duniani, jambo ambalo nakutegemea wewe kulifanya, mimi natakiwa kuwarudishia kumbukumbu zao wote ambao tutaondoka nao kwenda duniani, vinginevyo haitokuwa kazi rahisi kuwachukua" alielezea Sauda.

"ni lazima mimi ndio nikafanye kazi hiyo ya kuiba ufunguo? kwani hatuwezi kupata mtu ambaye yumo ndani kwa Magugi tayari?" niliuliza.

"haya ni maelekezo ya mzee Mikausho, ametabiri mafanikio makubwa kwenye kukutumia wewe, utabiri wa mzee huyu haujawahi kukosea" alifafanua Sauda.

"itatuchukua siku ngapi kuondoka Muifufu, nimeyachoka sana maisha ya huku" niliuliza.

"mimi itanichukua siku tatu kuhakikisha akili za watu tunaowahitaji zinakuwa sawa na kumbukumbu zao zinarejea, baada ya hapo tutakuwa tunakutegemea wewe uibe ufunguo na kumuua Magugi" alielezea.

"hiyo funguo ikoje kwani, na Magugi huwa anaiweka wapi?" niliuliza kutaka kujua ugumu wa kazi yenyewe..

"hakuna anayeujua huo ufunguo zaidi ya Magugi mwenyewe, itakupasa kupeleleza sana" jibu hili likanifanya kuona kuwa kazi ile haikuwa ya kitoto.

"sasa nitaingiaje kwa Magugi?" Niliuliza tena..

"muda mfupi toka sasa mzee Mikausho atakuja kukuchukua hapa na kukupeleka yeye mwenyewe...







Naam, muda ukafika na mzee Mikausho akaja kunichukua pale kwa Sauda na safari yetu ya kwenda kwa Magugi ikaanza "hatimaye uhuru wa watu wa Muifufu umewadia, ni kama ndoto, tumesubiri kwa muda mrefu sana" alisema mzee Mikausho kana kwamba tulikuwa tumefanikiwa tayari, ilhali mimi bado niliona tulikuwa na mlima mrefu wa kupanda na kulikuwa na uwezekano mkubwa tu wa kutofanikiwa. "lakini sio jambo rahisi kumuongopea Magugi, vipi kama atanigundua kabla zoezi letu halijatimia?" nilihoji, mzee Mikausho akasitisha mwendo wake na kubaki akinitazama, jambo lililosababisha na mimi nisimame. "Kijana, umepitia changamoto nyingi sana, sijui kwanini huoni kama ulipotoka ni pagumu kuliko uendako? Nguvu ya Magugi kuweza kugundua mambo yajayo ilitokana na majini, majini ambayo tayari waliomptia Magugi wamehatarisha maisha yao ili kuuondoa uaminifu wao kwa Magugi, unadhani atakugunduaje bila kuwa na silaha yake hiyo anayoitegemea? Magugi ni mwanadamu, sio Mungu jamani, kwanini mnampa uwezo ambao hata hana?" aliongea kwa jazba mzee Mikausho lakini maneno yake yakaniongezea ari ya kufanya kazi, nikajikuta naamini kuwa Magugi ni mwanadamu kama mimi na uwezekano wa kumshinda upo, hasa baada ya tegemeo lake kubwa kuwa limezimwa. Tulifika pale kwenye jumba la Magugi tukaingia mpaka ndani bila kuzuiliwa na mtu yeyote, nadhani ni kutokana na kuaminiwa kwa mzee Mikausho katika nyumba ile. Tulifika, mzee mikausho akanipeleka kwenye chumba kikubwa ambacho kilikuwa kama chumba cha bweni kukiwa na vijana wengi,wengine wakiwa wamelala wakati wengine walikuwa wakiongea hili na lile. Mzee Mikausho akanitaka kukaa ndani ya chumba kile huku yeye akienda kuandaa mpango ambao utatuwezesha kufikia malengo yetu. Vijana waliokuwepo mule chumbani walionekana kunishangaa nadhani ni kutokana na kutonijua, lakini hawakuniuliza wala kunisemesha chochote na ndani ya muda mfupi wakaendelea na mambo yao kama vile hakukuwa na mgeni yeyotekatika chumba kile, nami nikatafuta sehemu na kukaa, baadaye usingizi ukanichukua.

Nilikuja kushtuliwa na kelele za watu ambao walikuwa wakiamka na kuanza shughuli zao za kila siku, Mara alisikika mtu akilia kwa sauti na watu wakawa wanatoka mbio kuelekea nje ya chumba kile, nadhani walikuwa wakitaka kushuhudia nini kilikuwa kimetokea, nami nikaamua kuungana nao maana nilitaka pia kujua nini kilikuwa kinaendelea.

ITAENDELEA BAADAE KIDOGO
 
SEHEMU YA 40

Mbio zetu zikakomea katika eneo la wazi ambapo kulikuwa na kijana akiwa ametapakaa damu akiwa ameshika kisu mkononi mwake, akijichoma maeneo mbalimbali ya mwili wake huku akitoa kelele za kilio cha uchungu ?MIMI NI MSALITI, SISTAHILI KUISHI? kijana yule allikuwa akisema maneno yale ndani ya kilio cha uchungu wa maumivu, mwisho akajichoma kwa kisu kile shingoni na polepole nguvu zikawa zinamuishia, akakaa chini damu zikiendelea kumchuruzika mwisho akapoteza uhai. ?Chukueni maiti yake mkaitupe msaliti mkubwa huyo? alisema mzee Mikausho kuwaamuru vijana wale ambao walikuwa wamevaa sare nao wakatekeleza huku watu wakitawanyika katika eneo lile. ?nini kimemkuta huyu bwana?? nilimuhoji mzee Mikausho kwa sauti ya chini tukiwa tumeongozana kutoka eneo lile. ?huyu alikuwa mtumishi binafsi wa bwana Magugi, ameyatoa maisha yake ili kukuachia wewe nafasi hiyo? alielezea kwa kifupi mzee Mikausho, na kuniacha nikiwa sijaelewa vizuri. ?inamaana alikuwa mmoja wetu?? nilihoji ili kupata ufafanuzi zaidi. ?hapana, huyu alikuwa mtendaji muaminifu kwa Magugi, mauti ilikuwa njia pekee ya yeye kukupisha nafasi hii? alisema mzee Mikausho, maneno yake yakanifnya kugundua kuwa kifo cha kijana yule kilitokana na hila zake. ?sisi sio wauaji mzee, unawezaje kutoa uhai wa kijana asiye na hatia?? nilihoji swali ambalo mzee Mikausho hakulijibu, tukaingia kwenye chamba kimoja, mzee Mikausho akafunga mlango kisha akanisemesha kwa sauti ya chini ?maisha ya mtu mmoja yana thamani gani mbele ya ukombozi wa watu wote wa Muifufu? Unadhani unaweza kuitimiza lengo lililokuleta Muifufu kwa kufuata itikadi zako za kilokole?? alihoji mzee yule kisha akanikabidhi nguo ambazo zilikuwa sare za watumishi wa jengo lile, akanitaka kuzivaa haraka na kutoka chumbani mule huku yeye akitangulia kutoka, nami nikavaa nguo zile na kutoka chumbani mule na kuchanganyka na watu wengine. Watu wote walikuwa busy na majukumu mbalimbali, kasoro mimi ambaye sikuwa na chakufanya kwani kila jukumu lilikuwa na mtu maalumu ambaye aliwajibika kulifanya, hivyo mimi nikabaki nikitemmbeatembea tu ndani ya jengo lile.

Baada ya kama nusu saa mzee Mikausho akaja kunichukua akinitaka kwenda kutambulishwa kama mtumishi mpya mbele ya Magugi, nikjikuta nikiingiwa na hofu iliyopelekea mwili wangu kutetemeka. ?kumbuka jambo moja, yeye ni binadamu kama wewe? alisema mzee Mikausho, maneno yale yakanitia moyo. Ghafla nikakumbuka kaelezo ya Mnaro juu ya uwezo wa Magugi kuweza kutambua uoga wa kumsaliti kupitia pumzi ya msaliti, hivyo nilipaswa kumeza dawa ambayo Mnaro alinipa, hivyo nikamtaka mzee Mikausho kunipa dakika moja, nikakimbia mpaka ambapo ulikuwepo ule mkoba wangu na kuchukua kikopo kile chenye dawa ambayo ilifanana sana vikokoto vile vidogo sana, nikachukua kamoja na kumeza, kisha nikatoka kumrudia mzee Mikausho huku nikijaribu kubana pumzi ili nione kama nilikuwa naweza kujizuia kupumua, na kweli niliweza kufika mpaka alipokuwawepo mzee Mikausho bila kuvuta wala kutoa pumzi, nikajisikia faraja sana.

Tulikwenda mpaka kwenye chumba kikubwa ambacho kilionekana kama ofisi, tukamkuta Magugi akiwa amekaa kwenye kiti kikubwa chenye hadhi, baada ya kuigia kwenye chumba kile mwendo wa mzee Mikausho ukabadilika, akawa anatembea akiwa kainamisha uso wake kusogela eneo alilokuwepo Magugi, nami nikafanya kama yeye nikimfuata nyumanyuma, huku nikihakikisha sipumui, jambo ambalo lilikuwa jepesi tu kutokana na dawa ambayo nilikuwa nametumia. Pembeni ya Magugi alisimama mtu mrefu sana, mwenye nywele ndefu sana, macho ya mtu huyu yalikuwa ya bluu, na ngozi yake ilikuwa inaelekea kwenye rangi kama ya njano, hali iliyofanya mtu huyo kuwa na sura ya kutisha sana, hakuwa akipepesa macho wala kutingishika hata kidogo, alionekana kuwa mlinzi wa Magugi. ?mkuu huyu ndio kijana pekee ambaye ana uaminifu wa kutosha kuwa mtumishi wako? alisema mzee Mikausho na Magugi akasimama na kuanza kusoge kuja tulipokuwa tumesimama, huku mtu yule ambaye husimama tu pembeni yake kifuatia nyuma yake. ?nyanyua uso wako? alisema Magugi, nami nikatii na kuinua uso wangu japo sikuweza kumwangalia. ?umeshuhudia kinachotokea kwa mtu anayejaribu kunisaliti?? aliuliza Magugi kunichimba mkwara. ?ndio mkuu? nilijibu harakaharaka nikijifanya kuwa mwenye adabu nyingi mbele ya adui yule ambaye nilitamni afe muda wowote. Magugi akarudi kwneye kiti chake, ?mwelekeze majukumu yake? alisema Magugi na mzee Mikausho akaitikia, tukatoka.

Majukumu yangu hayakuwa makubwa sana, nilikuwa na kazi ya kufuata chakula jikoni na kumpelekea Magugi muda wa kula unapofika, pia nilikuwa na jukumu la kufua nguo zake na kumuandalia maji ya kuoga, hayakuwa maisha magumu kama ambavyo nilifikiria.
 
SEHEMU YA 41

Ilikuwa imekatika siku ya pili sasa nikiwa ndani ya nyumba ya Magugi, nikitumika bila malipo na sikuwa nimefanikisha hata sehemu ya lengo langu la kuwemo ndani ya jumba lile, yule mtu wa ajabu aliyekuwa pembeni ya Magugi (ambaye nilikuja kugundua kuwa alikuwa jini) hakuwa akibanduka ubavuni mwake hata akienda chooni hali iliyofanya kazi ile kuwa ngumu zaidi, nilihofia kufanya mambo yangu kwa kukurupuka nikijua kuwa iwapo sitokuwa makini jini yule anaweza kugundua hila zangu na kifo changu kitakuwa kimewadia bila kutimiza lengo langu la kwenda Muifufu. Hivyo niliamua kuwa mpole.

Ilikuwa usiku wa kama saa tano, nilikuwa nimelala kwenye chumba ambacho nilikuwa nimepewa ndani ya jumba lile, mara nilihisi upepo mkali ukipuliza na chumba kikajaa mwanga mkali ghafla, nikapatwa na hofu na kuinuka kuangalia kulikuwa na nini, macho yangu yakakutana ana kwa ana na yule jini ambaye hukaa pembeni ya Magugi. ?UMEKUJA KULETA MICHEZO YA AJABU HUMU NDANI UNAYAPENDA MAISHA YAKO KWELI??

Alihoji jini yule akinisogelea kwa karibu zaidi na sura yake ilionekana kutisha zaidi, akili yangu ikawa inafanya kazi haraka haraka kujaribu kujua namna gani nitajinasua kwenye janga lile, nikaukimbilia ule mkoba wangu ingawa sikujua kuna silaha gani ambayo ingeweza kupambana na kiumbe yule wa ajabu, lakini jini yule aliufikia mkoba ule kabla yangu, sijui aliwezaje. Sasa sikuwa na lakufanya zaidi ya kungojea kuona kiumbe yule alitaka kunipa adhabu gani maana sikuwa na nguvu wala mbio za kumzidi.







?hukuja kufanya maisha humu ndani, kuna watu wamejitolea maisha yao na mpaka wakati huu wanateseka kwaajili yako, lakini hakuna kitu cha maana unafanya zaidi ya kuwa muhudumu, unadhani umebaki muda kiasi gani kabla mzee hajakugundua?? alihoji jini yule sauti yake ikishuka kidogo nami nikapata amani, nikashangaa kuona kuwa kiumbe yule ambaye nilikuwa nikimuhofia kumbe alikuwa upande wangu, nilishindwa hata kumwambia kama alikuwa na mchango mkubwa katiaka kushindwa kwangu mpaka wakati ule. ?sijui hata pa kuanzia, kama kuna msaada wowote unaweza kunipa nitashukuru? nilimwambia jini yule kutaka kuona kama kulikuwa na namna yoyote ya kurahisisha kazi ile. Jini yule akanitupia ule mkoba wangu huku akisema ?umepewa dhana zote za kukuwezesha kukamilisha hii kazi, ni uzembe wako tu?, jini yule akapotea ghafla kama ambavo alikuja na kuniacha nikiwaza namna ya kuharakisha kazi ile, nikavimwaga chini vifaa vyote ambavyo vilikuwemo kwenye ule mkoba na kuanza kujiuliza kipi kingeweza kunifaa kwenye kazi yangu, bado nilikuwa na yai moja la bundi, ile dawa ya kuzuia kupumua pamoja na ule mkate ambao niliambiwa nikifanikiwa kumlisha mtu ninaweza kumuamuru chochote na akafanya, akili yangu ikavutwa zaidi na ule mkate, nikaona kama nitafanikiwa kumlisha Magugi basi huenda jambo langu likawa jepesi, tatizo likawa namna gani nitamlisha Magigi mkate ule wa zamani tena umekauka mno, nikakosa jibu na kuamua kulala, haikuchukua muda nikawa usingizini.

Asubuhi na mapema nikaamka na kuendelea na majukumu yangu ya kila siku, akili yangu ikiwaza juu ya ndoto ambayo niliiota usiku, ndanoi ya ndoto hiyo nilimuona Mnaro aakinielekeza mambo mbalimbali, tukafikia kuliongelea swala la mkate ule ambao nilitaka kumlisha Magugi, Mnaro akanambia ndani ya ndoto ile kuwa mkate ule ulikuwa na uwezo wa kumpumbaza mtu akafanya kama ambavyo ningetaka afanye lakini ni ndani ya saa moja tu na baada ya hapo atarejea katika hali yake ya kawaida, nilikuwa nikijiuliza je ile ilikuwa ndoto tu kama ndoto nyingine au nikweli Mnaro alikuwa amenifikishia taarifa? Ndani ya ndoto ile Mnaro pia alinipa kafimbo kadogo na akaniambia mchwi akichapwa na fimbo ile huugua hadi kufa, hivyo akanitaka kuitumia silaha ile kwaajili ya kuyaondoa maisha ya Magugi,ila nilipoamka sikukaona kafimbo kale,hivyo nikaona labda ilikuwa ndoto tu.

Ulikuwa umekaribia wakati wa kumpelekea Magugi chakula cha mchana, nikapata wazo la kusaga kamkate kale ili niweze kupata ungaunga ambao nikiuchanganya kwenye chakula chake itakuwa ngumu kwa Magugi kugundua hivyo atakula chakula kile na mkate ule utampumbaza ili niweze kupata nafsi ya kumuhoji aweze kunielezea namna ya kufungua mlango wa Muifufu tuweze kurejea diniani, lakini nikajiuliza itakuwaje kama kweli nguvu ya dawa ile ingedumu ndani ya saa moja tu ikiwa sikuwa nimewaandaa waondokaji kwa safari, je muda wa saa moja ungetosha kuwaandaa na kuondoka kabla Magugi hajarudi katika akili yake na kutuzuia? Mwisho nikaamua kuwa inanibidi kuijaribu ile dawa kuona kama kweli nguvu yake itakaa ndani ya saa moja tu, pia nilitaka kujua kama dawa ile ina nguvu juu ya mchwi mkubwa kama Magugi, hivyo nikakagawe kamkte kale japo kalikuwa kadogo ili sehemu yake itumike kwa majaribio lakini ibakie sehemu ambayo itatumika kutimiza lengo halisi.
 
SEHEMU YA 42

Nikaenda haraka mpaka kule chumbani, nikauchukua mkoba wangu na kuanza harakati za kuutoa ule mkate. Lakini nilishangaa kukuta ndani ya mkoba ule kulikuwa na kafimbo kale ambacho niliota Mnaro kinikabidhi kwaajii ya kumuulia Magugi, nikkajikuta nikiamini kumbe ile haikuwa ndoto bali msaada wa Mnaro katika kufanikisha kazi ambayo ilinipeleka Muifufu, hivyo nikaachana haraka na wazo la kufanya majaribio ya mkate ule na baadala yake mawazo yangu yakahamia kwenye kufikiri namna ya kumfikia Sauda kumjulisha kuwa alitakiwa kuwaandaa watu kwa safari maana safari ilikuwa imetimia. Nikatoka na kwenda kumtafuta mzee Mikausho ambaye nilimuelezea kila kitu na kumtaka kutafuta namna ya kumfikishia Sauda ujumbe ule, naye akakubali.

Tulipanda kuwa kwa kutumia mkate ule wakati nampa Magugi chakula cha usiku, Magugi atapumbaa na kunipa nafasi ya kumuuliza namna ya kufungua mlango wa Muifufu kisha nitamchapa na fimbo ile naye atakufa kisha tutaufungua mlango ule kutumia ujuzi atakaokuwa amenipa Magugi kisha tutaondoka Muifufu.

Nikamuacha mzee Mikausho akienda kuongea na Sauda huku mimi nikiendelea na kazi zangu huku nikingojea usiku ufike nifanye mambo yangu.

Hatimaye usiku ukafika, na muda wa Magugi kupata chakula ukawa umekaribia, lakini sikuwa nimeonana na mzee Mikausho hivyo sikuwa nikijua kama safari imeandaliwa au laa, nikabaki njia panda nisijue cha kufanya, ingawa mkate wangu nilikuwa nimeusaga tayari, niikuwa nangojea chakula kiwe tayari tu ili niweze kukichanganya na unga wa mkate ule na kumpelekea Magugi.

Kutokuonekana kwa mzee Mikausho kukaninyima uhuru wa kuendelea na kilichopangwa, nikaamua kuahirisha zoezi. Chakula kikawa tayari nami nikawa najiandaa kwenda kukichukua kwaajili ya kumpelekea Magugi bila kuweka ile dawa yangu, lakini wakati nikielekea kuchukua chakula nikakutana na mzee Mikausho ambaye alinipa ishara nimfuate, nami nikamfuata mpaka eneo la mafichoni kidogo ambapo tulisimama. ?mkeo anaumwa aisee, tumbo linamsumbua toka jana? alieleza mzee Mikausho, habari ambazo zilinishtua na kunifanya nitamani kumuona mke wangu, ?vipi kuhusu kumbukumbu zake? Zimerejea?? niliuliza. ?kumbukumbu zake ziko sawa, na anatamani sana kuonana na wewe, ila tunajiuliza ataiweza mikikimikiki ya safari na hali yake ya ujauzito na kuumwa?? alihoji mzee Mikausho. ?leo tunaondoka kwa hali yoyote? nilitoa jibu fupi na mzee Mikausho akakubaliana na mimi, ikanibidi kurudi chumbani ambapo nilichukua kale kafimbo na ule unga wangu nikaja kuchanganya kwenye kile chakula huku nikisaidiana na mzee Mikausho. Kila kitu kikawa sawa, nikaenda mpaka kwa Magigi ambaye alikuwa tayari akisubiri chakula ?leo chakula kimechelewa kwa dakika 20? alisema Magugi huku akinitizama machoni wakati nikimnawisha, mara zote hupenda kumtizama mtu kwa makini machoni kujribu kuona kama ana dhamira mbaya juu yake, na kama mtu anakuwa na dhamira mbaya lazima ataaingiwa na uoga na pumzi yake kubadilika na Magugi hugundua haraka, lakini kwangu hakuwa akifanikiwa kwamaana mara zote huenda mbele yake mara baada ya kumeza ile dawa yangu na kuzuia kupumua.

Magugi akala chakula kile bila kushtukia chochote, alipomaliza akaonekana kunitizama sana, mpaka nikaanza kuingiwa na wasiwasi ?chakula cha leo kilikuwa kitamu sana, kweli mambo mazuri hatayaki haraka? alisema Magugi wakati namnawisha. ?umekuwa ukifanya kazi yako vizuri sana mpaka natamani kukuzawaidia, ungependa nikupe zawadi gani?? aliuliza Magugi, nikajiuliza ni akili yake au dawa inafanya kazi, kwa maana hakuoneekana kama mtu ambaye anaweza kufikiri chochote juu ya mtu mwingine. ?ningeshukuru kama ungeniambia mlango wa kutokea Muifufu unafuguliwaje? nilijibu nikiwa na wasiwasi maana nilijua kama dawa ile haikuwa imefanya kazi swali lile lingeniweka pabaya. Kabla haasema chochote Magugi akamtizama jini yule ambaye mara zote husimama kando yake, kisha akasema ?ni mimi na huyu mlinzi wangu pekee ndio tunajua siri ya kufungua Mlango wa Muifufu, ila kwakuwa ndio zawadi pekee uliyoiona na wewe nitakujuza? aliweka kituo kidogo kisha akaendelea ?watu wengi wanatamani kuujua ufunguo wa Muifufu, hawajui kama ufunguo wa Muifufu ni mimi mwenyewe na siku nikifa mlango wa Muifufu utakuwa umefungwa milele? alisema Magugi maneno ambayo yalinishtua. ?unamaanisha nini?? niliuliza kutaka ufafanuzi zaidi ?mimi ndiye ninayajua maneno ambayo nikiyasema mlango unafunguka, na hata kama mtu mwingine kiyajua maneno hayo hayawezi kumfaa chochote kwani hayatendi mpaka niyatamke mimi, uhai wa mlango wa Muifufu pia umeungana na uhai wangu, siku nikifa basi mlango ule utajifunga na hautofunguka tena? alielezea vizuri Magugi.
 
SEHEMU YA 43

Sasa tutawezaje kuondoka kama baada ya kumuua Magugi mlango utajifunga?? nilijuiliza, lakini sikupata jibu, mwisho nikaamua kubadili mpango. Mpango mpya ukawa kumwambia Magugi aufungue mlango ubaki wazi ili tutumie muda ule usiozidi saa moja kutoroka kabla dawa ile haijamuisha akilini. Jambo pekee ambalo lilibaki kuwa tatizo ni ahadi niliyowekeana na watu wa mlima Kalingisi, watu wale walivunja mwiko wao ili kunisaidia mimi, kuvunjika kwa mwiko huo kunawasababishi wao laana, pengine wamekwishageuka Masokwe kama wale wenzao na wananitegemea mimi kumuua Magugi ili laana hiyo ifutike, lakini sasa sikuwa na nafasi ya kumuua Magugi, potelea mbali natatua kwanza tatizo lililopo mbele yangu, hayo mengine tutajua baadae. ?sasa leo ungeuacha mlango wazi angalau hewa iingie kidogo maana mlango ule umekuwa ukifungwa tu siku zote? nilimwambia Magugi naye hakubisha, akayaona maeneno yangu yalikuwa ya busara kweli, akasimama na kunyoosha mikono yake juu huku akisema maneno ambayo sikuyajua maana yake na wala siyakumbuki tena, ndani ya sekunde chache akawa amemaliza na kusema tayari mlango uko wazi, wacha hewa iingie leo. Hapo nikona tayari nilikuwa nimemuweza, nikaaga kuwa nilikuwa nakwenda kulala lakini nikaenda kwa mzee Mikausho nikamueleza kilichotokea, akafurahi sana na kunitaka tuharakishe mpaka eneo ambalo walikubaliana na Sauda kuwa tutawakuta hapo, kweli tuliwakuta wakiwa wamejificha wakitungojea sisi, mke wangu alifurahi kuniona akajitahidi kusimama na kunikumbatia kwa uchungu huku machozi yakimtoka, nami nalifurahi sana kumuona akiwa katika akili yake timamu. Kila mtu alikuwa na hamu ya kujua nini kiitokea lakini tukawataka kuondoka kwanza kwani tulikuwa nje ya muda, mengine wangeyajulia huko mbele ya safari. Tulikuwa jumla ya watu tisa ambao ni mimi, mke wangu, Sauda, mzee Mikausho, yule binti wa hakimu ambaye liifunika kesi yangu na kunitaka nimrejeshee binti yake, Hisham na vijana wengine watatu ambao sikuwa nimeyajua majina yao. Yule mzee ambaye alituelekeza kwenda kupata msaada kwa mzee Mikausho yeye niliambiwa aliikataa safari ile akidai anauona mwshilio mbaya mbele ya safari, hivyo wakampuuza na kumuacha na maisha yake ya Muifufu.



Mwendo wetu haukuwa wa kasi sana kutokana na kuwa na mke wangu ambaye alikuwa na mgonjwa pia binti yule wa hakimu ambaye mimba yake ilionekana kufikia mwishoni, hivyo walikuwa na mwendo wa kujivuta huku mimi nikimsaidia mke wangu na mmoja wa wale vijana akimsaidia binti yule wa hakimu, tukawa tunakwenda huku tukipumzika hapa na pale Sauda kituongoza njia kuelekea ulipokuwa mlango wa kutokea Muifufu, muda nao ulikuwa ukiendelea kututupa mkono, kwa haraka haraka nilihisi tulikuwa tumebakiwa na dakika zisizozidi ishirini hivyo niazidi kuwahimiza japo safairi haikuwa nyepesi.



Hatimye tukafika mpaka eneo la tukio lakini cha ajabu ni kwamba mlango haukuwa wazi kama ambavyo tulidhani tungeukuta. ?mmh! Mbona mlango wenyewe hauko wazi?? aliuliza Sauda ambaye ndiye alikuwa mwenyeji wetu kwenye swala la mlango huo, mimi sikuona chochote zaidi ya eneo la pori kama yalivyo maeneo mengine. Ikanibidi kuwaelezea kila kitu kilivyokwenda nyumbani kwa Magugi na namna ambavyo nilifanikiwa kumlisha ule mkate na kumfanya afungue mlango, sote tukaamini kuwa tulikuwa tumechelewa kufika pale ndani ya saa moja na sasa Magugi alikuwa amerudiwa na akili zake na kuufunga mlango ule haraka kabla hatujafika. Sasa tufanya nini? Tutakwenda wapi ndani ya Muifufu Magugi asitupate na kutuua, tulikuwa tukijiuliza, sote tuliona kuwa mwisho wa maisha yetu ulikuwa umewadia.



Mara tukoana miili yetu ikinyanyuliwa juu na kuiacha aridhi, tukabaki tukielea hewani ingawa hakikuonekana kilichotunyanyua, kwa mbali tulisikia sauti za watu wakisogea eneo lile, tukakimbia na kujifucha kwenye vichaka lakini sauti uti za watu wale ziliendelea kutufuata kila upande ambao tulielekea, nikatoa yale mafuta aliyonipa Mnaro nikampaka mke wangu kisha nikajpaka mimi na kuwapa wengine wote wajipake, Mnaro linimbia mtu akipaka mafuta yale hawezi kuonwa hata na wachawi, labda mchawi mwenye uwezo mkubwa sana, hivyo niliamua kujaribu na nadhani tulifanikiwa maana watu wale walipita kwa kasi wakituvuka palepale tulipokuwa na hawakuonekana kutuona, tukaendela kuulizana nini kifanyike baada ya kuwa lile limetukosa. Ghafla tukaona miili yetu ikinyanyuliwa juu na kuiacha aridhi, tukawa tunaelea hewani kama vile hatukuwa na uzito wowote, kwa mbali ikasikika cheko kubwa ikisogea tulipo, na ilisikika kama cheko ya mwanamke, miili yetu ikiendelea kuelea hewani ilitolewa kwenye kichaka tulichokuwa tumejificha na kwenda kusimama mbele ya mwanamke mrefu sana aliyekuwa na nywele ndefu mpaka zinaburuza chini, mwanamke yule alionekana mrembo lakini hakuwa na mcho, hakuwa hata na mashimo ya mcho. Mwanamke huyu alikuwa akiifanya miili yetu atakavyo kwa mikono yake, aliweza kutupeleka juu, chini mbele, nyuma na hata pembeni bila kutugusa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom