Simulizi: Mke wangu

mastory

Member
Dec 5, 2018
18
10
SIMULIZI;MKE WANGU.
MTUNZI;RAJA SAIDY.
WHATSAPP;0756920739.
SMS;0621047821.

SEHEMU YA KWANZA ( 1 )

Utangulizi.

Familia nyingi huaribika kutokana na sababu tofauti tofauti,ukweli na ufafanuzi wa jambo ili ni yakuwa mwanamke ndio mtu wa kwanza kuvunja mahusiano katika ndoa.

Wanaume huwa ni watu wenye upendo wa kweli na huwa makini na wanachokifanya hasa pale wanapoingia katika swala zima la ndoa.Bado haijajulikana tamati ya jambo ili,ila imani ipo yakuwa ipo siku wanaume ndio watakuwa wa kwanza kuvunja mahusiano katika ndoa na sio wanawake tena.

Huenda ikapunguza kuvunjika kwa ndoa nyingi,wazazi wanakazi kubwa ya kuwapa mafunzo wanawe ili wasije kuharibu na kuwatia aibu kubwa pale wapoolewa au kuowa.

Soma kisa hiki upate kujua nayozungumza yana maanisha nini.

Anza nayo

Mvua kali iliendelea kunyesha na kuwafanya watu wengi wanaotoka maofisini na kwenye miangaiko yao,kushindwa kurudi majumbani kwao na kuamua kujikinga katika makazi yao ya wanapofanyia biashara.

"Bosi hii mvua itaisha leo kweli!!"

"Anna sina cha kufanya itanibidi niisubirie,we si unaona kabisa gari lipo mbali na hapa unataka ninyeshewe."

"Kweli Bosi itakubidi huisubirie tu."

"Sawa Anna."

Francis aliendelea kusubiri mvua hiyo iliokuwa haitabiriki itaisha muda gani ili arudi nyumbani kwake.

"Daah hii baridi yote ukizingatia sina mke,ila leo mpaka nijaribu kwenda katika baa maarufu iliyopo eneo la Sanene, Segerea katika maegesho ya magari.Ili namimi nipate angalau wa kunitoa baridi hii."

Mvua kidogo ilianza kukata na kumfanya Francis kumuamuru mfanyakazi wake ili apate kufunga ofisi na yeye apate kwenda mahali anapotakiwa kwenda.

"Bosi funguo hizi hapa???"

Anna alizungumza huku akiendelea kupiga hatua za kuelekea mahali Francis alipo kwa lengo la kumkabidhi funguo huku Francis akiwa tayari ameshaingia ndani ya gari.

Safari yake ilikuwa ya kwenda kutafuta kahaba wa kulala naye.Hatimaye alifika mpaka mahali wanapopatikana makahaba hao.

Francis alipaki gari na kuwasha taa za gari hilo,ili kuwafanya makahaba kusogea mahali alipo.

"Kaka mimi hata Elfu mbili tunaenda."

"Kaka cheki shepu langu lilivyozuri bila hata kinga nakuruhusu bei yoyote utakayo."

"Jamani nipisheni huyu ni mteja wangu wa kila siku."

Mdada mmoja mwenye umri kati ya miaka 18,hadi ishirini alikuwa akizungumza huku akiendelea kuwasihi wenzake wampishe apate kuingia ndani ya gari la Francis.Kilichofanya dada hyo,kusema maneno hayo ilikuwa kama njia ya kuwafanya wenzake wampishe tu na wala maneno aliyozungumza yalikuwa hayana ukweli wowote ule.

Francis alimruhusu dada huyo, aingie ndani ya gari kisha akaanza kuendesha gari huku akiendelea kuzungumza na dada huyo.

"Unaitwa nani tafadhali???."

"Mary."

Dada huyo alikuwa akizungumza huku akiendelea kuchomoa paketi la sigara lililokuwa ndani ya pochi yake kisha akachomoa sigara moja na kulirudisha paketi hilo.

"Una kiberiti???"

Dada huyo alijulikanaye kwa jina la Mary,alizungumza huku akiendelea kutafuta kitu ndani ya pochi yake.

"Hapana sina."

Francis alimjibu na kumfanya Mary aongeze kasi ya kutafuta kiberiti chake.

"Waooh,nimekipata.."

"Mary unavuta sigara???."

"Yaa,unatumia na wewe nikuchomolee moja."

"Hapana."

"Mary mi nataka nikuoe na nikutoe mahali pale,msichana mzuri kama wewe unakaa mahali kama pale,unajizaririsha.."

"Kwa sasa sihitaji kuolewa,kwanza subiri usinitibue,shingapi utanipa tukienda kufanya mapenzi huenda hata ukawa hauna hela ya kunipa."

"Kwani wewe unataka nikulipe shingapi???."

"Mimi huwa ni Elfu kumi,sipunguzi na siongezi na kama hauna hiyo hela tafadhali naomba unirudishe uliponitoa."

Mary alizungumza huku akizidi kumkazia macho Francis.

"Mary mimi nitakupa laki moja ila naomba ukubali kuolewa na mimi."

Mary hakuamini kusikia hela kama hiyo inatajwa mbele yake ,maana ilikuwa hela kubwa na hakuwahi kuishika katika maisha yake.

"Waoooh kaka yangu,nashukuru sana na nitakupa raha kama zote..hahahahaha jamani siamini mimi,mashosti wangu watafrahije lazima tule bata."

Francis alimsikitikia sana Mary,alitamani kusikia hiyo laki atakayompa labda Mary atasema kuhusu swala zima la kununua kitu cha maana kitakachomuwezeha Mary kimaendeleo zaidi lakini ilikuwa sivyo.

"Mary nataka nikupe mtaji wa biashara na uachane na hiyo biashara ya ukahaba."

"Siwezi,hata kidogo."

Mary alizungumza huku akiendelea kuchomoa sigari nyingine ndani ya paketi kisha akarudisha paketi ndani ya pochi yake.

Francis alishindwa ni kitu gani atafanya ili Mary amuelewe na abadilike awe kama wanawake wengine wasiojiusisha na chochote kile kinachohusiana na ukahaba lakini alishindwa.

Francis alifika mahali anapoishi kisha akafungua geti na kuingia na gari lake hadi uwani mwa nyumba hiyo.

"Shuka Mary."

Mary alishuka ndani ya gari kisha akachomoa sigara nyingine na kutupa kipisi cha sigara alichokuwa anamalizia kukivuta.

Nyumba ya Francis ilikuwa kubwa na nzuri pia ilikuwa tulivu,Mary na Francis waliingia mpaka ndani ya nyumba hiyo.

Walieleka hadi chumbani yote sababu Mary alitaka afanye mapenzi na Francis kwa haraka kisha arudi kutafuta mteja mwingine.

Mary alianza kuvua nguo zake haraka haraka kisha akaamvua na Francis ili waanze kazi,Mary alikuwa mzoefu hivyo alichukua karoti ya Francis kisha akajiwekea kwenye ikulu yake,Mary alifanya kila kitu kinachozidisha mahaba ili Francis awahi kuchoka kisha amlipe na yeye aondoke.

"Umelidhika???"

Mary alimuuliza Francis baada ya kuwa amefanya naye mapenzi kwa muda mrefu.

"Ndio.."

Francis alijibu huku akionekana kuchoka sana.

"Naomba hela yangu niondoke.!!"

"Jamani Mary si nimekwambia nataka nikuoe."

"Hehehehe,Eti unioe.Wewe koma unauwezo wa kuwa unanipa kila siku laki mbili???"

"Ndio.."

"Kama hivyo sawa,nitakaa hapa kwako kila siku utakuwa unanipa hela hiyo ila usiponipa hata siku moja,hutaniona tena katika maisha yako."

Itaendelea.........
#Maoni yako ni muhimu,usisahau kushare.

#Ukitaka muendelezo wake,unaweza kuupata kwa ada ya shilingi 1,500 tu njoo whatsapp namba 0756920739 au sms namba 0621047841 nikutumie chapu.
1544428823573.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom