Sehemu ya 107.
“Hapana! Nipo singo now! Nyie wanaume wabaya sana ndiyo maana sitaki kuwaamini tena,” alisema Amanda.
“Ila naomba uniamini!”
“Sawa haina shida. Ila kwa nini umeniuliza hivyo?”
“Ninahitaji kufahamu kabisa kama kuna mtu, haimaanishi nitakwambia uachane naye, hapana, sitokwambia ila nitatakiwa kujua kuna mtu mwingine hivyo nina kila sababu ya kumuonyesha mtu huyo nampenda mpaka niuteke moyo wake kwa asilimia mia moja kabisa na huyo mwingine atoke moyoni mwake,” alisema John.
“Mh!”
“Ndiyo hivyo! Kila mwanamke mzuri unayemuona ana mwanaume, hivyo tunapofanikiwa kumpata mwanamke wa mtu basi tumpende kwa dhati, tumuonyeshe mapenzi makubwa, yule mwingine ataachwa tu,” alisema John.
“Kumbe!”
“Ndiyo! Kama mtu kwenye uhusiano wake kila siku anapigwa, anadharauliwa, ananyanyaswa na kufanyiwa mambo ya kishenzi halafu wewe ukaingia na kumuonyesha mapenzi ya dhati, ukamjali, kumsikiliza na mambo mengine, kwa nini usiuteke moyo wake? Ni rahisi Amanda,” alisema John. “Nimekuelewa!”
“Na kitu gani hupendi kufanyiwa na mpenzi wako?” aliuliza.
“Mengi! Zaidi kusalitiwa!”
“Sawa! Sitokusaliti!”
“Na wewe?”
“Sipendi kudanganywa! Ujinga wote unaanzia kwenye uongo. Mtu anapotaka kusaliti ni lazima aanze kudanganya, ajifanye anapenda sana kumbe nyuma ya pazia kuna kitu kingine. Uongo ndiyo dhambi ya kwanza duniani, si unalijua hilo?” alisema John na kuuliza.
“Ndiyo!”
“Basi ndiyo maana uongo ninauchukia sana. Inawezekana kama yule nyoka asingemdanganya Hawa pale bustanini na kuwafanya wale tunda, leo hii tungekuwa tunakula bata tu,” alisema John na kuanza kucheka.
“Yaani wewe!”
“Amanda mpenzi! Naomba usinidanganye, hata kama kitu kitaniumiza sana, naomba usinidanganye kwa sababu nikiujua ukweli baadaye na wakati umenidanganya, nitaumia sana,” alisema John.
“Usijali! Sitokudanganya!”
“Una uhakika?”
“Ndiyo mpenzi!”
|
|
Je, nini kitaendelea?