Simulizi: Mke Wangu Juliana

Simulizi: Mke Wangu Juliana

SEHEMU YA 55

“Kwa hiyo akaja kwako?” aliuliza mchungaji.
“Ndiyo!”
“Unaye?”

“Ndiyo! Nilimwambia arudi nyumbani lakini alikataa katakata!” alisema John.
Polisi waliagizwa kwa ajili ya kumchukua mwanaume huyo na kuondoka naye hivyo hicho ndicho walichokifanya, wakamfunga pingu na kuondoka mahali hapo.

Hakuwa na hofu, alipofikishwa huko, macho yake yakatua kwa wazazi wa Deborah ambao walionekana kuwa na hasira naye, hakujali, akachukuliwa na kuingizwa selo.

“Huyu muacheni akae humo hata siku tatu ili ashike adabu. Bila shaka Deborah atakuwa nyumbani kwake, naomba twende huko,” alisema baba yake Deborah.
“Unapafahamu anapoishi?”
“Sipafahamu ila kuna mshirika mmoja anaweza kutupeleka,” alisema mzee Abraham.

“Basi tumfuate huyo mshirika kanisani atupeleke kumchukua binti yako,” alisema polisi, hapohapo wakaingia ndani ya gari na kuanza kwenda kanisani kwa lengo la kumchukua mtu na kumpeleka nyumbani kwa John.
|
|

Je, nini kitaendelea?

Tukutane tena week ijayo jumatano au alhamisi.....
 
SEHEMU YA 55

“Kwa hiyo akaja kwako?” aliuliza mchungaji.
“Ndiyo!”
“Unaye?”

“Ndiyo! Nilimwambia arudi nyumbani lakini alikataa katakata!” alisema John.
Polisi waliagizwa kwa ajili ya kumchukua mwanaume huyo na kuondoka naye hivyo hicho ndicho walichokifanya, wakamfunga pingu na kuondoka mahali hapo.

Hakuwa na hofu, alipofikishwa huko, macho yake yakatua kwa wazazi wa Deborah ambao walionekana kuwa na hasira naye, hakujali, akachukuliwa na kuingizwa selo.

“Huyu muacheni akae humo hata siku tatu ili ashike adabu. Bila shaka Deborah atakuwa nyumbani kwake, naomba twende huko,” alisema baba yake Deborah.
“Unapafahamu anapoishi?”
“Sipafahamu ila kuna mshirika mmoja anaweza kutupeleka,” alisema mzee Abraham.

“Basi tumfuate huyo mshirika kanisani atupeleke kumchukua binti yako,” alisema polisi, hapohapo wakaingia ndani ya gari na kuanza kwenda kanisani kwa lengo la kumchukua mtu na kumpeleka nyumbani kwa John.
|
|

Je, nini kitaendelea?

Tukutane tena week ijayo jumatano au alhamisi.....
Nipo kuisubiri alhamisi nione kitakachoendelea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA 56

Polisi walifika kanisani ambapo wakamtaka mchungaji amteue kijana mmoja kwa lengo la kuwapeleka nyumbani kwa John. Hilo halikuwa tatizo, kijana mmoja akachukuliwa, akaingizwa ndani ya gari.

“Na mimi nataka kwenda!” alisema msichana mmoja, alikuwa amesimama mbele ya polisi, alikuwa Juliana.
“Wewe ni nani?” aliuliza polisi mmoja.
“Juliana!”

“Unataka kwenda kufanya nini?”
“Kumuona John!”
“Yupo kituo cha polisi cha Mwanga, nenda huko. Dereva washa gari tuondoke!” alisema polisi huyo, gari likawashwa na kuondoka mahali hapo.

Kijana yule alikuwa akiwaelekeza polisi njia mpaka walipofika nyumbani kwa John, wakaingia ndani ambapo huko wakamkuta Deborah akiwa kwenye godoro akilia, moyo wake ulikuwa na majonzi mazito.

Hawakutaka kuchelewa, haraka sana wakamchukua msichana huyo na kuanza kumtoa nje. Deborah alikuwa akilia, aliwaambia hakutaka kuondoka hapo kwani alijisikia amani na furaha kuwa humo kuliko nyumbani kwao.

Wazazi wake waliwaambia polisi ni lazima wamtoe kwani hakutakiwa kubaki humo, kazi ikafanyika na msichana huyo kutolewa haraka sana, akapakizwa ndani ya gari na kuanza kupelekwa nyumbani.

Njia nzima alikuwa akilia, hakuamini kama wazazi wake ndiyo walikuwa wakimfanyia hayo yote, aliwapenda, aliamini wangekuwa naye bega kwa bega kwa maamuzi aliyochukua lakini kitu cha ajabu kabisa, walibadilika, hawakutaka kabisa kumuona akiwa na John.

Walipofika nyumbani, akaingizwa ndani na kuambiwa atulie humo. Hakuwa na la kufanya, akakaa kitandani na kuendelea kulia kama kawaida.

Alikuwa binti mkubwa lakini wazazi wake walivyokuwa wakimchunga ni kama alikuwa msichana mdogo wa sekondari.

“Na yule kijana vipi?” aliuliza polisi.
“Muacheni akae! Nitawasiliana na bosi wake afukuzwe kazi! Manake nahisi ile kazi ndiyo inamtia kiburi!” alisema baba yake Deborah.

Polisi wakaondoka nyumbani hapo, mzee Abraham akachukua simu yake na kumpigia Bwana Masako, bosi wa kampuni ya samaki aliyokuwa akifanya Deborah. Simu iliita na baada ya sekunde chache, ikapokelewa.
“Kuna kitu nataka unisaidie,” alisema mzee Abraham baada ya salamu.
 
SEHEMU YA 57

“Kitu gani?”
“Ninahitaji sana umfukuze kazi kijana anayeitwa John!” alisema.
“John gani?”

“Yule mfanya usafi, ananiharibia binti yangu na ninajua kazi ndiyo inamtia kiburi,” alisema mzee huyo.

“Mh! Ishu ya kuajiri ipo chini yangu ila ya kufukuza mpaka niwasiliane na uongozi wa juu kabisa jijini Dar es Salaam,” alisema Bwana Masako.

“Mh!”
“Ndiyo! Kampuni ilinunuliwa na bosi mwingine miezi saba iliyopita kutoka huko, hivyo ameweka utaratibu wake, labda nitumie ubabe mzee mwenzangu!” alisema Bwana Masako.

“Basi sawa. Tumia ubabe!” “Haina shida.”
Mzee Abraham akakenua, aliyaona mafanikio makubwa, John alitoka jijini Dar es Salaam kwenda Kigoma kwa lengo la kutafuta maisha, akayapata lakini kwa bahati mbaya amri ilitolewa kwamba ni lazima afukuzwe kazi.

Muda huo wakati mazungumzo hayo yalipokuwa yakifanyika, kijana huyo alikuwa selo, moyo wake uliuma kupita kawaida, hakuamini kama yeye ndiye aliyekuwa akipitia maisha hayo kwa sababu tu hakuwa masikini.

Alihuzunika lakini hakujilaumu, kile alichokuwa amekifanya kilionekana kuwa sahihi kwake. Alionyesha upendo wa dhati kwa msichana aliyekuwa akimpenda, alikuwa tayari kufanya lolote kwa ajili ya Deborah na ndiyo maana hakuwahi kujilaumu hata kidogo.

Akiwa humo, majira ya saa kumi jioni akaambiwa kulikuwa na wageni waliokuja kumuona, akatolewa, alipofika kaunta, macho yake yakatua kwa washirika kadhaa akiwemo Juliana ambaye alimpelekea chakula.

Kila mmoja alionekana kuwa na huzuni, hapakuwa na mtu aliyeamini kile kilichokuwa kikiendelea. Alitia huruma, macho yake yalionekana kuwa mekundu hali iliyoonyesha alilia sana humo ndani.

Akazungumza nao, kila alipomwangalia Juliana, alikumbuka, alihisi tangu zamani kwamba msichana huyo alikuwa akimpenda, kwa jicho lile, aliamini kabisa alikuwa sahihi kwa asilimia mia moja.

Wakazungumza naye na baadaye kuondoka huku akibaki Juliana tu ambaye hakutaka kumficha kitu chochote kile, kwa sababu ya maisha aliyokuwa akipitia, aliamini yeye ndiye angekuwa tumaini lake.
“Ninakupenda John!” alisema msichana huyo.
“Najua sana!”
 
SEHEMU YA 58

“Ninahitaji unioe, tujenge familia pamoja. Nitakupenda maisha yangu yote!” alisema Juliana huku akimwangalia John.

“Hapana! Sijamalizana na Deborah! Bado ninampenda msichana yule!” alisema.
“Ila wazazi wake hawataki uwe naye!”
“Ila si yeye! Sijamalizana na Deborah!” alisema John.

Wakati wakiendelea kuongea, polisi wakamtaka Juliana kuondoka mahali hapo kwani muda ulikwisha, akatii na kuondoka zake.

Siku hiyo alilala selo. Moyo wake uliendelea kuwa na uchungu kwa yale aliyokuwa akipitia. Aliamini hapakuwa na jambo baya alilokuwa amelifanya kwa sababu kumpenda mwanamke ilikuwa moja maisha aliyokuwa akipitia kila mtu.

Asubuhi na maema Juliana alifika kituoni hapo akiwa na kapu lililokuwa na chai na vitafunio, akaitaji kuonana naye na kumpa vitu hivyo.

John akashukuru na kuanza kunywa. Mtu huyo ndiye ambaye alimuonyesha thamani ya kumpenda, ndiye ambaye alikubali kuwa naye bega kwa bega hata kwa hali aliyokuwa akipitia.

Deborah hakutokea hapo kituoni, alichungwa, hakutakiwa kuendesha gari kwenda ofisini, mama yake alimsindikiza huku akibaki hukohuko kuhakikisha hatoki hapo kwenda kumuona John kituoni.

Barua ya kufukuzwa kazi ikaandikwa haraka haraka na ilipofika majira ya saa sita, akapelekewa hukohuko kituoni, akaambiwa hakutakiwa kuonekana ofisini, yaani kwa sababu alipelekwa polisi basi nayo kazi ilikuwa basi.

Aliumia moyoni mwake, hakutegemea mwanzo wa mambo hayo yangefika huko. Alilia sana, alimuomba Mungu wake amsaidie kwani hakuona njia nyingine ya kufanya, kitendo cha kukosa ile kazi kilimaanisha angerudi tena mtaani na kuuza samaki.

Mzee Abraham alifanya yote kwa kuwa alitaka kumkomesha John. Alikuwa na pesa, aliheshimika hivyo alihitaji John akae huko wiki nzima ili ajifunze.

Mchungaji wake alikuwa akifika mara kwa mara kuomba kijana wake atolewe lakini hakutolewa, yaani kila kitu kilifanyika kwa kuwa mzee Abraham alitaka iwe hivyo.
Wiki ilipokatika, ndipo akaruhusiwa kutolewa kwa masharti kwamba hakutakiwa kuonana na Deborah wala kuwasiliana naye vinginevyo angerudishwa tena.

“Ila ninampenda!” alimwambia polisi.
“Kijana tutakurudisha ndani!”
“Basi samahani! Nashukuru sana,” alisema.
 
SEHEMU YA 59

Akachukuliwa na Juliana na kusindikizwa nyumbani kwake. Njiani walikuwa wakiongea mengi lakini akili ya John haikuwa kwa msichana huyo hata kidogo, alikuwa akimkumbuka Deborah wake aliyekuwa akimpenda kupita kawaida.

Walipofika nyumbani, akapokewa na baba mwenye nyumba ambaye alimpa pole kwa mkasa mzima uliokuwa umetokea kwani ulimgusa kila mtu.

“Ni maisha tunayopitia! Ninashukuru sana!” alisema John huku akimwangalia mzee huyo.
Wakaingia ndani na Juliana, wakakaa na kuanza kuzungumza mambo mengi. Muda wote msichana huyo alionekana kuwa na furaha tele, hakuamini kama alikuwa na John chumbani humo.

Hakunyamaza, suala lake la kumpenda na kumuhitaji alimwambia kila wakati lakini msimamo wa mwanaume huyo ulibaki vilevile kwamba hakuhitaji kuwa naye kwa kuwa hakuwa amemalizana na Deborah.

Siku hiyo ndiyo ilikuwa mwisho wa kila kitu kwa John, hakuweza kumuona Deborah, alipokwenda nyumbani kwao, hakuruhusiwa kuonana naye, ofisini alikimbizwa na kuambiwa hakutakiwa kuonekana hapo vinginevyo angerudishwa polisi.

Alilia sana na kuumia, hakuwa na simu, yake aliyokuwanayo waliichukua polisi na kuivunjavunja, laini wakaitupa kabisa.

Hakuwa na pa kushtaki, watu ambao ndiyo alizoea kusikia walikuwa watetezi wa wanyonge ndiyo walikuwa wakifanya hayo.
Kukaa bila Deborah yalikuwa maisha ya mateso ambayo hakuwahi kuyasikia kabisa.

Familia yake haikuja tena kanisa, moyo wake ulivurugika, alichanganyikiwa kupita kawaida.
Mtu pekee ambaye kwa kipindi hicho alikuwa akimpa furaha alikuwa mmoja tu, Juliana ambaye alijitoa kwa asilimia mia moja katika maisha yake.

Huyo ndiye alikuwa tegemeo lake, hakuwa tajiri, alikuwa masikini kama yeye lakini alikuwa radhi kuwa naye, hakumpenda kwa kuwa alitoka Dar es Salaam, alimpenda kwa kuwa moyo wake ulimwambia alikuwa mwanaume sahihi wa kuwa naye kipindi hicho.

John akairudia kazi yake ya samaki, aliamua kuweka nguvu zake huko, hakutaka tena kuajiriwa kwa kuwa tayari aliamini hapakuwa na mpango kwani chuki za mtu mmoja zinaweza kukufanya kupoteza ajira, akaona ni bora kujiajiri.
 
SEHEMU YA 60

Kwa muda wa miezi mitatu mfululizo picha ya Deborah haikutoka kichwani mwake, iliganda ubongoni mwake, ilimtesa kwa kipindi kirefu mno.

Juliana alijitahidi kuonyesha kila aina ya mapenzi kwa John, alijua kabisa moyo wake ulikuwa kwa mwanamke mwingine na si yeye hivyo alitakiwa kufanya kila liwezekanalo kuhakikisha anaupata moyo wa mwanaume huyo.
“Au kwa sababu sijafanya naye mapenzi?” alijiuliza.

Huo ndiyo ulikuwa mpango mwingine alioupanga kuufanya.
Aliamini alishindwa kuuteka moyo wa John kwa kuwa nafsi zao hazikuwa zimeunganishwa kupitia ngono, hivyo akajipanga, katika siku ambayo hakuwa na hatari ya kupata mimba akaenda nyumbani kwake.

Walikaa na kupiga stori kama kawaida, siku hiyo alikuwa na mipango yake, alianza kumshikashika John hapa na pale, alijilainisha kwake, mwisho kabisa akavua blauzi yake, kifua kilikuwa kimesimama.

John alipoangalia, akashtuka, hakuamini kile alichokiona, ni kweli alimpenda mno Deborah lakini macho yake kwa wakati huyo yaliona kitu ambacho kilimfanya kumuondoa Deborah kwa muda.

Juliana akamsogelea pale kitandani, akaanza kumfanyia utundu, John akachanganyikiwa, akajikuta akivuliwa nguo zake na hakubisha hata kidogo.

“Sijawahi kulala na mwanaume!” alisema Juliana maneno ambayo yalimshtua John.
“Unasemaje?” aliuliza John huku akionekana kutokuamini, msichana mkubwa kama Juliana bikira.

“Ndiyo hivyo! Kwa hivyo iwe taratibu. Umesikia baba watoto?” aliuliza Juliana huku akiachia tabasamu.
“Hakuna shida!”
Wakakubaliana na hatimaye kuanza kazi. Ni sauti za mahaba ndizo zilizokuwa zikisikika chumbani humo.

Kwa wasiojua, ngono kilikuwa kitendo kinachofanyika kwa mwili na kwa roho, kuna mahusiano makubwa mno baina ya roho mbili zinapokutana na hatimaye mwili kufanya mapenzi.

Na ndiyo maana wakati mwingine unaweza kufanya mapenzi na mtu fulani, maisha yako yakakunyookea mno mpaka ukawa unashangaa lakini kuna wakati mwingine unaweza kufanya mapenzi na mtu mwingine ukaona unaanza kuingia kwenye misukosuko, pesa inakatika, yaani kila kitu kinakuwa shaghalabaghala.
 
SEHEMU YA 61

Kitendo cha kumvulia nguo zake John ni kama kilibadilisha kila kitu, kichwa chake kikakaa sawa, akahisi akianza kumsahau Deborah.
Huyo Juliana akaanza kuingia kichwani mwake kwa kasi ya ajabu, kitendo cha kutukuona Deborah kwa miezi mitatu tu kilimfanya kuwa na nguvu zaidi ya kumsahai msichana huyo.

John akaanza kurudi katika hali yake ya kawaida, kila siku asubuhi alikuwa akiondoka nyumbani kwake na Jumanne kwenda kununua samaki na kwenda kuwauza kama kawaida yao.

Alifanikiwa kwa kiasi kidogo, pesa alizokuwa akizipata akazihifadhi kwani alijua kwa jinsi hali ilivyokuwa ikienda, kuna siku alihitaji kuoa na kuanza kuishi na mwanamke, hivyo ilikuwa ni lazima aweke akiba ya pesa.

Uhusiano wake na Juliana ulikua kwa kasi sana, watu walifurahi, hapakuwa na mtu aliyeumia kwa kuwa tu John maisha yake yalikuwa ni ya kimasikini, hata wanawake wengine walimuona Juliana akipotea kwa kumchukua mwanaume ambaye hakuwa na kitu.

Baada ya miezi nane tangu wakiwa pamoja, hatimaye wakakubaliana kutangaza uchumba kanisa, hilo likafanyika, wakavalishana pete na hatimaye kuingia kwenye hatua ya uchumba.

Ilikuwa ni furaha ya kila mmoja. Walizidi kupendana, wakapanga mwezi wa kuoana na kuwa mume na mke, hivyo mwezi huo wa sita, wakasubiri mpaka mwezi wa tisa ndipo harusi ifanyike na hatimaye kuishi pamoja.
“Ninakupenda mchumba wangu!” alisema John huku akimwangalia Juliana.
“Ninakupenda pia!” alisema Juliana, hapohapo wakabusiana, kila mmoja alimpenda mwenzake kupita kawaida.

|
|

Je, nini kitaendelea?

Tukutane tena week ijayo siku kama ya leo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom