moneytalk
JF-Expert Member
- Jan 23, 2017
- 8,040
- 16,870
Ahsante Smart
Kwa kweli hii ni ngoja tuone, yan natamani nione kilitokea nini mpaka John akaamua kwenda Kigoma afu akaenda kama mtu wa hali ya chini
Kibonge mwenzangu Yani hapa ulishanitoa madongo poromoka na kunipeleka posta kuanza kumfuatilia John kwa nyumaSehemu ya 98
“Si meza nzima tena?”
“Ukitaka napo hakuna shida!”
“Sawa. Nahitaji viwili nikasome!”
“Unahitaji kipi na kipi?”
“Dili la Dola Bilioni Nne na Damu ya Mwanamwali Kitandani,” alijibu msichana huyo.
“Hakuna shida.”
Akamsogelea muuzaji, mzee fulani wa makamo na kumpa kiasi cha pesa kilichohitaji na kisha kuendelea na safari, muda huu wakawa wanaongozana na kuongea pamoja.
Kila mmoja alionekana kuwa na furaha isiyo kifani, John alijisikia fahari mno, hakuamini kama hatmaye alikuwa akitembea na msichana mzuri kama Amanda.
“Naomba nichafue kitabu chako kimoja,” alisema John huku akimuomba kitabu, akapewa, akatoa kalamu yake na kuandika namba yake ya simuu.
“Naomba unitafute ukipata nafasi!” alisema huku akimrudishia.
“Sawa! Nikipata nafasi! Ahsante kwa vitabu!” alisema Amanda huku akitoa tabasamu.
“Usijali!” alisema John.
Akageuza na kuendelea na safari yake. Yaani msichana mrembo aliisitsha safari hiyo kwa muda. Ni kawaida ya wanaume wote duniani hasa wanapokutana na wanawake wazuri.
John alikutana na marafiki zake na kuanza kuongea kuhusu zawadi ambayo walitakiwa kwenda kumpa Cosmas katika sherehe yake ya ndoa ambayo alitarajiwa kufunga na mchumba wake mrembo.
Kwa kuwa alipenda sana kucheza game, wakapanga kumwandalia zawadi ya Play Station 4 itakayomfanya kuwa bize katika kipindi cha wikiendi, aache kwenda kuzurura kama kawaida yake.
Wakati wakizungumza hayo yote kichwa cha John kilikuwa na mawazo tele, alikuwa akimfikiria msichana aliyekutana naye muda mfupi uliopita. Alimwachia namna yake ya simu lakini hakuwa na uhakika kama angeweza kumpigia ama angemsubirisha kwa siku kadhaa.
Kila wakati alikuwa akiiangalia simu yake, moyo wake ulikuwa na presha kubwa, alipoisikia ikiita, haraka sana akaichukua na kuangalia kioo, alipokuta aliyekuwa akipiga si Amanda, uso wake ulikuwa na hasira mno.
Nipo kusubiri muendelezo.Sehemu ya 99
Baada ya kumaliza kikao hicho kifupi, akarudi ofisini kwake ambapo akachukua gari lake na kurudi nyumbani. Mawazo hayakumtoka, yaliendelea kumvuruga kichwa chake kiasi cha kuona muda wowote ule angeweza kukonda hata kama alikuwa na pesa nyingi kiasi gani.
Ilipita siku ya kwanza, ikawa kimya, ikapita ya pili, ya tatu mpaka ya nne ndipo akapokea ujumbe kutoka kwa msichana huyo, haraka sana hakutaka kusubiri, akampigia na kuanza kuzungumza naye.
“Amanda...” aliita huku uso wake ukiwa na tabasamu.
“Niambie John!” alisema msichana huyo.
“I’ve missed you a lot,” (nimekukumbuka sana) alimwambia kwa sauti laini kabisa, ile ya kubembeleza.
“I’ve missed you too!” (nimekukumbuka pia)
“Why didn’t you check on me?” (kwa nini hukunitafuta?) aliuliza.
“I’ve been busy the whole week! By the way! How are you doing?” (nimekuwa bize wiki nzima! Unaendeaje lakini?) alisema msichana huyo.
Wakaanza kupiga stori, moyo wa John ulikuwa na furaha tele, hakuamini kama msichana huyo angeweza kumpigia simu na kuzungumza naye.
Alikuwa na hamu ya kumuona, muda mwingi alikuwa akiiangalia namba ya msichana huyo, picha yake iliganda ubongoni mwake na haikutaka kutoka hata kidogo.
Akashindwa kuvumilia, akamuomba kuonana naye katika Hoteli ya Hyatt ambapo msichana huyo akakubaliana naye na siku hiyo wakaonana.
Ilikuwa ni kwa mara ya pili, alimwangalia jinsi alivyokuwa mzuri, alivyopendeza, kwake alionekana kuwa msichana mrembo kuliko wote ambao aliwahi kukutana nao.
Waliongea na kucheka, walifurahia kupita kawaida. Kwa kuwa msichana huyo alikuwa mchangamfu sana, hakutaka kuona akiondoka, akamuomba sana kama itawezekana basi siku hiyo wakae pamoja mpaka asubuhi.
“No!” (hapana) alisema Amanda.
“Kwa sababu gani?”
“Ninaishi na wazazi wangu! Itakuwaje nikilala nje ya nyumba yetu?” aliuliza.
John akanyamaza, kile alichokizungumza msichana huyo kilikuwa sahihi kabisa, kuamua kulala naye na wakati alikuwa chini ya wazazi wake haikuwa adabu hata kidogo.
|
|
Je, nini kitaendelea?
Kibonge mwenzangu Yani hapa ulishanitoa madongo poromoka na kunipeleka posta kuanza kumfuatilia John kwa nyuma
Sent using Jamii Forums mobile app




Endelea kumfatilia kibonge mwenzangu