Simulizi: Mkasa wa kweli | Aliyemuua Mchumba Wangu

Simulizi: Mkasa wa kweli | Aliyemuua Mchumba Wangu

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,746
Reaction score
25,672
James Matei alimshuhudia waziwazi mchumba wake Maria Temba akipigwa risasi na kuuawa, kitendo ambacho kiliyakatisha matumaini yake ya kufunga ndoa na kuoana na msichana huyo aliyempenda kuliko kitu kingine chochote.
Muuaji alipokamatwa na polisi, James alithibitisha kwa uchungu mwingi mbele ya polisi kuwa mtu huyo ndiye aliyempiga risasi mchumba wake. Akawataka polisi wahakikishe kuwa sheria inafuata mkondo wake.

Muuaji alifikishwa mahakamani na Matei alitakiwa kwenda mahakamani kutoa ushahidi, ushahidi ambao polisi waliamini ungetosha kumtia hatiani muuaji huyo.
Lakini Matei aliposimama kizimbani aliushangaza upande wa mashitaka alipobadilika ghafla na kumtetea muuaji huyo aliyemshuhudia akimuua mchumba wake. Akaitaka mhakama imuachie huru.

Hata baada ya kukumbushwa kuwa yeye ndiye aliyemthibitisha kituo cha polisi kuwa alimpiga risasi Maria na kusababisha kifo chake, James alikana maelezo yake na kusisitiza kuwa hakuwa akimtambua.

Mahakama ilipomuachia huru, James alimkumbatia muuaji huyo na kuishukuru mahakama kuwa imetenda haki.

Je imekuwaje Matei akabadilika ghafla?







ALIYEMUUA MCHUMBA WANGU


Kujuana kwao kulitokea kama bahati nasibu. Siku hiyo James Matei alikuwa katika matembezi yake ya kawaida akiwa kwenye gari lake aina ya Rav 4. Alikuwa akipita katika katika mitaa ya Kinondoni akitokea kwenye saluni moja alikokwenda kupunguzwa nywele.

Ilikuwa majira ya saa kumi na moja jioni. Hali ya hewa ilikuwa imebadilika tangu saa tisa. Wingu zito lilikuwa limetanda hewani na kusababisha mwanga wa jua kutoweka na kuwa na kila dalili ya kunyesha mvua.

Akiwa kwenye barabara ya Mwanamboka James alimuona msichana aliyekuwa amesimama peke yake kwenye kituo cha daladala. Wakati anakikaribia kituo hicho mvua ikaanguka ghafla. Yule msichana alianza kutota.

Kwa sababu tu za kibinaadamu James alipunguza mwendo akalisimamamisha gari karibu na kituo hicho. Alishusha kioo akamtazama yule msichana.

“Twende” alimwambia.

Msichana aliyekuwa amejikunja alikimbilia kwenye gari hilo akafungua mlango wa nyuma na kujipakia.
“Pole sana” James alimwambia msichana huyo mwembamba na mrefu wa wastani.

“Asante kaka” Msichana alimjibu huku akijifuta maji kwenye uso wake.

“Najua ulikuwa unasubiri daladala, unakwenda wapi?”

“Siendi tena, naomba msaada wako unirudishe nyumbani”

“Nyumbani ni wapi?”

“Twende mbele kidogo”

James alitia gea ya kwanza na kuiondoa gari.

“Mimi naitwa James, mwenzangu unaitwa nani?” James akamuuliza msichana huyo.

“Naitwa Maria”

“Bila shaka ni mwenyeji wa Arusha”

“Umejuaje?”

“Lafidhi yako ndiyo iliyonitambulisha”

“Mimi ni muarusha, wewe je?’

“Mimi ni mngoni lakini nilizaliwa Tanga”

“Nimefurahi kukufahamu”

“Na mimi nimefurahi kukufahamu. Unaishi hapa kinondoni?”

“Mtaa wa tatu tu utakuwa umenifikisha nyumbani”

Baada ya James kumfikisha katika mtaa huo, Maria alimuonesha nyumba aliyokuwa anaishi. Ilikuwa nyumba ya kota ya shirika la nyumba la taifa.

“Asante kaka yangu” Maria akamshukuru James wakati James alipolisimamisha gari mbele ya nyumba hiyo.

“Asante na wewe. Itabidi utote tena kidogo. Mlango wako uko mbali”

“Si kitu, umenisaidia sana”

Msichana alikuwa bado amesita kwenye siti kama vile kulikuwa na kitu akikisubiri kutoka kwa James. Pengine alidhani angeombwa namba ya simu au alihisi James angetaka wakutane siku nyingine ili ampe ahadi ya uongo.

Kama vile James alitambua mawazo yake, alimtazama na kutabasamu.

“Haya, jioni njema” akamwambia.

“Asante kaka”

Msichana akawa kama ameruhusiwa kutoka kwenye gari, akafungua mlango na kushuka. Aliufunga tena kisha akakimbia kuelekea kwenye mlango wa nyumba hiyo.

James akaliondoa gari na kuendelea na safari zake. Alivyoachana na msichana huyo alikuwa kama amemuondoa akilini mwake. Hakutarajia kama angekutana naye tena na hivyo mawazo yake yalikuwa kwenye mambo yake mengine.

Mvua ilikuwa ikiendelea kunyesha kwa nguvu na ndiyo iliyomfanya aamue kurudi nyumbani kwake mapema. Wakati anakaribia kufika nyumbani kwake Msasani akasikia simu ikiita katika siti ya nyuma.

Aligundua mapema kuwa haikuwa simu yake kutokana na kuwa na mlio tofauti. Kadhalika simu yake ilikuwa kwenye mfuko wake wa shati, haikuwa kwenye siti ya nyuma. Akashituka na kugeuza uso wake nyuma. Akaona simu iliyosahauliwa kwenye siti inaita. Akajiuliza ni simu ya nani?

Mara moja akapata jibu kuwa huenda msichana aliyempa lifti alikuwa amesahau simu yake. Aliegesha gari kando ya barabara kisha akaishika ile simu na kuitazama. Alijiuliza aipokee au aiache?

Kwa sababu ya kutaka kuwasiliana na mwenyewe aliona aipokee, akaipokea.

“Hallo!”

“Hallo…samahani kaka, nimesahau simu yangu” Sauti ya msichana iliyokuwa imejaa tashiwishi ilisikika kwenye simu.

“Wewe ni nani?” James akamuuliza.

“Mimi ni yule msichana uliyenipa lifti dakika chache zilizopita”

“Maria”

“Ndiyo Maria. Nashukuru kwa kunikumbuka”


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 02


ILIPOISHIA



Aligundua mapema kuwa haikuwa simu yake kutokana na kuwa na mlio tofauti. Kadhalika simu yake ilikuwa kwenye mfuko wake wa shati, haikuwa kwenye siti ya nyuma. Akashituka na kugeuza uso wake nyuma. Akaona simu iliyosahauliwa kwenye siti inaita. Akajiuliza ni simu ya nani?

Mara moja akapata jibu kuwa huenda msichana aliyempa lifti alikuwa amesahau simu yake. Aliegesha gari kando ya barabara kisha akaishika ile simu na kuitazama. Alijiuliza aipokee au aiache?

Kwa sababu ya kutaka kuwasiliana na mwenyewe aliona aipokee, akaipokea.

“Hallo!”

“Hallo…samahani kaka, nimesahau simu yangu” Sauti ya msichana iliyokuwa imejaa tashiwishi ilisikika kwenye simu.

“Wewe ni nani?” James akamuuliza.

“Mimi ni yule msichana uliyenipa lifti dakika chache zilizopita”

“Maria”

“Ndiyo Maria. Nashukuru kwa kunikumbuka”



SASA ENDELEA

“Sasa tufanyeje? Niko karibu kufika nyumbani kwangu”

“Nyumbani kwako ni wapi?”

“Msasani”

“Tafadhali kaka nakuomba unisaidie”

James alisita kidogo. Kurudi tena Kinondoni kulimpa uzito. Lakini baada ya kuwaza kidogo alimjibu.

“Nitakuletea”

“Utaniletea muda huu?”

“Ndio nageuza gari nirudi”

“Nashukuru sana kaka yangu”

Msichana akakata simu.

James akaweka gea ya nyuma kugeuza gari na kurudi. Alimkuta msichana amesimama barazani mwa nyumba yake akisubiri. Alipolisimamisha gari alishuka na kamfuata. Mvua ilikuwa ikimtosa. Msichana naye akaamua kumfuata. Wakakutana katikati. Wote wakawa wanatota.

James akamshika mkono msichana na kwenda naye barazani kwake.

“Ungenisubiri tu huku huku, unaona umetota bure” James akamwambia.

“Hapana. Wewe ndio ungenisubiri kwenye gari”

“Wakati nakuletea hii simu ungenisubiri tu. Kwanini utote?”

Msichana akatabasamu. James aliyaona meno yake meupe yaliyokuwa yamepangika vyema. Yalikuwa na mwanya mwembamba wa juu.

“Yaani utote wewe?” akamuuliza James.

“Atote mmoja, si sote” James akamjibu huku naye akitabasamu.

Maana hakuwa na la kusema. Aliendelea kutabasamu.

James alitoa simu yake na kumpa.

“Simu yako hii hapa”

“Asante sana kaka yangu. Katika dakika chache tu za kukufahamu wewe nimegundua kuwa wewe ni mtu mwema sana”

“Hata na wewe”

“Mungu akupe moyo huo huo”

“Asante sana”

“Hebu nisubiri”

Msichana aliingia ndani. Punde tu alitoka akiwa ameshika kitambaa kipya. Akampa James.

“Jifute maji usoni kwako”

“Asante”

James alikichukua kitambaa hicho akajifuta uso wake uliokuwa ukichirizika maji ya mvua.

Alipomaliza msichana alimwambia.

“Chukua namba yangu”

James akatoa simu yake.

“Ni ngapi?”

Msichana akamtajia.

James aliihifadhi kwenye simu yake kisha akampigia msichana. Simu ya msichana ikaita.
“Hii ndio namba yako” Msichana alimuuliza.

“Ndiyo hiyo”

“Asante. Sasa utasubiri mvua au utaenda zako?”

“Acha niende, mvua si tatizo kwa sababu nina gari. Kwa heri”

“Karibu sana kaka yangu”

James alitoka mbio kuelekea alikoliacha gari. Akafungua mlango na kujipakia. Wakati anaondoka msichana alimpungia mkono wa kumuaga na yeye akampungia.

Huo ulikuwa mwanzo wa James na Maria kujuana. Mawasiliano ya simu yakaanza taratibu. Siku James alimpigia Maria kumsalimia, siku nyingine Maria akampigia James.

Muda si mrefu wakawa marafiki. Hapo ndipo James alipoanza kumpenda Maria na alimueleza wazi kuwa alitaka awe mchumba wake.

“Mbona ninaye mchumba!” Maria akamwambia James.

“Unasema kweli?”

“Yesu Kristo…kwanini nikudanganye”

“Unajua nimekupenda sana”

“Ni sawa. Lakini hatukuandikiwa kuoana. Umechelewa”

“Una maana huyo mchumba ulikuwa naye tangu tunaanza kujuana?”

“Nilikuwa naye. Sema hukuwahi kuniuliza na mimi sikuwhi kukueleza”

“Ni vizuri. Mnatarajia kuoana lini”

“Karibuni tu”

“Maria sikuamini. Naona kama unanitania tu”

“Amini, siwezi kukutania”

James alikuja kugundua kuwa licha ya Maria kuwa na uhusiano na mtu mmoja ambaye hakumuelewa pia alikuwa na kesi ya jinai iliyokuwa inamkabili.

Alikuwa karani wa mhakama aliyekuwa amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma ya kupoteza kwa makusudi faili la kesi muhimu akiwa na lengo la kupoteza ushahidi.

Alikuwa nje kwa dhamana na kesi yake ilikuwa ikiendelea mahakamani.

Pamoja na kudai kuwa alikuwa na mchumba, Maria alianza kubadilika kidogo dogo na kuendeleza uhusiano wake na James. Ilifikia wakati ambapo James alimuuliza kuhusu mchumba aliyekuwa naye.

“Sina mchumba” Maria akamjibu.

“Si uliniambia una mchumba wako?’

“Nilikudanganya tu. Nilitaka kukupima nione kama utabadilika na pia nilitaka kukujua vizuri”

“Tangu mwanzo nilihisi kuwa unanidanganya”

“Unajua nini…nilitaka kukujua vizuri”

“Sasa umeshanijua vizuri”

“Sana”

“Ninafaa kuwa mchumba wako”

“Unafaa sana. Kawaone wazazi wangu. Kwa bahati njema wapo hapa Dar”



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 03


ILIPOISHIA



Alikuwa karani wa mhakama aliyekuwa amesimamishwa kazi kutokana na tuhuma ya kupoteza kwa makusudi faili la kesi muhimu akiwa na lengo la kupoteza ushahidi.

Alikuwa nje kwa dhamana na kesi yake ilikuwa ikiendelea mahakamani.

Pamoja na kudai kuwa alikuwa na mchumba, Maria alianza kubadilika kidogo dogo na kuendeleza uhusiano wake na James. Ilifikia wakati ambapo James alimuuliza kuhusu mchumba aliyekuwa naye.

“Sina mchumba” Maria akamjibu.

“Si uliniambia una mchumba wako?’

“Nilikudanganya tu. Nilitaka kukupima nione kama utabadilika na pia nilitaka kukujua vizuri”

“Tangu mwanzo nilihisi kuwa unanidanganya”

“Unajua nini…nilitaka kukujua vizuri”

“Sasa umeshanijua vizuri”

“Sana”

“Ninafaa kuwa mchumba wako”

“Unafaa sana. Kawaone wazazi wangu. Kwa bahati njema wapo hapa Dar”



SASA ENDELEA



Kwa kuonesha kweli alikuwa na nia ya kumuoa Maria, James hakuchelewa kuwaona wazazi wa Maria na kukamilisha taratibu za uchumba. Sasa wakawa ni wachumba wawili waliotarajia kuoana wakati wowote.

James Matei alikuwa mngoni aliyesomea Dar. Alipomaliza elimu ya chuo kikuu aliajiriwa na Wizara ya Mambo ya Ndani kama mtaalamu wa kompyuta. Baada ya kufanya kazi kwa mwaka mmoja tu alifanikiwa kununua gari lake alilokuwa akilitumia na alikuwa akiishi kwenye nyumba ya kupanga iliyokuwa Msasani.

Siku moja wakati akipata chakula cha mchana kwenye hoteli moja iliyokuwa kati kati ya jiji la Dar, alifika mtu mmoja ambaye alikaa kwenye meza moja na yeye, lakini mtu huyo aliagiza soda.

James alikuwa ameshamaliza kula, sasa alikuwa akijiandaa kuondoka.

“Samahani, nilikuwa nataka kukuuliza kitu” Mtu huyo aliyekuwa amevaa pama jeusi alimwambia James.

“Bila samahani, unaweza kuniuliza”

“Mimi naitwa Pascal, kama sikosei wewe ni Mr James Matei?”

“Ndiyo mimi”

“Sawa. Unamfahamu msichana mmoja anayeitwa Maria, aliwahi kuwa mfanyakazi wa mahakama”

James akashituka kidogo.

“Namfahamu. Ana nini?”

“Ni kweli kwamba ni mchumba wako?”

“Ndiyo ni mchumba wangu”

“Mnatarajia kuoana lini?”

“Kwani wewe ni nani?”

“Mtajie Maria jina langu, ananifahamu vizuri tangu Arusha”

Mtu huyo akainuka huku akitabasamu.

“Sasa ulikuwa na maana gani kuniuliza?” James aliendelea kumuuliza akiwa amepatwa na mshangao.

“Usijali, ni kutaka kujuana tu” Mtu huyo alimjibu na kuondoka.

James akabaki kumsindikiza kwa macho. Mtu huyo alipotoka kwenye mlango wa hoteli James akampigia Maria.

Maria alipopokea simu, James Alimuuliza.

“Unamfahamu mtu mmoja anayeitwa Pascal?’

“Pascal nani?” Sauti ya Maria ikauliza kwenye simu.

“Hakunitajia anaitwa Pascal nani lakini ameniambia nikikutajia jina hilo utamfahamu?”

“Mlikutana wapi?”

“Tulikutana hapa hoteli sasa hivi”

“Bado yupo hapo?”

“Ameshaondoka”

“Kwa kweli mimi simfahamu”

“Ameniambia mnajuana tangu Arusha”

“Simfahamu. Mlianzaje maneno yenu?”

“Nilikuwa nakula chakula akaja kuniuliza kama mimi ni James Matei. Nikamwambia ndiye mimi. Akaniuliza tena kama ninamfahamu Maria. Nikamjibu ninamfahamu”

“Maria wako wengi, alikwambia Maria nani?”

“Hakunitajia Maria nani lakini aliniambia aliwahi kuwa muajiriwa wa mahakama, nikajua ni wewe”

“Baada ya hapo alikwambia nini?”

“Alitaka kujua kama mimi ni mchumba wako”

“Ulipomjibu akasemaje?”

“Akaondoka”

“Huyo mtu mimi simfahamu. Ni wambea tu wa mjini, achana naye”

“Alitaka kujua tu kama mimi na wewe tuwachumba na tutaoana lini!”

“Huo ndio umbea wenyewe. Achana naye. Umeshakula mpenzi wangu?”

“Ndio nataka kuondoka”

“Umekula nini?”

“Ndizi kwa nyama”

“Sawa. Tutaonana jioni ukitoka kazini”

“Sawa”

James alikata simu akainuka na kutoka. Wakati anatoka alimuona yule mtu ameegemea moja ya magari yaliyokuwa kwenye eneo la maegesho la hoteli akizungumza kwenye simu.

Mtu huyo alipomuona James alifungua mlango wa gari akajipakia na kuondoka. Kwa haraka James akalifuata gari lake akaliwasha na kuliandama gari la mtu huyo.

Kwa vile Maria alishamthibitishia kuwa alikuwa hamjui mtu huyo, James alitaka kumfuatilia ili aweze kumuelewa ni nani na anatoka wapi.

Lakini kusudio lake halikutimia. Aliweza kuwa nyuma yake katika mitaa miwili tu, kufika mtaa wa tatu gari hilo lilimchenga. Hakuliona tena. Ikambidi James arudi kazini kwake.

Wakati wote akiwa ofisini alijiuliza mtu yule ni nani na kwanini alitaka kujua kuhusu uchumba wake na Maria. Alipoona hapati jibu akaamua kuachana na mawazo hayo. Aliendelea na kazi zake hadi jioni alipotoka ofisini.

Alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Maria Kinondoni. Wakati anaikaribi nyumba ya Maria alishituka alipoliona gari la yule mtu aliyemuandama likiondoka nyumbani kwa Maria.

“Huyu mtu anafahamiana na Maria?” James akajiuliza bila kupata jibu. Alilisimamisha gari akashuka na kuelekea kwenye mlango wa nyumba ya Maria.

Aliusukuma mlango na kuingia ndani. Alimkuta Maria akitoka kuoga.

“Ndio unafika?” Maria akamuuliza.

Badala ya kumjibu James naye alimuuliza.

“Ulikuwa na mgeni yeyote humu ndani?”

“Mgeni gani?’

“Yule mtu nilimuona akiondoka na gari hapo nje”

“Mtu yupi?”

“Yule niliyekueleza kwenye simu”



ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 04



ILIPOISHIA

Lakini kusudio lake halikutimia. Aliweza kuwa nyuma yake katika mitaa miwili tu, kufika mtaa wa tatu gari hilo lilimchenga. Hakuliona tena. Ikambidi James arudi kazini kwake.

Wakati wote akiwa ofisini alijiuliza mtu yule ni nani na kwanini alitaka kujua kuhusu uchumba wake na Maria. Alipoona hapati jibu akaamua kuachana na mawazo hayo. Aliendelea na kazi zake hadi jioni alipotoka ofisini.

Alikwenda moja kwa moja nyumbani kwa Maria Kinondoni. Wakati anaikaribi nyumba ya Maria alishituka alipoliona gari la yule mtu aliyemuandama likiondoka nyumbani kwa Maria.

“Huyu mtu anafahamiana na Maria?” James akajiuliza bila kupata jibu. Alilisimamisha gari akashuka na kuelekea kwenye mlango wa nyumba ya Maria.

Aliusukuma mlango na kuingia ndani. Alimkuta Maria akitoka kuoga.

“Ndio unafika?” Maria akamuuliza.

Badala ya kumjibu James naye alimuuliza.

“Ulikuwa na mgeni yeyote humu ndani?”

“Mgeni gani?’

“Yule mtu nilimuona akiondoka na gari hapo nje”

“Mtu yupi?”

“Yule niliyekueleza kwenye simu”


SASA ENDELEA

“Sijamuona, mimi nilikuwa naoga’

“Wakati nafika nilimuona anaondoka na gari”

“Mh! Mtu mwenyewe simjui na kwakweli hakuna mtu aliyeingia humu. Labda alibisha mlango, alipoona kimya akaondoka”

“Kama aliingia utajuaje wakati ulikuwa unaoga?”

Macho ya Maria yalikwenda kwenye simu yake aliyokuwa ameiweka kwenye kochi. Simu ilikuwepo.

“Sidhani kama aliingia…”

Maria aliichukua simu yake.

“Hii simu sikuiweka hivi…”

Maria alianza kuikagua simu yake kwa wasiwasi.

“Oh simu imetumika! Kuna picha zangu zimetumwa kwenye namba hii…!”

“Picha gani?”

“Picha nilizojipiga mwenyewe na picha tulizopiga tukiwa sote…hebu tazama”

James aliishika ile simu na kuangalia mfumo wa utumaji picha.

“Hii namba huifahamu?”

“Siijui” Maria alimjibu kwa wasiwasi na kuongeza.

“Huyo mtu aliingia kweli na kujitumia picha zangu sasa hivi”

“Lazima tumjue yule mtu ni nani na kwanini anatufuatafuta”

“Tutamjuaje na ameshakwenda zake”

“Muda ule nilimfuata na gari lakini alinichenga”

“Muda upi?”

“Pale hoteli. Nilipotoka nilimuona ameegemea gari akizungumza na simu. Aliponiona akaingia kwenye gari na kuondoka na mimi nikamfuata”

“Ukamuona anakwenda wapi?”

“Alinichenga tukapoteana. Sasa wakati naja kwako nikaona gari lake linaondoka”

Maria akatikisa kichwa.

“Sijui huyo mtu ni nani jamani!”

“Nitamchunguza na nitamjua”

James alibonyeza namba ya kutuma pesa. Akaingiza ile namba ya Pascal na kiasi cha pesa. Likaja jina la mmiliki wa namba ile. Lilikuwa Pascal Lazza.

“Anaitwa Pascal Lazza. Ndiye yeye. Aliniambia anaitwa Pascal”

“Hebu mpigie umuulize”

James akaipiga ile namba.

Sauti ya mtandaoni ikamwambia kuwa namba haipatikani.

“Ameshazima simu. Namba yake haipatikani”

“Mimi sipendi kuandamwa andamwa namna hii!”

“Nitaijaribu wakati mwingine. Ngoja niichukue”

James aliiweka ile namba kwenye simu yake akairudisha simu ya Maria.

Maria aliingia chumbani kwake na kuvaa kisha akarudi sebuleni.

“Mimi nafikiri kuna kitu, si bure” James alimwambia Maria.

“Kama kitu gani?” Maria alimuuliza kwa wasiwasi.

“Nafikiri tatizo liko kwenye uchumba wetu”

“Una maana kuna watu hawataki tuoane?”

“Kitu kama hicho”

“Wanajidanganya James, sisi tutaoana tu. Hakuna wa kutuzuia. Watakuuliza maswali, wataiba picha lakini haitasaidia”.

***********


Siku chache zilizopita, Mahakama ilikuwa imemuachia huru Maria baada ya kutomkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya kupoteza kwa makusudi faili la kesi ya mshitakiwa kwa lengo la kupoteza ushidi.

Ingawa hakuwa amerudishwa kazini, alishukuru kesi hiyo kuisha kwa vile ilikuwa imemuweka roho juu. Alijua kuwa alikuwa ametenda kosa lakini alitoswa na mtu ambaye alimshawishi kutenda kosa hilo bila kujua kuwa lingemletea balaa.

Licha ya kutorudishwa kazini, kule kusalimika na kifungo kulimuweka katika nafasi iliyomuwezesha kufunga uchumba na James, kijana ambaye alimpenda kidhati moyoni mwake.

Alijiambia kama atakosa kazi lakini atapata mume aliyempenda hakutakuwa na tatizo.

Alijitahidi sana kumficha James habari ya kesi yake, ingawa James alifahamu kuwa Maria alikuwa na kesi lakini hakuweza kuijua kwa undani kwa vile kesi hiyo iliisha siku chache tu kabla ya uchumba wao.

Siku iliyofuata baada ya siku ile ambayo walitokewa na Pascal, walianza kupanga harusi yao. Waliazimia kuoana siku chache zijazo wakati Jemes akiwa kwenye likizo. Na walianza maandalizi mapema.

Ilikuwa ni mwishoni mwa wiki ileile wakiwa kwenye maandalizi ya harusi yao, James akapokea meseji ya kushitusha kutoka kwa Maria. Ilikuwa saa mbili usiku. James alikuwa amemaliza kuvaa baada ya kutoka kuoga. Simu yake ilipotoa mlio wa kupokea meseji aliichukua na kuitazama. Akaona meseji iliyotoka kwa Maria.

Alipoifungua meseji hiyo iliandikwa.

“James njoo haraka yule mtu amekuja”



ITA ENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom