bioto
JF-Expert Member
- Oct 1, 2017
- 1,261
- 2,099
SIMULIZI-MJI WA LAANA-1
MTUNZI-SHADU
TELL-0677884981
UTANGULIZI.....
Kila mwanadamu ana mitihani ya kidunia ambayo
inaweza kumkatisha tamaa ili asifikie malengo yake
ambayo alikuwa amejipangia, kuna baadhi ya watu
huwa wanafikia hatua ya kutaka kujiua kabisa
wakizania ndiyo njia sahihi ya kukabiliana na
matatizo yao ambayo yanakuwa yamewasumbua
kwa muda mrefu bila kupata ufumbuzi. Matatizo
yanaweza kumfanya mwanadamu afikie hatua ya
kujuta kwa nini alizaliwa, wengine huwa
wanamkufuru Mwenyezi Mungu kwa sababu tu ya
matatizo waliyonayo. Matatizo hayo hayo ndiyo
yaliyopelekea leo hii niwe katika haya maisha
ambayo sikuwahi kuwaza kama nitaweza kuja
kuyaishi, Kwa majina naitwa Halima Ramadhani
kinoko, Ni mtoto wa mwisho kwenye familia ya
watoto watano, Sikuweza kufaidi malezi ya wazazi
wangu kwani niliambiwa na ndugu zangu wakaribu
ya kwamba wazazi wangu walishafariki kipindi cha
nyuma, kipindi ambacho nilifikisha miezi kumi.
Malezi yangu mengi nililelewa na bibi katika kijiji
cha Busamuda wilaya ya Maswa mkoani simiyu,
Nilipokuwa mdogo sikuweza kutambua umuhimu
wa wazazi kwakuwa sikuwa na akili ya kujitambua
vizuri, Bibi yangu alijitahidi kunihiza nisome sana ili
nije kumsaidia kwasababu wale kaka zangu wannne
walionitangulia hawakuonekana kumjali bibi, hata
mimi pia hawakuwa wananijali kwasababu ilipita
miaka takribani mitatu bila kuonekana pale kijijini,
Lile jambo lilimuumiza sana bibi yangu hivyo akawa
ananisisitiza kila siku nisome kwa bidii ili baadae
nije kuwa msaada mkubwa kwake. Nilivyofika
darasa la nne ndio nilianza kuona umuhimu wa
kuwa na wazazi kwani siku za maafari ya kishule
wanafunzi wenzangu wengi walikuwa wamekuja na
wazazi wao lakini kwangu hali ilikuwa tofauti,
sikuwa na mzazi hata mmoja, hakuwepo baba wala
mama ila mtu pekee ambaye nilikuwa namtegemea
kwa kipindi kile alikuwa ni bibi yangu aliyekuwa
anajulikana kwa jina la bibi kidawa, sikujuwa kwa
nini walikuwa wanamuita jina la bibi kidawa lakini
niliona watu wengi tu wamezoea kumuita hilo jina,
Nilipata uchungu kila nilipokuwa nawaona rafiki
zangu wakifurahi pamoja na wazazi wao, Bibi
alikuwa anajaribu kunifariji kila siku ili nisiweze
kuwawaza wazazi wangu lakini ilikuwa ni ngumu
sana, haikuwa kitu rahisi kuacha kuwawaza wazazi
wangu ambao sikubahatika japo kuwaona sura zao.
Niliendelea na elimu yangu ya msingi hadi
nilipomaliza darasa la saba. Mtihani wa taifa ambao
tulikuwa tumeufanya ulikuwa ni mgumu sana hivyo
sikuona miujuza yoyote ya kufaulu, Kitu ambacho
nilikuwa nakiwaza ni kupata mwanaume wakunioa
kwani wasichana wengi ambao walikuwa
wanamaliza darasa la saba katika kile kijiji cha
Busamuda walikuwa lazima waolewe, Ni wasichana
wachache sana ambao walikuwa wanapata nafasi ya
kuendelea na kidato cha kwanza. Baada ya matokeo
kutoka sikuwa miongoni mwa wanafunzi
waliochaguliwa kuendelea na elimu ya juu hivyo
nilibaki nyumbani nikiwa nasubilia mwanaume
wakuja kunioa. Sikuwa msichana mkubwa sana
lakini kwa miaka ile kumi na nne ambayo nilikuwa
nayo ilitosha kabisa kuwavutia wanaume wengi
ambao walikuwa wananitongoza kila kukicha,
Nilipata wakati mgumu sana kuchagua mwanaume
wakuweza kumkubalia kwasababu karibia wote
walionifata walionekana kuwa na maneno matamu
tena yakuvutia, wengine walikuwa wanadiliki kabisa
kumwaga machozi wakiahidi watanioa na
kuniendeleza kielimu. Baada ya kufanya uchunguzi
wa kutosha jina la Edger niliona ndio linafaa, kwani
Edger alionekana kuwa mwanaume wakujali sana,
Nilijaribu kumjibu ovyo kwa kumpima ili nijue kama
alikuwa na malengo na mimi lakini Edger
hakuoneshwa kukera na maneno yangu, Aliendelea
kila siku kunishawishi nikubali ombi lake la kuwa
wapenzi. Baada ya kumchunguza Edger kwa muda
mrefu mwishoni niliamua kumkubalia Edger lakini
kabla ya kufanya mambo mengine nilimuomba kitu
cha kwanza aje kwa bibi yangu(bibi kidawa)
kujitambulisha, Edger hakuwa na hiyana alikuja hadi
nyumbani kwa bibi akajitambulisha na kueleza kila
kitu ambacho alikuwa amekipanga juu yangu, Kwa
upande wangu nilifurahi sana kwani Edger aliongea
kwa nidhamu ya hali ya juu huku akijiamini. Baada
ya Edger kuongea vile nilimuona bibi akikasirika
huku akikunja sura, Kwa macho yangu mimi Halima
niliweza kumuona bibi yangu akimtemea makohozi
Edger huku akimwambia aondoke haraka kabla
hajachukua uamuzi mwingine, Nilistajabishwa na lile
jambo nikaamua kumuuliza bibi kwa nini amefanya
vile lakini bibi aliniangalia kwa macho ya hasira na
kusema hataki kumuona mwanaume mwingine akija
kuongea ujinga pale nyumbani kwake. Roho iliniuma
sana lakini sikuwa na lakufanya, Edger aliondoka
nyumbani huku akiwa amesikitishwa sana na kile
kitendo cha kutemewa makohozi na bibi yangu. Kila
siku nilikuwa namsumbua sana bibi kuhusu swala la
mimi kuolewa kwasababu nilikuwa bado ni
msichana mbichi na wanaume wengi wenye nia
ukiachana na Edger walikuwa wanazidi kujitokeza
lakini bibi alikataa kata kata. Bibi hakutaka niolewe
wala hakuwa na lengo lakunitafutia kitu cha kufanya
hivyo muda mwingi nilikuwa nipo nyumbani nikiwa
nimekaa tu bila kufanya kitu chochote. Kuna siku
niliamua kuvunja ukimya na kumuuliza bibi kwa nini
alikuwa hataki niolewe, Kwa kuwa ilikuwa ni saa
mbili usiku bibi aliamua kuwasha kibatari kisha
akaketi kwenye kigoda na kuanza kuongea, bibi
aliongea maneno ambayo hayakuniingia kabisa
akilini mwangu..."Siyo kwamba sitaki uolewe halima
bali nina lengo kubwa sana na wewe, ukiolewa
utakuwa umeharibu kila kitu, siku zangu za kuishi
duniani zinahesabika hivyo ni wewe pekee ndiye
ninayeona unafaa kubeba hii mikoba halima"...alion
gea bibi ambaye alikuwa anatafuna ugoro wake,
Nilihisi bibi huenda akawa amechanganyikiwa kwani
yale maneno ambayo aliniambia yalikuwa
yameniweka njia panda, Nilivyojaribu kumuuliza bibi
vizuri kuhusu lile jambo aliloliongea, Bibi aliamua
kuniweka wazi kuwa mimi ndiye niliyekuwa
nimechaguliwa kuridhi mikoba yake ya uchawi,
kumbe bibi yangu alikuwa ni mchawi tena mchawi
mwenye nyazifa kubwa sana katika serikali ya
kichawi. Sikuwa tayari kukubaliana na bibi kwani
niliuogopa sana uchawi lakini kitendo cha kukataa
ile mikoba ya bibi kiliweza kunisababishia matatizo
makubwa ambayo yalinitesa sana.