Simulizi: Mapito ya maisha

chongoe

JF-Expert Member
Mar 22, 2019
1,122
2,714
Habari zenu wakuu,

Mimi ni kijana ambaye kazi kubwa ni baharini; sio mvuvi ila mimi ni yule mshika usukani wa majahazi. Safari zangu ni za kupeleka mizigo tokea Mafia napeleka Kisiju au Zanzibar muda mwingine Kilwa, ndiyo kazi zangu. Nilitaka leo niwape story tu ninazokutana nazo hasa baharini maana mengi mno. Nitasimulia mawili mengine nitaendelea ikiwa nitaulizwa kwa mujibu wa story.

Story ya kwanza
Nakumbuka ilikuwa usiku natokea Kisiju naelekea Mafia, tupo safarini baada kupita kisiwa kimoja kinaitwa KOMA ndipo mauzauza yalipoanza. Kwa uzoefu wangu ndiyo mara ya kwanza kukutana na kioja kama kile wakati tunatembea baharini na jahazi ghafla mbele yetu ilitokea boti kubwa sana inakuja uelekeo wetu ilifika karibu kabisa mimi niljua wanatugonga; mara ghafla ikaturuka nzima mzima, kwa uoga wangu nilipiga kelele mpaka baadhi ya watu waliamka na kushtuka usingizini. Kuna mmoja wetu alivyoamka tu aliiona ile boti akaniuliza ile boti imetokea wapi nikamwambia ile imeturuka kimaajabu.

Hapa ndiyo maana nilipiga ukelele. Kusikia hivyo wale jamaa waliomka ikabidi watulie ghafla, ile boti ikawa inakuja uelekeo wetu nakutaka kutugonga; ilivyokaribia mule ndani ya jahazi yetu alikuepo mzee mmoja anaeishi Mafia. Sasa wakati boti inakaribia yule mzee alituambia tubaki kuwa kimya ghafla yeye akasimama sikujua kasema maneno gani ghafla nikaona boti inageuza kuelekea upande mwingine.

Zilichukua kama dakika mbili ile boti kupotea hatukuiona tena ndipo yule mzee akanambia usisafiri kama mwili wako mwepesi au acha kazi utakufa bure kumbe ile boti ilikuja kwa lengo la kutupoteza kuanzia ndio nikajitengeza sasa.

Story ya pili
Nilimpoteza ndugu yangu alikufa kwa ugonjwa wa kidole sababu yake wakati tunatokea Mafia tulipakia nazi za MZEE mmoja wakati wakudai nauli, yule mzee alikuwa hataki kulipa sasa alipo kuja kwangu dogo akawa ananisimulia huku anaonesha kidole kunipa ishara kwa yule mzee kuwa kagoma kulipa kumbe yule Mzee alkasirika baada kuona ananyooshewa kidole. Yule mzee akatamka kumwambia dogo hutanyoosha tena kidole; mimi nilidhani utani, dogo baada kufika jioni akaanza kuumwa na kidole siku ya tatu dogo akafariki. Hayo ndiyo nayopitia kwenye kazi yangu; yapo mengi ngoja nipumzike kwanza.

Sehemu ya Pili

Sehemu ya Tatu
 
Ngoja washirikina wenzako wata kufata in box muelekezane huko ulipo jiganga mkaliwe helazenu kwakuamini upuuzi.

Mwamini MUNGU tu katika maisha yako yote ili sikuukifa upate rehemazake.
Maisha nimafupi hao washirikina kunasiku wote mtaingia kwenye hukumu.
Mtafute YESU upate amani ya mwili na roho.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha kujidanganya kama hujui kaa kimya ww na mafumdisho ya kukariri
Ngoja washirikina wenzako wata kufata in box muelekezane huko ulipo jiganga mkaliwe helazenu kwakuamini upuuzi.

Mwamini MUNGU tu katika maisha yako yote ili sikuukifa upate rehemazake.
Maisha nimafupi hao washirikina kunasiku wote mtaingia kwenye hukumu.
Mtafute YESU upate amani ya mwili na roho.



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapito ya maisha: Sehemu ya Pili

Habari zenu wakuu,

Natumai mpo wazima. Naendelea kuwaletea mambo ambayo nakutana nayo kwenye kazi yangu ya bahari.

Kuna siku nipo Bandari ya Kisiju nasubiria mzigo ikiwa utatokea maana kazi zetu muda mwingine ni kama unabahatisha.

Ilikuwa saa kumi jioni kuna mtu alikuja na kuniambia ana mzigo unataka kwenda maeneo ya Mafia; mi nikamwambia haina tabu. Kumbe yule bwana alikuja na viroba vipatavyo 30, sasa mimi nikamwambia siwezi kwenda Mafia kwa viroba vichache labda tusubirie mzigo mwingine ukitokea, yule jamaa akawa hakubali, akaniuliza kwani tatizo liko wapi mpaka hutaki kubeba viroba vyangu?

Nikamwambia pesa tu, sababu baharia wapo wanne na mimi nahodha wa tano kwa viroba 30 utatoa kiasi gani, yule jamaa akauliza nyie mnataka shilingi ngapi mi nikamwambia bei yetu yakuondokea ni 80,000, yule jamaa akasema kasema tafuta wapakiaji wakapakie pesa nitawapa.

Dah! ikabidi nipigwe na mshangao, ikabidi niwaeleze baharia wangu tujiandae na safari ya kwenda Mafia kupeleka viroba 30 kwa 80,000. Wale baharia wangu wakauliza huyo mwenye mzigo ana akili timamu, nikawaambia ndiyo anaonekana ana akili zake.

Ikabidi wakubali tukatafuta wapakiaji wakapakia wakalipwa pesa yao ya upakiaji; ilivyofika usiku pia aliongezeka jamaa mwingine ana mzigo wa mafenesi anelekea Mafia maeneo ya Jibondo na yeye tukampakia na mafenesi yake ila yeye alitoa 30,000, tukijumlisha laki na kumi.

Muda wa safari ulipofika, ilikuwa saa kumi na moja asubuhi. Tukaanza kutoka, wakati tupo baharini, jahazi inatembea ikabidi mimi niamzishe story kati yangu Mimi na yule mwenye viroba na mwenye mafenesi.

Nikaanza kumuuliza mwenye viroba anapoelekea Mafia gani kwa maana mimi mzoefu sana wa Mafia, ila yeye sijawahi kumuona kwakuwa sisi watu wa majahazi wenye maduka tunawajua. Yule jamaa alichojibu watu wote tulishangaa.
Alijibu kwamba yeye hafiki mbali sana, atateremka njiani sehemu moja inaitwa Dira Mawe.

Kwa sisi tuliyozoea mambo ya bahari tukapigwa mshangao sana sababu eneo alotaja yeye ni baharini tu, eneo ambalo kwa mtu yoyote haiingii akilini. Ikabidi nimuulize tena unakusudia kweli unaenda Dira Mawe au unatania, akajibu kwa uhakika naenda Dira Mawe.

Wale baharia wangu wakamwambia kama unateremka Dira Mawe basi tupe nauli yetu, yule jamaa kasema akifika tu atatoa nauli, yaani pale mimi ujasiri wote ulipotea. Sijawahi kupakia mtu alafu akateremka njiani, alafu baharini.

Mimi nikaona hii kesi, sababu alivyopanda pale Kisiju watu wamemuona alafu tufike Mafia jamaa awe hayupo. Ikabidi nimwambie siwezi kumteremsha kati ya bahari, itakuwa kesi juu yangu.

Kwa mshangao, baada kuongea vile mimi, yule jamaa akasimama akaenda eneo vilipo viroba akawa anatoa kuonyesha ishara anakaribia kufika, anahakiki viroba. Alipomaliza hesabu akaongea kwa nguvu nishafika tueni tanga nishuke, akimaanisha ashafika tusimamishe jahazi, mi nikasema haiwezekani.

Yule jamaa akasema mkinipitisha eneo hili pesa yenu siwapi, alafu mimi mtanijua. Jamaa kapiga mkwara ikabidi wale baharia wangu wakaniambia acha tumshushe tuone itakuaje.

Dah! nikasimamisha jahazi muda huo ilikuwa saa tatu asbuhi, yule jamaa akaanza kutulipa pesa yetu 80,000 alafu akaanza tosa viroba baharini alipo maliza akajitosa na yeye.

Aisee mpaka leo hii nikipita eneo hilo nakumbuka hili na usikuu huu natarajia kupita tena maana natarajia kutoka kwenda Kisiju, maji yakijaa natokea Mafia napeleka nazi. Acha nipumzike kwanza ninayo mengi sana yanakuja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom