Simulizi: Makaburi ya wasio na hatia

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,435
0052566a7111fb14d858e398a29dde62.jpg


SEHEMU YA KWANZA:
JINA langu naitwa Togolai Mahimba, ni mtoto wa mwisho kati ya watoto saba wa baba yetu, Sinai Mahimba ambaye kwa sasa ni marehemu. Baba yetu alifariki miaka mitatu iliyopita baada ya kuugua ghafla.
Kifo chake kilitawaliwa na utata mkubwa na hata siku ya mazishi yake, kulitokea mambo mengi ya ajabu ambayo mpaka leo siwezi kuyaeleza. Ninayo mambo mengi ambayo ningependa kukusimulia ndugu msomaji lakini kwa kuanzia, naomba nikueleze mambo machache yaliyotokea kabla ya kifo cha baba yetu ambaye mimi ndiye nilikuwa mtoto anayenipenda zaidi.
Kabla hajafikwa na mauti, baba yetu alikuwa mtu maarufu sana kijijini kwetu, Makongorosi, Chunya mkoani Mbeya tulikokuwa tukiishi. Kilichofanya awe maarufu kiasi hicho, ni kazi yake ya uganga aliyokuwa anaifanya ambapo mbali na mambo mengine, alikuwa akiwafanyia matambiko wachimbaji wengi wa dhahabu ili wakiingia mgodini, wapate dhahabu kwa urahisi sambamba na wafanyabiashara wengine.
Umaarufu wa baba ulisababisha hata sisi watoto wake tuwe maarufu sana, hasa mimi ambaye muda mwingi nilikuwa nikiongozana naye kila alikokuwa anakwenda, kuanzia kwenye matambiko maporini, kwenye mazindiko migodini, kuchimba dawa msituni mpaka kilingeni kwake alikokuwa akifanyia shughuli zake za uganga.
Wengi walikuwa wakifupisha jina langu kwa kuniita Togo na hilo ndiyo lililokuwa maarufu kuliko hata jina langu halisi. Nakumbuka maisha yangu ya utotoni yalikuwa ya raha sana kutokana na jinsi baba alivyokuwa akinipenda. Hata ndugu zangu wengine tuliozaliwa pamoja, walikuwa wakinionea gere kwa jinsi nilivyokuwa nikipendwa.
Maisha yaliendelea vizuri, nikawa naendelea kukua huku pia nikijifunza mambo mengi aliyokuwa akiyafanya baba katika kazi zake. Mambo yalianza kubadilika siku moja tukiwa msituni na baba kutafuta dawa.
Baba akiwa ameinama akichimba mizizi ya mti wa mtangetange ambao ulikuwa ukitumika kwa kutibu magonjwa mengi, hata yale yaliyoshindikana hospitalini, ghafla alivamiwa na kundi la popo waliokuwa wanapiga kelele kwa nguvu. Baba akawa anahangaika kujaribu kuwazuia popo hao ambao waliendelea kumzonga hasa sehemu za kichwani.
Akiwa anaendelea kupambana nao, nilimshuhudia akifanya tukio ambalo sikuwahi kumuona baba akilifanya hata mara moja. Kwa kasi ya kimbunga, aliyeyuka na kupotea eneo hilo, nikabaki nimepigwa na butwaa, nikiwa ni kama siamini.
Ghafla wale popo baada ya kuona baba amepotea kimiujiza, walitawanyika na kupotea eneo hilo huku wakiendelea kupiga kelele kwa nguvu. Nikawa nageuka huku na kule kumtazama baba bila mafanikio, hofu kubwa ikatanda kwenye moyo wangu.
“Unashangaa nini Togolai,” sauti ya baba ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye lindi la mawazo, nikashtuka kwa nguvu. Cha ajabu, baba alikuwa amesimama palepale alipokuwepo, akiendelea na kazi yake ya kuchimba mizizi ya mtangetange kama hakuna kilichotokea.
“Baba mbona sielewi?”
“Huelewi nini tena?”
“Popo.”
“Popo? Wamefanya nini?”
“Hawajakuumiza?”
“Mbona sikuelewi Togo?” alisema baba huku akiacha kazi aliyokuwa anaifanya na kunisogelea. Sikutaka kuamini kama kweli baba alikuwa haelewi nilichokuwa nakizungumza, akanisogelea na kunishika begani.
“Uko sawa?”
“Ndi..yo baba, niko sawa,” nilibabaika kidogo, nikamuona baba akigeuka huku na kule kama anayeangalia kitu fulani. Na mimi nikawa nageuka kufuata usawa wa macho yake, ghafla macho yetu yakaganda eneo moja, nilipigwa na butwaa kubwa kwa nilichokuwa nakiona, nikajikuta nikianza kutetemeka.
Wanaume wawili waliokuwa uchi wa mnyama, walikuwa wakining’inia kwenye tawi la mti mkubwa uliokuwa mita chache kutoka pale tulipokuwa, wote wakitukodolea macho yao mekundu.
“Unawaona wale washenzi?” baba alisema huku akionyesha kutokuwa na hata chembe ya wasiwasi. Nikatingisha kichwa kama ishara ya kumjibu ‘ndiyo nawaona’.
“Wale ni wachawi wanaosumbua watu kijijini kwetu, naona wametangaza vita na mimi, hawanijui hawa,” alisema baba na kama ilivyotokea mara ya kwanza, aliyeyuka na kupotea eneo lile, wale wachawi nao wakapotea kwenye upeo wa macho yangu, nikasikia kelele za watu waliokuwa wakilia kwa sauti kubwa kama wanaolalamikia maumivu makali.
“Ndiyo dawa yao, na siku nyingine wakirudia watanikoma,” alisema baba, nikashtuka tena baada ya kumuona amesimama palepale alipokuwa mara ya kwanza, pembeni yangu lakini safari hii alikuwa akihema kwa nguvu kama mtu aliyetoka kukimbia. Nilijihisi kama nipo ndotoni.
“Baba mbona sielewi kinachotoke…” nilisema lakini kabla sijamalizia kauli yangu, macho yangu yalitua kwenye mkono wa baba uliokuwa na jeraha na alama kama ameng’atwa na mnyama mkali, huku damu nyeusi zikimtoka kwa wingi.
“Ninii!” baba alinihoji baada ya kuona macho yangu yameganda kwenye mkono wake.
“Umeumia baba, pole,” nilisema lakini baba hakunijibu kitu zaidi ya kuusogeza ule mkono wenye jeraha karibu na uso wake, akawa analichunguza vizuri lile jeraha.
Akasogea pale kwenye mti wa mtangetange na kuchuma majani yake, akayatia mdomoni na kuanza kuyatafuna kisha muda mfupi baadaye, aliyatoa mdomoni na kuyabandika juu ya kidonda chake, nikamuona akifumba macho kama ishara ya kuonyesha jinsi alivyokuwa akihisi maumivu.
“Nitakuwa sawa usijali, nimeshazoea kusumbuana na hawa wachawi. Inabidi na wewe uwe jasiri,” alisema baba huku akiendelea kujisafisha pale kwenye jeraha lake. Zile damu nyeusi zilizokuwa zinamtoka zikakata, akashusha pumzi ndefu na kuendelea na kazi ya kuchimba dawa.
Kwa kweli matukio yale niliyoyashuhudia yaliufanya moyo wangu uingiwe na hofu kubwa mno. Sikuwahi kudhani baba anaweza kuwa na nguvu za giza kiasi kile, siku zote niliamini alichokuwa anakifanya ni kutibu watu kwa mitishamba tu, basi! Hata hivyo, nilijikaza kiume na kuuficha mshtuko nilioupata, nikaendelea kumsaidia baba na hatimaye tukamaliza kazi yetu.
Wakati tunarudi kutoka msituni, baba alinisisitiza njiani kwamba sitakiwi kumwambia mtu yeyote kuhusu nilichoshuhudia, hata ndugu zangu wa tumbo moja. Akaniambia kwa kilichotokea, anahisi kuna madhara makubwa yatakuwa yametokea kijijini kwetu.
“Unamaanisha nini baba?”
“Wale wachawi waliotuvamia kule msituni, mmoja nimemuumiza sana sijui kama anaweza kuwa yupo hai mpaka muda huu.”
“Kwani ni akina nani wale?”
“Kwani wewe huwajui wale? Au hujawatazama vizuri?” baba alinihoji na kuanza kunifafanulia, akaniambia yule mmoja ni mzee wa kanisa pale kijijini kwetu, aliponitajia jina lake ndiyo nikamtambua vizuri. Alikuwa ni mzee Mwankuga, ambaye mara kwa mara alikuwa akiingia kwenye migogoro na baba kutokana na kugombea mpaka wa shamba kwa sababu shamba letu na lake yalikuwa yemepakana.
Nakumbuka kuna kipindi waliwahi kupelekana mpaka kwa balozi kutokana na ugomvi wao huo. Hata familia zetu hazikuwa na uhusiano mzuri, sisi tulikatazwa kabisa kuongea wala kucheza na watoto wa mzee Mwankuga na yeye hali kadhalika.
“Kwa hiyo unataka kusema mzee Mwankuga naye ni mchawi? Si mtumishi wa Mungu yule na kila Jumapili anaenda kanisani tena anakaa siti za mbele?”
“Mwanangu dunia ina mengi hii! Hutakiwi kumuamini mtu, pale kanisani waumini karibu wote huwa wanakuja kutafuta dawa kwangu, wengine wanataka wapandishwe vyeo, wengine wanataka kujikinga na wengine wana shida mbalimbali, usiwaamini binadamu,” alisema baba, nikabaki nimeduwaa. Hizo zikawa ni habari nyingine za kushangaza sana kwangu.
“Sasa pale si walikuwa wawili? Huyo mwingine ni nani?”
“Si yule mwalimu wenu, Mwashambwa?”
“Mwalimu wetu Mwashambwa anayetufundisha hesabu naye ni mchawi?” niliuliza kwa mshangao mkubwa huku mdomo nikiwa nimeuacha wazi.
“Ndiyo, hata ule mguu wake anaochechemea nasikia alikutana na kombora la kichawi ndiyo likampa ulemavu wa kudumu, siyo mtu mzuri kabisa, we turudi nyumbani utasikia chochote kuhusu watu hao wawili,” baba alisema kwa kujiamini, ukimya mrefu ukatanda kati yetu, hakuna aliyezungumza chochote.
Niliendelea kutembea huku nikiwa na furushi langu la dawa kichwani pamoja na panga, baba yeye alikuwa ametangulia mbele, naye akiwa amebeba dawa na jembe tulilokuwa tunalitumia kuchimbia dawa.
Ili kufika nyumbani kwetu, ilikuwa ni lazima upite nyumba kadhaa za nyasi na nyingine za bati zilizokuwa pembezoni mwa kijiji ndiyo uelekee nyumbani. Miongoni mwa nyumba hizo, ilikuwepo pia na nyumba ya mzee Mwankuga ambaye muda mfupi uliopita baba alikuwa akinisimulia mambo yake kwamba ni mchawi.
Tulipokaribia nyumbani kwa mzee huyo, baba alinionyesha ishara kwamba nisimame, nikafanya hivyo, tukawa tunasikia sauti za watu wengi wakilia kutoka nyumbani kwa mzee huyo, baba akanionyesha ishara kama anayesema ‘unaona?’, nikashika mdomo kwa mshangao. Sikutaka kuamini kwamba kweli mzee Mwankuga alikuwa amefariki dunia.
Je, nini kitafuatia? Usikose mwendelezo hapahapa
 
SEHEMU YA 02:

ILIPOISHIA:
Tulipokaribia nyumbani kwa mzee huyo, baba alinionesha ishara kwamba nisimame, nikafanya hivyo, tukawa tunasikia sauti za watu wengi wakilia kutoka nyumbani kwa mzee huyo, baba akanionesha ishara kama anayesema ‘unaona?’, nikashika mdomo kwa mshangao. Sikutaka kuamini kwamba kweli mzee Mwankuga alikuwa amefariki dunia.
SASA ENDELEA…
Nilijikuta nikishusha lile furushi la dawa na panga, nikawa nataka niende kushuhudia mwenyewe kama ni kweli lakini baba aliniambia nisithubutu kufanya hivyo, hasa kutokana na uhasama uliokuwepo kati yetu na familia hiyo. Bado niliendelea kuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kama ni kweli yule mzee amekufa.
Ilibidi baba anishike mkono, tukaenda mpaka nyumbani ambapo baba aliingia kwenye chumba chake cha uganga na kuanza kuchambua zile dawa tulizotoka nazo porini. Ni kama alijua kwamba nitamtoroka na kurudi kule msibani kwenda kushuhudia kilichotokea kwani aliniambia nikae palepale, nimuangalie jinsi alivyokuwa akichambua dawa.
Kweli nilitii maagizo yake, nikakaa pale lakini bado nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kilichoendelea. Nilipomuona baba amezama kwenye kazi yake hiyo, niliinuka na kuanza kuelekea mlangoni, akaniwahi na kuniuliza ninakokwenda.
“Naenda kujisaidia baba,” nilimdanganya baba, akanitazama usoni kisha akaendelea na kazi yake. Nilitoka na kwenda chooni ambako nako nilizunguka nyuma, nikatokomea huko na kwenda kutokea upande wa pili, nyumbani kwa mzee Mwankuga.
Kwa kuwa watu walikuwa wengi, hakuna aliyenitazama vizuri, kwa hiyo nikapata nafasi ya kujichanganya na waombolezaji ambao kadiri muda ulivyokuwa unazidi kusonga mbele ndivyo walivyokuwa wakizidi kuongezeka.
“Kwani alikuwa anaumwa?”
“Hapana alikuwa mzima wa afya kabisa na alikuwa akiendelea na kazi zake, mara akaanza kulalamika kwamba kichwa kinamuuma sana, damu zikawa zinamtoka puani na mdomoni, ghafla akadondoka na kugeuza macho, muda mfupi baadaye moyo wake ukasimama,” nilimsikia ndugu mmoja wa Mwankuga akimuelezea mmoja wa waombolezaji.
Ni hapo ndipo nilipoamini kwamba kweli Mwankuga alikuwa amekufa, kwa kuhofia kuonekana na watu, hasa ndugu zake ambao kama nilivyosema tangu awali hatukuwa na uhusiano nao mzuri, nilirudi kinyumenyume, kisha nikaondoka haraka kurudi nyumbani.
Nilimkuta baba akiwa amesimama nje ya nyumba yetu, akinitazama, nadhani alishashtukia kwamba nimemtoroka, aliponiona tu natokeza, akanibana kwa maswali magumu.
“Ulikuwa wapi?”
Nilikosa cha kujibu, nikawa najiumauma, baba akaniambia nina bahati sana vinginevyo angenifunza adabu, tukaingia ndani ambapo tulienda mpaka kule kwenye chumba cha uganga, baba akanikalisha chini na kuanza kuzungumza na mimi.
“Unajua wewe ndiyo mwanangu kipenzi na sasa umeshakuwa mkubwa, sina sababu ya kuendelea tena kukuficha mambo yangu ndiyo maana leo nimekuonesha baadhi ya mambo.
“Dunia imebadilika sana mwanangu, binadamu tunaishi kwa ubaya sana, hakuna anayemtakia mwenzake mema, watu wanawaonea wengine bila sababu, watu wasio na hatia wanakufa kila siku, ukienda makaburini, yaliyojaa ni makaburi ya watu wasio na hatia! Kila mmoja lazima ajilinde mwenyewe na ukishaweza kujilinda mwenyewe, unaweza pia kuwalinda wenzako,” alisema baba, maneno ambayo yaliniingia lakini bado sikuwa naelewa kile alichokuwa anakimaanisha.
Bado nilikuwa nataka ufafanuzi wa kifo cha mzee Mwankuga kwa sababu kwa akili yangu, niliona kama hakuwa amefanya jambo lolote kubwa kustahili adhabu ya kifo. Ni kama baba aliyaona mawazo yangu, akaniambia anajua najiuliza maswali mengi yasiyo na majibu kuhusu kilichotokea kule msituni.
“Kuna yule rafiki yako aliyekufa kwa kutumbukia kwenye kisima mwaka jana, unamkumbuka?”
“Alfred? Ndiyo namkumbuka,” nilimjibu baba huku nikiwa na shauku ya kutaka kusikia anachotaka kukisema. Akaniambia mazingira ya kifo cha Alfred, yalikuwa yamejaa utata wa hali ya juu na kwamba baada ya kuchunguza kwa kina, aligundua kwamba Alfred hakufa kifo cha kawaida, bali aliuawa.
Akaendelea kuniambia kwamba hata huko kuuawa kwenyewe, japokuwa kila mtu alikuwa anajua ni kweli amekufa na kuzikwa, lakini ukweli ni kwamba hakuwa amekufa bali alichukuliwa msukule.
“Kwani kuna tofauti gani kati ya mtu aliyekufa na mtu aliyechukuliwa msukule?” Nilimuuliza baba, akaniambia kwamba mtu aliyekufa kwa kifo cha amri ya Mungu, huwa mwili unatengana na roho, mwili unaenda kuzikwa kaburini na huo ndiyo unakuwa mwisho wa maisha ya kawaida ya hapa duniani.
Akaniambia pia kwamba kwa kawaida, nafsi au roho ya mtu huwa haiishi ila baada ya kutengana na mwili, huhama kutoka kwenye ulimwengu wa kawaida na kwenda kwenye ulimwengu mwingine. Nilipotaka kumuuliza kuhusu huo ulimwengu mwingine, aliniambia kwamba atanifafanulia siku nyingine.
Akaendelea kunieleza kwamba mtu anayechukuliwa msukule, huwa hafi bali anabadilishwa kichawi kiasi cha kila mmoja kuamini kwamba ni kweli amekufa lakini kinachotokea, huwa anachukuliwa na wachawi na kwenda kutumikishwa kichawi kwenye kazi mbalimbali, mpaka siku ambayo atakufa kwa amri ya Mungu lakini kwa kipindi chote hicho, huwa anaishi kama msukule.
“Sasa mbona Alfred alipokufa tulienda kumzika makaburini na hata siku ya kuaga mwili wake, wote tulipita kwenye jeneza lake na mimi mwenyewe nilimshuhudia akiwa amelala ndani ya jeneza?”
“Ni vigumu sana kunielewa hiki ninachokisema kwa maneno, lakini nataka nikuhakikishie kwamba rafiki yako hakufa na aliyefanya yote hayo ni huyu mshenzi Mwankuga,” alisema baba akionesha kuwa na jazba, akaendelea kunieleza kwamba, licha ya Alfred, walikuwepo watu wengine wengi tu ambao wengine waliuawa kwelikweli lakini kwa ushirikina, ikiwa ni uonevu unaofanywa na wachawi hasa wanapokaribia kutoa makafara yao, na wengine huchukuliwa misukule.
Bado sikuwa namuelewa anachokisema, akaniambia anataka akanithibitishie kwamba Alfred hakufa. Aliacha kila alichokuwa anakifanya, tukatoka nje ambapo watu walikuwa wakizidi kufurika kwenye msiba wa Mwankuga na sasa vilio vya wanawake vilikuwa vikizidi kuongezeka.
Wala baba hakujali chochote, tukatoka na kuelekea makaburini ambayo yalikuwa eneo maarufu linalofahamika kama msalabani, nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujionea mwenyewe kile alichokuwa anakisema baba kama ni kweli.
“Unakumbuka alizikwa kwenye kaburi gani?” baba aliniuliza, nikamwambia nakumbuka vizuri kwa sababu enzi za uhai wake, Alfred alikuwa rafiki yangu mkubwa na kifo chake cha ghafla, kiliniumiza mno moyo wangu. Kwa kuwa hata siku ya mazishi yake nilikuwepo mpaka makaburini, nilikuwa nalikumbuka vizuri kaburi lake.
Nikamuongoza baba mpaka kwenye kaburi la Alfred ambalo juu yake kulikuwa na msalaba ulioandikwa jina lake kamili, tarehe ya kuzaliwa na tarehe ya kufa kwake. Akaniambia niwe makini kwa kila atakachokuwa anakifanya, nikatingisha kichwa huku hofu kubwa ikiwa imetanda ndani ya moyo wangu kwani kiukweli nilikuwa nikiogopa sana makaburi na maiti.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 03:

ILIPOISHIA:
Nikamuongoza baba mpaka kwenye kaburi la Alfred ambalo juu yake kulikuwa na msalaba ulioandikwa jina lake kamili, tarehe ya kuzaliwa na tarehe ya kufa kwake. Akaniambia niwe makini kwa kila atakachokuwa anakifanya, nikatingisha kichwa huku hofu kubwa ikiwa imetanda ndani ya moyo wangu kwani kiukweli nilikuwa nikiogopa sana makaburi na maiti.
SASA ENDELEA:
Baba alianza kufukuafukua ule upande wa kichwani kwenye lile kaburim akaingiza mkono mfukoni na kutoa kichupa kilichokuwa na ungaunga mweusi, akaumwaga kuanzia upande wa kichwani mpaka miguuni, kisha akaniambia tuanze kulizunguka lile kaburi kwa kuanzia kushoto kwenda kulia.
Alianza yeye, na mimi nikafuatia, tukawa tunazunguka lakini kwa kutembea kinyumenyume, baada ya kuzunguka raundi sana, nilianza kusikia kizunguzungu kikali, baba akaniambia nikae, yeye akarudi kusimama palepale alipokuwa amesimama.
“Hebu muite jina lake mara tatu kwa sauti kubwa,” alisema baba, nikawa simuelewi anamaanisha nini. Yaani mtu alishakufa siku nyingi zilizopita halafu ananiambia nimuite jina lake, tangu lini maiti ikaitika? Hata hivyo, ilibidi tu nitii kile alichoniambia, nikamuita.
Nililitaja jina lake kwa mara ya kwanza, baba akawa ananionesha ishara kwamba niongeze sauti, nikamuita kwa mara ya pili kisha kwa mara ya tatu. Cha ajabu kabisa, nilisikia akiitikia, tena niliweza kuthibitisha kabisa kwamba ni yeye kwa sababu nilikuwa naijua sauti yake na hata akizungumza neno moja tu, nakuwa nimeshamtambua.
Nilitetemeka kuliko kawaida, nikawa nageuka huku na kule kwa sababu alivyoitikia, ilionesha kwamba hayupo pale kwenye kaburi bali yupo umbali wa mita kadhaa pembeni. Nikiwa bado siamini, baba alinionesha kwa kidole, akaniambia nitazame chini ya mti mkubwa wa mjohoro uliokuwa pembeni kidogo ya makaburi.
Nilitazama lakini sikuona kitu, nikamgeukia baba, akaniambia niendelee kutazama bila kupepesa macho. Katika hali ambayo sikuitegemea, nilimuona Alfred akiwa amesimama chini ya mti, nywele zake zikiwa zimekuwa ndefu na chafu sana, rangi ya ngozi yake ikiwa imebadilika na kuwa utafikiri amejipaka unga wa mkaa usoni. Akiwa ni kama na yeye amegundua kwamba nimemuona, Alfred aligeuka na kuanza kutimua mbio, muda mfupi baadaye akapotelea kwenye msitu mkubwa uliokuwa pemebi ya makaburi hayo.
Nilibaki nimepigwa na butwaa, nikiwa siamini kabisa nilichokiona, baba akanigeukia na kunitazama usoni.
“Unaona sasa? Mambo mengine usiwe unakuwa mbishi tu,” alisema, nikawa bado nimepigwa na butwaa, nikihisi kama nipo kwenye ndoto za kutisha ambazo sikuwa najua mwisho wake utakuwa nini.
Ilibidi baba anishike mkono na kuanza kunivuta, akili zangu zikarudi sawa, nikawa bado nageukageuka kutazama kule Alfred alikokuwa amepotelea. Nitakuja kueleza zaidi juu ya mazingira ya kifo cha Alfrted ambapo sasa na mimi nilianza kuamini kwamba hakikuwa kifo cha kawaida. Baba ni kama alikuwa amenifumbua macho.
Tulirudi mpaka nyumbani, tukakuta bado watu wanazidi kuongezeka pale kwenye msiba wa Mwankuga.
Tulienda mpaka nyumbani lakini kwa kuwa bado nilikuwa na maswali mengi kuhusu kifo cha mzee huyo, ilibidi nimtoroke tena baba na kwenda pale msibani. Safari hii watu walikuwa tayariw ameshakaa pale nje kwa kujipanga, kila mmoja akiwa na uso wa huzuni.
Kitendo cha mimi kuonekana tu eneo hilo, nilishangaa watu wakiacha kila walichokuwa wanakifanya na kunikodolea macho. Hata wale waliokuwa wanalia, wote walinyamaza, wakawa wananitazama. Sikuelewa kwa sababu gani hali hiyo imetokea, hofu kubwa ikatanda ndani ya moyo wangu.
Kwa mbali nikaanza kusikia minong’ono huku watu wakiendelea kunitazama. Mzee mmoja ambaye naye siku za nyuma nimewahi kusikia kwamba ana tabia ya kuwaibia watu fedha kwa uchawi wa ‘chuma ulete’, alisimama na kuongea kwa jazba.
“Baba yako alichokifanya ameona hakitoshi ameamua kukutuma na wewe uje kuendeleza uchawi wenu hapa. Mwaka huu mtaisoma namba, kamwambie anajikaanga kwa mafuta yake mwenyewe, mwisho wake umekaribia,” alisema mzee huyo na kusababisha watu karibu wote pale msibani wamuunge mkono, zogo kubwa likatokea huku wengine wakiinuka na kutaka kuja kunishushia kipigo.
Ni hapo ndipo nilipoelewa kwa nini watu walikuwa wakinitazama kwa macho ya chinichini nilipofika msibani hapo. Kumbe walikuwa wanahisi baba amenituma mwenda kufanya uchawi! Maskini, nilibaki natetemeka kwa hofu kubwa kwa sababu sikuwa najua chochote kuhusu uchawi wala kuroga.
Ili kuokoa maisha yangu, ilibidi nitimue mbio, wakaendelea kunisindikiza kwa maneno makali wakimtuhumu baba na sisi familia nzima kwamba tunahusika na mambo ya kishirikina na kwamba eti sisi ndiyo tumemuua mzee Mwankuga kutokana na ugomvi wetu wa kugombea mpaka wa shamba.
Nilirudi nyumbani nikiwa natweta, mtu wa kwanza kuniona alikuwa ni baba ambaye alikuwa amekaa nje ya nyumba yetu, kwenye gogo kubwa la mti wa mvule akiandaa dawa zake, akashangaa kuniona naingia mbiombio huku nikilia. Alinisimamisha lakini sikusimama kwa hofu kwamba wale watu watakuwa wananifuatilia, nikapitiliza mpaka ndani na kwenda kujifungia chumbani kwetu.
Nilijuta kwa kutosikiliza kile alichokuwa ameniambia, nikawa natetemeka kwa hofu kubwa ndani ya moyo wangu. Niliendelea kujifungia chumbani kutwa nzima, nikijiuliza maswali mengi yasiyo na majibu.
Kwa mujibu wa maelezo ya baba, kama Mwankuga alikuwa amekufa, mwalimu Mwashambwa ambaye naye alikuwa naye kwenye lile tukio la kule porini, naye angekufa, jambo ambalo kidogo lilikuwa gumu kwangu kuliamini.
Kilichotokea siku hiyo, kuanzia kule porini tulikokuwa tumeenda kuchimba dawa na baba, kifo cha Mwankuga, kilichotokea kule makaburini na kelele za watu waliokuwa wakiituhumu familia yetu kuwa ya kichawi, vilinifanya nianze kumtazama baba kwa jicho la tofauti.
Basi siku hiyo ilipita nikiwa na mawazo mengi sana kuhusu yale matukio yaliyotokea, kila nilipokuwa nikifikiria, nilikosa majibu. Gumzo kubwa liliendelea kutawala kijijini kwetu kuhusu uchawi wa baba, kuna ambao walidiriki hadi kuja jirani na nyumba yetu na kuanza kutoa vitisho kwamba dawa yetu inachemka.
Nilifedheheka sana moyoni mwangu. Siku tatu baadaye, Mwankuga alizikwa kwenye makaburi ya kijiji huku msiba wake ukitawaliwa na vituko vya kishirikina vya hapa na pale ambavyo bado watu wengi waliendelea kuamini kwamba familia yetu inahusika.
Hatimaye Mwankuga alizikwa na kidogo zile kelele tulizokuwa tunapigiwa zikaanza kupungua. Hata hivyo, siku ya kwenda shule ilipofika (kipindi hicho bado nilikuwa nasoma Shule ya Msingi Makongorosi, Chunya) nilikumbana na unyanyapaa mkubwa sana shuleni.
Wanafunzi wenzangu walikuwa wakinitenga na kuniita mchawi, wakawa wanaituhumu familia yetu kwamba inahusika na vifo vya watu wengi waliokuwa wanakufa katika mazingira ya kutatanisha pale kijijini kwetu. Hata hivyo, kama baba alivyotufundisha wanafamilia wote, hatukutakiwa kujibizana na mtu yeyote, nikawa nasikiliza tuhuma zote bila kujibu chochote.
Shauku yangu kubwa ilikuwa ni kutaka kumuona mwalimu Mwashambwa kwa sababu kwa mujibu wa baba, na yeye alikuwa pamoja na marehemu Mwankuga siku waliyokuwa wanapigana kichawi na baba kule porini. Nilikuwa na shauku kubwa ya kumuona mwalimu huyo kwa sababu nilitaka kujifunza kitu juu ya uchawi na wachawi.
Niliamini kwa kumtazama tu, naweza kugundua kitu kilichokuwa kimejificha nyuma ya maisha yake. Hata hivyo, baadaye ulipowadia muda wa kipindi cha hesabu, mwalimu wa darasa alikuja na kutuambia kwamba mwalimu Mwashambwa alikuwa anaumwa sana hivyo asingeweza kuja shuleni wala kuingia darasani mpaka atakapopona.
“Kumbe ni kweli!” nilijikuta nimeropoka kwa sauti kubwa, kauli iliyosababisha wanafunzi wote pamoja na mwalimu wanigeukie pale nilipokuwa nimekaa, nikasikia miguno ya chinichini ikitawala darasa zima.
“Ni kweli nini?” mwalimu wetu wa darasa, Madam Timbuka alihoji huku akinifuata pale nilipokuwa nimekaa. Nilijisikia aibu kubwa iliyochanganyikana na hofu, sikujua nimjibu nini mwalimu huyo kwani ndani ya akili yangu, nilikuwa nimezipokea taarifa hizo za ugonjwa wa mwalimu Mwashambwa na kile alichoniambia baba kwamba mwalimu huyo alikuwa mchawi na walikuwa wakishirikiana na marehemu Mwankuga.
“Naongea na wewe Togolai, ni kweli nini?” alihoji tena Madam Timbuka, safari hii akiwa amenikaribia kabisa pale nilipokuwa nimekaa, nikaanza kubabaika huku hofu kubwa ikishindwa kujificha kwenye uso wangu.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 04:

ILIPOISHIA:
“Naongea na wewe Togolai, ni kweli nini?” alihoji tena Madam Timbuka, safari hii akiwa amenikaribia kabisa pale nilipokuwa nimekaa, nikaanza kubabaika huku hofu kubwa ikishindwa kujificha kwenye uso wangu.
SASA ENDELEA…
“Kwamba mwalimu wetu anaumwa. Nilisikia asubuhi nikawa siamini,” nilidanganya, nikamuona mwalimu Timbuka akishusha pumzi ndefu, wanafunzi wenzangu waliokuwa wakinitazama kwa shauku, nao walionesha kuridhika na majibu yangu.
Baada ya kutoa taarifa hizo, mwalimu Timbuka alitutaka tusipige kelele bali tuutumie muda huo kujisomea, akatoka na kutuacha wote tukiwa kimya. Moyoni mwangu niliendelea kujiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
“Kwa hiyo mwalimu Mwashambwa naye atakufa?” nilijiuliza moyoni wakati nikiendelea kutafakari taarifa za ugonjwa wa mwalimu wetu. Nilijaribu kuunganisha matukio, hofu ikazidi kuongezeka ndani ya moyo wangu. Bado sikutaka kuamini kwamba baba alikuwa mchawi na alikuwa akihusika na kilichokuwa kinaendelea.
Muda ulizidi kusonga mbele, hatimaye ukawadia muda wa mapumziko. Kwa kawaida, ilikuwa ikifika muda wa mapumziko, kengele inagongwa mara mbili kuashiria wanafunzi wote tutoke madarasani lakini siku hiyo, kengele iligongwa tofauti. Iligongwa mfululizo huku walimu wakiwa wameshatoka na kusimama mstarini, kila mmoja akionekana kuwa ‘siriasi’.
“Kuna nini kwani?” nilijiuliza wakati nikisimama na kutoka pamoja na wanafunzi wenzangu, tukaelekea mstarini huku kila mmoja akiwa na shauku kubwa ya kusikia kilichofanya tukusanyike muda huo, jambo ambalo siyo la kawaida.
Mwalimu mkuu wetu, Nyerema alisimama na kututaka wote kutulia na kumsikiliza alichokuwa anataka kutuambia.
“Ni siku mbaya kwetu, najua wote mnajua kwamba mwalimu wenu, Mwashambwa alikuwa anaumwa sana, taarifa mbaya ni kwamba hatunaye tena, tumepokea taarifa za kifo chake muda huu, nawaomba nyote mtulie na muwe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu, taratibu nyingine mtatangaziwa baadaye,” alisema mwalimu Nyerema, vilio vikaanza kusikika kutoka kwa wanafunzi.
Siyo siri nilipatwa na mshtuko mkubwa sana, sikutaka kuamini kwamba mwalimu Mwashambwa ameondoka. Niliunganisha matukio na kile nilichoelezwa na baba, nikawa siamini.
“Ina maana baba ndiye anayehusika na kifo cha mwalimu wetu pia?” nilijiuliza moyoni nikiwa bado nimesimama palepale. Nikiwa katika hali ile, nilihisi kuna mtu ananitazama, nikageukia kule mtu huyo alipokuwepo. Hakuwa mwingine bali mwalimu Timbuka ambaye alikuwa akinitazama kwa makini. Kwa ilivyoonesha, alikuwa akinitazama kwa muda mrefu, nikabaki kubabaika kwa sababu sikuelewa kwa sababu gani ananitazama namna ile.
Ili kuvunga, nilijichanganya na wanafunzi wengine na kuondoka eneo hilo, nikarudi darasani ambako wanafunzi wengi walikuwa wakiendelea kulia kwa uchungu. Baadaye kengele iligongwa tena, tukatoka na kwenda mstarini ambapo tulipewa utaratibu wa namna ya kushiriki msiba wa mwalimu wetu.
Wakati wanafunzi wengine wakifunga safari kuelekea kwa mwalimu Mwashambwa, mimi nilichepuka na kukimbilia nyumbani, moyoni nikiwa na dukuduku kubwa.
“Amekufa kama ulivyosema.”
“Si nilikwambia? Umeamini sasa!”
“Kwa hiyo wewe ndiyo umemuua? Kwani baba wewe ni mchawi?” nilijikuta nikimuuliza baba swali ambalo hata yeye hakulitegemea, akanitazama kwa macho ya ukali.
“Nani aliyekwambia mimi ni mchawi?”
“Nimesikia watu wakisema, hata shuleni kwetu kote watu wananinyooshea vidole wakisema eti mimi na wewe tunashirikiana uchawi,” nilisema huku nikitetemeka, baba akanisogelea kisha akashusha pumzi ndefu.
“Mwanangu Togolai, lazima ujue kwamba hapa kijijini sisi tuna maadui wengi sana kwa sababu ya kazi ninayofanya baba yako. Watu wengi wananionea wivu kwa sababu hakuna mganga mwenye nguvu kama mimi ukanda wote huu. Sasa maadui zangu wameanza kunizushia na kunichafulia sifa nionekane mchawi lakini siyo kweli, mimi ni mganga wala siyo mchawi,” alisema baba kwa sauti iliyojaa busara na upole.
Licha ya maneno yote yaliyokuwa yanazungumzwa na watu, nilikuwa nikiamuamini sana baba. Niliyaamini maelezo yote aliyonipa kwa asilimia mia moja, na mimi nikashusha pumzi ndefu kisha tukawa tunatazamana na baba.
“Ikitokea mtu mwingine yeyote anakutania au anakuzodoa kuhusu uchawi, naomba uje unieleze moja kwa moja, wakati mwingine inabidi tuwe wakali ili kulinda heshima yetu,” alisema baba kisha akainuka na kuniacha nimekaa palepale, nikawa naendelea kuyatafakari maneno aliyoniambia.
Japokuwa nilikuwa nampenda sana mwlimu Mwashambwa, sikuweza kuhudhuria kwenye msiba wake nikihofia macho ya watu kwani tayari maneno yalikuwa yamesambaa sana kwamba baba alikuwa anahusika na vifo vya ghafla vya watu wawili, Mwankuga na Mwashambwa vilivyotokea mfululizo.
Hatimaye mazishi yalifanyika lakini manenomaneno yalizidi kuwa mengi kadiri siku zilivyokuwa zinasonga mbele. Siku moja nikiwa shuleni, nilisikia wanafunzi wenzangu wakinitena kwamba mwisho wa ubabe wa familia yetu ulikuwa umefika kwa sababu wanakijiji walikaa kikao cha pamoja na kufikia maazimio ya kwenda kumleta mganga mashuhuri kutoka Chitipa, Malawi kwa ajili ya kuja ‘kuwanyoa’ uchawi watu wote waliokuwa wakihisiwa kuhusika na ushirkina pale kijijini kwetu, akiwemo baba.
“Baba nimesikia eti kuna mganga amefuatwa Malawi kuja kuwanyoa uchawi watu wote wanaotajwa kuhusika kusababisha viofo vya watu wasio na hatia hapa kijijini, ukiwemo wewe,” nilimwambia baba baada ya kurejea kutoka shuleni.
Tofauti na nilivyotegemea, baba hakuonesha kushtushwa na kitu chochote, akawa anaendelea kukatakata mizizi ya dawa nje ya nyumba yetu huku akisema kwamba wanajisumbua kwa sababu yeye siyo mchawi.
“Watanyoana wenyewe kwa wenyewe, mimi hakuna mtu anayeweza kunigusa,” alisema baba kwa kujiamini, nikakosa cha kuendelea kuzungumza. Maisha yaliendelea kusonga mbele, siku saba baadaye, mkutano wa wanakijiji ulitishwa kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Makongorosi ambapo wanakijiji wengi walikusanyika.
“Baba wewe huendi kwenye mkutano?”
“Siendi, kama unataka nenda kaniwakilishe, nina shughuli zangu muhimu siwezi kuziacha kwenda kusikiliza upumbavu wa watu wa kijiji hiki,” alisema baba kwa kujiamini.
Kwa kuwa siku hiyo sikuwa na kazi, ilibidi nifanye kama baba alivyoniambia, nikaenda kumuwakilisha ingawa nililazimika kukaa nyumanyuma, sikutaka watu wajue kwamba niko pale. Niweke wazi kwamba tuhuma zilizokuwa zinamkabili baba na familia yetu kwa jumla zilitufanya tuikose amani kabisa.
Kila tulipokuwa tukionekana, ilikuwa ni lazima tunyooshewe vidole, jambo ambalo binafsi liliniathiri sana kisaikolojia. Nikapoteza kabisa uwezo wa kujiamini, nikawa naishi kama digidigi, hali kadhalika kwa ndugu zangu wengine ingawa kwa baba yeye alionekana kutojali chochote.
“Tumechoshwa na uchawi hapa kijijini kwetu. Kwa pamoja tumefanikisha ujio wa mganga Mabwanji kutoka Malawi kwa lengo la kusafisha kijiji chetu. Wale wote waliokuwa wanaringia uchawi wao, kiboko yao amewasili, karibu uwasalimie wanakijiji,” alisema mzee wa kimila pale kijijini ambaye tulizoea kumuita Mwene.
Mwanaume mzee mwenye macho mekundu sana na midomo myeusi, akiwa amejifunga shuka refu lenye rangi nyekundu na nyeusi, kichwani akiwa amejifunga kitambaa cheusi, shingoni akiwa na hirizi kadhaa na shanga, alisimama na kunyoosha juu mkia wa mnyama ambaye sikuwa namjua, watu wote wakashangilia kwa nguvu.
“Sina mengi ya kuzungumza, naomba ushirikiano wenu tuwakomeshe wachawi wa kijiji hiki,” alisema mwanaume huyo kwa Kiswahili kibovu, watu wakashangilia tena kwa nguvu kisha Mwene akaendelea na maelezo, akisisitiza kwamba kazi lazima ianze siku hiyohiyo usiku.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 
SEHEMU YA 05:

ILIPOISHIA:
MWANAUME mzee mwenye macho mekundu sana na midomo myeusi, akiwa amejifunga shuka refu lenye rangi nyekundu na nyeusi, kichwani akiwa amejifunga kitambaa cheusi, shingoni akiwa na hirizi kadhaa na shanga, alisimama na kunyoosha juu mkia wa mnyama ambaye sikuwa namjua, watu wote wakashangilia kwa nguvu.
SASA ENDELEA…
“Sina mengi ya kuzungumza, naomba ushirikiano wenu tuwakomeshe wachawi wa kijiji hiki,” alisema mwanaume huyo kwa Kiswahili kibovu, watu wakashangilia tena kwa nguvu kisha Mwene akaendelea na maelezo, akisisitiza kwamba kazi lazima ianze siku hiyohiyo usiku.
Baada ya maelezo marefu yaliyojaa vitisho kwa watu waliokuwa wakitajwa kuhusika na uchawi, mkutano uliahirishwa, watu wakatawanyika huku kiongozi huyo wa kijiji akiwataka watu wote kutoa ushirikiano kwa mganga Mabwanji atakapoenda kuwatembelea kwenye nyumba zao.
Hofu niliyokuwa nayo ilikuwa kubwa mno, kwa jinsi watu walivyokuwa wanatuchukia pale kijijini nilijua lazima moto utawaka. Baadhi ya wazee waliokuwa wanaheshimika pale kijijini, walianza maandalizi ya kumsaidia mganga huyo kwa kila alichokuwa anakihitaji, dawa zikaandaliwa na hatimaye muda uliokuwa ukisubiriwa na wengi ukawadia.
Saa tatu juu ya alama usiku, kazi ya kuzunguka kwenye nyumba za watu waliokuwa wakishukiwa kuwa wachawi ilianza, kutokana na jinsi nilivyokuwa na shauku kubwa ya kutaka kuona kazi hiyo inavyofanyika, nilichomoka nyumbani kimyakimya na kwenda kushuhudia licha ya kwamba baba alitutaka wote tukae ndani kwa sababu siku hiyo ilikuwa mbaya kwa familia yetu.
Mtu wa kwanza kufuatwa alikuwa ni mwanamke mjane ambaye tulizoea kumuita mama Chinga, Mmakonde kutoka Kusini ambaye alikuwa akifanya kazi ya kupika pombe za kienyeji.
Kwa kipindi kirefu nilikuwa nikisikiasikia kwamba eti mwanamke huyo alikuwa akitumia viungo vya binadamu kupikia pombe zake ndiyo maana alikuwa na wateja wengi sana hapo kijijini. Tangu nikiwa mdogo niliaminishwa kwamba eti ule ambao huwa tunaona kama ni mwiko mkubwa anaoutumia kukorogea mapipa yake ya pombe, ulikuwa ni mkono wa binadamu.
Watu hao walipofika, huku ngoma ikipigwa na pembe za wanyama zikipulizwa, kila mtu akiwa ameshika tochi za kienyeji ambazo hutengenezwa kwa kuviringisha matambara mbele ya kipande cha mti kisha kuchovya kwenye mafuta ya taa, nyumba yake ilizungukwa kisha mganga akaanza kazi yake.
Akawa anafanya uchawi wake pale, mara afukue kwenye kona ya nyumba na kutoa hirizi kubwa, mara afukue pembeni ya mlango na kutoa fuvu la mnyama wa ajabu, yaani ilikuwa ni patashika nguo kuchanika.
Mwanamke huyo na yeye akatolewa na kukalishwa chini, mbele ya nyumba yake, akapakwa unga mweupe kichwani na kuanza kunyolewa nywele huku ngoma zikiendelea kupigwa, mganga akawa anaimba nyimbo za ajabu na kumtolea vitisho vingi mwanamke huyo kwamba akirudia tena kujihusisha na uchawi lazima atakufa.
Baada ya zoezi hilo lililochukua karibu saa zima, watu wote waliondoka na kumuacha mwanamke huyo akilia kwa uchungu, huku akiendelea kusisitiza kwamba yeye siyo mchawi wala haujui uchawi. Safari ya kuelekea kwenye nyumba nyingine ikaanza, na mimi nikawa nawafuata kwa nyuma.
Cha ajabu, niliwaona wakielekea nyumbani kwetu, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kuliko kawaida, sikujua mwisho wake utakuwaje. Walipofika, walifanya kama walivyofanya kwa yule mwanamke, wakaizunguka nyumba yetu huku wakiimulika na tochi za kienyeji, ngoma ikawa inapigwa huku mganga akiimba nyimbo ambazo hakuna aliyekuwa anazielewa.
Akawa anazunguka huku na kule kama anayetafuta kitu fulani pale nje kwetu, ghafla nikaona mlango ukifunguliwa, baba akatoka kwa kasi na kuwapita watu wote, akasogea mpaka pale yule mganga alipokuwa amesimama, wakawa wanatazamana.
“Ni nani aliyekupa mamlaka ya kuingia kwenye miji ya watu na kutapeli ukijifanya unawatoa watu uchawi?”
“Wewe ni nani wa kunihoji maswali hayo? Wewe ni mchawi na wanakijiji wenzako wamekuchoka hapa kijijini. Hii safari ya ujio wangu ni kwa ajili yako, lazima nikunyooshe.”
“Wewe bado ni mwepesi sana kwangu, huna ubavu wa kushindana na mimi. Isitoshe mimi siyo mlozi kama wewe, mimi ni mtaalamu, tena gwiji,” alisema baba kwa sauti ambayo niliisikia vizuri kisha baada ya hapo akageuka na kurudi ndani, nikamuona yule mganga akivuta na kutoa pumzi ndefundefu kama anayejiandaa kufanya tukio moja kubwa sana.
Alipoingia ndani na kufunga mlango, huku nje yule mganga aliendelea kuzunguka huku na kule, wasaidizi wake wakawa wanampigia manyanga na kumuimbia nyimbo ambazo walizielewa wenyewe.
“Inatakiwa tumkamate kwa nguvu na kumtoa nje, anaonyesha ni jeuri sana,” alisema mganga huyo kwa Kiswahili kibovu, watu wote wakawa wanatingisha vichwa kuonyesha kukubaliana na alichokuwa anakisema.
Nilijikuta nikitetemeka sana pale nilipokuwa nimejibanza, nikajua arobaini za baba zilikuwa zimewadia. Japokuwa bado sikuwa na majibu kamili kichwani mwangu kama baba ni mganga au mchawi, bado sikukubaliana na kitendo alichokuwa anataka kufanyiwa kwa sababu ulikuwa ni udhalilishaji wa hali ya juu.
Wakati kundi la wanaume wakijiandaa kuingia ndani kwa nguvu na kuvunja mlango, nilimuona baba akitoka kwa kujiamini, kifua akiwa amekitanguliza mbele na kusimama tena mbele ya mganga, wale watu wote wakamzunguka kisharishari.
“Mnataka kutumia nguvu kunikamata? Hivi mna akili timamu nyie? Haya mwenye ubavu anyooshe mkono wake na kunigusa,” alisema baba kwa hasira. Nilibaki namshangaa baba kwani sikujua amepata wapi ujasiri wa kiasi kile. Kauli hiyo iliwashtua hata wale watu waliokuwa wanataka kumkamata, nikaona wote wakirudi nyuma lakini mganga aliendelea kusisitiza kwamba ni lazima wamkamate kwa nguvu.
Watu wote walipojaribu kufanya hivyo, tulishtuka kuona kimbunga kikubwa ambacho hata sikujua kimetokea wapi, kikianza kuvuma kwa nguvu pale baba alipokuwa amesimama, vumbi jingi na takataka za kila aina zikawa zinarushwa huku na kule, kufumba na kufumbua, baba hakuwepo tena eneo hilo.
Wale watu wote, akiwemo na mganga mwenyewe, walibaki wamepigwa na butwaa, kila mmoja akawa anajifuta vumbi. Sikuwahi kushuhudia kimbunga kikubwa kikitokea, tena usiku kama ule, nikabaki na maswali mengi yaliyokosa majibu.
“Ametukimbia! Ametukimbia!” alisema yule mganga kwa sauti ya juu, huku na yeye akionyesha dhahiri kuwa na taharuki kubwa ndani ya moyo wake.
“Siwezi kuwakimbia kwa sababu hakuna wa kunitisha hata mmoja kati yenu,” ilisikika sauti ya baba kisha nikashangaa kumuona akitokea gizani na kurudi tena pale alipokuwa amesimama awali, nikaona watu wote wakianza kurudi nyuma kwa hofu kubwa kwa sababu walishajua baba anaweza kufanya chochote muda wowote.
“Nataka hili liwe funzo kwako na kwa watu wengine wenye akili kama zako,” alisema baba kwa kujiamini huku akiendelea kumsogelea yule mganga, akafanya ishara kama ananyonga kitu kwa nguvu, kufumba na kufumbua mganga yule alidondoka chini na kuanza kutapatapa kama anataka kukata roho.
Kuona hivyo, watu wote waliokuwa wameandamana na mganga huyo, walitimua mbio, kila mmoja kuelekea njia yake na muda mfupi baadaye, wote walikuwa wametokomea gizani, ikabidi nitoke pale nilipokuwa nimejibanza huku na mimi nikiwa na hofu kubwa ndani ya moyo wangu.
“Hebu beba huko miguuni tuutoe huu mzoga hapa,” alisema baba, akimaanisha tumtoe yule mganga.
Huku nikitetemeka nilisogea mpaka pale yule mganga alipokuwa amelala, akiendelea kukoroma kwa nguvu, mimi nikamshika miguuni na baba akamshika kichwani, tukaanza kumkokota kumtoa nje ya eneo letu, tukaenda kumbwaga pembeni kabisa kwenye vichaka kisha tukarudi ndani. Ile tunaingia ndani tu, tukasikia mlango ukigongwa kwa nguvu.
Je, nini kitafuatia? Usikose
 
SEHEMU YA 06:

ILIPOISHIA:
Huku nikitetemeka, nilisogea mpaka pale yule mganga alipokuwa amelala, akiendelea kukoroma kwa nguvu, mimi nikamshika miguuni na baba akamshika kichwani, tukaanza kumkokota kumtoa nje ya eneo letu, tukaenda kumbwaga pembeni kabisa kwenye vichaka kisha tukarudi ndani. Ile tunaingia ndani tu, tukasikia mlango ukigongwa kwa nguvu.
SASA ENDELEA…
“Nani!”
“Fungua!”
“Sifungui mpaka mjitambulishe na mueleze shida yenu.”
“Ni mimi mzee Sifuni, mwenyekiti wa kijiji.”
“Unaonekana hauko peke yako!”
“Ndiyo, nimeongozana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama ya kijiji, fungua tafadhali,” baada ya mwenyekiti huyo kusema hivyo, baba alinioneshea ishara kwa mkono kwamba niende ndani kwa sababu alishahisi wale watu wamekuja kwa shari. Nikatii nilichoambiwa na kwenda chumbani lakini bado nilikuwa na shauku kubwa ya kutaka kuona kinachoendelea.
Baba alipofungua tu mlango, nilisikia wakimuamrisha jambo:
“Upo chini ya ulinzi.”
“Kwa kosa gani?”
“Kwa kumshambulia mganga wa kienyeji aliyekuwa anatimiza majukumu yake hapa kijijini kwetu.”
“Hivi nyie mna wazimu nini? Mbona mnanifuatafuata sana? Sasa anayejiona mbabe aniguse,” nilimsikia baba akifoka kwa jazba. Yule mwenyekiti akawa anaawamrisha mgambo wamkamate baba lakini kila mmoja akawa anamtupia mpira mwenzake kwa hofu.
Nadhani lile tukio la ‘kumzimisha’ mganga ambaye kila mmoja alikuwa akimuona kama ni kiboko, liliwajaza hofu kubwa ndani ya mioyo yao. Baadaye niliwasikia wakiondoka huku wakitoa maneno ya kumtisha baba kwamba eti siku zake zinahesabika, wakaelekea ule upande tulikomtupia yule mganga ambaye bado alikuwa akiendelea kukoroma kama anayetaka kukata roho.
Wakamchukua na kuondoka naye ambapo taarifa tulizozipata kesho yake ni kwamba alisafirishwa usiku huohuo kuelekea nyumbani kwao, Malawi akiwa na hali mbaya sana. Siku zilizidi kusonga mbele, uhasama kati ya familia yetu na wanakijiji wengine ukazidi kushamiri pale kijijini, kila mtu akawa anatuchukia na kutusema vibaya.
Wiki kadhaa baadaye, siku hiyo nikiwa narejea kutoka shuleni, nilipata taarifa kwamba yule mganga kutoka Malawi amerejea tena na safari hii, amekuja na jeshi la waganga wengine kadhaa kwa lengo la kuja kumkomesha baba kwa alichomfanyia.
Taarifa hizo zilinishtua sana, ikabidi nimfikishie baba haraka lakini tofauti na nilivyotegemea, alizipokea kwa dharau na kuendelea kusisitiza kwamba yeye siyo mchawi bali mganga na yeyote atakayethubutu kumuingilia kwenye mambo yake, atamshikisha adabu.
Niliishiwa maneno, ikabidi nikae kimya kusubiri kuona mwisho wa hayo yote utakuwa nini. Taarifa za ujio wa waganga hao kutoka Malawi zilizidi kusambaa kwa kasi ya kimbunga, wanakijiji wengi wakawa wanaonesha kufurahia ujio wao.
Hatimaye siku moja usiku, tukiwa tumemaliza kupata chakula cha usiku, kundi la wanakijiji wengi liliwasili pale nyumbani kwetu, wakiongozwa na wale waganga ambao jumla yao walikuwa watano.
Wakaizunguka nyumba yetu huku watu wakipiga kelele kwa nguvu wakitaka eti baba akomeshwe. Siyo kwamba namtetea baba yangu lakini binafsi, mpaka muda huo nilikuwa sielewi kwa sababu gani watu wanamchukia kiasi hicho wakati hakuwa mchawi kama mwenyewe alivyokuwa anasema bali mganga.
Vifo vya wanakijiji wawili, Mwankuga na Mwashambwa havikuwa vigezo vya kumuita baba mchawi kwa sababu wao ndiyo walioanza kumchokoza na mimi nilikuwepo siku hiyo. Nikawa nahisi kwamba huenda ni chuki za watu ndizo zilizosababisha yote hayo.
“Anyolewe! Anyolewe!” ule umati uliokuwa nje ya nyumba yetu ulikuwa ukipiga kelele kushinikiza eti baba anyolewe uchawi. Baba akatutaka wote tutulie ndani na asiwepo wa kutoka nje hata mmoja, akaingia kwenye chumba chake cha uganga na muda mfupi baadaye, alitoka mpaka nje kulikokuwa na wale watu.
Hata sijui nini kilitokea lakini muda mfupi baadaye tulisikia vishindo vya watu wakikimbia, huku wengine wakipiga kelele za kuombamsaada, muda mfupi baadaye tukamsikia baba akiiingia ndani na kufunga mlango, huku akitukana peke yake kuonesha jinsi alivyokuwa na hasira.
Muda mfupi baadaye alituita wanafamilia wote, akiwemo na mama, akaanza kutuambia kwamba pale kijijini hapafai tena sisi kuendelea kuishi kwa sababu tulikuwa na maadui wengi na kila mmoja alikuwa akijitahidi kadiri ya uwezo wake kutuangamiza.
Akasema anajiamini kwamba anaweza kuilinda vizuri familia yake kwa maana ya kujilinda yeye mwenyewe, sisi pamoja na mali zetu zote lakini akasema kuwa si vizuri kuishi mahali ulipozungukwa na maadui.
“Sasa tutafanya nini mume wangu?”
“Inabidi tuhamie mjini,” alisema baba, wote tukawa tunamtazama kwa macho ya shauku kubwa. Sisi tulizaliwa Makongorosi na maisha yetu kwa asilimia kubwa yalikua pale kijijini, hakuna aliyewahi kuishi nje ya pale, tukawa tunashangazwa na kauli ile ya baba ingawa kiukweli, mimi binafsi nilikuwa natamani sana kuishi mjini.
Alitwambia kwamba kuna rafiki yake wa siku nyingi waliyekuwa wakisoma pamoja, amewahi kumpa mwaliko wa kwenda kumtembelea jijini dar es Salaam na kuahidi kumpa hifadhi, akatuambia kwamba anadhani huo ndiyo muda muafaka wa sisi kuhamia Dar es Salaam.
Kiukweli, japokuwa nilikua nimeshinda nikiwa kama mgonjwa kutokana na hali halisi ya matukio yaliyokuwa yakiendelea kututokea, habari kwamba tunahama kutoka Makongorosi, Chunya mpaka Dar es Salaam zilinifurahisha mno.
Baba alifunga kikao na kututaka wote tuanze kujiandaa kwa sababu muda wowote mambo yatakapokuwa tayari, tutasafiri lakini akatusisitiza kutomweleza yeyote kuhusu suala hilo, tukakubaliana naye. Usingizi ulikuwa mtamu sana siku hiyo, kila mmoja akawa anafikiria namna tutakavyoenda kuyaanza maisha mapya jijini Dar es Salaam.
Si mimi peke yangu ambaye nilikuwa nimechoshwa na kashfa za kuitwa mtoto wa mchawi, famili ayetu nzima ilikuwa imechoshwa. Basi siku hiyo ilipita, kesho yake tukaamka asubuhi lakini baba ndiye aliyekuwa wa kwanza, tukamkuta yupo nje, akatusisitiza kwamba sote hatutakiwi kutoka kabisa hapo nyumbani siku hiyo kwa sababu za kiusalama.
Alinisisitiza zaidi mimi kwa sababu mara zote ndiyo nilikuwa namtoroka na kwenda mitaani, nikamuahidi kwamba sitaondoka. Basi baadaye baba aliondoka, hatukujua ameenda wapi, tukaendelea na maandalizi ya safari huku kila mmoja wetu akionesha kuwa na furaha kubwa moyoni mwake.
Baada ya kama saa mbili hivi kupita, tulimuona baba akija akiwa ameongozana na wanaume wawili walioonesha kwamba siyo wakazi wa Chunya, akaja nao mpaka pale nyumbani, akatutambulisha kwamba ni wateja waliokuwa wanatafuta shamba la kununua. Baba akatuomba familia nzima tukubali kuuza shamba letu moja kwa ajili ya kupata fedha za safari.
Nilichokuwa nampendea baba ni hapo tu, alikuwa anapenda sana demokrasia linapokuja suala la mambo ya familia, tulikubali na kwa akaniita mimi niongozane naye mpaka kwenye shamba letu moja. Wakaanza kupimishiana na baada ya kukubaliana kila kitu, walihesabiana fedha, wakaandikishana kisha tukaondoka kurudi nyumbani.
Wale wageni waliaga na kuondoka, baba akatuita tena ndani na kuanza kuhesabu fedha zilizopatikana. Zilikuwa ni shilingi milioni mbili na laki tatu, akasema zingetosha kabisa kwa safari yetu. Tukakubaliana kwamba tumalizie maandalizi na asubuhi ya siku ya pili tuianze safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam.
Je, nini kitafuatia? Safari ya Dar itawezekana?
 
SEHEMU YA 07:


ILIPOISHIA:
Wale wageni waliaga na kuondoka, baba akatuita tena ndani na kuanza kuhesabu fedha zilizopatikana. Zilikuwa ni shilingi milioni mbili na laki tatu, akasema zingetosha kabisa kwa safari yetu. Tukakubaliana kwamba tumalizie maandalizi na asubuhi ya siku ya pili tuianze safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam.
SASA ENDELEA…
Kweli usiku huo hakuna hata aliyepata lepe la usingizi, ‘kimuhemuhe’ cha safari kilitufanya tukae macho mpaka jogoo la kwanza lilipokuwa linawika. Baba alituagiza kwamba tubebe vile vitu vya muhimu tu kwa sababu maisha ya kijijini yalikuwa tofauti sana na maisha ya mjini.
Akatuambia vitu vingine tuviache palepale na vitakuwa salama kwa sababu kuna walinzi anawaacha kwa ajili ya kutulindia mji wetu. Aliposema walinzi sikumuelewa kwa haraka anamaanisha nini, akili nyingine zikanituma kuamini kwamba labda watakuwa ni mgambo lakini nilijiuliza anaweza kuwaacha mgambo ndiyo walinde nyumba yetu wakati hawakuwa wakielewana? Sikupata majibu.
Saa kumi na nusu za usiku, tulitoka na kuanza kutembea kuelekea stendi, kila mmoja akiwa na mzigo wake. Tukaenda mpaka stendi ambapo tulipanda gari la kwanza kabisa ambalo lilikuwa likielekea Mbeya mjini, lakini cha ajabu, wakati wote tumeshapanda kwenye gari, baba yeye alibaki chini.
Tukawa tunasubiri na yeye apande lakini hakufanya hivyo, sanasana tukamuona akiwa anazungumza na mama, kupitia dirisha la gari lile tulilokuwa tumepanda, nadhani alikuwa akimpa maelekezo muhimu sana kwa sababu muda wote mama alikuwa akitingisha kichwa kuashiria kuelewa kile alichokuwa akiambiwa.
Baada ya kumaliza kuzungumza na mama, baba alikuja moja kwa moja pale nilipokuwa nimekaa mimi, akanipa mkono na kuniambia kwamba tutangulie yeye atafuata, akaniambia ananiamini mimi zaidi kwa hiyo lazima niwe makini kuwalinda ndugu zangu.
Nilijisikia fahari sana kwa jinsi baba alivyokuwa akinipa kipaumbele kwenye mambo ya msingi japokuwa nilikuwa na kaka zangu na mimi ndiyo nilikuwa mdogo. Baada ya dakika chache, dereva aliingia ndani ya gari, akawasha na safari ya kutoka Makongorosi kuelekea Mbeya mjini ikaanza.
Safari haikuwa nyepesi, kwa sababu sehemu kubwa ya njia ya kutokea Chunya kuelekea Mbeya mjini, ni milima na mabonde makubwa, ikiambatana na miteremko ambayo kama dereva hayupo makini hamuwezi kufika salama. Ukizingatia na lile giza la alfajiri ile, kila mmoja alikuwa akiomba moyoni tufike salama. Baada ya safari ndefu, hatimaye tuliwasili Mbalizi, gari likashusha baadhi ya abiria na kuingia Barabara Kuu ya Mbeya-Tunduma ambayo ni ya lami, likaendelea na safari ya kuelekea Mbeya Mjini.
Nikiri kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kufika mjini na kila kitu kwangu kilikuwa kigeni. Sikuwahi kuona barabara ya lami, sikuwahi kuona magari mengi ya kila aina wala sikuwahi kuona nyumba nzuri na za kisasa, nyingine zikiwa na maghorofa.
Ilikuwa ni safari ambayo iliufurahisha mno moyo wangu, nikawa nachekacheka tu mwenyewe. Hali ilikuwa hivyohivyo kwa ndugu zangu wengine ambao nao walikuwa na ushamba ulioonekana waziwazi kwenye sura zao. Safari yetu ilienda kuishia kwenye Stendi Kuu ya Mabasi ya Mbeya au maarufu kama Mbeya Terminal.
Cha ajabu, wakati gari likikata kona kuelekea sehemu ya kushushia abiria, nilimuona baba akiwa chini, akilitazama gari tulilokuwa tumepanda. Nikabaki na maswali mengi yasiyokuwa na majibu, kwamba alifikaje kabla yetu? Kumbukumbu zangu zilinionesha kwamba kule Chunya, stendi kulikuwa na gari moja tu ambalo ndiyo hilo ambalo sisi tulipanda.
Na safari nzima, hatukupitwa na gari lingine lolote, wala chombo kingine cha usafiri, si bodaboda wala Bajaj, sasa baba alifikaje pale kabla yetu? Yalikuwa ni maswali ambayo sikuwa na majibu yake. Lakini cha ajabu, nilipomgeukia mama wala hakuonesha kushtushwa na uwepo wa baba eneo lile, nikamuona akimpungia mkono kama anayemwambia ‘tuko hapa’.
Gari liliposimama, baba ndiye aliyekuwa akitupokea mizigo, ndugu zangu wote walionekana kuchukulia uwepo wa baba eneo lile kama kitu cha kawaida, kwa kifupi hakuna aliyekuwa na akili ya udadisi kama niliyokuwa nayo mimi, nadhani ndiyo maana baba alikuwa akinipenda zaidi yao.
Alitupokea mizigo na kutusaidia kushuka, tukasimama pembeni ya gari, mimi nikawa namtazama nikiwa sina majibu ya maswali yangu kabisa. Mimi na ndugu zangu wote tulikuwa tumechafuka miili yetu kwa sababu ya kusafiri kwenye barabara ya vumbi kutoka Chunya lakini baba yeye alikuwa msafi kabisa.
“Tunasafiri na basi lile pale,” alisema baba kwa sauti ambayo wote tuliisikia vizuri, akatuonesha kwenye basi kubwa lililokuwa limeinama upande wa mbele kama ndege ya kijeshi, wote tukawa tunalitazama basi lile kwani muundo wake ulikuwa wa aina yake na sidhani kama kuna yeyote kati yetu ambaye aliwahi kuliona basi kama hilo kwa macho.
Basi tulibeba vifurushi vyetu na kuanza kumfuata baba ambaye alitupeleka mpaka kwenye lile basi, yeye akawa wa kwanza kuingia, akawa anatusaidia kupanda ngazi mmoja baada ya mwingine. Wa mwisho alikuwa mama ambaye alikuwa na mzigo mkubwa, baada ya kuingia, baba alianza kusoma namba za siti zilizokuwa zimeandikwa upande wa juu wa basi hilo kubwa, mpaka alipozipata.
Kila mtu alikuwa na siti yake, akawa anatuelekeza sehemu za kukaa, akampa mama tiketi zetu wote kisha nikamuona akizungumza naye mambo fulani, akaingiza mkono mfukoni na kutoa noti kadhaa za shilingi elfu kumikumi, mama akamshukuru, kisha akamuinamia sikioni na kumuongelesha mambo ambayo hakuna aliyesikia.
(Tembelea Simulizi za Majonzi )
Wakati akimnong’oneza mama, macho ya baba yalikuwa kwangu, nilipoona ananiangalia, ikabidi nikwepeshe macho yangu kwani tulifundishwa kwamba siyo heshima kuwatazama baba na mama wanapokuwa na mazungumzo yao ya siri.
Baada ya hapo, alikuja pale nilipokuwa nimekaa, akaniinamia na kurudia kuniambia maneno yaleyale aliyoniambia wakati tukiondoka kule Chunya. Aliniambia kwamba ukimtoa mama, mimi ndiye niliyepaswa kuwa mkuu wa msafara na lazima nihakikishe tunafika salama salmini tuendako, akanipigapiga mgongoni kisha akanipa mkono.
Alifanya hivyohivyo kwa ndugu zangu wengine pia, akawapa mkono mmoja baada ya mwingine kisha akarudi kwangu na kuniambia kwamba tutangulie yeye anafuata.
“Lakini baba… sisi wote ni wageni huko tunakoenda, kwa nini usikae na sisi kwenye hili basi? Tukipotea je?” nilimuuliza, swali lililomfanya anitazame usoni kwa makini, nikakwepesha macho yangu kwa sababu baba alikuwa na hali fulani ambayo akikukazia macho lazima utazame pembeni.
“Kwani kutoka Chunya kuja hapa nani alikuwa wa kwanza kufika?” aliniuliza, swali lililonifanya nipate nafasi ya kutoa dukuduku nililokuwa nalo moyoni.
“Tena nilitaka kukuuliza, kwani ulikuja na usafiri gani na kwa nini wewe hujachafuka kama sisi?”
‘Wewe ni mwanaume, lazima ujifunzwe kuwa na akiba ya maneno, siyo kila unachokiona ukizungumze au uulize, sijakuzaa kuja kuwa msindikizaji maishani mwako,” alisema kwa sauti ya chini ambayo ni mimi tu niliyeisikia lakini ilityokuwa imebeba ujumbe mzito sana ndani yake, nikashusha pumzi na kukaa vizuri kwenye sitio yangu.
Tayari dereva alishaanza kupiga ‘resi’ nyingi na kupiga honi, kuoneshakwamba muda mfupi baadaye safari ingeanza. Baba akatenbea harakaharaka kuelekea kwenye mlango wa kushukia, akateremka mpaka chini na akusimama upande ule tuliokuwa tumekaa, gari likaanza kuondoka ambapo alitupungua mikono, na sisi tukafanya hivyo.
Safari ikaanza, hiyo ilikuwa ni karibu saa kumi na mbili na nusu, basi likaanza kuchanja mbuga kuelekea Dar es Salaam.
Baada ya kusafiri umbali mfupi, tukiwa tumefika eneo maarufu liitwalo Mlima Nyoka, lililokuwa kilometa chache kutoka Uyole mjini, tulishangaa kuanza kuona gari likiyumbayumba. Nilikuwa nikisikia sifa za eneo hilo mara kwa mara kwamba magari mengi, hasa ya abiria yalikuwa yakipata ajali na kuua abiria wengi, mapigo ya moyo yakawa yananienda mbio kuliko kawaida.
Kulikuwa na mteremko mkali wenye kona za hatari, na baada ya kuvuka daraja kulikuwa na mlima mkali pia, jambo ambalo lilimaanisha kama dereva akishindwa kulimudu gari, ajali yake ingekuwa si ya mchezo. Dereva alizidi kuyumba huku gari likiongeza kasi, hali iliyofanya abiria waanze kupiga kelele kwa nguvu, wengi wakilitaja jina la Mungu.
Gari lilizidi kuongeza kasi, likawa linashuka kwenye mteremko huo kwa kasi kubwa huku likiendelea kuyumba huku na kule, kelele ndani ya basio zikazidi kuongezeka.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 08:


ILIPOISHIA:
Dereva alizidi kuyumba huku gari likiongeza kasi, hali iliyofanya abiria waanze kupiga kelele kwa nguvu, wengi wakilitaja jina la Mungu.
Gari lilizidi kuongeza kasi, likawa linashuka kwenye mteremko huo kwa kasi kubwa huku likiendelea kuyumba huku na kule, kelele ndani ya basi zikazidi kuongezeka.
SASA ENDELEA…
Katika hali ambayo hata sielewi ilikuwaje, nilijikuta nikipata nguvu na kusimama, nikawa natazama nje kwa kupitia kioo cha dereva. Cha ajabu na cha kushtua, nilimuona baba akiwa anapigana na mtu ambaye sikumtambua ni nani, pembeni ya barabara.
Kwa macho yangu, nikamshuhudia baba akimpiga yule mtu kwa nguvu, akamdondosha chini na kuanza kumbamiza kwenye lami, damu nyingi zikatapakaa eneo lote.
Kufumba na kufumbua, nilishtukia baba akiwa ameshika usukani wa lile basi tulilokuwa tukisafiria, sikuwahi kumuona baba hata siku moja akiendesha gari lakini eti siku hiyo ndiyo alikuwa ameshika usukani. Sikukumbuka ameingiaje ndani ya basi, tena likiwa katika mwendo mkali kiasi kile.
Kila kitu kilifanyika kwa kasi kama ya radi, akamtoa dereva na kumsukumia pembeni, akaanza kubadilisha gia huku akiwa ameung’ang’ania usukani, katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, gari liliacha kuyumbayumba ingawa halikupunguza mwendo, likawa linazidi kukimbia kwa kasi kubwa, likishuka kwenye mteremko mkali maarufu kama Mlima Nyoka.
Abiria wote walitulia, hata wale waliokuwa wakipiga kelele, walikaa kimya, wakawa wanaendelea kumuomba Mungu ndani ya mioyo yao, hakuna aliyeona mabadiliko yaliyofanyika upande wa dereva zaidi ya mimi nadhani na watu wachache waliokuwa wamekaa mbele.
(Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi)
Nilimshuhudia baba akiendelea kupangua gia kwa kasi, gari likaanza kupunguza mwendo na mita chache mbele, alifunga breki, gari likaserereka na hatimaye likasimama kandokando ya barabara, watu wote waliokuwa ndani ya basi walianza kushangilia na kumpongeza dereva huku wakikimbilia kwenye mlango wa kutokea nje.
Harakaharaka na mimi nilielekea kule mbele lakini lengo langu kubwa ilikuwa ni kwenda kumuuliza baba nini kilichotokea maana sikuwa naelewa chochote.
Cha ajabu, nilipofika pale kwenye siti ya dereva, nilimuona yule dereva ambaye ndiye aliyetoka na sisi Mbeya mjini akiwa ameegamiza kichwa kwenye usukani, akiwa ni kama amepitiwa na usingizi.
Nilibaki nashangaa kwa sababu kitendo cha kuinuka kutoka pale kwenye siti niliyokuwa nimekaa mpaka pale kwa dereva, sikuwa nimetumia hata dakika moja kamili, zilikuwa ni sekunde tu lakini eti baba hakuwepo tena na aliyekuwa amekaa pale kwenye usukani alikuwa ni dereva.
Niligeuka huku na kule kutazama kama nitamuona baba lakini sikumuona, abiria walikuwa wakiendelea kugombea kutoka na muda mfupi baadaye, wote walikuwa wameshateremka, kila mmoja akawa anamshukuru Mungu wake. Yaani kama ingetokea ajali, kwa jinsi mteremko ulivyokuwa mkali, sidhani kama kuna mtu angetoka salama ndani ya basi lile.
Ilibidi nimguse begani yule dereva ambaye bado alikuwa amelala na kuegamia usukani ili nimuulize nini kilichotokea. Cha ajabu, nilipomgusa, alishtuka sana, akawa ni kama aliyezinduka kutoka kwenye usingizi mzito, akawa anageuka huku na kule. Hakukuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya gari, isipokuwa mimi na yeye tu.
“Nini kimetokea? Hatujapata ajali? Mungu wangu,” alisema yule dereva huku akianza kujikagua mwili wake. Nilishangazwa sana na hali ile, yaani kumbe na yeye hakuwa anaelewa kilichotokea kwa hiyo kama zisingefanyika jitihada zile, ni kweli tungepata ajali mbaya sana.
“Kwani wewe unakumbuka nini?” nilimuuliza.
“Wakati tunauanza huu mteremko wa Mlima Nyoka, nilianza kuhisi kizunguzungu, nikajaribu kupunguza mwendo ili nisimame lakini cha ajabu, badala ya kukanyaga breki nilikanyaga mafuta, gari likaongeza mwendo na kizunguzungu kikazidi, sikumbuki tena kilichotokea,” alisema yule dereva huku akiendelea kugeuka huku na kule.
(Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi)
“Tushuke,” nilimwambia, harakaharaka akafungua mlango na kushuka, na mimi nikashuka. Wale abiria waliokuwa chini, walimzunguka dereva na kuanza kumpongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya. Ilibidi awe anaitikia tu lakini kiukweli hakuwa anajua nini kimefanyika na imekuwaje mpaka basi limesimama.
Akiwa anaendelea kupongezwa, tabasamu la uongo likiwa limechanua kwenye uso wake, alishtuka baada ya kuanza kuona damu zikimtoka puani, abiria wote nao wakashtuka. Mara ya kwanza alipojifuta, zilikuwa ni damu kidogo lakini mara ya pili, zilikuwa nyingi, tena zikiwa na weusi fulani hivi, kila mmoja akapatwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.
Kwa bahati nzuri, miongoni mwa wale abiria alikuwepo daktari ambaye ilibidi amshike mkono na kumsogeza pembeni, akawataka abiria wengine wasogee pembeni ili apate hewa, akamlaza chini na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
Nikiwa bado sielewi nini cha kufanya, nilimuona baba akiwa ng’ambo ya pili ya barabara, akanionesha ishara kwamba nimfuate. Nikaangalia kushoto na kulia, nilipoona hakuna gari, nilivuka barabara na kusogea kule baba alipokuwa amesimama.
“Huku nyuma, mama na ndugu zangu wengine walishangaa kwa nini navuka barabara, mama akaanza kuniita. Nilishangaa kwa nini ananiita mimi tu wakati pembeni yangu alikuwepo baba, nikakosa majibu.
“Vipi, umeona kilichotokea?” baba aliniuliza huku akinitazama usoni, nikawa namtazama huku nikiwa na maswali mengi yasiyo na majibu.
“Baba wewe si tulikuacha stendi? Umefikaje hapa? Halafu uliingiaje kwenye gari na kuzuia ajali isitokee? Yule uliyekuwa unapigana na…” nilijikuta maswali mfululizo yakinitoka. Alichokifanya baba, ilikuwa ni kuniziba mdomo kwa kutumia kiganja cha mkono wake, ambao bado ulikuwa na damudamu.
“Nimeshakwambia, ukiwa mwanaume maana yake unatakiwa kuwa na kifua, siyo kila unachokiona unatakiwa kukisema, umenielewa?” alinihoji baba huku akinitazama, nikatingisha kichwa.
Akaniambia kwamba safari yetu ilikuwa imeandamwa na mabalaa makubwa na mtu pekee ambaye angeweza kushirikiana naye kuhakikisha tunafika salama, ni mimi. Akaingiza mkono mfukoni na kutoa kikaratasi ambacho kilifungwa unga fulani mweusi, akaumimina kidogo mkononi na kuniambia natakiwa kwenda kumpulizia yule dereva usoni.
Akaniambia baada ya hapo, mambo yote yangekuwa sawa na akaniambia natakiwa kukaa siti ya nyuma ya dereva, nikiona jambo lolote haliendi sawa, nivue viatu kisha nivivae upya kwa kuvigeuza, yaani cha kushoto nivae kulia na cha kulia kushoto kisha nishike sehemu zangu za siri.
“Umenielewa?”
“Ndiyo baba.”
“Mimi natangulia kusafisha njia,” alisema kisha akaniambia nivuke barabara, nikafanya hivyo. Kwa bahati mbaya, wakati navuka barabara, safari hii sikutazama kushoto wala kulia, nikavuka tu kama ng’ombe. Nikiwa nimefika katikati ya barabara, nilisikia mama akipiga kelele kwa nguvu pamoja na watu wengine, wote wakinionesha ishara kwamba nikimbie.
Sikuelewa kwa nini wananiambia vile, ghafla niligeuka kutazama upande wangu wa kushoto, lori kubwa la mafuta, lilikuwa limeshanisogelea huku likiwa kwenye mwendo wa kasi kubwa, taa zote za mbele zikiwa zimewashwa.
“Mungu wangu!” nilisema kwani nilijua hakuna kinachoweza kuniokoa kutoka kwenye mdomo wa mauti, ilikuwa ni lazima linisagesage palepale kama chapati.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 08:


ILIPOISHIA:
Dereva alizidi kuyumba huku gari likiongeza kasi, hali iliyofanya abiria waanze kupiga kelele kwa nguvu, wengi wakilitaja jina la Mungu.
Gari lilizidi kuongeza kasi, likawa linashuka kwenye mteremko huo kwa kasi kubwa huku likiendelea kuyumba huku na kule, kelele ndani ya basi zikazidi kuongezeka.
SASA ENDELEA…
Katika hali ambayo hata sielewi ilikuwaje, nilijikuta nikipata nguvu na kusimama, nikawa natazama nje kwa kupitia kioo cha dereva. Cha ajabu na cha kushtua, nilimuona baba akiwa anapigana na mtu ambaye sikumtambua ni nani, pembeni ya barabara.
Kwa macho yangu, nikamshuhudia baba akimpiga yule mtu kwa nguvu, akamdondosha chini na kuanza kumbamiza kwenye lami, damu nyingi zikatapakaa eneo lote.
Kufumba na kufumbua, nilishtukia baba akiwa ameshika usukani wa lile basi tulilokuwa tukisafiria, sikuwahi kumuona baba hata siku moja akiendesha gari lakini eti siku hiyo ndiyo alikuwa ameshika usukani. Sikukumbuka ameingiaje ndani ya basi, tena likiwa katika mwendo mkali kiasi kile.
Kila kitu kilifanyika kwa kasi kama ya radi, akamtoa dereva na kumsukumia pembeni, akaanza kubadilisha gia huku akiwa ameung’ang’ania usukani, katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea, gari liliacha kuyumbayumba ingawa halikupunguza mwendo, likawa linazidi kukimbia kwa kasi kubwa, likishuka kwenye mteremko mkali maarufu kama Mlima Nyoka.
Abiria wote walitulia, hata wale waliokuwa wakipiga kelele, walikaa kimya, wakawa wanaendelea kumuomba Mungu ndani ya mioyo yao, hakuna aliyeona mabadiliko yaliyofanyika upande wa dereva zaidi ya mimi nadhani na watu wachache waliokuwa wamekaa mbele.
(Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi)
Nilimshuhudia baba akiendelea kupangua gia kwa kasi, gari likaanza kupunguza mwendo na mita chache mbele, alifunga breki, gari likaserereka na hatimaye likasimama kandokando ya barabara, watu wote waliokuwa ndani ya basi walianza kushangilia na kumpongeza dereva huku wakikimbilia kwenye mlango wa kutokea nje.
Harakaharaka na mimi nilielekea kule mbele lakini lengo langu kubwa ilikuwa ni kwenda kumuuliza baba nini kilichotokea maana sikuwa naelewa chochote.
Cha ajabu, nilipofika pale kwenye siti ya dereva, nilimuona yule dereva ambaye ndiye aliyetoka na sisi Mbeya mjini akiwa ameegamiza kichwa kwenye usukani, akiwa ni kama amepitiwa na usingizi.
Nilibaki nashangaa kwa sababu kitendo cha kuinuka kutoka pale kwenye siti niliyokuwa nimekaa mpaka pale kwa dereva, sikuwa nimetumia hata dakika moja kamili, zilikuwa ni sekunde tu lakini eti baba hakuwepo tena na aliyekuwa amekaa pale kwenye usukani alikuwa ni dereva.
Niligeuka huku na kule kutazama kama nitamuona baba lakini sikumuona, abiria walikuwa wakiendelea kugombea kutoka na muda mfupi baadaye, wote walikuwa wameshateremka, kila mmoja akawa anamshukuru Mungu wake. Yaani kama ingetokea ajali, kwa jinsi mteremko ulivyokuwa mkali, sidhani kama kuna mtu angetoka salama ndani ya basi lile.
Ilibidi nimguse begani yule dereva ambaye bado alikuwa amelala na kuegamia usukani ili nimuulize nini kilichotokea. Cha ajabu, nilipomgusa, alishtuka sana, akawa ni kama aliyezinduka kutoka kwenye usingizi mzito, akawa anageuka huku na kule. Hakukuwa na mtu mwingine yeyote ndani ya gari, isipokuwa mimi na yeye tu.
“Nini kimetokea? Hatujapata ajali? Mungu wangu,” alisema yule dereva huku akianza kujikagua mwili wake. Nilishangazwa sana na hali ile, yaani kumbe na yeye hakuwa anaelewa kilichotokea kwa hiyo kama zisingefanyika jitihada zile, ni kweli tungepata ajali mbaya sana.
“Kwani wewe unakumbuka nini?” nilimuuliza.
“Wakati tunauanza huu mteremko wa Mlima Nyoka, nilianza kuhisi kizunguzungu, nikajaribu kupunguza mwendo ili nisimame lakini cha ajabu, badala ya kukanyaga breki nilikanyaga mafuta, gari likaongeza mwendo na kizunguzungu kikazidi, sikumbuki tena kilichotokea,” alisema yule dereva huku akiendelea kugeuka huku na kule.
(Usiache kutembelea Simulizi za Majonzi)
“Tushuke,” nilimwambia, harakaharaka akafungua mlango na kushuka, na mimi nikashuka. Wale abiria waliokuwa chini, walimzunguka dereva na kuanza kumpongeza kwa kazi kubwa aliyoifanya. Ilibidi awe anaitikia tu lakini kiukweli hakuwa anajua nini kimefanyika na imekuwaje mpaka basi limesimama.
Akiwa anaendelea kupongezwa, tabasamu la uongo likiwa limechanua kwenye uso wake, alishtuka baada ya kuanza kuona damu zikimtoka puani, abiria wote nao wakashtuka. Mara ya kwanza alipojifuta, zilikuwa ni damu kidogo lakini mara ya pili, zilikuwa nyingi, tena zikiwa na weusi fulani hivi, kila mmoja akapatwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.
Kwa bahati nzuri, miongoni mwa wale abiria alikuwepo daktari ambaye ilibidi amshike mkono na kumsogeza pembeni, akawataka abiria wengine wasogee pembeni ili apate hewa, akamlaza chini na kuanza kumpa huduma ya kwanza.
Nikiwa bado sielewi nini cha kufanya, nilimuona baba akiwa ng’ambo ya pili ya barabara, akanionesha ishara kwamba nimfuate. Nikaangalia kushoto na kulia, nilipoona hakuna gari, nilivuka barabara na kusogea kule baba alipokuwa amesimama.
“Huku nyuma, mama na ndugu zangu wengine walishangaa kwa nini navuka barabara, mama akaanza kuniita. Nilishangaa kwa nini ananiita mimi tu wakati pembeni yangu alikuwepo baba, nikakosa majibu.
“Vipi, umeona kilichotokea?” baba aliniuliza huku akinitazama usoni, nikawa namtazama huku nikiwa na maswali mengi yasiyo na majibu.
“Baba wewe si tulikuacha stendi? Umefikaje hapa? Halafu uliingiaje kwenye gari na kuzuia ajali isitokee? Yule uliyekuwa unapigana na…” nilijikuta maswali mfululizo yakinitoka. Alichokifanya baba, ilikuwa ni kuniziba mdomo kwa kutumia kiganja cha mkono wake, ambao bado ulikuwa na damudamu.
“Nimeshakwambia, ukiwa mwanaume maana yake unatakiwa kuwa na kifua, siyo kila unachokiona unatakiwa kukisema, umenielewa?” alinihoji baba huku akinitazama, nikatingisha kichwa.
Akaniambia kwamba safari yetu ilikuwa imeandamwa na mabalaa makubwa na mtu pekee ambaye angeweza kushirikiana naye kuhakikisha tunafika salama, ni mimi. Akaingiza mkono mfukoni na kutoa kikaratasi ambacho kilifungwa unga fulani mweusi, akaumimina kidogo mkononi na kuniambia natakiwa kwenda kumpulizia yule dereva usoni.
Akaniambia baada ya hapo, mambo yote yangekuwa sawa na akaniambia natakiwa kukaa siti ya nyuma ya dereva, nikiona jambo lolote haliendi sawa, nivue viatu kisha nivivae upya kwa kuvigeuza, yaani cha kushoto nivae kulia na cha kulia kushoto kisha nishike sehemu zangu za siri.
“Umenielewa?”
“Ndiyo baba.”
“Mimi natangulia kusafisha njia,” alisema kisha akaniambia nivuke barabara, nikafanya hivyo. Kwa bahati mbaya, wakati navuka barabara, safari hii sikutazama kushoto wala kulia, nikavuka tu kama ng’ombe. Nikiwa nimefika katikati ya barabara, nilisikia mama akipiga kelele kwa nguvu pamoja na watu wengine, wote wakinionesha ishara kwamba nikimbie.
Sikuelewa kwa nini wananiambia vile, ghafla niligeuka kutazama upande wangu wa kushoto, lori kubwa la mafuta, lilikuwa limeshanisogelea huku likiwa kwenye mwendo wa kasi kubwa, taa zote za mbele zikiwa zimewashwa.
“Mungu wangu!” nilisema kwani nilijua hakuna kinachoweza kuniokoa kutoka kwenye mdomo wa mauti, ilikuwa ni lazima linisagesage palepale kama chapati.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 09



ILIPOISHIA:
SIKUELEWA kwa nini wananiambia vile, ghafla niligeuka kutazama upande wangu wa kushoto, lori kubwa la mafuta, lilikuwa limeshanisogelea huku likiwa kwenye mwendo wa kasi kubwa, taa zote za mbele zikiwa zimewashwa.
“Mungu wangu!” nilisema kwani nilijua hakuna kinachoweza kuniokoa kutoka kwenye mdomo wa mauti, ilikuwa ni lazima linisagesage palepale kama chapati.
SASA ENDELEA…
KUFUMBA na kufumbua, hata sielewi baba alitokea wapi, akanipitia kwa kasi ya radi na kunivutia kule nilikotokea, nikaangukia pembeni ya barabara, lile lori likapita kwa kasi kubwa huku likipiga honi kwa nguvu. Kila mmoja aliamini limenipitia maana niliwaona watu wakishika vichwa, huku mama akianza kuangua kilio kwa sauti kubwa.
Mimi mwenyewe sikuelewa nini kimetokea, niligeuka huku na kule, baba hakuwepo tena, nikawa najitazama mwili wangu nikiwa kama siamini. Sikuwa na jeraha lolote, nikasimama, watu wote wakapigwa na butwaa, mama akaacha kulia na kujishika mdomo.
Nilijikung’uta mwili, nikatazama huku na kule, nilipoona hakuna gari, harakaharaka nilivuka na kwenda mpaka pale mama na ndugu zangu walipokuwa wamesimama, wakiwa ni kama hawaamini walichokuwa wanakiona.
*(Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi )
“Togo!” aliita mama huku akinishika mkono, macho yakiwa yamemtoka pima. Nilimuitikia, akaniuliza kama nipo salama, nikamjibu nipo salama, akanikumbatia kwa nguvu huku akimshukuru Mungu wake.
Watu wote walikuwa wameacha kila walichokuwa wanakifanya, wakawa wananitazama mimi. Nadhani lile tukio la kukosakoswa na gari liliwashangaza sana. Hata mimi mwenyewe nilikuwa bado sijui baba aliwezaje kuniokoa.
“Kwani ulifuata nini kule ng’ambo ya barabara,” aliniuliza kaka yangu, nikamtazama usoni nikijiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu.
“Halafu mbona ulikuwa unaongea peke yako?” alihoji kaka yangu mwingine, nikazidi kushangaa. Ni hapo ndipo nilipogundua kuwa kumbe hakuna mtu mwingine yeyote aliyemuona baba zaidi yangu, kwa tafsiri nyepesi ni kwamba baba hakuwa akionekana kwa macho ya kawaida.
Nilitamani kusema kitu lakini nilikumbuka kauli ya baba aliyekuwa akinisisitiza mara kwa mara kwamba lazima niwe na uwezo wa kukaa na vitu kifuani, siyo kuzungumza hovyo.
Waliniuliza maswali mengi lakini sikujibu lolote, nikawa namtazama yule daktari aliyekuwa akiendelea kumpa huduma ya kwanza yule dereva ambaye alikuwa amelazwa chini na kumgeuzia juu ili kuzuia damu isiendelee kumtoka puani.
Kwa hali niliyokuwa naihisi, niliona ni bora nipande kwenye basi na kwenda kukaa kwenye siti yangu kusubiri dereva apate nguvu tuendelee na safari. Hakuna kitu ambacho huwa sikipendi kama kukaa mahali kila mtu anakutazama wewe.
Basi watu waliendelea kunitazama mpaka namalizia kupanda ngazi za basi, kwa kuwa hakukuwa na mtu ndani ya basi, nilienda kukaa kwenye siti iliyokuwa nyuma ya dereva kama baba alivyonielekeza. Kwa bahati nzuri, siti hiyo ilikuwa kwa juu na ya dereva ilikuwa kwa chini, jambo ambalo lingenirahisishia kazi ya kumnyunyizia ule unga mweusi niliopewa na baba endapo kutatokea tena tatizo lolote.
Ilibidi niutoe kwa ajili ya kufanya majaribio, nikachukua kidogo nakujaribu kuunyunyiza kwenye kiti cha dereva, nikaona kumbe ni suala ambalo linawezekana kabisa, nikakaa vizuri kwenye siti yangu.
Sijui nini kilitokea kwani sekunde chache baadaye, niliona watu wote wakianza kuingia kwenye basi, nikasimama na kutazama pale dereva alipokuwa akipewa huduma ya kwanza, nikashangaa kuona tayari alikuwa amesimama na sasa alikuwa akijimwagia maji kichwani na kunawa uso.
Kila kitu kilitokea kwa kasi kubwa sana kiasi cha kunifanya nibaki na maswali mengi yasiyo na majibu. Nilichohisi ni kwamba huenda kile kitendo changu cha kuumwagia ule unga pale kwenye siti ya dereva ndicho kilichompa nguvu haraka dereva huyo.
Kwa kuwa siti hiyo haikuwa yangu, mwenye siti yake alipokuja na kutaka kukaa, nilimuomba akakae kwenye siti yangu, kwa bahati nzuri hata yeye kumbe alikuwa akiogopa kukaa mbele hasa kutokana na ile hali ya kunusurika ajali iliyotokea, nikamuonyesha siti yangu ambapo alienda kukaa.
Muda mfupi baadaye dereva aliingia ndani ya basi huku akijifuta maji aliyonawa kwa kutumia kitambaa kidogo, akakaa kwenye siti yake na kufunga mkanda lakini kabla hajawasha gari aligeuka nyuma, macho yangu na yake yakagongana.
“Sura yako kama siyo ngeni,” alisema huku akinitazama kama anayejaribu kukumbuka jambo fulani. Kiukweli mimi sikuwa namjua wala sikumbuki kama niliwahi kuonana naye sehemu yoyote, nikatingisha kichwa kumkatalia, akawa bado anaendelea kung’ang’aniza kwamba kuna sehemu tumewahi kuonana. Ilibidi nimkubalie tu huku tabasamu la uongo likiwa limechanua kwenye uso wangu.
“Jamani naomba kila mmoja asali kwa imani yake kabla hatujaendelea na safari,” alisema dereva, kweli kila mtu akaanza kusali kwa imani yake. Ilichukua kama dakika mbili hivi, kumbe mle ndani kulikuwa na walokole ambao nao walianza kunena kwa lugha.
Baadaye dereva aliwasha gari, akapiga ‘resi’ nyingi kisha akaliondoa gari kwa mwendo wa taratibu, akaliingiza barabarani na kuendelea kuliendesha kwa mwendo wa taratibu, watu wote ndani ya basi walikuwa kimya kabisa.
Tuliendelea kushuka kwenye mteremko wa Mlima Nyoka mpaka tulipofika chini kabisa, akabadili gia na tukaanza kuupandisha mlima mkali uliopo eneo hilo. Kwa wakazi wa Mbeya au watu waliowahi kufika huko, watakuwa wananielewa vizuri ninapouzungumzia Mlima Nyoka.
Safari iliendelea na hatimaye tukaumaliza mlima huo, nikaona kila mtu ndani ya basi ameanza kurudi kwenya hali yake ya kawaida, stori za hapa na pale zikaanza, wengi wakimshukuru Mungu wao kwani pengine muda huo tungekuwa tukizungumza mengine.
Dereva naye alizidi kutulia kwenye usukani, akaongeza mwendo na sasa tukawa tunaenda kwenye mwendo ambao mabasi ya mikoani hutumia. Safari iliendelea vizuri huku wengi wakianza kusahau kilichotokea. Kwa upande wangu muda wote nilikuwa makini kabisa kuhakikisha natekeleza kile nilichoambiwa na baba.
Kwa bahati nzuri, hakukuwa na kikwazo kingine chochote kilichotokea, majira ya kama saa nane mchana tukawa tayari tumewasili Ilula, Iringa mahali ambapo abiria hupata mapumziko mafupi ya chakula cha mchana.
Dereva alitutangazia kwamba tuna dakika kumi ya kwenda ‘kuchimba dawa’ pamoja na kununua vyakula, abiria wote wakaanza kushuka. Mama na ndugu zangu nao walishuka, na mimi nikaungana nao.
Jambo la kwanza tulienda kuchimba dawa, tuliporudi mama akawa anatuuliza kila mmoja anataka kula chakula gani. Tuliagiza vyakula, kila mmoja anachokitaka, mama akatunulia na soda kisha tukarudi ndani ya basi.
Muda mfupi baadaye, abiria wote walirudi ndani ya basi lakini kabla hatujaondoka, dereva alituambia kwamba tunaelekea kwenye Mlima Kitonga ambao ni mbaya kuliko Mlima Nyoka, akatuambia kwamba kila mmoja asali tena kwa mara nyingine kwa sababu hajui kama tutavuka salama. Sikuwahi kufika Kitonga lakini stori nilizokuwa nikizisikia, ni kwamba lilikuwa eneo la hatari sana ambalo mara kwa mara ajali mbaya zilikuwa zikitokea na kusababisha vifo vya watu wengi kila kukicha.
Nilijikuta nikitetemeka sana lakini nikajipa moyo kwamba kila kitu kitakuwa sawa. Tuliendelea na safari na muda mfupi baadaye, tulifika eneo ambalo bila hata kuuliza, nililitambua kwamba ndiyo Kitonga, kutokana na jinsi lilivyokuwa.
“Kuna tukio baya linataka kutokea, kuwa makini,” nilisikia sauti ya baba ikiniongelesha sikioni mwangu, nikageuka huku na kule, baba hakuwepo, nikajua kwa vyovyote lazima alikuwa ameona jambo ndiyo maana akanipa tahadhari, nikajiweka vizuri kitini, nikawa natazama huku na kule.
Je, nini kitaendelea?
 
SEHEMU YA 10:


ILIPOISHIA:
“Kuna tukio baya linataka kutokea, kuwa makini,” nilisikia sauti ya baba ikiniongelesha sikioni mwangu, nikageuka huku na kule, baba hakuwepo, nikajua kwa vyovyote lazima alikuwa ameona jambo ndiyo maana akanipa tahadhari, nikajiweka vizuri kitini, nikawa natazama huku na kule.
SASA ENDELEA…
Niliingiza mkono mfukoni na kutoa ile dawa aliyonipa baba, nikaishika ili chochote kikitokea iwe rahisi kufanya kama nilivyoelekezwa. Tukaanza kuteremka kwenye mteremko mrefu, wenye konakona nyingi na makorongo ya kutisha wa Kitonga.
Nilielewa kwa sababu gani eneo hilo lilikuwa maarufu sana, barabara ilikuwa imechomngwa pembezoni mwa milima na mawe makubwa, hali iliyofanya kama upande mmoja kukiwa na ukuta wa mlima basi upande wa pili kuna bonde refu sana.
Yaani kwa kutazama tu urefu wa yale makorongo, nilijikuta nikihisi kizunguzungu, nikawa najiuliza ikitokea dereva akakosea na kupeleka gari kwenye yale makorongo nini kitatokea? Sikupata majibu.
Safari iliendelea, dereva akawa amepunguza sana mwendo, abiria wote ndani ya gari wakiwa kimya kabisa. Nadhani kila mmoja alikuwa na kumbukumbu ya kilichotokea Mlima Nyoka. Ghafla tulishtuka baada ya kuona kuna lori la mafuta, tena likiwa na trela kwa nyuma, likija kwa kasi kubwa nyuma yetu.
Tulishtushwa na kishindo kikubwa kilichosikika nyuma, wote tukageuka na kusimama kwenye siti, tukawa tunatazama nini kinachoendelea? Inavyoonesha, lile lori lilikuwa limepasuka tairi la mbele na kumshinda dereva, sasa likawa linayumba barabara nzima.
Abiria wote walianza kupiga kelele kwenye lile basi, hakuna ambaye alijua nini kitatokea kwa sababu kama lile gari lori lingeendelea kuja kwa mwendo ule, lingeligonga basi letu kwa nyuma na kwa ile kasi yake, maana yake lingeturushia kwenye korongo refu na kutuangukia kwa juu.
Sijui kama kuna mtu angepona, ukizingatia kwamba lilikuwa ni lori la mafuta na lilionesha kuwa na mzigo. Nilichokifanya, kwa haraka nilimnyunyizia ule unga dereva ambaye bado hakuwa akijua afanye nini. Nilipomnyunyizia tu, nilimuona akibadili gia haraka, akaongeza mwendo na kulifanya basi lianze kushuka mteremko ule kwa kasi kubwa.
Kuongeza kasi kwa ghafla kuliwafanya abiria wengine wazidi kuchanganyikiwa, kelele zikazidi ndani ya basi, lile lori nalo likawa linazidi kuja kwa kasi kubwa nyuma yetu.
Wakati dereva akizidi kukanyaga mafuta na kulifanya basi lishuke kwa kasi ya ajabu mteremko ule hatari, ghafla tulishtukia lori jingine likiwa limepaki mbele yetu, dereva na utingo wake wakiwa wamekata matawi ya miti na kusambaza barabarani, ishara kwamba lilikuwa limeharibika.
Kwa kasi ambayo gari tulilopanda lilikuwa likishuka nayo, hata mimi mwenyewe sikuamini kama dereva ataweza kulimudu na kulikweopa lile lori mbele yetu.
Hata hivyo, dereva alitumia kile ambacho wengi huita uwezo binafsi, bila kupunguza mwendo hata kidogo, alizungusha usukani kwa kasi, gari likageuka kama linaenda kugonga jiwe kubwa lililokuwa pemebini ya barabara, kisha akazungusha tena usukani kwa kasi, gari likageuka tena upande wa pili.
Kitendo kile kililifanya basi letu lipenye kwenye uwazi mwembamba uliokuwepo kati ya lile gari lililoharibika na ukuta wa upande wa pili, kufumba na kufumbua likapita pale katikati kwa kasi kubwa na kulipita lile gari bovu, dereva akaanza kupunguza mwendo huku akibadilisha gia.
Sekunde chache baadaye, kilisikika kishindo kikubwa nyuma yetu, lile lori la mafuta lilikuwa limeligonga lile lori jingine bovu kwa nyuma na kulisukuma mita kadhaa kabla ya yote mawili kuangukia kwenye korongo refu, watu wote wakawa hawaamini kilichotokea.
Cha ajabu sasa, wakati watu wote wakitazama kilichotokea kule nyuma, nilishtuka kugundua kwamba kumbe aliyekuwa akiendesha gari hakuwa yule dereva wetu bali baba, macho yakanitoka pima nikiwa siamini ninachokiona. Alipogundua kwamba namtazama, naye alinigeukia na kunitazama kwa sekunde chache, akawa aanendelea kubadili gia huku akifunga breki.
Mbele kidogo kulikuwana uwazi pembeni ya barabara ambao uliwekwa maalum kwa ajili ya magari yanayoharibika njiani, akaendelea kufunga breki na hatimaye, akalisimamisha kabisa basi letu. Wakati watu bado wakiwa bize kushangaa kule nyuma, alifungua mlango wa dereva, akashuka huku akiendelea kunitazama na kunionesha ishara kwamba nisiseme chochote.
Akapotea kwenye upeo wa macho yangu na kuniacha na maswali mengi yasiyo na majibu. Cha ajabu kingine, aliposhuka, pale kwenye siti ya dereva alikuwa amekaa dereva yuleyule, tena akiwa amefunga na mkanda kabisa lakini kama ilivyokuwa mara ya kwanza, naye alionesha kushtuka kama mtu aliyekuwa amelala usingizi mzito. Akageuka huku na kule, macho yangu na yake yakagongana.
‘Kwani kumetokea nini?” aliniuliza kwa sauti ya chini huku akitaka mtu mwingine yeyote asielewe. Nadhani hata yeye alishagundua kwamba kuna mambo yasiyo ya kawaida yalikuwa yakiendelea.
*(Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi )
“Ajali, ajali mbaya sana,” nilimjibu huku nikimuonesha kule nyuma tulikotoka ambako moshi mzito mweusi ulikuwa ukifuka kutoka bondeni. Tayari abiria wengi walikuwa wameshashuka kwenye basi na kuanza kurudi kule eneo la tukio. Harakaharaka dereva alifungua mlango na kushuka, na mimi ikabidi nishuke tena safari hii nilipitia pale kwenye mlango wa dereva.
Tukawa tunakimbilia pale eneo la tukio. Trela moja la lile lori la mafuta, lilikuwa limekatika na kuanguka katikati ya barabara kimshazari, jambo lililofanya mawasiliano kati ya pande hizo mbili za barabara yakatike. Hakukuwa na gari ambalo lingeweza kuvuka tena mpaka trela lile liondolewe.
Ajali ilikuwa mbaya kiasi cha kumfanya kila mmoja aliyeshuhudia, ainue mikono yake juu na kumshukuru Mungu kwa sababu kama isingekuwa miujiza iliyotokea, ilibidi basi letu ndiyo ligongwe na kuangukia kule bondeni kisha kuanza kuungua kama ilivyokuwa imetokea.
Tukiwa bado tunaendelea kushangaa kilichotokea, tulishangaa kuona mtu akitoka ndani ya lile lori la mafuta lakini mwili wake wote ukiteketea kwa moto, akawa anajaribu kukimbia lakini hakufika mbali, moto ukamzidi na kumfanya aanguke chini.
Kwa jinsi magari hayo yalivyodondokea chini bondeni, hakuna mtu yeyote ambaye angewahi kwenda kumsaidia yule mtu kwa sababu kwanza eneo lenyewe lilikuwa haliwezi kupitika kirahisi, watu wakawa wanapiga kelele huku tukimshuhudia yule mtu ambaye sijui ndiyo alikuwa dereva au utingo wa gari lililopata ajali akiteketea bila msaada wowote.
Muda mfupi baadaye, magari mengine mengi yalishawasili eneo hilo na kwa sababu barabara ilikuwa imefungwa, yalisimama na kupanga foleni ndefu, abiria na madereva wakawa wanashuka kuja kujionea kilichotokea.
Kila aliyekuwa anaona kilichotokea, alikuwa haamini kabisa. Ilikuwa ajali mbaya mno ambayo kama ingehusisha gari la abiria, sidhani kama kuna mtu yeyote angetoka salama.
Kwa kuwa tulikuwa nyuma ya muda na bado tulikuw ana safari ndefu, ilibidi turudi kwenye basi letu, dereva naye akawa anaonekana kuwa na maswali mengi kuliko majibu.
Japokuwa kwa mara nyingine abiria wote walikuwa wakimsifia kwa jinsi alivyoweza kuepusha ajali ile, mwenyewe alikuwa akijua kutoka ndani ya moyo wake kwamba siyo yeye aliyefanya kazi hiyo na hakuwa akijua chochote kilichotokea.
Tulirudi kwenye basi na baada ya kuhakikisha abiria wote wameingia, dereva aliondoa gari kwa mwendo wa taratibu, gumzo kubwa ndani ya basi likawa ni juu ya ajali hiyo. Wakati watu wakiendelea kujadiliana kuhusu ajali hiyo, mimi bado nilikuwa na maswali mengi mno kuhusu baba.
Bado sikuwa na majibu na hakukuwa na mtu yeyote wa kunijibu zaidi ya baba mwenyewe. Jambo kubwa ambalo lilikuwa likijirudia ndani ya kichwa changu, lilikuwa ni je, kweli baba ni mchawi?
“Unasemaje?” nilisikia sauti ya baba akiniuliza kwa ukali, nikageuka huku na kule lakini baba hakuwepo.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 11:



ILIPOISHIA:
Bado sikuwa na majibu na hakukuwa na mtu yeyote wa kunijibu zaidi ya baba mwenyewe. Jambo kubwa ambalo lilikuwa likijirudia ndani ya kichwa changu, lilikuwa ni je, kweli baba ni mchawi?
“Unasemaje?” nilisikia sauti ya baba akiniuliza kwa ukali, nikageuka huku na kule lakini baba hakuwepo.
SASA ENDELEA…
“Sijaongea kitu,” nilijibu, nikasikia baba akiachia msonyo mrefu kisha ukimya ukatawala. Kumbe nilipotamka lile neno ‘sijaongea kitu’, niliongea kwa sauti kubwa kiasi cha kuwafanya abiria wengi ndani ya basi, wanisikie.
“Kaka, unaongea na nani?” sauti ya msichana aliyekuwa akicheka kwa sauti ilisikika, ikifuatiwa na abiria wengine, ndiyo iliyonizindua kutoka kwenye lindi la mawazo. Nikashtuka na kukaa vizuri kwenye siti yangu.
“Anaogopa ajali huyo,” alipaza sauti abiria mwingine, watu karibu wote kwenye basi wakacheka. Nilimgeukia mama, nikamuona yeye yupo siriasi tofauti na abiria wengine, nikageuka na kukaa vizuri kwenye siti yangu.
Yule msichana aliyekuwa amekaa siti ya upande wa pili na pale nilipokuwa nimekaa, alivua ‘headphones’ zake, akawa anaendelea kunitazama huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.
Tangu tunaanza safari wala sikuwa najua kwamba kuna mtu kama yeye ndani ya gari, ni mpaka pale alianza kunicheka ndipo nilipoanza kumtilia maanani. Alikuwa ni msichana mdogo lakini wa kisasa, akiwa na simu ya kisasa mkononi, halafu akiwa amevalia mavazi kama wasichana wa mjini ambao nilizoea kuwaona kwenye TV.
Nilipoendelea kumtazama kwa macho ya kuibia, niligundua kwamba alikuwa na sura nzuri sana halafu akitabasamu kuna vishimo kwenye mashavu yake vinajitokeza, nikajikuta navutiwa kumtazama.
Safari iliendelea lakini mara kwa mara yule msichana alikuwa akinigeukia na kunitazama, tofauti na mara ya kwanza ambapo alikuwa kama anacheka kwa kunidharau, safari hii alikuwa akinitazama kwa makini.
Katika ujanja wangu wote niliokuwa nikiuonesha kijijini kwetu, makongorosi, Chunya, hakuna kitu nilichokuwa nakiogopa kama kuzungumza au kujichanganya kwa namna yoyote na wasichana, hasa wa rika langu.
Tangu naanza kupevuka, mpaka namaliza shule ya msingi na hata baada ya kuanza maisha ya mtaani, sikuwahi kuwa na mazoea na msichana yeyote, zaidi ya dada zangu kwa hiyo kitendo cha msichana huyo kuwa ananitazama mara kwa mara, tena msichana mwenyewe mrembo kwelikweli, kilinikosesha mno utulivu.
Kuna wakati nilikuwa natamani hata nirudi kule kwenye siti yangu ya mwanzo, nilikokuwa nimekaa namama na ndugu zangu lakini nilipofikiria kuhusu kazi nzito niliyopewa na baba, ilibidi nijikaze kiume.
Nilipoona anazidi kunitazama, kuna wakati nilifumba macho na kujifanya nimelala lakini nikasikia ile sauti ya ajabu ya baba ikinijia, akaniambia sitakiwi kulala kwa sababu nina jukumu la kuhakikisha safari inakuwa salama.
Nikawa sina cha kufanya zaidi ya kujikaza kiume, safari hii na mimi niliamua kuwa namtazama. Kama kawaida yake, alinigeukia, akawa ananitazama kwa makini, ikabidi na mimi nimgeukie, tukawa tunatazamana. Cha ajabu, alipoona na mimi namtazama japo kwa uso uliojawa na aibu, aliachia tabasamu pana.
Nikajikuta na mimi nikitabasamu, haraka nikakwepesha macho yangu na kugeukia upande wa dirishani, nikawa natazama nje. Safari iliendelea huku nikiendelea kujishtukia, baadaye nilipomgeukia tena yule msichana, niligundua kwamba tayari alishalala huku headphones zake zikiwa masikioni.
Nikashusha pumzi ndefu kama mtu aliyetua mzigo mzito kichwani, nikakaa vizuri kwenye siti yangu na kuendelea nakazi niliyopewa na baba. Kwa bahati nzuri, safari hii hakukuwa na kipingamizi chochote, safari ikaendelea mpaka tulipofika sehemu maarufu iitwayo Chalinze Choma Nyama.
Dereva alipunguza mwendo na kusimamisha basi, akatutangazia abiria kwamba anatoa dakika kumi tukachimbe tena dawa na kujinyoosha. Bila kupoteza muda, abiria walianza kuteremka, mimi nikageuka na kutazama pale mama na wale ndugu zangu walipokuwa wamekaa, nikawaona nao wakiinuka.
Ilibidi nisubiri abiria wengine wapite, ndugu zangu walipokaribia, niliinuka na kuungana nao, tukawa tunataniana na kaka na dada zangu kama kawaida yetu tunapokutana. Cha ajabu, eti nao walikuwa wakinicheka kwamba woga wa kupata ajali ulisbabisha niwatie aibu kwa kupayuka kwenye basi.
Wakawa wananicheka na kunisukumasukuma, jambo ambalo sikupendezewa nalo. Tuliposhuka chini, waliendelea kunitania lakini kwa kuwa sikuwa naupenda utani wao, niliamua kujitenga nao, nikazunguka mpaka nyuma ya gari, nikasimama nikiegamia basi huku nikitazama kule tulikotokea, uso wangu ukiwa umekosa amani.
*(Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi )
“Hawa washenzi wangejua mimi na baba ndiyo tuliowalinda wasipate ajali wasingekuwa wananicheka hivi,” nilisema huku nikikumbuka pia vicheko vya abiria wengine ndani ya basi, muda ule nilipopayuka kwa nguvu ndani ya basi.
Mawazo yangu yalizama kwenye hisia chungu, nikawa naendelea kuwaza mambo mengi ndani ya kichwa changu. Ghafla nilishtushwa na sauti ya kike pembeni yangu.
“Mambo!”
“Safi tu,” nilijibu huku nikianza kujichekesha, aibu zikiwa zimenijaa baada ya kugundua kuwa ni yule msichana wa kwenye basi aliyekuwa akinitazama sana.
“Mbona umekaa peke yako huku halafu unaonekana kama una mawazo sana?”
“Ahh! Kawaida tu, nahisi uchovu wa safari,” nilimjibu, huku lafudhi ya kijijini ikishindwa kujificha kwenye mazungumzo yangu. Aliendelea kunipigisha stori za hapa na pale, akionesha kuchangamka mno utafikiri tunafahamiana.
“Nisindikize kule upande wa pili nikanunue soda za kopo, naona huku hakuna,” alisema msichana huyo ambaye manukato yake mazuri aliyojipulizia, yalizifurahisha mno pua zangu.
Tulisimama pembeni ya barabara, akageuka huku na kule kuangalia kama hakuna gari linalokuja, na mimi nikawa namfuatisha kwa sababu sikuwa mzoefu sana wa barabara ya lami na sikuwa najua vizuri namna ya kuvuka barabara. Alipohakikisha kwamba hakuna gari, alinishika mkono, nadhani aliniona jinsi nilivyokuwa na hofu moyoni, tukaanza kuvuka.
Mikono yake ilikuwa laini mno kiasi kwamba nilifurahia jinsialivyonishika. Kwa mara ya kwanza maishani mwangu, nikaanza kuhisi hali isiyo ya kawaida. Tulivuka mpaka ng’ambo ya pili, akafungua pochi yake ndogo na kutoa noti ya shilingi elfu kumi, akampa muuzaji wa vinywaji aliyekuwa na kibanda chake pembeni ya barabara.
“Unakunywa soda gani?” aliniuliza huku yeye akichukua soda yake, nikakosa cha kujibu zaidi ya kuanza kuchekacheka tu.
“Nakuchagulia, nataka unywe ninayokunywa mimi,” alisema huku akinigeukia, akanipa soda ya Sprite ya kopo, akafungua ya kwake na kuingiza mrija, mimi nikawa nashangaashangaa kwa sababu sikuwahi kunywa soda ya kopo hata mara moja wala sikuwahi kutumia mrija.
Akiwa ameshapiga funda moja, alichukua lile kopo la soda mikononimwangu, anaipa ile ambayo alishaifungua na kunywa kidogo, nikawa namshangaa kwani hayo yalikuwa mambo mageni kabisa kwangu, nilizoea kuyaona kwenye video.
Alifungua na ile nyingine, nayo akapiga funda moja, nikawa sina cha kufanya zaidi ya kuendelea kunywa, akawa ananitazama kwa macho yaliyobeba ujumbe mzito.
“Unaitwa nani?”
“Togo,” nilimjibu kwa kifupi, akageuka kama anayetazama upande wa pili wa barabara, nikapata fursa ya kulisanifu vizuri umbo lake. Alikuwa ni msichana mzuri sana, upande wa nyuma alikuwa amejazia huku kiuno chake kikiwa kimegawanyika, kama nyigu ambao kule kijijini tulikuwa tukiwaogopa kutokana na sumu yao wanapokung’ata.
Suruali ya jeans aliyovaa, ililifanya umbo lake lijichonge vizuri, ghafla akageuka, akanibamba nikiwa namtazama kwa nyuma, nikazidi kujisikia aibu.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 12:


ILIPOISHIA:
Alikuwa ni msichana mzuri sana, upande wa nyuma alikuwa amejazia huku kiuno chake kikiwa kimegawanyika, kama nyigu ambao kule kijijini tulikuwa tukiwaogopa kutokana na sumu yao wanapokung’ata.
Suruali ya jeans aliyovaa, ililifanya umbo lake lijichonge vizuri, ghafla akageuka, akanibamba nikiwa namtazama kwa nyuma, nikazidi kujisikia aibu.
SASA ENDELEA…
“Mbona unaniangalia hivyo?”
“Mimi?” Nilijifanya kuvunga, akanisogelea na kunipiga kakibao kepesi begani huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye kwenye uso wake. Na mimi nikawa nacheka huku aibu zikiwa zimenijaa.”
“Dar es Salaam unaishi sehemu gani?” aliniuliza swali ambalo lilikuwa gumu sana kulijibu kwani ukweli ni kwamba sikuwa naijua Dar wala sikuwahi kufika kabla. Nikawa nababaika mwenyewe, akajiongeza na kuniuliza:
“Kwani hii ndiyo mara yako ya kwanza kufika Dar?”
“Ndiyo,” nilijibu harakaharaka kwa sababu alikuwa amenipunguzia sana kazi ya kumjibu. Akaniambia kwamba yeye anaishi na wazazi wake Kijitonyama. Akaniambia kwamba alikuwa amemaliza chuo akisomea uhasibu na alikuwa anatoka Mbeya kuwasalimu bibi na babu yake wa upande wa mama.
“Wanaishi Mbeya sehemu gani?” nilimuuliza, akaniambia wanaishi Katumba, njia panda ya kwenda Mwakaleli. Maeneo hayo sikuwa nimewahi kufika zaidi ya kusikia tu kwa watu, nikawa natingisha kichwa kumkubalia. Akaendelea kunieleza kwamba mama yake alikuwa Mnyakyusa lakini baba yake alikuwa ni mtu kutoka Mkoa wa Pwani ingawa hakunieleza ni kabila gani.
Hatimaye dakika kumi ziliisha, dereva akaanza kupiga honi akitupa ishara kwamba muda wa kuingia kwenye basi umefika. Kwa hizo dakika chache nilizokaa na msichana huyo, niligundua kwamba alikuwa mcheshi, mchangamfu na asiye na maringo kama walivyo wasichana wengi warembo kama yeye.
“Lakini hujaniambia unaitwa nani.”
“Unataka kujua jina langu?”
“Ndiyo.”
“Sitaki,” alisema huku akinipiga tena begani, akaanza kukimbia kuelekea kwenye basi. Sikuelewa kitendo hicho kilikuwa na maana gani, wakati anakimbia nilishuhudua kitu kingine ambacho kiliusisimua sana moyo wangu, mpaka nikawa najiuliza zile hisia nilizokuwa nazisikia kwa wakati huo zilikuwa na maana gani?
Kwa kifupi nilijisikia raha sana kufahamiana na msichana huyo. Niliendelea kumtazama akikimbia mpaka alipofika kwenye ngazi za kupanga kwenye basi, akageuka na kunitazama kisha akapanda ngazi. Na mimi nilitembea harakaharaka huku nikiendelea kuchekacheka mwenyewe, mkononi nikiwa na kopo la soda ambayo nilikua nimeinywa nusu.
Nilipopanda na kuingia ndani ya gari, ndugu zangu wote walishangaa kuniona nikiwa na soda ya kopo, tena nikinywa kwa mrija.
Niliwaona wote walivyomeza mate, wakawa wanaulizana nimeipata wapi soda hiyo? Sikuwajali kwa sababu bado nilikuwa na hasira nao, nikakaa kwenye siti yangu, nikageuka na kumtazama yule msichana ambaye mpaka muda huo hakuwa amenitajia jina lake, nikashtuka tena kugundua kwamba kumbe alikuwa ametulia akinitazama kila nilichokuwa nakifanya.
Macho yangu na yake yalipogongana, aliachia tabasamu hafifu halafu eti na yeye akakwepesha macho yake kwa aibu, yaani mwanzo mimi ndiyo nilikuwa nakwepesha macho yangu lakini ghafla na yeye alianza kukwepesha macho yake kwa aibu. Dereva aliondoa gari na safari ikaendelea.
Safari hii umakini ulikuwa ukinipungua sana kichwani mwangu kwani mara kwa mara tulikuwa tukitazamana na yule msichana na kuishia kuchekacheka tu. Nashukuru hakuna jambo lolote baya lililotokea mpaka tulipoanza kuingia mjini.
Tulipofika Kibaha, gari lilisimama na yule abiria aliyekuwa amekaa pembeni yangu, alisimama na kushuka, harakaharaka nikamuona yule msichana akikusanya kila kitu chake na kuja kukaa pembeni yangu. Aliponisogelea tu, nilianza tena kusikia harufu ya manukato aliyojipulizia, ambayo kiukweli yalinivutia sana.
Akakaa pembeni yangu na kuniegamia kimtindo kabla ya kujiweka vizuri kwenye siti yake.
“Yule niliyekaa naye hata stori hana, muda wote analala tu bora nikae na wewe,” alisema huku akinipigapiga begani, nikawa natabasamu tu kwani kiukweli hata mimi nilikuwa napenda kukaa naye siti moja.
“Ulisema unataka kujua jina langu?” alianzisha mazungumzo, niikamjibu kwa kutingisha kichwa, akaniambia ananipa mtihani nitafute mwenyewe jina lake. Kiufupi ni kwamba, kwa muda mfupi tu niliokaa naye, alionesha kupenda sana urafiki wetu uendelee, jambo ambalo hata mimi nilikuwa nalipenda ingawa mara kwa mara nilikuwa najishtukia.
Hata nilipokuwa nacheka, sikuwa napenda ayaone meno yangu kwani ya kwake yalikuwa meupe sana na masafi lakini kwangu mimi, hata sikuwa nakumbuka mara ya mwisho kupiga mswaki ni lini, si unajua tena maisha ya kijijini.
“Una simu?” aliniuliza swali ambalo lilinifanya nijisikie tena aibu. Sikuwa na simu, sikuwahi kumiliki wala sikuwa najua namna ya kuitumia, nikawa natingisha kichwa kukataa, akaniambia alikuwa na simu mbili lakini hiyo nyingine hakuwa akiitumia kwa sababu ilikuwa ya kizamani.
“Basi nipe mimi,” nilisema kwa utani kwani nilijua ni jambo ambalo haliwezekani, akacheka na kufungua kibegi chake kidogo, akatoa simu ndogo aina ya Nokia ya tochi na kunipa.
“Chukua utakuwa unatumia,” alisema. Nikapigwa na butwaa nikiwa ni kama siamini. Kuna wakati nilihisi kwamba pengine alikuwa akinitania lakini mwenyewe alisisitiza kwamba ni kweli amenipa. Muda huo, tayari gari lilikuwa limeshawasili Ubungo, sikuwa napajua zaidi ya kusikia tu watu wakisema hapo ndiyo ubungo.
Tayari giza lilishaanza kuingia, taa nyingi zilizokuwa zinawaka kila upande zikanifanya nijihisi kama nilikuwa kwenye ndoto.
Waliosema mjini kuzuri hawakukosea, Dar ilikuwa na tofauti kubwa sana na kule kijijini nilikozaliwa na kukulia, kila kitu kilikuwa kigeni kwangu. Wakati nikiendelea kushangaashangaa, nilisikia mama akiniambia kwamba natakiwa kuwa makini kuchukua mizigo iliyokuwa imewekwa kwenye buti.
Harakaharaka nikateremka na abiria wengine, hata sikukumbuka nilipotezana saa ngapi na yule dada, ushamba wa mjini ulinipa mchecheto mkubwa ndani ya moyo wangu, nikaenda mpaka kwenye buti nikiwa na wale ndugu zangu wengine ambao nao walikuwa wakishangaashangaa, tukafanikiwa kushusha mizigo yetu yote na kuiweka pembeni.
“Twendeni nilisikia sauti ya baba akizungumza, kugeuka pembeni, sote tulipigwa na butwaa kumuona baba akiwa anafungua milango ya teksi. Hakuna aliyejua baba alifika saa ngapi Dar es Salaam kwa sababu kama aliweza mpaka kuzungumza na dereva wa teksi na kukaa pale wakitusubiri, maana yake ni kwamba aliwahi sana kufika.
“Unajua wewe huna akili kabisa,” baba alianza kunifokea baada ya kumaliza kupakiza mizigo kwenye teksi, nikawa nashangaa kwa nini baba ananiambia maneno hayo.
“Yule uliyekuwa umekaa naye kwenye basi ni nani?”
“Ni rafiki yangu.”
“Unamjua wewe? Na hicho alichokupa una uhakika gani kama ni simu? Ujinga wako utaiponza familianzima,” alisema
 
SEHEMU YA 13:

ILIPOISHIA:
“YULE uliyekuwa umekaa naye kwenye basi ni nani?”
“Ni rafiki yangu.”
“Unamjua wewe? Na hicho alichokupa una uhakika gani kama ni simu? Ujinga wako utaiponza familia nzima,” alisema maneno ambayo yalinishangaza sana.
SASA ENDELEA…
“NI simu baba!”
“Sitaki kukuona naye tena na hiyo simu lete,” alisema huku akinipokonya ile simu. Nilizidi kumshangaa baba, nikaona kama anataka kunikosesha bahati ya bure. Kwa mara ya kwanza nilijikuta nikipandwa sana na hasira juu yake. Hata hivyo sikuwa na cha kufanya, tuliondoka Ubungo huku kila mmoja ndani ya gari tulilokuwa tumepanda, akiwa anashangaa mandhari ya Jiji la Dar es Salaam.
Japokuwa tulikuwa tumebanana sana kwenye ile teksi kwa sababu ya wingi wetu, kila mmoja alikuwa akitamani yeye ndiyo akae dirishani. Tulikatiza mitaa mingi na hatimaye tukaiacha barabara ya lami na kuingia kwenye barabara ya vumbi. Baada ya muda, tulitokeza kwenye nyumba moja nzurinzuri, baba akawa wa kwanza kuteremka kwenye gari, na sisi wengine tukafuatia na kuanza kushusha mizigo.
Wakati tukiendelea kushusha mizigo, geti kubwa lilifunguliwa, mwanaume wa makamo aliyeonekana wanafahamiana vizuri na baba, alimuita kwa jina lake, baba akaacha kila alichokuwa anakifanya na kwenda kumkumbatia, wote wawili wakionyesha kuwa na furaha kubwa kwa kukutana.
“Hii ndiyo familia yangu, shemeji yako na watoto,” alisema baba huku akituonyeshea sisi, akatusogelea na kusalimiana na mama, kisha akaanza kutupa mikono, mmoja baada ya mwingine huku akituuliza majina.
“Naitwa Togolai,” nilimwambia aliponifikia, akanitazama usoni.
“Wewe ndiyo Togo?”
“Ndiyo,” nilisema huku na mimi nikiachia tabasamu hafifu kwa sababu na yeye alikuwa akitabasamu. Baada ya hapo, alitukaribisha ndani, wakati tunabeba mizigo kuingiza, walikuja watu wengine watatu, wasichana wawili na mwanaume mmoja ambao kwa kuwatazama tu, walionyesha dhahiri kwamba ni wanaye kwa jinsi walivyokuwa wamefanana na kupishana umri.
Mkubwa alikuwa wa kike, aliyemfuatia alikuwa wa kiume na mdogo kabisa naye alikuwa wa kike. Hawakupishana sana umri, yule mkubwa alikuwa akilinganalingana na dada yetu Sabina.
Tofauti yao na sisi, ilikuwa kubwa sana, kuanzia jinsi walivyokuwa wamevaa na mpaka muonekano wa miili yao. Walikuwa na mwonekano wa kimjini haswaa wakati sisi tulikuwa na mwonekano wa ‘bushi’, kuanzia sura zetu, mavazi yetu mpaka jinsi tulivyokuwa tukizungumza.
Walitukaribisha mpaka ndani, tukaenda kukaa kwenye sebule kubwa na ya kisasa. Japokuwa tulikuwa wengi, lakini wote tulitosha kwenye masofa ya kisasa. Ushamba wetu uliendelea kujidhihirisha mle ndani kwani tulikuwa tukishangaa kila kitu, kuanzia taa za umeme, feni, mapazia, kuta zilizokuwa zimenakshiwa kwa rangi nzuri na marumaru, kila kitu kilikuwa kigeni kwetu.
Tuliandaliwa chakula na mama wa familia ile ambaye alikuwa mchangamfu na anayependeza kimwonekano kuliko mama yetu. Kilikuwa ni chakula kizuri mno, ambacho ama kwa hakika tulikifurahia. Tukala mpaka kumaliza, mwenzetu mmoja akawa anataka kulamba bakuli la mboga, mama akamkata jicho la ukali na kumfanya aogope.
Baada ya chakula, tulianza kushangaa runinga maana kule hakukuwa kuangalia, ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kuona runinga lakini achilia mbali runinga ya kawaida, ile iliyokuwa mle ndani ilikuwa kubwa sana, tena ya kisasa kabisa iliyounganishwa na spika ndogo za kisasa zilizokuwa zinatoa mdundo mzito.
Mpaka muda wa kulala unafika, hakuna aliyekuwa tayari kubanduka pale sebuleni, kila mmoja alikuwa anatamani kama akeshe palepale akitazama vipindi vizuri vilivyokuwa vinaonyeshwa. Ilibidi mama atumie ukali, kwani kwa muda huo baba ambaye ndiyo tunayemwogopa sana, alikuwa nje kwa mazungumzo na yule rafiki yake.
Kabla ya kwenda kulala, ilibidi kwanza tuende kuoga mmojammoja kuondoa vumbi na uchafu tuliotoka nao kijijini. Mimi ndiye niliyekuwa wa mwisho kwenda kuoga ambapo nilipoingia kwenye bafu hilo la kisasa, nilishangazwa kwa jinsi lilivyokuwa safi. Yaani hata kama ningeambiwa nikae mle ndani kwa siku nzima na kuletewa chakula nilie humohumo ningekubali kwa sababu ya usafi wake.
Kule kijijini tulizoea kwenda kuoga mtoni, wakati mwingine kuogelea lakini mjini mambo yalikuwa tofauti. Nilivua nguo zangu na kuzikung’uta kwanza kwa sababu zilikuwa na vumbi jingi. Kwa bahati mbaya, wakati nikiikung’uta suruali niliyokuwa nimevaa, nilisahau kwamba ile dawa niliyopewa na baba nilikuwa nimeiweka kwenye mfuko, nilipokung’uta ikadondoka chini na kwa kuwa choo na bafu vilikuwa vimeungana, yaani upande mmoja kuna bafu na upande wa pili kuna choo, iliteleza mpaka kwenye sinki la choo.
*( Simulizi za Majonzi)
Kutokana na umuhimu wa dawa hiyo, ilibidi niende kuiokota haraka lakini kabla sijafanya hivyo, niliitundika ile suruali kwenye bomba lililokuwa pembeni. Nikashtuka kuona maji yakianza kumwagika, yakaisomba ile dawa na kuipeleka kwenye shimo la choo, ikapotelea kwenye bomba la kutolea maji machafu.
Nilishangaa sana yale maji nani ameyafugulia lakini nilipotazama vizuri, niligundua kuwa kumbe pale nilipokuwa nimetundika suruali ile ilikuwa ni koki ya bomba ambayo kwa jinsi ilivyokuwa ya kisasa nilishindwa kuitambua.
“Ayaaa!” nilisema kwa sauti kubwa kwa sababu sikutegemea kabisa kile kilichotokea na hata sikujua nitamwambia nini baba kwa sababu wakati ananipa, alinisisitiza kuitunza sana dawa hiyo. Ilibidi nifunge maji kwanza, nikaegamia kwenye marumaru za bafuni, nikiwa na mawazo mengi juu ya nini cha kufanya.
Mwisho nilipiga moyo konde na kujiambia kwamba nitaenda kumweleza baba hali halisi na kwa sababu ananipenda na ananiamini. Nilimalizia kuvua nguo, nikawa nataka nioge maji kwa kutumia bomba linalomwaga maji kama mvua, kama nilivyokuwa nimeona kwenye runinga muda mfupi uliopita.
Kwa umakini mkubwa nilichunguza mahali ilipo koki yake, nilipoiona niliifungua, maji yakaanza kumwagika, harakaharaka nikaingia katikati yake na kuanza kujimwagia.
Ilibidi nifumbe macho wakati najipaka sabuni lakini taratibu nilianza kuona maji yanaanza kuwa ya uvuguvugu kidogo halafu yanakuwa kama mazito kidogo na yana chumvichumvi. Nikawa nikipaka sabuni haiishi mwilini, ikabidi nisogeze kichwa pembeni kidogo na kufumbua macho.
“Mungu wangu,” nilipiga kelele kwa nguvu baada ya kugundua kwamba kumbe kile nilichokuwa nikiamini kwamba ni maji, zilikuwa ni damu zikimwagika kama maji. Uda mfupi baadaye tayari nilikuwa kwenye mlango wa bafuni lakini cha ajabu, licha ya kutoa loki niliyoiweka wakati nikiingia, mlango uligoma kufunguka, nikawa nagongagonga kwa nguvu huku nikiendelea kupiga kelele.
Wa kwanza kufika alikuwa ni yule msichana ambaye alionyesha kuwa ndiyo mtoto mkubwa wa yule mzee, akasukuma mlango kwa nguvu kutokea nje. Nguvu alizotumia, ukichanganya na kwamba miguu yangu ilikuwa na majimaji, nilijikuta nikiteleza na kuanguka chini kama mzigo akaingia na kupigwa na butwaa kutokana na hali aliyonikuta nayo kwani sikuwa na nguo hata moja na bado nilikuwa nikipiga mayowe ya kuomba msaada.
Alichokifanya, haraka alivua khanga aliyokuwa amejifunga juu ya gauni lake na kunirushia ili nijisitiri kisha haraka akageuka na kutoka, nikamsikia akijifungia mlango wa chumbani kwake, nadhani alijisikia aibu sana kwa hali aliyonikuta nayo.
Cha ajabu sasa, wakati nageuka kutazama kule zile damu zilikokuwa zikimwagika, nilishangaa kuona kinachotoka si damu bali maji na wala hakuna dalili yoyote ya damu. Tayari kaka zangu walishafika na kunikuta nikihangaika kujifunga ile khanga niliyopewa, wakataka kujua nini kimetokea
Kelele hizo kumbe hata baba na yule mwenzake walizisikia, nao wakaja haraka kutaka kujua nini kimetokea.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 14:


ILIPOISHIA:
“MUNGU wangu,” nilijisemea, mapigo ya moyo yakiwa yananienda mbio kuliko kawaida, nikiwa sijui nini kitatokea, hasa ukizingatia kwamba nilikuwa ugenini na ndiyo kwanza tulikuwa tumewasili.
SASA ENDELEA…
ALINIACHIA huku naye akionyesha kushtuka, akashuka kitandani na kuokota khanga yake, akajifunga kivivu na kunionyesha ishara kwamba niingie kwenye kabati la nguo, nilifanya hivyo haraka, nikamsikia akifungua mlango.
“Baba amesema usije ukafunga mlango mkubwa wa nje, watachelewa kuingia ndani kwani kuna kazi wanaifanya.”
“Haya poa,” nilimsikia akizungumza na mdogo wake, akashusha pumzi ndefu na kuufunga mlango, nikamsikia safari hii akifunga kwa funguo kabisa, akaja pale kabatini na kufungua mlango, akanionyesha ishara kwamba nitoke.
Sikulaza damu, nilitoka harakaharaka nikiwa kama nilivyo, na yeye akauachia ule upande wa khanga, ukadondoka chini, tukawa tunatazama kama majogoo yanayotaka kupigana. Alipiga hatua moja mbele, miili yetu ikagusana, akazungusha mikono yake kwenye shingo yangu, na mimi nikiwa sijiaminiamini, nikaukumbatia ‘mlima’ wake.
Nikiri kwamba hiyo ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kuwa kwenye hali kama hiyo na nilichokihisi kwenye mwili wangu, sikuwahi kukihisi kabisa tangu napata akili zangu. Ni hapo ndipo nilipoanza kuelewa kwa nini watu wengi huwa wanayasifia sana mapenzi kwamba ni matamu kuliko asali.
Ni hapo pia ndipo nilipoelewa kwa nini watu wengine hufikia hatua hata ya kutoana roho, baada ya mmoja kugundua kwamba anatembea na mkewe au mpenzi wake. Dakika chache baadaye, nilikuwa nahema kama nataka kukata roho, ufundi wa mikono yake kuvinjari kwenye mwili wangu, ulinifanya mara kwa mara niwe natoa miguno ambayo sikuwahi kuitoa kabla.
Hata sikukumbuka nilifikaje kwenye uwanja wake wa fundi seremala, nilikuja tu kushtukia yeye yuko juu yangu nikiwa nimelala chali, huku nikiendelea kupumua kwa fujo, mapigo ya moyo wangu yakinienda mbio sana na ‘Togolai’ akiwa anazidi kuongeza hasira kadiri muda ulivyokuwa unasonga mbele.
Kwa ufundi wa hali ya juu, alimuelekeza njia ya kupita, nikajikuta nikianza kuzungumza kama bubu, maneno hayatoki wala hayaeleweki, kucheka natamani lakini muda huohuo natamani kupiga chafya, ilikuwa ni hali ya ajabu mno. Safari iliendelea, mwanzo alikuwa akipiga hatua fupifupi lakini baadaye nikaanza kumuona akinogewa na kuongeza huku akitoa ukelele fulani ulioongeza raha kubwa kwenye masikio yangu.
Baadaye ilibidi tubadilishane magoli kwenye mechi ile ya kirafiki isiyo na refa wala jezi, yeye akawa anapeleka mashambulizi Kaskazini mwa uwanja na mimi napeleka Kusini.
Japokuwa hata danadana sikuwa najua kupiga na siku hiyo ndiyo ilikuwa ya kwanza, nilijitahidi kuonyesha kiwango kwa sababu nimewahi kusikia kwamba ukicheza chini ya kiwango, huwa unadharaulika mbele ya viumbe hawa.
Akaongeza mno kasi ya mashambulizi kisha akanikaba kwa nguvu shingoni kama wanavyofanya wale watu wanaopora simu au fedha, akanishikilia kwa nguvu na kunibana, na mimi nikaongeza kasi, nikajisikia hali fulani hivi nzuri sana, akazidi kunibana kisha akaniachia na kudondokea upande wa pili, jasho likiwa limemlowanisha chapachapa na mimi nikiwa hoi bin taaban, nilijikuta nikicheka mwenyewe kwa furaha.
Hakuzungumza jambo lolote kwa dakika kadhaa, baadaye aliinuka na kukaa kitandani, akawa ananitazama kama ambaye haamini kitu fulani.
“Una miaka mingapi?”
“Kwa nini unaniuliza hivyo?”
“Kwa nje unaonekana mdogo lakini wewe ni zaidi ya mwanaume,” alisema na kunikumbatia tena, akaanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu huku akiniambia kwamba ananipenda na anaomba nisimuache ila uhusiano wetu uwe wa siri.
Bado sikuwa naelewa alichokimaanisha, akaendelea na uchokozi wake na hata sijui nini kilitokea lakini muda mfupi baadaye, nilishtukia tukiwa tena dimbani, safari hii kidogo nikawa sina ugeni na uwanja pamoja na mchezo wenyewe.
Mpambano mkali uliendelea mpaka baadaye ambapo ile hali iliyotutokea mwanzo ilitokea tena, tena kwa kila mtu. Safari hii, alipoangukia upande wa pili, haukupita muda mrefu akaanza kukoroma.
Kwa kuwa muda ulikuwa umeenda sana, harakaharaka niliinuka na kuvaa nguo zangu nikaenda kufungua mlango na kutoka huku nikinyata, nikaenda mpaka kwenye mlango wa kile chumba ambacho nitalala na ndugu yangu mmoja.
Kwa bahati nzuri, mlango haukuwa umefungwa, nikaingia mpaka ndani, tayari ndugu yangu naye alikuwa akikoroma, nikajilaza kitandani huku nikisikia uchovu wa kiwango cha juu, karibu kila sehemu kwenye mwili wangu ilikuwa inauma.
Tabasamu pana lilikuwa limechanua kwenye uso wangu, hasa kumbukumbu ya nilichotoka kukifanya ilipokuwa inanijia. Sasa na mimi nilijihisi kuwa mwanaume niliyekamilika. Bado nilikuwa siamini jinsi nilivyoweza kuuangusha mbuyu kwa shoka moja, haukupita muda mrefu nilipitiwa na usingizi.
“Motooo! Jamani moto… nakufaaaa,” sauti za mtu aliyekuwa akipiga kelele kuomba msaada, ndizo zilizonishtua kutoka kwenye usingizi mzito, nikakurupuka huku mapigo yangu ya moyo yakinienda mbio kuliko kawaida, nikatoka mpaka koridoni.
Sikuamini macho yangu kusikia sauti ile ilikuwa ikitoka kwenye kile chumba ambacho usiku huo mimi na yule dada tulilambishana asali. Moto ulikuwa umekolea kiasi kwamba hata sehemu ya kupita haikuwa ikionekana.
Mimi ndiyo nilikuwa wa kwanza kufika eneo hilo kwa sababu sikumkuta mtu mwingine yeyote, nikaona nikisema niende kuwaamsha baba na mama, dada wa watu anaweza kufa bure, nikapiga moyo konde na kuukanyaga mlango ambao ulikuwa ukiwaka moto, ukaangukia ndani.
Sikujali kuhusu moshi mzito uliokuwa umetanda kwani tayari nilikuwa na uzoefu wa kucheza kwenye moshi kwani kule kijijini ilikuwa kama tunataka kwenda kupakua asali kwenye mzinga, lazima tuwashe moto kwa kutumia miti inayotoa moshi mzito. Nilibana pumzi, nikaenda mpaka pale kitandani ambapo nilimkuta akiwa ameanza kuishiwa pumzi kutokana na kuvuta moshi mwingi.
Kwa kuwa mwili wangu ulikuwa na nguvu, si unajua tena maisha ya kijijini yanakufanya uwe ‘ngangari’ kutokana na kazi ngumu, nilimbeba na kutoka naye mpaka koridoni, moto ukawa unazidi kuwaka lakini kilichonishangaza sana ni kwamba haukuwa ukisambaa kwenye vyumba vingine.
Nikiwa koridoni, mikononi nikiwa nimembeba yule dada ambaye alishapoteza fahamu, nilikutana na baba na mwenyeji wake pamoja na mama na mwenyeji wake.
“Kuna nini tena? Rahma kapatwa na nini?” aliuliza baba yake, ni hapo ndipo nilipojua kwamba kumbe jina lake anaitwa Rahma. Sikuweza kuwajibu kwa sababu walikuwa wanamuona hali aliyokuwa nayo, baba yake na baba wakanipokea na kumkimbiza mpaka sebuleni, feni zote zikawashwa.
*(Usikose kutembelea Simulizi za Majonzi )
“Kumetokea nini?”
“Moto.”
“Motoo?”
“Ndiyo, chumbani kwake kunawaka moto,” nilisema huku nikishangaa kwa nini walikuwa wakiniuliza mara mbilimbili jambo ambalo lilikuwa wazi. Harakaharaka walielekea kule chumbani wakati mama yake akihangaika kumpa huduma ya kwanza lakini muda mfupi baadaye, walirudi mbiombio.
“Umesema chumbani kwake kunawaka moto?”
“Ndiyo, alikuwa anapiga kelele za kuomba msaada ndiyo nikaamka na kwenda kumsaidia, nilisema, nikaona baba na mwenyeji wake wakitazamana, sikuelewa walikuwa wanamaanisha nini. Ilibidi haraka nirudi kule chumbani kwake ili kuangalia moto umefikia wapi.
Cha ajabu, mpaka nafika mlangoni hakukuwa na moto wala dalili za moto isipokuwa mlango ulikuwa umevunjwa na nakumbuka vizuri mimi ndiye niliyeukanyaga kwa nguvu ukavunjika.
Huku nikiwa nimepigwa na butwaa, niliingia ndani ambako muda mfupi uliopita moto mkubwa ulikuwa umetanda kila sehemu lakini cha ajabu kila kitu kilikuwa sehemu yake, nikageuka huku nikiwa siamini, nikakutana na baba na mwenyeji wake ambao kumbe walikuwa nyuma yangu wakinitazama.
“Ulimaanisha chumba hiki au kingine?”
“Hikihiki, nashangaa sijui imekuwaje, kwani nyie hamjasikia kelele za kuomba msaada?”
“Mimi nimesikia kelele za mlango kuvunjwa tu, basi.”
“Mungu wangu,” nilisema kwa hofu kubwa, nikijihisi kama nipo kwenye ndoto ya kutisha.
“Na vipi kuhusu hii?” baba aliniuliza, huku akinionyeshea nguo yangu ya ndani iliyokuwa pale chini ya kitanda cha Rahma. Kumbe wakati muda ule navaa nguo zangu, niliisahau si unajua tena maisha ya kijijini kuvaa hiyo kitu hasa kwa sisi wanaume siyo kitu cha lazima sana? Aibu ya mwaka ilikuwa imenifika.
“Eti kumetokea nini kwani?” sauti ya mama yake Rahma ilisikika, akiwa ameongozana na binti yake ambaye sasa fahamu zilikuwa zimemrudia, wakiwa pamoja na mama. Nilishindwa hata cha kujibu, mate yakanikauka ghafla mdomoni.
Je, nini kitafuatia? Usikose next issue
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom