Simulizi: Macho ya ajabu

Simulizi: Macho ya ajabu

Sehemu ya pili
.....Ilipoishia.......
Hatimaye Walitoka wote na kufika wodini,Humph
akiwa kitandani anaweweseka huku Mara kwa Mara
akimtaja Sor,Mama Humph akamkumbatia mumewe
machozi yakizjdi kumtoka kwa uchungu.
.......Shuka nayo.........
Ukweli Ni kwamba alimuonea Huruma mno
mwanaye.
Lisa alirudi nyumbani kwao akiwa mpweke
ajabu,mawazo yalimtafuna mwili mzima,hata taxi
aliyopanda hakukumbuka kulipa baada ya
kufikishwa kwao. Dereva alishuka upesi na
kumfuata akiwa nusu akikimbia na nusu kutembea.
Kabla Lisa hajaingia getini mwa nyumba yao
akasikika dereva akiita kwa nguvu
"Binti!,Binti!" Lisa hakugeuka alizidi kuendelea na
safari
"Hela yangu vipi we binti?" Dereva alimvuta Lisa
blauzi huku akiuliza kwa ghadhabu
"Hela gani?,we nani kwanza?" Lisa alionekana
kumshangaa yule dereva ambaye sasa sura ilianza
kutengeneza matuta ya hasira.
"Kwani hii gari uliyopanda ni ya baba yako eti
wewe?" Dereva alihoji kwa hasira huku akimtikisa
Lisa ambaye hakuwa akijali kitu,hali iliyopelekea
mzozo mkali baina yao.
Mlinzi wa getini kwa akina Lisa alitoka nje mbio
mbio na kuanza kuamua kesi ile asiyoijua ndipo
Lisa akapata upenyo wa kuingia ndani akimuachia
mlinzi kasheshe ile..
Mpaka asubuhi Lisa alikuwa na kazi ya kuitazama
picha ya Humph biila kupata majibu ya kile
anachokiwaza. Alivyoona kumekucha akajiandaa na
kuelekea hospitali,alimkuta mama wa Humph akiwa
pale usiku mzima ulimuishia pale bila kujali chakula
wala kutafuta mahali sahihi pa kulala.
Alifika na kumuamsha taratibu mpaka
akaamka,baadaye waliingia wodini baada ya
kuruhusiwa kwenda kumtazama Humph.
Lisa aliketi kitandani na kumshika Humph kichwani.
"Dokta amesema mchana atakuwa ameshaamka
hivyo usiwe na shaka sawa mwanangu" mzee Kasai
alimwambia Lisa
"Sawa baba" Lisa alijibu
Mchana unafika Humph anafumbua macho taratibu
Lisa anawahi kumshika mkono na kutabasamu
lakini Humph haoneshi hata dalili ya
kutabasamu,Dokta Alex anaingia na manesi wawili
baada ya kuitwa
"Mfanyieni utaratibu wa kula" alizungumza Dokta
Alex wakati amemaliza na kumcheki Humph.
"Usiwe na hofu binti rafiki yako ni mzima kabisa na
baadaye ataruhusiwa,jitahidi kuwa naye karibu
maana vitu vingi hakumbuki hapo alipo tuliweka
kumbukumbu ya vitu vichache"
"Dokta Alex alimwambia Lisa na kumfanya aduwae
kidogo na kutambua kitu kipya kuwa Humph
hakutabasamu kwasababu hamkumbuki.
Baada ya Humph kuruhusiwa na kurudi nyumbani
Lisa alikuwa naye karibu mno kwa kila kitu lakini
kwa Humph haikuwa hivyo yeye alimchukulia
kawaida tu.
Lisa hakuona shida,wakati wameketi pamoja Lisa
aliamua kuanzisha maongezi ili kumuweka sawa
Humph.
" Hey,um! Nilisahau kujitambulisha toka awali
uliponiona,naitwa Lisa ni rafiki pekee wa karibu
kwako nikiamanisha "girlfriend" wako tangu tukiwa
tunasoma sekondari" Lisa aliongea huku akiminya
vidole vyake
"Ongeza Sauti kidogo mdada sijakusikia vyema"
Humph alijibu kwa pozi huku akiondoa (spika
ndogo za masikioni) earphone.
"Naitwa Lisa Ni mpenzi wako wa siku nyingi" Lisa
alijibu akiwa ameanza kukasirika kutokana na tabia
mpya aliyokuwa nayo Humph
"Mmh! Mpenzi tena,aaah! Sidhani,mbona sijawahi
kuwa na mpenzi,wewe Ni wa wapi labda?" Humph
akauliza kwa madoido akionesha wazi
kutomfahamu Lisa kiundani.
Lisa akatoka mbio analia mlangoni akapishana na
mama yake Humph lakini hakumsemesha,licha ya
mama Humph kujaribu sana kumuita Lisa bado
haikusaidia
"Umemfanya nini mtoto wa watu?" Ilikuwa Ni kauli
ya kwanza ya mama Humph baada ya kuingia ndani
na kumuuliza Humph
"Sijui,mi' amejitambulisha kuwa ni mpenzi
wangu,nikamuuliza wa wapi maana sijawahi kuwa
na mpenzi,ndipo akachukia na kutimua mbio huku
akilia" Humph alijibu bila wasiwasi Ni kama alikuwa
akiongea na rafikiye.
"Umeonesha dharau kubwa sana mbele yake,yule
msichana amejitoa kwa hali na mali isitoshe Ni wa
kwako kwa muda mrefu sasa haukupaswa
kumfanyia vile,hakustahili kwa kweli" mama Humph
alilalama
"Mama simfahamu yule binti na sitokaa nimfahamu
kamwe,na kama Ni wangu kwanini asiwemo karika
kumbukumbimu zangu za kila siku" Humph alisema,
mama Humph na mumewe pamoja na familia nzima
waliapa kukaa kimya kuhusu matatizo ya Humph ili
yasijirudie hivyo hawakuthubutu kusema lolote
"Kamuombe msamaha,mjinga mkubwa wee!"
Humph akainuka huku akiongea "sijamkosea mimi "
Mama Humph akaishia kutikisa kichwa tu huku
akionekana kutofurahia tabia mpya ya Humph
iliyotokana na kufutwa kumbukumbu zake
zilizoondoka na mambo mengi mno,mpaka wazazi
wake alikuwa akiwachukulia kama jamaa wa
kawaida walio karibu yake.
鈽呪槄鈽匤ourney to the falling Mountain鈽呪槄鈽?
鈽呪槄鈽匰afari ya mlima unaoanguka鈽呪槄鈽?
"Habari za asubuhi hii ndugu wanachuo,nafurahi
kufika siku hii ambayo imerejea tena mbele
yetu,kwa wale wageni wa mwaka wa kwanza yaani
wanachuo wapya hawalitambui suala hill na itakuwa
Ni Mara yao ya kwanza kulisikia" Akatulia kidogo
Mkuu wa chuo msaidizi akitafakari usikivu wa
wanachuo kwa muda kisha akaendelea
"Tuna mashindano mbalimbali ambayo huendeshwa
na kufanyika nje ya chuo chetu yakijumuisha vyuo
vingi vinavyotuzunguka,na kawaida yetu huwa
tunafanyia mashindano haya katika kisiwa cha
falling mountain (mlima unaoanguka) pia tutakuwa
na utalii wa muda katika milima yake na misitu pia
inayosemekana kubeba utajiri mkubwa pamoja na
kishamiri maajabu mengi ya kihistoria"
Wanachuo wote wakalipuka kwa shangwe nyingi
lakini mkuu wa chuo msaidizi hakuwa amemaliza
hivyo akanyoosha mikono kuwanyamazisha
wanachuo wote
"Hatuna muda mwingi,kesho safari itaanza na
niseme tu poleni kwa kuwastukiza,natumaini
mtajiandaa kuanzia sasa" alimalizia Mkuu wa chuo
msaidizi na kuwaacha wanachuo wote wakilipuka
kwa shangwe nyingi ikiwemo Humph
Lisa hakuwa na furaha hata kidogo mbaya zaidi
alimuona Humph alivyoifurahia safari ile ikiwa si
kawaida yake kabisa.
"Mambo mdada" Lisa akistukia akisalimiwa na
alipogeuka aliduwaa kuona ni Humph,akabaki
kujiuliza ni saa ngapi mtu yule amemfikia lakini
ukweli ulibaki kuwa muda alioutumia kuzama katika
dimbwi la mawazo ndiyo muda alioutumia Humph
kufika pale.
"Poa tu" Lisa alikumbuka kuijibu salamu ya Humph
lakini akiwa mnyonge mno
"Samahani,ulisema u nani vile?" Humph aliuliza
akiwa anatazama huku na kule
"Lisa" Lisa alijibu kwa mkato huku akimtazama
vyema Humph ambaye hakujua kama binti huyo
alikuwa akimuangalia.
"Sikia binti,Jana nusura mama apasuke ulivyotoka
unalia,sasa Fanya yaishe maana hapendi kabisa
nikichokifanya kwako" Humph alisema akiwa
anamuangalia binti mmoja aliyekuwa
anatabasamu,macho yao yakagongana
"Yameisha toka Jana Humph" Lisa alijibu akiwa
hana amani
"Poa,alafu nimempenda yule mdada sijui anaitwa
nani?,hey! Vipi unamfahamu hata kwa jina labda?"
Humph alimuuliza Lisa akiwa bado anamtazama
yule binti.
Lisa hakuvumilia ule upuuzi ulioonekana dhahiri
kuwa ni dharau kutoka kwa Humph,akaamua
kuondoka kimya kimya.
Humph anakuja kugeuka baada ya kukosa
jibu,anamkosa Lisa pale alipokuwa
amesimama,akaangaza huku na kule asimuone
kutokana na uwingi wa wanachuo.
 
Sehemu ya tatu
.....Ilipoishia.......
Humph anakuja kugeuka baada ya kukosa
jibu,anamkosa Lisa pale alipokuwa
amesimama,akaangaza huku na kule asimuone
kutokana na uwingi wa wanachuo.
......Shuka nayo......
"Shiit!" Humph akajisemea na kumfuata msichana
aliyemuona.
"Mambo mrembo" Humph alimsalimia msichana
yule huku akimzunguka kufaidi alivyoumbwa
akaumbika,naye msichana yule hakuwa nyuma
katika hiyo fani,akajigeuza geuza kama mgombea
urembo jukwaani au umiss na kumfanya Humph
ameze funda kubwa La mate.
"Niite Humph sijui mrembo wangu waitwa nani?"
Humph aliuliza akiwa na kimuhe muhe cha
kumfahamu binti yule.
"Sarah,niite hivyo" msichana yule alijibu kimadaha
huku aiizidi kujibinua binua.
"Tuongee faragha Tafadhali!" Humph akajaribu kete
yake na bila kukataliwa akaondoka na mrembo
yule. Muda wote ule Lisa alikuwa anausoma mchezo
unavyokwenda,chozi lilimshuka akainua kitambaa na
kujifuta.
鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄
Hatimaye safari ilianza,Humph pamoja na wanachuo
wengi walikuwa walikuwa ndani ya meli ghali ya
kifahari inayomilikiwa na chuo kile cha Sayansi
kilichojulikana mji mzima wa Reycity kwa sifa zake.
Bahari ilikuwa shwari,wanachuo wote walikuwa
tayari wanaiacha bandari ya lake shore kama
unaikumbuka vizuri ni bandari ambayo Samson
alipambana na Humph akiwa katika umbo LA sokwe
ume.
Lisa aliandika ujumbe mrefu wa maneno kupitia
simu yake akimkumbusha Humph kuwa aliwahi
kupambana eneo hilo.Humph alishangaa kuwa ni
madudu gani ambayo binti yule alikuwa alimwambia
pia stori ilikuwa mpya sana kichwani mwake,muda
huo alikuwa amempakata(kumlea) Sarah mapajani
mwake,mapenzi yakiwa yameanza kupamba moto.
Mpaka inatimia usiku bado safari ilikuwa
ikiendelea,kilichowafanya wanachuo wasichoshwe
na safari ni starehe zilizopatikana ndani ya meli
ile,safari ile ilitarajiwa kufika kikomo siku inayofuata
mida ya mchana katika kisiwa cha mlima
unaoanguka.
Asubuhi wanachuo walikuwa wamejipanga kutazama
mazingira baharini ghafla upepo usiojulikana
ulipotoka ukaanza kuvuma taratibu na kuwavutia
walio wengi na hatimaye bahari ikaanza
kuchafuka,upepo ukazidi kuwa mkubwa ,Sarah
alikimbia na kumuacha Humph.
Wanachuo wengine nao walikimbia kuingia ndani ya
meli,papa wakubwa wakaanza kuruka kutoka
upande mmoja kuelekea mwingine,Humph alianza
kutetemeka ni kama anayepigwa na shoti,mwisho
akaanguka chini na kulala kwa uoga huku akiziba
kichwa.
Wanachuo walikimbilia ndani ya meli,Lisa akiwa
wa.miongoni mwao lakini roho ilisita kuingia ndani
ya meli hivyo akafanya kugeuka nyuma,. alipogeuka
akamuona Humph akiwa amebaki,kengele ya hatari
ikapiga kichwani mwake,
Wanachuo wengi walipita na kumkanyaga kanyaga
Humph mgongoni kila mtu akijali maisha yake
kuyaokoa. Lisa alivyoona vile roho ilimuuma
akaamua kujitosa na kurudi alipo Humph, Papa wa
kubwa walikuwa wakiwakosa kosa wanachuo
kwaajili ya kitoweo,Lisa akafanikiwa kumfikia
Humph na kumshika mikono.
"Niache,niache sitaki kufa Mimi niache,usinibebe
Mimi nakuomba" Humph alilalamika akiwa
amefumba macho.
Lisa akampiga Kofi moja la nguvu mgongoni na
kumfanya Humph afumbue macho
"Wewe u...." Humph hakumalizia kauli yake Lisa
akawa amemnyanyua kwa.nguvu,walikuwa
wamebaki wao peke yao wengine wote walikuwa
tayari ndani ya.meli
Walikimbia kidogo kama hatua mbili,papa mmoja
akapita juu kidogo ya kichwa cha Lisa,mkia
unapomalizika ukamgonga Lisa kichwani na
kumfanya aanguke vibaya akibiringika na kupoteza
fahamu.
Humph akasimama akiwa ameshikwa na
butwaa,kwa Mara ya kwanza nafsi yake
inamsuta,akajisihisi maumivu makali sana moyoni
mwake baada ya kumtazama Lisa akiwa katika hali
ile. Pale pale macho ya Humph yakaanza kutoa
mwanga,hakuwa yeye tena,alihisi nguvu ikimtembea
mwili mzima kwa kasi ya ajabu.
Alijikuta akipata ujasiri wa ajabu na kujitoa
kimasomaso,alikuwa akiwakwepa wale papa kwa
namna ya ajabu mno, bado macho yake yalionekana
kuwa na mwanga mweupe bila yeye kujitanbua.
wanachuo waliokuwa wakishuhudia kinachotokea
walibaki kimya wasiamini kinachotokea kwa muda
ule,walishangazwa sana na ule uwezo wa Humph
ambao aliupata kwa muda mfupi na hawakuwahi
kumuona akiwa vile hapo kabla kutokana na upole
wake namuda wake mwingi alikuwa akiutumia na
Lisa kipindi hicho na hata walipoachana na Humph
kubadili tabia wanachuo walikuwa wakishangaa tu
na kujiuliza mengi bila kujua yaliyomo katikati ya
Humph na Lisa.
Humph alimfikia Lisa na kumnyanyua kwa
nguvu,akaanza kukimbia naye mpaka ndani na
kupokelewa na watu wa huduma ya kwanza. Humph
akabaki amesimama,macho yake yakiwa kawaida
kwa muda huo,akawa anajiuliza kwanini nafsi na
moyo wake vipitie maumivu mkali namna ile
kwasababu ya binti yule.
Alijiuliza sana,kwanini Lisa ajitose kumuokoa ikiwa
huwa anamfanyia mambo ya ajabu ajabu tena
katikati ya papa wote wale.
Humph anaamua kupotezea akiamini binti Lisa ana
mambo yake tu yanayomfanya amfuate fuate kila
mara japo kwa upande mwingine alihisi kuna jambo
LA ziada asilolifahamu.
Lisa anazinduka na kuhisi kichwa kizito anapotaka
kuamka,anakutana na sura ya Humph ikiwa na
tabasamu pana.
"Pole ila siku nyingine usijaribu kumuokoa mtu ikiwa
huna huo uwezo,utaingiza maisha yako hatarini bila
maana yoyote" Humph alisema
"Nilikuwa naokoa kitu changu cha thamani" Lisa
alijibu akiwa amemkazia macho Humph
"Mmh! Kitu cha thamani?,kitu gani hicho cha
thamani kupita uhai wako?" Humph alihoji huku
akijisogeza na kuketi vizuri jirani na Lisa huenda
angepata jambo fulani la muhimu analohisi
linajificha lakini kabla hajajibiwa Sarah akaingia
ndani ya kile chumba,Humph akageuka kumtazama.
"Hupaswi kufahamu hicho kitu alafu sikuwa na
muda wa kukusaidia kinyago kama wewe,ni huruma
tu ziliniponza" Lisa akajibu kwa jeuri baada ya
kumuona Sarah.
Sarah alivyosikia lisa amemtusi bwana 'ake
akasogea ili amfunze adabu lakini Humph akamzuia
na kumuomba Sarah watoke nje huku akimuahidi
Lisa kuwa atamtembelea kujua hali yake japo alihisi
wazi kuwa Lisa anaficha kitu Fulani muhimu maana
Humph alipogeuka nyuma wakati anaondoka
alishuhudia mashavu ya Lisa yakitiririsha machozi
ikiwa ni ishara ya wazi kuwa Yale maneno
aliyoyatamka Lisa yalikuwa yakimuumiza yeye
mwenyewe ndani kwa ndani ijapokuwa aliyatamka
kwa kinywa chake.
鈽呪槄鈽匢n another World鈽呪槄鈽�
鈽呪槄Katika Ulimwengu Mwingine鈽呪槄
Baada ya Humph na Mzee Mandevu kumuingiza Sor
ndani ya Portal,alienda moja kwa moja mwenye
ardhi ya mfalme Sangu ambayo kwa muda huo
ilikuwa ni ardhi ya waishio milele(immortals).
Sor hakupumzika alianzisha vita kubwa dhidi ya
utawala ule ili atwae madaraka na kuiongoza ardhi
ile, Sor alipambana na watu waliokaidi amri yake ya
kuungana nae akiwa kama Malkia wao mpya baada
ya kumuangamiza Mfalme Sangu ambaye nguvu
kubwa aliyokuwa akiitegemea ilitoka kwa mzee
Mandevu.
Sor alipita makabila mbali mbali akiwa na kichwa
cha mzee Mandevu,alipita makabila ya wanaotumia
moto tu,maji,upepo,radi,ngao na mengine kedekede
akitoa ofa ya wao kuungana naye kisha wanaobaki
hawana kwa kushika wanateketezwa wote,na kama
kabila zima likikataa kuungana naye hakuwa na
muda wa kuwabembeleza aliua wote.
Kumbuka:
Mapenzi yanauma hasa pale mtu ambaye ulikuwa
ukimpenda akibadilisha mwenendo ikiwa bado
unamuhitaji,usijali kama unampenda kuwa na subira
amini siku moja atabadilika na kukurudia,usikate
tamaa. Chukua hatua anza sasa
 
Sehemu ya nne
.....Ilipoishia.......
Sor alipita makabila mbali mbali akiwa na kichwa
cha mzee Mandevu,alipita makabila ya wanaotumia
moto tu,maji,upepo,radi,ngao na mengine kedekede
akitoa ofa ya wao kuungana naye kisha wanaobaki
hawana kwa kushika wanateketezwa wote,na kama
kabila zima likikataa kuungana naye hakuwa na
muda wa kuwabembeleza aliua wote.
......Endelea nayo........
Alipofika kwenye kabila la watu mwenye kutumia
barafu,mzee mmoja ambaye ni kiongozi wa ukoo
alimficha mjukuu wake wa kike na kumuonesha njia
ya dharura maalumu kwaajili ya kumfikisha
duniani,alimpa kidani kidogo chenye alama ya
fimbo ya mzee Mandevu akiimwanbia kuwa ni
lazima ampate mtu huyo ili kuja kuukomboa
ulimwengu wao.
Mzee yule alitoka na kujitolea kupambana na Sor na
endapo angeshindwa kabila lake lote lingekuwa
chini ya Sor.
Nani kama Malkia Sor?, hakuna malkia aliyewahi
kuifikia nguvu yake hata robo iweje kwa mzee kama
huyo,Sor hakusubili kipenga wala kujiandaa alinena
neno moja tu "thunder" akiamanisha "radi",ni kitendo
cha ghafla tu anga liliunguruma kwa nguvu mzee
yule akababaika na kuzikusanya barafu nyingi ili
kukabiliana na radi ile,Bahati haikuwa kwake baada
ya radi kubwa kumchangua vipande vipande.
Ilikuwa ni picha mbaya kwa watoto lakini hawakuwa
na wakumlilia,wote walisujudu mbele ya Sor naye
akaunguruma kama simba dume anayefurahia
mawindo yake.
Binti aliyetoroshwa na mzee yule alipatwa na ubaridi
wa ajabu,sauti ya babu yake ikimsihi kuwa arudi
kuipambania ardhi yake,hapo aliamini hayupo nae
tena. " upumzike kwa amani" alisikika akimalizia
kauli hiyo na kuserereka kwenye chemba ndefu
iliyokuwa ikielekea kusiko julikana.
Akiwa katikati ya chemba ile alishangaa kuwaona
vijana wengine kama yeye nao wakiwa
wanaserereka kuelekea mahali anapokwenda,aka
tambua kuwa hayupo peke yake.
Walifika mahali wakatokea duniani,kila mtu
alitemwa na chemba ile kivyake,waliporomoka
kama watu waliojiachia kutoka ndani ya bdege ikiwa
angani.
Baada ya Sor kumaliza vita ndani ya ulinwengu wao
huku akiwa amejinyakulia jeshi kubwa anaadhimia
kwenda duniani.
Akiwa anawahutubia watu wake alisikika akisema
"Tumebakiza siku chache kuhamia duniani na
kutwaa kila kitu pia nitakuwa mtawala daima,njia
ipo mikononi mwetu na nia tunayo,ikitimia siku ile
ambayo ni mwisho wa karne kumi mlango
utafunguka na nitawaruhusu watu wa jamii yangu
kwenda dunian"
Sor alijinadi mengi akiwa na taji la umalkia lakini
kwa kila sentensi aliyoiongea akili yake ilimuwaza
Humph. Sauti nyingi za nderemo zilisikika
zikiifurahia safari hiyo ambayo muda si mrefu
ingejitokeza,walifurahi kwasababu wengi Wao
walikuwa wakikusikia tu huko duniani.
Sor aliitoa ile portal (njia ya kuelekea duniani) na
kunyoosha mkono juu akiwa ameishika,watu
wakazidi kushangilia.
鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽�
Humph alikuwa ndani akijiandaa kwenda kwenye
mashindano ya mbio ndefu ghafla akaanza kuona
mawenge,kichwa kikaanza kumuuma. Akashika
kichwa lakini masikio nayo yalikuwa yanazisikia
kelele za watu wakishangilia.
Akainuka lakini akaishia kuyumba yumba huku na
kule akijitahidi kuzuia zile kelele,Mara matukio
ambayo aliyafanya huko nyuma yakaanza
kumuandama kichwani mwake yakipita kama
mapicha picha ya filamu Fulani isiyoeleweka,ma
pigo yake ya moyo yakaanza kubadilika.
Alianza kuhema juu juu na mwisho akakaa chini
akatulia tuli huku jasho jingi likiwa limemtoka.
Wanachuo wenzake walifika na kumwambia kuwa
zamu yao imefika,hawakujua kama Humph
amekumbwa na matatizo ya ghafla.
Humph aliinuka kwa kujikaza akiwa bado ana
mawenge,walifika na kukaribishwa na wasichana
waliotoa show uwanjani pale kisha wakawaachia
nafasi ya kuanza rasmi mashindano Yale.
Walijipanga mstari na kujitayarisha wakisubiri amri
ya muongozaji,wanachuo na watu waliopata nafasi
ya kwenda kushuhudia michezo ile walikuwa
wakiwashangilia kwa nguvu.
Kipenga cha kwanza kililia wakajiandaa tayari
kuanza mashindano,kipenga cha pili kikaruhusu
mbio zianze,Humph akakamata mkia,kichwa
kimemjaa mawenge akiwa anayashuhudia mapicha
picha kibao,anahema kwa shida mno huku jasho
likizidi kumtoka mwili mzima,mmoja wa washiriki
kutoka chuo chao akalegeza kamba na kumngoja
Humph
"Usikiaibishe chuo chetu Humph hatukuja kushindwa
huku Bali kushinda na kama unavyoona mzunguko
bado ni mkubwa,jikaze" Humph aliambiwa alafu
jamaa akaongeza mwendo mpaka nafasi ya pili.
Ilikuwa ni mbio ndefu za Marathoni,mzunguko wa
kwanza tu Humph anaonekana kuwa hoi,wanaingia
mzunguko wa pili bado Humph yupo
mbali,mzunguko wa tatu unafika Humph bado yupo
mzunguko wa pili,mpaka wanaingia mzunguko wa
nne bado Humph nd'o anaingia mzunguko wa tatu.
Si Lisa wala Sarah aliyekuwa ameridhika na
ukimbiaji ule wa Humph, Baada ya mwendo mfupi
Humph alianza kujihisi joto Kali mwilini,mwanga
hafifu ukaanza Ku one kana machoni mwake ni
kama tochi inayozima na kuwaka,ule mwanga ulizidi
kuongezeka nakupungua kila dakika.
Lisa alikuwa amekamata mawani ya shetani
(darubini) akiangalia mchezo unavyozidi kwenda
huku Mara nyingi akimsihi Humph na kumuonea
huruma huku akijisemea "usiwe mzembe mbona
unaniangusha shujaa wangu,jitahidi"
Humph akawa anaisikia sauti ya msichana ikigonga
ngoma zake za masikio ikimtaka ajitahidi,yeye si
mzembe. "Lisaaaaa!!" Sauti ilimtoka Humph na
mwanga machoni ukaongezeka,Lisa alipoangalia
macho ya Humph akashangaa kuuona mwanga
uliopotea kwa kipindi kirefu machoni mwa Humph,
tabasamu mwanana likamtoka na mwisho meno
yote akayaanika nje kwa furaha.
Humph alianza kuona vizuri alipotupa macho
upande wa pili wenzake walikuwa wanaingia
mzunguko wa mwisho,yeye yupo mzunguko wa tatu
katikati,hesabu za haraka zikakivaa kichwa
chake,miguu ikachanganya,watu wote wakatulia
uwanja mzima wakishangaa Yale maajabu ya
Humph aliyekuwa akikimbia kama anafukuzana na
upepo.
Sauti ya Lisa pekee ndiyo iliyosikika ikishangilia,Sa
rah alikuwa ameshatoka muda mrefu baada ya
kuudhika pale ambapo Humph alikuwa ameshika
mkia hivyo aliondoka mapema ili aibu ile abaki
nayo Humph pekee.
Humph bado aliisikia ile sauti ya Lisa akageuka
kumtazama macho yake yalimuona vyema kabisa
pale juu,akatoa tabasamu nzito,Lisa naye akazidi
kupunga mkono kwa furaha.
Watu nao waliibuka kidedea ni kama waliozinduliwa
kutoka usingizini. Lakini ghafla miungurumo mizito
ikaanza kusikika angani huku wingu zito likitanda
ambalo halijawahi kutokea hapo kabla
Watu walitulia kimya ni kama shetani amepita eneo
hilo ,vyote hivyo vilitokea sambamba na mabadiliko
ya Humph.
鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄鈽呪槄
Katika kisiwa cha mlima unaoanguka "the falling
mountain" radi na miungurumo vilizidi kuiandama
kila kona ya kisiwa hicho,hali ilionekana kuwa
mbaya kuliko sehem ambayo wanachuo walifikia.
Kitu cha duara kikichoambatana na moto kilitoka
angani na na kudondoka katikati ya msitu ule ,muda
huo huo milimani kulikuwa na wingu zito leusi
likizunguka,radi moja matata ilipiga ikiwa
imeteremsha kitu kilicho tu a kwenye kwamba
mgumu na kusababisha sehemu kubwa ya mwamba
ule izame chini.
Si hapo tu bali upande ule ule wa kisiwa cha the
falling mountain maeneo ya baharini maji
yalionekana kuacha uwazi wa duara na kutengeneza
shimo kubwa kwa juu,zile radi ziliendelea kupiga na
kuzidi kuifanya sehemu ile kutisha zaidi na zaidi.
Radi kubwa iliporomoka ikiambatana na mlio
mkubwa wa kutisha na kusababisha kitu cha bluu
kilichojitengeneza kama mpira kushuka kwa nguvu
kuelekea ndani ya maji pale palipojitengeneza
mduara ule wa maji.
Kumbuka:
Kama hukipendi kitu kibadiilishe,na kama huwezi
kukibadilisha badili muelekeo, usilalamike. Chukua
hatua anza sasa.
 
Sehemu ya tano
.....Ilipoishia.......
Radi kubwa iliporomoka ikiambatana na mlio
mkubwa wa kutisha na kusababisha kitu cha bluu
kilichojitengeneza kama mpira kushuka kwa nguvu
kuelekea ndani ya maji pale palipojitengeneza
mduara ule wa maji.
......Shuka nayo......
Upande wa pili mbio zilikuwa zimepamba moto
uwanjani,Humph akiwa anajitahidi kukimbia ili
aunyakue ushindi,sekunde kadhaa zilikuwa zmesalia
mashindano yafikie ukingoni. Lisa alikuwa
anashangilia kwa furaha mpaka anaruka ruka
akiamini Humph amerudiwa na fahamu zake yaani
kumbukumbu.
Humph alizidi kuishangaza halaiki ya watu kwa jinsi
alivyokimbia kama anayefukuzia upepo,tayari
alikuwa katika nafasi ya tano huku akiwa acha
wapinzani wake wakigubikwa na mshangao,si Wao
tu hata maahabiki uwanjani walikuwa wakijiuliza
sana kuhusu Humph maana wengine walithubutu
hata kusema kuwa yeye si nwanadamu wa kawaida.
Kadri Humph alivyoongeza kasi ndivyo radi na
miungurumo ilivyozidi kupamba moto,Humph
akashika namba moja na mwisho akavuka mstari na
kufikia mwisho wa mashindano akiwa acha wenzake
mbali kiasi.
Shngwe za mashabiki ziliongezeka maradufu
,wanachuo wenzake na wengine wote waliinuka na
kushabikia kwa nguvu.
Humph hakuchukua hata dakika tano alikuwa
akipumua kwa nguvu mno wakati huo akiwa
amebebwa juu juu,kizunguzungu kikali kikamshika
ghafla Giza nene likamuandama machoni na
mwisho akalegea na kupoteza fahamu.
"Humph! Humph! Humph! Humph!....." Sauti za
watu zilisikika zikimuita Humph ambaye nd'o
kwanza alikuwa anazinduka na kushangazwa na
umati wa watu ukiwa umemzunguka na sehemu
wakiacha wazi iili hewa ichukue mkondo wake.
Cha kwanza Humph alishika kichwa Chad ambacho
bado kilikuwa kikimuuma,wanachuo walimsaidia
Humph kuinuka,mchezo wa mbio ndefu ndiyo
mchezo pekee uliokuwa wa mwisho kufanyika eneo
hilo hivyo sherehe zilirindima na ugawaji wa medali
ukiwa unaendelea ambapo Humph alipata medali ya
ukimbiaji wa mbio ndefu "marathoni" huku akitajwa
kuvunja rekodi ya eneo hilo.
Lisa alimchunga Humph mpaka kwa daktari akiwa
anaamini kuwa kumbukumbu zimemrudia
barabara,daktari alimchukua baadhi ya vipimo hasa
kichwani na kutoa majibu kuwa kuna hali Fulani ya
vitu kama kumbukumbu vinavyoitesa akili yake kwa
kurudi nakupotea.
Hapo ndipo Humph alipotambua kwa kiasi Fulani
kuwa alishapotelewa na kumbukumbu zake za
zamani,akili ikamtuma kuwa huenda ni kweli
alifanya makosa kumtenga Lisa na hakuwa na hisia
naye kabisa.
Hakufikiria sana suala lile akamfuata Sarah ambaye
mpaka muda huo alikuwa akijishauri amfuate
Humph au la ! Kutokana na kitendo cha kumtenga
Humph akiwa kwenye mashindano pale uwanjani.
"Vipi Mpenzi mbona umenyong'onyea hivyo?"
Humph alimsemesha Sarah
"Najihisi baridi mwili mzima" Sarah aliongopea
Humph akamsogeza jirani na kumkumbatia
Sarah,Lisa alitoka katika chumba cha daktari
akawakuta Humph na Sarah wakiwa katika hai ile.
"Ina maana kumbukumbu hazijamrudia tu,aaah!" Lisa
alijisemea kwa hasira na kupita karibu yao alipofika
akawapandisha na kuwashusha kwa macho yake
kama mdoli huku akajitikisa kidogo alafu akaachia
sonyo refu na kuondoka haraka haraka kwa hasira.
Humph na Sarah wakabki macho kodo.
★★★★Rise of the Snowgirl★★★★
★★Kuibuka kwa Msichana Wa Barafu★★
Humph, Sarah,Lisa,John,Sajna na Like walikuwa
katika ziara yao ya mwisho katika misitu ya the
falling mountain wakitafuta sampo ya mimea
kwaajili ya utengenezaji wa dawa za magonjwa sugu
na kufanya tafiti ndogo ndogo katika misitu ile.
Wao kama wanachuo wa chuo cha Sayansi walihisi
kuwa misitu ile inaweza kuwa na mimea mahsusi
itakayosaidia kutengeneza dawa hizo maana miti ya
eneo lile ilikuwa tofauti na sehemu yoyote ile yamiji
ya pembezoni na ndani ya jiji la Reycity.
Lisa alichukia sana kuwekwa kwenye timu ya
Humph maana muda wote Humph alitembea
naSarah wakiwa wameshikana viuno,lile suala
lilimuuma Lisa si kidogo hasa ukizingatia Humph
alikuwa mtu wake.
Lisa aliamua kuwa karibu na Like ili kujiridhisha na
kupoteza muda japo kila hatua waliyoenda roho
ilizidi kumuuma vilevile .
Sajna alimuita Humph pembeni wazungumze,Sarah
akabaki peke yake akasogea sehemu Fulani yenye
miti ya maua mengi ya zambarau,kazi yake ikawa ni
kushika na kunusa harufu ya maua Yale . Lisa
akajichomoa kwa like na kusogea jirani na Sarah
akijifanya nae ananusa Yale maua.
"We Malaya " Lisa aliimuita Sarah ambaye aligeuka
haraka na cha ajabu akamfuata Lisa kwa hasira za
kuitwa "Malaya",akaishia kukamatwa namikono
imara ya Lisa iliyomkunja vyema mpaka kwenye
Yale maua.
"Unaniumiza Lisa,tatizo nini?" Sarah alihoji akiwa
anagugumia kwa maumivu
"Unajifanya haujui sio?,umenichukulia bwana 'angu
alafu bado unajiona gwiji unanijibu utakavyo sasa
utanitambua Leo" Lisa alisema kwa hasira jicho
limemtoka kuashiria hana mzaha na anachokifanya,a
kashusha Kofi la nguvu kwa Sarah,Sarah akafumba
macho,lile Kofi likaishia hewani baada ya kudakwa
na Humph
Sarah alipooona lile Kofi halifiki akafumbua macho
kwa uoga ili ajue kulikoni,akatahamaki kumuona
Humph akiwa amemakamata Lisa mkono
akimtetea.
"Niachie!,niachie nimuoneshe huyu Malaya,nv
nakwambia nitamuua,hajui tulikotoka huyoo" Lisa
alizidi kupaza sauti kabla ya kutolewa na Sajna na
Like.
"Hey! Hajakuumiza popote huyu mpuuzi?" Humph
alimuuliza Sarah
Sarah akaanza kulia kilio cha kudeka na
kumkumbatia Humph, "ameniumiza mikono yangu,
ihii! Hiiiii!" Akaendelea kulia makusudi huku
akimng'ong'a Lisa aliyekuwa mbele yake
akimtazama,muda huo Humph akimbembeleza kwa
kumpiga piga mgongoni.
"Humph hivi huyu alikuwa msichana wako wa
zamani(x girlfriend) au?" Sarah aliuliza kwa upole
akiwa anamuangalia Humph usoni
"Sifahamu japo huwa anasema hivyo hivyo na
kuning'ang'ania,Mimi namchukulia kama rafiki tu"
Humph alijibu akionesha dhahiri hamfahamu vyema
Lisa.
"Ni kweli hufahamu au nd'o unajipumbaza ili use na
Mimi alafu niingie matatizoni" Sarah alizidi kumhoji
Humph kwa kauli tata.
"Nielewe sifahamu chochote kumhusu" Humph
alijibu wakati huu huku akiondoka kwa hasira
"Nikimwambia kuwa hata Mimi nimesikia kuwa
alikuwa mpenzi wake wa muda mrefu
nitamkosa,ngoja niendelee kuwa kimya tu mpaka
mwisho" alijiwazia Sarah
Lisa,Sajna na like walikuwa mbele Humph na Sarah
nyuma,ghafla ukazuka muungurumo mzito,alikuwa ni
Simba kutoka kichakani "Rrrrrrrrrrrrr" alizidi
kuunguruma
Like Sajna wakachomoa bastola zao walizopewa
kwaajili ya kujihami mmoja anaangalia huku
mwingine kule
Humph na Sarah wakaanza kutetemeka wakijaribu
kutaka kukimbia kutokana na uoga,Sajna anatoa
ishara wasimame. Miungurumo ilikuwa ikitokea
pande mbili tofauti,pale pale wakatoka Simba
wakubwa wawili mmoja upande wa Sajna na
mwingine upande Like.
Wale Simba walikuwa dume wote na walionekana
kuwa na njaa mno,ni kama waliambizana wakaruka
kwa pamoja kuwania vitoweo Sajna na Like
wakaanza kufyatua risasi ili kuwanusuru wenzao.
Risasi zile ziliwakosa wale Simba.
Sarah alivyoona vile na hakuwa tayari kufa akageuka
nyuma na kuanza kunyata akimbie bila Humph
kujua. Lisa aliganda kama mti mkavu jasho
likimmwagika kama maji huku sala za kuomba
waokoke zikitiririka moyoni kwa kasi sana ili Mungu
awaepushe na malaika wale wa kifo.
Wanaume Sajna na Like walikuwa wakiviziana na
Simba kila mtu akijitahidi kupambana kufa na
kupona ili waokoke mdomoni mwa Simba wale.
Simba mmoja akaotewa risasi ya kichwa na Like
yule mmoja akapandwa na hasira kwa kasi akatoka
mbio amjeruhi Lisa,alikuwa kama mbogo
aliyejeruhiwa kila alichokiona alihitaji kukiangamiza.
Aliruka tayari kumjeruhi Lisa,Lisa akafumba macho
kwa hofu lakini ghafla simba yule akarushwa na
kombora lisilojulikana wapi limetokea,Humph
akastukia kitu mfano wa kijiti kinachomoza mkononi
mwake na hatimaye akakivuta ikatoka fimbo ya
mzee Mandevu.
 
Sehemu ya sita
....Ilipoishia.......
Aliruka tayari kumjeruhi Lisa,Lisa akafumba macho
kwa hofu lakini ghafla simba yule akarushwa na
kombora lisilojulikana wapi limetokea,Humph
akastukia kitu mfano wa kijiti kinachomoza mkononi
mwake na hatimaye akakivuta ikatoka fimbo ya
mzee Mandevu.
......Endelea nayo.....
Lile kombora hali kutoka kwa Humph bali nyuma ya
Humph,Humph alipogeuka akiwa na haraka zake
mkononi akiwa ameshika ile fimbo radi Kali ikatoka
kwenye ile fimbo. Ikumbukwe Mzee Mandevu
alikuwa na nguvu za radi (thunder energy). Zile radi
hazikutoka kimpangilio kumuelekea yule mtu
aliyerusha kombora.
Radi ya kwanza aliikwepa akatupa naye kombora la
barafu,Humph naye radi zikazidi kutoka katika fimbo
ya mzee Mandevu,Sarah akakimbia bila mpangilio
na kujikuta katikati ya Humph na yule mtu wa
barafu asiyejulikana.
Radi na zile kombora za barafu zikamuishia
Sarah,mwili wake ukaanza kupanda juu
ukielea,"hapanaaa(noooo!!)" Humph alipiga kelele
na kuitupa ile fimbo,Sarah akaanguka chini Yale
makombora ya barafu yakapitiliza kwa Humph na
kumrusha mbali akajipigiza kwenye mti na kuzimia.
Sajna na Like wakazidi kufyatua risasi ambazo
ziligandishwa kabla hazijafika alafu mtu yule
akapotea katika mazingira tatanishi. Lisa hakuelekea
popote alikuwa kama mtu aliyepigwa shoti,Yale
matukio yalimtisha mno kiasi kwamba mfumo
mzima wa fahamu ulikuwa haufanyi kazi mpaka
alipoguswa na like ndipo akastuka na viungo vyote
vya mwili vikamregea kwa kukosa ushirikiano.
★★★The Return of Amazing Eyes★★★
★★Kurudi Kwa Macho Ya Ajabu★★
"Anaonekanaje huyo mtu?" Profesa alikuwa anahoji
(mzoefu wa.misitu ile na mtafiti mkuu)
"Ni wa bluu bahari hivi hiyo rangi yake alafu
anarusha vitu kama barafu,ni barafu ile maana
inagandisha mpaka risasi," Like alielezea
"Nafikiri hayo ni maajabu mapya katika misitu ya
the falling mountain,kuanzia sasa haruhusiwi
kwenda mtu yeyote mpaka uchunguzi ukamilike"
Profesa wa misitu ile alisema.
Humph,Lisa na Sarah walilazwa chumba kimoja cha
matibabu,Lisa alikuwa amekosa nguvu tu lakini
Sarah na Humph hawakuwa na fahamu hata
chembe.
Humph alianza kuweweseka akilitaja jina la
Lisa,Lisa alivyosikia anatajwa akapata nguvu ghafla
na kumfuata Humph kitandani,hapo ndipo utaijua
nguvu ya mapenzi yaani mpaka mtu anapona ghafla
ni hatari ujue.
Lisa alikaa pembeni ya Humph akamuinua kichwa
na kumlea mapajani mwake,Humph akazidi
kuweweseka akipiga kelele akiwa anamuita
Lisa,Machozi ya Lisa yalizidi kumdondoka
akimuonea huruma Humph.
Humph akaanza kulitaja jina la mzee Mandevu Mara
nyingi Lisa akabaki kumshangaa tu huku machoz
yakitiririka kama bomba linalotoa maji.
Humph akatulia kimya ukabaki mkoromo tu,Lisa
akazidi kulia huruma na maumivu yakiwa
yanausonga moyo wake,mlango ukafunguliwa Lisa
akamuweka Humph kitandani na kusimama wima
huku akijitahidi kufuta machozi yasionekane.
Sajna na Like wakiongozana na daktari wakaingia
wakiongea mambo yao,wakashangaa kumuona Lisa
amesimama pembeni ya Humph.
"Heee! Mgonjwa umepona Mara hii?" Like aliuliza
akitabasamu lakini Lisa hakujibu neno.
"Jamani si unaulizwa?" Alidakia Sajna
"Mie mzima kabisa mbona,kwani nilikuwa
mgonjwa?" Lisa naye aliuliza
"Mmh! Haukuwa mgonjwa ila ni uoga wako tu nd'o
uliokufanya hivyo" sajna alijibu
"Aliganda kama amepigwa shoti" Like alitania.
"Hahahahahahaha!" Wote walicheka pamoja na Lisa
Lisa akatoka nje na kujiinamia mawazo kibao
yakitawala ubongo wake kubwa zaidi likiwa kuhusu
kumbukumbu za Humph zisizojulikana lini
zitamrudia waweze kuishi maisha kama awali.
Mwili wa Lisa ulikuwa umepungua kwa kiasi
kikubwa lakini hilo halikumfanya achuje bali
alionekana mrembo marafudufu kiasi kwamba hata
Sarah hakuufikia urembo wake hata kwa theluthi
moja.
Kwa unyonge Lisa akarudi wodini ambako wenzk
wenzake walipumzishwa,akiwa ameketi pembeni ya
Humph. Sarah hakuwa amepata fahamu mpaka
muda ule,alionekana kuathiriwa sana na nguvu za
radi pamoja na barafu japo daktari hakugundua
hilo,kuna wakati alibadilika rangi na kuwa wa ubluu
bahari na wakati mwingine macho yake yalipitisha
miale Fulani mieupe.
Lisa aliushika mkono wa Humph ambaye bado
hakuwa akijielewa kitandani pale na kuanza kuongea
taratibu.
"Haijalishi ni mangapi yamepita,mangapi
umenifanyia na mangapi nimekuudhi au umeniudhi
kwa namna moja ama nyingine lakini bado penzi
letu litaishi milele,si kwamba najipa moyo
hapana,Nina imani upendo wako kwangu ni kama
umeanza jana kuchomoza,bado nakusubiri,bado
nakutumainia Humph na bado nafurahia uwepo
wako maishani mwangu,amka basi unifariji,amka
unikumbatie,amka unipoze mtima amka unifanye
mwenye furaha milele Humph tafadhali" Lisa
aliongea kwa hisia machozi yakimshuka
Lisa alivyoona hamna linalosaidia akainuka na
kuondoka,alipoufikia mlango na kutaka kuufungua
akaisikia sauti ya Humph "Lisa,Lisa,nakupenda Lisa"
Lisa akasita kufungua mlango akihisi ni miujiza au
mauzauza yanamtokea akaamua kugeuka
haraka,cha ajabu anamuona Humph akiwa bado
kitandani akiweweseka,Lisa akarudi haraka na
kumbusu Humph kwenye paji la uso.
Ni kama busu lile lilileta muunganiko kati yao pale
pale Humph akaanza kutetemeka kama mtu
anayepigwa shoti za umeme ama amekumbwa na
mtetemo(vibration) mwilini mwake.
Lisa akaanza kurudi nyuma kwa uoga hasa baada ya
kuona vitu vyeupe vinatembea mwilini mwa Humph
mithili ya shoti,mikono yake ilikuwa ikipiga radi
ndogondogo kama hasi na chanya zinapokutana na
kutoa cheche na mwisho wa yote Yale ni mwanga
ambao ulijikusanya machoni mwa Humph.
Lisa akajigonga kwenye kitanda cha Sarah kwa hofu
anashindwa kuhimili mwili wake akastukia
ameangukia juu ya mwili wa Sarah huku akiwa bado
anamshangaa Humph.
Chumba kizima kilitawala mwanga mkali uliotoka
machoni kwa Humph na ghafla akastuka kutoka
katika Usingizi mzito aliokuwa nao. "Aaaaaah"
Humph alipiga yowe zito kisha akamgeukia Lisa
kule aliko
"Lisaaaa!" Sauti ya mshangao inamtoka Humph
Lisa akabaki ameduwaa asiamini kile kinachotokea
kwa wakati ule,Humph akainuka taratibu kitandani
na kumsogelea Lisa alipomfikia na kumgusa
mwanga wote ukapotea machoni kisha
akamkumbatia Lisa kwa nguvu.
Lisa bado hakuwa katika hisia za kibinadamu,alio
nekana kushindwa kuhimili kile anachokiona na
mwisho akadumbukia ndani ya dimbwi zito la
mawazo asilolitarajia na hata alipokuja kurudi katika
fahamu zake alikurupuka akitaka kukimbia lakini
Humph akamng'ang'ania kwa kumkumbatia kwa
nguvu zaidi.
"Nimekumisi sana Lisa wangu" ni kauli ya kwanza
iliyomrudishia Lisa uhai wa moyo wake akajikuta
naye akikubali kumbatio lile mwanana na bila
kufikiri Mara tatu akamkumbatia Humph huku
akiangua kilio cha nguvu.
"Nyamaza Lisa wangu nipo hapa kipenzi
chako,usilie nipo kwaajili yako Lisa" Humph
alimbembeleza Lisa huku akimpiga piga taratibu
bila kufahamu ni kiasi gani amemuumiza msichana
yule kwa kipindi chote kile ambacho hakuwa katika
kumbukumbu zake halisi.
Japo Lisa alitambua wazi kuwa halikuwa kosa lake.
 
Sehemu ya saba
....Ilipoishia.......
"Nyamaza Lisa wangu nipo hapa kipenzi
chako,usilie nipo kwaajili yako Lisa" Humph
alimbembeleza Lisa huku akimpiga piga taratibu
bila kufahamu ni kiasi gani amemuumiza msichana
yule kwa kipindi chote kile ambacho hakuwa katika
kumbukumbu zake halisi.
Japo Lisa alitambua wazi kuwa halikuwa kosa lake.
.....Endelea nayo.......
★★★★Rise of Immortals★★★
★★Kuibuka kwa waishio Milele★★
"Leo nisiku ya kipekee kati ya siku zote ambazo
mmewahi kuziona mkiwa katika kisiwa hiki, wengi
wenu hamjui kwanini kinaitwa kisiwa cha mlima
unao dondoka (the falling mountain), ziara ya Leo
itawapa majibu yote hayo, nawatakia safari njema".
Kiongozi wa kisiwa cha
The falling mountain Ali hutubia.
"Eeeeeeeh! yeleeyeleee!!" Kelele zilirindima eneo hilo
kutoka kwa wanachuo.
"Sarah akiwa ndani ya chumba cha matibabu vidole
vyake vilionekana kuanza kucheza cheza,alionekana
kupatwa na fahamu,ghafla mwili wake ulianza kutoa
mvuke wa baridi,hakuwa akijitingisha sana.
Baada ya mvuke ule kutoka kwa muda mrefu
hatimaye miale ya rangi ya bluu ilianza kupita
mwilini mwake mithili ya shoti za umeme ghafla
akafumbua macho.
Macho yake yalikuwa tofauti mno,yalionekana kuwa
na kiini cha rangi ya bluu bahari kinachopitisha
miale ya rangi nyeupe kwenye kiini.
Wanachuo wanaianza safari wakiwa makundi
makundi wakipiga soga za hapa na pale,Lisa akiwa
na furaha kumpata tena Humph,Sajna na like
wakiwa pamoja nao,mwisho wa msafara
anaonekana Sarah akipenya katika makundi Yale
mpaka alipofikia kundi la nyuma ya kina Humph.
Ilivyoonekana alikuwa akimtafuta Humph sasa
macho yake yaliwaona lakini yalitua barabara kwa
Lisa akiwa amepitisha mkono wake kiunoni mwa
Humph. Alikuwa na chuki isiyoelezeka baina ya
watu wale wawili.
Mwendo wa Sarah haukuonekana wa kawaida hata
kidogo kwa aliyemzoea,kazi ya kupandamlima ule
uliobeba jina la kisiwa kile ikaanza. Milima ule
ulionekana kuinama sana na ulikuwa mrefu mno
ambao kwa makadirio ingechukua masaa mengi
kuoanda mpaka kileleni.
Kiongozi aliwapa utaratibu wa kufunga kamba ili
kuzuia ajali zinazoweza kujitokeza lakini ilikuwa ni
kwa makundi makundi,Eneo lile lilikuwa salama
hivyo eneo la kukutana lilikuwa juu ya mlima.
Humph na Lisa waikuwa wa kwanza kufika kileleni
wakiwa na Sajna na Like.
★★★★★
Kundi kubwa la nyuki lilikuwa likipita katikati ya
misitu ya the falling mountain,haikuchukua muda
kundi hilo la nyuki liliwafikia wanachuo waliokuwa
wakipanda mlima ule na kuwafanya watawanyike
ovyo ovyo huku wwngine wakinusurika na ajali ya
kuanguka kutoka mlimani,wengi wao walihofia
kudhurika na nyuki wale.
Lisa,Humph, Sajna na Like walikuwa tayari wamefika
kileleni like na Sajna wakapita njia yao,Humph na
Lisa wakaenda sehemu yao bila kujua Sarah a
anachunguza mienendo yao.
Humph akahisi kuna kitu hakipo sasa,ghafla maono
yakamuijia pale pale akiwa amesimama (ndoto za
mchana) akamuona msichana mmoja akiwa
anamshambulia,alionekana si wa kawaida msichana
yule .
Humph akastuka na kumwambia Lisa atangulie
mbele,kwa kuwa giza lilikuwa limeanza kutawala
Humph akawaka macho yake eneo lote likatawala
mwanga.
"Jitokeze mahali ulipo maana sina uadui na wewe"
Humph alisema kwa sauti na kumfanya Sarah
ajitokeze.Humph alishangaa kumuona
Sarah,kumbukumbu zikapita haraka haraka kichwani
mwake akatambua kile kinachoendelea baina yake
na binti yule. Alikuwa na mahusiano naye
kimakosa!!
Mwili wa Sarah ulikuwa ukitoa mwanga na mvuke
wa bluu bahari,radi ndogo ndogo zilikuwa zikitawala
mikono yake,Humph alishangazwa sana na jambo
lile
"Unanipenda ama haunipendi? Nataka jibu moja tu"
Sarah aliuliza mdomoni akiwa akitoka mvuke Fulani
wa ajabu.
"Sikuelewi Sarah una maana gani kusema hivyo?"
Humph aliuliza akiwa anatafuta mbinu ya kumtuliza
Sarah.
"Sihitaji maneno mengi jibu unanipenda au
hunipendi" Sarah aliuliza tena
"Humph mpe jibu" Lisa aliingilia
"Nakupenda kama rafiki ila si kimahusiano ya
mapenzi" Humph alijibu kwa ujasiri
"Asante,wewe na Malaya wako mtawajibika kwa
hilo" kisha akasema kwa sauti ndogo "wrong
choice" kisha akaachia kombora la radi
zilizoambatana na barafu inayoyeyuka yaani ile
nyepesi mchaganyiko na maji.
Humph akastukia fimbo ya mzee mandevu
inajitokeza mkononi ghafla na kuzuia kombora lile
kwa nguvu zote lakini Sarah alimzidi Humph uwezo
maana Humph alikuwa akiserereka.
"Lisa kaa mbali na hili eneo" Humph alipaza sauti
kwa tabu huku akiwa anazuia kombora za Sarah.
Lisa akaanza kukimbia,lilikuwa kosa kubwa!. Sarah
akahairisha kumuadhibu Humph akaanza kurusha
makombora kumfuata Lisa,Humph kwa kutumia
macho yake akapata kazi ya kuyayumbisha
makombora Yale na kuchoma vichaka.
Sarah akakasirika baada ya kuona kuwa bado
Humph anatetea uhai wa Lisa,Sarah akajitutumua
kwa nguvu lakini muda ule ule nyuki nyingi
zikamfikia na kuanza kumzunguka.
"Iiiiiiiiiahaaaaaa!!" Sarah alisikika akipiga kelele na
kutoa radi nyingi zilizotawanya zile nyuki na kufanya
atokeee mtu wa kawaida aliyetupwa vibaya na radi
zile. Maajabu!!!
Sarah hakuzubaa Akamfuatanishia mvua ya
makombora akiwa na nia ya kummaliza kabisa
lakini kwa baati mbaya kombora zake zikagonga
kizuizi,nwanaume aliyeshiba alikuwa ametengeneza
ngao na kuzuia makombora yae kutoka kwa Sarah.
Sarah akafanya mashambulizi ya kustukiza kwa
Humph ambaye mpaka muda huo alikuwa na
bumbuwazi juu ya watu wale waliojitokeza,alirushwa
kuelekea chini ya mlima ule mrefu,mwanaume yule
aliyetengeneza ngao akajitosa kumfuata Humph.
Sarah akatabasamu na kujiona mshindi kwa kuwa
alimuona Lisa hana msaada kwa muda huo,akiwa
anatembea kwa maringo na kujiandaa
kumshambulia Lisa lakini ghafla akapigwa na
kombora la barafu lililokomaa haswaa
nakumyumbisha,alikuwa ni msichana wa barafu.
Sarah akajiweka sawa na kuanza kushambulia
upya,msichana yule wa barafu alikuwa akitumia
ujuzi wa ajabu na kumshinda Sarah aliyekuwa
akitumia nguvu nyingi kuliko ujuzi.
Ndipo Makombora yao yalipokutana katikati,msicha
na wa barafu akaonekana anazidiwa uwezo,Mzee wa
nyukinyuki akajigeuza haraka nakumfuata Sarah
lakini hakufika popote baada ya Sarah kumchapa
kombora la nguvu lililomrudisha kwa
kishindo,alipomgeukia msichana wa barafu
akamrusha mbali.
Wakati ule ule duara kubwa likaonekana kutokea
chini ya mlima alikodondokea Humph nakutua
karibu na Sarah,Sarah akagadhibika na kumtupia
Humph kombora,likazuiwa na mwanaume mwenye
kutengeneza ngao.
"Sarah mi' sio adui yako tafadhali tulia
tuyazungumze" Humph alisema huku akipiga hatua
kumfuata Sarah
"Sina la kuzungumza na nyie,nitawapata tu" Sarah
alijibu na kupotea kama radi inavyopiga na kupotea
pale pale. Ilistaajabisha!!!!
Mpaka muda huo Lisa alikuwa amejificha nyuma
yamti,alishuhudia matukio yote Yale,hayakuwa ya
kawaida hata kidogo japo aliwahi kushuhudia vita
kati ya Lamson na Humph ambayo haikufua dafu
kwenye vita ile mpya.
Ilikuwa nusura alowanishe kichaka kile ila kibofu
kikamsitiri kwa muda,Mdada wa barafu na mzee wa
Nyuki waliinuka na kuungana na mwenzao wa ngao
(shield) kwa pamoja wakainama kumpa Humph
heshima yake.
 
Sehemu ya nane
....Ilipoishia.......
Ilikuwa nusura alowanishe kichaka kile ila kibofu
kikamsitiri kwa muda,Mdada wa barafu na mzee wa
Nyuki waliinuka na kuungana na mwenzao wa ngao
(shield) kwa pamoja wakainama kumpa Humph
heshima yake.
.....Endelea nayo......
Humph hakuelewa kwanini wanafanya vile ikabidi
aulize
"Nyie akina nani na kwanini mmenisaidia?"
Mmoja wao akatoa kidani chenye Alama iliyochorwa
kwenye fimbo ya mzee Mandevu na
kumrushia,Humph alipodaka kile kidani ile alama
ikatoa miale ya radi na kurudi kawaida,Humph
alibaki kutoa macho tu.
Wakati huo Lisa alimfuata Humph na kusimama
nyuma yake,
"Sisi tumetoka ulimwengu wa immortals (waishio
milele) bila shaka unakufahamu vyema" Humph
akatikisa kichwa akiwa na hofu
"Kuna vita kubwa aliyoileta Sor iliyopelekea hata
Mzee Mandevu kufariki,sisi pekee ndiyo tuliosalia
na waliobakia wote wameungana na Sor,hivyo ni
jukumu letu kuungana nawe ili kuilinda amani ya
dunia"
"Inawezekanaje ikiwa ile njia ilifungwa?" Humph
alihoji
"Ni kweli ile portal ilishafungwa lakini kuna njia
nyingine ya siri iliyotumiwa na wazee wa zamani
kama Mzee Mandevu na Mfalme Sangu, pia ni
makabila matatu pekee ndiyo yaliyokuwa
yakiifahamu njia hiyo na ndiyo maana tupo hapa"
alijibu mwanaume wa ngao.
"Niite Shani " alijitambulisha msichana wa barafu
kwa utiifu
"Ben hapa" mzee wa nyuki nyuki akajitambulisha pia
"Ukiwa kama kiongozi wa kuhakikisha kuwa Sor
anateketea,nitafuata njia yako,nakwenda kwa jina la
Shed" alisema mwanaume wa ngao kwa ukakamavu
"Nitawaaminije?" Humph aliuliza
" Utatuamini pale ambapo Sor atatua na jeshi lake
lote kuiangamiza dunia na wewe pia" Alijibu Shed
mwanaume wa ngao kwa hasira baada ya kuona
hawaaminiwi.
"Tukutane nyumbani kwenu" Ben mwanaume wa
nyuki alimalizia kauli ile na wote wakapotea eneo
lile
"Ooooof" Lisa alishusha pumzi
"Nafikiri unaelewa jukumu linalo nikabili kwa sasa
na ni ngumu kuliko yote yaliyowahi kutokea,nahitaji
kukulinda na kuilinda amani ya dunia hivyo utabidi
ukae mbali Lisa" Humph alimuomba Lisa
"Nimesubiri sana urudiwe na kumbukumbu ili
niyafaidi mapenzi yako niliyoyakosa kwa kipindi
kirefu,siwezi kuvumilia hili kwa kweli, sikuachi
popote uendapo" Lisa alijibu akimkumbatia Humph
"Una hatari sana mrembo wangu,huofii maisha yako
sijui kwanini lakini?"
"Unafahamu ni kwanini,usijitie kiziwi ama kipofu juu
yangu" Lisa alisema kwa sauti ya chini yenye
ushawishi wa kuhitaji kitu Fulani
Humph hakutegea akamuinamia na kumshika
mahali kiunoni,Lisa akatoa mguno mdogo wa
mahaba kisha midomo yao ikakutana na kuanza
kufaidi kinywaji adimu kuwahi kutokea duniani tena
chenye midadi kibao na amsha amsha ya mashetani
ya mwili wa binadamu yaani "ashki"
"Koh! Koh! Koh! Koh! Mmm! Mmm! Mmm!" Sauti
za watu zilisikika zikiguna na nyingine kujikohoza
jirani na akina Humph wao wakiwa wamezama
ndani ya dimbwi la mapenzi.
Ndipo Humph na Lisa walipostuka na kugeuka
maana tayari mikono yao isiyo na adabu ilikuwa
imeanza kazi yake. Wanachuo wengi walikuwa
wamefika pale,like na Sajna walikuwa pamoja nao.
"Hivi hamjaona vitu vikipita pita huku juu kama radi
radi vile?,maana mwanga ulikuwa kila sehemu"
aliuliza mmoja wa wanachuo
"Kaka,naona umekosa wa kuwauliza yaani
umewakuta watu na starehe zao sasa ni SAA ngapi
wameona hivyo vitu au hujui starehe hiyo
inavyobamba" mwanachuo mwingine alijibu kwa
niaba ya Humph na Lisa.
"Hhahahahahahaha!" Wanachuo wakaishia kucheka
na kumfanya mwenzao ajisikie vibaya akaondoka
akiwa amekasirika.
Taarifa kutoka kwa mkuu wa msafara ikafika kuwa
eneo lile si salama tena hivyo wote wanaombwa
wakutane ilipowekwa kambi kuu. Humph
akiambatana na Lisa waliongozana kuelekea
kambini.
★★★★★★★★★★★★
"Niache nakwambia nitakuua,niache , usinishike
hebu niache , soooor!" Humph Ali kurupuka
"Humph vipi Mbona kelele hivyo kuna nini
ulichoota?" Lisa alimuuliza Humph akiwa anajaribu
kumtuliza
"Ni ndoto tu,ndoto mbaya" Humph alijibu na
kuelekea dirishani akafungua pazia,mwanga
ukapenya ndani kuonesha kuwa asubuhi imefika.
Lisa akafika nakumkumbatia kwa nyuma akiwa pale
pale dirishani.
"Acha uchokozi basi,si unaelewa kuwa Leo nd'o
Siku ya safari kurudi Reycity,haihitajiki tuwe
wachovu sana" Humph aliongea akiwa anaipapasa
mikono ya Lisa iliyozunguka kiunoni mwake.
"Mh! Aya nitafanyaje ikiwa nd'o tayari ushasema"
Lisa alijibu na Humph akamgeuza haraka na
kumkumbatia kwa nguvu.
"Nakupenda Lisa,kumbuka hilo daima" Humph
aliongea akiwa kwenye hisia Kali kisha akamchumu
Lisa katika paji lake la uso.
★★★GREETINGS★★★
★★★SALAMU★★★
Safari ikiwa imekolea kuelekea bandarini,wakati huo
wanachuo walikuwa ndani ya basi kabla ya kufika
bandarini na kupanda usafiri waliokuja nao hapo
awali.
Wanachuo walikuwa wakifanya maongezi na
wengine wakiwa wanafanya vitu wanavyovipenda.
Humph na Lisa walikuwa wakifaidi maongezi ya
nyakati za mwisho kabla hawajatengana kiusalama
zaidi.
Ghafla Humph akashuhudia zile ndoto za mchana
zikimtokea tena(maono),moto ulikuwa ukishuka
toka juu mfano wa vimondo ulipotua uligeuka na
kuwa sokwe wakubwa wa ajabu wenye manyoya
meusi tii.
Walikuwa wakiwaka moto vichwani mwao,mmoja
wao akaunguruma akitamba kwa kujipiga piga
kifuani,moto mzito ukamtoka kinywani na kumfanya
Humph apige kelele zilizowagutusha wanachuo
wote ndani ya basi.
Breki Kali ikafungwa katikati ya barabara watu wote
wakamtazama Humph
"Kuna nini?" "Nani huyo jamani?" "Kuna mgonjwa wa
akili humu?" "Shida nini wanachuo?" Yote yalikuwa
maswali ya kila mtu aliyejisikia kuuliza
"Ni ndoto,alikuwa amelala. Msameheeni bure"
aliongea Lisa kwa upole .
"Dereva Fanya yako,huyu boya alikuwa amelala"
mwananchuo mmoja akaropoka na kuwafanya
wengine waangue vicheko
Kabla hata dereva hajafika mbali tangu Humph
akurupuke kutoka katika maono na kutoa kioja anga
likabadilika rangi na kuwa leusi hatari,hali ya hewa
ikawa nzito ghafla na ya kutisha.
Ilionekana ni kama mvua kubwa ilitarajiwa kunyesha
muda mfupi ujao.
"Wanakuja kuanza vita" Humph aliongea akiwa
hajiamini kabisa,uoga ulionekana wazi hata katika
mboni zake za macho
"Akina nani?" Lisa aliuliza,ndipo Humph akaonyesha
kwa kidole jinsi ambavyo anga linatisha kupitia
dirishani.
Miungurumo mikubwa ikalipasua anga lile na
kuwafungua masikio wanachuo, Lisa alistuka vibaya
mno
"Mbona siwaoni Humph, wako wapi?" Lisa aliuliza
akiwa tayari hofu imemvaa kuliko hata Humph.....
 
Sehemu ya tisa
....Ilipoishia.......
"Mbona siwaoni Humph, wako wapi?" Lisa aliuliza
akiwa tayari hofu imemvaa kuliko hata Humph.....
.....Endelea nayo........
"Wanakuja,tulia usitoke upande wangu vinginevyo
nitashindwa namna ya kukulinda" Humph alijibu
kuchomoa fimbo ya mzee Mandevu ambayo Mara
nyingi imekuwa ikijificha mikononi mwake lakini
kwa wakati huu haikujitokeza.
"Unataka kufanya Nini Humph?" Lisa alihoji
"Kupambana nao" Humph alijibu
Wakati huo huo anga likaongezeka miungurumo
flani giza nalo likazidi kutawala na ghafla vimondo
vingi vikaanza kushuka kwa kasi kulielekea basi.
Dereva aliliona lile pia wanachuo nao hawakuwa
nyuma kwa kupiga kelele za uoga,dereva hakuwa
mtu wa pole pole alikwepesha gari kila Mara na
kwa ujuzi wa ajabu ambao hakuna aliyetegemea
kuwa anaweza kuwa nao.
Kimondo kimoja wapo kikapiga tairi la basi lile na
kusababisha liyumbe huku na kule
"Bismilah rahman rahim" "Yesu tusaidie" walisikika
baadhi ya wanachuo wakikemea hali ile ya hatari
kwa imani tofauti tofauti.
Basi lilisimama Humph alikuwa tayari na kitambaa
chake usoni,Lisa alipoangalia pembeni yake
akaambulia patupu na kuishia kuita ,"Humph "
"Kila mtu nje,kwa usalama wa maisha yenu" ilisikika
sauti nzito ikiwa imejifunga kitambaa usoni.
Lisa akapumua kwa nguvu na kuinuka kutoka
kwenye siti amfuate Humph ambaye ndiye
aliwaomba wanachuo watoke nje.
"Msimuamini huyo mtakufa" Mwanachuo mmoja
akaropoka na kuwafanya watu wasite kwenda
mlangoni
"Kweli,kweli,kweli" zilisikika sauti za wanachuo
zikiongea chinichini.
Humph akazubaa kidogo akitafuta uamuzi wa
kufanya,ghafla akavutwa kwa nyuma na kurushwa
kwa nguvu na kuanguka. Kumbuka wakati vimondo
vile vilikuwa vikianguka vilikuwa vikigeuka kuwa
sokwe.
Fimbo ya mzee Mandevu ikajitokeza ikiwa ndefu
mkononi,sokwe wawili walikuwa wakilitikisa basi
kwa nguvu,wanachuo wakipiga kelele za kuomba
msaada.
"Radiii!!!" Ilisikika sauti nzito ya sokwe likiwa mbele
ya Humph tayari kwa kukabiliana naye.
"Aaaaah!" Moto mkali ukatoka mdomoni mwa
sokwe lile,Humph akajirusha kando na kuinuka
haraka. Macho yake yakang'aa zaidi na
kuwasimamisha sokwe waliokuwa wakilitikisa gari
lakini ghafla akiwa anafanya vile kimondo kingine
kikawa kinashuka usawa aliosimama hivyo
akajipinda na kukikwepa.
Pale pale sokwe wale wakamzunguka, fimbo ya
mzee Mandevu ikawazadia mvua ya radi sokwe
wale,alipoona kuwa wamepungua akauendea
mlango wa basi ambao sehemu zake nyingine
zilikuwa zimeshika moto.
Wanachuo wengi walitokea madirishani na wale
waoga walibaki ndani akiwemo Lisa. Humph alianza
kuwashusha lakini ghafla yowe za wanachuo
zikaanza kurindima ili Humph ageuke nyuma.
Alichelewa,sokwe wanne wakamrusha kwa sokwe
wengine wawili waliomchangamkia kama supu ya
mlevi.
Humph alipigiga mno mpaka mwanga wa macho
yake ukawa hafifu kupindukia,akaendelea kupigwa
huku na kule,wanachuo waliendelea kushuhudia lile
sokomoko,Lisa aliishia kububujikwa na machozi na
kwa bahati mbaya zaidi mlango wa basi ulikuwa
ukilindwa hivyo wa ndani walibaki ndani na wa nje
walibaki nje wakishuhudia kipigo kinavyotembezwa
kwa Humph.
Hakuna mwanachuo aliyeweza kutoka eneo
lile,Moshi mzito ukazidi kulisonga lile basi kwa
ndani,hatimaye wanachuo wakaanza
kukohoa,Humph akajaribu kukikusanya ili awaisaidie
lakini haikuwezekana.
Mlango wa basi ukafungwa ili wanachuo waliobaki
wafie mle ndani,ndipo sokwe moja likaamua
kummaliza Humph kwa kumchoma moto.
Lilipoachama domo lake moto mkali ukatoka
kinywani mwake,Humph akafumba macho.
Yowe kali zikasikika pembeni yake, yalikuwa ni Yale
masokwe yakitoa mayowe ya uchungu,akafumbua
macho haraka kutazama kilichotokea,alishuhudia
sehemu ile ikiwa nyeupe kwa sekunde
kadhaa,mbele ya Humph alisimama Ben l,Shed na
Shani.
Wanachuo walitolewa wote na kujikusanya sehemu
moja wakipeana huduma ya kwanza na wengine
wasiojielewa wakiwa wanashangilia na kupiga
picha.
Shani alipogeuka na kukutana na flash nyingi
akaanza kuonesha mbwembwe akitoa barafu
mikononi mwake na wakati mwingine akitengeneza
vitu vya ajabu ajabu.
"Uwezo wako umepungua mno,tukutane jijini
Reycity" Ben aliongea na kutangulia kuondoka akiwa
katika umbo la nyuki wengi na kuwaacha wanachuo
wakishangilia na wengine kuonekana kushangazwa
na maajabu Yale.
Shani aling'ang'ania kuendelea kupigwa picha
mpaka pale Shed alipoamua kutumia nguvu
kuondoka naye akiwa amemuweka ndani ya ngao
yake(shield).
Humph naye akatoweka na kutokea nyuma ya basi
kisha akarudi kama sio yeye aliyekuwa mbele ya
wanachuo muda ule,alifika mpaka pembeni ya Lisa
akiwa amejishika kiuno na kifua.
"Pole mpenzi" Lisa alimwambia Humph kwa sauti ya
chini.
"Sijapoa,hawa jamaa ni wauwaji kabisa hawana hata
chembe ya Huruma"
Baada ya muda mrefu kupita basi lingine lilikujja
likiongozana na zima moto pamoja na watu wa
huduma ya kwanza,safari ikaendelea kuelekea
bandarini. Njiani kila mtu alieleza kile alichohisi ni
sahihi kulingana na macho yake yalivyokuwa
yakiona.
Mpaka basi linafika bandarini wanachuo hawakuwa
na habari zaidi ya kuzungumzia yaliyotokea,Humph
alisaidiwa na Lisa kushuka kutoka ndani ya basi
sanjari na wanachuo wengine waliokuwa
wamedhurika na hali ile ya Moshi uliotokana na vita
ile.ya muda mfupi.
Taarifa zilisambaa kama kifuu cha nazi kiichoshika
moto,zikielezea binadamu wenye vipaji
waliopambana na sokwe wa ajabu(aliens)
wanaozalisha.moto vinywani mwao.
Wanachuo mbalimbali walielezea namna ilivyotokea
na kile walichokiona kipo sahihi kulingana na
macho yao yalivyoona. Wengine walifika mbali zaidi
na kusema kuwa huenda ni adhabu kutokana na
dhambi walizoendekeza binadamu huku wakilikuza
zaidi suala lile kwa kusema kuwa huenda ule ni
mwanzo na ipo siku watakuja kuuteketeza
ulimwengu mzima.
★★★The Power Of The Spell★★★
★★★Nguvu Ya Kunuia★★★
Humph anastuka usiku anashangaa kuona watu
wakiwa wamemzunguka katika mtindo wa pembe
tatu
"Ni muda wa kukuandaa" Ben aliongea na wote
watatu wakatokomea kwenye Giza Nene
Humph akatoka nje na fulana akasogea mpaka eneo
la bustani na kuwakuta wenzake wametengeneza
duara katikati ikiwemo Alana ya nyota.
Humph akaambiwa aingie katikati ili waanze
kumuandaa kama walivyokusudia.
 
Sehemu ya kumi
....Ilipoishia.......
Humph akaambiwa aingie katikati ili waanze
kumuandaa kama walivyokusudia.
....Endelea nayo.......
Humph alipoingia tu Shed,Shani na Ben
wakanyoosha mikono na kuanza kuzitoa nguvu zao
kumuelekea Humph pale katikati,nguvu zile
zikakutana eneo moja.
Humph akaanza kupiga kelele na kupiga
magoti,macho yakaanza kutoa mwanga
mweupe,kelele za Humph zilipozidi mawingu mazito
yakaanza kujikusanya eneo lile,ngurumo kali zikazidi
kuunguruma kila pande ya mji wa Reycity.
Ile fimbo ya mzee Mandevu ikajitokeza na kuelekea
juu usawa wa kichwa cha Humph,radi zikazidi
kurindima. Radi moja Kali ikaipiga ile fimbo na
kusababisha mabadiliko ya hali ya hewa zaidi
Ile radi ilibadilisha fimbo ile na kuwa ya bluu huku
ikipiga shoti za ajabu pia radi ile iliungana moja
kwa moja na mawingu ukatokea mstari mmoja wa
bluu (radi) kisha moja kwa moja radi ile ilinyoosha
mpaka kichwani kwa Humph.
Taratibu Humph akaanza kunyanyuliwa juu,macho
yake yakabadilika mwanga na kuwa ya bluu
bahari,radi zikazidi na upepo ukawa mkali sana
usiopimika,Shed na wenzake hawa kujali
waliendelea kutoa nguvu zao ili kumtengeneza
Humph katika ubora
Baada ya muda mrefu hali ya hewa ilianza kutulia,ile
radi iliyounganisha fimbo ya mzee Mandevu na
mawingu ikatoweka kisha Ben,shed na Shani
wakaaanguka chini wakiwa wamelegea,Humph nae
akashuka kwa kishindo akaangukia goti moja huku
macho yakiwa bado ni ya bluu.
Alikuwa akijihisi ni mwenye nguvu za ajabu ambazo
uzito wake hakuwahi kuuhisi hapo kabla, akainua
mikono yake na kujitazama radi za bluu zikazidi
kupiga mikononi mithili ya shoti za umeme,aliogopa
ile hali na kurusha mikono kama anayetupa kitu hilo
likawa kosa kubwa kwani radi nzito ilimtoka na
kuunguza maua ya bustanini kwao.
Humph kwa wasiwasi akanyoosha mikono chini
loooh! Shani aliona kile kitendo akajilazimisha
kuinuka "tulia usifanye chochote" ilikuwa kauli ya
Shani lakini alikuwa amechelewa kutoa onyo
Mikono ya Humph ilikuwa imeshaanza kumimina
radi chini na kumpandisha juu kwa nguvu huku radi
zikizidi kutoka u gesi zilizomfanya azidi kuelea juu
juu.
"Aaaaaaaaa!" Humph alianza kupiga kelele
akizunguka juu Kama tiara na kusababisha Ben na
Shed waangue vicheko,shani alikuwa na wasiwasi
mno kuwa lolote baya linaweza kumtokea Humph,
akatengeneza kombora la barafu haraka haraka na
kumtupia Humph kwa bahati mbaya halikulenga
shabaha.
Humph alivyokoswa na kombora lile akazidi
kupagawa,hali ile ikamfanya akose muelekeo na
kurudi chini kwa kasi na kuvamia miti.
★★★Rise of Bats★★★
★★★Kuibuka kwa Popo★★★
Asubuhi moja tulivu iliyo na mawingu na kibaridi
cha wastani ilimkuta Humph akiwa bustanini kwao
akiweka mazingira vyema,mama yake alipotoka nje
alishangazwa na uharibifu ule japo haukuwa
mkubwa kiasi cha kuharibu bustani yote.
Kwakuwa Humph alikuwa akitambua kinachoendelea
alimueleza mama yake kuhusu radi kali zilizokuwa
zikirindina usiku wa kuamkia siku hiti naye
akamuelewa bila kipingamizi chochote.
Baadae Humph alionekana akiwa maabara na
baadhi ya wanachuo,walikuwa wakifanya utafiti wa
kisayansi kwa kutumia mimea waliyotoka nayo
katika kisiwa cha "Mlima unaoanguka",wakiwa
wanaendelea na utafiti kwa mbali giza nene
likaonekana likifunika anga likiwa limetengenezwa
kwa mawingu mazito yaliyokuwa yakijongea kutoka
mashariki .
Lile wingu hali kufika mbali sana anga likasikika
likitoa mpasuko mkubwa uliofanana na dalili za
kunyesha kwa mvua kubwa yenye dhoruba lakini
haikuwa hivyo mpasuko ule ulisababisha popo
wengi washuke kutoka angani,Humph akastuka na
kuangusha bika aliyokuwa nayo mkononi . ni wazi
kuwa aliliona suala lile!!
Wanachuo wote wakamgeukia na Kumshangaa,ili
kuua soo Humph akatoka maabara na kuingia
chumba cha kubadilishia nguo akatoa apron (koti la
maabara na kupotea).
Lisa anafik sehemu ya kubadilishia nguo
anashangaa kuona ukimya umetawala ,alipo tazama
kabati la Humph kulikuwa na karatasi ndogo yenye
ujumbe" jihifadhi chumba salama " Lisa aka choka
maana alikuwa akizielewa hatari zinazo wakabili kwa
muda huo.
Akasogea dirishani kutazama mazingira ,
akashuhudia giza moja nene mithili ya wingu
likiteremka,alpotazama vyema alishuhudia ldadi
kubwa ya popo ikiteremka wakiwa wameshonana.
Kwa mbali Lisa akaona miale ya mwanga ikigonga
yale makundi ya popo na kuyateketezea mbali, Lisa
akasogea zaidi kwenye dirisha la vioo akiwa
haamini kinachotokea,akahisi kivuli kinakuja upande
wa pili alipotazama upande unaotokea kile kivuli cha
wingu zito aliona popo wengi wakiwa wanakuja
upande wa jengo lile alilosimama.
"Ooooh! No!" Sauti ya Lisa zilisikika punde baada ya
kuliona kundi lile la popo likiwa limesogea kabisa
mahali pale,akageuka nyuma haraka na kukimbilia
kitufe cha dharura na kubofya.
Hakufika mbali vioo vikasikika kupasuka,Lisa
akawahi kujitupa chini kwa nguvu,kundi kubwa la
popo likapita mgongoni kwake,ukimya
ukatawala,Lisa alipoinua kichwa kutazama
akakumbana na mduara ulioundwa kwa popo wale
wakiwa wanazunguka.
Lisa akapiga ukunga wa uoga kwa nguvu zote,kile
kitendo cha kufungua kinywa tu wale popo wote
wakaingia kinywani mithili ya Moshi mweusi mzito
uliomfanya Lisa akakamae kama mwanajeshi
anayekaguliwa kwenye gwaride,kinywa kikiwa wazi.
★★★★★★★★★★★
Humph alikuwa jengo la pili na Ben na Shed pamoja
na Shani wakiwa wanajaribu kuwazuia popo
wale,kwa kuwa walikuwa wengi nguvu yao ilitosha
kuwadhibiti popo wale
Wakiwa katika mpambano ule Humph alionekana
kuzimudu nguvu zake mpya kwa kiasi Fulani,Ghafla
anga likapasuka na kundi kubwa la popo likatoka
lilikielekea ghorofa lile la chuo cha sayansi .
"Lisaaa" sauti iligonga kichwani mwa Humph na
wakati huo huo maono yakapita machoni kwa
Humph,Lisa akiwa ameingiliwa na ule Moshi
uliotokana na popo wale
Humph alizubaa akiwa analitazama jengo lile,
Macho yake yalipenya mithili ya mawani ya shetani
mpaka ndani ya jengo lile, kwa mbali akasikia
kelele alipotazama vyema kelele zinapotokea
aliwaona popo wengi wanapita juu ya mwili wa mtu.
Akatambua yakuwa ni Lisa kabla hajachukua
maamuzi akasikia sauti nyingine ikiwa jirani naye
"Humph watch out!" (Humph angalia) alipogeuka
kundi kubwa la popo likamgonga na kumuangushia
nyuma ya jengo alilokuwepo,Shani akataka kwenda
Ben akamzuia "usihofu yupo salama"
Aliposema vile nyuma yao wakaisikia sauti ya
Humph.
"Wuhuuuuuuuu! It's amazing(inastaaajabisha)" Shani
akatoa tabasamu zito baada ya kumuona Humph.
Humph alikuwa akielea kwa kutumia ule uwezo wa
radi na nguvu ya macho yake ya ajabu,kwa mwendo
wa hatari akaelekea pale ambapo popo walielekea
katika jengo la chuo,alipofika tu dirishani
akarudishwa kwa kishindo na popo wengi.
"Ooh! Ooh! Ayaa! Au! Au!" Zilikuwa ni kelele za
maumivu wakati Humph akidondoka kuelekea chini
ya ghorofa kwa kishindo na popo wale huku akitoa
kila aina ya mlio wa maumivu wakati anajigonga
gonga huku na kule mpaka juu ya roof ya ghorofa
nyingine.
Lisa naye alifuatana na popo wale akiwa na macho
mekundu pamoja na mbawa kubwa zilizochomoka
ubavuni.
"Lisaaaaaa!" Humph akamuita Lisa kwa nguvu akiwa
haamini kile kilichomtokea Lisa,Kutokana na kuitwa
kule Lisa alimuona Humph na hilo likawa kosa
lingine,Lisa akatoa popo wengi kinywani wakimfuata
Humph,Humph akawachangua kwa radi.
Humph alipowachangua popo wale Lisa
hakuonekana mbele yake,akiwa anajiuliza ni wapi
alipoenda akapitiwa kwa nyuma,kucha Kali
zikamkwarua mgongoni,(ouch!) Ukelele wa
maumivu ukazidi kumtoka. Mtendaji wa tukio lile
alikuwa ni Lisa aliyepita kwa kasi kubwa.
Lisa akiwa ameathiriwa na popo wale akatazama
juu na kutoa mlio mkali ambao popo huwa
wanautumia usiku wakiwa wanapishana
Anga likapasuka tena na kutoka popo wakubwa
zaidi ya wale wa mwanzo,safari hii walikuwa na
miili ya watu isipokuwa meno yaliyokuwa kama ya
papa wa baharini.
 
Sehemu ya kumi na moja
....Ilipoishia.......
Anga likapasuka tena na kutoka popo wakubwa
zaidi ya wale wa mwanzo,safari hii walikuwa na
miili ya watu isipokuwa meno yaliyokuwa kama ya
papa wa baharini.
......Shuka nayo.......
Vita ilizidi kuwa ngumu,Humph na wenzake
walizidiwa haswaa,popo wale walikuwa wakubwa
wakubwa kupita maelezo na uwingi wao ulitisha
mno.
Humph alikuwa katika wakati mgumu zaidi ikiwa ni
piga nikupige,wakati yote yanaendelea watu wa jiji
la Reycity waliipata vita ile kupitia vyombo vya
habari moja kwa moja kutokana na teknolojia
mficho iliyokuwa ikitumika kuchukua matukio yale .
Ben aliutumia mwanya huo kujigeuza nyuki lakini
aligeuzwa chakula kwa popo wale na aliporudia
umbo la kawaida hakutamanika kwa namna
alivyoshambuliwa,baada ya vita kuwa Nene Shed
akatengeneza ngao kuwakinga wenzake japo Mara
kwa Mara popo wale waligonga kizuizi kile ili
kukiregeza.
Wote walikata tamaa ya kupambana na wale popo
watu wasioeleweka sayari waliyotoka,wakiwa katika
hali ile ya kukata tamaa kwa mbali milio ya
helikopta ikaanza kusikika ikisogea maeneo
yale,zilikuwa ni helikopta za kijeshi,wananchi
walirudisha matumaini na kuanza kushangilia pia
Humph na wenzake waliona ushindi ukiwa waziwazi
baada ya kuupata msaada ule wa dharura.
Mabomu mazito yalianza kutupwa yakishambulia
popo wale na kuwateketeza kwa kasi mno,cha ajabu
na cha kuwashangaza wanajeshi wale idadi ya popo
ilizidi kuongezeka maradufu,helikopta za kijeshi
zikakumbwa na kadhia ya kusukumwa huku na kule
na nyingine kudondoka vibaya na kulipuka.
Shed alikuwa na kazi ya kuweka vizuizi ili madhara
Yale yasiwaasili raia wa kawaida,kwa asilimia nyingi
alifanikiwa lakini kwa upande wa wanajeshi hali
ilikuwa tete.
"Naenda chini,unanipata hapo,naenda chini nahitaji
msaada,unanipata hapo" sauti zilisikika zikiwa
zinaomba msaada wa dharura
Hali ilizidi kuwa tete,ile picha ilitisha mno kuliko
hata ile ya vita ya pili ya dunia
"Retreat!!,wote rudi nyuma! Hali imekuwa tete" sauti
ya kiongozi ilisikika,hakuna hata helikopta moja
iliyosikika ikijibu majibu Yale
"Shit!! Wamekufa wote" kiongozi alipiga meza na
kushika kichwani akiwa amehamanika vya
kutosha,ghadhabu ikiwa inamtafuna mwili mzima.
"Fikisha ripoti kwa Chifu" "mkuu" zilikuwa ni sauti za
kupokea amri
★★★Ndani ya hekalu la miujiza★★★
Sor alikuwa amefumba macho ndani ya hekalu la
miujiza akizidi kuomba kwa imani kuu,mbele yake
kukiwa na chungu pamoja na ile portal.
Chungu kile kilikuwa kikitoa Moshi mzito uliokuwa
ukiizunguka portal ile ambayo mpaka muda ule Sor
hakupata njia ya kuifungua aelekee duniani
Nje ya hekalu lile la miujiza watu wa Sor walikuwa
wakimsindikiza katika maombi yake hasa wasichana
wenye mavazi meupe waliokuwa wamepiga magoti.
★★★Tumaini Jipya★★★
★★New Hope★★★
Watu waliacha kushangilia ushindi wa vita
ile,majonzi pekee ndiyo yaliyotawala eneo lile,Shed
akiwa anatweta,Humph akizidi kujilazimisha
kupambana dhidi ya wale popo akiwemo Lisa
ambaye alikuwa akiendeshwa na moja ya mapopo
wale.
Kwa mbali alianza kuisikia sauti ikimuita,alijiuliza
sana ile sauti aliwahi kuisikia wapi lakini hakupata
jibu,akageuka kushoto na kulia kwa mbali
akamuona Sarah akiwa anatazama bila
kujishughulisha na chochote.
Humph akatumia nafasi ile kumshawishi Sarah
awape msaada katika vita ile.
"Sarah tafadhali tusaidie maana hii vita si yangu tu
bali hata wewe pia,natambua wazi unavyonichukia
na hata yote niliyokukosea hukustahili kutendewa
vile,naimani huhitaji kunisamehe zaidi ya kuniona
nateketea lakini vipi kuhusu hawa mamilioni ya watu
utawaacha wateketee mikononi mwako Sarah?,
nakuomba uwahurumie japo kidogo tu" Humph
aliongea kwa uchungu machozi yakimdondoka huku
akiraruriwa kwa makucha na popo wale.
"Siwezi Humph,binadamu si wema hata uwatendee
mazuri mengi kiasi gani,hawaridhiki Humph waacge
wateketee"
"Sarah! Tafadhali fikiria Mara mbili,hata wewe ni
binadamu pia kama wao Sarah"
"Humphhhhhh! Mimi sio binadamu" Sarah alikasirika
machozi yakaanza kumdondoka
"Sarah huwezi kulipinga hilo,tafadhali usiache
tuangamie" Humph alizidi kumbembeleza Sarah na
wakati huo huo akiwa amejisahau kama
anapambana na popo wale.
Akiwa vile vile ghafla akararuriwa mgongoni
akaanguka chini akiwa na maumivu makali,popo
wengine wakampitia tena mgongoni, yowe Kali la
maumivu likamtoka
Wakati huo huo radi Kali zikavuma na kuwachoma
popo wale,sauti Kali ya msichana ilisikika ikipiga
kelele kwa hasira
"Iiiiiiaaaaahaaaaa!!" Hakuwa mwingine bali Sarah
Humph akiwa chini Sarah anafika na kumshika
mkono,walivyoshikana tu radi kali zikaanza kupiga
angani,mwili wa Humph ukaanza kupitisha radi
ndogo ndogo za bluu.
Popo wengi wakazidi kuongezeka,Humph akaanza
kuelea kama puto lililoachiwa na mtoto Mdogo
kuelekea angani.
Shani,Ben na Shed walibaki kutazama hali ile
inayomtokea Humph,popo wote walimfuata Humph,
ilikuwa ni idadi kubwa mno ambayo iliogopesha
kwa kiasi kikubwa.
Humph akawekwa kati na kuanza kushambuliwa
lakini haikuchukua dakika nyingi mwanga wa bluu
ukaanza kuonekana ukipenya miongoni mwa popo
wale,Humph akajikunja kama mtu aliyezidiwa na
baridi awapo kitandani na kujiachia kwa nguvu
akipiga kelele Kali
"Iiiiiiyahaaaaa!!" Mwanga mkubwa ulioambatana na
radi Kali zenye ngurumo za kutisha ukatawanya
popo wale wakiwa majivu huku watu walioshuhudia
tukio lile wakifumba macho kutokana na mwanga
mkali uliosambaa.
Humph akadondoka kutoka juu akiwa hana
fahamu,wananchi hawakuamini kama vita ile
imeishia pale,Giza lilitoweka na kuacha mwanga
angavu.
Ndipo Shed alipotoa kizuizi kilichokuwa kikiwakinga
wananchi dhidi ya maangamizi ya popo wale, kisha
akapaaa juu akitumia ngao yake na kumdaka
Humph wakati huo huo Ben na Shani
wakigonganisha mikono na kusikika wakisema kwa
pamoja "Hakika anaweza hahahahaha!"
Sarah hakuonekana tena maeneo yale,Shed
aliposhuka na Humph,Shani na Ben waliwahi
kwenda kuangalia hali yake .
"Freeze fools! This is police" (Mpo chini ya ulinzi
wapumbavu! Hii ni polisi" "hands up (mikono juu)
sauti za polisi zilisikika nyuma ya wakina Ben
ambao walikuwa juu ya paa la ghorofa.
Ben akashangaa na kumuuliza Shani " nd'o vitu gani
hivi mbona siwaelewi hawa watu" "ni wale
waliokuwa wakitusaidia kupambana ,Fanya kitu Ben"
alijibu shani akikaa mkao wa tahadhali
Ben akainuka na kuanza kuwasogelea taratibu
"Hatua moja zaidi napasua ubongo" alizungumza
polisi aliyeonekana ni kiongozi wa wenzake na
kuishika silaha yake vyema
Ben akasimama na kuwa makini zaidi "mikono
kichwani na ugeuke nyuma,udanganyifu wowote
naondoa kichwa chako" polisi yule alikazia zaidi
Ben akainua mikono juu lakini wakati huo ma wale
wengine walikuwa wakiwashurutisha wakina Shani
wainuke na kufanya kama mwenzao
alivyoamriwa,muda huo huo Ben akafanya kitu cha
kushangaza polisi wale,aliachama domo lake nyuki
wengi wakatoka mdomoni kuwafuata polisi wale.
Palikuwa hapatoshi!!
Shani,Shed na Ben wakiwa wamembeba Humph
wakatoweka eneo lile.
Kumbuka:
Mashujaa siku zote hupambania kile wanachohisi
kuwa ni hatma yao,lakini ushujaa hauji ukiwa hauna
mtazamo wa mambo ya mbeleni. Kuwa Shujaa wa
moyo wako kwanza kabla ya kuwa shujaa wa watu
wengine. Chukua hatua anza sasa
 
Sehemu ya kumi na mbili
....Ilipoishia.......
Shani,Shed na Ben wakiwa wamembeba Humph
wakatoweka eneo lile.
.....Twende sambamba........
Upande mwingine Sor alifumbua macho ghafla
akiwa ameikunja sura yake,akainuka haraka haraka
na kufungua milango ya hekalu.
"Sijafeli sana,nimepata ugeni" Sor aliongea na
kuangalia juu ,popo mkubwa akashuka kutoka
angani,hakuwa mwingine bali Lisa.
Alipofika maeneo fulani,Moshi mzito mweusi
ukatoka mdomoni mwake na kuwa popo mkubwa
aliyemnyakua Lisa mpaka usawa aliopo Sor na
kumuachia,Sor akamdaka kisha yule popo
akayeyuka na kuwa Moshi na kupotelea ndani ya
hekalu.
Sor akatabasamu kisha akaingia ndani na Lisa
mpaka katika jiwe la hekalu na kumlaza kisha
akampulizia hewa nyepesi iliyoonekana kuwa na
wekundu inapotoka mdomoni mwake.
"Lala Usingizi mnono mtoto,mpaka pale atakapofika
mwenzako" yalikuwa ni maneno ya Sor kwa
Lisa,akimuacha Lisa akikoroma
"Muweke mahali panapomfaa" alimalizia kwa kauli
hiyo na Mara moja akajitokeza mwanaume mmoja
aliyeshiba na kumbeba juu juu
★★★Ilivyokuwa Upande wa Sor★★★
Ule wakati wa Humph kuongezewa nguvu na timu ya
Ben,Sor alikuwa amelala kitandani kwake,ghafla
akastuka akiwa anatweta,Macho yamemtoka mno
ndipo mlinzi wake wa karibu akamfuata haraka na
kumuhoji kwa upole tatizo linalomsumbua.
Sor alikuwa ameingiwa na uoga wa ajabu,kwa hofu
akamkumbatia mlinzi wake huku akiwa amejikunyata
mno.
"Ndoto! Ndoto mbaya,aaah! Inatisha mno" aliongea
Sor
"Nisimulie nikupatie ufumbuzi,eeh malkia wangu"
aliongea kwa unyenyekevu mlinzi yule
"A...a...me....o....nge....ze....wa...nguvu
zaidi,naogopa mwisho wangu umefika" alizungumza
Sor akiwa anatetemeka kwa hofu ni kama mtu
aliyeshikwa na baridi Kali.
"Nani huyo malkia wangu anayekuadhibu hivyo?"
Mlinzi wake akauliza kwa taharuki huku macho
akiyatupa huku na kule akiwa anajaribu kutazama
huenda angemuona mtu huyo anayekatisha Usingizi
wa malkia wake.
"Yule mtoto,yule mwenye macho ya ajabu" Sor
alijibu kwa woga zaidi akibabaika
Haraka yule mlinzi alitambua kuwa lile ni tatizo
akamchukua Sor na kutoka nje akielekea kwa
mganga wao mkuu.
"Anatatizo (malkia) mshughulikie" aliongea mlinzi
mkuu wa Sor baada ya kufika kwa mganga mkuu
"Sina tatizo,ni yule mtoto ameongezewa nguvu" Sor
alijibu kauli ya mlinzi mkuu kwenda kwa mganga
mkuu akiwa anatetemeka
"Hawezi kukushinda malkia wangu,wewe ni mwenye
nguvu mno" aliongea mganga mkuu akiwa mwenye
tabasamu.
"Unasemaje wewe?" Sor alijikuta akiinuka ghafla na
kumkamata mganga mkuu kooni mpaka akainuka
urefu wa sentimita kadhaa.
"Unaniona navyoteketea wazi wazi alafu
unazungumza upuuzi wa kunipambia sio?" Sor
alibwata
"Ha...pa...na" mganga mkuu alijibu kwa tabu huku
taratibu akiunyoosha mkono ulioelekeza mezani na
kutokea jumba Fulani la dhahabu likiwa katika
mfano wa hekalu. Sor alipotazama ule upande na
kukiona kijumba kile kilichotokea kimaajabu
akamuachia taratibu mganga yule na kulisogelea
jumba lile la dhahabu,mganga mkuu akaishia
kukohoa mfululizo
"Liko wapi hili hekalu?" Sor aliuliza kwa hamaki
mikono yake ikiwa inatetemeka mno,ilionekana wazi
alikuwa akilitambua
"Lilifichwa zamani sana,twende ukamuoneshe huyo
mtoto kuwa bado wewe ni bibi yake tu,huishiwi
maarifa" mganga mkuu aliongea kwa tabu akiwa
amelishika koo lake.
Haraka haraka Sor akatoka nje akiwa
amemtanguliza mganga mkuu,walitembea umbali
mrefu mpaka sehemu yenye mawe makubwa ndipo
mganga mkuu akatoa boksi dogo la mbao
akalifungua na kuingiza mkono ambao ulizama
kabisa tofauti na muonekano wa boksi lile
uliolingana na boksi la kutunzia wino wa mihuri.
Mkono ulipotolewa ulitoka na jumba dogo
lililofanana wazi na kijumba kile cha dhahabu
alichokiacha kwake,hiki kilikuwa na mwonekano
thabiti wa hekalu,akaliweka kiganjani na kulipuliza.
Kadri jumba lile lilivyopulizwa na pumzi ya mganga
mkuu ndivyo lilivyozidi kukua mpaka lilipofikia eneo
husika na kutua kwa kishindo huku likitimua vumbi
kubwa lililotimka kwa kasi na kuwafanya wote
waliopo pale wazibe macho yao.
Lilikuwa ni hekalu kubwa lililoonekana mbele
yao,hakuna aliyetarajia kitu kile kuonekana mahali
pale baada ya kupita maelfu ya miaka tangu heku
lile lifungwe mahali yote kwa yote ni kutokana na
kuhofia miujiza yake mikuu ingeweza kutumika
kuleta maaafa. Sasa liko chini ya Sor,Hatariii!!
Sor akawa wa kwanza kuingia ndani ya hekalu lile la
miujiza,alipoingia tu sura yake ikaonekana kila
mahali "kweli ni hekalu la miujiza" Sor alijisemea
moyoni akiwa anasogea mbele mahali palipowekwa
vitu vingi mno.
Kabla hajafika ndege mmoja anayeng'aa akajitokeza
na kumfuata Sor,Sor akatabasamu na kuinua kiganja
ili atue lakini ndege yule hakuwa wa kawaida,alitele
za ghafla na kuingia kifuani mwa Sor,akabaki
amwachama mdomo na kutoa macho yaliyokuwa
yanatoa mwanga wa kung'aa uliokuwa kwa yule
ndege.
Mwanga ule ulikuwa mithili ya moto kadri muda
unavyokwenda,macho ya Sor yaligongana ana kwa
ana na sanamu lililojengelewa vizuri ndani ya hekalu
lile la miujiza.
Macho ya sanamu lile yakapata uhai,Sor
akanyanyuliwa juu kwa juu akiwa anavutwa taratibu
kulielekea sanamu lile,alipokaribia mwanga mkali
ukatoka machoni mwa sanamu lile na kuzama tena
kifuani mwa Sor uliomfanya azidi kutoa mguno
usiojulikana kuwa ni wa maumivu au raha.
Sor akatua chini akiwa amerudi katika hali ya
kawaida isipokuwa katikati ya paji lake la uso
palionekana salama inayong'aa kama taa ikiwa
inazima na kuwaka. Taratibu akaisogelea ile meza
yenye vitu vya ajabu ajabu ikiwemo chungu kimoja
kilichokuwa kikiwaka moto na kuzima huku Moshi
mkali ukiwa unatoka ndani yake.
Mlango wa hekalu ukajifunga,nje kukiwa na
wanawake waliotayari kufanya nae ibada,Sor
akaaanzisha ibada ile aliyoifahamu yeye akiwa na
malengo mahususi.
Ndipo pale tuliposhuhudia dunia ikivamiwa na popo
wa ajabu na kufanikiwa kuharibu vitu vingi pia
walifanikiwa kuondoka na Lisa.
★★★The Chase¿¿Wanted★★★
★★Mkimbizano¿¿Msako★★★
Magazeti na vyombo vya habari vyote vilikuwa
vikitangaza sura za watu wanne ambako walikuwa
wakitafutwa kwa udi na uvumba ili wajibu mashtaka
juu ya ule uvamizi wa viumbe wale jamii ya popo
(creatures). Kiongozi aliyepewa dhamana ya ulinzi
katika jiji la Reycity alisikika akisema
"Vita haina macho wala mwenyewe,uwe ni mtoto
Mdogo mama mkubwa haibagui hivyo basi haijalishi
ulikuwemo ndani ya vita ile ama haukuwemo lazima
uwajibike"
Humph alikuwa bado amepoteza fahamu na hata
alipokuja kuzinduka alipewa taarifa za kustusha
kuwa Lisa ametoweka kabla anga halijafunga,
Humph aliinuka na kuanza kuanza kutafuta huku na
kule kama chizi,mwisho akakaa chini akilia,watu
wote hawakutaka kumgusa mpaka alipotulia
mwenyewe uchungu ukiwa umepungua ndipo
akapewa taarifa nyingine mpya kuwa wanatafutwa
na polisi kila mahali.
 
Macho ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na tatu

....Ilipoishia.......

Humph alikuwa bado amepoteza fahamu na hata alipokuja kuzinduka alipewa taarifa za kustusha kuwa Lisa ametoweka kabla anga halijafunga, Humph aliinuka na kuanza kuanza kutafuta huku na kule kama chizi,mwisho akakaa chini akilia,watu wote hawakutaka kumgusa mpaka alipotulia mwenyewe uchungu ukiwa umepungua ndipo akapewa taarifa nyingine mpya kuwa wanatafutwa na polisi kila mahali.

......Shuka nayo.....

Meno ya Humph yakazidi kuumana kwa hasira,alichukulia lile suala uzito ambako si waka waida na aliona wazi kuwa kuna haja ya kumalizana na polisi kisha amfuate Sor mahali aliko.

"Kwanini tusiongee na hawa pilasi kuhusu hili suala" Shani alichombeza kidogo
"Hahahaha! Sio Pilasi Shani wanajiita polisi" Shed alimcheka Shani na kumrekebisha kauli

"Kwani hawa polisi ni watu wangapi mbona wamekuwa kiherehere na kuonekana kila mahali?" Ben aliuliza kwasababu huko kwako hakukuwa na vitu kama hivi anavyokumbana navyo

"Sikilizeni jamani hawa polisi ni kama askari wa mfalme wanaolinda ufalme ama milki yao na wametapakaa kila mahali ili kuhakikisha mlinzi wa raia ma Mali zao" Humph aliamua kuingilia kati na kulitolea maelezo jambo lile.

"Sasa kwanini tusiwaombe msaada tukapambane na Sor" Shed aliongea

"Kweli kabisa wanatufaa wale" Shani alidakia

"Mmmh! Mmmh!" Humph akajikohoza "nisikilizeni hawa si watu wakuaminika hata kidogo hivyo ondoeni hilo wazo,kingine tunahitaji kuwakwepa kwa gharama yoyote wakati tunatafuta njia ya kumpata Sor lakini mkae mkijua kuwa nyie mnatumia nguvu ya asili ambayo ni kama zawadi kwa kila kizazi chenu na wao wanatumia sayansi" Humph alijaribu kuiweka ile hoja sawa.

Kila mtu alikosa cha kusema hiyo ikampa nafasi Humph kuvuta mtoto wa meza na kuchukua kitabu ambacho Mara ya mwisho alimsomea mzee Mandevu wakati ule alipokuwa anataka kufahamu namna ya kuipata portal.

Shani Shed na Ben wakatulia baada ya kukiona kitabu kile.

★★The Transformation★★
★★★★Mbadilishano★★★

"Sasa Kama portal haiwezi kufunguka basi tuitumie kama njia ya kufanyia mashambulizi" Sor alimwambia mganga mkuu

"Hiyo njia haiwezi kupitishwa binadamu kwa namba yoyote ile ni lazima afe,Mimi naona njia nzuri ni hii ya kuwashambulia bila kujitokeza nafikiri itasaidia kuwadhoifisha mpaka pale portal itakapofunguka" Mganga mkuu alishauri

"Nahitaji vitendo tafadhali" alizungumza Sor

"Umeiona hiyo medali ya mtu aliyeshika upanga akiwa juu ya hilo joka lenye vichwa vitano?" Mganga mkuu alimuuliza Sor huku akimuonesha mahali ilipo ile medali

"Nimeiona ndiyo"

"Iangalie vizuri,kwa ukaribu zaidi" mganga mkuu alisisitiza,Sor akasogea na kuitazama vyema zaidi

"Mbona ni kama ya tofauti hivi,naona kwa ndani kuna kivuli cha mtu" Sor alijibu

"Haswaa,hiyo medali ni gereza la Zedusa mfalme wa majoka ya zamani sana,alipofanya makosa akaadhibiwa kwa kuwekwa humo tangu karne na karne lakini medali kama hiyo ipo duniani na ni moja tu duniani kote" Aliitolea maelezo ile medali

"Sasa itafanya kazi gani hiyo medali ikiwa mtu mwenyewe yupo kifungoni?" Aliuliza Sor akionesha wazi kuwa hajaona thamani ya kuwa na ile medali

"Endapo tutaunganisha nguvu yangu na yako tunaweza kumuhamisha toka kwenye hii medali na kutokea kwenye ile medali dunjani akiwa huru" Mganga mkuu alipambia akiwa na tabasamu murua.

"Siwezi kusubiri zaidi,tuanze kazi" Sor alijibu akiwa mwenye tabasamu.

Mganga mkuu alimfuata Sor na kushikana mikono wakainua juu kisha wakaanza kunena maneno ya ajabu kwa pamoja wakianzia sauti ndogo na kadri muda unavyokwenda sauti zao zilizidi kuwa kubwa zaidi na zaidi

Medali ile ilianza kutoa mwanga Mdogo taratibu ukazidi kuongezeka na kuanza kutoa mwanga mkali uliosambaa hekalu nzima kisha ukatoweka ndipo wakashusha mikono wakiwa wanatabasamu

"Zoezi letu limefanikiwa" alisema mganga mkuu

"Limefanikiwa Mara mbili,unajisikiaje? Najua unajihisi mwepesi kuliko kawaida eeeh?" Sor alijibu na kuangua kicheko cha kejeli

Mganga mkuu akastuka na pale pale akaanza kuzeeka kwa kasi(uzee ulimvaa ghafla) huku akikosa pumzi,ukumbuke kuwa hawa watu walikuwa hawazeeki.

Alimnyooshea mkono Sor na mwisho akafa huku mwili wake ukipukutika kama vumbi.

"Aaaaah! Najihisi mwenye nguvu zaidi,hahahaha!" Sor alijisemea na kutoka ndani ya hekalu.

★★★The Rise Of Snake Warrior (Zedusa)★★
★★Kuibuka Kwa Shujaa Wa Majoka★★

Katika sehemu fulani duniani,ndani ya jumba moja la kale linalotunza vitu vingi vya kale ulitokea mwanga mkali sana. Mzee aliyekuwa analinda ndani ya jumba lile hakuwa mbali nalile eneo akasogea kwa tahadhari ili atazame kinachoendelea sehemu ile.

Alipochungulia tu akakumbana na joka lenye vichwa vitano likiwa limebeba mtu mwenye miraba minne mkononi akiwa na upanga,katika hali ya kustuka akaparamia vitu vilivyokuwa jirani naye.

Kabla hata hajainuka joja lile likawa limeshamfikia,likamrukia na kusababisha damu zitapakae kila mahali.

Humph akastuka kutoka kitandani,jasho jingi nikiwa linamtoka mwili mzima. Shed Shani na Ben wakatokea mle ndani haraka yote ni kutokana na ulinzi na hisia walizokuwa nazo.

"Kuna mtu mwenye upanga akiwa juu ya joka lenye vichwa vitano ametoka ndani ya medali na kufanya mauaji" Humph alieleza

"Ni shujaa wa majoka aliyefungwa karne nyingi ndani ya gereza ambalo ni hiyo medali alimotokea,tuna kazi kubwa ya kufanya" Shani alitoa ufafanuzi mfupi

"Niliwahi kumsikia tu katika hadithi za kale kumbe ni kweli?" Shedi aliuliza nd'o hiyo na sasa utapambana naye live" Ben alijibu mbona huwa wanasema hafi hata kwa nguvu gani ,haiwezi kumteketeza ^ shedali ongea kwaupole.

"Kufa kwake mpaka medali iteketezwe" Shani alikata kauli, "tunaipataje hiyo medali sasa? Humph aliuliza nakabra hawajamjibu kwenye runninga ikarushwa habari kuhusu kifo cha mfuzaji wavitu vingi vya Kale akiwa ameandikwa maneno mgongoni ambayo Shani aliyatafsiri vyema kwani yaliandikwa kwa lugha yao.

" mtalipa kwa unyama niliotendewa" Humph alijijuta akiingiwa na ubaridi maana jitu lile lilikuwa linatisha ukilinganisha na yale majoka aliyopanda. Ben Shed na Shani wakaishia kushusha pumzi ndefu

"Hii ni hatari kwa kweli" Ben alijisemea

Ben alikuwa na uwezo wa kutambua harufu,akaongozana na Humph kumtafuta Zedusa yule shujaa wa majoka huku Shani na Shed wakienda eneo la tukio kuchukua medali kwaajili ya kuiteketeza.

Humph na Ben walifika eneo moja lenye watu wengi wanaopenda kwenda kubarizi maeneo mazuri na tulivu ya ufukweni. Sehemu ile ilikuwa na miti kadha wa kadha iliyopendezesha mazingira Yale. Ben akasimama na kuvuta harufu vizuri ghafla miti akaanza kurushwa kuwaelekea watu waliokuwa wakibarizi ufukweni,Humph akapata kazi ya kupotea na kuzuia miti ile kila sehemu inapotupiwa mwisho Zedusa akajitokeza,mkia wake ukiwa umemkunja mtoto mdogo.

Vichwa vitano vyote vilikuwa vinatoa ndimi nje kwa uchu wa kumtafuta yule mtoto,Humph akasimama akiwa amechoka,macho yakiwa na mwanga mweupe.

Ben akaanza kumfuata Zedusa,hasira ikiwa imempanda kuliko kawaida, Picha ya Ben akiwa anatawanywa vipande vipande ikapita machoni mwa Humph,Humph akapotea haraka na kutokea mbele ya Ben na kumzuia,Ben akaleta ubishi,wakiwa wanabishana Zedusa akamrusha mtoto lakini Humph akawa ameshamuona kwa spidi ya ajabu akapotea na kutokea juu kumdaka yule mtoto akakumbana na mkia wa Zedusa uliomchapa na kumrusha mbali.

Humph akaishia kutoa mguno wa maumivu,Ben hakusubiri akajirusha kabla hajafika akakutana na ubapa wa panga uliomrudisha alikotokea. Humph akasimama akiwa na yule mtoto ambaye alimdaka alipomuangalia vizuri alikuwa tayari amezirai.

Kumbuka:

Watoto ni Taifa la kesho kama ilivyo wewe Leo,haijalishi ni mtoto wako,wajirani yako au mtu mwingine yeyote. Hao wote wanaliandaa na kulijenga taiga la kesho kama unavyofanya wewe kwa sasa. Tuwapende tuwalinde na kuwaongoza katika misingi iliyo bora zaidi. Chukua hatua anza sasa
Tunasonga mbele,nicheki kwa 0625444578
 
Macho ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na nne

....Ilipoishia.......

Humph akaishia kutoa mguno wa maumivu,Ben hakusubiri akajirusha kabla hajafika akakutana na ubapa wa panga uliomrudisha alikotokea. Humph akasimama akiwa na yule mtoto ambaye alimdaka alipomuangalia vizuri alikuwa tayari amezirai.

.....Shuka Nayo........

Humph akamshusha chini kistaarabu kisha akasimama tena,Zedusa hakusogea popote alibaki pale pale akiwa anasubiri wajipange,mkia wa yule nyoka ukiwa unatikisika na kutoa kamlio ka kipekee "chekechekecheke"

Kumbuka kuwa nguvu za Humph zikizidi macho yake yanakuwa na mwanga wa bluu bahari japo nguvu zile hakuwa na uwezo wa kuzimudu.

Humph akaanza kumsogelea Zedusa taratibu,radi zikaanza kupiga mikononi mwake taratibu kama cheche za moto vile.

Zedusa akakaa chonjo,tabasamu pana likautawala mdomo wake "kama Mandevu,hamjatofautiana kwa lolote" manebo yalimponyoka Zedusa

Humph akaanza kuchanganya miguu na mwisho zikawa mbio kumfuata Zedusa pale alipo,kasi yake ilikuwa mithili ya kimbunga,alipomkaribia Zedusa aliyekuwa akitazama kwa umakini mkubwa akapotea na kutokea upande wa mgongoni,mashambulizi yakakolea lakini yote yalikuwa yakitolewa vyema na Zedusa kiasi kwamba ikaonekana Humph ni kama anaupasha mwili wa Zedusa ambao bado haukuwa ukihisi kuchemka kwa mpambano ule.

Baada ya Ben kuona vile akaamua kuutumia mwanya ule kuongeza nguvu ya kushambulia,akajigeuza nyuki na kuanza kuving'ata vile vichwa vya nyoka,nyoka wale wakaanza kupiga kelele za kuzidiwa na sumu ya nyuki,Zedusa akakasirika na kumtwanga Humph kipigo kitakatifu kila alipotokea.

Humph akawa hoi kwa kipigo kile,ndipo Zedusa alipoachama domo lake sambamba na nyoka wale,upepo mkubwa ukatoka mdomoni mwake lakini kwa wale nyoka mate ya sumu ndiyo yaliyotawala eneo lile.

Kwa Mara nyingine tena Humph akatumia macho yake kutoa nuru kali iliyoyafanya mate Yale kusimama kwa muda na hapo akaongezea radi zilizokuwa zikitoka mikononi kukausha sumu ile lakini bado hakushinda vita ile baada ya Zedusa kuunguruma zaidi kwa hasira na kuufanya upepo uongezeke maradufu na kuwabamizia mbali.

Humph na Ben wakabaki chini wakigaragara kwa maumivu makali,Ndipo Zedusa akachomoa panga lake ambalo halikutumika hata kidogo katika mpambano ule,kile kitendo cha kulichomoa panga kutoka ndani ya ala,kelele Kali zikasikika ikiwa ni msuguano wa panga na ala yake.

Humph na Ben wakaziba masikio ambayo mpaka panga lile linachomoka yalikuwa yameanza kuvuja damu,Humph akaona maono pale pale namna ambavyo anaenda kukatwa katwa na Zedusa akiwa pale chini

Akaamua kujikakamua ili aliepuke tukio lile lakini miguu ilimkatalia,Zedusa akaanza kusogea kwa maringo akiwa na sura mbaya isiyoelezeka ukatili uliojaa ndani yake.

Humph akaona njia pekee ya kuijtetea ni kutumia fimbo ya mzee Mandevu,akaichomoa mkononi na kujaribu kuitumia kuinuka lakini haikuwezekana

Kidogo Zedusa akapata mshangao kuiona fimbo ile,mwendo wake ukawa wa tahadhari kidogo maana aliufahamu mziki wa fimbo ile. Humph hakuwa na nguvu hata ya kujiinua kutoka pale chini.

Zedusa akarusha panga lake tayari kummaliza Humph,kwa bahati likagonga kizuizi. Akaonekana Shedrack akiwa mbele ya Humph ameweka kizuizi kile.

Mama wa barafu akaachia kombora matata(Shani) likampiga nyoka yule na kumsogeza nyuma kwa hatua chache akiyumba yumba.

Mpaka Zedusa anakuja kutulia,kundi LA watu wanne lilikuwa mbele yake likimtazama kwa uchu wa kumgawa vipande vipande. Shed akajizungusha na kuisukuma ngao yake iliyotoka kama upepo iliyomsogeza Zedusa nyuma kwa nguvu mno kisha Shed akawahi kwa haraka juu ya vichwa vile vya nyoka na kuvigonga gonga kwa aina ya kipekee sana.

Joka lile kubwa lililobeba vichwa vitano likapata mawenge na kutaka kummwaga Zedusa huku wakiwa wanapiga kelele "hssssssss"

"Nimefurahi kupambana na we we shujaa wa joka lenye vichwa vitano" Shed alipaza sauti akiwa amerudi katika mstari wa watu wanne.

Zedusa akainua joka lake kama wafanyavyo wapanda farasi,kwa kasi akamfuata Shed,Shank akaachia tena kombora la barafu lililopanguliwa na Zedusa,Shed akawahi kutengeneza ngao yake baada ya Zedusa kuachama domo lake lenye upepo mkali,kitendo cha kuzuia upepo,mkia wa joka lile ukamchapa Shed aliyemgonga Shani wote wakaangukia pembeni.

Humph tayari alikuwa ameinuka na fimbo yake,haraka akainyoosha kwa nguvu kumfuata Zedusa,radi kali ikatoka ikiambatana na vumbi.

Zedusa akaukinga upanga wake akiutumia kama ngao yake,ila nguvu ya ile fimbo ya mzee Mandevu ilikuwa kubwa kiasi cha kumtawanya yeye na nyoka wake. Haijulikani lile vumbi lilitoka wapi maana lilidumu kwa muda kiasi,Shani akarusha ile medali kwa Humph,Humph alivyoidaka tu macho yake yakaongeza nuru ikawa ya rangi ya bluu bahari.

Mkono ulioshika medali ukazidi kutoa radi zilizofanya ile medali ianze kuelea, zedusa akatahamaki kuiona medalist ikielea ambapo hapo kabla aliitambua kama sehemu ya gereza alilokuwa amehifadhiwa kwa karne nyingi mno.

Joka lake likiwa na vichwa viwili pekee vilivyo hai,Zedusa akajikokota kumfuata Humph ili afanye kitu kwaajili ya kujitetea.

Ndipo Humph akainua na mkono wa pili kuunganisha nguvu,Zedusa akapiga yowe la uchungu,medali ile ikatawanyika vipande vipande na kutoa mwanga wa bluu

Vivyo hivyo kwa upande wa Zedusa mwanga wa bluu ulikuwa ukimpasua kila sehemu ya mwili wake pamoja na joka lake mpaka pale walipopotea kabisa na kubaki alama za uwepo wa joka lile la ajabu.

Hali ya hewa ikaanza kutulia,nyasi na baadhi ya mimea ilionekana kukauka kutokana na nguvu alizotumia Humph kutoka kwenye fimbo ya mzee Mandevu.

Wakiwa wamemaliza tatizo lile ghafla helikopta ya polisi inasikika maeneo Yale huku kipaza sauti kikisikika kufanya kazi yake vyema.

"Kuanzia sasa mpo chini ya ulinzi,mtu yeyote asithubutu kujigusa,kosa lolote litagharimu maisha yenu" sauti ile ilipokoma milio ya bunduki ikasikika kila upande ikiondolewa usalama, Humph,Ben,Shed na Shani wakabaki midomo wazi wasijue la kufanya.

★★★In Magic Temple★★★
★★Ndani ya Hekalu la Miujiza★★

Medali iliyokuwa upande ule wa hekalu la miujiza iliwaka mwanga wa bluu na mwisho ikasambaratika vipande vipande,Sor akaghadhibika na kuinua mikono juu huku amekunja ngumi, kelele alizopiga zilisababisha hekalu zima kutetemeka.

Mlinzi wake wa karibu akaingia mbio mbio kutazama usalama wa mle ndani,alistaajabu kumuona Sor akiwa anawaka katika paji la USO,haukuwa mng'ao wa kawaida hata kidogo pia ulikuwa mng'ao kama wa taa itoavyo mwanga.

Sor alikuwa ni kama ametokwa na fahamu baada ya kuonana na mlinzi wake ana kwa ana akainua mkono wake ambao ulionekana kama umeshika kitu,kadri alivyouinua ndivyo mlinzi wake alivyozidi kuinuka juu.

Taratibu Sor akaanza kumvuta mpaka shingo ya yule mlinzi wake ilipofikia mikononi mwake, muda huo wote yule mlinzi alikuwa akihangaika kujitoa bila kumdhuru malkia Sor ama kutumia nguvu yoyote.

Sor akazidi kubana shingo ya mlinzi wake mpaka pale ambapo mlinzi yule alianza kuhisi anakosa pumzi na kuamua kujinusuru na mauti isiyoyalazima kwa kuushika mkono wa Sor na kutumia nguvu zake zilizopemya mwilini mwa Sor na kurushwa mbali mlinzi yule ni kama mtu aliyepigwa shoti.

Kumbuka:

Haijalishi ni wema kiasi gani unaufanya si kwa watu au mtu,bado kuna watakao yaona hayo kuwa ni mambo mabaya kwao na yasiyowafaa kwa upande wao. Binadamu hawajakamilika kama malaika hivyo Fanya kila kitu kwa sehemu yako/sehemu uliyobarikiwa. Chukua hatua anza sasa

Tukutane sehemu inayofuata. Likeee hazitoshiii jamani hata 100 hazifiki
 
Macho ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na tano

....Ilipoishia.......

Sor akazidi kubana shingo ya mlinzi wake mpaka pale ambapo mlinzi yule alianza kuhisi anakosa pumzi na kuamua kujinusuru na mauti isiyoyalazima kwa kuushika mkono wa Sor na kutumia nguvu zake zilizopemya mwilini mwa Sor na kurushwa mbali mlinzi yule ni kama mtu aliyepigwa shoti.

.....Endelea nayo.....

Mlinzi yule aliangukia sakafuni huku Sor akirudiwa na ufahamu baada ya ule msuguano wa nguvu zao,Sor alijikagua mwili wake na mikono yake akiwa haamini kuwa zile nguvu zote ni za kwake.

★★★The Rescue★★★
★★★Ukombozi★★★

Humph hakuwa vizuri hata kidogo,hata ile nguvu ya kuinuka hakuwa nayo,Shed alionekana wazi kuupenda ule mchezo wa polisi kuwafuata fuata,akatabasamu na kuanza kuongea kwa hisia na wenzake .

"Jiandaeni tunaondoka hapa sasa hivi" Shed alizungumza na kujiandaa kuchomoka kutoka mikononi mwa polisi.

Polisi nao walikuwa bado wakisubiri amri kutoka makao makuu juu ya watu wale.

Vyombo vya habari havikuwa mbali,matangazo yalirushwa moja kwa moja kila mtu akiushuhudia mtanange ule,ikumbukwe kuwa 'mwanzo Humph alisaidia sana wananchi enzi zile ambazo Sor alikuwa duniani,watu walivyoona polisi wanamtafuta wakidai ni mhalifu Ndipo picha mpya ikajijenga vichwani mwa wananchi wakishangaa uonevu wa jeshi lile la kulinda usalama wao.

Pale pale mabomu ya machozi yakatupwa eneo la tukio na kufanya Moshi mzito uliowatawanya polisi waliopata shambulio la kustukiza. Dakika mbili mbele risasi zilirindima ovyo mpaka pale Moshi ulipotawanyika lakini kundi zima la Humph halikuwepo eneo lile,polisi wakazidi kuchanganyikiwa na shambulizi lile lililowafanya wapoteze wahalifu wale.

Kwa upande wa pili wananchi walishangilia baada ya kuona kundi lile la Humph limetoroka mikononi mwa polisi japo "Si kila akuchekeaye basi anakupenda au anapenda vile unavyofanya"

★★★★★★★★

"Kooh! Kooh!! Kooooh!" Humph alikuwa akikohoa Ndipo akapewa maski yenye hewa safi avute. Ben,Shed na Shani walikuwa wakishangazwa na kundi la watu wale ambao walifanya kazi ya kuwakomboa kutoka katika mikono ya polisi ndani ya dakika chache na kwa wepesi wa ajabu.

Pia Ben,Shed na Shani hawakusumbuliwa na hewa ile huenda ni kwasababu wao walikuwa watu waishio milele yaani immortals.

"Niite Kamanda One ni kiongozi wa kikosi hiki cha ukombozi cha kujitegemea na hawa ni ....." Alijitambulisha kiongozi aliyekuwa na kombati nyeusi za kijeshi.

"Jaco" "Jen" "Sai" "Rose" "Ivan" "karibuni katika kikosi chetu" Walisema kwa pamoja Ndipo Ben,Shed na Shani wakapata amani,wakapewa mikono na kuipokea kwa shamra shamra.

Walipofika makao makuu ya kikosi kile wakahitaji kumpa Humph kitanda ili akapatiwe matibabu lakini Shed na wenzake wakaomba chumba ili wamfanyie huduma ile ya kwanza,Matibabu yalianza Humph akiwa katikati ya wote huku kila moja akiutumia uwezo wake kunrudisha Humph katika hali ya kawaida.

Yote hayo wakati yanafanyika kamanda One alikuwa akitazama vyema kabisa na kufuatilia hatua kwa hatua haikujulikana ni kwanini anafanya vile.

Haukupita muda mrefu Humph akawa amerudiwa na fahamu na nguvu zake,mwili wake haukuwa na jeraha lolote lile. Shani akatoka na kuomba chumba kwaajili ya kumpumzisha Humph.

★★★The Attack★★★
★★★Shambulizi★★★

Ikiwa ni siku moja tu baada ya tukio zito la kundi la Humph kuwatoroka polisi,katikati ya jiji la Reycity anaonekana Sarah akiwa katika hali isiyo ya kawaida,mwili wote ulionekana kutetemeka.

Akiwa amejichanganya kwa watu wengi ghafla akaonekana akishika kichwa na kupiga goti moja chini,akaanza kupiga kelele ikionekana wazi kuwa nguvu zile alizonazo zimemzidia.

Ikumbukwe kuwa Sarah alipata nguvu zile kama ajali tu baada ya kukutanishwa kati ya nguvu za Humph na za Shani kipindi wapo katika misitu ya mlima unaoanguka.

Ile hali ya kutetemeka ikazua balaa lingine la maumivu lililomfanya apige ukunga wa maumivu ulioambatana na radi na mabonge ya barafu yaliyokuwa yakitawanyika ovyo.

Kama ilivyoada polisi wa mji walikuwa wepesi kufika katika eneo la tukio na waandish wa habari nao hawakuwa nyuma kutafuta ulaji wa siku hiyo.

Waandishi wale walizidi kusogea pale alipo Sarah kwa kasi kubwa huku raia wa kawaida wakiwa wanasogea kiuoga uoga.

"Hakuna kizuri kisichokuwa na kasoro" hivyo ndivyo ambavyo ilitokea kwa Sarah,nguvu zile zilimzidi na kumfanya ajisikie vibaya,akaanza kushambulia kila anachokiona,magari,majengo na watu waliokaribu naye.

Upande mwingine Ben,Kamanda One walienda chumbani kwa Humph kumjulia hali,Humph anadai bado hali yake si njema sana na papo hapo taarifa zilizotokea punde zinatangazwa kuwa katikati ya jiji la Reycity kuna msichana mwenye nguvu za asili anafanya vurumai.

Humph akaomba picha ile ikuzwe na hapo Ndipo alipogundua kuwa ni Sarah,akapata nguvu ya kuinuka huku akisikika akinong'ona

"Sarah! Lazima nije kabla hujadhurika" Kamanda one kusikia vile akamzuia na kuomba aende yeye kwa kuwa Humph alikuwa bado yu katika hali mbaya.

"Si mtu mbaya yule lazima nifanye kitu" Humph alijibu akionekana wazi kuwa na wasiwasi hasa kutokana na polisi wale ambao walikuwa wakiongezeka kila muda.

"Mimi na timu yangu tutatenda msaada juu ya hili" Kamanda one alisisitiza.

"Hapana sihitaji mpatwe na lolote baya" Humph alijibu huku akiinuka kwa kujilazimisha

"Hapana Humph acha watupe msaada" aliingia Shani na kudokeza

"Sawa" alijibu Humph kiunyonge

Upande wa Sarah polisi waliomba ajisalimishe kabla mambo hayajawa magumu,Sarah hakuelewa wala kukubali suala lile na ndipo polisi walipoamua kurudisha majibu kwa kumtupia Sarah risasi

Kwa Sarah waligonga mwamba haswaa,kiasi cha kuwafanya polisi wazidi kuongezeka zaidi na zaidi. Helikopta ya Kamanda one ilifika eneo la tukio.

Kabla hawajaamua la kufanya Humph akajitosa kutoka juu kumfuata Sarah bila kujali kuwa risasi zinazotupwa ovyo zinaweza kumdhuru.

Ikumbukwe kuwa Sarah alikuwa na nguvu mbili mchanganyiko kutoka kwa Humph na kwa Shani na hii ilimfanya awe na nguvu zaidi kuliko mtu yeyote isipokuwa Humph japo naye hakuwa na uwezo wa kumdhibiti sawa sawa.

"Oh Gosh! Anajiamini nini huyu!" Alisikika Kamanda one akipiga kelele baada ya kumuona Humph akijitosa.

"Sheeed Fanya kitu" Shani alisikika akipaza sauti, Shed bila kuuliza naye akajitosa kwa kasi kuliko Humph

"Wow!!" Sauti ya Jen ilisikika ikifurahia kitendo kile cha kishujaa kilichooneshwa na Shed.

"Inastaajabisha! Yaani wanashuka bila parachuti na hawaofii" Sai alishangazwa mno

"Sio binadamu wa kawaida hao,hawafai kuigwa" Rose alimalizia kwa kauli hiyo na kufanya waliomo ndani ya helikopta kucheka.

Humph alitua kwa kishindo mpaka eneo lile likazama kidogo kisha akainuka haraka na kumfuata Sarah lakini kwa wakati huo Sarah hakuwa katika ufahamu wake wa kawaida.

Humph aliposogea akaanza kushambuliwa na Sarah,Humph hakuwa vyema kiasi cha kupambana,alikwepa Mara mbili ya tatu akaanza kujihisi kizunguzungu,Shed akafika na kuweka ngao(shield).

Kumbuka:

Wema siku zote ni akiba ya miaka na miaka lakini pia ubaya nao ni akiba vile vile,ikiwa utatenda mema Leo ipo siku utatendewa pia wema kama huo haijalishi ni yule yule uliyemtendea au mwingine ila kila kitu kina namna yake ya kurudishwa kama ulivyotoa hata ubaya ni vivyo hivyo. Jitahidi kuwa mwema na kutenda wema ukitegemea kulipwa na wengine au huyo uliyemtendea ikiwa kama si Leo basi ni kesho. Chukua hatua anza sasa

Tukutane sehemu inayofuata.
 
Macho ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na sita

....Ilipoishia.......

Humph aliposogea akaanza kushambuliwa na Sarah,Humph hakuwa vyema kiasi cha kupambana,alikwepa Mara mbili ya tatu akaanza kujihisi kizunguzungu,Shed akafika na kuweka ngao(shield).

......Shuka nayo......

Kamanda One akapaza sauti "code 0425 sitisha mashambulizi,ova!,narudia code 0425 sitisha mashambulizi ova!"

Polisi wakasimamisha mashambulizi yake baada ya kuona kikosi kile kinachoaminika kupambana na matatizo sugu ya uhalifu kimefika eneo lile.

Humph akatumia mwanya huo kumfuata tena Sarah kwaajili ya kumtuliza. Watu wote wakatulia kimya maana walimfahamu vyema Humph,Si polisi wala raia wote walikuwa wakisikilizia kitakachotokea kwa mbabe yule.

Sarah akageuka baada ya kuhisi kitu,alipomuona Humph tukio moja likapita kichwani mwake ila hakulipata sawa sawa. Akajitahidi kukumbuka ikashindikana na zile nguvu zilivyozidi kumuathiri hakumtambua tena yule aliye mbele yake ni nani.

Humph akafika na kumshika Sarah mkono,Sarah alikuwa ameinamisha kichwa chini kutokana na maumivu aliyokuwa akiyapata, kutokana na kushikwa mkono na Humph nguvu zao zikaanza kubadilishana katika miili yao na hilo likawa kosa lingine kwa Sarah,mvurugano wa nguvu zake ukazidi na kusababisha aanze kumtupia makombora ya barafu zikichanganyikana na radi.

Shed akawahi na kuweka uzio makombora Yale yakagonga kizuizi,raia waliokuwa wakishuhudia tukio lile wakaanza kushangilia kwa furaha.

Shed akatumia ngao yake na kumuweka Sarah katikati,muda huo huo Ben na Shani walikuwa wameshafika eneo lile wakazu nguka ngao ile ambayo ilifanya mashambulizi ya Sarah kuishia ndani yake.

Ndipo Humph, Ben na Shani walipoanza kutupa makombora yao juu ya ile ngao na kufanya nguvu ile ipenye ndani na kumdhoofisha Sarah.

Sarah alizodi kupiga kelele na kurusha makombora ovyo yaliyoishia mle ndani,ikafikia hatua akazirai. Raia na polisi wakazidi kupiga kelele za shangwe huku kamanda one akiwaongoza Humph na kundi lake kuelekea ndani ya helikopta wakiwa wamembeba Sarah.

★★★The Reborn★★★
★★Kuzaliwa Upya★★

Sarah hakuwa na unafuu wowote tangu achukuliwe kutoka katikati ya jiji la Reycity,alipelekwa sehemu mbalimbali za matibabu bila mafanikio yoyote yale .

Humph aliirudia droo yake na kutoa kitabu alichoachiwa na mzee Mandevu,kwa kumshangaza kamanda one kitabu kile hakikuweza kusomwa pasipo macho ya ajabu kutoka kwa Humph pekee tena yakiwa yanatoa nuru nyeupe.

Humph alipitia sana kile kitabu mwisho akaiona sehemu moja iliyoandikwa "MOYO WA UZIMA" pembeni yake kukiwa na ramani pamoja na picha yenye kuonesha miti mingi ambayo kwa haraka haraka ni msitu mzito.

Kupitia macho ya Humph ramani nzima ikajionesha kichwani mwake mpaka sehemu yenyewe ambayo Moyo ulionekana upo mahali Fulani palipo na mwanga wa moja kwa moja kutoka juu lakini sehemu yote ikiwa imezungukwa na Giza huku moto ule ukiwa unaelea na kudunda kama upo ndani ya mwili wa binadamu.

"Nimepata jibu,tunaenda mahali panaitwa ' MOYO WA UZIMA',kwa namna yoyote ile lazima tumuokoe mwenzetu"

"Tutajaribu kumsaidia kadri ya uwezo wetu" alijibu Ben lakini Shani hakuwa mbali akadakia "ikitokea akatudhuru,Humph utawajibika kwa hilo" kisha akaondoka kwa ghadhabu

"Ni mambo ya wanawake tu hayo usiudhike" Kamanda one alimwambia Humph

Safari ilianza kwa kutumia helikopta ya kikosi cha Kamanda one mpaka karibu na msitu mnene ambao Humph na timu yake walishuka na kuahidi kuwa watarejea wakiwa wamefanikiwa kumuokoa Sarah.

Kamanda one aliomba awasubiri kwa siku tatu mfululizo na endapo hawatatokea basi angerudi kuendelea na kazi ya kulijenga taifa.

★★The Rise of Seven Souls★★
★★Kuibuka kwa Nafsi Saba★★

Sor akiwa ndani ya hekalu la maajabu kengele zikaanza kujigonga gongs zikiashiria hatari,wakati huo huo zile nguvu za petani alizokuwa nazo Sor zikachukua nafasi katika paji lake la uso.

Mng'ao wa kushangaza ukazidi kujionesha katika paji la uso la Sor,kwa uwezo wa ajabu Sor anainuka mahali alipokuwa amepiga magoti kwa namna ya kipekee akiwa anaelea na kutua mbele ya dhabahu lenye vitu vingi,akainua kitabu kimoja kwa macho kisha kikaanza kujifunua kwa kasi mno.

Kitabu kilipotulia,macho ya Sor yakatazama picha ile iliyopo katika ule ukurasa,ulikuwa ni msitu mnene usioelezeka. Mara moja akatambua kuwa pale ni sehemu yenye "MoYo WA UZIMA".

Kwa kutumia nguvu zile alifanikiwa kuwaona watu wakizamia ndani ya msitu ule wakiwa wamembeba mtu mmoja kwenye machela,Sor akatambua kuwa ni Humph na timu yake. Akili ikamtuma kuwa ile ni mbinu nyingine ya kumuangamiza

Kwa hasira akapiga kile kitabu kwa nguvu zake zote,vikatoka vitu kama goroli vikiwa saba na kupanda juu vikiwa vinaelea na kuzunguka kufuata mduara,kati ya vile saba sita vilikuwa vya mviringo(duara) na kimoja pekee kilifanana na funguo.

Sor akapiga ukelele mkali uliosababisha paji lake la uso lizidi kung'aa zaidi,mdomoni mwake ukatoka moto mkali uliomeza vitu na kuvirudisha tena ndani ya kitabu kisha Sor akatoa kalipio Kali

" Nimewapa uhai kwa Mara nyingine na sasa nendeni mtende kadri mnavyoweza enyi nafsi saba" Ndipo Sor akadondoka na kupoteza fahamu pale pale.

★★★The Falling★★★
★★★Kuanguka★★★

Upande wa pili Humph akiwa na timu yake wanasonga mbele ghafla tetemeko Kali la ardhi likajitokeza na kusababisha mpasuko katikati yao,hii yote ilisababishwa na nguvu za Sor pale alipogonga kitabu kwa nguvu na kuzipa uhai tena zile nafsi saba.

Bonde kubwa likajitokeza eneo lile na kuwagawanyisha Ben na Shani upande wao na Humph na Shed wakiwa wamembeba Sarah kwenye machela nao upande wao. Kwakuwa ilitokea pasipo wao kutarajia walijikuta wakiporomoka ndani ya bonde lile kubwa lililokuwa likiendelea kupasuka kwa kasi ya ajabu.

Humph alifanikiwa kujishikiza mahali huku mkono mmoja akiwa amemdaka Sarah ambaye hakuwa akijitambua,Shed alizidi kuporomoka kuelekea chini kabisa ya bonde lile na kila alipojaribu kutengeneza ngao ilishindikana kutokana na udongo na mawe kumuangukia kila Mara.

Shani alifanikiwa kutengeneza barafu lililonasa na kumshikilia vyema akiwa upande ule wa pili na Ben ambaye alipokuwa akiporomoka kuelekea chini ya bonde lile alijigeuza umbo lake na kuwa nyuki akarudi juu kwa kasi iliyomnyanyua Shani na kumtupa juu ya bonde lile wote wakiwa hoi

Humph alikuwa bado amening'inia,mkono ukiwa unatereza taratibu kutokana na uzito wake pamoja na wa Sarah,alijitahidi mpaka macho yake yakawaka,kitendo kile kilimfanya awe na nguvu za ziada zilizomfanya atoboe ardhi yake kwa vidole na kujishikilia barabara ili asiende chini.

Kumbuka:

Katika maisha hasa unapoelekea kwenye mafanikio changamoto ni nyingi pia nd'o mwanzo wa maadui wengi kujiinua mbele yako ili usifanikiwe,haijalishi ni binadamu au magonjwa hautakiwi kusimama,kazabuti songa mbele. Chukua hatua Anza sasa
 
Macho ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na saba

....Ilipoishia.......

Humph alikuwa bado amening'inia,mkono ukiwa unatereza taratibu kutokana na uzito wake pamoja na wa Sarah,alijitahidi mpaka macho yake yakawaka,kitendo kile kilimfanya awe na nguvu za ziada zilizomfanya atoboe ardhi yake kwa vidole na kujishikilia barabara ili asiende chini.

.....Shuka nayo......

Shed alikuwa tayari amefanikiwa kutengeneza ngao na kupanga juu moja kwa moja akamchukua Humph na Sarah mpaka juu ya bonde lile

"la! uuh! Oof! Jitahidi uweze kufikia matumizi ya kiwango cha juu cha nguvu zako" Shed alimwambia Humph huku akitweta

"Bado sielewi nifanye nini na sijui kwanini hili tukio sijaliona kabla halijatokea" Humph alijibu akiwa anaonekana kweli haelewi .

"Ni kweli kabisa huenda huu msitu una mambo si bure" shed alijibu kisha wakajiinua kwa tabu na kutafuta namba nyingine ya kumbeba Sarah kisha safari ikaendelea huku wakiwa wametengana na akina Ben.

Walipofika eneo fulani ndani ya msitu ule walikuta mahali pana uoto wa kijani mtupu unaopendeza mno,kitendo cha kukanyaga eneo lile lenye uoto wa kijani sehemu yote ikaanza kuzunguka,majira yakabadilika na kuwa usiku wenye giza la ajabu.

Wakatambua kuwa wakati huo wameingia sehemu ya tofauti kabisa Ndipo Humph akatumia macho yake kama mwanga wa kuwafikisha wanakoelekea.

Wakiwa wametembea umbali mfupi,wingu zito likaghubika angani,kwa mbali ikawa inasikika sauti ya kitu kikidunda taratibu.

Uwezo aliokuwa nao Humph ulikuwa mkubwa mno hasa wa kutazama mbali,Ndipo Humph akasimama na kutazama kwa makini,akauona moyo ukiwa mahali unadunda taratibu.

"Tumekaribia" Humph alisema na kuongoza njia,walipokaribia zaidi katika sehemu ile yenye "MoYO WA UZIMA" Ndipo mapigo yake ya moyo ule yakaanza kusikika vyema zaidi.

Humph na Shed wakazidisha umakini,muda huo Ben na Shani haikujulikana wamefika sehemu gani.

Lahaulaaa!! Moyo wa Uzima ulionekana mbele yao ukiwa unaelea katikati ya mwanga mkali uliojipenyeza kutokea juu angani usijulikane ni wa jua au mwezi.

Ulikuwa ni mkubwa usiotosha hata ukubwa wa kifua cha binadamu wa kawaida,huo ulikuwa mtihani mwingine kwamba ni vipi ungeweza kutosha ndani ya kifua cha Sarah.

"Hatimaye tumefika" Humph alipaza sauti na kupiga hatua moja kabla ya kusimamishwa na Shed kwa Sauti Kali "Sima....." Hakumalizia Humph akarushwa mbali akiunganishwa na Shed

Ilikuwa ni mithili ya umeme mkali uliowarusha,Humph akainuka haraka na kumfuata Sarah alipomtazama aligundua hajadhurika Ndipo alipogeuka kwa hasira,macho yakiwa yamevuka mipaka na kuwa ya bluu bahari,Shed naye akasimama haraka na kumuwekea Humph ngao kisha kwa kutumia nguvu nyingi Humph akavuka eneo lile lenye nguvu za hatari ambazo wakati anapita chenye kali zilimwagika kutokana na msuguano mkali uliokuwepo baina ya nguvu zile na nguvu za Humph na Shed.

Mbele ya Humph walitokea Shani na Ben wakiwa jirani kabisa na miale ile mikali ya mwanga ulioushikilia moyo ule wa uzima huku wakijaribu kuwazuia kwa ishara Humph na Shed na mdomoni wakionekana kuongea maneno yasiyosikika kabisa.

Humph kwa hasira akasogea mbele kwenda kuwatoa,ni wazi alikuwa hawezi kujitawala na nguvu zake hivyo alikuwa nje ya mawazo yake,hakufika mbali kikatokea kiduara kingine kilichojitengeneza na kusababisha Shed apaze sauti ya tahadhari kwa Humph huku akiwa na wasiwasi mkubwa

"Ni nafsi sabaaaa,Kaa mbali Humph!" Humph alisita kwenda mbele

"Nafsi hizo ni za maangamizi Humph zilizotolewa uhai na kufungwa ndani ya kitabu milenia mbili zimepita,hazijawahi kushindwa na hakuna wa kuzizuia abadani katika vizazi vya Leo" Shed alizidi kupaza sauti akitoa maelezo kuhusiana na nafsi zile na kumfanya Humph akose chaguo.

Humph alishikwa na ganzi kusikia hazijawahi kushindwa nafsi zile na hakuna wa kuzizuia katika kizazi cha leo,likabaki kuwa fumbo kichwani mwake!

"Nitawalinda rafiki zangu na dunia nzima,niliapa" Humph aliongea kwa sauti nzito yenye matumaini kisha akajikusanya na kusababisha radi zianze kusambaa mikononi mwake,kwa kasi ya upepo akapotea kuzifuata nafasi zile.

Ni mayowe ya maumivu pekee ndiyo yaliyosikika,mtu akarushwa kutoka kusikojulikana na kuanguka pembeni,Shed akamtazama vyema kugundua alikuwa ni Humph macho yake yakiwa meupe.

Humph akainuliwa na Shed taratibu,akaomba Shed amuache na kusimama nwenyewe,nafsi zile saba zikatengeneza vivuli vya watu saba wakiwa ni wanawake watatu na wanaume wanne.

Sauti zao zilikuwa za ajabu ajabu zenye kutisha lakini Humph akaingia katikati kupambana nao,ulikuwa ni mchuano mkali uliomrudisha Humph nje kwa Mara ya pili akiwa hoi kisha nafsi zile zikarudi katika duara na kuendelea kuzunguka.

Shed akamuinua Humph taratibu akiwa na huzuni asijue nini cha kufanya kwasababu alitambua uwezo wake ulikuwa ni Mdogo mno kutosha kupambana hata na nafsi moja kati ya zile saba.

Alilia kwa uchungu na ndipo hapo alipokumbuka maneno ya kale kutoka kwa babu yake aliyokuwa akipenda kuyasema kila Mara anapomfundisha kuwa

'ndani ya saba ipo moja,moja iliyobeba udhaifu'

'Katika nguvu muungano na kupambana,moja huwaangusha kutoka kilele cha juu'

Ndipo akamtazama Humph kwa Mara nyingine na kusema "ndiyo! Ndiyo! Kuna nafsi moja ni dhaifu,ila zote zinafanya kazi kwa umoja,ukiitambua hiyo utaziangusha nyingine" Humph hakuelewa maana yake Ndipo Shed akamtikisa na kumwambia kwa nguvu

"Nafsi moja haionekani kwa macho ya kawaida na hiyo ndiyo udhaifu wa nafsi zote,kwa hiyo pekee utaziangusha nafsi zote,na ndiyo maana mpaka Leo nafsi hizo hajiwahi kushindwa kwa macho ya kawaida"

Humph akatabasamu na kucheua damu,akaomba Shed amuinue na kusimama sawa sawa kisha akafumba macho na kuvuta hisia. Upepo mkali ukaanza kuvuma eneo lile,wingu zito la angani likaanza kutoa miungurumo na radi za ajabu kisha Humph akafumbua macho yake yakiwa ya bluu bahari huku kiini cha macho yake kikipitisha radi mithili ya shoti za umeme.

Shed hakuamini alikuwa akitazama kwa kuvizia kutokana na upepo ule mkali,Humph alizitazama nafsi zile kwa u karibu na kugundua kuwa moja ina umbo la funguo na hiyo ipo tofauti na nyingine.

Humph akatoweka na kutokea katika mzunguko ule wa nafsi zile akaanza kuzunguka sambamba nazo huku akitengeneza radi Kali zilizosababisha ule mzunguko uongeze kasi kama aliyonayo Humph huku lengo lake akiwa anavizia nafsi ile moja na kuichomoa katika mhimili ule.

Shed alivyoona wanafanikiwa akawahi kumuinua Sarah na kumpeleka sehemu yenye moyo ule wa uzima,kitendo cha mwili wa Sarah kugusa ile miale akavutwa katikati na kuanza kuelea mpaka jirani na ule moyo ambao ulianza kuyeyuka taratibu kuingia kifuani mwa Sarah.

Nafsi saba zikakasirika kuona kitendo alichokifanya Shed, Humph akatupwa mbali akisindikizwa na kipigo kikali japo hakuanguka wala kuonekana alipoelekea,Shed akawahi kuweka ngao na kusababisha akoswe na shambulio Kali la nafsi zile.

Shed alizidiwa nguvu,akapiga magoti akijitahidi kuzuia,damu zilizidi kumchuruzika mdomoni na puani lakini wakati huo huo moyo wa uzima ulikuwa unamalizika kuingia kifuani mwa Sarah,ulipoingia wote Sarah akapiga yowe Kali ambalo lilifanya nafsi zile saba kukimbilia katika mwili wa Sarah kupitia mdomoni. Sintofahamu!!

Wakati zile nafsi saba zinamvaa Sarah Ndipo Ben na Shani waliachiwa huru.

Kumbuka:

Unapomsaidia rafiki,ndugu au mtu yeyote kwa kujitoa kwaajili yake usitarajie naye atajitoa kama ulivyojitoa ila jitoe ukiamini kuwa ipo siku kuna mtu atajitoa kwaajili yako kama ulivyojitoa wewe kwa rafiki,ndugu au mtu yeyote. Chukua hatua anza sasa

Like hazitoshi nikikatisha tusilaumiane maana natumia bando kupost
 
Macho Ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na nane

....Ilipoishia.......

Wakati zile nafsi saba zinamvaa Sarah Ndipo Ben na Shani waliachiwa huru.

....Shuka nayo........

Humph Ben Shani na Shed wanashangaa wasiamini kile kinachotokea mbele yao,muda huo Sarah bado anajinyoosha akiwa anaangalia juu huku akiunguruma chini chini

"Agggggggggaaaaah!"

"Humph Fanya kitu" Shed alisikika akiongea lakini Ben na Shani wakaingilia kati kunsaidia Humph kupambana,Humph macho yake yalitua kifuani kwa Sarah akaiona ile nafsi moja ambayo ipo kama funguo ikizunguka.

Humph alikuwa mpya,Ben Shed na Shani waliduwaa haswaa kumuona Humph ameingia katika ile hali ambayo Mara nyingi huwa anashindwa kuistahimili. Humph akatumia mwanya ule kuzichomoa

Sarah akajikusanya nguvu zote,akitumia nguvu za radi,barafu na zile za nafsi saba akawatawanya wote kama mbegu za uwele

Humph akazidi kugugumia kwa maumivu lakini Sarah hakujali,kumbuka kuwa Sarah akimshika Humph nguvu za Humph huongezeka na macho yanakuwa ya bluu,pale pale Humph alianza kuhisi mjazo,macho yaliyokuwa yakififia yakaanza kutoa mwanga wa bluu.

Muungano wa nguvu za Humph na Sarah ukaanza kuziathiri zile nafsi saba,Sarah akaanza kupiga yowe kali akimtingisha Humph kwa nguvu kama bua la mahindi. Ghafla akamuachia Humph na kushika kichwa akiyumba huku na kule.

Humph alikuwa mpya,Ben Shed na Shani waliduwaa kumuona Humph ameingi LA katika ile hali ambayo Mara nyingi huwa anashindwa kuistahimili,Humph akatumia mwanya ule kwenda kuzichomoa nafsi zile.

Sekunde chache alikuwa mbele ya Sarah,kitendo cha Sarah kutahamaki akiuacha mdomo wazi Humph akapiga ngumu nzito iliyotua kifuani barabara na kusababisha nafsi zile ziruke kwa nguvu na kuchomoka kifuani mwa Sarah.

Shed akazizuia ndani ya ngao zikawa zimefungwa. Sarah akaanguka chini na kuzirai,Humph akawahi ili aziteketeze nafsi zile lakini Shani akawahi na kumzuia.

"Usiziteketeze maana ni muhimu mno zikiwa pamoja nasi" "kivipi,Mbona sielewi?"
Humph alijibu kwa kitetemeshi

"Ni hizo pekee zinazoweza kutusaidia kumuangamiza Sor" Ben alijibu

"Na ni msaada wa pekee uliobaki kwetu" Shed alimalizia na kufunga kiganja chake na kukifungua,funguo ndogo ikaonekana katika kiganja chake

Humph akatoa macho ya mshangao "zi mikononi kwako sasa,ni muda wa kumuangamiza Sor" shed alisema na kumrushia Humph funguo iliyokuwa ikipitisha miale Fulani ya mng'ao.

"Now it's over Sor" (sasa ni mwisho Sor) Humph alijikuta akijisemea na kuiminya funguo kwa nguvu machozi yakimtiririka huku taswira ya Lisa ikimjia kichwani mwake,akastukia anatabasamu na kuibusu ile

"Nakuja mpenzi" alimalizia kwa neno lile lililobeba hisia Kali za mapenzi.

Watu wote walikuwa wakimtazama na kumuonea Huruma Humph huku kwa Mara ya kwanza Shani akibubujikwa na machozi ambayo hayakuvuka mashavu yaliganda na kufanya zaidi kupendeza kutokana kumeremeta kwa machozi Yale yaliyoganda

"Kooih! Koooh! Koooh!" Sarah alikohoa na kuwastua wote waliopo pale,Ben akamsogelea na kumuinua taratibu

"Asante Humph " ilikuwa ni kauli ya kwanza kutoka kwa Sarah kumshukuru Humph ambaye aliishia kutabasamu tu na kwenda kumkumbatia kwa nguvu.

★★★The Unite★★�?
★★★Muungano★★�?

"GPS denied,ti ti ti tiiiiiii" ulikuwa ni mlio kutoka kwenye mitambo ya kamanda One

"Shit! Ni mwezi sasa umepita hawa watu hawapatikani au wame...." Kabla kamanda one hajamalizia akasikia mtambo ukilalamika tena "new search connected" (inatafuta upya) akagonga meza kwa hasira na kuufuata mlango wa kutokea nje ulipo ghafla akastushwa na mlio mwingine "tiii! Tiiii! Tiii!" Uliomfanya asite kufungua mlango

"GPS connected,area detected tiiiiiii!!" (GPS imeunganishwa,eneo limefahamika)

Kamanda One akageuka haraka kuangalia mitambo akiwa haamini anachokisikia,mkono ukatumbukia mfukoni na kutoa kitufe kidogo na kubofya "moja,mbili,moja,mbili,eneo limetambulika. Narudia moja mbili moja mbili eneo limefahamika" akajibiwa upande wa pili naye akaagiza helikopta iandaliwe muda huo huo,akajikuta akitokwa na tabasamu huku akipiga saluti mfululizo bila kujielewa

Upande wa pili majani na miti ilianza kunyauka kwa kasi,ile miale iliyokuwa inautunza moyo ule ikaanza kuchoma uoto wa maeneo Yale yote. Humph na timu yake wakasaidiana kuinuana na kuanza kukimbia kutoka nje ya msitu ule.

Walikimbia sana kadri wawezavyo lakini hawakuweza kuishinda kasi ya moto ule,Shani alijaribu kuziba kwa barafu lakini ukali wa moto ule uliyeyusha barafu kwa dakika chache mno.

Ndipo Shed alipoamua kuwahifadhi wote ndani ya ngao na kutumia kama usafiri,moto uliteketeza msitu wote ule huku Humph na.timu yake wakiwa ndani yake.

Kwa mbali helikopta ya Kamanda One ilionekana ikisogea eneo lile na kushangaa likiwa linateketea kwa moto mkali, Kamanda One alipoangalia kifaa chake aliona alama inamuonesha kuwa Humph yumo ndani ya moto na anasogea kwa kasi ya ajabu.

"Jamani tazameni kule" Kamanda One aliwaonesha wenzake na ghafla kikatoka kitu cha duara kikiwa na watu ndani yake mpaka umbali Fulani kutoka ndani ya msitu ule.

Alikuwa ni Humph na timu yake wakiwa.ndani ya ngao ya Shed,walikuwa wamechoka kuliko kawaida,walisimama na kutazama msitu ule ulivyokuwa ukimalizika kwa kuteketea na moto.

Dakika chache baadae wote walikuwa ndani ya helikopta kubwa ya kijeshi wakiwa wanshughulikia matumbo yao.

"Ulijuaje kama tunarudi?" Humph alimuuliza kamanda one

"Nilikuwekea chipu ndogo ya kutambua mahali ulipo" Kamanda one akamuonesha Humph kifaa maalumu na kuchukua mashine moja ndogo akampitishia mwilini mwake ikatoa ukelele maeneo ya shingoni

Kamanda One akatoa kidude kidogo kilichokuwa kimenasa barabara ndani ya tisheti la Humph kisha akamuonesha jinsi kifaa kile kinavyoonesha mahali alipo na popote aendapo.

★★★★★★★★�?

Sor akiwa ametulia hekaluni akitafakari mambo kadha wa kadha akaanza kuhisi harufu ya kitu kikiungua,alipofumbua macho na kutazama alishuhudia kitabu chake kikiwa kimeshika moto na kuungua na mbaya zaidi kilikuwa kikielekea kuwa majivu.

Sor aliogopa na kuinuka,alikitazama sana kile kitabu na kugundua kuwa amefeli kwa Mara nyingine na yote ni kwasababu moyo ule umeshachukuliwa na ndiyo maana msitu wote uliwaka moto. Muunganiko wa kitabu na msitu ule ulikuwa ni mkubwa kiasi cha kusababisha hata kitabu kiteketeee kwa moto.

Sor alipiga ukunga wa ghadhabu mpaka hekalu likajibu sauti yake kwa kutetemeka. Alilaani kitendo cha yeeye kukutana na Humph katika vita zake zote ambazo bila hiyana alielemewa mno.

★★★★★★★★★★★★

Humph Ben Shani na Shed walikuwa ndani ya chumba kimoja maalumu wakijadili mambo mengi yanayowakabili kubwa likiwa ni kumuomba Sarah aongeze nguvu katika kikundi chao ambacho wao walijiita familia.

Sarah aliungana nao kwa moyo mmoja ili kuutetea mji wa Reycity na kumuangusha Sor iwe kwa damu au kwa gharama ya maisha yake.

Kumbuka:

Umoja ni nguvu katika kutenda jambo jema. Shirikisha wenzako mawazo yako ili nao wakuongezee na kuyatanua mawazo hayo kwa upana zaidi,hiyo ni njia pekee na rahisi ya kufanikiwa kwani kidole kimoja bado si kitu katika suala nzima la kumvunja chawa. Chukua hatua anza sasa

Tukiwa tunaelekea mwisho nawaalika wote wenye mioyo safi kumuunga mkono kwa kununua vipande vilivyobaki,kunichangia bando au hata kunitumia SMS tu kunisabahi. Napatikana kwa namba 0625444578 Hamphrey(Humph)
 
Macho Ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani

Sehemu ya kumi na tisa

....Ilipoishia.......

Sarah aliungana nao kwa moyo mmoja ili kuutetea mji wa Reycity na kumuangusha Sor iwe kwa damu au kwa gharama ya maisha yake

......Shuka na dude hilo......

Kamanda One akatumia fursa hiyo kutangaza katika vyombo vya habari na dola kwa ujumla kwa kulisafisha kundi lile na kuweka wazi nia yao ya kuisaidia dunia ikiwemo jiji la Reycity.

★★★The Shock★★★
★★★Mshtuko★★★

Mzee Kasai akiwa sebuleni ameketi na familia iliyobakia,yaani Sifa na mama wa Humph wanaishuhudia taarifa ile iliyorushwa moja kwa.moja katika vyombo vya habari.

Mzee yule akaduwaa kidogo na kuinuka kutoka alipoketi mpaka jirani na runinga yake akasimamisha picha ile na kuiongeza ukubwa akimtazama kijana yule aliyeongelewa kama shujaa na kiongozi wa kundi lile wa wakombozi wa jiji la Reycity.

Kwa muonekano alimfananisha na.kijana wake Humph japo asilimia hazikutimia kutokana na kitambaa alichokuwa amejifunga kijana yule (Humph) kuanzia puani kushuka chini pamoja na macho yake kutoa mwanga mweupe.

Mama wa Humph hakuelewa kinachoendelea ikambidi kumuita mumewe maana hakumuelewa elewa.

"Mume! Mume! Mume wangu! Hee jamani,we mzee Kasai! Baba Humph!"
Mama wa Humph aliita bila mafanikio akaamua kumsogelea mumewe na kumgusa bega na kumfanya astuke kiasi

"Amaa! Umefika muda gani hapa nilipo?" Mzee Kasai aliuliza lakini hakujibiwa sawa sawa na swali lake

"Una matatizo gani mume wangu?" Mama Humph aliuliza kwa upole baada ya kugundua kuwa mumewe hayuko sawa.

"Huyu kijana ananitatiza kwa jinsi anavyofanana na mwanangu Humph" mzee Kasai alieleza hisia zake bila kumficha mkewe

"Kumbe ni hilo tu mume wangu,usiwe na shaka kuhusu huyo kijana maana duniani wawili wawili mume wangu pia kama Humph angekuwa hivyo ni lazima ungefahamu mapema kwakuwa wewe ndiye mzazi wake" mama Humph alimtoa hofu mzee Kasai

"Sawa japo damu ni nzito kuliko maji,naimani siku moja nitaonana naye ana kwa ana kijana huyu hapo nitahakikisha kuwa si mwanangu Humph" mzee Kasai alijibu huku hisia za kuwa yule ni mwanae zikianza kuyeyuka taratibu

"Baba anavyompenda mwanae mpaka anamfananisha na hao jamaa" Sifa alimwambia baba yake mzee Kasai huku akiwa ameachia tabasamu la kutosha na kufanya afanane na mama yake ni kama walitolewa nakala(kopi)

★★The Perfect Combo ★★

Humph alikuwa ametulia akisoma kitabu alichoachiwa na mzee Mandevu, kilikuwa ni kitabu chenye kurasa nyingi mno kiasi cha Humph kutofikia hata robo yake yangu ameanza kukisoma enzi za uhai wa mzee Mandevu.

Alipenda kujifunza mambo kadha wa kadha kupitia kitabu kile,alifikia kurasa fulani iliyokuwa ikizungumzia muunganisho wa nguvu ambazo zinaweza kutumika Kama nguvu moja na kumshambulia adui mwenye uwezo mkubwa kuliko wao.

Alivyohakikisha ameelewa vyema alitoka na kile kitabu mpaka ilipo timu yake na kuwakuta wakiwa wanabadilishana mawazo na baadhi ya makamanda wa kikosi maalumu kilichopo pale kambini.

"Hey! Washkaji(guy's)! Um! Samahani kwa kuwaingilia kuna kitu murua hapa naomba niwashirikishe,mtupishe kidogo makamanda" Humph aliongea akiwa na tabasamu mwanana kama ilivyo kawaida yake

"Ooooh Yap! Unaweza kutueleza sasa" Ben alijibu nakuwaangalia ndugu zake wengine waliojibu kwa kichwa kuashiria wamekubaliana nae

"Uuum!nilikuwa napitia pitia hiki kitabu cha kale na kugundua kuwa tuna uwezo wa kuunganisha nguvu zetu kumshambulia adui mwenye uwezo mkubwa kwa shambulizi moja tu" Humph aliweka kituo na kuwatazama

"Kivipi? Elezea zaidi tafadhali" Shani aliuliza na wote wakatikisa vichwa kuwa aendelee kuelezea

"Aaah! ni rahisi naomba tuingie kwenye majaribio" Humph alijibu na Sarah akawa wa kwanza kuinuka na wengine wakafuata nyuma

Kamanda One alishangazwa na ugeni wa ghafla wa timu ile

"Samahani kwa ujio wetu wenye kustukiza" Humph alizungumza kwa uchangamfu

"Bila shaka japo mmenitisha kidogo,ni salama lakini?" Kamanda One alijibu akijiweka sawa kitini akiacha shughuli ya kuunganisha bunduki kubwa ya Scorpion rifle(ya kudungulia)

"Tunajaribio la hatari tunahitaji kulifanya hapa hivyo tungependa kupata ruhusa kutoka kwako na chumba maalumu ambacho kinaweza kutufaa kwa jaribio hilo"

"Nifuateni" kamanda One alijibu na kuongoza njia kutoka pale alipokuwa ameketi

Walifika chumba fulani ambacho huko hawakuwahi kuingia,walivyoingia tu milango ikajifunga na Kamanda One akabaki nje akiwatazama kupitia vioo vizito na kuwasikiliza vyema kila walichokuwa wakiongea

Kamanda One aliagiza makamanda wawili wafike kushuhudia lile jaribio huku wengine wakilishuhudia kupitia kamera zilizopandikizwa eneo lile.

Humph alisimama na kuomba wengine wamfuate nyuma wawili wakiwa kushoto na kulia wakitengeneza pembe tatu isiyo kamili.

"Wekeni mikono yenu mgongoni mwa aliye mbele yako na mnifuatishe maneno haya mkitumia nguvu zenu" Humph alielekeza huku mbele yao kabisa kukiwa na sanamu kubwa la chuma

Humph akaanza kuongea kwa sauti "anga,mwezi,jua,mawingu na nyota fungua njia" pale pale Humph akaanza kutoa mwanga mweupe,ukawa wa bluu bahari kisha ukawa mwekundu

"Waooooh!" Alisikika Kamanda One akishangaa na kustaajabishwa na kundi lile bila kujua madhara ya nguvu zile za pamoja.

Mwisho mikono ya Humph iliunda duara kubwa lililokuwa likipiga radi zenye miale ya rangi nyekundu kila mahali,kwa nguvu zake zote Humph alielekeza duara lile kwenye sanamu la chuma,radi moja kubwa ikachomoka kutoka kwenye duara lile na kutawanyisha sanamu lile la chuma,ikabaki majivu tu.

Tetemeko kubwa likaikumba kambi ile huku ving'ora vikilia ovyo kuashiria hatari katika maeneo Yale. Baada ya takribani robo saa tetemeko lile lilitulia na watu wakapata amani huku kundi la Humph likitoka ni kama hakuna jambo lililotokea muda mfupi uliopita.

Kamanda one akiwa anakutana na watu wale ghafla king'ora(alarm) ndogo ya mfukoni mwake ikamfinya ikimtaka aeleke mahali, akawataka Humph na wenzake wamfuate mbio mbio kuelekea chumba cha ulinzi

Alipofika tu akapokelewa na maelezo

"Kuna tatizo mkuu,katikati ya Jiji la Reycity mtambo wetu umehisi Bomu lenye uzito mkubwa likiwa limetegwa karibu kabisa na bahari ambapo ni kilomita chache tu kutoka eneo lile na pia ni sehemu yenye watu wengi kuliko eneo lolote jijini kiasi kwamba watu watakaokufa ikiwa Bomu litalipuka ni wengi mno"

Kamanda One alishusha pumzi nzito akionekana wazi kushiba maelezo yale,akainua kipaza sauti

"Kikosi namba moja tukutane underground (chini ya ardhi) over and out"

Alipofika chini ya ardhi akakuta kikosi kazi kikiwa tayari,ramani ikaoneshwa kwa.teknolojia safi kabisa kamanda One akatoa maelekezo ya namna ya kufanya na jinsi ya kudhibiti tukio lile kwa uharaka zaidi

Humph na timu yake walifika na kukuta kila kitu kimemalizika,wakaomba wakatoe msaada lakini Kamanda one akawatoa hofu kuwa lile sio tukio la kutumia nguvu za asili(supernatural) Bali ni kutumia akili na vifaa vya kisasa zaidi ili kulidhibiti.

Kumbuka:

Mabingwa na washindi huwa hawatengenezwi bali ni wale waliozaliwa na mioyo ya kushindana na kuzishinda hali zote za ushindani katika maisha. Wewe ni bingwa mmoja wapo mwenye moyo wa kushinda,Shindania ushindi na ushinde kwa uhakika. Chukua hatua anza sasa
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom