Simulizi: Macho ya ajabu

Simulizi: Macho ya ajabu

Sehemu ya arobaini
★★Ilipoishia★★
Kwakuwa kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka
kusikia kile ambacho kilimkuta Humph hawakusubiri
walianza na maswali ya moja kwa moja.
★★★Endelea nayo★★★
"Enheee!! tuambie mwenzetu ilikuwaje mpaka
ukapotea dume zima hivyo" aliuliza Sifa kwa utani
"mmmh! sifa maswali gani hayo kwa kaka yako"
aliingilia mama yao
"Sasa mama nisimuulize wakati Mimi nilikuwa
nimemkumbuka jamani kila muda nilikuwa peke
yangu tu eeeeh!" aliongea Sifa kwa sauti ya kudeka
"Aya kwani nd'o nimesema uanze kulia,ndiyo baba
ulikuwa wapi siku zote hizi?" mama wa Humph
aliamua naye kupigilia msumari kwa Humph
mzee Mandevu alimuangalia Humph kwa jicho lile
la usiseme chochote na Humph akawa ameelewa
hivyo akajifanya Kama mtu anayefikiria jibu japo ni
kweli maswali Yale yalimrudisha masaa machache
nyuma alipokuwa katika kisiwa cha giza.
Mzee Mandevu aliutumia mwanya ule wa Humph
kujifanya amezama katika mawazo lukuki na
kulimaliza swali kiakili
"Jamani nafikiri mnaiona hali ya mgonjwa jinsi ilivyo
maana ni dakika hizi hizi ametoka kuzinduka na
hatuwezi kufahamu ni mambo mangapi aliyoyapitia
huko alikotoka hivyo nawaombeni muwe wapole
walau mgonjwa wetu apumzishe akili ndipo
tumuhoji akiwa ametulia au nimesema vibaya
wajameni" mzee Mandevu alimaliza kwa mtindo huo
na kuwarushia swali la mtego
"Hapana mzee wangu upo sahihi kabisa itabidi
tumuache apumzike kwanza na badae tutapata
wasaa mzuri wa kuongea naye." alijibu mama wa
Humph akionesha kukubaliana na wazo la mzee
Mandevu
"Sawa sawa nadhani sasa twende sebuleni
tumuachie kamda kidogo apumue" aliongea mzee
Mandevu kwa uchangamfu
★★★★★★★★★★
Sor alihesabu kuwa ni siku ya tano mpaka muda ule
na kwa bahati mbaya zaidi kile kisiwa kiliitwa
kisiwa cha giza yote ni kwasababu mtu aliye nje ya
kisiwa kile hata awe na nguvu kiasi gani hawezi
kutazama yanayoendelea mle ndani ya kisiwa.
Sor alikuwa na furaha isiyo kifani maana aliamini
kuwa hakuna mtu anayeweza kuepuka mateso
yanayopatikana katika kisiwa kile,alienda moja kwa
moja mpaka
katika njia za upenyo alizojitengenezea yeye
mwenyewe wakati anaingia kisiwani mle bila
kutambulika na mtu yeyote.
Kama kawaida Sor alifanikiwa kuingia ndani ya
kisiwa kisha kwa kutumia nguvu alizojaaliwa
akaanza kumtafuta Humph mahali alipojifia,Alitafuta
sana lakini hakuambulia chochote.
Sor alipofika sehemu Fulani alipagawa kukuta watu
wakiwa wamekufa isipokuwa mmoja tu aliyekuwa
anaugulia maumivu ya mwishoni ili aungane na
wenzake walipokwenda
Sor alifika na kuwaangalia kwa makini watu wale
kitendo cha kumshika yule wa mwisho ambaye
hakuwa amekufa alipigwa shoti iliyosababishwa na
radi ile waliyopigwa kwani bado ilikuwa ikiendelea
kuzunguka mwilini mwao.
Alistuka sana baada ya kupigwa na ile shoti
akaanza kujiuliza ni kwanini watu wale wafe kirahisi
vile ikiwa hakuna mtu ambaye ananguvu ya
kuwasambaratisha isipokuwa yeye na watu wa
karibu sana na mfalme enzi zile japo tayari
walishapoteza maisha
lakini pia alitambua kwamba kwa siku ambazo
humph alikaa mle kisiwani ni wazi kuwa macho
Yale hayakuwa na nguvu tena kwani muhusika
hakuweza kuzimudu kutokana na majanga
yaliyomkumba ndani ya kisiwa kile.
Akiwa na mawazo Yale ya msimu yaliyokiharibu
kichwa chake ghafla kuna kit anakiwaza ilikuwa ni
karne kadhaa enzi za tawala zao.
Na papo hapo akakumbuka matukio mengi mno
yaliyo wahi kupita huko nyuma ikiwemo watu wenye
nguvu za kila aina walizojaaliwa na baadhi ya vita
walivyowahi kupambana na mwisho katika matukio
hayo yote
akili yake ikatua kwa mzee mmoja ambaye enzi
hizo alimvutia mno kwa mitindo yake ya upambanaji
na umaridadi wake lakini kubwa zaidi alikumbuka
jinsi ambavyo mzee huyo mwenye ndevu nyingi
pindi ni kijana
alipomsaidia wakati wa vita alipotaka kuuwawa kwa
kuwapiga wapinzani wake radi iliyotengeneza shoti
Fulani baada ya kuwapiga watu wale na kuwajeruhi
vibaya.
"mmmh! haiwezekani hata kidogo ina maana yule
Mandevu bado anaishi mpaka Leo hapana,ni kitu
kisichowezekana hata kidogo ngoja" alijiongelea Sor
akiwa haamini kilichotokea
Aliinama chini ya mwili mmoja usiokuwa na uhai
akafanya anavyojua kisha akaushika kifuani,matukio
yote yaliyotokea nyuma wakati Humph amejiegesha
pembeni ya jiwe akiwa hoi
Pia aliona jinsi watu wale wa ajabu walivyoanza
Kumsogelea Humph pale pale akaiona radi moja
matata ikipiga na kumshusha mtu,Sor akarudia lile
tukio na kuliwekea umakini hakika alifanania na
mpelelezi mmoja makini mno
Sor akaona haitoshi ni kama vile hakumuona vizuri
mtu yule aliyeshushwa na radi ya ajabu akaamua
kujiingiza katika tukio hilo na kukaa jirani kabisa na
radi ile ilipomshushia mtu yule japo pale awali
Humph aliona ni radi tu ya kawaida hakujua kama
ilimshusha mzee Mandevu.
Sor alibaki ametoa macho baada ya kumuona mzee
Mandevu akishushwa na radi ile kwa maringo tele
japo ilishuka kwa kasi na fujo zote,Hakuishia hapo
bakuli lake lilibaki wazi bila kufungwa(mdomo).
Alimfahamu vyema mtu yule hakuwahi kuwa na
utani hata chembe hasa anapotetea mahali
anapoamini kuwa anatenda haki,pia aliujua uwezo
wake fika kuwa kama unataka kupambana naye ni
lazima uwe umeshasaini kifo chako yote ni
kwasababu mzee Mandevu hakujua neno huruma
kwa adui yake na alia mini kuwa usipommaliza adui
yako basi atakumaliza wewe mwenyewe.
Kwa mara ya kwanza Sor anakiri kuwa vita
imemshinda baada ya kushuhudia kila kitu
kilichofanywa na mzee mpaka anapoondoka na
Humph.Sor alikaa chini akijiuliza nini hatima yake
kwani toka yeye alipoasi kwa mfalme na kuanza
kupambana naye ndipo walipokosana na mzee
Mandevu kisa tu mzee Mandevu alikuwa akimsaidia
mfalme Sangu.
Sor alibaki amelegea kwa mtindo huo tena
kilichommaliza zaidi ni pale ambapo alilikumbuka
jeshi lake lililoteketezwa na Humph kila alipojaribu
kuunda jeshi jipya.Kiukweli Sor alikuwa amepatikana
haswaa tena si kitoto ila kiutu uzima zaidi
 
Sehemu ya arobaini na moja
★★Ilipoishia★★
Sor alibaki amelegea kwa mtindo huo tena
kilichommaliza zaidi ni pale ambapo alilikumbuka
jeshi lake lililoteketezwa na Humph kila alipojaribu
kuunda jeshi jipya.Kiukweli Sor alikuwa amepatikana
haswaa tena si kitoto ila kiutu uzima zaidi
★★★Shuka nayo★★★
Sor akapiga hesabu kuwa kuliko kurudi nyuma ni
bora angalie nini cha kufanya na hicho ndicho
kitakachokuwa kitu cha mwisho katika Maisha yake
ya duniani.
Baada ya kufikia maamuzi sahihi aliinuka akiwa na
uchungu mno na wazo lake lilikuwa ni kukutana na
Humph uso kwa uso ili ajulikane nani mshindi.
"Aaaaaaaaaaaaaaaaah!!" ilikuwa ni sauti ya sor
akipiga kelele kwa hasira
★★★★★★★★★★★★
Mzee Mandevu alifika na mama wa humph pamoja
na Sifa sebuleni wakaketi kwaajili ya maongezi
mafupi.Huwezi amini mpaka muda huo
hawakumfahamu mzee Mandevu kwasababu
alijibadilisha muonekano kidogo tu nakufanya watu
wote wamuone ni mgeni machoni mwao japo Sifa
alihisi ni kama anamfananisha vile mzee huyo.
Mzee Mandevu kama kawaida yake aliwatazama
wote katika nyuso Zao kwa Zamu na kugundua
kuwa wote wanasubiri aanzishe mazungumzo mbali
na hayo yote aligundua kitu machoni mwao ilikuwa
ni uvimbe ambao ulisababishwa na kilio cha kila
siku kilichohusiana na ndugu yao Humph.
"Nafikiri wote mtakuwa mnajiuliza swali kuhusu
huyu kijana nilimpata wapi mpaka kumfikisha hapa"
akameza mate kidogo na kuwaangalia kwa zamu
tena
"Jibu ni rahisi kwanza kabisa naitwa mzee.Mandevu
na ninaishi mtaa wa Nase road(barabara ya
Nase),pia nimewahi kufika hapa Mara moja kama
mnakumbuka kuna tukio moja liliwahi kutokea hapa
nikatoa msaada mdogo nikiwa nashirikiana na
kijana wenu" Alijieleza kwa urefu mzee Mandevu
Mama wahumph na Sifa ndipo wakaikumbuka sura
ya mzee Mandevu kwa ufasaha
"Eeeh!! kweli mimi nilikuwa najiuliza hivi
nakufananisha au maana kumbukumbu zangu ni
Kama niliwahi kukuona mahali.kumbe ni wewe wa
siku ile hahahaha!!" aliongea Sifa kwa furaha
"Ni Mimi mjukuu wangu una kumbu kumbu nzuri
mno,sasa huyu kijana wenu nimemkuta katika mtaa
Fulani mbali kidogo kutoka hapa nilikuwa naelekea
matembezini ndipo niliposogea kutazama na kwa
bahati niliweza kumtambua kuwa ni kijana wa hapa
nd'o maana nimefika moja kwa moja bila kupotea"
Safari hii mzee Mandevu aliongea akiwa katika sura
ya kazi
"Mmmh!! inauma kiukweli sijui watu hawa
wanatutafuta nini sisi Mungu wangu eeeh!
tumewakosea nini lakini hii familia mpaka
wanatuandama hivi" alilalmika mama yake Humph
huku akilia
"Hapana mama usilie kwani mtoto wako
amepatikana salama sawa jitulize tafadhali"
aliongea mzee Mandevu
Ikabidi Sifa ainuke na kwenda kumbembeleza mama
yake
"Siwezi yaani siwezi baba yake mpaka sasa yupo
hospitalini hana hata fahamu na mtoto tena
wanamfuata fuata looh! nimechoka Mimi " alizidi
kunung'unika mama Humph
"Ni kweli uyasemayo lakini naamini kila kitu
kinatokea kwasababu Fulani hivyo jitahidi kukaza
moyo kwani muda si mrefu yote haya yatafikia
mwisho" alimpa matumaini mama wa Humph
"Mama jaribu kufuata maneno ya babu eeeh! ili
urudi katika ubora wako hebu angalia baba bado
anakuhitaji si hivyo tu na sisi tupo hapa kwaajili
yako sawa mama yangu jikazee" Sifa alimpoza
mama yake
"Nimewaelewa nahitaji muda wa kupumzika nitulize
akili yangu" mama wa Humph alijibu
Humph alistuka kitandani baada ya kuota ndoto
mbaya,alishuka kitandani pale akiwa na wasi wasi
mno,akatoka hivyo hivyo amenyoosha mpaka
sebuleni
Hata mzee Mandevu alistuka akiwa pale sebuleni
mpaka Sifa na mama yake.wakamstukia.
Humph alipofika sebuleni watu wote wakabaki
wanamshangaa kwani mwanzo alikuwa hajapata
hata nguvu ya kusimama na sasa anatembea
mwenyewe bila msaada wa mtu yeyote
Kabla hajaulizwa kulikoni anatoka mbio mbio namna
ile anawahi kwa kuwakata kauli
"Samahani kwa kuwakatisha maongezi
yenu,nakuomba Mara moja mzee Mandevu Nina
shida kidogo" aliomba radhi humph na kuelezea
shida yake
Mzee Mandevu bila kipingamizi aliinuka na
kumfuata Humph pale alipo kisha kwa pamoja
wakaongozana kuelekea chumbani kwa Humph
Baada ya kuingia tu mzee Mandevu alifunga mlango
vizuri na kusogea kwa Humph aliyekuwa ameketi
kitandani
"Umeona nini Humph " lilikuwa swali la kwanza
kutoka kwa mzee Mandevu
"Nimemuona sor akipiga kelele nyingi mnoo" alijibu
Humph
"Sawa sasa nimeelewa,inatakiwa upone haraka kuna
kazi ngumu ya kuifanya huko mbeleni kwahiyo
unahitaji muda mzuri wa kupumzika" Aliongea mzee
Mandevu kwa mafumbo
"Sawa haina shaka Mimi ni tayari muda wote
utakaonihitaji" Alijibu Humph
Mzee Mandevu alirudi sebuleni akiwa amejikaza
asionekane Kama ana wasi wasi na tukio linalokuja
kutokea hapo mbele.
"kuna tatizo gani mbona mnaitana wenyewe tu
hamtushirikishi"Aliiuliza mama wa Humph
"mmmmh!! ni...hamna tatizo hata kidogo alikuwa
ananionesha michubuko midogo aliyonayo"
aliongopea mzee Mandevu
"Si ameumia sana mwanangu jamani" Mama wa
Humph alianza tena kulalama,ile hali hakuipenda
hata kidogo mzee Mandevu akaomba aende na
atarudi siku nyingine kumuona mgonjwa.
"Hivi mama we unamuamini huyu mzee mpaka
unamkabidhi mwanao". Lilikuwa swali la kwanza
kutoka kwa sifa baada ya mzee Mandevu kuondoka
 
Sehemu ya arobaini na mbili
★★Ilipoishia★★
"Hivi mama we unamuamini huyu mzee mpaka
unamkabidhi mwanao". Lilikuwa swali la kwanza
kutoka kwa sifa baada ya mzee Mandevu kuondoka
★★★Endelea★★★
"asilimia 90 namuamini maana ameshafanya
makubwa katika familia hii na wewe umefikiria nini
mpaka umesema hivyo" aliuliza mama wa Humph
"Aaaah!! amna ni swali tu limenipitia ila anafaa
kuwa mmoja wa familia yetu si eti mama" alisema
Sifa kwa kudeka
"mmh! muone kazi umbea tu hapa unataka uanze
kunichota akili unadhani Mimi mtoto mwenzio,toka
huko!!" aliongea mama wa Humph
"Mama naye hutaniwi,kidogo tu umekasirika huyooo"
alijibu Sifa huku akiinuka
"Kaandae chakula cha jioni mi njaa imeanza
kulikoroga tumbo langu alaaa! utani utani,utani
mpaka kwa mama yako bwana mi nina mawazo
yangu hapa akaaaa!!" ilionyesha wazi ni jinsi gani
siku ya mama wa Humph ilivyokucha vibaya mpaka
amahamishia hasira zake kwa mtoto wake
★★★★★★★★★★★★★★
Asubuhi na mapema familia ya watu watatu yaani
Sifa,Humph na mama yao waliwasili hospitalini
kumtazama mzee Kasai ambaye mpaka muda huo
daktari alikuwa amethibitisha kuwa anaweza kuamka
muda wowote.
Mama wa Humph aliwaomba wanae watoje nje
kidogo wamuache mle wodini.Alianza kuongea na
Mme wake ambaye mpaka mud a huo ikumbukwe
kuwa alikuwa ndotoni,ndoto ambayo alipewa na
mzee Mandevu ambayo ingeisha endapo kazi yao
ya kumuangamiza Sor ingetimia.
"Baba watoto tambua kuwa mkeo nina hali ngumu
kuliko kawaida,mzigo ulioniachia ni mkubwa zaidi
tofauti na uwezo nilionao" akatulia kidogo kufanya
kimya kipite
"Huyu mwanao Humph ni juzi tu hapa kaleta
majanga,mwenzio nimehangaika lakini nashukuru
Mungu amerejea tena,Nakuombea sana Mme wangu
urudie hali yako ya zamani ili ukamilishe ndoto za
watoto wako.Wanakusubiri kwa hamu mno uamke"
akahitimisha hayo huku akiruhusu machozi
yateremke kisha akayafuta kwa kitambaa laini
alichokuwa nacho mkononi
Kwa kutumia mkono wake ule wenye Pete ya ndoa
akamshika Mme wake kuonyesha bado ana
mapenzi naye chungu nzima,Cha ajabu zaidi ni
kwamba baada ya kumshika mkono mzee Kasai
naye aliushikilia barabara
Si kwamba mzee Kasai alitambuà kile
kinschoendelea ila katika ndoto mzee Kasai alikuwa
anaota yupo sehemu moja yenye maporomoko ya
maji wakiwa wanayatazama na mke wake na kwa
muda huo huo wanakutanisha mikono na kushikana.
Mama wa Humph alitabasamu na kuona sasa
mumewe anaelekea kupona kabisa siku za
usoni,alitoka na furaha mno mpaka watoto wake
wakapatwa na wasi wasi wakihisi kuna jambo
ambalo.linamtatiza mama yao tena kama si
kuchanganyikiwa basi ameanza kuwehuka.kutokana
na mambo yanayomsibu yote hayo waliyafikiria
baada ya kuuliza na kuambulia ukimya badala ya
majibu.
Familia ya mzee Kasai ilifika moja kwa moja katika
vituo mbalimbali vya polisi na kufutwa kwa
utafutwaji wa kijana Humph pia walifika vituo vya
kurushia matangazo na kusitisha zoezi la kutangaza
upotevu wa kijana huyo ambaye amekwisha
patikana.
★★★★★★★★★
Mzee Mandevu hakurudi mahali anapopatumia
kujihifadhi Mara kwa Mara badala yake alienda
katika jumba moja la makumbusho waswahili
wanaita majumba ya kale na kule kwetu tunasema
Museum
Lengo lake kubwa alitaka kuutatua mgogoro uliopo
kichwani mwake,alikuwa akijiuliza sana jinsi ya
kummaliza sor maana kama akichelewa basi
atawahiwa yeye.
Na kulingana na ile sauti ya Sor aliyoisikia ikipiga
kelele ilidhihirisha wazi kuwa haikuwa ya kheri hata
kidogo na isitoshe alimfahamu vyema Sor akiwa
amepandwa na hasira.
Mzee Mandevu aliipata historia ya zamani zile
walizoishi wao,kipindi wanamsaidia mfalme
sangu,aligundua kitu kingine kipya ambacho
kilikuwa ni kama fumbo kwake lililokijaza kichwa
chake sawa sawa.
Aliumiza kichwa nini maana ya kile kidude
alichokiona lakini alishindwa hii ilikuwa ni
kwasababu hakuwa anafahamu maandishi
yaliyoandikwa pale kwani hayakufanana na
maandishi waliyokuwa wakiyaandika wao enzi zile.
Baada ya mzee Mandevu kushindwa kulifumbua
fumbo lile anapata wazo lingine wazo ambalo
halmashauri yake ya kichwa inakubaliana
nalo,alihitaji kuondoka na ile karatasi.
Angewezaje ilihali mahali pale hakuruhusiwa mtu
awaye yote kuondoka na chochote,kikawa ni
kikwazo kingine kilichohitaji ufumbuzi wa kina na
ikibidi aambatanishe na maelezo binafsi.
Mzee Mandevu alichoka akaona kabisa jinsi
ambavyo Sor anammaliza kiakili na.kweli alikiri
kuwa Sor ni mjuzi ijapokuwa ni mwanamke lakini
vitu vyake vilienda kisomi zaidi ya vile alivyotarajia.
mzee Mandevu alitulia pale kwa muda akitafakari
kipi cha kufanya na mara hiyo hiyo akakumbuka
kuwa yeye si binadamu wa kawaida yeye ni mtu
aishie milele(immortal).
Akatabasamu kabla ya kuipeleka mikono
yake.katika kitabu kile na ksratasi ikatii kumezwa
na.mikono yake bila mtu yoyote kubaini mchezo ule
mchafu aliokuwa.akiucheza.bila mwamuzi (refa)
Sasa mzee Mandevu aliitimiza azma yake
ila.alipotaka kuinuka ili akakabidhi kitabu kile
macho yake yalitua sehemu ile ya kukabidhisha
vitabu ambapo moja kwa moja alishuhudia
mashine.zikitumika kukagua vitabu vile kama viko
salama ama vimechakachuliwa.
Mzee wa watu alijibwaga katika kiti kama mtu
aliyechoshwa na safari ndefu mno,ikumbukwe kuwa
mzee.huyu ni mmoja kati ya wale watu wenye
nguvu za ajabu yaani waishio milele lakini hakuona
haja ya kutumia nguvu zake vibaya kwani huenda
zingesababisha madhara makubwa kwa watu wasio
na hatia hata kidogo.
 
Sehemu ya arobaini na tatu
★★Ilipoishia★★
Mzee wa watu alijibwaga katika kiti kama mtu
aliyechoshwa na safari ndefu mno,ikumbukwe kuwa
mzee.huyu ni mmoja kati ya wale watu wenye
nguvu za ajabu yaani waishio milele lakini hakuona
haja ya kutumia nguvu zake vibaya kwani huenda
zingesababisha madhara makubwa kwa watu wasio
na hatia hata kidogo.
★★★Teremka nayoo★★★
Mzee Mandevu alikosa uamuzi sahihi akaamua
akae pale pale mezani akiendelea kusoma mambo
mbalimbali katika kitabu kile kinachoelezea mambo
mengi yaliyotokea enzi zao.
★★★★★★★★★★
Humph na familia yake kwa ujumla walikuwa
walirudi nyumbani lakini wakiwa njiani Sifa
anakumbushia tukio la siku mbili zilizopita kuwa
lisa alikuja nyumbani kwao kuulizia kama Humph
amepatikana na anautofauti mkubwa kati ya kipindi
cha mwanzo na wakati ule
Lisa alikuwa amepungua kwa kiasi kikubwa
(mawazo) yote kwa yote sababu inaonekana ni
kukosekana kwa Humph ndani ya siku hizo
chache,Humph anabadili mwelekeo pale pale baada
ya kuzisikia zile habari anashuka garini na kuiacha
familia yake ikimshangaa ananyoosha moja kwa
moja nyumbani kwa kina sifa.
Alipofika cha kwanza anamuomba mlinzi amwite
Lisa ila asimwambie lolote kumhusu yeye na mlinzi
anakubaliana naye japo hata mlinzi alikuwa na
shauku ya kujua ni kipi ambacho kilimtokea Humph
mpaka akapotea katika mazingira ya kutatanisha.
Lisa aligoma kabisa kutoka nje na muda wote
alikuwa ameikumbatia picha ambayo iliwahi
kuchorwa na Humph,alikuwa amekonda haswaa na
ni kwa muda mfupi tu,nafikiri ilikuwa ni halali yake
kuwa vile kwasababu aliwapenda watu wawili kwa
nyakati tofauti ambao wote hao wawili walikuwa ni
mtu mmoja ambaye ni Humph na kilichomuumiza
zaidi ni pale ambapo wote walitoweka katika kipindi
alichowahitaji kuliko kawaida.
Ule mkufu wa Humph wenye msalaba ulikuwa
shingoni mwa Lisa ukining'inia tu.Wazazi wa lisa
walipata kipindi kigumu kwani licha ya mtoto wao
kuwa mwenye mawazo muda wote na asiyeshaurika
pia alikuwa ni mtoto wa pekee kwao.
Mlinzi hakuona haja ya kuendelea kumbembeleza
mtoto wa bosi wake alirudisha majibu kwa Humph
jinsi hali halisi inavyokwenda mle ndani
Wakati Humph akielekea ndani kumuona Lisa mlinzi
alimsimamisha na kumuuliza
"Samahani bwana mdogo nikuulize kitu" alisema
mlinzi
"uliza tu kuwa huru" alijibu Humph bila hofu
Mlinzi akamsogelea Humph na kunong'ona(kuongea
kwa sauti ya chini)
"Huwa mnawapa nini hawa wasichana eeh! mfano
huyu mda wote anakuwaza hata kula hataki,nielekez
e na Mimi niwakamate"
Nusura Humph acheke akajikaza ili asionekane
amemdharau mkubwa wake
"Sio uchawi kaka wala nini jitahidi kumjali kwa kila
kitu na kujenga ukaribu kila anapokuwa na uhitaji na
wewe utayaona mafanikio" baada ya kusema Yale
Humph akaendelea na safari ya kuelekea ndani
Humph alimkuta Lisa akiwa katika hali ile ile ya
upweke,bila kuuliza alianza kumfuata pale alipo ila
cha ajabu zaidi Lisa hakuji hangaisha kutazama ni
nani aliyeingia mle ndani
Humph aliligundua hilo na pia aliiona huzuni ile
aliyonayo Lisa ndipo akatambua kuwa Lisa
amemuweka moyoni japo hakuwa na uhakika kuwa
ni upande upi aliopo Lisa kati ya urafiki au mapenzi
yanayomsumbua kama unavyojua moyo wa mtu ni
kiza kinene na si rahisi kutambua kilichomo ndani
yake.
Humph alikosa uamuzi wa moja kwa moja nini
ambacho alihitajika kufanya wakati huo,akajipa
moyo na kumsogelea Lisa kisha akamkumbatia kwa
nyuma na kukilaza kichwa chake mabegani kwa
Lisa.
Lisa alistuka kwa kutoa sauti moja tu "Humph" na
Humph akaitika pale pale bila kusita "nipo hapa
rafiki yangu kipenzi"
Lisa akajiinua haraka na kugeuka kisha
akamkumbatia Humph kwa furaha.
"Siamini kama ni wewe,siamini kabisa au ni ndoto
hii" alisema Lisa akiwa anatokwa na machozi ya
furaha
"amini ni mimi Humph wako na wala si ndoto kama
unavyodhani"
★★★★★★★★★★
Mzee Mandevu alipochoshwa na baadhi ya
maandishi na picha alizozielewa aliona hakuna jinsi
kwa kutumia utaalamu wake wa enzi zile mpaka
kufanikiwa kuunda macho ya ajabu anatengeneza
karatasi tena katika kitabu kile lakini na ile karatasi
ya awali inabakia mikononi mwake.
Mzee Mandevu anafika mahali pa kukabidhi kitabu
chake na kuanza kuondoka kabla hajaruhusiwa,an
apofika mlangoni king'ora cha hatari kinaanza kulia.
Walinzi wanamzunguka mzee Mandevu na kabla
hawajafanya lolote mzee yule anamtazama dada
yule anayepokea vitabu vya pale na kufanikiwa
kumtupia kitu kinachomlainisha na kuwaamuru Mara
moja walinzi wale wamuachie ili arudie ukaguzi.
Baada ukaguzi wa awamu ya pili kitabu
kinaonekana kipo salama ndipo mzee Mandevu
akaruhusiwa kutoka,mzee Mandevu alishusha pumzi
ndefu ni kama amefanikiwa kufika katika kilele cha
mlima Kilimanjaro.
"Sikuwa na haja ya kuwadhuru ila mngeniletea fujo
Leo ahaaa! sijui nafikiri familia zenu wangekuwa
mashahidi kwa lile ambalo lingewatokea" alikuwa
akijiongelea mzee Mandevu wakati anatoka katika
jumba la kale(makumbusho).
Gia ya kwanza ni kwa Humph akafafanue hili jambo
kabla ya kesho maana roho haikai kabisa,Huyu
mtoto anaweza kukuua muda wowote akijisikia,yaan
i toka alipoacha umalkia basi amekuwa na roho
chafu kuliko kawaida.
Mzee Mandevu alizidi kukata mitaa na mwisho
akachoka kutembea,akafuata kichochoro kilichopo
jirani na maeneo Yale alipoona pako salama
akapotea mithili ya kimbunga Fulani kidogo.
 
Sehemu ya arobaini na nne
★★Ilipoishia★★
Mzee Mandevu alizidi kukata mitaa na mwisho
akachoka kutembea,akafuata kichochoro kilichopo
jirani na maeneo Yale alipoona pako salama
akapotea mithili ya kimbunga Fulani kidogo.
★★★Shuka nayo★★★
Mzee Mandevu alifanikiwa kufika katika nyumba ya
kina Humph kwa bahati nzuri alikuta dirisha liko
wazi akaingilia hapo kwa mtindo ule ule wa
kimbunga.
Alichukua jukumu lile la kupitia dirishani kwasababu
alitambua wazi kuwa haikuwa rahisi kwa familia ya
Humph kumruhusu aingie chumbani humo ikiwa
mmilki wa chumba hakuwepo maeneo hayo
Alijitupa kitandani hapo akiwa anajaribu kupitisha
mawazo kadhaa kichwani mwake ili kupoteza muda
wakati Humph anarejea kutoka matembezini(kwa
lisa)
★★★★★★★★★★
Humph alimuachia Lisa baada ya kukumbatiana kwa
muda,macho yake yalitua shingoni mwa Lisa
ambapo kulipendezeshwa na mkufu uliomkaa vizuri
uliomfanya Humph astuke na bila kutarajia akauliza
"Huo mkufu ni wangu,we uliutoa wapi?"
"Mmmmh!! huu mkufu ni wako,acha masihara
bwana" Lisa alijibu akijua ni utani tu wa Humph
"Lisa ni mkufu wangu huo niliupoteza kipindi kirefu
mno nilipokuwa...." akashindwa kumalizia baada ya
kukumbuka kuwa tayari amejinasisha katika mtego
aliokuwa akiukwepa kwa gharama kubwa mno
"nini? aaah! usinifanye niamini hili,yaani unasema au
ina maana,hapana haiingii akilini hata kidogo"
alisema Lisa akiwa ni kama mtu aliyechanganyik
iwa.
"Lisa tulia kwanza Niku..." Humph hakumalizia Lisa
akadakia
"Nasema haiwezekani hata kidogo ina maana Yule
ambaye kila siku anaelezewa kwenye
magazeti,runninga na kwa kila mtu wakimpamba na
kumsifu kwa majina mazuri ndiyo wewe,hapana
sitaki kuamini hili" Alisema Lisa akiwa anajishika
kichwa
"Lisa nisikilize eeeh!! sijasema kuwa ni Mimi Ila...."
hakumalizia Humph akakumbana na kauli nyingine
ya Lisa
"Ila nini Humph utanidanganya nini hapo,Mimi sio
mtoto mdogo wa kuniletea pipi nikubali kiurahisi
kile unachosema sawa" akatulia kidogo ili yale
maneno yamuingie Humph kisawa sawa
"Nadhani sasa nimekuelewa na hata matukio
yalivyokuwa kwa mfano siku ile unaniokoa sauti
yako haikuwa ngeni kwangu pia kule ilipopigwa
risasi haukuwa na mwendo wa kawaida ukaniokoa
na sasa huu mkufu wako,aaaah! vituko vyote vile
kumbe ni wewe hata mateso ya moyo niliyoyapata
yote ni kwasababu yako,haiwezekani." alisema Lisa
maneno hayo kwa uchungu kwani hata bomba ya
machozi ilikuwa tayari imeanza kufanya kazi yake.
"Tafadhali lisa nipe nafasi nizungumze,sikufanya
yote yale kwa kupenda,nilihitaji kukulinda kwa
gharama yoyote ile nakupe......"
"Weeee!! ishia hapo hapo tena usinivuruge
nakwambia ungekuwa unaujua upendo ungenifanyia
hivyo wewe tena usitake kunichefua sasa hivi eti
nakupenda,samahani nakuomba utoke kwa usalama
wako" aling'aka Lisa kwa hasira
"Ina maana Lisa yote haya ninayoyasema kwako ni
bure,basi nisamehe nimakosa nimeyatenda na
ninaahidi.." Humph alianza kupiga magoti
"Thubutu!! hunifahamu wewe aya inuka hapo na
utoke mbele yangu kabla sijakuitia mlinzi" alisema
Lisa kwa jazba
Humph hakuujua moto wa Lisa na mpaka pale
tayari hakuwa na jipya zaidi ya kujikusanya taratibu
na kuanza kuondoka huku akimuacha Lisa akiwa
hataki hata kuiona sura yake kutokana na matendo
aliyofanyiwa na Humph
Humph alijuta kwa kumficha Lisa ule ukweli jinsi
alivyo japo hakuwa anapenda kile kitendo cha
kumficha Lisa pia alikuwa akimpenda mno na ndiyo
maana alijitahidi kumlinda vile awezavyo na kila
ilipobidi kutoa msaada wake alifanya bila kinyongo.
Humph alitoka katika nyumba ya kina Lisa akiwa na
mawazo tele mpaka akampita mlinzi bila kumuaga
kama ilivyozoeleka.
Lisa akiwa amebaki ndani alikimbilia chumbani
mwake na kujifungia kwa ndani kisha akajitupa
kitandani kwake na kilio cha kwikwi kikamtawala
kila alipozidi kumfikilia Humph na kulinganisha na
yale aliyokuwa akiyasema.
Lisa alilia sana mpaka usingizi ukampitia bila kujua
ni saa ngapi alipolala.
★★★★★★★★★★★
Humph alifika kwao akiwa na mawazo mengi pia
furaha yake ilikuwa imetoweka ghafla na kubaki ni
kama mtoto aliyefiwa wazazi kwa mkupuo(pamoja)
na na kubaki bila msaada.
Sifa na mama wa Humph walipatwa na mshangao
juu ya hali ya Humph ilivyobadilika ghafla na
walipohitaji kumjulia hali hakuwajibu lolote zaidi ya
kuendelea na safari kuelekea chumbani kwake.
Sifa na mama yake walibaki na sintofahamu hali ya
viulizo na maswali yasiyo na majibu yaliupamba
vyema ubongo wao na kuwafanya wabaki kujisemea
kila mtu lake ilimradi tu wajaribu kuotea kile
kinachomsibu Humph.
Humph alifika mpaka chumbani kwake na moja kwa
Moja akakifuata kitanda na kupanda bila kutambua
kuwa mzee Mandevu alikuwa pale muda mrefu
uliopita na alikuwa akimngoja yeye tu ili apate
ufumbuzi wa janga lake lakini kwa bahati mbaya
zaid mtahiniwa akarudi akiwa na hali mbaya
isiyotegemeka.
Katika hali ya kuduwaza Humph hakumuona mzee
Mandevu yeye alichojali ni mawazo yake kuhusu
Lisa na alifikiri labda jambo lile lingemfanya Lisa
amkubalie Kwakuwa alikuwa ameshaufahamu ukweli
halisi kuhusu humph.
 
Sehemu ya arobaini na tano
★★Ilipoishia★★
Katika hali ya kuduwaza Humph hakumuona mzee
Mandevu yeye alichojali ni mawazo yake kuhusu
Lisa na alifikiri labda jambo lile lingemfanya Lisa
amkubalie Kwakuwa alikuwa ameshaufahamu ukweli
halisi kuhusu humph.
★★★Shuka nayo★★★
Badala yake Lisa alicharuka na kuanza kumshutumu
Humph kuwa ametenda makosa makubwa mno.
Sauti ya Lisa ilizidi kujirudia kichwani mwa Humph
na kumfanya aanze kugalagala kutoka na na
maumivu anayohisi moyoni mwake.
Mzee Mandevu hakujaribu kumsemesha Humph
maana tukio lote lilivyotokea tayari lilishanasa kwa
mzee Mandevu na kumfanya azidi kupagawa kwani
naye alihitaji msaada wa kijana huyo lakini kwa
tukio lililotokea angewezaje kumuuliza chochote
ama kumpatia kile anachokiita yeye kazi.
Humph aligalagala sana hadi pale mzee Mandevu
alipoamua kuchukua jukumu la kumzimisha ili
kuituliza ile ghasia iliyokuwa inamsumbua kichwani
mwake,Baada ya kufanya vile akaanza kutafakari
njia sahihi ya kumtuliza kijana Humph ili kazi yao
waliyoianza nayo isilale maana kama wao
watachelewa.kumdhibiti sor basi yeye angewadhibiti
mapema.
Mawazo mengi aliyapitia mzee Mandevu na hapo
ndipo alipogundua kuwa huo ni wakati mgumu
kuliko nyakati zote alizowahi kupitia.wakati huo huo
mzee Mandevu akaibuka na wazo aliloliita "mwisho
wa matatizo"
Wazo hilo lilikuwa ni linalohitaji ujasiri fulani
kulitekeleza,Mzee huyo aliyekula chumvi nyingi
kupitiliza alimsogelea Humph na kuiweka mikono
yake kkatika.kichwa cha Humph na kusema maneno
kadhaa aliyohisi ni sahihi kwake kisha akaitoa
mikono yake kichwani hapo na kusubiri matokeo
huku akijinadi kuwa "kuwa immortal (wanaoishi
milele) si jambo la mchezo,hakuna kinachoshindika
na mbele yao".
Ilipita saa nzima ndipo Humph akaamka,mzee
mandevu hakushangaa kile kitendo zaidi ya
kutabasamu tu huku akimuangalia Humph usoni.
"Inaonekana umefika muda mrefu sana" alihoji
Humph akiwa anajinyoosha
"Ni muda mchache tu wala usihofu kijana wangu"
alijibu mzee Mandevu bila hofu
"Sawa,nakuja muda si mrefu ngoja nifike sebuleni
kwanza nina maagizo yao"
★★Kilichotokea★★
Mzee Mandevu alipoweka mikono kichwani kwa
Humph alipandikiza roho nyingine ya chuki na ujasiri
wa hali ya juu.kiasi kwamba hata kama alikuwa na
mapenzi kiasi gani kwa Lisa basi angebakiwa na
asilimia chache mno za kumpenda.
Mzee Mandevu hakufanya vile kwa kupenda la!
isipokuwa hali ya Humph ingeleta madhara katika
kuzitumia nguvu zake na angeshindwa kuzidhibiti
vilivyo.
Kama alivyotarajia mzee Mandevu ndicho
kilichotokea kwani baada ya Humph kuamka
matendo aliyokuwa akiyafanya ni kama vile alikuwa
ni roboti linaloendeshwa na kiongozi(rimoti).
Humph alienda mpaka sebuleni na kumkuta mama
yake akiwa anaongea na Sifa walipomuona tu
wakakaa kimya na kumuangalia Humph
Humph hakuonesha hata dalili ya kustuka vile
alivyoangaliwa yote ni kutokana na roho yake mpya
aliyopandikizwa,Alipofika akaanza kutoa maagizo
"Lisa akifika hapa mwambieni sipo" bila kusubiri
hata majibu akageuza na kuondoka zake,
Sifa na mama yake wakabaki wametumbua macho
kwani hawakuelewa tatizo ni nini ama chanzo cha
Humph kukataa kuonana na Lisa.
Wao walimtambua Lisa kama binti asiye na makuu
hata chembe iweje siku hiyo Humph aanze
kumchukia,hilo lilibaki ni fumbo vichwani mwao
lililohitaji ufumbuzi wa Lisa au Humph mwenyewe.
★★★A Precious Portal★★★
★★Mlango wa Thamani★★★
mzee Mandevu alizitoa zile karatasi na kumkabidhi
Humph ili amsomee Yale maelezo yaliyoandikwa.m
le ndani
Bila kuchelewa Humph alitupia jicho lake.pale
kwenye karatasi na ubongo wake ukafanya kazi
chapuchap ya kuchambua kilichoonekana kisha
ukarudisha taarifa iliyoanza kusemwa na Humph
bila kusitasita
"Baada ya kutoweka kwa himaya yenye nguvu ya
mfalme sangu,baadhi ya vitu vya thamani kutoka
katika falme hiyo vilihamishwa na vingine viliwekwa
sehemu nyeti sana ambazo hazifikiwi na watu wa
kawaida na pia katika vitu viliyofichwa kimojawapo
ni geti au mlango unaotenganisha dunia na
ulimwengu mwingine uliosheheni watu wanaojiita wa
milele gani(immortals).Na inasadikika kuwa nguvu
alizokuwa nazo.mfalme Sangu ndiyo hizo
zilizomfanya aingie katika ulimwengu huo mpya
uliojaa watu mashuhuri wenye nguvu na vipaji tofauti
tofauti japo bado mfalme sangu anahisiwa kuwa
anaishi kama mtawala wa eneo hilo(ulimwengu wa
nje)" alimaliza kusoma ukurasa mmoja wa karatasi
hiyo iliyo na picha ya vitu vya thamani vilivyotajwa
na Humph kutoka katika ukurasa wa karatasi ile.
"Bwana mdogo hicho ndicho haswaa nilichokuwa
nakitafuta kwa miaka mingi ili nimrudishe huyo
malkia Sor katika dunia yake na iliposhindikana
ndipo ikabidi itumike njia ya kumpunguzia miaka ya
kukaa huku katika ulimwengu wenu tukiwa
tunaamini kuwa angeweza kuleta madhara makubwa
mno kwa viumbe hawa wasio na nguvu ya kujitetea
lakini cha kustaajabisha ni pale ambapo "macho ya
ajabu" niliyoyatengeneza mimi na kikosi changu
yalionekana bado yapo huku na endapo Sor
angefanikiwa kuyapata basi angeufanya huu
ulimwengu kuwa milki yake milele na ndiyo maana
nikaja kumzuia" Mzee Mandevu alidadafua kile
kilichotokea hapo awali na kilichomfanya awe pale.
Humph hakuelewa kipi cha kushika na kipi cha
kuacha na mwisho akauliza swali ambalo
lilimrudisha mzee Mandevu kwenye mada
"Sasa tufanyaje hapo maana Mimi sielewi mwanzo
wala.mwisho nipo nipo tu."
"Mmmh! umeuliza swali la msingi sana,kwasababu
unahitaji amani katika Maisha yako itabidi
tumuondoe Sor na ili kumuondoa tunahitaji kupata
huo mlango utakaosaidia kumrudisha Sor katika
ulimwengu wake akapatiwe adhabu" Alieleza mzee.
Mandevu
"Mimi Niko tayari kwaajili ya usalama wangu na wa
watu wengine ila je tunaupataje huo mlango?"
aliuliza Humph
"Aaaaah!! labda! mmmh!,hebu geuza ukurasa wa
pili huenda tukapata lolote la maana" alijibu
mzee.Mandevu akiwa hana uhakika
 
Sehemu ya arobaini na sita
★★Ilipoishia★★
"Aaaaah!! labda! mmmh!,hebu geuza ukurasa wa
pili huenda tukapata lolote la maana" alijibu
mzee.Mandevu akiwa hana uhakika
★★★Teremka nayo★★★
Humph hakutegea akaigeuza ile karatasi na.kuanza
kuisoma kwa sauti
"Pamoja na vitu hivyo vya thamani kufichwa sehemu
zisizoingilika kiurahisi lakini baadhi ya vitu hivyo
havikuchukua muda vilitoweka huku ikisemekana
kuwa vilipelekwa katika ulimwengu ule wa ajabu na
wengine walidai ni wizi ulifanyika,Kitu pekee
kilichosalimika ni mlango wa unaotenganisha dunia
na ulimwengu huo ambapo inakadiriwa kuwa
mlango huo unapatikana katika mji wa zamani (Old
city) ambao unapatikana katika bahari ya Siri (hii ni
bahari iliyopo jirani kabisa na mji wa Reycity,mji
anaoishi Humph) na mlango huo unalindwa vikali na
watu wasiofahamika." Humph akaweka kituo na
kumuangalia mzee Mandevu ambaye aliishia kukuna
ndevu zake bila kutoa jibu
★★★★★★★★★
Lisa alijifikiria Mara mbili juu ya.kile alichomfanyia
Humph akaona amekosea kwani dhumuni la Humph
halikuwa baya kwake bali kumuweka.katika hali ya
usalama ili asidhurike na yale majanga ya kila
kukicha.
Lisa alikosa njia sahihi ya kufanya maamuzi kwani
kama ni kulia ameshalia mno isitoshe bado alikuwa
na mapenzi mazito kwa Humph bila kujali vile
alivyo sirika yake.
Hakutazama athari zitakazojitokeza hapo mbele
yeye alichojali ni mapenzi yake.Alianza kujipanga
namna ya kumuomba Humph msamaha mpaka
amkubalie,akaanza kazi ya kumeza maneno ili
kujijengea ujasiri wa kuzungumza mbele ya Humph
bila kutetereka
Hakika alikuwa na kazi mno ya kufanya kitu
ambacho kamwe hajawahi kukifanya na hapa ndipo
utaamini kuwa mapenzi ni uchizi kwani Lisa alidiriki
hata kusimama mbele ya kioo na.kuanza kuongea
nacho akichukulia mfano kuwa yupo na Humph
kiukweli ilikuwa ni vichekesho.
Baada ya kuona kuwa anauwezo wa kujimudu mbele
ya Humph akaanza kutafuta vazi nzuri
litakalomfanya avutie machoni mwa Humph endapo
wakionana,alijitahidi kuchagua na mwisho
akafanikiwa kulipata gauni moja bomba sana
lililomfanya azidi kuonekana mrembo zaidi ya
warembo wa dunia yaani kiufupi jinsi
alivyotokelezea si wa dunia hii mpaka akawa
anajisemea yeessss!!(ndiyoo) hapa nimekolea
pilipili kama saamaki mbichi.
Safari ilianza ya kuelekea.kwa Humph tena kipindi
hiki mtoto wa watu alivuta mkoko(gari) mmoja
adimu sana kama ilivyo hadhi yao akakanyaga
mafuta akitaka kuwahi kule kwa ampendae.
★★★★&★&★★★★
Mzee Mandevu alikuwa amechemka damu haswaa
baada ya kuisikia ile habari ya kupatikana kwa
mlango utakaomsaidia yeye kumtoa Sor katika
ulimwengu ule mpaka katika ulimwengu wao.
"Mimi nina wazo kwanini hii kazi tusiifanye
kesho,tujipange Leo kwanza" Humph alivunja
ukimya uliokuwepo kwa muda mrefu
"Hapana,tunatakiwa kuianza Leo hii kazi kwani hivi
ninavyokwambia hatuko peke yetu." aliongea mzee
mandevu,mzee anayefahamu vitu vingi mno
"unanitisha,mzee kwanini unasema hivyo?. aliuliza
Humph kwa uoga
"Sina maana mbaya ila ninachokikumbuka ni kuwa
jamii ya watu Kama sisi huwa tunahisia mno juu ya
kitu chochote kile kinachotaka kufanyika mahali"
Aliijibu kauli ya Humph
"Eeeh! kazi ip,sasa tunaanzaje?" Humph alionekana
kuchoshwa
"Wala usiwaze ni rahisi kabisa Mimi nitaelekea huko
na wewe utabaki nje kama mlinzi kwaajili yakutoa
msaada utakapohitajika sawa" alisema
mzee.Mandevu
"Hapana sikubaliani na.wewe kwanini uende wewe
na si mimi?" aliuliza Humph
"kwasababu wewe bado hauna nguvu ya kutosha
kujilinda na kukabili watu wenye nguvu zaidi yako"
Aljibu.kiufasaha mzee Mandevu
"Sawa haina shida" alijibu kiunyonge Humph
"Nimebadili mawazo kwakuwa wewe ni kijana na
damu yako bado inachemka.utaanza kwenda alafu
mimi nitabaki kutoa msaada wa dharura" Aliongea
mzee Mandevu
"Hapo sasa ndipo nilipopataka" alichekelea Humph
uamuzi alioutoa.mze mandevu
Huwezi amini.kile alichokuwa anakifanya Humph
kuwa kilitokana na.msukumo wa ile roho ya ujasiri
aliyopandikizwa kwa muda.
★★%★★★★★★★★★★
Lisa alifika katika nyumba ya kina Humph na
kukaribishwa ndani,si mama yake Humph wala.Sifa
walioshangazwa na mtoko wa aina yake aliokuwa
ameuvaa Lisa na kuonekana mrembo kuliko siku
zote.
Mama yake Humph alimsifu mwanae kwa kujua
kuchagua kama ilivyokuwa yeye enzi zake
alipompata kijana wa.mwendokasi ambaye kwa
sasa ni.mzee Kasai ambaye pamoja na umri
kukimbia lakini hakuwa amechoka kiasi cha kuitwa
mzee.
Lisa alikumbana na maswali kadhaa kuhusiana na
Humph yaliyozidi kumlegeza na kumfanya ajute
kumfokea Humph
"Lisa mwanangu leo umechomoka kweli mpaka
nimetamani ungekuwa mkwe wangu" mama Humph
alianza maneno ya uchokozi ili apate tiketi ya kujua
kisa. cha Humph kukasirika
"Haaaa! kumbe hatana wewe mama
umeona,ingependeza kweli familia yetu kuwa na wifi
kama Huyu" Sifa naye alizidi kupambia
"Asanteni kwa pongezi zenu" Lisa alijibu huku
akiinamia
"Alafu kaka Humph ametoka kidogo na muda Fulani
aliporudi alikuwa kanuna huyo ni kama atapasuka
sijui kilimkera nini kule alipotoka" alianza kueleza
Sifa ili kumchimba Lisa
 
Sehemu ya arobaini na saba
★★Ilipoishia★★
"Alafu kaka Humph ametoka kidogo na muda Fulani
aliporudi alikuwa kanuna huyo ni kama atapasuka
sijui kilimkera nini kule alipotoka" alianza kueleza
Sifa ili kumchimba Lisa
★★★Shuka nayo★★★
"We Sifa! hebu acha bhana ni nini hivyo
unavyoongea" aliingilia kati mama wa Humph
kumtetea Lisa aliyeonesha ameanza kuelemewa na
mzigo wa maneno
"Eee! mwanangu Humph ametoka kidogo nafikiri
kuna mahali ameelekea kwahiyo usijali sana ila kwa
dalili alizonazo nahisi kuna kitu kinamsumbua"
mama Humph alisema
"Hata Mimi nilimuona akiwa hivyo hivyo na
sijabahatika kufahamu kinachomsumbua hasa."
Alijibu Lisa akiwa anaongopea
"Mmmh!! atakuwa na yake tu yanayomsibu si
unamjua kaka yangu alivyomsiri kama baba yake
akitatua jambo nd'o analiweka wazi" alisema Lisa .
"sawa ngoja tuone kitakachotokea,mi nipo ndani
lisa,karibu sana" alijibu mama Humph na kuaga
akielekea chumbani kwake ili watoto wabaki na
Uhuru wa kuongea mambo yao.
★★★★★★★★★★★★
Sor alishaufahu mpango mzima wa kupata mlango
umaoyenganisha ulimwengu aliotoka na huo
anaoishi kwa muda huo,alishindwa afanye nini
maana aliyeachiwa lindo ni mzee Mandevu na
humph ndiye anayetakiwa kwenda kutafuta mlango
huo.
Alikuwa akiiumiza kichwa jinsi ya kupata mlango ule
kabla mzee Mandevu hajaufikia lakini yote
aliyowaZa aliyaona hayana mashiko hata
kidogo,lakini wazo lake moja akahisi lina maana
sana
Sor alikusudia kutangulia mle katika mji wa zamani
kama unavyoitwa ili akapambane na humph ili
achukue huo usukani wa kuupata mlango huo.
Kwakuwa hakufahamu muda muafaka wa tukio
aliamua kuwahi muda huo huo kabla
hajawahiwa.Alifika baharini na kujitosa ndani ili
kumsubilia humph mpaka pale atakapofika.
★★★★★★★★★
mzes Mandevu alikuwa tayari amejiandaa vya
kutosha hasa pale atakapovamiwa muda
wowote,Humph naye hakuwa nyuma kimaandalizi
alijiandaa vyema kuuvaa mji wa zamani maana
alifahamu sehemu kama hizo huwa hazikosi
changamoto na mshike.mshike za hapa na pale.
Baada ya kuwa kila kitu kipo sawa walipotea kila
mmoja kwa mtindo wake huku waliopo ndani mle
wakiamini Humph amelala chumba ni kwake na si
vinginevyo.
Walitokea katika ufukwe wa bahari bila kupoteza
muda Humph akavaa nguo za kazi lakini alikuwa na
wasi wasi wa kufia majini kutokana eneo alilokuwa
anaenda kuwa lenye kina kirefu haswaa
"Mzes Mandevu mbona haujabeba mitungi ya gesi?"
lilikuwa swali la Humph
"Hatuna kazi nayo,nguvu ulizonazo zimatosha sana
kukufikisha chini ya maji bila kulowana hata
chembe" alijibu mzee Yule
"inastaajabisha!!,nawezaje kufanya hivyo?".
"swali nzuri leo nakufundisha kukimbia,vuta pumzi
mpaka mapafu yajae hewa bila kuiachia kisha
chomoka kama mshale mpaka pale macho yako
yatakapozidisha mwanga maradufu ndipo utakapo
zamia,itakuwa ni katikati ya mji wa zamani,narudia
usiachie pumzi mpaka utakapofika katika kituo
nilichokuelekeza na ukumbuke kuzungumza kwa
hisia kama unahitaji msaada nitakusikia,bahati
njema" alisema mzee Mandevu
Humph bila kukawia akaanza kufanya majaribio ya
kuvuta pumzi mpaka alipohisi kuwa pumzi yake
inatosha kumfikisha amahali alipoambiwa
Alianza kuhesabu moyoni kutoka tatu,mbili,moja
akaanza kukimbia na kila alipozidi kukimbia ndivyo
mwendo(speed) ilivyoongezeka na kumfanya awe
kama upepo unaopita katika maji ya bahari na
kumsaidia kupita bila kuzama
Alikimbia kama dakika tano akastukia macho yake
yametoa nuru zaidi ya ile ya mwanzo,pale pale bila
kuchelewa akajitosa baharini kwa kuruka ule mtindo
wanauita kama shale(kimshale) na kupotelea ndani
ya maji.
Humph alianza kupishana na samaki wa kila aina na
hakuwa akiloana hata chembe,Alipendezwa sana na
mazingira ya ndani ya maji yanavyovutia na kung'aa
ni kama kuna watu walioajiriwa kwaajili ya
kuyapamba mazingira hayo kwa aina tofauti tofauti
za mitindo.
Mzee Mandevu akiwa pale ufukweni akaisikia sauti
ya Sor ikisema "sasa anakuja lazima nifanye
kitu",Mzee Mandevu akabaki mdomo wazi kuwa
inamaana Sor ameshafika kabla yao na Humph hana
nguvu za kutosha kushindana na Sor
Mzee Mandevu alihisi kitu kinamkaba
kooni,akaanza kuiona damu ya Humph isiyo na hatia
ikienda kuteketea bila mtetezi na yeye hakuwa na
njia mbadala ya kufika kule chini.,
Humph alipotua chini akakumbana na mifupa ya
watu iliyochakaa mno hakujali hilo akaanza kusonga
mbele na kwa bahati zaidi kulikuwa na mwanga
kama mchana wakati huo huo alikotoka Humph
kulikuwa kumeanza kuwa usiku.
Humph alipotembea umbali mfupi alianza kuona
kitu kama nyumba hivi kubwa lakini kabla hajafika
anatokeza msichana mbele yake, Humph anasogea
mpaka karibu yake sura haikuwa ngeni ilikuwa ile ya
sor,mwili ukamsisimka hasira zikaanza kumjaa hasa
alipokumbuka kuwa huyo ndiye msababishi wa
maradhi ya baba yake na yeye kuishi bila amani,
Sor alitabasamu maana alitambua analowaza
Humph kwasababu yeye alikuwa na uwezo mkubwa
na ndiyo maana aliitwa malkia
Kumbuka:
katika kupambana na adui yako unahitaji moyo wa
ujasiri na sio moyo mwepesi wa kukata tamaa,pia
kila vita ya kiakili huisha kiakili hivyo msome adui
yako anataka nini ndipo upambane nae,naamanisha
udhaifu wake ndiyo ushindi wako.Tulia sasa chukua
hatua
Whoaaaa!! tuansonga mbele kwa like yako
comment na share.Karibuni tena
 
Sehemu ya Arobaini na nane
★★ilipoishia★★
Sor alitabasamu maana alitambua analowaza
Humph kwasababu yeye alikuwa na uwezo mkubwa
na ndiyo maana aliitwa malkia.
★★teremka Nayo ★★★
Mzee Mandevu alizidi kuhaha,wasi wasi
haukumuisha alijaribu kutembea kushoto na kurudi
kulia lakini yote ikawa ni bure tu,aliwaza na
kuwazua ni njia gani rahisi ya kupata msaada wa
kumsaidia Humph lakini hakuweza kupata wazo
lolote.
Alivyozunguka mpaka akachoka akaamua kukaa
katika ule mchanga wa ufukweni na punde si punde
tabasamu hafifu likaupamba mdomo wake
Mzee Mandevu alikumbuka neno la mwisho
alilomuambia Humph kuwa endapo atazidiwa na
chochote atumie hisia zake kumtaarifu.
Humph baada ya kumuona msichana sor mbele
yake alianza kujiandaa kwa lolote litakalotokea,t
aratibu akawa anasogea alipo Yule msichana na
ghafla msichana yule akapotea bila ya Humph
kutimiza lengo lake
★★★★%★★%★★★★
Wakati Sor amesimama mbele ya Humph
akimsubiri,Humph alizidi kuja kwa kujiamini kitu
ambacho Sor alikiona mapema na pale wazo
likamuijia kuwa endapo atapambana na Humph
mpambano unaweza kuwa mkali kiasi cha
kusababisha yeye Sor akapoteza nguvu nyingi na
kushindwa kupata alichokikusudia.
Sor aliamini kabisa kuwa sehemu anayoenda Humph
lazima itakuwa na upinzani mkubwa utakaomchosha
na.kuzipunguza nguvu zake kwa kiasi Fulani na
baada ya kufanikiwa ndipo yeye ajitokeze na
kumpora kiurahisi bila kutumia nguvu nyingi.
Hivyo Sor hakuona sababu ya kuendelea kubaki pale
akimsubiri Humph,akapotelea mahali alipoona
panafaa kwa yeye kujificha mpaka pale Humph
atakapofanikiwa kuupata mlango ule.
★★★★★★★★★★★★
Lisa alipoona giza linaingia akaaga nakuahidi kuwa
atarudi siku inayofuata ili amjulie Humph hali yake.
Lisa alifika nje lakini hakumuona humph roho ilizidi
kumuuma kwa kitendo alichokifanya ikionekana
ameamua maamuzi ya kipuuzi,alipoingia katika gari
yake na kufunga vioo akaanza kulia.
Aliporidhika kulia akakanyaga mafuta kuelekea
kwao,njiani hakuwa na raha alijitahidi kuangalia kila
upande wa Barbara lakini hakumuona Humph wake.
Lisa akaona haitoshi kabisa na wala haingii akilini
kurudi nyumbani kwao bila kumuona
humph,aliegesha gari yake pembeni ya barabara
kisha akaanza.kutembea taratibu akiwa na
mawazo.mno huku mkononi kitambaa chake kikizidi
kulowanishwa kwa machozi kila anapoyafuta.
Lisa alifika mpaka katika daraja ambalo Mara nyingi
alikuwa akilitumia na Humph has a nyakati za jioni
katika maongezi mbalimbali.Lakini siku hiyo hakuwa
na Humph bali yeye peke yake na upweke ndiyo
uliomsindikiza mpaka mahali pale
Ilikuwa inasikitisha sana kumuona binti mzuri namna
ile akilia pasipo kupigwa,Hakika ilitia simanzi mno.
★★★★★★★★★
Mzee Mandevu alianza kuhisi amani Fulani
ikiutawala moyo wake,moja kwa moja akajua Sor
ametoweka kule kwa Humph na kama hajafika
kwake basi kuna mahali anaelekea.
Mzee Mandevu alijiwekà.sawia kupambana na Sor
wakati wowote.
Humph alizidi kuelekea katika lile jumba alilokuwa
akiliona kwa mbali na taratibu likazidi kusogea,njia
nzima aliyokuwa akipita ilitawaliwa na mifupa mingi
mno ya watu walioonekana wanamiaka mingi sana
tangu wapoteze uhai wao.
Humph alizidi kusogea na.mwisho akashuhudia
hekalu moja kubwa lililinakshiwa vizuri kwa nje ila
lilikuwa limefungwa.
Humph alitembea kwa tahadhari mno mpaka
akaifikia milango ya hekalu lile na kabla hajaigusa
ilijifungukia yenyewe na kumfanya Humph kustuka
kidogo.
Ukimya ulikuwa umetawala mno katika hekalu
lile,macho ya Humph yakaanza kutoa nuru pasipo
kuamrishwa na Humph
Ikumbukwe kuwa Humph alikuwa na uwezo mkubwa
wa kuangalia mbali kama darubini na hata punje za
ulezi zingemwagwa chini basi ni wazi angeweza
kuziona.
Macho ya Humph yalitazama mbele kabisa ya
hekalu lile ambapo yalipata kuona nguzo fupi yenye
kitu kama mkono ulioshika kitu Fulani cha mviringo
kama mpira.
Bila kuambiwa Humph akakitambua kuwa huenda
kile kitu mfano wa Mpira ndicho anachokitafuta
hivyo kwa haraka haraka zake akapoteza umakini na
kuanza kuharakisha akachukue ule mfano wa mpira.
Humph alipiga hatua ya kwanza na wakati
anashusha hatua ya pili akaisikia sauti ile
inayopenda kuongea naye ikimwambia "angalia
hapo"
Puuuuh!! ikasikika sauti ya kuanguka kwa kitu na
sakafu ikaachia,Humph alikuwa amechelewa kwani
mguu wake ulikuwa umeshakanyaga pale sakafuni
na kusababisha atumbukie mwili mzima huku
sehemu ile ikiwa imepasuka eneo kubwa
linalotosha kumdumbukiza kule chini kusikojulikana
kuna nini haswa.
Kwa bahati nzuri Humph aliwahi kujishikilia katika
sakafu ile ya juu na kumfanya abaki amening'inia,al
ipojaribu kuangalia ndani au chini alikokuwa
anapaswa kudondokea alikumbana na giza kali na
hata nuru ya machoni mwake haikufika kule chini.
kwa kutumia nguvu zote alizonazo Humph alijivuta
juu na kutua tena sakafuni kwa hofu kuu akihofia
labda ile sakafu itaachia tena.
 
Sehemu ya Arobaini na tisa
★★ilipoishia★★
kwa kutumia nguvu zote alizonazo Humph alijivuta
juu na kutua tena sakafuni kwa hofu kuu akihofia
labda ile sakafu itaachia tena.
★★Shuka nayo★★
akawa ameganda kama sanamu akisikilizia kwa
muda,baada ya kuridhika kuwa sakafu haipasuki
tena akaanza kutembea kwenda mbele akiwa
makini kuliko kawaida.
Sakafu ya hekalu lile ilikuwa ya rasimu(draft) hii
ilimfanya Humph kuwa na mashaka kidogo kuhusu
hali ya mle ndani.
Mara akili ya Humph ikang'amua kitu"mtego" hilo
ndilo wazo lililomjia lakini ukweli ulibakia kuwa
katika hekalu lile kuna mafumbo kadha wa kadha
yanayohitaji kufumbuliwa kwa kutumia akili ya
ziada.
Hatua tano mbele unaibuka msumari katika chumba
kimoja wapo cha rasimu ile(draft) na kumfanya
Humph kuganda tena akifikiria njia ya kuitumia
kuukwepa ule msumari na katu hakujua kuwa kuna
misumari mingi zaidi ya ule aliouona.
Mzee Mandevu alikaa muda mrefu akimsubiri Sor
bila mafanikio yoyote na mwisho aliona bora akae
tu akiwa anamngoja Humph ambaye aliamini ni
lazima autwae ushindi kwa hali yoyote ile.
★★★★★★★★★
Sifa na mama wa Humph walianza.kupatwa na wasi
wasi kwanini Humph haendi kujumuika nao katika
chakula cha usiku,Sifa akainuka na kuelekea katika
chumba cha kaka yake.
Alibisha hodi mara nyingi awezavyo na.kuna wakati
alilazimika kumwita kaka yake lakini hakuna
kilichozaa.matunda kati yambinu zake hizo
alizotumia.
Sifa aliamua.kurudi sebuleni na kumwambia mama
yake kuwa huenda Humph bado anahasira na ndiyo
maana hataki kutoka kwahiyo waendelee kula na
Kwakuwa Humph anapafahamu vyema jikoni basi
akijihisi ana njaa ataenda kujichukulia.
Mama wa Humph hakuwa na matatizo zaidi ya
kumsikitikia mwanae kwa kuwa na hasira za kijinga
zisizo.na maana hata kidogo zaidi ya kumuongezea
magonjwa yasiyo ya lazima.
★★★★★★★★★★★
Humph aliona ni bora atumie njia ya kukimbia
songombingo ama kwa kule kwetu tunaita zigzag
(zigizaga) na bila kupoteza muda akaanzisha
kukimbia
Kila sehemu aliyopita Humph kulichomoza msumari
hiyo ni baada ya kuondoa tu unyayo wake na
msumari uliochongoka vizuri unajitokeza kwa kasi
ya ajabu.
Humph alipokatisha vyumba kadhaa kulikuwa
hamna kitu chochote kinachojitokeza akaamua
kusimama avute pumzi kidogo.
Aliporidhika na mapumziko hayo yasiyo rasmi
akajaribu jaribio la kitoto la kugusisha mguu katika
chumba kingine cha sakafu ile,Mara baada ya
unyayo wake kugusa kile chumba kwa mbali,meno
yakachomoka haraka pande mbili ili yaubane mguu
ila Humph alikuwa ameshaliona suala hilo na kwa
wepesi wa ajabu akaurusha mguu wake kurudi pale
alipokuwa ameasimama
Yale meno yakajibana yenyewe kwa nguvu na
endapo kama yangeukuta mguu wa Humph
angekuwa kilema mud aule ule.
Humph alishusha pumzi za kufa mtu asiamini
kilichotokea eneo lile,sasa ikabaki ni kuotea
vyumba vya kupita mpaka katika ule mkono
ulioshika kidude mfano wa mpira.
Humph alifanikiwa kuvuka vyumba kadhaa na akiwa
amebakiza safu mbili tu kuufikia ule mkono mguu
wake unatua kwenye chumba kimoja kisichoonesha
dalili ya kuwa na mtego wowote.
Baada ya Humph kushusha guu lake la pili inatoka
ngumi moja kubwa iliyomrusha Humph juu na
kusababisha ajigonge katika paa lililokuwa mbali
mno kwa urefu wake
Humph alipoteza muelekeo akawa anaona nyota
nyota zinakiandama kichwa chake na kigiza Fulani
cha ajabu kikatanda machoni mwake.Aliposhuka
chini alijibamiza karibia na ule mkono ulioshika kile
kidude mfano wa mpira.
Humph akapoteza mawasiliano kati ya kichwa na
kiwiliwili(kuzirai nusu) na nusu alikuwa
akijitambua.Baada ya kulala muda mrefu pale chini
ndipo nguvu zinaanza kumrejea tena
Humph anasimama huku akipepesuka pepesuka
(kuyumbayumba) kama mle I wa mchana
anayesindikizwa na jua.
Taswira ya kila anachokiona ilipokaa sawa
akatazamana na ule mkono uliokuwa mbele yake
ukimsubiri,kwa hatua za kivivu Humph akasogea na
kushika ule mpira autoe lakini ikashindikana.
Akaanza kupiga mateke napo ikawa sawa
na.kusukuma gari mlimani,akatafuta kitu cha
kutolea lakini hakupata chochote kwani mle ndani
hamkuwa na chochote zaidi ya sakafu na ule
mkono.
Humph alichoka akageuka kutazama alipotoka yaani
toka mwanzo wa hekalu mpaka pale.alipofika na
vikwazo alivyokutana navyo roho ikazidi kumuuma
na kujiuliza moyoni "sasa kulikuwa na haja gani ya
kuja humu na kitu chenyewe hakitoki"
Humph akiwa pale akahisi kitu,macho yake
yalikuwa hayana nuru tena na wazo likamuijia labda
macho yake yanaweza kutoa kile kidude
kinachofanana na mpira japo kilikuwa na ukubwa
wa kati usiolingana na mpira.
Pale pale akaanza jaribio lingine la kuamrisha
macho yake yatoe nuru,kwa zaidi ya Mara tatu
mfululizo ndipo akafanikiwa kuyatawala macho yake
kisha kwa mwendo mdogo akausogelea ule
mkono....
 
Sehemu ya Hamsini
★★ilipoishia★★
Pale pale akaanza jaribio lingine la kuamrisha
macho yake yatoe nuru,kwa zaidi ya Mara tatu
mfululizo ndipo akafanikiwa kuyatawala macho yake
kisha kwa mwendo mdogo akausogelea ule
mkono....
★★Shuka nayo★★
Humph alishika ule mkono ulioshikilia kile kidude
kifananacho na mpira,ghafla mkono ule ukaachia
vidole vyake nakufanya lile dude kama.mpira libaki
wazi
Kwa haraka Humph akachukua na kugeuka ili
aondoke,Alipogeuka alishangaa kuona kila kitu
kilichokuwa kwenye sakafu kinarudi kama mwanzo
alipoingia.
Amani ikatawala moyoni mwa Humph lakini ghafla
amani ile ilitoweka baada ya hekalu lile kutikisika
kwa ghafla kama tetemeko linapita.Udongo mwingi
ulianguka na kumfanya Humph kuingiwa na wasi
wasi
mbele kabisa ya hekalu lile sakafu ilianza kupasuka
kuelekea juu ikiamanisha kuna kiumbe kinatoka pale
muda mfupi ujao.Humph akaduwaa akili yake
ikampeleka katika filamu alizozoea kuona
Kichwa kilitangulia kutoka na kumfanya hunph
ajisemee moyoni "ooooooh!! kimenuka" sambamba
na kuanza kukimbia kutoka nje.
Kiumbe kilichotoka pale kilikuwa ni kenge mmoja
mkubwa mno japo hakufikia paa la lile
hekalu,alijichomoa mpaka akamalizika kabisa na
kuanza kumfukuzia Humph.
Humph aliiona hatari inavyomnyemelea na kama
angezubaa basi angekuwa kitoweo cha kenge yule
ambaye hata angefanikiwa kumtafuna Humph
asingeshiba na nadhani Humph angeishia mwenye
meno tu.
Humph alikimbia kwa bidii zote akijaribu kuuokoa
uhai wake kwa Mara nyingine,Kenge alipokuwa
akikanyaga kila hatua moja ilifanya hekalu lile lizidi
kutikisika na kuanza kubomoka.
Mbele ya hekalu lote kulididimia ardhini na kadri
yule kenge alivyoongeza hatua ndivyo alivyozidi
kumsogelea Humph na hii yote ilitokana na ukubwa
aliokuwa nao yule kenge.
Kabla Humph hajafika nje kenge alikuwa amemfikia
na kuanza kuutoa ulimi wake amnase humph ,Kazi
ikawa ngumu kwa Humph akijitahidi kukwepa ule
ulimi usimpate.
Humph alikuwa ni mtu mmoja mwenye bahati sana
maana pamoja na kukimbia kote aliishia katikati ya
miguu ya kenge na kila alipojaribu ilishindikana
kumpita yule kenge lakini kwa maajabu zaidi Yule
kenge alikanyaga ile sehemu iliyomfanya Humph
atumbukie kipindi anaingia ndani ya hekalu.
kenge alivyokanyaga lile eneo hakuchukua hata
sekunde akaporomoka kuelekea chini na kibaya
zaidi
Humph alikuwa katikati ya miguu ya kenge yule.
Humph alijaribu kufumba macho apotee lakini
haikuwezekana hata kidogo,hakukata tamaa
akajichomoa kadri awezavyo ili ule uwazi uliobaki
kabla kenge hajatumbukia mwili mzima yeye awe
amepita.
Kenge alipoona anatumbukia ardhini akajishikilia
kwa nguvu akipingana na shimo ili asiende chini na
Humph bila kutegea akajirusha kwa kutumia nguvu
zote alizonazo
Humph akapita katika ule uwazi akiwa juu kwa juu
na kabla hajauvuka ule uwazi kenge akawa
amekiona kitoweo chake kinamkwepa nae
akazungusha kichwa chake kwa nguvu ulimi ukiwa
nje
Kile kichwa cha kenge kilimkosa Humph ila ncha ya
mwisho ya ulimi wake ukamgonga Humph na
kumfanya mwendo wake(speed) iongezeke zaidi
kuelekea nje ya hekalu huku akijibamiza katika kuta
za hekalu lile na kuziongezea kubomoka.
Baada yakenge kumkosa Humph kiçhwa chake
kilikutana naukuta mgumu wa hekalu,Kwakuwa.
nangozi ya kenge ni ngumu vilivyo ukuta ulishindwa
kuhimili ule uzito na kuanguka kuelekea mle
shimoni
na kuufanya uzito uongezeke maradufu kwa kenge
hali iliyomfanya ashindwe kustahimili pale
alipojishikiza na kuangukia katika lile shimo huku
hekalu nalo likifuata kwa juu na kufukia eneo lile.
Humph alikuwa ameangukia nje kabisa ya hekalu
lile,akaanza kukohoa na kujitahidi kuinuka pale
alipolala.
Wakati anainuka akaanza kusikia milio kama ya miti
mikavu inayokatwa "kekekekekeke! nkooooh!"
ikabidi
ainue kichwa kutazama ni kitu gani
Loooooh!! ilikuwa ni kizaa zaa kingine kimeibuka
pale chini ile mifupa ilikuwa inajikusanya na
kutengeneza watu ambao ni mifupa mitupu wanaiita
mafuvu au maskeletoni
Humph alibaki ametoa macho kwa mshangao na
akajikuta anaropoka "hapana,hapana,hapana, sio
tena aaaaah!" alizidi kulalamika humph ni kama yale
mafuvu yanamuelewa.
Kutokana na ule umbali uliokuwepo.kutoka
pale.alipoangukia.Humph wakati anaingia katika mji
wa zamani(old city) mpaka katika hekalu ulikuwa ni
umbali mrefu sasa chukulia kama mita mia mbili
hivi
kwa uchache mafuvu yamesimama,ni jeshi kubwa
kiasi gani.
Humph alikaa chini kwanza akitafakari kitu cha
kufanya maana alijua wazi ile vita ni ya kufa na
kupona na mbaya zaidi hakujua ni jinsi gani
anavyoweza kiwadhibiti wale wanajeshi(mafuvu).
Kaskeletoni kamoja kalimsogelea Humph nadhani
kalikuwa ni kakimbelembele au chambo Kama
wanavyoita wengine,Humph aliinuka haraka na
kujiandaa kukakabili na Mara kakaanzisha vurumai
ambalo Humph alilidhibiti mapema kwa kung'oa
kichwa chake.
Humph alijiona kumbe ni kidume anayeweza
kuimaliza ile vita bila msaada,kwa maajabu zaidi
kale kaskeletoni(kafuvu) kakaanza kutafuta kichwa
chake mpaka kakakipata na kukirudisha kilipokuwa
Humph alipigwa na butwaa kwamba inamaana yale
mafuvu hayafi,itakuwaje sasa,alihisi tayari hanabudi
kujisalimisha.
Kabla hajaafikiana na halmashauri ya kichwa chake
anamkumbuka mzee Mandevu mzee aliyeahidi
kumsaidia pindi awapo na tatizo.
Kwa hisia kali Humph akaanza kuwasiliana na mzee
Mandevu kabla vita haijaanza,kwa utulivu wa hali ya
juu ujumbe unafika kwa mzee Mandevu na bila
kuchelewa mavazi yake yanageuka rangi pale pale
yanakuwa yakung'aa sana tena haikuwa rangi
nyingine ila ile ya umwagaji damu hapa
nazungumzia
rangi nyekundu.
 
Sehemu ya Hamsini na moja
★★ilipoishia★★
Kwa hisia kali Humph akaanza kuwasiliana na mzee
Mandevu kabla vita haijaanza,kwa utulivu wa hali ya
juu ujumbe unafika kwa mzee Mandevu na bila
kuchelewa mavazi yake yanageuka rangi pale pale
yanakuwa yakung'aa sana tena haikuwa rangi
nyingine ila ile ya umwagaji damu hapa
nazungumzia
rangi nyekundu.
★★Endelea nayo★★★
Mzee Mandevu alikuwa na hamu na ile vita kwani ni
kipindi kirefu mno kimepita bila kujihusisha na
maswala ya vita.
Humph alipofumbua macho yake akakutana na
ngumi iliyokomaa iloyomfanya ajisikie maumivu
makali mno shavuni.
Kabla hajakaa sawa akasikia makofi yakipigwa
nyuma yake,alipogeuka akakutana ana kwa ana,jino
kwa jino na Sor aliyekuwa ametabasamu.
Humph akakosa pozi akabaki anamtazama Sor
kwani
mwanzo alikimbiwa na sor na sasa yupo mbele
yake
lakini licha ya kuwa Sor amefika pia mafuvu yale
yanamtaka Humph ni hatari iliyoje kwa Humph.
Ghafla unasikika upepo maeneo hayo na unapoisha
anaonekana mzee Mandevu amesimama sambamba
na Humph
"Habari yako malkia usiyejitambua,nafikiri ni karne
kadhaa sasa hatujaonana toka kipindi umetoroka
kwa mfalme." alisema mzee Mandevu akiwa na
tabasamu murua
"Acha upuuzi we mzee,Leo hii lazima mmoja wetu
abaki huku akisaidia kulinda na haya makatuni"
aliongea Sor kwa dharau
Mzee Mandevu hakupoteza tabasamu lake
akamgeukia Humph na kumuuliza "vipi
umeshafanikisha lile suala"
"Asilimia mia moja mzee wangu" Humph alijibu
huku
akiwa na tumaini jipya la kupona kutoka mikononi
mwa maskeletoni na Sor
Mzee Mandevu alisogea kule yaliko mafuvu na
humph akamfuata Sor ili kulipa kisasi .Humph
alipopiga hatua moja ya pili alijikuta akiambulia
makombora mfululizo yaliyomfanya arushwe mbali.
Mzes Mandevu aliinua fimbo yake juu na ghafla
wingu moja matata likatanda juu kuanzia pale
yalipokuwa Yale mafuvu mpaka mwisho wao
yalikoishia.
Humph alijiinua taratibu na kukaa sawa "Kama
unajiamini kwanini utumie udanganyifu,twende
mkono kwa mkono"
lengo la Humph kusema vile alitaka kuhakikisha Sor
anakufa kifo cha taratibu na chenye maumivu ya
hali ya juu.
Kwa kustukiza sor alimfikia Humph na kuanza
kumshushia kipigo cha paka mwizi ,hakumruhusu
Humph atue wala kupumzika yaani kiufupi Humph
aligeuzwa ni gunia la.mazoezi waswahili wanaliita
punching bag
Mzee Mandevu alisubiri wale mafuvu waanze kuja ili
afanye yake,na Kama alivyofikiria mmoja wa Yale
mafuvu aliyeonekana kama kiongozi wao alisimama
na kutoa ishara iliyoambatana na mlio Fulani kama
wa mluzi ama filimbi hivi na kuwafanya maskeletoni
wote kuanza kusogea mbele kwa kasi.
Mzee Mandevu bila kukawia akatikisa fimbo yake
iliyosababisha radi moja adimu kupiga angani kisha
akashusha ile fimbo yake kwa nguvu na
kusababisha
radi nyingi zishuke eneo lile la maskeletoni na
kuwafanya wasambaratike wote na kubaki unga
unga wa mifupa.
Humph alipokea kipigo hadi akiona Sor ananyoosha
mkono anajificha usoni ili asione anavyopigwa,Sor
hakuona haja ya kumbakiza Humph kwani alijua
itafikia kipindi Humph atataka kulipiza kisasi
Kabla Sor hajamalizia pigo la mwisho aliloliandaa
mahsusi kummaliza Humph mzee Mandevu
anaelekezea fimbo yake kwa Sor na kuachia radi
moja matata iliyomrusha Sor mbali huku akiachia
yowe la uchungu.
★★★★★★★★★
Ilikuwa ni asubuhi nyingine tena iliyomkuta Lisa
akiwa chumbani mwake amejiinamia jicho
limemuiva
kama nyanya mshumaa,yote kwa yote kukosa
usingizi usiku mzima kulimfanya azidi kuonekana
mchovu kupita maelezo.
Mlango wake ulisikika ukigongwa kwa nguvu huku
sauti ya mama yake Lisa ikizidi kuita,cha ajabu Lisa
hakujali wala kuonyesha kuisikia ile sauti
inayomwita.
Lisa alizidi kuziona picha za Humph kichwani
alivyokuwa akimsihi na kumwambia kuwa
anampenda,alijiona mwenye hatia mno kwa Humph
na alihisi kuwa itakuwa vigumu kwa Humph
kuurejesha moyo wake kwake bila kujua vita
inayomkabili Humph kwa muda huo na aidha arudi
hai ama amekufa.
Lisa alijiona mjinga kuendelea kulia na wakati
anaweza kujitafutia nafasi ya mwisho na kujenga
uamimifu mpya utakaomuwezesha kuwa karibu na
Humph.
Lisa aligutuka kitandani na kwenda kufungua kabati
akaanza kujikwatua bila hata kujali macho yake
yaliyobadilika na kuwa mekundu.
Alfungua mlango na bila kumsemesha mama yake
akakimbilia nje kuchukua usafiri ili awahi nyumbani
kwa kina Humph.
Mama yake na Humph pamoja na Sifa walikuwa
mezani wanapata kifungua kinywa lakini Humph
hakuwepo hali iliyomfanya mama huyo kupata
wasiwasi kwa mwanae
"Sifa mbona kaka yako hajafika mpaka sasa au
haujuamtaarifu kuwa chakula tayari."
"Si hayo tu huyo mwanao mi simuelewi,chakula cha
Jana hajagusa hata tonge na asubuhi hii yuko kimya
chumba ni make."
"Hebu nipe funguo zile za ziada nimfuate huenda
ana tatizo alafu toka Jana moyo unanienda mbio
mbio kweli sijui tatizo nini"
Like share invite na toa maoni uwezavyo ili
kuboresha kazi hizi
 
Sehemu ya Hamsini na mbili
Fainali
★★ilipoishia★★
"Hebu nipe funguo zile za ziada nimfuate huenda
ana tatizo alafu toka Jana moyo unanienda mbio
mbio kweli sijui tatizo nini"
★★Shuka nayo★★
"Nimeshajaribu kufungua lakini inavyoonesha
amefunga na komeo kwa ndani" Alijibu Sifa
"aaaah!! huyu mtoto ni kasheshe kama nd'o
hivi,Muache ikiimuuma labda atatoka au tuvunje
mlango ili atoke kwa lazima."
"sasa mama huko unakofika mbali kaka anajitambua
k'o atakuja mwenyewe usijali"
"Haya mtetee ila yakimkuta yakumkuta utanigeuka
hapa"
"Basi mama inatosha"
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa
wakajiandaa kwenda hospitali kwa dokta Alex Jr
wapate kujua hali ya mzee Kasai.
★★★★★★★★★★★★★
Mzew Mandevu alimfuata Humph na kumuinua
taratibu na wakati huo huo Sor aliinuka ni kama
aliyepandwa na wazimu,kwa kutumia ujuzi alionao
akaachia kombora lililotoka kama upepo hivi na
kuwatawanyisha mzee Mandevu na Humph.
Sor alisimama imara sasa na kujipanga kuwakabili
Humph na mzee Mandevu
"Naona bado upo katika ubora wako ule ule"
aliongea mzee Mandevu huku akijiinua
"acha maneno sogea huku tupambane,dume zima
unapigana kwa kutumia fimbo" aliongea sor,likawa
kosa kubwa kwani aliamsha mashetani yote ya
mzee
Mandevu japo lilikuwa ni kosa moja kubwa
alilolifanya mzee huyo pamoja na nguvu zake zote
lakini aliendekeza hasira zilizomuongoza kwenda
kwa Sor
Mzee Mandevu alikurupuka na kabla hajafika mbali
Humph naye akasimama na kuanza kumfuata mzee
huyo huku akijaribu kumwita ili atulie lakini Sor
alikuwa ameshawawahi na kuachia kombora lingine
lililomkusanya mzee Mandevu na Humph na
kuwatupilia mbali.
Sor alianza kucheka kidogo kidogo na kisha
akaangua cheko kubwa sana.
Pale alipoangukia mzee Mandevu ndipo kile kidude
mfano wa mpira,mzee Mandevu alipokitazama
akakifahamu moja kwa moja kuwa nd'o mlango
wenyewe kwa haraka akanyakua na kuanza
kujitahidi kuinuka.
Humph alikuwa anagala gala tu kwa
maumivu.Macho ya Sor yalitua kwa mzee Mandevu
"Umeisha ng'ombe mzee,huna jipya kabisa hata zile
nguvu ulizokuwa unatamba nazo enzi zile
zimekwisha." alijigamba Sor
Mzee Mandevu hakujali maneno ya Sor alizidi
kujipigania ainuke,Na hatimaye alifanikisha zoezi
lake
Soralikunja sura kisha akainua mikono yake
iliyofanya hali ya hewa ibadilike na kuwa na upepo
mwingi uliokuwa ukijikusanya mikononi mwa Sor
Mzee Mandevu alifahamu kinachoenda kutokea
wakati huo kuwa ni hatari kwa Maisha yao hivyo
kwa haraka akaushika ule mlango na kuunyooshea
kwa Sor kisha akapiga kelele
"humphhhhhh! Fanya sasa." alisema mzee Mandevu
kwa sauti kali iliyomstua Sor
Kama mzimu Humph alijibinua na kusimama wima
kisha kwa nguvu zote akatoa ile nuru ya macho
yake kuelekea kwenye ule.mlango wa kwenda
ulimwengu mwingine.
Mwanga ulipenya ukiwa Mweupe na ulipotokea
upande wa pili ulikuwa wa njano,Sor akatoa macho
kama mjusi aliebanwa na mlango baada ya ule
mwanga wa njano kumfikia
Sor akaanza kuyeyuka akielekea mle katika ule
mlango na baada ya kuyeyuka mpaka akaishia
katika
ule mlango mwanga ule wa njano ukatoweka baada
ya Humph kudondoka chini na kupoteza fahamu.
Mzee Mandevu akamnyanyua Humph na kutoka
naye katika mji wa zamani(Old City)
★★★★★★★★★★★
Lisa alifika nyumbani kwa kina Humph na kukuta
mama wa Humph akijiandaa kutoka na Sifa
wakielekea hospitalini.
Baada ya kumuona Lisa alivyovimba macho kwa
kulia walitambua kuwa kuna kitu kinaendelea baina
ya humph na Lisa kwani waswahili wanasema kama
kuambiwa hausikii hata picha ikushinde kuona
kweli? hilo lilikuwa jibu tosha kwa Sifa na mama
yake
Walimjibu jibu lile lile.kuwa Humph hayupo na
wakaomba Lisa awasindikize hospitalini naye bila
hiyana akakubali kuongozana nao.
★★★★★★★★★★
Humph alistuka akiwa kitandani kwake na pembeni
alikuwepo mzee Mandevu
"Nimefikaje hapa?" lilikuwa swali la kwanza la
Humph kwa mzee huyo.
"Usijali kila kitu kimeisha,unastahili pongezi nyingi
na pia sina zawadi ya kukupa ila hayo macho pekee
niliyoyaunda kwa.mikono yangu na wazo
langu,Hongera sana kwa kuifanya dunia kuwa na
amani."
"Asante ila nikushukuru wewe kwa msaada wako wa
hali na mali mpaka.kufikia hapa". alitoa shukrani za
dhati Humph kwa mzee Mandevu
"Nahitaji kuondoka lakini kabla sijafanya hivyo
nahitaji kuitimiza ahadi yangu kwako niliyoahidi"
alisema mzee Mandevu akiwa mwenye furaha muda
wote
"Ahadi gani hiyo mzee?. alihoji Humph
"Nataka nikufanye kuwa.mwenye furaha tena" alijibu
mzeeMandevu
"Jiandae kuna sehemu tunapaswa kufika" aliongeza
mzee Mandevu
Humph alitoka chumbani na kukuta nyumba ikiwa
tupu,akakiendea kifungua kinywa na kujiweka sawa
kisha wakatoka na mzee Mandevu
Lisa,Sifa na mama wa Humph walikuwa wakirudi
nyumbani kutoka hospitalini na Humph pamoja na
mzee Mandevu walikuwa wakiingia hospitalini hapo
kwa njia ya kawaida kabisa hivyo walipishana
kidogo
tu.
Walipofika wodini mzee Mandevu akamuomba
Humph asimame mlangoni ili amlinde mzee
Mandevu ilimradi akamilishe ahadi yake aliyoahidi.
"Ni wakati wa kuamka sasa kwani ndoto uliyoota na
imani imekuchosha mno japo umeifurahia"
akamalizia na maneno hayo mzee Mandevu huku
akimshika mzee Kasai kichwani
"Hatokumbuka lile tukio lililotokea zaidi ya
kufahamu
kuwa alipata ajali ndogo" alisema mzee Mandevu
"Asante sana kwa upendo wako hakika sina cha
kukulipa" aliongea Humph akiwa analengwa lengwa
na machozi
"Usijali tupo pamoja kijana" alijibu mzee Mandevu
"Huu mlango nitaulinda Mimi kuanzia sasa hivyo
ondoa shaka juu ya lolote kumhusu Sor na watu
waliopo katika ulimwengu with(immortals),Kwaheri
na ukihitaji msaada nipo kwaajili yako muda
wowote" alimalizia mzee Mandevu na kutoweka.
"Hatimaye nimekuwa mtu huru sasa,baba ni wakati
wako wa kumuona kijana wako amekua na mwenye
ndoto nyingi za kuijenga dunia,ndoto yako ya kuwa
na.mtoto shupavu na msaada.kwa.kila mtu
imetimia,amka ufurahie Maisha mapya" aliyasema
hayo Humph akiwa pembeni ya baba yake
★★★★★★★★★
Jioni ilifika na Lisa akaelekea katika daraja akiwa
mwingi wa mawazo,kwa.mbali akaanza kuona kama
kuna mtu amesimama pale katika daraja,hamu ya
kumfahamu ikamvaa akajikuta tayari anahisia za
kwamba yule ni Humph
Alikimbia mno na alipofika alimgeuza yule bwana
kwa nguvu akijua ni Humph,akakutana na sura ngeni
yenye mshangao
"Samahani" ni sauti iliyomtoka Lisa
"pumbavu wewe kazi kuvamia usiyowajua,una bahati
hiyo samahani yako imekuokoa sijui ningekufanya ni
ni?" aliongea yule mtu na kuondoka
Lisa alikata tamaa machozi yakazidi kumshuka
lakini
ghafla akakumbatiwa kwa nyuma.Hakuamini
akageuka haraka na kumkuta Humph akiwa na
tabasamu pana
Lisa alimkubatia kwa nguvu Humph wake na kuanza
kusema
"Nisameh....."
"shhhhhhhhh!! usiseme kitu" alijibu Humph
★★★★★★★★★★
Asubuhi iliyofuata familia ilikuwa pamoja katika
kifungua kinywa kasoro mzee Kasai,simu ya mezani
iliita na walipoipokea waliambiwa mzee.Kasai
amerejewa na fahamu,kwa shangwe zote waliwahi
hospitalini na.kumkuta mgonjwa amekuwa.mzima.k
abisa tena katika ubora wake.Familia ya Humph
ikarudisha furaha iliyopotea.
★★★★★★★★★
Humph alistuka toka usingizini akiwa amelowa
jasho
muda huo alikuwa katika basi la chuo cha Sayansi
na teknolojia akiwa na wanachuo wenzake
wametoka katika ziara.
Mji ule haukufanana na mji waliokuwa wakiishi hapo
zamani,huo mji ulipambwa kwa.maghorofa na
majengo pamoja na kila.aina ya usafiri wa kisasa
yote ni.kutokana na kukua kwa sayansi na
teknolojia
Ile ndoto aliyoiota Humph haikujulikana lakini wakati
basi linasonga mbele ghafla mzee.Mandevu
anatokea mbele ya Humph akiwa amempa
mgongo,kwa haraka humph akainuka na kimfuata
pale alipo
Alipomfikia akamgusa begani,Mzee Mandevu
aligeuka na kudondoka Humph akamdaka na
kushuka naye chini taratibu akiwa amemshikilia
vizuri
Mzee Mandevu alikuwa anatokwa damu puani na
mdomoni,aliongea kwa tabu mno mpaka Humph
akawa anadondokwa na machozi "Watu wote
wameungana na Sor na kunigeuka Mimi,wote
wanataka kuitawala dunia yenu" akakohoa kidogo na
bonge la damu likaruka
"Tunza zawadi hiyo niliyokuachia usikubali watu
wanyanyasike,Usikubali hata kidogo watu hawa
wakaitwaa dunia yenu,usikubali waipoteze amani
mliyonayo,pigana mpaka tone lako.la mwisho la
damu na ukumbuke kuwa vita inayokuja ni kubwa
kuliko vita yoyote ile uliyowahi kupigana" alimalizia
maneno hayo ambayo aliongea kwa tabu kuonesha
alipitia maumivu makali sana kabla ya kufika pale.
Alimkabidhi Humph ile fimbo yake kisha kwa
tabasamu pana mikono yake ilong'ang'ania shati la
Humph kisha ikalegea kuonesha tayari amepoteza
maisha.
Humph alilia kwa uchungu mno akiwa tayari
amempoteza mtu muhimu ambaye ni dira kwake na
mwenye thamani ya kipekee sana.
‡‡‡Mwisho wa msimu wa kwanza‡‡‡
 
Sehemu ya ishirini
........Ilipoishia..........
Alinyoosha mikono juu baada ya kumaliza maneno
hayo huku akiwa ameishika vyema hazina
hiyo.Tahamaki ni kwamba saa sita ilikuwa tayari
imefika hivyo moto ukazima wenyewe na hazina
ikapoteza nuru yake na kuwa jiwe la kawaida
Mzee Mandevu alipiga magoti kwa uchungu na
kushusha pumzi ndefu..
..........endelea.............
Hakufanya vile kwa ridhaa yake bali ni kutokana na
muda kumtupa mkono,alifadhaika mno kwa kitendo
kile kilichotokea ambacho ukweli ulibaki kuwa
walifanya kazi isiyo na faida licha ya taabu zote
walizopitia
Humph nae aligundua kuwa tayari amechelewa
kufikisha hazina hiyo.Alianza kulia maana alipoteza
watu muhimu mno katika Maisha yake,si hivyo tu
bali kupoteza ndugu katika hali ya utata namna hiyo
si jambo jema hata kidogo ukizingatia uwezo wa
kuwaokoa ulikuwa ndani ya uwezo wake.
wote waliomboleza haswaaa mpaka ikafikia mahali
kila mtu akakaa peke yake akitafakari nini afanye
japo Humph alikuwa kila sekunde anamlaani Sor
kwa kitendo alichomfanyia.
Wakiwa katika hali hiyo ghafla kikohozi kikavu
kilianza kusikika kikitokea sakafuni na chafya
mfululizo,walipotazama kwa pamoja walishangaa
kuona Sifa ameamka na muda huo huo na wengine
nao wakaanza kukohoa huku wakijitahidi kuinuka
sakafuni hapo.
Vilio vilikata na furaha ikaanza kuchanua upya baada
ya kuona familia imerejea tena katika ubora wake
.Mzee Mandevu akamgeukia Humph "leta maji ya
kunywa Fanya haraka" na Humph bila kuuliza akatii
Baada ya kupewa maji kila mtu na kunywa ndipo
fahamu zikawarejea,wakainuliwa rasmi na kuketi
kisha mazungumzo mafupi yakafuatia
"Poleni sana ndugu zangu kwa matatizo
yaliyowakumba" mzee Mandevu aliongea huku
akiwatazama kwa zamu
"Niseme asante Kwakuwa umetoa pole lakini
sijafahamu haswaa hiyo pole inahusu nini Mzee"
aliongea mzee Kasai akiwa ameyatumbua macho
yake kwa mzee Mandevu
"Hii pole ni kwasababu mlipatwa na ajali
iliyosababishwa na gesi chafu ambayo ilipulizwa
katika nyumba yenu na haijulikani ni nani aliyefanya
hivyo na kwa lengo lipi" aliongopea mzee Mandevu
"oooh! kwahiyo...? au...? aaah...? sawa sawa
nashukuru kwa msaada wako" Alishindwa kuongea
mzee Kasai yote ni kwasababu ya kushindwa
kuelewa ni nani hasa aliyefanya hivyo na hata
akijaribu kuvuta kumbukumbu ya maadui alionao
hakupata jibu maana yeye ni mtu mwema sikuzote
na hata kama wangekuwa na nia mbaya kwanini
hawajabeba kitu chochote kile hilo ndilo
lililomsumbua kichwani mwake
Humph alikuwa akitabasamu tu na kustaajabishwa
na akili za mzee Mandevu katika kubadilisha ukweli
wa mambo kuwa vile anavyotaka.
Hatimaye mzee Mandevu aliaga na kuondoka akidai
kuwa alikuwa mpita njia tu ili asitiliwe shaka huku
akiwa amejizolea shukrani nyingi ambazo kama
wangefungashia basi angeondoka na pipa nzima la
shukrani.
**************************
Lisa hakuwa na subira hata kidogo kwani alihisi
kabisa kuwa endapo atafanya mchezo basi yule
mwokozi wake atanyakuliwa na msichana mwingine
kabla yake,alikuwa na shauku mno ya kumfahamu ili
amwambie yanayomsibu kila siku amfikiriapo mtu
huyo.
Alipanga kuwa ifikapo asubuhi awahi shuleni kisha
akutane na Humph na ajaribu kumshawishi
amuonyeshe huyo mtu ambaye anautesa moyo wake
kwa asilimia kubwa.
Hakuchi hakuchi hatimaye kulikucha Lisa akiwa na
hamu ya kufika shuleni na hivyo ndivyo ilivyokuwa
kwani alifika mapema kuliko kawaida yake,akiwa
ameegemea ukuta huku ameushika mkufu na
kujiongelea kama chizi Humph nae alikuwa anapita
maeneo hayo akiwa anachechemea kwa mbali na
alama Fulani ya kibao ikiwa imejichora shavuni
pake.
Alivutiwa na mtindo aliokuwa amekaa Lisa ambao
ulimpa hamasa ya kumsogelea pale alipo,alipomfik
ia alishindwa kuelewa maneno ambayo yalikuwa
yanatamkwa na Lisa na kingine.kilichomuacha hoi
ni pale ambapo Lisa hakugundua uwepo wake eneo
lile.
Humph alipiga hesabu akaamua kumstua kwa
kupiga kelele"arrrrrrrrrrrrrr" zilizomfanya Lisa
akurupuke na kurukia pembeni huku ameshikilia
kifua chake na kuhema kwa fujo mno.
Humph bila kujali alikuwa amekauka kwa kicheko
mpaka machozi yakawa yanatiririka aiseeeee!
duniani kuna watu huwa wanacheka ni kama
midomo yao inatumia mashine na mbavu zao zina
jenereta.
Lisa alichukia mno kwa kitendo hicho akazira na
kuondoka eneo hilo akiwa tayari amesahau ni kitu
gani kilimpeleka pale katika ukuta ule. Humph
alikuwa ameshalikoroga hivyo inambidi atumie njia
mbadala kumrudisha hemani ndege yule mwenye
uzuri wa kila rangi ambaye ni Lisa.
*******------**********
yapata mida ya saa tisa alasiri Lisa akiwa njiani
anarejea kwao baada ya masomo,kwa muonekano
tu alidhihirisha kuwa hayuko sawa na ndivyo
ilivyokuwa kwani alikuwa amezama mno katika
dimbwi la mawazo juu ya kumpata mkombozi wake
ambaye mpaka wakati huo hakufahamu kuwa ni
Humph.
Humph anamkimbilia Lisa kisha wanaongozana
kurudi nyumbani,wakiwa wanatembea Humph
anaamua kuvunja ukimya
"Hey! um! aaaaah!! najua kama..."
"umenikwaza lakini haina haja ya kuniomba
msamaha" alidakia Lisa kwa sauti inayoamanisha
"Hapana nimetenda kosa tena kosa kubwa
linalostahili msamaha tafadhali nimekosa na
ninahitaji msamaha wako" Humph alikuwa akijieleza
kwa upole
"Isingekuwa nimempenda yule mwanaume ambaye
alinikomboa hakika huyu nae alikuwa ananifaa
kabisa" alijiongelea Lisa moyoni
"Usijali Humph wewe ni rafiki mwema kwangu hivyo
sina budi kukusamehe uwe na amani" Lisa aliamua
kumaliza kabisa tatizo hilo
Walitembea njia nzima wakiwa wametawaliwa na
ukimya wa aina yake ambao ulivunjika pindi Lisa
alipokumbuka kuwa alihitaji msaada wa Humph
kumfahamu yule aliyemuokoa mara kadhaaa
"Humph kuna kitu nahitaji unisaidie" aliongea Lisa
huku akimgeukia Humph
"Nakusikiliza Lisa" Humph alijibu kwa unyenyekevu
"Sijui kama utanielewa lakini nd'o hivyo ninavyotaka"
Lisa alizidi kuongea huku akiwa hajiamini
"Sema tu nipo kwaajili yako kama rafiki yako"
alisema Humph
"Humph Mimi namtaka Yule rafiki yako ambaye
aloniokoa kuna kitu natamani nimwambie tukiwa
wawili hivyo nahitaji msaada wako unikutanishe
nae" Lisa alijitetea
 
Sehemu ya Hamsini na mbili
Fainali
★★ilipoishia★★
"Hebu nipe funguo zile za ziada nimfuate huenda
ana tatizo alafu toka Jana moyo unanienda mbio
mbio kweli sijui tatizo nini"
★★Shuka nayo★★
"Nimeshajaribu kufungua lakini inavyoonesha
amefunga na komeo kwa ndani" Alijibu Sifa
"aaaah!! huyu mtoto ni kasheshe kama nd'o
hivi,Muache ikiimuuma labda atatoka au tuvunje
mlango ili atoke kwa lazima."
"sasa mama huko unakofika mbali kaka anajitambua
k'o atakuja mwenyewe usijali"
"Haya mtetee ila yakimkuta yakumkuta utanigeuka
hapa"
"Basi mama inatosha"
Baada ya kumaliza kupata kifungua kinywa
wakajiandaa kwenda hospitali kwa dokta Alex Jr
wapate kujua hali ya mzee Kasai.
★★★★★★★★★★★★★
Mzew Mandevu alimfuata Humph na kumuinua
taratibu na wakati huo huo Sor aliinuka ni kama
aliyepandwa na wazimu,kwa kutumia ujuzi alionao
akaachia kombora lililotoka kama upepo hivi na
kuwatawanyisha mzee Mandevu na Humph.
Sor alisimama imara sasa na kujipanga kuwakabili
Humph na mzee Mandevu
"Naona bado upo katika ubora wako ule ule"
aliongea mzee Mandevu huku akijiinua
"acha maneno sogea huku tupambane,dume zima
unapigana kwa kutumia fimbo" aliongea sor,likawa
kosa kubwa kwani aliamsha mashetani yote ya
mzee
Mandevu japo lilikuwa ni kosa moja kubwa
alilolifanya mzee huyo pamoja na nguvu zake zote
lakini aliendekeza hasira zilizomuongoza kwenda
kwa Sor
Mzee Mandevu alikurupuka na kabla hajafika mbali
Humph naye akasimama na kuanza kumfuata mzee
huyo huku akijaribu kumwita ili atulie lakini Sor
alikuwa ameshawawahi na kuachia kombora lingine
lililomkusanya mzee Mandevu na Humph na
kuwatupilia mbali.
Sor alianza kucheka kidogo kidogo na kisha
akaangua cheko kubwa sana.
Pale alipoangukia mzee Mandevu ndipo kile kidude
mfano wa mpira,mzee Mandevu alipokitazama
akakifahamu moja kwa moja kuwa nd'o mlango
wenyewe kwa haraka akanyakua na kuanza
kujitahidi kuinuka.
Humph alikuwa anagala gala tu kwa
maumivu.Macho ya Sor yalitua kwa mzee Mandevu
"Umeisha ng'ombe mzee,huna jipya kabisa hata zile
nguvu ulizokuwa unatamba nazo enzi zile
zimekwisha." alijigamba Sor
Mzee Mandevu hakujali maneno ya Sor alizidi
kujipigania ainuke,Na hatimaye alifanikisha zoezi
lake
Soralikunja sura kisha akainua mikono yake
iliyofanya hali ya hewa ibadilike na kuwa na upepo
mwingi uliokuwa ukijikusanya mikononi mwa Sor
Mzee Mandevu alifahamu kinachoenda kutokea
wakati huo kuwa ni hatari kwa Maisha yao hivyo
kwa haraka akaushika ule mlango na kuunyooshea
kwa Sor kisha akapiga kelele
"humphhhhhh! Fanya sasa." alisema mzee Mandevu
kwa sauti kali iliyomstua Sor
Kama mzimu Humph alijibinua na kusimama wima
kisha kwa nguvu zote akatoa ile nuru ya macho
yake kuelekea kwenye ule.mlango wa kwenda
ulimwengu mwingine.
Mwanga ulipenya ukiwa Mweupe na ulipotokea
upande wa pili ulikuwa wa njano,Sor akatoa macho
kama mjusi aliebanwa na mlango baada ya ule
mwanga wa njano kumfikia
Sor akaanza kuyeyuka akielekea mle katika ule
mlango na baada ya kuyeyuka mpaka akaishia
katika
ule mlango mwanga ule wa njano ukatoweka baada
ya Humph kudondoka chini na kupoteza fahamu.
Mzee Mandevu akamnyanyua Humph na kutoka
naye katika mji wa zamani(Old City)
★★★★★★★★★★★
Lisa alifika nyumbani kwa kina Humph na kukuta
mama wa Humph akijiandaa kutoka na Sifa
wakielekea hospitalini.
Baada ya kumuona Lisa alivyovimba macho kwa
kulia walitambua kuwa kuna kitu kinaendelea baina
ya humph na Lisa kwani waswahili wanasema kama
kuambiwa hausikii hata picha ikushinde kuona
kweli? hilo lilikuwa jibu tosha kwa Sifa na mama
yake
Walimjibu jibu lile lile.kuwa Humph hayupo na
wakaomba Lisa awasindikize hospitalini naye bila
hiyana akakubali kuongozana nao.
★★★★★★★★★★
Humph alistuka akiwa kitandani kwake na pembeni
alikuwepo mzee Mandevu
"Nimefikaje hapa?" lilikuwa swali la kwanza la
Humph kwa mzee huyo.
"Usijali kila kitu kimeisha,unastahili pongezi nyingi
na pia sina zawadi ya kukupa ila hayo macho pekee
niliyoyaunda kwa.mikono yangu na wazo
langu,Hongera sana kwa kuifanya dunia kuwa na
amani."
"Asante ila nikushukuru wewe kwa msaada wako wa
hali na mali mpaka.kufikia hapa". alitoa shukrani za
dhati Humph kwa mzee Mandevu
"Nahitaji kuondoka lakini kabla sijafanya hivyo
nahitaji kuitimiza ahadi yangu kwako niliyoahidi"
alisema mzee Mandevu akiwa mwenye furaha muda
wote
"Ahadi gani hiyo mzee?. alihoji Humph
"Nataka nikufanye kuwa.mwenye furaha tena" alijibu
mzeeMandevu
"Jiandae kuna sehemu tunapaswa kufika" aliongeza
mzee Mandevu
Humph alitoka chumbani na kukuta nyumba ikiwa
tupu,akakiendea kifungua kinywa na kujiweka sawa
kisha wakatoka na mzee Mandevu
Lisa,Sifa na mama wa Humph walikuwa wakirudi
nyumbani kutoka hospitalini na Humph pamoja na
mzee Mandevu walikuwa wakiingia hospitalini hapo
kwa njia ya kawaida kabisa hivyo walipishana
kidogo
tu.
Walipofika wodini mzee Mandevu akamuomba
Humph asimame mlangoni ili amlinde mzee
Mandevu ilimradi akamilishe ahadi yake aliyoahidi.
"Ni wakati wa kuamka sasa kwani ndoto uliyoota na
imani imekuchosha mno japo umeifurahia"
akamalizia na maneno hayo mzee Mandevu huku
akimshika mzee Kasai kichwani
"Hatokumbuka lile tukio lililotokea zaidi ya
kufahamu
kuwa alipata ajali ndogo" alisema mzee Mandevu
"Asante sana kwa upendo wako hakika sina cha
kukulipa" aliongea Humph akiwa analengwa lengwa
na machozi
"Usijali tupo pamoja kijana" alijibu mzee Mandevu
"Huu mlango nitaulinda Mimi kuanzia sasa hivyo
ondoa shaka juu ya lolote kumhusu Sor na watu
waliopo katika ulimwengu with(immortals),Kwaheri
na ukihitaji msaada nipo kwaajili yako muda
wowote" alimalizia mzee Mandevu na kutoweka.
"Hatimaye nimekuwa mtu huru sasa,baba ni wakati
wako wa kumuona kijana wako amekua na mwenye
ndoto nyingi za kuijenga dunia,ndoto yako ya kuwa
na.mtoto shupavu na msaada.kwa.kila mtu
imetimia,amka ufurahie Maisha mapya" aliyasema
hayo Humph akiwa pembeni ya baba yake
★★★★★★★★★
Jioni ilifika na Lisa akaelekea katika daraja akiwa
mwingi wa mawazo,kwa.mbali akaanza kuona kama
kuna mtu amesimama pale katika daraja,hamu ya
kumfahamu ikamvaa akajikuta tayari anahisia za
kwamba yule ni Humph
Alikimbia mno na alipofika alimgeuza yule bwana
kwa nguvu akijua ni Humph,akakutana na sura ngeni
yenye mshangao
"Samahani" ni sauti iliyomtoka Lisa
"pumbavu wewe kazi kuvamia usiyowajua,una bahati
hiyo samahani yako imekuokoa sijui ningekufanya ni
ni?" aliongea yule mtu na kuondoka
Lisa alikata tamaa machozi yakazidi kumshuka
lakini
ghafla akakumbatiwa kwa nyuma.Hakuamini
akageuka haraka na kumkuta Humph akiwa na
tabasamu pana
Lisa alimkubatia kwa nguvu Humph wake na kuanza
kusema
"Nisameh....."
"shhhhhhhhh!! usiseme kitu" alijibu Humph
★★★★★★★★★★
Asubuhi iliyofuata familia ilikuwa pamoja katika
kifungua kinywa kasoro mzee Kasai,simu ya mezani
iliita na walipoipokea waliambiwa mzee.Kasai
amerejewa na fahamu,kwa shangwe zote waliwahi
hospitalini na.kumkuta mgonjwa amekuwa.mzima.k
abisa tena katika ubora wake.Familia ya Humph
ikarudisha furaha iliyopotea.
★★★★★★★★★
Humph alistuka toka usingizini akiwa amelowa
jasho
muda huo alikuwa katika basi la chuo cha Sayansi
na teknolojia akiwa na wanachuo wenzake
wametoka katika ziara.
Mji ule haukufanana na mji waliokuwa wakiishi hapo
zamani,huo mji ulipambwa kwa.maghorofa na
majengo pamoja na kila.aina ya usafiri wa kisasa
yote ni.kutokana na kukua kwa sayansi na
teknolojia
Ile ndoto aliyoiota Humph haikujulikana lakini wakati
basi linasonga mbele ghafla mzee.Mandevu
anatokea mbele ya Humph akiwa amempa
mgongo,kwa haraka humph akainuka na kimfuata
pale alipo
Alipomfikia akamgusa begani,Mzee Mandevu
aligeuka na kudondoka Humph akamdaka na
kushuka naye chini taratibu akiwa amemshikilia
vizuri
Mzee Mandevu alikuwa anatokwa damu puani na
mdomoni,aliongea kwa tabu mno mpaka Humph
akawa anadondokwa na machozi "Watu wote
wameungana na Sor na kunigeuka Mimi,wote
wanataka kuitawala dunia yenu" akakohoa kidogo na
bonge la damu likaruka
"Tunza zawadi hiyo niliyokuachia usikubali watu
wanyanyasike,Usikubali hata kidogo watu hawa
wakaitwaa dunia yenu,usikubali waipoteze amani
mliyonayo,pigana mpaka tone lako.la mwisho la
damu na ukumbuke kuwa vita inayokuja ni kubwa
kuliko vita yoyote ile uliyowahi kupigana" alimalizia
maneno hayo ambayo aliongea kwa tabu kuonesha
alipitia maumivu makali sana kabla ya kufika pale.
Alimkabidhi Humph ile fimbo yake kisha kwa
tabasamu pana mikono yake ilong'ang'ania shati la
Humph kisha ikalegea kuonesha tayari amepoteza
maisha.
Humph alilia kwa uchungu mno akiwa tayari
amempoteza mtu muhimu ambaye ni dira kwake na
mwenye thamani ya kipekee sana.
‡‡‡Mwisho wa msimu wa kwanza‡‡‡

Bonge la story...

Chapter Closed...



Cc: mahondaw
 
Riwaya:Macho ya Ajabu 2
Mwandishi:Humph Isack
Mawasiliano:0629314605
Ukurasa:Simulizi Kali na Burudani
Sehemu ya kwanza聽
UTANGULIZI
Maisha huwa ya furaha hasa pale unapokuwa na
wale uwapendao yaani ndugu,jamaa na
marafiki.Lakini maisha haya haya hugeuka majonzi
na huzuni pale unapishindwa kuwalinda uwapendao
na Kuwapoteza katika uso wa dunia ikiwa uwezo na
nguvu za kuwalinda kwa gharama yoyote unazo.聽
NA HUU NI MWANZO WAKE
Mzee Mandevu alipotea kwa mtindo ule uliomuuma
sana Humph na kuweka kidonda kisichopona katika
maisha yake. Mzee Mandevu sasa aligeuka majivu
ambayo yalipanda hewani kama moshi na
kupotelea.
Humph alibaki na fimbo mkononi,alipiga kelele
zilizowastua wanachuo wenzake ndani ya basi,Lisa
akainuka haraka na kumfuata Humph pale alipo
kisha akamuinamia,wanachuo颅 wote waliacha
kufanya mambo yao na kumtazama Humph ambaye
sasa alikuwa na Lisa.
Ilikuwa ni kama filamu Fulani ya kustaajabisha
iliyofikia kwenye utamu na kuwafanya watu
kusikilizia kile kinachojiri.
Lisa hakujali alimtazama Humph lakinj alistuka sana
baada ya kuiona fimbo mkononi mwa humph.
Alipotaka kuhoji hakuiona tena mahali pale,Si
kwamba ilipotea la! Bali ilibaki ndogo kabisa kwa
mfano wa kalamu ya wino.
"Nini kimekusibu mpenzi?,inuka basi
wanakutazama". Lisa alisema huku akijitahidi
kumuinua Hupmh ambaye kwa muda huo miguu
haikuwa na nguvu tena kutokana na mstuko
alioupata.
Lisa alijitahidi lakini hakufua dafu kwa Humph na
nd'o kwanza Humph akaanza kupiga kelele kama
mwendawazimu聽
"Sor! Soooooor!! Nitakuuuwa kwa mkono wangu."
Wanachuo waliposikia vile wakatambua kuwa
huenda Humph kapata uchizi
Wakainuka wanaume kadhaa na kwenda kumshika
kwa nguvu,Basi lilisimamishwa mkufunzi(mwalimu
wa chuo) akatoka kwa dereva kuja kutazama tatizo
lililojitokeza baada ya kusikia kelele kali kutoka
sehemu waliyopo wanachuo ambao ni upande wa
abiria.
"Amepatwa na nini? Na mbona mmemshikilia
hivyo?" Alitupa maswali mkufunzi Mara baada tu ya
kuingia upande wa abiria na kuikuta hali ile
isiyoelezeka聽
"Ameanza kupiga kelele hovyo,mi nahisi atakuwa na
homa Kaliinayomsabaishia kichaa ama maumivu
makali." Alijibu mmoja wa wanachuo wale聽
Lisa alikuwa ameweka mikono mdomoni akilia
taratibu baada ya kuiona hali ile iliyomkumba
Humph.
"Muwekeni kwenye siti mkae nae huku na huko
hakikisheni hatoki mpaka tutakapofika hospitali"
Mkufunzi alimalizia na kurudi kwa dereva kwaajili ya
kuiendeleza safari.
********************颅***
Simu ilipigwa nyumbani kwa kina Humph na
kupewa taarifa kuwa wanahitajika hospitalini.
"Hellow! Mrs Kasai hapa naongea" Mama wa
Humph alijitambulisha baada ya kupokea simu聽
"Dokta Alex Jr hapa naongea,u mzima shemeji?"聽
"Ooooh! Ni wewe shemeji,nimeipotea kabisa sauti
yako,nipe habari?" Mama wa Humph alijibu kwa
furaha聽
"Kuna tatizo dogo limejitokeza kwa mtoto wetu
Humph,kama hutojali naomba ufike Mara moja"
Dokta Alex alijibu聽
"Mmmh! Ni salama kweli Shemeji?" Mama wa
Humph alipata wasiwasi
"Usiwe na hofu.Usalama upo" Dokta Alex alijibu na
kukata simu聽
Mama wa Humph alitoka nyumbani mbiombio,akiwa
njiani anampigia simu mumewe na kumpatia taarifa
kuwa wakutane hospitali kwa dokta Alex Jr,Dakika
chache anafika na kumkuta Lisa mapokezi.
"Mamaaa!!" Lisa anamkimbilia mama wa Humph na
kumkumbatia machozi yanamtoka聽
"Kuna nini kimetokea mbona unalia?" Mama wa
Humph aliuliza聽
"Humph mama Humph,sielewi hata amekuwaje
mama,naogopa Mimi" Lisa alijibu kwa kilio huku
akizidi kumkumbatia mama Humph kwa nguvu聽
"Atakuwa salama msijali" Sauti ya mzee Kasai ilijibu
kutoka ilisikika ikijibu聽
"Afadhali umekuja mapema,twende kwa dokta"
mama wa Humph alisema huku akimtoa Lisa baada
ya kuwa wamekumbatiana kwa muda na kumfariji
kwani alifahamu wazi anavyompenda mwanae聽
"Ndiyo Dokta Alex Jr nipe ripoti" alianzisha
mazungumzo mzee Kasai聽
"Aaaah! Hakuna kitu kibaya kilichompata kijana
ila...?" Dokta Alex Jr hakumaliza ile kauli Mzee
Kasai akadakia
"Najua si salama Dokta,tafadhali nahitaji kufahamu
hali ya mwanangu"聽
"OK! Ok! Ni mstuko tu uliompata na Mara kwa Mara
anamtaja mtu au kitu nadhani,kila anapoamka ama
akiwa usingizini* Dokta alijibu聽
"Mstuko?, aaah! Na hilo neno au jina? Hebu
nieleze." Mzee Kasai aliongea kwa mshangao na
jazba iliyojionesha wazi wazi聽
"Anataja neno Sor,Mara nitakuuwa,ila "Sor" hilo neno
analitaja Mara nyingi mno". Dokta Alex Jr alieleza na
kumfanya mama wa Humph kumgeukia Lisa聽
"Unamfahamu huyo Sor au hicho kitu kinachoitwa
Sor?" Mama Humph aliuliza akiwa na shauku ya
kutaka kufahamu聽
"Hapana mama hata Mimi nilimsikia Humph anataja
hilo jina akiwa amekaa ndani ya basi na hapo ndipo
tatizo lilipoanzia" Lisa alijibu kwa kilio cha kwikwi聽
"Jamani Mimi na madaktarj wenzangu tunejitahidi
sana kumfanyia uchunguzj wa kumrejesha katika
hali yake ya awali lakini imeshindikana." Dokta
akaweka kituo na kuwatazama nyuso zao聽
"Oooooofu! Mwanangu Mimi" Mama Humph
alilalamika huku pumzi ikiwa inapishana juu chinj聽
"Hivyo uamuzi uliofikiwa ni kwamba kama mnahitaji
apone inatubidi tukubaliane kitu na kama sivyo
ataathirika sana huyu na itachukua muda mrefu
mpaka apone kabisa japo si kwa asilimia mia
moja,hapa naamanisha hatokuwa na akili timamu."
Dokta Alex Jr alieleza kwa kina
"Nachohitaji ni mwanangu apone,tafadhali nieleze
kipi cha kufanya" Alijibu kwa upole mzee Kasai
huku akimtazama mkewe kwa jicho la huruma聽
"Vyema sana mzee Kasai sasa ili arudiwe na
ufahamu asilimia mia moja ni lazima tuifute
kumbukumbu yake ya matukio ya nyuma,kisha
atapandikiziwa kumbukumbu mpya" Dokta Alex
aliiongea kwa kujiamini聽
Lisa aliuona ugumu hapo kwani ni wazi kuwa kuna
hati hati ya kusahaulika kabisa kichwani mwa
Humph聽
Lisa alijiandaa kuweka mgomo maana alifahamu
vyema hata siri ya Humph jinsi alivyo,ikitokea
amefutwa kumbukumbu basi kila kitu kitakuwa
kimeishia pale.
Akiwa anawaza namna ya kupinga kwa hoja ghafla
akagutushwa na sauti ya Dokta聽
"Binti naomba utoke nje Mara moja kuna mambo
tunahitaji kuyajadili hapa" Dokta alimstukiza lisa
kwa mtindo huo聽
"Lakini..." Lisa akataka kujitetea mzee Kasai
akamuwahi na kumkata kauli聽
"Usijali binti kila kitu kitaenda vile inavyotakiwa"聽
Lisa bila hiyana akaondoka tarafibu
"Hatuna namna baba humph suala mtoto apone
maana najisikia uchungu mno" Mama Humph
aliongea machozi yakimtiririka聽
"Sawa mke wangu, Dokta nadhani umesikia na
unajua la kufanya mpaka sasa,kwa lolote nitaarifu"
mzee Kasai aliiongea akiwa amejikaza kisabuni
Hatimaye Walitoka wote na kufika wodini,Humph
akiwa kitandani anaweweseka huku Mara kwa Mara
akimtaja Sor,Mama Humph akamkumbatia mumewe
machozi yakizjdi kumtoka kwa uchungu.
Je unafikiri ni kitu gani kitamkuta Humph? Na je
vipi kuhusiana na Sor ndo amekufa mazima au?聽
Huu ni mwanzo tu usikose kufuatilia moto huu.
 
Sehemu ya pili
.....Ilipoishia.......
Hatimaye Walitoka wote na kufika wodini,Humph
akiwa kitandani anaweweseka huku Mara kwa Mara
akimtaja Sor,Mama Humph akamkumbatia mumewe
machozi yakizjdi kumtoka kwa uchungu.
.......Shuka nayo.........
Ukweli Ni kwamba alimuonea Huruma mno
mwanaye.
Lisa alirudi nyumbani kwao akiwa mpweke
ajabu,mawazo yalimtafuna mwili mzima,hata taxi
aliyopanda hakukumbuka kulipa baada ya
kufikishwa kwao. Dereva alishuka upesi na
kumfuata akiwa nusu akikimbia na nusu kutembea.
Kabla Lisa hajaingia getini mwa nyumba yao
akasikika dereva akiita kwa nguvu
"Binti!,Binti!" Lisa hakugeuka alizidi kuendelea na
safari
"Hela yangu vipi we binti?" Dereva alimvuta Lisa
blauzi huku akiuliza kwa ghadhabu
"Hela gani?,we nani kwanza?" Lisa alionekana
kumshangaa yule dereva ambaye sasa sura ilianza
kutengeneza matuta ya hasira.
"Kwani hii gari uliyopanda ni ya baba yako eti
wewe?" Dereva alihoji kwa hasira huku akimtikisa
Lisa ambaye hakuwa akijali kitu,hali iliyopelekea
mzozo mkali baina yao.
Mlinzi wa getini kwa akina Lisa alitoka nje mbio
mbio na kuanza kuamua kesi ile asiyoijua ndipo
Lisa akapata upenyo wa kuingia ndani akimuachia
mlinzi kasheshe ile..
Mpaka asubuhi Lisa alikuwa na kazi ya kuitazama
picha ya Humph biila kupata majibu ya kile
anachokiwaza. Alivyoona kumekucha akajiandaa na
kuelekea hospitali,alimkuta mama wa Humph akiwa
pale usiku mzima ulimuishia pale bila kujali chakula
wala kutafuta mahali sahihi pa kulala.
Alifika na kumuamsha taratibu mpaka
akaamka,baadaye waliingia wodini baada ya
kuruhusiwa kwenda kumtazama Humph.
Lisa aliketi kitandani na kumshika Humph kichwani.
"Dokta amesema mchana atakuwa ameshaamka
hivyo usiwe na shaka sawa mwanangu" mzee Kasai
alimwambia Lisa
"Sawa baba" Lisa alijibu
Mchana unafika Humph anafumbua macho taratibu
Lisa anawahi kumshika mkono na kutabasamu
lakini Humph haoneshi hata dalili ya
kutabasamu,Dokta Alex anaingia na manesi wawili
baada ya kuitwa
"Mfanyieni utaratibu wa kula" alizungumza Dokta
Alex wakati amemaliza na kumcheki Humph.
"Usiwe na hofu binti rafiki yako ni mzima kabisa na
baadaye ataruhusiwa,jitahidi kuwa naye karibu
maana vitu vingi hakumbuki hapo alipo tuliweka
kumbukumbu ya vitu vichache"
"Dokta Alex alimwambia Lisa na kumfanya aduwae
kidogo na kutambua kitu kipya kuwa Humph
hakutabasamu kwasababu hamkumbuki.
Baada ya Humph kuruhusiwa na kurudi nyumbani
Lisa alikuwa naye karibu mno kwa kila kitu lakini
kwa Humph haikuwa hivyo yeye alimchukulia
kawaida tu.
Lisa hakuona shida,wakati wameketi pamoja Lisa
aliamua kuanzisha maongezi ili kumuweka sawa
Humph.
" Hey,um! Nilisahau kujitambulisha toka awali
uliponiona,naitwa Lisa ni rafiki pekee wa karibu
kwako nikiamanisha "girlfriend" wako tangu tukiwa
tunasoma sekondari" Lisa aliongea huku akiminya
vidole vyake
"Ongeza Sauti kidogo mdada sijakusikia vyema"
Humph alijibu kwa pozi huku akiondoa (spika
ndogo za masikioni) earphone.
"Naitwa Lisa Ni mpenzi wako wa siku nyingi" Lisa
alijibu akiwa ameanza kukasirika kutokana na tabia
mpya aliyokuwa nayo Humph
"Mmh! Mpenzi tena,aaah! Sidhani,mbona sijawahi
kuwa na mpenzi,wewe Ni wa wapi labda?" Humph
akauliza kwa madoido akionesha wazi
kutomfahamu Lisa kiundani.
Lisa akatoka mbio analia mlangoni akapishana na
mama yake Humph lakini hakumsemesha,licha ya
mama Humph kujaribu sana kumuita Lisa bado
haikusaidia
"Umemfanya nini mtoto wa watu?" Ilikuwa Ni kauli
ya kwanza ya mama Humph baada ya kuingia ndani
na kumuuliza Humph
"Sijui,mi' amejitambulisha kuwa ni mpenzi
wangu,nikamuuliza wa wapi maana sijawahi kuwa
na mpenzi,ndipo akachukia na kutimua mbio huku
akilia" Humph alijibu bila wasiwasi Ni kama alikuwa
akiongea na rafikiye.
"Umeonesha dharau kubwa sana mbele yake,yule
msichana amejitoa kwa hali na mali isitoshe Ni wa
kwako kwa muda mrefu sasa haukupaswa
kumfanyia vile,hakustahili kwa kweli" mama Humph
alilalama
"Mama simfahamu yule binti na sitokaa nimfahamu
kamwe,na kama Ni wangu kwanini asiwemo karika
kumbukumbimu zangu za kila siku" Humph alisema,
mama Humph na mumewe pamoja na familia nzima
waliapa kukaa kimya kuhusu matatizo ya Humph ili
yasijirudie hivyo hawakuthubutu kusema lolote
"Kamuombe msamaha,mjinga mkubwa wee!"
Humph akainuka huku akiongea "sijamkosea mimi "
Mama Humph akaishia kutikisa kichwa tu huku
akionekana kutofurahia tabia mpya ya Humph
iliyotokana na kufutwa kumbukumbu zake
zilizoondoka na mambo mengi mno,mpaka wazazi
wake alikuwa akiwachukulia kama jamaa wa
kawaida walio karibu yake.
鈽呪槄鈽匤ourney to the falling Mountain鈽呪槄鈽?
鈽呪槄鈽匰afari ya mlima unaoanguka鈽呪槄鈽?
"Habari za asubuhi hii ndugu wanachuo,nafurahi
kufika siku hii ambayo imerejea tena mbele
yetu,kwa wale wageni wa mwaka wa kwanza yaani
wanachuo wapya hawalitambui suala hill na itakuwa
Ni Mara yao ya kwanza kulisikia" Akatulia kidogo
Mkuu wa chuo msaidizi akitafakari usikivu wa
wanachuo kwa muda kisha akaendelea
"Tuna mashindano mbalimbali ambayo huendeshwa
na kufanyika nje ya chuo chetu yakijumuisha vyuo
vingi vinavyotuzunguka,na kawaida yetu huwa
tunafanyia mashindano haya katika kisiwa cha
falling mountain (mlima unaoanguka) pia tutakuwa
na utalii wa muda katika milima yake na misitu pia
inayosemekana kubeba utajiri mkubwa pamoja na
kishamiri maajabu mengi ya kihistoria"
Wanachuo wote wakalipuka kwa shangwe nyingi
lakini mkuu wa chuo msaidizi hakuwa amemaliza
hivyo akanyoosha mikono kuwanyamazisha
wanachuo wote
"Hatuna muda mwingi,kesho safari itaanza na
niseme tu poleni kwa kuwastukiza,natumaini
mtajiandaa kuanzia sasa" alimalizia Mkuu wa chuo
msaidizi na kuwaacha wanachuo wote wakilipuka
kwa shangwe nyingi ikiwemo Humph
Lisa hakuwa na furaha hata kidogo mbaya zaidi
alimuona Humph alivyoifurahia safari ile ikiwa si
kawaida yake kabisa.
"Mambo mdada" Lisa akistukia akisalimiwa na
alipogeuka aliduwaa kuona ni Humph,akabaki
kujiuliza ni saa ngapi mtu yule amemfikia lakini
ukweli ulibaki kuwa muda alioutumia kuzama katika
dimbwi la mawazo ndiyo muda alioutumia Humph
kufika pale.
"Poa tu" Lisa alikumbuka kuijibu salamu ya Humph
lakini akiwa mnyonge mno
"Samahani,ulisema u nani vile?" Humph aliuliza
akiwa anatazama huku na kule
"Lisa" Lisa alijibu kwa mkato huku akimtazama
vyema Humph ambaye hakujua kama binti huyo
alikuwa akimuangalia.
"Sikia binti,Jana nusura mama apasuke ulivyotoka
unalia,sasa Fanya yaishe maana hapendi kabisa
nikichokifanya kwako" Humph alisema akiwa
anamuangalia binti mmoja aliyekuwa
anatabasamu,macho yao yakagongana
"Yameisha toka Jana Humph" Lisa alijibu akiwa
hana amani
"Poa,alafu nimempenda yule mdada sijui anaitwa
nani?,hey! Vipi unamfahamu hata kwa jina labda?"
Humph alimuuliza Lisa akiwa bado anamtazama
yule binti.
Lisa hakuvumilia ule upuuzi ulioonekana dhahiri
kuwa ni dharau kutoka kwa Humph,akaamua
kuondoka kimya kimya.
Humph anakuja kugeuka baada ya kukosa
jibu,anamkosa Lisa pale alipokuwa
amesimama,akaangaza huku na kule asimuone
kutokana na uwingi wa wanachuo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom