Simulizi: Macho ya ajabu

Simulizi: Macho ya ajabu

Sehemu ya ishirini na moja
........Ilipoishia..........
"Humph Mimi namtaka Yule rafiki yako ambaye
aloniokoa kuna kitu natamani nimwambie tukiwa
wawili hivyo nahitaji msaada wako unikutanishe
nae" Lisa alijitetea
.......Tiririka nayo........
Humph alivyosikia hivyo akabaki na mshangao
maana ule ulikuwa ni mtihani ambao kwa mtazamo
wa kawaida si rahisi kukubaliana nao japo kwa
upande mwingine Humph aliona kama ndiyo muda
wa kumpata lisa.
"unataka kuonana nae lini na umwambie nini kwa
mfano maana hapatikani kiurahisi kama unavyoona
sasa ikibidi niagize nami nitafikisha ujumbe"
aliongea Humph akitarajia kuambiwa kile
kinachomsibu Lisa
"aaaah!! hapana hii ni siri yangu na yake Kama
hautaki kunisaidia basi yaishe" aliongea Lisa kwa
sauti iliyokata tamaa
Humph akajifikiria kwa sekunde kadhaa akaamua
akubali ombi la Lisa
"unakumbuka pale ambapo huwa tunakutana "
aliuliza Humph
"Wapi au pale katika lile daraja?" Lisa ailuliza nae
akijaribu kukumbuka eneo lile
"yap pale pale ndipo nitamwambia mkutane saa
moja usiku sawa" aliongea Humph
"Nitashukuru kama nikimuona" alijibu Lisa
★★★★★★★★★★★
Upande wa Sor mambo yalikuwa yamemwendea
kombo kila akibuni mbinu mpya inagundulika
mapema na Humph sasa muda huu alikuwa katika
pango moja kubwa akitafakari ni kitu gani cha
kufanya ili amtie adui yake mikononi.
Alifikiria sana ili apate njia mpya itakayo mtesa
vilivyo bwana mdogo Humph lakini suala
lililomuumiza hasa ni jinsi gani atakavyompata
maana watu wake wengi wanazidi kuteketea na pia
anatumia nguvu nyingi kuwatengeneza.
akiwa katika mawazo hayo ghafla akakumbuka
kuwa kuna kisiwa kimoja ambacho hakuna
binadamu mwenye uwezo wa kufika kule isipokuwa
wa jamii yao tu na endapo utatupwa huko ni shida
mtindo mmoja mpaka pale mauti itakapo kufika.
Sor aliafiki hilo wazo moja kwa moja na muda huo
huo akaanza kujipanga namna ya kumpeleka
Humph huko maana bila ujanja hawezi kufanikisha
azma yake.
★★★★★★★★★★★★★★★
Lisa alikuwa ameupara kweli kweli akiwa na shauku
ya kukutana na Humph pamoja na kijana ambaye
alimkomboa katika hatari nyingi zilizomkumba.
Alifika eneo la tukio nusu saa kabla,yote ni
kwasababu ya uhitaji wa moyo wake kuwa karibu na
mtu yule. Alikaa mno akisubiri mpaka wakati
mwingine alihisi huenda dakika zimeganda japo
hakuchoka hata chembe kusubiri kile alichoahidiwa.
Mvumilivu hula mbivu hatimaye muda uliwadia
lakini bado dalili yoyote haikujionesha kuwa Humph
au yule kijana anakuja.
Kumbe muda wote ambao Lisa anasubiri Humph
alikuwa amesimama mahali anamtazama jinsi
anavyohangaika kutoka sehemu moja kwenda
nyingine huku anaminya minya vidole vyake.
Humph hakuwa na amani juu ya kile ambacho
anaenda kuambiwa na alihisi wazi kuwa Lisa
atakuwa na mapenzi mazito moyoni mwake.
Humph alijishauri na mwisho akaamua liwalo na
liwe,akavuta kitambaa chake usoni na kofia yake
akaiweka vizuri kisha akaanza kusogea pale alipo
Lisa.
Lisa alimuona mtu akija kwa upande
wake,Hakumfikiria sana kama anaweza kuwa ni mtu
yule ampendae,baada ya Humph kusogea jirani
kabisa ndipo Lisa anamtambua na kwa kitendo cha
kustukiza anamrukia Humph kwa furaha naye
Humph bila kutegemea anamdaka kisha wanabaki
wanatazamana huku Lisa akitoa tabasamu la
ushindi.
Kwakuwa Humph alikuwa katika vazi lake la kazi
haikuwa rahisi kufahamika,Lisa anashushwa chini
taratibu kisha Humph anasogea jirani kabisa na
daraja lile akiwa na lengo la kuyatazama maji hii
ilikuwa ni kwa muonekano lakini akili yake ilimtuma
amuulize Lisa anakusudia nini bila kumtazama
usoni.
Lisa anaduwaa kwa muda akiangalia tukio
analolifanya Humph.Anaamua kumsogelea Humph
kwa mwendo wa madaha kulingana na viatu vya bei
kali alivyovaa.
Kabla Lisa hajamfikia Humph,Humph anaanza
kuzungumza kwa sauti nzito tofauti na ile sauti yake
iliyozoeleka masikioni mwa Lisa.
"Nimeambiwa na rafiki yangu wa karibu kuwa una
jambo la msingi unataka kuniambia,nipo hapa
kukusikiliza" Alifafanua Humph bila kugeuka nyuma
"Samahani kama nitakuwa nimekukwaza na
kukupotezea muda wako" Lisa akatulia kidogo
akimtazama Humph na kuendelea
"Naitwa Lisa na..na..na..?" akashindwa kumalizia
akashikwa na kigugumizi
Humph anautumia udhaifu huo wa Lisa kugeuka na
kumkazia macho ambayo yanawaka mwanga hafifu
usiotisha
"Mbona unasita Lisa niko hapa kwaajili yako nieleze
tu" Aliongea Humph kwa upole
Lisa akajipa moyo kuwa ni kheri kusema ukweli
kuliko kufa na maumivu moyoni ikiwa mtu
anayepaswa kuambiwa ukweli huo yu karibu nae na
ametahayari kumsikiliza kile akisemacho
"Usinifikirie vibaya ni moyo wangu nd'o umenituma
hili na hisia nzito nilizonazo kwako ni...." Kabla
hajamalizia kusema lile suala huku anaminya vidole
vyake kelele kubwa ikasikika kutoka upande wa pili
Ilikuwa ni sauti ya mwanamke akiomba
msaada,Humph bila kuchelewa akakurupuka na
kukimbilia eneo ambalo sauti imetokea.
Lisa alishindwa kumzuia Humph na pia kutokana na
kitendo cha Humph kuondoka eneo lile Lisa aliona
kuwa hajatendewa haki hata chembe kwani hakuwa
amemaliza kusema yaliyo moyoni mwake. Alibaki
amekaa pembeni ya daraja lile asijue nini cha
kufanya kati ya kumfuata Humph anakoenda au
amsubiri aone ni kipi kitakachotokea.
Humph alipofika eneo la tukio alishuhudia mama
mmoja akiwa anazunguka huku na kule mara ashike
kichwa nakuachia na wakati mwingine alikuwa
akipiga magoti pembeni ya bwawa linalopitisha
maji eneo lile.
Kwa ufahamu wa haraka Humph alitambua kuwa
kuna mtu ametumbukia katika bwawa lile.....
 
Sehemu ya ishirini na mbili
........Ilipoishia.........
Kwa ufahamu wa haraka Humph alitambua kuwa
kuna mtu ametumbukia katika bwawa lile...
.......Tiririka Nayo......
Humph alipomfikia yule mwanamke aliyeonekana ni
mtu mzima kiasi aliambiwa"nisaidie,naomba
unisaidie tafadhali,mwanangu jamani mwanangu
anakufa"
Humph hakusubiri amri itoke ya kusema tumbukia
umuokoe mhanga huyo ila yeye mwenyewe
alijirusha ndani ya maji japo alikuwa na wasi wasi
kuwa tangu amezaliwa hajawahi kujifunza kuogelea
na wala hakuwa na ujuzi huo.
Kiukweli ni kwamba Yale macho ambayo aliyapaya
Humph yalikuwa ni ya ajabu kweli maana hamna
kitu ambacho aliwahi kushindwa kufanya yote
aliweza katika sehemu zenye hatari mbalimbali.
Basi baada ya Humph kutumbukia katika bwawa lile
mwanga wa macho yake uliongezeka na kumfanya
aweze kumuona mtoto ambaye tayari alikuwa
ameishiwa nguvu na kuzama maji hivyo bahati
ikawa upande wake baada ya Humph kumtoa ndani
ya maji.
Alikuwa ni mtoto mkubwa kiasi wa kike ambaye
nd'o kwanza dodo zake zilikuwa zimeanza kuchanua
wale wenzetu wanaita maua saa sita na huku kwetu
tunaita "matiti" sasa na kile kigauni chake
kilivyokuwa kimelowa na kushikana na mwili
kikamfanya Humph aogope kumpa huduma ya
kwanza.
Lakini kwa kuwa Yule binti hakutakiwa kufa Humph
aliamua kujikaza kiume na kumpandia(kumkalia)
kwa juu kisha akaanza kumminya tumbo binti yule
lililotoa maji mengi mno kupitia mdomoni hii
ilidhihirisha wazi kuwa ni jinsi gani binti huyo
alikunywa vibaba bila kipingamizi.
Humph alijitahidi kumsaidia binti yule mpaka pale
alipoanza kukohoa mfululizo na mwisho akawa
amerudiwa na fahamu,mama yake alisogea jirani
kumtazama mwanae huku akiwa amejishika kifua
kuonyesha kuwa presha na hofu vimeanza
kupungua.
Lisa alifika mpaka eneo la tukio kwa hatua mnyato
(za kunyatia) ikiamanisha kuwa amepoteza
matumaini ya kumwambia Humph kilichopo moyoni
mwake.
Humph aliinuka pale alipokuwa binti yule na mama
yake lakini punde tu baada ya kugeuka nyuma
alikutana ana kwa ana na sura yenye majonzi,sura
iliyochoka kuvumilia,iliyopoteza tabasamu,hiyo
ilikuwa sura mpya na mwonekano mpya wa Lisa
Humph aligundua udhaifu uliompata Lisa kwa muda
huo mchache na kabla hajaamua kupiga hatua
kumfuata Lisa pale alipo alisikia sauti ile ipendayo
kusema naye ikimwambia "Huyo binti anakupenda
kwa dhati toka moyoni mwake ila chunga sana kaa
mbali nae muda ukifika mtakuwa pamoja"
Kwakuwa Humph huwa anaiamini sana sauti ile
hakutaka kupingana nayo alienda moja kwa moja
mpaka kwa Lisa,alipomfikia alimshika begani na
kumwambia maneno machache kwa upole
"Samahani Lisa natambua kuwa nipo hapa
kwasababu yako lakini ni jukumu langu kuwasaidia
watu wenye kuhitaji msaada wangu wakati wowote
na pia naomba radhi Kwakuwa inanibidi kuondoka
maana nguo zote zimelowa tafadhali naomba
uniruhusu"
Lisa hakuwa na namna pia hakutaka kuonekana
mbishi ikiwa hata hajammiliki mhusika,aliitikia kwa
kichwa japo moyoni alikuwa akihisi amepigiliwa na
msumari wenye ncha kali.
Humph aliondoka bila hata kuwaaga wale watu
aliowasaidia hii yote ni kwasababu huwa anaogopa
sana kushukuriwa(shukrani) ikiwa kuokoa ni moja
ya jukumu lake.
★★★★★★★★★★★★★
Asubuhi na mapema Humph alikuwa shuleni,akiwa
darasani katika meza yake ghafla anapatwa na zile
ndoto zake za mchana aka tuite maono kuwa Sor
alifika shuleni hapo na alikuja akiwa kama mzazi
Alipofika ofisini akaomba kuonana na mwalimu
Jona ambaye muda mfupi ujao ana kipindi darasani
kwa kina Humph,Baada ya kuingia ofisini kwa
mwalimu jona akadai kuwa anahitaji mwanafunzi
Humph akitoka mapumzikoni amfuate Sor katika
mgahawa wa shule.
Kutokana na uzuri alionao Sor haikuwa rahisi kwa
mwalimu jona kukataa ombi lile.Sor aliaga na kabla
hajaondoka alimpa mwalimu jona mkono huku
tabasamu murua likiupamba uso wake.Mwalimu
jona alijikuta katika wakati mgumu baada ya
kuambatanishiwa mkono na hela kisha akakonyezwa
naye bila shaka lolote akajibu kwa kutabasamu.
Humph alistuka darasani na aliona hatari
inamkaribia na Kwakuwa hakuwa mbali na dirisha
alitupa macho koridoni hakufanikiwa kuona
chochote. Baada ya dakika kadhaa alitupa tena
macho koridoni yote hii ni kutokana na wasi wasi
aliokuwa nao,Hakuambulia chochote na alipotaka
kurudisha macho katika meza yake alihisi kivuli
kimesimama dirishani.
Alipoangalia tena akakumbana na sura yenye mvuto
iliyopambwa kwa tabasamu jepesi lenye kunakshiwa
na vishimo vidogo vilivyotumbukia mashavuni mwa
mrembo huyo ajulikanaye kama Sor na mwisho
akapotea na kumfanya Humph apige kelele ni kama
mtu aliyestuka usingizini kutokana na ndoto mbaya
iliyomkumba.
Kumbe wakati Humph anakurupuka baada ya
kumuona adui yake Sor na mwalimu jona alikuwa
anaingia darasani akiwa na macho mekundu mno
tofauti na alivyozoeleka.
Mwalimu jona alisimama mbele ya darasa na
kuitikia salamu ya wanafunzi wake kisha
akamuamuru Humph asogee mbele nae akatii amri
hiyo.
Mwalimu jona bila kuuliza swali alishusha vibao
viwili vya nguvu kwa Humph na kumkwida shati
lake nadhifu na kuanza kuondoka akiwa amemkwida
(kumkunja) vile vile huku akiwaacha wanafunzi
midomo wazi.
Mwalimu Jona alifika ofisini na kuanza kumpiga
Humph ovyo ovyo hali iliyopelekea walimu wengine
kutoka katika ofisi zao kushuhudia mkasa huo
ambao ulikuwa ni kama filamu ya kuigizwa.
Kumbe wakati mwalimu jona akiwa anampiga
Humph,Humph alikuwa akifanya kazi ya kupangua
bila kurudisha mashambulizi huku kichwani akiwa
anajiuliza ni jinsi gani atamsaidia mwalimu huyo.
Mwalimu jona alizidisha kipigo kwa Humph,Humph
akaanza kupandwa na hasira na mwisho macho
yake yakaanza kutoa nuru taratibu na kwa bahati
nzuri mwalimu Remijo alikuwa pale akishuhudia
tukio lile.
Mwalimu Remijo alipoona ile nuru machoni kwa
Humph aligundua kuwa lazima mwalimu jona
atapigwa kipigo ambacho hajawahi kuona toka
amezaliwa hivvyo kwa akili za haraka haraka
alichukua jukumu la kuingia katikati ya Humph na
Mwalimu jona.
 
Sehemu ya ishirini na tatu
........Ilipoishia..........
Mwalimu Remijo alipoona ile nuru machoni kwa
Humph aligundua kuwa lazima mwalimu jona
atapigwa kipigo ambacho hajawahi kuona toka
amezaliwa hivvyo kwa akili za haraka haraka
alichukua jukumu la kuingia katikati ya Humph na
Mwalimu jona.
★★★shuka nayo★★★
Walimu wengine walivyoona vile ndipo na wao
wakapata akili ya kwenda kumshika mwalimu
Jona,Mwalimu Remijo alimchukua Humph mpaka
ofisini mwake na kumkalisha katika kiti na alikuwa
na mshangao wa wazi wazi juu ya ile nuru machoni
mwa Humph maana hakuwahi kubahatika kuiona
zaidi ya kusimuliwa na watu waliowahi kumuona.
Humph alitulia kwa muda akijitahidi kuwa kama
awali yaani kuzishusha hasira zake mpaka
akafanikiwa,kwa wakati wote huo alipokuwa
akiyafanya hayo nwalimu Remijo alikuwa
amemkodolea macho bila kupepesa ni kama
kamdoli Fulani hivi.
Baada ya Humph kurudi kawaida aliinua uso wake
na kumtazama madam Remijo ambaye alistuka
kama amepigwa shoti ya umeme kisha akaangalia
pembeni kwa hofu ya kile alochokiona.
Mwalimu jona hakukubali kushikwa kirahisi namna
ile alianza kufurukuta na kuleta fujo,aliwamwaga
watu watano chini na kabla hajaifikia ofisi ya
mwalimu Remijo waalimu wale walimuwahi na
kumshikilia
walivutana huku na huko lakini mwalimu jona
alionekana ananguvu fulani inamsaidia nd'o Maana
amawashinda walimu wenzake,kwa Mara nyingine
tena akawatupa mbali na kuifuata ile ofisi ya
madam Remijo alipoufikia mlango Humph alikuwa
tayari amechezwa na machale akawahi kuuzuia
mlango.
Mwalimu Jona alijitahidi kusukuma mlango lakini
ikashindikana akaamua aanze kupiga "push",Walimu
walipoona kuwa mwalimu jona hakamatiki ikabidi
waombe msaada kwa walinzi ambao walikuja
haraka haraka na bila kuchelewa mlinzi mmoja
akawahi kumzimisha mwalimu jona.
Humph alibaki ameshikilia mlango jasho likiwa
limemtoka haswaaa,madam Remijo alikuwa
anatetemeka kwa uoga. Mlango uligongwa na
madam Ode ndipo Humph akafungua nakutoka
akifuatiwa na madam Remijo.
Walinzi na baadhi ya walimu walimsaidia mwalimu
jona kwa kumbeba mpaka kivulini na kuanza
kumpepea. Humph alitambua kila kitu
kinachoendelea lakini hakutaka kuzungumzia habari
zile.
Mwalimu jona aliamka akiwa anajishika kichwani ile
sehemu aliyopigwa mpaka akapoteza
fahamu,aliangalia kushoto na kulia akakuta kila mtu
anamwangalia yeye kwa macho ya kiulizo ikabidi
avunge lakini akagundua kuwa wote wanamshangaa
yeye akaona bora avunje ukimya
"Ndugu walimu mbona tunaangaliana hivyo kuna
tatizo gani na kwanini niko hapa?"
"Ina maana wewe hautambui ulichokifanya eti?"
alijibu mwalimu mmoja kwa jazba
"kwani nimefanya nini jamani mbona mnaniweka njia
panda" aliendelea kujitetea mwalimu jona
★★★Ilivyokuwa★★★
Wakati Sor akiwa anajiandaa kwenda katika shule ya
St.Machele alichukua noti moja Kisha akanuia
maneno kadhaa ikapotelea mkononi mwake kisha
akaianza safari ya kuelekea shuleni.
Alipokanyaga tu ardhi ya shule ya St.Machele
akapata jina la mwalimu jona ambaye muda mfupi
ujao alitakiwa aingie darasani kufundisha hivyo
mtego wa Sor ukawa umeshika penyewe.
Baada ya mazungumzo kati ya Sor na mwalimu
jona,Sor alipndoka na kumuacha mwalimu jona
akiwa anaitazama ile noti ambayo
alipewa na Sor lakini ghafla alianza kuhisi
kizunguzungu na mwisho akadondoka chini.
Zilipita dakika mbili mwalimu jona akainuka akiwa
katika muonekano mpya yaani macho yake yalikuwa
mekundu tofauti na hapo mwanzo.
Sor alifika mpaka katika darasa la kina Humph
katika dirisha lililopo usawa wa Humph,Sor alikuwa
katika sura nzuri yenye mvuto iliyomfanya Humph
abaki na.kiwewe kutokana na uzuri aliokuwa nao
Sor
Mambo yalibadilika ghafla baada ya Sor kubadilika
na kuwa na sura mbaya isiyoelezeka iliyomfanya
Humph apige kelele na muda huo huo mwalimu
jona alikuwa amewasili lengo ikiwa si kufundisha ila
kumtia adabu Humph kulingana na nguvu zile
zinavyomwendesha katika ufahamu wake wa akili.
★★★★★★★★★★
Madam Remijo alimsaili Humph maswali machache
kuhusu lile tukio na baada ya kuelewa
kinachoendelea alimuomba Humph akamtetee
mwalimu jona ili kibarua chake kisipotee kwaajili ya
kosa ambalo hakulifahamu.
Humph alitoka ofisini na kuwafuata walimu
walipokuwa wamesimama wakimshangaa mwalimu
jona kwa mbwembwe anazowafanyia ambazo katu
hazikuwaingia vichwani mwao wao kama wasomi.
"Mwalimu jona samahani kwa kufanya vile.haikuwa
dhamira yangu hivyo naomba unisamehe nimekosa
sana" Aliongea Humph kwa sauti ya majuto
Walimu wote walishangaa kile anachokiongea
Humph maana hawakuelewa anaamanisha nini na
wakiwa katika mshangao na mwalimu Remijo nae
anakazia kile alichokiongea Humph lengo likiwa.ni
kusafishia njia mwalimu jona.
"Jamani walimu wenzangu naombeni mnielewe kwa
hili,mwalimu mwenzetu hapo.alikuwa akiendeshwa
na hasira na ikawa si rahisi kujitawala(kucontrol)
hivyo kwa niaba yake naomba tumsamehe kwa hilo"
alihitimisha mwalimu Remijo
"Ni kweli kabisa nilikuwa na hasira ghafla nikamvaa
kijana huyu,naombeni mnisamehe na hili tatizo
halitoweza kujitokeza tena" Alijitetea mwalimu jona
Walimu wote walishindwa la kufanya ikabidi
wakubali kwa shingo upande kuwa suala lile
limeisha kabisa.
Humph aliondoka akiwa hana amani hata kidogo
maana alijua muda wowote Sor atamfuata popote
pale aendapo,sasa aliona hatari inazidi kumsogelea
na endapo hata Fanya lolote la kumsaidia basi
Maisha yake yatakuwa hatarini zaidi ya hapo.
Mwalimu jona aliitwa na madam Remijo wakelekea
ofisini ambako huko alimpa maelekezo machache
ya kuifanya AFYA yake irudi katika ubora wake.
Siku ilisha bila vioja vyovyote vile kutokea tena na
mwisho wanafunzi wote walikuwa wakirudi
nyumbani,Lisa alimfuata Humph na kumpa pole juu
ya kile kilichomkuta.
Walipiga soga mbili tatu kama ilivyo kawaida yao
na mwisho Lisa akaamua kumueleza Humph
yaliyomkuta usiku uliopita kwani hakuona haja ya
kumficha ikiwa yeye ndiye msaada wa mwisho
uliobakia.
"Mwenzio jana si nikakutana na huyo rafiki yako
sasa nilipokuwa katikati ya maongezi majanga
yakatokea yaani sijui wale watu hata walitokea wapi
wakaniharibia mpango mzima niliokuwa nao"
aliongea Lisa akiwa anakunja mdomo wake
kuonesha ni jinsi gani amekereka
 
Sehemu ya ishirini na tano
........Ilipoishia..........
Walikuwa wakicheka kwa furaha bila kufahamu
kuwa kuna mtu amelenga shabaha upande huo huo
waliosimama.
★★★Teremka nayo★★★
Samson alifanikiwa kuweka target yake katika
kichwa cha Humph na kabla hajabofya kifyatulio
ama trigger kwa lugha yetu ya kikubwa Humph
alipitiwa na zile ndoto za mchana a.k.a maono.
Alimuona mwanaume mmoja akiwa katika jengo
moja refu ameshikilia mtutu(bunduki) kubwa
lililolenga upande wao,vidole vya yule mwanaume
vilikuwa vinaelekea katika kifyatulio ama trigger.
Humph alistuka na kumvuta Lisa kwa nguvu risasi
ikapita ikiambatana na mlio mkubwa pamoja na
kuchimbua eneo dogo la daraja,Lisa alipatwa na
hofu kuu iliyomfanya aanze kulia.
Humph aliinuka haraka pale alipokuwa
amedondokea na Lisa kitendo cha kugeuka tu
macho yake yakaanza kutoa nuru iliyochanganyika
na hasira kali,Aliangalia majengo yote yale akiwa na
lengo la kutambua ni wapi adui yake alipojificha na
ikumbukwe kuwa baada ya Humph kukabidhiwa
rasmi nguvu zile za macho ya ajabu alikuwa na
uwezo wa kuona umbali mrefu mno.
Humph alifanikiwa kumuona Samson ambaye
alijaribu kumuua na zoezi likashindikana,alipotaka
kumfuata akamuadabishe akakumbuka kuwa Lisa
atafahamu uhalisia wake hivyo pale pale akajituliza
na kuyarudisha macho yake katika hali ya kawaida.
Samson alipoona dili limekuwa dirisha alianza
kuifungua bunduki yake kwa haraka haraka ili awahi
kabla polisi hawajafika eneo lile,kutokana na
ushapu aliokuwa nao haikuchukua muda
kukamilisha zoezi lake.
Samson alitoka katika chumba chake na.kukuta
watu wanakimbia ovyo ovyo huku wanapiga
makelele nae akajichanganya na kuanza kutoka
nje,Polisi walikuwa tayari wamefika karibu na jengo
hilo.
Ving'ora vilikuwa vinasikika kila sehemu katika jiji
hilo la Reycity,Samson alifanikiwa kufika nje ya
jengo hilo na Kwakuwa hakwenda na usafiri binafsi
aliingia katika taxi na kuomba kusogezwa mbele.
Akiwa ndani ya gari dereva alikuwa ni mcheshi mno
na alijaribu kuzungumzia hali halisi ya jiji hilo kwa
wakati huo
"Bro yaani hili jiji limechafuka balaa na nadhani
kuwa siku za mbele tutakuwa na vita kubwa"
alisema dereva huku akiongeza umakini barabarani
"Kwanini unasema hivyo rafiki" Samson aliuliza kwa
kudadisi
"Ina maana bro haujashuhudia matukio kadhaa
yaliyotokea siku chache zilizopita" aliongea dereva
"Hapana sikuwepo hapa jijini kwa muda mrefu".
Samson aliongeza uongo
"Yaani hivi ninavyokwambia yalikuwa majitu ya
ajabu yanapambana na ka kijana kadogo lakini cha
ajabu kale kalishinda,huwezi amini bro" dereva
aliongea kama cherehani
"alaaaa!! kumbe jiji limechafuka namna hiyo?"
Samson alihoji.
"Haaa! we unauliza makofi polisi kuna jamaa
lilikuwa linatoa makombora ya barafu si.mchezo
ningekuwa mimi wangekoma yaani
ningewachezesha sebene la hatari maana kila siku
wanatupiga faini zisizo na msingi" dereva alizidi
kumwaga mchele.kwenye kuku wengi
"Mmmh! kazi ipo" aliguna Samson kwa wasi wasi
"Oohooooo!! bro hayo tisa kumi ni hii ya leo pale
hotelini ulisikia ule mlio wa risasi?"
"Nimefika bwana nashukuru kwa msaada wako."
Samson alimkatisha dereva mcharuko na kutoa
kiasi kidogo cha fedha kisha akaaga
"Chenchi baki nayo utakunywa soda bhana" Samson
akaenda zake na kumuacha dereva yule anacheka
cheka na kukanyaga mafuta
★★★★★★★★★★★★
Humph alimnyanyua lisa na kuanza kuondoka naye
huku akimpa maneno yenye kuleta matumaini
ilimradi tu Lisa asahau tukio liliotokea muda mfupi
uliopita.
Njiani Humph na Lisa walipishana na polisi
waliokuwa wanaelekea eneo ambalo muda mchache
uliopita wao walipatwa na mkasa huo unaotisha.
Walifanikiwa kutembea mpaka kufika katika lango la
kina Lisa na moja kwa moja Humph akabofya kitufe
cha kengele kinachopeleka mawasiliano ndani ya
nyumba ya kina Lisa.
Dakika kadhaa zilipita mlango wa geti ukafunguliwa
na mlinzi akatoka na kukutana uso kwa uso na Lisa
pamoja na Humph ambao wote walikuwa na sura za
huzuni.
Mlinzi hakushangazwa na ujio wa Humph eneo lile
maana alimtambua kama rafiki mkubwa wa Lisa na
wanasoma pamoja yaani classmates.
Humph aliondoka eneo hilo akiwa na mawazo
kedekede juu ya adui yake mpya ambaye
ameisakama roho yake.
★★★★★★★★★★★★★
Samson alikatisha vichochoro kadhaa kisha
akaanza kukimbia taratibu yote hii ilikuwa ni uoga
uliotokana na zile simulizi za dereva taxi na vile
ambavyo Humph aliikwepa risasi.
Alifika nyumbani kwake akiwa salama na pia
alijihakikishia kuwa hamna mtu anayemfuatilia toka
kule alikotoka mpaka nyumbani kwake.
Samson aliwasha runninga yake kupitia rimoti na
kutafuta chaneli yenye habari motomoto,alifanikiwa
kuipata chaneli ya Nase TV iliyorusha matangazo ya
moja kwa moja kutoka katika hotel iliyosadikika
kuwa kuna mhalifu alikuwa akifanya mauaji ambapo
hakuna mtu yeyote aliyepatikana akiwa majeruhi
ama amekufa.
Samson alishusha pumzi ndefu na kulikumbuka lile
tukio kumbe mbali na umahiri aliokuwa nao katika
kulenga shabaha lakini alifanya uzembe mkubwa
ambao ungegharimu Maisha yake.
Wakati anashambulia hakukumbuka kufunga
kiwambo cha kuzuia sauti,ndiyo sababu kubwa
iliyofanya watu waanze kukimbia bila mpangilio kila
mmoja akijaribu kuokoa nafsi yake.
Samson alivuta kompyuta mpakato yaani laptop
yake na kuziingilia kamera za hoteli ile(hacking)
kisha akafuta kila rekodi iliyomuonyesha akiwa eneo
lile vile vile alifuta na rekodi za barabarani ambazo
zilikuwa karibu kabisa na hoteli ile ili asiingie
hatiani....
 
Sehemu ya ishirini na sita
........Ilipoishia..........
Samson alivuta kompyuta mpakato yaani laptop
yake na kuziingilia kamera za hoteli ile(hacking)
kisha akafuta kila rekodi iliyomuonyesha akiwa eneo
lile vile vile alifuta na rekodi za barabarani ambazo
zilikuwa karibu kabisa na hoteli ile ili asiingie
hatiani....
★★★Shuka nayo★★★
Samson alipomaliza kila ndipo akakumbuka
kuiwasha simu yake ijapokuwa mpelezi mwenye
dhamana kubwa namna ile kama yeye alipaswa
kuwa hewani masaa 24 lakini yeye alithubutu
kuifunga simu yake.
Alipoifungua tu simu ikaingia ya mkubwa wake wa
kazi ambaye alikuwa akifoka tu na kuweka matusi
kama kiunganishi cha maneno yake kila
ayatamkapo.
Alimtaka Samson afike mara moja kuangalia ni
mpuuzi gani huyo anayechezea sharubu za
serikali,Bila kuchelewa Samson akaanzisha safari ya
kuelekea hotelini ambapo ndipo tukio hilo la
kustukiza lilijitokeza.
★★★★★★★★
Humph alifika nyumbani kwao akiwa hoi lakini
alivunga ili wazazi wake wasielewe chochote
kinaxhoendelea japo walikuwa na wajibu wa kujua ni
kipi kinachomtatiza mtoto wao na ikibidi watoe
msaada kwake.
Baada ya pilika pilika nyingi za hapa na pale kama
unavyojua manyumbani kwetu huwa kuna mambo
mengi ya kufanya mpaka uimalize siku,Humph
aliingia kulala hazikupita dakika nyingi kamanda wa
jeshi akampitia na kumpigisha kwata za kutosha si
mwingine bali alikuwa ni usingizi wa pono.
Asubuhi na mapema Humph alikuwa shuleni japo
kichwa chake hakikuwa sawa juu ya maswaibu
yanayomkuta kila kukicha ukizingatia kuwa bado ni
kijana mdogo ambaye anahitaji uangalizi wa wazazi
na pia hakuhitajika kuchanganua mambo makubwa
makubwa katika ubongo wake ambayo kwa
vyovyote vile yangepelekea kudhoofika kwa afya
yake.
Lisa nae hakuwa na raha hata chembe alihisi kichwa
chake kinacheza bingili bingili Lila muda yote ni
kutokana na ule mlio wa bunduki.
Ilipita wiki nzima hali ikiwa shwari katika jiji la
Reycity vile vile Humph na Lisa walikuwa tayari
wameanza kusahau kuhusu yaliyowakumba.
Wanafunzi walipokuwa wametoka shuleni Humph
alionekana akitembea peke yake na baadae Lisa
alikuja anakimbia na kumfikia Humph pale alipo
"Wee mwanaume mambo?"
"daaah!! ni wewe tena,umenistua,mmmm! poa lakini
vipi kuhusu wewe?"
"mi sijambo kabisa ila nimekuja na maswali kibao
Leo nataka ujibu"
"eeeh! aya kama nikiyaweza lakini maana mtihani
mwepesi ni ule uliotunga mwenyewe kwasababu
majibu unayo"
"Humph bhana daima huwa hauishiwi tuma neno
maneno twako"
"kawaida,fanya basi uulize" alijibu Humph
"Humph unajua mpaka Leo hii najiuliza kuhusu lile
tukio la siku ile hivi wewe unadhani ni kwanini
tulishambuliwa?" Lisa aliuliza
"Hata Mimi nilikuwa najiuliza hivyo hivyo lakini
nahisi yule mtu alikuwa na mbaya wake kwa bahati
mbaya akashambulia upande wetu" Humph
alipindisha ukweli wa mambo
"etiiii!! inawezekana lakini akili yangu inakataa
kabisa kuwa hilo ni jibu" alieleza hisia zake wazi
"sasa kama akili yako inagoma kuwa sio jibu fikiria
tena alafu utoe jibu sahihi" Aliongea Humph kwa
mzaha
"mmmh! aaah! enheee! itakuwa walifanya vile
kwasababu nilitoka nae huyo shujaa wao auti(out)
siku ile" alivutia kwake suala lile mrembo Lisa ili
ionekane kuwa yeye ndiye kisababishi yaani eti yote
hayo ni kutokana na wivu kisa tu alitoka na Humph
"sawa mdada ila jaribu kukaa mbali na yule jamaa
usijekufa kabla ya wakati wako ikiwa sisi wengine
bado tunakuhitaji" Humph alijaribu kumuonya Lisa
"Kumbe unanipenda eeh! basi nitajitahidi sana kuwa
mbali naye" Lisa alikubali kirahisi lakini moyoni
alijisemea simuachi mpaka kieleweke
Basi walibadilisha mada nakuanza kuongelea
mambo mbalimbali ikiwemo ya shule na hatimaye
ilifika sehemu wakaachana kila mtu akaenda
nyumbani kwao.
★★★★★★★★★★
Mzee Kasai au ukipenda muite baba mzazi wa
Humph alikuwa ameketi sebuleni kwake akifikiria
mwenendo wa mtoto wake ambaye toka amerudi
kutoka katika ile ziara kishule alionekana kubadilika
vitu vingi ikiwemo tabia hili jambo lilimpa wasi wasi
mno na kumkosesha raha kwa kipindi hicho.
Toka awali Humph alikuwa na malezi mazuri
ikiwemo kuwahi kurudi nyumbani na vile vile
alipenda sana kujumuika na wazazi wake wakati wa
kula pamoja na kutembelea sehemu mbalimbali siku
za mapumziko kifamilia.
Hata hivyo Humph hakuweza kulala bila kuungana
na familia nzima kusali pamoja ndipo alale.Baada
ya mzee huyo kufikiria sana aliona jambo la busara
si kumwambia mke wake maana waswahili huwa
wanasema "tabia za mtoto wa kiume huzirekebisha
baba yake na pia huzitatua yeye vile vile kwa mtoto
wa kike na ikishindikana ndipo wazazi wote wawili
hukaa na kushauriana wafanye nini ili kumsaidia
mtoto wao"
Moja kwa moja mzee Kasai alianza kutafuta muda
wa ziada ili aongee na mwanae lakini alipokuwa
anawaza jinsi gani ataupata huo muda wazo lingine
likajitokeza kuwa kwanza amfuatilie ili ajue tatizo
kisha aweke nae kikao na aliamini hiyo itakuwa njia
rahisi ya kulifumbua tatizo hilo.
★★★★★★★★★
Wakati Humph akiwa anatoka shuleni mzee Kasai
hakuwa mbali nae alianza kula sahani moja na
mwanae ili amrekebishe kabla hajapotea.
Humph akiwa na Lisa walizidi kusonga mbele
wakiongea mambo kedekede na hadi wanaachana
hamna aliyestuka kuwa wanafuatiliwa kutokana na
mzee Kasai kubadili muonekano na kutumia njia za
kisasa zaidi kumfuatilia mwanae.
Kila siku jioni Humph na Lisa walikutana katika
kituo tofauti na kile cha mwanzo pia walipunguza
muda wa kuongea walitumia dakika tano tu na
kutawanyika.
Mzee Kasai aliishia kutabasamu tu na kujisemea
"like father like son" kama baba kama mtoto maana
hata kipindi ni kijana alikuwa na msichana mrembo
mno na huyo ndiye mama yake na Humph mpaka
muda huo.
Mzee Kasai hakuona haja ya kuendelea kufuatilia
Kwakuwa tayari jibu alikuwa nalo kichwani ila aliona
ni bora aanze kumlia doria Humph ili aendane na
muda wa nyumbani na wakati huo huo akiendelea
na ratiba ya kukutana na lisa.
Bado Humph hakuhisi lolote kuhusu baba yake
hivyo alizidi kujiongezea asilimia za Uhuru wa
kufanya mambo yake na katu hakujua Kama dawa
yake ipo jikoni inachemka na muandaaji ni baba
yake mzee Kasai.
 
Sehemu ya ishirini na saba
........Ilipoishia..........
Bado Humph hakuhisi lolote kuhusu baba yake
hivyo alizidi kujiongezea asilimia za Uhuru wa
kufanya mambo yake na katu hakujua Kama dawa
yake ipo jikoni inachemka na muandaaji ni baba
yake mzee Kasai.
★★★Teremka nayo★★
Mzee Kasai aliomba mkewe ammwekee chakula na
kijana wake ili pale atakapo rudi basi wale
pamoja.Mke wa mzee Kasai hakutambua sababu
iliyomfanya mzee huyo achukue maamuzi kama
hayo lakini aliamini Mme wake anamaana kubwa
sana kufanya hivyo.
Mara nyingi mzee huyo hufanya kitu mwenyewe na
kikimshinda ndipo huomba msaada japo Mara
nyingi sana amekuwa si mtu wa kushindwa kirahisi
rahisi na ndiyo maana mama yake Humph hakutaka
kumbugudhi(kumsumbua).
Baada ya muda kwenda sana hatimaye Humph
alifika nyumbani ilikuwa yapata saa tatu kasoro
usiku,Mzee Kasai hakuwa akipendezwa na tabia
hiyo ya mtoto wake lakini Kwakuwa tayari
ameshapevuka na anaelewa anachokifanya ikambidi
awe mpole.
Walikaa mezani pamoja wakapata chakula kisha
mzee Kasai bila kupoteza wakati akaanzisha
mazungumzo maana alijua wazi kuwa baada ya
kijana huyo kumaliza kula basi angeelekea moja
kwa moja chumbani kwake kujipumzisha ama
kupitia mawili matatu aliyojifunza shuleni.
"Humph mwanangu hivi unapenda kula peke yako
kama mchawi?" ni swali kutoka kwa mzee Kasai
"Ha..hapana baba kwanini umesema hivyo?" Humph
alijibu bila kujiamini na kurudisha swali kwa baba
yake
"Najua haufahamu kwasababu unahisi upo sahihi
lakini ukweli ni kwamba unatukosea sana wazazi
wako,je unajisikiaje ulivyokula na Mimi"
"Nimejisikia vyema kwani nina siku nyingi
hatujashiriki pamoja chakula" alijibu Humph
"ooh! sawa kabisa,unaweza kuniambia ni kitu gani
kinachofanya utoke nyumbani saa moja usiku na
kurudi saa tatu"
"Ndiyo hakika ndiyo huwa naenda kumtembelea
rafiki yangu" alijibu Humph akiwa bado haelewi
kinachoendelea
"vizuri kijana wangu Nina imani haudanganyi,sasa
kosa lako ni kuchelewa kurudi nyumbani pia si
kwamba nakataa wewe kuwatembelea marafiki
hapana ila bado upo chini yetu na tunapaswa
kuweka uangalizi kwako na.kuzifuata sheria
tulizoweka sisi na si unazoweka wewe"
"Samahani baba nimekosa" Humph alijishusha
mapema baada ya kutambua kuwa baba 'ake
amechukia
"Usijali kama umetambua kosa basi inabidi tu
ubadili ratiba Fanya mambo yako mapema mwisho
ni saa moja na nusu na sitapenda kuyarudia haya
vinginevyo nadhani unanielewa." alisisitiza mzee
Kasai
"Sawa baba nimekuelewa na nina kuahidi kuwa
sitorudia makosa" alikiri Humph kwa moyo wote
"Aya unaweza kwenda kupumzika sasa maana muda
umekwenda mno" alimaliza mzee Kasai na kuelekea
kulala akiwa tayari huku nyuma ameyasahisha
makosa ya mwanae.
Kichwa cha Humph kilijaa maji na hapo ndipo
alitambua kuwa kumbe mapenzi ni upofu yote hii ni
Kwakuwa hakutambua kama ni mkosaji kwa wazazi
wake yeye alichojali ni kuwa karibu na Lisa.
Mapenzi bwana ni kasheshe ngoja tuwaachie wenye
nayo.
★★★★★★★★
Samson alimaliza siku kadhaa akiwa tayari
amelizima sakata la kumtafuta mhalifu aliyetaka
kuua raia wema. Leo hii alikuwa mpango mpya
kabisa wa kumuangamiza Humph.
Samson alikusanya zana za kazi huku kichwani
akiwa anawazo moja tu kuvamia nyumbani kwa kina
Humph maana aliamini hiyo itakuwa njia rahisi ya
kumtia mbaroni kijana Yule anayekisumbua kichwa
chake.
Alianza kwa mpango A huu ulikuwa ni endapo
atamkuta Humph mwenyewe nyumbani kwao
amteke alafu akamuulie mbali na kama akimkosa
basi mpango B utakuwa ni kuondoka na mtu yeyote
atakaye jitokeza katika familia hiyo ya Humph.
Alijiandaa kwa mrefu mno lengo lake asifanye kosa
kama awali, ali pomaliza aliingia sebuleni kwake na
kukaa akiusubiri muda wa kazi ufike.
★★★★★★★★★★★
Kama kawaida Humph alimtembelea Lisa na
kuzungumza mawili matatu wakiwa kama marafiki
walioshibana sasa pia walikuwa na Uhuru baada ya
kusahau tukio la uvamivi lililowatokea pindi wapo
matembezini kama ilivyozoeleka kwao.
Humph alijitahidi sana kuzizuia hisia zake kwa Lisa
lakini ni jambo ambalo halikuwezekana hata kidogo
kwani macho tu yalitosha kuonyesha Kuwait Humph
amezama katika mapenzi tena mapenzi mazito kwa
binti lisa.
Lisa alilitambua hilo mapema kutokana na vitendo
alivyokuwa akionesha Humph ila hakutaka
kujishughulisha naye maana moyo wake alimkabidhi
mtu ambaye alimuokoa na kujiapiza kuwa kamwe
hawezi kumsaliti mtu huyo abadani afe na utamu
wake.
Licha ya kwamba Lisa hakujishughulisha na hisia za
Humph lakini moyoni alikiri kuwa Humph hakuwa
mzuri tu bali ni mwanaume anaejali na mwenye
vigezo vya kupendwa na kila msichana aliekamili.
Humph akiwa karibu kabisa na Lisa alipatwa ghafla
na ndoto zile za mchana alimuona mtu mmoja
akiwa na manyoya ya kutisha amesimama na hapo
hapo ikapita picha nyingine iliyokuwa ikimuonesha
baba yake Humph akipiga kelele.
★★★★★★★★★
Samson aliona ni muda muafaka wa yeye kwenda
kuifanya kazi ile,alipoinuka tu ili aanze kuondoka
ghafla taa za ndani mwake zikaanza kucheza cheza.
Samson alipatwa na wasi wasi kuwa huenda
amestukiwa na polisi wenzake,kwa haraka akashika
bastola yake vizuri ili kukabiliana na chochote
kitakachotokea.
Akiwa na mashaka mengi sauti za viatu zinaanza
kusikika pale sebuleni na ule mwanga ulivyokuwa
unawaka waka ukamfanya apate kiwewe
ukomandoo wake ukaanza kuyeyuka baada ya viatu
kusikika mbele nyuma katikati mara karibu yake na
mtu anayefanya hivyo asionekane.
Samson alianza kujisemea kimoyo moyo "sitaki
kufa Leo jamani bado kuna mambo mengi
sijayafanya eeh! nionee huruma walau nimuage hata
Anna" na maneno mengine mengi yalizidi
kumponyoka yote ni kutokana na mtindo ule
uliotumiwa kuvamia si wa kibinadamu.
 
Sehemu ya ishirini na nane
........Ilipoishia..........
Samson alianza kujisemea kimoyo moyo "sitaki
kufa Leo jamani bado kuna mambo mengi
sijayafanya eeh! nionee huruma walau nimuage hata
Anna" na maneno mengine mengi yalizidi
kumponyoka yote ni kutokana na mtindo ule
uliotumiwa kuvamia si wa kibinadamu.
★★★Shuka nayo★★★
Akili yake ilionekana wazi kuchanganywa lakini
Kwakuwa alikuwa ni askari wa daraja la juu kabisa
alikumbuka kuwa unapokuwa katika uwanja wa vita
usipoteze umakini wako. Moja kwa moja akajitahidi
kuituliza akili yake ili ajue wapi ambapo adui
anatokea.
Ghafla kivuli kikaanza kuonekana kikitokea katika
giza hapo hapo Samson akaanza kupiga risasi
kukielekea kivuli kwa bahati mbaya kivuli kile
kikapotea ndipo Samson alipopatwa na wazimu
akawa anapiga risasi ovyo ovyo kila sehemu
ambayo alihisi huenda adui yake yupo.
Kiukweli mjanja siku hiyo alikutana na mjanjuzi
yaani Samson mjanja na Sor mjanjuzi,baada ya
Samson kuona an a Aliza risasi bure ikambidi
asitishe zoezi lake kwanza na kabla hajafanya lolote
akaisikia sauti ya Sor ikitoa amri
"Weka silaha yako chini kabla sijakutawanyisha"
alinadi Sor
Bado Samson alizidi kuishikilia silaha yake
barabara kuonyesha ni jinsi gani yeye ni mbishi
"Naona una kiburi sana Sam ngoja nikuonyeshe"
alijigamba Sor huku akijitokeza kutoka kwenye
giza,gauni lake nzuri lililomkaa vyema lakini
halikuonekana kufaa tena baada ya kuwa na matobo
yaliyopitiliza mpaka upande wa pili wa mwilli wake
Sam alipatwa na mstuko mpaka mdomo wake
ukabaki wazi kuonesha ni jinsi gani alishangazwa na
mtu huyo si kwa urembo alionao la! ila kwa zile
risasi ambazo alikuwa amepiga kile kivuli kumbe
zilimpata Sor japo hazikuleta madhara zaidi ya
kutengeneza matobo matobo(mashimo).
Kile kitendo cha Samson kubaki na mshangao
ikawa njia nzuri kwa Sor kumuonyesha maajabu
mengine ambayo Samson hakuwahi kuyaona Sor
alijiunga pale pale na zile alama za mashimo
zikafutika kabisa akabaki nadhifu kama awali.
Samson alizidi kuchoka nakujiona hana bahati siku
hiyo,Sor alitabasamu na kuanza kumsogelea
Samson,Samson alianza kutetemeka mpaka bastola
ikamdondoka macho kayatoa kama mjusi
aliyebanwa na mlango.
Sor alimfikia Samson na kumshika mikono muda
huo Samson alikuwa tayari amepiga goti moja,Sor
alianza kuongea maneno ya ajabu ajabu
yaliyomfanya Samson azirai pale pale kisha Sor
akaondoka kwa mwendo wa madaha.
Samson alipozinduka akili yake haikuwa ile tena
huyu alikuwa ni Sam mpya mwenye malengo
asiyeijua huruma hata chembe kwa wakati ule zaidi
ya kuua kile kitakachojitokeza mbele yake.
★★★★★★★★★★★
Humph alipoona yale maono hayaelewi ikambidi
alazimishe kichwa chake kuivuta ile taswira ili aone
ni kitu gani kinaendelea,alijaribu sana mpaka
akafanikiwa kumuona baba yake akiwa amepiga
magoti na pembeni kulikuwa na huyo mtu wa ajabu
ambaye Humph hakufanikiwa kumuona vizuri.
Humph alistuka na kurudi katika hali ya kawaida
lakini kwasababu alikuwa amelazimisha kichwa
chake kutambua tatizo aliloliona kwa ukaribu
zaidi,kichwa kilianza kumuuma kwa fujo zote mpaka
akaanza kupiga kelele na mwishowe akaanza
kugalagala chini.
Lisa alibaki na mshangao maana hakuwahi kumuona
Humph katika hali kama ile hapo awali ilibidi
amuwahi pale chini na kuanza kumuuliza tatizo
nini.Humph alizidi kugalagala huku akilalamika
kichwa kinamuuma na mikono yake ikiwa kichwani
Humph akiwa pale chini alianza kuona ukungu mzito
ukitanda machoni na mwisho akaacha kuona kabisa
kinachoendelea. Lisa alikuwa amechanganyikiwa
mara amshike Humph na kumuachia alafu anainuka
tena anarudi na kuanza kumuamsha Humph
aliyetulia tuli.
Lisa akapata wazo baada ya kuyaona Yale maji
yayopita katika ule mto uliojirani na daraja,akatoa
kitambaa chake na kuelekea mtoni akakiloweka
kisha akarudi na kukiweka katika paji la uso la
Humph .
★★★★★★★★★
Samson alinyoosha moja kwa moja mpaka katika
nyumba ya kina Humph,alipofika akabisha hodi na
kujibanza pembeni. Mama yake Humph akafika na
kufungua mlango lakini hakuona mtu ikambidi atoe
kichwa nje kuchungulia kama kuna mtu yeyote.
Hakika alifanya kosa,kosa lililomgharimu kwani
kitendo cha kuchungulia tu akakutana na kitako cha
bastola katika paji la uso kilichomfanya adondoke
kama mzigo,
Kishindo kile kilimstua mzee Kasai akainuka
alipokuwa ameketi na kuelekea mlangoni
kulikotokea kishindo kile.
Mzee Kasai alipojitokeza tu moja kwa moja
akakumbana na mdomo wa bastola ukimuangalia
akabaki anaweweseka wasi wasi ukizidi kumtawala
asijue ni kwanini kadhia ile imemfuata nyumbani
kwake.
"Sina shida na wewe usalama wako ni kuniambia
wapi alipo Humph " Samson alimkoromea mzee
Kasai aliyekuwa anatetemeka mwili mzima.
"Ni..ni..bo..bo...ra..uni...uni..ue ila mwanangu
umuache hai" alijitetea mzee Kasai
"hahahahaha!! nadhani utalipa kwa hili" Samson
alisema maneno hayo huku akiambatanisha na
ngumi nzito iliyopelekea mzee Kasai apoteze
mawasiliano kati ya kichwa na kiwili wili.
Samson hakupoteza muda akamnyanyua mzee
Kasai na kumbeba begani na kutokomea nae mahali
kusipojulikana.
Sifa ambaye ni mdogo wake Humph alirudi
nyumbani akiwa ametokea dukani alipofika
mlangoni alipokelewa na mwili wa mama yake
ukiwa chini bila fahamu.
kwa kutumia akili za ziada alikimbilia simu ya
mezani na kupiga katika gari ya wangonjwa ya
dharura kisha akarudi na kumlaza mama yake katika
mapaja yake huku machozi yakimdondoka.
"kimekukuta nini mama'angu eeeh! mbona
nimekuacha mzima Mimi jamani,mama...m
ama....mama...amka mama'angu" Sifa alizidi kulia
akijitahidi kumuamsha mama yake aliyepoteza
fahamu.
Gari ya wagonjwa ilifika mara moja na kumpakia
mgonjwa na kuondoka wakiwa pamoja na Sifa
aliyekaa pembeni ya mama yake huku akilia kilio
cha chini chini.
 
Sehemu ya ishirini na tisa
........Ilipoishia..........
Gari ya wagonjwa ilifika mara moja na kumpakia
mgonjwa na kuondoka wakiwa pamoja na Sifa
aliyekaa pembeni ya mama yake huku akilia kilio
cha chini chini.
★★★Chaaoooo★★★Shuka nayo★★
Watu waliokuwa ndani ya gari walimuonea huruma
sana binti yule ukipenda muite Sifa na siku zote
waswahili wanasema ukiona mtu anamajonzi juu ya
yule ampendae usimnyamazishe ila muache aondoe
sumu yote iliyondani yake ndipo umfariji na hivyo
ndivyo ilivyokuwa kwa manesi wale.
★★The lost of Humph's power★★
★kupotea kwa nguvu za Humph★
Humph alizinduka akiwa miguuni mwa lisa ambaye
tabasamu lilianza kuchanua baada ya kuona Humph
amerejea katika ubora wake,lakini licha ya kwamba
Lisa alikuwa anatabasamu lakini macho yake
yalikuwa mekundu kama pilipili na uvimbe Fulani
ambao ulisababishwa na kilio alicholia kwa muda
mrefu.
Humph aliliona hilo akamfuta machozi kiasi kwa
kiganja chake yaliyokuwa yanateremka taratibu
katika mashavu ya Lisa.
"Nilijuwa umekwenda moja kwa moja maana mwili
wako ulikuwa wa baridi mno hata mapigo ya moyo
yalikuwa hayasikiki kabisa." aliongea Lisa akiwa
ametawaliwa na huzuni.
"Mmmmh! Mungu ni mkubwa niko salama usiwe na
shaka tena kuhusu Mimi sawa rafiki yangu kipenzi"
aliongea Humph akijitahidi kutabasamu japo moyoni
alikuwa na maumivu mno kutokana na maneno ya
Lisa.
"Sawa ila tafadhali nimekuzoea usijekuniacha
mpweke" Lisa aliongea kwa mapenzi mazito lakini
si yale ya wapendanao ila ya kirafiki.
Humph aliinuka na kuondoka na Lisa ikafikia mahali
wakiwa wanataka kuachana kila mtu aende kwao
Lisa akagoma kata kata akidai huenda Humph
akazidiwa njiani hivyo ni bora amfikishe kwao ndipo
yeye aweze kwenda kwao.
Humph alimshawishi Lisa ilimradi tu arudi kwao ili
ajue namna gani atailinda familia yake kabla ya
tatizo aliloliona halijatokea bila kujua kuwa
ameshachelewa.
Lisa alikubali kwa shingo upande huku akimuasa
Humph awe makini njiani kwani hali yake si nzuri
hata kidogo. Humph alipokuwa njiani alikuwa.akijiul
iza maswali mengi na kubwa lililomuumiza kichwa
ni.kuhusu familia yake.
Tukiachana na mambo aliyokuwa akiyafikiria Humph
pia alikuwa akihisi ubaridi mwilini tofauti na
alivyozoea hali ya.mwili wake.
Humph alifika nyumbani kwao akiwa amechoka
vilivyo,alishangazwa na ukimya wa ajabu
uliompokea nyumbani kwao. Akili yake ilifikiria
kuwa tayari wamevamiwa mle ndani.
kwa tahadhari ya hali ya juu aliingia kwa kunyatia
mpaka sebuleni ambako kulikuwa kumetulia
mno,alipoangalia mezani akakutana na karatasi na
moja kwa moja akaifuata na kuisoma ikiwa
inasema"Mama amelazwa hospitali upatapo ujumbe
huu fika haraka Sifa "
Humph alishusha pumzi ndefu akijua kazi
imeanza,kitu kingine kikamvamia akili yake kengele
ya hatari ikaanza kulia katika ubongo wake na Hapo
akapatwa na swali je, kama mama amelazwa
hospitalini na baba atakuwa wapi?.
Hilo swali likaanza kumuumiza kichwa tena lakini
kabla hajapata jibu simu ya mezani ikaanza
kuita,Humph akaifuata na kutaka kuipokea lakini
akasita simu ile ikakata.
Humph alipotaka kuondoka ile simu ikaita tena
akaifuata na kuipokea kwa hasira na kabla
hajaongea akasikia sauti inamuongelesha
"Chukulia rahisi kijana mdogo,najuwa kuwa
unahasira sana baada ya kumkosa baba yako.Hasira
haisaidii fika Bandari ya Lakeshore (ufukwe wa
ziwa) na mzigo wangu sasa hivi" ilikuwa ni sauti ya
Samson.
Humph kwa hasira alitupa mkonga wasimu chini na
kutoka ndani akiwa anaelekea bandarini lakin cha
ajabu zaidi ni kwamba macho yake yalishindwa
kutoa ile nuru akawa kawaida tu japo alikuwa na
hasira mno.
Ile hali ikamshangaza na yeye pia akahisi labda
hajakasirika vizuri ikambidi ajaribu kupotea ili
atokee bandarini na hilo likashindikana kabisa.
Humph hakuchoka akahisi huenda ule ubaridi
alionao ndiyo unasababisha yeye ashindwe kufanya
yale lakini swali likabaki kuwa kwanini iwe hivyo.
Humph hakuwa na jinsi akaanza kukimbia kuelekea
bandarini akijuwa kuwa labda kufanya vile
kungerudisha nguvu zake. Alikimbia mno ila
mwendo ule haukufanana na ule aliouzoea akiwa
na.nguvu zile za ajabu.
Humph alizidi kukimbia na hatimaye mwili ukapata
joto na mwisho jasho likaanza kumtoka kutokana
na kukimbia umbali mrefu.Baada ya.kuona vile
akajaribu tena bahati yake kuzitumia zile nguvu
alizonazo lakini jibu kilikuwa lile lile kuwa nguvu
zile zimetoweka.
Humph alikaa chini na kulia kwa uchungu maana
alijuwa kabisa kuwa bila zile nguvu yeye si kitu na
bila zile nguvu kwa wakati ule baba yake anaenda
kuangamia.
Alilia sana mpaka mawingu mazito yakatanda
angani na radi kubwa zikiwa zinapiga kuashiria
mvua kubwa itanyesha mda mfupi ujao.Kwa upande
mwingine Yale mawingu na zile radi zilionesha tukio
la kihistoria ambalo halikuwahi kutokea hapo kabla.
Humph hakuona haja ya kuendelea kulia
alijikakamua na kuinuka kisha taratibu akaanza
kujivuta kuelekea katika bandari ya ocean shore
(fukwe ya bahari).Akiwa njiani alikumbuka wakati
ambao alikuwa na Lisa alipoliona lile tukio na ghafla
kichwa kikamuanza hapo akatambua wazi kuwa
ndipo tatizo lilipoanzia la kupotelewa na nguvu
zake.
Basi hakuona haja ya kuendelea kuumiza kichwa
kuhusu nguvu zile,akaelekeza akili yake yote katika
bandari ile ambayo alielekezwa na Samson kuwa
ndilo eneo analohitajika kufika.
 
Sehemu ya thelathini
........Ilipoishia..........
Basi hakuona haja ya kuendelea kuumiza kichwa
kuhusu nguvu zile,akaelekeza akili yake yote katika
bandari ile ambayo alielekezwa na Samson kuwa
ndilo eneo analohitajika kufika.
★★★Tereza nayooo★★★
Humph alifika eneo husika kwa mbali alionekana
Samson akisubiri kwa hamu sana ila pembeni yake
alikuwepo mzee Kasai amepigishwa magoti mikono
ikiwa imefungwa kwa nyuma na mdomoni
aliwekewa gundi aina ya plaster ili asizungumze
lolote wala kupiga kelele.
Samson alikuwa amesimama juu ya kontena kati ya
makontena mengi yaliyopangwa bandarini
hapo.Humph alisogea taratibu mpaka akawa
anaiona vizuri taswira ya samson.
Humph alimuonea huruma sana mzee Kasai kwani
hakuna kitu ambacho alikitambua kumhusu yeye
zaidi ya kumfahamu kama mtoto wake alielelewa
katika misingi imara.
"Dogo hatuna muda tena weka mzigo wangu hapo
chini ugeuke nyuma kisha piga hatua kumi bila
kugeuka na usithubutu kufanya ujinga wowote ule
utakaopelekea nifanye upumbavu." aling'aka Sam
kwa sauti yenye kitetemeshi.
Mzee Kasai alitikisa kichwa kuonesha kuwa
mwanae asikubali kufanya vile amavyotaka
Sam.kumbe wakati mzee Kasai anatoa ishara ile
Sam aliona kila kitu alichokifanya ni kumpiga mzee
Kasai Kofi la nguvu lililomfanya Humph afumbe
macho kwa uoga.
Taratibu hasira za Humph zilianza kuongezeka huku
chozi la uchungu likiwa linamdondoka.Samson
hakuwa anatania alianza kubadilika
mikononi,manyoya yalianza kutoka na kumfanya
atishe zaidi.Alizidi kunikazia macho kwa hasira.
★★★★★★★★★★
Lisa alikosa usingizi siku hiyo maana kila
alipojitahidi kuulaza ubavu wake uligoma
kabisa,alipojaribu kufunga kope zake nazo
zilimsaliti kwa kiasi kikubwa mpaka yeye
mwenyewe akahisi huenda kuna tatizo.
Moyo wake ulizidi kumuenda mbio na kila
alipojaribu kujiuliza maana yake nini hakupata jibu
la kuridhisha.Aliamua kutoka kitandani na kulielekea
jokofu ama friji lililopo chumbani mwake na kutoa
maji baridi aliyoyafakamia yote mdomoni mwake.
Baada ya kunywa maji akahisi huenda amemaliza
tatizo kumbe la! alijidanganya kwani alipoulaza
mgongo wake kitandani akaanza kuiona picha ya
Humph toka kipindi ambacho walikuwa
wanaongozana wakitoka shuleni mpaka
matembezini na mwisho likapita tukio lile la Kugala
gala kwa Humph.
Kwakuwa Lisa alikuwa tayari ni mtu mzima
alijitambua mapema kuwa ameanza kuangua katika
penzi la Humph,moja kwa moja alianza kujipiga
vibao na kujisemea "Usimpende huyo ni rafiki yangu
sawa moyo wangu sawa eeeh!! mpende yule
aliyeokoa Maisha yako"
Baada ya kitambo kirefu Lisa alipitiwa na usingizi
bila kujua ni saa ngapi ulipompata.
★★The return of amazing eyes ★★
★★Kurudi kwa macho ya ajabu★★
Samson alipoona Humph hatishiki na macho yake
mabaya alianza kujiongelesha
"Dogo inaonekana wewe ni mbishi sana sasa ngoja
nikuoneshe dawa"
Humph hakuwa na la kujitetea mbele ya Sam maana
hata zile nguvu alizokuwa nazo hazikuwepo tena,na
ni hizo hizo nguvu ambazo Samson alikuwa
akizihitaji.
Safari hii samson hakutaka mchezo kwani hats
kabla sijamjibu alianza kuota manyoya(vinyweleo)
kwa kasi ya ajabu mwili mzima pamoja na kutanuka
na kuongezeka kimo na misuli woaaaaaaaa!!
Humph alibaki ameduwaa mwili mzima ukaanza
kutetemeka na bila kutarajia miguu yake ikaanza
kurudi nyuma bila kujielewa mpaka pale miguu ya
Humph ilipogongana na kumfanya aanguke.
Samson alibadilika kabisa na kuwa na umbile
linalifanana na sokwe halisi."Rrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr" Sam
aliunguruma kwa ghadhabu.
Humph hakutambua nini cha kufanya akabaki
amekaa chini akitetemeka,hali ilikuwa mbaya
uhakika wa kupona haukuwepo kabisa kwani
inasadikika kuwa historia ya hawa viumbe hasa
sokwe unapoingia anga zao hakuachi mzima.
Sam hakuwa yule wa mwanzo ambaye alikuwa
akimbembeleza Humph ample yale macho ya ajabu
huyu alikuwa akitisha sana.Si mwili tu wa Sam
uliotosha kuogopesha la! hata macho yaliogopesha
mno kuliko hapo awali.
Sam alimgeukia mzee ambaye mpaka.muda huo
alihisi huenda anaota na pia alitamani sana ardhi
ipasuke atumbukie kwani kile alichokiona kilitosha
kabisa kuuondoa uhai wake.
Humph aliiona hatari inayoenda kutokea kwa baba
yake kwani Yale matukio aliyoyaona kwenye maono
ndiyo yale yaliyokuwa yanaelekea kutokea.
Humph hakutaka kuwa muoga tena aliamua kujitoa
kimaso maso ili mradi atetee uhai wa baba yake.
Aliinuka kwa kujikaza na kuanza kupiga hatua
kuyaelekea yale makontena.
Samson alipoona vile hakutaka kuchelewa alimuinua
mzee Kasai kwa mkono mmoja na kwa nguvu zote
alishusha Kofi la mwaka ambalo lilimgharimu
Humph katika kipindi kirefu cha Maisha yake.
Lile Kofi lilitua barabara usoni,kutokana na ukubwa
wa kiganja cha Sam kuwa kikubwa kupita kiasi
mzee Kasai alifunikwa uso mzima na kurushwa
mbali kutoka katika lile kontena walilokuwa
wamesimama mzee Kasai na Sam hadi katika
kontena linalofuata.
"hapanaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa" Humph alipiga
kelele za uchungu zilizoambatana na radi kali
pamoja na mwanga mkali zaidi ya ule ambao
aliwahi kutoa katika siku za nyuma.
Mwili wa Humph ulikakamaa ghafla kisha ukaanza
kujaa na kuongezeka kidogo.
Humph alichomoka mbio zisizo za kawaida mpaka
wakati mwingine alipita Kama upepo lakini aliona
haitoshi ni kama vile hafiki kwa mlengwa akaanza
kujirusha na kukwea makontena moja kuelekea
lingine kama nyani afanyavyo akiwa anahama
kutoka katika mti mmoja kwenda mti mwingine.
.Sam alikuwa amesimama nakuanza kujipiga piga
kifuani kama sokwe wafanyavyo akiwa anaonesha
ubabe au ameshinda vita iliyokuwa ikimkabili.Alizidi
kuunguruma lakini alisitisha zoezi lake baada ya radi
kubwa kupiga na mwanga mkali uliokuwa
umetawala eneo hilo na kujiuliza kulikoni maana
kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana
 
Sehemu ya thelathini na moja
★★Ilipoishia★★
Sam alikuwa amesimama nakuanza kujipiga piga
kifuani kama sokwe wafanyavyo akiwa anaonesha
ubabe au ameshinda vita iliyokuwa ikimkabili.Alizidi
kuunguruma lakini alisitisha zoezi lake baadaa ya
radi kubwa kupiga na mwanga mkali uliokuwa
umetawala eneo hilo na kujiuliza kulikoni maana
kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana.
★★Shuka nayo★★
Sam alifumba macho maana mwanga ule haukuwa
wa kawaida,Humph akatumia mwanya huo kumfikia
Sam na kumpiga kikumbo kizito ambacho badala
ya kumuangusha Sam kilimsogeza tu kidogo kutoka
pale alipokuwa.
Humph alidunda katika mwili wa sam ni kama
mpira unapogonga mwamba na kurudi
ulipotokea,Sam alikasirika na kumfuata Humph
lakini kabla hajamfikia alipokelewa na kiwiko cha
koromeo kilichomfanya Sam ashikilie koo lake na
kabla hajafanya lolote Humph alimrukia kichwani
kwa nguvu zote.
Walidondoka wote kutoka juu ya makontena yale
mpaka chini Humph hakuishia hapo akapanda juu
ya mwili wa Sam nakuanza kumtandika makonde
mfululizo ya usoni.
Haikusaidia kitu kwani Sam alihisi Humph
anampapasa tu na wala hakumuumiza hata
chembe,kwa mkono mmoja Humph alinyanyuliwa
juu Kisha akaanza kubamizwa katika makontena.
Maumivu aliyokuwa akiyasikia Humph si ya nchi ile
lakini hakuwa na la kufanya zaidi ya kukabiliana
nayo kiume,Sam alikuwa na nguvu mno kwani ule
mkono aliomshika Humph haukuteteleka hata
kidogo japo Humph alitumia nguvu nyingi kujinasua.
Baada ya Sam kutosheka kumbamiza Humph
alimtupa kwa kumrusha,Humph alijibamiza vibaya
chini na damu zilikuwa zikimtoka puani na
mdomoni.
Samson hakuishia hapo alianza kutafuta kitu kizito
kitakachomuua Humph mapema,katika zunguka
zunguka yake a lions mahali kuna vyuma
vimepangwa kama jukwaa akaamua kwenda
kuving'oa.
Sam akiwa anaendelea na zoezi lake la kuong'oa
vyuma huku akiamini kuwa Humph hawezi kuinuka
kutokana na kipigo kizito alichompatia alifanya
kosa!!.
Humph alishuhudia Sam.anavyojitahidi kung'oa
chuma kikubwa ambacho kwa kila dalili kilionesha
kimeanza kukubali kung'oka.Humph alifikiria afanye
nini lakini jibu likawa hakuna,
Humph alia za kuangalia kila.kona ya sehemu hiyo
ili aone kama atapata kitu cha kumsaidia na bahati
ilikuwa.upande wake maana mahali alipokuwa
amesimama sam
kulikuwa na kontena limening'inia.
Kwa hesabu za haraka haraka Humph aliona ni bora
ainuke lakini kila alipojitahidi kusimama miguu
ilikataa,hakuwa na jinsi akajilaza tena pale chini.
Sam alizidi kuvuta kile chuma mpaka upande
mmoja ukakatika,akahamia upande wa pili ili
amalizie alichokianzisha.
Humph alishangazwa na nguvu za Sam
alivyonyofoa kile kipande cha chuma aliona kwa hali
ile ataupoteza uhai wake buree.Alikumbuka jinsi
baba yake alivyopigwa na Sam uchungu ukazidi
kumshika mara dufu,hasira ikaanza kuwaka upya
moyoni mwake.
Humph akajikuta roho yake inapaya uhai tena,nguvu
za ajabu zikaujaa mwili wake na akili ikaandika
neno kisasi na kweli hicho kilikuwa ni kisasi
kinachohitaji malipo tena malipo ya damu ya Sam.
Kwa kasi ya ajabu mwanaume Humph alisimama na
kumuangalia Sam kwa jicho la chuki lakini alipotaka
kupiga hatua akamaizi kitu Kuwa atakuwa amefanya
kosa la milenia.
Sam alihisi kitu nyuma yake ikambidi asitishe kile
alichokuwa.akifanya ile anageuka nyuma Humph
akapotea na.kutokea juu ya kontena.
Sam alipomkosa Humph pale chini kengele ya
hatari ikagonga kichwani mwake akajiuliza "atakuwa
wapi huyu mpuuzi?" na kabla hajapata jibu ulisikika
mlio wa chuma kuachana kutoka juu,Kwa haraka
Sam.akatazama juu aone ni kitu gani kinachendelea
Sam alikuwa amekwisha cheleewa kwani muda ule
Humph alipopotea alitokea juu ya kontena lile na
kuviachanisha vyuma(mnyororo) ilioshikilia kontena
lile kisha akajirusha kwa nguvu kuelekea upande
unaofuata ambapo aliangukia katika kontena.
Sam alibaki ametumbua macho asijue pa kufanya
mpaka kontena lile lilipomdondokea na.kumsaga
vipande vipande.Hadithi ya afande Sam ikaishia
pale.
Humph alijiinua kwa uchovu na maumivu ya hali ya
juu akiufuata mwili wa baba yake alipoufikia kitu
cha kwanza alitaka kufahamu kama ule mwili una
uhai,Aliposhika maeneo ya shingoni aliusikia moyo
ukipiga kwa mbali.
Humph alijitahidi kumuinua baba yake na kuanza
kuondoka eneo hilo la bandari ya ocean
shore,walipofika mbali na eneo hilo walianza
kusikia ving'ora vikirindima kuja kwao.
Kwakuwa Humph ndiye alikuwa mzima pekee
hakutaka kuingia matatizoni ikiwa hata hali ya baba
yake hafahamu hatma yake.
Kitu cha MSIngi alichokumbuka ni kuwa anaweza
kupotea na mtu,kwa ustadi na nguvu kiasi
akamnyanyua babs yake mikononi wakati huo huo
gari moja ya polisi ilifika ikiwa imemulika mwanga
mkubwa(full light) upande ule ule.aliokuwepo
Humph na baba yake.
Humph aliliona hilo akafumba macho haraka huku
akiwa na wasi wasi na.kutoweka eneo hilo.Gari ile
ya polisi ilisheheni polisi wawili mmoja alikuwa bize
na.usukani na mwingine alikuwa akitazama kila
upande wa barabara.
Yule polis aliyekuwa akitazama kila upande wa
barabara alimuona Humph akiwa amemshika baba
yake lakini ghafla akambulia patupu ikabidi
ayafikinye macho yake kama anaota au la lakini jibu
lilikuwa hamna kitu pale alipoona.......
 
Sehemu ya thelathini na mbili
★★Ilipoishia★★
Yule polis aliyekuwa akitazama kila upande wa
barabara alimuona Humph akiwa amemshika baba
yake lakini ghafla akambulia patupu ikabidi
ayafikinye macho yake kama anaota au la lakini jibu
lilikuwa hamna kitu pale alipoona.......
★★Shuka nayo★★
yule polisi ilimbidi amgeukie mwenzake ambaye
alikuwa.ameuganda usukani na.kumuuliza
"Afande J umeona wale watu waliokuwa pale"
aliuliza afande yule aliyeitwa Mtani
"aaaah! Afande Mtani najua umeshaanza uoga wako
tena" alisema afande J kwa hasira
"Si uoga rafiki yangu nimewaona kabisa lakini
wanepotea ghafla" alisisitiza.afande mtani
"Mmmh! labda ni kiini macho ila kwa karne hii
hamna kitu kama hicho" alizidi kupigilia msumari
afande J
"Tatizo lako nd'o hilo mi niko siriasi(serious) we
unachukulia mzaha aya bwana shauri yako" aliongea
afande mtani
"Hauna lolote kazi uoga uoga tu kama mwanamke."
aliongea akiwa amekasirishwa na afande mtani.
Walifika eneo la tukio kisha wakaanza kupima
maeneo hayo kuanzia sehemu zenye mikwaruzo
mpaka katika tukio lenyewe na hapo ndipo lilitokea
jambo jingine.
Mzee Mandevu alivalia mavazi ya kipolisi na
kuonekana akiwa katika kitengo cha uchunguzi na
wala haikujulikana ni muda gani alifika mahala
pale.Alipomaliza kupima aliokota vinyweleo kiasi
nakuvitupia katika kijifuko maalumu cha kuhifadhia
ushahidi.
kisha akasogea eneo ambalo walikuta vipande vya
nyama baada ya kuinua kontena,mzee Mandevu
alimuona yule aliyelala pale ni binadamu lakini wale
polisi waliona ni sokwe mkubwa aliyesagwa na
kontena lile.
Baada ya kukabidhi ripoti kwa askari wale mzee
Mandevu na timu yake ya uchunguzi walisonga
mbele mpaka katika uongozi wa bandari
na.kuhojiana na mkuu huyo ambaye alidai kuwa
taarifa kamili inapatikana chumba cha kuongozea
kamera.
Kazi ya mzee.Mandevu ilikuwa ni kuhakikisha
Humph anaikwepa kesi hivyo lengo la kufika pale
kilikuwa ni kubadili ukweli kwenda kwenye uongo.
kila sekta mzee Mandevu alipewa kipaumbele
mpaka wakati wa kuona ile video iliyorekodiwa na
wasimamizi wa chumba cha kuongozea
kamera.Wasimamizi wale walidai kuwa walimuona
sokwe huyo akiwa juu ya kontena na kisha akajitupa
chini wao walihofia kumfuata kwasababu waliogopa
kujeruhiwa.
Pia walieleza sokwe yule alivyoanza kung'oa.vyuma
mpaka.akafanikiwa upande mmoja na kabla
hajamaliza upande wa pili ndipo akaangukiwa na
kontena.
Polisi walikagua video ambayo iliendana kabisa na
maelezo ya wasimamizi wale.Yote hiyo ilikuwa ni
kazi ya mzee Mandevu maana hata ndani ya video
ile Humph hakuonekana hata chembe wala baba
yake.
Baada ya mzee kuhakikisha kila kitu kimeenda vile
alivyotaka alitokomea kusiko julikana.
★★★★★★★★★★
Humph alitokea karibu kabisa na geti La hospitali ya
Dr Alex Jr na kuingia bila kustukiwa na mlinzi wa
eneo hilo.
Aliingia akiwa anaita kwa sauti "nesi nesi nesi "
huku akielekea ulipo mlango wa kuingilia hospitalini
humo,Nesi mmoja alipomuona alikimbilia kitanda
na kumfuata Humph na kumpakia mzee.Kasai
Wakiwa wanapita koridoni mbio mbio Sifa hakuwa
mbali na eneo lile.Alimuona Humph na kumkimbilia
ajue kulikoni mbona amekuja mbio mbio hivyo.
Sifa alipofika alikuta tayari mwili ule wa mzee Kasai
umeingizwa chumba cha matibabu,Humph akiwa
amechanganyikiwa ghafla anakumbana na Sifa
Macho yanamtoka Sifa baada ya kuona kuwa kaka
yake amechakaa namna ile si kwa vumbi tu bali
ikiwemo na.damu iliyogandana mwilini.
Sifa alimkumbatia kaka yake na kuanza kulia kilio
cha kwikwi kilichomfanya Humph ajisikie vibaya
kwani bila yeye yote hayo yasingalitokea katika
familia yake.
Humph alipoyafikiria hayo alimtoa haraka Sifa na
kumwambia kwa upole
"Kaza moyo dada yangu najua ni maumivu kiasi
gani unayopitia na.mimi pia napitia kipindi kigumu
namna hiyo si wewe pekee,tafadhali amini wote
tutakuwa salama"
Yalikuwa ni maneno mazito mno kwa Sifa ambaye
aliuliza swali lingine lililozidi.kuuchoma moyo wa
Humph
"na..na...na.baba kimemkuta nini mbona amekuwa
vile?"
Humph alitamani alie alipokumbuka lile Kofi
lilivyotua usoni kwa baba yake lakini hakutaka
kuonyesha udhaifu kama mkubwa katika familia yao
"Nilimkuta amezirai ndipo nikamuwahisha hospitalini
ila hali yake si mbaya sana." alieleza Humph kwa
masikitiko
Sifa alianza kuangua kilio upya ikabidi Humph
atumie ubabe kumnyazisha maana alishahisi
kinakoelekea wote wataanza kulia Kama watoto
wadogo ilihali wanajitambua na uwezo wa kujizuia
walikuwa nao pia wazazi wao hawakuwa
wamepatwa na umauti hivyo ilipaswa wajifariji ili
kujua ni namna gani watakabiliana na hali ile.
"Sifa hebu nitazame usoni" Humph alimwambia Sifa
Sifa hakuwa tayari kumtazama kaka yake
Humph,Humph akamshika kichwa chake ili
watazamane vizuri
"Nasema hivi niangalie mimi Sifa" alirudia Humph
na Sifa akafanya vile alivyoambiwa
"Sikiliza Sifa Mimi Nina uchungu pia lakini silii
kama wewe na hata kama tukikaa na kuanza kulia
haitasaidia kitu wala kuyamaliza haya matatizo la
msingi ni sisi kukaa na kutafakari jinsi ya
kuwahudumia hawa wazee sawa Sifa" Humph
aliweka kituo
Sifa akajibu kwa kichwa kuwa ni sawa alichokisema
Humph
"Aya futa machozi mama sawa tuelekee kwa dokta
kuulizia hali ya mama iko vipi".
 
Sehemu ya thelathini na tatu
★★Ilipoishia★★
Sifa akajibu kwa kichwa kuwa ni sawa alichokisema
Humph
"Aya futa machozi mama sawa tuelekee kwa dokta
kuulizia hali ya mama iko vipi".
★★Teremka nayoo★★
Wakati wanataka kuondoka dokta katika chumba
cha mzee Kasai akatoka,Humph na Sifa
wakamkimbilia wakimuuliza "dokta,dokta hali ya
baba yetu ikoje?"
Dokta hakujibu kitu zaidi ya kuwaomba wamfuate
ofisini kwake ili akawape maelezo ya kina.
Walipofika ofisini dokta aliwaomba waketi na kwa
bahati nzuri zaidi Dr Alex alikuwa akifahamiana na
mzee Kasai vyema hivyo haikumpa shida ya
kumhudumia.
"Kwanza niwape pole kwa matatizo yaliyowakumba
naamini kila binadamu huwa anapitia hali tofauti
tofauti katika kipindi chote cha Maisha yake hasa
vipindi vigumu kama ilivyo kwenu" Dokta Alex
alizungumza
"Bado hatujapoa dokta we tueleze tu hali halisi
usizunguke" alisema Humph
"Sawa ni hivi kwa hali aliyonayo mama yenu
inaridhisha kabisa na muda mfupi baadae
ataruhusiwa kutoka hospitalini lakini...lakini" dokta
akaishia hapo
"Dokta,dokta lakini nini endelea sisi tupo hapa
kupata majibu" Humph alikuwa akiongea.kwa
uchungu
"Lakini baba yenu hali yake si nzuri sana na
haijulikani itachukua muda gani mpaka arudiwe na
fahamu maana majibu yanaonesha aligongwa na
kitu kizito mno maeneo ya kichwani"
Ilikuwa ni Kama pigo kwa Humph na Sifa maana
tayari walishamzoea watawezaje kuishi wao tu,huo
ukawa ni mtihani
Sifa aliangua kilio upya ikambidi dokta Alex kutoka
katika kiti chake na.kwenda kumbembeleza lakini
kubwa zaidi Dr Alex aliwaambia kila kitu kitakuwa
chini ya uangalizi wake kuanzia.matibabu mpaka
mahitaji mengine.
Licha ya kuwa dokta huyo alijitolea vilivyo lakini
asingeweza kukaimu nafasi ya mzee Kasai.
★★★★★★★★★
Siku ilikuwa ndefu kwa Lisa,toka ameingia darasani
hakumuona Humph,alishinda hana raha akiwa
anajiuliza kuna tatizo gani mbona Humph hatokei.
Ulifika muda wa kuondoka ndipoadam Remijo
akaingia darasani humo na kutoa tangazo "kuna
taarifa zimetufikia hivi punde mwenzenu Humph
amepatwa na matatizo ya kifamilia na
ninavyozungumza hapa familia yake ipo hospitalini
wahanga ni wazazi wake hivyo ambaye atapata
muda wa kwenda kumuona na jumps pole anaweza
kutoka katika hospital ya Dr Alex Jr nadhani kila
mtu anaifahamu." alimaliza madam.Remijo na
kuondoka
Lisa hakungoja kengele aliinuka na kibegi chake
begani akaanzisha safari muda huo huo akamuone
Humph.
Lisa akiwa njiani alijishangaa jinsi alivyo na
mchecheto wa kumuona Humph mpaka
akajistukia,alipokumbuka na siku iliyopita
akagundua kuwa tayari amezama kwa Humph na si
vinginevyo maana muda mwingi akiwa peke yake
hakukosa kumfikiria hata kidogo.
Hatimaye Lisa alifika hospitalini na kuulizia
mapokezi ambapo alielekezwa moja kwa moja wodi
aliyokuwepo Mzee Kasai
Lisa alifuata korido ndefu Kisha akafuata ngazi za
kuelekea juu na huko ndipo alipoanza kuhesabu
wodi zile na alipoifikia ile wodi aliyoambiwa
alimkuta Humph akiwa amejiinamia katika benchi
Uchungu ulimshika Lisa na huruma ikamjaa baada
ya kuiona hali aliyonayo Humph ,alimsogelea
Humph na kumshika mikono alafu akahamisha
mkono mmoja na kumuinua paji la uso ambapo
alikutana na macho mekundu yaliyoashiria kuwa
Humph alilia kwa muda mrefu.
Lisa hakuongea kitu zaidi ya kumkumbatia Humph
kwa nguvu na kumnong'oneza kwa sauti ya chini
"yote ni haya ni mapito jipe moyo utayashinda"
Sifa alitoka wodini na kuwakuta wawili hao
wamekumbatiana akabaki anawashangaa na
alipoona hawajastuka ikamlazimu akohoe kidogo ili
kuwafahamisha uwepo wake pale.
Lisa aliinuka haraka haraka na kuanza kuvunga kama
hamna kilichotokea huku akiona ona aibu ndipo
Humph akaamua kuvunja ukimya ule uliotawala kwa
muda mfupi
"Lisa kutana na mdogo wangu Sifa,Sifa huyu ni Lisa
rafiki yangu wa karibu pia ni mwanafunzi
mwenzangu" Humph aliwatambulisha
"Nashukuru kukufahamu" aliwahi Lisa kumshika
mkono Sifa akiwa na tabasamu jepesi lililopokelewa
vyema ma Sifa japo kichwani mwake alikuwa
akijisemea "Ina maana wananizuga hawa mbona
kama wanamahusiano lakini poa sio mbaya
itajulikana tu,ila kama ni wifi yangu huyu kaka
anajua kuchagua vyombo aisee!!"
Sifa alipokuwa akiwaza hayo alijisahau kabisa Kama
amemshika Lisa mkono mpaka Humph alipomstua
kwa kumuita "we Sifa mbona hivyo una tatizo gani"
Sifa akamuachia mkono Lisa na kumwambia "Hata
Mimi nimefurahi kuonana na wewe"
"poleni na matatizo na ninaamini ni mipango ya
Mungu hivyo tumuachie yeye mwenyewe maana
analijua alitendalo" alitoa pole Lisa
"Asante mwaya nd'o imeshatokea hivyo hakuna
jinsi"
Basi hawakuendelea tena kuongea wakaelekea
wodini kwenda kumtazama mama yake Humph na
baada ya hapo wakaenda kumjulia hali baba yake
Humph ambaye mpaka muda huo alikuwa hajielewi.
★★★★★★★★★★
Sor hakuwa na raha hata kidogo hiyo yote
ilisababishwa na Humph ambaye kila kijana
aliyeandaliwa na Sor aliishia kuteketea katika
mkono wake.
Alijiuliza sana ni njia gani stahiki anayopaswa
kuipata ili amkomeshe.kijana Humph lakini
hakuipata.Sor alihesabu siku alizobaki nazo duniani
zilikuwa ni chache mno na bila kujihangaisha
kamwe hatofanikiwa kubaki duniani kama
anavyotaka.
Siku hiyo Sor aliamua kuitumia katika matembezi ya
hapa na pale na hatimaye akafika katika pango
moja lililokuwa kuu kuu kwa nje lakini ndani
lilionekana ni Kama limeanza kutumiwa Jana tu kwa
jinsi lilivyopambwa.
Sor alizunguka zunguka mle ndani akiwa na mawazo
tele juu ya ni kipi kitakachomfanya ayapate macho
ya ajabu.Akiwa pale katika uwazi mkubwa macho
yake yanatua katika ramani moja iliyotandikwa
vizuri.
Alipoisogelea aliitambua,ilikuwa ni ramani ya miaka
mingi mno ambayo kwa karne hii ilikuwa haitumiki
tena.Katika tazama tazama yake macho yakatua
sehemu moja palipoandikwa kisiwa cha Giza(The
dark island) akatabasamu.
 
Sehemu ya thelathini na nne
★★Ilipoishia★★
Alipoisogelea aliitambua,ilikuwa ni ramani ya miaka
mingi mno ambayo kwa karne hii ilikuwa haitumiki
tena.Katika tazama tazama yake macho yakatua
sehemu moja palipoandikwa kisiwa cha Giza(The
dark island) akatabasamu.
★★Shuka nayo★★
Tabasamu lake liliyeyuka pindi alipojuiliza ni njia
gani rahisi itakayomfanya Humph atumbukie katika
kisiwa kile.
Katika kisiwa cha giza(the dark island) ni vigumu
kwa mtu wa kawaida kugundua kuwa kuna kisiwa
hicho kilichodumu kwa zaidi ya karne na pia watu
wa jamii kama ya sor ambao hapo zamani
walipofanya makosa ndipo walitupiwa katika kisiwa
hicho ambacho kuna wengi walikiita kisiwa cha
laana maana kilikuwa na kila aina ya mateso.
Wengine walithubutu kukiita kisiwa kifo yote ni
kwasababu ukitumbukizwa katika kisiwa hicho
hakuna njia nyingine ya kutokea isipokuwa pale
utakapisamehewa kabla ya mauti kukukuta au
wasimamizi wa kisiwa kile wakutoe kwa huruma
zao japo hawakuwahi kuonekana kwa macho.
Sor alitafakari sana akijiuliza njia ipi itakayomtia
Humph majaribuni lakini akashindwa king'amua
lolote la maana litakalomsaidia katika mpango
wake huo.
★★★★★★★★★
Wanafunzi wengi walijitahidi kuhudhuria hospitalini
ili kuijulia familia ya Humph hali zao hasa baba
yake ambaye mpaka wakati huo hakuwa na hata
chembe ya fahamu.
Humph alikuwa ni mtu wa kujiinamia Mara kwa
Mara na afya yake ilianza kudhorota kutokana na
mawazo yanayokisonga kichwa chake kwa kipindi
kirefu.
Sifa alikuwa karibu sana na mama yake ambaye
aliimarika kiafya japo hakuwa na raha hata kidogo
yote ni kwasababu Mme wake kipenzi alikuwa
katika hali mbaya isiyoelezeka.
Lisa naye hakuwa mbali na Humph kila alipopata
mud a wa kuwa karibu yake.Alimfariji sana Humph
ili walau apate hata moyo wa kurudi darasani
kuendelea ma masomo.
Yote hayo yaliingia masikioni mwa Humph na
kutokea upande wa pili ni kama vile hakuusikia
ushauri wa Lisa pamoja na wanafunzi wenzake.
Siku zilizidi kukatika hatimaye mama wa.Humph
akapewa ruhusa ya kwenda kujiuguza
nyumbani,lakini hali hiyo haikumfanya ajisahau
kurudi hospitali ama kushinda hospital hapo akiwa
anaongea na Mme wake muda wote huku wakati
mwingine akilia na kuna wakati alikuwa akicheka
pia.
Kuna siku Humph alifika hospitali pale na kwenda
kumuona baba yake,alipokuwa ameketi kitandani
mkononi akiwa ameushika mkono wa baba yake
akijaribu kumuomba msamaha kuwa kosa ni lake
ghafla alisihisi mkono umemshika begani.
Humph alipogeuka alikutana na sura ya majonzi
kutoka kwa mzee Mandevu ambaye alipokutanisha
macho na Humph chozi lilimshuka kuonesha ni
kiasi gani alivyoguswa na ile hali.
Humph hakujizuia zaidi ya kuungana na mzee
Mandevu ambaye alimkumbatia Humph kwa nguvu.
"Humph jikaze kiume matatizo ni ya kila mtu"
aliongea mzee Mandevu
"Hapana hapana siwezi mzee Mandevu inaniuma"
alijibu Humph
"Huna budi kukaza moyo Humph Tafadhali"
"lakini ni baba yangu mzee Mandevu nawezaje
kuushinda moyo au kukaa kimya juu ya hili" alisema
Humph akiwa na uchungu
"Natambua hilo na pia nafahamu ni jinsi gain
unavyopitia kipindi kigumu lakini ipo njia salama ya
kulimaliza hili jambo.Je unaniamini?" aliuliza.mzee
Mandevu
"Mimi nakuamini,niambie ni njia gani hiyo nitafanya
chochote kile kunusuru roho ya baba yangu".
"usiwe na haraka nitakuweka wazi.kwanza nimsaidie
baba yako aache kupumulia mipira na tukimaliza
nitafanya kitu kwaajili yake nakuahidi" alijibu mzee
Mandevu
Humph aliingiwa na furaha isiyo na kifani mzee
Mandevu akamsogelea mzee Kasai lakini kabpa
hajafanya lolote alimgeukia Humph
"Baada ya hili hakikisha unaanza kwenda shule
sawa,Muite dokta haraka"
Humph huwa si mbishi daima aliikimbilia nje huku
akiita kwa kiwewe "dokta,dokta,dokta"
Mzee Mandevu aliitumia.nafasi hiyo vyema
kwa.kuiweka mikono yake juu ya kichwa cha mzee
Kasai na.kumuambia
"Natumaini utaota njozi njema mpaka pale
tutakapommaliza Huyu shetani". Aliongea mzee
Mandevu kisha akatoa mikono kichwani kwa mzee
Kasai kisha akasimama pembeni yake.
Muda mfupi badae mlango ulifunguliwa na dokta
akiwa anakimbia mpaka pale alipolazwa mzee
Kasai.Mzee Kasai alionekana kutetemeka mno na
ghafla akatulia,dokta alianza kupima mapigo ya
moyo ya mzee Kasai ambaye hata mashine
ilionesha kuwa mapigo ya moyo yamezima kabisa.
Dokta akaagiza.mashine ya kustulia mapigo ya
moyo iletwe lakini kabla nesi hajafika mlangoni
mashine ilisoma tena kuwa mapigo ya moyo ya
mzee Kasai yamerudi sawa sawia na safari hii
alionesha kumudu kupumua mwenyewe bila
mashine hivyo dokta akamtolea vifaa vya kupumulia
na kumgeukia Humph na manesi wengine.
"ooooooffff!!!! Mgonjwa hana tatizo nafikiri alikuwa
akipitia mabadiliko madogo yaliyosababishwa na
mfumo wake mzima wa fahamu" alitoa ufafanuzi
dokta.
Humph alimgeukia mzee Mandevu ambaye
hakuonekana na mtu yeyote mle ndani,Mzee.Mand
evu akamuonesha dole gumba akiashiria mambo
safi.
Hatimaye Humph anapata amani iliyokuwa imeanza
kutoweka na kijitabasamu kwa mbali kilianza
kujitokeza akijiona tayari yu mshindi wa kila jambo.
 
Sehemu ya thelathini na tano
★★Ilipoishia★★
Hatimaye Humph anapata amani iliyokuwa imeanza
kutoweka na kijitabasamu kwa mbali kilianza
kujitokeza akijiona tayari yu mshindi wa kila jambo.
★★Endelea★★
Lisa,Sifa na mama wa Humph walifika hospitalini na
kushangazwa na hali ya mgonjwa ilivyobadilika
ghafla,ilikuwa furaha kwa kila mtu ijapokuwa mzee
Kasai hakuwana fahamu.
Mzee kasai alikuwa katika ulimwengu mwingine
kabisa ambao ulitengenezwa na mzee
Mandevu,ulikuwa ni ulimwengu wa ndoto
isiyokwisha ambayo ilijumuisha familia nzima ya
mzee Kasai ikiwa inaishi Maisha ya furaha na amani
japo haikuwa na majirani na nyumba yao ilikuwa
imezungukwa na bustani maridhawa iliyosheheni
kila aina ya miti na maua mazuri yasiyoisha hamu
ya kuyatazama endapo ungefanikiwa kufika.
Mke wa mzee Kasai alijaribu kumshika mmewe
mkono naye akatabasamu bila kufungua macho hali
iliyozidi kumuongezea asilimia mama huyo kuwa
siku si nyingi mumewe ataamka.
Kumbe wakati mzee Kasai anashikwa na mkewe
yeye katika ndoto alikuwa amekumbatiwa na mkewe
ndiyo maana alitabasamu moja kwa moja.
Humph alipofika hospitali aliikuta familia yake ikiwa
na furaha tele na hata yeye alionekana vivyo hivyo
anafuraha kama ilivyofamilia yake.
Maisha yalianza upya Humph akarejea shuleni
kwaajili ya kumalizia mtihani wa kufungia
shule.Humph akiwa shuleni aliyakumbukaa maneno
ya mzee Mandevu
"Fanya hima umalize mitihani salama ili katika
kipindi hiki kifupi tulimalize suala hili la malkia sor"
Alitabasamu Kisha akaendelea kusubiri wasimamizi
wa mitihani wagawe mitihani hiyo waliyokuwa
wakiisubiri kwa kipindi kirefu cha mwaka mzima.
★★★★★★★★★★★
Hii ilikuwa ni siku maalumu kwa kila mtu maana
kila mmoja wetu aliipata nafasi adimu kabisa ya
kwenda kupumzisha akili yake katika kipindi cha
mwezi mzima pia ilikuwa ni furaha kwani kila
mmoja alitakiwa kwenda kusheherekea sikukuu ya
krismasi na mwaka mpya.
Humph aliutumia muda wake vizuri kuongea na Lisa
kuhusu ratiba yao ya kuonana na kwa bahati nzuri
Lisa hakuona ubaya kuendelea kumtembelea Humph
nyumbani na kwenda mara moja moja kumtazama
baba yake na humph hospitalini.
★★★★★★★★
Sor alitumia akili nyingi mno katika kutafakari ni njia
gani itakayompeleka Humph katika kisiwa cha giza
na hatimaye hisia zake zikamnasa binti mrembo
ambaye mara nyingi yupo na Humph,
Alipogundua uwepo wa Lisa karibu na Humph tayari
akawa amepata njia mbadala itakayomfanikishia
jambo lake bila bugudha ya aina yoyote ile.
Njia aliyoiwaza ilikuwa ni ya kutumia sauti ya Lisa
kumnasa humph na aliamini itamsaidia kwa asilimia
mia moja na hata zikipungua yaweza kuwa asilimia
tisini na tisa na pointi kadhaa.
Sor alianza kumfuatilia Lisa jinsi anavyoongea na
yeye akawa anaiga kwa kuifuatisha sauti ile.Mara
chache sana Humph aliweza kuhisi kuwa kuna mtu
anawafuatilia lakini alipuuzia kwa kujua kwamba
hisia zake si za kweli.
Kadri siku zilivyosonga ndivyo Sor alivyozidi
kuongeza ujuzi katika kutumia sauti ya Lisa na
mwisho wa siku akafanikiwa kabisa.
Humph akiwa ameketi pembeni ya baba yake
alimuongelesha ongelesha ghafla ndoto za usiku
ama maono yalimpata pale "Alijiona akiwa katika
shimo refu kisha akatokea katikati ya ardhi yenye
barafu kali akiwa anatetemeka bila msaada"
Humph alistuka na hofu ikamvaa zaidi akajiuliza ni
nini hicho kinachoenda kumtokea na ni nani
atakayefanya vile.Lakini swali kubwa lilikuwa ni
wapi ambapo tukio hilo litatokea kulingana na
mazingira aliyoyaona,jibu hakulipata pia aliogopa
kulazimisha kichwa chake maana shughuli yake
aliifahamu vyema.
Usiku wa siku hiyo Sor alifika nyumbani kwa kina
Humph akakagua mazingira na alipoona yapo sawa
alitoka mpaka umbali mchache kutoka wigo wa
nyumba ya kina Humph ma alipofika
alipopategemea
Akaanza kunena mane no Fulani huku akiwa
ameunyooshea mkono mduara mdogo uliopo
ardhini.Kwa maajabu ardhi ile ilianza kuzunguka
kama kimbunga hivi mpaka likatokea shimo katikati
ambalo bado lilizidi kuzunguka.
Sor baada ya kufanilisha adhma yake sasa alia za
kutembea taratibu had alipofika jirani kabisa na
wigo ule kisha akaweka mikonp mdomoni na
kuanza kupaza sauti...
"Humph,Humph,Humph,Humph,Humph,Humph...."
cha kushangaza ile sauti ilikuwa kubwa na hakuna
cha Sifa wala mama yake Humph aliyeisikia ile
sauti isipokuwa Humph.
Sauti ile ilipenya moja kwa moja katika ngome za
masikio ya Humph na kuanza kumkera,kutoka na na
usingizi mzito alikuwa nao nd'o Kwanzaa alivuta
shuka lake vizuri na kujifunika gubigubi.
Kile kitendo alikiona Sor na kilimkasirisha mno sasa
akaamua amkomeshe Humph kupitia njia mbadala
ambayo yeye aliita mpango B baada ya mpango A
kukwama.
Safari hii Sor alibadilisha mtindo wa kuita akaanza
kuita kwa sauti nyembamba mno iliyotoka kama
mruzi Fulani hivi lakini huu haukuwa mruzi halisi
bali sauti iliyopenya vilivyo katika masikio ya
Humph.
Humph na usingizi walikuwa wakipatana sana kwani
hakujali yale maumivu nd'o akaamua kabisa
kuyaziba masikio yake huku akilaani hicho kitu
kinachomharibia usingizi wake.
Sor aliona ni upumbavu kumbembeleza Humph kwa
kasauti kadogo namna ile sasa aliapa kumkomoa
Humph kuliko hapo a wali.mpaka. aamke,akatumia
sauti kama ya popo ambayo ilikuwa inakera kupita
maelezo
Hakka Sor aliwezea maana sauti moja mtu
ilimkurupua Humph kitandani akijiuliza ni.kitu
gain.kinàchotoa kelele namna ile lakini kabla
hajapata jibu akaanza kusikia akiitwa.na. sauti ya
kike inayotokea nje.
 
Sehemu ya thelathini na sita
★★Ilipoishia★★
Hakka Sor aliwezea maana sauti moja mtu
ilimkurupua Humph kitandani akijiuliza ni.kitu
gain.kinàchotoa kelele namna ile lakini kabla
hajapata jibu akaanza kusikia akiitwa.na. sauti ya
kike inayotokea nje.
★★★Endelea nayo★★★
Kwakuwa Humph alikuwa na usingizi mzito ambao
ulimchanganya ikawa si rahisi kuitambua ile sauti
ikambidi atoke nje kuangalia ni nani anayemwita.
Humph alifanikiwa kufika nje lakini Giza lililokuwepo
lilitishia amani kwa kiasi kikubwa hali iliyomfanya
Humph aogope kidogo,kadri ile sauti ilivyozidi kuita
kwa nakshi zilizopambwa na Sor jumlisha na
urembo wa sauti yake nd'o basi tena.
Humph alipogundua kuwa ile ni sauti ya Lisa
alishikwa na butwaa,inawezekanaje msichana kama
Yule aje usiku mwingi vile tena akiwa peke yake na
ulinzi wa kwao ameukwepaje? hilo likawa swali la
kwanza
Usingizi ulimpaa Humph pale pale akaanza.kuifuata
ile sauti ili ajue kulikoni msichana yule afike
kwao.muda kama ule ana matatizo gani au anahitaji
nini cha msingi.
Sor alifurahi baada ya kuona mbinu yake imefikia
asilimia Sabin na tano,taratibu akaanza kurudi
nyuma na kuipunguza sauti yake.
Humph hakujua mtego aliowekewa na sir akawa
anajipeleka kwa kuifuata sauti ile aliyoamini Kuwa ni
ya Lisa bila kujifikiria mara mbili kuwa inaweza
ikawa hatari kwa Maisha yake.
Sor alivuka shimo lake la mtego na kusimama eneo
moja lisiloonekana vizuri.Humph alipofika karibia
ma shimo akaanza kuita
"uko wapi Lisa ,Lisa ,Lisa ,wewe Lisa u wapi"
"Nipo huku ,naogopa njoo" alizungumza Sor kwa
sauti ya Lisa
Humph bila kujishauri akaanzisha mwendo kumfuata
lisa pale alipojificha.Ukisikia ndege mjanja hunasa
katika tundu bovu nd'o hapaa maana Lisa
hakutambua kuwa Humph anayale macho ya ajabu
na hapo ndipo Sor alipootea kwani Humph
hakuthubutu hata chembe kumulika kwa kutumia
nuru ya macho yake.
Sor alijipongeza kwa kazi nzuri aliyoifanya toka
awali japo hakuwa amefanikiwa moja kwa
moja.Humph alisogea mpaka lilipokuwa lile shimo
hamadii!! alitumbukia kama alivyo na ule mzunguko
haukufanya ajizi ulimzungusha kwa kasi mno
kuelekea chini.
Sor alijitokeza na kuanza kucheka kicheko kikubwa
na cha dharau,muda huo Humph alikuwa akimalizika
kichwa chake wakati anazamishwa kuelekea chini ya
ardhi.
Hatimaye Humph alizama kabisa na ghafla
akashushwa kwa nguvu katika ardhi moja ngumu
iliyosababisha Humph apoteze fahamu.
Sor alihitimisha kazi yake kwa kunyoosha mkono
wake juu ya ardhi ile na kunena maneno mengine
yaliyopelekea ardhi ile ijifunge yenyewe.Kisha kwa
tabasamu pana Sor akaondoka eneo lile huku
kichwani akianza kuhesabu siku zilizobaki za uhai
wa Humph.
★★★★★★★★★
Asubuhi ya siku mpya kabisa ilimkuta Sifa akiwa
anaandaa kifungua kinywa na baada ya kumaliza
alielekea chumbani kwa mama yake na
kumkaribisha.
Ila alihisi utofauti kwa kaka yake ambaye siku zote
huwa ni mtu wa kuwahi kuamka na kumsaidia
mdogo wake kazi ndogo ndogo za hapa na
pale,Alifikiri kuwa huenda Humph ni mgonjwa hivyo
kwa haraka alienda katika chumba cha kaka yake
nakuanza kubisha hodi.
Alibisha hodi kwa muda mrefu na hatimaye
akaamua kuingia ili ajue tatizo linalomsibu kaka
yake. Sifa alipokelewa na ukimya wa ajabu
uliomfanya aduwae kwanza na macho yake
yalipotua kitandani kwa Humph palikuwa patupu na
palionyesha muda mfupi uliopita Humph aliamka.
Sifa alirudi katika chumba cha kulia chakula (dinning
room) na kuendelea kupata kifungua kinywa bila
kujua kaka yake amepatwa na mazito.
Mama wa Humph alipomkuta Sifa peke yake
hakuvumilia akauliza ni sababu gain iliyomfanya
Humph ashindwe kujumuika mezani pale lakini jibu
alilokutana nalo ni hakutaka kuuliza tena japo
kichwani alifikiri huenda Humph ameewahi
hospitalini kumuona baba yake na upande mwingine
alijiuliza ni kwanini humph hakuaga.
Kila siku kabla ya mama wa Humph kuelekea kazini
alikuwa na utaratibu wa kupitia hospitalini kumjulia
hali mmewe kisha anaelekea katika majukumu ya
kulijenga taifa.
Sifa naye aliongozana na mama yake mpaka
hospitalini kumuona baba yake lakini Humph
hakuonekana eneo hilo.Suala hilo halikuwaumiza
vichwa walichokifanya ni kuondoka bila kuuliza hata
manesi wa eneo hilo.
Dokta Alex Jr aliendelea kushughulikia taratibu zote
za matibabu mpaka pale mzee Kasai atakapo pona
kabisa.
★★★★★★★★★★★★
Humph alizinduka na kuanza kushangaa maeneo
aliyopo kichwa kikiwa kinamuuma mno kutokana na
kuanguka vibaya.Kilichomshangaza zaidi ni lile giza
totoro.lililoshamiri eneo lile.
Alianza kukumbuka kilichotokea mpaka akafika
eneo hilo,hakukubaliana na majibu eti Lisa nd'o
alifanya yote yale,kwa hakika alitambua kuwa kale
kamchezo amechezewa na Sor na si mtu mwingine.
Chuki na hamu ya kulipiza kisasi ikaanza kumvaa na
kujikuta akitamani atoke eneo lile mapema
akamtafute Sor bila kupumzika hata siku moja
mpaka ammalize.
Akiwa katika tafakari nzito ghafla akahisi kitu
kimemchoma na kabla hajakaa sawa akachomwa
sehemu nyingine kwa haraka akatoa nuru ya macho
yake na kuangalia kulikoni,wakati huo maumivu
yalikuwa yanasambaa mwili mzima
Humph alipotazama chini alikutana na rundo la ng'e
wadogo wadogo waliokuwa wakizunguka zunguka
pale chini.Moyo wake ukalipuka,alipojaribu
kutazama upande wa pili looooh!! ng'e kubwa
zilikuwa zinakuja upande ule
Humph hakungoja kuambiwa inuka ukimbie,pale
pale alijiinua haraka na kuanza kusogea upande
mwingine na cha kushukuru ng'e waliomuuma
walikuwa ni wadogo wadogo hivyo alijisikia
maumivu na mwisho ikawa ganzi tu mwili mzima.
Humph aliona hatari zilizopo mbele yake ni kubwa
kuliko maelezo,aliona miti ikiwa imesongamana
umbali mfupi tu kutoka pale alipo akahisi labda
eneo like linaweza Kuwa salàma kwake
Kwa haraka.akafuata kichaka hadi mahali pale
palipo na miti,kwa kutumia macho yake akakagua
usalama na aliporidhika.nao.akakaa chini ya.mti
mmoja mkubwa akijipumzisha.
Kutokana na ile sumu ya ng'e aliregea Kweli kweli
na usingizi ukampitia akiwa pale chini ya mti.
 
Sehemu ya thelathini na saba
★★Ilipoishia★★
kutokana na ile sumu ya ng'e aliregea Kweli kweli
na usingizi ukampitia akiwa pale chini ya mti
★★Teremka nayo★★★
baada ya kitambo kifupi alianza kusikia sauti ya kitu
kikiunguruma chini chini ila kutokana na ule uchovu
akaendelea kulala,ile sauti ilizidi kuwa kubwa
ikiamanisha kitu hicho kimekaribia kusogea
Kitu ambacho Humph hakutambua ni kuwa katika
kisiwa hicho hakuna kupumzika hata kidogo ni
matatizo.mwanzo mwisho mpaka mauti
ikukute.Humph alizidi kulala lakini muungurumo
ulipozidi akaamka ili aone ni.kitu gani
kinachounguruma vile.
Kama alivyojishauri ndivyo alivyofanya alitoa ile nuru
kali ili aone vizuri,majani ya kwenye kichaka
yalianza kulia kwa fujo ikiwa yanaamanisha kuna
kitu kinahilazimisha kupenya kuelekea upande wa
pili.
Humph aliyatoa macho yake barabara ili
akishuhudie kitu hicho lahaulaaa!! liliibuka bonge la
mnyama yaani ngiri sio ngiri hakieleweki alafu
kilikuwa ni kikubwa cha wastani.
Humph alistuka na moyoni mwake alijisemea
"kumekucha" na kabla hajafanya lolote yule mfano
wa ngiri alifyatuka kwa kasi "ohoooooooo!!!" Humph
alisema.huku akigeuka nyuma nakuanza kukimbia
"hapa nd'o haunikamati kabisa na tumbio twako
huto" Humph aliendelea kujisemea lakini hakujua
tatizo ni moja anakokimbilia hakufahamu.
Walikimbizana mno na mwisho Humph alifika
sehemu fulani kulikuwa na shimo la wastani
akatumbukia ili kumpoteza yule mnyama.Kitendo
cha kutumbukia na kuangalia pembeni anakutana na
joka limejiviringisha linamtazama
Humph alitoka ndani ya shimo akipiga makelele
"mamaaaaaaaaaa"
★★★★★★★★★
Sor alihesabu tayari siku moja imepita na ailfahamu
wazi kuwa mwanaume hawezi kukaa siku saba bila
kula lazima afe na si.njaa pekee itakayomuua
Humph Bali na visa vilivyopo mle kisiwani.
Katika historia ya kisiwa kile hamna mtu aliyewahi
kutoroka hata siku moja.Hayo yote yalimfanya Sor
atabasamu kila muda kwa kujiona mshindi tena
alichosubiri ni siku ifike akachukue macho yake ya
ajabu.
Upande wa familia ya humph vichwa vilizidi
kuwauma kwani siku moja ilikuwa imeisha na sasa
walikuwa wakiitafuta siku ya pili bila kumuona
Humph
Lisa alipewa taarifa ya kutokuonekana kwa
Humph,alishindwa afanyaje maana Humph hakuwa
na marafiki wa wengi na ukizingatia shule
ilishafungwa muda sasa na.kila mtu alielekea
mahali ambako alihisi patamfaa kusheherekea
sikukuu hizo zinazofuata.
Sifa na mama yake Humph walishauriana wasubiri
na siku hiyo ipite na kama Humph hajaonekana
ndipo watoe taarifa vituo vya polisi na vituo vya
kurusha matangazo(vyombo vya habari)
★★★★★★★★★★
Humph alipotoka katika lile shimo alikutana na yule
mnya anayefanana na ngiri kwa maumbile ikabidi
Humph asimame na kumlia doria yule ngiri.
Yule ngiri alipoona wanatazamana na Humph akajua
nd'o.muda.wa kujipatia kitoweo akaanza kuparua
chini kwa.kwato zake kama mbogo aliyejeruhiwa
Humph alijua kinachofuata maana aliwahi kuona
filamu nyingi za wanyama,ambapo tabia kama ya
mnyama huyo huwa wanakuwa Nayo mbogo na faru
kabla yule mnyama.hajaachia mbio nyuma ya
Humph kulianza.kusikika mlio.Fulani wa
"hssssssss" moyo wa Humph ukaanza kukimbia
mbio mbio
Mjanja kuwahi ndivyo ilivyokuwa kati ya joka lile
likubwa na ngiri,wote walikuwa wanawinda windo
moja yaani humph aliyekuwa katikati yao.
Joka lilijitanua tayari kwa kujirusha limviringishe
Humph na muda huo ngiri alikuwa amejiandaa
kuchomoka ili amrarue Humph.
Yote hayo Humph aliyatambua kupitia ufahamu
wake wa akili na moja kwa moja akajipanga
kumkwepa mmoja wao au wote ikiwezekana
Na bahati bado ilikuwa upande wake kwani Joka
lilijiachia kwa kasi na muda huo huo ngiri naye
alichomoka kwa kasi,Humph akajirusha upande wa
pili kwa kujipinda mno.
Ngiri na joka lile vikagongana na kutoa mlio mkali
ambao ulitokana na maumivu makubwa baada ya
kugongana.Humph aluangukia pembeni bila kuumia
sana,Akakaa na kupumzika kidogo kabla hajaliona
jiwe Fulani kubwa linalong'aa kwa mwanga hafifu na
kwenda kujipumzisha.
★★★★★★★★★
Mama wa Humph hakuwa naraha hata kidogo alihisi
kuchanganyikiwa yote ni kutoka na na mfululiZo wa
matukio yanayoiandama familia yake,baba mwenye
nyumba amelazwa hospitalini na mwanae wa kiume
hajulikani aliko hilo suala lilimtia wazimu mno.
Sifa na mama yake walifika katika vituo mbali mbali
vya habari na polisi kutoka taarifa za kupotea kwa
kijana wao,Matangazo yalianza kuruka hewani na
mtu ambaye angefanikisha upatikanaji wa Humph
aliahidiwa donge nono.
Watu walianza msako wa Kumtafuta Humph kila
mahali kwani Hamna mtu ambaye hakupenda
kupata kitita cha hela kilichotangazwa baada ya
kumpata mtahiniwa.
Lisa pia hakuchoka kumtafuta Humph kila mahali
alipohisi huenda angefanikiwa kumuona,alijitahidi
kila jioni kufika sehemu ambayo walikuwa
wakikutana mara kwa mara lakini matokeo yalikuwa
yale yale Humph hakutokea na yeye alizidi
kutonesha vidonda ambavyo kila siku alijitahidi
kuvificha ili visijitokeze yaani mapenzi yake
yaliyoanza kuchanua kwa Humph alijitahidi kuyaficha
ila sasa yalimsurubu vilivyo.
Lisa alitamani hata angekuwa anamfahamu rafiki wa
Humph ambaye aliwahi kumuokoa kipindi cha
matatizo huenda Huyo angemsaidia kumpata
Humph.
Kila siku inapofika muda wa chakula katika familia
ya Humph watu walikosa raha si mama yake
Humph wala Lisa wote walikuwa na majonzi.
 
Sehemu ya thelathini na nane
★★Ilipoishia★★
Kila siku inapofika muda wa chakula katika familia
ya Humph watu walikosa raha si mama yake
Humph wala Lisa wote walikuwa na majonzi.
★★★Shuka nayo★★★
lakini hawakuwa na la kufanya zaidi ya kusubiri
majibu kutoka kwa mtu am aye angefanikisha
kumleta Humph akiwa hai ama amekufa.
Kiukweli familia ilikuwa imepoa sana hasa
ukizingatia mazoea yalivyo na taabu,walizoea kupiga
soga kutaniana pamoja na kujadili mambo kadha
wa kadha ila sasa familia ya watu wanne imebaki na
watu wawili.
Hata usingizi kwao ulikuwa ni mtihani na Mara
kadhaa waliona bora wafunge safari wakakae
hospitalini na mwili wa baba yao ambao mpaka
muda ule haukuwa na fahamu.
Mama yake Humph alipenda sana kumsisitiza
mmewe kila anapokwenda kumuona kuwa "toka
umelala hapa mambo mengi yamekuwa
yakinielemea na ni adhabu tosha kwangu,tambua tu
kuwa kuishi bila mwongozo ni kazi ngumu tafadhali
amka uone haya yanayotukumba familia yako labda
wewe utajua namna gani utaweza kuyafumbua."
Lakini yote yalikuwa ni sawa na kutwanga maji
kwenye kinu kwani mzee Kasai hakuweza kusikia
neno hata moja kati ya yote yaliyotamkwa na mke
wake.
★★★★★★★★★★★
Hatimaye Humph alimaliza siku tano akiwa
anazunguka katika kisiwa kile kidogo na
kilichomstaajabisha zaidi ni baada ya kuelekea
magharibi na kuja kutokea mashariki ni kama vile
kile kisiwa kilikuwa cha duara Fulani maana hata
alipoenda kusini alitokea kaskazini.
Ile hali ilizidi kumtisha akawa hana jinsi zaidi ya
kurudi katika jiwe lile lenye mwanga hafifu ambalo
alilitumia kama maficho na ngao vile vile maana
katika kisiwa kile kilikuwa na vitu vingi vya ajaabu
ajabu kwa mfano kuna wakati Humph alisikia sauti
za watu wakipita huku wakiongea lugha za ajabu
ajabu ambazo hakizielewa.
Na wakati mwingine Humph alijitahidi kuwafuata
lakini hakuona wanakoishia kwasababu walipotea
katikaa mazingira yasiyoeleweka,pia alijitahidi sana
kupotea lakini kilichompata alishindwa kurudia tena
l,Mara ya kwanza kupotea alitokea kwenye kundi la
dubu weusi hali iliyomlazimu apotee tena haraka
kabla hajanaswa na kugeuzwa bucha.
Humph alizidi kuteseka na njaa pamoja na kiu kikali
na mpaka siku hiyo ya nne mwanga wa macho yake
ulikuwa umefifia mno kama tochi iliyoisha
betrii,sasa hata nguvu ya kuinuka ilimuishia akabaki
amejiegesha katika jiwe lile kubwa akisubiri kifo
chake.
★★★★★★★★★★
Mzee Mandevu alitembelea chumbani kwa Humph
amjulie hali ili waanze rasmi msako wao wa
kumuangamiza sor,cha ajabu alikutana na kitanda
tu,alipokisogelea na kushika akapata matukio yote
yaliyotokea kwa Humph.
Mzee Mandevu alimuona jinsi Humph alivyotoka nje
lakini hakujua ni kwanini alitoka na alipoona alifika
mahali akapotea pia mzee Mandevu hakuambulia
lolote pale akaamua kutumia njia anayojua yeye
kumtafuta Humph kwasababu yeye ndiye
alimkabidhi macho Yale ya ajabu alijua na njia ya
kumpata kiurahisi zaidi.
Alisimama sana chumbani mwa Humph akijaribu
kumtafuta lakini hakupata kitu ndipo machale
yalianza kumcheza na kuhisi huenda kitu kibaya
kimemkuta Humph
Akili ya mzee Mandevu iliingiliwa na virusi ambavyo
viliitafuna kweli akili yake havikuwa vingine bali
mawazo yaliyokisonga kichwa chake kwa muda
mfupi tu. Hakika mzee huyu wa makamo alichoka
kupita maelezo.
Mpaka ikafikia hatua akaamua kukaa kitandani kwa
Humph yote ni kudhihirisha jinsi alivyochoka na
kitendo kile ndipo hata Mimi nikagundua kuwa Sor
si wa kitoto kwani amesumbua hata wazee
wazamani akili zao.
★★★★★★★★★★
Humph aliona kifo kilivyo kuwa jirani yake na hapo
hapo mvua ya barafu ikaanza kushuka na
kumsurubu vilivyo,baridi kali ikawa inauzonga mwili
wake .
Akaanza kutetemeka mithili ya simu ya Nokia ya
tochi inapokuwa mezani ikiita,Bila shaka alihitaji
joto na kwa bahati mbaya joto hilo yalikuwa kwake
bali mahali ambapo hata angetumia ubabe gani
asingepafikia.
Sasa Humph alianza kuhisi anaelekea kukata moto
(kuzirai) na kwa Mara ya kwanza akili yake ikafanya
kazi,kazi ambayo hata yeye aliisifu na kujisemea
moyoni kuwa Kama akili ingekuwa inaonekana basi
ningeipa akili yangu zawadi.
Kitu ambacho kilimjia Humph kichwani ni msaada
tena msaada kwa mtu ambaye aliapa kumsaidia
wakati wowote na popote pale bila kujali hali ya
mahali anapohitajika kutoa msaada.
Huyu alikuwa mzee Mandevu na ndipo hapo
ambapo akili ya Humph ilisimama dede,akaanza
kuita lakini sauti haikutoka kutokana na ukavu wa
koo lake
akaamua kuyakusanya mate yake na kuyameza kwa
nguvu mpaka yakamletea maumivu kisha akajaribu
kufumbua mdomo wake lakini nao haukutii,Akatoa
ulimi wake nje na kuziramba papi za midomo yake
ili kuzilainisha na kujaribu tena kumuita mzee
Mandevu
Sauti ilitoka kwa tabu mno lakini akiwa pale pale
chini bila matumaini anasikia sauti za watu wale
wanaoongea lugha za ajabu wakipita na ghafla
wanakaa kimya na kusimama na baada ya muda
mfupi walianza kusogea kule alipojiegesha Humph
wakiwa na tahadhari ya hali ya juu.
Mzee Mandevu anaisikia sauti ya Humph ikimwita
kwa shida na ndipo hapo mzee huyo anapostuka na
kuangalia kila pande za dunia ni Kama anatafuta
kitu na mwisho alichukua mkongojo wake na
kupotea nao.
Wale watu wanaoongea lugha za ajabu walimfikia
Humph mmoja akachomoa kisu kidogo kutoka
katika ara yake na kumsogelea Humph kwa kunyata
na hapo ndipo Humph alipoona anakufa kizembe
akajitutumua kuliita jina la mzee Mandevu na sauti
ikatoka kubwa na kumfanya yule mtu kuogopa
kwanza na kurudi nyuma
Radi kali ilipiga maeneo hayo na kuwafanya watu
wale wageuke nyuma ikawa ni kosa kubwa kwao
kwani walikutana na mzee Mandevu ana kwa ana
akiwa amefura kwa hasira na bila kupoteza muda
alitoa radi moja matata katika mkongojo na
kusababisha wale jamaa kugeuka majivu pale pale.
Humph alivyoona vile alitabasamu na kuzirai pale
pale(kuzimia)..
 
Sehemu ya thelathini na tisa
★★Ilipoishia★★
Radi kali ilipiga maeneo hayo na kuwafanya watu
wale wageuke nyuma ikawa ni kosa kubwa kwao
kwani walikutana na mzee Mandevu ana kwa ana
akiwa amefura kwa hasira na bila kupoteza muda
alitoa radi moja matata katika mkongojo na
kusababisha wale jamaa kugeuka majivu pale pale.
Humph alivyoona vile alitabasamu na kuzirai pale
pale(kuzimia)..
★★★Teremka Nayo★★★
Mzee Mandevu alifiika na kumnyanyua Humph na
kutoweka nae eneo hilo kwa mbwembwe za
hatarii.Alimfunika Humph na nguo Fulani za zamani
nzito zilizokaa kama taulo hivii.
Mzee Mandevu hakutaka kupita njia ya mkato
aliamua kutokea ndani ya wigo wa nyumba ya kina
Humph na kwenda kugonga mlango uliofunguliwa
na Sifa ambaye macho yalimtoka baada ya
kumuona kaka yake akiwa amebebwa mikononi
mwa mzee yule.
Uwepo wa mzee Mandevu ndiyo uliyomstua na
kumfanya akimbilie ndani huku akimuita mama yake
aje kuona kile kilichotokea.
Sifa alisahau hata kumkaribisha mgeni ndani na
mzee Mandevu hakuwa na haraka aliganda pale pale
bila kuingia ndani.
Mama wa humph alitoka mbio na hakujali ule uzee
wake na kwa furaha kubwa iliyochanganyikana na
huzuni akafanikiwa kufika mlangoni na kumkuta
mzee Mandevu akiwa bado amemshikilia Humph
akisubiri kukaribishwa.
Mama Humph alimkaribisha mzee yule kwa kilio
kikuu nadhani hata wakina mama mnatambua ni
kwanini huyu mama alilia badala ya kupiga vigere
gere.
Mzee Mandevu aliruhusiwa kuingia ndani na moja
kwa moja akaketi kitini ili wajadili kidogo ndipo
taratibu nyingine zifuatie
"Habari yako mama,pole na matatizo" alianza
kuzungumza mzee Mandevu
"Nashukuru baba sijui hata nikushuruje" akaanzisha
kilio upya baada ya kutamka maneno yale
Sifa anaanza kumbembeleza mama yake.atulie
ndipo mzee Mandevu anaendelea na maneno yake.
"Pole sana na pia naomba ujikaze Kwakuwa
mwanao yuko salama salmini hivyo tafadhali jaribu
kujali kwanza afya yake usijipe presha sawa mama"
alizidi kuongea mzee Mandevu
"Nimekuelewa baba sijui hata nikupe nini lakini
Mungu pekee atakulipa maana nilicho nacho ni kiasi
kidogo kitakachokusogeza mbele ndani ya siku
mbili tatu hizi" alijibu mama wa humph
"Hapana,hapana sihitaji chochote kutoka kwenu
Mimi ni raia mwema tu na nimefanya hivi Kwakuwa
natambua vyema sana uchungu wa kupotelewa na
mtoto" alisisitiza mzee Mandevu
"Kazi uliyoifanya ni kubwa mno na isitoshe Huyu ni
mwanangu pekee wa kiume,kwahiyo nakuomba
uchukue hata hiki kidogo tulichokiandaa" alizidi
kushikilia msimamo wake mama wa Humph
Mzee Mandevu aliamua kuinuka huku akizidi
kukataa kata kata baada ya kuona Sifa anaelekea
katika mtoto wa kabati yaani droo na kuifungua.
Mama wa Humph baada ya kuona mzee Mandevu
anaondoka akasitisha zoezi lile na kumuomba mzee
yule arudi na kuketi tena.
Mzee Mandevu alirudi safari hii akiwa na tabasamu
pana usoni mwake,alipoketi akaanzisha tena
mazungumzo
"Hatuna muda wa kuangaliana tena wewe binti
nenda kaandae uji mwepesi sasa hivi na wewe
mama nipeleke bafuni sasa hivi ili nimuhudumie
kijana wako" Mzee aligawa madaraka ambayo
hakuna aliyepinga zaidi ya kuyatekeleza
baada ya dakika chache.mzee Mandevu alikuwa
bafuni akimsafisha Humph maana alikuwa
ametapakaa kila aina ya uchafu si tope wala vumbi
vilivyomfanya azidi kuonekana amefubaa vilivyo
kupita kawaida,Nguo alizovaa mwilini zilikuwa
zomechoka na kutoa harufu Fulani ambayo haifanani
na marashi yoyote duniani nikiamanisha haiwezi
ikapita saa nzima haujaugua mafua na ikiwa hivyo
basi una pua adimu isiyoingilka kiurahisi.
Mzee Mandevu hakuwa mtu wa kawaida wale
wenzetu wa kimombo wanawaita watu wa namna hii
"immortals" yaani watu wanaoishi milele na sijui ni
kwanini alikuwa wa milele ila utatambua mbele.
Baada ya Humph kuogeshwa akiwa hana fahamu
vile vile alibebwa mpaka.kitandai ambako kila mtu
alingojea arudiwe na fahamu lakini mzee Mandevu
aliomba uji aliogiza upikwe na mara moja akaanza
kazi ya kuupoza na kumnywesha Humph ambaye
kwa maajabu kabisa aliupokea na kumeza bila
kufumbua macho yake.
Wote walishangaa inawezekanaje mgonjwa asiye
nafahamu anywe uji bila kufumbua macho? lakini
jibu lilibaki kwa mzee Mandevu ambaye hiyo ilikuwa
kazi yake katika kuhakikisha kijana wake anakuwa
sawa.
Mzee Mandevu alipomaliza kumnywesha Humph uji
alimuacha na kuomba Sifa na mama yake wazidi
kungoja mpaka pale Humph atakapozinduka,kiufupi
tu Humph alipitia matatizo kibao(mengi,) katika Kile
kisiwa cha giza kiasi kwamba wakati amelazwa
kitandani aliendelea kupiga kelele akiwa anaota
mpaka ikawalazimu muda mwingine kumshikilia
Humph asianguke kutokana na mtetemo aliokuwa
nao.
Hayawi hayawi sasa yalikuwa Humph aliamka akiwa
anashangaa sehemu aliyopo maana mazngira
yalikuwa tofauti na Yale ya kisiwa cha giza.
Mama yake Humph alilipukwa na shangwe za kufa
mtu na kumkumbatia mwanaye huku Sifa akiwa
anatabasamu tuu na mzee Mandevu aliwasindikiza
na kuwapa ushirikiano kwa kutabasamu pia.
Kwakuwa kila mtu alikuwa na shauku ya kutaka
kusikia kile ambacho kilimkuta Humph hawakusubiri
walianza na maswali ya moja kwa moja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom