Simulizi: Laana Za Maiti

Simulizi: Laana Za Maiti

SEHEMU YA MWISHO

Nilishtuka kuwaona wakitokea kwenye w wa kuelekea nilipokuwa nimesimama huku nimechanganyikiwa. Sikukubali wanikamate kwani maneno yao yalionesha wana hasira na mimi. Niliwapowaona wakinisogelea bila kuangalia nitaangukia wapi nilijiachia nilipokuwa nimesimama na kujitupa chini.

Nilipotua chini kilichoendelea sikujua mpaka nilipozinduka siku ya tatu na kujikuta nipo hospitali nikiwa nimevunjika mguu mmoja wa kushoto. Mke wangu na rafiki yangu Somati waliniuliza kipi kimenisibu kuwa katika hali ile. Mke wangu na watu wengine niliwaeleza niliteleza wakati nazungumkia ujenzi na kuangika chini.

Lakini nilipobakia na Somati nilimweleza ukweli kitu kilichoinitokea ambacho alikipinga kwa kusema lazima ile ilikuwa ndoto.
“Mawazo si kweli hakuna kitu kama hicho hiyo ilikuwa ndoto.”
“Somati ninachokueleza ni kitu cha ukweli kabisa hata mimi mwanzo niliona labda ndoto.”

“Mawazo mimi nimefanya kazi hii zaidi yako na nimefanya mambo ya kufuru kuliko wewe, mbona haikunitokea na kama waganga ninaotumia mimi ndiyo niliokupeleka.”
“Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, ile ilikuwa nini?”

“Ile maiti ya mtoto ipo wapi?”
“Hata sijui kwa vile toka nilipojirusha sijui nini kilichokuwa kikiendelea.”
“Ngoja niulizie kwa vijana wako.”
“Hapana nenda mwenyewe katika chumba nilicho uweka mwili wa kile kichanga.”
“Sawa wacha niende.”
“Kama vipi maliza kila kitu na umpelekee jamaa utakupa mzigo.”

“Hakuna tatizo.”
Somati aliondoka na kuniacha nimejilaza kitandani huku nikijiuliza kilichonitokea kilikuwa kitu gani kwa vile jambo lile niliamini ilikuwa ni ndoto lakini yenye ukweli. Kutokewa na maiti nilizowahi kuzikata viungo pia maajabu ya kichanga kulia kikiwa hakina uhai.

Kwa vile bado mguu ulikuwa na maumivu ya mbali nilipewa dawa za usingizi na kujilaza. Nilishtuka baada ya saa nne, wakati huo ilikuwa saa kumi na mbili jioni, pembeni ya kitanda changu alikuwepo mke wangu na dereva wangu. Wote walionekana wana nyuso za huzuni kitu kilichonitisha.

“Vipi jamani kulikoni?”
“Kuna habari si nzuri.”
“He! Mbona mnanitisha?” Nilishtuka.
“Shemeji Somati amefariki dunia.”
“Ati nini?” sikukubaliana na taarifa ile.
“Shemeji Somati kafariki dunia,” mke wangu alirudia.

“Hapana hapana acheni utani, mchana si nilikuwa naye.”
“Ni kweli bosi kutokana na maelezo ya mlinzi, mchana alikwenda kwenye site na kuomba kuingia ndani. Kwa vile anafahamika aliruhusiwa, baada ya muda alitoka akipiga kelele kama anafukuzwa na kitu cha kutisha. Alitoka mbio kwenye geti bila kuangalia wakati anavuka barabara aligongwa na gari ambalo halikusimama.

“Mlinzi alipotoka alikuta tayari ameisha kata roho huku ulimi na macho vikimtoka pima, watu wamejaribu kuurudisha ulimi na kumfumba macho imeshindikana.”

“Mmh!” taarifa ile ilinitisha na kujua hali imekuwa mbaya kama mtu niliyekuwa nikimtegemea amekufa kifo kibaya hasa baada ya kuingia chumba cha maiti ya kichanga.
“Sasa maiti yake ipo wapi?”
“Ipo hospitali ya mkoa, ndugu zake tumeishawapa taarifa lakini hatukuwaeleza sababu ya kifo chake bali amepata ajali.”

“Mtakuwa amefanya jambo la maana kwa vile ile ni lawama.”
“Mume wangu nyumba yako ina nini? Juzi wewe, leo mchana rafiki yako kipenzi amekufa. Kuna nini?” mke wangu aliniuliza.
“Mke wangu hebu hilo liache tutazungumza nyumbani.”

“Utatoka lini maana mguu umevunjika mara mbili?”
“Hilo lisikutie shaka kuna dawa za asili nikifunga ndani ya wiki mbili natembea.”
“Mmh! Haya.”
Mke wangu alikubali kwa shingo upande huku akiwa na maswali yasiyo na majibu juu ya matukio mawili yaliyotokea kwenye jumba langu la kifahari.

Nilitaka kumtuma kijana wangu kwenda kuuondoa mwili wa kichanga lakini nilihofia kumkuta yaliyomkuta rafiki yangu Somati.
Lakini sikuwa na jinsi ilikuwa lazima kiumbe kile kitolewe kabla hakijaanza kunuka na kusababisha harufu mbaya. Nilimweleza kwa siri akautoe ule mwili na kwenda kuutupa au kuuzika. Baada ya kuondoka nilikuwa na wasiwasi wa kusikia habari mbaya.

Lakini baada ya muda alirudi na kunieleza amefanya kama nilivyoelekeza mwili wa kichanga ameuzika nyuma ya nyumba. Nilishukuru kwani kama mwili ungekutwa mule ndani kesi yangu ya kuuza viungo vya mwili ingefumuliwa upya. Lakini nimsisitiza abakie na siri ile asimwambie mtu.

Mazishi ya Somati yalifanyika kijijini kwetu lakini kutokana na hali yangu sikuweza kushiriki. Nami niliendelea vizuri na matibabu ya mguu kwa kutumia dawa za asili ambazo zilinisaidia kuweza kutembea haraka japo nilikuwa sikanyagi mguu kwa nguvu lakini hali ile nilijua ingeisha baada muda na kutembea vizuri.

Baada ya kuwa katika hali nzuri nilipanga kwenda kwa mganga niliyepelekwa mara ya pili na marehemu Somati aliyeimaliza kesi yangu kimiujiza. Muda wangu wa kurudi kazini ulipofika, nilihofia hali ile kujirudia nitakapoingia chumba cha maiti. Nilipanga kuanza kazi mpaka nitakaporudi kwa mganga.

Nilimchukua dereva wangu ambaye ndiye niliyemfanya msiri wangu kwa muda ule baada ya rafiki yangu kipenzi Somati kufa kifo cha ajabu na sababu kubwa nikiwa ni mimi.

Nilipanga kuondoka mwisho wa wiki ile mwanzo wa wiki niwe kazini, nilitaarufu tuna safari.
Baada ya kuiandaa safari tuliondoka alfajiri ili tuwahi kufika kupata huduma na kurudi. Tulianza vizuri safari yetu vizuri, tulipofika nusu ya safari tulikutana na watu waliokuwa wakienda kuzika.

Siku zote ilikuwa desturi ukikukatana na watu wanaokuwa wanakwenda kuzika lazima usimame na ubebe kidogo ndipo uendelee na safari.
Nilimwambia dereva asimamishe gari na mimi kuteremka, nilichepua mwendo kuwahi mbele na kushika jeneza na kuanza kutembea. Lakini ajabu baada ya kutembea hatua mbili nilimsikia maiti aliyekuwa ndani ya jeneza akisema kwa sauti kubwa:

“Jamani huyo atanikata viungo.. nakufa nakufa muueni na yeye.”
Niliamini sauti ile wote wanaisikia, woga ulinishika nashukuru nilikuwa nimeisha liacha jeheza bila hivyo ningeliachia. Niliwaangalia watu wote waliokuwa wako bize na kwenda kuzika. Nilijiuliza ina maana sauti ile hawaisikii, kwa sababu ilikuwa ya juu sana.

Nilimsikia akiendelea kupiga kelele huku akisema kama wameshindwa kunitia adabu basi anatoka yeye. Nilianza kuliona jeneza likicheza kuonesha yule maiti anataka kutoka kunifuata kunitia adabu. Niliwaona watu wakihangaika kulitulituliza jeneza lililokuwa halitulii mabegani.

Nilipowaona wanaliweka chini nilichanganyikiwa zaidi baada ya kumuona maiti akitoka kwenye jeneza ili anifuate. Nilitimua mbio huku nikipiga kelele, kilichoendelea sikujua mpaka nilipojikuta kwa mganga wa kienyeji. Nilipojiangalia nilikuwa nimedhoofu mwili pembeni alikuwa mke wangu ambaye naye alionekana amedhoofu pia.

Mke wangu alionekana mwenye mawazo mengi, nilitembeza macho na kuyaona mazingira kama ya wa mganga. Nilipojichunguza niligundua nimefungwa kamba kwenye shina la mti. Nilijishangaa kuwa kwenye hali ile, nilinyanyua mdomo wangu kumwita mke wangu.

“Mke wangu.”
Ajabu mke wangu badala ya kuitikia alishtuka na kunikimbia, nilijiuliza mbona amenikimbia. Baada ya muda alirudi na mzee wa makamo ambaye alionekana ndiye mganga na vijana wake na kusema:

“Mfungueni kamba.”
Walinifungua kamba na kusimama, nilikuwa nimevaa kaniki kifua wazi, nilijiuliza pale nimefikache. Kabla sijajua nimefikaje pale nilipigwa na maji ya uso yaliyonizindua na kuzidi kujishangaa. Nilipojiangalia nilijikuta nimebakia mfupa na nguzo nywele nyingi na ndevu nyingi.
Nilichukuliwa na kwenda kuogeshwa kisha nilipewa dawa ya kunywa na kinifanya nilale mpaka siku ya pili.

Ndipo nilipopata nafasi ya kuzungumza na mke wangu na mganga na kuelezwa kuwa imepita miaka sita toka nilipopata tatizo la ugonjwa wa akili baada ya kusindikiza msafara wa mazishi kama walivyoelezwa na dereva wangu. Nilipovuta kumbukumbu nilikumbuka kilichotokea miaka hiyo sita kama walivyosema. Nilielezwa tokea siku ile niliugua ugonjwa wa akili kwa kukimbia mabarabarani bila nguo.

Mke wangu alinieleza alinihaingaikia kila kona kwa waganga na kwenye maombi bila mafanikio. Kila nilipopata nafuu kidogo nilipoliona jeneza au makaburi kichaa kilianza upya mpaka walipompata yule mzee ambaye aliwahakikishia atanitibu kwa muda mfupi kwa vile tatizo langu aliliona.
“Mume wangu kwa nini uliyafanya yote yale?” mke aliniuliza mkono shavuni huku machozi yakimtoka.

“Yapi mke wangu?”
Alinieleza siri yote ya mambo niliyokuwa nikifanya ya kuuza viungo vya maiti na kusababisha laana yao inirudie na kama nisingempata mganga yule ningekufa kama rafiki yangu Somati aliyeuawa na mizimu ya marehemu wale hata gari lililomgonga na kumuua halikuwa gari kweli.

Baada ya maelezo yale alinieleza jinsi mali yangu yote ilivyoteketea kwa ajili ya kutafuta tiba yangu iliyokuwa ikila pesa kila kukicha.
“Mume wangu imebakia nyumba moja tu tunayoishi, nimeuza kila kitu ili nikutibie.”

“Mmh!”
“Na mganga amesema na ile nyumba tuiuze na fedha yake zitengenezwe ili tuweze kuzitumia bila hivyo nazo zitateketea. Sikuwa na la kusema nilikubali kila kitu kifanyike kwa kusimamiwa na mke wangu. Baada ya kitu kwenda kama alivyoelekeza mganga.
Niona hakuna haja ya kuendelea kukaa mjini nilirudi kijijini na pesa tuliyouza nyumba nilianzia maisha nyumbani.

Namshukuru Mungu sasa hivi mimi na familia yangu tumemrudia bwana tumeokoka, maisha yetu yaliyobaki tumeyakabidhi mikononi mwake.
Kila siku siachi kumuomba msamaha Mungu wangu anisamehe kwa yote niliyoyafanya ambayo yalimchukiza pia kuendelea kunipa uhai ili niweze kutubu na kuweza na kuutoa ushuhuda.

Japo nina maisha magumu lakini nimerizika nayo kwa vile yananipa uhuru pia kunipa nafasi ya kuwa karibu na muumba wangu. Ndugu zangu hapa ni mwisho wa simulizi yangu. Ila nataka kuwaambia maisha yaliyo mazuri ni kuyafanya yamfuraishayo muumba wako na kuyaacha yote yamchukizayo.

Chini ya jua hakuna kimbilio zaidi ya kujikabidhi mikononi mwa muumba wako kwake yeye ni kila kitu. Heri kuwa maskini mali ya Mungu kuliko kuwa tajiri uliye mali ya shetani. Jiepushe na utahiri wa kutegemea nguvu za giza siku zote yana mwisho mbaya.
Mwisho

Dah!! Mafanikio kwa njia za mkato siyo vizuri kabisa...

Ni nzuri ila inatisha...

Chapter closed...


Cc: mahondaw
 
Nyuzi zako nazifuatilia kwa udi na uvumba ndio jambo la kwanza ninapoingia jf

Zina mafunzo ya kutosha juu ya ulimwengu mwingine tusioujua hivyo mtu akiamua kupata mali za mkato atakuwa na A, B, C nini mbeleni kitafuata baada ya kula mali za shetani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nyuzi zako nazifuatilia kwa udi na uvumba ndio jambo la kwanza ninapoingia jf

Zina mafunzo ya kutosha juu ya ulimwengu mwingine tusioujua hivyo mtu akiamua kupata mali za mkato atakuwa na A, B, C nini mbeleni kitafuata baada ya kula mali za shetani

Sent using Jamii Forums mobile app
Asante sana mkuu karibu

Kuna nyingine pia zinaendelea nahisi umeshaziona
 
Habari mambo naitwa Mr Equator Nimeandika ujumbe huu kuku omba swala moja tu!
Mimi nimetengeza website ya ku share story ambayo ni http://www.equatorstory.com/
Je umekuwa ukipata tabu kupost story zako hapa?
Hili ndo suluhisho lako.
Mimi nataka nkupe nafasi ya kuwa mmoja wapo wa kwanza kutumia hii website
unda account yako na uweze kupost story yako mpya.
 
Duh inasikitisha kuona jamaa pesa,Mali na vyote alivyohangaikia miaka yote ili akiacha kazi aje afaidi vimeteketea! Kwa maana nyingine amefanya kazi bure maisha yake yooote!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom