Simulizi: Laana Za Maiti

Simulizi: Laana Za Maiti

SEHEMU YA MWISHO

Nilishtuka kuwaona wakitokea kwenye w wa kuelekea nilipokuwa nimesimama huku nimechanganyikiwa. Sikukubali wanikamate kwani maneno yao yalionesha wana hasira na mimi. Niliwapowaona wakinisogelea bila kuangalia nitaangukia wapi nilijiachia nilipokuwa nimesimama na kujitupa chini.

Nilipotua chini kilichoendelea sikujua mpaka nilipozinduka siku ya tatu na kujikuta nipo hospitali nikiwa nimevunjika mguu mmoja wa kushoto. Mke wangu na rafiki yangu Somati waliniuliza kipi kimenisibu kuwa katika hali ile. Mke wangu na watu wengine niliwaeleza niliteleza wakati nazungumkia ujenzi na kuangika chini.

Lakini nilipobakia na Somati nilimweleza ukweli kitu kilichoinitokea ambacho alikipinga kwa kusema lazima ile ilikuwa ndoto.
“Mawazo si kweli hakuna kitu kama hicho hiyo ilikuwa ndoto.”
“Somati ninachokueleza ni kitu cha ukweli kabisa hata mimi mwanzo niliona labda ndoto.”

“Mawazo mimi nimefanya kazi hii zaidi yako na nimefanya mambo ya kufuru kuliko wewe, mbona haikunitokea na kama waganga ninaotumia mimi ndiyo niliokupeleka.”
“Hapo ndipo ninapochanganyikiwa, ile ilikuwa nini?”

“Ile maiti ya mtoto ipo wapi?”
“Hata sijui kwa vile toka nilipojirusha sijui nini kilichokuwa kikiendelea.”
“Ngoja niulizie kwa vijana wako.”
“Hapana nenda mwenyewe katika chumba nilicho uweka mwili wa kile kichanga.”
“Sawa wacha niende.”
“Kama vipi maliza kila kitu na umpelekee jamaa utakupa mzigo.”

“Hakuna tatizo.”
Somati aliondoka na kuniacha nimejilaza kitandani huku nikijiuliza kilichonitokea kilikuwa kitu gani kwa vile jambo lile niliamini ilikuwa ni ndoto lakini yenye ukweli. Kutokewa na maiti nilizowahi kuzikata viungo pia maajabu ya kichanga kulia kikiwa hakina uhai.

Kwa vile bado mguu ulikuwa na maumivu ya mbali nilipewa dawa za usingizi na kujilaza. Nilishtuka baada ya saa nne, wakati huo ilikuwa saa kumi na mbili jioni, pembeni ya kitanda changu alikuwepo mke wangu na dereva wangu. Wote walionekana wana nyuso za huzuni kitu kilichonitisha.

“Vipi jamani kulikoni?”
“Kuna habari si nzuri.”
“He! Mbona mnanitisha?” Nilishtuka.
“Shemeji Somati amefariki dunia.”
“Ati nini?” sikukubaliana na taarifa ile.
“Shemeji Somati kafariki dunia,” mke wangu alirudia.

“Hapana hapana acheni utani, mchana si nilikuwa naye.”
“Ni kweli bosi kutokana na maelezo ya mlinzi, mchana alikwenda kwenye site na kuomba kuingia ndani. Kwa vile anafahamika aliruhusiwa, baada ya muda alitoka akipiga kelele kama anafukuzwa na kitu cha kutisha. Alitoka mbio kwenye geti bila kuangalia wakati anavuka barabara aligongwa na gari ambalo halikusimama.

“Mlinzi alipotoka alikuta tayari ameisha kata roho huku ulimi na macho vikimtoka pima, watu wamejaribu kuurudisha ulimi na kumfumba macho imeshindikana.”

“Mmh!” taarifa ile ilinitisha na kujua hali imekuwa mbaya kama mtu niliyekuwa nikimtegemea amekufa kifo kibaya hasa baada ya kuingia chumba cha maiti ya kichanga.
“Sasa maiti yake ipo wapi?”
“Ipo hospitali ya mkoa, ndugu zake tumeishawapa taarifa lakini hatukuwaeleza sababu ya kifo chake bali amepata ajali.”

“Mtakuwa amefanya jambo la maana kwa vile ile ni lawama.”
“Mume wangu nyumba yako ina nini? Juzi wewe, leo mchana rafiki yako kipenzi amekufa. Kuna nini?” mke wangu aliniuliza.
“Mke wangu hebu hilo liache tutazungumza nyumbani.”

“Utatoka lini maana mguu umevunjika mara mbili?”
“Hilo lisikutie shaka kuna dawa za asili nikifunga ndani ya wiki mbili natembea.”
“Mmh! Haya.”
Mke wangu alikubali kwa shingo upande huku akiwa na maswali yasiyo na majibu juu ya matukio mawili yaliyotokea kwenye jumba langu la kifahari.

Nilitaka kumtuma kijana wangu kwenda kuuondoa mwili wa kichanga lakini nilihofia kumkuta yaliyomkuta rafiki yangu Somati.
Lakini sikuwa na jinsi ilikuwa lazima kiumbe kile kitolewe kabla hakijaanza kunuka na kusababisha harufu mbaya. Nilimweleza kwa siri akautoe ule mwili na kwenda kuutupa au kuuzika. Baada ya kuondoka nilikuwa na wasiwasi wa kusikia habari mbaya.

Lakini baada ya muda alirudi na kunieleza amefanya kama nilivyoelekeza mwili wa kichanga ameuzika nyuma ya nyumba. Nilishukuru kwani kama mwili ungekutwa mule ndani kesi yangu ya kuuza viungo vya mwili ingefumuliwa upya. Lakini nimsisitiza abakie na siri ile asimwambie mtu.

Mazishi ya Somati yalifanyika kijijini kwetu lakini kutokana na hali yangu sikuweza kushiriki. Nami niliendelea vizuri na matibabu ya mguu kwa kutumia dawa za asili ambazo zilinisaidia kuweza kutembea haraka japo nilikuwa sikanyagi mguu kwa nguvu lakini hali ile nilijua ingeisha baada muda na kutembea vizuri.

Baada ya kuwa katika hali nzuri nilipanga kwenda kwa mganga niliyepelekwa mara ya pili na marehemu Somati aliyeimaliza kesi yangu kimiujiza. Muda wangu wa kurudi kazini ulipofika, nilihofia hali ile kujirudia nitakapoingia chumba cha maiti. Nilipanga kuanza kazi mpaka nitakaporudi kwa mganga.

Nilimchukua dereva wangu ambaye ndiye niliyemfanya msiri wangu kwa muda ule baada ya rafiki yangu kipenzi Somati kufa kifo cha ajabu na sababu kubwa nikiwa ni mimi.

Nilipanga kuondoka mwisho wa wiki ile mwanzo wa wiki niwe kazini, nilitaarufu tuna safari.
Baada ya kuiandaa safari tuliondoka alfajiri ili tuwahi kufika kupata huduma na kurudi. Tulianza vizuri safari yetu vizuri, tulipofika nusu ya safari tulikutana na watu waliokuwa wakienda kuzika.

Siku zote ilikuwa desturi ukikukatana na watu wanaokuwa wanakwenda kuzika lazima usimame na ubebe kidogo ndipo uendelee na safari.
Nilimwambia dereva asimamishe gari na mimi kuteremka, nilichepua mwendo kuwahi mbele na kushika jeneza na kuanza kutembea. Lakini ajabu baada ya kutembea hatua mbili nilimsikia maiti aliyekuwa ndani ya jeneza akisema kwa sauti kubwa:

“Jamani huyo atanikata viungo.. nakufa nakufa muueni na yeye.”
Niliamini sauti ile wote wanaisikia, woga ulinishika nashukuru nilikuwa nimeisha liacha jeheza bila hivyo ningeliachia. Niliwaangalia watu wote waliokuwa wako bize na kwenda kuzika. Nilijiuliza ina maana sauti ile hawaisikii, kwa sababu ilikuwa ya juu sana.

Nilimsikia akiendelea kupiga kelele huku akisema kama wameshindwa kunitia adabu basi anatoka yeye. Nilianza kuliona jeneza likicheza kuonesha yule maiti anataka kutoka kunifuata kunitia adabu. Niliwaona watu wakihangaika kulitulituliza jeneza lililokuwa halitulii mabegani.

Nilipowaona wanaliweka chini nilichanganyikiwa zaidi baada ya kumuona maiti akitoka kwenye jeneza ili anifuate. Nilitimua mbio huku nikipiga kelele, kilichoendelea sikujua mpaka nilipojikuta kwa mganga wa kienyeji. Nilipojiangalia nilikuwa nimedhoofu mwili pembeni alikuwa mke wangu ambaye naye alionekana amedhoofu pia.

Mke wangu alionekana mwenye mawazo mengi, nilitembeza macho na kuyaona mazingira kama ya wa mganga. Nilipojichunguza niligundua nimefungwa kamba kwenye shina la mti. Nilijishangaa kuwa kwenye hali ile, nilinyanyua mdomo wangu kumwita mke wangu.

“Mke wangu.”
Ajabu mke wangu badala ya kuitikia alishtuka na kunikimbia, nilijiuliza mbona amenikimbia. Baada ya muda alirudi na mzee wa makamo ambaye alionekana ndiye mganga na vijana wake na kusema:

“Mfungueni kamba.”
Walinifungua kamba na kusimama, nilikuwa nimevaa kaniki kifua wazi, nilijiuliza pale nimefikache. Kabla sijajua nimefikaje pale nilipigwa na maji ya uso yaliyonizindua na kuzidi kujishangaa. Nilipojiangalia nilijikuta nimebakia mfupa na nguzo nywele nyingi na ndevu nyingi.
Nilichukuliwa na kwenda kuogeshwa kisha nilipewa dawa ya kunywa na kinifanya nilale mpaka siku ya pili.

Ndipo nilipopata nafasi ya kuzungumza na mke wangu na mganga na kuelezwa kuwa imepita miaka sita toka nilipopata tatizo la ugonjwa wa akili baada ya kusindikiza msafara wa mazishi kama walivyoelezwa na dereva wangu. Nilipovuta kumbukumbu nilikumbuka kilichotokea miaka hiyo sita kama walivyosema. Nilielezwa tokea siku ile niliugua ugonjwa wa akili kwa kukimbia mabarabarani bila nguo.

Mke wangu alinieleza alinihaingaikia kila kona kwa waganga na kwenye maombi bila mafanikio. Kila nilipopata nafuu kidogo nilipoliona jeneza au makaburi kichaa kilianza upya mpaka walipompata yule mzee ambaye aliwahakikishia atanitibu kwa muda mfupi kwa vile tatizo langu aliliona.
“Mume wangu kwa nini uliyafanya yote yale?” mke aliniuliza mkono shavuni huku machozi yakimtoka.

“Yapi mke wangu?”
Alinieleza siri yote ya mambo niliyokuwa nikifanya ya kuuza viungo vya maiti na kusababisha laana yao inirudie na kama nisingempata mganga yule ningekufa kama rafiki yangu Somati aliyeuawa na mizimu ya marehemu wale hata gari lililomgonga na kumuua halikuwa gari kweli.

Baada ya maelezo yale alinieleza jinsi mali yangu yote ilivyoteketea kwa ajili ya kutafuta tiba yangu iliyokuwa ikila pesa kila kukicha.
“Mume wangu imebakia nyumba moja tu tunayoishi, nimeuza kila kitu ili nikutibie.”

“Mmh!”
“Na mganga amesema na ile nyumba tuiuze na fedha yake zitengenezwe ili tuweze kuzitumia bila hivyo nazo zitateketea. Sikuwa na la kusema nilikubali kila kitu kifanyike kwa kusimamiwa na mke wangu. Baada ya kitu kwenda kama alivyoelekeza mganga.
Niona hakuna haja ya kuendelea kukaa mjini nilirudi kijijini na pesa tuliyouza nyumba nilianzia maisha nyumbani.

Namshukuru Mungu sasa hivi mimi na familia yangu tumemrudia bwana tumeokoka, maisha yetu yaliyobaki tumeyakabidhi mikononi mwake.
Kila siku siachi kumuomba msamaha Mungu wangu anisamehe kwa yote niliyoyafanya ambayo yalimchukiza pia kuendelea kunipa uhai ili niweze kutubu na kuweza na kuutoa ushuhuda.

Japo nina maisha magumu lakini nimerizika nayo kwa vile yananipa uhuru pia kunipa nafasi ya kuwa karibu na muumba wangu. Ndugu zangu hapa ni mwisho wa simulizi yangu. Ila nataka kuwaambia maisha yaliyo mazuri ni kuyafanya yamfuraishayo muumba wako na kuyaacha yote yamchukizayo.

Chini ya jua hakuna kimbilio zaidi ya kujikabidhi mikononi mwa muumba wako kwake yeye ni kila kitu. Heri kuwa maskini mali ya Mungu kuliko kuwa tajiri uliye mali ya shetani. Jiepushe na utahiri wa kutegemea nguvu za giza siku zote yana mwisho mbaya.
Mwisho
 
Ila umeweka picha zinatisha jamani!
 
Huuuu
Sehemu ya 08

Baada ya mazungumzo mganga alinipa dawa ya kutega ofisini kwangu, niliaga na kuondoka. Nilirudi nyumbani mapumziko ya kukesha kazini, nilioga na kujitupa kitandani. Niliamka jioni na kujiandaa kwenda kazini, kabla ya kwenda kazini nilipitia sehemu kushtua akili.

Muda ulipofika nilikwenda kazini kama kawaida, majira ya saa nne usiku niliweka dawa niliyopewa na mganga. Niliweka dawa kama nilivyoelekezwa, baada ya zoezi lile niliendelea ma kazi kama kawaida kwa kujipumzisha ofisini kwangu.

Kwa vile mchana sikulala vizuri sikuchelewa usingizi ulinichukua.
Kishindo cha watu kuanguka na vilio vya maumivu kilinishtua toka kwenye usingizi mzito, baada ya kuamka nilitulia na kusikia sauti za watu wakisema:
“Mmh! Hii ngoma ngumu.”
“Sasa tutafanyaje?”
“Kama nilivyowaeleza yote tumeyataka wenyewe.”
“Mnafikiri kama amegundua tulimfanyia kitu itakuwaje?

“Itabidi tutumie njia nyingine.”
Kwa vile walikuwa wakiondoka eneo la chumba cha maiti yaliyoendelea sikuyasikia. Nilibakia na maswali juu kile kilichotokea cha muanguko na vilio vya watu pia kauli zao juu ya kushindwa kuingia chumba cha maiti.

Niliamini kweli dawa za mganga zimefanya kazi nilijiuliza kauli yao ya kusema wamekwenda kujipanga watarudi vipi.
Nikiwa nipo katikati ya mawazo simu yangu ya mkononi iliingia, ilikuwa namba ngeni. Nilipokea na kuzungumza:

“Haloo.”
“Haloo, nina imani mazungumza na Mawazo?”
“We nani?” sikutaka kujibu mara moja.
“Najua hunijui, namba yako ya simu nimepata toka kwa ndugu yako Somati.”
“Ooh! Unasemaje?”

“Nina shida nawe, kesho ukitoka kazini tuonane.”
“Wapi?”
“Kuna mtu atakufuata hapo kazini.”
“Sawa.”
Nilikata simu na kujiuliza jamaa ana shida gani kama bidhaa za kazini kwangu angekuja kazini kwangu. Lakini sikutaka kuumiza kichwa kwa vile kesho haikuwa mbali pia sikuwa na wasiwasi baada ya kupewa namba na rafiki yangu Somati.

Baada ya muda Somati alipiga simu kuniuliza kama nimepigiwa simu, nilimkubalia na kuniambia kikifanikisha dili lile nitapata fedha nzuri. Baada ya kazi sikutoka haraka nilisubiri mtu kunifuata kutokana na makubaliano na mteja wangu. Robo saa toka muda wangu wa kazi kuisha nilipigiwa simu ambayo nilipokea.

“Haloo.”
“Haloo, samahani wewe ndiye Mawazo?”
“Ndiyo, nani mwenzangu?”
“Nimetumwa nikufuate kama mlivyo kubaliana jana.”
“Ooh! Upo wapi?”
“Njoo mpaka nje ya hospitali nipo kwenye maegesho ya magari utaona Prado nyeupe njoo moja kwa moja na kuingia mlango wa mbele.”

“Sawa nakuja.”
Baada ya kukata simu nilitoka hadi nje ya hospitali, nilielekea kwenye maegesho wa magari yanayoingia hospitali. Sehemu ile kulikuwa na magari machache, nililiona Prado ambalo lilikuwa lipo peke yake sehemu ile.

Nilikwenda na kuingia katika mlango wa mbele na kufunga mlango.
Utashangaa sikuwa na wasiwasi wowote ilitokana na mteja yule kuletwa na rafiki yangu Somati lakini angekuwa simjui nisingekubali. Pamoja na kuifanya kazi ile hatukumjua mzuri na mbaya unayeweza kuingia kichwakichwa kumbe ishu ya biashara ya viungo imevuja unaangukia mikononi mwa wazee.

Baada ya kukaa dereva wa gari aliyeonekana kijana mdogo alinisalimia:
“Habari za asubuhi Brother?”
“Nzuri sijui zako.”
“Zangu nzuri.”

Baada ya salamu hakuzungumza lolote aliondoa gari, nami sikusema lolote kwa vile nilijua yule kazi yake ilikuwa kunifuata tu, hivyo sikutakiwa kuzungumza chochote baada ya salamu. Gari lilitembea kwa dakika ishirini baada ya kutoka mjini na kuelekea sehemu zenye nyumba za kifahari za watu wanene.
Nikiwa ndani ya gari nilikuwa na mawazo mengi juu ya wito ule na kujiuliza kuna biashara gani inataka kufanyika tena nje ya eneo la kazi.

Baada ya muda gari lilisimama mbele ya geti la jumba moja la kifahari. Mlango ulifunguliwa na gari kuingia ndani. Gari kutembea kidogo mpaka kufia jumba la kifahari kutokana na geti kuwa mbali kidogo na nyumba. Baada ya gari kusimama dereva aliteremka na kuzunguka kunifungulia kama mgeni rasmi na kunikaribisha.

“Karibu.”
“Asante.”
Niliongozana naye hadi ndani ya jumba la kifahari ambako alinikaribisha kwenye sebule ya kifahari na kuniomba nimsubiri mzee. Nilitulia kwenye sofa kumsubiri mwenyeji wangu. Nikiwa bado nimebung’aa nikitembeza macho kila kona ya sebule ile.
Alitokea mhudumu wa kike akiwa na beseni la chupa ya maziwa na kahawa na kuniwekea mbele yangu na kunikaribisha kwa heshima zote.

“Karibu kaka.”
“Asante.”
Baada ya kuondoka nilijimiminia kahawa kwenye kikombe na kutulia kumsubiri mwenyeji wangu. Baada ya nusu saa alitokea yule kijana aliyenifuata na kunieleza naitwa ndani. Nilinyanyuka na kumfuata mpaka kwenye sebule nyingine na kumkuta mzee wa makamo akiwa amekaa kwenye kochi.

“Karibu sana.”
“Asante.”
Nilijibu huku nikikaa na yule kijana aliyenipeleka pale akiondoka, baada ya kukaa nilimsalimia kwa vile alikuwa akinizidi umri.

”Shikamoo mzee.”
“Marahaba, karibu sana.”
“Asante.”
“Sasa kijana bila kupoteza muda kuna kitu nimekuitia hapa ili tuzungmze kwa siri sikutaka sehemu yoyote kwa kuhofia macho ya watu kwa hiyo nahitaji msaada wako.”

“Msaada upo mzee?”
“Nina imani wewe na Somati ni ndugu?”
“Ndiyo.”
“Kama kweli nina imani hutaniangusha kwa kazi nitakayokupa.”

“Sawa kabisa.”
“Unajua kijana sisi matajiri tuna mambo mengi ambayo yanatofanya tuwe na fedha, kuna baadhi ya vitu lazima tuvifanye ili kuilinda fedha tunatokuwa nayo. Hivyo basi kuna jambo nataka unisaidie kwa usiku wa leo.”
“Japo gani?”

“Nahitahi maiti ya mjamzito leo.”
“He! Unataka uipeleke wapi?” nilishtuka japo haikuwepo.
“Tena ya mapacha wawili.”
“Sawa, unataka kuipeleke wapi?”
“Hapana kuna kitu nataka kufanya kwa muda mfupi kisha naondoka.”
“Mmh! Sijawahi kupokea maiti yenye kiumbe tumboni, mara nyingi mwanamke akifariki anafanyiwa upasuaji na kuletwa akiwa ametenganishwa na watoto au mtoto wake.”

“Leo kuna maiti ya mjamzito italetwa kinakosa, kabla hawajashtuka na kuifuata ninatakiwa nije nifanye mambo yangu na kuondoka.”

“We umejuaje?” nilishtuka kusikia vile.
“Bwana Mawazo mengine tutazungumza siku inayofuata naomba itekeleze hili kwanza.”
“Kama atakuwepo mimi sina tatizo.”
Mzee alinyanyuka na kuingia ndani baada ya muda alitoka na mfuko wa kaki na kunikabidhi.

“Nina imani kiasi hiki kitatosha kwa kazi ya leo.”
Nilipokea bahasha ile ambayo ilikuwa nzito bila kujua kuna kiasi gani.
“Basi kijana kapumzike tutaonana usiku.”

“Sawa mzee.”
Nilinyanyuka ili nitoke wakati huo kijana aliyenileta alikuwa amefika na kuniongoza kutoka nje ili nirudi nyumbani kupumzika ili mujiandaa na kazi ya usiku. Nilitoka hadi kwenye gari na yule kijana alinipeleka mpaka sehemu ambayo nilijua nitamkuta dereva wangu.

Baada ya kuniacha nilimpigia simu dereva wangu ambaye hakuwa mbali, alifika na kunichukua mpaka nyumbani. Alipofika nilifikia chumbani nikiwa na shauku wa kujua kwenye bahasha kuna kiasi gani. Nilipozihesabu sikuamini kupewa pesa kiasi kile, nilijiuliza mbona kanipa pesa kiasi kile kwa kazi asiyo na uhakika nayo.

Sikutaka kuzitumia niliamua kuziweka kwanza ili kazi ikishindikana ni mrudishie, niliziweka kabatini na kuzifungia na ufunguo nilificha mke wangu asiuone. Baada ya kuhakikisha pesa zipo kwenye usalama nilikwenda kuoga kisha nilipata supu na kupanda kitandani kulala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ishiii
Sehemu ya 09

Kama kawaida muda ulipofika niiingia kwenye gari langu mpaka kwenye bar ya Somati ambayo ndiyo niliyoichagua kupata kinywaji kabla ya kutimua zangu ofisini. Uvaaji wangu ulikuwa na tofauti na wenzangu wenye kufanya kazi kama yangu, nilikuwa navaa kama nakwenda ofisi ya kawaida hivyo nilijipenda.

Nguo za nyumbani nilikuwa navua na kuziweka sehemu nzuri na nilipomaliza kazi nilioga na kubadili nguo huku nikijipulizia utuli.

Ilikuwa vigumu mtu kujua nafanya kazi za kuhudumia maiti. Bahati nilikutana na rafiki yangu Somati ambaye tulipotezana kwa muda wa wiki mbili baada ya kwenda nyumbani kuwasalimia wazazi.
“Vipi za siku mbili tatu?”
“Mmh! Nzuri, vipi wazazi nyumbani?”
“Hawajambo, nilifika hadi kwenu wote hawajambo.”

“Nashukuru kaka mi nipo nakomaa na maisha.”
“Ndicho kilichotuleta mjini, komaa ndugu yangu najua kazi ngumu ila kwa muda mfupi unaweza kubadili maisha yako na kuachana nayo.”

“Ni kweli kazi ile ngumu kuna kipindi huwaza mengi, hivi mfano maiti waaamke unafikiri mimi nitafanya nini?”
“Hao mawazo ya uoga tu aliyekufa amekufa atakayeamka ujue hajafa huyo.”
“Nasikia kuna maiti huamka toka chumba cha maiti?”

“Mi ilinishatokewa mara mbili, japokuwa madaktari alihakikisha kuwa amekufa lakini ajabu sehemu niliyomlaza nilishtuka kuona viungo vikimcheza. Japo nilipata mshtuko mkubwa lakini nilipiga moyo konde na kumsogelea. Baada ya kumuangalia vizuri niligundua yupo hai ndipo nilipotoa taarifa.

“Walikuja kumchukua na kumrudisha wodini na baada ya matibabu alitoka katika afya njema. Lakini nilipata taarifa mtu yule alitoweka baada ya wiki katika mazingira ya kutatanisha, mpaka leo sijapata habari zake kama alionekana au alitoweka moja kwa moja.”

“Mmh! Una moyo, mimi ningetimua mbio.”
“Ukimbie nini wakati ile ndiyo kazi tuliyoichagua, kingine kama nilivyokueleza hakuna kiumbe kinachofufuka, ukiona kaamka basi jua huyo hajafa unatakiwa kumsaidia haraka kwa kupeleka ripoti ili apatiwe huduma ya haraka.”

“Mmh! Kazi ya kuhudumia maiti yataka moyo, pamoja na kuanza kuizoe kuna kipindi huingia woga baada yasikia upepo ukipita kisha panapita ukimya wa ajabu mpaka nywele huwa zinanisimama na kuingia na woga wa ajabu.”
“Hali hiyo huendelea kwa muda gani?”
“Kama dakika tano kisha hurudi katika hali yake ya kawaida, lakini dakika tano kama miaka mia tano.”

“Hiyo hali ya kawaida, sehemu ile ina mambo mengi hasa kutokana na kuwa na maiti, vitu vingine vikitokea unaachana navyo. Ukitaka kujua yote kila unaloliona au kusikia kazi ile huifanyi. Tena shukuru mzee yule kukupatia dawa bila hivyo usingekaa sehemu maiti zinapokaa kuna mauzauza ya ajabu.

Unaweza kusikia watu wanaingia mara droo zinafunguliwa watu huwaoni, wachawi wakorofi sana tena wasumbufu sana wanapenda kuwatisha watu ili wapate njia ya kufanya mambo yao.”
“Pesa tunapata, lakini chumba cha maiti kigumu sana hasa nyakati za usiku, kuna suku taa zilizimika ghafla nusra haja ndogo initoke hali ilikuwa inatisha. Baada ya hapo droo za maiti zikawa zinafunguliwa ovyo kisha palitulia na taa kuwaka. ”

“Kweli nimekumbuka, jana usiku mzee Ufunguo alikupigia simu?”
“Ndiyo na asubuhi nilipitia kwake.”
“Basi mzee yule mzungu hulipa kabla ya kazi, akienda naye vizuri atafurahi.”
“Lakini Somati anataka maiti ya mjamzito nitaipateje?”

“Itapatikana tu.”
“Hata ikipatikana si itakuwa tayari imefanyiwa upasuaji?”
“Mawazo, yule mzee akichokisema ana sababu zake maiti itapatikana na atafanya anachotaka kufanya.”
“Sasa anataka kufanya nini na maiti ya mjamzito, nahofia anaweza kuinyofoa kiungo akanitia matatani.”

Somati alicheka kusikia nilichokizungumza kisha alisema:
“Unajua ndugu yangu uoga umekutawala sana, yule mzee huwa ana utajiri wa ndagu(dawa). Ukiona anatafuta maiti ya mapacha basi ujue mali zake zimeanza kupungua kuna kosa amefanya.

Ili kuirudisha lazima alale na maiti ya mapacha ambayo ni sawa ya yeye mali yake kuongezeka mara dufu. Baada ya mali yake kuongezeka lazima apate maiti ya bubu ambayo huikata ulimi ili kufanya mali isitoke.”

“Sasa ya bubu tutaipata wapi na nitaijuaje?”
“Kila kitu muachie huyo mzee Ufunguo, mganga wake ana darubini yake akiona anakupigia simu ujue siku hiyo utapata maiti anayoitaka.”

“Somati hayo yote umeyajulia wapi?” nilishangaa Somati kuyajua yote.
“Nilimuuliza mganga aliyekusaidia yule mzee anajua vitu vingi sana hasa vya wachawi. Alinieleza vitu vingi kuhusiana na viungo vya binadamu vinavyochukuliwa na watu au wachawi vinafanya kazi gani.”

“Mmh! Kazi ipo, sasa kama haitapatikana?”
“Mawazo, yule mzee ana mganga wake ambaye hujua nini kitatokea mbele, hiyo maiti itapatikana leo.”

“Mmh! Sawa.”
Kwa vile muda ulikuwa umekwenda sana kutoka na mazungumzo ya muda mrefu ambayo yalinifanya hata nisinywe sana kwani nilikuwa makini na mazungumzo mazito kama yale ambayo sikutakiwa kupepesa macho. Ilibidi nichukue mzinga wa pombe kali ambayo ningekuwa kazini baada ya kazi kupungua.

Niliagana na Somati ili niwahi kazini kwani muda ulikuwa umekimbia sana, dereva wangu alinichukua kuniwahisha kazini na kuniacha karibu na hospitali. Sikutaka ajue nafanya kazi gani siku zote alizonibeba aliniacha barabrani na siku iliyofuata alinifuata palepale na kurudi naye nyumbani.

Kama kawaida nilipofika ofisini nilibadili nguo na kuvaa sare ya kazi, kabla ya kupokea shifti nilipitia ripoti ya mchana na kukuta kuna maiti saba zimetoka na sita kuingia. Ripoti ilielezea kulikuwa na maiti tatu wanawake wawili na mwanaume mmoja zilizokuwa zikisubiri kutambuliwa na ndugu zake na kukosa na siku ile ilikuwa ya mwisho hivyo zilitakiwa zizikwe na manispaa siku ya pili.

Maiti zile ndizo zilizokuwa biashara nzuri kwa washirikina kwani unakuwa na uhuru wa kuuza kiungo chochote bila kuulizwa na mtu. Mwanzo nilikuwa nikifanya biashara huku hofu ya Mungu ikiwa mbele, lakini baada ya kupata fedha woga ulinitoka na kutamani kuuza maiti wote ili nipate pesa.

Asikuambie mtu moyo wa tamaa huna hauna hofu ya Mungu, nilijikuta tamaa ya fedha ikinitawala na kutamani kujenga nyumba kama ya Somati ya ghorofa mbili. Somati aliniambia ghorofa alilipata kwa biashara ya watu wawili tajiri wa kiarabu na mswahili ambao wote walikuwa wakisifika kwa utajiri.

Mmoja alitaka sehemu za siri za binti bikira na jamaa mwingine aliyetaka nyeti ya mwanaume asiye riziki. Aliniambia ilikuwa kazi kuvipata kwani alichukua miezi mitano kupata vitu vile ambavyo aliahidiwa pesa nyingi na alipovipata alipewa kiasi kile kilichomfanya ajenge nyumba ya ghorofa mbili.

Nami nilijikuta nikiingia tamaa ya kupata mteja mwenye kutaka kiungo kwa fedha nyingi. Ilifika kipindi nikakosa roho ya huruma na kuwaona wanadamu wenzangu kama bidhaa iliyokuwa sokoni.
Kila maiti zilizokosa ndugu nilipata pesa nzuri kitu kilichofanya kuondokwa na moyo wa kiutu.

Baada ya kusoma ripoti, nilikagua kuangalia kama kweli maiti walioandikwa kwenye kitabu kama zipo sawa. Baada ya kujiridhisha kila kitu kipo sawa niliagana na mwenzangu na kuanza kazi rasmi kwa kuingia ofisini kujipanga kwa kazi ya usiku.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom