Simulizi -Kitabu kilichojaa majina yote

SURA YA 18
MELBOURNE –AUSTRALIA 2016
World Bosses ni kikundi cha matajiri wakubwa ndani ya Taifa la Australia , kikundi hiki kilikuwa chini ya uongozi wa waziri mkuu wa taifa la Australia bwana Roy Andrew , kwa manano marahisi ni kwamba hiki kikundi cha World Bosses mwanzilishi wake alikuwa ni huyu Roy ambae ni waziri mkuu wa taifa na bara hili la Australia , moja ya malengo makuu ya hiki kikundi ni kuwa na nguvu kubwa duniani ,lakini si hivyo tu kikundi hiki kilikuwa na mpango wa kulifanya taifa la Australia kuwa Taifa lenye nguvu kubwa sana Duniani .
Katika mpango wa kutimiza malengo yao hayo mwaka 2016 ndio mwaka ambao matajiri wakiongozwa na waziri mkuu walikutana katika kujadili utekelezaji wa mipango yao , kati ya matajiri waliohudhuria katika kikao hiki alikuwa ni mwanamama Victoria , ambaye alikuwa profesa ndani ya chuo kikuu cha Monash.
Katika kikao hiki ambacho kilifanyika ndani ya makazi ya mapunziko ya Waziri mkuu Andrew , jambo moja lililokubaliwa katika kutekelezwa ni juu ya upatikanaji wa kitabu cha Book of all names , jambo ambalo kwa mara ya kwanza waziri Roy analitamka kwa wanachama hawa walishangaa .
Waziri huyu aliwaambia wanachama wake kwamba ili Taifa lao liweze kuwa a nguvu basi wanapaswa kumiliki kitabu hiko mara moja , lakini aliwatahadharisha kwamba kitabu hiko kinatafutwa sana na UMOJA NAMBA TISINI NA SABA , jambo ambalo matajiri hawa walilishangaa , kwani licha ya hawa matajiri kuwa wanachama wa huu umoja lakini hawakuwahi kusikia juu ya uwepo wa hiki kitabu.
Kama ilivyokuwa madhumuni ya waziri Andrew juu ya kutaka kuifanya Austalia kuwa nchi kubwa Duniani , ndio maana aliunda kikundi hiki ambacho kilikuwa hakifahamiki ndani ya U-97, lakini jambo hilo katika kulijadili , waliona kwamba hawawezi kupata kitabu hiko kama tu hawatakuwa na mtu sahihi ambaye ataweza kuwasaidia katika kukipata hiko kitabu.
Ndipo mwanamama Victoria alipokabidjiwa kazi ya kumtafuta mtu ambaye atakuwa ni mtu sahihi kwa kazi hio , kwanzia siku hio ya kikao mpaka miaka mitatu mbele , mwanamama huyu aliweza kumpata mtu huyo na moja kwa moja alimueleza waziri juu ya jambo hilo na waziri mara baada ya kuambiwa juu ya upatikanaji wa mtu kwa ajili ya kuandaa mpango wa kukipata kitabu hiko ndio aliona ni jukumu lake kukutana na mtu huyo moja kwa moja.
Mtu ambae alitambulishwa kwake alikuwa ni Erick Peter mtoto wa Rania ambae wakati huo alikuwa ndio amemaliza chuo kutoka Monash, waziri mkuu kwa kumtumia Victoria na Victoria kwa kutumia ukaribu wake na Rania aliweza kumshawihi Erick kwa ajili ya kuonana na waziri Andrew.
Siku ya ijumaa ndio siku ambayo Waziri Andrew alipoweza kukutana na kijana Erick , lakini ndio siku ambayo ilimbadilisha kimtazamo kabisa Erick , lakini ndio siku ambayo Erick aliweza kupata kuujua umoja NAMBA TISINI NA SABA lakini pia ndio siku ambayo aliweza kujua uwepo wa kitabu cha Book of all names.
Maneno ya waziri Andrew yalijirudia rudia ndani ya kichwa cha Erick , kwani siri alizoambiwa na waziri huyu zilimpagawisha sana ,lakini na kumpa morali kwa wakati mmoja .
Moja ya jukumu ambalo Andrew alimwambia Erick ni juu ya uanzishaji wa The Truth kwani waziri Andrew aliamini kupitia kikundi hiko angeweza kukusanya taarifa mbalimbali duniani zile zilizokuwa zinaonekana na zile ambazo hazikuwa zikionekana.
Haya yote wakati yanafanyika kwa kijana Erick alikuwa ni moja ya vijana ambao kwa maneno marahisi tunaweza kusema walikuwa akili zao zilikuwa zikiwaza starehe tu , hivyo kitendo cha kupata malengo mapya katika maisha yake , ni kama alikuwa ametolewa usingizini.
Katika kufanikisha kikundi cha The Truth mheshimiwa Andrew aliweza kumpa Erick siri zilizokuwa zipo chini ya Umoja Namba Tisini Na Saba na katika siri hizo ndipo kijana huyu aliweza kumjua Damiani Rabani au Stephano Lamberk.
Hivyo kikundi cha The Truth ni kikundi ambacho kipo ndani ya kikundi cha World Bosses ambacho mkuu wake ni waziri wa Australia , ambao na wenywe wanaamini kwamba kwa kupata kitabu cha Book Of All Names moja kwa moja watakuwa ni kikundi chenye nguvu sana .
Katika ulifanikisha hilo ndio waliweza kununua meli ambayo kikundi hiki cha The Truth ndio makao yao hata Erick alipomuomba mama yake kiasi cha dola milioni kumi ilikuwa ni sehemu ya kununua hisa ndani ya kikundi hiki cha The Truth.
Erick katika harakati zake za kuandaa mipango ya kukipata kitabu hiko , aliona mtu sahihi wa kumsaida katika kazi hio ni Damiani Rabani , na hili alilitoa kwa wakubwa wake na wao kwa pamoja walimuunga mkono kwani walikuwa wakijua uwezo uliokuwa ndani ya Damiani Rabani.
*****
Erick hakujua ni kwasababu ipi Damiani alikuwa amemuomba kukutana , lakini kutokana na kwamba alikuwa akiheshimu mchango wa Damiani katika malengo yake na ya kikundi kukamilisha mpango wa kukipata kitabu cha Book Of All names basi hakutaka kuwa mkaidi.
Kwa kutumia boti aliweza kufanikiwa kurudi nchi kavu na moja kwa moja kuelekea ndani ya hoteli ya Volcanic view hotel chumba namba 289.
Baada tu ya kufika ndani ya hoteli hii moja kwa moja alienda mpaka ndani ya chumba hiki na kugonga , na hapo ndipo alipopigwa na mshangao mara baada ya kuona mtu aliekuwa mbele yake ambae ni mama yake , na kwanzia dakika hio aliamini kwamba Damiani alikuwa amemblack mail .
Licha ya hivyo wawili hawa mwana na mama walifurahia kuonana tena kwani ni kipindi cha muda mrefu sana tokea waonane , lakini pia Erick aliona hio ni nafasi ya pekee kwa ajili ya kumwambia mama yake jambo ambalo alikuwa akikusudia kumwambia katika safari yake ya kutimiza malengo yake.
Baada ya muda wa kuongea hili na lile hatimae Erick aliweka jambo lake mezani.
“Mama nataka unitambulisha kwa baba yangu mzazi” Aliongea Erick na kumfanya mwanana mama huyu kushangaa kwani hakujua ni kipi kimempata Erick mpaka Kutaka kumjua baba yake.
“lakini Erick si nilishakwambaia kuwa baba yako amekwisha kufariki”.
“Mama najua vyema kwamba baba yangu ni mzima na kuniambia kama amefariki ni mbinu ya kutaka kunitenganisha na baba yangu , hivyo naomba unitimizie haki yangu ya msingi ya kumjua baba yangu “Aliongea Erick akiwa kwenye hali ya usiriasi kabisa jambo ambalo Rania alilishuhudia , lakini pia jambo hilo lilimfanya Rania kutokuwa na usemi.
“Naomba kufikiria Erick”Aliongea Rania na kwa Erick hakuwa na haja ya kumlazimisha mama yake . , lakini alijua hio ni haki yake hivyo mama yake alipaswa kumtimizia kwa hio hakuwa na wasiwasi juu ya hilo , alimwacha mama yake huku akimpa namna ya kuwasiliana nae pale tu atakapo kuwa amefanya maamuzi .
Rania licha ya kwamba ombi la mwanae lina mantiki , lakini alikuwa kwenye hali ya wasiwasi kweli , kwani ni miaka mingi tokea aonane na peter , lakini pia ni miaka mingi tokea ale kiapo cha kutokuja kumtafuta Peter tena katika maisha yake , licha ya kwamba ilikuwa ni haki ya Erick kuonana na baba yake , lakini kwake jambo hilo lilikuwa gumu mno.
Alijikuta akifikiria juu ya jambo hilo usiku kucha , hata pale alipoagana na mpenzi wake mpya Damiani jambo hilo aliendelea kulifikiria , alikuwa akitaka kulitolea maamuzi swala hilo kabla ya kurudi nchini Australia .
Kwa upande wa Erick yeye aliamini kwamba njia pekee ya kumshawishi Ambrose aamini kama wao ni ndugu ni kukutana na Peter baba yake hakuwa na nia wala hamu ya kuonana na baba yake Peter lakini aliamini kwamba pasipo kufanya hivyo basi asingeweza kuwa na ukaribu na Ambrose , hivyo jambo pekee lilikuwa ni kuonana na Peter baba yake.
Alijua vyema kuna historia mbaya sana kati ya baba yake na mama yake , lakini bado aliamini kwamba wawili hao wanaweza kukutana kwa mara nyingine , lakini pia na yeye kutimiza maengo yake .
*****
JNIA –DAR ES SALAAM
Ni nje kabisa ya TerminaL namba tatu kijana Erick akiwa pamoja na mama yake walionekana wakitoka ndani ya eneo hilo wakiwa na mabegi yao , kwa Rania alijikuta akiangalia juu angani na kuvuta pumzi kwa nguvu , hakuwa akiamini kama amerudi ndani ya Tanzania kwa mara nyingine Zaidi ya miaka ishirini tokea aondoke, kuna namna ambayo ilimfanya mwanadada huyu kujihisi ni mwenye furaha , lakini mwenye shauku ya kukutana na ndugu zake kwa mara nyingine .
Alijikuta akimkumbuka Nasma na Najma wadogo zake , hakuwahi kuwa nao na mawasiliano tokea aondoke nchini , na hakujua kama bado wapo Tanzania au lah , lakini pia aliweza kumkumbuka mama yake kipenzi na baba yake kipenzi ambao pia hakuwahi kuwa na mawasiliano nao Zaidi y miaka ishirini .
“Mama tushafika “Aliongea Erick na kumshitua mama yake aliekuwa katika mawazo kwani walikuwa mbele ya hoteli ya Serena.
“Erick ndio mara yake ya kwanza kufika ndani ya taifa hili akiwa anaakili timamu , kwani kipindi anaondoka na mama yake alikuwa mdogo sana.
“ I can wait to meet father Mom”
“Am just glad you are going to meet your father , never once thought the coming of this day everything just happened”.
SURA YA 19
Joseph ni moja ya vijana wachapakazi sana ndani ya taifa la Tanzania , alikuwa ni moja ya wafanya bishara chipukizi ndani ya taifa hili ambao wamepiga hatua , maisha yake yalikuwa ni ya furaha sana yeye pamoja na mke wake Johan huku furaha yao ikiwa kubwa Zaidi baada ya kupata mtoto wao Ambrose.
Licha ya maisha mazuri aliokuwa nayo Joseph lakini kuna hadithi ya kusikitisha nyuma ya maisha yake , hadithi ambayo imemfanya mpaka leo hii kutokumbuka maisha yake ya nyuma kwani alikuwa hana kumbukumbu za aina yoyote ile kutoka kitabu cha Masaa mawili ya kumbukumbu inaelezwa kwamba baada ya Joseph kuokolewa na kikundhi cha The hollic shadow hakuwa Peter aliekuwa Peter bali alikuwa Peter ambae hana kumbukumbu na hajui nini kilitokea katika maisha yake
Leah ambae ndio Johan ndie mwanamke pekee ambae aliweza kumpokea Peter mara baada ya kurudi nchini akiikamilisha ahadi ya baba yake ya kuoana na Peter huku ikiwa ni sehemu ya kuomba msamaha juu ya yale aliomnfanyia Peter katika utoto wake.
Maisha ya wawili hawa yalikuwa yakupendana sana , kwa Johan alikuwa akijua nusu ya yale yaliokuwa yamemtokea Pete lakini jambo moja ambalo hakuwa akijua ni uwepo wa Erick katika maisha ya Peter wala uwepo wa Rania katika maisha ya Peter , anachojua tu ni kwamba Peter ni mhanga wa mambo kadha wa kadha ya kutisha yaliomtokea katika maisha yake , jambo ambalo hakuwahi kumgusia kabisa Peter .
Ni kawaida ya wanafamilia hawa kudamka kila mtu asubuhi kwa ajili ya kwenda kaznni , kwani kila mmoja alikuwa na kampuni yake . Johani yeye alikuwa anamiliki Law Firm(kampuni ya maswala ya kisheria ) yake , na pia Joseph yeye alikuwa akimiliki kampuni yake yake ya mawasiliano.
Ni siku hii ya asubuhi baada ya Joseph kufika ofisini kwake mtaa wa mawasiliano ndani ya jengo la PSPF ndipo sekratary wake alivyomtaarifu bosi wake juu ya uwepo wa watu ambao wanahitaji kuonana nae nje ya kazi , jambo ambalo lilimshangaza sana Joseph kwani hakuwahi kupata mgeni ambaye anataka kuonana nae nje ya kazi , kwani hakuwa ni mtu wa miingiliano mingi.
Joseph hakuwa na hiyana alimruhusu katibu wake awaruhusu wageni hao kuingia na hapo ndipo alipokutana na nyuso ambazo hakuwahi kuziona , moja akiwa ni mwanamke ambaye akili yake ilikiri kuwa alikuwa mrembo na nyingine alikuwa mwanaume wa makamo ya ujana ambae alikiri kuwa alikuwa mtanashati.
*****
Rania alikuwa ni mwenye kushangazwa sana na utafiti wa mwanae , hakujua ni namna gani Erick aiweza kujua kuwa baba yake alikuwa hai , lakini sio hivyo tu hakuweza kujua kuwa ni kwa namna gani Erick alikuwa na taarifa zote zinazomuhusu Peter , alishangaa kwa ujumla wake , kwani yeye hakuwa kabisa na habari na Peter na ni miaka mingi , na hata kuja ndani ya taifa la hili hakujua anaanzia wapi kumpata peter , lakini kila kitu Erick alikuwa akijua.
Ilikuwa ni asubuhi na mapema baada ya kunywa chai ndio walianza safari yao kwenda kwenye kampuni ya Peter , njia nzima Rania alikuwa ni mwenye kujawa na wasiwasi alikuwa akiangalia picha ya Ambrise , picha ambayo amepewa na Erick na kutaarifiwa huyo ni mtoto wa Peter, alikiri AMrose alikuwa akifanana vitu vingi sana na Erick .
Walifika ndani ya kampuni ya Peter huku baadhi ya watu wakimshangaa Erick kwani alikuwa amefanana mno na Joseph bosi wao na hata kwa katibu muhtasi wa Joseph alishangazwa na muonekano wa Peter , kwani licha ya kwamba mwanadada huyu alimtamani Erick kimapenzi , lakini alikiri kwamba alikuwa amefanana na Peter.
*****
Rania alijikuta akishangaa sana , hakujua ni dharau Peter alizokuwa akimuoneshea au ni kwamba alikuwa amemsahau , alijikuta hasira zikimpanda ila hakutaka kuziweka wazi mahali hapo , aliamini anaweza kuharibu kabisa , hata pale walipokaribishwa na Peter alikuwa akishangaa sana kwani Peter alionyesha hali ya kutomjua kabisa Rania.
“Peter inamaana umenisahau kabisa?” Rania alijikuta akikosa kabisa uvumilivu na kumuuliza peter hilo swali huku akionekana machozi kutanda ndanni ya mboni za macho yake.
Kwa Erick hata yeye alikuwa akishangaa , kwani hakuwa akijua kwamba Peter hakuwa na kumbukumbu za maisa yake ya nyuma na hapo alipo hata yeye mwenyewe alikuwa akiwashangaa.
“Jamani mimi sio Peter labda mmenifananisha”.
Ilikuwa ni kauli ilioibua kicheko wa Rania lakini iliojawa na mshangao kwa Erick , wakati hayo yakiendelea mlango wa Joseph au Peter ulifunguliwa na aliengia hapo ni rafiki yake Peer aliekuwa akiitwa Steve lakini kitendo cha Steve macho yake kutua kwa Rania alijikuta akitoa macho na kuita
“Shemeji Rania?”
Kwa Rania alikuwa kwenye mshangao mara baada ya kuitwa jina hilo na mtu ambae hakumfahamu lakini aliona ni afadhali kwa mtu huyo amemkumbuka.
“Yaani Peter watu wa pembeni wananikumbuka ile wewe umeshindwa kunifahamu kweli au nidharau”
“Jamani jamani nawaambieni mimi sio Peter mimi naitwa Joseph, Steve hebu ongea nao bhana mimi sio Peter”
“Shemeji Rania naomba kwanza tuongee hapo nje naamini mimi nawewe tutatelewana , uzuri ni kwamba mimi nakufahamu vyema na hata Peter mwenyewe ananifahamu” Aliongea Steve akiingilia hio hali maana aliona kama jambo hilo litaendelea lingevuta watu .
Steve alikuwa ni moja ya marafiki wakubwa wa Peter lakini pia ni mmiliki mwenza wa kampuni yao hio ya mawasiliano na walikuwa wameshirikiana kuifungua , steve alikuwa ni rafiki yake Peter tokea kipindi wapo wadogo hivyo hata Peter aliporudi nchini akiwa hana kumbukumbu. Na haikueleweka kipi kilifanyika , lakini vyeti vyote vya Peter viliwezwa kubadislishwa jina na kuwa Joseph na hizi zote zilikuwa ni harakati za kumficha Peter juu ya maisha yake ya nyuma.
“Rania kwanza nikupe pole kwa yote yaliotokea , niliweza kusikia historia yako , lakini nataka nikuambie tu kwamba Peter sio Peter yule unaemfahamu , huyu wa sasa ni Joseph”
“Una maanisha nini ?”
“Yapo mengi ya kusikitisha yaliomtokea Peter na hata kupotea kwake hakukuwa kwa matakwa yake ni kwamba alitekwa na kuepelekwa Marekani , lakini katika kurudi kwake hakuwa na kumbukumbu , kwa maana hio Peter hakumbuki chochote kuhusu maisha yake ya nyuma” Aliongea Steve na kumfanya rania kushangaa sana , kwani swala hilo hakuwahi kulifahamu , alijikuta chozi likimtoka , kumbukumbu zilianza kurudi nyuma siku ambayo Rania aliweza kukutana na Peter wakati akielekea Australia na Peter hakumsemesha yote hayo alianza kujua sababu.
“Ina maana Peter hakumbuki chochote hata jina lake , na kama ni hivyo kwanini mlipa jina linguine”
“Hilo sifahamu Rania”
“Nataka kuongea nae kwanza “ Aliongea na bila hata ya kusubiri jibu kutoka kwa Steve alikuwa ashanyanyuka , aliingia kwenye ofisi ya Peter jambo ambalo lilimshangaza Peter mwenyewe na baada ya kufika alitoa picha baadhi kwenye mkoba wake na kuziweka mezani .
Joseph alishangaa , lakini alichukua zile picha na kuanza kuziangalia moja moja , na hapo ndipo alipojikuta akishangaa , kwani mtu aliekuwa kwenye hizo picha alikuwa ni yeye kabisa akiwa amekubatiwa na Rania , alijikuta akichukua picha nyingine na kuzinagalia m na alizidi kushangaa , hakuwa akijua kipi kinaendelea , lakini alikiri ni yeye kabisa .
“Peter sijui ni kipi kimekutokea , na nahuzunika sana kwa ajili yako , lakini haya yote uliyasababisha wewe mwenyewe na naamini ni sehemu ya madhambi uliofanya , huyu ni mwanao Erick wa Damu na kwanzia sasa kaa ukijua hilo” Aliongea Rania na kisha alimwambia Erick waondoke.
SURA YA 20
BAADA YA MIEZI MIWILI
FRORIDA –MAREKANI(USA)
Ambrose Joseph ni kijana ambaye aliwashangaza wengi ndani ya shule hii ya North Broward , sio kwa walimu , sio kwa wanafunzi wenzake, ambao hawakuacha kushangaa juu ya uwezo wa kijana huyyu likija swala la kuchanganua mambo(Reasoning) , kijana huyu alionyesha uwezo wa hali ya juu sana kiasi kwamba hata walimu wake walishangaa pale walipojua kua kijana huyo alikuwa ni mtanzania , kwani walimu hawa wa kizungu walikuwa wakiamini kwamba ndani ya bara la Afrika hakuna mtu ambaye anaweza kuwazidi akili wazungu au raia waliokulia katika mataifa yaliondelea.
“I cant believe he is from Tanzania ,this boy is Exceptional Nick”
“ I agree with you Alian , he is Gifted kid and I can foresee his future”.
Haya ni mazungumzo ya mwalimu Nick Jonas na Madam Alian wakimsifia Ambrose , kwani katika majaribio ambayo wanafunzi wa Class A walipewa Ambrose alikuwa amepata asilimia mia moja kwa kila somo , jambo ambalo liliwafanya walimu hawa kushindwa kujizuia na kumsifia.
Ililikuwa ni miezi miwili kuelekea mitatu tokea kijana ambrose awasili ndani ya shule hii ya North Broward , ndani ya miezi hio tokea akutane na mwalimu Nick Jonasi mwalimu wake wa maswala ya kisaikolojia , Ambrose alikuwa amebadilika sana , alitoka kuwa yule kijana ambaye alikuwa akipenda kila kitu na kuwa kijana ambaye anapenda kitu kimoja yaani mambo ya historia ya kale .
Mwalimu Nick Jonasi alikuwa ni mwenye furaha sana juu ya hatua aliokuwa ameipiga katika kazi aliokuwa amepewa na U-97 ya kumfanya kijana Ambrose kupenda mambo ya historia ya kale , alijiona ni mshindi , lakini pia aliamini kutokana na jambo hilo kuwa na umuhimu kwa Umoja huo ambao yeye pia alikuwa ni mwanachama , aliamini ni lazima angepandishwa cheo kutoka levo aliokuwepo na kwenda levo nyingine .
Na nikweli jambo hili lilikuwa ni sehemu ya furaha sana kwa Profesa Mike Alan ambaye alikuwa akifuatilia kwa ukaribu sana maendeleo ya Ambrose , alijawa na furaha pale alipoona kwamba kijana huyo alikuwa akifanya kama kile umoja wao ulichokuwa ukitaka Ambrose akifanye.
Upande wa Ambrose baada ya kupewa jambo jipya katika maisha yake la kutafuta maana ya maneno ya kitabu ambayo yalikuwa yameandikwa kwa lugha ambayo hakuwa akiijua wala mtu yoyote duniani kuijua , aliamini ni wajibu wake kujua maana ya maandishi hayo katika kitabu hicho.
Kwa matendo ambayo kijana huyu alikuwa akiyafanya alikuwa akioneysha namna ambayo alikuwa akifanana sana na kaka yake Erick , kwani wote walikuwa wametawalia na ile shauku ya kutimiza jambo kubwa katika maisha yao.
Ratiba za Ambrose baada ya kumaliza vipindi vyake ilikuwa ni kujichimbia ndani ya maktaba na kusoma mambo mbalimbali yaliokuwa yakihusiana na mambo ya kale , jambo ambalo hata kwa wanafunzi wenzake liliwashangaza sana , kwani kila siku katika meza yake ya kujjisomea kulikuwa na mavitabu mengi yaliokuwa yakihusiana na historia za mambo mengi ya historia ya maswala ya kale.
“I must solve this Riddle no matter what , I am going to make my name be known through generations and all this can only be fulfilled by holding the keys of every door of Universe” Aliongea kijana huyu akimaanisha kwamba lazima afumbue fumbo lililoko mbele yake anaendelea na kusema kwamba lazima alifanye jina lake kukumbukwa vizazi na vizazi , na hilo litafanikiwa tu kama atakuwa na funguo za kila mlango ulimwenguni.
Haya ni maneno machache kijana huyu aliyokuwa akijiambia kila siku alipokuwa akirudi kujisomea juu ya mambo ya kale , yalikuwa ni maneno machache lakini yaliokuwa na nguvu sana katika maisha ya kijana huyu , licha ya kwamba umri wake ulikuwa mdogo , lakini alikuwa ni mwenye ndoto kubwa ambayo pengine ni watu wachche sana kuwa nayo ndani ya dunia ya leo.
Maneno alioambiwa na mwalimu Nick juu ya uwepo wa funguo ya kufungua kila mlango hapa duniani aliyaamini moja kwa moja na kuyafanya ndio dini yake na hili lilifanya kazi kubwa sana katika ubongo wa kijana huyu , kwani kitendio cha kujiaminisha sentesi yake ya kulifanya jina lake likumbukwe iliendelea kuwa na nguvu katika maisha yake.
Katika ulimwengu wa saikolojia , wataalamu wanaamini kwamba nguvu moja inayoweza kumfanya mtu kuwa na mafanikio makubwa katika maisha yake hapa duniani ni kwa njia ya kuwa na maono , wanafafanua kwamba maono ni sawasawa na mtu kutambua kusudi lake alilokuwanalo katika dunia na kusudi hilo kuishi ndani ya mtu. Wanaendelea kwa kusema kuwa kuna nguvu kubwa sana ya mtu kujiambia maneno ya aina moja kila siku , yaani kama wewe unataka kuwa labda daktari mkubwa duniani na ukajiambia kila siku kuwa wewe ni daktari mkubwa duniani kila siku , maneno haya husihi ndani ya mtu na kuwa kitu hai na kitu kikishakuwa hai inamaanisha udhihirisho.
*****
Siku ya Alhamisi siku hii ndani ya U-97 ni siku ya kutafakari juu ya mipango ya baadae , katika umoja huu lengo kuu katika malengo yote lilikuwa ni kuwaleta watu wote duniani pamoja katika kila Nyanja, walikuwa wakiamini kwamba dunia itakuwa mahali salama endapo watu watakuwa na namna moja ya kufikiria ,kusali , kuuza na kununua ,hata mfumo wa kiuongozi.
Katika kukamilisha malengo haya umoja huu ulikuwa na siku maalumu ya kufanya tafakari juu ya lengo hili kubwa ambayo ni Alhamisi katika tafakari zao hizo ziliendana na kuandaa kwa ripoti ya kusomwa kila siku ya ibada ambayo hufanyika katikati ya ijumaa na jumamosi , yaani ibada ya umoja huu ilikuwa ikianza saa tano na dakika arobaini na tano mpaka saa sita dakika kumi na tano masaa ambayo hutengeneza miingiliano ya ijumaa na jumamosi .
Hi yo katiika siku ya Alhamisi wanachama wote huandaa siku hii kwa kukutana katika makundi maaliumu kutokana na malengo makuu , katika makundi yoote , kundi moja ambalo lilikuwa likiheshimiwa lakini pia lilikuwa likipewa uzito ni kundi ambalo lilikuwa likiratibu Mpango Zero.
Siku hii ya tafakuri ya malengo makuu ya U-97 yaani Alhamisi, saa mbili kamili za usiku ndani ya hekalu moja lililokuwa ndani ya jimbo la Virginia kulikuwa na kikao cha siri sana kilichokuwa kikifanyika , kikao ambacho kilikuwa kikiongozwa na mtu ambae hakuweza kufahamika jina lake , lakini moja ya watu waliokuwa wamehudhuria kikao hiko ni Profesa Mike Alan.
Ajenda kuu ya kikao hiki cha siri ilikuwa ni juu ya ukamilishaji wa Mpango Zero , wanachama hawa ambao kwa ujumla wao walikuwa kumi na moja , walimpngeza Profesa katika hatua aliokuwa amepiga juu ya kijana Ambrose , Lakini licha ya kumpongeza waliamini hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa , kwani hali ya kiafya ya XY ilikuwa mbaya sana .
“Profesa we need this plan to be accomplished within two month , XY is in Critical Condtion and there is only one option for U-97 which is Ambrose”aliongea bwana mmoja ambae nilishindwa kumfahamu jina , ambaye alionekana kuwa ndio kiongozi ndani ya kiikao hiki .
“You have To prepare Ambrose for his Reborn ,you have got only two month at maximum for the preparations , date of ritual ceremony will be announced one weak before D-day for security reason and the whole process will be structured in order for all members to be informed as we know this is one of sacred process within our Unity ”
“Unatakiwa kumwandaa Ambrose aweze kuzaliwa kwa mara ya pili unayo miezi miwili kamili kwa ajili ya maandalizi , tarehe ya sherehe hii ya kitamaduni itatajwa wiki moja kabla ya siku ya mwisho kwasababu za kiusalama ,mchakato wote utaundwa ili kila mwanachama apewe taarifa , kama tujuavyo hili ni tendo takatifu ndani ya umoja wetu” Aliongezea.
Masaa mawili kikao kilionekana kuisha na Profesa Mike alionekana akitoka ndani ya Chopa iliomrudisha kutoka katika kikao hicho cha siri cha Umoja Namba Tisini Na Saba
Ni muda wa saa tano kamili ambao Profesa huyu aliweza kufika nyumbani kwake ndani ya hoteli aliokuwa amefikia ndani ya jimbo hilo la Virginia.
“Nina muda mchache sana wa kumuandaa Ambrose mpaka siku yake ya kuzaliwa upya ni jukumu letu kwanzia sasa ulinzi wa Ambrose kuongezewa na kutoruhusiwa kukutana na mtu yoyote yule.” Aliongea profesa huyu baada tu ya kujilaza ndani ya chumba chake.
*****


MWAKA MMOJA NYUMA KABLA YA D-DAY(KABLA YA SIKU YA AMBROSE KUSIMULIWA SIMULIZI YA BOOK OF ALL NAMES)
TANGA –BOMBO HOSPITAL
Ni nje ya hospitali hii ya rufaa ya mkoa wa Tanga , nje kabisa ya sehemu ya jengo la idara ya upasuaji mkubwa , alionekana kijana mmoja mdogo mwenye makadirio ya umri wa miaka kumi na saba akiwa amejiinamia chini akionekana ni mwenye mawazo mengi sana , huku kila baada ya sekunde chache huinua k kichwa na kuangalia mlango wa chumba cha upasuaji ,chumba ambacho ilionesha ni Dhahiri kuna mtu wake muhimu aliekuwa akifanyiwa upasuaji.
“Haya yote ni mimi ndio nimeyasababisha . nisamehe baba sikujua kama mimi ndio nakuja kukusababishia ajali” Aliongea maneno haya huku akionekana ni mwenye majuto makuu .
Baada ya lisaa moja kupita hatimae mlango wa chumba kile ulifunguliwa na akatoka dokta mmoja mwanamama akiwa na mavazi ya kufanyia upasuaji , baada ya mwanamama huyu kutoka alijikuta akisimamishwa na kijana huyu huku akipewa maswali mfululizo jambo ambalo alikuwa amelizoea kwa ndugu wengi wa wagonjwa pale anapofanyia watu upasuaji , lakini kwa kijana huyu kuna kitu alikiona kwenye macho yake.
“Dokta baba anaendeleaje “
Mwanamama huyu daktari alijikuta akimwangalia kijana huyu kwa macho ya huruma.
“Upo na nani ?”
“Nipo na rafikii yake baba ameenda kuwasiliana na ndugu zetu kwa aili ya kupata gharama za matibabu”Aliongea yule kijana na ile anamaliza tu alitokea mzee mmoja wa makamo hivi aliekuwa amevalia mavazi yake yaliochakaa .
“Dokta mgonjwa anaendeleaje , upasuaji umefanikiwa?”
“Nifuateni ofisini”
Aliongea yule daktari na kisha alitangulia kuelekea zilipo ofisi yake.
“Tumejitahidi kadri ya uwezo wetu kumuokoa mgonjwa ,lakini mpaka sasa hatunae tena” aliongea yule daktari kwa sauti ya masikitiko na kufanya kijana huyu kuanza kulia kwa nguvu .
“Pole sana Hassani ni mipango ya Mungu huna haja ya kulia sana” Aliongea yule mzee akimfariji Kijana huyu ambae tunajua jina lake kama Hassani .
Hakika ilikuwa ni simanzi kubwa sana kwa kijana huyu na katika kilio chake alionekana kama mtu mwenye majuto makuu sana , kiasi kwamba hata watu waliokuwa eneo hilo la hospitalini walimuonea huruma .
Kati ya watu waliokuwa wakimangalia Hassani akiomboleza ni Lisa msichana aliekuwa katika mavazi ya kidaktari,mwanadada huyu alionekana kuguswa sana na tukio lile , sio kama hakuwahi kuona watu wakipoteza wapendwa wao , ila ni kwamba kwa namna ambavyo kijana huyu alivyokuwa analia huku akionekana akijilaumu , swala lile lilimgusa na lilimwambia kabisa kuwa kuna jambo ambalo lilitokea Zaidi ya kifo cha baba yake..
“Pole sana”Ilikuwa ni sauti ndogo nyororo ya kuvutia sana iliosikika kwenye ngoma za masikio ya kijana Hassani , lakini kwa wakati huo sauti hii licha ya unyororo wake haikumstua kabisa na wala Hassani hata hakutaka kumwangalia mtu ambaye alikuwa anampa pole kwani alinyanyuka alipokuwa amekaa na kukimbilia nje kabisa barabarani..
Masaa kadhaa baada ya taarifa ile kutokea , kijana huyu alionekana eneo la Raskazoni akiwa ameketi kwenye vimbweta akiangalia upande ambako kulikuwa na maji ya bahari , huku kila baada ya dakika akifuta machozi yaliokuwa yakimwagika kwa kiganja cha mkono wake. .
“Mungu kwanini unanifanyia hivi , kwanini unanipa uwezo wa kuota matukio yanayotokea kweli lakini ukaninyima uwezo wa kujiokoa katika matukio hayo, haya sasa nimesababisha baba kufariki , ndoto hizi kwangu hazina maana”Aliongea kijana huyu kwa kusikitika sana .
SURA YA 21
Upande wa huku hospitalini yule baba aiekuja na kijana huyu hospitalini , alikuwa katika hali ya wasiwasi sana na hii ni baada ya kumtafuta Hassani kila kona pasipo kumuona , alijikuta akichanganyikiwa na kuogopa kwa wakati mmoja , alihofia Hassani asije akafanya kitendo hatarishi , kwani alikuwa kwenye majonzi.
Mwanadada Lisa alionekana ni mwenye kuguswa sana na tukio lile . hali ile ilimfanya kukosa amani na kujikuta akiomba wenzake ruhusa kwamba anarudi nyumbani walikokuwa wamepanga , kwani walikuwa ndani ya hospitali hii ya Bombo kwa ajili ya mafunzo ya vitendo .
Baada ya kurudi nyumbani alijikuta akikosa raha kabisa , ni kama mtu ambaye alikuwa akikukumbuka matukio ya nyuma ambayo yalimkosesha Amani , baada ya kuona mawazo bado yanamwandama , alitoka ndani na kisha alisogea upande wa barabarani na kuita bodaboda iliompeleka mpaka mtaa wa Raskazoni sehemu ambayo alikuwa akipendelea sana kukaa pindi anapokuwa na mawazo .
Baada ya kushushwa alijikuta akitembea taratibu sana kutafuta sehemu ya kukaa na ile anageuza upande wa kulia alijikuta akimuona yule kijana aliekuwa hospiutalini akilia , Lisa alijikuta akisogelea na kukaa kwenye kile kimbweta alichokuwa amekaa huyu kijana.
“Pole sana”Ni sauti iliosikika kwa mara ya pili kwenye masikio ya kijana Hassani na kujikuta akigeuza macho yake na kumwangalia mtu anaempa pole , maana hakuwa akijua kuwa pembeni yake kulikuwa na mtu aliekuwa amekaa .
Kijana huyu ambae alionekana kuwa na maisha Duni kutokana na maazi yake aliokuwa amevaa , alijikuta akimwangalia mwanadada huyu mwenye uzuri wa ajabu .
Lakini Lissa ni kama alikuwa amefungulia kilio kwa wakati mwingine kwa kijana huyu , kwani alianza kulia tena kwa kwikwi akionyesha alikuwa kwenye machungu makubwa sana.
“Nimemuua baba , sistahili kuonewa huruma”Aliongea kijana huyu jambo ambalo lilimfanya mwanadada huyu kushangaa ni kwanini kijana huyu anatamka neno kama hilo .
“Sio kweli hupaswi kujilaumu , kila kitu hutokea kwasababu ni mipango ya Mungu”Aliongea mwanadada Lisa huku akionekana kumuonea huruma kijana huyu .
“Kifo cha baba nimekisababisha mimi , na wala sio mpango wa Mungu”
“Sio kweli ni mipango ya Mungu usiseme hivyo”
“Kama Mungu amenionyesha hili jambo kabla ya kutokea , huu sio mpango wa Mungu hata kidogo , mimi ndio wa kupaswa kulaumiwa”Aliongea na kisha alinyanyuka na kuondoka .
Hakika maneno haya yalimchanganya sana mwanadada huyu Lisa , hakuelewa ni kwanini kijana huyu anaongea maneno hayo , alitamani sana kujua ni kwasababu ipi kijana huyu alikuwa akisema amemuua baba yake ,jambo ambalo ni mara chache sana kulisikia ,na hata kama ni kweli kwannini kijana huyo alikuwa akili ilihali alimuua baba yake , na hata kama ilikuwa ni nahati mbaya je ilikuwaje , hayo yote yalikuwa ni maswali aliojiuliza Lisa huku akiendelea kuangalia maji ya bahari .
*****
Naam Ndani ya kijiji cha Nkumba wilayani Muheza ndani ya nyumba moja ndogo sana iliokuwa imeezekwa kwa nyasi tofauti na nyumba zote zilizokuwepo ndani ya kijiji hiki , walionekana baadhi ya wanakijiji waliokuwa na hali ya simanzi kwenye nyuso zao , na hii ni mara baada ya kupokea mwili wa Mzee Nyangwe aliekuwa amefariki ndani ya hospitali ya Bombo Tanga .
Licha ya mazingira kuwa finyu ndani ya eneo hilo , lakini watu walionekana kujaa kwelikweli,huku kijana Hassani aliekuwa amejibanza pembeni ya nyumba yao alionekana ni mwenye huzuni kweli , mrafiki zake kutoka shule ya sekondari Nkumba walikuwa wakimpa pole lakini badi hawakuweza kutoa hali ya huzuni aliokuwa nayo kijana huyu .
Baada ya kama masaa manne kupita ndipo mwili wa marehemu ulitolewa nje na Shekhe alianza kuswali dua kwa ajili ya kuombea mwili huo , kitendo ambacho kilifanyika kwa lisaa na baada ya hapo safari ya kuupeleka kwenye nyumba yake ya milele ilianza , vijana walipokezana kubeba mwili huo kwa kujipanga njiani kuelekea lilipo shamba la Mzee Nyangwe sehemu ambayo ndio kaburi lake lilikuwa limechimbwa.
Ni ndani ya masaa kadhaa baada ya kuupeleka mwili wa mzee Nyangwe katika nyumba yake ya ,milele , muda wa saa sita kamili ndani ya nyumba hii ya mzee Nyangwe kulionekana kumepoa kutokana na kwamba maziko yalikuwa yamekwisha kufanyika na hakukuwa na lingine la kufanyika hapo nyumbani , kwani familia mzee nyangwe maisha yake ya hapo kijijini yalikuwa ni ya kimasiikini sana , kiasi kwamba hata kwenye huo msiba hakuna chochote kilichokuwa kimepikwa.
Ni karibu watu watano tu ndio waliiokuwa wamebakia hapo nyumbani mmoja akiwani rafiki yake wa karibu wa Hassani na wengine walikuwa ni family ya mzee Kitasa ambae ni yule aliemsindikiza Hassani Hospitalini.
Wakati hayo yakiendelea mara baada ya dakika chache walionekana vijana kadha wakiingia ndani ya eneo hilo huku wakiwa wameongozana na mwanadada Lisa ambae haikueleweka amefikaje ndani ya kijiji hicho , , watu wengi wa kijiji hicho walimshangaa sana mwanadada huyo , hasa pale alipoeleza kwamba amekuja kwenye msiba wa Mzee Nyangwe Jambo ambalo liliwashangaza wanakijiji hawa , kwani walikuwa wakimjua mzee ?nyangwe hakuwa na ndugu mjini na juu ya yote ni mwanadada huyu kuja akiwa na gari la kifahari . .
Hassani alijikuta akishangaa sana ujio wa mwanadada huyu , kwani katika kumbukumbu zake ni kwamba mara walipoonana kule Raskazoni hawakuongea chochote Zaidi ya Hassani kunyanyuka na kuondoka .
“Pole sana”
Ni neon ambalo kwa mara ya tatu mwanadada huyu analitamka akimwambia Hassani.
“Asante”Aliongea Hassani huku akimwangalia kwa Mshangao wanadada huyu .
“Karibu sana Dokta kiti”Aliongea Mzee Kitasa kwani alikuwa akimkumbuka mwanadada huyu kama moja ya madaktari waliokuwa wamemfanyia mzee Nyangwe upasuaji jambo ambalo lilimshangaza kidogo Hassani.
Lisa alieleza kwamba amekuja kwa ajili ya msiba , lakini pia alieleza kuwa alikuwa amegunswa na maneno ambayo kijana Hassani alikuwa akiyatamka , alitaka kujua ni kwanini kijana huyo alikuwa akisema kwamba yeye ndie aliemuaa baba yake
Na hapo ndipo alipoweza kusimuliwa kisa ambacho kilimsisimua na kumsahangaza sana mwanadada huyu .
*****
Kwa majina yangu halisi naitwa Hassani Hamisi Nyangwe nimezaliwa hapa hapa kijijini kwetu na kukulia hapa hapa , mpaka kufikia umri huu wa miaka kumi na sita nikiishi na baba yangu Nyangwe , kwani mama yangu alifariki punde tu baada ya kunileta duniani.
Maisha yetu kwa ujumla sio mazuri sana na naweza kusema kwamba kwa hapa kijijini ni familia yetu pekee ambayo ilikuwa ni ya umasikini uliokithiri , lakini licha ya hivyo sikuwahi hata mara moja kujilaumu kuzaliwa katika aina hii ya familia , kwani nilichokuwa nikiamini katika maisha yangu ni kwamba Mungu ndio mpaji wa yote.
Licha ya umasikini wetu nilikuwa nikimpenda sana baba yangu mzee Nyangwe na hata yeye ia alikuwa akinipenda sana , naweza kusema kwamba tokea nifikie umri wa kujielewa Mzee Nyangwe kwangu ndio baba ndio mama kwangu na kwangu nilimchukulia kama zawaidi ambayo Mungu amenipa
Maisha yetu hapa kijijini kwa ujumla wake licha ya kuwa masikini , yalikuwa ni ya furaha sana , kwani mimi na baba tuliishi maisha kama washikaji , na tulikuwa tumezoeana sana kiasi kwamba hata baadhi ya wanakijiji walikuwa wakishangaa namna ambavyo nilikuwa nimemzoea mzee .
Lakini licha ya furaha niliokuwa nayo katika maisha yangu , kuna jambo moja tu ambalo lilikuwa likinisumbua sana katika maisha yangu na hili ni jambo ambalo nilizaliwa nalo , sikuwahi kujua uwezo huu ambao nilizaliwa nao ulikuwa ukimaanisha nini katika maisha yangu na siku niliokuja kuanza kujua nina uwezo huu ni kipindi nikiwana miaka kumi.
Ilikuwa ni siku ya ijumaa jioni baada ya kumaliza kujisomea kwani kipindi hicho nilikuwa darasa la pili, kama ilivyokuwa kawaida baada ya kusoma nilipanda kitandani na kuutafuta usingizi , kitanda ambacho nilikuwa nikilala na baba , kwani nyumba yetu ilikuw ani ya vyumba viwili tu yaani jiko na sehemu ya kupikia .
Basi wakati nikiwa kwenye usingizi ilinijia ndoto nikiwa naenda shule asubuhi siku ya jumatatu , siku ambayo kwenye ndoto niliona ni siku ambayo ilikuwa na mvua, na hata mwendo ambao nilikuwa nikitembea ni wa kukimbia ili kuepuka kuloanisha nguo na madaftari , basi wakati nafika shule ya sekondari Nkumba , shule ambayo ilikuwa imepaka na shule ya msingi Nkumba , nilijikuta nikiteleza na kutumbukia kwenye mtaro ambao ulikuwa ndio kama mpaka kati ya shule ya sekondari na ya msingi Nkumba , na kutokana na kwamba siku hio mvua ilikuwa imenyesha sana na ule mtalo ulikuwa umejaa maji machafu , yalinichafua mwili mzima na kufanya wanafunzi wenzangu ambao walikuwa wamesimama kwenye korido za madarasa kunicheka .
Kabla ya ndoto kuisha nilijikuta nikiamshwa na baba .
“Wewe hassani Amka kumekucha tujiandae twende shambani”
Basi niliamka baada ya baba kuniamsha na niliwasha moto na kuchemsha mihogo ambayo kwa kipindi hicho ndio kilikuwa chakula chetu kikubwa , kwani ni zadi ya miezi tisa mvua hazijawahi kunyesha na hata msimu wa kulima mahindi ulikuwa unakaribia kupita , lakini mvua bado haikuwa hata na dalili.
Basi hatimae tulienda shambani na kulima na kurudi nyumbani muda wa jioni huku tukiwa tumechoka sana .
“Hivi Hassani mvua isponyesha sijui maisha yatakuwaje miezi ijayo , maana sio kwa hili jua”Aliongea mzee huku akirusha Jembe chini .
“Nimeota mvua itanyesha Jumatatu”
“Hio ni ndoto tu , sidhani kama itanyesha” Aliongea baba na mimi nikacheka na kupotezea na hata siku hio ilipita na siku pia ya jumapili ilipita na siku ya jumatatu ikafika , siku ambayo nilichelewa sana kuamka kiasi kwamba baba ndie alieniamsha .
“Wewe Hassani amka mvua imepungua uwahi shuleni utachelewa”Aliongea baba ambae alinifanya nikurupuke na kuanza kujiandaa kuelekea shuleni , huku nikiwa nimechelewa kweli halafu wiki hio iliokuwa inaanza ilikuwa ni zamu ya mwalimu Bony , mwalimu ambae alikuwa akiogopeka sana kwa kuchapa , alikuwa ni mkurya na alikuwa na kajimsemo kake akitaka kukuchapa anakwambia “Okoa muda” na hata kwenye meza yake ofisini alikuwa ameandika hilo neno la “Okoa Muda” sasa shuleni ndio tulikuwa tunamuita kwa jina hilo la Mzee wa kuokoa Muda , na siku ukiona mwalimu huyu anakwambia okoa Muda basi jua tu anamaanisha lala ule zako ambapo ukiamka baada ya kichapo wiki nzima utakuwa unakaa kwa maumivu mengi sana darasani na pengine usije kabisa shuleni.
Basi nilijiandaa harakaharaka na kunywa chai isiokuwa na sukari na kisha ninakimbia kuelekea shuleni huku mvua ikiwa inayesha japo sio sana , niliungana na wanafunzi wenzangu na kuendelea na safari , huku nikiwa nimesahau kabisa ndoto niliokuwa nimeota usiku wa kuamkia jumamosi , basi ile nilivyofika katika mtalo nilijikuta nikteleza na kutumbukia mtaloni na kuchafuka mwili mzima , huku wanafunzi wenzangu wakiwa wanazomea na kucheka , hakika ilikuwa ni aibu sana kwangu , nilijiangalia na kujiona sifai kuendelea kubaki hapo shuleni na kugeuza taratibu kurudi nyumbani kwani nisingeweza kuendelea na masomo kwa namna ambavyo nilikuwa nimechafuka na nilikuwa nikitoa harufu.
Sasa wakati narudi ndio nikaanza kukumbuka ile ndoto niliokuwa nimeota , hakika nilishangaa kabisa , kwani kila kitu kilichokuwa kwenye ile ndoto ndio kilichokuwa kimenitokea nilishangaa lakini mwisho wa siku niliipotezea japo pia nilimwambia baba , lakini hata yeye hakuizingatia sana.
Basi siku zilipita na baada ya wiki nilijikuta nikiota ndoto nyingine na hii ilikuwa ni ndoto ambayo nilimuona baba aking`atwa na nyoka , ndoto hii wakati naona ilikuwa ni siku ya jumaanne kuelekea Jumatano na jambo la kushangaza ni kwamba siku hio hio ya Jumatano wakati narudi shuleni nilipokea taarifa kutoka kwa mke wa mzee Kitasa kwamba baba ameng`atwa na nyoka na amepelekwa hospitali ya Teule , taarifa hio ilinishitia mno na kunishangaza kwa wakati mmoja , kwani nilichokuwa nimeota ndio hiko hiko kilichokuwa kimetokea na nilichokuwa nikitaka kuhakikisha ni sehemu ambayo baba alikutwa na janga hilo , na baada ya siku mbili za kutoka hospitali ya Teule ndio nikamwambia baba anionyeshe mahali ambapo alikutwa na mkasa huo wa kung`atwa na nyoka na sehemu alionipeleka ni pale pale ambapo nilipashuhudia ndotoni na hili swala niliamua kumsimulia na baba akaniambia kwamba .
“Hizo ni ndoto tu Hassani hazina maana yoyote “
“Lakini baba hii ni mara ya pili naota kitu kinatokea kweli bahati mbaya haitokeagi mara mbili”
“Basi tufanye hivi kama itatokea umeota mara ya tatu na ikawa kweli nitakupeka kwa mzee Kigo asome nyota yako huenda ukawa Nabii”Aliongea mzee na mimi nikakubaliana nae.
Basi ilipita mwezi namini nilisahau kabisa lile swala na tulikuwa kwenye mfungo wa Ramadhani mwezi wa tano , kipindi ambacho tulikuwa tukielekea kumaliza muhula wa kwanza shuleni ili tufunge shule .
Basi siku moja niliota nyumba ya Mzee Kesi ikiungua na moto huku yeye na familia yake yote wakiwa ndani , na tena ilikuwa ni muda wa usiku kabisa , Mzee kesi alikuwa ni moja ya watu waliokuwa na pesa hapo kijijini , kwani alikuwa akimiliki ‘Chain Saw’(mashine ya kukatia miti na mbao) na kupitia mashine yake hio alikuwa akijipatia pesa nyingi sana kwa kuuza mbao lakini pia kukodisha , mzee huyu alikuwa na familia ya watu saba , mke wake, yeye mwenyewe , Ratifa ambae alikuwa Sekondari Nkumba , Abasi ambaye alikuwa ni mkubwa kabisa ashamaliza shule ila alikuwa akiishi na wazee wake oamoja na wajukuu zake watatu mmoja akiwa ni mtoto wa Abasi aliezaa na mwanamke ambaye alimkimbia na wengine wawili walikuwa ni watoto wa mtoto mkubwa wa mzee Kesi aliekuwa akifahamika kwa jina la Mwantumu ambae alikuwa jijini Dar es salaam.
Basi siku ile kwangu nilikuwa na wasiwasi sana juu ya ile ndoto na mbaya Zaidi sikuwa nyumbani Nkumba siku hii , kwani tulikuwa tumeenda Magila kupasua mawe mimi na baba na Mzee Kitasa , wakati tupo njiani nilimweleza mzee huyu juu ya ndoto hio lakini hakuwa ni mtu wa kuzingatia namimi nikapotezea .
Nakumbuka siku hii tuliweza kurudi muda wa saa moja kasoro hivi na wakati tunafika Nkumba bahati nzuri niliweza kukutana na Ratifa ambae alikuwa amebeba ndoo ya maji akiwa ametangulizana na mtoto wa Abasi aliekuwa akifahamika kwa jina la Adam aliekuwa anasoma Chekechea akiwa na yeye amebeba maji kwenye kigaloni cha lita tatu .
“Dada Rat nimeota ndoto nyumba yenu inaungua”
“Wewe mtoto hebu acha kutuwangia bhna” Aliongea Ratifa kwa dharau na mimi sikumjali sana nikasepa zangu kwani kipindi hiki nilikuwa mtoto na hata ningemwambia mtu asingeniamini. .
Basi nilikuja kuamshwa na vilio vya watu muda huo ilikuwa ni saa Sita za usiku na hata nilipoangalia pembeni baba sikumuona , nilijikuta nikitoka nje na ile natoka tu niliona wingu la moshi likiwa limetanda uelekeo wa nyumba ya Mzee kesi , lakini ile nashangaa sauti za vilio huku nikisia wamam wanaongea kwa sauti ‘Nyumba ya mzee kesi jamani inaungua na wenyewe wapo ndani”
Kusikia hivyo tu nilijikuta nikipatwa kama mshituko wa moyo huku mapigo ya moyo yakienda kwa kasi sana , nilitoka na kuelekea upande huo , sehemu ambayo ulikuwa ukivuka nyumba nne tu unakuwa umefika na ile nafika ni kama vile nipo ndotoni , kwani vile vile moto ulivyokuwa unawaka ndio nilicyo ota , huku watu wakihangaika kuokoa watu waliondani , na maji kumwagwa , lakini ni kama moto ulikuwa ukizidi .
“Bahati nzuri ni kwamba wazee wa kijiji walifanikiwa kutoboa tundu na kuanza kuitia jina la Mzee Kesi wakimwambia atoke lakini tulichoweza kusikia ni neno moja tu kwa mzee Kesi , kwamba hawezi kutoka ilihali familia yake yote imeshateketea kwa moto , wanakijiji walijaribu kumbembeleza mzee Kesi atoke , lakini halikusaidia kwani hakutoka.
Mpaka inafika saa tisa za usiku moto ulikuwa umezima , lakini vilio vilikuwa vya aina yake , sio watoto sio wazee watu walishindwa kujizuia ,kila aliekuwa akiangalia miili iliokuwa imetolewa na kupangwa nje ikiwa imeungua vibaya alijikuta akilia sana , Siku hii pia nililia mno , yaani sana huku nikijiona mkosaji sana .
Tukio hili liliniathiri vibaya sana kisaikolojia kiasi kwamba hata usiku nilikuwa nikiogopa kulala kwa kuhofia kuota jambo baya , na ukiachilia kwamba hiki kipindi bado nilikuwa mtoto ,,Baba nae alijaribu kuniweka sawa , lakini bado niliogopa sana kwa wakati mmoja .
Basi baada ya wiki kupita mzee alinichukua na kunipelka kwa mzee kigo kwa ajili ya nyota yangu kuangaliwa
Mzee kigo alikuwa ni mganga aliekuwa akifahamika sana pale kijijini na kuogopeka sana , alikuwa akifichua wachawi wengi lakini pia kutibu watu wengi wenye shida mbali mbali , na wengi walikuwa wakitoka mpaka mikoani kwa ajili ya kuja kupata huduma kwa mzee Kigo.
Basi nilipokelewa na kuanza kufanyiwa tiba pale , akachukua kioo chake flani hivi alikuwa akikipaka unga flani ambao sikuwa nikiujua halafu anakirusha juu kinatua chini huku anaongea maneno anayoyajua yeye halafu anaangalia tena , na anakirusha tena juu na kinatua chini , , alivyomaliza , alikichukua akaitumbukiza kwenye maji yaliokuwa yamejaa kwenye chungu kikubwa na kisha aliweka unga flani hivi kama majivu na kisha akakitoa kile kioo na kukifuta na kisha akanisogelea na kukiweka kwenye uso wangu , yaani mimi nikiangalia nyuma ya kioo na kisha yeye akiangalia mbele ya kioo.
Baada ya dakika mbili alijikuta akishituka sana na kukidondosha kile kioo na kisha akanza kuniangalia kwa umakini huku akiokota kile kioo na wakati huo baba alikuwa anaangalia tu kinachoendelea .
Baada ya kama dakika kumi hivyo alionekana kumaliza kile alichokuwa anakifanya na kisha alinipa kisu na kuniambia nichukue Jogoo ambae tumekuja nae , maana kwa huyu mzee sheria zake kama unataka kusomewa nyota yako , basi unatakiwa kuja na jogoo mweupe na mchanga wa mlangoni , yaani pale kwenye mlango wa kutokea unachimba chini na unachukua mchanga..
“Tayariii ….. Tayariii …. Hassaniii …” aliongea kwa sauti yake ya kutisha pale na tulikuwa tayari kwa kupokea majibu
SURA YA 22
“Kijana umezaliwa na bahati kubwa sana kwenye maisha yako , Mababu wa ukoo wako wamekupatia uwezo wa kutambua mambo yatakayokuja”
“Unamaanisha nini Mzee Kigo?”Aliuliza baba
“Hassani ni Mlinzi mkuu wa kijiji hiki , mababu wa koo zote hapa Nkumba wamemchagua kama mlinzi , ilikuwa kosa kubwa sana kuruhusu familia ya mzee Kise kuungua na moto , ulitakiwa kuwaokoa, maana ni jukumu la mababu wa koo waliokupatia na hivi sasa wamekasirika na wanapaswa kutulizwa” aliongea Mzee Kigo na kumfanya Mzee wangu kushituka na kujawa na wasiwasi , kwangu mimi sikuwa na imani sana na mambo ya kiganga tofauti na Mzee ambae yeye alikuwa ni muuminni mzuri tu.
“Kwa hio tunafanyaje mzee Kigo”.
“Kafara ya Mbuzi kwa kila koo inatakiwa kufanyika kwa ajili ya kuwatuliza mababu wa koo”.
Basi kama alivyolekeza tuliweza kutoa kafara ya Mbuzi ambayo tunachinja huko juu milimani kabisa kwenye pango moja , pembeni kabisa na kilipo chanzo cha maji ambayo ndio hutumiwa na watu wa kijijini kwetu kwani kulikuwa kumeunganishwa mabomba .
Basi baada ya hapo niliendelea kuota ndoto za kweli tu na katika kuota ndoto hizo , hakuna siku ambayo hata moja niliweza kuzuia ndoto mbaya kutokutokea , yaani nilichoweza mimi ni kuota tu lakini sikuweza kuzuia kile nilichokuwa nikiota kutokutokean kama ni kibaya , licha ya maneno ya Mzee Kigo kwamba ninatakiwa kuzuia.
Basi baada ya miaka kupita , siku ya ijumaa kuelekea jumamosi , mzee wangu muda wa usiku aliweza kuniambia kuwa siku ya kesho wanaelekea Muheza mjini kwa ajili ya kuuza vitunguu na Mzee Kitasa, huku akiniachia kazi ya kwenda kumwagilia pilipili asubuhi na mimi nilikubali na kisha tukala tukalala , basi usiku niliweza kuota ndoto mzee anagongwa na pikipiki Muheza mjini.,ndoto ambayo nilivyokuja kushituka ilikuwa ni saa kumi na moja kama na nusu hivi asubuhi na nilipoangalia pembeni sikumuona mzee ,nilijikuta nikikurupuka na kutoka nje kumwangalia kama mzee yupo lakini sikumuona , nilichokifanya ni kutulia na kusubiria , kwani mzee aliniambia ni asubuhi na huwaga hana ile tabia ya kuondoka pasipo kuniamsha , nilirudi ndani na kusubiri mpaka saa moja na robo ndipo hofu ilipo nijaa na kujua lazima mzee atakuwa amekwisha kwenda Muheza , niliinuka mbio na kwenda nyumbani kwa Mzee kitasa na nilimkuta mke wake akiwa nje anafagia nilimsalimia na kisha kumuuliza kama mzee alikuwa ashaenda mjini na jibu lake ndio liliniacha hoi kwani aliniambia kuwa walikwisha kwenda toka saa kumi na moja .
Nilijihisi kuchangayikiwa na hilo hata kwa mama Jabu aliliona hilo .
“kwani kuna nini Hassani?”
“Baba atakufa , nimeota anakufa” Niliongea na mama Jabu alijikuta akishituka mno kwani pia hata yeye alikuwa akijua uwezo wangu huo wa kuota vitu vinatokea .
“jamani jamani sasa tunafanyaje ?”
“naenda ,mjini mama Jabu niazime hela kidogo”
Basi mama Jabu alinipatia elfu moja na miatano ya nauli na kisha nikapanda bodaboda kuwahi mjini kumuokoa baba , safari ambayo kama ningejua nisingeenda , kwani ile nafika uwanja wa jitegemee , sijui ilikuwaje , kuna mtoto alikuwa barabarani na sisi tukawa tupo kwenye spidi kali halafu mbele yetu kulikuwa na gari ya Tanesko inakuja , sasa katika harakari za kumkwepa mtoto yule bodaboda alijikuta akichukua uelekeo wa kwenda hopitali ya Teule na hapo ndipo nipokuja kushitukia baba yupo mbele yetu na pikipiki ilikuwa kwenye spidi kali ,na kilichotokea ni kwamba baba tulimgonga na kumrusha upande mwingine na akaenda kuvaa chuma cha mashine ya kupasulia mbao upande wa kushoto na kujigonga kisha akatumbukia mtaloni huku damu zikiwa zimetapakaa .
****
“Pole sana Hassani , sasa hukujiona kwenye hio ndoto ukiwa kwenye pikipiki?”
“Hapana sikujiona nilchoota ni baba kugongwa na pikipiki tu ila sikujua pikipiki hio ndio itakuwa nitakayopanda” Alijibu Hassani huku mwanadada Lisa akiguswa mno na simulizi hio , licha ya kushangaa uwezo aliokuwa nao Hassani wa kuota mambo yanayotokea kweli , lakini swala la ajali ya baba yake kusababishwa na yeye mwenyewe katika harakati za kumuokoa lilimgusa mno , na aliona ni kweli kijana huyu alikuwa na haki ya kutamka yale maneno ya kwamba amemuua baba yake .
“Mimi naamini kuna kitu cha ziada juu yako , labda hujakitambua bado”
“:Sidhani kama kuna kitu kama hicho ,, hii ni laana kwangu , haiwezekani niote vitu ambavyo ni vya kweli ila nishindwe kuzuia matukio mabaya ninayoota”
“Ushawahi kutoa tukio lolote ambalo sio la kutisha ?”
“Sijawahi kuota “
“Basi kunasababu ya kuwa hivyo Hassani , naamini ni uwezo ambao Mungu kakupatia akiwa na sababu zake”
“Siamini hivyo Sister”
Basi mwandda huyu alitoa rambirambi yake na kisha kuaga huku akiahidi kurudi Nkumba akiwa na jibu juu ya uwezo wa Hassani.
Je simulizi hii inauhusiano gani na Book of all names tuendelea tulipoishia
*****
MIEZI MIWILI BAADA YA MAANDALIZI. ,SIKU MOJA KABLA YA SIKU AMBROSE AKISIMULIWA SIMULIZI YA BOOK OF ALL NAMES
WACO –TEXAS
Ni ndani ya shamba moja kubwa lililokuwa likimilikuwa na bwana mmoja aliekuwa akifahamika kwa jina la Hudson , shamba hili lilionekana kujaa mahindi mengi ambayo yalikuwa akikaribia kuvunwa , kwani yalikuwa kwenye hatua za mwisho , ilikuwa ni muda wa mchana , muda ambao bwana Hudsoni akiwa kwenye banda lake kubwa la Ng`ombe alipokea wageni , mmoja akiwa ni mwanamke rangi ya kiafrika mrembo alievalia suruali ya jeans na tisheti ya Puma , na mwingine alikuwa ni mwanaume pia akiwa ni rangi ya kiafrika alievalia jeans na tisheti nyeupe huku akiwa na koti la suti rangi ya ugoro . .
Mabwana hawa walijitambulisha mmoja akiitwa Linda na huyu mwanaume alijitambulisha kama Zakayo , ujio wa watu hawa ndani ya nyumba ya bwana Hudsoni ilikuwa ni kwa ajili ya kukodi Ghala lake moja la kuhifadhia mahindi kwa muda wa wiki moja , jambo ambalo lilimshangaza bwana Hudson kwa watu hao kuomba Ghala lake ambalo ni mwezi uliopita tu alitoka kulisafisha kwa ajili ya kuweka mahindi mapya na kutoa yale ya zamani .
“Mnahitaji ghala langu kwa madhumbuni yapi?”
“Hilo hatuwezi kuliweka wazi Mr Hudson ila tatalipa pesa nyingi sana Zaidi ya mara mbili ya bei utakayotutajia kukodi eneo hilo kwa wiki moja”
Mzee Hudsoni mwenye umri wa miaka 61 alijikuta akishawishika kwa utayari wa watu hawa kutaka kumlipa mara mbili ya pesa ambayo atawatajia , lakini licha ya kushawishika huko hakuwa tayari kutoa Ghala lake , kwani alikuwa na wasiwasi wa kile watu hao watakifanya pale tu atakapo toa hilo Ghala lake ,na maamuzi alioyafanya ni kutaja bei kubwa Zaidi kuliko s thamani ya Ghala lake na hapo watu wale yaani Zakayo na Linda walitabasamu na kuzidisha mara tatu ya hela aliotaja mzee huyu na kisha wakamwambia watampatiakiasi hicho , jambo ambalo liliibua mshangao na matamanio ya kiasi hicho cha pesa kwa mzee Hudson na moja kwa moja alikubali na kuwapeleka watu hawa kwenye Ghala kwa ajili ya kuangalia lakini pia na kuwaachia mlango .
Lakini licha ya hivyo mzee Hudsoni alitaka malipo yake hapo hapo na ilichukua dakika moja tu malipo yaliweza kufanyika na kuingia kwenye akaunti yake ya benki , kitendo ambacho mzee huyu alitoa macho , kwani hakuwahi kuzania kama anaweza kupata kiasi hiko cha pesa kwa muda mfupi na aliona kwa hela hizo zinamtosha kabisa katika uzee wake na hata asipolima tena .
Basi baada ya Linda na Zakayo kukabidhiwa ufunguo wa ghala hili ambalo lilikuwa na umeme , muda wa saa moja kamili iliingia gari nyingine na hii ilikuwa ikiendeshwa na Erick Peter.
“Kazi nzuri sana mmefanya , lakini ninawasiwasi na mzee Hudsoni asije kuta taarifa”.
“Halafu hilo tumeshau ila nitayaweka sawa na mzee huyu na kutokana na pesa tuliompatia nadhani hatafanya jambo kama hilo”Aliongea Zakayo huku wakisaidiana kutoa baadhi ya vitu kama vile tarakishi , mikoba na mazaga mengine na kuyaingiza kwenye hili Ghala , uzuri ni kwamba hili Ghala lilikuwa limejitenga kwa umbali wa mita kadhaa na nyumba aliokuwa akiishhi Mzee Hudsoni na hata kilichokuwa kinaendelea huku hakuwa ni mwenye kuona .
Ndani ya dakika kadhaa tu , ghala hili liligeuka kama ofisi ya kitehama , kwani kulikuwa na tarakishi moja kubwa na baadhi ya vifaa vingine ambavyo sikujua maana yake , lakini pia kulikuwa na meza na viti , lakini pia kulikuwa na kiti kimoja ambacho kilikuwa wazi , lakini kiti hiki pia kikiwa kimeunganishwa na umeme .
Ilikuwa ni muda wa saa nne kamili za jioni gari nyingine aina ya Range iliingia na kwenda kupaki mbele kabisa ya Ghala hilo . na ndani ya dakika kadhaa tu alionekana Janeth akiwa na mzee mmoja wa kizungu ambae alikuwa amezibwa zura yake huku akiwa na pingu kwenye mikono yake iliofungwa kwa nyuma .
Baada ya madakika sekunde kadhaa mzee alikuwa amekarishwa kwenye kile kiti ambacho kilikuwa wazi lakini kilikuwa kimefungwa na kwa kuunganishiwa umeme .
“Bruno lamberk hatimae upo kwenye mikono yangu”Aliongea mwanadada Janeth na kumvua mzee huyu lile kofia walilokuwa wamemvalisha na hapo mzee huyu aliangalia watu waliokuwa mbele yake kwa mshangao huku akichunguza mandhari ya eneo hilo.
“Janeth unachokitaka kukifanya hutofanikiwa , baba yako alijitahidi sana lakini naamini unajua kilichomkuta watu mnaocheza nao ni watu wa hatari sana na huenda wako njiani kuja eneo hili”Aliongea huyu mzee kwa ujasiri amao ulimpandisha hasira sana Janeth , lakini alijizuia na kutabasamu.
“Tutaona kama utakuwa na ujasiri wa kuongea baada ya kuona kinachoendelea ISLAND X” Aliongea janeth na kisha walifunga karatasi nyeupe mbele ya Bruno na kisha walielekeza Projecta kwenye lile karatasi , huku Linda akimpiga gundi ya mdomo mzee huyu .
Wakati huo hayo nayaendelea Erick Upande wa nje alikuwa akirusha Drones ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kuangalia usalama wa eneo hilo .
Baada tu ya kurudi alisogelea tarakishi ile kubwa na kisha alianza kubonyeza batani kwa spidi na ndani ya dakika chache ule upande kulikokuwa na projecta , projecta mbalimbali kulionekana Picha mbalimbali zikionyesha eneo kubwa la kisiwa.
Na ndani ya madakika kadhaa tu , tu picha ilibadilika na kuonesha eneo la nje la Jumba moja kubwa lililokuwa katikati ya Mikoko likiwa limejengwa kwa ustadi mkubwa sana huku mbele kabisa ya jengoo hilo kukiwa na maandishi makubwa yaliosomeka ISLAND X –U-97 ECLUSIVE HEADQURTER .
Ni kitendo kilichokuwa kikionesha kama Movie kwani ndani ya madakika kadhaa tu , picha zilionekana zikionesha ndani kabisa ya jumba hili , huku watu eneo hili likiwa na makachero waliokuwa wakilinda kuanzia juu ya paa , pembezoni mwa ukuta ,getini na ndani ya eneo hili .
Baada ya madakika kadhaa tu video ile ilionesha eneo la nje ya kisiwa hiki mita kadhaa kutoka kwenye hili jumba , eneo hili lilikuwa ni sehemu ya Ndege kutua yaani kulikuwa na kiwanja kikubwa cha ndege ambacho kwa haraka haraka kilionekana kutosha ndege kubwa ya abiria kutua kwenye hili eneo .
Zilipita dakika chache tu chopa moja ilifika ndani ya hili eneo huku ikiwa na wanajeshi ambao walishuka na Kamba na kuimarisha ulinzi wa hili eneo , hakika ilikuwa ni jambo la kushangaza na ilikuwa ni kama kwenye Muvi .
Yote haya wakati yanaendelea , Janeth ,Linda , Erick pamoja na Zakayo walikuwa wakifatilia kwa ukaribu kabisa , lakini hilo pia kwa upande wa Bruno pia alikuwa akiangalia kile kilichokuwa kinaendelea huku akionekana ni mwenye kuwa na wasiwasi mkubwa.
Baada ya dakika kadhaa za ulinzi kuimarishwa hatimae ndege moja kubwa ya saizi ya kati ilionekana kutua eneo hili na baada ya kama nusu saa hivi , walionekana wanaume na wanawake waliotoka katika hili ndege wakiwa na mavazi yaliokuwa kama yale ya Majaji wanayovaa , na baada ya watu hawa kutoka , walifuatia watu wanne waliovalia nguo nyeusi wakiwa wamebeba kitu kama jeneza , lakini hili halikuwa jeneza ,ni mfano wake tu lakini likiwa la kioo huku watu wale wakiwa wanabeba kwa umakini mkubwa sana .
Baada ya jeneza hilo kushushwa hatimae alionekana , kijana Ambrose alietoka akiwa amevalia Suti akiwa ndani ya hili eneo na wakati haya yote yanafanyika ilikuwa ni mchana kweupe na jambo hili lilidhihirisha kwamba eneo walilokuwepo hao watu ni bara linguine kutokana na utofauti wa muda..
Basi baada ya ya kijana Ambrose kutoka na kuelekea kwenye Gari hatimae alitoka mtu ambae alimfanya Janeth ageuze Macho na kumwangalia Bruno kwa hasira .
Huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni mwanaume ambae alikuwa anafanana kwa kila kitu na mwanaume aliekuwa amefungwa kwenye kiti alichokuwa amekalia Bruno , jambo hili lilimfanya mzee huyu afurukute kwenye kiti chake , jambo ambalo lilimfanya Janeth kutabasamu.
“huu ndio mwisho wa U-97 kuwa na nguvu duniani , tunakwenda kusambaratisha kila kitu mlichokiandaa karne na karne wewe pamoja na hao mashetani wenzako”Aliongea janeth akimwagnalia Bruno na kumfanya mwanaume huyu azidi kufurukuta kwani hakuwa na uwezo wa kuongea neno lolote kwani alikuwa amefungwa na gundi mdomoni.
“Operesheni Island X inaanza kuanzia sasa na nataka wote muwe makini , kwani hili ndio jambo ambalo tulikuwa tukilisubiria kwa muda mrefu na hakutakiwa kuwa na makossa ya aina yoyote ile” Aliongea kijana huyu kwa kujiamini huku akiendelea kuchezesha cidole vyake kwenye komputa .
Naam nini kilitokea mpaka kufikia hatua hii ???????.....TUTAKUTNA IJUMAA PANAPO MAJALIWA
UNAWEZA KUIMALIIZIA KWA KULIPA 2000 TU NAMBA NI 0687151346AIRTELL AU0657195492 TIGO AU 0623367345 HALOPESA JINA ISSAI SINGANO UKILIPA TUMA MESEJI WATSAPP NAMBA 0687151346
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom