Simulizi -Kitabu kilichojaa majina yote

singanojr

JF-Expert Member
Sep 24, 2020
1,346
7,643

SIMULIZI HII NI YA KUTUNGA HAIUSIANI NA MTU YOYOTE WALA KIKUNDI CHOCHOTE , MAENEO , OFISI NA MAJINA YALIONDANI YA HII SIMULIZI NI YA KUBUNI

ENJOY

SURA YA 01​

Ilikuwa ni siku iliokuwa ikisubiriwa na kila mmoja ndani ya Taifa la Tanzania , kila mwananchi alionekana kufurahia lile jambo ambalo linakwenda kutokea muda mfupi ujao , nchi nzima ilionekana kuwa katika hali ya shangwe , huku kila mwananchi mmoja mmoja alikuwa akionesha kutoa maoni ya kufurahia jambo kubwa lililokuwa likienda kukamilika muda mfupi ujao.

Lakini licha ya wengi wa wananchi wa taifa hili kuwa katika hali ya shangwe na furaha , upande mwingine hali ilikuwa mbaya na hii yote ilitokana na watu hao waliokuwa katika upande mwingine kutokuamini kile kilichotokea , hawakuamini kabisa.

Naam ilikuwa ni siku ya kuapishwa kwa raisi Awadhi Abdukarim Jembe raisi wa awamu ya kumi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na hii yote ni baada ya bwana Jembe kushinda kwa kishindo na kuweka historia ya chama pinzani kuchukua madaraka ndani ya Taifa la Tanzania huku chama Tawala na mgombea wake kushindwa vibaya sana , jambo ambalo liliushangaza ulimwengu , kwani hakuna alieamini kama kuna siku chama tawala ndani ya taifa hili kinaweza kuondolewa madarakani baada ya miongo yote hio ya kutawala taifa la Tanzania kwa kushinda kila chaguzi tokea kuanzishwa kwa mfumo wa vyama vingi nchini .

Mara baada ya raisi Jembe kumaliza kula kiapo uwanja wa Uhuru ulifurika kwa shangwe kubwa huku neno ‘Jembe ni jembe’ likiwa limetawala uwanja mzima , na yote hayo hayakuwa ndani ya uwanja huo tu bali kila kona ya Tanzania kwa wale waliokuwa wakifatilia kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya siku hio katika uwanja wa Uhuru walikuwa wakishangilia na kulitaja jina la Jembe ni Jembe.hakika bwana Jembe alikuwa akikubalika sana , jambo ambalo liliushangaza ulimwengu , kwani vyombo vingi vya habari Duniani kote vilikuwa vikionyesha yale yaliokuwa yakiendelea ndani ya taifa la Tanzania huku wakijaribu kuweka nakshi juu ya neno “Chama Pinzani cha weka rekodi ya kuchukua madaraka ya nchi baada ya kukishinda chama Tawala “,lakini pia kitendo cha Raisi wa China kuhudhuria uapisho huo ilikuwa ni historia nyingine .

Basi taratibu zote za Raisi jembe kuapishwa ziliendelea huku akibadilishana madaraka na mtangulizi wake , viongozi mbali mbali waliohudhuria hafla hio ya kushuhudia bwana Jembe akipewa madaraka walimpongeza kila mtu kwa nafasi yake , huku wengi wao wakiahidi kumpa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha Taifa la Tanzania linafikia maendeleo ambayo wananchi wanatamani kuyaona chini ya utawala wa raisi Jembe.

Hata kwa raisi Jembe mwenyewe alikuwa na shauku kubwa ya kuwaongoza watanzania hususani katika kipindi hicho ambacho matukio ya kiuhalifu yalizidi kuongezeka ndani ya taifa la Tanzania, kwani ni wananchi wengi walikuwa na hofu na kile kinacho endelea ndani ya Taifa , kwani mtaani kulikithiri matukio mengi ya kikatili yaliokuwa yakifanyika huku serikali ikishindwa kutoa maelezo ya kueleweka kwa wananchi juu ya matukio hayo .

Na hio ikawa sababu kubwa kwa chama pinzani kuwashinda wagombea wa chama tawala kwa kishindo kikubwa , na hio yote ilitokana na wananchi kuchoshwa na hali ya hatari iliokuwa ikiendelea ndani ya Taifa la Tanzania .

Raisi jembe mwenyewe hakutegemea kama angeweza kushinda katika uchaguzi huo ,kwani alijua mambo ambayo yalikuwa yakifanywa na chama tawala katika kila uchaguzi , mambo ya kuiba kura za wananchi , lakini katika uchaguzi huu jambo hili lilimshangaza sana ,lakini pia lilimfurahisha sana , kwani lilijenga picha kamili kwenye kichwa chake kwamba wananchi wa Tanzania kwa awamu hio wameamua kuona mabadiliko yanatokea ndani ya nchi kupitia sanduku la kura.

Basi baada ya shughuli za uapisho kukamilika hatimae viongozi mbalimbali waalikwa walianza kuondoka ndani ya uwanja huo huku gari ya kwanza kuondoka ndani ya uwanja wa Uhuru ilikuwa ni gari iliombeba Raisi Jembe akiwa na msafara wa gari saba , gari ambazo zilikuwa zimejaa wanausalama kutoka kitengo cha usalama wa Taifa wa Tanzania na wale pia waliokuwa ndani ya Ikulu. .

Raisi mteule Jembe alikuwa kwenye wasiwasi mno , licha ya kuapishwa kuwa raisi lakini alionekana kuna jambo lililokuwa likimsumbua kichwa chake .

“Jiandae kuingia Ikulu muheshimiwa Jembe “ ni neno ambalo lilikuwa likijirudia mara kwa mara ndani ya kichwa chake , neno hili alipata kulisikia siku chache kabla ya siku mbili kuingia kwenye zoezi la kupiga kura , wakati akiwa anaingia nyumbani kwake akitokea kwenye hitimisho la kampeni iliofanyikia ndani ya viunga vya jiji la Dar es salaam katika kiwanja cha Tanganyika park Kawe.

Siku hio wakati anaingia nyumbani kwake Kigamboni ndipo alipoweza kupigiwa simu na mtu asiemfahamu na kumwambia hayo maneno ya kwamba ajiandae kuingia ikulu , mtu huyu hakuweza kujitambulisha kwake , kwani mara baada ya kuongea maneno hayo simu iliweza kukatwa hapo hapo na alijaribu kuipigia namba hio , lakini alijjikuta akishindwa kwani namba hio ilikuwa ni private.

Hata matokeo yalipotangazwa na kuibuka kidedea katika uchaguzi huo mkubwa alijikuta akishangaa sana , lakini pia na kupatwa na hofu kubwa , jambo kubwa lililompa hofu licha ya kushinda kihalali ni juu ya mtu huyo aliempigia simu na kumwambia kwamba ajiandae kwenda Ikulu , aliamini kama mtu huyo alikuwa na nguvu ya kuutabiri uchaguzi na kweli yeye kushinda basi mtu huyo hakuwa peke yake , huenda ni kikundi cha watu ambacho kilikuwa kikifanya kazi nchini ambacho kilikuwa na malengo ambayo hakuyajua yeye na chenye nguvu sana , na aliogopa maelengo ya kikundi hicho yanaweza kuwa hatarishi kwa taifa lakini pia kukinzana na mtazamo wake juu ya maendeleo ambayo anatamani kuyaona yakitokea chini ya utawala wake .

Msafara uliokuwa umembeba raisi Jembe uliingia ndani ya barabara ya Nelsoni Mandela na kukunja kushoto na kuingia ndani ya barabara ya kilwa , wakati wa huu msafara unaendelea kusonga kwa mwendo wa taratibu sana huku Raisi akiwa amesimama kwenye gari maalumu akiwapungia wananchi waliosimama kando ya barabara,Upande mwingine mita miamoja ndani ya jengo la nyumba ya makazi (Apartment) lililokuwa likifahamika kwa jina la Sokoine House nyumba namba sabini na nane gorofa ya tano alionekana kijana mmoja alievalia kofia nyeusi ya kampuni ya Nike , akiwa na mavazi meusi kabisa huku mkononi akiwa amevalia gluvusi (Gloves) lakini kubwa Zaidi bwana huyu alionekana kushika mtutu(Sniper riffle gun 5 SAKO TRG 42 kutoka Finland) akiwa ameuelekezea barabarani huku sikioni akionekana kuvaa visikilizishi (Earpieces) vya rangi nyeusi vyenye mkanda ulioelekea shingoni vinavyofanana kabisa na vile wanavyovaa wanausalama , bwana huyu kwanza muonekano wake ulionesha kabisa sio mzawa wa Taifa la Tanzania na hii yote ni kutokana na Rangi yake nyeupe na nywele zake.

Haikueleweka moja kwa moja ni kwa namna gani bwana huyu aliingia ndani ya jengo hilo na kuweka makazi yake hapo akiwa na mtutu akiulekezea barabarani kwani njia hio ilikuwa imekaguliwa na wanausalama , kwani ndio njia ambayo ilikusudiwa kwa raisi mteule Jembe kupitia mara baada ya uapisho akiwa anaelekea Ikulu magogoni .

Zilikuwa ni dakika kadhaa wananchi walio jipanga katika barabara ya Sokoine kushangilia na kumfanya bwana huyu alieshikilia mtutu kuongeza umakini kuelekea barabarani , na umakini wake ulimfanya kutabasamu na hilo ni mara baada ya kuona kile alichokuwa akikisubiria.

“Target is at 12 O`clock and clear Need permission”(Mhusika yuko kwenye shabaha mbele yangu naomba ruhusa “) Bwana huyu alionekana kuongea maneno hayo na hii ni mara baada ya kumuwekea shabaha raisi mteule yaani Mheshimiwa Jembe ambaye alionekana kutokuwa na habari na kinachoendelea upande wa pili , kwani sura ya furaha iliokuwa imeupamba uso wake iliwafanya wananchi wazidi kushangilia .

“I need permission”.(Nataka ruhusa )

“Umeruhusiwa “Ilisikika sauti nzito upande wa pili na baada ya bwana huyu kupata ruhusa aliseti vizuri kioo chake cha lenzi na kisha alivuta triga akimlenga raisi jembe , alionekana kuwa makini kweli na mbobezi katika kazi yake , kwani alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa na kile alichokuwa akikifanya .

Kilichosikika ni mlio uliokatika hali ya utulivu kabisa na hio ni mara baada ya bwana huyu kuachia Triga na kuruhusu risasi iliokuwa katika shabaha , huku akiamini risasi hio isingemkosa bwana jembo kwa namna yoyote ile .

Kitendo cha kumaliza kuachia risasi hio hapo hapo alijikuta akipigwa na kitu kizito kwenye shingo na kudondokea pembeni kwenye mlango wa kwenda jikoni huku akijihisi maumivu makali mno , lakini licha ya maumivu hayo hakutaka kuzubaa kwani pale pale alinyanyuka kwa kasi na kusimama na hapo ndipo alipo jikuta akishangaa kwani mtu aliekuwa mbele yake alikuwa ni mwanamke tena akiwa katika hali ya urembo kabisa , jambo lililomfanya bwana huyo aangalie mara moja bunduki lake lililodondokea pembeni ikifuka moshi kama mtu aliekuwa akihakikisha kwamba risasi ilitoka vyema kwenye bunduki hilo na kisha kumwangalia mwanadada huyu huku akijipanga kimapigano .

Lakini katika hali ya kushangaa alijjikuta akifikiwa na mwanadada huyo na mapigo ya haraka sana staili ya Krav Maga , roundhouse kick iliompata kisawa sawa na ile anajiweka vizuri kupangua pigo la pili alijikuta akishindwa kwani mwanadada huyu alievalia suti nyeusi alionekana kujua anachokifanya kwani ndani ya sekunde tano tu bwana huyo alikuwa amedhibitiwa vyema .

*****

SIKU TATU NYUMA KABLA YA UAPISHO

Licha ya kwamba chama tawala kilishindwa uchaguzi , lakini hakikiwa katika hali ya kukata tamaa kabisa ya kuachia nchi kwenda chama pinzani, kitendo cha wao kushindwa katika boksi la kura ilikuwa ni jambo baya sana kwao kuruhusu kutokea , hawakuelewa mara moja ni nini kilitokea mpaka swala la wao kishindwa likatokea , kwani kila kiongozi aliekuwa amewekwa kwa ajili ya kusimamia kura , walikuwa ni mtu wao , lakini bado walikuwa wameshindwa , jithada zote walizofanya katika kuhakikisha kwamba wanashinda uchaguzi huo licha ya kujua mwaka huo uungwaji mkono wao na wananchi ulikuwa mdogo sana lakini waliamini kwa kutumia nguvu yao kama serikali basi kusingekuwa na shida ,, lakini jambo la kushangaza ni pale walivyoona anaetangaza matokeo kwenda kinyume na matakwa yao na kumtangaza mheshimiwa Jumbe kuwa raisi mteule , jambo hilo kwa kila mwanachama kuanzia kwenye jeshi , viongozi na usalama wa Taifa kwa ujumla walifedheheshwa na jambo hilo kwa ujumla , hakuna aliekuwa akiamini kwamba jambo hilo limetokea la chama tawala kukosa kura za kushinda na kuwapeleka ikulu na kuendelea kuingoza nchi kama ilivyokuwa kawaida kwa miongo yote tokea kwa kuanzishwa kwa vyama vingi .

Hali sasa ilikuwa hali kwao , kwani waliamini yale maslahi yao waliokuwa wamejiwekea ndani ya serikali wanakwenda kuyakosa kama tu hawatafanya kitu kuokoa hali hio iliowakumba.

Viongozi wakubwa wote wa chama akiwemo raisi anaekwenda kuachia madaraka bwaba Mathayo kilubwa , mkuu wa majeshi ya nchi ambae na yeye alikuwa ni mwanachama kindakindani wa chama tawala , mkuu wa usalama wa taifa , na baadhi ya maraisi wastaafu walionekana kuwa katika meza ndani ya jengo la usalama wa Taifa Osterbay jijini Dar es salaam .

“Hatuwezi kuruhusu Jembe kuapishwa kwa namna yoyote ile “ Aliongea raisi anaekwenda kuachia madaraka au alieyamaliza muda wake huku akionekana kumaanisha kile anachokiongea kwa haiba ya sura yake

“Kila mtu ni tamanio lake hilo muheshimiwa , hatuwezi kuruhusu hilo litokee , na nadhani siku ya leo baada ya kikao hiki kumalizika tutakuwa na muafaka juu ya hili , sisi wote tulio hapa ni viongozii wakubwa wa nchi hii , naweza kusema kwamba sisi ndio serikali yenyewe hatuwezi kukosa muafaka” Alizungumza Nassoro kinga mkuu wa usalama wa Taifa.

“Naunga mkono hoja , Nadhani ni swala la sisi kuangalia ni namna gani tunaweza kulifanikisha hili…”Aliongezea mkuu wa majeshi ,Lakini wakati akiendelea kuongea mara mlango ulifunguliwa na aliingia mwanadada mmoja aliekuwa amevalia suti afahamikae kwa jina la Lucy , huyu alikuwa ni moja ya Special agent aliekuwa akimlinda raisi .

Basi baada ya Lucy kuingia alimsogelea moja kwa moja mheshimiwa Mathayo raisi anaemaliza muda wake madarakani na kisha alimwambia jambo kwa namna ya chini kabisa , na kumfanya bwana huyu kutabasamu na kisha alimruhusu Lucy kuondoka lakini pia aliongea na kumpa maelekezo mengine , na ilichukuwa takribani dakika moja tu alionekana mwanaume mwingine wa kizungu kuingia ndani ya ofisi hio iliokuwa ikifanyika kikao .

Bwana huyu alikuwa mzee kiasi makadirio ya umri wake si chini ya miaka sitini , akiwa na mwili wenye afya , alikuwa amevalia suti ya rangi ya bahari(bluu ambayo haijakolea ) , shati jeupe na tai ya kahawia huku nywele zake zilizoacha nafasi ya uwararaza zikiwa zimechanwa vyema alionekana ni wale wazee wanaojipenda sana kwa muonekano wake. . “Karibu sana mheshimiwa Kent nilifikiri utachelewa kufika “Aliongea raisi Mathayo akimkaribisha bwana Kent .

“Nisingeweza kuchelewa kutokana na jambo hili kugusa moja kwa moja Umoja wetu , na naweza kusema ni jambo ambalo linauhusu umoja kwa asilimia mia moja , kwa hio nadhani na mimi ni sahihi kabisa kuwepo mahali hapa kuliongelea “.

Baada ya makaribisho mheshimiwa raisi Mathayo aliitoa kwa ufupi kile walichokuwa wakieongelea katika kikao hicho na kisha baada ya kumaliza alimkaribisha bwana Kent kwa mchango wake .

“Nimekuja hapa nikiwa na madaraka kamili kutoka U-97, na maagizo niliopewa ni kuhakikisha Jembe anakufa kabla ya kuapishwa “Aliongea Kent na kufanya hali ya chumba hiko kuwa kimya kila mtu akitafakari jambo alilokuwa akiongea kwa kina .

“Inawezekana vipi , kwani mpaka sasa Jembe hajulikani alipo , mimi nadhani kwa sasa atakuwa amechuku a Tahadhari za kutosha mara baada ya kutangazwa kuwa Raisi hivyo itakuwa ngumu kwa sasa kumpata “

“ Ni kweli mpaka sasa hatujui Jembe alipo , mimi nadhani tusubiri siku ya kuapishwa kwake” “Lakini hili lazima lifanyike kabla ya yeye kuapishwa , kwani kama atapishwa kuwa Raisi hata tumuue haitokuwa na maana kwani mtu atakae mrithi atakuwa ni makamu wake kikatiba, hivyo tutakuwa tumefeli”Aliongea raisi .

“Umoja ulikuwa na tahadhari na kila kilichokuwa kikiendelea nchini , kwani umoja ulitambua hali ya kushinda kwenye boksi la kura ilikuwa ni nusu kwa nusu , hivyo tulichukuwa tahadhari mapema”Aliongea Kent

“Tahadhari gani hizo wakubwa wamezichukua?”

“Mgombea mwenza wa Jembe ni mfuasi wetu “.Aliongea Kent na kuwafanya watu waliokuwa ndani ya chumba hiko kupigwa na mshangao .

“Kwa muda gani alikuwa moja ya wanachama wa U-97?”

“Miaka kumi “Alijibu Kent na kuwafanya kila mtu hapo ndani ashangae .

“Hivyo misheni yetu ni kumuua Jembe , jembe akishaondoka duniani basi naamini hakuna mtu hata mmoja hapa ndani atapaswa kuwa na wasiwasi , kwani sisi wote ni wanachama na wanachama tunalindana kimaslahi “Aliongea Kent na kuwafanya kila mtu hapo ndani apumue . “Basi mpaka hapo naona jambo rahisi la kutimiza azima yetu ni siku ambayo Jembe atakuwa ashaapishwa litakuwa jambo jepesi sana kukamilisha misheni hio , kwani wanausalama wetu ndio watakuwa wanamlinda “Aliongea Kinga na kila mtu aliunga mkono hoja yake .

Walikubaliana siku ya kuapishwa kwa Jembe kabla ya kufika Ikulu basi awe ni mfu , lakini licha ya kupanga jambo hilo walitafakari nini ataenda kutimiza azma hio ya kumuua Raisi mteule Jembe, na wanajumuia hao waliokuwa na mipango yao inayokiuka katiba ya Jamhuri walimgeukia tena Kent kuona ni mtu gani anaweza kumuua raisi mteule Jembe.

“Mtu wa kukamilisha zoezi hilo tayari yupo “Aliongea bwana Kent na kisha alitoa simu yake na kumpatia Kinga na kisha alianza kusoma taarifa ya mtu ambae ndie atakaekwenda kukamilisha jambo hilo .

Peskorov Sunik special agent kutoka kitengo cha walenga shabaha kutoka nchini Ukraine ndie mtu ambae alitakiwa kukamilisha jambo hilo .

Kinga aliridhika na sifa za bwana Peskorov na kuwaangalia wenzake wote hapo ndani , na kuwaashiria kuwa jambo hilo ni jema likafanywa na bwana Peskorov .

“Mnachotakiwa ni kuhakikisha siku ya uapisho kila kitu kinakuwa chini ya TISS , kwanzia ukaguzi wa usalama na kila kitu , ili kumuwezesha bwana Peskorov kufanya kazi yake kiufanisi “Aliongea Kent na Mkuu wa majeshi na wengine wote walikubaliana .

SURA YA 02​

Swala la kumruhusu Peskorov kufanya mauaji ya Raisi mteule Jembe lilikuwa limefanikiwa kwa asilimia mia moja ,kwani alipatiwa chumba mahususi kabisa ndani ya jengo la Sokoine , kwa ajili ya kukamilisha mauaji hayo, huku waliokuwa wakiratibu shughuli nzima ya mauaji hayo ni wakuu kabisa wa usalama wa Taifa la Tanzania , yaani kuanzia kwa mkuu wa majeshi, mkuu wa usalama wa Taifa na viongozi wengine waandamizi wa maswala ya kiusalama wa Nchi.

Hata pale bwana Peskorov alipo omba ruhusa ya kuruhusu risasi baada ya kumuweka raisi Jembe kwenye shabaha , alietoa ruhusa hio alikuwa ni mkuu wa majeshi akiwakilishwa na msaidizi wake , kwani yeye kwa wakati huo alikuwa uwanjani kwa ajili ya kuhakikisha shughuli za uapisho zikienda vyema kabisa .

Lakini wakati mpango huo ukiendelea upande mwingine alionekana mwanadada mrembo sana akiwa anapita mbele kabisa ya jengo la mtaa wa Nyerere square , Mwanadada huyu aliekuwa amevalia suti yake nyeusi , alionekana kutokuwa na wasiwasi kabisa , hata pale alipokuwa akikaribia kutoka kabisa nje ya barabara ya mwendo kasi , hakuonyesha ishara yoyote ya wasiwasi , mwanadada huyu alitembea kwa haraka kabisa mpaka kufika ndani ya jengo la Sokoine House na baada ya kufika katika lango la kuingilia , alisimamishwa na wanaume wawili ambao walikuwa wamevalia kiraia , baada ya mwanadada huyu kusimamishwa , alijjikuta akigeuza shingo yake kama mtu ambae alikuwa akikagua uwepo wa watu ndani ya eneo hilo , na ile baada ya kuridhishwa kwa kuona kwamba eneo hilo hakukuwa na watu wengi , aliwaangalia wale mabwana na kisha alitoa kitambulisho na kuwakabidhi , na kisha aliruhusiwa kuingia .

Baada ya kuingia ndani ya Lift alijigusa eneo la shingoni kama mtu anaejifinya na kisha alitamka maneno kadhaa ambayo hayakusikika , na wakati huo ndipo lift ile ilifunguka , lakini ni kama alikuwa anasubiriwa kwani ile lift inafunguka wanaume wawili waliovalia mavazi ya kiraia walionekana kusimama katika korido iliokuwa ikitenganisha nyumba ya namba 77 na 79 watu hawa ni kama walikuwa wakimsubiria katika eneo hilo , kwani kitendo cha yeye kutokea tu walimnyooshea bastora .

“Nyoosha mikono yako juu ,ukileta ubishi hii itakuhusu “Aliongea mwanaume huuyo mmoja kati ya wale wawili kwa sauti nzito kabisa ambayo haikuwa na mzaha , lakini licha ya hayo mwanadada yule mrembo hakuonesha hata sura ya wasiwasi Zaidi ya kufanya kile alichokuwa ameambiwa , lakini wakati wote huo alionekana kupanga yake kichwani , kwani alimwangalia yule mwanaume wa pili yake ambaye alionekana kuwa bize kumkagua na jambo hilo lilimfanya kufurahia moyoni.

Ilikuwa ni kitendo cha kushitukiza tu cha mwanadada huyu kupiga bastora ya mwanume aliekuwa amemlenga na kwenda pembeni , na hii ni baada ya mwanaume huyu kumwangalia mwenzake wakati wa kumsachi na hilo ndilo lilikuwa kosa kubwa sana kwake , kwani mwadada huyu kwa ustadi wa hali ya juu kabisa alitumia nafasi hio na kisha aliipangua ile bastora na kudondokea mbali , lakini hakuishia hapo tu kwani alikuwa tayari ashaachia pigo lililomyumbisha mwanaume yule aliekuwa akimkagua na kumtegua taya , lakini kwa wakati mmoja akijiandaa kupambana na mwanume ambaye alikuwa amepiga kerebu na bastora kwenda pembeni .

Jambo lililomfurahisha mwanadada huyu ni pale alipoona adui yake hakuwa na mafunzo ya kimapigano kama alivyokuwa ametegemea na aligundua adui yake siraha yake kubwa ilikuwa ni ile bastora kwani baada ya kudondoka pembeni aliikimbilia pasipo kuchukua tahadhari na hilo ndilo lilimfanya mwanadada huyu ampige teke la shingo na kumzimisha kabisa na baada ya kuona zoezi lake lilimalizika alimgeukia yule mwingine ambae alikuwa akihaha na kisha na yeye alimpiga shingoni na kuzima huku akiacha mdomo wazi kwani alikuuwa ameteguliwa taya lake.

Kitendo cha kufungua mlango wa nyumba na sabini na nane ndipo alipoweza kumshuhudia mwanume wa kizungu akiwa amelenga shabaha kuelekea barabarani , lakini ni kama alichelewa kwani ile anamfikia tayari mwanaume yule alikuwa alisharuhusu risasi kutoka katika bunduki lake hilo refu la kudungulia .

“Mhalifu yuko chini” Alitamka mwanadada huyu kwa sauti ya kikamavu .

“ Vizuri sana ajenti Linda , hakikisha unatoweka kwenye eneo kabla ya wanausalama kufika hapo “

“Copied” Umeeleweka “

Mwanadada yule mara baada ya kumaliza kazi yake aliacha alama ya utambulisho katika paji la uso la bwana Peskorov na kisha akatoweka ndani ya eneo hilo huku mdunguaji akiwa hajitambui .

Huku upande wa nje baada ya bwana Peskorov kuachia Risasi ile moja kwa moja ilimpiga Raisi Jembe kifuani na akadodoka chini , huku taharuki ndani ya eneo hilo ikizuka , wanausalama waliokuwa wakitoa ulinzi walijikuta wakianza kuimarisha ulinzi wa eneo hilo huku wengine wakitawanyika kufuatia upande ambao waliamini ndiko Risasi ilitokea .

Dakika chache gari ilioonekana kumbeba mheshimiwa ilitoka ndani ya eneo hilo kwa haraka sana ikielekea upande wa hospitali ya Muhimbili .

Hakuna alieweza kuamini jambo kama hilo lingeweza kutokea , sio wananchi sio wanausalama waliokuwa wakitoa ulinzi.

Dakika chache mbele baada ya Raisi Jembe kuwahishwa hospitalini , hatimae bwana peskorov alitolewa kwenye jengo hilo la Sokoine na wakati huo akiwa anajitambua , lakini akiwa chini ya ulinzi wa wanausalama wa Taifa.

Vyombo mbalimbali vilianza kutangaza habari ya raisi Jembe kupigwa risasi akiwa njiani kuelekea ikulu mara baada ya kuapishwa , Jambo hilo lilikuwa ni jambo ambalo halijawahi kutegemewa kutokea ndani ya Taifa la Tanzania , kila mwanahabari aliongea lake , huku sintofahamu ikiendelea kuibuka juu ya hali ya mheshimiwa.

****

BAADA YA MASAA MAWILI

Baada ya masaa mawili ya kutokea kwa tukio la kushitusha sana ndani ya Taifa la Tanzania katika lango la kuingilia ndani ya hospitali ya taifa ya Muhimbili zilionekana gari nne aina ya V8 zikiingia hospitalini hapo na kwenda kwenye maegesho ya muda mfupi pembeni kabisa ya jingo la magonjwa ya moyo .

Baada ya gari hizi kusimama walionekana watu watatu wakiwa wameingia ndani ya hospitali hio , mtu wa kwanza kabisa kuonekana alikuwa ni mkuu wa majeshi bwana Nduli Semongo , mtu wa pili alikuwa ni raisi mstaafu alieachia madaraka masaa mawili yaliopita bwana Mathayo Kilubwa , mtu wa tatu alikuwa ni Nassoro Kinga huyu akiuwa ni mkuu wa usalama wa

Taifa .

Mara baada ya watu hawa kwa jumla yao waliongozana na wanausalama wengine na kuelekea ofisi za mganga mkuu wa Hospitali hio na mara baada ya kukaribishwa na mganga mkuu afahamikae kwa jina la Magreth Singano , walienda moja kwa moja katika kutaka kujua hali aliokuwa nayo mheshimiwa Jembe , lakini jibu lililotoka kwa mwanamama huyu mwenye umri usiopungua miaka arobaini liliwaacha hoi na katika tafakuri nzito.

“Raisi jembe licha ya mimi kusikia Taaifa zake , sikuweza kumpkea hospitali hii mpaka wakati huu “

“Unamaanisha Raisi Jembe hakueletwa hapa”

“Ndio muheshimiwa , mimi ndio mganga mkuu hapa na taarifa ya mgonjwa mwenye mamlaka makubwa kama hayo akifika hapa lazima nijulishwe kuandaa utaratibu wa kiulinzi na matibabu “Aliongea mwanamama huyu na kuwafanya wazee hawa ambao kila mmoja alioneesha umri kwenda , walionekana kusawajika nyuso zao mara baada ya jibu hilo , kila mtu alijiuliza swali linalofanana na mwenzake .

“Kama Jembe hakuletwa hapa , kapelekwa hospitali gani ?“ Hilo ndio swali la kwanza lililoibuka katika vichwa vya watu hawa , kwani ujio wao ndani ya hospitali hio ilikuwa ni kuja kuthibitisha kifo cha Jembe tu , ili wakitangaze rasmi , lakini kitendo cha kufika mahali hapo na kukuta taarifa ambazo zilikuwa nje ya mategemeo yao walishangaa na kupatwa na mshituko kwa wakati mmoja.

Waliamua kuondoka mara baada ya kupata taarifa hizo ,huku wakimwamrisha mganga huyo kutotoa kauli yoyote kuhusiana na kile kinacho endelea juu ya raisi mteule Jembe.

Taarifa ziliwafikiwa wakuu wa nchi ambao ndio waliandaa na kuidhinisha mpango mzima wa mauaji ya Jembe ,taairfa hizo ziliambatana na kikao cha dharula na hii ni baada ya msako kwa kila hospitali ya kujua mahali ambapo raisi mteule alikuwa akipatiwa matibabu au maiti yake ilipokuwepo , mpaka masaa mawili kupita ya msako huo hakukuwa na majawabu yaliokatika uhakika juu ya maswali mawili :

Swali la kwanza kwa wapangaji hawa wa tukio lilikuwa ni ‘Maiti ya jembe iko wapi’ na swali la pili ‘Ni nani alifanikisha kuificha maiti ya Jembe’.

Walikuwa wanayo kila sababu ya kujiuliza maswali hayo kwani waliamiani mpango wa ulikuwa umefanikiwa kwa asilimia mia moja , na jambo lililowafanya waamini hivyo ni kutokana na sehemu ambayo Risasi ilioruhusiwa na bwana Peskorov ilipompata raisi , kwani kwa kutumia mtaalamu wao wa ‘Anatomy’ Professa Shukuru Omari waliweza kujua kwamba risasi ile ililenga katika eneo la moyo na kwa mantiki hio ni kwamba asilimia za raisi Jembe kupona risasi hio ni asilimia moja tu .

Walifanya tafiti zote za kuhakikisha Risasi ile ilimpata Jembe , mpaka kupima vinasaba vya damu iliomwagika katika eneo alilodondokea Raisi jembe na vikathibitisha damu hio kuwa yake , kupitita CCTV kamera waliweza pia kuona Risasi hio ilimpata Raisi Jembe hivyo uhakika wao wa kwamba Raisi Jembe kusalimiana na Kuzimu ilikuwa ni asilimia tisini na tisa .

“Jamani mpaka sasa hatujui Maiti ya Raisi mteule Jembe iko wapi.Na wanausalama waliohusika katika kumpeleka Raisi jembe hospitalini pia hawaonekani walipo , jambo ambalo linatuacha katika maswali “ Aliongea Mheshimiwa Raisi Mstaafu bwana Mathayo Kilubwa.

“Nadhani kwa taairfa tulizonazo mpaka sasa zintupa maswali mawili ambayo yanawakilisha asiliama za ushindi kwa kile tulichopanga“Aliongea Nassoro .

“Naunga mkono hoja mpaka sasa Tuna asilimia moja tu ya kusema Raisi jembo yupo hai , nadhani maswali yetu yajikite kutafuta mwili wa Jembe ili akaiage ikulu kabla ya kwenda kusalimiana na kaburi “Aliongea Mkuu wa majeshi bwana Nduli .

“Ninaunga mkono hoja ya kila lililoongelewa katika kikao hichi , lakini bado swala la upotevu wa mwili wa Jembe ni swala ambalo tunatakiwa kulifikiria kwa kina na kujua ni wapi mwili wake ulipo na ni nani walihusika katika kuuchukua mwili hio , na ni kwa madhumuni gani“ Aliongea bwana |Kent na kufanya wenzake wote waliokuwepo hapo ndani kuunga mkono hoja.

“Lakini mpaka sasa ni Zaidi ya masaa manne hatujapata kujua ni wapi Raisi jembe alipo na wananchi wanataka kufahamu raisi wao alipo“.

“Mheshimiwa makamu nadhani kauli yako uirekebishe kidogo ni vizuri ukisema ni wapi maiti ya jembe Ipo wapi kuliko kusema ni wapi Jembe alipo“Aliongea Raisi akimrekebisha makamu wake ambaye pia alikuwa yupo ndani ya mpango huo , makamu huyu alikuwa akifahamika kwa jina la Anandumi Kiwia .

Masaa yalizidi kusonga , wanausalama waliokuwa wamepewa jukumu la kufatilia ni wapi maiti ya jembe ilipo mapaka wakati huo hawajapata mwanga, wananchi nao walitaka kujua ni nini kinaendelea juu ya raisi wao mpendwa Jembe , waandishi nao walikuwa na maswali ambayo hayakuwa yamepata majibu mpaka kwa wakati hio,kila taasisi ya habari ilitaka kujua na kuripoti ni hali gani aliokuwa nayo Jembe, walichoweza kujua ni taarifa za kwamba raisi mteule huyo alikuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya Muhimbili , jambo ambalo liliwafanya wananchi wengi waliokuwa na hasira kali juu ya kile kilichomtokea raisi wao kufurika katika hospitali hio huku kila mmoja akiwa na bango lake , wengine walikuwa wakimuombea raisi hiyo aweze kupona , wengine walikuwa wakihitaji muhusika wa shambulio hilo , hakukuwa na gari iliokuwa ikiingia wala kutoka ndani ya hospitali , hakuna kiongozi wa hospitali wala wa taifa aliejitokeza kuongea na waandishi , jambo ambalo liliibua taharuki ndani ya Taifa la Tanzania na nje ya Mipaka yake.

Upande wa jengo la umoja wa usalama wa Taifa viongozi wa juu wa taifa walionekana wakiwa katika sehemu zao kwa masaa kadhaa huku wakijadiliana juu ya maamuzi ya kuchukua , jambo kubwa liliowafanya kubaki hapo ni kutaka kupata ripoti ya ufatiliaji wa wapi alipokwepo Raisi jembe , baada ya kama nusu saa ya kusubiri hatimae taarifa ya kipelelezi iliowakilishwa na jasusi wa kimataifa bwana Bakari Nyuu au Mister white kama walivyojuwa wakipenda kumuita akiwa kazini , ripoti hio ilisomwa .

Ripoti hio ilikuwa ikieleza tukio zima mara baada ya mheshimiwa Jumbe kutolewa eneo la tukio na gari la wangonjwa aina ya Landcruiser yenye namba za usajili THB 1011 gari ilnayomilikiwa na hospitali ya Muhimbili , Ripoti iliendelea na kusema gari hio ilionekana ikiptia baadhi ya maeneo , ambayo kamera ziliweza kuinasa , na katika ufuatiliaji hio waliweza kugundua kwamba gari hio iliingia ndani ya hospitali ya Muhimbili ikiwa na mgonjwa Mahututi aliekuwa akifahamika kwa jina la Semeni yahaya akiwa ametolewa hospitali ya Amana , akaendelea na kusoma kwa mpangilio wa ufatiliaji wa gari hio waliweza kukisia huenda kulikuwa na gari aina hio hio lenye namba za usajili hizo hizo ambazo ndio ziliweza kumbeba raisi Jembe .

Taairfa hio ilionekana kuwachosha tu waheshimiwa hao , kwani haikuwa na mwanga wowote huo hivyo mpaka kwa wakti huo waliona jambo la busara ni kufanya maamuzi .

Na maamuzi walioyaona yanafaa ni kutangaza kifo cha Raisi jembe na kuandaa utaratiubu wa kumuapisha makamu wa raisi wa jembe yaani mheshimiwa Madiru Seba kuwa Raisi wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,lakini licha ya kufanya maamuzi hayo walipanga kuchukua tahadhari zote juu ya asilimia moja ambayo walikuwa wakiamini kwamba huenda mheshimiwa Jembe angekuwa hai , hivyo mpango wa kiusalama ulikuwa ni kuhakikisha siku ya kumuapisha makamu wa Raisi bwana Madiru kuwa Raisi , walidhamiria kuhakikisha hakuna kitu chochote cha kuingilia zoezi hilo hata kama ingekuwa mzimu wa Jembe walidhamiria kuuzuia kutokuharibu uapisho huo .

Hivyo Muafaka ulikuwa ushaamuliwa na vyombo vya habari vilikuwa vishapewa taarifa ya kufika ndani ya ukumbi wa serikali kwa ajili ya kujua kile kilichokuwa kikiendelea . ambapo mkuu wamajeshi akiambatana na makamu wa wa Raisi ndio watu ambao walikusudiwa kutangaza .

Wakati watu hao wanajiandaa kwenda kutangaza kifo cha raisi mteule Jembe , wengine walibaki wakiendelea kujadiliana maswala mbali mbali ya kiuongozi katika taifa hilo huku kubwa Zaidi likiwa ni juu ya kuimarisha nguvu ya Umoja namba tisini na saba ndani ya Taifa la Tanzania .

Baada ya masaa mawili kupita , ndani ya ukumbi wa kitaifa unaomilikuwa na Serikali walionekana waandishi wengi wakiwa wamefurika ndani ya eneo hilo wakitaka kujua kile kinachoendelea juu ya sintofahamu juu ya shambulio la raisi mteule Jembe .

Havikuwa vyombo vya habari vya ndani ya nchi tu bali kulikuwa na vyombo vikubw Duniani ambvyo vyenyewe vilikuwa msitari wa mbele kutaka kuripoti kile kinacho endelea ndani ya Taifa la Tanzania , wananchi nao hawakua mbali n a Runinga zao ,kwani walikuwa wakifahamu fika mkutano wa waandishi wa habari huo unaokwenda kufanyika muda huo

Makamu wa Raisi , akiambatana na wakuu wa chama , pamojana mkuu wamajeshi , walikuwa mbele ya maiki zilizokuwa zimepangiliwa kwa ustadi wa hali ya juu ili kunasa sauti .

Makamu wa raisi alianza kujitambulisha pia na kutoa pole kwa watanzania kwa hali inayo endelea nchini huku akitoa wito kwa watanzania kuwa watulivyo kwa kipindi hicho …. Wananchi waliokuwa wakifatilia matangazo hayo yaliokuwa yakirushwa moja kwa moja ni kama walimuona makamu huyo kuwachelewesha kwani walichokuwa wakitaka kwa wakati hio ni kujua jibu moja katika mawili yaliokuwa yakiwasumbua yaani raisi wao kuwa hai ama kafariki .

“Nasikitika kutangaza ki…..”Wakati akikaribia kutangaza alijikuta akishituliwa na mguso na kusita kutangaza na kisha akageuka nyuma na kukutanisha sura ya mkuu wa majeshi ambae ndie aliekuwa anamwangalia , jambo ambalo pia liliwashangaza waandishi wa habari pamoja na wote waliokuwa wakifatiliwa matangazo hayo .

Baada ya kugeuka nyumba mkuu wa majeshi alimkabidhi karatasi nyingine na kuchukua ile aliokuwa ameshikilia makamu wa raisi na kisha alimwambia anapaswa kutangaza kilicho andikwa humo . Kitendo kile kiliwachanganya sana waandihi na watu wengine waliokuwa wakishudia tukio hilo .

Baada ya makamu wa raisi kupewa karatasi ile alijikuta akipitia haraka haraka na kujikuta macho yakimtoka , lakini alijitahidi kuficha mshituko wake .

“Nasikitika kutangaza hali ya kiafya ya mheshimiwa Jembe sio nzuri sana na mpaka wasaa huu bado anaendelea na matibabu , kutokana na hali ya kiusalama nasita kutangaza hospitali ambayo anapatiwa matibabu kwani tukio la leo linaonekana sio la kawaida , na wahusika wote ambao wamehusika na shambulio hilo tunaendelea kufanya uchunguzi na tunawahakikishia wananchi watu waliohusika watapatikana na watafikishwa mbele ya sheria ,.hivyo wananchi tunaomba muwe na watulivu na tuzidi kumuombea raisi Jembe kupona haraka ili kuendelea na majukumu yake ya kuliongoza Taifa ”Yalikuwa ni maneno machache sana yaliokuwa kwenye karatasi hio tofauti na ile ya mwanzo ambayo ilionekana kuwa Zaidi ya kurasa mbili..

SURA YA 03​

“Mpaka kufikia hatua hii ni dhahiri Damiani ushafanikiwa kumpata mwanangu na pia umefanikiwa kupata kidani , lakini pia umefanikwa kunisaidia kulipiza kisasi kwa walioimaliza familia yangu , lakini pia kuangalia vidio hii inamaanisha Bendera kafanikiwa kunizuia kutimiza malengo yangu hivyo misheni naweza kusema kwamba imefeli .

Nina sikitika kukuambia kwamba mimi ndio mtu niliehusika kumuua mama yako Damiani na si mtu mwingine , na yote ililikuwa kwenye mpango wangu ambao nimeupa jina la mpango x .

mmi nipo hai ni mzima wa afya na sikufa kama dunia inavyo fahamu pamoja na wewe pia , mtu aliekufa siku ya tukio sio mimi bruno lamberk bali ni clone yangu .

Mimi bruno lamberk halisi sijawahi kuonana na wewe ana kwa ana zaidi ya kukupa maagizo ya kila hatua unayopita kwa msaada wa Nara .

Hivyo kutokana na kifo cha mama yako ambae mhusika mkuu ni mimi nakuomba msamaha , lakini pia natengua kauli yangu ya kukumilikisha mali zangu zote kwanzia sasa na mmiliki halali atakuwa ni mtoto wangu .

Mwisho mama yako hakufa bure ila kafa kwa ajli ya watanzania wote hivyo ahadI niliowekeana na bendera ni kukuambia siri ya MPANGO ZERO , na hii ni kama zawadi kwa Bendera baada ya kunishinda na kuzuia mpango wangu wa kuwaangamiza maadui tisini katika karatasi niliokupatia .

MPANGO ZERO ni mpango ambao unahistoria ndefu hivyo kuujua kwa undani mpango huu nenda kasome kitabu cha ‘BOOK OF ALL NAMES ‘.”

Huwa kila ninapoangalia hii video Napata uchungu mwingi , nashindwa hata kuelezea kile ninchojiskia nikiangalia video hii , kwani uchungu ninaoupata huwa ni mkali sana , na unaweza ukashangaa kwanini napenda kuangalia video hii mara kwa mara japo inanifanya kuwa na uchungu mwingi sana , jibu ni kwamba huwa nafanya hivi makusudi kabisa , maumivu ambayo niliyapata siku ya mama yangu kupoteza maisha na siku ambayo mwanamke ambae nilikuwa nimetokea kumpenda kufa mbele yangu ni jambo ambalo mtu aliezoea kuliona hili neno ‘maumivu’ pasipo kupata udhoefu wa maana halisi ya neno lenyewe hawezi kuelewa kile ninachomaanisha na naangalia video hii mara kwamara ili kutozisahau siku ambayo Bruno alinisababishia maumivu katika maisha yangu

Bruno Lamberk ni mtu ambae nilikuwa nikimfikiria usiku na mchana, ni Zaidi ya miaka kumi sasa sijawahi kulisahau jina hili , ni adui yangu namba moja duniani ambae nilikuwa nikiamini siku ambayo nitamtia mikononi mwangu sijui hata ni kipi nitakifanya ili kuridhika juu ya maumivu alionisababishia katika maisha yangu .

Katika miaka yangu yote kumi ya mafunzo ya kijasusi na kikomandoo jina moja ambalo lilikuwa likinifanya nipambane Zaidi ili kujiweka sawa ni juu ya huyu mtu anaefahakika kwa jina la Bruno Lamberk na umoja wake unaofahamika kwa jina la U-97.

Kila siku nilikuwa nikirudia rudia video hii mara kwa mara hii yote ni kutotaka kusahau hata mara moja uchungu niliokuwa nao moyoni , wanawake wangu wawili niliotokea kuwapenda ndani ya dunia hii kufa na msababishaji mkuu akiwa ni U-97 huku umoja huu ukiongozwa na Bruno , swala hili lilinifanya niweke kisasi ambacho niliamini kwa kukitimiza hiko ndani ya maisha yangu nitaweza kuishi huru japo si kama zamani .

Nipo nchini kwa miezi kadhaa tokea nitoke kwenye mafunzo yangu Cuba ambako nilikaa kwa miaka mitano nikisomea maswala ya kimapigano na kipelelezi baada ya kutokea nchini Urusi nikijiimarisha Zaidi katika maswala ya kimapigano , naweza kusema mpaka sasa mimi ni mtu hatari sana kutokea ndani ya taifa la Tanzania tokea kuanzishwa kwake , kwani uwezo wangu niliokuwa nao ni mkubwa sana na mimi ndio mwanajeshi pekee mabae nimepata mafunzo kwa

miaka mingi sana na kufanya operesheni nyingi sana za hatari nikiwa mafunzoni na kuzifanikisha kwa asilimia mia moja .

Jambo moja lililonirudisha nchini ni juu ya uchaguzi mkuu ndani ya taifa la Tanzania , nilidhamiria ndani ya uchaguzi huu raisi atakae ingia madarakani lazimia awe mwanachama katika kitengo chetu cha siri ambacho viongozi wengi wa kiserikali wanaamini kwamba walikikomesha ndani ya utawala wa raisi Mathayo Kilubwa lakini jambo ambalo walikuwa hawalifahamu ni kwamba kitengo hichi hakikutokomezwa nchini bali kilikuwa kikifanya kazi zake kwa kutokuonekana huku ma ajenti wengi wa kikundi hiki wakiwa mafunzoni wakiongozwa na mimi mwenyewe .

Kati ya wanafunzi tuliokuwa katika mafunzo nchini Urusi na Cuba tulikuwa jumla ya wanafunzi nane ambao tulikuwa chini ya kitengo chetu cha siri ambacho kilipata kuvumbuliwa na Raisi John Bendera na kukipa jina la Mzalendo .

Basi ni asubuhi ya leo nikiwa ndani ya barabara ya Bagamoyo nikiwa eneo la Mbezi beach nikitokea nyumbani kwangu Makongo Juu , foleni siku hii ilikuwa ni kubwa mno kiasi kwamba sisi wenye magari tulikaa barabarani kwa muda mrefu sana , licha ya foleni hio kubwa , kwangu haikunikera kabisa kwani niliweza kupata wasaa wa kuangalia video aliaoniachia Bwana Bruno Lamberk .

Siku hii ya leo kulikuwa na Shamra shamra nyingi sana kwani ilikuwa ni siku ambayo mheshimiwa Jembe raisi mteule alikuwa akiapishwa na ndio kitu ambacho kilisababisha foleni kubwa sana kwa siku hii , kwangu nilijikuta nikiwa na furaha sana na pia kujiona nimepiga hatua kubwa sana ya kuhakikisha mheshimiwa Jembe anashinda uchaguzi na hatimae kuapishwa , kwangu hio ilikuwa ni hatua ya kwanza katika mipango yangu zidi ya U-97 ,umoja ambao ulikuwa ukiongozwa na Bruno lakini pia umoja ambao ulimfanya raisi Bendera kuunda kitengo cha Mzalendo, kikundi ambacho lengo lake kuu ni kuutokomeza umoja huu ndani ya taifa laTanzania

Siku ya leo siku panga kwenda kushuhudia uapisho wa Raisi Jembe .licha ya Mzalendo na mimi nikiwa kama mkuu wa kitengo hichi kuhusika na kushinda kwake ,kwani kama isingekuwa sisi licha ya Jembe kuungwa mkono na wananchi wengi , lakini kwa serikali ya chama tawala asingefua dafu kwani kulikuwa na tabia ya wizi wa kura .

Nilikuwa nimepanga niende moja kwa moja mpaka kwenye kambi yetu ya siri ya Mzalendo kwa ajili ya kushugulikia misheni ambayo tulikuwa tukidhamiria kuifanya kwa siku hio , na muda huo ambao nilikuwa kwenye gari ni kwamba ajenti wa Mzalendo walikuwa kwenye majukumu yao kama kawaida.

Baada ya masaa mawili niliweza kufika ndani ya kiwanda changu cha maswala ya Tehama kilichokuwa maeneo ya Kurasini , mara baada ya kuingia zangu ofisini na kusalimiana na wafanya kazi ,moja kwamoja nilielekea ndani ya ofisi yangu , na mara baada ya kuingia ndani ya ofisi hii na kuweka mambo sawa , nilitoka na kuingia kwenye lift tena na kisha nilibonyeza vitufe kwa mfumo wa ‘commbination button’ na lift moja kwamoja ilinipeleka mpaka kwenye

‘basement’ Vyumba chini ya ardhi , ambako ndio sehemu chimbo letu la wanaMzalendo tilikuwa tukifanya kazi humo na kuandaa operesheni mbalimbali ambazo zinalenga moja kwa moja katika kuuuondoa U-97 nchini.

Baada tu ya kuingia ndani ya ‘basement’ hii ambayo ilikuwa na ulinzi wa hali ya juu sana , kiasi kwamba kwa mtu ambae sio muhusika wa kitengo hichi akijaribu kuingia kwenye kambi hii ni Dhahiri kabisa ataishia kwenye kizuizi namba moja , kwani hii sehemu licha ya teknolojia yake kuwa kubwa , lakini pia ilikuwa ikilindwa na mionzi mikali ambayo kama ikikunasa inabadilisha kabisa mfumo wako wa akili .

Basi baada ya kuingia ndani ya hii ‘basement’ mtu wa kwanza kuonana nae alikuwa ni Janeth , kwa wasiomjua huyu mwanadada kifupi ni kwamba ni moja ya watoto wa mzee Bendera warembo sana , yaani ana umbo flani hivi ukiliangalia lazima umeze mate , huyu bibie kuwaweka wazi tu ni kwamba huwaga najipigia tu na ninachofahamu ni kwamba ananipenda sana na anatamani siku moja tuyajenge maisha tukiwa pamoja , lakini kutokana na majukumu yetu ambayo tunayafanya , jambo hilo kwangu na kwake pia linaonekana gumu , Huyu bibie japo ya kuwa mrembo lakini pia ni moja ya wanawake wenye akili nyingi sana ndani ya taifa hili na kuthibitisha akili yake ni kwamba aliweza kupata PhD yake akiwa na umri wa miaka ishirini tu , Ni mtu ambae namkubali sana katika maswala ya teknolojia , na ndio mtu pekee ambae anafanya kitengo chetu kuwa ‘invicible’(kutokuonekana ).

“Babe!!!” Mara baada tu ya Janeth kunitegemea wakati nikiingia ndani ya kambi hio alinikimbilia na kunihug , kanapenda kujibebisha sana haka katoto yaani naweza kusema katika videmu vyangu ambavyo nimeweza kutembea navyo , hakuna anaemshinda Janeth kwa kuwa ‘Romantic’.

“Nataka kujua maendeleo ya operesheni”

“Mpaka sasa naweza kusema mipango yetu ipo kwa asilimia moja , kila ajenti yupo kwenye mkao kuendana na operesheni”

“Safi , inatakiwa kuhakikisha hakuna kosa linaloteokea kwani tukizembea kidogo tu tunaweza kumpoteza Raisi jembe “Niliongea nikiweka msisitizo , kwani mpaka wakati huo tulikuwa tuna taarifa zote za mpango ambao umeandaliwa juu ya kumuua raisi jembe kabla ya kuingia ikulu na taarifa hio tulikuwa tumeipata kutoka kwa moja ya wanamipango hio ambae ni shushu wetu .

Mpango wenyewe uko hivi : baada ya kutangazwa kwa raisi Jembe kuwa raisi tuliamini kwamba chama tawala kisingemruhusu kuchukua madaraka , kwani siasa ilikuwa imesambaa mpaka kwenye vyombo vya usalama wa nchi jambo ambalo lilikuwa likimuweka Jembe katika hali hatarishi Zaidi .

Hivyo baada ya Jembe kutangazwa kushinda, tulimpa maelekezo kwa njia ya simu kwa kwenda sehemu ambayo tulikuwa tumeandaa sisi , ambayo tulikuwa tukiamini ni sehemu salama ambayo mtu yoyote hawezi kuifikia , unaweza kudhani ni kwa namna gani Jembe aliweza kutumaini , ukweli ni kwamba kabla ya kuingia kwenye zoezi la kupiga kura tulimtaarifu raisi Jembe kwamba lazima atashinda na sisi ndio tutafanikisha hilo hivyo yeye ajiandae kwenda ikulu .

Na baada ya yeye kushinda alituamiani kwani hata yeye mwenyewe alikuwa akijua kuwa asingeweza kuwashinda chama tawala katika sanduku la kura , labda tu kungekuwa na Tume huru jambo ambalo hata jembe mwenyewe katika maisha yake ya siasa alikuwa akilipigia Debe kila siku lakini halikuweza kusikilizwa na watu wa chama tawala .hivyo alikuwa ni kama anachangamsha uchaguzi tu kwani alikuwa anaamini yeye kushinda ilikuwa ni kwa asilimia ndogo sana .

Basi baada ya kuhakikisha Raisi mteule yupo sehemu salama mpaka siku ya uapisho wake , tuliendelea kufatilia mienendo ya watu kutoka chama tawala , kwani tuliamini kwa namna yoyote ile ni lazima wangepanga jambo ambalo lingepelekea raisi Jembe asiingie Ikulu na hapo ndipo kwa kutumia shushu wetu tulipoweza kupata taarifa kamili za mpango huo , tuliweza kumjua Peskorov kama moja ya wadunguaji hatari sana kuwahi kuwepo katika uso wa dunia kutumika katika mpango huo , na kwanzia siku ambayo bwana huyu wa kizungu anaingia nchini kila hatua aliokuwa akipiga , alikuwa akifatiliwa na Ajenti Linda moja ya wanachama wa kitengo cha Mzalendo na huyu Linda na yeye alikuwa ni moja ya wanafunzi ambao tulikuwa wote mafunzoni Nchini urusi kabla ya mimi kuelekea Cuba , na niseme tu huyu ajenti na yeye ni hatari Zaidi , kwani licha ya Urembo wake wa kikabila la Kirangi , lakini alikuwa ni mwepesi sana likija swala la mapigano na kwa sifa alizokuwa nazo Peskorov basi tuliona Linda anaweza kummudu vyema .

Kwakua mpango wote tulikuwa nao basi jambo hili tuliweza kulipangilia kwa akili sana , kwanza tulihakikisha kuwa na gari ya wagonjwa katika msafara wa raisi kuelekea ikulu na ndio maana mara baada ya raisi kupigwa risasi ya kifua na bwana Peskorov ambae nilimkubali sana kwa ulengaji wake , kwani sehemu ambayo alikuwa amekusudia kulenga ndio hapo hapo risasi ya mheshimiwa Jembe ilipotua.

Baada ya Risasi ile kumpiga mheshimiwa Jembe , wanausalama ambao walikuwa chini ya mpango wa Mzalendo ambao walikuwa wamejichanganya na kundi la wanausalma kutoka kitengo cha usalama wa Taifa , waliupakia mwili wa mheshimiwa katika Ambulance ,baada ya kufika mbele kidogo ya ukumbi wa aghakani mjini Posta mbele kidogo tuliweza kufanya mabadilishano ya kimagari , yaani gari ambalo lilikuwa likitoka Amana hospital lilikuwa likifanana na la kwetu ambalo tulikuwa tumelipandikiza na kuendeshwa na wanasalama wa kitengo chetu , hivyo gari ile ya kubebea wagonjwa iliokuwa ikitokea Amana iliendelea na safari ya kuelekea Muhimbili na gari ya kwetu ilisogea mpaka mkabala wa njia inayoingia mtaa wa Mindu na baada ya kufika hapo tulikuwa tunamawasiliano na watu wa Temple ya wachina na gari yetu ile iliingia hapo na baada tu ya kuingia hapo , raisi tulimtoa katika ile gari na kumuigiza katika V8 na kumleta kambini huku tukihakikisha hakuna namna yoyote ile tunaacha hatua nyuma, kwani mara baada ya kutoka kwenye hio Temple gari ile ilifanyiwa kazi na mafundi kubadilishwa rangi , na tulihakikisha kamera zote tunazipa taarifa tunazotaka sisi zionekane na wanausalama wa kitengo cha Taifa .

Naam mpango ukawa umekamilishwa na ajenti Elvice , ajenti Linda .Ajenti Karim , Ajent Patrick, ajenti Janeth , Ajent Nasra mrembo sana huyu ila ananikazia ila aataingia kwenye kumi na nane zangu , Ajenti Zakayo Na mimi mwenyewe Damiani Rabani mkuu wa kitengo cha Mzalendo Sisi wote ni special ajenti na kupambana na sisi inahitaji akili ,ujuzi na maarifa , tupo ndani ya Taifa hili kwa ajili ya kupambana na U-97.

*****

Mheshimiwa Jembe alijikuta akishituka na kukutana na nyuso ambazo zilikuwa zikimuangalia , zilikuwa ni nyuso za watu kumi jumla waliokuwa wakimwangalia wakiwa wamevalia mavazi ya aina moja , yaani rangi nyeupe , kitendo kilicho mfanya ajifikiche macho , kwani aliamini wakati huo ni lazima watu waliokuwa mbele yake walikuwa ni malaika , lakini akili yake iligoma kukubali kuwa watu hao ni malaika , kwani alikuwa ni moja ya watu waliopata kusikia habari mbali mbali zilizokuwa zikihusiana na malaika , kuwa wengi wao ni wazuri na hawana makunyanzi na sio weusi , lakini kwake kitendo cha kuona baadhi ya watu hao kuwa na sura mbaya baadhi yao na ndevu zisizokuwa katika mpangilio , aliamini bado hakufa , aliamini bado huenda hayo ndio mavazi ya watu wa Ikulu wanayovaa wakati wakiwa wanamhudumia Raisi , na hapo yupo kwenye chumba maalumu ambacho anasubiriwa aamke ili ahudumiwe .

“Karibu duniani mheshimiwa “Aliongea Damiani na kumfanya Jembe anyanyuke , lakini wakati anajilazimisha kunyanyuka alijihisi maumivu kwenye kifua na hapo ndipo alipokumbuka kwamba alipigwa Risasi kwani akili zake mpaka wakati huo hazikuwa sawa bado , lakini jambo la kushangaza alijihisi maumivu ya kawaida sana jambo ambalo lilikuwa mshangao kwake , kwani katika maisha yake alipata kuambia kwamba risasi ikikupata lazima itoboe nyama , lakini kwake hakuwa hata na tundu la risasi Zaidi ya maumivu .

“Hapa ni wapi ?”

“Upo ndani ya kambi ya Mzalendo “

“Kambi ya Mzalendo!, Nchi gani ?”

“Upo ndani ya Nchi yako Muheshimiwa , chini ya Kambi ya kitengo cha siri cha Mzalendo na sisi unaotuona hapa ndio ajenti kumi wa kitengo hichi “Aliongea Damiani kwa Urefu jambo ambalo lilimfanya Jembe ashangae , kwani hakuwahi kusikia juu ya kitengo cha Siri , lakini alivyokumbuka kwamba yeye ni raisi , na huo ni mwanzo wa kujua siri za nchi aliona jambo hilo ni la kawaida na kwa muda huo anachohitaji yeye ni maelezo ya kina .

“Sisi ndio tuliokupigia simu na kukueleza juu ya safari yako kuelekea Ikulu, sisi ndio tuliokupigia simu na kukupa ulinzi mpaka siku ya kuapishwa kwako , sisi ndio tuliokuokoa katika kifo”Maneno hayo ndio yaliomfanya sasa mheshimiwa Jembe kujua anazungumza na watu gani, wale watu ambao walikuwa wakimuumiza akili yake sasa wapo mbele yake , hakika alistaajabu , hakuweza kuamini watu hao kumi ndio walioweza kuudhibiti uchaguzi na kushinda kihalali .

“Nahitaji kuwajua Zaidi , na tukio zima la mimi kupigwa risasi “Aliongea mheshimiwa Jembe na kuwafanya wanamzalendo kutabasamu .

Mheshimiwa mara baada ya kuomba kuwajua Zaidi , wanamzalendo , aliombwa kunyanyuka na kuendelea chumba ambacho ndio shughuli zote za kitengo hichi cha siri zilikuwa zikifanyika , alijikuta akishangaa mno , kwani kwa kila chumba alichokuwa akipitishwa ndani ya ‘basement’ hii alijikuta akihusudu muundo na mpangilio wa eneo hilo .

“Sijawahi kupata kuingia sehemu kama hii kwenye maisha yangu” aliongea mheshimiwa Jembe mara baada ya kufikiwa eneo maalumu ambalo lilikjuwa na mitambo mikubwa ya kisasa , huku tarakishi kubwa zilizokuwa zimefungwa zikionyesha eneo zima la jiji la Dar es salaam .

Damiani hakutaka kumueleza mheshimiwa Jembe kwa njia ya mdomo bali alivuta faili kweye tarakishi na kumruhusu mheshimiwa aanze kusoma , na mheshimiwa hakutaka kuchelewa alianza kusoma faili hilo , na kadri alivyokuwa akiendelea kusoma mwili ulikuwa ukimsisimka , alitumia madakika kadhaa kumaliza kusoma ripoti hio ya mzalendo mpaka kuimaliza , katika mambo yote aliosoma alielewa kasoro jambo moja tu ambalo kwake hakuliewa kabisa , na alihitaji ufumbuzi Zaidi .

“UMOJA NAMBA TISINI NA SABA nataka kujua Zaidi kuhusu huu umoja “ Aliongea na

Janeth hakukawia alimvutia faili linguine na kumpatia Mheshimiwa na , alianza kupitia tena na faili hilo , na hapa ndipo mwili ulipozidi kumsisimka , kwani kwa mambo alioyasoma alikiri kwamba kiti cha uraisi kilikuwa cha moto , hakuamini kama ndani ya taifa la Tanzania kulikuwa na Nguvu ambayo ilikuwa ikiliendesha Taifa kwa namna ya siri kabisa , huku viongozi wakiwa kama masanamui tu Pale Ikulu , lakini Zaidi ya yote alijikuta akimhusudu sana mheshimiwa John Bendera , alikiri kwamba huyo bwana alikuwa ni shujaa wa nchi.

“Ni hali ya kutisha kwelikweli , sikupata kujua kwamba taifa lipo kwenye mikono ya watu kama hawa”Aliongea mheshimiwa Jembe huku akijifuta jasho .

“Ni kweli uyasemayo mheshimiwa na nadhani mpaka sasa umepata kuelewa nini maana ya Mzalendo”

“Kwanza niwape pongezi kubwa sana , kwa jambo ambalo mnalifanya kwa taifa hili , hii ni historia ambayo mnaandika , ambayo itakumbukwa na vizazi vingi , ni ushujaa wa hali ya juu sana mnaoufanya , na nadhani itakuwa vyema kwa mimi kuwafahamu kwa kila mmoja , japo baadhi yenu nawafahamu , akiwepo Profesa hapa”Aliongea mheshimiwa huku akimwangalia ?Janeth na kumfanya atabasamu

Damiani aliwatambulisha ajenti wote wa Mzalendo , pamoja na kuelezea historia yake yote ya mambo ambayo amekumbana nayo mpaka kufikia wakati huo (Hakikisha umesoma U-97WARAKA WA RAISI ), aliamweleza mheshimiwa juu ya mambo yote ambayo yalikuwa yamefanywa na wanamzalendo kwanzia kuundwa kwake , mafanikio yote .

“Nataka kujua kabla ya yote imewezakana vipi mimi kupona ile risasi “

“Mheshimiwa suti uliovaa siku ile ilikuwa imeundwa kwa muundo wa Bullet proof kwa teknolojia ya hali ya juu ambayo kwa sasa watengenezaji wa suti hizo ni Z-Styllish wear inayomilikuwa na moja ya familia ya wanamzalendo”

“Inamaana kuna wanafamilia wengine ambao wapo chini ya mzalendo ?”

“Ndio mheshimiwa kuna wengi ambao wapo undercover”.

“Nimefanikiwa kusoma maelengo yenu ya kitengo hichi cha siri , lakini sijapata kujua ni kwa namna gani mtaweza kuondoa umoja huu ndani ya Taifa hili , kwani kwa kile ninacho ona ni kwamba umoja huu ni wenye nguvu sana Duniani”.

“Ni kweli kabisa mheshimiwa , umoja huu ni wenye Nguvu kubwa Duniania na kila siku unaendelea kujipanua katika Nyanja zote ,lakini sisi kama wazalendo tunaamini kwamba hakuna jambo ambalo halina udhaifu”

“Unamaanisha nini bwana Damiani?”

“Kila jambo ndani ya dunia hii lina udhaifu wake Mheshimiwa , na hicho ndio kitu ambacho kitengo hichi tunafanyia kazi , na swala hili tunampa pongezi sana mheshimiwa bendera kwani kabla ya kifo chake aliacha waraka”

“Unahusu nini huo waraka ?”

“Damiani hakutaka kuongea sana , alivuta kitabu kimoja kilichoandikwa na mwandishi nguli kabisa SinganoJr na kisha akamkabidhi , kitabu hicho juu kabisa kinasomeka kwa jina la

UMOJA NAMBA TISINI NA SABA –WARAKA WA RAISI KABLA YA KIFO.
 
SURA YA 04​

Kutokana na muda kuwa mdogo wa Muheshimiwa kukaa ndani ya kambi hio ya Mzalendo ,Damiani alifungua kulasa tatu za mwisho za kitabu cha U-97 waraka wa rasi kabla ya kifo na kumwambia mheshimiwa asome ,

“Nimesoma lakini nataka kuelewa Zaidi”Aliongea mheshimiwa na kumfanya Damiani atoe video ambayo ilikuwa imeachwa na Bruno lamberk na kisha waliangalia wotea hapo ndani , na wakati huo yote hayo yanaendelea , wanamzalendo wengine walikuwa kwenye majukumu mengine , ni Damiani na Janeth ndio walikuwa wapo na mheshimiwa wakijaribu kumuelewesha

“Mheshimiwa nadhani baada ya kusoma kitabu hicho utapata kuelewa kabisa kuhusu kile kinacho endelea hapa nchini Hususani uanzishwaji wa Mpango zero hapa nchini ambao mpaka sasa sisi hatujui mpango huu unahusiana na nini , kwani imekuwa siri kubwa ndani ya U-97” “Udhaifu ambao mpaka sasa tunaamini utaweza kutufanya tujue ni nini maana ya huu Mpango Zero ni kitabu kinachofahamika kwa jina la Book Of All Names(Kitabu cha majina yote)”.Aliongea Janeth .

“Kwa hio unamaanisha kwamba baada ya kupata hiki kitabu , tunaweza kujua nini kipo chini ya Mpango Zero , na kama jibu ni ndio je hiki kitabu kinapatikana wapi?”

“Ndio mheshimiwa , na sio kujua tu Mpango Zero bali baada ya kupata kitabu hichi tunaweza kupata mambo mengi yanayohusiana na umoja huu , mpaka sasa hatujajua hiki kitabu kipo wapi na kwanini kinaitwa kitabu chenye majina yote”.

“Sasa kama ni hivyo huoni kwamba huu umoja utakuwa na hiki kitabu , na kama wanacho na kina siri nyingi juu ya Umooja huu , je itawezakanaje kwa sisi kukipata kitabu hiki kwani kitakuwa kinalindwa sana kama lulu na umoja huu ?”

“Ni kweli mheshimiwa,uzungumzayo, lakini njia ya kuuondoa umoja huu ndani ya taifa hili ni kupata hiki kitabu na hakuna namna nyingine , na ni lazima sisi wanamzalendo tukipate kitabu hichi kwani mpaka sasa ni damu nyingi zilizomwagika kwa ajili ya sisi kuunda umoja huu ndani ya taifa hili , hivyo hakuna kuogopa juu ya upatikanaji wa kitabu hichi , tutakitafuta mahali popote pale na kwa gharama zozote zile ili damu zote zlizomwagika zisiende bure”

Aliongea Damiani kwa hisia kubwa na kumfanya Jembe kujua ni kwa namna gani kijana huyu alikuwa amedhamitria kupata kitabu hicho ,, lakini pia kwa jinsi ya muonekano na utayari wa

kiongozi huyu aliamini kuna mengi Zaidi ya kuyajua , lakini aliona ni wakati wa kutulia ili akapate wasaa mzuri wa kusoma kitabu cha U-97 WARAKA WA RAISI KABLA YA KIFO CHAKE .

“Mheshimiwa mpaka sasa kuna sababu kubwa sana ya sisi kukulinda mpaka kufikia hii leo , na naweza kusema kuingia kwako madarakani ni jambo ambalo sisi kama Mzalendo wa nchi hii tulitamani sana, najua yapo mengi sana ambayo umewaahidi wananchi katika kuyatimiza , lakini nasikitika kukwambia kwamba mambo hayo ulioyaahidi yanaweza kutokufanikiwa “ “Unamaanisha nini wakati mimi ndio raisi wa Nchi hii ?

“Mheshimiwa Nchi hii haijalishi nani anakaa pale ikulu , anaeongoza nchi hii ni U-97 na hao ndio wanakupa maelekezo kipi ufanye na kipi usifanye , kwahio wewe pale ikulu ni kama sanamu tu linaloitambulisha nchi kama inayo raisi na ni ya kidemokrasia na nchi huru , lakini mengi yanafanywana huu umoja”

Jembe alijikuta akikuna kichwa, kwa maneno mazito alioongea Damiani , alijaribu kutafakari japo hakuwa akiujua undani wa umoja huu , lakini aliamini ni umoja wenye nguvu kubwa sana .

“Huna haja ya kuwaza sana mheshimiwa . hio ndio hali halisi ya umoja huu ndani ya taifa letu , na kukuleta hapa ni kukufanya moja ya wanafamilia wa mzalendo , na tunataka kwa kinywa chako ule kiapo cha kuwa mwanaumoja na sisi tutakupa muongozo wa kipi ufanye ili hatimae kufanikiwa kuuondoa umoja huu ndani ya taifa hili “

“Niko tayari kula kiapo”Aliongea mheshimiwa na kuwafanya Damiani na Janeth kutabasamu

, kwani waliona jambo walilikuwa wamelipanga linakwenda kama wanavotaka , basi mheshimiwa alifata utaratibu wote wa kula kiapo na kuwa mwanachama wa Mzalendo.

Mambo yalikuwa yakiendeshwa kiharaka haraka kweli kwani waliamini kama kupotea kwa raisi wakipoteza muda mwingi basi ni dhahiri huenda watu wa chama tawala wakafanya maamuzi mengine .

Baada ya tararibu zote za mheshimiwa raisi kula kiapo hatimae taarifa iliingia katika mtandao wa kitengo cha Mzalendo ju ya yale ambayo yanaendelea katika vikao vinavyo endeshwa ndani ya kitengo cha usalama wa Taifa

“Mheshimiwa huna muda wa kupoteza , kuna mpango wa makamu wako kuapishwa kuwa raisi kurithi nafasi yako hivyo inapaswa kutokea hadharani “

“Lakini watu hawa sio waliopanga kuniua , huoni kwamba nikitoka hadharani wataniaua tena ?”

“Tumeandaa mpango wa wewe wa kutokuwa hasimu wa Umoja huu”Aliongea Janeth

“Mpango gani huo ?”

“Unapaswa kujiunga na Umoja Namba Tisini Na Saba”Aliongea Damiani na kumfanya mheshimiwa Jembe kutoa macho .

“Hapana siwezi kuisaliti nchi yangu na kujiunga na huu umoja , never Nitakuwa nimesaliti kiapo changu kwa wananchi wa taifa hili”

“Mheshimiwa jambo tunalotaka sisi ni kuhakikisha tunarahisisha mapambano yetu zidi ya umoja huu , na wewe kuingia ikulu ni njia pekee ya sisi kufanya kazi zetu kwa ufanisi , swala la wewe kujiunga na kikundi hiki ni swala pekee ambalo litakufanya kukalia kiti cha uraisi , hatukuambii ujiunge umoja huu kwa kuwa mwanachama , bali tunakuomba ujiunge na umoja huu kwa ajili ya kuingia ikulu , na sisi kuweza kupata nafasi ya kufanya kazi zetu , lakini pia kuweza kupata taarifa za ndani ya umoja huu kwa kila kitu ambacho kitakuwa kinafanyika , hivyo utakuwa ni kama kivuli tu ndani ya Umoja huu huku uhalisia utakuwa ni Mzalendo wa Nchi hii na baada ya mapambano yetu kuisha utakuwa shujaa utakae andikwa katika vitabu vya kihistoria vya nchi hii na kukumbukwa vizazi na vizazi” Aliongea Damiani na kumfanya mheshimiwa atikise kichwa kuonesha kwamba ameelewa na kile anachoongea bwana Damiani , mkuu wa kitengo cha Mzalendo .

Mheshimiwa raisi alipeana mkono na kila mwanachama wa kitengo hicho kuonesha kwamba kwanzia wakati huo wako pamoja , bega kwa bega katika kuhakikisha adui huyu alieingia ndani ya taifa hili anatokomezwa , walikuwa na kazi kubwa mbele yao , kwani kupambana na umoja huu ilikuwa ni kama kitencho cha taifa la Tanzania kupambana na taifa la Marekani , kwani nguvu iliokuwa ndani ya umoja huu haikuwa ndogo , lakini baya Zaidi ni kwamba umoja huu ulikuwa ukifanya kazi zake kwa namna ya siri sana jambo ambalo linakuwa gumu sana katika mapambano hayo .

Baada ya makubaliano kufanyika ya raisi jembe kuingia ikulu , mpango wa kuwasiliana na wawakilishi wa Umoja huu ndani ya taifa la Tanzania ulifanyika , huku usimamizi wa mawasiliano hayo ukiwa chini ya Mzalendo .

Kwakuwa kitengo hichi kilikuwa kina taarifa kwa kile kilichokuwa kinaendelea ndani ya ukumbi wa usalama wa taifa ndani ya eneo la Osterbay jijini Dar es salaam , haikuwa kazi kwao

Mheshimiwa raisi alitolewa ndani ya kambi hio ya mzalendo kwa njia salama Zaidi na kwenda kuhifadhiwa ndani ya moja ya nyumba ya siri ambayo ilikuwa ikimilikiwa na kitengo hichi , nyumba iliokuwa ikipatikana ndani ya eneo la Mbweni .

*****

Ni ndani ya lisaa limoja baada ya maamuzi kufanyika , maamuzi ambayo yalifanywa na watu hawa wanaojiita serikali ya taifa , yaani viongozi wa chama tawala ambao walikuwa hawataki kuruhusu uongozi wa bwana Jembe kushika hatamu ndani ya taifa la Tanzania .

Ndani ya kitengo cha mawasiliano cha umoja wa usalama wa taifa waliweza kupaata mawasiliano kutoka kwa watu ambao hawakuweza kuwafahamu , baada ya kupokea mawasiliano haya , walijikuta wakishangaa na hii ni mara baada ya mtu aliefanya mawasiliano hayo kujitambulisha kama raisi wa taifa la Tanzania yaani Mheshimiwa Abdukarimu Jembe .

Baada ya watu hawa kuweza kufahamu mtu waliekuwa wakiwasiliana nae , haraka mawasiliano yalifanyika kwenda kwenye chumba cha mikutano, na baada ya mawasiliano hayo kufanyika ndani ya chumba cha mikutano , Bwana Nassoro alitoa amri ya kuunganishwa kwa mawasiiano hayo na chumba hicho na hapo ndipo walipoweza kumuona bwana Jembe laivu kwani mawasiliano hayo yalikuwa ni kwa njia ya video .

Hakuna alieamiani kati ya watu waliokuwa hapo ndani , kila mmoja alishangaa ,inawezekanaje mfu akawa hai , kila mmoja alikuwa akiwaza swala la aina moja , yaani mfu kufufuka , hakika ilikuwa ni mshituko kwa mabwana hawa ambao walikuwa ni waroho wa madaraka , waliokuwa wakizidi kuizoofisha nchi kwa kuruhusu mambo ya ajabu kutawala ndani ya taifa hili.

Kilikuwa ni kikao cha kama nusu saa kati ya raisi mteule jembe na wazee hawa , Raisi jembe alitoa msimamo wake wa kujiunga na chama cha U-97 huku akiahidi kutoa ushirikiano wa kila namna kama moja ya mwanafamilia wa umoja huo , jambo ambalo kwa wakongwe hawa wa mambo na figisu walishindwa kuamini kabisa kwani ni kweli bwana huyu alikuwa akitaka kujiunga ndani ya umoja wao , kwani walikuwa wakimjua vyema Jembe kwa msimamo wake .

Baada ya kikao hiko kisicho rasmi kufanyika wazee hawa waliomba kujadili swala hili kwa undani wao kwa wao na hata pia kuwasiliana na makao makuu ya umoja huu kwa ajili ya kupelekea maombi ya bwana Jembe kujiunga na umoja .

“Jamani nadhani kila mtu amesikia msimamo wa bwana Jembe kutaka kujiunga na umoja huu , jambo ambalo linatuacha katika maswali na tafakuri nzito ya kuipima nia halisi ya bwana huyu “Aliongea bwana Mathayo Kilubwa .

“Ni kweli kabisa , lakini nadhani kabla ya kuendelea na kikao hiki kuna jambo la kwanza lazima kufanyika , kila mtu sasa anafahamu kwamba Jembe yupo hai , na mpaka sasa mkuu wa majeshi na makamu wanaelekea kwenye mkutano na waandishi wa habari , hili ndio jambo la kwanza linapaswa kufanyika “Aliongea Nassoro .

“Inabidi aghairishe mkutano huo “Alichangia IGP bwana Kocho

“Hapna haina haja ya kughairishwa kwa mkutano huo , inabidi mumuwahi na kumkabidhi ripoti mpya inayoelezea raisi yupo hai yupo kwenye matibabu hali yake sio nzuri , na kuwaasa watanzania juu ya kuwa watulivu na kumuombea Jembe “Aliongea Kent .

“Lakini mheshimiwa bado hatujafanya maamuzi ya aidha kumpokea bwana Jembe ama kutompokea”Aliongea makamu wa raisi msaafu .

“Hilo sio swala la kuhofia kwa sasa , itakuwa kioja kama tukitoa taarifa ya mheshimiwa kupoteza maisha halafu atoke hadharani aseme yupo hai “Aliongea bwana Kent na kila mmoja alionekana kuunga mkono kwa ile alicho kuwa akiongea .

Baada ya kukubaliana, taratibu za kuwahi kwenye ukumbi wa serikali , sehemu ambayo ndio mkutano wa waandishi wa habari ulikuwa ukifanyika na bahati nzuri ni kwamba hawakuchelewa kufika mahali hapo kwani ile bwana Madiru anataka kutakma kwamba raisi Jembe keshpoteza maisha ndipo mkuu wa maheshi alimbadilishia ripoti ile na kumwambia asome hio .

*****

Kila mwananchi ambae alikuwa akimkubali mheshimiwa Jembe , alikuwa na hali ya furaha mara baada ya kupata habari kwamba yupo hai , kila mmoja aliamini kwa kimya ambacho kilikuwa kimettawala kwa masaa kadhaa kilikuwa kikiashiria kwamba raisi huyo mteule alikuwa amepoteza maisha .

Lakini mara baada ya taarifa hio wananchi walifurahi huku wengi wao wakiingia katika maombi ya kumuombea raisi wao kupona na kuingia ikulu kwa ajili ya kuendelea kuliongoza taifa na kuleta maendeleo yale ambayo wananchi wengi wa kitanzania walikuwa wakitamani kuona , chini ya utawala mpya.

Baada ya wiki mbili kupita hatimae , raisi jembe kwa mara ya kwanza tokea apatwe na shamubilio hilo , aliweza kurejea ikulu . na kulihutubia taifa , lilikuwa ni jambo kubwa sana kwa wananchi wa taia la Tanzania , kwani wengi wao waliamini raisi wao huyo huenda akapoteza maisha , lakini kitendo cha raisi Jembe kurejea ikulu kilileta tumaini jipya kwa taifa .

Wananchi wengi wa taifa la Tanzania walikuwa na Imani kubwa sana juu ya Jembe , waliamini muda si mrefu watakuwa wanapata kile walichokuwa wakikisubiria kwa muda mrefu sana , maisha bora kwa kila mtanzania , hilo ndio jambo kubwa ambalo kwa kila mtanzania alikuwa akitamani kuliona ndani ya utawala wa raisi Jembe .

Hotuba ya mheshimiwa jembe iliwagusa wananchi wengi , kila mmoja alikuwa akitoa ya moyoni kwa namna ambavyo mheshimiwa huyo alipata kutoa hotuba hio , ilikuwa ni hituba ambayo ilikuwa imejaa ujasiri wa aina yake , kwani licha ya madhira ambayo yalimkumba raisi huyu , lakini kwa muonekano wake alionesha hakuwa na jambo la kuogopa kwa wakati huo , jambo ambalo liliwafurahisah sana wananchi wa taifa la Tanzania .

Mheshimiwa jembe alimalizia hotuba yake kwa kuvunja kamati zote kwanzia ya chakula mpaka ulinzi ikulu , huku akimteua mlinzi wake wa pembeni , ambae alikuwa ni moja ya ajenti kutoka kitengo cha Mzalendo .

Zikiwa zimepita siku kadhaa baaada ya mheshimiwa kulihutubia taifa , , siku ya kumi na moja ya uongozi wake , Mheshimiwa alipata kupokea barua kutoka Umoja namba tisini na saba , barua hio ilikuwa ikimtaka mheshimiwa kusafiri mpaka Nchini Marekani kwa ajili ya kula kiapo cha uanachama wa U- 97.

Raisi mwenyewe alishangazwa na uharaka wa jambo hilo kwani ni siku chache mno kwake kula kiapo kwa ajili ya kujiunga na umoja huo , kwani mpaka wakati huo hakuwa ameunda serikali yake kikamilifu .

Wakati anamaliza kusoma barua hio , ilikuja ripoti nyingine ambayo na ripoti hii ilikuwa ikitoka makao makuu ya U-97 Afrika , makao makuu ambayo yapo nchini Nigeria , ripoti hii ilimshitusha sana muheshimiwa , kwani ni ripoti ambayo ilikuwa na majina ya serikali yake mpya , yaani kuanzia waziri mkuu mpaka mawaziri , jambo hili lilimkera sana mheshimiwa, na kujikuta akikumbuka maneno ya bwana Damiani kwamba haijalishi ni raisi gani anaingia ikulu , kwani kila kitu kinaendeshwa na umoja huu , na jambo hilo ndio alikuwa akilishuhudia kwa wakati huo , jambo la kufanywa shushu , aliamini kwa mlolongo huo wa matukio hatokuwa na uwezo wa kuwaletea watanzania maendeleo ambayo alikuwa ameyaahidi , kwake ilikuwa ni kama kukalia misumari ndani ya kiti hicho cha ikulu , kwani alijiona m yeye sio kama raisi wa nchi hii , alikosa madaraka kamili , lakini kwa wakati mwingine alikuwa na hofu na jambo litakalo mtokea .

Alikumbuka maneno ya mwisho wakati akiwa anaagana na wanachama wa Mzalendo

“Saa ya ukombozi inakuja mheshimiwa , inakupaswa kuwa na moyo wa uvumilivu , wafanye wakuamini kwa namna yoyote ile , hata kama ni kwenenda kinyume na matakwa ya wananchi , unachokifanya ni kuliokoa taifa hili katika mikono ya hawa maharamia , haijalishi watu watakuangaliaje ,ilihali unalolifanya ni kwa ajili ya taifa sio kwako binafsi basi huna haja ya kuogopa , saa ya ukombozi inakuja “ Mheshimiwa alijikuta akikukumbuka maneno hayo na kisha aliichukua upya ile ripoti na kuisoma .

Hakuona haja ya kwenenda kinyume na ripoti hio , alipanga kuteua watu hao kama umoja huo unavyohitaji, kwake jambo hilo aliona ni kama mtego , kwani umoja huu ulikuwa haujamwamini bado , na kama Damiani alivyosema kuwafanya wamwamini . basi aliona haikuwa na haja ya yeye kwenenda kinyume na ripoti hio .

Kama ilivyokuwa desturi kwa kila chama kinachoingia madarakani kuweka watu wa chama ili kusaidiana kuliongoza taifa basi ndio kilichokuwa katika majina hayo , umoja huu ulikuwa umependekeza majina ambayo watu wake walikuwa ni wanachama wanaotkoka katika chama cha raisi Jembe, jambo ambalo liliibua maswali mengi sana katika kichwa cha raisi huyu mteule , kwani watu ambao walikuwa wamependekezwa walikuwa ni watu ambao alikuwa akiwaamini sana na pia alikuwa akinuia kuwapa uongozi katika serikali yake , lakini kitend cha majina hayo kuletwa na umoja huo aliona moja kwa moja kuna jambo , na jambo lenyewe ni watu hawa aidha kuwa wanachama wa Mzalendo, au kama sio wanachama basi huenda umoja huu umeona kuna maslahi katika watu hao kuchaguliwa kwao .

Mheshimiwa raii alijikuta katika tafakuri nzito , wakati akiwa anafikiria hili na lile , katibu muhtasi mwanadada aliekuwa akifahamika kwa jina la Jennifer , aliingia na kumtaarifu mheshimiwa kuwa kuna mgeni wake , na bila hiyana mheshimiwa alimruhusu mgeni huyo kuingia ofisini kwake kwa upande wa kuonana na wageni .

“Karibu sana bwana Mboneche “Aliongea mheshimiwa mara baada ya kumuona mtu alieingia ndani hapo kuwa ni mtu anaemfahamu , na alimfahamu katika uongozi wa raisi Henry mushi , ambapo kijana huyu alikuwa ni mkurugenzi wa mawasiliano Ikulu .

“Asante ana mheshimiwa nilikuwa na wasiwasi hautweza kunifahamu”

“Nakufahamu sana bwana Sabi Mboneche na hata baba yako nililikuwa nikifahamiana nae sana”

“Asante ana mheshimiwa nimekuja kujitambulisha kwako kama mwanafamilia ndani ya wazalendo wa nchi hii”

“Nashukuru sana kwa kujitambulisha kwako bwana Mboneche , ninafuraha sana kukuona kama moja ya wazalendo wa nchi hii , hakika ni jambo la kujivunia sana kwa kijana kama wewe”

“Asante sana mheshimiwa, nipo hapa kwa ajili ya kufikisha ujumbe kutoka kwa wazalendo wa nchi hii”

“Karibu sana” Raisi alijiweka sawa kupokea ujumbe kutoka kwa wazalendo na ni jambo ambalo lilikuwa ni tumaini kubwa kwake kila mara anapokuwa anakutana na mwanachama wa Mzalendo ama kupokea taarifa yoyote inayotoka kwa wanachama hawa.

Sabi alitoa laptop kampuni ya Apple katika mkoba wake na kisha alichomeka Flashdisk katika ile tarakishi mpakato na baada ya kufanya hivyo alifungua faili na kisha akamgeuzia mheshimiwa tarakishi ile kwa ajili ya kusoma.

RaisiJembe alichukua muda mfupi tu kukamilisha kuoma ujumbe huo na kupumua kwa nguvu kwani ni kama mtu ambae alipata ahueni.

SURA YA 05​

Kazi ya kumfikisha raisi Jembe ndani ya ikulu ilikuwa imekamilika kwa asilimia mia moja , na kwa hatua hio kwetu sisi kama timu ya wazalendo tuliona ni hatua nyingine ambayo tulikuwa tumepiga katika mapambano yetu zidi ya huu umoja .

Tokea siku ambayo mheshimiwa jembe aingie ikulu , hatukulala,tulikuwa na muda miezi sita tu wa kukamilisha misheni ya kujua wapi kitabu cha Book Of all names kilipo , na ndio maana kila siku tulikuwa tukifanya upelelezi wa kupata muelekeo wa vyanzo mbalimbali ambavyo vinaweza kutupa muongozo au mwanga wa kukipata kitabu hichi.

Haikuwa kazi rahisi katika kupata muelekeo , kwani ni juhudi nyingi tulikuwa tumefanya na tunaendelea kufanya za kuweza kupata muelekeo wa misheni yetu,Jambo kubwa ambalo tulipanga mpaka wakati huu zaidi ya siku kumi kupita ni kuhakikisha tunawatambua viongozi wakubwa wa umoja huu , lakini pia jambo hilo halikuwa rahisi kwani viongozi wakubwa wa Umoja huu walikuwa hawatambuliki kabisa na hata baadhi ya wanachama wenyewe walikuwa hawawajui, kama umesoma kitabu cha Waraka wa Raisi kabla ya kifo utanielewa ninachomaanisha , katika Umoja huu madaraja ya kiuongozi hupangwa kwa mfumo wa levo(Level) ni kimaanisha kuna level 01 ambaye huyu ni mkuu kabisa wa Umoja huu , yaani tunaweza kusema Raisi , halafu kuna Level 02 mpaka level 07 hawa ni viongozi wakubwa kwa kila bara na kila bara lina makao makuu ambapo kama kuna mkutano unafanyika kwa kiila bara basi wanakutana katika makao hayo makuu na kiongozi mkuu wa bara ndie anaeongoza, jambo jingine ndani ya umoja huu ni kwamba katika hawa viongozi nane yaani kuwanzia level 01 mpaka 08 hawawezi kutoka madarakani mpaka pale kifo kitakapowakuta ama kupata tatizo ambalo linapelekea kutotimiza majukumu yao , na kama tu moja ya kiongozi akifariki basi jina lake huweka hadharani katika huu umoja kwa kila mwanachama yaani kwa maneno mafupi ili kwa wanachama walio kwenye level za chini ili waweze kumfahamu mkuu fulani wa bara ama Level 01 ni mpaka pale atakapo kufa, sasa hio ni sehemu tu ya sheria za umoja huu.

Hivyo mpaka sasa mimi na timu yangu hatujaweza kupata namna ambavyo tunaweza kuwatambua hawa wanachama wa Umoja huu na hapa nazunguzia wale wanachama wenye vyeo vikubwa , kwahio misheni yetu ya kwanza ni kutambua hawa wanachama ambao wanavyeo vikubwa , kwani tunaamini kwa kuwatambua hawa tunaweza kupata mwanga wa kile kitu tunachokitafuta yaani Book of all names.

Nikiwa zangu nyumbani siku ya alhamisi yaani siku ya nane ya kuingia madarakani kwa raisi

Jembe muda wa jioni jioni hivi niliweza kupata mawasiliano na moja ya ajent ambae alikuwa anafanya utafiti namna ya kuwapata hawa viongozi , na utafiti huo alikuwa akiufanyia nchini Marekani .

Taarifa alionipatia ajenti huyu ambae anafahamika kwa jina la Kino ilinifanya nitabasamu na kunifanya ninyanyuke nilipokuwa nimekaa na kuelekea ndani ya chumba changu cha kulalia , chumba ambacho licha ya kuwa chumba changu lakini sijawahi kukizoea kutokana na muundo wake , na sio mimi tu hata Janeth alikuwa akikisifia sana chumba hiki na mara kwa mara alikuwa akipenda kulala katika hiki chumba na hata siku hii ambayo nimepokea taarifa kutoka kwa ajenti Kino mrembo huyu alikuwa amelala akiwa amekibinua kishundu chake juu huku akiwa na nguo ya kulalia , kwa jinsi alivyokuwa akionekana kwenye macho yangu ni kwamba alikuwa mkao wa kuliwa tu hakuna namna na mimi sikutaka kumchelewesha kwani lile jambo ambalo nilikuwa nimelipanga kulifanya ndani ya chumba hicho lilisahaulika , kama nilivyosema mtoto huyu mzuri ambae hakinaishi alikuwa ameiva kwani ile kugusa tu alikuwa rojo na mimi sikuwa na ajizi katika kuhakikisha matendo yangu ya kiume yanathibitika katika akili za mrembo huyu kwani nilipiga bakora za kimkakati .

“Asante mpenzi”

“Hio asante ya nini tena”

“Kwa unacho nifanyia na kueendelea kunifanyia”.

“Basi hio asante bora uitunze mpaka pale nitakapomaliza kukufanyia hivyo vitu ambavyo naendelea , maana utachoka kunipa asante kila siku” “Ushaanza mambo yako Damini “ Huku akinifinya .

“Nilianzaga zamani sasa hivi nipo kwenye mwendelezo”.

“Hahahaha..Una maneno sana wewe mwanaume”

“Mbele ya mrembo kama wewe lazima niwe na maneno , maana kwa jinsi ulivyoumbika nashindwa hata kuzishinda tamaa za mwili wangu , hata lile jambo nililoingia nalo hapa nilijikuta nikilisahau”

“Kumbe ulikuwa na jambo, haya niambie nadhani sasa hivi unalikumbuka”

“Kino kanipatia taarifa ambayo imenifanya nitake kukuambia na inaweza kuwa msaada mkubwa katika misheni yetu”Niliongea , lakini ni kama huyu mwanamke hanisikilizi kile ninacho ongea kwani alikuwa akichezea karumanzila na kumfanya asisimke tena na kwa jinsi alivyojichanua na mapaja yake yalivyonona nilijikuta nikiishia kubadilisha topic na kuingia kwenye matendo .

“Taarifa hio inahusu nini ?”Aliniuliza Janth na muda huu alionekana kuridhika na hii ni baada ya kumpelekea moto kwa muda wa madakika kama arobaini hivi .

“The Truth”

“Ndio nini ?”

“Hii ni kitengo cha siri kinacho uza taarifa kinachopatikana katika jiji Sydney Australia , na kutoka kwa maelezo ya Kino ni kwamba hiki kikundi kina kila aina ya Taarifa duniani kote”

“Mhmh !kwa maana hio unataka kusema wanaweza kuwa na taarifa ya Book Of All Names”. “Hilo sijui, lakini inawezekana wakawa nayo , au wakafahamu mtu ambae anaweza akawa na taarifa ya kitabu hicho , lakini pia wanaweza wakawa wanajua U-97 kuliko tunavyoijua sisi”

“Kwa hio ?”.

“Nataka niingie nchini Australia , lakini kabla ya yote nataka kwanza tufanye utafiti juu ya hii organisation , tuijue nje ndani ili nikifika ndani ya Sydney nipate pakuanzia”.

Janeth alionekana kunielewa mara baada ya kumuambia jambo hilo , na kwa haraka haraka mara baada ya kujadiliana jambo hili tulioga haraka haraka na kwenda kwenye chimbo letu la udadavuzi , sehemu ambayo ilikuwa ikionekana ni ndogo lakini tulikuwa na uwezo wa kupata taarifa nyingi duniani , unaweza kutufananisha na kitengo cha kijasusi cha kimarekani kifahamikacho kwa jina la NSA(National security Agency).

“Linda nataka kuanzia sasa tutafute taarifa zote zinazohusiana na The Truth”Niliongea mara baada ya kufika ndani ya Basement yetu na kukutana na huyu mrembo afahamikae kwa jina la Linda , na nikisema ni mrembo ni mrembo haswa , ashawahi kuniingiza matatizoni wakati tukiwa mafunzoni nchini Urusi kwani kipindi hicho nilikuwa nikijipigia huyu mtoto , lakini kumbe mkufunzi wetu alikuwa akimtaka Linda na sio kumtaka tu ni kwamba Linda alikuwa ashampa uchi muda tu na mkuu huyu akanogewa na mnato wa Linda, kitendo kilichomfanya mkufunzi wetu kuanza kufatilia nyendo za Linda na kujua muhuni hapa ndio nilikuwa nikimega kiulaini tena bila nguvu , kwanzia siku hio niliishi kwa mateso makubwa ndani ya kambi ,kwani mazoezi niliokuwa nikipigishwa yalikuwa ni kufuru lakini sio mazoezi tu , nilikuwa nikipewa majaribio ya kimafunzo ambayo yalikuwa ni kufa na kupona , lakini kushukuru Mungu ni kwamba nilikuwa na kichwa chepesi sana katika kutatua matatizo ninayokumbana nayo .

“The Truth ni Organisation(kikundi au kashirika) yenye makao makuu nchini Australia katika jiji la Sydney , moja ya kazi kubwa inayofanywa na kikundi hichi ni kukusanya taarifa zile zinazoonekana na sizizoonekana na kuwauzia watu mbalimbali wenye uhitaji nazo, ni Organisationa ambayo imeanzishwa na bwana Erick Peter raia wa Tanzania anaeishi nchini humo “

“Erick Peter!!,Naomba kumfahamu huyu bwana “Niliongea huku nikionyesha mshangao inawezakanaje mtanzania kuwanzisha kikundi ambacho kinasifika kwa kuuza kila taarifa .

“Erick Peter ni mwanasayansi kutoka chuo kikuu cha Monash, akichukua maswala ya Computer Science , akiwa ndio mwanafunzi pekee alieongoza kwa kupata asilimia mia katika masomo yote na kupata GPA ya 5.0 , anaishi na mama yake tokea wafike nchini Australia , Mama yake anafahamika kwa jina la Rania Samir” “Nipe taarifa ya huyu mama yake”

“Rania Samiri ni Mtanzania na mfanya biashara mkubwa ndani ya jiji la Sydney ni mtoto wa tajiri marehemu Samir Rafaeli mswaki , Alihamia nchini Australia mara baada ya kifo cha mume wake marehemu Tajiri Hemedi kibajia|”.

“Kwanini ahamie nchini Australia , naamini kuna jambo la ziada hapa ambalo hatulijui ,Janeth naomba uendeleee kuchimba taarifa za hawa watu”.

“Vipi kuhusu Mheshimiwa Jembe”

“Hatuna la kufanya juu yake , inatupasa kumuandikia ujumbe kwa kumtia Tumaini . lakini pia ahadi yetu kwake ni ndani ya Miezi sita tutakuwa tumefanikiwa kupata Kitabu cha Book Of all names’ na kuutokomeza umoja huu na hatimae kuwa huru , taarifa hio inatakiwa kupewa Sabi aipeleke kwani ndio atakuwa mtu pekee ambaye atakuwa karibu na Mheshimiwa kwa sasa Na mawasiliano yetu na mheshimiwa yatapitia kwake”.

Zilipita siku mbili yaaani siku ya kumi na moja ya utawala wa mheshimiwa Jembe hatimae niliweza kuliacha Anga la Tanzania nikielekea chini Australia kukutana na kikundi cha ‘the truth’ kikundi ambacho tulikuwa tukiamini wanaweza kuwa na taarifa zinazohusiana na U-97 pamoja na kitabu Cha Book of all names.

Sikuwa na mizigo mingi ambayo nilikuwa nimepanga kuingia nayo nchini Australia , sikuwa na siraha Zaidi ya kuwa na FBM(Full body mask) siraha yangu ambayo nilikuwa nikiiamini sana , na naweza kusema ni moja ya Mask hatari sana kutengenezwa katika uso wa Dunia , huku mtengenezaji akiwa ni Profesa janeth ,Ndio Ni janeth yule ambaye analilia dudu yangu kila akiniona , lakini ni waambie tu ni moja ya wanawake majiniasi sana .

Full Body Mask nikijaribu kuielezea kwa uharaka wake tu ni kwamba ni mask ambayo ilivumbuliwa nchini China na Mtanzania ambaye ni Profesa anafahamika kwa jina la Janeth Bendera mtoto wa Raisi John Bendera , Mask hii inauwezo wa kukubadilisha muonekano wako kwa asilimia mia moja na kukupa muonekano mwingine kabisa, licha ya FBM kuwa na uwezo wa kukubadilisha muonekano lakini pia ilikuwa na uwezo wa kumfanya mtu kuwa na uwezo mkubwa sana kimapigano , kwani inaweza kuongoza akili yako na viungo vya mwili na kuwa mtu mwingine kabia hususani pale unapokuwa katika hatari , jambo jingine ni kwamba FBM ina uwezo wa kumkinga mtu na kitu cha hatari kwa mfano risasi.

Nikiwa ndani ya ndege nilikuwa nikiwaza mengi na kubwa Zaidi ni juu ya Mpango Zero , mpango ambao mpaka sasa tumeshindwa kuujua unahusiana na nini haswa , kwanini mpango huu ukatekelezwa ndani ya Taifa la Tanzania , una malengo gani haswa kwa taifa la Tanzania , hayo ndio maswali ambayo nilikuwa nikijiuliza katika safari yangu hio , nakufanya hamu ya kutaka kukipata kitabu cha Book Of All Names izidi kuongezeka .

Niliwaza mengi sana tokea siku mama yangu anapigwa risasi , kashikashi zote nilizopitia kwanzia kwenda nchini Thailand na kujifunza mapigano ya kithai , namna ambavyo niliweza kukutana na Sabi Mboneche na kusimuliana mapito katika maisha yetu simulizi ambazo ya kwangu na ya Sabi zikiwa zinaendana.

Lakini pia niliwaza namna ambavyo niliweza kufika china na kuingia katika bodi ya wakurugenzi wa kampuni ya Huawei , namna ambavyo niliweza kuonana na waziri wa mambo ya ndani ya China , ambaye sasa ni Raisi wa China lakini pia niliweza kukumbuka namna ambavyo niliweza kurudi nchini na kuendeleza mapambano ya kumtafuta mtu ambae alihusika na kifo cha mama yangu mpaka pale nilipokuja kugundua mtu aliehuika na kifo cha mama yangu alikuwa ni mtu ambae nilikuwa nikimfanyia kazi muda wote ,lakini pia nilishikwa na huzuni pale nilipokumbuka kumpoteza mwanamke wangu wa kwanza kumpenda kwa moyo wote mwanadada mrembo kuwahi kutokea kwenye taifa la Tanzania ‘Merina Bruno Lamberk.

Nilijikuta nikiwaza mengi katika safari hio nzima , mpaka pale tulipokaribia ndani ya uwanja wa kimataifa wa Sydney kingsford Smith international Airport na kufunga mikanda baada ya kupta maelekezo kutoka kwa mhudumu wa ndege .

Dakika kama tano mbele nilikuwa nikitoka nje ya ndege ya uwanja huu wa kimataifa wa Kingsford ni uwanja mkubwa sana na umejengeka vyema sana , nilijikuta nikivuta harufu ya bara hili huku nikitangulizana na wasafiri ambao nilikuwa nao katika safari nzima ndani ya ndege hii ya shirika la Qatar Airways , jiji la Sydney ni jiji lililojengeka sana kimiundo mbinu na mpangilio mzima na hili nililishuhudia baada ya kutoka ndani ya Airport na kuingia ndani ya Taksi , ni mara yangu ya kwanza kufika kwenye jiji hili na nchi hii ya Australia na nilichokuwa nafanya wakati huu ilikuwa ni kushangaa tu na kujitahidi kusoma kila mtaa tunaopita .

Tulianzia mtaa wa Marsh tunkaingia mtaa mmoja ufahamikao kwa jina la Qantas na safari yangu muda huu ilikuwa ni kuelekea katika hoteli ifahamikayo kwa jina la Park hyatt , na mnaweza mkashangaa kwanini nimechagua hoteli hii , jibu ni kwamba mmiliki wa hoteli hii alikuwa ni mwanamama Rania ambaye ndio mama wa mtoto anaeongoza kikundi cha The truth , hivyo niliamini kwa kwenda kulala ndani ya hii hoteli ingenirahishia katika kazi yangu. .

Basi baada ya kuingia barabara ifahamikayo kwa jina la Mill pond tulinyoosha moja kwa moja mpaka M1 Road tukaja kutokea kwenye mtaa ambao unafahamika kama City N sehemu ambayo pia ilikuwa imejengeka sana , yaani ndani ya hili jiji kulikuwa kuna majengo yale ya zamani na haya mapya ambayo unaweza kuyaona hata ndani ya Tanzania , basi baada ya muda mchache hatimae niliweza kuingia mtaa mmoja ambao nilipata kuujua kama Hikson Street na mbele kabisa ndio lilikuwa jengo hili la hotel ya Park hyatt hotel ,ni bonge ya hoteli haikuwa na jengo refu kwenda juu ,lilikuwa refu kwenda ‘horizontal’ na lilikuwa pembeni kabisa mwa bahari yaani ulikuwa ukiiona bahari kwa uzuri kabisa , mazingira ya hoteli yalikuwa mazuri sana tena sana kimbembe kilikuwa ni kwenye gharama ndani ya hoteli hii , lakini hayo yote ya uzuri sikutaka kuyawaza sana japo jambo moja tu ambalo lilinifanya kuwaza ni juu ya umiliki wa mwanamama Rania hoteli hii kubwa.

Basi niliingia mapokezi pale na kukutana na mrembo mmoja wa rangi ya kizungu alievalia sare za hoteli hio , na mara baada ya kuniona tu aliachia tabasamu kama ananifahamu vile kumbe ni ucheshi mbele ya wageni , na mimi bila ajizi nilipokea tabasamu lile kwa kuachia langu.

“Nilikuwa nishafanyiwa Booking kabisa ndani ya hii hoteli hivyo kufika mapokezi nilijitambulisha na kupewa kadi yangu tu , utaratibu ulikuwa mzuri hakukuwa na maswali mengi ,jambo ambalo nilikuwa nikiwapendea sana wazungu.

Watu wengi ambao nilipishana nao ndani ya hii hoteli ni wa rangi nyeupe sana sana , yaani rangi ya kiafrika ile nyeusi sikuwa nimeiona ndani ya hoteli hii na naweza kusema huenda mimi ndio nikawa mtu pekee ndani ya hoteli hii ambae ni mwenye kuwa na rangi nyeusi .

Nilifanikiwa kufika mbele ya mlango wa chumba changu na kuweka kadi yangu na kisha bila hiyana mlango ulitii amri na kufunguka , kilikuwa ni chumba kizuri mno kilicho jaa ufahari na kiliendana na bei yake ya kulala hapo usiku mmoja yaani milioni tatu.

Baada ya kuingia ndani ya hoteli hii jambo la kwanza kufanya ilikuwa ni kukikagua chumba hichi , hizi ni mbinu za kijasusi yaani huwezi kumkuta jasusi mbobezi ambae yupo kwenye misheni akaingia kwenye chumba na akafanya mambo yake bila kukagua chumba .

Nilitafuta uwepo wa kamera ndani ya chumba hiki lakini sikuambulia kitu , na baada ya kijihakikishia hakuna kitu chochote cha kutegwa , niliweka kijibegi changu chini na kisha nikapunguza nguo .

Hali ya hewa ya nchi hii kwa ujumla wake si baridi sana wala si joto sana , japo kwa kufatilia katika mitandao niliweza kugundua kuna kipindi kunakuwa na baridi sana na hata barafu , lakini mwezi huu nilioingia hapa nchini hakukuwa kipindi cha baridi.

Niliwasiliana na kitengo cha Mzalendo kuwajulisha nipo nchini Australia na baada ya kufanya hivyo nilisogelea dirisha na kutoa pazia na kuangalia mandhari ya nje , Australia ni moja ya nchi nzuri sana , sipo hapa nchini Australia kwa ajili ya kuisifia lakini nashindwa kujizuia kuisifia kwa mazingira yake , sijajua maeneo mengine ya hii nchi lakini hili jiji la Sydney ni bonge la jiji .

Basi nilikuwa na siku kumi tu za kukamilisha swala langu la kuwasiliana na hiki kikundi cha The truth , niliamini kwa kukaa ndani ya hoteli hii lazima ningeweza kupata pakuanzia.

Unaweza ukashangaa kwanini nisiende moja kwa moja mpaka makao makuu ya kikundi hiki na kueleza shida yangu , jibu ni kwamba hiki kikundi taarifa zake zilikuwa zikipatikana kwenye mtandao, na kwa kugoogle tu utaambiwa makao yake makuu ni ndani ya jiji la Sydney lakini ukweli ni kwamba kikundi hiki ndani ya nchi hii kilikuwa ‘invicible’ yaani kilikuwa kinafanya kazi zake ndani ya jiji hili pasipokuonekana wala hakikuwa na sehemu maalumu ambayo utasema ni ofisi yao

Hivyo kazi yangu ya kwanza ilikuwa ni kutafuta namna ya kuwasiliana na kikundi hiki na ndio dhumuni kuu la kuja kulala kwenye hoteli hili la kifahari , Muda ambao nilikuwa nimeingia ndani ya nchi hii ilikuwa ni saa kumi na moja kwenda kumi na mbili kwa muda wa nchi hii , hivyo mpaka wakati huu nililikuwa nimetumia lisaa limoja ndani ya hili taifa la kizungu.

Basi yalipita kama masaa manne tokea niingie ndani ya hoteli hii , na ilikuwa ni saa tatu za usiku ., muda huu nilikuwa natoka kwenda kupata chakula cha usiku kwani tokea niingie ndani ya hoteli hii sikula chochote Zaidi ya kulala kupunguza uchomvu , kwa maana hio kimahesabu nilikuwa nimelala masaa matatu , nilikuwa na uwezo wa kuagiza chakula changu chumbani lakini sikutaka kufanya hivyo kwani kuja kwenye nchi hio sio kwa ajili ya ‘vacation’ bali ni swala la kijasusi ndio limenifikisha hapo , hivyo kula ndani ya mgahawa wa hoteli hii ilikuwa ni sehemu ya kazi, kwa mtu ambae huna uelewa na maswala ya ujasusi unaweza ukajiuliza kwaninin ninasema kula mgahawani ni sehemu ya kazi yangu , jibu ni kwamba majasusi wengi kula sehemu yenye watu wengi ni namna ya kuwasoma watu , katika mafunzo ya ujasusi tunafundishwa pia kutambua mambo kwa kuona , yaani ninaweza kumjua mtu mbaya na mzuri kwa kumwangalia tu .

Hivyo mimi kwenda eneo la mgahawa huo kula ilikuwa ni kutafuta watu wabaya,jasusi yoyote yule hanaga muda na mtu anaeonekana kuwa hana hatia ya aina yoyote ile , tunatafuta wale watu ambao wanaviashiria vya uhalifu .

Hii hoteli ilikuwa ikinukia pesa tu , jambo ambalo lilikuwa likinisisimua sana , sio kwamba mimi sina pesa , wanaonijua wanaelewa ninachozungumza na ndio maana kama haujanisoma katika kitabu cha Waraka wa raisi kabla ya kifo naomba unisome na utanielewa vizuri sana na huenda ukafurahia kila kitu ninachokwambia hapa

Hivyo nikisema sehemu hii inanukia pesa, kwanza kabisa muundo wa hoteli hii, jambo la pili mpangilio wa huu mgahawa na watu waliokuwa ndani , kila uso nilioweza kuuona na kuuscan niliona ukwasi wa pesa

Watu katika mgahawa huu hawakuwa wengi sana na waliokuwepo walikuwa bize kupata chakula , nilizungusha macho kutafuta kitu ambacho kinaweza kunivutia lakini sikuona kitu japo kuna jambo moja kidogo lilinivutia na hii ni mara baada ya kuona watu wengi ndani ya huu mgahawa wapo kwenye ‘dinner date’.

Nilisogea upande wa kulia sehemu ambayo ilikuwa ni wazi sana , yaani nilikuwa nikiona mtu anaeingia na kutoka, baada ya kuketi alikuja muhudumu wa kike mrembo na kisha alinikabidhi kitabu huku akiwa ameachia tabaamu na mimi nilipokea kile kitabu na kuanza kuangalia vyakula vinavyopatikana.

Na baada ya kuona chakula ninachokipenda kipo kwenye orodha niliagiza hicho ,chakula hiki kilikuwa kikifahamika kwa jina la Jiaozi , ni chakula cha kichina ila nilitokea kukipenda sana mara ya kwanza nilivyokula nilipokuwa nchini China , watu wengi wanakipenda chakula hiki na mpaka sasa kimeingia katika orodha ya International Food(Vyakula vya kimataifa )

Vyakula vya kimataifa ni vile vyakula ambavyo kila hoteli kubwa utakayo ingia duniani kote lazima uvikute , hivyo kwa mfano labda kwa mara ya kwanza ukashinda mchezo wa Biko na ukaamua kujitoa ‘vacation’ nje ya nchi na ukafika kwenye hoteli ya watu na hujui chakula gani uagize basi nenda zako ‘Google’ na andika orodha ya vyakula vya kimataifa utapata orodha yote na wewe bila kuhangaika wewe agiza tu , nakwambia kwakuwa ni mara yako ya kwanza kula vyakula vya ubora wa hali ya juu chakula utakachokula siku hio utaamini ndio chakula kizuri Zaidi duniani lakini na kwambia vipo vizuri Zaidi ya hivyo na ndio maana vikapewa hadhi ya kimataifa.

Basi mrembo mhudumu alichukua bili yangu na kisha aliachia tabasamu na kuondoka kwa madaha , sifa ya hii nchi pia ni kuwa na warembo , yaani inawatoto ni wakalii ile mbaya japo wengi wao wanakosa sifa ambazo wanaume wa kibongo tunaipenda sana.

Wakati nikisubiria oda yangu nilijikuta mwili ukinisisimka mara baada ya kuepeleka macho kwenye mlango wa kuingilia ndani ya mgahawa huu.

SURA YA 06​

Licha kampuni ya Innova kupata mafanikio katika projekti iliokuwa ikifahamika kama mpango Zero hawakukaa chini kwa kutulia , bado akili zao hazikuwa zimeridhika na kile kilichokuwa wakikiita mafanikio ya mpango huo , ni majaribio Zaidi ya sitini ambayo yalikuwa yamefanyika kwa vitoto vichanga lakini mtoto Ambrose pekee ndie aliepita katika majaribio hayo huku vitoto vichanga hamsini na tisa vikipoteza maisha , kitu ambacho kilizidi kuwashangaza ni kwamba licha ya mtoto Ambrose kupita katika majaribio hayo hakukuwa na mabadiliko ya aina yoyote ile ndani ya mwili wa mtoto huyo jambo ambalo lilikuwa nje ya mategemeo yao ya kisayansi .

Sasa ni miaka kumi ya umri wa mtoto Ambrose , lakini pia ni miaka kumi tokea mpango huu zero kufanikishwa ndani ya taifa la Tanzania , mpango ambao ilitekelezwa na kampuni ya Innova ukifadhiliwa kwa asilimia mia na umoja wa siri ufahamikao kwa jina la U-97(Umoja Namba Tisini na saba).

Katika miaka yote kumi ya ukuaji wa mtoto Ambrose yapo mengi ambayo yalikuwa yakushangaza ambayo yalikuwa yakionyeshwa na mtoto huyu , kwani alipofikisha miaka mine tu Joseph(Peter) na Johani(Leah) wazazi wake walimwanzisha darasa la awali katika shule ya Feza boys ndani ya jiji la Dar es salaam , mwanzo wa masomo kwa mtoto Ambrose ndio mwanzo wa mshangao kwa wanafunzi , walimu , pamoja na wazazi wa Ambrose kwani mtoto huyu aliweza kudhihirisha uwezo mkubwa sana wa akili ,hakuwa akisahau kile ambacho alikuwa akifundishwa , alikuwa na uwezo wa kukumbuka mpaka nukta.

Jambo hili la uwezo mkubwa wa akili wa mtoto huyu liliwafanya wanasayansi wa kampuni hii ya Innova ambao walikuwa wakimfatilia kwa miaka yote wafurahi , kwani moja ya mafanikio ambayo waliyategemea juu ya projekti yao hio ya Mpango Zero ni pamoja na uwezo wa akili kwa muhusika.

Mwalimu Elon scholz ndio alikuwa amepewa jukumu la kuangalia mwenendo mzima wa mtoto

Ambrose ,Mwalimu huyu raia wa Israeli alikuwa na jukumu zima la kumfundisha

Ambrose,lakini pia alikuwa ndani ya shule hio kimkakati kwani alikuwa ni moja ya wanachama wa Umoja Namba Tisini Na Saba aliepewa jukumu la kutoa ripoti ya maendeleo ya ukuaji wa Ambrose .

Ni siku mbili tokea kijana huyu aingie ndani ya taifa la Marekani , katika jimbo la Florida shule inayofahamika kama North Broward Preparatory School kuendelea na masomo yake , ambayo yalikuwa yakigharamiwa kwa asilimia hamsini na kampuni ya Innova huku wakiwa kama wafadhili .

Siku ambayo wafadhili hawa walipofika shuleni hapo kwa ajili ya kuweka nia yao ya kumfadhilia Ambrose kimasomo , walimu wake walikubali akiwemo mwalimu Elon , lakini kwa wazazi wa Ambrose ilikuwa nikizungumkuti , kwanza hawakutaka mtoto wao kufadhiliwa kwani walikuwa wanauwezo wa kumsomesha kwa asilimia mia moja pasipo kufilisika katika shule yoyote ile duniani .

Lakini kwa ushawishi wa Profesor mike Alan walijikuta wakikubali Ambrose kwenda kusomea nje ya nchi huku na wao wakitaka kulipia nusu ya gharama ya masomo ya mtoto wao , kwani ni jambo ambalo lilikuwa likiwafurahisha kuhangaika kwa ajili ya mtoto wao wa kipekee.

North Broward ni shule ghali sana ndani ya Taifa la marekani , ambayo ilikuwa na jukumu la kufundisha watoto kwanzia miaka miwili mpaka kumi na nane , shule hii inahistoria pana sana katika swala zima la ufundishaji tokea kuanzishwa kwake miaka Zaidi ya hamsini nyuma , na inahistoria nzuri katika kutoa wanasayansi wakubwa sana duniani na kuibua vipaji vya watoto .

Yaani moja ya jukumu la shule hii ni kusoma tabia za mtoto katika maisha yake ya kila siku ili kuweza kutambua kipaji chake au kile anachopendelea , na hilo ndio dhumuni kubwa la kampuni ya Innova kumpeleka ndani ya shule hio , kwani licha ya kujua kwamba Ambrose alikuwa na akili nyingi , lakini hawakujua alikuwa na kipaji gani na alikuwa akipendelea nini kwani muda wote alikuwa na wazazi wake jambo ambali lilikuwa gumu kujua akiwa nyumbani anapendelea nini Zaidi ya wao kumuona shuleni tu , hivyo kumpeleka nje ya nchi kimasomo ulikuwa ni mpango wa kutaka kuisoma Zaidi tabia ya mtoto huyu na jambo hilo walikuwa wamefanikiwa. .

Moja ya taratibu za shule hii ni kuanza kumpima IQ(Inelligency quotient)kila mwanafunzi anaenza masomo katika shule hio ,hivyo ndani ya siku mbili za kufika kwa Ambrose asubuhi yake yaani siku ya jumanne,alianza na utaratibu huo.

Ni baada ya masaa kumi na moja kupita baada ya mtoto Ambrose kupitia hatua zote za kujiunga na shule hio ikiwemo ya kupima IQ, muda huo ndani ya chumba cha mikutano kilichokuwepo ndani ya Jengo la Millenium Calfornia ndani ya chumba kilichokuwa kimeandikwa VVIP walionekana mabwana wanne jumla yao, watatu wakiwa na asili ya kizungu , mmoja akiwa na asili ya kiafrika iliochanganyika na rangi ya kiarabu ,moja ya watu hawa alikuwepo Profesa Mike Alan ambaye alikuwa ni mkuu wa kitengo cha utafiti wa kisanyansi Ndani ya kampuni ya Innova , lakini akiwa pia ni mkufunzi na mhadhiri wa chuo cha Stanford.

Profesa huyu alionekana kuwa ndio kiongozi mkuu aliekuwa akiongoza kikao hicho ambacho kilionekana sio rasmi , na ajenda kuu ya kikao hicho ni kujadili juu ya mafanikio ya Mpango Zero.

“ 145 is a big score that has exceeded our expectations Professor , it proves how we succeeded in the first stage of this program”

“Maksi 145 ni maksi kubwa sana ambazoo zimepitiliza matarajio yetu profesa , hii inaonesha namna ambavyo tumefanikiwa kwatika huu mpango”Aliongea bwana ambae alikuwa na rangi ya kiafrika na mchanganyiko wa kiasia”

“It`s true 145 is superior IQ Score Marc, but we need more results than this in order for our plan to succeed ,I cannot call this success yet without knowing what is behind Ambrose passing our tests without finding even particle of harm in his blood”

“Ni kweli maksi hio ni kubwa sana bwana Marc ,lakini tunahitaji matokeo mengine Zaidi ya haya , siwezi kuyaita haya mafanikio bado ilihali sijui nini kipo nyuma ya Ambrose kuweza kupita majaribio yetu bila kupata hata chembe ya madhara katika mwili wake”Aliongea Prefesa Mike wakijadiliana juu ya maksi kubwa za Ambrose .

Kwani kisayansi katika kumpima mtu uwezo wa akili , anaangaliwa ni maksi ngapi anapata katika mfululizo wa majaribio ya IQ , kiwango cha juu kabisa cha maksi ambacho kinamfanya mtu kuwa na akili sana ni kati ya 120 mpaka 140 lakini kwa matokeo ya Ambrose ni kwamba alikuwa amepata 145 akiwa amepitiliza viwango vilivyowekwa , lakini licha ya kupitiliza viwango hivyo Profesa Mike bado hajaridhika na majibu hayo .

“I also agree with Mike , but what will be our next step ?”

“Naunga mkono hoja ya Mike , lakini ni ipi hatua nyingine ambayo tunafanya “Aliuliza bwana mmoja wa kizungu, alieonekana kuwa mzee anaejipenda , anamwonekano kama wa Billgate tajiri wa dunia .

“Moja ya hatua ya kwanza ya Mpango Zero ni kutengeneza binadamu mwenye akili nyingi ili kuweza kufumbua fumbo ambalo limehangaisha wengi karne na karne , na hatua ya kwanza zidi ya matokeo tulio hitaji tumeyapata , hivyo napingana na hoja ya bwana Mike kwamba haya sio mafanikio , hatuhitaji kujua nini kipo nyuma ya kufanikiwa kwa Ambrose kupita katika majaribio yale “Aliongea bwana mwingine ambae alikuwa ameketi karibu kabisa na Profesa Mike huyu bwana muonekano wake ulikuwa ni kama wa Elon Musk.

“Umeongea sahihi Jeff , hoja ya Profesa ni kwamba katika majaribio yetu tulidhamiria kuzalisha kiumbe mwenye akili , lakini ambae anaweza kufikiria jambo moja tu ambalo ni hili jambo ambalo limewasumbua wengi ,Ambrose anaweza kuwa na akili nyingi lakini asiwe na matamanio ya kile tunachokitaka sisi”Alichangia bwana mwingine aliekuwa amevalia suti ya Zambarau ,huyu alikuwa na mwonekano kama wa Phill knight mmiliki wa kampuni ya Nike .

“Kuna njia za kumfanya mtu kuwa na matamanio ya juu ya kitu Fulani kwa njia ya kisaikolojia , kwanini tusitumie hizo tofauti na kujibizana juu ya jambo hili , nadhani hili litakuwa limerahisisha muda wa jambo hili , kumbukeni mpango huu lazima ufanikiwe ndani ya miezi sita kwanzia sasa”Aliongea Marc na wazo lake lilionekana kuwa na mantiki na kuwafanya mabwana hawa walipe uzito , na ajenda ikabadilika kutoka mafanikio ya Mpango Zero kwenda maswala ya kisaikolojia .

“Kwa hio matamanio ambayo tunamuingizia Ambrose ni yapi ili kuendana na mpango wetu?” Aliuliza bwana anaefanana na Elon Musk .

“Ni rahisi sana , Tunatakiwa kumpa kazi mwanafalsafa ili amjengee Ambrose matamanio ya kupenda historia ya kale (Anciety history)Na kwakuwa mwanasaikolojia huyu atatoka ndani ya U-97 basi itakuwa ni rahisi ya kumshawishi Ambrose na hapo ndipo tutampa fumbo hilo fumbo”Alijibu bwana yule anaefanana na Phill Knight na jambo hilo lilionekana kuungwa mkono , na majadiliano yaliendelea , huku muafaka ni Mtoto Ambrose kujengwa kupenda matamanio ya kujifunza mambo ya kale (Anciety history).
 
SURA YA 07.

Jambo la kwanza lililonivutia mara baada ya macho yangu kugonga juu ya mwili huu wa huyu mwanadada ,ni rangi yake , alionekana kuwa ni mwanamke kutoka bara la Afrika bila shaka , alikuwa mrefu saizi ya kati , mwenye rangi nyeupe iliofifia lakini inayovutia , sura yake ilikuwa ni ya kuchongoka , akiwa na nywele ambazo kwa kule nyumbani tunaweza kuiziita za kishombe shombe ndefu zilizomfika mabegani , jambo kubwa lililonivutia zaidi juu ya huyu mwanamke ni Shepu yake, alikuwa na umbo namba nane ambalo lilikuwa ni ugonjwa kwa wanaume wakitanzania wengi bila kunitoa kundini .

Mwanadada huyu alikuwa ametangulizana na kijana wa makamo kati ya miaa 28 hivi, alikuwa ni mzungu na ni kama kuna jambo kijana huyu alikuwa akumuelewesha huyu mwanadada mara baada ya kuingia ndani ya mgahawa huu , muda wote huu nilikuwa nikiwachora tu , huku pepo langu la kimatamanio likiwa juu .

Sura yake kwanza huyu mwanadada ilikuwa ikija na kupotea jambo ambalo niliona ni uchuro , kwani nilikuwa na njia nyingi za kumtambua mtu kwa njia ya DREAMER T.

Kwa wale msiofahamu DREAMER T ni mtandao wa kijasusi unaoendeshwa na serikali ya China wenye taarifa ya kila mtu duniani , mtandao huu uligunduliwa na rafiki yangu Luang Shu ambaye ni mtoto wa Raisi wa China.

Moja ya sababu zilizonifanya kufahamiana na Luang Shu ni koneksheni ambayo ilijengwa na Marehemu Raisi Bendera , moja ya maraisi wangu bora waliowahi kuliongoza taifa la Tanzania , raisi John bendera alikuwa ni wale maraisi ambao walikuwa wakifikiria maslahi ya taifa kulivko wanavyojifikiria yeye mwenyewe.

Na kuthibithisha hilo yeye yupo peponi mimi nipo hapa nchini Australia nikiendelea kufanya kazi ambayo hakuimaliza , kazi ambayo haimfaiidishi yoyote , Zaidi ya faida zote kwenda kwa Taifa .

Basi nilitoa miwani yangu ya kijasusi iliokuwa na teknolojia ya hali ya juu sana , miwani ambayo inavaliwa na ajenti wa Mzalendo pekee , na hio ni kwamba alieitengeneza ni mzalendo mwenzetu .

Basi baada ya kutoa miwani hii nilitoa simu yangu yenye chata la M(yaani mzalendo) ilikuwa ni simu mahususi kwa ajili ya kazi yangu na pia ilikuwa ikitumiwa na sisi wazalendo pekee , Nilivaa miwani ile na kunifaya nipendeze Zaidi na kisha baada ya kuivaa nilugusa ‘Icon’ moja kwenye simu yangu na kisha kukatokea maandishi ‘M smart device connected with AI SUPER GLASS’.

Baada ya kuona sasa simu yangu imeunganishwa na miwani nilimuacha huyu mrembo aniangalie na kisha nikampiga picha , yaani miwani ilikuwa ni kama Camera , baada ya kupiga picha ile niliipandisha(Upload) kwenye DREAMER T na kuomba kumtambua mtu huyo , na ndani ya sekunde mbili tu nilikuwa na maelezo yote .

“Bingo!!” Alikuwa ni Rania Samir mmiliki wa hii hoteli ya kifahari , sasa hapa niliona njia pekee ya kuwapata The Truth ni kupitia huyu mwanamama , ndio nimebadilisha jina kutoka mwanadada kwenda mwanamama ,kwani ana mtoto ambae ndio huyu anaemiliki kikundi hiki cha The truth , lakini si mwanamama tu hawa tunawaita kwa kimombo ‘Milf’ yaani mwanamke aliezaa lakini hajapoteza mvuto.

Sasa picha ya mpango ambao niliona utarahisisha kazi yangu , ni kuzoeana na huyu mwanamke japo niliamini ni mwanamke matawi ya juu lakini pia akionekana kuwa mkubwa kwangu kwani alikuwa amenizidi kama miaka minne lakini sikuwazia juu ya hilo kwani ni jambo ambalo pia tuna mafunzo .

Niliwaza namna ya kuanzisha ukaribu na mwanamama huyu , na hapo hapo nilipata picha la kihindi ambalo lilinifanya nitabasamu , sikuwa na haraka juu ya mpango wangu huo , basi niliendelea kula chakula changu kwa mbwembwe zote huku nikiendelea kumchora mwanamama huyu ambae kwa haraka haraka niligundua alikuwa akikagua hilo eneo , alifika mpaka upande wangu na kisha baada ya kuniona nikiwa kwenye rangi yangu ya kitanzania alitabasamu na mimi nikamrudishia tabasamu na kisha aliondoka .

Baada ya kuona ameondoka haraka haraka nilifanya mawasiliano na Janeth nikimuomba aniunganishe na simu yangu nipate kujua mwanamama huyu kila eneo atakalokuwepo na ndani ya dakika chache tu kwa kutumia ‘Face recognition system’ nilikuwa namuona mwanamama huyu akiwa bado yupo ndani ya hii hoteli.

Baada ya kuona zoezi hilo limefanikiwa niliona sina haja ya kuwa ndani ya hilo eneo la mgahawani , nilinyanyuka baada ya kulipa kwa kadi yangu ya benki na kisha nilirejea kwenye chumba changu kupumzika , nilijitupa kitandani huku nikiendelea kuangalia simu yangu kuuona ni eneo gani Rania yupo, lakini niliona bado yupo ndani ya eneo hili la hoteli,sikuona haja ya kuendelea kumfuatilia niliamua zangu kupiga usingizi kwani wakati huo ilikuwa ni saa nne hivi na madakika.

Asubuhi kulivyokucha jambo la kwanza kuangalia ni simu , kuona huyu mwanamama yuko upande gani na niliona bado yupo ndani ya hoteli hii , jambo ambalo lilinipa jibu kwamba huenda kalala ndani ya hoteli hio .

Basi nilioga vizuri baada ya kumaliza nilivuta begi langu dogo la nguo na kisha nilizimwaga nguo zote kwenye kitanda , na baada ya hapo nilitoa kitu kama kichwa cha chajio ya simu na kuchomeka kwenye swichi(switch) ya umeme , na kisha nilitupa taulo pembeni na kubakia uchi , kisha niingiza miguu ndani ya begi lile na kusimama , na ndani ya sekunde chache tu nilikua nimebadilika na kuwa Stephano Lamberk, najua wengi hawanijui ukitaka kujua vyema kuhusu hili jina uwe umesoma kitabu cha waraka wa raisi kabla ya kifo.

Nilikuwa ndani ya FBM nikiwa nimebadilika kabisa kimuonekano, na kuwa mzungu kamili yaani huwezi kujua kwamba nimevaa mask .

Stephano Lamberk ni jina nililopata ndani ya Taifa la uchina , na ndio jina ambalo nilikuwa nikitambulika nalo kama moja ya wanabodi wa kurugenzi ya kampuni ya Huwaei , kama utagoogle jina langu utaweza kunisoma nikiwa moja ya matajri wakubwa ndani ya Afrika wenye umri mdogo .

Jamani hayo sio maigizo ni kweli kabisa nina pesa ndefu ,unaweza ukanijua kama Damiani lakini pia nafahamika kama Stephano Lamberk kijana mwenye pesa kutokea Taifa la Tanzania , na mara nyingi huwa nikihudhuria mikutano yote inayohusu biashara zangu huwa natumia jina na sura ya Stephano Lamberk .

Basi baada ya kuwa kwenye muonekano mwingine , nilivaa suti yangu nadhifu kabisa ambayo ilinikaa vyema , na muonekano wangu wa kihandsome , ni Dhahiri mwanamke yoyote ambae anapenda wanaume wenye mvuto atavutiwa na mimi , usishangae kuna wanawake hawanaga

‘standard`s’ yaani hawajali mwanaume anaetoka nae ilimradi awe na pesa , hawa hawajali mvuto , sasa mimi pesa ninayo , halafu mvuto ni nao yaani ni swala la plus plus kumvutia mwanamke .

Niliangalia simu na kuona bado Milf wangu yupo ndani ya hoteli , hivyo nilitoka , huku nikiwa na nia kwanza ya kwenda kupata kifungua kinywa , swala la pili niliwaza namna ya kukutana na mrembo Rania.

Nilipata kifungua kinywa ndani ya sehemu ile ile ya jana , pasipo kumuona Rania ,lakini sikuwaza sana kwani alionekana kwenye simu , basi baada ya kumaliza nilifika mapokezi na kuulizia kuhusu kwenda eneo la peace lounge .

Ndani ya hii hoteli kulikuwa na hii huduma kwa mtu ambae anataka kutuliza mawazo , yaani kama unamistress yako huko ya maisha au mapenzi basi ukienda hili eneo akili yako inatulia tuli na kufurahia maisha , hii huduma pia inapatikana ndani ya kisiwa cha Ilbiza huko Spain.

Nyie hii sehemu kweli ilikuwa ni kwa ajili ya kutuliza mawazo , bwana bwana , ilikuwa na muonekano flani hivi wa kipekee sana yaani kuna muda ndani ya hili eneo linabadilika linakuwa kama mbuga ya wanyama , lakini pia kuna muda hili eneo linabadilika linakuwa kama upo chini ya bahari , yaani kila aina ya kitu cha kushanganza na kuchangamsha ubongo kilikuwepo , ilikuwa ni kama upo ndani ya Chupa kubwa sana ukiwa umezungukwa na vioo.

Ni sehemu ambayo haikuwa na watu wengi , nadhani ni kutokana na muda ambao niliingia ndnai ya eneo hilo , kulikuwa na baadhi ya watu kulia kwangu wasiozidi kumi , lakini pia kushoto kwangu sehemu ambayo ilikuwa na swimming pool kulikuwa na watru wasiozidi watano , lakini mbele kabisa kwenye bustani kulikuwa na mtu, sio watu, sikuweza kumuona kwa upande ambao nilikuwa nimesimama ila niliambulia kuona kofia kubwa ya mviringo rangi nyeupe(Floppy hat) ikiwa inaonekana kwa nyuma ya kiti cha kuegamia , yaani mtu huyo alikuwa amenipa kichogo , basi niliona nichague mahali pa kwenda , na nikaona ni vyema nikienda mbele yangu kwani ni eneo ambalo halikuwa na watu wengi na mimi pia nilikuwa nikipenda maua .

Baada ya kusogea karibu kabisa yaani kushoto mwa mtu ambaye alikuwa ndani ya hili eneo , upande wa kushoto , moyo ulijikuta ukipiga paah! , kwani mtu ambae nilikuwa nikitamani kuonana nae, kumuona ndio aliekuwa eneo hilo, nilijikuta nikisimama nikimwangalia mwanamke huyu kwa uzuri aliokuwa nao , lakini pia pozi ambalo alikuwa ameweka ndani ya eneo hilo , niliendelea kumsaminisha pasipo yeye mwenyewe kutambua uwepo wangu , huku akiwa ameshikilia glass ya wine .

Baada ya kuona nimeridhika na sinema hio ya bure nilisogea upande wa kushoto wake kwenye kiti cha pembeni na kukaa.

“Mambo mrembo !!”Nilisalimia kwa lugha ya Kiswahili kabisa , na nilifanya hivyo makusudi kwani nilijua mwanamama huyu alishawahi kukaa Tanzania hivyo ni lazima atakuwa anaelewa lugha ya Kiswahili vyema , lakini pia hio ndio gia yangu niliopanga kuingia nayo kwa mwanamama huyu ili kujenga ukaribu .

Basi baada ya kumpa salamu hio aligeuza shingo akiwa kama ni mtu ambae alikuwa kwenye mshangao , na mimi niliupokea mshangao huo kwa Tabasamu.

“Haaa!!!.. Stephano”Kibao jamani kilinigeukia , kwani licha ya kujua kuwa mimi ni tajiri ila sikujua kwamba naaweza kufahamika na mrembo huyu , hivyo namimi ikawa zamu yangu kushangaa , lakini sikutaka kulionyesha hilo kwani nitakuwa nimeonesha udhaifu , nilitabasamu.

“Wow! , sijatarajia kuona mwanamke kama wewe unalifahamu jina langu hususani ukiwa ndani ya nchi ya mbali kama hii”.

“I know you, na nahisi pia unanifahamu kwani kitendo cha kunisalimia kwa Kiswahili pia kimenipa maswali”.

“Naweza kusema ndio au hapana kwa wakati mmoja”

“Kwanini hapana na ndio hakuna jibu hapo”Huku akitabasamu .

“Kwa sababu nina siku moja , saa na dakika chache tokea ni kukufahamu”.Alishangaa huku akionekana kuchangamka tofauti na nilivyomkuta na huo niliona ni ushindi namba moja . “So can you tell me , umenifahamu je within that short time and how ?”Hili swali mara nyingi mtu yoyote akikuuliza , yaani pale unapoita jina lake halafu akashangaa , na akakuuliza hili swali basi jua ana ‘trust issues’ shida ya kutokuamini watu , na kama ni mwanamke jua huenda alishawahi kusalitiwa na mtu anaempenda sana na sisi majasusi mara nyingi tunaangalia na ‘Complexion’ muonekano unaombatana na hili swali .

“ Mazingira na luxuries ndani ya hii hoteli ndio ilinifanya nikufahamu , I am businessman na nimeipenda sana hii hoteli” Mpaka hapo nilikuwa nimejibu maswali yote kwa mpigo, kwa wewe ambae hujawahi kuwa mfanya biashara huwezi kuelewa , na hapa nazungumzia wafanya biashara wale wakubwa,huwa kuna lugha ambazo wafanya biashara wakubwa wanatumia pindi wanapokuwa katika mazunguzo ya kuingia mkataba au dili Fulani, mara nyingi wanakuwa na maneno ya kimikato lakini yaliobeba Zaidi ya maana.

“Karibu sana kwenye hoteli yangu Stephano , I am so happy to meet you in person”.

“Na mimi pia nimefurahi kukutana na wewe mwanamke mzuri unaemiliki hoteli nzuri, lakini nina shauku ya kujua zadi how umenifahamu”.Alipoteza tabasamu jambo ambalo lilinichanganya kidogo .

“Ni hadithi ndefu , but its all about Erick my son”Sasa sehemu ambayo niliitala ndio hapo , niliona sasa kazi yangu inaenda kuwa rahisi , na nilipanga kutumia mbinu zote za kijasusi kumchimba huyu mwanamke , yaani nikitoka katika mazungumzo hayo niwe nimepata mwanga wa misheni yangu.

“Kumbe una mtoto! , vipi kuhusu Erick?”.

“Yess one and only , but I am so sad when I think about him” ndio ninae mtoto mmoja wa kipekee , lakini najikuta nikiwa kwenye huzuni pindi ninapomuwaza”Aliongea na mpaka hapo nilijua kuna jambo kubwa kumuhusu Erick, nilijikuta nikinyamaza kwani mwanamama huyu alionekana akianza kutokwa na machozi , jambo ambalo ndio mtihani mkubwa kwangu , yaani katika maisha yangu nilikuwa ninauwezo wa kumfanya mtu afurahi lakini siwezi kumfariji mtu sasa nashindwa kuelewa maneno yangu yana mantiki lakini ndio hivyo, ndio maana mara nyingi napenda kuongea na watu wenye furaha..

“Niambie Zaidi kuhusu Erick”Niliongea na wakati huu nilikuwa nishanyanyuka nilipokuwa nimeketi na kukaa kwa kupiga magoti pembeni ya kiti chake karibu na tumbo lake ,japo mwanamama huyu kuwa katika hali ya huzuni lakini , alikuwa akinivutia mno , yaani kivazi cha kizungu alichovaa kilifanya nitamani tendo.

“Amepotea, ni mwaka mmoja sasa”Nilijikuta nikishangaa, kwani mpaka hapo niliona kabisa kazi yangu inaanza kuwa ngumu wa kupata hiki kikundi cha The Truth.

“Pole sana, but kwanini kupotea kwa mwanao kuwe ni stori ndefu ya kunifahamu?”.

“Kama unao muda nataka nikuoneshe kitu , nadhani itakuwa rahisi kwa mimi kukuhadithia”Aliongea na nilikubaliana nae.

Basi mwanamke huyu alitangulia mbele akiniacha nyuma nikijilia kwa macho , dakika tatu mbele haatukuwa upande wa hoteli hii , tulikuwa eneo hilo hilo lakini j engo tofauti la pembeni lenye goorofa tatu kwenda juu .

“Hapa ni nyumbani kwangu Stephano , karibu sana”Aliongea na hapa ndipo nilipata kufahamu kwanini wakati nikiwa namwangalia kwenye ramani alikuwa akionekana ndani ya hoteli hii , kumbe alikuwa akiishi hapo.

“Asante sana Rania”Niliongea kisha akaniangalia na kutabasamu.

Haikuwa nyumba lilikuwa ni jumba la kifahari , ni jumba ambalo lilikuwa likivutia mn ,kwanzia muundo wake , mpaka thamani na naksi zilizowekwa ndani ya hii nyumba.licha ya uzuri wa nyumba hii , hamu yangu ya kuoneshwa hiko kitu haikukauka na ilikuwa ikiongezekwa kwa kila dakika , wakati tukiwa tunapanda ngazi za kuelekea gorofa ya juu ya nyumba hii .

Tulikuja kusimama katika chumba ndani ya gorofa ya pili , na Rania alifungua mlango huo kwa kuweka kidole sehemu maalumu ya kutumia ‘fingerprint’ na ndipo tulipozama katika chumba hiki.

Kilikuwa ni chumba kikubwa mno kwa masikini lakini cha kawaida kwa watu matajiri kama mwanamke huyu , upande wa kulia wa chumba hiki ulikuwa na picha ya mchoro wa Kasuku ukiwa umetundikwa , na hapa ndipo nilipokumbuka ‘logo’ ya The truth waliokuwa wkiitumia , muda huu wote wakati tunaingia kwenye hii nyumba nilikuwa nimevalia miwani yangu , kama zile wanazotumia wagonjwa wa macho , lakini hii ikiwa na kazi maalumu kurekodi kila kona ya jumba hii na picha kuzituma katika kitengo chetu cha Mzalendo kwa tafsiri Zaidi .

Tuliweza kuingia kwenye chumba kikubwa kingine yaani ndani kwa ndani , na nilichogundua ni kwamba chumba hiki kina milango miwili , yaani kuna mlango ambao unaweza kutumia kwa kuingilia ukiwa kwenye korido na pia ukiwa ndani ya chumba hiki pia unaweza kutumia mlango wa ndani kuingilia kwenye chumba kingine , ndani ya chumba hiki kulikuwa ni kama ofisi ya Profesa flani hivi kwani kulikuwa na majivitabu mengi sana , tena yale makubwa yaliopangwa kwa mpangilio mzuri kama maktaba.

Nilikuwa nikipitisha macho yangu kwa kila kona ya chumba hiki ili nisije kosa’details’ ya aina yoyote ile , nilijikuta nikisogelea baadhi ya vitabu vile na kuviangalia , nilichogundua ni kwamba karibia vitabu vyote vilikuwa ni vya kihistoria , kuna vilivyokuwa vimeandikwa kwa lugha ya kilatin , lakini pia kuna vilivyoandikwa kwa lugha ya kigiriki na kingereza pia

“Ndio hii picha Stephano” Aliongea Rania na mimi nilijikuta nikigeuka na kuangalia hio picha na hapo ndipo nilipopigwa na mshangao , kwani picha ile ilikuwa ni ya kwangu tena zikiwa mbili ya kwanza ikiwa ni ya sura yangu halisi yaani Damiani ,ya pili ikiwa ni yakwangu halisi, jambo hili nilijikuta likinishangaza sana kwani sikuwa nimetegemea kwamba picha zangu zote mbili ile feki na ile halisi kuwa mahali hapo.

Nilijikuta nikishangaa huku nikisahau kwamba nipo kwenye chumba cha mmiliki wa kikundi cha The Truth, kikundi ambacho kilikuwa maarufu sana katika mtandao wa Deepweb , kwa kuuza taarifa mbalimbali, na kwa maana hio kuonekana kwa picha hizo hapo ilimaanisha moja kwamoja hawa The Truth walikuwa wakinifahamu nje ndani.

Niliangalia picha hii ya Stephano Lamberk kwa muda huku mwanamama huyu akiniangalia na kisha niligeukia picha yangu halisi inayonitambulisha kama Damiani.

“Kuna picha mbili hapa ya kwanagu na hii nyingine , hadithi hio inakaa vipi?”Niliongea hivyo makusudi nilikuwa nikijaribu kupima uelewa wa mwanamke huyu juu ya mimi kuwa na sura mbili, Alitabasamu…

“I know you are Damiani and even yesterday night I recognised you”Nakujua Damiani hata jana usiku nilikufahamu.

SURA YA 08

Ni siku kumi baada ya kikao kilichowakutanisha Profesa Mike Alan , na wenzake wanne wakizungumzia juu ya mafanikio ya Mpango Zero, lakini pia wakiwa wamezungumzia mpango wa kumfanya mtoto Ambrose kupenda historia ya mambo ya kale .

Mwanzo wa wiki yaani siku ya Jumatatu ,ndani ya shule ya North Broward alionekana mwanaume mmoja wa kizungu akiwa anaingia katika darasa ambalo anasomea kijana Ambrose yaani Class A.

Baada ya mwanaume huyu kuingia ndani ya darasa hili alianza kujitambulisha kwa jina la Nick Jonas mwalimu wa maswala ya saikolojia , baada ya mwalimu huyu kujitambulisha aliendelea kufundisha wanafunzi hawa ambao walionekana wachache lakini wenye kusikiliza kwa makini kile ambacho mwalimu Nick anafundisha.

Mwalimu Nick Jonasi alikuwa ni mrefu wa wastani , mwenye nywele nyeusi zilizojaza kichwwa chake na kumfanya kupendeza , alikuwa na umri kimakadirio sio chini ya miaka therathini na tano.

Staili yake ya ufundishaji iliojaa ucheshi iliwafanya wanafunzi hawa wa Class A kuvutiwa sana na mwalimu huyo akiwemo Mtoto Ambrose ,Alikuwa akifundisha mambo ya saikolojia kwa mfumo wa hadithi za zama za kale.

Baada ya nusu saaa ya mwalimu huyu kufundisha alijipatia wasaa wa kufahamiana na wanafunzi hao kwa kila mmoja na ndoto zake za baadae , alijikuta akishangazwa na mengi juu ya yale mambo ambayo watoto hao walitaka kuyakamilisha katika maisha yao ya kimasomo, licha ya kufurahishwa na mambo ambayo wanafunzi hao walikuwa wakimweleza , jambo moja tu ndio lilimshangaza lakini pia na kumfurahisha kwa wakati mmoja ni juu ya mtoto Ambrose , kwani baada ya kuulizwa ni kipi angependa kukifanikisha katika maisha yake ya baadae alijibu hakuwa na chaguo la aina yoyote kwani mpaka wakati huo alikuwa akipenda kila kitu huku akiwa hana sababu ya kuchukua kimoja na kuacha vingine .

Kwa namna ambavyo Ambrose alijibu swali hilo ,Sir Nick alikiri kweli Ambrose alikuwa na akili nyingi , lakini licha ya kukiri hivyo aliona misheni yake ambayo alikuwa amepewa na Umoja Namba Tisini Na Saba anakwenda kuifanikisha kiurahisi sana.

“This mission is going to be interesting and smooth , directing him to stick with Ancienty history is goimg to be easy as of his multiple interest”

“Kumfanya apende mambo ya zama za kale ni jambo rahisi mno kwani mpaka sasa hanakitu ambacho anamalengo nacho au alikuwa anapenda kufanya”

Hio ndio namna ambavyo mwalimu Nick akiwasiliana na mtu ambae hakujulikana kwenye simu akimpa hayo maelekezo , baada ya mwalimu huyu kumaliza kuongea na mtu huyo alitabasamu kwa muda na kisha alichukua mvinyo wake na kunywa na kuketi katika sofa ndani ya nyumba yake hio aliopewa ndani ya shule hio ya North Broward.

“Lakini kwanini ni mfundishe kupenda mambo ya kale ?”Ni moja ya swali ambalo bwana huyu alijiuliza , kwani kazi ambayo alikuwa amepewa na wakuu wake kwa mtoto Ambrose ni kumfundisha kupenda hostoria ya zama za kale ,lakini hakupewa sababu ya kufanya hivyo kwa mtoto huyo ilikuwa ni nini.

Siku iliofuata Sir Nick kama kawaida alikuwa na kipindi na Class A , siku hio aliwahi sana kufundisha na kumaliza na mara baada ya kipindi hicho alimuita Ambrose ofisini kwake kwani alikuwa na mazungumzo nae .

“Ambrose umekuwa mwanafunzi wa kipekee sana niliowahi kufundisha katika swala zima la saikolojia”.

“Kwanini unasema hivyo mwalimu , ni kipi cha kipekee ambacho umepata kuona kutoka kwangu”

“Wenzako wote wana ndoto za kukamilisha katika maisha yao , lakini wewe pekee ndio umesema unapenda kila kitu , kwangu jibu lako ndio la kwanza kupata kutoka kwa mwanafunzi wa umri wako hivyo naweza kusema ni la kipekee sana”.

“ Asante sana mwalimu , lakini kwangu ni swala la kawaida , kwani mpaka sasa sina sababu ya kupenda hiki na kuchukia kile , najiona naweza fanya kila kitu”

“Dunia inavitu vingi ambavyo vinaatakiwa kuendelezwa kila siku na kwa wewe mtu mmoja huwezi kumaliza kufanya kila kitu ,Je utajisikiaje kama kuna kitu kimoja ambacho unaweza fanya na kukupatia majibu ya vitu vyote”.

“Sijakuelewa mwalimu”.

“Utajisikiaje pale utakapo pata ufunguo wa siri ya kila kitu ndani ya dunia hii”

“Nitakuwa na furaha sana mwalimu , kwani nitakuwa nina uwezo wa kufanya kila kitu kwani napenda vyote”

“Ipo siri kubwa ndani ya hii dunia ambayo itakuwezesha kufanya kila kitu kwa ufanisi mkubwa na endapo utaweza kufanya hivyo ni Dhahiri utakuwa mtu mkubwa wa kuogopwa ndani ya dunia hii , na unaweza ukawa mfalme wa Dunia”.

“Ni kweli hayo mwalimu”Awamu hii Ambrose aliulza kwa kwa hali ya shauku kubwa , na jambo hili lilimfanya mwalimu huyu , kufurahi kwania aliona kazi yake ya kumfanya Ambrose kupenda mambo ya kale inakwenda vizuri .

Moja ya falsafa ya mwalimu Nick katika shule zote alizowahi kufanya kazi na kutatua matatizo mbalimbali ya maswala ya kisaikolojia , alikuwa akiamini kwamba kuna sababu moja kubwa ambayo inamfanya mtu kupenda kitu sana kuliko vitu vingine , na sababu hio inajengwa na tamanio lenye nguvu(Motivated desire),huku akiamini kwamba tamanio lenye nguvu mara nyingi huchipua kutokana na shauku ya mtu juu ya kitu Fulani(Curiosity).

Hivyo kitendo cha kumwambia Ambrose kwamba kuna ufunguo wa kumfanya kufanya kila kitu katika uso wa dunia na kuwa mtu mkubwa duniani , ilikuwa ni kujenga shauku yake ili hatimae kuweza kumjengea tamanio lenye nguvu.

Alikuwa ashamsoma tabia ya Ambrose tayari na kugundua ni mtu ambae anapenda vitu vikubwa , na kitendo cha kumjibu kwamba alikuwa akitaka kufanya kila jambo katika uso wa dunia , swala hilo lilimfanya amtamue Ambrose kama kijana mwenye ‘ambition’ kubwa . na hilo aliona ni jambo ambalo litamuwezesha Zaidi katika kumfanya kijana huyo kupenda historia ya mambo ya kale.

“Naongea ukweli Ambrose ,, hii ni siri ambayo nakwambia sasa , na hupaswi kumwambia mtu yoyote yule nikikueleza siri hii ,nimekuchagua wewe kwani unaonekana kuwa na akili nyingi kuzidi wenzako wote”

“Ni siri gani hio mwalimu , nahitaji kujua”.

“Sio rahisi hivyo Ambrose kukuambia siri hii kubwa , kwani ili kuielewa lazima kwanza upende kusoma mambo ya historia ya kale , ukielewa kwa ufasaha mambo ya historia ya kale ndio utakuwa umekidhi vigezo vya kujua siri hii , na nitakupeleka sehemu ambayo utakutana na mtu ambae anafahamu siri hio”.

“Nina weza kufanya hivyo mwalimu , lakini mpaka nipate uthibitisho wa jambo unalolisemea kama lina ukweli ndani yake”Aliongea Ambrose huku akionekana kumaanisha kile ambacho anaongea , na jambo hilo kwa mwalimu Nick lilimfurahisha , kwani kwanza hakutegemea kwa mtoto kama huyo ambae akili yake ilikuwa kubwa kuwashawishika bila ya kuwa na ushahidi .

Basi baada ya mwalimu Nick na Ambrose kufanya mazungumzo hayo , kazi ilibaki kwa Nick , swala la Ambrose kutaka ushahidi wa kile alichokuwa anakizungumzia lilikuwa ni kazi kwani mpaka wakati huo hakujua ni kwa namna gani anaweza kupata ushahidi ambao unaweza kumfanya Ambrose kuukubali.

Baada ya kutoka kazini alihitaji kuoanana na boss wake aliempa kazi hio , alimtafuta kwa simu na kuweka miadi ya kuonana muda wa jioni ndani ya mgahawa wa Rosela katikati ya jiji la Frolida .

Muda wa saa moja za jioni kwa saa za Kimarekani , Nick Jonasi alionekana akiwa ndani ya mgahawa huu tulivu kabisa wenye mandhari ya kuvutia , na nadhani hii ndio sababu ya watu hawa kukubaliana kukutana mwamahali hapo , kwani ndani ya hili eneo kulikuwa na utulivu wa ahali ya juu sana , japo kulikuwa na watu wa mbalimbali waliiokuwa wakipata kahawa , lakini hakukuwa na makelele.

Bwana Nick ambae tunamjua ni mwalimu wa saikolojia katika shule anayosomba Ambrose alikuwa ameketi ndani ya mgahawa huu wa kisasa upande wa kulia mbele kidogo na kaunta ya vinywaji , alionekana kupata kahawa huku akimsubiria mtu ambae alikuwa na miadi naye ya kukutana ndani ya muda hio , aliangalia saa na kuona alikuwa amewahi kuliko isivyokawaida .

Lakini mara baada ya kufika muda saa kumbi na mbili na dakika hamsini na tisa , alionekana mwanaume mfupi wa wastani alievaliaa jacketi refu jeusi ambalo limemziba miguu , bwana huyu alikuwa ni wale watu ambao washavuka daraja la ujana miaka mingi , kwani kichwa chake cha uwararaza kilichojaa mvi kilikuwa kikiongea kila kitu .

Baada ya bwana huyu kuingia moja kwa moja alinyoosha mpaka sehemu ambayo alkuwa amekaa Nick , na mara baada ya kufika aliweka begi lake aina ya Briefcase nyeusi pembeni karibu kabisa na miguu ya Nick na kisha aliketi huku wakisalimiana.

Mzee yule na yeye aliagiza kahawa yake ya kuzugia na baada ya hapo waliingia kwenye mazungumzo na hapo ndipo Nick alipomueleza bwana huyu juu ya mazungumzo yake na mtoto Ambrose , baada ya mzee huyu kuelewa hitajio la mwalimu Nick alivuta mkoba wake aliokuja nao na kuufungua na kutoa kitabu na kumpatia mwalimu Nick.

Juu kabisa ya kitabu hiki kulikuwa na nembo kubwa ya pete yenye mchoro usioeleweka ,mwalimu Nick alikiangalia kitabu hicho na kugundua kuwa kilikuwa kimeandikwa kwa lughaambayo hakuwa na uelewa nayo .

“Huo ndio uthibitisho ambao utamfanya Ambrose kukubaliana na wewe”..

“Huu unawezaje kuwa uthibitisho , naona ni kitabu ambacho kipo kwa lugha ambayo sijawahi pata kuiona”

“Mpe kijana kazi ya kutafuta maana ya hio lugha na njia pekee ambayo anaweza kupata kufahamu hio lugha ni kwa njia ya kusoma mambo ya historia ya kale , akiweza hilo misheni yako itakuwa imekwisha”Aliongea mzee huyu na kisha alinyanyuka akimuacha mwalimu Nick akiwa kwenye maswali , alikiangalia kitabu hicho na kujikuta akishangaa kile kilichoandikwa katika hiko kitabu , hakuelewa lugha iliokuwa imetumika ndani ya hiko kitabu ilikuwa ni ;iugha gani .Siku iliofuata mwalimu Nick aliingia darasani kama kawaida kwa ajili ya kipindi na wanafunzi wa Class A.

Baada ya kipindi alimwita tena Ambrose kwa ajili ya kuendeleza mazungumzo yao walioishia siku ya jana , hakutaka sana kuongea mengi , alichofanya ni kutoka kile kitabu na kumkabidhi Ambrose.

“HIko ni kitabu ambacho lugha yake mpaka sasa haifahamiki ni lugha gani , wanahistoria wa mambo ya kale wametafua namna mbalimbali ya kujua lugha hio lakini mpaka sasa hakuna ambae alipata kujua kupambanua lugha hio”.

Swala lile lilimshangaza mno kijana Ambrose , hakuamini kwamba lufha ilioandikwa katika kitabu hicho ilikuwa haifahamiki kama mwalimu wake anavyosema .

SURA YA 09.

MIAKA KUMI NA MBILI NYUMA.(kutoka kitabu cha 2HOURS OF MEMORIES kilichoandikwa na mtunzi ISSAI SINGANO)Rania anasimulia…..

Ni miaka kumi na mbili nyuma nilipoingia kwa mara ya kwanza ndani jiji la Sydney kutokea Tanzania , nchi yangu ambayo niliona ni chungu sana kwa mimi kuishi kutokana na mambo makubwa yalionitokea ya kuumiza .

Jambo lililonileta ndani ya taifa hili La Australia mbali na Nchi yangu ni kwa ajili ya kuishi , lakini pia kupata wasaa mzuri wa kupona kwa yale ambayo niliweza kuyapitia wakati nilipokuwa nchini Tanzania .

Niliingia katika nchi hii nikiwa na mwanangu Erick aliekuwa na umri wa miaka miwili tu, kwa wakati huo mwanangu Erick ndie aliekuwa faraja yangu kwa kipindi chote nilichoweza kufika ndani nya taifa hili , kwani tokea nifike sikuwa na kazi maalumu ambayo nilitaka kuanza kufanya , kwani akili yangu kwa wakati huo haikuwa sawa nilikuwa kwenye majuto makuu kwa yale ambayo yalisababishwa na familia yangu .

Ilinichukua muda wa miezi minne kwa akili yangu kukaa sawa , unaweza ukajiuliza kwa muda wote huo nilikuwa nikiishi vipi , jibu ni kwamba nilikuwa nikiishi hotelini kwa wakati wote huo kwani nilikuwa na pesa ya kutosha kuishi ndani ya jiji hili linalosifika kwa kuwa ghali Zaidi duniani.

Basi baada ya miezi minne ya kuwa ndani ya Sydney niliweza kukutana na Rasi ndani ya hoteli ya Four Season hoteli ambayo nilikuwa nikiishi kwa muda wote wa miezi hio minne , Ras ni moja wanaume wacheshi sana ambao nimewahi kukutana nao , lakini pia naweza kusema ni rafiki yangu wa kwanza kuwa nae ukiachana na Peter ambae ndie baba mzazi wa Erick ambaye na yeye pia ndie aliechangia mimi kuja ndani ya taifa hili.

Ras alikuwa ni Floor manager ndani ya hoteli hii , na floor ambayo alikuwa akisimamia ndio hio ambayo nilikuwa nimechukua chumba , na naweza kusema hilo lilichangia sana kwa mimi kufahamiana na Rasi kwani nilikuwa mteja wa pekee ambae nilikuwa nimeishi kwa miezi mingi ndani ya hoteli hio .

Mwanzo wa kufahamiana na Ras ndio mwanzo wa akili yangu kuamka kibiashara Zaidi , na hili ni kama Rasi aliliona kwangu kwamba nilikuwa nikiwaza kufanya biashara , kwani mara nyingi kila nilipoweza kukutana nae alikuwa akuzungumzia maswala ya biashara na hii yote ni pale nilipomueleza nia yangu ya kutaka kuwekeza ndani ya taifa hili.

Nakumbuka siku ambayo nilimueleza nia yangu ya kuwekeza swali moja kuitoka kwake lilikuwa ni kama ninao mtaji kiasi gani , na nilipomtajia kwamba nilikuwa na mtajji wa kiasi cha Dollar Milioni Hamsini , ndipo alipoweza kushangaa sana lakini pia kufurahishwa kwa wakati mmoja na nadhani kilichomfurahisha kwa wakati huo ni kwamba aliona fursa kupitia mimi .

Siku moja Rasi aliomba kukutana na mimi kwa ajili ya mazungumzo , na mimi nilimkubalia na tuliweza kukutana ndani ya hoteli hii kwenye mgahawa , siku hii alikuja sio kama mfanyakazi kwani alikuwa amevalia kiraia kabisa, jambo ambalo alinieleza siku hio ni juu ya hoteli ya Avani Park ilioukuwa imefilisika na ilikuwa sokoni kwa kuuzwa .

Siku hii ndipo nilipokuja kugundua kuwa Ras alikuwa ni kichwa likija swala la biashara , kwani alinipa maelezo yalioshiba ya sababu ya mimi kununua hoteli hii ambayo ilikuwa ikiuzwa kwa bei rahisi sana nusu ya pesa ambayo nilikuwa nayo .

Baada ya kurishidhishwa na maelezo ya Rasi hatimae alipanga kikao cha kunikutanisha na mmiliki wa hoteli hio kwa ajili ya mazungumzo ya bei , mmiliki alikuwa ni mmama Profesa kutoka chuo kikuu cha Monash Alikuwa akifahamika kwa jina la Victoria Lambert mwenyeji wa jiji la Mellbourne , maongezi yangu na mwanamama Victoria yalienda vyema sana kiasi cha kwamba tulijenga ukaribu kwa masaa kadhaa tu ya mazungumzo yetu.

Basi niliweza kununua hoteli hio kwa asilimia themanini huku mwanamama huyu akibakisha asilimia 20 kwahio kwanzia siku mbili mbele za kusaini makaratasi ya manunuzi nikawa mmiliki kwa asilimia thamanini za hoteli hii ambayo nilikuja kuibadilisha jina na kuita Park Hyatt Sydney.

Nilipangua utendaji mzima wa hoteli hio huku nikimuweka Ras kama Manager mkuu , na katika hili sikumpendelea kabisa kwani alikuwa akitosha kabisa katika nafasi hio na hili liilidhihirika baada ya mwaka mmoja wa kuchukua hoteli hii , kwani kwa ukarabati tuliofanya na uboreshaji wa huduma iliweza kuvutia wateja wengi sana ndani na nje ya Australia , jambo ambalo mimi mwenyewe lilinishangaza sana .

Kwani ndani ya miezi kumi na nne ya umiliki wangu matajiri wakubwa waliweza kufikia ndani nya hoteli hii ,lakini pia hoteli yangu iliweza kushinda zabuni nyingi za kimataida na za ndani ya nchi .

Mwanzo wa mafanikio makubwa niliokuwa Napata ,ndio mwanzo wa kusahau mambo yalionitokea ndani ya taifa la Tanzania, na kwa kiasi Fulani furaha yangu kurudi upya , na kwa kipindi chote hicho Ras alikuwa rafiki yangu mkubwa , japo alishawahi kunitongoza lakini nilimkatalia katakata , kwani ndani ya moyo wangu licha ya mambo ambayo Peter alinifanyia sikuwahi kumsahau hata mara moja , na nilijiapiza sitokuja kuwa na mwanume mwingine tokea pale mume wangu Hemedi alipofariki Dunia.

Upande wa Erick ukuaji wake ulikuwa ni wa kushangaza sana kuliko isivyo kawaida na hili halinikushangaza mimi tu lakini pia madaktari wengi wa hospitali ya Randwick ambayo nilikuwa nikimpeleka katika ratiba za ufuatiliaji wa ukuaji wake .

Ndani ya miaka mitano ya Erick alikuwa akiongea kama mtu mzima , na alikuwa na kichwa chepesi mno katika kukumbuka vitu, na nilipongezwa sana na walimu wa Sydney Grammer School kwa kupata bahati ya kuwa na mtoto kama Erick , jambo hilo kwangu lilikuwa la lfaraja mno , kwani ukichana na mambo ambayo yalinitokea katika maisha yangu ya nyuma , kwangu Erick ni kama bahari Mungu alionipatia.

Muda ulisonga miaka ikapita , na ukuajji wa Erick ukaendelea kushangaza wengi husani katika maendeleo ya shule.

Nilichokuja kugundua ni kwamba Erick alikuwa na akili nyingi sana na naweza kusema kwamba ni jiniasi kwani baada ya miezi kadhaa ya mwanangu kuhudhuria shule ya Grammer School , alikuwa amewaacha mbali sana wenzake ambao alikuwa akisoma nao darasa moja , lakinii pia niliweza kuletewa ripoti ya maksi alizopata mara baada ya kupimwa IQ(Intelligency Quontient ),maksi zake zilikuwa ni 140 maksi ambazo mwalimu Ashley aliniambia ni kiwango cha juu kabisa kwa binadamu wenye uwezo mkubwa wa akili .

Jambo hilo kwangu lilinifurahisha sana , lakini naweza kusema ndio mwanzo wa msururu wa matukio mbalimballi ambayoo yalikuwa yakitokea kwa mwanangu , kwani mara nyingi alikuwa akifuatwa na watu mbalimbali , wengine wakiwemo watu wakubwa wakimuhoji vitu mbalimbali , jambo ambalo lilikuwa likinitia wasiwasi juu ya usalama wa mwanangu ,, nilijaribu kuongea na walimu wa Sydney Grammer School na waliishia kunitoa hofu kwamba sina haja ya kuwa na wasiwasi kwani wanatoa ullinzi wa kutosha kwa wanafunzi wanaosoma ndani ya shule hio , na mimi niliona kama na kuwa ‘paranoid’ hivyo niliona jambo la kutoa wasiwasi wasi wangu juu ya usalama wa Erick ni kujikita katika biashara Zaidi .

Baada ya mwaka mmoja kupita yaani mwaka wa sita wa mimi kuwa ndani ya nchi hii ya Australia niliweza kumuhamisha Erick kutoka shule aliokuwa anasoma na kwenda kusoma katika shule ya vipaji maalumu , hii ni shule ambayo ilikuwa ikimilikiwa na Victoria mwanamama Profesa ambaye aliniuzia hoteli ambaye naweza kusema kwamba alikuwa ni mmiliki mwenza ,yeye ndio alioniushauri kumpeleka Erick katika shule yake iliokuwa ikifahamika Hope School of Elite Kid (HSOEK),Ilikuwa ni shule kubwa na yenye hadhi ndani ya taifa hili la Australia na ilikuwa ikifahamika sana ndani na nje ya nchi , ilikuwa na level zote mpaka High School na kilichonifurahisha na kunishawishi kumpeleka Erick katika shule hiii ni historia kubwa ya shule hio katika kutoa wanafunzi bora kitaifa ambao walikuja kufanya mageuzi katika Nyanja mbalimbali.

Biashara zangu zilikuwa zikisonga vyema jambo ambalo pia lilikuwa likinishangaza lakini pia baadhi ya wafanya biashara wenzangu kunishangaa kwa hoteli yangu kukua sana ndani ya muda mfupi huku wengi wao wakitaka kujua ni siri gani ambayo ninaitumia mpaka kufanya biashara kuniendea vizuri ,lakini sikuwa na majibu sahihi ya kuwapa , kwani kama ni ubora wa huduma hoteli nyingi ndani ya Jiji la Sdney zinakuwaga na huduma zenye ubora wa hali ya juu sana na naweza kusema hata kuzidi hoteli yangu ,japo hata hoteli yetu ilikuwa na huduma bora.

Miaka ilisogea biashara zilienda vyema , lakini pia Maendeleo ya Erick yalikuwa ni ya kufurahisha sana , kwani aliendelea kuwashangaza watu kwa uwezo wake wa kufikiria na kutatua matatizo mbalimnbali , alikuwa akipenda sana Masomo ya computer na hili naweza kusema kwamba ni kama alikuwa amerithi kutoka kwa baba yake , kwani yeye pia alikuwa akipenda sana maswala ya Computer na hata kipindi ambacho ninakutana nae kwa mara ya kwanza ni kutokana na tatizo la kitehama lilillotokea ndani ya Benki yetu , tatizo ambalo liliwashidna wafanya kazi wa ndani ya benki.

Baada ya Erick kumaliza masomo yake ndani ya HSOEK moja kwa moja alijiunga ndani ya chuo cha Monash kilichokuwepo ndani ya jiji la Melbourne akichukua kozi ya maswala ya komputa (Computer Science).

Alisoma ndani ya chuo hicho mpaka kumaliza akiwa ni kinara kati ya wanafunzi wote kwa kupata GPA kubwa , jambo ambalo liliwainua wanasayansi kutoka makampuni makubwa ndani ya nchi na nje wakitaka kumuajiri katika kampuni zao za maswala ya kiteknolojia , lakini kwa mwanangu Erick alikuwa hataki kusikia swala la ajira jambo ambalo hata kwangu halikunishangaza kwani hata mimi pia nilikuwa nikichukia sana maswala ya kuajiriwa , hivyo nilipanga kumsapoti kwa namna yoyote ile pale tu atakapo taka kujiajiri.

Siku moja wakati nikiwa nyumbani nilishangaa kumuona Erick akiwa nyumbani , jambo ambalo siio kawaida yake , kwani hakuwa mtu wa kukaa kabisa nyumbani , na nilikuwa nikimuona mara chache sana na hata mara nyingine wakati nikiwa nimemmisi kumuona huwaga nafunga safari na kwenda kumuona Mellbourne , naweza kusema japo ya kwamba alikuwa akionesha kunijari sana na kunipenda kama mama yake lakini hakuwa na ile tabia ya kuja kunisalimia mara kwa mara , na hata chumba chake kilikuwa kipweke muda mwingi , na pia nilikuja kugundua kuwa Erick alikuwa ni mtu wa wanawake sana , alikuwa akibadilisha sana wanawake , hii tabia nilijaribu kumkataza na kumuonya lakini hakuiacha ., ni kama ilikuwa starehe yake , nilipunguza hata kumpa hela nyingi lakini nalo halikusaidia kwani alizidi kunishangaza kwa namna ambavyo alikuwa akijitanua katika visiwa mbalimbali ndani ya nchi na nje ya Nchi , swala ambalo lililikuywa fikirishi kwangu pia ni kwa namna gani anapata pesa , lakini sikuweza kupata jibu kwani kila nilipokuwa namuuliza alikuwa akinipa jibu kwamba nimuache na maisha yake , na hahitaji pesa yangu kuijua dunia .

Sasa siku kumkuta nyumbani jambo hilo lilinishangaza kidogo ,, lakini pia lilinifurahisha kwani nilikuwa nimemisi uwepo wake ndani ya nyumba , baada ya kusalimiana nae , hatimae aliniambia nia yake ya kurudi nyumbani , jambo ambalo lilinifurahisha na kulipokea kwa mikono miwili , lakini hakuishia hapo tu aliweza kuniomba kiasi kikubwa cha pesa , ilikuwa ni dolla za kimarekani milioni kumi , kiasi ambacho kilikuwa kikubwa sana na nilitaka kujua sababu ya yeye kutaka kiasi hicho cha pesa na jibu alilonipa ni kwamba alikuwa akitaka kufungua kampuni yake , kwangu swala hilo lilinifurahisha mno kwani ndio jambo ambalo nilikuwa nikilisubiria sana kutoka kwake .

Sikutaka kumuhoji sana kwani mwanangu alikuwa na tabia ya kususa pale unapomuhoji sana , na mimi kwaua kipindi hicho nilikuwa na pesa nyingi na nilikuwa moja ya wawekezaji wanaochipukia wakubwa ndani ya Austraslia basi niliandaa kiasi hicho cha pesa na nikamuingizia kwenye akaunti yake.

Kama alivyo ahidi alikuwa amebadilika kabisa alikuwa akiishi nyumbani na hata ile tabia yake ya kutoka toka na wanawake maeneo mengi ya starehe aliacha, alikuwa na mwanamke mmoja tu ambae alikuja kunitambulisha kama mpenzi wake , alikuwa ni mzungu mwanadada aliekuwa akifahamika kwa jina la Sarah.

Siku moja niliingia kwenye chumba chake na hii ni mara baada ya kumgongea sana pasipo kufungua jambo lilonitia wasiwasi , sikuwa na utaratibu wa kuingia kwenye chumba chake japo ya kwamba vyumba vyetu vilikuwa mkabala .

Siku hio ndio nilishangaa mno ndani ya hiki chumba kwani nilikuta kilikuwa kimezagaa makaratasi mengi ambayo yalikuwa yametupwa chini mengine yakiiwa na michoro mbalimbali , mingine ikiwa ya ndege , mingine ikiwa ni ya kitaalamu ambayo sikuielewa , lakini pia niliweza kuona mavitabu mengi ambayo yapo juu ya meza yakiwa yametapakaa mpaka juu ya kitanda yakiwa yamefunuliwa, lakini jambo ambalo nilishangaa pia ni kwamba vitabu vingi vilikuwa ni vya lugha ya Kilatini na kigiriki ambavyo nilishindwa kusoma .

Nilisogea ndani ya chumba chake huku nikimwita , na baada ya kumkosa nilisogea kwenye chumba ambacho nilikitenga kama sehemu ya kusomea na hapo ndipo nilipo mkuta akiwa amevaa maheadphone .

“Yeeeeeessssss….!!!!!. Yes , Yes , Yes……. “ Ni maneno aliokuwa akitamka na ni kama mtu ambaye alikuwa akitafuta jambo Fulani na wakati huo alionekana kufanikiwa na alikuwa akishangilia , na hakujua kama nipo na mwangalia mpaka pale ambapo aligeuka na kuniona na alinikimbilia na kunikumbatia huku akionyesha kushindwa kuzuia furaha yake , jambo ambalo kwangu liliongeza shauku ya kutaka kujua ni kipi hicho kilicho mfanya kufurahi kwa namna hio.

“Mom ! I did it , I made it”

“You did what Erick , tell me” niliongea na kumfanya aniangalie na kisha akatabasamu na kurudi kwenye meza na kuchukua karatasi tatu na kunionyesha .

“Hii ndio alama inayowakilisha kampuni yangu (logo)” Aliongea huku akinionyesaha ndege aina ya Kasuku akiwa amesimama kwanye kijiti , karatasi ya pili alinionesha ikiwa na jina la kampuni lililosomeka kwa kama The Truth, Karatasi ya tatu ilikuwa na maandishi yaliosomeka kwa jina ONLY GIFTED KNOW THE TRUTH(akimaanisha kwamba waliozaliwa na kitu cha ziada ndio wanaoujua ukweli) ,nilishangaa lakini na kutabasamu kwa wakati mmoja huku kilichonifanya kutabasabu siku hio hata sikuwa nikijua . ni nini lakini nilichokuja kugudnua baadae ni kwamba , kwa miaka mingi sikuwahi kumuona Erick akiwa kwenye furaha ya aina hio na niliamini kwa kitu ambacho amepatia huenda kikawa kikubwa , kwani nilikuwa nikijua kuwa ana uwezo mkubwa wa akili na siku zote watu wenye akili kubwa ni mara chache sana kueleweka kwa kile ambacho wanakifanya na mimi japo ya kuonionesha makaratasi hayo nilitabasamu kuwa nina furaha kwa ajili yake kwa kila anacho kifanya , lakini ukweli ni kwamba sikuona mantiki kabisa kwa kile alichonionesha.

“Mom uneweza usielewe nilichokuonesha , lakini vitu vitatatu vinamaana kubwa sana ambazo kama unamacho ya kuona utaelewa ni kama mchoro wa Monalisa”.

“Nieleweshe nipate kuelewa maana hii hali ya hapa ndani naamini ulichofanya nikikubwa”

“Even more mom , Do you know there is only one Secret in the world that hold all the truth ?”Ni Zaidi ya hayo mama ,Je unajua kwamba dunia ina siri moja kubwa ambayo inabeba ukweli wa mambo yote”

“Ukweli upi Erick?”

“Hilo ndio jina la kampuni yangu , Kampuni yangu itakuwa ni kwa ajili ya kutambua ukweli unaoonekana na ule usio onekana ,Ukweli ni nguvu , ukweli ni madaraka , ukweli ni utajili katika dunia hii na ni wachache sana katika hii dunia wanaujua ukweli na wanatafuta namna ya kuujuha ukweli , watu watahitaji ukweli kwa namna yoyote ile iwe ni kwa kununua ama kwa njia nyinginezo.Watu ambao wanakitu cha ziada ndani yao ndio wamepewa uwezo wa kuujua ukweli ,Ukweli usionekana ndio unanguvu kubwa ndani ya dunia hii , wanaoujua ukweli ni watu wenye madaraka makubwa ndani ya dunia hii na hawa watu wanaulinda ukwei huo usionekane ili wawe ndio pekee wenye nguvu Zaidi katika dunia”.

Yalikuwa ni maneno mengi sana kutoka kwa Erick lakini mpaka wakati huo bado sikuelewa anachomaanisha , japo maneno yake yanamaana kwa kiasi chake , lakini kwa upande wa biashara sikuona namna ambavyo atatengeneza pesa na hio ngio mantiki ambayo nilikuwa nikiitafuta katika maneno yake , lakini sikuipata .

Sikuweza kuongea sana na Erick , nilimuacha aendelee na mambo yake huku nikimwambia kuwa mimi nataka mafanikio yanayoonekana sio hadithi na hilo aliniahidi kwa asilimia mia moja kwamba atanithibitishia .

Zilipita siku mbili tena nilienda kumuamsha Erick , lakini ile nafika kwenye chumba chake huku nikijua kwamba yupo ndani , nilimuona akiwa ndio anafika , huku akiwa ameshhikilia karatasi mbili , nilisalimiana nae na kisha aliniambia anakitu anataka kunionyesha na mimi sikuwa na hiyana , niliingia ndani ya chumba chake ili kuona hiko kitu .

Zilikuwa ni picha mbili alizonionesha na picha hizo zilikuwa za mwanaume ambaye aliniambia kuwa mwanaume huyo alikuwa ni Mtanzania ambae amevaa Mask , sikumwelewa , lakini aliendelea kunionyesha kwa ushahidi huku akiniambia watu wawili tofauti ambao nawaona katika picha ni mtu mmoja , na kilichhofanya watu hao kuonekana tofauti huku akiwa mtu mmoja ni teknolojia , alimalizia na kuniambia swala hilo ndio kama swala analozungumzia yaani ninachokiona ndio ukweli unaonekana na nisichokiona kwa mtu huyo kuwa mtu mwingine ndio ukweli ambao haunekani , huku akimalizia kwamba kisicho onekana ndio nguvu ya mtu huyo .

Nilimuuliza kuhusu jina la mtu huyo na hapo ndipo alipo nitajia jina la Damiani Raban na Stephano Lamberk, kwanzia siku hio sikumwelewa na kumuamini kabisa , kwani watu ambao alinionyesha walikuwa ni watu wawili tofauti ambao sikuwa nikiwajua .

Siku moja ikiwa ni Jumapili nikiwa naelekea kanisani , aliamka mapema Erick na kuniaga kwamba anaenda kutafuta ukweli , huku akiniahidi kwamba atarejea , hio ndio ikawa siku yangu kuonana na mwanangu , kwani kwanzia siku hio mpaka sasa ni miaka miwili sijawahi kuonana na Erick.

Katika haarakati za kumtafuta Erick ndio nilianza kufatilia picha ambazo alikuwa ameweka chumbani , picha ya mtu ambae aliniambia kwamba alikuwa ndio Damiani Rabani ambaye pia anafahamika kwa jina la Stephano Lamberk,dhumuni ilikuwa ni kutaka kujua kile ambacho alikuwa akimaanisha Erick kwani mpaka wakati huo sikuwahi kumuelewa na hata hela ambayo nilimpatia kwa ajili ya ufunguzi wa kampuni sikujua iko wapi kwani kwa kufaatilia akaunti za kibenki niligundua kuwa zilikwisha kutolewa , lakini pia nilijaribu kuwahusisha polisi na wanausalama wa taifa , na wao pia hawakua na majibu ya kueleweka kwa uchunguzi waliokuwa wameufanya .

Katika kufatilia habari ya Stephano Lamberk na Damiani Rabani ndipo nilikuja kupata kitabu cha WARAKA WA RAISI KABLA YA KIFO CHAKE kilicho andikwa na mwandishi ISSAI SINGANO (SINGANOJR) nilisoma kitabu hicho lakini bado sikuamini juu ya FBM mpaka siku ambayo niliweza kuonana na mtu ambaye alikuwa akizungumziwa na Erick , lakini pia na mwandishi SINGANOJR ndani ya hoteli yangu ya Hyat Park.

SURA YA 10

Kwangu simulizi hii ya huyu mwanamama ilikuwa ni ya kusisimua sana na kushangaza kwa wakati mmoja hususani kwa upande wa kijana Erick , mpaka wakati huo nilikuwa na ufahamu nusu wa kwanini Erick alianzisha kampuni aliokuwa ameiita The Truth .Licha ya kwamba nilikuwa nimejua nia yake kubwa ni kuujua ukweli lakini katika simulizi hii nijikuta nikijua mambo makuu matatu kuhusu Erick , jambo la kwanza Erick alikuwa ni mtu mwenye akili kubwa sana yaani ‘Genius’ na mimi katika maswala ya kijasusi haya mamb huwa mara nyingi yanazingatiwa sana , kwa mfano tu nchi ya Marekani wana idara za maswala ya kiusalama kwa mfan FBI , CIA ,NSA sasa katika harakati zote za maswala ya kudahili(Recruitment/Admission) kigezo kikubwa ni akili ya mtu , ukionekana una akili kubwa(IQ) , pamoja na baadhi ya vigezo vingine mfano kuwa na afya njema basi unakuwa ‘best candidate’ kwenye hizi idara .Si kwa Marekani tu , mashirika mengi ya kijasusi duniani huwa yanachukuwa watu wenye akili kubwa kwa mfano MOSSAD kutoka Israeli ,M16 kutoka

England na hata TISS kutoka Tanzania na hii yote ni kwamba hizi idara za kijasusi mara nyingi ni kama uhai wa taifa katika Nyanja zote ndio maana hata kwa sisi Mzalendo ajenti wetu ni majiniasi.

Swala la pili nililgundua kutoka katika simulizi hii yta mwanamama Rania ni ‘Ambition’ nashindwa hata kualiongelea kwa lugha yetu ya Kiswahili hili neno lakini maana yake ni kwamba ni mtu mwenye malengo makubwa yenye msukumo ndani yake , hivyo niligundua kuwa licha ya kijana huyu Erick kupewa akili kubwa ni kwamba alikuwa ni mtu mwenye malengo makubwa sana na hili linamfanya kuwa mtu hatari sana, kwani mara nyingi watu wa aina hii watafanya kitu chochote kile ilimradi kukamilisha malengo yao hata kama ni kutumia njia za giza (njia zisizohalali).

Swala la Tatu nililogundua ni kwamba licha ya kijana Erick kuwa katika umri mdogo lakini alikuwa ni mtu alietengeneza koneksheni na ni mtu ambae anaiafahamu dunia vyema na kwa simulizi ya mwanamama Raniua naungana na Erick pale aliposema kwamba Ukweli usioonekana ni Nguvu(Power) hili naliunga mkono kwa asilimia kubwa sana kwani katika uliumwengu wa kijasusi hili pia kwetu ni sehemu ya somo , Watu wanaojua ukweli au siri kubwa ndani ya hii dunia ndio watu wenye nguvu kubwa , hivi unadhani ni kwanini mashirika makubwa kama Freemasons , UMOJA NAMBA TISINI NA SABA ,Illuminat na mengineyo wanakuwa ni watu ambao hawaonekani , jibu ni kwamba kitu kisichoonekana kinakuwa na nguvu kubwa sana , na hili sitaki hata nikulazimishe kuniamini lakini unaweza ukajiuliza swali moja je ushawahi kumuona Mungu????.

Hivyo ukweli usionekana (Hidden Truth) ndio wenye nguvu kubwa na ndio unaoendesha dunia, lakini ndio unaofanya taifa na taifa kuogopana , wengi hapa ni mashahidi leo hii hakuna anaejua uwezo halisi wa kijeshi wa Marekani , au Urusi , au china hii yote ni kwamba kuna vitu ambavvo havionekani kwenye nchi hizo na hizi idara za kijasusi mara nyingi zinajikita kujua hivyo vitu visivyo onekana.

Hivyo kwa kijana Erick kuwa na malengo ya kuutafuta ukweli namuona ni kama Jasusi wa kujitegemea , kitendo cha kujua uhalisia wangu mpaka hapo ni kwamba kijana huyu kampuni yake hii ya The Truth hakuianzisha kizembe zembe, ninacho amini ni kwamba mpaka kupata wazo la kuanzisha hii kampuni au kikundi ni kwamba alianza kukutana na jambo , na hilo jambo huenda lilikuwa kubwa kwake na lilikuwa likihusiana na ukweli uliofichika na katika hilo jambo alinusa nguvu kubwa ilioambatana na kweli hio aliokumbana nayo .Kwangu hayo ni makisio tu. “Nimeguswa sana na hii simulizi ya kijana Erick”Niliongea huku nikimwangalia mwanamama huyu , na wakati huu tulikuwa tumeketi muda wote kwenye kitanda cha Erick ndani ya chumba chake huku mbele kabisa kukiwa na picha ya Kasuku pembeni kukiwa na picha zangu zilizotundikwa .

Mwanamama huyu alikuwa akionesha hali ya huzuni sana , lakini sio huzuni tu lakini pia alionyesha ishara kama zote za upweke , na jambo hili lilidhihirika ndani ya nyumba hii , kwani licha ya wafanyakazi wawili ambao niliowaona wakati wa kuingia ndani ya hiii nyumba sikuona harufu ya mtu mwingine ambaye naweza kusema ni mtu wa karibu wa mwanamama huyu.

“Nitahakikisha Erick anapatikana Rania”Niliongeea huku nikiwa nimemkazia macho usoni nikiyaangalia machozi yake yaliozidi kupendezesha uso wake ,Nilinyoosha mkono wangu na kisha nikayafuta kwa kiganja cha mkono jambo ambalo lilimfanya mwanamama huyu kupoa kiasi lakini kunikazia macho ambayo kwangu niliona ulegevu wa macho , jambo ambalo pepo la ngono lilianza kuninong`oneza nimkule huyu mwanamke.

“Vipi kuhusu Peter baba wa mtoto Erick ?”

“Long gone , nishaanza kumsahau kwasasa na sijui hata yupo hai au amekufa”

“Kwanini unasema hivyo ?”

“Ni stori ndefu sana iliotokea nchini Tanzania na hata sitaku kuikumbuka”

“Kwa hio sasa hivi umeolewa au upo kwenye mahusiano ya namna yoyote ile?” Nilijikuta nikiuliza swali hilo la kipumbavu kabisa , kwani kwa urembo wa mwanamama huyu ni Dhahiri kabisa wanaume watakuwa wamepangiliwa vyema, Aliniangalia usoni huku akionekana ni mtu ambae anavuta pumzi na kuzitoa hali ambayo niligundua alikuwa akijiandaa kwa kunijibu lakini alikuwa kwenye ‘dilemma’.

“Sijawahi kuwa kwenye mahusiano ya aina yoyote ile tokea niingie ndani ya nchi hii , japo ya kukutana na vishawishi mbalimbali kutoka kwa wanaume wengi sana wenye nazo na wasio nazo , wazungu wahindi , , arabs na hata wa Afrika walikuwa wakitaka kuwa na mahusiano na mimi lakini sijawahi kuruhusu moyo wangu kumuamini mtu , sitaku kuzungumza sana kuhusu hayo Damiani Stop making me talk about those things. they are boring enough”.

“Okey nimeacha na nakuamini kwa maneno yako japo inaweza kunigharimu”Niliongea huku nikitabasamu na yeye pia kutabasamu kwani alikuwa ashaelewa nilicho kuwa nikimaanisha .

“Nataka kukuona ukiwa kwenye ‘African Colour’ kama Damiani nachukia rangi nyeupe unajua , lakini pia nataka nione unavyobadilika”Aliongea huyu mwanaume maneno matatu ambayo ukijumlisha yote ni ombi lakini ukiyachambua unapata maneno mawili ya kawaida lakini la mwisho lenye uhatari , unaweza usijue ni uhaatari wake ila utanielewa kwa vitendo.

Sikuwa na haja ya kumbania mwanamama huyu kumuonesha kile ambacho alikuwa akitaka kuona , niliongozana nae mpaka kwenye chumba changu kwa ajili ya kuivua hii FBM m sikuwa na haja hata ya kumjali , alionekana ni mwenye kujiamini wakati tukiwa tunaingia hapa ndani kwenye hiki chumba , lakini kadri ya matendo yangu niliokuwa nikiyafanya nilimuona akiaza kupoteza kujiamini , sheria za FBM ni kwamba lazima niwe Uchi ili kuivua na hili nilidhamiria kufanya mbele yake , yeye si alitaka aone jinsi ninavyovua na kuvaa basi namimi niliona nimtimizie ombi lake .

Lakiwa akiniangalia kwa wasiwasi sana wakati huo nikiwa nimebakisha boksa tu , ni kama mtu ambae alikuwa haamini kama ninakwenda kuvua ile boksa na kufumba na kufumbua nilikuwa uchi tena nikimgeuzia upande ule bwana kalumanzira aliolala , dakika chache mbele nilikuwa Damiani Rabani, na hapa ndipo mwanamama huyu alipozidi kushangaa na kupagawa , nilijikuta nikimsogelea pale aliposimama yeye akiwa hasogei , na kuhesabu sekunde kadhaa tu nilikuwa nishamfikia na kumshika mkono , alionekana kuwa dhaifu mno , kama mtu ambae hajapata chakula kwa siku nyingi sana na mbele yake kulikuwa na chakula .

Sekunde sabini mbele Rania alikuwa chini huku mimi nikiwa juu yake tukipiga Romansi , mwanamke alikuwa na mwili laini huyu sijapata ona , kila sehemu niliokuwa nikigusa utadhani patachanika , na kwa jinsi alivyokuwa wa moto msisimko nilioupata hapo sikuwahi kuupata mahali popote pale , akili zangu zilihama kwa muda , kwa mdakika kadhaa ya kumshika shika alikuwa amelegea mno huku akipanua miguu yake Zaidi akionekana kuwa ni mwenye uhitaji wa juu sana wa uanaume wangu kumuingia , na mimi sikuwa na ajizi nilimpa kile alichokuwa anataka na hapo ndipo nilipomshuhudia mwanamama huyu kupanua mdomo huku akitoa machozi , sikujua ni ya utamu au nini lakini sikutaka kujali sana , nilipeleka chini juu mpaka pale nilipoona sauti yake inakauka kwa kilio ndipo nilipopunguza , nilimgeuza na kumgeuza huku nikijisikia utamu wa ajabu sana ambao sikuwahi kuupata , na weza kusema mtoto alikuwa mtamu huyu , nadhani hili ni kutokana na kutokukuguswa kwa muda mrefu sana kwani kitu ilikuwa mnato sana .

Dakika arobaini mbele wote tulikuwa tumechoka huku tukihema kama mbwa aliekimbia maili nyingi ,nilimwangalia mwanadada huyu na kujikuta nikipokea tabasamu ambalo liliufanya uchomvu wangu wote wa safari ndefu kuisha hapo hapo na kujikuta tukiiingia kwenye mtanange na awamu hii ulinoga sana kiasi cha kunifanya nitoe mbegu wengi sana ndani ya uanamke wa Rania .

Wakati nikimaliza ni kama Janeth alikuwa akiona kile nilichokuwa nikifanya kwani simu yangu ilitoa mlio na kuichukua.

“Damiani najua unacho kifanya lakini naomba uache , tumegundua ile picha ya Kasuku sio mchoro wa kawaida “

“Unamaanisha nini ?”

“Namaanisha unatakiwa kurudi kwenye chumba cha Erick na tutakupa maelekezo mengine “Aliongea janeth huku nikimuona kama mtu ambae anajizuia hisia zake zisiingilie kazi , lakini alikuwa amekwisha kuzoea , alikua akijua kabisa mapenzi yangu aliondoka nayo Merina.

“Hio picha ina rangi mbili ambazo hazijaungana , rangi ya juu ni rangi ambayo unaweza kuifuta kwa kuimwagia maji ya moto , naamini kuna kitu kimefichwa kwenye hio piucha “Aliongea janeth na nikampa maelekezo Rania ya kuleta maji ya moto , na dakika chache yalikuwa tayari na tuliimwagia ile picha maji baada ya kuiweka sakafuni .

“Kipi kinafuata janeth ?”

“Chukua brash ya kupakia rangi na fanya kama unaaza kuipaka rangi upya”

Nilifanya kama Janeth alivyokuwa anaelekeza na hapo ndipo mimi na Rania tulivyoweza kupigwa na mshangao kwani kila sehemu unayopitisha Brash rangi inapotea ‘Colour

Repracement’hii kitu ilinishangaza sana , nilichokuwa najua hii njia inaweza kufanyika kwenye komputa tu kumbe hata kwenye picha ya kawaida.

Ni namba kumi na mbili ambazo ziliandikwa kwa mfumo wa kirumi sikuelewa ni namba za nini , nilipiga picha na kisha nikazituma kwa Janeth ili kuzipatia maana yake na ndani ya dakika chache alikuwa na majibu .

“Ni ‘Cryptography’ namba”

“Zinamaanisha nini?”

“Hapa mpaka kuzitambua , hilo swala ili lifanikiwe nitahitaji Serial number za Kompiuta zilizopo hapo ndani” Aliongea na mimi nilimtumia na kwa mbaali nilielewa anacho maanisha , kwani kwa ninachojua kuhusu Cryptography ni kwamba huu ni mfumo wa kuficha maneno kwa muundo wa kodi , zinaweza kuwa namba au mfumo(format) wowote ule, hii njia ndio inzifanya Cryptocurrency kuwa na hali ya juu ya usalama kwani hata serikali haiwezi kujua hizi namba.

“NImefanikiwa kutambua hizo namba maana yake ni SANTORIN” “Santorin?” Niliongea na kumfanya mwanamama Rania aniangalie .

“Santorin ni kisiwa kilichopo ugiriki”.Aliongea Rania na hapo hapo nilipata kujua huenda The Truth haipo Australia kama tulivyodhania bali ipo Ugiriki.

“Erick atakuwa Ugiriki”Niliongea na mwanamama huyu alijikuta akishangaa lakini Janeth kuniunga mkono kwa kile ambacho nilikuwa nasema , na hili niliona ni swala ambalo linaleta Mantiki , kwa kazi ya hiki kikundi niliamini kabisa ni lazima wawe watu wa kujificha sana .

SURA YA 11

DAR ES SALAAM –TANZANIA

Zikiwa zimepita siku kadhaa tokea kuchaguliwa kwa waziri mkuu pamoja na mawaziri , lakini pia ikiwa imepita siku moja tokea mheshimiwa Raisi Jembe kusafiri kuelekea nchini Marekani kwa ajili ya kula kiapo cha kujiunga na umoja wa siri wenye nguvu duniani Umoja Namba Tisini Na Saba ,Ndani ya jijiji hili lenye pilikapilika za kila namna katika moja ya gorofa ndefu iliokuwa ikimilikiwa na mfanya biashara mkubwa nchini pembeni kabisa na zilipokuwepo ofisi za kampuni ya INNOVA ndani ya jengo hilo kulikuwa na kikao cha siri kilichokuwa kikiendelea .

Ndani ya hili jengo ndio zilipokuwepo ofisi za Umoja huu wa siri kwa eneo la Tanzania na ndio maana siku hio kikao hiki kilikuwa kikiafanyikia ndani ya hilo jengo.

Katika meza kubwa ndani ya chumba kikubwa ndani ya jengo hili katika floor ya kumi na tano chumba kilichokuwa na maandishi makubwa mlangoni yaliosomeka kwa lugha ya kingereza TOP LEVEL MEMBER OFFICE (TLMO) kulikuwa na mabwana wapatao kumi , watano walikuwa wakifahamika kwa majina yao kutokana na kwamba walikuwa ni viongozi wakubwa ndani ya serikali ya Tanzania, wengine hawakuwa wakitambulika kwa majina yao kwani walikuwa sio raia wa Tanzania na rangi zao zilithibitisha hilo .

Katika kikao hiki ajenda kubwa zilikuwa mbili , ajenda ya kwanza ambayo ilianza kujadiliwa ni wasiwasi wa uanachama wa mheshimiwa Jembe Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, japo ya Umoja huu kukubali ombi la raisi Jembe kujiunga na Umoja Namba Tisini na Saba lakini mabwana hawa walionekana kuwa werevu Zaidi kutokana na wasiwasi wao.

Mkuu wa majeshi , Mkuu wa kitengo cha usalama wa taifa ,Raisi mstaafu aliachia madaraka kwa Jembe ,Makamu wa raisi mteule aliengia madarakani , pamoja na mkuu wa jeshi la polisi ndio watu waliokuwa wakitambulika katika kikao hicho , lakini pia ndio viongozi wakubwa ndani ya nchi ya Tanzania walikuwa wakiunga mkono umoja huu wa siri ambao haukufahamika malengo yake kwa Taifa .

Mabwana hawa walikuwa wakijua fika mheshimiwa Jembe hakuwa na nia thabiti ya kujiunga na umoja huo , jambo ambalo mabwana hawa waliona linaweza kuufanya umoja huu kutojiimarisha vyema ndani ya nchi , walihofia juhudi walizokuwa wamefanya katika kurudisha nguvu ya umoja huu ndani ya Taifa la Tanzania zinaweza kupotea .

Jambo la kwanza liliowafanya mabwana hawa kutilia mashaka nia ya bwana Jembe ilikuwa ni siku ya kuapishwa kwake , kitendo cha Peskorov kupigwa na kuzirai siku ambayo amefanya tukio la kumpiga risasi mheshimiwa Jembe na kugundulika kwa alama ya Mzalendo iliokuwa imeachwa katika paji la uso la bwana huyo liliwafanya mabwana hawa waamini kwamba mheshimiwa jembe alikuwa na ushirikiano na kikundi hichi ambacho walikuwa wakiamini kwamba kilikuwa kimepotea ndani ya nchi hii yaani Mzalendo.

Lakini kitendo cha Jembe kupita katika uchaguzi , lakini pia kupona risasi , lakini pia kupotea mara baada ya kupigwa risasi , lakini pia kujitokeza na kutaka kujiunga na U-97 , lakini pia alama ya Peskorov katika paji la uso ilioachwa na mtu ambae alipambana nae mambo hayo yote yaliwafanya waamini kwamba Mzalendo ambayo ilikuwa imetokomezwa miaka kumi iliopita imerudi upya tena ikiwa na nguvu Zaidi kuliko awali. Kwani matukio yaliotokea hayakuwa yakufanywa na mtu mmoja , walimini matukio hayo kwa yeyote aliekuwa akihusika alikuwa na nguvu kubwa sana.

“Unatoa ushauri gani bwana Kinga juu ya rangi halishi ya bwana Jembe ?” Swali hili lilitoka kwa bwana Kent kwenda kwa mkuu wa usalama wa Taifa ,Kent ambaye alikuwa ni muwakilishi wa U-97 Afrika mashariki alikuwa akimuamini sana Kinga , katika vikao vyote alivyokuwa amefanya alikuwa akifurahishwa na michango ya kimawazo ya Kinga , kwani siku zote waliweza kufikia maaumuzi na mawazo yaliokuwa yakitolewa na bwana huyu na ndio maana kwa kila kikao alikuwa akimfanya kuwa mtu wa mwisho katika kuchangia .

“Mkuu kwanza kabisa naamini kwa asilimia mia moja kuna mpango ambao anao mheshimiwa jembe ,tena mpango huu ukiratibiwa na kikundi hiki cha Mzalendo na yeye akiwa ni moja ya jumuia ya kikundi hiki , na hata swala la yeye kutaka kujiunga ndani ya hiki kikundi nimeweza kufikiria na kuja na mambo makuu mawili kwa mheshimiwa kutaka kujiunga na umoja wetu , la kwanza ni kutaka kukalia kiri cha uraisi , kwake swala hili limekuwa ndio njia rahisi ya kupata usalama wa kufika pale ikulu kutokana na tukio lililomtokea , swala la pili , mlolongo woote wa matukio yaliotokea katika siku ile ya kupigwa risasi ni Dhahiri bwana huyu alikuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea , na ni jambo ambalo lilikuwa limepangwa kwa ustadi mkubwa sana na ninyi wote hapa ni mashahidi kwamba hakuna mtu duniani ambaye anaweza kupigwa risasi kwenye kifua na kupona tena bila hata ya kuwa na jeraha isipokuwa tu kama jambo hilo mtu huyo awe analifahamu na kuvaa ‘Bullet Proof’ , lakini tunaweza kusema labda mheshimiwa jembe aliweza kuvaa ‘Bullet Proof’ , lakini ni vipi kuhusu kufichwa kwake mara baada ya kupigwa risasi , tena akifichwa na wanausalama wetu ambao mpaka sasa hatujui mahali walipo,hivyo ninacho amini kwa sasa ni kwamba swala hili hatuwezi kulichukulia kwa urahisi , hili ni swala la dharura na tunapaswa kulichukulia kwa udharura wake ili kuchukua tahadhari zote , tunapambana na watu wenye maarifa na wenye nguvu , mpaka sasa mkuu wa tume ya uchaguzi hatujui aliko yeye pamoja na familia yake haya yote sio mambo ya bahati mbaya , ni maswala ya kupangwa . tena ya kupangwa kwa muda mrefu , hivyo ushauri wangu kwasasa ni kuhakikisha tunaweka nguvu zetu zote kukisaka hiki kikundi na kukitokomeza moja kwa moja na kuhakikisha tunatoa mizizi yote ili kuepusha kuchipuka tena”

Aliongea bwana kinga na kufanya watu wote waliokuwa katika kikao hicho kutafakari maneno hayo , lakini si hivyo tu kila mtu aliweza kuwaza na kuvuta picha kamili ya kikundi cha Mzalendo kwa kuunganisha matukio machache yaliotokea siku kadhaa zilizopita.

“Umeongea vyema sana bwana Kinga , lakini kwanza kabisa naomba nikutoe hofu lakini pia niwatoe hofu watu wote mliopo ndani ya hiki chumba , kwanza kabisa Mzalendo ni kakikundi kadogo sana ambako kalibahatisha kufanya matukio yaliotokea , lakini yakaleta athari kubwa , lakini kubahatisha kwao hakumaanishi kwamba kikundi hiki kinanguvu na maarifa kutuzidi sisi ,tulichokosea nikuwadharau hawa watu na kakikundi kao , lakini mpaka sasa hali imerudi kama ilivyokuwa na naweza kusema kila kitu kinaenda kama tulivyopanga na muda mfupi ujao tutawakamata wahusika wotea wa kikundi hiki”

“Swala hilo litakuwa gumu kutokana na kwamba watu hawa bado hawafahamiki na ndio maana nimeshauri kulichukulia tahadhari”Aliongea Kinga na kumfanya Bwana kent kutabasamu , moja sifa kubwa ya bwana Kent ni dharau alikuwa akiwadharau sana watu weusi , unaambiwa tokea akiwa mdogo katika historia yake ya shule zote alizopita bwana huyu alikuwa mbaguzi wa rangi wa waziwazi , sifa yake ya pili alikuwa ni ‘Sadist’ hawa ni watu ambao wanapenda kuona wenzao wakiteseka kwa kuwasababishia maumivu licha ya bwana huyu kutibiwa lakini ni kwamba hakupona kikamilifu, hata tabasamu alilokuwa akumuoneshea Kinga licha ya kwamba alikuwa akimkubali katika michango yake , tabasamu hilo lilikuwa la dharau lakini usingeweza kumjua .

“Huna haja ya kuwa na wasiwasi bwana Kinga U-97 ilijengwa na watu wenye akili na mpaka sasa tuliobaki wote tunakili , hivyo hata hawa Mzalendo hawawezi kushindana na sisi maana sisi sio nchi bali sisi ni Dunia hivyo mtu mmoja hawezi kushindana na Dunia ,Swala la Mzalendo kumtumia Jembe katika mipango yao ni makossa makubwa waliofanya na hili linadhihirisha uwezo wao mdogo wa kufikiria ,Jembe huko anakoenda anaenda kuwataja hawa panya wote na kazi itakayobaki ni sisi kuwakamata hapa Tanzania na kuhakikisha hakuna hata mmoja anaekimbia wala kukosekana”

“Itawezekana vipi kwa mheshimiwa Jembe kuwataja wafuasi wake ?”Aliulizwa Kilubwa raisi mstaafu aliechia madaraka akiwa kwenye hali ya mshangao.

“PSYOPS” Aliongea Kent na baadhi ya watu hapo ndani walielewa huku wengine wakiwa hawajaelwa na walihitaji ufafanuzi .

“Kinga atawafafanulia ninachomaanisha na mpaka sasa kikao kimekwisha na ninagharisha mpaka kikao kingine tutakapozungumzia kuhusu Mpango Zero”Aliongea Kent na kisha kuondoka huku akiwaamuru walioelewa neno aliloongea waondoke na ambao hawajaelewa wabaki , na wale wazungu wote waliweza kuondoka ikidhihirisha kwamba walikuwa wameelewa kile ambacho Kent aliongea ila viongozi wote wakubwa hawakuelewa isipokuwa kwa bwana Kinga aliekuwa amepewa jukumu la kuwafafanulia wenzie juu ya maana ya neon PSYOPS.

*****

JOHN F KENNEDY INTERNATIONAL AIRPORT –NEW YORK, USA 18:00.

JFK ni moja ya viwanja vya ndege bora kimataifa vilivyokuwa bize sana ndani ya jiji hili la New York , Zaidi ya ndege 70 huruka na kutua kwenda na kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi ya Marekani , uwanja huu upo sehemu inayoitwa Queens ndani ya New York , ni uwanja wenye jumla ya terminal sita sifa inayodhirisha ukubwa wake, huku kila terminal kiwa na huduma bora kabisa..

Lakini sifa za ukubwa wa uwanja huu unaendana na umaarufu wa Jiji la New York , ni moja ya jiji lenye watu wengi Zaidi ndani ya nchi hii ya Marekani , na moja ya sehemu ambayo ina uhuru wa kuishi na kutafuta maisha ni ndani ya jiji hili , ukuaji wa jiji hili ulikuwa ni wa haraka sana ukilinganisha na majiji mengine .New York ndio kitomvu kikubwa cha biashara ndani ya taifa hili la Marekani na nje ya nchi pia kwani wafanya biashara wengi hutembelea sana jiji hili kwa ajili ya maswala ya kibiashara , moja ya maeneo maarufu ndani ya jiji hili ni kama Wall Street hili ni eneo ambalo maswala yote ya kiuchumi na kifedha yanafanyika , ndio sehemu ambayo makampuni makubwa ya kifedha na kibenki yanapatikana , ni sehemu ambayo maswala ya masoko ya hisa yapo , sehemu nyingine ni Time Squre hili ni eneo lenye watu wengi wanaotembea kwa miguu ni sehemu inayofahamika kwa majina ya kiutani mengi na moja wapo ni kama ‘Heart of the world’, pia moja ya utambulisho mkubwa wa NYC ni uwepo wa ‘Statue of liberty’,NYC ndio mji wenye magrofa marefu na mengi Zaidi ndani ya nchi ya Marekani na ndio eneo pekee ambalo hutembelewa na watu wengi Zaidi ndani ya nchi ya Matekani. Licha ya umaarufu mkubwa wa jiji hili nje na ndani ya Marekani lakini pia yapo mambo mengi yaliokuwa yakifanyika mengine yakiwa ni halali na mengine yakiwa sio halali

Nje kabisa ya mlango wa Terminal 4 alionekana mheshimiwa Jembe akitoka ndani ya mlango uliokuwa na maandishi makubwa yaliokuwa yameandikwa ARRIVALS akiwa ameambatana na walinzi wake pamoja na wasaidizi , Ndege aliokuwa amefika nayo mheshimiwa Jembe ilikuwa ni ya shirika la Fly Emirate . ndege ambayo alikodi kwa ajili ya usafiri huo .

Mara baada ya kutoka ndani ya jengo hili la kisasa kabisa alifuatwa na mabwana wawili mmoja akiwa ni mweusi na mmoja alikuwa ni mzungu wote wakiwa wamevalia suti nyeusi na miwani za jua , hawa mabwana kabla ya kumfikia Raisi Jembe walizuiliwa na walinzi na hapo ndipo walipotoa vitambulisho vyao .

Mabwana hawa walijitambulisha kama CIA mmoja akiitwa Ben Horowtz na bwana mwingine alijitambulisha kama Sam Snowden , mabwana hawa walijieleza kama moja ya watu waliokuwa wameagizwa kwa ajili ya kumpokea mheshimiwa na kumuongoza kuelekea mahali ambako anatakiwa kufika .

Walinzi wa mheshimiwa Jembe walijiridhisha na mabwana hao na kisha waliongozana nao mpaka kwenye maegesho ya magari na walimuonyesha mheshimiwa gari ambalo lilikuwa limeandaliwa kwa ajili yake

Baada ya kuingia ndani ya gari hili pamoja na mlinzi wake wa karibu ‘Bodyguard’ huku wale walinzi wengine wakipanda kwenye gari zingine ambazo zilikuwa pia zimeandaliwa, gari hizo ziliondka ndani ya eneo hilo.

Safari ya mheshimiwa Jembe ndani ya Marekani haikua ya kikazi na wala uongozi wa Marekani hawakuwa na taarifa rasmi za raisi Jembe kudhuru ndani ya Taifa hilo na jambo hili kwa namna yake lilishangaza kidogo kwani walipokelewa na CIA. .

Jumla ya gari zilikuwa nne , zilizokuwa zikimsindikiza mheshimiwa Jembe ndani ya muda mfupi gari zile zilikuja kusimama ndani ya nje ya uzio mkubwa wa nyumba , eneo lilokuwa likifahamika kama Shirley Chishom State Park, ndani ya Broklyn.

Lilikuwa ni jumba kubwa mno la kifahari lilikuwa ndani ya uzio huu , licha ya kwamba baadhi ya ,majumb ya pembeni kutokuwa na uzio lakini hili eneo lilikuwa limezungukwa na ukuta na hii ilionesha ni mahali ambapo si pakuingia ingia tu kama sio muhusika. .

Eneo lilikuwa tulivu sana lakini lenye madhari mazuri mno , ilikuwa ni kama hoteli huku muundo wa jingo hili ukiwa ni ule wa kizamani kabisa , ni kama yale majengo ambayo mengi utayakuta Italy hususani ndani ya Vatican city , baada ya magari yale kwenda kusimama sehemu maalumu ambayo ilikuwa ikitumika kama maegesho, mheshimiwa aliamriwa kushuka na ndani ya dakika chache kulitokea wanawake wawili wakiwa wamevalie mavazi ya suti na walionekana walikuwa mahali hapo kwa ajili ya kumpokea mheshimiwa Jembe.

“Welcome Mr President wing 7 House , my name is Hellen , Iam head of house meet my Assistant Sasha we have been waiting for you eagerly”

“Karibu mheshimiwa nyumba tawi namba saba jina langu ni Hellen ndio mkuu wa nyumba kutana na Sasha msaidizi wangu, tulikuwa tukikusubiria kwa hamu” Aliongea mwanamama huyu aliejitambulisha kwa jina la Hellen huku akiweka tabasamu pana usoni mwake.

“Asante sana Hellen” Alijibu mheshimiwa na kisha mwanamama huyu alimuongoza njia mheshimiwa pamoja na walinzi wake baada ya kuwahakikishia usalama

Mandhari ya jumba hili yalikuwa yakuvutia sana kiasi kwamba hata mheshimiwa Jembe alishangaa , yalikuwa ni Mandhari ya kifalme , kwanzia wafanyakazi waliokuwa wamesimama kwa kujipanga huku kumpa mheshimiwa Jembe ishara ya heshima , lakini pia thamani zilizokuwa zimetumika kupamba eneo hilo zilikuwa ni za kiwango cha juu sana .

Hata wasaidizi wa mheshimiwa walishangaa mapokezi ya aina hio , kwani baadhi yao ambao walikuwa ni wazoefu katika kusindikiza maraisi hawakuwahi kupata mapokezi ya aina hio ya kipekee licha ya kuwa hakukua na kiongozi mkubwa aliekuwepo ndani ya eneo hilo lakini mpangilio wa matukio ya hapo ndani yalikuwa ni heshima kubwa sana kwa mheshimiwa Jembe kupata , hata ile hofu aliokuwa nayo kiasi flani ilipungua .

“Mheshimiwa hii ni nyumba maalumu kwa ajili yako kuishi kwa kipindi chote utakachokuwepo ndani ya nchi hii , kuna kila kitu utakacho kihitaji cha kiofisi na kimalazi , utaweza kutimiza majukumu yako ya kiuongozi ukiwa hapa mpaka pale utakapokamilisha hatua tano za kula kiapo”Aliongea huyu mwanamama ambae alionekana umri umemtupa mkono na maneno yale kidogo yalimshangaza mheshimiwa Jembe lakini hakutaka kutia neno .

Basi aliweza kuonyeshwa maeneo mbalimbali ndani ya jumba hilo la kifahari kabisa , lilikuwa ni jumba kubwa lenye eneo kubwa ambalo lilikuwa na kila kitu kuanzia bwawa la kuogelea , uwanja wa Gofu pamoja na wa Tennisi .

“Uzuri wa hili eneo ni Zaidi ya Ikulu ya nchi yangu”Aliongea mheshimiwa mara baada ya kuoneshwa chumba ambacho takuwa akilala na kumfanya mwanamama Hellen kutabasamu . .

SURA YA 12

Ni siku nyingine ndani ya nchi ya Marekani ndani ya jumba la kifahari ambapo mheshimiwa Jembe alikuwa ameandaliwa na U-97 kwa ajili ya kuishi .

Asubuhi hii mara baada ya taratibu zote kuisha kama kupata kifungua kinywa na mengineyo , mwanamama Hellen alimtaarifu mheshimiwa Jembe kujiandaa kuingia ofisini kwani kuna mgeni ambae anatarajiwa kufika kwa ajili ya hatua ya kwanza.

Na ndani ya nusu saa tu ya mheshimiwa Jembe kuingia ofisini hatimae bwana mmoja wa makamo mwenye rangi mchanganyiko yaani ya kizungu na kiafrika alitinga ofisini hapo, alikuwa ni bwana mmoja kwa makadirio ya umri wake si chini ya miaka therathini , alikuwa amevalia suti nyeusi na kipepeo shingoni huku nywele zake akiwa amezichana kuelekea nyuma.

.

“Naitwa Dave Hamton afisa levo 32 ndani ya U-97 mimi ni mtaalamu wa maswala ya kiuchambuzi Duniani”utambulisho huo ulimfanya mheshimiwa Jembe kushangaa , kwani alaichotegemea ni hatua ya kwanza ya kula kiapo lakini anachokutana nacho ni mtu ambae amejitambulisha kama moja ya wachambuzi wa maswala ya kiuchumi duniani jambo ambalo kwake lilimshangaza kidogo .

“Karibu sana Dave”

“Asante sana mheshimiwa , Naamini umeshangazwa na utambulisho wangu”Aliitikia kwa kichwa

“Dhumuni la kikao chetu mheshimiwa ni juu ye kukuelezea juu ya malengo ya U-97 kwa Afiraka nzima kwa upande wa kiuchumi”Aliongea na kisha alitoa tablet yake na kumkabidhi mheshimiwa .

Mheshimiwa raisi alishangazwa na mambo mengi ambayo bwana Dave aliweza kumwambia , alikiri yeye mwenyewe katika kikao hicho kilichochukua masaa mawili kwamba umoja huu wa siri licha ya kwamba hakuwa akijua madhumuni yao makuu kwa mataifa ya kiafrika lakini kwa upande mwingine walikuwa wamesaidia ukuaji wa maendeleo kwa kiasi kikubwa sana , hususani katika swala zima la miundombinu na kuboresha maisha ya wananchi wengi , licha ya hivyo Dave aliweza kumuonesha nguvu ya umoja huu ndani ya mashirika makuu duniani kama vile IMF ,WB,UNICEF,WHO,ILO na mengineyo mengi makubwa .

Jambo hili kwa mara ya kwanza hakulielewa vyema mpaka pale alipoweza kufafanuliwa nguvu ya umoja huu ndani ya haya mashirika katika kuisadia Afrika ,bwana Dave alimwambia mheshimiwa kuwa U-97 ndio mara nyingi wanaohimiza mataifa mengi ya Afrika kupara misaada ya kufanya maendeleo na hii ni kwa zile nchi tu ambazo zitakuwa chini ya umoja huo .

Siku hio ilikuwa ni ya Vikao tu kwa mheshimiwa na watu hawa waliojitambulisha kwake kama wafuasi wa umoja NAMBA TISINI NA SABA ,

Mpaka inafika muda wa jioni wa vikao mheshimiwa alikuwa amepata uelewa mkubwa sana juu ya U-97 licha ya kutojua yandani ya umoja huo yaliokuwa yakitendeka lakini alipata kuweza kufahamu kuwa umoja huo kwa namna moja ama nyingine ulikuwa na faida kwa watanzania na alikiri kwamba watu aliokutana nao walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwake.

Hatua za mwanzo za kula kiapo zilikuwa ni za kawaida na katika hatua zote hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kuandaliwa kisaikolojia tu , hatua ya mwisho ndio ilikuwa ni ya kuogopesha sana kwa mheshimiwa Jembe , kwani katika hatua hii alikuwa akitakiwa kutubu dhambi zake zote , na ili uweze kupata nafasi ya kuweza kutubu dhambi anatakiwa kuweka siri zake zote wazi.

Siku iliofuata ilikuwa ni ya mheshimiwa Jembe kuingia kwenye chumba cha utakaso , hiki ni chumba ambacho sheria yake kubwa ni kwamba ili uweze kutakaswa na kula kiapo hutakiwi kuwa na jambo ambalo unalifich ndani ya moyo wako (Siri) , sheria za hiki chumba ni kwamba kama utaingia basi kunauwezekano mkubwa wa mtu kutoa siri zake zote kwa kile umoja huu ulichokuwa unakiita kuungama , yaani unaweka siri zako zote wazi ili uweze kupata nafasi ya kuungama na hatimae kuwa mwanaumoja kamili ambae huna makando makando , na kupitia hiki chumba cha utakaso siri nyingi ziliweza kupatikana juu ya mataifa mbali mbali . na si hivyo tu lakini pia kwa kila mwanachama ambae aliingizwa katika chumba hiko akitoka anakuwa mtu mpya na mtiifu kwa umoja, yaani kwa mnaneno marahisi ni kwamba kama ulikuwa na lengo baya dhidi ya umoja basi ukishaingia humo ndani , ukitoka utakuwa na malengo mazuri kwa umoja na utatii kila maelekezo utakayopewa na viongozi wa juu wa U-97.

Basi baada ya mheshimiwa Jembe kumaliza kujiandaa na kupata kifungua kinywa , walinzi wake walitaarifiwa kwamba mheshimiwa ataondoka ndani ya hio nyumba na kwenda katika kikao cha siri ambacho kitachukuwa takribani masaa kumi na mbili .

Hawa walinzi wake pamoja na wasaidizi kwanza kabisa hawakuwa wakijua kile kilichokuwa kikiendelea juu ya raisi wao kiula kiapo cha kujiunga na Umoja namba Tisini na saba , walichokuwa wakijua ni kwamba mheshimiwa alikuwa ndani ya taifa hilo kwa ajili ya maswala ya kitaifa, mtu mmoja pekee aliekuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea ni mlinzi wa karibu wa raisi (Bodyguard) na huyu katika safari hio ya kwenda kwenye kikao alikuwa amepewa nafasi ya kutangulizana nae , huku walinzi wengine wakiwa wamebakia ndani ya jumba la Wing 8.

Saa tatu kamili ndio saa ambayo mheshimiwa Jembe aliweza kutoka ndani ya nyumba aliokuwa amefikia kuelekea katika hekalu la Utakaso sehemu ambayo atakula kiapo rasmi cha kujiunga na umoja namba tisini na saba. Lakini pia sehemu ambayo alitakiwa kutakaswa na kuwa mpya .

Usafiri uliokuwa umetumika kumchukua mheshimiwa ndani ya Wng 8 house ulikuwa ni wa njia ya anga kwa kutumia chopa , huku ndani ya ndege hio akiongozana na mlinzi wake wa karibu na bwana mmoja ambae alijitambulisha kwa jina la Henlsink , bwana huyu alikuwa ni raia kutoka Mexico , alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi.

Ndani ya nusu saa tu walikuwa wapo ndani ya eneo ambalo mheshimiwa raisi na mimi mwenyewe sikueza kulitambua , lakini ndani ya eneo hilo lililokuwa limezungukwa na miti mingi kulikuwa likionekana jengo kama hekalu .

Chopa iliweza kukanyaga veyema eneo husika lenye alama kubwa ya H na baada ya hapo mheshimiwa alitoka na kuja kupokelewa na wanadada wawili , waliokuwa wamevalia kama masista , baada ya kupokelewa na hawa wadada ambao walijitambulisha kama wahudumu wa jumba hilo liliokuwa na maandishi makubwa mlangoni U-97 LODGE X .

Mheshimiwa Jembe alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa kila alipokuwa akikumbuka maneno ya mwanamama Hellen juu ya jambo ambalo linafanyika ndani ya hekalu hilo kwa ajili ya utakaso, alikuwa na hofu ya kutoa siri zake na siri kubwa aliokuwa akihofia kuitoa ilikuwa ni juu ya mpango wa Mzalendo .

Aliamini kama kweli alichoambiwa na mwanamama huyo juu ya uwezekano wa kuweka siri zake hadharani , swala hilo lilimuongopesha sana , kwani aliamini kwa kufanya hivyo ni kwamba anakwenda kuharibu kila kitu na ile mipango ambayo alikuwa amejiwekea na kitengo cha Mzalendo inakwenda kukwama.

Baada ya utaratibu wa awali kukamilika wa mheshimiwa Jembe kupewa mavazi mengine kama yale ya wagnjwa wa hospitalini , aliweza kuingizwa kwenye chumba kimoja kilichokuwa kina maandishi makubwa mlangoni kama PSYOPS ROOM , maneno ambayo kwa mheshimiwa hakuweza kuyaelewa kabisa .

Ndani ya hili jumba ni kwamba muonekano wake ulikuwa ni kama wa hospitali , kwa nje lilionekana kama hekalu ila kwa ndani ni jEngo ambalo lilikuwa limejengwa kwa ustadi wa kutenganisha vyumba , na ilionekana hio ni sehemu maaliumu kabisa kwa ajili nya U-97 , ukutani kulikuwa na michoro mingi ambayo ilikuwa imechorwa na haikueleweka maana yake ni nini kwa mara moja .

Mlinzi wa mheshimiwa raisi bwana Tomasi Kibwe alikuwa kwenye wasiwasi mwingi , kwani ni takribani masaa nane tokea mheshimiwa aingie ndani ya chumba ambacho hakuelewa ndani ya ke ni kitu gani kilikuwa kikifanyika , ubaya ni kwamba hakuweza kutoka mahali alipo kwani alikiuwa amewekewa ulinzi , wasiwasi wake ulikuwa juu japo ya wahusika wa jumba hilo kumhakikishia usalama wa mheshimiwa Jembe ,, lakini yeye kama mwanausalama hakuweza kuwa katika hali ya utulivu , aliamini kama kuna jambo baya lolote likamtokea Raisi basi yeye moja kwa moja angewajibika na hakuelewa angewaeleza nini watanzania.

Lakini wasiwasi wake ulikuja kukoma mara baada ya kusubiri lisaa limoja mbeleni na hapo ndipo alipoweza kumuona mheshimiwa Jembe akitoka ndani ya chumba alichoingizwa akiwa na mavazi yake ya suti , lakini kwa bwana Tomasi aligundua jambo ambalo si la kawaida kutoka kwa mheshimiwa Jembe , hali ya furaha iliokuwa imetanda kwenye uso wake.

“kila kitu kipo sawa Tomasi huna haja ya kuwa na wasiwasi Zaidi” Aliongea mheshimiwa na Tomasi alipiga Saluti kuonyesha kwamba anakubali kile mheshimiwa alichokuwa anasema .

Basi kwa kutumia njia ile ile mheshimiwa aliweza kurudi Wing 8 House lakini akionekana kuwaza jambo .

“Sikuwa na jinsi ilinibidi kueleza kila kitu juu ya Mzalendo , hatuwezi kushindana na hawa watu kamwe njia moja ya mimi kuliongoza taifa la Tanzania ni kula sahani moja na hawa watu ” Aliongea mheshimiwa wakati akiwa anaingia ndani ya Wing 8 na kupokelewa na kikosi chake cha usalama ambacho muda wote kilikuwa kipo katika hali ya wasiwasi juu ya usalama wa Mheshimiwa.

“Hongera sana mheshimiwa kwa hatua yako ya mwisho”

“Nashukuru sana Hellen”

“Kesho ni siku yako ya mwisho ya ukaribisho ndani ya U-97 lakini pia ndio siku utapata fursa ya kuzungumza na wafanyabiashara wakubwa ambao kama mazungumzo yako yataenda vyema ni fursa kwa watanzania wote” Aliongea Hellen na Jembe alikubaliana nae na baada ya hapo aliaga na kuondoka

*****

Upande mwingine nchini Tanzania masaa machache mara baada ya kukamilika kwa hatua ya mwisho ya Raisi jembe ndani ya Tanzania , ndani ya ofisi ya mkuu wa kitengo cha usalama wa Taifa bwana Nassoro Kinga alipokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa namba ambayo hakuweza kuifahamu ujumbe huo ulikuwa ukisomeka ‘MZALENDO BASE AT KURASINI

NLT TOWER GROUND FLOOR ,Damiani Rabani , Janeth Bendera , Linda ….’

Meseji hii ilimsisimua sana mheshimiwa na hakutaka kusubiri , dakika hio hio aliinua simu na kumpigia Kent na kumueleza ujumbe huo , lakini jibu kutoka kwa Kent lilimfanya atabasamu kwani hisia zake zilikuwa ni kweli na hii ni mara baada ya Kent kumwambia Nasoro kuwa andae operesheni ya dharula ya kuvamia jingo la NLT sehemu ambayo walikuwa wakijua kuwa ndio makao makuu ya kambi ya Mzalendo .

Baada ya Kinga kuweka simu yake chini hakutaka kuchelewa hata kwa dakika , kwani alinyanyua simu yake na kutoa maagizo na ndani ya dakika moja tu bwana mmoja aliejazia mwili aliingia ndani ya jengo hilo , huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Mr White .

“kuna operesheni ya dharula inatakiwa kufanyika usiku wa leo”

“Misheni gsani hio mheshimiwa ?”

“Tumepata eneo la maficho ya kambi ya Mzalendo hivyo nataka usiku wa leo tukavamie hio kambi , lakini kabla ya hilo kufanyika nataka watu hawa wafuatao tujue mahali walipo”Aliongea Kinga na kutoa kumtajia majina Mr White , yalikuwa ni jumla ya majina kumi na mbili ya ajenti wote wa Mzalendo.

“Mishenni hii inatakiwa kufanyika kwa weledi wa hali ya juu sana , sitaki makossa , watu tunaoenda kupambana nao ni watu makini hivyo lazima na sisi tuwe makini , watu hawa sitaki akosekane mtu hata mmoja , unda timu ambayo itavamia usiku Kurasini na unda timu nyingine itakayowafatilia mahali walipo hawa wanaojiiita wazalendo wa nchi hii “ Aliongea mheshimiwa Kinga na kisha Mr white aliondoka kwa ajili ya kupanga timu yake kuipeleka kwenye mapambano..

Ndani ya masaa kadhaa tu tokea Mr white apewe jukumu la kuunda timu kwa ajili ya kufatilia wanamzalendo , alikuwa akitoa taarifa kwa mheshimiwa Kinga juu ya hatua ambayo wamepiga .

“Tumeweza kujua jumla ya ajenti saba walipo kwa muda huu na vijana wapo wanawafatilia kwa kila hatua, walioweza kupatikana ni Janeth bendera , Linda ,Zakayo ,Kassimu ,Sabi Mboneche………”Aliongea ajenti Nyuu au Mister White.

“Hawa wengine wako wapi ?”

“Mkuu kuna uwezakano hawa kuwa katika kambi yao”

“Huo ni uwezekano tu Bakari ninachotaka ni uhakika kama kweli wapo kwenye kambi yao , hususani huyu Damiani Rabani , ndio mtu muhimu sana kwenye hiki kitengo na ni lazima tujue ni wapi alipo kwani kossa la kumpoteza huyu ni kwamba misheni yetu imefeli”.

“Ndio mheshimiwa ngoja tuendelee kufalitilia mahali walipo kabla ya muda wa operesheni kufika “ aliongea ajenti nyuu au Mr White na kisha aliondoka , akimuacha bwana Kinga katika mawazo mawazo ya hapa na pale , lakini muda mfupi baada ya kutoka kwa Mister White Kinga alipokea simu kutoka kwa Kent .

“Operesheni imefikia wapi ?” ilisikika upande wa pili .

“Ajenti saba wapo katika macbo yetu , wengine watano hatujui walipo akiwemo Damiani Rabani , tunakisia wanaweza wakawa ndani ya kambi yao”Aliongea Kinga .

“Piga bomu hio kambi , sambaratisha kila kitu na kuhusu hao wengine waliopatikana hakikisha mnawakama wakiwa hai”Aliongea Kent na kisha simu ilikatwa .

Jambo hili kidogo lilimuacha Kinga katika mshangao lakini hakuwa na jinsi , alikuwa yupo tayari kufata maelekezo ya Kent ya kupiga bomu kiwanda cha NLT Kurasini , baada ya kufikiria kwa dakika kama mbili , alitoka na moja kwa moja alienda mpaka chumba cha ufatiliaji wa operesheni hio .

“wapi mmefikia ?”

“Janeth bendera anaonekana kuelekea upande wa Kurasini , vijana wapo kazini wanaendelea kumfatilia , nadhani hili litakuwa jambo jema tukivamia akiwa ndani ya kambi “ aliongea Bakari”

“Vipi kuhusu wengine sita ?”

“Tupo nao macho na wanaonekana kutoondoka katika maeneo ambayo wameonekena “ “Operesheni ya leo usiku ni kupiga bomu katika kambi yao , haitajarisha ni nani yupo ndani ya kambi ninachotaka kambi hio ndani ya masaa sita yajayo pawe vumbi tu ndio linaloonekana”Aliongea mheshimiwa Kinga na kufanya watu wote washangae . “Uko siriasi mheshimiwa, hilo jambo ni hatari sana kwani wengine ambao hawahusiki wanaweza kupata madhara , na isitoshe tunawezo wa kuingia ndani ya kambi hio na kuwakamata wahusika bila kufanya uharibifu mkubwa”

“Bakari maamuzi yangu ni hayo na yanatoka moja kwa moja kutoka kwa mheshimiwa Raisi , hivyo saa tatu kamili ya usiku nataka kiwanda cha NLT kiwe vumbi , andaa vijana kwa hio misheni” Ajenti nyuu alijikuta akishangazwa sana na maamuzi hayo , lakini hakuwa na kupinga kwani mkuu wake wa kazi alikuwa ashaafanya maamuzi na ni moja ya jukumu lake kufata maamuzi ya mkuu wake .

“Ni shambuilio la bomu la aina gani linapaswa kutumika?”

“Tutatumia shambulio la Anga”

******

Captain Juma hizza alikuwa ndio kwanza anaingia nyumbani kwake Tegeta muda wa saa kumi na mbili za jioni , kwake hiio ndio muda wake wa siku zote wa kufika nyumbani akitokea kazini , na bwana huyu alikuwa ni moja ya watu ambao walikuwa wakipenda sana kurudi nyumbani mapema na kuiona familia yake , hii ni tabia ambayo alikuwa amejijengea lakini pia ni tabia ambayo ilimpa heshima kubwa sana kwa majirani zake .

Kwani ni tabia ya kawaida sana na iliozoeleka kwa baadhi ya wababa wafamilia kuchelewa kurudi nyumbani baada ya kazi , kwani wao mara baada ya kazi walipitia sehemu mbali mbali wanazozijua wao kwa ajili tu ya kupoteza muda ili wasirudi nyumbani mapema .

Jambo hili lilikuwa tofauti kwa Juma kwani yeye alikuwa akiwahi sana kurudi nyumbani , basi baada ya kulakiwa na watoto wake wawili Salma na Hamisa aliingia chumbani na kujimwagia maji ili kuondoa uchomvu , lakini wakati anaendelea kuoga mara mke wake aliita akimtaarifu kwamba simu yake ilikuwa ikiita na jina la mpigaji lilikuwa ni bossi .

Baada ya kusikia jina hilo alitoka na kuchukua simu hio na kupokea kwani aliamini sio kawaida kwa bossi wake kumpiigia kwa wakati huo tena mara baada ya kurudi kazini .

Baada ya kuweka simu sikioni ndani dakika chache aliweza kupata maelekezo ya kurudi kazini kuna opetesheni ya dharula ambayo alikuwa akipaswa kuifanya usiku huo , huku akielekezwa na mkuu wake huyo wa kazi kwamba eneo husika atapewa akiwa angani.

Juma hizza alikuwa ni moja ya marubani wa ndege za kijeshi waliokuwa wakiaminiwa sana na kitengo cha dharula cha jeshi cha maswala ya makombora ya kurushwa kwa Anga , licha ya kufanya kwake kazi miaka mingi hakuweza kuutumia usomi wake katika kurusha ndege na kwenda kushambulia eneo , kwani ndani ya taifa letu kulikuwa na Amani kubwa sana kiasi kwamba ni mara chache sana ndege za kivita zilikuwa zikitumika .

Sasa siku hio mara baada ya kupokea taarifa hio ya kutumia ndege yake kwa ajili ya kwenda kushambulia ni kama walimpa mzuka kabisa , kwani jambo alilokuwa akilitaka siku zote ni hilo litokee ili aweze kuonyesha manjonjo yake .

Lisaa limoja mara baada ya kupewa maelekezo alikuwa ndani ya ndege yake kubwa ya kivita iliokuwa ikifahamika kwa jina la Bird killer ndege iliokuwa imetengenezwa nchini Urusi , ndege hio iilikuwa na uwezo wa kubeba mabomu yasiooungua mia moja na kushambulia kwa umbali mrefu kutoka angali bila kukosa Target.

Saa mbili na nusu za usiku Captain juma hiza alikuwa akielea angani akiwa na shauku kama zote za kufanya shambulio katika eneo ambalo wakubwa wake walimuelekeza kumtumia ‘cordinates’

“Ndani ya dakika kumi na tano tu za kuwa angani hatimae aliweza kupokea uelekeo husika wa Terget yake anayopaswa kwenda kufanya shambulio .

“Target locked . need permission to engage” aliongea Juma akiomba ruhusa ya kuachia kombora kwani tageti alikuwa ashaipata .

“ umeruhusiwa” mIlikuwa ni neno dogo lakini lililoleta madhara makubwa sana , kwani ndani ya sekunde kadhaa ndani ya eneo lote la Kurasini lilikuwa halitamaniki , lakini si hivyo tu , wakazi waliokuwa kuwa maeneo ya karibu na eneo hilo walikuwa katika taharuki kubwa kwani ni jambo ambalo hawakuwahi kulishuhudia kwenye maisha yao ukilinganisha na historia ya taifa la Tanzania kutokuwa na matukio ya ajabu kama hayo ..

SURA YA 13

Linda mara baada ya Damiani kuelekea nchini Australia alijikuta akipendana na kijana wa kipemba aliekuwa akijulikana kwa jila la Hamadi , kwa mara ya kwanza ya Linda kukutana na Hamadi ilikuwa ni siku aliokuwa mapumzikoni ndani ya kisiwa cha Unguja ndipo alipoweza kuonana na mfanya biashara Hamadi na kwanzia siku hio ya kukutana waltokea kupendana sana kwa muda wa siku chache walizodumu pamoja .

Siku ambayo mheshimiwa Jembe anaelekea nchini Marekani ni siku ambayo Linda akiwa ndani ya kambi ya Mzalendo aliweza kuwekeana ahadi na Hamadi kuonana siku mbili mbele kwani Hamadi alikuwa akija bara akitokea Dubai alipokuwa bize kibiashara , jambo hili kwa Linda lilimpa munkari sana ukijumlisha na namna ambavyo alikuwa amemmiss Hamadi , alijua fika kazi yake haikuwa ikimruhusu kupenda , lakini kwa kijana Hamadi alikuwa ameloea kwani kijana huyo alikuwa akijua kumdekeza mno Linda kiasi cha kumchanganya sana .

Siku mbili mbele kama walivyo ahidiana , hatimae Hamadi alifika nchini na kumtaarifu Linda kwamba yupo hoteli ya Golden Tulip katikati ya jiji la Dar es salaam , Muda ambao Linda anawasiliana na Hamadi alikuwa ndani ya kambi ya Mzalendo na ilikuwa ni muda wa saa saba na nusu kwenda nane wakati wakiwa wanawasiliana na walipanga saa kumi na moja za jioni Linda atafika hotelini hapo .

Siku hii ndani ya kambi hii walikuwemo jumla ya watu watatu waliokuwa zamu katika kuhakikisha kila mipango inaenda sawa , yaani Linda alikuwa na wenzake wawili ambao wote kwa ujumla wao walikuwa wakihusika na maswala ya kitehama ndani ya kambi hii ya Mzalendo.

Ilipotimu muda wa saa kumi na robo Liuda aliwaacha wenzake wakiendelea na majukumu na yeye alitoka kwa ajili ya kwenda kuonana na mpenzi wake Hamadi, mwanadada Linda alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Crown nyeupe na ni gari ambayo alikuwa akiipenda sana kutembelea nayo licha ya kwamba alikuwa na gari nyingine aina ya BMW lakini gari hio ya kijapani ndio moja ya gari alizokuwa akipendelea sana kutembelea .

Kuna jambo ambalo lilimtia wasiwasi , na hio ni mara baada ya kuingia ndani ya maegesho ya magari ndani ya hoeli ya Golden Tulip , kwani kuna gari aliitilia mashaka , kwani tokea anatoka Kurasini gari hio ni kama ilikuwa nyuma yake , japo mwanzoni hakuwa akiitilia mashaka , lakini kitendo cha kuegesha gari yake ndani ya hoteli hio na kuiona lile gari swala hilo lilimpa mashaka kidogo lakini hakuwa akitaka kulifatilia sana , kiufupi alipotezea swala hilo na kuendelea na mambo yake na hilo kwake lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo amelifanya.

Baada ya kuingia mapokezi aliweza kuwasiliana na chumba ambacho alikuwepo mwanaume wake aliekuwa akimpenda na baada ya kuruhusiwa moja kwa moja alielekea huko , na kitendo cha kutoka tu mapokezi , waliingia wanaume wawili waliovalia kikawaida na moja kwa moja walielekea mapokezi na walitoa vitambulisho vyao vya kazi na kumuonesha mwanadada wa mapokezi na yeye baada ya kuwatambua watu hao ni wakina nani alitoa ushirikiano wa kutosha

Baada ya swala lile kuisha pale mapokezi mwanaume mmoja aliekuwa amevalia tisheri nyekundu ya Form six alibakia eneo la mapokezi na yule mwingine aliingia kwenye Lift .

Huku upande wa linda baada tu ya kuingia chumba alichokuwa Hamadi walirukiana na kupeana mabusu na kunyonyaka mfululizo jambo ambalo liliwapandisha sana hisia zao za kufanya mapenzi na ndani ya dakika chache tu walikuwa wote wapo kama walivyozaliwa na kijana Hamadi alionekana vyema katika kuumiliki mwili wa mpenzi wake Linda .

Hata pale simu ya Linda ivyotoa mlio wa kuashiria kuna ujumbe wa meseji umeingia hakushughulika nayo.

Nusu saa za purukushani mlango wao uligongwa na aliekwenda kufungua alikuwa ni Hamadi , lakini ile anafungua alijikuta akikutana na mwanaume ambae alikuwa katika uso wa kazi huku akiwa amemnyooshea bastora kitendo kile kilimfanya Hamadi atetemeke sana na hilo kwa Linda lilionekana mara moja lakini ni kama alichelewa kwani mwanaume yule alikuwa ashamtumia Hamadi kama kinga yake huku akimwamuru Linda asilete ubishi kwani akifanya jambo lolote la kijinga mwanaume huyo atapasuliwa ubongo .

Linda aliekuwa amejifunika na Shuka alijifikiria kwa muda na kisha aliinuka alipokuwa amekaa na kumsogelea mwanaume yule huku akipewa tahadhari za kutosegea hata hatua moja , lakini ni kama Linda hakujali hilo kwani alizidi kusogea licha ya mwanuaume yule kutishia kumpiga lisasi Hamadi .

Ilikuwa ni kitendo cha dakika chache , Hamadi alikuwa chini akiwa amepigwa risasi na mwanaume yule , lakini upande wa yule mwanaume alikuwa akiangalia bastora yake iliokuwa imedodokea mbali mara baada ya kupigwa teke na Linda .

Mwanaume yule alionekana kuwa akijiamini sana kwa mapigano , lakini kwa Lnda pia alichokuwa akiamini katika maisha yake ni kwamba katika taifa la Tanzania ukimtoa Damiani hakuna mtu mwingine ambae anaweza kumpiga na kumuangusha, hivyo hakuwa na presha hata kidogo , kwani ile mwanume yule analeta pigo za haraka za ngumi upande wa Linda alizipangua kama hana adabu nzuri huku akiendelea kumsoma adui yake , na alipoona adui yake kimafunzo alikuwa ni wa kawaida sana , alimpatia kile alichokuwa anataka , kwani kwa s spidi ya hali ya juu alirusha teke moja na mguu wa kushoto lisilo na nguvu lakini lililoonekana na adui yake na adui yake akataka kulipangua na hilo ndio likawa kosa kwani kama panya alimrukia na kwenda kutua shingoni mwa mwanaume yule huku papuchi yake ikigusana na macho ya yule mwanaume , lakini hakupewa hata mwanya wa kuangalia madini yaliokuwa ndani ya mgodi kwani aligongwa utosini na kisha alilegea na kushuka na Linda mpaka chini.

Linda alichukua simu yake na kisha aliangalia ujumbe uliokuwa humo na kujikuta akitoa tusi ni kama mtu aliekuwa akijitukana kwa kutoangalia huo ujumbe na baada ya kuona hivyo alivaa haraka haraka, alimwangalia Hamadi aliekuwa amelala sakafuni damu zikiwa zimetapakaa , alijilaumu kwa kujiingiza katika mapenzi nae kwani yote hayo yasingemtokea ,, aliinamna huku akionekana mwenye huzuni na kumfumba macho yake na kisha alitoka ndani ya chumba hicho na kutokomea .

Yule bwana aliekuwa ameachwa Mapokezi alijikuta akishaangaa kumuona Linda akitokezea na hapo hapo alitoa simu yake kumtafuta mwenzake , na hakupata majibu na hakutaka kuendelea kubaki pale alidhamiria kupanda juu kumtafuta mwenzake.

Lakini alichoweza kukutana nacho mara baada ya kufika ndani ya chumba alichokuwa Linda kilikuwa ni cha kuogopesha .

Alitoka mbio mbio ili kumuwahi Linda lakini alikuwa amekwisha kuchelewa kwani ajenti linda alikuwa ashatokomea kusiko julikana .

****

Saa kumi kamili za jioni wakati Linda akifikiria kwenda kuonana na mpenzi wake , upande wa huku Makongo juu mwanadada Janeth alikuwa amekaa amejipunzisha huku akifikiria hili na lile katika swala zima la kazi aliokuwa anaifanya , jambo moja ambalo lilikuwa likimuumiza kwa wakati huo ni juu ya Damiani , kwani alijua kwa namna yoyoe ile ni lazima mwanaume huyo alikuwa ashazini na mwanamama Rania , na kwake hilo lilimchanganya sana kila akikumbuka nyakati tofauti alizokiwa akipewa mapenzi na Damiani na kulinganisha na muda huo mwanamke mwenzake akipewa tamu aliokuwa akililia kila siku alijikuta roho ikimuuma kwani alikuwa akimpenda sana Damiani. .

Wakati akiendelea kuwaza juu ya hatima ya mapenzi yake simu yake iliingia ujumbe wa maandishi , na alifungua simu yake ili kuusoma huo ujumbe na hapo ndipo alipokutana na neno kidogo lililomchanganya , lakini neno hili lililokuwa katika ujumbe wa meseji ulitokea kwa jina lililokuwa limeseviwa kama SHUSHU. Yalikuwa ni maneno mawili tu yaliosomea PSYOPS to Jembe

Kwanza alishangazwa na nenp hilo , na alitumia dakika kadhaa kung`amua maana ya neno hilo kwanini litumwe kwenye simu yake , na mara baada ya kukumbuka kuwa mheshimiwa Jembe yupo nje ya nchi kwa ajili ya kula kiapo,alijikuka akitoa tusi baada ya kukumbuka kuwa neno hilo linamaana ya psychologival Operations , na ni mbinu ambayo jeshini hutumika mara nyingi kwa adui ambae wahusika wanataka kupata taatifa kutoka kwake ,na mara kama mbinu hii itatumika kwa mtu basi ni Dhahiri kwamba atamwaga siri zotemkama tu hautakuwa na mafunzo maalumu ..

Kitendo cha kudaka maana ya hilo neno aliamini kwamba kama mheshimiwa Jemebe ataweza kufanyiwa hilo jambo basi ni Dhahiri kwamba amekwisha kutoa siri ya juu ya mahali kambi yao ilipo na si hilo tu lakini pia atakuwa amewataja ajenti wote wa Mzalando na hilo lingewaweka katika hali ya hatari.

Baada ya kugundua uhatari wa swala hilo mara moja alituma ujumbe wa maandishi kwa ajenti wote kukutana mahali ambapo aliwaelekeza haraka sana hususani wale ambao mheshimiwa Jembe alikuwa akiwajua , huku akisisitiza wote walio katika kambi kutoka haraka..

Hivyo Janeth hakutaka kubakia hapo ndani alitaka kuhakikisha ajenti wote wa Mzalando hakuna hata mmoja anaekutwa na madhira ya kuingia kwenye mikono nya U-97 , alitoka haraka na kuingia kwenye gari yake kuelekea kurasini , wakati akiwa yupo bagamayo road kuna hisia zilizokuwz ikimwambia kuwa alikuwa akifatiliwa na jambo hilo alikuja kulithibirisha alivyokuwa Mwenge , lakini swala hilo halikumpa shida. Aliendelea kuendesha gari mpaka alivyokuja kuwachenga wale waliokuwa wakimfatilia na ndani ya muda mfupi alikuwa ndani ya jingo la NLT .

Baada tu ya kuingia ndani ya ‘basement’ aliwatoa wataalamu wawili ambao walikuwa wakihangaika na tarakishi zao kwamba waondoke kwani mahali hapo si salama tena .

Ndani ya dakika kadhaa kila kitu kilikuwa kwenye mkao na Janeth alikuwa ashachukua tahadhari zote na kutoka ndani ya ‘basement’ hio na kwenda kwa Rebeca ambaye alikuwa ndio mkuu wa usimamizi wa maswala ya kiwanda na kumpa maelekezo kwamba kiwanda hiko kifungwe mapema kabla ya saa kumi na mbili.

Baada ya Janeth kutoa maelekezo hayo aliingia kwenye ofisi yake na kisha alivuta begi lililokuwa lipo kwenye kabati na akavua nguo zake zote na kisha alisimama kwenye begi hilo na ndani nya sekunde chache tu alikuwa si Janeth tena , alikuwa ni mwanamke mweupe wa taifa la Korea , alijiangalia kwenye kiooo na kisha alitabasamu na kutoka na kuingia kwenye gari nyinginie tofauti na ile aliokuja nayo.

Baada ya kuingia kwenye gari alitoka hapo ndani huku akipishana na gari ile iliokuwa ikimfatilia , alitabasamu na kisha aliondoka .eneo hilo na ndani ya nusu saa alikuwa akipita Bunju kuelekea upande wa bagamoyo .

Dakika aribaini na tano mbele alikuwa eneo la Kiwangwa kwa mbele kabisa kulikuwa na shamba la katani , alikunja na kuchukua njia ya vumbi na kutembea umbali wa mita kadhaa na kufikia kwenye jumba moja la gorofa tatu lililokuwa limezungushiwa ukuta na mahali hapo kukiwa na baadhi ya nyumba kadhaa za watu waliokuwa wakiishi pembezoni , baada ya kuingiza gari alipaki na mtu aliekutana nae alikuwa ni Sabi mboneche .

"Vipi mmeweza kufika wote sabi?”

“ Hapana miss Janeth tupo wanne ambao tumefika hapa , shukrani kwa ujumbe wako tumeweza kutokukamatwa” aliongea Sabi huku wakiingia ndani na ndani ya dakika chache na Linda nae aliweza kufika ndani ya eneo hilo huku akifatiwa na wengine waliokuja kwa kupishana kwa muda kidogo.

Dakika kama kumi na tano ajenti wote kumi na mbili wa kambi ya mzalaneo walikuwandani ya kambi yao nyingine ndani ya eneo la Kiwangwa , hii sehemu hakuna ajenti aliekuwa akifahamu uwepo wake Zaidi ya Damiani na Janeth. .

Kwa nje ilionekana kama nyumba ya kawaida ya kuishi watu wenye maisha ya juu lakini chini ya nyumba hio kulikuwa na kila kitu tena Zaidi ya vitu vilivyokuwa ndani ya ‘basement’ ya Mzalendo kurasini lakini hii ikiwa ni ya kisasa Zaidi. .

Kila mmoja alishangaa baada ya kuoneshwa eneo hilo .

“Mimi na Damiani tulikuwa tukijua kuna siku jambo kama hili litatokea na ndio maana kambi hii iliweza kujengwa na kuanzia leo tunahamishia makao yetu yote mahali hapa ” Aliongea Janeth na kumfanya linda aliekuwa katika hali ya hudhuni kutabasamu , jambo ambalo hata Janeth lilimshangaza kwani hakumzoea Linda kwa hali aliokuwa nayo .

Baaada ya masaa kadhaa yaani saa mbili kamili za usiku , ajenti hawa walikuwa wapo bize kuangalia kama ni kweli kambi yao ilikuwa imegundulika , kwanni licha ya kwamba waliweza kufika mahali hapo , lakini walikuwa hawana uhakika asilimia mia moja kwamba eneo lao la mwanzo limegundulika , katika kufatilia ndipo muda wa saa tatu walipoweza kushuhudia kitu ambacho kiliwafanya kila mmoja azibe mdomo , kwani eneo lote la kiwanda chao lilibakia wingi zito mara baada ya kushuhudia ndege ikiachia bomu .

Hakuna alieweza kuamini kwamba watu hao wangeweza kuchukua hatua ya namna hio , walijikuta wakiongopa kwa wakati mmoja kwa tukio hilo .

“Shit , hii ni lazima tulipe” Aliongea Janeth kwa hasira huku akipiga ngumi kwenye meza .
TUTAENDELEA , RATIBA NI VIPANDE VIWILI KWA SIKU
MAWASILIANO NI WHATSAPP TU TUMA MESEJI 0687151346
 
Mkuu tunakungoja uku
 
Mkuu Singanor Jr ulisema vipande viwili Kwa siku, tukihesabu toka Alhamisi mpaka Leo tunavipande vyetu 12
 
SURA YA 12

Ni siku nyingine ndani ya nchi ya Marekani ndani ya jumba la kifahari ambapo mheshimiwa Jembe alikuwa ameandaliwa na U-97 kwa ajili ya kuishi .

Asubuhi hii mara baada ya taratibu zote kuisha kama kupata kifungua kinywa na mengineyo , mwanamama Hellen alimtaarifu mheshimiwa Jembe kujiandaa kuingia ofisini kwani kuna mgeni ambae anatarajiwa kufika kwa ajili ya hatua ya kwanza.

Na ndani ya nusu saa tu ya mheshimiwa Jembe kuingia ofisini hatimae bwana mmoja wa makamo mwenye rangi mchanganyiko yaani ya kizungu na kiafrika alitinga ofisini hapo, alikuwa ni bwana mmoja kwa makadirio ya umri wake si chini ya miaka therathini , alikuwa amevalia suti nyeusi na kipepeo shingoni huku nywele zake akiwa amezichana kuelekea nyuma. .

“Naitwa Dave Hamton afisa levo 32 ndani ya U-97 mimi ni mtaalamu wa maswala ya kiuchambuzi Duniani”utambulisho huo ulimfanya mheshimiwa Jembe kushangaa , kwani alaichotegemea ni hatua ya kwanza ya kula kiapo lakini anachokutana nacho ni mtu ambae amejitambulisha kama moja ya wachambuzi wa maswala ya kiuchumi duniani jambo ambalo kwake lilimshangaza kidogo .

“Karibu sana Dave”

“Asante sana mheshimiwa , Naamini umeshangazwa na utambulisho wangu”Aliitikia kwa kichwa

“Dhumuni la kikao chetu mheshimiwa ni juu ye kukuelezea juu ya malengo ya U-97 kwa Afiraka nzima kwa upande wa kiuchumi”Aliongea na kisha alitoa tablet yake na kumkabidhi mheshimiwa .

Mheshimiwa raisi alishangazwa na mambo mengi ambayo bwana Dave aliweza kumwambia , alikiri yeye mwenyewe katika kikao hicho kilichochukua masaa mawili kwamba umoja huu wa siri licha ya kwamba hakuwa akijua madhumuni yao makuu kwa mataifa ya kiafrika lakini kwa upande mwingine walikuwa wamesaidia ukuaji wa maendeleo kwa kiasi kikubwa sana , hususani katika swala zima la miundombinu na kuboresha maisha ya wananchi wengi , licha ya hivyo Dave aliweza kumuonesha nguvu ya umoja huu ndani ya mashirika makuu duniani kama vile IMF ,WB,UNICEF,WHO,ILO na mengineyo mengi makubwa .

Jambo hili kwa mara ya kwanza hakulielewa vyema mpaka pale alipoweza kufafanuliwa nguvu ya umoja huu ndani ya haya mashirika katika kuisadia Afrika ,bwana Dave alimwambia mheshimiwa kuwa U-97 ndio mara nyingi wanaohimiza mataifa mengi ya Afrika kupara misaada ya kufanya maendeleo na hii ni kwa zile nchi tu ambazo zitakuwa chini ya umoja huo .

Siku hio ilikuwa ni ya Vikao tu kwa mheshimiwa na watu hawa waliojitambulisha kwake kama wafuasi wa umoja NAMBA TISINI NA SABA ,

Mpaka inafika muda wa jioni wa vikao mheshimiwa alikuwa amepata uelewa mkubwa sana juu ya U-97 licha ya kutojua yandani ya umoja huo yaliokuwa yakitendeka lakini alipata kuweza kufahamu kuwa umoja huo kwa namna moja ama nyingine ulikuwa na faida kwa watanzania na alikiri kwamba watu aliokutana nao walikuwa na ushawishi mkubwa sana kwake.

Hatua za mwanzo za kula kiapo zilikuwa ni za kawaida na katika hatua zote hizo zilikuwa ni kwa ajili ya kuandaliwa kisaikolojia tu , hatua ya mwisho ndio ilikuwa ni ya kuogopesha sana kwa mheshimiwa Jembe , kwani katika hatua hii alikuwa akitakiwa kutubu dhambi zake zote , na ili uweze kupata nafasi ya kuweza kutubu dhambi anatakiwa kuweka siri zake zote wazi.

Siku iliofuata ilikuwa ni ya mheshimiwa Jembe kuingia kwenye chumba cha utakaso , hiki ni chumba ambacho sheria yake kubwa ni kwamba ili uweze kutakaswa na kula kiapo hutakiwi kuwa na jambo ambalo unalifich ndani ya moyo wako (Siri) , sheria za hiki chumba ni kwamba kama utaingia basi kunauwezekano mkubwa wa mtu kutoa siri zake zote kwa kile umoja huu ulichokuwa unakiita kuungama , yaani unaweka siri zako zote wazi ili uweze kupata nafasi ya kuungama na hatimae kuwa mwanaumoja kamili ambae huna makando makando , na kupitia hiki chumba cha utakaso siri nyingi ziliweza kupatikana juu ya mataifa mbali mbali . na si hivyo tu lakini pia kwa kila mwanachama ambae aliingizwa katika chumba hiko akitoka anakuwa mtu mpya na mtiifu kwa umoja, yaani kwa mnaneno marahisi ni kwamba kama ulikuwa na lengo baya dhidi ya umoja basi ukishaingia humo ndani , ukitoka utakuwa na malengo mazuri kwa umoja na utatii kila maelekezo utakayopewa na viongozi wa juu wa U-97.

Basi baada ya mheshimiwa Jembe kumaliza kujiandaa na kupata kifungua kinywa , walinzi wake walitaarifiwa kwamba mheshimiwa ataondoka ndani ya hio nyumba na kwenda katika kikao cha siri ambacho kitachukuwa takribani masaa kumi na mbili .

Hawa walinzi wake pamoja na wasaidizi kwanza kabisa hawakuwa wakijua kile kilichokuwa kikiendelea juu ya raisi wao kiula kiapo cha kujiunga na Umoja namba Tisini na saba , walichokuwa wakijua ni kwamba mheshimiwa alikuwa ndani ya taifa hilo kwa ajili ya maswala ya kitaifa, mtu mmoja pekee aliekuwa akijua kile kilichokuwa kikiendelea ni mlinzi wa karibu wa raisi (Bodyguard) na huyu katika safari hio ya kwenda kwenye kikao alikuwa amepewa nafasi ya kutangulizana nae , huku walinzi wengine wakiwa wamebakia ndani ya jumba la Wing 8.

Saa tatu kamili ndio saa ambayo mheshimiwa Jembe aliweza kutoka ndani ya nyumba aliokuwa amefikia kuelekea katika hekalu la Utakaso sehemu ambayo atakula kiapo rasmi cha kujiunga na umoja namba tisini na saba. Lakini pia sehemu ambayo alitakiwa kutakaswa na kuwa mpya .

Usafiri uliokuwa umetumika kumchukua mheshimiwa ndani ya Wng 8 house ulikuwa ni wa njia ya anga kwa kutumia chopa , huku ndani ya ndege hio akiongozana na mlinzi wake wa karibu na bwana mmoja ambae alijitambulisha kwa jina la Henlsink , bwana huyu alikuwa ni raia kutoka Mexico , alikuwa amevalia suti ya rangi nyeusi.

Ndani ya nusu saa tu walikuwa wapo ndani ya eneo ambalo mheshimiwa raisi na mimi mwenyewe sikueza kulitambua , lakini ndani ya eneo hilo lililokuwa limezungukwa na miti mingi kulikuwa likionekana jengo kama hekalu .

Chopa iliweza kukanyaga veyema eneo husika lenye alama kubwa ya H na baada ya hapo mheshimiwa alitoka na kuja kupokelewa na wanadada wawili , waliokuwa wamevalia kama masista , baada ya kupokelewa na hawa wadada ambao walijitambulisha kama wahudumu wa jumba hilo liliokuwa na maandishi makubwa mlangoni U-97 LODGE X .

Mheshimiwa Jembe alionekana kuwa na wasiwasi mkubwa kila alipokuwa akikumbuka maneno ya mwanamama Hellen juu ya jambo ambalo linafanyika ndani ya hekalu hilo kwa ajili ya utakaso, alikuwa na hofu ya kutoa siri zake na siri kubwa aliokuwa akihofia kuitoa ilikuwa ni juu ya mpango wa Mzalendo .

Aliamini kama kweli alichoambiwa na mwanamama huyo juu ya uwezekano wa kuweka siri zake hadharani , swala hilo lilimuongopesha sana , kwani aliamini kwa kufanya hivyo ni kwamba anakwenda kuharibu kila kitu na ile mipango ambayo alikuwa amejiwekea na kitengo cha Mzalendo inakwenda kukwama.

Baada ya utaratibu wa awali kukamilika wa mheshimiwa Jembe kupewa mavazi mengine kama yale ya wagnjwa wa hospitalini , aliweza kuingizwa kwenye chumba kimoja kilichokuwa kina maandishi makubwa mlangoni kama PSYOPS ROOM , maneno ambayo kwa mheshimiwa hakuweza kuyaelewa kabisa .

Ndani ya hili jumba ni kwamba muonekano wake ulikuwa ni kama wa hospitali , kwa nje lilionekana kama hekalu ila kwa ndani ni jEngo ambalo lilikuwa limejengwa kwa ustadi wa kutenganisha vyumba , na ilionekana hio ni sehemu maaliumu kabisa kwa ajili nya U-97 , ukutani kulikuwa na michoro mingi ambayo ilikuwa imechorwa na haikueleweka maana yake ni nini kwa mara moja .

Mlinzi wa mheshimiwa raisi bwana Tomasi Kibwe alikuwa kwenye wasiwasi mwingi , kwani ni takribani masaa nane tokea mheshimiwa aingie ndani ya chumba ambacho hakuelewa ndani ya ke ni kitu gani kilikuwa kikifanyika , ubaya ni kwamba hakuweza kutoka mahali alipo kwani alikiuwa amewekewa ulinzi , wasiwasi wake ulikuwa juu japo ya wahusika wa jumba hilo kumhakikishia usalama wa mheshimiwa Jembe ,, lakini yeye kama mwanausalama hakuweza kuwa katika hali ya utulivu , aliamini kama kuna jambo baya lolote likamtokea Raisi basi yeye moja kwa moja angewajibika na hakuelewa angewaeleza nini watanzania.

Lakini wasiwasi wake ulikuja kukoma mara baada ya kusubiri lisaa limoja mbeleni na hapo ndipo alipoweza kumuona mheshimiwa Jembe akitoka ndani ya chumba alichoingizwa akiwa na mavazi yake ya suti , lakini kwa bwana Tomasi aligundua jambo ambalo si la kawaida kutoka kwa mheshimiwa Jembe , hali ya furaha iliokuwa imetanda kwenye uso wake.

“kila kitu kipo sawa Tomasi huna haja ya kuwa na wasiwasi Zaidi” Aliongea mheshimiwa na Tomasi alipiga Saluti kuonyesha kwamba anakubali kile mheshimiwa alichokuwa anasema .

Basi kwa kutumia njia ile ile mheshimiwa aliweza kurudi Wing 8 House lakini akionekana kuwaza jambo .

“Sikuwa na jinsi ilinibidi kueleza kila kitu juu ya Mzalendo , hatuwezi kushindana na hawa watu kamwe njia moja ya mimi kuliongoza taifa la Tanzania ni kula sahani moja na hawa watu ” Aliongea mheshimiwa wakati akiwa anaingia ndani ya Wing 8 na kupokelewa na kikosi chake cha usalama ambacho muda wote kilikuwa kipo katika hali ya wasiwasi juu ya usalama wa Mheshimiwa.

“Hongera sana mheshimiwa kwa hatua yako ya mwisho”

“Nashukuru sana Hellen”

“Kesho ni siku yako ya mwisho ya ukaribisho ndani ya U-97 lakini pia ndio siku utapata fursa ya kuzungumza na wafanyabiashara wakubwa ambao kama mazungumzo yako yataenda vyema ni fursa kwa watanzania wote” Aliongea Hellen na Jembe alikubaliana nae na baada ya hapo aliaga na kuondoka

*****

Upande mwingine nchini Tanzania masaa machache mara baada ya kukamilika kwa hatua ya mwisho ya Raisi jembe ndani ya Tanzania , ndani ya ofisi ya mkuu wa kitengo cha usalama wa Taifa bwana Nassoro Kinga alipokea ujumbe wa maandishi kutoka kwa namba ambayo hakuweza kuifahamu ujumbe huo ulikuwa ukisomeka ‘MZALENDO BASE AT KURASINI NLT TOWER GROUND FLOOR ,Damiani Rabani , Janeth Bendera , Linda ….’

Meseji hii ilimsisimua sana mheshimiwa na hakutaka kusubiri , dakika hio hio aliinua simu na kumpigia Kent na kumueleza ujumbe huo , lakini jibu kutoka kwa Kent lilimfanya atabasamu kwani hisia zake zilikuwa ni kweli na hii ni mara baada ya Kent kumwambia Nasoro kuwa andae operesheni ya dharula ya kuvamia jingo la NLT sehemu ambayo walikuwa wakijua kuwa ndio makao makuu ya kambi ya Mzalendo .

Baada ya Kinga kuweka simu yake chini hakutaka kuchelewa hata kwa dakika , kwani alinyanyua simu yake na kutoa maagizo na ndani ya dakika moja tu bwana mmoja aliejazia mwili aliingia ndani ya jengo hilo , huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Mr White .

“kuna operesheni ya dharula inatakiwa kufanyika usiku wa leo”

“Misheni gsani hio mheshimiwa ?”

“Tumepata eneo la maficho ya kambi ya Mzalendo hivyo nataka usiku wa leo tukavamie hio kambi , lakini kabla ya hilo kufanyika nataka watu hawa wafuatao tujue mahali walipo”Aliongea Kinga na kutoa kumtajia majina Mr White , yalikuwa ni jumla ya majina kumi na mbili ya ajenti wote wa Mzalendo.

“Mishenni hii inatakiwa kufanyika kwa weledi wa hali ya juu sana , sitaki makossa , watu tunaoenda kupambana nao ni watu makini hivyo lazima na sisi tuwe makini , watu hawa sitaki akosekane mtu hata mmoja , unda timu ambayo itavamia usiku Kurasini na unda timu nyingine itakayowafatilia mahali walipo hawa wanaojiiita wazalendo wa nchi hii “ Aliongea mheshimiwa Kinga na kisha Mr white aliondoka kwa ajili ya kupanga timu yake kuipeleka kwenye mapambano..

Ndani ya masaa kadhaa tu tokea Mr white apewe jukumu la kuunda timu kwa ajili ya kufatilia wanamzalendo , alikuwa akitoa taarifa kwa mheshimiwa Kinga juu ya hatua ambayo wamepiga .

“Tumeweza kujua jumla ya ajenti saba walipo kwa muda huu na vijana wapo wanawafatilia kwa kila hatua, walioweza kupatikana ni Janeth bendera , Linda ,Zakayo ,Kassimu ,Sabi Mboneche………”Aliongea ajenti Nyuu au Mister White.

“Hawa wengine wako wapi ?”

“Mkuu kuna uwezakano hawa kuwa katika kambi yao”

“Huo ni uwezekano tu Bakari ninachotaka ni uhakika kama kweli wapo kwenye kambi yao , hususani huyu Damiani Rabani , ndio mtu muhimu sana kwenye hiki kitengo na ni lazima tujue ni wapi alipo kwani kossa la kumpoteza huyu ni kwamba misheni yetu imefeli”.

“Ndio mheshimiwa ngoja tuendelee kufalitilia mahali walipo kabla ya muda wa operesheni kufika “ aliongea ajenti nyuu au Mr White na kisha aliondoka , akimuacha bwana Kinga katika mawazo mawazo ya hapa na pale , lakini muda mfupi baada ya kutoka kwa Mister White Kinga alipokea simu kutoka kwa Kent .

“Operesheni imefikia wapi ?” ilisikika upande wa pili .

“Ajenti saba wapo katika macbo yetu , wengine watano hatujui walipo akiwemo Damiani Rabani , tunakisia wanaweza wakawa ndani ya kambi yao”Aliongea Kinga .

“Piga bomu hio kambi , sambaratisha kila kitu na kuhusu hao wengine waliopatikana hakikisha mnawakama wakiwa hai”Aliongea Kent na kisha simu ilikatwa .

Jambo hili kidogo lilimuacha Kinga katika mshangao lakini hakuwa na jinsi , alikuwa yupo tayari kufata maelekezo ya Kent ya kupiga bomu kiwanda cha NLT Kurasini , baada ya kufikiria kwa dakika kama mbili , alitoka na moja kwa moja alienda mpaka chumba cha ufatiliaji wa operesheni hio .

“wapi mmefikia ?”

“Janeth bendera anaonekana kuelekea upande wa Kurasini , vijana wapo kazini wanaendelea kumfatilia , nadhani hili litakuwa jambo jema tukivamia akiwa ndani ya kambi “ aliongea Bakari”

“Vipi kuhusu wengine sita ?”

“Tupo nao macho na wanaonekana kutoondoka katika maeneo ambayo wameonekena “

“Operesheni ya leo usiku ni kupiga bomu katika kambi yao , haitajarisha ni nani yupo ndani ya kambi ninachotaka kambi hio ndani ya masaa sita yajayo pawe vumbi tu ndio linaloonekana”Aliongea mheshimiwa Kinga na kufanya watu wote washangae .

“Uko siriasi mheshimiwa, hilo jambo ni hatari sana kwani wengine ambao hawahusiki wanaweza kupata madhara , na isitoshe tunawezo wa kuingia ndani ya kambi hio na kuwakamata wahusika bila kufanya uharibifu mkubwa”

“Bakari maamuzi yangu ni hayo na yanatoka moja kwa moja kutoka kwa mheshimiwa Raisi , hivyo saa tatu kamili ya usiku nataka kiwanda cha NLT kiwe vumbi , andaa vijana kwa hio misheni” Ajenti nyuu alijikuta akishangazwa sana na maamuzi hayo , lakini hakuwa na kupinga kwani mkuu wake wa kazi alikuwa ashaafanya maamuzi na ni moja ya jukumu lake kufata maamuzi ya mkuu wake .

“Ni shambuilio la bomu la aina gani linapaswa kutumika?”

“Tutatumia shambulio la Anga”

******

Captain Juma hizza alikuwa ndio kwanza anaingia nyumbani kwake Tegeta muda wa saa kumi na mbili za jioni , kwake hiio ndio muda wake wa siku zote wa kufika nyumbani akitokea kazini , na bwana huyu alikuwa ni moja ya watu ambao walikuwa wakipenda sana kurudi nyumbani mapema na kuiona familia yake , hii ni tabia ambayo alikuwa amejijengea lakini pia ni tabia ambayo ilimpa heshima kubwa sana kwa majirani zake .

Kwani ni tabia ya kawaida sana na iliozoeleka kwa baadhi ya wababa wafamilia kuchelewa kurudi nyumbani baada ya kazi , kwani wao mara baada ya kazi walipitia sehemu mbali mbali wanazozijua wao kwa ajili tu ya kupoteza muda ili wasirudi nyumbani mapema .

Jambo hili lilikuwa tofauti kwa Juma kwani yeye alikuwa akiwahi sana kurudi nyumbani , basi baada ya kulakiwa na watoto wake wawili Salma na Hamisa aliingia chumbani na kujimwagia maji ili kuondoa uchomvu , lakini wakati anaendelea kuoga mara mke wake aliita akimtaarifu kwamba simu yake ilikuwa ikiita na jina la mpigaji lilikuwa ni bossi .

Baada ya kusikia jina hilo alitoka na kuchukua simu hio na kupokea kwani aliamini sio kawaida kwa bossi wake kumpiigia kwa wakati huo tena mara baada ya kurudi kazini .

Baada ya kuweka simu sikioni ndani dakika chache aliweza kupata maelekezo ya kurudi kazini kuna opetesheni ya dharula ambayo alikuwa akipaswa kuifanya usiku huo , huku akielekezwa na mkuu wake huyo wa kazi kwamba eneo husika atapewa akiwa angani.

Juma hizza alikuwa ni moja ya marubani wa ndege za kijeshi waliokuwa wakiaminiwa sana na kitengo cha dharula cha jeshi cha maswala ya makombora ya kurushwa kwa Anga , licha ya kufanya kwake kazi miaka mingi hakuweza kuutumia usomi wake katika kurusha ndege na kwenda kushambulia eneo , kwani ndani ya taifa letu kulikuwa na Amani kubwa sana kiasi kwamba ni mara chache sana ndege za kivita zilikuwa zikitumika .

Sasa siku hio mara baada ya kupokea taarifa hio ya kutumia ndege yake kwa ajili ya kwenda kushambulia ni kama walimpa mzuka kabisa , kwani jambo alilokuwa akilitaka siku zote ni hilo litokee ili aweze kuonyesha manjonjo yake .

Lisaa limoja mara baada ya kupewa maelekezo alikuwa ndani ya ndege yake kubwa ya kivita iliokuwa ikifahamika kwa jina la Bird killer ndege iliokuwa imetengenezwa nchini Urusi , ndege hio iilikuwa na uwezo wa kubeba mabomu yasiooungua mia moja na kushambulia kwa umbali mrefu kutoka angali bila kukosa Target.

Saa mbili na nusu za usiku Captain juma hiza alikuwa akielea angani akiwa na shauku kama zote za kufanya shambulio katika eneo ambalo wakubwa wake walimuelekeza kumtumia ‘cordinates’

“Ndani ya dakika kumi na tano tu za kuwa angani hatimae aliweza kupokea uelekeo husika wa Terget yake anayopaswa kwenda kufanya shambulio .

“Target locked . need permission to engage” aliongea Juma akiomba ruhusa ya kuachia kombora kwani tageti alikuwa ashaipata .

“ umeruhusiwa” mIlikuwa ni neno dogo lakini lililoleta madhara makubwa sana , kwani ndani ya sekunde kadhaa ndani ya eneo lote la Kurasini lilikuwa halitamaniki , lakini si hivyo tu , wakazi waliokuwa kuwa maeneo ya karibu na eneo hilo walikuwa katika taharuki kubwa kwani ni jambo ambalo hawakuwahi kulishuhudia kwenye maisha yao ukilinganisha na historia ya taifa la Tanzania kutokuwa na matukio ya ajabu kama hayo ..

UNAWEZA KUIPATA KWA SHILINGI 2000 SOFTCOPY WATSAPP NAMBA NI 0687151346 AIRTELL MONEY AU 0657195492 TIGOPESA AU 0623367345 HALOPESA JINA ISSAI SINGANO UKISHATUMA TUMA SKRINISHOT YA MUAMALA WATSAPP KWA NAMBA 0687151346
 
SURA YA 13​

Linda mara baada ya Damiani kuelekea nchini Australia alijikuta akipendana na kijana wa kipemba aliekuwa akijulikana kwa jila la Hamadi , kwa mara ya kwanza ya Linda kukutana na Hamadi ilikuwa ni siku aliokuwa mapumzikoni ndani ya kisiwa cha Unguja ndipo alipoweza kuonana na mfanya biashara Hamadi na kwanzia siku hio ya kukutana waltokea kupendana sana kwa muda wa siku chache walizodumu pamoja .

Siku ambayo mheshimiwa Jembe anaelekea nchini Marekani ni siku ambayo Linda akiwa ndani ya kambi ya Mzalendo aliweza kuwekeana ahadi na Hamadi kuonana siku mbili mbele kwani Hamadi alikuwa akija bara akitokea Dubai alipokuwa bize kibiashara , jambo hili kwa Linda lilimpa munkari sana ukijumlisha na namna ambavyo alikuwa amemmiss Hamadi , alijua fika kazi yake haikuwa ikimruhusu kupenda , lakini kwa kijana Hamadi alikuwa ameloea kwani kijana huyo alikuwa akijua kumdekeza mno Linda kiasi cha kumchanganya sana .

Siku mbili mbele kama walivyo ahidiana , hatimae Hamadi alifika nchini na kumtaarifu Linda kwamba yupo hoteli ya Golden Tulip katikati ya jiji la Dar es salaam , Muda ambao Linda anawasiliana na Hamadi alikuwa ndani ya kambi ya Mzalendo na ilikuwa ni muda wa saa saba na nusu kwenda nane wakati wakiwa wanawasiliana na walipanga saa kumi na moja za jioni Linda atafika hotelini hapo .

Siku hii ndani ya kambi hii walikuwemo jumla ya watu watatu waliokuwa zamu katika kuhakikisha kila mipango inaenda sawa , yaani Linda alikuwa na wenzake wawili ambao wote kwa ujumla wao walikuwa wakihusika na maswala ya kitehama ndani ya kambi hii ya Mzalendo.

Ilipotimu muda wa saa kumi na robo Liuda aliwaacha wenzake wakiendelea na majukumu na yeye alitoka kwa ajili ya kwenda kuonana na mpenzi wake Hamadi, mwanadada Linda alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Crown nyeupe na ni gari ambayo alikuwa akiipenda sana kutembelea nayo licha ya kwamba alikuwa na gari nyingine aina ya BMW lakini gari hio ya kijapani ndio moja ya gari alizokuwa akipendelea sana kutembelea .

Kuna jambo ambalo lilimtia wasiwasi , na hio ni mara baada ya kuingia ndani ya maegesho ya magari ndani ya hoeli ya Golden Tulip , kwani kuna gari aliitilia mashaka , kwani tokea anatoka Kurasini gari hio ni kama ilikuwa nyuma yake , japo mwanzoni hakuwa akiitilia mashaka , lakini kitendo cha kuegesha gari yake ndani ya hoteli hio na kuiona lile gari swala hilo lilimpa mashaka kidogo lakini hakuwa akitaka kulifatilia sana , kiufupi alipotezea swala hilo na kuendelea na mambo yake na hilo kwake lilikuwa ni kosa kubwa sana ambalo amelifanya.

Baada ya kuingia mapokezi aliweza kuwasiliana na chumba ambacho alikuwepo mwanaume wake aliekuwa akimpenda na baada ya kuruhusiwa moja kwa moja alielekea huko , na kitendo cha kutoka tu mapokezi , waliingia wanaume wawili waliovalia kikawaida na moja kwa moja walielekea mapokezi na walitoa vitambulisho vyao vya kazi na kumuonesha mwanadada wa mapokezi na yeye baada ya kuwatambua watu hao ni wakina nani alitoa ushirikiano wa kutosha

Baada ya swala lile kuisha pale mapokezi mwanaume mmoja aliekuwa amevalia tisheri nyekundu ya Form six alibakia eneo la mapokezi na yule mwingine aliingia kwenye Lift .

Huku upande wa linda baada tu ya kuingia chumba alichokuwa Hamadi walirukiana na kupeana mabusu na kunyonyaka mfululizo jambo ambalo liliwapandisha sana hisia zao za kufanya mapenzi na ndani ya dakika chache tu walikuwa wote wapo kama walivyozaliwa na kijana Hamadi alionekana vyema katika kuumiliki mwili wa mpenzi wake Linda .

Hata pale simu ya Linda ivyotoa mlio wa kuashiria kuna ujumbe wa meseji umeingia hakushughulika nayo.

Nusu saa za purukushani mlango wao uligongwa na aliekwenda kufungua alikuwa ni Hamadi , lakini ile anafungua alijikuta akikutana na mwanaume ambae alikuwa katika uso wa kazi huku akiwa amemnyooshea bastora kitendo kile kilimfanya Hamadi atetemeke sana na hilo kwa Linda lilionekana mara moja lakini ni kama alichelewa kwani mwanaume yule alikuwa ashamtumia Hamadi kama kinga yake huku akimwamuru Linda asilete ubishi kwani akifanya jambo lolote la kijinga mwanaume huyo atapasuliwa ubongo .

Linda aliekuwa amejifunika na Shuka alijifikiria kwa muda na kisha aliinuka alipokuwa amekaa na kumsogelea mwanaume yule huku akipewa tahadhari za kutosegea hata hatua moja , lakini ni kama Linda hakujali hilo kwani alizidi kusogea licha ya mwanuaume yule kutishia kumpiga lisasi Hamadi .

Ilikuwa ni kitendo cha dakika chache , Hamadi alikuwa chini akiwa amepigwa risasi na mwanaume yule , lakini upande wa yule mwanaume alikuwa akiangalia bastora yake iliokuwa imedodokea mbali mara baada ya kupigwa teke na Linda .

Mwanaume yule alionekana kuwa akijiamini sana kwa mapigano , lakini kwa Lnda pia alichokuwa akiamini katika maisha yake ni kwamba katika taifa la Tanzania ukimtoa Damiani hakuna mtu mwingine ambae anaweza kumpiga na kumuangusha, hivyo hakuwa na presha hata kidogo , kwani ile mwanume yule analeta pigo za haraka za ngumi upande wa Linda alizipangua kama hana adabu nzuri huku akiendelea kumsoma adui yake , na alipoona adui yake kimafunzo alikuwa ni wa kawaida sana , alimpatia kile alichokuwa anataka , kwani kwa s spidi ya hali ya juu alirusha teke moja na mguu wa kushoto lisilo na nguvu lakini lililoonekana na adui yake na adui yake akataka kulipangua na hilo ndio likawa kosa kwani kama panya alimrukia na kwenda kutua shingoni mwa mwanaume yule huku papuchi yake ikigusana na macho ya yule mwanaume , lakini hakupewa hata mwanya wa kuangalia madini yaliokuwa ndani ya mgodi kwani aligongwa utosini na kisha alilegea na kushuka na Linda mpaka chini.

Linda alichukua simu yake na kisha aliangalia ujumbe uliokuwa humo na kujikuta akitoa tusi ni kama mtu aliekuwa akijitukana kwa kutoangalia huo ujumbe na baada ya kuona hivyo alivaa haraka haraka, alimwangalia Hamadi aliekuwa amelala sakafuni damu zikiwa zimetapakaa , alijilaumu kwa kujiingiza katika mapenzi nae kwani yote hayo yasingemtokea ,, aliinamna huku akionekana mwenye huzuni na kumfumba macho yake na kisha alitoka ndani ya chumba hicho na kutokomea .

Yule bwana aliekuwa ameachwa Mapokezi alijikuta akishaangaa kumuona Linda akitokezea na hapo hapo alitoa simu yake kumtafuta mwenzake , na hakupata majibu na hakutaka kuendelea kubaki pale alidhamiria kupanda juu kumtafuta mwenzake.

Lakini alichoweza kukutana nacho mara baada ya kufika ndani ya chumba alichokuwa Linda kilikuwa ni cha kuogopesha .

Alitoka mbio mbio ili kumuwahi Linda lakini alikuwa amekwisha kuchelewa kwani ajenti linda alikuwa ashatokomea kusiko julikana .

****

Saa kumi kamili za jioni wakati Linda akifikiria kwenda kuonana na mpenzi wake , upande wa huku Makongo juu mwanadada Janeth alikuwa amekaa amejipunzisha huku akifikiria hili na lile katika swala zima la kazi aliokuwa anaifanya , jambo moja ambalo lilikuwa likimuumiza kwa wakati huo ni juu ya Damiani , kwani alijua kwa namna yoyoe ile ni lazima mwanaume huyo alikuwa ashazini na mwanamama Rania , na kwake hilo lilimchanganya sana kila akikumbuka nyakati tofauti alizokiwa akipewa mapenzi na Damiani na kulinganisha na muda huo mwanamke mwenzake akipewa tamu aliokuwa akililia kila siku alijikuta roho ikimuuma kwani alikuwa akimpenda sana Damiani. .

Wakati akiendelea kuwaza juu ya hatima ya mapenzi yake simu yake iliingia ujumbe wa maandishi , na alifungua simu yake ili kuusoma huo ujumbe na hapo ndipo alipokutana na neno kidogo lililomchanganya , lakini neno hili lililokuwa katika ujumbe wa meseji ulitokea kwa jina lililokuwa limeseviwa kama SHUSHU. Yalikuwa ni maneno mawili tu yaliosomea PSYOPS to Jembe

Kwanza alishangazwa na nenp hilo , na alitumia dakika kadhaa kung`amua maana ya neno hilo kwanini litumwe kwenye simu yake , na mara baada ya kukumbuka kuwa mheshimiwa Jembe yupo nje ya nchi kwa ajili ya kula kiapo,alijikuka akitoa tusi baada ya kukumbuka kuwa neno hilo linamaana ya psychologival Operations , na ni mbinu ambayo jeshini hutumika mara nyingi kwa adui ambae wahusika wanataka kupata taatifa kutoka kwake ,na mara kama mbinu hii itatumika kwa mtu basi ni Dhahiri kwamba atamwaga siri zotemkama tu hautakuwa na mafunzo maalumu ..

Kitendo cha kudaka maana ya hilo neno aliamini kwamba kama mheshimiwa Jemebe ataweza kufanyiwa hilo jambo basi ni Dhahiri kwamba amekwisha kutoa siri ya juu ya mahali kambi yao ilipo na si hilo tu lakini pia atakuwa amewataja ajenti wote wa Mzalando na hilo lingewaweka katika hali ya hatari.

Baada ya kugundua uhatari wa swala hilo mara moja alituma ujumbe wa maandishi kwa ajenti wote kukutana mahali ambapo aliwaelekeza haraka sana hususani wale ambao mheshimiwa Jembe alikuwa akiwajua , huku akisisitiza wote walio katika kambi kutoka haraka..

Hivyo Janeth hakutaka kubakia hapo ndani alitaka kuhakikisha ajenti wote wa Mzalando hakuna hata mmoja anaekutwa na madhira ya kuingia kwenye mikono nya U-97 , alitoka haraka na kuingia kwenye gari yake kuelekea kurasini , wakati akiwa yupo bagamayo road kuna hisia zilizokuwz ikimwambia kuwa alikuwa akifatiliwa na jambo hilo alikuja kulithibirisha alivyokuwa Mwenge , lakini swala hilo halikumpa shida. Aliendelea kuendesha gari mpaka alivyokuja kuwachenga wale waliokuwa wakimfatilia na ndani ya muda mfupi alikuwa ndani ya jingo la NLT .

Baada tu ya kuingia ndani ya ‘basement’ aliwatoa wataalamu wawili ambao walikuwa wakihangaika na tarakishi zao kwamba waondoke kwani mahali hapo si salama tena .

Ndani ya dakika kadhaa kila kitu kilikuwa kwenye mkao na Janeth alikuwa ashachukua tahadhari zote na kutoka ndani ya ‘basement’ hio na kwenda kwa Rebeca ambaye alikuwa ndio mkuu wa usimamizi wa maswala ya kiwanda na kumpa maelekezo kwamba kiwanda hiko kifungwe mapema kabla ya saa kumi na mbili.

Baada ya Janeth kutoa maelekezo hayo aliingia kwenye ofisi yake na kisha alivuta begi lililokuwa lipo kwenye kabati na akavua nguo zake zote na kisha alisimama kwenye begi hilo na ndani nya sekunde chache tu alikuwa si Janeth tena , alikuwa ni mwanamke mweupe wa taifa la Korea , alijiangalia kwenye kiooo na kisha alitabasamu na kutoka na kuingia kwenye gari nyinginie tofauti na ile aliokuja nayo.

Baada ya kuingia kwenye gari alitoka hapo ndani huku akipishana na gari ile iliokuwa ikimfatilia , alitabasamu na kisha aliondoka .eneo hilo na ndani ya nusu saa alikuwa akipita Bunju kuelekea upande wa bagamoyo .

Dakika aribaini na tano mbele alikuwa eneo la Kiwangwa kwa mbele kabisa kulikuwa na shamba la katani , alikunja na kuchukua njia ya vumbi na kutembea umbali wa mita kadhaa na kufikia kwenye jumba moja la gorofa tatu lililokuwa limezungushiwa ukuta na mahali hapo kukiwa na baadhi ya nyumba kadhaa za watu waliokuwa wakiishi pembezoni , baada ya kuingiza gari alipaki na mtu aliekutana nae alikuwa ni Sabi mboneche .

"Vipi mmeweza kufika wote sabi?”

“ Hapana miss Janeth tupo wanne ambao tumefika hapa , shukrani kwa ujumbe wako tumeweza kutokukamatwa” aliongea Sabi huku wakiingia ndani na ndani ya dakika chache na Linda nae aliweza kufika ndani ya eneo hilo huku akifatiwa na wengine waliokuja kwa kupishana kwa muda kidogo.

Dakika kama kumi na tano ajenti wote kumi na mbili wa kambi ya mzalaneo walikuwandani ya kambi yao nyingine ndani ya eneo la Kiwangwa , hii sehemu hakuna ajenti aliekuwa akifahamu uwepo wake Zaidi ya Damiani na Janeth. .

Kwa nje ilionekana kama nyumba ya kawaida ya kuishi watu wenye maisha ya juu lakini chini ya nyumba hio kulikuwa na kila kitu tena Zaidi ya vitu vilivyokuwa ndani ya ‘basement’ ya Mzalendo kurasini lakini hii ikiwa ni ya kisasa Zaidi. .

Kila mmoja alishangaa baada ya kuoneshwa eneo hilo .

“Mimi na Damiani tulikuwa tukijua kuna siku jambo kama hili litatokea na ndio maana kambi hii iliweza kujengwa na kuanzia leo tunahamishia makao yetu yote mahali hapa ” Aliongea Janeth na kumfanya linda aliekuwa katika hali ya hudhuni kutabasamu , jambo ambalo hata Janeth lilimshangaza kwani hakumzoea Linda kwa hali aliokuwa nayo .

Baaada ya masaa kadhaa yaani saa mbili kamili za usiku , ajenti hawa walikuwa wapo bize kuangalia kama ni kweli kambi yao ilikuwa imegundulika , kwanni licha ya kwamba waliweza kufika mahali hapo , lakini walikuwa hawana uhakika asilimia mia moja kwamba eneo lao la mwanzo limegundulika , katika kufatilia ndipo muda wa saa tatu walipoweza kushuhudia kitu ambacho kiliwafanya kila mmoja azibe mdomo , kwani eneo lote la kiwanda chao lilibakia wingi zito mara baada ya kushuhudia ndege ikiachia bomu .

Hakuna alieweza kuamini kwamba watu hao wangeweza kuchukua hatua ya namna hio , walijikuta wakiongopa kwa wakati mmoja kwa tukio hilo .

“Shit , hii ni lazima tulipe” Aliongea Janeth kwa hasira huku akipiga ngumi kwenye meza .

UNAWEZA KUIPATA KWA SHILINGI 2000 SOFTCOPY WATSAPP NAMBA NI 0687151346 AIRTELL MONEY AU 0657195492 TIGOPESA AU 0623367345 HALOPESA JINA ISSAI SINGANO UKISHATUMA TUMA SKRINISHOT YA MUAMALA WATSAPP KWA NAMBA 0687151346
 
Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom