Simulizi -Kitabu kilichojaa majina yote

SURA YA 14​

Ugiriki ni moja ya nchi zilizokuwa na nguvu sana enzi hizo ndani ya bara la ulaya na duniani kwa ujumla , ndio sehemu pekee ambayo falsafa ilizaliwa na ndio sehemu pakee duniani ambayo demokrasia ilianzia , watu kama Socrates na Plato ndio watu maarufu waliowahi kuwapo katika Ugiriki ya kale .

Ni mara yangu ya kwanza kufika ndani ya nchi hii katika jiji hili la Athen , jiji kubwa ndani ya taifa hili la Ugiriki .Athen ni moja ya sehemu iliojengeka sana kimiundombinu licha ya kwamba haikuwa kubwa sana , lakini ilikuwa ikivutia sana kwa muonekano wake .

Sehemu kubwa ya Ugiriki ni visiwa ukilinganisha na sehemu nyingine ndani ya bara la ulaya , ugiriki inavisiwa takribani elfu mbili huku chini ya mia mbili ndio visiwa pekee wanavyoishi watu .

Kisiwa maarufu sana ndani na nje ya ugiriki ni Santorin mahali ambapo ndio nilikuwa nikitarajia kwenda muda mfupi ujao baada ya kutua ndani ya uwanja huu wa ATH hapa Athen , sifa inayoupa umaarufu wa kisiwa hichi kwa nilivyosoma ni muonekano wa kisiwa chenyewe , miinuko ya visiwa vya Santorini iliosababishwa na mlipuko wa volcano katika bahari ya Aegen ndio uliokuwa ukiipa chati sana ugiriki na kufanya ipendwe kutembelewa na watu wengi .

Muda ambao nimeingia hapa Athen ni muda wa saa kumi na mbili za jioni na sikuwa na nia kabisa ya kulala ndani ya jiji hili moja ya mpango wangu tokea natoka Sydney ni kulala ndani ya kisiwa cha Santorini kwani niliamini kwa kulala huko ninaweza kupata mwanga wa kumpata Peter na kikundi chake cha The truth , niliweza kupata ndege ya moja kwa moja kwenda Santorin ya kampuni ya ndani ya nchi hii yenye jina ambalo nashindwa hata kulitamka vyema .

Ni mwendo wa nusu saa tu ulionichukuwa kuwa angani mpaka kufika katika visiwa hivi ndani ya sehemu iliokuwa ikifahamika kwa jina la Fira , baada ya kufika ndani ya uwanja huu wa ndege wa Santorin , sikutaka kupoteza muda kabisa kwani muda ulikuwa umeenda sana , nilipakia Taxi ambayo moja kwa moja ilinipeleka hoteli moja iliokuwa ikifahamika kwa jina la Volcanic view hotel .

Ilikuwa ni hoteli nzuri na moja kubwa ndani ya kisiwa hichi ambayo nilipenda kulala mahali hapo , na niliamini pia kwa kulala ndani ya hoteli hio nisingeweza kukosa namna ya kuwasiliana na kikundi hiki cha The Truth,

Naam hatimae nipo kwenye chumba ndani ya hoteli hii ya kisasa kabisa , niliweka vitu vyangu na kujiweka sawa kimwili baada ya kumaliza niliona sasa ni wakati wa kuwaza namna ya kuwasiliana na kikundi hiki cha The Truth , ukweli ni kwamba muongozo ulikuwa ukinileta tu hapa santorin lakini sikuwa na namna ya kuwasiliana na kikundi hiki , lakini nilijua lazima kuna namna na mimi ndio nilikuwa nikipaswa kuitafuta .

Siku hii ambayo nipo hapa Santorin ndio siku ambayo nilipata taarfa kwamba mheshimiwa Jembe alikuwa akienda Marekani kwa ajili ya kula kiapo sikushangaa sana kwani niliamini ni moja ya taratibu za umoja huu ulionileta ndani ya nchi hii ya Ugiriki kutafuta uelekeo wa kupata kitabu cha Book of all names ili kuutoomeza umoja huu ndani ya taifa la Tanzania .

Muda ambao nipo kwenye hiki kisiwa ndani ya hii hoteli ilikuwa yapata saa mbili kasoro za usiku , hali ya hewa ni ya baridi ukiwa nje , lakini ukiwa ndani ya hii hoteli joto lake ni la wastani linaloendana na mwili.

Moja ya mpango wangu kwa usiku hio ni kwenda katika Casino ya aina yoyote ile ,. Niliamini kwa kuingia ndani ya Casino hizo ningeweza kupata njia ya kuwasiliana na kikundi hiko , kwani niliamini ni lazima kuna mtu ashawafi kufanya kazi na kikundi hiki .

Basi baada ya kujiweka sawa nilitoka ndani ya chumba changu huku nikikiangalia kitanda kwa uchu kwani nilikuwa na uchomvu kwa mbali uliokuwa unashawishi kulala , nilitoka na moja kwa moja kwenda upande wa mapokezi ili kupata taarifa za uwepo wa Casino ndani ya hii hotel na bahati ilikuwa kwangu kwani hoteli hii ilikuwa na Casino kubwa tu iliokuwa ghorofa ya Tano , sikutaka kuchelewa wala kufikiria swala la msosi nilitaka kumaliza kila kitu usiku huu ili asubuhi niamke na jambo lingine .

Niliweza kuingia ndani ya hii Casino iliokuwa ikifahamika kwa jina la Grand V casino , ilikuwa ni kubwa kweli kweli iliokuwa imesheheni watu ambao walikuwa bize wakicheza kamali , huku mziki mzuri usiokuwa unachosha ukisikika , ukiambatana na wadada waliovalia nguo za ndani wakiwa wanawapa watu burudani na kupendezesha Zaidi madhati ya Casino.

Walinzi wa hapa ndani walikuwa wakinikodolea macho kweli utadhani niliingia kuiba ila mimi sikutaka kuwajali kabisa , niliingia ndani kabisa huku nikipita baadhi ya meza ambazo zilizungukwa na wanaume kwa wanawake waliokuwa wakicheza kamali huku wakiwa wameshikilia mvinyo iliokuwa ikiwasindikiza katika kazi yao hio waliokuwa wakifanya .

Nilisogea upande wa Bar , upande wa kushoto wa Casino hii na kisha kuketi kwenye viti virefu , sehemu hii nimeipenda kwani ilikuwa inaonesha karibia nusu ya watu wote waliokuwa wapo ndani ya Casino hii , na mimi kukaa hapo niliona ni vyema kwani ningeweza kupata muongozo ninao utaka .

Baada ya kukaa hapo na kuagiza Whiskey nakuanza kunywa taratibu huku macho yangu yakiwa yanatembea ndani ya chumba hiki kila upande , sura nilizoweza kuziona ndani ya hii casino nyingi ni za kizungu , kihindi na kijapani , sura zenye rangi ya kiafrika zilikuwa chache sana , na za kuhesabika tena kwa upande wa ngozi nyeusi hapa ndani wengi niliwaona kama mabaunsa wanaotoa ulinzi binafsi kwa matajiri hawa waliokuwa wakicheza Kamali .

Niliendelea kudumu kama kwa dakika kumi na tano mpaka pale , mtu mmoja kati ya wengi waliokuwa ndani ya hii Casino kunivutia , bwana huyu kwanza ulinzi wake ulionekana kuwa mkali sana , lakini pili ni kwamba huyu bwana uchezaji wake wa kamali ulionekana ni washari sana na jambo hili kidogo lilinivutia niliamini huyu bwana kwa vyovyote vile biashara zake na kila kitu anachokifanya katika maisha yake kumuingizia pesa si halali na hilo ndio jambo ambalo nilikuwa nikilitafuta kwa muda mrefu na hapo hapo niliamuwa bwana huyu ndio tageti yangu kwa usiku huu.

Niliendelea kuingalia tageti yangu , huku nikiwa nimevalia miwani yangu ya kijasusi , nilitaka kwanza kumjua kwa undani huyu mtu ni nani kabla sijachukua hatua ya kumvamia , niliweza kunasa sura yake na kuituma kwenye Dreamer T na ndani ya sekunde chache tu nilikuwa na majibu yalionifanya nitabasamu .

Jina lake maarufu alikuwa akijiita Nikemura ni raia kutoka Japani mfanya biashara lakini pia jambo la kufurahisha ni kwamba bwana huyu anamiliki kampuni ya Ulinzi ndani ya Japani akilinda matajiri na mali zao , lakini jambo hili sikukubaliana nalo kwani bwana huyu alionekana kama wale viongozi wa Mafia yaani hulka zake zote zilionyesha hivyo na swala hili lilinipa munkari kidogo ya kutaka muda wangu ufike nione napambana na mtu gani na je ni kama hisia zangu ni sahihi kama bwana hiyi angeniwezesha kupata mwanga wa kukutana na hiki kikudni cha The Truth.

Baada ya masaa mawili Nikemura alinyanyuka na kutoka katika meza yake likiongozwa na mabaunsa yake manne, niliona wanachukuwa uelekea wa kutokea nje na jambo hilo kwangu niliona ndio linafaa kwani nilipanga kuwavamia kwenye lift.

Sikutaka kuchelewa tena nilitoa hela ya watu ya Whiske na kuiweka kwenye meza chini ya glass na kisha nikasogea uelekeo waiokuwa wameelekea , ilinichukua dakika moja kufanya vitenndo vyote hivyo Ile natoka tu niliona lift waliongia inataka kujifunga na mimi niliikimbilia na kuizuia na kisha nikaingia jambo ambalo niliona kabisa halikumfurahisha , nilipita na kukaa nyuma yao na moja ya baunsa likanizuia nisiende nyumba na sikutaka kuchelewesha hapo hapo nilifanya pigo la kushitukiza na nilimpiga shingoni akalegea nikamzungusha na kumuweka kama ngao , uzuri ni kwamba hii lift ni kubwa ilikuwa na uwezo wa kubeba watu hata kumi baada ya kumlegeza wale waengine walipaniki nilimwangalia kihelehele na kisha nilimrushia yule baunsa alielegea kwenda kwake na kisha nikamfata mwingine na kumpiga staili ya Krav Maga ili kumzimisha kabisa na pigo hilo lilifanikiwa , uzuri ni kwamba hawakuwa na bastora , sasa nilikuwa nimebakia na mabaunsa mawili na Nikemura aliekuwa akihema kwa nguvu na nilipanga nifanye tukio hilo dakika chache kabla ya lift kufunguka , wale mabaunsa walikuja kizembe na mimi sikuwachelewesha moja nililipiga teke la korodani na kuliegeza vibaya na sikuchelewa nililipiga lile linguine ngumi ya kifua na ikadunda nikaona nikilieta uzembe anaweza kunizidi , niliamua kulipiga double hit karate , ya mbavu , yaanin hii pigo unapiga kwa mikono yote miwii kwenye mbavu na ukifanikiwa vyema adui yako anakosa pumzu ya ghafa na hilo ndio kilichotokea , na sikumchelewesha baada ya kuona anavuta hewa kwa tabu kama ana korona nilimpiga pigo la shingo na kumzimisha nikamrudia yule mwingine na kisha nikambutua na teke moja na akaenda chini mkuku , lakini ile namgeukia Nikamura nikaona kaninyooshea Bastora , niliangalia namna ambavyo ameishika huku akionekana kutojiamini na hilo lilikuwa kosa kwake kwani ndani ya sekunde ilikuwa mikononi mwangu .

“Tutatoka kimya kimya mpaka nje ya maegesho ya gari bila usumbufu wowote ukileta ujinga utakufa kwa siraha yako”niliongea kwa lugha ya kingereza na alionekana kunielewa .

Sekunde chache tu nilikuwa nje ya eneo la mapokezi na tulipita bila shida yoyote ile mpaka kwenye parking ya magari , nilimwamuru atoe ufunguo na aelekee kwenye gari waliokuja nayo na akafanya kama nilivyomwagiza na sekunde chache nilikuwa siti ya nyuma yeye akiwa ya mbele na kisha akalitoa gari nje kabisa ya geti na tukatokomea barabarani.

Tuulichukua umbali wa dakika kama kumi tu hivi niliona sehemu salama kwa gari kusimama na nilimwamuru asimamishe na akatii , na bwana huyu alionekana kuwa bandidu kweli kwani hakuonekana kuwa na wasiwasi licha ya kwamba nilikuwa nikimpa maelekezo na kuyatii na hili liliniambia kwamba huenda alikuwa akikumbana na matukio ya namna hii mara kwa mara .

Nilimwamuru asimamishe gari na kisha nilitoa picha ya kasuku iliokuwa na jina chini yake na kumuonesha .

“Nataka namna ya kuwasiliana na hiko kikundi , ukinipa ushirikiano mzuri nakuachia uende ukiwa salama , usipo nipa jibu ninalotaka basi mabaunsa yako yatakuokota kwenda kukuzika”Alionekana kunielewa , aliangalia picha ile kwa dakika kadhaa na kisha alinigeukia na kisha alionekana kucheka jambo ambalo lilinishangaza lakini niliendelea kuonyesha usiriasi wangu .

“Caprino Club”

“Ndio nini ?”

“Nenda Caprino Club nunua tiketi za Zeus Club daraja la kwanza na maelekezo mengine utayapata”

“Caprino Club inapatikana wapi?”

“Unaonekana kuwa mgeni, Caprino ipo hoteli tuliotoka Ghorofa ya mwisho kabisa”Taarifa hio niliona inanitosha kabisa , nilimuamuru ashuke kwenye gari na nilivyo ona kashuka nilirukia siti ya dereva na kisha nilifunga mlango na kuondosha gari huku nikimuacha ananitukana matusi ya kila namna , baada ya kukaribia hotelini nilipaki gari mbali kidogo na kisha nikashuka huku nikiacha gari lile likiendelea kunguruma na kuingia hotelini.

Caprino club ilikuwani moja ya Club kubwa iliokuwa ndani ya hoteli hii ambayo sikuweza kuifahamu kwa mara ya kwanza uwepo wake , kulikuwa na kila aina ya ngoma zilizokuwa zinachezwa humu ndani , baada ya kuingia nilijisogeza upande wa kulia wa kaunta na kisha nikaagiza whine , na baada ya kupewa nilimuuliza yule bwana aliekuwa muhudumu .

“Chumba namba nane , nenda kulia “ aliongea kwa lugha ya kingereza na mimi sikutaka kuchelewa nilinyanyuka nikiwa na chupa yangu na kwenda upande wa kulia na kweli niliona chumba namba nane , nilisukuma mlango na kuingia na hapo ndipo nilipokutana na mwanadada mrembo sana wa kizungu akiwa amezungukwa na watu wa tatu akishikwa shikwa , baada ya kuniona alinifata kwa madaha kabisa na nikamueleza shida yangu na akanambia nifate , nilisoge upande mwingine , na nilichogundua ni kwamba hiki chumba kilikuwa kama ni mlango wa kuingia vyumba vingine.

“There is qualifications not everyone can handle Zeus ticket “ aliongea yule mwanadada akisema kuna vigezo vya kupata hio tiketi kwani sio kila mtu anaweza kuinunua .

“I am business man , Stephano lamberk from Tanzania , you can chek my name on social media posted everywhere”.alitabasamu. na kisha alitoa simu na sikujua kitu anachokifanya kwani alionekana kuandika meseji ndani ya dakika tano aliniangalia na kutabasamu .

“Welcome Mr Stephano Lamberk I will be honered to serve you , as for your Ticket you have to make payment first then everything will follow” nilitoa kadi yangu ya benki na kisha kumpatia na ndani ya dakika tano alikuwa ashafamnya malipo tayari huku uzunguni mambo yanaenda kwa Credit card huna haja ya kutembea na Cash muda wote .

Zilikuwa ni pesa ndefu zilizokuwa zimetoka katika hio kadi , ila sikujali kabisa kwani dhumuni langu ni lazima litimie usiku huo kabla hakuja kucha.

“ you are ready to go Mr Stephano , Follow me” aliongea na mimi sikuwa na maswali mengi nilinyanyuka na kisha kumfata.

Tuliingia kwenye lift ambayo ilitupeleka moja kwa moja mpaka chini na kutoka nje kabisa na ndani ya dakika chache tulikuwa kwenye gari aina ya Bentley nyeusi .

“How about other client , seem leaving your office?”

“You are my last client and one of great deal for today” aliongea huku akimaanisha Kwamba mimi ni mteja wake wa mwisho lakini mwenye uzito wake kwa siku ya leo .

“How am I of great Deal?”.

“You are Stephano Lamebrk” aliongea na sikutaka kuongezea neno zaidi , ndani ya dakika kumi na tano tulikuwa upande mwingine kabisa wa fukwe , sehemu hii ilikuwa ni kama bandari , mbele yangu kulikuwa na bonge la meli ya kifahari kabisa iliokuwa na maandishi makubwa ya Zeus super luxury Club.

Yule mdada ambae hakujitambusliaha jina kwangu aliniangalia baada ya kusimamisha gari na kutabasamu na kisha alitoa kikadi Fulani kama cha benki kile na kunikabidhi.

“that is your ticket” aliongea na mimi nilichukua huku akinipa ishara na kunionyesha kwamba napaswa kuendelea mwenyewe kwanzia hapo , nilitoka nje ya gari na kusogea mbele kabisa sehemu iliokuwa na ulinzi mkali , nilitoa kadi ile na kupitisha katika kizuizi na kikafunguka na nikapita.

SURA YA 15​

Baada ya kuingia kwenye lango ambalo pia nilitumia kadi ile ile kufungulia , nilipokelewa na bwana mmoja hivi aliekuwa amevalia uniform za club hio mzungu lika la ujana , alijitambulisha kwangu kama muhudumu na kisha alinipatia kitabu , nilifungua ukurasa wa kawaida , na nikagundua kuwa kile kitabu kilikuwa kikionesha madaraja na sehemu ambazo nilipaswa kuchagua ili kwenda , niliangalia ukurasa wa kwanza hapakunifaa , nikaenda ukurasa wa pili na penyewe hapakunifaa , ukurasa wa tatu ndio ulionifaa kwani niliona nembe nilio kuwa nikiitafuta , nembo ya The Truth.

Nilimuonesha na kisha aliniambia nimfate , na mimi sikupinga , Hii meli ilikua ni kubwa mno , kubwa sana na iliukua ya kifahari mno , ni aina za meli ambazo sikuwahi kufikiria kupanda katika maisha yangu licha ya kwamba nilikuwa na vihela lakini sikuwahi kufikiria kuja kupanda katika hii meli , muonekanao wake ulikuwa ni kama hoteli kubwa ya kitalii kwani ilikuwa ni kama gorofa kwenda juu , nilitembea kwa sekunde kadhaa na kisha nilisimama sehemu ya kukaguliwa na hapa sio kukaguliwa na watu hapana yaani unasimama katika ya alama ya duara na unapigwa na mwanga flani wa laser wa rangi ya blue na kisha kama hauna kifaa chochote cha hatari mlango unafunguka , muda wote huo muhudumu huyu alikuwa nyuma yangu , huku mimi nikiwa nimejawa na shauku ya kupata kile kilichonisumbua siku kadhaa bila kukipata.

Basi ndani ya dakika kadhaa za kutembea hatimae nilikuwa mbele kabisa ya mlango mkubwa uliokuwa na picha kubwa la kasuku , mlango ule ulifunguka wenyewe na kisha niliingia huku yule muhudumu akiondoka kwa kuniambia kuwa alikuwa ashanifikisha , baada ya kuingia eneo la ndani ya hii sehemu nilikuta nikishangaa mkao wake .

Ilikuwa ni sehemu kama kampuni kabisa kwani upande wa kulia kwangu ilikuwa ni sehemu ya mapokezi na hii sehemu alikuwa amesimama mwandada mmoja wa kizungu alievalia akapendeza huku upande a kulia wa hili eneo ilikuwa ni sehemu yenye viti vya kukaa.

“Sorry for any of our service to be served there is entry fee you must pay prior to anything” aliongea huyu mwanadada namimi sikuwa na hiyana , nilitoa kadi yangu iliokuwa na pesa ndefu na kisha kumpatia .

Na baada ya dakika moja alinipa kadi nyingine inayofanan na ile ya mwanzo

“unataka huduma gani hapa ndani?”

“Kuna taarifa nataka kununua kama itakuwepo”

“we have all information here”

“ then that will serve me better” niliongea na kisha alinipa maelekezo ya kwenda upande wa kushoto na niingie chumba chenye alama X na nitatumia hio kadi kufungulia hiko chumba na huduma zangu zote nitapata hapo.

Sikuwa na ubishi nilisogea upande huo wa vyumba na kupata chumba ambacho kilikuwa na hio alama na kisha kwakutumia kadi niliolipia pesa nyingi na kisha kilifunguka , kilikuwa ni chumba chenye kiti kimoja na tarakishi ambayo sikuona CPU yake Zaidi ya hio monitor ya inch 32 kama sikosei.

Mpaka hapo nilikuwa nishaelewa nini kinaendelea , na mimi sikuwa mshamba wa aina hio , nilisogea kwenye ile tarakishi na baada ya kuigusa tu ilionesha maandihi ya kunitaka kuingiza kadi yangu niliopewa kama vile ATM na nilichomeka ile kadi upande wa kushoto ambao kulikuwa na sehemu ya kuchomeka na baada ya hivyo pale pale jina langu liliotokea

“Welcome Mr Stephano Lamberk we are the Truth and you can ask us anything”Hayo ndio maandishi yaliokuwa yakisomeka kwenye Screen .

“Natafuta uwepo wa kitabu ‘Book of all names’ Niliongea maana hakukuwa na sehemu ya kuandikia na kilionekana kialama cha kwa juu kikiniruhusu kuongea lugha yoyote zilizoorodhshwa hapo , Kiswahili hakikuwepo hivyo nilitumia kingereza.

“Wait moment”

“That is high classified information, to unlock this info please enter your credit card for additional payment of about 100000$”Aisee kilikuwa ni kiasi kikubwa mno cha pesa Zaidi ya milioni mbili za kitanzania nilijifikiria kwa dakika chache lakini niliona sina jinsi nilitoa kadi na kuichomeka sehemu ile ile pembeni kidogo.

“There is no book of all names found till now but there is one high classified ancient story about book of all names and that is one of top sacred classified story within U-97 and only high Rank level member know about it ”

Hakuna uwepo wa kitabu cha majina yote duniani mpaka sasa kilichogunduliwa lakini kuna hadithi ya kale kuhusiana na hiko kitabu na hio story ni moja ya stori takatifu kuwapo ndani ya U-97”

“Nawezaje kuwapata hawa wafuasi wa juu wa U-97?”

“That is another info with different payment you are requesting Mr Stephano Lamberk , to unlock your answer re-insert your credit card for payment verification “ Nilichomoa kadi yangu na kisha nikaichomeka tena na ndani ya sekunde kiasi kingine kama kile kile kilikuwa kimekatwa , yaani jumla ya milioni 500 za kitanzania zilikuwa zimenitoka .

“ We have Proffessor Mike Alan from Stanford university as one of top rank member of U-97”.

Baada ya kupata taarifa hio sikutaka kuuliza maswali mengine kwani niliamini pesa ingezidi kukata , nilitamani kuuliza Erick yupo wapi lakini sikuona haja ya kufanya hivyo , nilipanga kumpa hatua kwa hatua Rania ili aweze kumfatilia mwanae kwani niliamini kwa namna yoyote atakuwa ndani ya hii meli akila bata huku mama yake akihangaika kumtafuta.

Jambo moja tu ambalo nililikubali sana ndani ya hiki kikundi ni namna ambavyo makato yao yapo juu , niliamini ile stori ya mwanamama Rania juu ya mtoto wake kuanzisha kampuni iliokuwa imejaa ukweli ambao niliushuhudia kwa macho yangu ilikuwa ni ya kuaminika , utaratibu wa kupata taarifa ndani ya kikundi hiki ilikuwa ni wa kipekee sana ambao ulikuwa ukiendesha kidigitali Zaidi.

Nilitoka nikiwa na maswali makuu mawili ambayo yalihitaji ufumbuzi wangu , kwanza nilipanga kumtafuta huyu profesa Mike ili niweze kujua hio historia ya book of all names kwanza , kwani swala hili lilinichanganya , kwani nilichokuwa nikiamini ni kwamba kitabu hiki kipo , sasa swala la the Truth kuniambia kuwa hakuna hiko kitabu duniani lilinichanganya sana , lakini lilifanya kazi yangu izidi kuwa ngumu mno .

Niliangalia saa wakati huu nikiwa nimeketi ndani ya ukumbi wa bar ndani ya meli nikiangalia ustaarabu wa kutoka kwani mpaka wakati huo tulikuwa katikati ya bahari ilikuwa yapata saa nane za usiku.

Nilitoa simu yangu mara baada ya kuona mlio wa meseji umeingia , niliangalia na kuona ulikuwa ukitoka kambi ya Mzalendo yalikuwa ni maelezo yaliokuwa yakimuhusu bwana Mike Alan na sehemu anayopatikana kwa muda huo , alikuwa yupo chini Marekani na mimi hapo hapo niliona ni wakati wa kutoka kwenye hii meli na kuanza safari ya kwenda Marekani kumfatilia Mike Alan.

Wakati nikiendelea kuwaza nilijikuta nikizungukwa na mabwana wanne waliokuwa wameshiikilia bastora zao wakiwa wamevalia suti nyeusi na miwani , kilikuwa ni kitendo cha ghafla sana kuzungukwa na hawa mabawana ambacho hata mimi sikukitegemea kwani niliamini ndani ya hili eneo kulikuwa na usalama mkubwa.

“Nyoosha mikono yako juu na usilete ujinga wa aina yoyote maana kitendo chochote cha kutujaribu utakuwa ni mfu kwa wakati huo” Aliongea mwanaume ambae alionekana kuwa ndio kiongozi wao , hawa mabwana wote walikuwa ni wa rangi nyeupe yaani wazungu.

Sikutaka kupinga nilinyoosha mikono juu kusalimu amri kwani niliamini hapo nikileta ujinga ninaweza kupasuliwa na risasi

SURA YA 16​

Niliweza kufungwa pingu mikononi na kisha nikatupiwa kwenye chumba ambacho niliamini kilitumika kama selo na pia sehemu ya mateso ndani ya hii meli , kwani ndani ya hili eneo licha ya uwepo wa kitanda lakini kulionekana pia vifaa vya kufanyia mateso , lilikuwa ni eneo gumu sana kutoroka kama tu utataka kufanya hivvyo ,kulikuwa na kadirisha kadogo sana ambako hata mwanga kalikuwa hakapitishi vizuri .

Wale mabwana baada ya kunitupa walitoka nje na kuniacha ndani ya kile kichumba nikisubiria hukumu yangu , sikujua ni kipi kinafuata lakini nilikuwa tayari kuweza kukabiliana nacho na sikuwa na woga hata kidogo .

Jambo moja tu ambalo nilikuwa nina uhakika nalo ni kwamba nitatoka ndani ya hii meli na kusepa zangu kwenda Marekani kumfatilia Profesa Mike Alan , nilibaki kwa takribani nusu saa ndipo mlango ule ulifunguliwa tena na hapa ndipo nilijikuta nikishuhudia mtu ambae nilitaka kuulizia taarifa zake , huyu hakuwa mwingine bali alikuwa ni Erick Peter Mtanzania mwenzangu , lakini mtoto wa Rania , alikuwa ni kijana mdogo kimuonekano tofauti na nilivyokuwa nikimkadiria , lakini licha ya kuwa mdogo alionekana ni kijana ambae alikuwa akijiamini mno na hilo nililishuhudia katika macho yake na utembeaji wake.

Aliingia hapo ndani akiwa ametangulizana na wale watu waliokuwa wamenikamata , baada ya kuniangalia kwa sekunde alitabasamu na kisha aliwaamuru wale vijana wanifungulie zile pingu na kisha akawaambia watoke walinde kwa nje .

“Mr Damiani Rabani a.k.a Stephan Lamberk” aliongea huku akiketi kwenye kiti kilichokuwa hapo ndani na mimi nikiwa kwenye kile kijitanda .

“Kuwa na heshima dogo”.

“Hahahaha … Damiani Rabani kulala na mama yangu kitanda kimoja kusifanye unaweza ukawa baba yangu , kumbuka upo ndani ya himaya yangu na ninaweza kuamua chochote kuhusu maisha yako sasa” aliongea na mimi nikiwa na mwangalia tu akijitahidi kuweka usiriasi wake ambao ulimezwa na sura yake ya kitoto.

“Naweza nikawa ndani ya himaya yako lakini kumbuka nipo hapa kwa matakwa yangu mwenyewe na nitaondoka kwa matakwa yangu vilevile”.

“Nakujua vyema bwana Damiani Rabani”.

“Unanijua vipi na kwanini ulikuwa na picha yangu kwenye chumba chako?”

“Mimi ndio mwanzilishi wa The Truth na sisi kama kampuni tunamiliki ukweli unaonekana na usio onekana na nadhani umeishuhudia nguvu yangu katika hilo”

“ Sina shaka juu ya hilo lakini nataka kujua kwanini unapicha yangu na katika huo ukweli wako unaonekana na usio onekana nipo kwenye kundi lipi?”

“Wewe ni ukweli unaonekana na usionekana upo kwenye makundi yote mawili na kuhusu kukujua naweza kusema wewe ndio ulionipa sababu ya mimi kuunda kikundi hiki mara baada ya kujua historia nyuma ya maisha yako , lakini pia uhatari wa jambo unalotaka kulifahamu”

“Jambo gani hilo nataka kulijua linaloniweka katika hatari?”

“Book of all names and U-97”.aliongea huku akitoa tablet yake na kunipatia .

“Hiko ni kiasi nilichoahidiwa kupatiwa endapo nitatoa taarifa ya kile ulichokuwa unataka kukijua kutoka kwetu na si wewe tu, kwa kila atakaetaka kujjua ukweli kuhusu Book of all names , na mpaka sasa nimeingiza pesa nyingi sana kuwauzia watu kuhusu ukweli na pia nimewauza watu ambao walitaka kuujua ukweli kuhusu Book of all names, kama unavyojua kampuni yangu inauza ukweli hivyo kila nikipata ukweli ambao una mteja nina uuza na wewe ni sehemu ya ukweli ambao tayari nina mteja yupo tayari kuununua”

“Kama mimi ni sehemu ya biashara yako kwanini mpaka sasa hujaniuza ukajipatia pesa?”

“Mimi ni mfanyabiashara na kati ya watu wote wewe pekee ndio mtu ambae niliona kuna nafasi ya sisi wawili kukaa chini na kuongea , kwani niliona pesa kubwa Zaidi kuliko ambayo ningepata kama tu ningekuuza”Sauti ya Erick ilinifundisha mambo makuu mawili kuhusu yeye mwenyewe , alionekana ni kijana ambae ashaanza kunusa pesa na pesa ambayo alikuwa akipata alitaka mara mbili yake , lakini si hivyo tu niliona ni kijana ambae anapenda kuwa na madaraka makubwa.

“Unajua nini Zaidi kuhusu Book of all names?”

“Huko ndio tunakoelekea na ndio sababu kubwa ya mimi kukuleta mahali hapa na kuwa na haya mazungumzo”

“Endelea”

“Kwanza niseme tu kwamba bwana Stephano swala unalolifatilia hujui uhatari wake , na laiti ungekuwa unajua uhatari na nguvu iliopo juu ya Book of all names ungeacha kabisa kulitamka hilo neon na kurudi nchini Tanzania kuendelea na maisha yako”.

“Nipo hapa kwasababu sina maisha ya kuendeleza na nipo hapa kwakuwa nipo tayari kukutana na aina yoyote ile ya hatari ilimradi tu kutimiza malengo niliokuwa nayo , hivyo naomba uniambie kile unachokijua kuhusu hiki kitabu”

“Sina mengi ya kukuambia , kila kitu uliweza kulipia na kupata ukweli wako , ninachokusisitizia tu ni kwamba futa katika kichwa chako juu ya uwepo wa book of all names japo naaminni kitabu hiko kitakuja kuwepo”

“Bado sijakuelewa na naona kama unajikanyaga mwenyewe unaniambia nifute katika kichwa changu uwepo wa kitabu hicho huku unaniambia kitakuja kuwepo , jibu sahiihi ni lipi?”

“Jibu sahihi ni kwamba kitabu hicho mpaka sasa kipo katika hadithhi tu”

“Unaongea kama una ukweli wote juu ya kitabu hiko , ninachoamini ni kwamba kitabu hiko kitakuwepo ila wewe hujui kama kipo”

“ kama kipo wewe unadhani kitabu hiko kitakuwa na nani ?”

“U-97”

“Hahahaha .. kwanza kabisa niseme kwamba mpaka sasa najua kwama haujui nguvu ilioko ndani ya umoja huo unaoutaja , lakini pili haujui mipango yote ambayo inafanywa na hup umoja kwa ajili ya kukipata kitabu hicho , sasa niambie kama umoja huo wenye nguvu kitabu hiko hawana na wanafanya kila mpango kukipata wewe unawezaje kuthibitisha hilo , labda tu ni kuulize ni malengo yapi unayo pale utakapo pata kitabu hiko?”

“Hilo ni juu yangu, lakini kubwa Zaidi ninataka kwanza kujua Mpango Zero unamaana gani na njia pekee ninayo amini inaweza kunipa majibu yote ni juu ya kupata kitabu hiko” Niliongea huku akionekana kutabasamu , alionekana kujua kila jambo ninalozungumza .

“Tunapoteza muda mwingi bwana Damiani kutokana na kwamba upo katika kiza kinene , dhumuni langu kubwa kukuleta hapa ni kutaka kukusaidia kutimiza malengo yako kwa njia rahisi kabisa huku ukinisaidia mimi kufikia malengo yangu”aliongea na mimi nilimshangaa kidogo .

“Malengo yako ni yapi na kwanini unadhani ninaweza kukusaidia kufikisha malengo yako?”

“Malengo yangu ni kuhitaji unisaidie kupata book of all names na mimi nitakusaidia kuuondoa umoja namba tisini na saba ndani ya Tanzania , lakini pia utapata fursa ya kulipiza kisasi kwa wale wote waliohusika na kifo cha mama yako na wengineo nadhani hayo ndio malengo yako”.

“Nitakusaidia vipi kutimiza malengo yako ilihali kitabu chenyewe umesema kwamba kipo katika hadithi tu , lakini nina sababu ipi ya mimi kukusaidia kupata hiko kitabu”

“Kwasababu malengo yako ni kuondoa Umoja Namba Tisini Na Saba ndani ya taifa la Tanzania na mimi malengo yangu ni kumiliki kitabu hicho na kwa kuanzia tu mpaka sasa ninajua nini maana ya mpango Zero na kama utakubaliana na ofa yangu basi kwanzia sasa nitakueleza nini maana ya mpango huo ndani ya Taifa la Tanzania “

“Unamaanisha unajua nini kipo nyuma ya Mpango Zero?”

“Najua kila kitu kuhusu hilo na najua mengi Zaidi ya hayo ni wewe kukubaliana na mimi kusaidiana kukipata kitabu hiki na mimi kukusaidia kutimiza melengo yako ni hivyo tu , kama utakubaliana na mimi useme hapa na kama hautiokubaliana na mimi basi hautakuwa na thamani tena kwangu nitakuuza kama nilivyo uza wengine na kujipatia pesa”

“Niambie nini maana ya mpango Zero”

“Swali hilo linamaanisha kwamba umekubali kufanya kazi na mimi”

“Ndio”

“Kwa kifupi tu ni kwamba mpango Zero ni sehemu ya hatua ambazo zinafanya na U-97 katika kutafuta Book of all names na hii ni baada ya hatua yao waliokuwa wakiitegemea kwa karne nyingi kufeli”

“ Hatua gani hio?”

“Time Travel Technology “

Kwanza nilishangaa kwa Erick kuniambia kuhusu hili neno , sio kwamba nilishangaa kwa kutolijua , la hasha kilichonishangaza ni kwa vipi mpango Zero unahusiana na Time Travel kwani ninachojua mimi ni kwamba Time Travel nikitendo cha kwenda mbele au nyuma ya muda , yaani ni kwamba kama unataka kusafiri kwenda utoto wako basi kitendo hiko ndio kinaitwa Time Travel na hii safari sasa ingewezakana kama tu kungekuwa na uwepo wa Time Machine , kwa wale ambao waliwahi kuwangalia Movie ya Avenger watakuwa wanaelewa ninachomaanisha hapa.

“Nadhani unajua kwa miaka mingi wanasayansi walikuwa wakifanyia utafiti juu ya Time machine ili kuwezesha uwezo wa mtu kusafiri mbele au nyuma ya muda , sasa hizi harakati zote za uvumbuzi wa hii mashine ulikuwa ukifadhiliwa na U-97”.

“Kwanini walikuwa wakitaka hio teknolojia kupatikana kwa hamu kubwa kiasi hicho?”

“Book of all names”

“ How?”

“Sababbu hio sijaijua bado ila nakaribia kuijua ila juu ya hilo nahitaji sana msaada wako , lakini kuendelea ni kwamba , baada ya umoja huu kuona teknolojia hii kuchukua muda mrefu na wao wanataka kukamilisha misheni yao ya kuitawala dunia mapema(NEW WORLD ORDER) ndio walipokuja na njia mbadala ya time Travel”

“Njia gani hio?”

“Hapo sasa ndio ulizaliwa mpango Zero , huu ni mpango ambao ni mbadala wa Time Travel , kupitia wanasayansi wengi waliopo chini ya U-97 wanaamini kwamba kuna uwezekano wa akili ya mtu kusafiri mbele au nyuma ya muda ikiwa tu mtu atakuwa na uwezo wa kuutumia ubongo wake kwa asilimia Zaidi ya ishirini , hivyo mara baada ya kupata hio nadharia waliingia katika majaribio ya kuweza kutafuta mtu ambae atakuwa na uwezo wa kutumia ubongo wake kwa asilimia hizo , na swala hili liliwachukua miongo mingi kidogo kulifatilia lakini kwa njia za kawaida walishindwa kupata mtu ambae ana uwezo wa kutumia ubongo wake kwa asilimia kubwa, hivyo njia mbadala ilionekana ni kwa njia ya kutengeneza mtu maabara na hapo ndipo Mpango zero ulipozaliwa. Hivyo kwa maneno machache ni kwamba Mpango Zero ni mpango wa kuzalisha binadamu mwenye uwezo mkubwa wa akili duniani ambae atakuwa na uwezo wa kutumia ubongo wake kwa Zaidi ya asilimia ishirini na mpango huo unaonekana ulifaa Zaidi kufanyika ndani ya Afrika mashariki , kwani inasemekana katika stori hio ya Book of all names , Nchi za Afrika mashariki zinahusika Zaidi , huo ndio nusu ya ukweli ninao ujua kuhusu Mpango Zero”

“Je mpango huo ulifanikiwa?”

“Inavyosemekana ni kwamba mpango huo ndani ya Taifa la Tanzania ulifanikiwa kwa asilimia mia moja “

“ Kwa hio unataka kumaanisha kwamba ndani ya Tanzania kuna kiumbe aliezaliwa mwenye uwezo wa kutumia akili yake kwa Zaidi ya hizo asilimia?”

“Ndio na ni ndugu yangu wa Damu , Mdogo wangu kutoka Tanzania”

“Unamaanisha una mdogo wako ndani ya Tanzania?”

“Ndio Ambrose Joseph , au unaweza kumuita Ambrose Peter , ni mtoto wa baba yangu Peter”

“Kwa hio Ambrose anahusikaje na Book of all names?”.

“Ili kujua hayo yote ndio inatupaswa kwanza kupata kujua ni stori gani ipo nyuma ya Book of all names , tukishapata hio hadithi ndio tutapata njia rahisi ya kukisogelea kilipo kitabu hicho”

“Nani anaijua hio stori?”

“Kuna binadamu mmoja tu duniani ambae anaijua hio simulizi “

“Unataka kumaanisha nini ?”

“Kwanza kabisa nikwambie tu hio simulizi ni kama kitu cha thamani Zaidi kuliko vyote ndani ya U-97 , hivyo kuilinda hii stori waliamua kuihifadhi kwa njia kuu tatu , njia ya maandishi ,njia ya sauti na njia ubongo sasa katika hii njia ya ubongo ndio maana nimesema kwamba kuna mtu mmoja tu ambae anaijua na ni huyo ambae ubongo wake ulitumika kuhifadhia simulizi hio”

“Huyo mtu ni nani na tutampataje ?”

“ Huyo mtu simjui lakini mtu ambae anaandaliwa kwa ajili ya ubongo wake kutumika kuhifadhia hio simulizi ninamfahamu”

“Ni nani ?”

“Ni Ambrose Joseph chini ya Mpango Zero”

“Hili linafanyikaje?’

“Hali ya kiafya ya mtu alietoa ubongo wake kwa ajili ya kuhifadhia hio simulizi imefikia ukingoni hivyo mtu mwingine wa kurithi hio kazi anaandaliwa ambaye ni Ambrose , jambo hili linafanyika ana kwa ana , kwa hio ni kwamba Ambrose ni lazima atakutana na huyu mtu na kisha atasimuliwa na akishamaliza simulizi hio huyo mtu atapigwa sindano ya sumu hapo hapo na atakufa kwani kazi yake itakuwa imeisha hapo na kwanzia siku hio Ambrose atakuwa chini ya ulinzi mkali wa U-97 ,kazi yake kubwa ni kufundishwa namna ya kurudi nyuma ya muda au kwenda mbele , jambo hilo naamini lina uhusiano mkubwa na kitabu hicho , na kama ni kweli basi U-97 kuna fumbo wanajaribu kulifumbua na inawezekana ni mahali kitabu hiko kilipo au inawezekana kitabu hiko kipo au kimekosa kurasa hivyo siwezi kujua Zaidi , ninachotaka nikujua kwanza hio simulizi na hili ndio nataka unisaidie kulifanyia kazi”

“Mpango wako uliouwandaa ukoje?”.

“Hapa ndio misheni yako ndio inakuja sasa , kazi yetu sisi ambayo itakuwa rahisi Zaidi ni kubuni njia ambayo itaweza kutuwezesha kuijua hio simulizi siku ambayo Ambrose atakwenda kusimuliwa ,na ili kulifanikisha hili ni lazima tujue ni lini kitendo hiko kitafanyika , na mtu pekee ambaye anajua muda na saa ni Profesa Mike Alan kwa hio jukumu lako ni kuhakikisha tunapata taarifa hizo kutoka kwa profesa na hio ndio misheni yako , sijui ni namna gani utaifanya ila lazima ulikamilishe , mimi nitafanya kazi ya kumshawishi Ambrose ili akubaliane na mpango wetu , lakini pia kumtahadharisha juu ya hatari ilio mbele yake”

SURA YA 17​

Ilikuwa ni jambo kubwa sana ambalo nilikuwa silijui na kijana huyu Erick amenifumbua macho , nakiri kabisa nilikuwa kipofu juu ya hiki kitabu cha Book Of All Names , nilikuja kugundua kuwa Bruno alikuwa akiendelea na mchezo wake wa kunichezea akili , kwani kitendo cha kuniambia nitafute hiki kitabu ilihali yeye kama moja ya wakuu wa U-97 wanajua fika kwamba kitabu hiko kilikuwa katika historia , niliona kabisa alifanya makusudi na muda wote alikuwa akinicheka katika harakati zangu za kupata hiki kitabu , ile hali niliokuwa nayo ya mwanzo ya juu ya kukipata kitabu hiki ndani ya miezi sita kama nilivyokuwa nimemuahidi mheshimiwa Jembe ilikuwa imepotea kabisa , niliamini jambo ambalo lilitumia miongo kadhaa ya miaka kutafuta kitabu hiki , mimi ni nani nitumie miezi sita kukamilisha hilo.

Niliagana na kijana Erick mara baada ya kupeana namna ya k uwasiliana huku akinisisitizia nifanye kazi ndani ya muda , sikuweza kumpinga na nilichoweza kumuahidi ni kwamba nitaweza kutimiza majukumu yangu ndani ya muda tuliopanga , nilitoka ndani ya hii meli kwani sikutaka kukaa Zaidi , nilichokuwa nawaza kwa muda huo ni kurudi hotelini kwangu ili kuwangalia namna ya kusafiri kuelekea Marekani kwa ajili ya kuanza kazi nyingine ya kumfatilia Profesa Mike Alan.

Nilirudi kwa kutumia boti ambayo nilipewa na kijana Erick na ndani ya masaa kadhaa ya kupangua maji nilikuwa nishafika sehemu niliopandia ile meli , na safari ya kuelekea hotelini kwangu ilianza mara moja , nilikuwa na njaa kali kweli kwani tokea niingia ndai ya taifa hili sikuwa nimepata kitu chochote Zaidi ya kunywa bia , jambo ambalo lilifanya kuhisi tumbo langu kuuma.

Baada ya kupata usafiri wa taxi ambao ulinipeleka moja kwa moja mpaka hotelini , jambo la kwanza kabla ya yote lilikuwa ni kula na hilo nilifanikiwa kulifanya ndani ya muda mfupi tu , kwani ndani ya nusu saa nilijiona nguvu zimerudi na naweza kufikiria kisawa sawa kwani nilikuwa nimeshiba.

Nilikuwa mwenye kuwaza mambo mengi kwa wakati mmoja , lakini kubwa Zaidi lilikuwa ni hili la hiki kitabu mawazo yangu yalinipelekea kulala moja kwa moja na nilikuja kushituka siku nyingine kabisa asubuhi kwenye muda wa saa mbili kama na nusu hivi jambo ambalo lilinishangaza kwani haikuwa kawaida yangu kulala muda mrefu kiasi hiko .

Baada ya kujiandaa kwa ajili ya kifungua kinywa ili nianze kupanga safari yangu ya kuelekea Marekani mlango wangu uligongwa jambo ambalo lilinishangaza kidogo kwani sikuwa nikitegemea mgeni na hata chai nilipanga kwenda kunywa mgahawanni ndani ya hoteli hio.

Nilinyanyuka na kwenda kufungua na hapo ndipo nilipojikuta nikipigwa na butwaa , kwani mtu aliekuwa mbele yangu alikuwa ni kama malaika ambae amekuja kunitembelea asubuhi asubuhi, hakuwa mwingine bali alikuwa ni mrembo Rania , nilishangaa sana uwepo wake eneo hilo .

Baada ya kuangaliana kwa sekunde kadhaa nilijikuta nikirukiwa na kukumbatiwa , kumbatio ambalo sikuwahi kulipata katika maisha yangu ya mapenzi.

“Rania unafanya nini hapa nchini si tulikubaliana unabaki nchini Austrakia ?” Ndio nilikuwa nina haki ya kuuliza swali hilo, kwani licha ya mwanamama huyu wakati nasafiri kuja hapa Ugiriki alitaka kuja na mimi lakini nilimkatalia kwani nilijua uhatari wa kazi yangu , na niliona angekuwa pia kikwazo katika kukamilisha kazi yangu na ndio maana licha ya kuomba sana kuja na mimi nilimkatalia , nilichogundua ni kwamba licha ya mimi kukutana na mwanamama huyu siku chache nyuma lakini alikuwa akionekana kunipenda sana na jambo hilo hata mimi lilinishagaza sana , lakini naweza kusema si kwa upande wake tu hata mimi kuna hisia ambazo huwa nakuwa nazo ninapokuwa karibu na mwanamama huyu , hisia ambazo sikuwahi kuwa nazo hapo kabla , ni kitu ambacho ni tofauti kabisa na hata ninapokuwa na janeth huwa sipati ile raha ninayokuwa nayo nikiwa na Rania .

“Nilishindwa kuvumilia Damiani you are so clueless of how I have just got to love you”Kwanza nilishangazwa na hili jibu , nilitegemea moja kwa moja ataniambia ameshindwa kuvumilia kunisubiria nikimtafutia mtoto wake kumbe ananiambia ameshindwa kuvumilia kwasababu ananipeda hii ni hatari kwangu .

Nilijikuta nikimwangalia huyu mrembo nikizidi kumthaminisha na kadri nilicvyokuwa nikimwangalia nilijikuta akili yangu ikiniambia huyu mwanamke ni chombo , katika wanawake niliokutana nao kwanzia Merina , Linda na Janeth . Rania anamuonekano wake mmoja wa kipekee sana licha ya kwamba siwezi kusema kwamba amemzidi Merina kwa uzuri , Merina alikuwa ni wa kipekee sana kwangu na naweza kusema ndio mwanamke ambaye nafasi yake ndani ya moyo wangu haitakuja kupata mtu.

Hakukuwa na mazungumzo mengi kati yetu Zaidi ya miili yetu kukutana , jambo ambalo baada ya kufika mwisho wa mechi niligundua nilifanya kosa kubwa sana , na kosa hilo lilikuwa ni kufanya mapenzi nikiwa nimevaa FBM, hapa huwezi kunielewa lakini ukweli ni kwamba nikifanya mapenzi na hii Mask Janeth anakuwa anajua kila kitu ninachokifanya , ila sikutaka sana kujutia makosa yangu nilichokifanya ni kuivua na kuwa Damiani halisi .

“Unampenda nani kati ya Damiani na Stephano?”Niliuliza swali hili la kijinga kabisa , lakini jibu lake lilikuwa Fatal kwani nilirukiwa na kuanza kunyonywa mkuyenge upya , hali ilionipelekea kuinua hisia za ngu kwa kiwango cha SGR , na mimi sikuona haja ya kumchelewesha tena huyu mwanamke , niliona kwanza nilifanya kazi kubwa sana usiku wa jana mpaka kukutana na mwanae hivyo niliona kabla sijampa habari kuhusu Erick kwanza nijilipe kabisa na utelezi. Damn it mtoto mtamu huyu wadau , yaani ni kama ananitegeshea kiwango cha joto na ute ute kwenye kinu chake .

Hii siku niliona kabisa safari ya kuelekea Marekani nighailishe kabisa ili nimuinjoi vizuri huyu mwanamke, na halmashauri yangu ya ubongo ilikuwa ishapitisha kabisa hili.

Basi siku hii tuliweza kuinjoi sana na Rania kwani tuliweza kutembelea maneo mbalimbali ndani ya Santorin .Hiki kisiwa kilikuwa kizuri sana , naweza kusema kwamba jana yake wakati naingia hapa ilikuwa usiku na sikuweza kushudia uzuri wa hiki kisiwa, Rania haikuwa mara yake ya kwanza kufika katika hiki kisiwa na ni kama yeye alikuwa mwenyeji wangu na kwa hili alinifanya niinjoi sana , na mimi siku hii niliona niweke mambo mengine pembeni kabisa nifurahie huu wakati , nilichokuwa najua kabisa kwa wakati huu Janeth yupo katika hali mbaya sana , kwani nilikuwa nikijua kwamba alikuwa akinipenda sana , lakini jambo moja ambalo lilikuwa likinizuia kutompenda Janeth ni Merina , kitendo cha mimi kutoka na mdogo wake kilinifanya mahusiano yangu na yeye yawe katika wasiwasi mkubwa na hata mama yake Merina alishawahi kuniasa nilinde heshima ya Merina kwani alikufa kwa ajjili yangu , na jambo hilo lilikuwa na uzito wake sana katika maisha yangu , kwani ni kweli kabisa kwamba Merina alikufa kwa ajili yangu na hili naamini kabisa kwamba sidhani kama kutakuja kuwa na mwanamke alienipenda kama Merina .

Hii ni siku ambayo niliweza kuweka pia kumbukumbu nzuri katika maisha yangu , lakini ni siku nyingine ambayo niliweza kusahau kwa muda mambo ambayo yanaendelea katika maisha yangu , na naweza kusema yote haya yamewezekana kutokana na uwepo wa huyu mwanamke , nilijikuta nikimuangalia na kuishia kutabasamu tu.

“Nimekutana na Erick”Niliongea na kumfanya Rania aliekuwa amejifunika Straw Hat anyanyuke na kuniangalia .

“Serious?”

“Yes we did talk and he seems well updated about everything in yout life , he even knows about us”

“You mean he know about us being in relationship?”

“Yes , I think he is so close to you more than you think , He got such unique care about you”

“What if !, Kama kweli ananijali aisingeniweka katika hali hii ya wasiwasi”

“Niamini mimi mpenzi”

“Mh! Vipi lakini yuko salama , anaonekanaje , naweza vipi kuwasiliana nae , I reel need to meet him Damiani”

“Nadhani yupo tofauti na mara ya mwisho ulivyomuona , sasa hivi anaonekana ni mwenye pesa , kuhusu kuonana nae sijui kama naweza kulifanikisha hilo , lakini nataka kwanzia sasa uondoe wasiwasi mwanao yuko poa kabisa ni mzima wa afya”Licha ya kumwambia hayo maeno alionekana kutonielewa , na hilo nililishuhudia katika hali ya muonekano wake.

Kesho ndio siku ambayo nilipanga kuondoka ndani ya hii nchi na hakukuwa na mjadala kesho ilikuwa ndio siku yangu , lakini niliamini kwamba naweza kuwakutanisha wawili hawa wakutane kabla ya kuondoka , naamini hilo ndio jambo pekee ambalo ninaweza kulifanya kwa ajili ya Rania .

Ilikuwa ni muda wa saa moja kamili ndio tuliweza kurudi hotelini, na nilikuwa nishawasiliana na Erick kuonana na mimi ndani ya hoteli hii hii na hilo nilikuwa nimemdaganya kwani mtu ambae alikuwa anaenda kuonana nae alikuwa ni mama yake.

Nilichopanga ni wawili hawa kuwakutanisha na mimi kurudi katika chumba changu ili kupangilia safari ya kesho .

Wakati wote huu sikuwa nimeangalia simu hata mara moja na nilipoigusa ndio nilipojikuta nikiwa katika mshangao kwani kulikuwa na notification nyingi za kuonesha Janeth alikuwa amenitafuta , ilibidi nichukue simu yangu na kumtafuta , na hili lilishindikana kabisa kwani mfumo ulikuwa haufanyi kazi jambo ambalo lilinipa wasiwasi , na jambo pekee ambalo niliweza kukisia kwa kila wakati mfumo wetu wa mawasiliano usipo fanya kazi ni hatari , nilichokifanya nilitumia mawasiliano ya B2 hili ni jina la kambi yetu nyingine ambayo nilikuwa nikijua uwepo wake mimi na Janeth tu na ilijengwa kipindi nipo kambini na rafiki yangu Luang Shu , mtoto wa kwanza wa kiume wa raisi wa China .

Bahati nzuri niliweza kumpata na hapo ndipo alipoweza kuniambia jambo ambalo liliniacha wazi na hili ni juu ya mheshimiwa Jembe kutoa siri ya mahali uwepo wa kambi yetu lakini pia na majina yetu , hili lilikuwa ni jambo la hatari kwetu ambalo sikulifikiria , lakini kwa upande mwingine niliona sikuwa katika nafasi ya kumlaumu mheshimiwa Jembe hasa pale Janeth aliponiambia kuwa ni PSYOPS ndio iliofanya kazi kwa mheshimiwa Jembe .

Psychological Operations nilikuwa nikiijua vyema na katika mafunzo yangu ya kijasusi , pia ilikuwa ni somo , kwani kuna kipindi mnakutana na hali mnataka kupata taarifa kutoka kwa adui na njia ya mateso imeshindikana hivyo inawapasa kutumia hii njia , ni njia ambayo ni ngumu sana kwa mtu asie na mafunzo kuhimili , kwani hii ni moja ya njia ya ‘Mind control’ iliokuwa ikifanyika kwa adui na kuleta matokeo bora .

Njia hii mtaalamu wa saikolojia akikufanyia ni Dhahiri kabisa utatoa kila aina ya siri ambazo hauko tayari kuzitoa , hivyo swala hili sikulifikiria kama U-97 wangeweza kulifanya kwa mheshimiwa Jembe .

Muda wa saa tatu ndio muda ambao niliweza kushudia jambo ambalo sikuwahi kuwaza kama linaweza kutendeka ndani ya ardhi ya Tanzania , bomu ambalo limerushwa ndani ya kiwanda chetu lilikuwa ni Fatal , kwani hakukuwa na kitu kulichobakia , na hili ni kwamba kwa mahesabu ya haraka haraka nilikuwa nimepoteza pesa nyingi sana kwa wakati mmoja , kwani eneo lile kulikuwa na kiwanda kikubwa cha vifaa vya kilectoniki vilivyokuwa vikitegenezwa.

Cha kushukuru Mungu ni kwamba tu hakuna mtu ambae amepata majeraha au kukumbwa na mkasa huo na kwa hili nilimsifu sana Janeth , jambo moja la uhakika ambalo niliamini sababu za U-97 kulipua eneo lile ni kama kutupa onyo , lakini kwangu sikuona kama onyo niliona ni kama mtu kuchokoza nyuki waliokuwa wapo kwenye eneo lao la makazi wametulia , na kwa hili niliapia lazima nilipe kisasi mara mbili na walichofanya.

Ni siku nyingine kabisa ambayo nilikuwa nipo ndani ya ndege la shirika la KLM nikielekea chini Marekani kwa ajili ya misheni ya kumpata Profesa Mike Alan.Nilikuwa nikiwaza mambo mawili kwanza nilikuwa na furaha kwamba Rania kafurahia kwa mimi kumkutanisha na mwanae ,, lakini pia nilikuwa nikiwaza namna ambavyo janeth alikuwa akinilalamikia , lakini pia nilikuwa nikiwaza namna ambavyo nakwenda kukamilisha kazi yangu , kwani sikuichukulia kama kazi rahisi kwani niliamini Profesa Mike atakuwa ni mtu makini sana .

Ni Muda wa saa Nane za mchana nilioingia ndani ya JFK Airport .

KUTOKANA NA UBIZE WANGU NITAKUWA NA POST KILA IJUMAA VIPANDE SITA KUFIDIA WIKI NZIMA WASAU ., TUKUTANE IJUMAA KUNAKOMAJALIWA
UNAWEZA KUIPATA KWA SHILINGI 2000 SOFTCOPY WATSAPP NAMBA NI 0687151346 AIRTELL MONEY AU 0657195492 TIGOPESA AU 0623367345 HALOPESA JINA ISSAI SINGANO UKISHATUMA TUMA SKRINISHOT YA MUAMALA WATSAPP KWA NAMBA 0687151346
 
“Wait moment please

“That is high classified information, to unlock this info please enter your credit card for additional payment of about 100000$”Aisee kilikuwa ni kiasi kikubwa mno cha pesa Zaidi ya milioni mia mbili za kitanzania nilijifikiria kwa dakika chache lakini niliona sina jinsi nilitoa kadi na kuichomeka sehemu ile ile pembeni kidogo.

“Yes we did talk and he seems well apdated about everything in yout life , he even knows about us”

“You mean he know about us being in relationship?”

“Yes , I think he is so close to you more than you think , He got such unique care aboot you”

“What if !, Kama kweli ananijali aisingeniweka katika hali hii ya wasiwasi”

“Niamini mimi mpenzi”

“Mh! Vipi lakini yuko salama , anaonekanaje , naweza vipi kuwasiliana nae , I reel need to meet him Damiani”

“Nadhani yupo tofauti na mara ya mwisho ulivyomuona , sasa hivi anaonekana ni mwenye pesa , kuhusu kuonana nae sijui kama naweza kulifanikisha hilo , lakini nataka kwanzia sasa uondoe wasiwasi mwanao yuko poa kabisa ni mzima wa afya”Licha ya kumwambia hayo maeno alionekana kutonielewa , na hilo nililishuhudia katika hali ya muonekano wake.

Kesho ndio siku ambayo nilipanga kuondoka ndani ya hii nchi na hakukuwa na mjadala kesho ilikuwa ndio siku yangu , lakini niliamini kwamba naweza kuwakutanisha wawili hawa wakutane kabla ya kuondoka , naamini hilo ndio jambo pekee ambalo ninaweza kulifanya kwa ajili ya Rania .

Ilikuwa ni muda wa saa moja kamili ndio tuliweza kurudi hotelini, na nilikuwa nishawasiliana na Erick kuonana na mimi ndani ya hoteli hii hii na hilo nilikuwa nimemdaganya kwani mtu ambae alikuwa anaenda kuonana nae alikuwa ni mama yake.

Nilichopanga ni wawili hawa kuwakutanisha na mimi kurudi katika chumba changu ili kupangilia safari ya kesho .

Wakati wote huu sikuwa nimeangalia simu hata mara moja na nilipoigusa ndio nilipojikuta nikiwa katika mshangao kwani kulikuwa na notification nyingi za kuonesha Janeth alikuwa amenitafuta , ilibidi nichukue simu yangu na kumtafuta , na hili lilishindikana kabisa kwani mfumo ulikuwa haufanyi kazi jambo ambalo lilinipa wasiwasi , na jambo pekee ambalo niliweza kukisia kwa kila wakati mfumo wetu wa mawasiliano usipo fanya kazi ni hatari , nilichokifanya nilitumia mawasiliano ya B2 hili ni jina la kambi yetu nyingine ambayo nilikuwa nikijua uwepo wake mimi na Janeth tu na ilijengwa kipindi nipo kambini na rafiki yangu Luang Shu , mtoto wa kwanza wa kiume wa raisi wa China .

Bahati nzuri niliweza kumpata na hapo ndipo alipoweza kuniambia jambo ambalo liliniacha wazi na hili ni juu ya mheshimiwa Jembe kutoa siri ya mahali uwepo wa kambi yetu lakini pia na majina yetu , hili lilikuwa ni jambo la hatari kwetu ambalo sikulifikiria , lakini kwa upande mwingine niliona sikuwa katika nafasi ya kumlaumu mheshimiwa Jembe hasa pale Janeth aliponiambia kuwa ni PSYOPS ndio iliofanya kazi kwa mheshimiwa Jembe .

Psychological Operations nilikuwa nikiijua vyema na katika mafunzo yangu ya kijasusi , pia ilikuwa ni somo , kwani kuna kipindi mnakutana na hali mnataka kupata taarifa kutoka kwa adui na njia ya mateso imeshindikana hivyo inawapasa kutumia hii njia , ni njia ambayo ni ngumu sana kwa mtu asie na mafunzo kuhimili , kwani hii ni moja ya njia ya ‘Mind control’ iliokuwa ikifanyika kwa adui na kuleta matokeo bora .

Njia hii mtaalamu wa saikolojia akikufanyia ni Dhahiri kabisa utatoa kila aina ya siri ambazo hauko tayari kuzitoa , hivyo swala hili sikulifikiria kama U-97 wangeweza kulifanya kwa mheshimiwa Jembe .

Muda wa saa tatu ndio muda ambao niliweza kushudia jambo ambalo sikuwahi kuwaza kama linaweza kutendeka ndani ya ardhi ya Tanzania , bomu ambalo limerushwa ndani ya kiwanda chetu lilikuwa ni Fatal , kwani hakukuwa na kitu kulichobakia , na hili ni kwamba kwa mahesabu ya haraka haraka nilikuwa nimepoteza pesa nyingi sana kwa wakati mmoja , kwani eneo lile kulikuwa na kiwanda kikubwa cha vifaa vya kilectoniki vilivyokuwa vikitegenezwa.

Cha kushukuru Mungu ni kwamba tu hakuna mtu ambae amepata majeraha au kukumbwa na mkasa huo na kwa hili nilimsifu sana Janeth , jambo moja la uhakika ambalo niliamini sababu za U-97 kulipua eneo lile ni kama kutupa onyo , lakini kwangu sikuona kama onyo niliona ni kama mtu kuchokoza nyuki waliokuwa wapo kwenye eneo lao la makazi wametulia , na kwa hili niliapia lazima nilipe kisasi mara mbili na walichofanya.

Ni siku nyingine kabisa ambayo nilikuwa nipo ndani ya ndege la shirika la KLM nikielekea chini Marekani kwa ajili ya misheni ya kumpata Profesa Mike Alan.Nilikuwa nikiwaza mambo mawili kwanza nilikuwa na furaha kwamba Rania kafurahia kwa mimi kumkutanisha na mwanae ,, lakini pia nilikuwa nikiwaza namna ambavyo janeth alikuwa akinilalamikia , lakini pia nilikuwa nikiwaza namna ambavyo nakwenda kukamilisha kazi yangu , kwani sikuichukulia kama kazi rahisi kwani niliamini Profesa Mike atakuwa ni mtu makini sana .

Ni Muda wa saa Nane za mchana nilioingia ndani ya JFK Airport .

KUTOKANA NA RATIBA ZANGU KUBANANA SANA NITAKUWA NAPOSTI SIMULIZI HII KILA IJUMAA JUMLA YA VIPANDE SITA , HIVYO NAOMBA TUVUMILIANE.

UNAWEZA KUIPATA SIMULIZI HII KWA KULIPIA SHILINGI 2000 TU KWA NAMBA 0687151346 AIRTEL MONEY AU 0657195492 TIGO PESA AU 0623367345 HALOTEL JINA NI ISSAI STEPHANO SINGANO UKISHAMALIZA KULIPIA TUMA SKRINSHOT YA MUAMALA WATSAPP IKWA NAMBA 0687151346
 
WIKIENDI NJEMA WADAU WANGU WA NGUVU HAKIKISHA UNAACHA NENO LOLOTE KWA A JILI YA KUFANYA WATU WENGI WAONE HUU UZI , KADRI WATU WANAOSOMA WANAVYOKUWA WENGI NDIO NINAKAVYOZIDI KUWEKA VIPANDE VINGI KWA WAKATI MMOJA
 
shukran sana singanojr
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom