Mr Acky
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 234
- 313
- Thread starter
- #41
KISANGA (Hisia za Mrithi)
Mtunzi Akida Siri Rambao
Sehemu 4F
Ilipoishia....
.... wa Nkole yupi, Nkole kwani anamtoto?!” Fiyona alisema sasa akisimama katoa macho huku akizivuta kumbukumbu taratibu, Mbonde akimshanga tu “…ina...Ohh! yule ni mtoto wa Nkole!?” “Unashangaza sana wewe, naz utashangaa mengi mwaka huu, ni mtu usiyejali kabisa hisia za mtu mwengine umejawa na ubinafsi tu” Mbonde alisema nakutoka nje mkuku mkuku akimuacha Fiyona njia panda.
Tuendelee...
MUDA HUO HUO
MTAA WA KIPASO-JIJINI NYATUMBU
Gotwa hofu ilikuwa machoni akihema akichungulia, mbele yake wanaume wasioleweka lakini shari ikiwa wazi wakisemeshana kwa ishara nyuso zikiwa na vinyago, bastola mikononi wakitawanyika kila kona ya nyumba “Hakikisheni tuna upata mzigo haraka iwezekanavyo. Bila kuacha ushahidi na kumuacha Nkole salama” mmoja aliongea kwa sauti kavu na nzito yenye amri. Mti Mkavu alishtuka kusikia sauti hiyo akapatwa na shangazo “Mbona hii sauti sio ngeni” alijismea kwa kunon’gona kiasi cha kumshangaza Mti Mkavu na kisha akatingisha kichwa kukubali “Inamaana wamekuja tena au..” alisema tena Gotwa na kuikumbatia vzuri tarakilishi mpakato.
Mti Mkavu pembeni yake akionekana kuweka ulinzi dhidi yake aliduwaa akimtazama Gotwa “Mzigo huu hapa nimeupata” mmoja alisikika akiongea “Shabbash imekaaa vizuri sasa yuko wapi Nkole muda huu?!” aliongea bwana yule wa mwanzo akitaraji jibu kwa watu walio mzunguka kwa kuwatazama kwa zamu “Twendeni hili ni muhimu zaidi” huyo mbele yao nyuma akifatwa na vibaraka wake. “Mti Mkavu nafikiri umeshahakikisha vya kutosha inatosha tuanze kazi yetu” sauti ya Burushuti ilimpitia Mti Mti Mkavu “…naona akili yake inavyofanya kazi haraka, ameigundua karata inayotumika mara mbili” alisema Mti Mkavu aliyekusanya mikono yake kifuani akimtazama tu Gotwa kwa makini sana akimchimba.
Si muda, Mbonde akapaki gari yake kando ya barabara umbali wa mita khamsini hivi na kuzima taa za gari mikono ikiwa usukanini akijiwazia. Macho mbele, uso wake ukabadilika “Kina nani tena?!” akajituliza akiangalia vizuri watu kama sio saba basi nane wakiingia kwenye gari mbili nyeusi wakitokea kwenye nyumba ya Nkole na kutimka zao “Mhhh!” akatoka garini na kuelekea kwenye nyumba ya Nkole. Mngurumo toka surualini ndio ulio mshtua kiasi cha kushika kifua chake huku macho kayafumba asiamini, aliitoa na kupokea “…aisee jamaa tulia waambie amenitoroka tulipokuwa tukipata staftahi pale Yombo…ndio waeleweshe hivyo hivyo mtu wangu…nakuaminia” akakata na kuirejesha simu mfukoni akatafakari kidogo akafonyaa huku akichalanga mbariga.
Alikomea nyuma ya nyumba akaingia kwa mtindo aliuzoea huku akitazama madirishani. Burushuti akiwaz karibu yake akimfatilia tu. Mbonde akaupiga mluzi na kutulia ukasikika mluzi upande wa ndani akatabasamu, huyo akaufata mlango na kuingia. Macho kwa macho alikutana na Gotwa amesimama “Vipi mjomba baba yupo wapi?” lilikuwa ni swali la Gotwa uso mashakani “Yupo sehemu salama…” aliongea huku akishangazwa na mazingira yalivyo kila kitu kimechanguka, akaikunja midomo yake kisha kamtazama Gotwa akiyaona majibu usoni mwake akauma meno “…lakini sio salama sana, Gotwa hivi kuna kitu unachokijua kuhusu baba yako na unaweza niambia walau kiduchu” “Ndio mjomba nifate kuna kitu mimekigundua kipindi tu ulipo toka wewe” Gotwa akatangulia huku Mbonde akimfata nyuma. “Ndugu yangu kuna mambo mengi yanaendelea kumuhusu huyu Mbonde kama tulivyo wasiliana ni wazi ana msaada lakini si wa kuaminika naomba tumpe nafasi kidogo ya leo tupate majibu kamili kabla ya kumkausha” aliongea Burushuti wakipiga hatua kuwafata “Sawa naona unakaribia kushinda” alisema Mti Mkavu na kutabasamu. Safari yao iliishia kwenye moja ya chumba.
Chumba kilichoonesha wazi ndio hasa chumba cha mwandishi Nkole kutokana na nguo zake pamoja na picha za ukuta zikining’inia hakukuwa na haja ya kuuliza. “…mjomba baba sio mtu wa kawaida ukimuona kama mjinga mjinga lakini ni mtu mwenye kufanya mambo makubwa hebu ona” Mbonde alitamani kucheka lakini akajizuia akifata maelekezo ya Gotwa asiye na shaka akijua akifanyacho, Ajabu! Gotwa akasogea hadi kwenye kabati lililojengewa ukutani akazitoa nguo kulikuwa na kitu kama mfuniko mweupe akauzungusha na kamlango kadogo ka mbao kakafunguka Mbonde mdomo ukamshuka macho katumbua “…nifate mjomba” Gotwa aliongea na kumtoa Mbonde kwenye Mgando, wakaingia kwa kuinama.
Kachumba kadogo kalikuwa mbele yao chenye upana wa mita tatu kwa mbili.
Mbonde macho kayatumbua akitazama tarakirishi mbili moja ikiwa imewaka ikionesha matukio yanayoendelea nyumba nzima kwa kamera zilizo tegeshwa akatabasamu aliona bunduki ndogo mbili mezani kando ya komputa , vifaa vya kisasa vya uchunguzi, picha za viongozi kazaa ukutani magazeti kazaa ya kitaifa na kimataifa “Nkole wewe ni nani hasa!!!?” alijikuta akiongea Mbonde kwa mshangao asiamini anachokiona “Baba ni Mpelelezi kama wewe” aliongea Gotwa pasina wasiwasi bila uwoga, Mbonde akashtuka akimtazama vizuri kwa jicho la Umejuaje? Akimtafakari kwa udogo wake na namna mazneno mazito ayatoayo pasina shaka “Ndio mjomba nimejua ulivyoondoka tu nilichunguza kila kitu nilimchunguza namna alivyokuwa msiri kuyafanya mambo yake”
Mbonde mdomo ukabaki wazi Mwaa! “We mtoto mbona unahatari…baba yako anajua kuwa unajua siri zake?” “Angeshaniua” aliongea Gotwa kwa kujiamini akimtazama Mbonde “Mjomba hii yapa tarakirishi yake” Gotwa akaifungua tarakirishi na kuweka password kwa neno JASUSI kwa herufi kubwa Mbonde yupo tu kama mtu aotae macho wazi “Umeona mjomba…subiri hapo hapo…” kwa wepesi na hali ya uzoefu Gotwa akaanza kuperuzi mafaili kiasi cha kumfanya Mbonde kushika kiuno akimshangaa Gotwa namna alivyokuwa akiitumia tarakilishi hiyo kama mali yake “Tazama mjomba” Gotwa alimsogezea Mbonde Tarakilishi “Mhhhhh we mtoto unajua ni kiasi gani ni hatari lakini” Mbonde aliongea huku akitazama na kuendelea kutazama mambo mazito ayaonayo
“Najua ndio maaana nikakuonesha wewe mjomba nimekuona muda mrefu ni mtu mzuri na hilo halikwepeki na pia niliona hakuna mtu wa kukuthibitishia kuwa baba ni mtu mzuri nikaamua kuwa mimi wewe pia unampeleleza baba nje ya upolisi wako si ni kweli? Nime kuona na kukusikia ukitoa tarifa za uongo kuhusu baba” Mbonde alishtuka macho yasifiche hisia zake akayasogeza pembeni mwili ukimkataa kuzificha hisia zake aibu hii yapa Gotwa akimkazia macho tu. ‘Huyu mtoto atakuja kuniumbua huyu’ alijisemea nafsini “…tuachane nayo sio muhimu sana naomba tafadhari msaaidie baba tafadhari yeye sio mtu mbaya na wewe ni askari mzuri si ndio? Ni ahidi utamsaidia baba” Mbonde alichoka hoi, akasogeza kiti cha matairi na kukaa “Gotwa nani kakufundisha mambo yote haya”
Mbonde uvumilivu ulimshinda baada ya sekunde kazaa aliongea “Shuleni, kuna mwalimu alikuwa ananifundisha tarakirishi na mimi pia napenda sana kujifunza kwa ajili ya kusaidia watu kama baba” aliongea haraka haraka kwa kujiamini “Sawa sasa Gotwa..Mhh sijui nisemaje sawa wale watu walio ondoka walikuwa wanasemaje?” aliongea Mbonde huku akikusanya mikono yake kifuani akimtazama Gotwa aliyemuacha hoi “Mjomba wale walikuja kufata mzigo wao na mimi nilijua tu kuwa watakuja tena hivyo nilikuja kuukuta huku nikautegesha sehemu ambayo haitakuwa na maswali sana kule sebureni ili tu waondoke zao wasikijue hiki chumba cha siri’’ aliongea Gotwa na kumuacha Mbonde akitabasamu aone kama sinema za kizungu “ Wewe mtoto ni shida si wakawaida una akili sana umenivutia sana, unakipaji na akili yako inafanya kazi kwa haraka sana utakuja kuwa mtu mkubwa sana wewe” aliongea Mbonde huku akimshika kichwa “…Nitakusaidia na nitamlinda baba yako kuanzia sasa na sema kuanzia sasa” aliongea Mbonde na kumfanya Gotwa amtazame kwa muda ni kama hakuelewa au kushangazwa na maneno hayo naye akavunga kwa tabasamu “Asante mjomba” akasogea na kumkumbatia, nyuma akionekana kuuvimbisha mdomo wake.
Itaendeleaa...