Mr Acky
JF-Expert Member
- Nov 24, 2019
- 234
- 313
- Thread starter
- #21
KISANGA!!!!
(Hisia za Mrithi)
Mtunzi Akida Siri Rambao
MSIMU 1
Sehemu 2 C
Tuendelee Sasa
....sio kawaida” aliongea Nkole mkono wake ukiwa umeshikwa na Mbonde “Mambo sio shwari kiongozi tupo hapa kuokoa maisha yako” “Maisha yangu?...” Nkole alishtuka jicho likamtoka akamtazama mwanawe ambaye alikuwa bize kanyanyua shingo akifatilia watu wanaoshuka kwenye basi, Nkole alionekana kuwaza kidogo akashika kiuno na kubana meno yake, kisha akamtazama Mbonde
“Gari ipo tayari kukuchukua wewe na mwanao, nitawapeleka mimi mwenyewe hatuna muda nifate” wakaongozana moja kwa moja hadi kwenye gari ndogo ya binafsi “Tafadhari naomba uingie” aliongea tena Mbonde, wakati wote huo Nkole alikuwa kwenye sintofahamu macho yake yakidhihirisha kitu Fulani kinachoendelea akilini mwake Mbonde alibaki kumuangalia kwa kuibia ibia mara kabla ya kuingiza mwili mzima garini Nkole akashtuka “Kwenye Siti number 28 kwa juu kuna begi mbili moja jeusi na lingine la njano ni ya kwangu” aliongea Nkole akimtazama Mbonde, Mbonde alionekana kuelewa haraka akaelekea kwenye basi. “Nini kinaendelea hapa” aliongea Burushuti akimtazama Mti Mkavu “Tusubiri tuone” aliongea Mti Mkavu akimkodolea macho Nkole mwenye mawazo kichwa kakiegemeza kwenye Kioo.
“Sasa tunaweza kwenda kila kitu kipo tayari” aliongea Mbonde akiingia garini akivuta mkanda wa usalama na kuufunga, akaliwasha gari. “Kwa kweli ulifanya maamuzi sahihi sana yaani naona wazi unamaadui wengi sana nyuma yako tena wenye mtandao mkubwa na hapa nahisi tutakuwa tunafatiliwa”
aliongea Mbonde akitupia macho kwenye saitimila, muda wote Nkole alibaki kumkazia macho kwa ishara Fulani, Gotwa nyuma yao nae njia panda akionekana kusumbua bongo lake masikio yamemsimama kuhofiwa kupitwa na habari akisikiliza bila kufahamu kushotoni na kuliani kwake yupo na vizuka asio waona, hakuna aliye waona wakiwa pamoja nao ila walikuwa nao safarini “Nafikiri sio pahala pake kuyaongelea hayo tupo na mtoto hapa” Nkole aliongea kwa sauti kavu, afande akageuza shingo macho yakautana na ya Gotwa asijue kuwa wapo na vizuka na sio Gotwa pekee akatingisha kichwa kuelewa jambo.
Vizuka kuliani na kushotoni mwa Gotwa wakabaki kutazamana tu.
Baaada ya lisaa kupita.
“Enhe hebu nieleze vizuri anaonekana amelala…ilikuwaje mbona inashangaza” Nkole aliongea sasa akimtazama Mbonde, Vizuka wakiwa tuli wakitazama tu zamu zamu
“Sina hakika…lakini inavyoonekana wapinzani wako wameshajua utawaangusha kama ulivyofanya mwezi uliopita na kuzua tafrani balaa zito kisha kupotea kama mzuka…wamenuia kukupoteza kabisa, yaani ni vile unajificha nyuma ya kalamu si rahisi watu kukujua kwa macho, wanaweza shtukia tu umepigwa kisu au risasi wasijue kwanini” aliongea mbonde na kumuacha Nkole katumbua macho ya umejuaje? Kabla hajauliza Mbonde akaongea tena
“..nimeunganisha matukio, kwanza gari yako kukutwa imetobolewa tank la mafuta kwa makusudi na kulegezwa breki na leo kusemekana kuna watu wasio julikana kupanga kukuteka ndani ya basi” Nkole akashtuka na macho kayatoa akibwenza bweza. Wale vizuka wakatazamana kwa mshangao “…haupo salama, tusingelazimisha safari siku ya leo ungekuwa kwenye matatizo zaidi” aliongea Mbonde akisikitika kwa kichwa huku akifungua karatasi akatoa bablish na kuibugia “Nyinyi mlijuaje mkaja mbiombio? Na kwanini nikuamini wewe” Nkole alihoji akimtazama kwa makini
“...ni mambo ya kipolisi cha msingi amini upo sehemu salama” aliongea akiwa bize na usukani akiendelea kutafuna “Sehemu salama unachekesha Mbonde” Nkole aliongea akimaanisha kwa uso wa mashaka “…Nkole ni hivi kuna abiria waliokuwa wakitiliwa shaka kwa kuwa walikuwa wakikufatilia mala zote lakini watu hao wameonekana mara kazaa kwenye maeneo unayoishi na mmoja kati yao ulipanda nae gari leo na muda huu ninao kwambia yupo kizuizini na ushahidi upo” Mbonde aliachia mkono mmoja na kutoa bahasha moja na kuzimwaga picha pembeni yake huku akiendesha kwa mkono ulio baki.
Nkole alizitazama picha zile kwa awamu na alipofika kwenye picha tatu za mwisho alionekana kushtuka na akakaza macho kama mtu aliyekumbuka kitu Fulani macho yakaingiwa wasiwasi akamtazama Mbonde aliyekuwa bize akiiendesha akauma meno akiwaza na mara akaangua kicheko cha dharau na kuongea huku akimnyooshea kidole “Mnatania mnanitengenezea skendo sio, mmetumwa?!” Mbonde akageuza shingo kumtazama Nkole kwa mshangao “Skendo…sijakuelewa unamaanisha nini, unaongea ujinga gani?!” aliongea Mbonde uso ukiwa umejaa hamaki ya tani akimaanisha kwa macho ya viulizo “Mnanitengenezea mtego ili mzijue siri zangu vizuri, aisee umekosea mimi siamini watu kirahisi hivyo,
mnajifanya mnanijaali ili mniingize kwenye mtego eti mnanilinda serikali hii au nyingine nishamjua mtu aliye kutuma, alafu wanakutumia wewe unazani nitakuamini hata kama nakujua?” aliongea Nkole kwa hasira na mara akapiga yowe “Simamisha gari Mbonde nasema simamisha gari” aliongea Nkole macho kayatoa kifua juu kakinyanyua akimtazama Mbonde. Gotwa akiwa kajilaza akapenyua macho fififi kushuhudia. “Sawa…sawa sawa nimekuelewa” Mbonde alisalimu amri akatia brek gari na kuegesha kandoni mwa barabara kwenye
Itaendeleaa...