Simulizi: Kazi ya mzungu

Simulizi: Kazi ya mzungu

KAZI YA MZUNGU 26
MTUNZI: DAVID NGOCHO SAMSON

Masu alikata tiketi ya ndege siku hiyo. Alijipa moyo kwa ule msemo wa kizungu, usichokiona kwa macho, hakikai akilini. Alijua atamsahau Molio. Asingependa aendelee na kile walichokuwa wamefanya. Hatia ya usaliti ilimgongelea nyundo moyoni.

Jioni, Issa Musa na Yara walirejea. Vifaa walivyodhania kwa zoezi lile walivipata lakini kwa njia za panya. Kifaa muhimu kikiwa kile ambacho kinaweza kusoma ni wapi ilipowekwa chip mwilini na cha pili kikiwa cha kuitia virus ile chip ili isiweze kuitikia maagizo ya kompyuta za ENTRY. Kifaa cha mwisho alitakiwa mtaalamu wa upasuaji. Huyo pia waliambatana naye.

Molio akitaka kumuoneshea Masu kuwa alimaanisha alichosema hapo awali, hakuonesha tabia tofauti na kawaida alipokuwa kaiona toka awasili Oman, alikuwa kando ya Issa Musa akimuonesha mahaba kama ilivyokuwa awali. Na zaidi hakuonesha dalili hata moja ambayo ingeonesha walakini kwa Issa Musa kuwa kuna kitu kikifanyika kisogoni mwake.

Hali hiyo ndio iliyomchanganya zaidi Masu. Mwanamke huyu hakuwa wa kawaida. Hakuonekana hata kidogo kuwa anajutia usaliti uliofanyika. Mbaya zaidi, kwa jinsi alivyokuwa anaonekana, ni kama kweli hakikutokea kitu baina yao. Masu akajiuliza kama Yara naye hangeingizwa kwenye mtego na binti huyo mrembo na mtata. 'Kama Molio ni jasusi, angekuwa jasusi hatari.' Masu alijiwazia mwenyewe. Maana si kwa tabia hiyo aliyoishuhudia. Masu akashukuru vile kesho angeondoka kwenda Zanzibar. Kuendelea kukaa Oman, angejikuta anakosana na Issa Musa. Maana moyoni mwake, Masu alikiri, Molio alikuwa ni mwanamke hatari.

Jioni ya saa mbili, daktari mwenye asili ya kikorea Myung Sun Han, aliwasili Jawhareit apartments. Akapokelewa kwenye apartment ya Issa Musa. Zoezi likaanza.

***

Akiwa maabara ambamo komputa zilizokuwa zinasoma eneo walipo wafanyakazi wa ENTRY popote pale walipo, Philip Mwangaza aligundua kitu kisicho cha kawaida. Alikuwa hasa amezingatia kuangalia mwenendo wa Molio. Alikuwa kwa siku nyingi anamuwazia binti huyo mapenzi. Ilikuwa inamuuma kwamba Molio kwa siku za hivi karibuni, alikuwa halali kabisa kwenye apartment yake iliyopo mtaa wa Al Gawarif bali alionekana kuwa alilala kwenye apartment mbili tofauti pale Jawhareit apartments. Wivu huo na mapenzi kwa mwanamke huyo, yakamfanya Philip kuwa mfuatiliaji sana (stalker) kwa mwanamke huyo.

Mara, akahisi kama kuna kitu ambacho si cha kawaida kimetokea. Akacheki komputa yake vizuri kwa jicho la mshituko lakini likidadisi kwa undani. Je alichokiona kilikuwa sahihi? Au kuna namna usingizi ulimkamata na kumfanya aote kuwa anashuhudia badiliko la ghafla la mahali alikokuwa mrembo huyo.

Philip alivua miwani yake ya macho, akaifuta kwa kitambaa laini. Akaitazama komputa kwa mshituko bayana. Molio alisemekana yuko New York huko Marekani. Dakika kumi kabla hajagundua badiliko hilo, komputa hiyo ilimuonesha kuwa Molio alikuwa Jawhareit apartments, sasa vipi ndani ya dakika kumi tu awe ameondoka Salalah na awe yupo huko Marekani? Philip Mwangaza akalisogelea karo na kuruhusu maji yatiririke kwenye bomba. Akayakinga kwenye viganja vyake hayo maji, akajirushia usoni kama kusudio la kufukuzia usingizi mbali na macho yake. Moyoni mwake akaomba akirejea kwenye komputa, awe sahihi kuwa ilikuwa mawenge yake tu. Na kweli, Philip alipoyarejesha macho yake kwenye skirini, akamuoma Molio akiwa kwenye moja ya apartment za Jawhareit. Akavuta pumzi ndefu ya kutuliza moyo. Molio alikuwa bado ndani ya uangalizi wa ENTRY. Pumzi hiyo aliyovuta ikamkumbusha vile uhai ni muhimu. Maana kupotea kwa mtu wa ENTRY kwa umbali wa New York kutokea Salalah, ingemaanisha kwamba, hawangeweza kumpata kwa urahisi. Ingeingiza ENTRY kwenye gharama za kuwatuma watu wao huko na kama wangelazimika kum-gandisha mtu wao Molio, kumgandisha ilikuwa na maana kwamba walikuwa na uwezo wa kumtia radi kwenye ubongo akawa kama mtu aliyeumwa ghafla, maumivu makali ambayo yasingemruhusu kuendelea na shughuli yoyote popote ambapo angekuwa. Kwa umbali huo, wangekuwa na uwezekano wa kumpoteza jumla. Hakuwa tayari kulishuhudia hilo.

Kitu kimoja hakujua, ile tahadhari ya mwanzo ilikuwa ya muhimu kufanyiwa kazi. Alipoipuuza kama ni wenge lake binafsi alikuwa kafanya kosa kubwa sana.

Asubuhi mapema, Philip Mwangaza alipokeza kijiti usimamizi wa mitambo kwa kijana mwingine asili ya kiarabu, akaondoka zake kupumzika nyumbani.

***

Baada ya kuiona ile chip mwilini mwa Molio, Yara akitumia program zake za ki-Russia, alimudu kuichanganyia habari, akaipa eneo jipya, New York City, ikakubali, sasa ilikuwa inapokea maelekezo toka kwa komputa ya Yaraslav na si kwa komputa za ENTRY. Akaiamrisha isome tena Oman, hapo walipokuwa wao, Jawhareit apartments. Sasa, Daktari Myung Sun Han akamweka Molio kitandani. Operesheni ndogo ya kuichomoa chip ikafanyika. Dakika arobaini na tano zoezi likiwa limekamilika, daktari akafunga mizigo yake na kuondoka zake.

"Free at last." (Huru hatimaye) Molio alitamka kwa furaha. Ingemchukua takribani wiki mbili kuwa sawa kabisa. Teknolojia ya mionzi aliyotumia Daktari Myung Sun Han, haikuacha alama kuonyesha kuna operesheni imefanyika. Ilikuwa teknolojia ya kisasa zaidi. Hangegundulika kabisa kwa muda mrefu, kuwa alikuwa kafanyiwa operesheni. Hakukuwa na dalili ya kovu kwamba mtu huyo kafanyiwa operesheni.

Ile chip sasa ilihifadhiwa kwenye kifaa maalum, ikaprogramiwa upya ili iwe na safari za jijini Salalah, safari zilizotengenezwa kufuatia maelezo ya ratiba za Molio za kila siku. Muda wa kuwepo kazini, kwenda airport kuchukua mizigo (watu). Kwenda sokoni, club, mazoezini, na maeneo mbalimbali aliyokuwa na kawaida ya kwenda mara kwa mara. Zoezi hilo lingeendelea hadi pale ambapo Molio angekuwa keshaondoka Oman na kuishilia zake mbali na mkono wa ENTRY.

Masu jioni hiyo akaaga kwa marafiki zake Issa Musa na Yara, alikuwa aondoke kurejea Zanzibar kesho yake. Wakati akiwaaga wenzake, Molio pia alikuwepo hapo. Akaona ili abaki kwa muda na mwanaume huyo alitakiwa kufanya jambo ambalo lingemlazimu Masu kubakia. Akamweleza Masu hatima ya mwanae kama angesalia mkononi mwa mzee Kisiki.

'Pale alipo mzee Kisiki, ana wake watano. Wote walikuja wakiwa ni wajawazito. Ana kawaida ya kuoa wajawazito. Anafanya hivyo kwa sababu, lengo ni watoto wanaozaliwa na mabinti hao kuwa faida kwa ENTRY. Wakishazaliwa watoto hao, hunyonya kwa mama zao kwa miezi sita, halafu huhamishwa kutoka Oman kwenda Dubai. Huko kuna Lab (maabara) kubwa ambapo watoto hao huwa chini ya uangalizi wa wanasayansi wa ENTRY wakifanyiwa majaribio mbalimbali. Kuna dhana ambayo sijathibitisha kwamba watoto hao hufunzwa kufanya mambo ya kikatili bila hisia, na kwa hatua ya juu zaidi, hutumika kutengenezewa watu wengine. Wanaita clones. Yaani watu ambao hutengenezwa maabara wakiwa wanafanana kwa kila kitu na original wao. ENTRY in mpango mbaya sana na dunia hii Masu. Kwa sababu ENTRY ni sehemu tu ya genge kubwa kabisa duniani ambalo linakusudia kupunguza idadi ya watu duniani kwa njia za kikatili.' Molio alimweleza vizuri kabisa habari hizo Masu mbele ya Issa Musa na Yara. Wote walikuwa kimya wakiwa wamevutika na simulizi hiyo. Molio akaendelea kusimulia.

'Lengo la ENTRY sio zuri kwa sababu, hebu fikiria, wanachukua watoto wadogo miezi sita wanawafanyia majaribio ya kisayansi ili wawe kama silaha. Watoto hao baadaye wanatumika kama vile maroboti kukusanya data kutoka mataifa mbalimbali ambayo ENTRY ina maslahi nazo aidha kwa faida au hasara. Ona kwa mfano, yule binti niliyemchukua leo asubuhi, Anastela Kilapi, wasichana warembo kama yule, huchukuliwa, wakapendezeshwa kwa madawa ya maabara na upasuaji wa kuboresha viungo vya mwili (Plastic surgeries), halafu huchomwa sindano za viruses mbalimbali ili kueneza magonjwa hatari kwa walimwengu. Maana baada ya hapo, warembo hao husambazwa kwenye maeneo mbalimbali ya starehe, vilabu vya usiku, madanguro na kadhalika. Hao wasichana naopokea mimi wanaotoka Afrika Mashariki, yupo mtu mwingine ambaye anapokea wanaotoka Thailand, Singapore, na mataifa ya Asia. Kila eneo, duniani, ENTRY hutafuta vijana na kuwafunza lugha muhimu wanazoona vema ili kuzitumia kuwasiliana kwa ajili ya kazi za ama kusafirisha binadamu au dawa za kulevya. Hayo na mambo mengine kibao, ikiwamo kuwatumia wanasiasa wa mataifa mbalimbali duniani kuruhusu mambo ya hovyo kama biashara ya umalaya, ushoga na hata sera za kuzuia uzazi.

'Unaambiwa wana lengo la kupunguza watu duniani kwa sababu wanaamini kuwa, dunia inapoelekea itaangamizwa na idadi kubwa ya watu wanaozidi kuongezeka kila leo. Wanaamini, ni wajibu wao kuhakikisha dunia inaendelea kuwepo kwa miaka milioni na milioni kwa siku za usoni. Kwa idadi ya watu waliopo duniani, ENTRY wanaamini kuwa huenda miaka mia ijayo ikashuhudia anguko la dunia nzima, watu wakiuana kwa sababu ya njaa, jua kali likangamiza watu baada ya miti kupotea vile matumizi ya mimea yamezidi kuwa makubwa na hovyo. Oxygen itauzwa kwa vile itabaki ya kuzalishwa maabara, baada ya kuteketea miti na oxygen asilia. Kutakuwa hakuna maji fresh maana vyanzo vya maji vitakuwa vimeangamizwa na idadi kubwa ya watu wanaosaka maisha kwa kutegemea kilimo, ujenzi, madini, kazi zote hizo zikihitaji matumizi makubwa ya maliasili na mimea.

Wanaamini idadi kubwa ya watu itahitaji kulishwa, na hivyo wanyama watatumika zaidi kama vitoweo, wakiisha wa kufugwa, wataingia kutafuta wa mwituni, wakimaliza hao, wataanza kukulana wao kwa wao. Wanakadiria kwamba hadi kufikia hapo, binadamu wote watapotea duniani kama walivyopotea dinosaurs wa kipindi cha mamilion ya miaka iliyokwishapita.

'ENTRY, wanaamini namna pekee ya kuhifadhi kizazi cha binadamu, ni kuwa na kiwango fulani cha idadi ya watu duniani, idadi ambayo inaweza kuishi vema bila ya kuhofia raslimali na mahitaji yao kupotea. Idadi hiyo, imekwisha kupita na sasa dunia ina mara sita ya watu wanaostahili kuwepo duniani. ENTRY wanaamini wapo ili binadamu adumu kuwepo. Watu bilioni sita ni ziada ya watu wanaopaswa kuwepo duniani. Hakuna namna zaidi ya kukomesha ukomo wa binadamu isipokuwa kupunguza idadi hiyo kubwa angalau, dunia ibakiwe na watu bilioni moja na nusu hivi. Majaribio yanayofanyika maabara, yanalenga kupunguza uzazi kwa binadamu, kuondoa wasiohitajika kwa maaana jamii ambazo zinachukuliwa kuwa ni less intelligent, (jamii duni kiintelijensia) na jamii hizo ni kama vile waafrika, waaboriginal, watu wa America ya Kusini, baadhi ya jamii za Asia, waarabu na jamii zote zinazoonekana duni. Kigezo wanachotumia kuzitambua jamii hizo ni maendeleo yao na tamaduni zao duni na dhaifu. ENTRY wanaamini kuwa jamii zote zinazoonekana kuwa na imani zaidi kuhusu Mungu au miungu, yaani ambazo culture zao zinaishi kwa kutegemea miungu au Mungu, basi ni jamii duni ambazo zinastahili kuondoka.

'Lakini ajabu ni kuwa lengo sio kuziondoa jamii hizo zote kwa ujumla wao, hapana, kwa sababu ENTRY huamini kuwa, hakuna jamii duniani isiyoamini kwa Mungu au miungu. Hivyo, ENTRY wanachofanya ni kuhakikisha wanatengenza utamaduni mpya unaofanana, ambao hauamini kwenye Imani hizo asilia, isipokuwa kwenye sayansi na uwezo mkubwa wa binadamu. Wao wanaamini kwamba, kuamini kwenye kitu zaidi ya binadamu mwenyewe kujiaminia, ndio kumepelekea dunia kuwa hovyo kwa kutowajibika na kutegemea nguvu ya ziada. Watu wamekaa wakingojea Mungu au miungu iwatendee, na kwa kufanya hivyo wameiacha dunia izidi kuharibika kwa kutowajibika kwao….' Molio aliendelea kusimulia, lakini maelezo hayo yote yalipita sikio la kushoto yakatokea sikio la kulia la Masu, kitu pekee kilichokuwa akilini mwake, ni hiyo habari ya mtoto wake na Mwamvita. Alikuwa anapanga namna ya kumtorosha mwanamke huyo, usiku huo huo, ili aondoke naye kesho yake.

ITAENDELEA.....
JamiiForums528126083.jpg
 
KAZI YA MZUNGU 27
MTUNZI: DAVID NGOCHO SAMSON

'Namtaka mke na Mwanangu Molio. Siwezi kurejea Zanzibar bila Mwamvita. Nahitaji kuondoka nao.' Masu alizungumza akionekana mwingi wa mawazo, lakini kauli yake ilikuwa thabiti. Sasa alionekana kubadili kabisa mawazo juu ya suala la kumuacha Mwamvita Oman.

'Anza kwa kuahirisha safari, wapigie simu usitishe safari ya kesho.'

'Wazo zuri sana.' Masu alitamka kwa kifupi na kunyanyuka kitini. Akaichukua simu yake, akapiga namba za shirika la ndege alilokata tiketi.

'Hello, Ethiopian airways, karibu tukuhudumie' ilisikika sauti ya mrembo.

'Asante, naitwa Masuke Masuke, hapa ninayo tiketi ya kuondoka Salalah kesho saa tano asubuhi siti namba 68, nimepata dharura, kuna mtu mwingine nataka kumkatia tiketi, anatakiwa akae na mimi. Hilo linawezekana?'

'Karibu sana Mr Masuke, hilo linawezekana ikiwa utakubali kubadilishwa siti ili mpewe wewe na mwenzako siti za pamoja. Hapa mnaweza kupata siti namba 119 na 120!'

'Sawa, fanya hivyo tafadhali.'

Molio na wenzake walibaki mdomo wazi! Masu aliwashangaza.

'Unamaana gani sasa wewe jamaa?' Yara alihoji kwa mshangao bayana.

'Ndugu zanguni, nawashukuru sana kwa ukarimu wenu. Imekuwa heri sana mimi kukutana na nyinyi na urafiki wetu nina imani utadumu zaidi na zaidi. Lakini, nilichofuata Salalah ni mwanamke wangu. Baada ya maelezo ya Molio, nalazimika kufanya kitu kwa ajili yake. Hata kama hanipendi tena, siwezi kuacha maisha ya mtoto wetu yaangamie mikononi mwa ENTRY. Napaswa kufanya jambo bibi na waungwana. Hata hivyo, nitahitaji msaada wenu kukamilisha misheni hiyo usiku huu huu.' Masu alijieleza kwa ujasiri. Ni hali ambayo Issa Musa na Yara hawakuwa wamepata kuiona kwa jamaa. Alijawa ujasiri na kulikuwa na kila dalili kwamba alichokusudia, lazima kingefanyika usiku huo huo.

'Una mpango gani Masu?' Molio aliuliza.

'Babe, sasa upo huru dhidi ya ENTRY, nini kinakukwamisha kuondoka Salalah?' Issa Musa alimuuliza Molio. Swali hilo likaamsha hamu mpya ndani ya Molio. 'Hivi kumbe sipaswi kubaki utumwani?' akawaza Molio.

'Hakuna cha kunibakiza utumwani babe. Hivi ulivyoniuliza ndio akili yangu imezinduka usingizini, kwa maana hata baada ya chip kuondoka bado nilikuwa nawaza ratiba zangu za kitumwa nilizowekewa na ENTRY. We have to leave as soon as possible' (tunafaa kuondoka utumwani haraka sana iwezekanavyo mpenzi)

'That's exactly my point darling.' (Hiyo ndiyo hoja yangu hasa mpenzi)

'And I was also planning on leaving here tomorrow!' (Mimi pia nilipanga kurudi Zanzibar kesho) Yara naye akatamka kwa furaha.

'Ok, Kumbe tupo safari moja, misheni yako ni misheni yetu sasa. Hebu rudi kitini, tupe mpango wako ili kila mtu ajue nafasi yake kwenye misheni itakuwa nini?' Issa Musa alizungumza huku akimpigapiga Masu mgongoni kama namna ya kumtia hamasa. Masu akamtazama jamaa huyo akahisi hatia kwa kule kumsaliti alikofanya hapo awali. Lakini kwa mbali, akaisikia sauti ya Molio ikimweleza hakukuwa na hatia. Na alipomtazama mwanamke huyo, jicho la Molio lilionekana kukazia kauli hiyo. Ni kama mwanamke huyo sasa alikuwa amepata funguo ya kumsoma mawazo yake.

Masu aliketi chini, akachukua penseli na karatasi, akaanza kuwachorea mpango. Akawaeleza ulinzi nyumbani kwa Kisiki ulivyo, akawachorea ramani ya nyumba ya mzee Kisiki ilivyo, na kila kona ya jengo hilo, na kuwaonesha maeneo muhimu ambayo wangeyatumia kuingilia na hata kutoka bila kushitukiwa na walinzi. Mpango wake kama ungefanikiwa kwenda bila kikwazo ungechukua dakika kumi tu. Baada ya kumaliza maelezo hayo, akauliza kama kuna mwenye swali. Wote walikuwa wameganda kwa mshangao.

'Wewe ni nani hasa?' Molio akauliza kwa mshangao. Hadi kufikia muda huu, alikuwa bado hajamjua huyu jamaa kama alivyodhani hapo awali.

'Swali gani hilo Molio?' Masu alijaribu kubeza, akikwepa kuwekwa kikaangoni.

'Hapana, nijibu swali langu Masu, haiwezekani wewe mgeni, tena hata nyumbani kwa Kisiki hujafika lakini uelezee jengo lile kama vile unaishi ndani yake. Wewe ni nani Masu?' wenzao wote pia walionekana kukubaliana na hoja ya Molio. Muda wa kuwekwa wazi ulikuwa huu. Hawakutaka kuingia kwenye misheni ya mtu ambaye hawamjui kabisa eti kisa walikutana tu siku mbili zilizopita. Masu akajikuta kawekwa mtu kati.

'Niliposema kama kuna swali, nilikusudia swali kuhusiana na mpango nilioweka mezani. Sasa mbona mnaanza kuuliza maswali binafsi?' Masu akaamua kuwazuga kwa namna hiyo. Hata hivyo, alijua kabisa kwamba amekwama. Hawakumjibu kitu lakini walimtazama kwa namna ambayo ilionesha kwamba hawakuwa na muda wa kupotezewa na kwamba hoja yao ilikuwa thabiti kabisa. Macho yao yalimtazama kwa kutarajia majibu.

'Sawa, nitawaeleza. Sote hapa tunajua kwamba nimekuja kwenye misheni ya kumuokoa mpenzi wangu ambaye niliamini kwamba kuletwa kwake huku ilikuwa kinyume na matakwa yake. Ilikuwa bahati kwamba mlipata taarifa za uwepo wake huku na mkafanya uungwana kunijuza. Nilikuwa sijawahi kufika huku. Hii ni mara ya kwanza kabisa na nililazimika kuja. Swali lenu linatokana na kwamba nimewachorea ramani ya kasri la mzee Kisiki, jamani, hii ni karne ya ishirini na ngapi waungwana? Ukihitaji hata ramani ya ikulu mbona unaipata tu. Nilipoondoka Zanzibar nilifanya mpango na rafiki yangu aitwaye Yusuf, ni mtaalamu wa IT, kwa hiyo nilimpa location ya jengo na yeye akafanya maujanja yake akanitumia ramani ya nyumba na hata picha zake. Ni hivyo tu!'

Maelezo yake yalionekana kuwashawishi Yara na Issa lakini si Molio. Lakini hali hiyo ya kutojulikana vilivyo kwa Masu ni kama ilizidi kumfanya Molio apagawe zaidi juu ya mwanaume huyo. Molio alionekana kupenda zaidi wanaume ambao wana aina fulani ya nguvu zaidi ya kawaida. Kwa Molio, Masu alionekana kumiliki sifa adimu. Wazungu huita mystery. Molio alipenda viumbe wa aina hiyo. Wasiotabirika, hatari, wanaonesha vipaji vipya na uwezo kila wanapokumbana na changamoto. Watu wasio na woga kukabili hatari, lakini wakionekana kuwa na akili kubwa ya ku-survive. Molio alimuona Masu kwenye kundi hilo. Alimpenda. Na hasa kwa sababu alipenda mtu anayeshughulikia changamoto. Akaamua kujifanya mjinga, kuwa hajabaini kuwa Masu bado alikuwa na siri.

'Mh, hapo sawa. Kuhusu huu mpango, sina shaka kama ni mpango madhubuti. Lakini mimi nina Plan B. Plan ambayo inaweza isishitukiwe wala kuhisiwa kuwa ni plan janja. Sote tunakubaliana kuwa kesho tunaondoka kwenda Zanzibar. Hakuna mtu wa ENTRY anayejua mpango huu isipokuwa sisi wanne. Hatuna haja ya kukimbizana na watu wa ENTRY usiku usiku. Mimi asubuhi nitaamka na kuelekea kazini. Kuna mzigo nitaenda kupokea airport saa kumi na mbili. Yara, itakubidi ile chip aidha unifungie na iwe inasoma harakati zangu ili ENTRY waendelee kuamini bado nipo chini ya uangalizi wao. Issa utakata tiketi zetu asubuhi hiyo hiyo. Nikitoka uwanjani, napita kwa mzee Kisiki. Huko nitamchukua Mwamvita kama nilivyofanya siku ile, halafu nitamleta kwa Masu, Masu ataondoka naye kwenda airport. Wakati huo, chip yetu tutaiwekea location mpya, kwenye supermarket iliyo jirani na kwa mzee Kisiki. Itabaki hapo hadi masaa mawili au matatu, halafu itaoneshwa ipo kule kwenye apartment yangu. Wakati huo sisi tutakuwa tumeshaingia Zanzibar.'

'Vipi kuhusu mzee Kisiki, utamchukua Mwamvita kwa gia gani?' Masu akahoji. Kiujumla alikubaliana na mpango huo. Hakukuwa na haja ya kumwaga damu ikiwa wangeweza kutumia akili namna hiyo na kuhifadhi nguvu zao kwa ajili ya mmbo mengine ya msingi.

'Mzee Kisiki yupo Marekani. Kuna kikao cha ENTRY na branches zao zingine. Na kinahudhuriwa na viongozi wa kanda tu.'

'Ok, nimependa sana huo mpango.' Masu aliongea, nuru ya macho yake ikitambulisha furaha yake.

'Naam, mpango uko vizuri sana. Lakini tunalazimika kuwa na hakika hakuna siri inayovujishwa. Yule daktari Myung Sun Han, nahisi aligundua kuwa tunachofanya ni kitu gani. Labda awe mjinga, lakini, anaweza kutu-blackmail au kutuuza yule. Tunatakiwa kumdhibiti awali ya yote.' Yara alizungumza.

'Dah, unajua wewe ni bonge la kichwa! Fikiria hiyo ingeweza kuwa kikwazo namna gani?' Issa Musa aliongea akimgonga gonga Yara mgongoni.

'So tunafanyaje?' Molio akauliza.

'Hapa dawa ni kumfahamu vizuri. Si wanasema mchawi lazima awe anakujua vizuri? Tukijua ana familia au mke au mama, wapi walipo tutakuwa tumemaliza mchezo.' Masu alizungumza.

‘Unamaana tuteke mtu katika wapendwa wake?' Yara akauliza.

'No, sio lazima. Lakini tunaweza kutumia taarifa hizo kumfanya ajue kujaribu kitu kama hicho, ni kuangamiza familia yake kwa mikono yake mwenyewe.' Masu akaeleza. Yara akatikisa kichwa kukubaliana na hoja hiyo, halafu akaingia mtandaoni kusaka habari binafsi za daktari Myung Sun Han. Alidukua mfumo wa data ya hospitali alikofanya kazi daktari. Haikuchukua nusu saa alikuwa na taarifa kamili. Wakapiga simu.

'Daktari Myung hapa' Daktari Myung akapokea simu.

'Naam Daktari Myung, unazungumza na Issa, umetoka hapa kwangu kwa operesheni ya kuondoa kifaa kwa ndugu yangu.'

'Oh, bwana Issa, Ndiyo ndugu, mgonjwa anaendeleaje? Kuna shida?'

'Hapana shida Daktari kama wewe utasahau kwamba umefanya hii operesheni. Binti yako Myung Hae Sun, nasikia anafanya vizuri sana pale chuo kikuu Seoul, nimeambiwa kuwa sasa hivi anatoka na Profesa Robert Laban kimapenzi na amekusudia kumuoa, una taarifa hizo?'

'Ndugu Issa, ni nini mbaya tena?'

'Hakuna mbaya Daktari, kama huna mdomo mkubwa. Pole sana kwa kumuuguza mama. India wameweza kutibu tatizo kama la mama kwa ufanisi. Jaribu kumpeleka huko.'

'Usiwe na mashaka na mimi ndugu Issa. Hatujawahi kukutana, na wala sijawahi kukutibia mgonjwa kabisa.' Daktari Myung aliona hatari. Ingawa mara kadhaa alifanya ishu hizi kwa ufanisi na kufanikisha kujipatia mshiko wa maana kwa ku-blackmail, hapa alikuwa kafanyiwa uviziaji hatari.

'Asante sana Daktari' Issa akakata simu

Issa alipomaliza mazungumzo Hayo, wenzake wote wakampigia makofi.

'Kumbe babe wewe ni mafia namna hiyo? Sipati picha mkorea wa watu alivyoshituka maskini. You're a very bad boy' (wewe ni hatari) Molio alimwambia Issa na kumbusu shavuni. Kila mtu alikuwa na furaha.

Usiku huo, kila mtu akalala akiwaza yake. Molio aliuona uhuru wake mbele yake, na mwanume aliyelala pembeni yake ndiyo aliufanikisha. Akambusu shavuni na kumkumbatia kwa furaha. Wakati akifanya hayo, Issa Musa alikuwa ndotoni akiota familia ya watoto kumi na mbili aliozaa na Molio. Masu yeye alikuwa anawaza wapi atamficha Mwamvita wake awe mbali na mkono wa ENTRY.

Wakati hao wakiota na kuwaza mambo yao, Yaraslav Yvanovitch alikuwa anatabasamu kwa furaha. Misheni yake ilikuwa inakaribia kufanikiwa kwa asilimia 75. Hakuamini jinsi ambavyo mipango ilivyokuwa inajipanga yenyewe bila kutumia nguvu nyingi. Hakuwahi kuamini kwenye bahati au maombi kufanya kazi, lakini sasa aliamini.

Ilikuwa anahesabu tu muda na mpango wake ungekamilika ipasavyo.

Itaendelea.....
JamiiForums528126083.jpg
 
KAZI YA MZUNGU 28
MTUNZI: DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

Pengine episode hii itakutoa nje ya mtiririko tulioanza nao. Usijali. Ni hatua muhimu itakayoifanya simulizi hii ilete maana niliyokusudia mtunzi wako.

Twende pamoja...

Mwaka 2015, mwanasayansi Steve Curl, mwanasayansi tajiri na mwenye ukwasi wa kutosha, alipata mwaliko kukutana na matajiri wenzake wakubwa duniani. Kikao kilifanyika katika moja ya kumbi za mikutano ndani ya Hotel yake, jijini New York. Steve Curl alipendekeza kuwa hivyo, kwa sababu, ilikuwa ni mbinu ya kuonesha nguvu ya misimamo yake, na pia kwake aliona ni salama zaidi akiwa kwenye uwanja wake wa kujidaia. Kikao hicho kililenga kumshawishi tajiri Steve Curl, kujiunga na kundi la ENTRY. Watu hao wakampa sababu kama kumi hivi muhimu kwa nini ajiunge na kundi hilo. Walimweleza nguvu waliyokuwa nayo na jinsi ambavyo angefaidika kama angejiunga na kundi hilo. Hata hivyo, hadi kikao kinaisha, ENTRY hawakuwa wamepata jibu la hakika kutoka kwa bwana huyo.

Steve Curl alishangazwa sana na ujio wa ujumbe ule wa ENTRY. Hakuamini kuwa kulikuwa na watu wenye uchu na ulafi mkubwa kama wale. Wengi wa watu wale, walikuwa ni watu aliowaheshimu sana kabla, lakini Sasa aliwadharau. Aliwaheshimu kwa vile walikuwa matajiri wakubwa wenye kutajika kote duniani, lakini nia ya kumtaka ajiunge nao kwenye umoja wao wa ENTRY na lengo lao, Ni kitu kilichomfanya awadharau. Alibaini kwamba walikuwa watu wenye uchu na ulafi mkubwa wa sifa na pesa.

Steve Curl, tofauti na matajiri wale wa ENTRY, hakufanya juhudi kubwa sana ili kupata utajiri aliokuwa nao. Alifanya bidii tu katika tafiti zake za kisayansi na ubunifu. Ubunifu huo ukampatia tenda nyingi za kibiashara na kuvutia mikataba minono iliyomwingizia fedha nyingi. Kwake yeye, utajiri wake ulitokana na kufanya utafiti, akagundua kitu na kitu alichogundua kikamzalishia maradufu utajiri mkubwa. Akaajiri wataalamu ambao walisimamia miradi yake na jina lake daima likabaki kutamkwa midomoni mwa raia wa dunia kama mtu tajiri. Hata siku moja hakuwahi kuwaza kwamba atafanya hila imwezeshe kuwa tajiri. Na ndio maana, tajiri huyu aliishi maisha ya kawaida na hata baadhi ya watu hawakumdhania kuwa ndiyo yule mmiliki wa Scientific Reality Inc (SRI). Kampuni kubwa kabisa duniani kibiashara na kisayansi.

Usiku wa siku ile alipopokea ujumbe wa ENTRY, Steve Curl akiwa nyumbani kwake amelala, aliota ndoto. Katika hospital kubwa kabisa iliyomilikiwa na Scientific Reality Inc alikuwa amezaliwa mtoto wa kiume. Lakini katika hali iliyoshangaza wengi, mama wa mtoto huyo, hakujulikana alipotoka. Kwa utaratibu wa Marekani, kila raia alikuwa na social security card au namba ya kumwezesha kupata huduma za kijamii. Ni mfumo ambao ulimwezesha raia wa nchi hiyo kupata huduma muhimu za kijamii yakiwemo matibabu. Lakini mama huyo mzazi wa kichanga hakuwa nayo. Hata hivyo, mama huyo alikuwa kwenye hali mbaya, alihitaji kusaidiwa, na madaktari wakaona busara wamsaidie mama huyo kujifungua na baadaye ndio wangefuatilia habari zake kwa kina. Yaani yeye ni nani na wapi alipoishi na taarifa nyinginezo hali kadhalika.

Mama huyo akajifungua mtoto wa kiume, mtoto huyo alifanikiwa kuishi lakini mama yake ikawa bahati mbaya. Mama yule alikufa. Mtoto aliyezaliwa hakuwa mtoto wa kawaida. Aliwashangaza madaktari na wahudumu wa Hospitali ile. Alikuwa na damu ya kijani. Maumbile na vitu vingine alikuwa sawa kabisa, tena mwenye afya njema. Lakini kuwa na damu ya kijani? Ulikuwa muujiza wa aina yake kuwahi kushuhudia. Mara, tajiri Steve Curl akashituka usingizini akiwa amehamanika vilivyo. Mkewe akamuuliza kulikoni. Steve akamsimulia kilichokuwa kimetokea kwenye ndoto. Mkewe akamwambia kuwa itakuwa ni mambo ya tafiti zake tu za kisayansi. Kutwa kushinda na makemikali maabara si kazi ya kitoto. Akamwambia alale kila kitu kingekuwa sawa. Wakalala.

Asubuhi alipoamka mapema, kitu kilichokuwa akilini mwake ni huyo mtoto wa ajabu aliyemuota ndotoni. Tajiri Steve akaamua ofisini angeenda baadaye, akaamua kufanya ziara kwenye ile hospitali alikoota habari hizo ili kujiridhisha kwamba ni ndoto tu. Hakujua kwa nini, lakini ndoto hii ilikuwa tofauti na ndoto alizowahi kuota hapo awali. Hii ilikuwa dhahiri mno! Ilikuwa kama sio ndoto bali uhalisia wa mambo. Aliikumbuka vizuri kila kitu tofauti na kawaida, ambapo angeota ndoto ambazo hata kukumbuka hakukumbuka kulipokucha.

Ajabu ya Musa kuona ya firauni. Alipofika hospitalini, akakuta madaktari wapo kwenye kikao. Tukio lilikuwa limetokea hospitalini hapo la ajabu. Hapo kikaoni walikuwa wanapeana mikakati ya kulimudu suala hilo lisiingie kwenye mikono ya waandishi wa habari. Akakaribishwa kwenye kikao baada ya uwepo wake kutambulika kwa mganga mkuu wa hospitali hiyo. Daktari akampa taarifa kwa ufupi. Taarifa aliyopewa ilikuwa ni ile ndoto aliyoota akiwa nyumbani.

Tajiri Steve Curl akashikwa na hamu ya kutaka kufanya utafiti wa suala hilo. Mwanamke aliyefariki akizaa mtoto huyo, alikuwa na asili ya Africa. Katika moja ya vitu vilivyokuwamo kwenye mkoba binafsi wa mama yule, ambavyo Steve aliomba kukabidhiwa, kulikuwa na karatasi yenye maandishi yaliyoandikwa kwa lugha ambayo madaktari hawakuifahamu. Ilikuwa lugha ya zamani miongoni mwa lugha ambazo zilipatikana katika eneo la Africa Mashariki miaka mingi iliyopita. Lugha hiyo haikuwapo tena duniani.

Lugha ambayo baada ya utafiti wa miaka miwili, Steve Curl aligundua kwamba lugha ile ilikuwa inajulikana kama Qwadza au Ngomvia. Lugha hiyo ambayo ina asili ya Africa na Asia, ilisemekana kupotea kabisa duniani, huku mzungumzaji wa mwisho wa lugha hiyo akikadiriwa kufa kati ya miaka ya 1976 hadi kufikia mwaka 1999 hivi. Ugunduzi wa Steve Curl ukaonesha kuwa lugha hiyo iliendana sana na lugha ya kabila dogo sana la nchini Tanzania, kabila la wasandawe.

Mtoto yule mwenye damu ya ajabu, akiwa ameasiliwa na tajiri Steve Curl, sasa alikuwa na miaka miwili.

Steve baada ya kukusanya taarifa kadha wa kadha, akaazimu kufunga safari mwaka 2017 kwenda nchini Tanzania. Lengo lake akutane na wasomi kutoka kabila la wasandawe nchini humo, ambao wangeweza kumtafasiria maandishi yale yaliyoachwa kama ujumbe na mama Yeraz, jina ambalo Steve alimpa yule mtoto likiwa na maana ya ‘ndoto’. Aliingia jijini Dar mnamo mwezi wa pili. Akawasiliana na ubalozi wa marekani na kuomba usaidizi wa kutafutiwa wasomi kutoka kabila hilo.

Matangazo yalisambazwa katika vyuo vikuu vyote nchini. Hakutokeza mtu, Steve akaomba kibali cha kuwafuata wasandawe katika wilaya yao huko Chemba, mkoani Dodoma.

Wasandawe ni jamii ambayo kwa miaka mingi imekuwa ikiishi maisha ya kijima, kwa kutegemea kuwinda, kuchimba mizizi na kula mazao yanayojiotea porini. Hadi miaka ya karibuni ilisemekana kwamba watu hao hatimaye walianza kuiga maisha ya majirani zao wagogo na sasa walimudu kulima na kufuga. Kwa asili wasandawe ni watu wenye ngozi nyeupe au tuseme njano, na sio watu wenye miili mikubwa sana. Hata hivyo inasemekana kuwa wanawake wa kisandawe ni wanawake wenye maumbo mazuri, warembo. Midomo yao myembamba, na wamejaaliwa unene wa kutosha chini ya kiuno kwa maana ya makalio na mapaja. Lugha ya wasandawe, ni moja kati ya lugha kongwe zaidi Africa na inaaminika kuwa yale makabila ya Africa Kusini ya khoisan, yanachukua asili yao kwa wasandawe, na huenda walitawanyika kutokea Africa ya Mashariki wakimeguka kutoka kwenye kabila la wasandawe. Hata hivyo, utafiti juu ya lugha hizo kuwa na asili moja bado kufanyika, ila kinachoonesha ulinganisho kati ya wakhoisan na wasandawe, ni utamkaji wa maneno, kwa namna ambayo wazungu huita clicking sound. Lugha hiyo imeonesha kuwa lugha ngumu sana kujifunza hasa kwa majirani zao wagogo.

Huko wilayani Chemba, Steve Curl alipata kijana Mwanafunzi wa kutokea kabila hilo, mwanafunzi wa kidato cha tatu, kutoka Shule ya sekondari Farkwan, akawa mtafasiri wake. Siku mbili za mizunguko zikawafikisha kijijini Bubutole ambako walielezwa aliishi mzee mmoja kikongwe sana ambaye hakuwa asili ya kabila hilo la kisandawe. Haikuwahi kujulikana kabila lake, lakini ilisemekana alitokea kaskazini, mkoa wa Manyara miaka ya nyuma sana na akapokelewa hapo na wenyeji, hatimaye akawa ni mmoja wa watu jumuishwa wa kabila hilo. Mzee huyo alisemekana kuwa na umri uliokadiriwa kufikia mia moja ishirini (120) na ushei.

Mzee huyo alipofika hapo kijijini alikuwa na miaka 56 mwaka 1956. Alisoma elimu ya watu wazima enzi za hayati baba wa taifa. Na hata kufikia umri huo wa miaka mia moja ishirini na ushei, mzee Ngomvia alimudu kusoma na hata kuandika akitumia miwani aliyodai alizawadiwa na mjerumani Lukas von Leon mwaka 1976. Ikaonekana alichohitaji Steve Curl si mkalimani wa kisandawe bali mkalimani wa kiswahili. Bahati njema pia, Steve alikuwa kaambatana na mwanafunzi kutoka chuo kikuu cha Dar es salaam, Abel Maginga ambaye alikuwa msaada mkubwa sana kwa tajiri Steve Curl katika suala zima la kutafsiri Kiswahili kwa Kiingereza.

Mzee Ngomvia, alielezea historia yake kwa ufasaha. Alitokea Mbulu huko mkoani Manyara akiwa na umri wa miaka 29. Alikuwa na mke na watoto wanne ambao walikufa kwa mlipuko wa ugonjwa wa polio, ugonjwa ambao kwa wakati huo ulikuwa hauna chanjo. Mzee Ngomvia akawakumbushia jinsi ugonjwa huo ulivyopata kumlemaza hata Franklin Roosevelt mnamo mwaka 1921, akiwa na miaka 39, mtu ambaye alikuja kuwa raisi wa Marekani kwa baadaye mwaka 1933.

Mzee Ngomvia alieleza kwamba, baada ya jamii yake kukumbwa na gonjwa hilo na kufariki sana, aliamua kuondoka na kuelekea kusini. Akapokelewa hapo kijijini ambako alidai, aliongozwa na Mungu na kusisitizwa hatakufa hadi pale ambapo ugeni huu ungemfikia. Mzee Ngomvia alimweleza Steve Curl kuwa, siku mbili kabla hawajafika hapo, alikuwa kapata maono. Lugha yake ya zamani ya Qwadza, ilikuwa itumike kutoa tafsiri ya maagizo ya Mungu ili kuokoa kizazi cha binadamu. Habari hiyo ikamshangaza zaidi Steve Curl na ujumbe wake kwani, walikuwa bado kumueleza kusudi lao la kumtafuta na tayari akaonesha kujua kilichowaleta wageni wake hao.

Itaendelea....

JamiiForums528126083.jpg
 
KAZI YA MZUNGU 29
MTUNZI DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

Mzee Ngomvia mwenye takribani miaka 120 na ushei, hakuonekana kumiliki umri huo. Ni sahihi kwamba kulikuwa mikunjo kadhaa usoni mwake, lakini ngozi yake ya njano ilionesha mikunjo hiyo kama ya umri wa mtu mwenye miaka 70 labda. Hakuwa mrefu, lakini pia hakuwa mfupi. Sauti yake ilikuwa na kitetemeshi kwa mbali, lakini haikuwa dhaifu. Alimudu kutabasamu na kucheka na alipendezea furaha. Na hasa siku hii alipokutana na Mzungu Steve Curl, Ngomvia alionekana kuchangamka sana. Kwa namna ya maumbile yake, uso mdogo wa mviringo, mwili mdogo, kichwa chenye nywele nyeusi, bila shaka alipendelewa mwili mzuri na roho njema.

Mzee Ngomvia alivuta kiko chake toka chini ya kiti chake cha kuning'inia kama bembea, akaweka mkaa na kukoleza moto wake, akawa anavuta wakati alipoanza kuelezea kilichoandikwa kwenye ujumbe ule. Aliichukua karatasi ile ya ujumbe mkononi mwa Steve, akavaa miwani yake, akaisogeza mbele mbali na macho yake, akayafinya macho yake kwa kuvuta makini kuusoma ujumbe ule kwa mara ya pili.

‘Wanangu, nimeishi miaka mingi, na sikudhani ningeishi kuyaona haya yakitimia. Kabla sijawaeleza yaliyoandikwa humu, niombe kuwapa habari yangu binafsi inayohusiana na barua hii. Wakati ndugu zangu wote wanateketea kwa polio mwaka 1929, nikiwa nimelala, niliota ndoto. Kwenye ndoto ile, alikuja mzee mwenye umri mkubwa, nikamwamkia. Baada ya kusalimiana naye akanambia, Ngomvia, kizazi cha watu wako kinapotea kwa huu ugonjwa wa Polio, hakuna wa kusalia ila wewe pekee. Kamwe usiisahau lugha yako ya qwadza, umebakishwa ili siku moja uokoe ulimwengu kwa tafsiri. Ajabu ni kwamba ndoto hiyo nimeiota tena jana. Na safari hii nikapewa na maelekezo ya kukupeni.

Ujio wenu unakuja ili kunikutanisha na ndugu zangu waliokwisha tangulia. Hivyo, zingatieni maelezo nitakayowapa. Maana baada ya maelezo haya, mtawajibika kunihifadhi ardhini. Mtanizika jirani na nyumba yangu hii. Nilikwisha andaa malazi yangu tangu nikiwa na miaka 80. Nitakuonesheni.' mzee Ngomvia alieleza, halafu akaiinamia karatasi ile kwa kusudi la kuusoma ujumbe ule.

'Siku zinakaribia, nazo zimekwishakuweko. Wataiangamiza dunia kwa mikono yao wenyewe. Wataiangamiza dunia kwa kudhani wanaiokoa. Damu ya kijani ndiyo kinga ya dunia. Ukitokea mlipuko, heri yake atakayekuwa na tone la kijani mishipani mwake.' mzee Ngomvia alimalizia kuutafsiri ule ujumbe.

'Mmeusikia ujumbe. Maelezo niliyopewa mimi kwenye ndoto ni haya yafuatayo. Watoto mia moja wanazaliwa, na wengine wamekwisha kuzaliwa. Watoto wa ajabu, watoto hao wana damu za kijani mishipani mwao. Huo ujumbe kwamba damu ya kijani ndiyo kinga, unamaanisha kuwa, watoto hao wanaweza kuokoa kizazi cha dunia kisiteketee na janga linalokuja kuikumba dunia. Janga hilo litaibuka na kuenea dunia nzima hadi kufikia mwaka 2030, litateketeza wengi. Watapona wenye damu ya kijani mishipani mwao. Tone moja tu litakuwa kinga dhidi ya tauni hiyo.

'Kwa nini wewe, Steve, umechaguliwa kulisimamia hili suala? Kwa sababu unazo namna za kuweza kuhakikisha hili linafanikiwa. Uwezo wa kifedha na Sayansi yako vinafaa kutumika kuokoa dunia, lakini muhimu zaidi, hakikisha unawakusanya hao wenye damu ya kijani kutoka kila kona ya dunia. Kundi ovu kabisa duniani, linalokusudia kuokoa dunia litaangamiza dunia. Kundi hilo lisipate kutia mkono wake kwa watu wenye damu ya kijani. Andaa kabisa watu wa kuwasaka watu hao wawe kwenye mikono salama. Mikono yako.' Mzee Ngomvia alimalizia kuongea, akanyanyuka na kutembea kuelekea upande wa nyuma wa nyumba yake. Nyumba iliyojengwa kwa fito na nyasi kama ilivyokuwaga asili ya nyumba za wasandawe. Kwa muda wote huu, Steve Curl alikuwa anashangazwa na haya yaliyokuwa yanaendelea. Mzee Ngomvia, alikuwa ameeleza suala la mtu wa damu ya kijani, ikiwa yeye alishuhudia mtu wa aina hiyo na hakuwa amemweleza chochote kuhusiana na huyo mtoto. Hakuwa na shaka kuwa, alipaswa kutekeleza maelekezo hayo. Ilikuwa ni nguvu ya juu kuliko alivyodhania hapo awali.

'Hapa ndipo nitakapopumzika ndugu zanguni.' Alizungumza mzee Ngomvia akiwa anawaonesha kwa kidole chake cha shahada eneo ambako kulionekana shimo. Lilikuwa ni kaburi ambalo mzee huyo alikuwa keshajiandalia. Halafu akaendelea kutoa nasaha zake huku akivuta tumbaku iliyokuwa kwenye kiko chake.

'Ni vizuri sana ukatumia ushawishi wako, au fedha zako ili kuisambaza kinga hiyo, ikilazimu duniani kote. Iwe chanjo kwa watoto wanaozaliwa, wakubwa na vijana. Hivyo ndivyo dunia itabaki salama.' mzee Ngomvia alirejea kwenye kiti chake kinachobembea, akavuta tena mkupuo mmoja wa kiko chake, akakohoa halafu akabaki anabembea. Kimya. Zilipita dakika tano za ukimya ndipo mwenyekiti wa Kijiji cha Bubutole akawaeleza wenzake walioambatana na Steve Curl kuwa mzee alikuwa kapumzika jumla.

Siku hiyo, mbiu ikapigwa kijijini, wanakijiji wote wakakusanyika kwa mzee Ngomvia kumpa heshima yake ya mwisho. Akazikwa kama alivyoelekeza. Kijiji kikakumbwa na simanzi. Ngomvia alikuwa kamaliza kusudi lake duniani. Yakazungumzwa mengi, lakini moja likabaki bayana, mzee huyo aliishi miaka mingi akisubiri kutoa salamu ambazo zingeokoa dunia.

Steve Curl alipoondoka kijijini Bubutole, alirejea Dar na akiwa huko, akapata maono ya kuanzisha maabara kubwa Zanzibar kwa ajili ya shughuli aliyokuwa kapewa. Ajabu ni kuwa alipata maelekezo na hata ramani ya eneo ambako alipaswa kutengeneza maabara yake. Eneo lenyewe kama alivyoliona kwenye maono yake, lilikuwa limejengwa Hotel ya kisasa, hotel iliyojulikana kama Safari Hotel. Steve Curl akaitembelea hotel hiyo, akaangalia na maeneo yake, ilikuwa na eneo kubwa sana la wazi. Akaazimu kuinunua hoteli hiyo na eneo kubwa la wazi lililokuwa nyuma yake.

Alipoweza kuimiliki hoteli hiyo kwa hisa asilimia 70, Steve akaanza kujenga maabara yake chini ya ardhi kama alivyoona kwenye maono yake. Kule ambako Masu na mwenzie Yusuf walipoingia baada ya kusaini mkataba na Steve Curl kama wafanyakazi wake.

Baada ya kukamilisha mradi huo, Steve Curl akaamua kuanzisha program ya kusaidia afya ya mama na mtoto. Kwa kutumia program hiyo, akawa na uwezo wa kuchunguza damu za watoto waliozaliwa wenye damu ya kijani kama ilivyokuwa kwa Yeraz. Ndani ya miaka miwili baada ya kuondoka kwa mzee Ngomvia, Steve alimudu kupata watoto kumi na watatu tu kati ya mia moja alioambiwa. Huo ukiwa ni mwaka 2018. Mwaka ambao pia alikutana na vijana Masu na Yusuf.

***

Haya, Sasa turejee kwenye mtiririko wetu wa awali.

Ilikuwa Zamu ya Philip Mwangaza kukaa kwenye control room, siku moja baada ya Molio na wenzake kuondoka Oman. Kama kawaida yake ya kupenda kumfuatilia sana Molio, na kwa jinsi alivyomzimikia binti huyo, Philip alimuona Molio akiwa eneo la supermarket kwa kitambo kikichompa mashaka. Nusu saa ikakata, Molio alionekana kutulia sehemu moja kwa muda mrefu mno. Akili ya Philip ikagoma kuamini kuwa Molio atakuwa kaketi tu bila kazi kwa muda wote huo. Kwa miaka karibia sita sasa akiwa anafanya kazi hii, kwa miaka yote hiyo, Philip hakuwahi kumuona Molio kaketi eneo moja kwa zaidi ya dakika tano. Heri basi ingekuwa kwenye apartment yake, Philip angedhania kuwa ameamua kujipumzisha, lakini supermarket? Ah a- a, kulikuwa na jambo, na jambo hilo halikuwa jambo hivi hivi. Aidha alikuwa anaumwa au katekwa na kufichwa kwenye mastoo ya supermarket ile.

Philip alinyanyua simu na kumpigia mmoja kati ya kijana miongoni mwa wale waliofunzwa kama maroboti tangu wakiwa na miezi sita. 'S12, nenda kacheki status ya M89'

'Message delivered' akajibiwa na komputa kwa sauti ya robot.

Baada ya hapo, Philip alikaa kitako akimwangalia S12 akikatiza mitaa kuelekea supermarket.

S12 alikuwa na kifaa cha ku-track chip zilizopandikizwa kwenye miili yao, na katika kazi yao, walijulikana kwa namba za chip zilizopandikizwa miilini mwao. Ajabu, S12 alifika eneo iliposoma chip M89, lakini hakumuona Molio. Mara ghafla, ikaonekana kwenye kifaa chake kuwa M89 ilikuwa inasoma kwamba yuko New York. Walikuwa wamechelewa. Issa Musa aliiprogram chip ile kwamba ikihisi kutafutwa inabadili eneo.

Taarifa zikapelekwa USA, washirika wa ENTRY waliopo huko, wakapewa jukumu la kumsaka M89, harakati zikaanza, kila walipoiona, walipofika hapo, walikuta hola, walipofika iliposemekana ipo chip M89, mashine yao ikawaambia, yupo Dubai. Wakaushitukia mchezo, lakini hadi hapo, wiki moja ilikwishapotea. Mzee Kisiki akapata habari, wiki moja ilikwishapotea na mkewe Mwamvita akiwa ameondoka na Molio. Mzee Halfani Nassor akafura kwa hasira, msako wa kufa kupona ukatangazwa Zanzibar.

Vijana wale wa Dubai, watu wasio na hisia, wakapewa jukumu la kuifumua Zanzibar ndani nje hadi wamemtia mkononi Molio, Masu na Mwamvita.

Katika harakati hizo, Ustadh Abuubakr akiwa katulia dukani kwake, mzee Kisiki akamuibukia.

'Wewe mzee utanambia mke wangu yuko wapi, waswahili pumbafu sana nyinyi. Kamata huyo twende naye.' Kisiki alikuwa kavimba balaa. Akaagiza mzee mwenzie kuwekwa mkononi mwa ENTRY.

***

Baada ya misheni kukamilika, na wao kurejea Zanzibar, Molio na Issa Musa waliondoka na kwenda zao ushelisheli, nchi pekee Africa imayotambuliwa na benki ya dunia kama taifa lenye HDI (Human Development Index) kubwa na Pato kubwa la kiuchumi. High Income Economy. Hapo pia, Issa Musa alikuwa na vitega uchumi kadhaa katika jiji kuu la ushelisheli, Victoria. Alikuwa na kampuni ya uanamitindo.

Kwa upande wa pili, Masu baada ya kubaini kuwa sasa alipaswa kuwa makini zaidi, aliamua kumficha Mwamvita huko Iringa kwa rafikiye Bakari au Paulo ukipenda. Yule ambaye walimpa milioni 10 na yeye akaamua kuwekeza huko kwao kwenye mashamba ya miti ya biashara na duka kubwa la jumla. Paulo sasa alikuwa na uchumi unaoeleweka kiasi na hakuona shida kurudisha fadhila kwa rafiki yake. Alimpokea Shemejie na kumkabidhi kwa Dada yake. Hapo Mwamvita akaishi kama yuko nyumbani kwa namna ya upendo aliooneshwa na wenyeji wake. Masu akarejea Zanzibar. Ilikuwa ni wiki ya kuanza kazi ya Mzungu.

Itaendelea….

JamiiForums528126083.jpg
 
KAZI YA MZUNGU 30
MTUNZI DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

Disclaimer: Hii ni simulizi ya kubuni. Tafadhali soma kama sehemu ya burudani. Yaliyoandikwa humu hayana uhusiano na ukweli wowote ule na kama ikitokea hivyo itakuwa sadfa tu.

***
Kama alivyosema Yusuf hapo kitambo alipokuwa akimjulisha Masu juu ya kazi yao mpya, kazi ya Mzungu Steve Curl haikuwa kazi ngumu kama ile ya kubeba mizigo waliyokuwa nayo hapo awali. Lakini kama alivyosema Mzungu mwenyewe, Steve Curl, ni kazi ambayo ilihitaji ujasiri kweli kweli. Ndio maana aliwapa mafunzo ya kiintelijensia na kijeshi, kwa lengo la kukabili hali hizo watakapoingia kazini. Waliporejea kazini ili kuanza kazi, Steve aliwakumbushia kiapo chao. Akawakabidhi mikononi mwa mtaalam Master Park Hye kukumbushwa walichofunzwa na kufahamu kama bado walikuwa na ratiba ya kufanya mazoezi kama alivyoelekeza hapo awali. Vijana hawa walikuwa makini kwa kila hali na walionekana kuwa bora hata zaidi ya walivyokuwa mwanzo.

Master Park Hye, alitumia ujuzi wake kuwapa maelekezo juu ya shughuli waliyokuwa waifanye. Shughuli ya kuhakikisha dunia inakuwa salama dhidi ya kundi hatari ambalo likikusudia kuokoa dunia, kwa kuondoa karibu robo tatu ya binadamu wote waishio duniani. Kazi yao hasa ilikuwa ni kuhakikisha wanazalisha chanjo za kutosha, na kuzitawanya kote duniani. Kazi hiyo ya kuzalishwa chanjo, ilikwishaanza, na tayari wao pia walikwishachomwa sindano ya chanjo hiyo katika hatua za mwanzoni kabisa walipokuwa wanafundishwa mazoezi yale ya kijeshi. Umakini wao na mafunzo yao, yalilenga kuhakikisha kuwa chanjo hiyo haiingii mikononi mwa lile kundi hatari, ambalo Masu alibaini kuwa ENTRY, walikuwa ni washirika wa kundi hilo hatari.

Pamoja na kusambaza chanjo hiyo duniani kote, pia kazi nyingine ilikuwa ni kuwasaka na kuwakusanya wale watu wenye damu ya kijani. Kazi hiyo ilionesha kuwa ngumu na hatari zaidi kwa maana watu hao, walikuwa na uwezo mkubwa sana, japokuwa walisumbuliwa sana na uraibu. Uraibu wa tabia za hovyo hovyo na ule wa dawa za kulevya. Ndio wale ambao hapo awali, Masu na mwenzie Yusuf, waliwashuhudia kwenye ile club ya kisasa chini ya ardhi kule Safari Hotel walipokuwa wanaelekea kwa master Park Hye. Watu hao, wa rangi tofauti tofauti, walipatikana katika mazingira hatarishi hatarishi tu. Wengi wao, wakitopea kwenye uraibu wa dawa za kulevya kulikotokana na msongo wa mawazo. Ni viumbe ambao walihisi hapa duniani sio kwao, ni kama walikuwa viumbe kutoka sayari nyingine ambao walijipata wametupiwa huku duniani na hivyo kujikuta kwenye msongo mkali wa mawazo na sonona. Wengine wao uraibu wao ulikuwa starehe tu. Kunywa pombe na kufanya ngono.

Hata hivyo, tajiri Steve na jopo la wanasayansi waliokuwa kwenye kampuni la Scientific Reality Inc, walipowafanyia uchunguzi vijana hao, walibaini kwamba watu hao walikuwa na Intelligence Quotient (IQ) kubwa kuliko binadamu wa kawaida. Hivyo, wakaamua kuwafundisha mambo kadha wa kadha ya kisayansi, kijamii na kadhalika. Walikuwa wepesi wa kushika kile walichofundishwa na hata wakatokea kuwa watu wenye uwezo wa kipekee. Kwa usaidizi wao, Steve akashirikiana nao kutengeneza kifaa ambacho kiliwezesha kutambua walipo wenzao, watu wenye damu ya kijani kama wao. Uwepo wa watu wenye damu ya kijani kwenye kampuni ya Scientific Reality Inc, kuliwezesha kampuni hilo kuwa juu sana kiutafiti na kuvumbua ama kugundua sayansi mpya ambazo zilileta mapinduzi ya kisayansi na kiteknolojia na hivyo kuteka masoko ya dunia kwa vumbuzi zao mpya. Kila siku, Scientific Reality Inc (SRI) ilikuwa inapiga hatua kubwa kiuchumi, na kuwa kampuni lililoongoza kwa ukwasi duniani, huku likiingiza bidhaa mpya kabisa sokoni mara kwa mara.

Safari yao ya kwanza, Masu na Yusuf walipeleka chanjo nchi jirani ya Kenya, katika mpango uliopewa jina, Steve Curl Post Natal Care Program (PNCP). Mradi ambao ulikubalika mapema na serikali ya Kenya na kuifanya nchi hiyo kuwa miongoni mwa mataifa ya mwanzo kabisa kupokea chanjo hiyo. Mataifa mengine Africa ambayo yalikuwa mstari wa kwanza kupokea chanjo hiyo yalikuwa; Sudan Kusini, Uganda, Zambia, Gambia, Liberia, Congo, na Tanzania. Tayari mataifa kadhaa ya Asia ukitoa yale yaliyojiona kuendelea sana, yalikuwa tayari kupokea chanjo na mipango ilikuwa inaratibiwa kuisambaza chanjo hiyo.

Katika kuifanya ENTRY na washirika wao wasishituke kuwa huu ulikuwa mpango kinzani na mpango wao wa kuangamiza robo tatu ya dunia, waliitangaza chanjo hiyo kuwa ni chanjo ya kuzuia maambukizi yanayoshambulia kinga ya mwili. Kuna watu, kama ilivyo kawaida ya binadamu, tayari walianza kueneza uvumi kuwa hiyo ilikuwa chanjo ya kujikinga na UKIMWI. Hata hivyo, SRI kupitia kitengo chao cha mawasiliano na umma, kilikanusha uvumi huo na kutoa ufafanuzi wa nini ikikuwa dhima ya chanjo yao.

Wakati hayo yakiendelea, ENTRY na washirika wao, walikuwa kwenye harakati za kutekeleza mipango yao vile vile. Walitumia ushawishi wao, kuyashawishi mataifa ya ulaya na Marekani kuikataa chanjo ya kampuni la kisayansi SRI. Hiyo, ikiwa ni katika kumkwamisha Steve Curl, kwa kile kilichoonekana ni kupuuzwa kwa pendekezo lao la kumtaka tajiri huyo kuwa sehemu ya mpango wa ENTRY. Ilikuwa Vita ya kiuchumi. Mataifa hayo, kwa vile viongozi wao walikuwa miongoni mwa wanachama wa kundi la ENTRY, hoja ya ENTRY ilipita bila kupingwa. Hiyo ikamfanya Steve Curl na kampuni yake kuelekeza nguvu kwenye mataifa yaliyoonesha kuwa na utayari. Mpango wa mama na mtoto ulikubalika kirahisi, lakini lilipokuja suala la kuwa wanaume wapate chanjo hiyo, utekelezaji wake ulifanikiwa kwa asilimia thelathini tu. Hata hivyo, SRI, ilibuni namna mpya ya kuhakikisha chanjo hiyo inawafikia watu wengi kadri iwezekanavyo. Pendekezo kutoka kwa wanasayansi wa SRI, watu wenye damu kijani, wakapendekeza chanjo kutolewa mashuleni na vyuoni.

***

Dr Wu Han, akiwa na jopo la wanasayansi wenzake katika kituo cha kisayansi nchini China katika jimbo la Beijing walikuwa wamefanikiwa kutengeneza chanjo dhidi ya kirusi hatari ambacho kilisemekana kwamba chanzo chake ni kutokana na mamalia aitwaye popo. Kirusi hicho kilisemekana kuwa katika kundi la virus wanaojulikana kama Corona. Makundi mengine ya virus aina ya Corona ni pamoja na MERS na SARS.

Corona ni virus hatari ambao wanakuwa na uwezo wa kujibadili ili kuishi katika kiumbe mpya walikofanikiwa kuingia. Hii ikiwa na maana kuwa, wanapotoka kwa kiumbe mmoja na kuingia labda kwa binadamu, wanajifaragua na kujifanya ni wenyeji, na hivyo huigiza kama wenyeji wa mwili huo mpya ili wapate kuishi bila usumbufu huku wakimdhoofisha mwenyeji wao. Kitaalamu kitendo hicho huitwa mutation.

Hali hiyo ya kubadilika kutoka mtu/kiumbe mmoja na kubadilika tena kinapoingia mtu/kiumbe mwingine kulingana na mazingira mapya(adaptive), ndicho kitendo ambacho kiliwafanya virus wa kundi la corona kuwa virus hatari sana. Uhatari wao ukiwa na maana kwamba, kama ungefanikiwa kudhibiti kirusi kwenye mwili wa kiumbe mmoja, haingekuwa hakika kwamba ungedhibiti kirusi huyo katika mwili wa kiumbe mwingine. Na hiyo ingepelekea viumbe wengi kufa, kwa sababu, virus hao tofauti na wale wa UKIMWI ambao huambukizwa kwa njia ya kujamiiana au damu, virus wa corona, huenezwa kwa njia ya matone ya chafya au kohoo.

Hawa corona sawa na wale wa ugonjwa wa Ebola, namna ya kuwazuia kuenea ilikuwa kuwatenga wagonjwa mbali na wale wazima. Vinginevyo, virus hao ambao wanaweza kuishi nje ya mwili kwa masaa nane hadi sabini na mbili kutegemea na mazingira walikoachwa, ni rahisi zaidi kuambukizwa kama mtu atagusa tone la chafya au kohoo lilioachwa na mgonjwa katika eneo fulani kwa kipindi cha kati ya saa nane hadi sabini na mbili. Yaani siku tatu. Iwe kwenye kiti cha basi, au kwenye bench kwenye maeneo ya wazi, nyumbani, shuleni, ofisini au eneo lolote ambako watu hukutana.

Katika kuhakikisha watu hawaambukizani, ilibidi mtu kuzingatia usafi na kuepuka mambo kama; kusalimiana kwa kugusana, kukusanyana makundi makundi, kugusa uso kwa mikono baada ya kugusa kitu ambacho usalama wake dhidi ya vitone haujajulikana, kukaa jirani chini ya umbali wa meta moja, kubusiana n.k. Ni mambo ambayo kikawaida, hayakuwa rahisi kutekeleza, na hivyo ni kusema, virus hao wangeenea haraka mno na kusababisha vifo kwa wingi sana hasa kama mhanga angekuwa anasumbuliwa na magonjwa mengine ambayo kwa namna moja ama nyingine yanakuwa yamelegeza kinga ya mwili.

Baada ya tafrija ndogo ya kupongezana kwa kumudu kutengeneza chanjo hiyo madhubuti dhidi ya corona, Dr Wu akapokea simu kutoka ofisini kwa mkurugenzi wa taasisi yake, Dr Myers Futodo. Katika ofisi ya Futodo, kulikuwa na meza moja ndefu bapa, meza maalumu kwa ajili ya kufanyia vikao. Wazungu huita conference table. Huko Dr Wu alikuta meza ile imeenea wageni, waliovalia suti nadhifu. Chumba kilinukia harufu ya ukwasi kutokana na hadhi ya wageni waliouwemo. Alikaribishwa na kupewa nafasi katika mzunguko ule maridadi. Hakupoteza muda, aliketiketi chini akiwa na muhali wa sintofahamu. Mbona ghafla? na mbona hakupewa taarifa? Ni maswali yaliyokuwa yanazunguka kichwani mwake wakati akizungusha macho yake taratibu kama vile kuwasaili wageni hao wa kizungu.

Dr Futodo alisimama na kumtambulisha Dr Wu kwenye kikao.

'Gentlemen, this is Dr Wu Han, the head of our CRC scientist group that has led to our very celebrated breakthrough'. (Waungwana, huyu ndio Dr Wu Han ambaye ameongoza jopo la wanasayansi wetu wa CRC na kutuletea mafanikio tunayosherehekea hivi sasa.) Futodo aliongea halafu akamgeukia Dr Wu na kusema;

'Dr Wu, karibu Sana. Najua imekua ghafla sana lakini naamini hili ni suala muhimu sana kwa taasisi yetu na kwako binafsi. Waungwana hawa wamekuja na pendekezo la kununua formula ya uzalishaji wa chanjo hii uliyogundua. Nina hakika kuwa kwa dau wanalopendekeza, maisha yako yatabadilika kabisa. Sharti lao ni moja tu, wakishachukua formula, wewe na wenzako, hamtatakiwa kujihusisha na suala hilo la chanjo hiyo. Na kusema kweli Dr, binafsi najua hilo sio tatizo kwa vile kuna mambo chungu nzima ya kufanyia utafiti na huenda yakaja na mibaraka mingine kedekede kama huu. Pamoja na malipo ambayo wanapendekeza kununua formula, wewe na wenzako mtaendelea kupata gawio la faida ya mauzo na uzalishaji wa chanjo hiyo, kwa kipindi chote cha uhai wenu kwa mfumo wa kulipwa mshahara kila mwezi. Dr Wu, nataka nikueleze ukweli ndugu yangu, sijawahi kuona dili lenye faida kama hilo tangu nizaliwe. Naamini ni chizi pekee ambaye anaweza kulikataa dili hilo ikiwa anapata mshahara kiduchu unaopata kwa sasa na kwa kazi kubwa hii ambayo umekamilisha.' Dr Futodo alijieleza kwa ushawishi mkubwa hata kumudu kumshangaza Dr Wu.

Wakati anamaliza kuyaeleza hayo, Dr Wu alikuwa anajiuliza ni nini hicho ambacho kiliwafanya hawa jamaa watake formula ya chanjo hiyo kwa gharama kubwa kiasi hicho? Leo, Dr Futodo, anasema anamlipa mshahara kiduchu, wakati mara zote amekuwa akidai yeye ndiyo mtu pekee anayelipa mshahara mnono kwa watumishi wake?. Huo wa hawa jamaa ni mnono kiasi gani? Dr Wu, akapata mashaka. Something fishy was cooking.

'How much are we talking about here?' (Tunaongelea kiasi gani hapa?) Dr Wu akauliza kwa yakini. Pesa aliyoambiwa, hakuwahi kuota kama atakuja kuimiliki. Ni mabilioni ambayo yangeishi hadi kizazi cha sita cha uzao wake wakiwa hawafanyi kazi na wakila raha zote za dunia ikiwamo kutembea kote duniani kujionea vivutio vya kila aina. Na bado, kulikuwa na mshahara mnono ambao ulikuwa mara tano ya ule aliolipwa na Dr Futodo. Mshahara ambao angelipwa hadi anapozama chini kukutana na wahenga. Dau hili, lilikuwa kubwa zaidi ya dau ambalo alikuwa ametajiwa na tajiri Steve Curl ambaye naye alionesha nia ya kuchukua formula hiyo. Dr Wu, akaomba apate siku mbili walitafakari suala hilo na watu wake.

Alipotoka mle ofisini, Dr Wu hakuwa katika hali ya kawaida. Dau lile lilikuja kama jaribu kubwa sana kwake. Akili yake ilikuwa kwenye mvutano wa aina yake. Hakudhani kuwa wazungu wale wa kimarekani walikuwa na nia njema na chanjo yake. Hivyo alijikuta kila akitafakari haoni jema mbeleni. Akashawishika kuchimba kwanza kuijua kampuni hii iliyotaka kununua formula hiyo waliyoipa jina Anti Corona Virus Vaccine(ACVC) kinagaubaga.

Ilikuwa kampuni ya kimarekani, lililoitwa Earth Vision 2050. Kampuni hii ilisemekana inahusika na uhifadhi wa mazingira kwa afya. Maono ambayo walitegemea yakamilike ifikapo 2050. Ilimiliki taasisi kadhaa za utafiti ambazo zilipata ufadhili wa shirika la afya duniani WHO. Kampuni Hilo la earth Vision 2050, lilikuwa na makao yake makuu nchini Marekani katika jimbo la Atlanta. Kilichomshitua kidogo, ni makala kadhaa zilizohusianisha kampuni hilo na kampuni maarufu ambalo liliendesha mambo yake kisiri, kampuni la ENTRY. Alikuwa na taarifa kiasi kuhusu kampuni la ENTRY, halikuwa kampuni zuri. Hakupenda kuamini conspiracy theories, lakini alijikuta kwa kampuni hilo anajenga mtazamo hasi kulihusu.

Dr Wu akapata mashaka. Hivyo akadhamiria kukataa ombi hilo. Alikusudia kumshawishi Dr Futodo kuwa formula ile kubaki mikononi mwao kungeleta faida zaidi kwa taasisi ya CRC kuliko kuitoa. Hakuwa na shaka kwamba wenzake wangekubaliana naye.

Aliwapigia simu wanasayansi wenzake walioshirikiana kutengeneza formula ile ili kuwashirikisha mpango wake. Kitu ambacho Dr Wu hakujua, ni kwamba akaunti za wenzake tayari zilikuwa zinasoma mamilioni ya dola za kimarekani. Yeye tu, ndio alikuwa mtu wa kutazamiwa.

Dr Wu alipokutana na wenzake, ambao kila mmoja kwa wakati wake alikuwa anatarajia kikao hiki baada ya kushawishiwa, walimpa masikio Dr Wu. Wao sasa walitarajia kile walichoelezwa kuwa ni fungu la pamoja kama angewashawishi wenzake kukubali mpango wa mauzo ya formula. Dr Wu alijikuta yuko mwenyewe mwenye mtazamo wa kuibakiza formula kwenye taasisi. Kila mmoja alionekana kushawishi formula iondoke na Earth Vision 2050.

Alipojaribu kumshawishi Dr Futodo, yeye pia alimuona kama ana uchizi unaomsumbua. Hakumuelewa kabisa. Hata hivyo kwa vile alikuwa mtu pekee aliyejua formula kwa ukamilifu, wale wengine wakiijua kwa sehemu ndogo, ufahamu wa suala hilo ukampatia kiburi. Akagomea mpango huo katakata.

Earth Vision 2050, wakiwa wamepata fununu kuwa Dr Wu analeta vikwazo kwenye mpango wao, wakaenda hatua moja mbele. Aliporejea nyumbani tokea ofisini akakutana na ujumbe, akubali dili, au familia yake iteketee. Tena safari hii wakimweleza hatapata kitu. Dr Wu akachanganyikiwa. Familia yake iteketee? Hapo akajua wale si watu wema kabisa. Akapanga kufanya kitu. Kutoa taarifa kwa serikali yake tukufu juu ya hili jambo lililoashiria kuwa la hatari.

Alipokuta wanawe watatu na mama yao wametekwa, Dr Wu katika hali ya kuhamanika, akatoka mbio ndani akiwa amebeba briefcase ambayo huenda ilikuwa na ile formula. Akaingia kwenye gari lake na kulitia moto. Moja kwa moja akaelekea wizarani. Wizara ya tafiti na sayansi. Ilipopita siku moja bila Dr Wu kuonesha jitihada za kukomboa familia yake, watu Earth Vision 2050, wakahisi Dr Wu atakuwa ameamua kuitoa sadaka familia kuliko kutoa formula. Msako wa kumtafuta ukaanza.

Itaendelea Kama nitapata mrejesho chanya kuwa kuna wasomaji wanafuatilia......
JamiiForums528126083.jpg
 
Kaka nafatilia kila nukta ya strory hii. Now ni saa sita na nusu usiku. Jiulize ni jinsi gani nafatilia. Ni bonge moja la story lenye mtiririko makini kabisa. English iliyonyooka na nahisi kabla ya kuandika umetafiti mambo mengi sana. It is a brainporn.

Itaendelea Kama nitapata mrejesho chanya kuwa kuna wasomaji wanafuatilia......View attachment 1699435
 
Asante Sana mkuu. Nimefurahia Sana maoni yako. Nimepata hamasa.
 
Tunaifuatlia kila inavyosogea mkuu.....kazi nzuri sana ya kipekee.
 
Hakika riwaya hii inapita riwaya zako zote ulizo Wahi kuandika kwa ubora,elimu,burudani. Umefanya utafititi wa kina imezungumzia migogoro mipya inayo tupata kwa sasa. Sikupaki Mafuta kwa mgongo wa chupa. Mwaka Kesho Naomba ushiriki tuzo za MABAT. lakini yapo machache ya kurekebisha ili watu wa MABAT wakupitishe.Utamuona Enock Maregesi atakusaidia. 2022 TUZO YA MABAT upande wa riwaya ni yako. Sitashiriki kwa Maana umenishinda hata kabla sijaweka riwaya yangu MABAT
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom