Simulizi: Kazi ya mzungu

Simulizi: Kazi ya mzungu

Hakika riwaya hii inapita riwaya zako zote ulizo Wahi kuandika kwa ubora,elimu,burudani. Umefanya utafititi wa kina imezungumzia migogoro mipya inayo tupata kwa sasa. Sikupaki Mafuta kwa mgongo wa chupa. Mwaka Kesho Naomba ushiriki tuzo za MABAT. lakini yapo machache ya kurekebisha ili watu wa MABAT wakupitishe.Utamuona Enock Maregesi atakusaidia. 2022 TUZO YA MABAT upande wa riwaya ni yako. Sitashiriki kwa Maana umenishinda hata kabla sijaweka riwaya yangu MABAT
Asante Sana Kaka. Nitashiriki na kuzingatia ushauri wako mkuu
 
KAZI YA MZUNGU 31
MTUNZI: DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

Dr Wu aliingia kwenye geti la wizara ya tafiti, Sayansi na teknolojia kwa mwendo wa fujo. Mwendo alioingia nao eneo hilo ulikuwa hatari. Hata hivyo, alihisi umuhimu wa kufika wizarani hapo ulihitaji mwendo zaidi ya huo aliotumia kufika hapo. Alishuka garini na kutembea mwendo wa nusu kimbia nusu tembea. Hakupoteza muda, aliingia kwenye lifti iliyompandisha juu ili kuingia kwenye afisi ya katibu mtendaji wa wizara hiyo muhimu kwa serikali ya China. Kwa muda sasa simu yake ilikuwa inaita lakini hakuipokea kutokana na ukweli kwamba alikuwa amezingatia zaidi kuendesha gari. Akiwa kwenye lift, akaisikia tena simu yake ikiita kwa bidii. Bila shaka mpigaji alikuwa na jambo muhimu. Dr Wu aliichomoa simu hiyo kutoka mfukoni na kuitazama. Jina kwenye skirini ya simu hiyo lilimtambulisha vema mpigaji. Alikuwa mkurugenzi wake wa CRC, Dr Futodo. Hakupokea. Tayari alikuwa keshafikia mlangoni mwa ofisi ile aliyokusudia kwenda. Kwa haraka aliyokuwa nayo, Dr Wu alizama ofisini kwa katibu mkuu bila kubisha hodi. Kitu cha kwanza kukiona ilikuwa ugeni uliokuwa umetamalaki ofisini humo. Akajipata anapatwa na mshituko mkubwa uliosimamisha mapigo yake ya moyo kwa sekunde kadhaa. Majamaa wawili kati ya wale waliokuwa kwenye kikao hapo awali kwenye ofisi ya mkurugenzi wa taasisi yake, Dr Futodo, wazungu wa Earth Vision 2050, walikuwa wamemakinika sana wakizungumza kwa ushawishi na katibu mkuu wa wizara hii ya tafiti, Sayansi na teknolojia. Sio ajabu kwamba hawakujua uwepo wake hapo mlangoni. Kuwaona watu hao mahali hapa, kuligonga kengele ya tahadhari kichwani mwa Dr Wu. Akili hiyo iliyogonga kichwani haikumpa muda Dr Wu kufikiria mara ya pili, la hasha! Dr Wu alichofanya ni kugeuka haraka sana na kutoka mle ndani bila kushitukiwa na watu wale.

Dr Wu sasa aliweza kubaini ni kwa kiwango gani wazungu wale walivyokuwa wamejipanga vya kutosha. Hawakuwa na mchezo dhidi ya kufikia lengo lao la kuitia ACVV mikononi mwao. Bila shaka ilikuwa wazi kwamba walikusudia kwa njia yoyote ile waitie formula mkononi mwao. Dr Wu alishuka tena kwa kutumia lift, akatafuta jina kwenye orodha ya majina kwenye simu yake, akampigia simu afisa mmoja waliyefahamiana vema. Afisa kutoka idara ya usalama wa taifa ya uchina, Ministry of State Security (MSS). Li Wenqing. Li na Dr Wu walioa sehemu moja, ikiwa ni Li aliyeoa dada wa mkewe Dr Wu. Wakati huo tayari alikuwa keshalifikia gari lake aina ya Harrier nyeusi na kulitekenya kwa funguo kisha kuliondosha hapo kwa mwendo ule ule aliokuja nao hapo awali.

Ajent Li alipopokea simu tu, Dr Wu alianza kutiririka maneno yake yaliyojaa hofu yake dhidi ya adui zake. Akiwa mbio, Dr Wu alishuhudia magari kadhaa nyuma yake yakija waruwaru ungedhani wapo kwenye mashindano ya magari. Dr Wu aliwatambua watu hao kuwa ni wale wazungu wa Earth Vision 2050. Hali hiyo ikamtia wasiwasi.

'Li, nina nyaraka muhimu sana ambazo hivi napoongea kuna wamarekani wanazifuatilia, hapa nilipo nawakimbia lakini naona wananifukuzia. Kama wakizitia nyaraka hizi mikononi mwao, usalama wa taifa letu utakuwa mashakani. Kama likitokea lolote kwangu, ongea na mkeo, mtaa wa Zanzibar kuna mapinduzi baada ya milipuko ya bomu, mkeo atakupa funguo,.' Dr Wu aliongea akiwa anahemea juu juu. Sentensi zake, hazingeeleweka kwa mtu mwingine, lakini Li Wenqing alijua Dr Wu anaongea kwa lugha ya kificho, kwa lengo la kuwapoteza maboya wale ambao huenda wangekuwa wanayanasa mazungumzo hayo.

'Uko wapi sasa?' Li Wenqing aliuliza huku akiliwasha moto gari na kuliingiza barabarani.

'Nakaribia Tiananmen square, kama upo ofisini utaona napita hapo nikifukiziwa na gari jeusi nyuma yangu.' Eneo la Tiananmen na makao makuu ya ministry of state security ni mwendo wa dakika chache tu. Hazikupita dakika mbili, ajenti Li akiwa anachekecha usukani wa gari lake aingie barabarani akashuhudia gari la Dr Wu na nyuma yake kweli gari mbili nyeusi aina ya Forrester yakimfukuzia. Ajenti Li hakutaka tena kupoteza muda, akaingia kwenye mtanange huo wa kushindana mbio. Sasa magari yale ya jamaa wa Earth Vision 2050 yalikuwa kati ya Dr Wu na agent Li.

Waliendelea kufukuzana katika barabara hiyo kuu inayoanzia Fuxing, ambako majengo ya wizara ya tafiti, sayansi na teknolojia yapo. Sasa walikuwa wanaenda nayo kwa mwendo mkali sana na hatarishi kwa watumiaji wengine wa barabara. Mara ajent Li akawashuhudia jamaa wa Earth Vision 2050, wakianza kuligonga gari la Dr Wu kiupande upande. Dr Wu akajitahidi kulimudu gari lake na kulirejesha katikati ya barabara mara kadhaa baada ya kusogezwa pembezoni mwa barabara. Hata hivyo, haikuchukua muda mrefu kabla hajakumbana na kishindo kingine nyuma yake.

'Usisahau maelekezo yangu tafadhali' Dr Wu akaongea kwenye simu halafu akaongezea;

'Wameshikilia familia yangu na….' hakufanikiwa kumaliza kauli, gari lake likagongwa tena, mara hii, halikusalia barabarani. Likaviringika mara kadhaa na kutoka nje kabisa ya barabara kisha likaanza kuwaka moto. Majamaa wa Earth Vision 2050 hawakusimama. Wakaendelea kama vile hapakutokea kitu.

Wakati agent Li alishangaa kuona jamaa yake amefanyiwa ile hujuma, akiwa amepaki gari pembeni, gari moja sawa na lile lililosababisha ajali lilishika break mbele yake, wakaruka majamaa wawili na kulifuata gari la Dr Wu. Wakati ajent anasogea ili kusaidiana na wale jamaa kufanya uokoaji, akawashuhudia jamaa wakirejea kwenye gari lao wakiwa na brief case ya Dr Wu. Katika kuonesha kuwa walijua yeye ni nani, au kwa ajili ya tahadhari, wale jamaa walilishambulia gari lake kwa risasi na kuondoa upepo kwenye matairi. Ajenti Li akawashuhudia jamaa wakitoweka mahali hapo kwa mwendo wa hatari. Agent Li hakuwa na ujanja. Hata hivyo, Sasa alianza kuona hatari aliyokuwemo Dr Wu.

Baada ya wazungu wale kuondoka, ajenti Li alilisogelea gari la Dr Wu, akafanikiwa kumvuta na kumtoa kwenye hatari zaidi ya kuungua na Moto ule. Hata hivyo, ile amemchomoa tu, wakasukumiwa mbali na mlipuko mkubwa wa gari hilo. Mlipuko huo, haukuwa wa kawaida. Zaidi ya mlipuko wenyewe wa gari, ni kama kulikuwa na mlipuko wa ziada wa bomu. Bila shaka jamaa walikusudia kumteketeza kabisa Dr Wu.

Agent Li alipopata fahamu baada ya kupumbazwa kwa muda na mlipuko ule, aliubeba uliowahi kuwa mwili wa Dr Wu na kuelekea eneo lenye usalama. Wasamaria wema walikuwa wanasogea kujaribu kutoa usaidizi. Mmoja wa raia wale ambao walikuwa kwenye mgahawa wa jirani na ilikotokea ajali, akajitolea gari lake kuwawahisha jamaa hospitalini. Wakampeleka kwenye hospital ya wajapani, Ito Yokado. Mtaa jirani wa Qianmen E.

Walipofika hospitalini hapo, madaktari hawakuwa na kazi. Dr Wu Han, alikuwa ng'ambo ya pili kutokea duniani. Baada ya uchunguzi wa maiti yake, kulionekana tobo la risasi. Washenzi wale waliipenyeza risasi kwenye moyo wa Dr Wu bila huruma. Kwao haikutosha kumnyang'anya ile formula. Walikusudia kumpoteza akiwa shahidi pekee ambaye angeeleza nani walikusudia kumnyang'anya ile formula. Earth Vision 2050, hawakuwa na mashaka tena na mpango wao. Wanasayansi wenzie Dr Wu, tayari walikuwa wamesaini mkataba na kupokea marupurupu manono. Sasa, huko ng'ambo ya pili, kumfikia ilikuwa muhali, ajent Li hakuwa na kitu Cha ziada Cha kuwafahamu wale wazungu Ni nani. Dr Wu alikufa akimwachia kitendawili kigumu Cha kutegua. Alibaki akitafakari kauli ya Dr Wu kuwa "Zanzibar Kuna mapinduzi baada ya milipuko ya bomu". Ulikuwa mtihani mgumu kweli kweli. Hata hivyo Agent Li, alibaki kuwa na wajibu wa kutekeleza, kushughulikia maandalizi ya msiba na pia akalazimika kutoa taarifa kwa familia ya Dr Wu.

***

Habari kwamba Dr Wu alikufa akijaribu kutetea taifa lake, tena habari kwamba familia yake ilikuwa mateka, ziliamsha amsha-amsha hatari jijini Beijing. Wananchi na wanaharakati Jijini humo waliitaka serikali kuhakikisha familia ya Dr Wu inarejeshwa. Maandamano makubwa yakashuhudiwa, ya kuishinikiza serikali kuu kuhusiana na familia ya Dr Wu na kutaka majibu ya nani waliomuua Dr Wu, mtu ambaye siku za karibuni alikuwa amebainisha ugunduzi wake wa chanjo dhidi ya gonjwa la Corona. Wachina walikuwa bado hawajasahau virus hao hatari walivyopata kuteketeza maisha ya ndugu zao katika Jimbo la Guangdong mnamo mwaka 2002. Kirusi wa wakati huo alipewa jina SARS COVID 1. Wengi Sasa walihesabu kuwa mwarobaini wa virus hao umepatikana. Kwa vyovyote vile, kulikuwa na hujuma inaendelea.

Hamasa hiyo ya wananchi, ikizingatiwa pia kwamba Earth Vision 2050, walikuwa wameitia briefcase ya Dr Wu mkononi mwao, hawakuona haja ya kuendelea kuishikilia familia ya Dr Wu. Kesho baada ya siku hiyo ya maandamano, familia ya Dr Wu ikaachiwa huru na kutelekezwa kwenye eneo maarufu wanakoonekana watu wa mataifa mbalimbali, mtaa wa San Li Tun. Hata hivyo, walikutwa hapo wakiwa wamefungwa kwa kudu pamoja. Waliporudishwa nyumbani, familia ya Dr Wu hawakujua kuwa baba wa familia yao alikuwa tayari keshaenda zake ng'ambo ya pili. Hivyo, kufika Kwao nyumbani na kukuta msiba wa baba wa familia kukaibua vilio na maombolezo makubwa. Familia hiyo, ikakumbwa na kilio, baba wa familia hangeonekana Tena akiwa hai. Mtafiti na mgunduzi wa tiba kubwa na muhimu nchini China alikuwa kahujumiwa uhai wake na watu wa Earth Vision 2050.

Mkewe Dr Wu, alionekana kuwa na wasiwasi sana. Hawa waliomuua mume wake walikusudia nini? Akakumbuka mume wake alimdokezea juu ya chanjo aliyokuwa amevumbua na jinsi ambavyo ilitokea kuvutia makampuni mbalimbali ya utafiti. Kuanzia kampuni maarufu la mmarekani Steve Curl, Scientific Reality Inc, na Sasa kampuni lingine la kimarekani la Earth Vision 2050. Kampuni hili la pili Dr Wu alimweleza kuwa alikuwa na mashaka nalo, kwa sababu, alihisi kuwa kampuni hili lilikuwa na nia ovu dhidi ya chanjo hiyo. Alipomuuliza kwa nini, Dr Wu alikuwa kamwambia;

'Ni kama wamekusudia kuitia mikononi mwao kwa udi na uvumba. Wanatangaza dau ambalo, linatia tamaa, ili mtu asifikirie mara mbili kutafakari ofa yao', hivyo ndivyo alivyopata kumjibu. Halafu akakumbuka Tena usiku wa siku hiyo, wakiwa wamelala usiku wa manane, na labda yeye ndio alilala, maana Dr Wu hakuonekana kabisa kama alipata usingizi, Dr akamwamsha. Alipoamka, Dr Wu alimweleza maneno haya;

'Mke wangu, nataka ujue kuwa nawapenda sana. Nakupenda sana mpenzi na sipati picha ikiwa nitapata shida halafu niwe mbali na nyinyi…' Dr alikuwa anaongea kama anayewaza. Aliyatamka maneno hayo huku akili yake ikiwa mbali sana hakuwa hapo kimwili, hivyo ndivyo ungetafakari ongea yake usiku ule. Sheng, aliliona hilo lakini akadhania zitakuwa ni stress za kazini zinamsumbua mumewe.. Hapo ndipo Sheng, mkewe Dr Wu akamkatisha kauli na kumwambia.

'Mume wangu mpenzi, unawaza sana baba watoto. Hebu acha akili yako ipumzike mpenzi. Umechoka na bado unalazimisha kufikiria vitu. Ona sasa, unaanza kuwaza mambo ambayo huhitaji kuifikirisha sana akili yako juu yake. Mimi na wanao, tunakupenda sana mpenzi. Lisikufikirishe sana hilo. Lala mpenzi, njoo tulale.'

'Asante mke wangu, kulala tunalala. Kuna kitu nataka nikushirikishe maana asubuhi nitawahi sana kutoka. Pale sebuleni, ile kalenda yetu, kuna tarehe nimezizungushia kwa kalamu, hizo namba ni muhimu sana. Ikitokea nimepata shida kabla chanjo kuzalishwa, hizo tarehe zitakuwa ni funguo ya kuokoa watu. Nahisi wale watu wa Earth Vision 2050 wanakusudia kuangamiza watu wetu kwa aina mpya ya virus ambavyo chanjo yake nimetengeneza. Na ikitokea limenipata baya, Ukipata nafasi, kuna hiyo simu yangu, kuna wimbo nimerekodi, nimeupa jina 'mpenzi dunia' usikilize. Utakupa tafakuri ya liwazo.' Sheng sasa aliona Dr Wu anabwabwaja mno. Unafahamu mazoea ni mabaya sana. Wanawake kwa wanaume hutengeneza mazoea fulani ambayo, hupelekea upuuzaji wa masuala ya msingi kwa kule kuzoeana na wenzi wao. Hivyo ndivyo ilivyoonekana kwa Sheng, hakuyazingatia sana maneno ya mumewe wakati alipokuwa anayaongea. Sasa wakati huu msiba ulipomfika, ndio akakumbuka haya masimulizi ya mumewe usiku ule kabla ya ajali na kuuawa.

Kumbukumbu hiyo, ikamkurupua Sheng mkewe Dr Wu. Akanyanyuka haraka na kuingia ndani chumbani. Juu ya meza jirani na kitanda, akaiona ile simu ya Dr Wu. Kawaida, Dr Wu alikuwa na simu ya mkononi kwa masuala ya kazini na halafu kuna simu hii ambayo mara nyingi alikuwa anarekodi mambo ya kifamilia, haikuwa na laini, bali ilikuwa na memory card yenye ujazo mkubwa, na ndanimwe alijaza video za watoto, mke na yeye mwenyewe. Humo pia alirekodi nyimbo walizoimba wanawe, mkewe au yeye mwenyewe. Simu hii, kwake ilikuwa kama kirekoda cha matukio ya familia, kumbukumbu ya hatua za ukuaji wa wanawe kwa nyakati za furaha na huzuni za familia yake.

Sheng alipoichukua simu hiyo, alifungua bila shida, maana haikuhitaji nywila, ilikuwa huru kutumiwa na mwanafamilia yeyote yule. Akili yake ilitaka tu kupata hicho ambacho mume wake alikuwa amesema kingempa liwazo wakati huu wa majonzi. Ilikuwa kama Dr Wu alitabiri kifo chake. Aliperuzi kwenye audio clips, zilikuwepo nyingi mno, hakuwa na muda wa kuzisikiliza zote. Akaingia kwenye mraba wa kutafutia mafaili, hapo akaandika 'mpenzi dunia'. Ikajitokeza hiyo clip. Sheng akapachika earphones masikioni na kuicheza hiyo audio clip.

'Mambo mpenzi? Kama umekuja hapa kwenye hii clip, basi nitakuwa nimepatwa na jambo, navyokujua wewe, usingekuja hapa kama si kumbukumbu ya kile nilichokuambia. Nakujua sana mpenzi. Basi nikupe pole kwa wakati mgumu unaopitia sasa. Pole mpenzi. Wanangu pia wape pole kwa niaba yangu. Nimekuita hapa kwa sababu hata kama sipo hapo, bado tunaweza kufanya jambo kubwa na la msingi. Tunaweza hatimaye kuokoa kizazi chetu kisiangamizwe na maharamia kutoka nje ya taifa letu. Kunazo njama nimebaini. Taasisi yangu CRC imeingiliwa na mamluki. Wapo tayari kuuza nchi kwa faida zao binafsi. Na mimi sitaishi kuona hilo likitokea. Na nikifa, basi nitakuwa nimekufa mimi, na labda watu wengine pia wakafa endapo utachelewa sana kuupata huu ujumbe. Lakini kama utaupata, hakikisha unamwambia mume wa dada yako, agent Li. Zile namba za kalenda, ni funguo dhidi ya virus vinavyokusudiwa kuachiliwa ili viangamize robo tatu ya wakaazi wa dunia. Namba hizo, zinafungua briefcase ambayo ndani yake kuna formula ya uzalishaji chanjo dhidi ya virus hivyo. Mpenzi, kama nikifa, nakuomba uwe huru. Wewe ni mwanamke mrembo ambaye hastahili kuishi kama mjane. Usiniomboleze mno, maana kufa kwangu ni kupona wengi. Kusudi langu litakuwa limekamilishwa. Nakupenda mpenzi, nakupenda dunia, mpenzi dunia.' Sauti ya marehemu Dr Wu ikahitimisha ujumbe. Sauti ya mumewe hakika ilimtia simanzi, vipi angenyamaza? Sheng alikuwa analia mlango wa chumbani kwake ulipogongwa. Ilikuwa sauti ya dada yake, mke wa agent Li Wenqing. Ujio wa dadake ukamuongezea kilio maradufu.

***

Baada ya kuhakikisha kuwa briefcase yenye formula ipo mikononi mwao, na kwamba Dr Wu sasa hangekuwa kikwazo, watu wa Earth Vision 2050, walielekea kwenye ofisi zao za muda zilizokuwa eneo jirani kabisa na makao makuu ya MSS. Walilichagua eneo hilo, kwa sababu pamoja na mengine, walikuwa katika ujasusi dhidi ya idara hiyo muhimu kwa China, wakiwa wameweza kupenyeza mtu wao ndani ya idara hiyo. Ni kusema kwamba watu Hawa wa Earth Vision 2050 walikuwa wanaweza kupata taarifa muhimu kutoka ndani idara hiyo nyeti.

Kuipata briefcase, ilikuwa hatua muhimu katika harakati zao. Walikuwa na hakika kuwa sasa watafanikisha misheni yao.

Earth Vision 2050 kama lilivyo jina lao, lilikuwa kampuni miongoni mwa makampuni washirika na lile kampuni lingine la ENTRY. Hawa walikuwa na agenda ya Siri. Kampuni hili likiwa na agenda moja kubwa, kufikia 2050, duniani kuwe na idadi ya watu wasiozidi billion 1.5. Sawa na Entry, Earth Vision walikuwa na lengo moja tu. Kuiokoa dunia dhidi ya kile walichodai kuangamia na kupoteza kabisa jamii ya binadamu. Kwa kile walichosema, ni ongezeko kubwa kabisa la binadamu ambalo lingeifanya dunia isiwe salama tena kwa viumbe kuishi kwa utengamano. Walikadiria kuwa Kama ongezeko la watu lingeendelea kuachiliwa kuongezeka kihobela hobela, Basi Kama vile mijusi mikubwa ya zamani (Dinosaurs) ilivyotoweka, ndivyo ingetokea kwa binadamu, matokeo ambayo waliona yanatokea muda si mrefu. Mambo kadhaa yalikuwa Kwao Ni ishara iliyowataka wachukue tahadhari kuzuia kutoweka kwa kizazi Cha binadamu na viumbe wengine. Mioto iliyokuwa inajitokeza kwenye misitu mikubwa ya Amazon huko America, mingine huko Australia na kwingineko duniani, mioto iliyodumu na kushindwa kudhibitiwa na binadamu, kwao ilikuwa ni ishara. Ishara kwamba dunia inaelekea kubaya. Matokeo yake waliyahusianisha na wingi wa binadamu. Suluhu waliyoona, ni kupunguza idadi ya wanadamu duniani.

Katika hatua za awali, walihamasisha na kuanzisha program za uzazi wa mpango. Lakini walibaini kuwa program hizo hazikufua dafu hasa kwa mataifa yanayoendelea huko Africa, Asia na America ya kusini. Ni kweli kwamba kwa kutumia chanjo mbalimbali za magonjwa mbalimbali, walimudu kupunguza kasi ya uzaanaji wa binadamu. Lakini hata hivyo, idadi ya binadamu ilizidi kuongezeka kwa spidi kubwa. Earth Vision 2050 walikadiria kuwa dunia ingefikisha idadi ya watu takribani billion tisa hadi kumi kufikia mwaka 2050. Kwa idadi hiyo ya watu, Earth Vision 2050 waliona dunia ikiangamia. Uchafuzi wa hewa, maji na mazingira ungeichakaza dunia. Magonjwa ya milipuko yasingepata wa kuyasimamisha. Mvua za tindikali, magonjwa ya mfumo wa hewa, mioto kwenye misitu mikubwa inayotegemewa kuzalisha vyanzo vya maji laini, ukame, njaa, n.k. Hivyo ni vitu vilivyotarajiwa kujitokeza mapema hata kabla ya 2050. Earth Vision 2050, waliona wana sababu ya kufanya jambo. Waliona dunia inastahili kuwepo na wanadamu pia wanastahili kuwepo. Hata hivyo, ilihitaji kufanya jambo ambalo si kila mtu angeliafiki. Kuuawa watu ili kuponya watu. Wasingeeleweka, hivyo, wao na washirika wenzao, waliamua kuyafanya haya kimya kimya. Jamii yao ikawa ni jamii ya siri, ikiratibu mambo yao kwa siri.

China pekee ilikuwa na idadi kubwa kuliko idadi yote ambayo kwa makadirio yao, ilistahiki kuwa idadi ya wanadamu wote duniani. China ilikuwa na idadi isiyopungua watu billion moja na nusu, ikifuatiwa na India. Baada ya uzazi wa mpango kushindwa kudhibiti ongezeko la watu duniani, Earth Vision 2050 na washirika wao, wakaamua kutengeneza magonjwa kadha wa kadha lakini usambaaji wake na uangamizaji wake haukuwa kwa ufanisi waliotaka. Sasa walitengeneza kirusi ambacho uambukizaji wake ulikuwa rahisi zaidi. Kwa Vitone vya kohoo, mate, chafya na kamasi, kirusi hicho kingeenea haraka sana. Na kwa uhakika zaidi, kifo kutokana na kirusi hicho, hakisubiri muda mrefu sana hasa kilipompata mtu mwenye kinga hafifu ya mwili. Hatua ambayo walikwishairahisisha hapo awali. Chanjo za awali, zilizokwisha kutolewa zikilenga kukinga magonjwa kadha wa kadha, waliziwekea pia udhaifu. Kusambaratisha uimara wa kinga ya mwili, na kuna baadhi ya visa viliripotiwa vya baadhi ya chanjo kusababisha badiliko la kijenetiki na DNA kwa wahanga.

Kinga dhidi ya virus vipya walivyokuwa wameunda, sasa ilikuwa mkononi mwao. Earth Vision 2050 wakajua mpango wao mapema ungeingia kwenye hatua muhimu. Lakini Earth Vision 2050 wakiwa bado hawajafanya kitu, jimboni Wuhan, jimbo ambalo lipo katikati ya nchi ya China, ulitokea mlipuko wa gonjwa la Corona, safari hii virus hao wakapewa jina SARS Covid 2. Gonjwa ambalo Dr Wu na jopo lake walikuwa wamefanikisha kutengeneza chanjo dhidi yake. Chanjo ambayo, wanasayansi hao walianza kuitafuta kufuatia mlipuko wa awali wa Kirusi aina hiyo kilichopewa jina, SARS covid 1, kikiripotiwa kuibukia huko Guangdong mapema mwaka 2002. Chanzo chake kilisemekana kuwa ni nyoka au popo. Chanjo ya Dr Wu, ilisemekana kuwa ni chanjo ambayo pia ingetumika kama tiba. Chanjo hiyo sasa ikiwa mkononi mwao, Earth Vision 2050 walipata kiburi cha kuachia virus vya SARS covid 2. Lakini kabla ya kuviachia virus hao, mwishoni mwa mwaka 2019, Virus hao wakaenea haraka sana kutokea jimboni Wuhan. Earth Vision 2050, wakashangaa sana maana hawakuwa wahusika. Haikujulikana nani kakiachia kirus hicho kabla ya wao. Hatari yake ikawa bayana kwani wao pia hawakujiandaa kwa mlipuko wa gonjwa hilo. Hata hivyo, hawakuwa na hofu sana. Waliamini kuwa na formula ya ACVV ilikuwa kinga yao madhubuti.

Itaendelea ......

JamiiForums528126083.jpg
 
View attachment 1701741
Shusha vitu
 
32

Jopo la wanasayansi wa Earth Vision 2050 lilikaa kwenye meza yenye umbo la yai. Jumla yao watu kumi na mmoja. Katika meza hiyo, ilikuwepo ile briefcase ya Dkt Wu, briefcase iliyoaminiwa kubeba formula muhimu dhidi ya kirus cha SARS COVID 2. Watu hao walikuwa wanamngojea Dkt Futodo, Mkurugenzi wa CRC, kwa ajili ya kuifungua briefcase hiyo. Namba za siri za briefcase hiyo iliyohifadhi formula ya ACVV, ilikuwa kwa watu wawili pekee. Dkt Wu ambaye sasa alikuwa hayupo tena duniani na Dkt Futodo ambaye alikuwa bado angali hai.

Dakika mbili mbele, Dkt Futodo akaingia kwenye ofisi hiyo mbele ya meza iliyozungukwa na watu wa Earth Vision 2050. Watu wa Earth Vision 2050, wakafurahi sana kumuona, wakamkaribisha kwa bashasha, walijua ingekuwa rahisi tu. Wao, walikwisharatibu kitakachofanyika. Ndiyo. Baada ya Dkt Futodo kufungua briefcase ile, walipanga kumuangamiza kwa risasi. Hivyo, ilikusudiwa kwamba akishaifungua brief case tu, angekula shaba, na zile fedha nyingi walizomwekea kwenye akaunti, walikuwa na mpango mwingine wa kuzirejesha mikononi mwao. Tayari walikwishadukua taarifa zake za kibenk, na tayari walikwishaandaa clone (inahusika na sayansi ya kutengeneza mfanano halisi wa kiumbe kwa kutumia DNA ya kiumbe huyo) yake kwa ajili ya kuzichomoa zote kutoka benki huko nchini uswizi. Baada ya kumuua Dkt Futodo kwa shaba, mwili wake ungeteketezwa kwenye tindikali na kumiminwa kwenye mfumo wa maji taka. Na wale wengine, wale madaktari walafi na wabinafsi, ambao walikuwa tayari kuweka maslahi yao binafsi dhidi ya maslahi mapana ya kuwaokoa binadamu wengi waliotegemea tiba na chanjo hiyo, mpango ungekuwa kama huo, isipokuwa tu, wao wangeitwa kwenye kikao, ambacho katika chumba cha mkutano, humo kungeachiliwa gesi ya sumu, na kwa njia hiyo wangekutana na vifo vyao huku fedha kwenye akaunti zao zikirejeshwa tena mikononi mwa Earth Vision 2050 kwa mtindo ule ule.

Kwa hiyo, Dkt Futodo alipoingia akiwa na bashasha kubwa usoni mwake, hakujua tu, alikuwa anaingia kwenye mikono ya kifo pasi na taarifa. Fikrani mwao watu wa Earth Vision 2050, waliona kitu kama uji-uji mwekundu ukitiririka katika mfumo wa majitaka hapo baadaye akishakuwapatia kitu muhimu walichokikusudia kukipata. Nywila ya kufungulia briefcase ile. Dkt Futodo aliitazama briefcase ya Dkt Wu, tabasamu likachanua mdomoni mwake. Hii ilikuwa na maana kuwa, malipo ya mwisho kwa mujibu wa makubaliano yake na watu hawa, yangeingia kwenye akaunti yake na kumfanya tajiri mmoja mkubwa nchini mwake. Kiongozi wa kundi hili la Earth Vision 2050 aliyeongoza jopo la watafutaji wa chanjo hii, aliyejulikana kama Professor Tahari, myahudi kutoka Israel, akimiliki uraia wa Marekani, akamkaribisha na kumwambia afungue briefcase. Dkt Futodo hakuwa mjinga kama walivyomdhania, hivyo ndivyo alivyowaza alipowaambia;

'Nikamilishieni muamala wangu kwanza.' maneno hayo, Dkt Futodo aliyatamka kwa kujiamini. Zaidi yake, alijua, hapakuwepo mwingine wa kuifungua briefcase ile. Alikuwa na kila sababu ya kuweka madai yake mezani na uhakika wa kutekelezewa.

Professor Tahari akiwa hataki kumpeperusha ndege wake, akakubaliana naye. Akamwonesha ishara kijana mmoja katika kundi lao. Ishara iliyomtaka kijana huyo kutekeleza takwa la Dkt Futodo. Komputa mpakato ikaletwa na kuwekwa mbele yao. Kijana yule, akaikamata 'mouse' na kuanza taratibu za kukamilisha muamala. Muamala ukafanyika mbele ya macho ya Dkt Futodo. Kwa muda wote huo, Dkt Futodo alikuwa anayawaza maisha ya kifahari atakayoishi siku za usoni.

Akaivuta briefcase ya Dkt Wu na kubonyeza namba kadhaa za siri, lakini kama vile alishituka jambo, kabla Dkt Futodo hajakamilisha namba mbili za mwisho, akili ya ziada ikamwingia kichwani. Aliyatazama macho ya watu wale, yalikuwa yanamtazama kwa matarajio makubwa, aliona hila ndani ya macho yao. Akajiuliza swali la muhimu, 'nikishakamilisha kazi yao, nitakuwa na faida gani kwao? Kama wamemuua Dkt Wu, kichwa kilichogundua chanjo, mimi ambaye sijui abc za chanjo hii wataniacha salama?' Akasita. Macho yao wote yalikuwa kwake. Yalikuwa yakimwangalia kwa makini sana. Sana hasa professor Tahari, ambaye zaidi ya umakini, alimtazama Dkt Futodo kama fisi mwenye uchu, anayesubiri windo la mzoga wake kwa hamu.

'Vipi? Mbona unasitasita?' Professor Tahari akauliza kwa taharuki. Alihisi analipoteza windo lake kama akizembea.

'Napataje uhakika kuwa nitatoka hapa mzima nikishakamilisha kazi yenu?' Dkt Futodo alimtupia swali Dkt Tahari.

'Hatuaminiani? Tumemaliza kukutumia fedha zako hapa, sivyo?' Tahari alihoji akionesha kukasirishwa kwa kiwango cha juu.

'Ndio, lakini hiyo hainihakikishii kutoka hapa salama' Futodo hakutaka kukubali kuchezeshwa shere kwenye uwanja wa nyumbani.

'Kwa hiyo unatakaje Dkt Futodo?' Profesa Tahari akauliza kwa mkazo.

'Nataka niwe eneo ambako usalama wangu utakuwa hakika. Niondoke na mmoja wenu, nikiwa kweupe, atarudi na namba za siri mfungue wenyewe.'

Wazungu wale wakatazamana, halafu wakakubaliana na wazo lake.

'Ondoka na huyo, akifika huko atatupigia simu, tukishafungua briefcase ndio ataachana na wewe. Usijaribu ujanja wowote Dkt, hili ni suala muhimu na nyeti sana kwetu. Usione pesa hizo ukadhani zinatolewa kama msaada.' Professor Tahari akamweleza kinagaubaga. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Mtu yule aliyepewa kufuatana naye, angekuwa chanzo cha taarifa na udhibiti kama mambo yasingeenda sawa.

Umbali wa kukadiria kama kilometa mbili hivi kutoka kwenye chumba kile cha mkutano, yaani ofisi ile ya watu earth Vision 2050, Dkt Futodo aliona panatosha kwa usalama wake, akamweleza namba za siri kijana yule. Kijana akawapigia wenzake na kuwajulisha namba husika. Hawakuchelewa, wakaziweka namba zile bila kusita. Kitu cha ajabu kikatokea. Walipomalizia tarakimu ya mwisho ya nywila, ghafla tu, ulisikika mvumo wa sauti mfano wa ngurumo. Chumba walichokuwa wazungu wa Earth Vision 2050, kikafuka Moshi na ndimi za moto zikawa zinapambana kuchomoza kwenye wingu la moshi uliotanda eneo lile. Bomu lililipuka na kuteketeza timu nzima ya Professor Tahari na yeye mwenyewe akiwa miongoni mwa wafu hao. Alisalia mmoja tu. Yule aliyekuwa na Dkt Futodo. Dkt Futodo aliweza kushuhudia kile kilichotokea, akajua hatari gani inayomkabili. Wakati yule kijana mlinzi wake akihamaki, Dkt Futodo akili ikamtuma kufanya jambo, akanyanyua mguu akamtwika guu la kiuno, yule kijana akaenda chini mzima mzima, anapokuja kunyanyuka, Dkt Futodo alikuwa keshaingia mitini, alitimka mbio hizo, mfukuza upepo mahiri Usain Bolt angeambulia kuvuta vumbi alilolitimua, lakini asingemkaribia asilani. Ulikuwa mwendo wa farasi.

Dkt Wu bila shaka hakuwa mjinga apoteze maisha yake halafu, eti formula yake adhimu iangukie mikononi mwa watu hatari! Hakuruhusu hilo kutokea.

Baada ya mbio za kufa na kupona, Dkt Futodo alipokatiza mtaa wa pili tu, akachukua teksi na kwenda nyumbani kwake. Kulikuwa na kila dalili ya maisha yake kukabili hatari. Alikuwa sasa anawaza afike nyumbani achukue passport yake ya usafiri ili aondoke Beijing na ikiwezekana ajifiche kwa muda nchini Japan. Hakukuwa mbali, dakika ishirini na tano hivi, Dkt Futodo alikuwa anaingia nyumbani kwake. Haraka sana, akafungua mlango wa sebuleni kwa pupa. Ile tu anaingia sebuleni akakutana na wanaume wa kazi. Ilikuwa ghafla mno. Alijikuta anasimama hajui afanye nini. Mbele yake walikuwa wameketi wanaume wa ngozi nyeupe kwa raha kabisa wanafuatilia kipindi kwenye runinga yake. 'Ah, dadeki. Nani akamatwe kizembe?' Dkt Futodo akawaza huku akigeuka arejee nje. Ile tu anataka kugeuka, akajigonga kichwa kifuani mwa kamanda mwingine ambaye hakumdhania angekuwepo hapo. Mtu huyo alikuwa jitu lenye mwili ulioenda hewani. Limejaa misuli mkononi mithili ya mbeba vyuma. Dkt Futodo akajikuta tayari amekwama. Ilikuwa bahati kuwa, familia yake ilikuwa likizo huko jijini Shanghai. Dkt Futodo akatiwa nguvuni mwa wanaume wale na kuingizwa kwenye gari kubwa SUV na gari hilo likaondoka kuelekea airport. Beijing.

Hawakukawia kuondoka airport, waliondoka na ndege ya kukodi. Nusu saa baadaye ndio Dr Futodo akabaini alikua ameangukia kwenye mikono ya majasusi wa Urusi. Lugha yao, ikawa imehusika kumjulisha hilo kwa sababu aliifahamu kwa kiasi kidogo.

***

Kwingineko huko jijini Wuhan.

Mgonjwa mmoja mwanaume aliingia kwenye hospital kubwa jijini Wuhan akiwa kwenye machela ya kubebea wagonjwa mahututi. Alikuwa ameletwa na ambulance kwenye Hospital hiyo inayojulikana kama Huoshenshan Hospital. Mgonjwa alikuwa analalamika kikohozi na homa kali iliyoambatana na maumivu ya kichwa. Kifua kilibana na kumfanya apumue kwa shida sana. Alikuwa na kila dalili za ugonjwa mpya wa SARS Covid 2. Shida ikawa kwamba, ugonjwa huo ulikuwa mpya, lakini kwa vile kulikuwa na historia ya mlipuko wa ugonjwa aina hiyo SARS Covid 1 huko Guangdong mwaka 2002. Basi, tahadhari zilichukuliwa. Mgonjwa akawekwa karantini. Kesho yake, mke wa mwanaume huyo naye akaonesha dalili za ugonjwa ule. Mwanaume akafa jioni ya siku ya pili baada ya kulazwa hapo hospitalini. Mwanamke hakupata lau nafasi ya kumuaga mumewe, akawekwa karantini.

Kesho yake hospital ikapokea wagonjwa watano wenye dalili zile zile. Kutanabahi, wiki moja baadaye, hospitali ilijaa wagongwa wa virusi vya SARS Covid 2. Mganga mkuu akawasiliana na serikali na kuwaeleza kuwa ugonjwa huo ni tauni mpya. Tahadhari kubwa ilipaswa kuchukuliwa. Shida ikawa siasa. Watu wa serikali hawakutaka kuweka taharuki kwa wananchi kwa kutoa matangazo ya tahadhari. Walikusudia kulikabili jambo hilo kimya kimya. Hata hivyo, isingewezekana katika ulimwengu wa leo wa mitandao ya kijamii. Hofu ikaenezwa haraka sana kupitia mitandaoni. Watu wakaanza kufa mithili ya kuku wenye kideri. Kila leo watu walikufa japokuwa wapo waliopona.

Habari za vifo hivyo zikamfikia agent Li akiwa jijini Beijing. Akasononeka sana. Tayari watu wapatao mia tano walisemekana kufa huko Wuhan, na katika kudhibiti hali ya mambo, jiji hilo likawekwa kwenye 'lockdown'. Hakuna kuingia jijini humo wala kutoka. Wananchi wakashauriwa kusalia majumbani mwao. Taratibu za kiafya zikatakiwa kuzingatiwa. Kunawa mikono kwa sabuni mara kwa mara, kuacha kujishikashika usoni. Salam za kushikana mikono zikapigwa marufuku, misongamano haikutakiwa hivyo wananchi wakalazimika kusalia majumbani, shule zikafungwa kwa kipindi kisicho na ukomo hadi hali itakapotengamaa. Ilikuwa vita ya aina yake. Vita iliyopiganwa kwa sabuni, sanitizer na kujifungia ndani badala ya kuingia uwanja wa vita kwa bunduki, vifaru na zana nyinginezo za kivita. Askari wakiwa ni madaktari na wanasayansi.

Roho ikamuuma sana ajent Li kujua chanjo na tiba ya gonjwa hilo ilikuwa imepatikana lakini watu dhalimu wakawa wametokomea nayo huku wakiachia virus vya SARS Covid 2 kwa makusudi kabisa. Akakumbuka mazungumzo aliyofanya na shemeji yake Sheng. Akakumbuka na ile clip ambayo Dkt Wu alimrekodia mkewe. Akajiuliza, kama Dkt Wu alijua Dkt Futodo ana nywila za briefcase, alikuwa na haja gani ya kumweleza mkewe, tena akijua Dkt Futodo ni msaliti? Kuna kitu kilikuwa hakileti maana hapa. Dkt Wu hakuwa amesahau. Utafiti uliochukua muda mrefu, tangu mlipuko wa SARS COVID 1 mwaka 2002 huko Guangdong, vipi ulikuwa umeingia mikononi mwa maadui kirahisi hivyo. Utafiti uliozingatia hatua zote nne za kisayansi? Kuanzia kujaribishwa kwa wanyama, hadi kujaribishwa kwa binadamu na kuchapishwa kwenye majarida ya kisayansi kuonesha ufanisi wake. Vipi Dkt Wu angeruhusu hilo kutokea? Ajenti Li aliendelea kutafakari.

Dkt Wu hakuwa na imani na taasisi yake. Lazima kuna jambo ambalo lilimpa uhakika kwamba taarifa anayoacha kwa mkewe ingekuwa na manufaa. Lakini tena ajenti Li alipowaza kwamba Dkt Wu alipompigia simu alikuwa na nia ya kumpatia ile briefcase, halafu akakumbuka jamaa walimuwahi na kutokomea nayo kusikojulikana, akajua basi, mambo yatakuwa hayakuenda kama Dkt Wu alivyoyapangilia. Mpango wa Dkt Wu haukuwa alivyokuwa ameupanga. Agent Li akajilaumu sana kwa kutomfikia Dkt Wu mapema.

Akiwa anayawaza hayo, agent Li akapokea simu ya mkewe marehemu.

'Naam shemeji' Li akaipokea simu.

'Shemeji tafadhali njoo nyumbani. Tafadhali sana wahi.' Sauti ya Sheng ilikuwa ya hamaniko.

'Kuna nini shemeji'? Nini mbaya mke wangu.' Hivyo ndivyo ambavyo Dkt Wu na agent Li walivyotaniana na mashemeji zao. Ndio maana Dkt Wu alipowasiliana na agent Li katika zile harakati za kukimbizana na watu wa Earth Vision 2050, alitamka neno mkeo, alikuwa anamaanisha mke wake, yaani mkewe mwenyewe Dkt Wu.

'Ni muhimu ukiwahi hapa mume' Sheng alimwambia agent Li.

Agent Li hakutaka kupoteza muda. Aliingia kwenye gari lake akaikamata barabara, mbio, kwenda nyumbani kwa Dkt Wu. Alipofika nyumbani, alimkuta Shemeji na watoto wakiwa sebuleni.

'Oh afadhali umekuja shemeji. Wakati naisikiliza audio clip ya mume wangu, nikakutana na hili faili limeandikwa Zanzibar. Vitu ambavyo ameongea kwa kweli sijavielewa vizuri lakini ninahisi vinahusiana na mambo ya briefcase.'

Agent Li akakumbuka kauli ya Marehemu Dr Wu alipokuwa anaongea naye kabla ya ajali;

'Ongea na mkeo, mtaa wa Zanzibar kuna mapinduzi baada ya milipuko ya bomu, mkeo atakupa funguo.' Dkt Wu alitoa kauli hiyo. Na sasa anasikia tena habari za Zanzibar kwa shemejie hapa zikihusishwa na briefcase. Agent akajipata anapata hamu ya kutaka kujua Dkt Wu alikuwa na siri gani. Wiki ya tatu toka kifo chake, takribani watu 1120 walikuwa wamepoteza uhai kwa ugonjwa ambao tiba yake ilikuwa imegundulika.

'Hebu niisikie shemeji.' Agent Li akaipokea simu na kusikiliza ujumbe huo. Ilikuwa lugha ya mafumbo.

'Walipodhani Zanzibar ni nchi kumbe ni sehemu ndani ya nchi na ajabu inayo serikali yake, na ndiyo, ni kweli ilikuwa ni nchi. Ikiwa na raisi na baraza la mawaziri, lakini ni sehemu ndani ya nchi. Tanzania. Sebuleni ndipo kulipokuwa na nywila ya kuingilia chumbani. Mlipuko ukawapata walipoitumia nywila ya stoo, mlipuko uliwameza. Mlango wa stoo hauna tofauti na wa chumbani, waliona wakadhani ndiyo, kumbe siyo, milango iliundwa na mtu mmoja. Mkeo anazo nywila, sebuleni kaziweka. Zipo wazi, tarehe zimezungushwa kwa wino wa blue. Mkoba wa zana, upo salama. Nenda kisiwani Zanzibar, si bara. Mgahawa wa Zanzibar'

Baada ya kuisikiliza hiyo sauti ya marehemu, agent Li sasa akaanza kuchanganua maana fiche kwenye maneno hayo. Ilimchukua karibu siku nzima kuweza kugundua maana ya maneno ya marehemu Dkt Wu. Ugunduzi wake ukitokana na habari ambayo aliikumbuka. Mlipuko ambao uliua raia wa kigeni takribani 10. Mlipuko huo ulisemekana kusababishwa na mlipuko wa bomu lililokuwa limetegwa ndani ya mkoba wa mmoja wa wajumbe wa kikao hicho. Hiyo ilikuwa taarifa ya polisi. Alipozidi kuchimba undani wa taarifa hiyo, akabaini kuwa bomu lilikuwa ndani ya briefcase. Hapo ndipo kulipompambazukia agent Li. Kumbe Dkt Wu alikuwa anaongelea briefcase, milango iliyoundwa na mtu mmoja ilikuwa na maana kwamba, kulikuwa na briefcase mbili zenye ufanano. Nywila walizotumia kwenye mlango wa stoo wakidhani ni chumbani ulipelekea mlipuko kuwameza. Jamaa waliokufa kwa mlipuko, walikuwa ni ma-agent wa Earth Vision 2050. Agent Li alizidi kufumbua fumbo.

'Shemeji, Zanzibar ni wapi kwani? Namaanisha mgahawa wa Zanzibar!'

'Ni mgahawa upo mtaa wa San Li Tun, mara nyingi akiwa na muda, hutupeleka hapo kwa ajili ya chakula cha jioni.!' Sheng alijibu, halafu akakumbuka mumewe hakuwa hai tena, akaongezea

'Alipokuwa hai.' Sheng akatamka chozi likimdondoka. Ingemchukua muda kuweza kukubali kuwa Dkt Wu hakuwapo tena duniani.

'Naomba nipeleke huko tafadhali.' agent Li akamweleza Sheng. Sheng hakuwa na pingamizi, wakaingia kwenye gari kuelekea San Li Tun. Huu ni mtaa ambao ulikuwa maarufu kwa maduka, migahawa na bar zilizomilikiwa na au kuhudhuriwa zaidi na raia wa kigeni. Katika mtaa huo, kulikuwa na mgahawa uliokuwa unaitwa Zanzibar Restaurant. Ni mgahawa ambao Dkt Wu alipendelea sana kupata chakula hapo. Uendaji wa mara kwa mara kwenye mgahawa huo, kulimfanya Dkt Wu ajenge mahusiano ya karibu sana na mmiliki wa mgahawa huo, mtanzania aliyeitwa Massawe.

Massawe na Dkt Wu, walikuwa wanafahamiana tangu miaka ya nyuma sana. Mwaka 2002, akiwa Daktari kijana bado, walikuwa na safari ya kiutafiti huko Tanzania. Walifikia kwenye Hostel za Jeshi la Wokovu, Mgulani jijini Dar es salaam wilayani Temeke. Huko, Massawe alikuwa ni mfanyakazi katika Hosteli hiyo. Miaka kumi mbele, Massawe akafunga safari ya China, akamjulisha Dkt Wu kuwa alikuwa yupo China. Na alikuwa kaanzisha mgahawa hapo San Li Tun. Alipomuuliza ilikuwaje, akasema waligawiwa urithi na yeye akaona huo ndio mtaji alikuwa anataka. Yeye alikuwa kaachiwa urithi eneo kubwa pale Moshi mjini. Ambalo aliamua kumuuzia mfanyabishara mkubwa kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda. Akachukua mamilioni yake na kuishia hapo China. Urafiki wao ukazidi kushamiri hata wakawa kama ndugu wa damu kwa jinsi walivyoshibana.

Ajent Li na shemejie Sheng walipoingia tu mgahawani, Massawe alimuona Sheng, akanyanyuka na kumfuata.

'Pole sana shemeji. Nilisikia habari, nimekuwa nikikusubiri kwa wiki zote hizi. Dr Wu alikuwa mtu mwema. Karibu kiti tafadhali.' Massawe aliwakaribisha ndani ya ofisi yake ndogo mle mgawahani.

'Asante sana Shemeji.'

'Inasikitisha sana. Ni kama alijua kifo kinamfuata.' Massawe aliongea.

'Kwa nini wasema hivyo Massawe?' Massawe akataka kuongea akasita.

'Na huyu ni nani shemeji'?' Massawe akauliza akiwa anamaanisha agent Li. Bila shaka alipata mashaka. Hakupaswa kuweka siri za watu hadharani kwa watu wasiohusika.

'Oh pole bwana Massawe, nimekosa uungwana kutojitambulisha kwako. Naitwa Li Wenqing, nimemuoa dada yake Sheng.' agent Li akamweleza Massawe.

'Usiwe na shaka shemeji, alikuwa pia rafiki mkubwa wa marehemu.'

'Naam, alishawahi kutaja jina hilo wakati fulani. Basi hamna shaka. Nimesema alijitabiria kifo kwa sababu aliponiachia mzigo ambao wewe umeufuata, alinieleza kuwa nitatakiwa nikukabidhi kama nitasikia amekufa.' Masawe aliwaeleza Sheng na agent Li. Halafu akawataka radhi, akaingia kwenye kastoo ndani ya ofisi hiyo akatoka na briefcase. Ilikuwa ni briefcase ambayo ilifanana vilivyo na ile ambayo Dkt Wu alikuwa nayo wakati wa zile harakati za barabarani na watu wa Earth Vision 2050. Sheng na agent Li wakashikwa na butwaa, Massawe aliporejea akiwa na hiyo briefcase. Walikuwa wamefanikiwa kufumbua kitendawili. Hakika tabasamu lilitanda nyuso zao walipobaini sasa SARS Covid 2 ingepata mwarobaini wake.

Itaendelea..
 
KAZI YA MZUNGU 33

Ndege ya kukodi waliyotumia majasusi wa Urusi, ilitua nchini Korea kaskazini jijini Pyongyang. Baada ya kutoka hapo, walichukuliwa na gari na kuelekea nje kidogo ya jiji hilo. Huko walifikia kwenye jengo kubwa la kisasa ambalo Dkt Futodo alibaini ni maabara ya kisayansi ya aina yake. Hapa kulikuwa maabara ya kisasa zaidi kuwahi kuiona. Dkt Futodo akakiri kuwa wakorea hawa walikuwa wamejiwekeza kweli kweli. Waliingia kwenye ofisi ya mkurugenzi wa taasisi hiyo.

'Karibu sana Dkt Futodo. Nimekuwa mwenye bahati sana kuonana nawe mkuu. Sifa za taasisi yako zimekuwa kubwa sana siku za karibuni na mimi ninadhani ni kwa sababu wewe ndiyo kichwa cha taasisi hiyo ya China Research Center (CRC). Tumegundua tunakuhitaji ili taasisi yetu pia ipate kuwika kwenye uga wa kimataifa. Naitwa Mikhail Vahdeem.' Lilikuwa jina la watu wa Urusi.

Dkt Futodo alibaki kimya hajui nini cha kujibu. Hiyo ikampa nafasi Dkt Mikhail aendelee kutamba kwenye uwanja wa nyumbani.

'Kama unavyojua, kirusi cha SARS covid 2 kimeshalipuka huko Wuhan na unajua vile kinavyosambaa kwa haraka. Haraka sana utasikia mataifa jirani yameanza kutangaza kesi za ugonjwa huo, maambukizi mapya, vifo vipya vitaripotiwa. Haja yetu ni kuwa taifa ambalo litakuja na suluhu ya tatizo hilo. Kwa sasa hao wanaojiita wakubwa wa uchumi waache washikane mashati kwanza. Sasa hivi tunavyoongea, serikali ya China inalaumu Marekani kuwa imetumia kirusi hicho ili kudhoofisha shughuli zake za kiuchumi. Marekani inashangaa kwa tuhuma hizo maana haihusiki, tunahusika sisi. Muda si muda kirusi kitaingia Marekani, hapo ndio wamarekani wataanza vilio. Wataigeukia serikali yao na kuilaumu. Wengi wataamini serikali yao ilitengeneza kirusi na sasa China imekiboresha na kukirejesha Marekani kikiwa hatari maradufu. Na hiyo ni kwa sababu watu wengi watakufa sana Marekani hata kuliko China.'

'Hapa tunaongelea serikali gani hasa Dkt Mikhail, naamini hapa tuko Pyongyang, Korea kaskazini. Napokusikiliza, napokuangalia sioni Korea. Wewe ni mrusi kwa kila hali, niweke wazi, ili nijue tunaongelea upande gani hapa.' Dr Futodo aliongea akionesha uso wa dhihaka.

'Angalia sana mdomo wako usijekuponza. Huwezi kunifananisha mimi na hawa panya. Urussi ni taifa kubwa sana.' Mikhail Vahdeem alizungumza kwa tambo akionyesha jinsi alivyo mnazi wa taifa lake.

'Mnanitakia nini mimi?' Dkt Futodo akauliza kwa mshangao, labda alishangazwa na taifa kubwa kumuhitaji yeye ambaye mbari yake hakutofautiana sana na ile ya wakorea ambao huyu bwana mkubwa aliwaona panya bila haya, tena akiwa ndani ya himaya yao. Kiburi cha binadamu huyu kilizidi majivuno ya kinyonga na rangize, pamoja na mwendoe wa kunyata.

'Tunakuhitaji kwa sababu tunahitaji formula ya chanjo na tiba ya SARS covid 2.'

‘Na mmeambiwa mimi ninayo?'

‘Tunafahamu wewe ni mkuu wa taasisi husika. Lazima unazo taarifa hizo.'

‘Huenda aliyewapa taarifa hizo si mweledi wa kutosha. Mimi ni mkuu wa taasisi, lakini si mvumbuzi wa hiyo tiba. Kwa taarifa yenu ni kwamba hadi hivi tunapozungumza, mgunduzi wa tiba hiyo ameuwawa, na mnajua kwa nini? Kwa sababu alikataa kuitoa hiyo formula.' Dkt Futodo alijua hawa ni washenzi, lakini kiburi chao kisingewapa nafasi ya kumwacha hai. Alikuwa sasa anaongea kama mtu aliyehiari umauti. Alionesha kiburi kama alichoonesha Dkt Mikhail.

'Sikiliza wewe mjinga, unadhani ni nani unayezungumza naye? Toa majibu yatakayokuweka hai, unaweza kufa muda wowot……'

'Unisikilize wewe, mimi siogopi kufa, wewe na watu wako ni watu duni sana kiintelijensia, mnafanya mambo yenu kizamani mno. Bado mnadhani ukubwa wa mwili ni jambo la kujisifia. Mimi hiyo formula sina na navyoongea nanyi, formula ipo mikononi mwa Earth Vision 2050. Wale wamarekani wako vizuri sana kuwazidi ninyi na ubabe wenu.' Futodo alijibu kwa nyodo, japo alijua na alikuwa na uhakika kwamba fomula ile ilikuwa imepotea pamoja na wazungu wale katika ule mlipuko wa Beijing.

'Huo ubabe wetu ndio utatuwezesha kupata taarifa tunazotaka kutoka kwenu…..' Dkt Mikhail Alikuwa anazungumza simu yake ya mkononi ilipoita.

'Naam!' Dkt Mikhail alipokea simu kwa sauti yake nzito, sauti ya zege.

‘Ni mimi Yaraslav, nimekutumia ripoti kamili kwa njia ya email.' Yaraslav Yvanovitch alizungumza kwenye simu.

'Nimeshakuambia mara ngapi usitume ripoti kwa njia hiyo. Umesahau hawa nguruwe wa Marekani wanaweza kudukua mawasiliano yetu?'

'Sio rahisi kama ambavyo wanaweza kudukua mawasiliano ya simu ukiwa unawaeleza habari hizi!' Yaraslav Yvanovitch aliongea akionesha kukerwa na hulka ya Mikhail. Ni dhahiri Mikhail alikuwa na mtizamo (attitude) wa hovyo sana, alikuwa anapungukiwa kwa sehemu kubwa maarifa ya kimawasiliano.

Alipomaliza kuzungumza na jasusi Yaraslav Yvanovitch, Mikhail akakata simu na kumuita mmoja kati ya walinzi amuondoe Dkt Futodo mle ofisini.

'Mpelekeni shimo la Lev huyo hadi aeleze hiyo formula iko wapi.' Mikhail Vahdeem alitoa agizo.

Yaraslav Yvanovitch alikuwa ameandika ripoti yake vizuri kabisa. Jasusi Mikhail aliisoma kisha akatikisa kichwa. Akasimama na kuelekea kule walikokuwa watu wake na Dkt Futodo, shimo la Lev. Chumba cha mateso. Alimkuta Dkt Futodo akiwa keshachakazwa vya kutosha.

'Mwacheni. Bahati mbaya sana kumbe alikuwa anasema ukweli. Watu wa Earth Vision 2050, ni wamoja na watu wa ENTRY ambao Agent Yaraslav Yvanovitch amekuwa akipeleleza. Kwa maana hiyo, huyu wala hana faida kwetu tena. Atapelekwa shambani akawe msosi wa Lev. (Lev kwa ki-Russia ina maana ya Simba.) Kwa sasa tunatakiwa kwenda Oman, baadhi yetu, na baadhi yetu tutaenda Zanzibar. Huko yupo kiongozi wa ENTRY, anaitwa Halfani Nassor aka mzee Kisiki. Tunatakiwa kumteka na kupata taarifa za ilipo formula haraka kabla hawajaanza kuitumia kuzalishwa tiba ya SARS covid 2.' Jasusi Mikhail Vahdeem aliwaeleza wenzake.

Wanasema kuna watu katili? Mikhail Vahdeem, huyu alikuwa ni zaidi ya katili. Alitengenezewa ukatili akingali kinda. Akiwa mdogo, alikulia kwa mama wa kambo ambaye hakuisha kumnyanyasa leo hata leo. Alipofika umri wa miaka kumi na nane, akajiunga na jeshi, idara ya ujasusi ya nchi yake maarufu kama FSB. Katika moja ya misheni alizotumwa, alikamatwa na majasusi wa kimarekani. Mateso aliyopata katika mikono ya watu hao, yakapelekea bwana huyu kupoteza nguvu za kiume akiwa kijana mdogo wa miaka 26 tu. Msiba ulioje? Akajaribu kujiua mara kadhaa kwani alipatwa na sonona iliyompa fadhaa kubwa. Majaribio matatu na bado akajipata yu hai. Tangu hapo, Mikhail alijiumba upya. Akazaliwa katili Mikhail Vahdeem.

Dkt Futodo aliingizwa kwenye gari kuu kuu na safari ya kuelekea shamba ikaanza. Lilikuwa sio shamba kihalisia. Ilikuwa ni jengo kama stoo, ambalo lilikuwa nje ya jiji kama maili hamsini hivi kutokea pembezoni mwa jiji la Pyongyang. Huko, Jasusi Mikhail alifuga simba dume na majike wawili. Walitengeneza eneo hilo maalumu kabisa kwa ajili ya kupoteza watu ambao kwao hawakuwa na umuhimu tena. Hasa maadui wa Russia wakitupwa humo, au tuseme adui wa Mikhail? Maana ukatili wake, ulikuwa katika ngazi ya binafsi, ni kama alitaka kuonesha nguvu zake za kiume kwa njia hii baada ya kuzipoteza kihalisia.

Dkt Futodo alitupiwa mle akiwa uchi wa mnyama, huku akilia kilio kikuu cha majuto na simba wale wakamfanya kitoweo bila kujali kelele zake. Habari yake ikaishia hapo. Safari ya Oman na Zanzibar ikawiva kwa majasusi hawa wa Urusi waliojichimbia nchini Korea Kaskazini.

***

Hasira alizokuwa nazo mzee Kisiki, haki ya nani angemtia M'bara mkononi, wallahi angemmeza kama afanyavyo joka aina ya chatu anapopata kitoweo chake. Kwake ilikuwa kafanyiwa dharau kubwa sana na kijana huyo. Alipokumbuka kwamba hata hakupata nafasi ya kumgusa binti yule, Kisiki alihisi maumivu kama ya mtu aliyekutana na dhahama ya kuhasiwa. Aliwasambaza watu wake kisiwani humo ili kumtafuta Mwamvita na huyo kijana jeuri Masu.

Ilikuwa bahati njema kwamba Masu alimficha Mwamvita huko bara na sasa yeye mwenyewe alikuwa ni mtu wa masafa. Hivi ni kusema Kisiki na watu wake walipokuwa wanamsaka, Masu alikuwa safarini huko Singapore. Walikuwa wanagawa chanjo ya ule mpango wa tajiri Steve uliojulikana kama 'mama na mtoto' na ile chanjo maalumu kwa wanafunzi. Kazi yake pamoja na ugawaji wa chanjo hizo, ilikuwa ni ulinzi wa msafara wao, na ukusanyaji wa taarifa za kiintelijensia.

Baada ya msako wa wiki mbili bila mafanikio, mzee Kisiki alifanya kikao na watu wake. Kwa muda sasa alikuwa kajiingiza kwenye masuala binafsi ya kumsaka Mwamvita na Masu, akasahau habari ya Molio. Hili suala la Molio lilikuwa suala kubwa kwenye shirika la ENTRY. Kupotea kwa Molio chini ya uangalizi wa mitambo yao kulikuwa ni tishio kubwa kwa kundi hilo hatari. Ilikuwa na maana kwamba, yeyote aliyefanikisha zoezi hilo, basi alikuwa si mtu wa hivi hivi. Alikuwa ni mtu hatari sana. Angeweza hata kuingilia mitambo yao na hata kuanika siri zao hadharani. Na ukweli ni kuwa habari za Molio kwa kiwango kikubwa zilimpa nafasi kubwa Yara kujikusanyia data za maana sana kwa shirika lake la FSB. ENTRY walipaswa kuweka mikakati mahsusi ya kumtambua mtu huyo. Kikao hiki kililenga kuweka mipango hiyo sawa sawia.

Walizungumza mengi ndani ya kikao hicho cha siri, na mwishowe wakatoka na mpango mkakati wa kumsaka mtu huyo. Upelelezi ukaelekezwa kuanza kufuatilia nyendo za Molio kwa wiki mbili kabla ya kutoweka. Alizungumza na nani, wakiwa wapi, alipendelea kukaa wapi na akiwa na nani. Picha za cctv za maeneo aliyopita Molio zikapewa kipaumbele. Ilifaa wasipuuzie hata chembe ya fununu ambayo ingewawezesha kupata walichokitafuta.

Harakati zikaanza rasmi. Baada ya siku mbili, kundi hilo la wafuatiliaji likabaini watu wanne ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa walengwa wao. Masu, Issa Musa, Yaraslav na Daktari Myung Sun Han. Ikaonekana hao watatu hawakuwepo tena Oman isipokuwa daktari Myung Sun Han. Hivyo, Daktari Myung Sun Han akaingia mikononi mwa ENTRY katika kusaidia kutoa taarifa nyeti ambazo zingefunua na kuanika wazi uhusiano wake na watu hao wengine.

Dr Myung alikutwa akimfanyia mrembo mmoja upasuaji wa kuweka sawa matiti yake. Akawasihi wampe nafasi ya kumalizia upasuaji ule, lakini watu hawa hawakuwa na muda wa kumsikiliza. Walimvuta kama vile ni jambazi, wakimuacha mgonjwa kwenye meza ya upasuaji akiwa nusu kaputi. Wakaondoka na Daktari.

Mahojiano yao na Daktari Myung yakawasaidia kubaini nani hasa alikuwa anadukua mitambo yao. Yaraslav Yvanovitch. Waligundua majina yake baada ya kuingiza sura ya Yara iliyonaswa kwenye moja ya kamera katika uwanja wa ndege wa Salalah kwenye mitambo yao ya utambuzi. Program maalumu kwenye computer ambayo iliweza kuhusianisha sura na taarifa za mhusika. Program hiyo ilikuwa na uwezo wa kuchimba faili zote ambazo zingekuwa na taarifa za mhusika, iwe fiche au za wazi. Ugunduzi huo ukapelekea jamaa hawa wa ENTRY kubaini kuwa Yaraslav Yvanovitch alikuwa ni miongoni mwa majasusi hatari wa shirika la ujasusi la Urussi, FSB. Hata hivyo, ikaonekana kuwa alikuwa ni mwajiriwa wa kampuni ya kimarekani iliyojulikana kama Amchip kama ficho la utambulisho wake halisi. Moja kwa moja, wataalamu wa ENTRY, wakajua, Yara alikuwa Amchip kwa shughuli za kijasusi. Utambuzi huo ukamuondoa daktari Myung kwenye hatia. Wakamwachia huru. Kazi ndio kwanza ilikuwa inaanza.

Daktari Myung aliporejea kituoni kwake, mteja wake alikuwa ni marehemu tayari. Kifo si mshikaji kabisa, hata katika kilele cha ubora wako, anaweza kukunyang'anya uhai wako. Hafai kifo. Binti yule ambaye sasa alikuwa atambe kwa mbwembwe, mtaani wamjue, Instagram wamtambue, Loh, urembo wake ukawa ndio sababu pekee aliyotumia kifo kuvuna uhai wake. Wivu tu!

Itaendelea...
 
  • Thanks
Reactions: ram
KAZI YA MZUNGU 34
DAVID NGOCHO SAMSON
0629077792

Masuke mwana wa Masuke kwa kifupi Masu, alimaarufu M'bara, alikuwa amerejea Zanzibar kutoka safari zake za kuzunguka dunia wakisambaza chanjo, yeye na jopo la watu wengine kama yeye waliokuwa wanamfanyia kazi Mzungu Steve Curl. Kwa sasa alikuwa anaishi kwenye jengo la kisasa alilokuwa kanunua katika mtaa wa Forodhani.

Ndani ya jengo hilo la ramani ya kisasa, lenye vyumba vitatu vya kulala, sebule pana ambayo ilikuwa imeenea fenicha za kisasa, Masu aliweka macho ya CCTV camera kila kona muhimu. Si hivyo tu, aliweka vifaa vilivyomudu kuhisi ujio wa mtu mwenye silaha, au mwenye wahka ukapeleka taarifa ndani kwa kutoa king'ora ambacho kilisikika kwa mtu aliye ndani ya jengo na kama hakuwemo ndani, basi mhusika alipata king'ora hicho kupitia ile simu janja ya mkononi.

Hicho ndicho kilichotokea dakika mbili baada ya kujilaza kitandani. Alisikia king'ora cha hatari. Akakurupuka pale kitandani na kuchungulia simu janja yake. Akaiona sura ya Yara ikiwa imehamanika vya kutosha. Jamaa alikuwa anahema juu juu. Akiwa hajaondoa macho yake kwenye saa hapo, akamshuhudia Yara akitoka nduki, mara kiwiliwili cha mtu mwingine kikaonekana kifukuzana na Yara. Akashituka. Mshikaji alikuwa hatarini. Walishakuwa marafiki sasa. Anapoendelea kutafakari hayo, akamuona na Jamaa mwingine akajua ni kundi moja na wale waliokuwa wanafuatilia Yara. Akanyanyua simu na kumtafuta Yusu. Yusu aliishi mtaani hapo kama nyumba ya nane hivi kutoka kwa Masu.

'Oya, yule mwana nilokuambia alisaidia kurahisisha mchakato wa kuondoka na Mwamvita yuko hatarini. Nahisi ni watu wa ENTRY, Si unajua wamekuwa wananitafuta kwa udi na uvumba? Alikuwa anakuja hapa lakini waliokuwa wanamfukuzia walikuwa jirani. Hivi napoongea na wewe nipo nawacheki wanavyomfukuzia. Kama vipi, nguvu yako ni muhimu sana.' Masu alizungumza akiwa keshatoka, kiunoni akiwa ameficha 'mguu wa kuku'. Mdogo mdogo akiwa juu ya piki piki akaanza kufukuzia watu wale.

Akampigia simu Yara.

'Hao jamaa vipi?' akahoji baada ya simu kupokelewa.

‘Wanataka kunikamata. Walishashitukia ule mchongo tuliofanya kule Oman, ile ishu ya chip ya Molio. Walikuwa wananiulizia kwa kuonesha picha yangu kwa wahudumu wa hotelini. Mhudumu mmoja alinitonya, nikajaribu kusepa lakini kuna mtu walimweka eneo fulani kucheki wanaotoka hotelini. Huyo aliponiona akawashitua wenzake wakaanza kunifuatilia. Nipo hatarini ndugu yangu. Wapo watatu na nahisi ni majasusi.' Yara aliongea huku akihema kufuatia zile mbio.

'Dah, ngoja nione nachoweza kufanya hapa. Cha msingi jaribu kujichanganya na watu kadri unavyoweza.' Masu alimwambia huku moyoni akijisemea, 'inamchukua jasusi kumtambua jasusi mwingine'. Alikwishamshitukia mapema Yara kuwa ni jasusi. Na sasa kama anawindwa na majasusi ni kwa vile yeye mwenyewe ni jasusi. Alitafakari hivyo.

'Kujichanganya ndio inakuwa ngumu maana kutokana na mambo ya Covid 19, kila mtu anajaribu kujiweka mbali na mikusanyiko. Hapa nachofanya nataka niingie kwenye huu mjengo mbele yangu.' Yara alizungumza wakati akiingia kwenye jengo kuukuu la tangu enzi za utumwa.

‘Yap, zama humo, iwe mtafutano na mimi nitakuwa nishafika kukusaidia. Masu alimwambia Yara, halafu akafanya mawasiliano na kumjulisha Yusuf wakutane kwenye hilo jengo. Ni moja kati ya majengo ya kizamani ambayo yalibaki kama historia, kwa maana ya maghofu ya kihistoria. Hili lilisemekana kujengwa zamani na Sultani Barghash mnamo mwaka 1883. Inasemekana jengo hilo la ghorofa tatu lilipoteza maisha chungu nzima ya waafrika wasio na hatia kwa sababu tu za ubwana na utwana ulioendekezwa na ubaguzi wa rangi. Kwamba waafrika wengi waliuwawa kama sehemu ya tambiko za kuwezesha ujenzi wa jengo hilo. Hata hivyo, inasemekana tu kama masimulizi lakini hakuna anayeweza kuthibitisha pasipo na shaka kuwa ni kweli waafrika walichinjwa kama kondoo ili kuwa kafara kwa ajili ya ujenzi huo.

Dakika moja baada ya wale majasusi wa ENTRY kuingia mle ghofuni, Masu naye alizama akiwa na silaha zake alizokuwa amebeba, bastola kiunoni na visu kadhaa kwenye mifuko ya koti lake refu. Alijibanza sehemu, alipopata upenyo wa kumuona mmoja wa maadui akiwa amempa mgongo, alimshitua na 'hey', jamaa alipogeuka, likawa ni kosa kubwa. Masu akarusha kisu chake kikatua kwenye bega la mkono wa adui uliokuwa umeshika bastola, jamaa bastola ikamdondoka wakati akiugulia maumivu. Haraka sana Masu akamfikia na kumpa kono la bapa nyuma ya sikio na kumzimisha kwanza. Akamburuta na kumficha kwenye kona. Akakaa tayari tena. Mara akamuona Yara akijivuta chini. Alikuwa amekula shaba mguuni na jamaa alikuwa anamfuata ili kumbeba. Masu akajihimu kabla jamaa hajamuona, amrushie adui kisu, badala yake akamshuhudia jamaa anaenda chini mzima mzima. Yusuf alikuwa katekeleza tukio hilo. Sasa walikuwa wanatazamana kwa kuoneshana ishara ya ushindi alipotokeza jamaa wa tatu akiwa amenyoosha bastola yake kichwani kwa Yusuf, bahati nzuri Yara akawa amemuona na bila kuchelewa akampiga risasi ya mkono ambayo ilisaidia kuikwepesha risasi iliyokuwa ivune uhai wa Yusuf. Yusuf alisikia mvumo wa risasi hiyo ambayo ilikwangua sikio lake kidogo na kuenda kujikita ukutani. Ilikuwa jirani sana. Isingekuwa Yara amemuwahi yule mpuuzi, Yusuf alikuwa anapotea.

Jamaa aliyepigwa risasi ya mkono na Yara, alikuwa anaugulia kwa maumivu. Kilio chake kilitosha kutambulisha maumivu makali yaliyokuwa yanamnyanyasa. Yusuf alimfuata akampiga pigo moja la kininja, jamaa akalamba udongo. Akamfuata pale chini, lakini jamaa akageuka haraka sana na kumzawadia Yusuf teke moja mujarabu sana, ambalo lilimpata vizuri kwenye mbavu zake. Yusuf akahisi kuna mbavu imevunjwa. Lakini haikuwa hivyo. Jamaa alinyanyuka akataka kusepa, Yara akamtwika risasi ya kisogoni, akafumua medulla oblangata ya jamaa. Pigo la kitoto. Pigo ambalo halina heshima. Pigo linalompa heshima aliyepigwa na si aliyepiga. Jamaa akalala mauti. Sasa walikuwa wamebakiza mtu mmoja tu hai. Yule ambaye Masu alimzima na bapa ya kono lake la kushoto.

Walimnyanyua Yara na kumpa huduma ya kwanza, wakafunga kidonda kile ili kisiendelee kuvuja damu. Walipomaliza hilo, wakambeba na pia wakataka wambebe na yule jamaa wa ENTRY, lakini Yara akawaambia hapana.

'Wanakuaga na chip hao, watamfuatilia wamkute tulipo iwe shida nyingine kwetu.' alitamka Yara kwa sauti ya maumivu.

'Kwa hiyo tunamwacha hapa?' alihoji Yusuf

'No, huyo atatufaa ili kujua alipo kiongozi wao. Wana kitu ambacho ni muhimu kwa shirika langu.' Yara alizungumza na kuthibitisha ile hisia ya Masu tangu waliposafiri wote kwenda Oman kuwa huyu jamaa alikuwa ni jasusi.

'Tunahitaji kuiondoa hiyo chip kwanza tuondoke naye.' Yara alimalizia.

'Tangu awali nilijua tu wewe ni jasusi la FSB. Kipi hicho walichonacho hawa jamaa wa ENTRY?' Masu alihoji.

'Hiyo taarifa ni ya Siri, lakini kwa vile mmeshanifahamu na mmeniokoa, nitawaeleza. Lakini mnaonaje tuichomoe hiyo chip tuondoke eneo hili na tukiwa eneo salama nitawajuza?'

'Uko sahihi, hatupaswi kuendelea kukaa hapa. Haya tupe mwongozo.' Masu alizungumza.

'Hizo chip zao zinawekwa kwenye ngozi ya tumbo karibu na kitovuni. Wanafanya hivyo ili kuwapa wasiojua hofu kuwa ipo ndani ya utumbo. Niligundua hili wakati wa ile operesheni ya Molio. Kwa hiyo, tumia kifaa hicho cha kutambua chip, ili kuweza kufahamu ilipo chip, ukishaiona unachofanya ni kuvuta ngozi ya eneo hilo halafu unachana na kiwembe unaivuta, chip zao ni kubwa kama za wanyama, ni rahisi kuiona.'

'Ah kudadeki, sifanyi kazi hiyo. Hapo ulipo unaweza kuifanya bana, wewe ndio mtaalam.' Masu alijibu. Yara akamwangalia Yusuf kama kutaka kusema 'Basi fanya wewe', Yusuf akaelewa angalia yake. Akabetua mabega yake na kutamka

'I don't touch some ENTRY shits blood' (ah wapi sishiki damu ya mpuuzi wa ENTRY)

Ilimlazimu Yara kufanya kazi hiyo. Haikuchukua dakika mbili. Wakaondoka zao eneo la tukio.

***

Daktari aliletwa nyumbani kwa Masu, Yara akapewa huduma ya jeraha lake, risasi iliyokuwa imebana kwenye nyama za mguu wake, ilitolewa kidonda kikasafishwa akafungwa bandeji. Haikuwa tatizo kubwa, ilikuwa ni kidonda cha kawaida tu, risasi haikugusa mfupa. Ingemchukua siku kadhaa kuwa sawa, lakini leo hii alitakiwa kupokea ugeni wa majasusi wenzake tokea Korea kaskazini. Hawa ni pamoja na mtu katili Mikhail Vahdeem. Mkuu wa ENTRY alitakiwa kueleza ilipo chanjo ya SARS Covid 2.

Yara aliwaeleza Masu na Yusuf kwamba ENTRY walikuwa wameiba formula ya ACVV, na kwa hali ambayo pia ilionesha watu hao ndio walitengeneza kirusi cha SARS covid 2, kwa kusudi la kuangamiza idadi kubwa ya watu waliyodai imezidi na huenda ikaangamiza dunia. Akaongezea kudai, wao kwa maana ya shirika lile la Urussi likiipata chanjo hiyo, itazalisha na kugawa duniani kote ili kuepusha dunia na janga la kuangamizwa na ENTRY na washirika wao Earth Vision 2050.

Habari hiyo ya Yaraslav Yvanovitch ikamkumbusha Masu juu ya makubaliano yaliyokuwa yanaendelea kufanyika na Dr Wu, kabla ya kifo chake, makubaliano yaliyolenga SRI (Scientific Reality Inc) kununua formula hiyo kwa mfumo wa kupata leseni ya uzalishaji kwa niaba, yaani kupewa mamlaka ya kuzalisha kama sehemu ya taasisi ile ya uchina CRC (China Research Center). Habari hii ya FSB kuisaka chanjo hiyo, haikuwa njema. Hii ilikuwa na maana kwamba, taifa hilo kubwa lilikusudia kunufaika na chanjo hiyo kwa kile ambacho kilionekana kama vita ya kiuchumi kwa silaha za kibayolojia.

Kwa muda sasa mataifa ya Marekani na China yalikuwa yanachuana vikali kiuchumi. Huku China ikionekana kuteka soko la bidhaa zake Africa, Asia, America, bidhaa za China zilisambaa kote duniani. Na katika kitu kilichotishia Marekani na washirika wake, ilionekana China sasa inasaini mikataba ya ushirikiano na mataifa ya Asia, na Africa. Nchi za mataifa hayo sasa hazikuhitaji tena mikopo kutoka Marekani na washirika wake, walielekeza macho yao uchina ambako walipata mikopo yenye nafuu na makampuni ya ujenzi ya China sasa yaliibadilisha kabisa taswira ya uduni iliyokuwa nayo Africa, Africa ilianza kuonesha maendeleo. Barabara za lami, majengo ya kisasa mijini na miundo msingi mbalimbali.

Masu akahisi, kwa vyovyote vile, Urussi ilikuwa inakusudia kugombanisha mafahari hao wawili, wakati wanapohangaika na vita hiyo, yeye atumie fursa hiyo kutengeneza uchumi wake. Kwa jinsi gonjwa hilo lilivyokuwa likiendelea kusambaa kote duniani, kama chanjo hiyo ingehodhiwa na Urussi, pata picha ingejitajirisha vipi kwa kuiuza kote duniani? Ingekuwa kama janja iliyotumiwa na Marekani kuwa taifa kubwa ulimwenguni wakati wa vita kuu za dunia. Wakati ambao Marekani ilijipambanua kwa sera yake ya, ‘isolation policy’, sera ya kujitenga. Wakijifanya hawahusiki na vita ile, huku wakinufaika kwa kuuza silaha zilizotumika kwenye vita hizo. Yaraslav ni rafiki yake, lakini hii njama yao, Masuke hakuiafiki hata kidogo.

'ENTRY wameiba formula hiyo wapi?' Masu aliuliza. Yaraslav Yvanovitch akaonekana kubabaika kulijibu swali hilo. Alijipata njia panda. Bila shaka alijiuliza vipi akidanganya na rafikiye huyu awe tayari anaujua ukweli? Isingemweka kwenye nafasi nzuri.

'Ah, kwa kweli sina hakika sana. Wakuu wangu walinambia tu hivyo na kunipa majukumu ya kupeleleza ENTRY' kauli hiyo, ikampa Masu muda wa kutafakari, hadi kufikia hapo, Masu alibaini kuwa hakukuwa na jema lolote kwa FSB kumiliki chanjo hiyo kwa sababu ilikuwa wazi, FSB ilikusudia kuitumia ACVV kama silaha dhidi ya Marekani na China. Si ajabu hata kirusi chenyewe kikawa kilipandikizwa na Urussi. Aliwaza Masu

Kama hivyo ndivyo, alianza kuona picha ya kilichokuwa kikiendelea. Vita ya maneno kati ya serikali ya Marekani na serikali ya China. China ikiishutumu Marekani kutengeneza kirusi hicho kwa lengo la kudhoofisha uchumi wake. Hayo hasa yakisikika wakati mlipuko ulipoanza kusambaa China na mataifa ya jirani. Huenda na wamarekani walidhani hivyo pia. Lakini kirusi hicho kilipovuka mipaka na kuingia Marekani, lawama zikageuka. Marekani ikadai China ndio wametengeneza kirusi hicho ili kudhoofisha uchumi wake na wa washirika wake NATO, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani ambako kirusi hicho kilishika kasi kwenye mataifa hayo kuliko hata China kwenyewe.

Masu aliazimu kumjulisha bosi wake Steve Curl habari hii.

Dah, mambo ya majasusi wala sitaki kujihusisha nayo, ikijulikana tunaujua mpango wenu, unadhani wenzako watatuamini? Kwa ajili ya usalama wetu, itakubidi urudi hotelini na usigusie kutufahamu kabisa.' Masu alimweleza Yaraslav Yvanovitch.

Nami nilidhani hivyo ndivyo inapaswa kuwa. Mmenifaa sana na nisingependa niwaingize kwenye utata zaidi. Nawashukuru sana ndugu zangu.' alitamka Yaraslav.

Walimchukua kwenye gari na kumpeleka Hotelini alikofikia.

***

Jioni saa moja, Masu na Yusuf walikuwa hotelini, Safari Hotel. Pamoja nao alikuwepo tajiri Steve Curl. Walikuwa katika moja ya migahawa ndani ya Hotel hiyo ya kitalii. Hotel ambayo wenyeji waliamini ni kwa ajili ya matajiri pekee. Wastaafu na bila shaka wazungu wenye fedha za kuwatosha. Ndivyo ilivyokuwa. Aliyeingia safari Hotel alikuwa ni mtu mwenye ukwasi kweli. Kulala kwa usiku mmoja ndani ya Hotel hii, kungekugharimu takribani shilingi za kitanzania milioni mbili na ushei.

Walikuwa wanapiga soga huku wakipata mlo wa jioni. Masu akatumia fursa hiyo kumweleza dukuduku lake juu ya FSB na msako wao wa chanjo. Hofu yake ikionekana kuwa huenda wangebaini kuwa wao pia walikuwa na tiba dhidi ya SARS covid 2. Jambo hilo lilimshitua sana Steve Curl. Ni kama Steve aliiona hatari kama kungetokea kitu kama hicho. FSB kumiliki chanjo ya SARS COVID 2

'BGK hawapaswi kujua kabisa juu ya shughuli zetu. Huyo rafiki yako, anaelewa kiasi gani kazi unayofanya?'

'Hajui chochote zaidi ya kuwa mimi ni mtaalamu wa mambo ya mifumo ya ulinzi wa Hotel hii.'

'Safi, itakuwa vema ibaki hivyo hivyo. Kwa sasa jiandaeni kwa safari ya kwenda China. Nataka mkafanye upelelezi wa kutosha juu ya kifo cha Dr Wu Han.'

'Sawa bosi.' Masu na Yusuf waliitikia kwa bashasha. Habari kama hiyo kwao ilikuwa ni habari njema. Ilimaanisha pesa zaidi kwenye akaunt zao.

'Nasikia kuna 'lockdown' huko bosi, ni kama, hawaruhusu watu kuingia hovyo nchini mwao.' Masu alitoa taarifa.

'Ni kweli, nchi nyingi zimechukua tahadhari kama hiyo. Kuzuiliwa hamtazuiliwa, lakini mtapimwa kisha mtawekwa karantini kwa muda wa siku kumi na nne. Jambo hili ni la muhimu zaidi, we can't afford to let FSB take hold of the vaccine, not even the IAC.' (Hatuwezi kuacha chanjo iangukie mikononi mwa FSB au IAC ya wamarekani).

ITAENDELEA...
 
  • Thanks
Reactions: ram

Similar Discussions

Back
Top Bottom