Simulizi: Kazi ya mzungu

Simulizi: Kazi ya mzungu

KAZI YA MZUNGU 13
DAVID NGOCHO SAMSON

#TULIPOISHIA
'Hilo la kheri sheikh wangu, SI vema kuendelea kumweka hapa shughuli zake zikiendelea kulala. Ila hapo utachangia shilingi elfu hamsini TU, kufidia usumbufu uliojitokeza kwa jeshi la polisi'
'Hamna tabu, wacha tulimalize hili.' sheikh Abuubakr akatamka akijua wazi ile Ilikuwa hongo. Lakini yeye hakuona Hilo, alijua baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi kwa hongo Ni chuma kwa sumaku, na hapa alikuwa anakimbizana na muda! Wapenda haki walimpa muda mahsusi kutekeleza Rai yao.

KAZI YA MZUNGU 13

Million 75 kwa kila mmoja wao, Ilikuwa Ni hela kubwa. Nzinyangwa alijua ingekuwa rahisi kuwakamata wezi wake. Alikadiria kwamba, wezi wake wangeonesha umwamba, kutumia isivyo Kawaida. Anasa kwa wingi. Akawapanga vijana wake kuzungukia maeneo ya starehe kuangalia watu ambao wangekuwa na matumizi yasiyo ya Kawaida. Hiyo ingekuwa Kweli kama Masu na Yusuf wangekuwa waswahili, kwani waswahili huamini maskini akipata sijui nini hulia mbwata. Alipoteza muda.

Masu na Yusuf walikuwa na Wazo tofauti. Walikubaliana kuhifadhi zile fedha na kutulizana kwanza. Waliwaza kuwa kutumia pesa isivyo Kawaida yao, ingevutia nzi Kama inavyokuwa kwa mizoga. Kila mmoja akaichimbia alikoona Salama. Hawakuzihifadhi benki. Kama kazi ya Mzungu ingeonekana namna gani, walikusudia kuondoka Zanzibar na kuanzisha biashara au kuwekeza fedha zao kwenye makampuni makubwa kwa mtindo wa kununua hisa au hatifungani. Nzinyangwa asingewapata.

Mara baada ya kuachiliwa huru, Bakari aliona Zanzibar kunamwekea usiku. Rafikize walipompatia Kiasi kile Cha fedha, aliondoka Zanzibar na kurejea kwao Iringa. Fedha ile akaitumia kununua mashamba yenye miti izalishayo mbao, Cyprus na pines. Kiasi Kidogo akaanzisha biashara ya duka la jumla. Mungu akaibariki kazi yake mpya. Akafanikiwa sana. Miaka mitano mbeleni, Bakari, ambaye Sasa alijulikana kwa jina lake halisi Paulo, alikadiria kwamba angepata mamilioni ya fedha kwa kuchana na kuuza mbao kwa ile miti yake.

***
Siku moja baada ya kuachiwa kwa Bakari, Masu na Yusuf waliomba kikao na sheikh Abuubakr. Sheikh Abuubakr akawakaribisha nyumbani, wakawa wameketi wanakunywa ghahawa. Masu alikusudia kumweleza sheikh Abuubakr, kuwa kusudio la safari yao hapo Nyumbani, Ilikuwa kuutaka mkono wa bintiye Mwamvita kwenye ndoa tukufu.

'Sheikh, sisi Ni vijana wako, tupo hapa kwa sababu tunahitaji kuzungumza nawe.. Mimi naitwa Yusuf, na huyu mwenzangu anaitwa….'
'Naitwa Masuke Masuke mzee wangu!' Masu alidakia kabla Yusuf hajamalizia kumtambulisha. Lafudhi yake ya bara ikimtambulisha vilivyo kuwa yeye Ni mtu kutoka bara. Akaunyoosha mkono wake amsalimie sheikh Abuubakr. Ah wapi!? Sheikh Abuubakr aliposikia jina Hilo, kumbu kumbu yake ikamtendea haki. Ikamweleza kuwa mkewe mama Mwamvita akikwishamwelezea hofu yake kuwa Masu alihusika na mimba ya binti yao. Haikuwa kitambo, Ilikuwa usiku wa Jana baada ya kumweleza habari za Bakari. Aliyakumbuka vema Maelezo ya mkewe.
'Mume wangu, Kama ulosema Ni sahihi, Basi mie namhisi kijana mmoja, rafikiye huyo Bakari, kuwa ndiye mhusika wa hiyo mimba. Aitwa Masu. Nasema hivyo kwa sababu, huyo kijana alikuwa na mazoea ya kuniita mamkwe, na si mara moja alipomwita Mwamvita Malkia nikaliona huba machoni mwa binti yetu kwa kijana huyo. Sikutilia maanani kwa sababu kijana mwenyewe alikuwa mwadilifu sana, ila alipotoweka ghafla, Hakuna alojua kendaapi, zikavuma habari alitekwa na wasiojulikana! Hivi unapoongea habari za Bakari, ndio umenifanya niliwaze hili.'

Hasira zikamvaa sheikh Abuubakr, akaona kijana huyo alikuwa analeta dhihaka. Akanyanyua bakora yake amtandike nayo kijana huyo. Mara akaisikia sauti ya mkewe.
'Sheikh Abuubakr mume wangu.' sheikh Abuubakr akaishusha chini bakora yake.
Busara yake ikamshawishi kutuliza hasira na kuwasikiliza hao wageni wake.

'Enhee, mwasemaje vijana?' akauliza, macho kayatua barabara usoni mwake Masu.
Huenda akawa SI huyu, maana Masuke aliyenieleza mke wangu alikuwa mlalahoi, mla kwa jasho litokanalo na kusukuma guta na mikokoteni, akajiwazia Sheikh Abuubakr. Alimtazama kijana huyo, akajaribu kutafuta hiyo hadhi ya msukuma mikokoteni asiione. Huyu.., ah! huyu alionekana kuwa mtumishi wa serikali, kitengo nyeti chenye kucheua marupurupu na mshahara mnono bila shaka. Masuke alikuwa katinga suti Safi ya hudhurungi. Nywele zake nyeusi zilichanwa Vema na kungara kwa mafuta ghali ya nywele. Mguuni alitinga moka safi, Loh, hakuvaa soksi. 'Vijana wa siku hizi!' akawaza Sheikh Abuubakr. 'Hawafanyi kitu kikamilike wasikitie doa, kapendeza lakini kaharibia hapo tu, mbona asivae soksi?' akaendelea kujiuliza.

'Eeh, mzee tumekuja na kijizawadi Kidogo. Tunaomba ukipokee kabla hatujaeleza dhumuni la ujio wetu.' Yusuf akazungumza, Huku Masu akitoa bahasha na kumkabidhi mzee huyo. Sheikh akaipokea zawadi. Akachungulia ndani na kuona burungutu la fedha.
'Nyie vijana Ni Nani? Mnataka Nini? Hii maana yake Nini?' Sheikh akalipuka kwa hasira.

'Tumekuja kuomba radhi kwa usumbufu tulokusababishia. Tunajua Kuna namna tumekufanya uwe na hasira na hata kufikiria vibaya. Kama nilivyojitambulisha awali, Mimi naitwa Masuke. Mimi ndio mhusika wa mimba ya Mwamvita.' Masuke akajieleza. Safari hii akachezea bakora.
'Wapuuzi Sana nyie watoto, kwa hiyo mmeona mlete dhihaka hapa, sivyo?' Sheikh alikuwa kasimama Sasa. Amefura kwa hasira!
'Hapana mzee, Tumekuja kwa Nia njema TU. Tunatakutaka radhi na pia tunaomba ruhusa ya kumuoa binti yako Mwamvita.' Yusuf akaingilia Kati.
'Mmeona haitoshi kumtia mimba Mwanafunzi Sasa Unataka kunihonga Mimi nishiriki makosa yako? Jela ndiko kunakokufaa. Mjinga mmoja wewe?' sheikh Abuubakr alikuwa mbogo.

Mwamvita alikuwa chumbani kwake. Uzuri wa chumba chake, dirisha lake lilitazama hapo walipokaa Masu, Yusuf na wazazi wake, Chini ya mnazi. Alishuhudia harakati zile zilizokuwa zinaendelea. Masu alivyokula bakora, Mwamvita uvumilivu ukamshinda, Heri hizo bakora azipate yeye pia. Akatoka ndani akilia.
'Mimi ndiyo nastahili hizo bakora baba, Mimi ndio nikiyekufedhehesha. Sikumpa nafasi Masu kufanya maamuzi Sawa, Mimi ndio niliyemfuata kwake na kusababisha hii Hali. Kama Ni adhabu nastahili Mimi. La sivyo, nakuomba baba, tafadhali tusamehe. Yalikwisha tokea ya kutokea, tusamehe baba, tunahitaji baraka zako tuanze familia.'
'Sheikh Abuubakr mume wangu. Hebu punguza jaziba baba watoto. Wasikilize watoto. Wameonesha kujutia makosa yao, wape nafasi ya kujisahihisha tafadhali!' mama Mwamvita akaongea kwa hekima kubwa. Sheikh Abuubakr yakamwingia Hayo maneno. Mara nyingi, sauti ya mkewe Ilikuwa na athari kwenye moyo wake. Tangu alipomuoa, sauti yake Ilikuwa sauti iliyompa tumaini na kumpitisha kwenye changamoto. Aliiheshimu sauti hiyo. Akatuliza munkari. Akapumua Vema. Akapata kufikiri Vema bila ushawishi wa hasira.
'Hamna wazazi nyie?' lilikuwa swali la msingi.
Swali ambalo huenda vijana hao hawakulitarajia.
Wakabaki wanatazamana.
'Kama lengo Ni kuleta barua ya posa, nyie hamjui taratibu?' akaongezea Tena Sheikh Abuubakr.
'Ah, mzee wangu Hilo litafuata hivi punde. Sisi tulitaka tu tuweke Mambo sawa kabla ya kuanza hatua rasmi za taratibu za kuoa. Tumekuja kwa lengo la kukutaka radhi.'
Sheikh Abuubakr akarudisha moyo wa imani.
'Mama Mwamvita mke wangu, hebu kawaandalie chakula wageni wetu.'
'Rabeka mume wangu, naenda Sasa hivi. Haya, amka twende mama!' mama Mwamvita akazungumza huku akimwashiria Mwamvita kuongozana naye. Nyuso zao ziling'ara kwa tabasamu. Mwamvita alifurahi mno!
'Enhee, Sasa naweza kuwasikiliza. Jitambulisheni Tena tufahamiane vizuri. Hivoo, umesema wewe wafanya kazi gani?' Sheikh akauliza. Alikuwa akitafakari habari kwamba, kijana huyo alotaka kumuoa bintiye Ni mbeba mizigo. Akatafakari pia juu ya yule mzee aliyeonesha Nia ya kutaka kumuoa binti yake, aluwatani Kisiki.

Mzee Kisiki alijulikana Sana hapo mtaani. Mwanajeshi mstaafu aliyetukuka kwa sifa kibao, ikiwamo ile ya kuongoza kikosi kilichofanikisha kurejesha amani visiwani Comoro. Mzee huyu, alikuwa na jumla ya wake nane, hivyo Ni kusema Mwamvita angefikisha namba Tisa. Kilichomfanya mzee Kisiki amudu kuwa na wake wengi hivyo Ni uchumi wake mzuri. Alikuwa Ni miongoni mwa watu wenye hisa nyingi kwenye makampuni makubwa anuai hapo Zanzibar na kule bara. Mahotel ya nyota tatu Hadi tano, mzee alikuwa na mkono wake ndani. Alitumia Vema nafasi yake ya ukubwa jeshini wakati wake, kuwekeza.

Sheikh Abuubakr alitafakari Sana. Moyo wa bintiye ulikuwa umemwangukia mhuni, msukuma guta.. angeishi maisha hovyo Sana ya kimaskini kwa kuambatana na kijana huyo. Wakeze Kisiki walikula maisha, wengi aliwaoa TU ili kuwanusuru. Alifanya Kama kuoa Ni sadaka kuwasaidia wanawake waliokimbiwa na kuachiwa mimba, ama kutelekezwa na watoto wao. Hao ndio wakeze Kisiki. Aliwachukua hao, akawapatia maisha, kila mmoja akawa na uhakika wa kuingiza kipato. Akawafungulia miradi wasimamie. Hata ikawa kila mkewe, aliweza kula na kulala pazuri, kusomesha watoto kwenye skuli za kufunza kwa kiingereza, na wote waliendesha magari kwa ufahari. Huyo ndiyo mtu alotaka achukue dhamana ya bintiye. SI mhuni mmoja kutoka bara!

Sasa akabaki yuajiuliza, namna gani bintiye alichagua mtu lofa, avujaye jasho kupata' mkate usotosha hata kusaza? Sheikh Abuubakr akajikuta kwenye mtihani mgumu. Akatega sikio amsikilize kijana huyo, huenda akabaini hicho kilichomfanya bintiye azuzuke. SI Ni Kweli kwamba wapo maskini wa Mali lakini wakawa matajiri wa busara? Alitafakari..

Masuke moyo ukamlipuka kwa furaha, akaweka tabasamu usoni kwake na kuanza kujieleza, tayari alikwisha hisi ushindi Unamnyemelea! Akajikohoza Kidogo na kulegeza Kidogo tai yake, akaweka pozi la ushindi.

'Ah, mzee wangu Mimi naitwa Masuke Masuke, Ni mzaliwa wa kijijini Malonje mkoani Morogoro. Kwa Zanzibar, huu Ni mwaka wa pili Sasa tangu nilipokuja Huku, SI haba, mwenyezi Mungu aliniangazia Nuru zake tangu nakanyaga hapa, akanibariki kupata' kipato changu Kidogo lakini halali, kwa kujituma kutumia mikono na nguvu zangu. Nimekuwa nafanya kazi ya kubeba mizigo lakini kwa Sasa natarajia kuanza kazi yangu mpya mwezi ujao, kwenye Hotel moja ya Mzungu hapa hapa kisiwani. Itakuwa kazi yenye maslahi mazuri na nakuahidi binti yako atakuwa kwenye mikono Salama, inshallah, kwa uwezo wa Mungu. Huyu mwenzangu Ni rafiki yangu ambaye tumekuwa tukifanya naye kazi pamoja'. Masuke alijieleza kwa ufahari.

Mzee Abuubakr alimtazama kijana huyo akakosa tumaini. Suti hii ya gharama, Kumbe kapewa na Mzungu kwa ajili ya kazi ya uhudumu hotelini. Eti maslahi mazuri, kwa kazi gani? Kwa mtu alozoea kupewa Mia tano miambili akfu moja, kazi nzuri itakuwa ya shilingi ngapi? Laki moja kwa mwezi? Sheikh Abuubakr akamdharau Sana kijana. Hata hivyo hakutaka kuonesha Hali hiyo. Wakaendelea kupiga soga, chakula kikaletwa wakala na hatimaye wakaagana.

'Kumbuka kunisalimia wazazi wenzangu huko. Bila shaka tunawatarajia kwa ajili ya kukamilisha Taratibu hizi. Muhimu wakinipa taarifa mapema juu ya ujio wao.' Sheikh Abuubakr akachombeza.

Masu na Yusuf wakaondoka wakiwa na nyuso za furaha. Mwamvita furaha yake ndio kabisa, Ilikuwa haisimuliki.

***
'Naam Sheikh, …… nakupata vizuri Sheikh……. Hewalaa sheikh wangu. Sasa, Mimi Nina mpango maalumu wa kutatua Hilo tatizo, Wala lisikusumbue Hilo, sisi watu wazima bwana, watoto hawawezi kutuzingua kabisa. Unaonaje tuonane baada ya swala ya jioni nikushirikishe mpango huo?' Ilikuwa sauti ya mzee Kisiki!
'Naam, nitafanya hivyo!'

Jioni ya siku hiyo iliwakutanisha mzee Kisiki na sheikh Abuubakr. Wakazungumza mengi. Alipotoka hapo, Sheikh Abuubakr alikuwa na jibu dhidi ya suala la bintiye. Katu hangeridhia fukara msukuma mikokoteni ayaharibu maisha ya bintiye

2020
David Samson Ngocho
FB_IMG_1583317191932.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAZI YA MZUNGU 14
David Ngocho Samson

#Tulipoishia
Jioni ya siku hiyo iliwakutanisha mzee Kisiki na sheikh Abuubakr. Wakazungumza mengi. Alipotoka hapo, Sheikh Abuubakr alikuwa na jibu dhidi ya suala la bintiye. Katu hangeridhia fukara msukuma mikokoteni ayaharibu maisha ya bintiye.

KAZI YA MZUNGU 14

Kulikuwa na Hali ya furaha tele nyumbani kwa Sheikh Abuubakr. Furaha iliyochagizwa na wazee hao kuridhia uhusiano wa Mwamvita na M'bara, Masu. Mazungumzo yakanogea zaidi kwa kutangaziana msamaha baina yao. Lakini furaha ikazidi simu ilipopigwa kutoka Oman, shangaziye Mwamvita aishiye huko alikuwa anawasalimia. Mwamvita akamshirikisha furaha yao.

'Oh hongera Sana shangazi yangu, natamani ningelikuwa hapo tufurahi pamoja. Hata hivyo, kwa furaha niliyonayo, nitafanya kitu kwa ajili yako' shangazi Amina akamweleza Mwamvita.

'Kitu gani shangazi?'
'Siri yangu!'
'Nambie buana, shangazi!' Mwamvita akaongea kwa deko.
'Haya, kwa vile umesisitiza, unaonaje nikutumie nauli uje huku nikufanyie shopping kabla ya harusi yako? Hivi itakuwa lini hiyo harusi?'
'Bado haijapangwa shangazi, ila nitaongea na wazazi kwanza Kama watanikubalia nitakuja Mara moja!'
'Haya shangazi, Mie nakutakia kila la Heri!' shangazi Amina akatamka.
'Shukrani Sana shangazi. Nitakuja inshallah!
Wakafurahi Sana.

Kesho ya siku hiyo, Mwamvita akaitika wito wa babaake.
'Shangazi yako katuma nauli, itakubidi uende forodhani pale zilipo ofisi za 'money gram', ukazichukue. Neno la Siri Ni 'vita' kifupisho Cha jina lako. '
'Shangazi kweli amefurahi Sana. Mara hii keshatuma!'
'Naam, Hakuna kitu anachopenda shangaziyo Kama anavyokupenda wewe, ulipokuwa mdogo, Basi alikuwa muda wote yuakuangalia wee, muda wote kukutekenya mashavu yako, alikuwa anakuita Malaika. Nahisi kumbukumbu zile, Sasa zinamtamanisha akuone ulivyokuwa mdada, Tena anaposikia Una mimba, ah anajua utamletea katoto akatekenye mashavu yake katabasamu na kucheka Kama ilivyokuwaga zamani za utoto wako.' Sheikh Abuubakr alizungumza na kuamsha kicheko. Wakacheka sana, Mwamvita akifurahia hiyo kumbukumbu aliyoambiwa. Akafanya hima, akachukua usafiri wa boda boda kuwahi forodhani, kufuata hizo fedha za nauli Kama zilivyotumwa na Shangazi yake. Alipofika forodhani kwenye afisi za money gram, aliulizwa neno la Siri, akawaeleza, akakabidhiwa riali za Oman Mia mbili hamsini, sawa na pesa za Tanzania shilingi million moja na nusu. Akaomba kubadilishiwa, na uzuri hapo hapo jirani na afisi hiyo kulikuwa na duka la banyani mmoja la kubadilisha fedha za kigeni, wenyewe' huita 'bureau de change'. Akafurahi mno. Akarejea nyumbani akiwa mwingi wa tabasamu.

Mwamvita hakutaka kumtia wasiwasi mumewe mtarajiwa. Akadhamiria kuifanya safari ya Oman Siri. Alikusudia kwenda huko atumie siku mbili tatu na zikiwa nyingi tano, arejee mapema. Hivyo kwa siku mbili alizokuwa anapanga mipango ya safari alikuwa anawasiliana vizuri na Masu. Hata siku aliyokuwa uwanja wa ndege Kisauni, alimpigia simu Masu na kumweleza alikuwa anasafiri Kidogo, na huko alikokuwa anaenda huenda asingepatikana kwenye simu. Masu alijawa na wasiwasi. Wapi alikuwa anaenda, kwa Nini asipatikane kwenye simu?, yeye akadai maeneo Yale mtandao ulikuwa tabu sana. Wapi? Masu akasisitiza, Mwamvita akalazimika kusema uongo.
Kisiwani Mafia. Kulikuwa na umuhimu gani wa kwenda huko kipindi hicho? Masu aliuliza, lakini akahisi amezidisha wivu, akahiari kumruhusu.
'Basi uwe makini, sitaki Jambo baya likupate wewe, Wala mwanetu, ukiona namna gani,..' akasita, halafu akamalizia, ' ..sawa, umesema simu yaweza isipatikane. Uwe makini tafadhali,' Masu alionesha wasiwasi. Hali hiyo ikamfurahisha Sana Mwamvita, ilimfanya aone jinsi gani mwanaume wake alivyomjali sana. Wakati bado tabasamu halijesha usoni mwake, ujumbe mfupi ukaingia kwenye simu yake. Ulikuwa mwamala wa fedha, alikuwa ametumiwa elfu hamsini na Masu. Mwamvita moyo wake ukatakata, SI wanasema pesa sabuni ya roho?

Baada ya makubaliano Kati ya mzee Abuubakr na Masu, Masu aliazimia kwenda nyumbani kuwashirikisha familia yake habari hizo ili kuchakata mipango ya harusi yake. Hivyo, Masu na Mwamvita walijua kinachofuatia ni wao kuanza familia.

Alipowasili kijijini Malonje, Masu aliitazama Nyumba ya wazazi wake, Ilikuwa Nyumba kubwa, lakini Ilikuwa ya zamani. Bati zilishaweka kutu, akaazimu moyoni, baada ya miezi mitatu hivi, angewawekea jengo la kisasa kabisa hapo kijijini. Angeweza kuwahamishia mjini lakini alijua wazazi wake walivyokuwa wabishi. Wangekataa na kuleta hadithi za Paukwa Pakawa. Wangesema mkataa Kwao mtumwa. Akaazimu kuwapelekea mahitaji muhimu pale pale.

Kabla ya kwenda Malonje, alikuwa kapitia chuo Cha mifugo pale Morogoro, akaulizia Bei ya ng'ombe wa maziwa wa kisasa, gharama za kuandaa mabanda na taratibu za utunzaji, akawapata na wataalamu wa kuweka miundo mbinu hiyo vizuri. Baada ya wiki moja, wazazi wake wangekuwa na mifugo hao. Aliwapasha wazazi habari hizo, mama yake akafurahi mno. Baba yake akafurahi Sana pia. Lakini habari iliyowafurahisha zaidi Ilikuwa juu ya kuoa. Hawakuwa na kipingamizi.

***

Wakati anaingia kwenye ndege uwanja wa Kisauni, Mwamvita alijaribu kuwasiliana na Shangazi yake Amina. Simu yake haikupatikana. Akakumbuka pia Jana ya siku hiyo alijaribu kuwasiliana naye lakini hakupatikana. Hata hivyo hakujali Sana, baba yake alikuwa kawasiliana na Shangazi na kumhakikishia angempokea katika uwanja wa ndege wa Salalah, ambapo wangepanda gari kuelekea yalipo makazi ya Shangazi yake huyo, jijini Salalah kwenye mitaa ya watu wenye fedha zao, mtaa wa sultan Qaboos.

Safari ilianza, akiwa na matumaini mengi. Ndani ya ndege walifurahia huduma za shirika la ndege la Qatar, na hata huduma hizo ikawa ndio chanzo Cha mazungumzo Kati yake na kijana aliyekuwa pembeni mwake. Kijana huyo alijitambulisha kwake kwa jina la Issa Musa, na alimsimulia Mambo mengi kuhusu nchi ya kifalme ya Oman. Alimweleza kuwa yeye alikuwa na uwenyeji huko kwa sababu alikuwa Ni mfanyabiashara ambaye biashara zake alizifanyia Zanzibar, Dar, Oman na Dubai. Mwamvita furaha yake ikawa timilifu kwa sababu alipata mtu wa kupiga naye soga.

Mara ya Mwisho kwa Mwamvita kwenda Oman Ilikuwa kitambo Sana, alipokuwa na umri wa miaka sita au Saba hivi. Hivyo hakukumbuka mengi na unajua Tena umri huo utoto huwa mwingi, kiasi kila kitu aliona sawa na kilichomfurahisha zaidi ikawa Ni michezo tu na binamu zake Farouk na Farihad. Kumbukumbu ya shangazi yake pia Ilikuwa ile sura ya kipindi hicho, taswira ambayo huenda ilimdanganya. Lakini, si Kweli pia kwamba yeye mwenyewe Mwamvita alikuwa kabadilika? Aliuona mtihani mbele yake. Sema Nini, hakuwa na shaka yoyote. Shangazi angempokea!

Walipotua Salalah airport, Mwamvita aliteremka akiwa na bashasha.
'Alhamdulilah, tumefika Salama inshallah!' alimweleza Issa Musa.
'Inshallah, imekuwa Heri. Hivyo tutaonana lini Tena bibie?' Issa Musa akauliza.
Ah, kusema Kweli sijui, maana Kama nlivyokueleza mie huku mgeni na sijui chochote hapa. Tuombe uzima, inshallah tutakutana TU Kama ilivyokuwa leo!'
'Loh, zama hizi bado watu hutumia kudra juu ya kukutana? Fanya kitu kimoja bibie, nipe anuani ya utakapokuwa au Basi namba ya simu tutawasiliana' Issa Musa alitaka urafiki udumishwe.
'Hapa tu, ntafanya kusubiri mwenyeji wangu, sijui anuani ya wanakoishi, enzi zile alikuwa aishi mtaa wa sultan Qaboos, Sasa huenda weshabadilisha makazi. Simu, labda nikupe nayotumia nikiwa Zanzibar!' Mwamvita alijieleza.
'Nshakufahamu, na hapo kitu rahisi Sasa itakuwa Mimi kukuachia namba yangu ili wewe upatapo namna utanipigia, naweza kukutembeza uifahamu vizuri Oman.' Issa Musa alipendekeza.
Shukrani Sana Musa, kitu Cha kwanza ntafanya nikifika nendako, itakuwa kukujulisha, nimefurahi kufahamiana nawe. Wakaagana!

Alipokelewa na mwanamke mwenye umri wa kukadria miaka 24 au 25 hivi. Huyu alikuja akiwa hamjui mgeni wake kwa sura Wala picha, alikuwa na kibao TU chenye majina yake, akimuonesha kila mdada aliyetoka kwenye ndege, na ilionekana Kama alikuwa anaangalia wanawake wenye mimba tu. Mwamvita alikuwa na mimba kubwa Sasa, lakini Ilikuwa sio rahisi kugundulika haraka, ilijificha kwenye mavazi aliyovalia. Miezi miwili mbeleni, angejifungua. Alikiona kibao chenye majina yake, Mwamvita Abuubakr, akajua huyo ndio mwenyeji wake. Akamfuata.

'Mwamvita? Karibu Sana, Mimi naitwa Mariamu, Shangazi yako alipata dharura tangu Jana akawa amesafiri kwenda Dubai, huenda leo akarudi. Ila Wala usijali, kila kitu Kiko sawa. Pole na safari' Mwamvita alikaribishwa.
'Asante Sana Mariamu, na je, hiyo dharura ni ya Nini?'
'Ni ile shida yake ya Mara kwa Mara, SI unajua amekuwa anasumbuliwa Sana na tatizo la Figo, Eeh, hivyo ikitokea ghafla amezidiwa, ana daktari wake huko Dubai.' Mariamu alimweleza wakiwa wanatoka nje ya uwanja huo wa Salalah. Kuna kitu kilimtatiza Sana Mwamvita. Huyu mwanamke. Kuna hofu ilimkabili kwa huyu mwanamke. Lakini pia, sauti yake, sauti yake haikuwa ngeni masikioni mwake, na hicho ndio kitu kilichomtia hofu zaidi. Hii sauti alipata kusikia, lakini lini na wapi, hakukumbuka. Moyo wake Hata hivyo, ulimweleza, Kuna kitu hakikuwa sawa!

Waliingia kwenye gari, Toyota Camry nyeusi yenye vioo vyeusi, tinted, huwezi kuona ndani ya gari kunani. Ndani mlikuwa na watu wawili, Dereva na kijana mwingine, wote waarabu. Walipomuona walizungumza kwa kiarabu, wakabaini hakuzungumza lugha hiyo.
'Karibo Sena Salalah!' Dereva alizungumza na kuondoa gari. Lafudhi yake ikamjulisha Mwamvita Hawa hawakukijua kiswahili vema.
'Asanteni sana.' Mwamvita alijibu akilazimisha tabasamu. Hakuwa katika Hali njema kabisa. Hakujisikia vizuri.
Safari iliendelea akiwa hajui lolote, hajui wapi wako, wapi wanaelekea!.
'Hivo bado Shangazi anaishi pale pale!'
'Pale pale wapi?' Mariamu alihoji, Kisha Kama vile alijishitukia, akatamka haraka
'Oh, unamaanisha mtaa wa sultan Qaboos, haha, aah alihamaga haha, unajua Ni miaka mingi Sasa!' Mariamu aliongea huku akitoa kicheko kilichodhamiria kumpumbaza Mwamvita, kicheko kilichodhihiri Nia fiche.
Hii sauti ya huyu mwanamke, hii sauti...Akili ya Mwamvita ilikuwa inafanya uchakataji wa taarifa juu ya hiyo sauti. Wapi, lini aliisikia?.
'Oh, kwa hiyo alihamia wapi?'
'Alihamiaa, panaitwaa, unajua majina ya Oman bana, kunaitwa mtaa wa Umm Al Ghawarif' Mariamu alimweleza. Ah, akili ya Mwamvita bado Ilikuwa kazini, lakini Sasa ilifikia majibu. Kumbukumbu ilimwijia barabara. Akachoka kwa ufahamu huu. Akajua ameuzwa Kama mbuzi kwenye gunia. Baba yake, Sheikh Abuubakr, alikuwa kamuuza bintiye, iwe kwa kujua ama kutokujua. Shangazi yake Amina, bila shaka hakujua chochote juu ya mpango huu. Maana sauti ya Mariamu ndiyo sauti ya Shangazi waliyezungumza naye kwenye simu siku mbili zilizopita. Machozi yake yalivyo jirani, uchozi ulimdondoka Mwamvita. Akazuga kwa kulifikicha jicho lake. Akajuta kumdanganya Masu. Nani atamuokoa sasa?

2020
David Ngocho Samson
FB_IMG_1583317191932.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAZI YA MZUNGU 15

David NGOCHO Samson

#Tulipoishia
Kumbukumbu ilimwijia barabara. Akachoka kwa ufahamu huu. Akajua ameuzwa Kama mbuzi kwenye gunia. Baba yake, Sheikh Abuubakr, alikuwa kamuuza bintiye, iwe kwa kujua ama kutokujua. Shangazi yake Amina, bila shaka hakujua chochote juu ya mpango huu. Maana sauti ya Mariamu ndiyo sauti ya Shangazi waliyezungumza naye kwenye simu siku mbili zilizopita. Machozi yake yalivyo jirani, uchozi ulimdondoka Mwamvita. Akazuga kwa kulifikicha jicho lake. Akajuta kumdanganya Masu. Nani atamuokoa sasa?

KAZI YA MZUNGU 15

GARI liliingizwa kwenye geti la kifahari. Ndani ya geti Hilo kulikuwa na uwanja mpana TU wa maua, kijani kikitawala kwa maana maua na majani yaliyopamba mandhari ya kasri ndani ya wigo huu, yalimwagiliwa kwa Maji muda wote kwa kutumia springs. Mbele yao, Mwamvita akajionea tafsiri halisi ya ufahari. Jumba la kifalme, sio la mashahidi, kifalme kwa maana ya mamlaka isiyo na mamlaka zaidi yake. Wazungu huita, absolute monarchy,. Alijua Oman ni nchi ya kifalme, je alikuwa kapelekwa kwa sultan? Aliwaza.

Kulikuwa na Walinzi kila mahali ndani ya jengo hili. Aliingia ndani na kupokelewa kwa mapambo yenye thamani kubwa. Mapambo ghali kabisa yaliyoakisi tamaduni za kiarabu. Sebule Ilikuwa ukumbi wenye samani chache lakini za gharama kubwa. Zulia lilitambaa sebule yote, likiipatia miguu burudani ya kipekee. Raha. Aliketi kwenye sofa, akakodoa jicho kwenye skrini kubwa ya runinga. Mara, akamuona mtu anateremka ngazi kutokea juu, maana jengo hili lilikuwa la orofa tatu.
Alikuwa Ni mwanaume, mtu mzima. Mwamvita alijua atakuwa mwenye Nyumba hii. Akajiweka sawa ili kutoa heshima yake. Mwanaume yule akazidi kujongea.
'Innallah maasabrin' Mwamvita akahamaki.
Huyo hakuwa mwingine, alikuwa yule aliyekuwa kamhofia Toka awali. Mzee Kisiki. Alikuwa kavalia kanzu yake ya rangi ya maziwa, kichwani barakshia rangi ya dhahabu. Alitembea kwa kujiamini Sana. Tabasamu likicheza midomoni mwake.
'Asalaam alaikum, binti Abuubakr. Karibu ujisikie nyumbani. Nimefurahi Sana ujio wako. Wayaonaje mazingira Haya, karibu Sana Oman'
'Alaikum salaam. Shikamoo, mazingira yanavutia. Una Nyumba kubwa Sana hapa, ya kisasa na gharama yake itakuwa Ni kubwa Sana sio mzee Kisiki?'
'Kabisa' akatamka huku akiachia tabasamu laini, halafu akaongezea,
'Hili laweza kuwa lako, huhitaji kufanya kitu kingine ila kunikubali niwe mmeo. Na .. wala usihofie kwa habari ya mwanao, huyo atakuwa mwanangu pia. Unaweza kufikiria maisha Bora ya mwanao Kama atakulia katika maisha Kama Haya. Wewe Ni mrembo, Mungu alikupendelea uzuri, umalkia, unastahili kuishi katika himaya ya Malkia. Hebu kwanza usinipe jibu lako, chukua muda wa kutafakari, Kama hata baada ya mapendekezo yangu utaona Heri ukaishi na yule msukuma kokoteni, tafakari upya itakufaidi Nini usikie kakuacha mjane na mwanao!' mzee Kisiki alipomaliza sentensi hiyo alimwangalia Mwamvita Kama vile alikusudia kukazia ufahamu kwenye akili ya Mwamvita. Halafu akatamka Tena.
'Nimekuwa mshindi daima, sijawahi kushindwa na sitarajii Hilo litokee kamwe. Likitokea, Kisiki atakuwa SI Kisiki Tena. Aatakuwa kumbukumbu yake.'
Mwamvita hakujua Nini Cha kusema, ulimi ulikuwa mzito kusema neno, mikono ilitota kwa jasho, na pua yake nyeupe ikang'aa zaidi kutokana na mwanga wa taa pale sebuleni kuakisi ung'aro uliotokana na kijasho chembamba hapo puani. Alihisi joto, homa ya ghafla.

***
Issa Musa alipotoka uwanjani, akielekea nje kwenye teksi, alipishana na dada ambaye alimfahamu vema. Akajua Kuna shida inajitokeza. Alikwisha fanya biashara kadhaa na mwanamke huyo kabla hajagundua Ni Mafia. Mwanamke hatari ambaye biashara zake halali zilikuwa geresha TU kuficha kile kilichofanywa na genge lake hatari lililojiita 'Entry'. Miongoni mwa biashara za genge Hilo Ilikuwa Ni usafirishaji wa binadamu.
Issa Musa akashawishika kutaka kujua Molio alikuwa na ishu gani hapo uwanjani, aliingia kwenye mgahawa akawa anasubiri kumuona Molio angetoka na Nani.
Genge maarufu la 'Entry' lilimiliki makasino na maeneo mbalimbali ya burudani katika mataifa ya ulaya, Marekani, Asia na Africa. Kwa Africa waliweka makao yao makuu Afrika ya Kusini, lakini Zanzibar kilikuwa kituo muhimu kichosimamiwa na mzee Kisiki, mzanzibar mwenye mchanganyiko wa kizungu na kiafrika. Mama yake Kisiki, alikuwa mtumbatu, na baba yake hakuwahi kumfahamu. Ilisemekana mama yake alikuwa dobi na katika moja ya Nyumba za wateja wake katika mitaa ya Michenzani, ndiko alikopatia ujauzito uliomleta Kisiki duniani. Jina lake halisi likiwa Ni Halfani Nassor. Kisiki Ni jina alilopata akiwa jeshini kutokana na uwezo alioonesha katika drill za kijeshi. Alikuwa na uwezo wa kumudu kujificha na ukampita bila kujua Kama Kuna mtu hapo, wenzake kwa utani wakambandika jina Hilo. Likakolea Zaidi pale alipojaribu kulikataa kwa ghadhabu nyingi. Mwishowe akaliridhia. Akawa akiitwa anaitika. Likawa jina maarufu zaidi kuliko jina lake la Halfani Nassor.

Issa Musa aliagiza kikombe Cha kahawa akawa anakunywa taratibu akimsubiri Molio arejee. Mara akamshuhudia Molio akiwa kaambatana na yule mjamzito aliyekuwa kasafiri naye Toka Zanzibar, Mwamvita. Akashituka Sana. Alikuwa anampeleka wapi mjamzito? Mara nyingi biashara yake ilihusisha wasichana wadogo, miaka 12, 13, Hadi kumi na sita. Wasichana ambao kwenye biashara yao hiyo walihakikishia upatikanaji wa faida. Walikuwa Ni rahisi kuwarubuni na kuwatiisha chini ya genge lao kwa vitisho, madawa ya kulevya na hata kuwanyima chakula. Kazi yao kubwa ikiwa kuwaridhisha wanaume waliopenda kutoa fedha nyingi ili kuushiriki ngono na hao watoto.

Issa Musa Mara moja akabaini kuwa Mwamvita Yupo kwenye hatari. Lakini angemsaidiaje ikiwa genge Hilo lilijaa watu katili, wengi wao wakiwa ni vijana ambao waliendeshwa Kama maroboti. Hawakuwa na hata chembe moja ya hisi? Mjamzito? Hakuelewa.

Waliopotoka na kuingia na ndani ya Toyota Camry, Issa Musa akadhamiria kuwafuatilia ili afahamu kituo Chao kilikuwa wapi. Hakujua kwa Nini aliamua kujihususha na hili. Labda Ilikuwa ile historia iliyokuwa baina yao hapo awali. Uhusiano Kati ya Issa Musa na Molio, ulikuwa zaidi ya biashara. Walikuwa wapenzi hapo awali. Mahusiano ambayo alilazimika kuyasitisha baada ya kubaini nyendo ambazo hazikumpendezea. Kitu kilichomtia hofu zaidi Ni ukweli kwamba mwananmke huyo katili, alikuwa mtiifu Sana kwake na yeye alidhani alimmiliki. Na huo ulikuwa ni ukweli mwingine ambao ulimshangaza. Hata baada ya kugundua upande wa pili wa mwanamke huyo, alipoamua kuachana naye kimahusiano, Molio alimlilia, akamsihi asimuache. Akambembeleza Sana. Issa Musa alichanganyikiwa. Hakuwa ametarajia kuwa Molio angeendelea kujishusha kwake, alihofia kuwa mwanamke huyo angembadilikia na kumuoneshea makucha yake, haikuwa hivyo. Zaidi, ilionekana kuwa mwanamke huyo aliathiriwa vibaya kihisia na tangazo la kuachana Kwao.

Issa Musa alipolitafakari Sana suala Hilo, alibaini kuwa, mwanamke huyo alimpenda kwa dhati ya moyo wake. Lakini kwa Nini hakuwa tayari kuachana na 'Entry' ili wawe pamoja? Hapo ndio akagundua kuwa Huenda alikuwa ndani ya kundi Hilo kwa shinikizo. Mwanamke aliyempenda alikuwa Ni mateka, akitumikia kundi Hilo hatari kwa shinikizo kubwa. Kwa mapenzi aliyokuwa nayo Molio, kulikuwa na uwezekano wa kuachana na kundi Hilo, lakini uwezekano huo usingemhakikishia kudumu kwenye penzi lao. Wangempoteza. Issa Musa akajua, maisha ya mwanamke huyo yalishikiliwa na uwepo wake kundini, na kutoka kundini Ilikuwa kusaini mauti yake mwenyewe. Hakuwa na namna ya kumsaidia! Issa Musa akaumia Sana lakini baadaye akaamua kumtoa kichwani mwake na moyoni mwake.

Kumuona Tena hapa, ulikuwa mtihani. Mbaya zaidi, yule msichana mdogo, mjamzito, naye alikuwa anaingizwa kwenye genge hili hatari. Je angemudu kulitazama hili likitokea? Moyo wake ulijaa simanzi, akili yake ikamtuma kujaribu kuwasaidia watu Hawa. Huenda lingewezekana Sasa. Lingewezekana Kama angepata kampani ya mtu mwingine mwenye mapenzi na mmoja wa Wanawake hao, Mwamvita. Mwamvita alikuwa kamwelezea maisha yake ya kimapenzi na kijana Masu, akamweleza mvutano uliokuwepo Kati yake na familia yake ikimtaka aolewe na mzee umri sawa na wa baba yake, mzee Kisiki. Akakumbuka alivyomuuliza kwa utani wakiwa ndani ya ndege. 'Kwani huyo babu Ana sura mbaya kiasi gani, au Unadhani kazeeka haiwezi kazi?'
'Haha, we Kaka unalo lako jambo, maswali gani kuniuliza? Enewei, siyo mzee Sana, maana baba yangu mwenyewe SI mzee kihivyo, Ni miaka 45 hivi na Wala Hana sura mbaya hata Kidogo, nadhani wengi wanamuona mtanashati, Kumbuka Ana wake nane na Ni tajiri, isipokuwa moyo wangu umemwangukia msukuma mikokoteni ha!ha!. Lakini SI haba, tangu niwe na Masu maisha yake yamebadilika, sio msukuma mikokoteni Tena. Maisha yake yamebadilika na hivyo mie naamini Ni kwa sababu ya muunganiko wa nyota zetu. Na Nina amini atakuwa tajiri kuliko huyo babu! Kwa sababu nyota zetu zinang'ara zaidi tukiwa pamoja.'
Issa Musa akakusudia kumtafuta huyo Masu wawe kitu kimoja kuokoa Wanawake waliowapenda, ingawa hakuwa na hakika Kama Molio angekuwa tayari kuokolewa, hata hivyo, aliona Heri kujaribu.

Teksi iliyokuwa inalifuata gari la Molio, ambaye alijitambulisha kwa Mwamvita kama Mariamu, ilifika nje ya jengo lile la kifahari na kuzama ndani ya geti. Kulikuwa na kibao hapo nje chenye maandishi, 'Halfani Nassor residence', kulikuwa na CCTV camera na ili kutowapa mashaka waliokuwa nyuma ya camera hizo, akamwelekeza Dereva kuendelea mbele na safari. Tayari angekuwa na pa kuanzia.

***
Alipomaliza kuongea maneno Yale, Kisiki aliwaagiza watumishi wake kuhakikisha wanampatia huduma za nyota tano mgeni wake. Yeye akatoka huku akionekana kuzungumza kwenye simu na mtu ambaye Mwamvita alidhania kuwa anaweza kuwa Ni baba yake sheikh Abuubakr.

Aneth Ni binti ambaye alikuwa umri sawa na wa Mwamvita, Ni huyo aliyekuwa amepewa jukumu la kumhudumia Mwamvita. Mtoto wa kiafrika, mrembo kwa sura na umbo lakini mpole asiye na maneno mengi. Aneth alimtembeza Mwamvita ndani ya jengo Hilo akimwelekeza kila sehemu na matumizi yake. Mwamvita akabaini yeye hakuwa Malkia pekee humu ndani, mfalme Kisiki alikuwa na wake wengi nao waliishi humu humu ndani. Kwa Maelezo ya Aneth, wenzao watatu walikuwa wametoka kwenda kufanya shopping kwa ajili yake. Aneth, alikuwa Ni mke mwenza, Kama angemkubalia mzee Kisiki.

Kuna namna Mwamvita na Aneth walionekana kuwa na uelewano. Mwamvita akatumia fursa hiyo kuulizia Mambo muhimu. Aliyoambiwa yakamchosha na kumnyong'onyesha. Kulikuwa na hatari kubwa mbele yake.

2020
David Ngocho Samson
FB_IMG_1582711137383.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAZI YA MZUNGU 16

#Tulipoishia
Kuna namna Mwamvita na Aneth walionekana kuwa na uelewano. Mwamvita akatumia fursa hiyo kuulizia Mambo muhimu. Aliyoambiwa, yakamchosha na kumnyong'onyesha. Kulikuwa na hatari kubwa mbele yake.

KAZI YA MZUNGU 16

'Umesema tuko watano, vipi sioni mtoto mdogo hata mmoja humu ndani?' Mwamvita akamhoji Aneth.
'Watoto hawaishi hapa, alishawajengea jengo huko Dubai, huko ndiko wanaishi hao watoto. Ukishazaa, unanyonyesha mtoto miezi sita tu, anapelekwa huko Dubai, watoto hao hulelewa na kukuzwa na watu wenye mafunzo! Anadai watoto hao watakuja kuwa watu muhimu hapo mbeleni.'
'Na mnaruhusu Hilo litokee bila kukataa?'
'Utafanya Nini? Kwa taarifa yako, hapa utaishi Kama Malkia lakini Kuna Mambo utaona Ni Kama uko utumwani. Mzee Kisiki Ni mgonjwa wa akili nakwambia, maisha yake Ni ya kihuni Sana! Sijui ni Nini kinawafanya watu huko nje wamuone Kama Ni mtu mwema na kumpa heshima wanayompa. Lakini, hata ukijua huna Cha kufanya, Heri kuishi'
'Una maana gani?' Mwamvita akahoji kwa umakini.
'Ya Nini kuandikia mate ilhali wino upo, umefika, kuwa mstahimilivu, utajionea mwenyewe! La kukusisitiza dada Mwamvita, usijaribu hata Kidogo kufikiria kutoroka. Matokeo yake hutayapenda.'
'Aneth unanitisha!'
'Hapana, dada Halima alijaribu kufanya hivyo, akawasiliana na boyfriend wake, wakasuka mipango yao, bahati mbaya Sana, walimkamata huyo kijana, walimfanyia udhalilishaji mkubwa Sana. Halafu wakamwachia. Kijana wa watu alijiua mwenyewe. Huyu Kisiki Ni mtu mchafu Sana. Hafai.'
'Walimdhalilisha vipi?'
'Cha msingi Ni kutambua kuwa hafai, nisingependa kufafanua Sana huo udhalilishaji. Ah, labda nikueleze TU kuwa biashara zake ukiacha mahoteli ya kisasa, makasino, lakini pia anamiliki mitandao ya kusambaza picha za ngono. Hapo ndo ujue Ni udhalilishaji gani nazungumzia. Madawa ya kulevya, yaani biashara zote haramu, ndio Mambo yake.'
'Mh, mbona Haya Ni mateso Aneth?' Mwamvita alizungumza, akaona jinsi alivyokuwa kaingia kwenye shida. Akayakumbuka maneno ya mzee Kisiki, kwamba je alikuwa tayari kuukana utajiri na bado amkose mtu wake? Kisiki alikuwa kaweka kitisho chake bayana. Alimweleza kumkatalia Ni kukubali ujane. Maana kwamba mzee Kisiki alikuwa tayari kumuua Masu. Habari ya Aneth nayo Ni Kama ilizidisha chumvi kwenye kidonda. Udhalilishaji? Alipokumbuka ulinzi uliopo hapo nje, wale vijana walioongozana na Mariam, uwezo wa kifedha wa Kisiki dhidi ya Masu, Mwamvita akachoka. Alijua Nini Cha kufanya. Alimpenda Sana Masu kiasi Cha kutoruhusu baya limkute. Alimpenda mno asingempenda Tena! Labda mbeleni, Huenda baada ya muda angepata namna ya kumtoroka mzee Kisiki, lakini kwa Sasa mtego wa mzee Kisiki ulinasa windo lake na asingeweza kujinasua. Akili yake ikamweleza ili kumlinda Masu sharti anaswe kwenye mtego wa mzee.

***
Jioni,mzee Kisiki alirejea na wakeze watatu. Mahanjumati yakaandaliwa ya kiwango Cha mgeni rasmi. Mzee Kisiki akatumia fursa hiyo kumhoji Tena Mwamvita juu ya ombi lake.
'Ningependa nikutambulishe, ila sijajua bado msimamo wako. Kama utaona vema, naweza kukutambulisha Kama dada yangu kwa leo, Hadi utakapokuwa tayari kwa heshima ya mke wangu. Je, ungependa nikutambulisheje?' Mwamvita akapepesa macho, Kidogo apaliwe na kinywaji alichokuwa anakunywa. Akatafakari kile kitisho Cha mchana. Akamtamkia Kisiki kwa Sauti laini,
'Nimekuwa naliwaza ombi lako tangu tulipozungumza mchana. Kusema Kweli, labda Ni utoto TU ulikuwa unanisumbua. Siwezi kuacha nafasi hii muhimu unayonizawadia mzee Kisiki. Waliosema vya kale dhahabu hawakukosea. Kwa hakika naaamini mzee wangu Sheikh Abuubakr, aliona mbali kwa hili. Nipo radhi kuolewa nawe mpenzi' Mwamvita alizungumza, Hilo neno mpenzi likimkinai moyoni, alilazimika kulitamka. Akili yake ilimpa tumaini. 'Nafanya hivi kwa ajili ya mwanangu na kipenzi changu Masu. Nakubali hili ili nipate kujipatia muda wa kuweka mipango yangu sawa. Mzee Kisiki, kwa hili sitakusamehe kamwe, nitakufanya ujutie maisha yako'. Mwamvita alijiapiza moyoni. Usoni alionekana kutabasamu na kujawa furaha wakati Halfani Nassor aka mzee Kisiki akimtambulisha kwa ufahari kwa wake wenza.

'Haya tusikilizane kidogo' mzee Kisiki alitamka. Watu wote wakampatia masikio yao, akajikohoza Kidogo kurekebisha Sauti akiwa kasimama. Mikono ya kanzu yake kaikunja Hadi kwenye kisuguti. Alikuwa mwanaume jabali, mgumu Kama Kisiki, bila shaka kazi ya jeshi ilimfunza Vema kugangamara.
'Aneth, Samira, Halima na Eva, Leo tumepata ugeni, najua wote tuliutarajia, na Ni furaha yangu kumtambulisha kwenu mke wangu Mwamvita binti Abuubakr. Mwamvita dear, hawa hapa Ni dada zako, wake zangu Eva, Halima na Samira. Najua Aneth mmeshakutana na kufahamiana tayari. Kama uonavyo, hapa tunaishi kwa umoja na upendo. Ni matumaini yangu utaishi Vema na wenzako. Kwa leo, tumeonelea Vema tukibaki wanafamilia, lakini Kesho utatambulishwa kwa watumishi mbalimbali wa hapa nyumbani. Karibu Sana, cheers!' Akajinyanyulia glass yake ya wine na kugonganisha na ya Mwamvita, halafu zoezi likaendelea kwa wakeze wengine na wote wakigonganisha glass zao.

Mwamvita, alibaini kuwa wake wenza sawa na yeye hawakutofautiana Sana kiumri. Mkubwa wao Eva alikuwa na miaka 18, hao wengine walikuwa Ni miaka kumi na Saba isipokuwa Aneth, huyu alikuwa mdogo zaidi, miaka 16. Wote waliingia mikononi mwa mzee Kisiki kwa shinikizo la wazazi wao. Na wote kilichosababisha wajikute kwenye himaya ya Kisiki, Ni kule kutokujua kwao, kukimbilia mapenzi bila kujua Nini ingekuwa matokeo yake. Ule upole wao ukawaponza, wapenzi waliwapachika mimba na kulala mbele. Walipojikuta na mimba na kukimbiwa na wapenzi, mzee Kisiki alipendekeza kuwaoa, kuwaepusha na adha ya kunyooshewa kidole kwa kule kubeba mimba wakingali makinda. Lakini Kwani hiyo Ilikuwa dhambi kubwa Kiasi gani hata wajikute kwenye maisha ya kidhalili!

Sio Kama waliyafurahia maisha waliyoishi hapo, la hasha, walilazimika kuishi. Hawakuwa na namna nyingine. Kisiki alidhani walifurahia maisha aliyowapa. Akaufurahia ule ushirikiano wao. Hakujua tu. Walimdharau. Ushirikiano wao uliumbwa zaidi na ile Hali kwamba walilazimika kuwa naye. Ule ukweli kwamba hakuwepo aliyehisi wivu dhidi ya mwenzake kwa vile hakukuwa mapenzi ya dhati. Walimwigizia. Lakini pia ile tambia mbaya aliyofurahia zaidi mzee huyo, iliwafanya wakeze waishi naye kwa kuigiza ili kuepusha familia au watu wao na kichaa Cha mzee huyo. Kisiki hakuwahi kudhani kuua Ni kosa, kwake ilikuwa burudani TU kuunyofoa uhai wa mtu bila woga! Walimwogopa mno lakini haikupaswa kuwa bayana machoni pake. Hivyo, walimwigizia.

Alichokisema Aneth juu ya mzee huyo kuwa kichaa, Mwamvita alijionea usiku huo huo. Mzee huyo hakuwa na Soni hata Kidogo. Alikuwa chizi.

'Muda wetu tayari. Mke wangu mpenzi Mwamvita jiandae mama, Ni muda mwafaka ukutane na mumeo.' mzee Kisiki alitamka Kisha akaoneshà ishara kwa vidole vyake. Halima akatoka kwenda chumbani, aliporudi alikuwa na kamera mkononi. Video camera.

***

Issa Musa kutokana na safari zake za Mara kwa Mara huku Oman, na hasahasa jijini Salalah, aliamua kupanga kwenye apartment katika mtaa wa Al Muntanzah ili kupunguza gharama kubwa za kulala mahotelini. Apartment yake Ilikuwa ya wastani, ilimfaa Sana kwa maana hiyo. Pale alipokuwa hayupo, apartment hiyo ilifanyiwa usafi na kampuni la usafishaji Nyumba la jijini humo, maarufu Kama Clean Home Co. LTD. Kwa kawaida aliporejea, wafanyakazi wa kampuni hiyo walipata taarifa ili kuhakikisha anakuwepo mtu wa kukabidhi funguo. Alipofika alimkuta Ramla akimalizia usafi, wakasalimiana, akapata taarifa mbili tatu, Ramla akaondoka.

Issa akaweka mizigo yake, begi dogo lenye vitu vyake muhimu. Akafanya mawasiliano na wafanyabiashara kwa ajili ya kuweka Oda au appointment ya kuonana. Alipomaliza, akachukua kitabu Cha anuani, akatafuta jina Halfani Nassor residence. Akanakili namba ya simu. Akaiacha mezani na kishajara chake Kidogo. Akaingia bafuni kuoga. Baada ya mipango yake ya Kesho, alikusudia kupiga simu nyumbani kwa huyo tajiri Halfani Nassor walikoingia Mwamvita na Molio. Alitaka kufanya upelelezi wake kabla ya kuchukua hatua madhubuti kwa ule mpango aliokuwa anaandaa akilini mwake. Kuwaokoa Molio na Mwamvita.

Usiku ulipoingia, Issa alielekea kwenye mgahawa maarufu pale mtaani kujipatia chajio. Akiwa hapo, alimuona mmoja Kati ya wale vijana wa kiarabu waliokuwa na Molio wakati wanamfuata Mwamvita pale uwanja wa ndege. Issa akapata Wazo! Huyu lazima atakuwa na mawasiliano ya Molio. Tangu walipoachana na Molio, aliona Vema kufuta namba za mwanamke huyo. Wazo lake lilikuwa hatari. Alihitaji namba ya Molio, asingeweza kuipata hivi hivi. Asingeweza kumuomba kijana yule mwenye tattoo mikononi na shingoni. Angeweza kuipata kwenye simu ya kijana huyo.

Alijongea mezani alipokuwa amekaa kijana yule akiangalia mechi Kati ya Liverpool na Manchester. Alikuwa shabiki wa mashetani wekundu kutokana na rangi ya jezi aliyovalia.

'Ah, tayari mashetani washafanya yao?'
Issa alizungumza akikusudia kumvuta kwa mazungumzo kijana yule.
'Hatukawiagi sisi, mtu mbaya Pogba keshafanya yake.' kijana alijitapa. Wakaendeleza porojo zao za mpira na hatimaye akapata alichohitaji.
'Naitwa Ibra, nimefurahi kukufahamu. SI vibaya nikipata namba yako ya simu. Umesema Una biashara Zanzibar, Mimi hufika hapo Mara kadhaa, naamini nimepata mwenyeji'
'Kabisa kabisa. Issa ndio jina langu Kaka. Nipe simu nikuandikie namba yangu.' Ibra akimkabidhi bila wasi wasi. Issa Musa alipoishika simu ya Ibra moja kwa moja akaingia kwenye simu zilizopigwa. Akaliona jina la Molio. Akaikariri namba ile kichwani halafu akamwandikia namba yake Ibra. Alipomaliza zoezi Hilo, aliihifadhi namba ya Molio Kisha wakaendeleza soga zao za mpira. Liverpool walikuwa wamesawazisha kupitia penalti iliyochongwa vyema na kiungo mshambuliaji Salah.

Aliporejea kwenye apartment yake, Issa alimpigia simu Molio.
'Hallo' Sauti yake haikubadilika, Ilikuwa vile vile. Sauti tulivu isiyo na pupa. Kikawaida usingeamini mwanamke huyo alikuwa sehemu ya genge hatari kabisa la 'Entry'.
'Mambo vipi Molio, unazungumza na…'
'Najua, nikusaidieje?' Molio alimkatisha na kuuliza swali lililotafsiri chuki au kuchokwa kulikokinaisha.
'Nahitaji kuonana na wewe. Kuna Jambo…'
'Kinachokufanya uhisi Nina muda wa kupoteza na wewe Nin…'
Safari hii Issa aliamua kudinda. Akamkatisha kauli Molio na kuzungumza.
'SK apartments, no 23. Ukitaka Njoo ukiona vipi acha.' Issa akakata simu. Hakutaka mwanamke huyo amwendeshe. Alimfahamu Vema. Kubembeleza kungechelewesha Mambo lakini pia alijua kwa staili hiyo Molio angebaki njia panda. Angetaka kujua Ni Nini hicho kilichomtia kiburi. Na kusema Kweli, Issa hakuwa na hakika ya lolote. Aliamua kucheza patapotea. Kama asingetokea, angelazimika kupiga simu ya nyumbani kwa Halfani Nassor ili kupata mawasiliano na Mwamvita. Akaamua kupotezea swala Hilo, akawasha runinga ajionee yanayoendelea ulimwenguni.

Mwendo wa saa tano hivi, usingizi ukiwa unaanza kushika hatamu, akasikia hodi mlangoni. Akanyanyuka Taratibu, na kusogea mlangoni. Akachungulia kwenye kitasa. Nje alisimama Molio. Issa akatoa tabasamu na kufungua mlango.

2020
David Ngocho Samson
FB_IMG_1583317191932.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAZI YA MZUNGU 17
David Samson Ngocho

#Tulipoishia
Mwendo wa saa tano hivi, usingizi ukiwa unaanza kushika hatamu, akasikia hodi mlangoni. Akanyanyuka Taratibu, na kusogea mlangoni. Akachungulia kwenye kitasa. Nje alisimama Molio. Issa Akatoa tabasamu na kufungua mlango.

KAZI YA MZUNGU 17

Mlango ulipofunguliwa TU, Molio akaingia ndani bastola ikiwa mkononi. Issa Musa hakuelewa. Akashituka mno na kuhofia maisha yake.
'Unafurahi kucheza na hisia zangu sivyo? Unachonitaka Ni Nini? SI ushanikataa? Kunifuata fuata maana yake Nini?' Molio aligeuka mbogo. Alishajishusha Sana kwa mwanaume huyo, akambembeleza kwa magoti, lakini jamaa akajifanya kauzu.
'Siwezi kuwa nawe Tena. Labda uachane na Entry.' Ilikuwa kauli yake ya Mwisho. Kauli iliyomfanya Molio anyanyuke kimya kimya na kuondoka zake kwa unyonge. Alimpenda Sana Issa angeweza kufanya chochote kwa ajili yake isipokuwa kuachana na 'Entry'. Hiyo Ilikuwa ngumu. SI kwa sababu alifurahia Sana kuwa ndani ya genge Hilo. La! Bali kwa sababu alikuwa mtumwa, ambaye maisha yake yaliendeshwa na kundi Hilo. Alishajaribu kutoroka. Lakini daima walikuwa na namna ya kumpata. Na Mara zote walimpata akiwa nusu kaputi au kwenye maumivu makali. Wakubwa wa 'entry' walitumia teknolojia kuwaweka chini ya himaya yao daima. Akakumbuka jaribio lake la Mwisho.

Alikwisha fika Zanzibar na Kesho yake alikuwa apande boat kwenda jijini Dar. Kutoka hapo alikusudia kwenda kijijini Kwao huko Bukoba. Alikuwa amejiwekea vijisenti vya kutosha ambavyo angemudu kuweka duka la vinywaji na angeishi maisha ya Kawaida. Hakutaka Tena maisha ya kutumikishwa kufanya kazi iliyodhalilisha Wanawake. Lakini ilipofika saa Tisa usiku, akiwa hotelini, alianza kuhisi maumivu ya kichwa. Akaamka apate walau Panadol za kuyatuliza maumivu yale. Hazikusaidia. Muda ulivyozidi kwenda alihisi anapata wazimu. Macho yake hayakuweza kuona Tena, akajaribu kutoka akapate huduma ya daktari. Akaanguka chini na kuzima. Alipoamka, alikuwa Oman. Mara ya kwanza pia ilimtokea Hali Kama hiyo, akajua Ni ugonjwa TU. Alikuwa airport Salalah, wakamfuata hapo. Mara ya pili, ndio alibaini kuwa sehemu fulani mwilini mwake kulipandikizwa microchip ambayo ilimletea shida hiyo. Na zaidi pia, ilitumika kuwaonesha wapi alipokuwa ili wao wamfuate.

Hivyo, ombi la Issa Musa kwamba aachane na 'Entry' lilikuwa gumu kutekeleza. Asingeweza. Hakujua namna ya kujitoa kundini humo ikiwa waliyaweka maisha yake mkononi mwao.

'Hey hey hey, tafadhali Sana mpenzi, bastola hiyo' Issa Musa alitamka huku akinyanyua mikono yake juu, akirudi nyuma kwa kihoro.
'Nani mpenzi wako? Unacheza na maisha yangu? Unaona sawa kuchezea hisia zangu?'
'Ungenisikiliza kwanza Molio, hujui nimekuitia Nini, mbona Una maamuzi ya ghafla ghafla hivyo?' Issa Musa alikuwa kakifikia kiti pale sebuleni. Akajibweteka bwete bila kupenda. Jasho lilikuwa linamvuja usoni Kama kanyeshewa, Hali hiyo ikamfanya Molio afurahi moyoni. Kicheko kikaishia kooni. Akajikaza kukizuia na kuendeleza ubabe wake.
'Enhee umeniitia Nini?' akatamka Molio, akishusha bastola yake, Kisha akaangua kicheko.
'Hahaha, dah sijawahi kuona mwanaume mwoga wa kifo Kama wewe! haha!. Sijui hata nilikupendea Nini lol, mwonee!'

Issa alikuwa kalowa jasho. Alikuwa anahemea juu juu. Hofu yake Ilikuwa bayana. Tangu alipotambua uhusika wa Molio kwenye genge la Entry, alianza kumuogopa. Alifahamu ukatili wa watu hao. Hawakuwa na hisia hata chembe na ukatili Ilikuwa hobby yao. Walikuwa wanaweza kuua huku wakicheka, na Hadi ukifikie kifo, ulikuwa uwe umepitia mateso makali Sana. Watu wa entry hawakuwa binadamu, walikuwa maroboti. Majitu yasiyo na hisia za huruma Wala hofu ya kifo. Hicho ndicho kilichomtoa jasho. Vipi Kama Molio alikuwa keshafikia kiwango hicho. Na SI hatari zaidi kwamba alimtia chuki kwa kule kumuacha wakati yeye alimpenda?. Issa alikuwa taabani.

'Tafadhali Molio, plizz iweke mbali hiyo silaha.!'
'Mbona unaniogopa hivyo Issa, Ni Mimi, Molio. Unaweweseka Ni Kama umeona jini jamani! Huwezi kutaniwa?'
'Tatizo sio wewe mpenzi, unajua sikuogopi, shida Ni kwamba sijui Kama umekuja Kama Molio au Kama 'Entry'. Nawafahamu entry, wale Ni zaidi ya jini. Wanaogopesha. Na ulivyoingia hapa,kusema Kweli umeingia Kama entry. Umenitisha Sana!'
'Mh, Haya Basi, hebu nyanyuka bwana, Ni Mimi Molio, nimekuja kuitikia wito wako. Wasemaje Issa?' Molio akatamka kwa Sauti tulivu, ile Sauti aliyozoea Issa.
'Oh, Nahitaji maji ya kunywa, naona kiu.' Molio akamchukulia maji kwenye jokofu na kumkabidhi Issa.
Alipokwisha kunywa, wakaketi kwenye sofa, Molio akimfuta jasho kwa kitambaa chake. Issa akatulizana.
'Nimekumiss Sana mpenzi, nimejaribu kuwa bila wewe, siwezi. Nakuhitaji. Amini, kwa Kweli sitanii kabisa Molio' Issa alitamka. Muda wote akiyazungumza hayo, Molio alikuwa anamwangalia TU usoni. Hisia zikijijenga taratibu. Alimhusudu kijana huyo. Hivi Ni kwamba Jamaa alipokuwa akijieleza, Molio alikuwa anapiga hesabu itakavyokuwa muda mfupi ujao. Maelezo ya Jamaa aliyokuwa anaeleza Wala hayakuwa yanamfikia Molio. Alikuwa kazama kwenye ndoto zake kihisia.
'Molii' Issa akaita kwa Sauti, lakini kimahaba. Molio akazinduka. Akapanda miguuni kwa Issa wakawa wanatazamana Ana kwa ana, Molio akaishika shingo ya Issa wakakutanisha midomo yao. Ni Kama walikuwa na njaa ya mabusu. Maana Ilikuwa Kama wanashambuliana. Issa Musa akanyanyuka juu akiwa kashika chini ya makalio ya Molio kwa uthabiti. Akambeba na kwenda naye chumbani.

***
Ilikuwa ijumaa tulivu. Habari zilizohusika na kuvuma siku hiyo zilikuwa habari za matokeo ya kidato Cha nne. Masu alizisikia habari hizo akiwa jijini Dar es salaam. Miongoni mwa waliofanya mtihani huo ambao katibu mkuu wa baraza la mitihani alitangaza ongezeko la ufaulu kwa asilimia tano, alikuwa Ni mpenziwe Mwamvita. Mwamvita ambaye kwa siku ya pili Sasa alikuwa hampati kwenye simu Kama alivyokuwa kamweleza. Alikuwa na wasiwasi mwingi juu yake, lakini alipokumbuka kauli ya mrembo huyo kuwa Hilo la simu kutopatikana linaweza kutokea, alituliza mtima wake.

Aliingia mtandaoni na kugoogle 'matokeo kidato Cha nne 2018', akaletewa machaguo mengi kutoka kwenye websites na blogs kibao. Akaamua kutambaa na website ya NECTA, alipoingia hapo, akaona link iliyokuwa na maandishi yenye wino mwekundu yakianza na neno 'new', matokeo kidato Cha nne 2018. Akaibonyenza. Link ikafunguka. Kwenye search, akaandika Maji kupwa sec. Jina Hilo likatokeza na yeye akalibonyeza, matokeo ya Maji kupwa yakaonekana barabara. Kwenye summary pale juu ya ukurasa huo, ilionesha Shule ilifaulisha wanafunzi 00 kwa daraja la kwanza, yaani Div I, Watano Div II, 59 Div III, 168 Div IV, waliopata zero, walikuwa 92 na watoto 34. Akajiuliza Mwamvita atakuwa kundi gani. Hiyo ikamtia mshawasha wa kutaka kuyajua matokeo ya mkewe tarajali. Akatafuta namba ya mtihani ya Mwamvita, namba 167. Akatabasamu, Mwamvita alikuwa miongoni mwa wale waliopata Div III, ya kwake ikiwa inang'ara kwa point 21, Ni kusema alikosa point moja tu, kupata Div II. Akachukua simu yake ampigie Tena Mwamvita, hakupatikana. Akaazimu Kesho yake kuingia Zanzibar.

Kama kawaida, Masu alipoingia Zanzibar, alimtafuta msela wake Yusuf, akamweleza anataka wafike ukweni. Yusuf akatinga suruali ya kitambaa nyeusi na shati jeupe na kiatu chake Cha mchongoko. Ile gari ist, ilikuwa hapo kwa Yusuf, kamanda Masu alimwachia bila kinyongo apigie misele. Na watoto wa kike walimkoma kwa siku tatu hizi alipokuwa na gari hiyo. Alipotoka nje, aligundua gari hiyo Ilikuwa na vumbi kutokana na misele hiyo. Kama akiipeleka car wash, atamchelewesha rafiki yake. Ilionekana Masu alikuwa na furaha kubwa Mwamvita kufaulu mtihani. Alitaka awashirikishe, au kuwa sehemu ya furaha ya famia yake. Alikuwa keshapiga simu kwa Sheikh Abuubakr na kumweleza kuwa wangefika hapo kwa mazungumzo. Sheikh Abuubakr akauliza muda gani, Masu kwa furaha Sana akamweleza saa Tisa alasiri. Miadi ikakubalika!

Sasa, Ilikuwa yapata saa Tisa kasorobo. Master Park Hye alishawafundisha kufanya Mambo kwa muda, Yusuf akaona heri wakienda na piki piki yake aina ya Kapoor, ile iliyotumika pia kwenye tukio kwa Nzinyangwa tapeli. Walipokutana, wakashangaa kujiona wamevaa sare. Ungedhani walipanga hivyo. Walipendeza SI Kidogo. Watanashati wawili.

Waliingia kwa Sheikh Abuubakr saa Tisa kamili. Wakakaribishwa. Chakula kilikuwa kimeandaliwa na Mama Mwamvita akishirikiana na dada wa kazi. Sheikh Abuubakr alikuwa kaalika wazee wenzake watatu, mzee Abdalla, mzee Juma na mzee Khamis. Wote majirani zake. SI haba kwamba wao pia walikuja na wake zao. Basi ikawa Kama sherehe hivi, maana wamama wale wa kizanzibar, walipiga vigelegele Masu na Yusuf walipoingia na sare zao. Mazungumzo yakashika hatamu, Masu akaeleza mpango wake wa kuhakikisha Mwamvita anaendelea na masomo ya kidato Cha tano baada ya kujifungua. Wazee wale wakamsifu Sana kwa uungwana huo. Ilikuwa furaha. Ila, Kuna vile Sheikh Abuubakr alionekana kukaa tenge Sana, akawa yuatazama Sana getini muda mwingi, na Hali hiyo Yusuf aligundua. Mlango wake wa fahamu, ule wa sita waliofundishwa na Master Park Hye, ulikuwa unampa taarifa. Lakini, ah, akaamua kujumlisha na kugawanya, akapata sawa sawa na wasi wasi wa bure. Yaani akahisi kuwa,Huenda mzee huyo alikuwa tu na mchecheto wa kawaida.

Mara, akamuona Sheikh Abuubakr anaomba udhuru Kidogo. Akatoka nje ya geti. Mh! Alamu kichwani kwa Masu ikagonga kengele. Hataa! Kuna Jambo. Haiwezekani. Akamnong'oneza Masu.
'Ebwanaee, mkweo mbona simusomi, simwelewi walahi'
'Ah Yusuf mtu wangu, unakuwa aleti muda wote. Tulizana. Huyo atakuwa kuna mgeni anamtarajia Sema kachelewa kufika. Hapo ameona heri ajue Kulikoni. Atakuwa kaenda kuchungulia Kama yuakuja na asipomuona, atamrukia hewani.'
'Yaa, Hilo litakuwa Hivo bila shaka'. Yusuf akaona heri kulipotezea. Wakaendelea kujichana kwa kuku, pilau, soda, roast ya nyama, mboga mboga, Jamaa, mamkwe mpishi nyie!

Sheikh Abuubakr akarejea. Wasiwasi ule aliotoka nao, alionekana kuutua huko huko nje! Ile sehemu iliyokuwa wasiwasi Yusuf akaona ridhiko, yaani Kama vile kulikuwa na uhakika na SI mashaka Tena. Chochote alichofanya huko nje, kilimpa tulizo la moyo, moyo ukatuama. Lakini Hali hiyo, kwa Yusuf iliamsha Tena wasiwasi wake maradufu. Akamsogelea Tena Masu na kumnong'oneza,
'Kaka, kaa kikamanda, nna uhakika mzee wako bado ana gubu, Kuna kitu hapa hakiko sawa, nahisi harufu ya Shari. Huyu mzee wako sijawahi kumwamini toka alipokutandika bakora hapahapa.'
Wakati anamalizia kuongea, Masu akiwa anataka kujibu hoja, kukasikika hodi getini.
Huyoo!
Sheikh Abuubakr akakurupuka kwa Kasi ya kimbunga. Akaelekea getini. Hata Masu Sasa akajua hapa Pana msala. SI kwa haraka ile aliyosimamia mzee Abuubakr. Vijana wakakaa mguu sawa!
Ah! Jamaa!. Masu na Yusuf wakamuona mzee anarudi, nyuma yake walikuwa wajomba. Askari wa jeshi la polisi wanne. Ule muungurumo wa gari nje, Kumbe Ilikuwa defender la polisi. Sasa Sheikh Abuubakr alikuwa anawanyooshea kidole chake, na Sauti yake ilisikika barabara.
'Huyo mjinga kamtia mimba binti yangu, Sasa kamficha sijui wapi, na anathubutu kuja hapa akitaka amuoe, binti mdogo, mwanafunzi wa skuli Hapo maji kupwa. Nataka muwashughulikie vizuri na washitakiwe kwa kosa la ubakaji na utekaji!' Sheikh, Sauti yake ilitoka kwa Sauti ya mrindimo mithili ya subwoofer, mishipa ikimsimama barabara shingoni. Povu Kama lote. Na alionekana kubadilika rangi ya ngozi yake usoni, alifura na kuwa mwekundu, Kama mtu anojaribu kujizuia asibanje! Kijasho chembamba kikimshuka kwenye pua yake ndefu!

Hakika ulikuwa mshituko mkubwa Sana. Mama Mwamvita Kiasi azimie, wazee wenzake,Sheikh, majirani waliokuwa a furaha muda mfupi uliopita, walibaki vinywa wazi kwa mshituko.... Kilikuwa kisanga Cha aina yake.

2020
David Ngocho Samson
FB_IMG_1583317191932.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
KAZI YA MZUNGU 18
David Ngocho Samson
0629077792

#Tulipoishia
Hakika ulikuwa mshituko mkubwa Sana. Mama Mwamvita Kiasi azimie, wazee wenzake,Sheikh, majirani waliokuwa a furaha muda mfupi uliopita, walibaki vinywa wazi kwa mshituko.... Kilikuwa kisanga Cha aina yake.

KAZI YA MZUNGU 18

Masu na Yusuf, waliona kumekucha. Sheikh Abuubakr alikuwa kafanya kosa kubwa Sana ambalo angelijutia. Kosa ambalo, asingemsamehe. Hii Ilikuwa Vita. Waliwatazama wajomba wakijongea, mmoja alikuwa na kitambi kikubwa, bila shaka huyo akiwa kiongozi wa wale wengine. Wale watatu, walionekana vijana shababi. Damu ikachemka mishipani mwa Masu na Yusuf. Wakaona ushindi upande wao, wasingekubali kwenda kituoni. Hawakuwa na muda wa kuozea jela. Walipaswa kuchomoka.

'Hii ni amri halali ya jeshi la polisi, Masuke Masuke, upo chini ya ulinzi wa jeshi la polisi kuanzia Sasa, lolote utakalozungumza au kutenda litatumika dhidi yako katika mahakama tukufu. Unayo haki ya kukaa kimya!' Afande bonge, mwenye kitambi alitoa tangazo Hilo kwa Sauti kubwa ajabu, hawakuamini Sauti Ile ingetoka kwenye koromeo lake.
Masu akainua mikono juu. Askari wale wakamsogelea wakiwa na pingu mkononi. Mmoja Kati ya wale shababi, akaushika mkono wake wa kulia ili aurudishe nyuma, apigwe pingu.
Kosa!
Jamaa alikula kipepsi Cha kilo nne, akaanguka chini na kuzima. Kipepsi kile kilimpata sawasawa, kwenye Taya yake ya kushoto na kumtenda ubaya. Tayari Masu alikuwa kesharuka na kukamata koromeo la Askari mmoja huku guu lake la kushoto lenye ujazo wa heavyweight kickboxer, likitua kwenye utosi wa Askari yule kibonge, mfupi Kama kiroba cheusi Cha Laura Pettie, Askari yule akamwagika chini kwa style ya msamba. Yusuf, alikuwa keshamdaka Askari aliokuwa kasalia na kumketisha chini kwa ngwara moja mujarab. Akamkalisha chini kitako. Askari Hawa hawakutarajia Haya. Bunduki moja waliyokuja nayo Askari Hawa, Sasa Ilikuwa mikononi mwa Masu. Masu alikuwa amechafukwa roho, mama Mwamvita yeye alikuwa keshazima kitambo, akina mama jirani walikuwa hapo chini ya mnazi wakimpepea.

Sasa Masu alikuwa anamfuata Sheikh Abuubakr, mzee huyo alikuwa kalowa jasho, na sina ushahidi Kama chini ya miguu yake lilikuwa jasho au mkojo, sina hakika ya Hilo, isipokuwa, naweza kukueleza kinagaubaga msomaji wangu, kwamba, kulionekana doa kubwa Sana kwenye kanzu ya mzee huyu eneo Hilo la uzazi! Alikuwa anatetemeka Kama mgonjwa wa degedege.

'Oya Yusuf, mlete huyo mjomba anayepumua bado, nataka achukue ushahidi mpya hapa.' Masu aliunguruma. Askari watatu waliopitia mkononi mwa Masu, wote walikuwa nusu kaputi, wakibarizi kwenye korido za akhera pamoja na waliotangulia huko. Hata hivyo, Masu alijua watarejea tena baada ya muda wa saa moja ama mbili. Wakati huo, wao wangekuwa wamefutika hapo nyumbani kwa baba mkwe.

'Kwa hiyo mzee, muda wote ulikuwa unatuigizia?' lilikuwa Swali kutoka kwa Masu kwenda kwa Sheikh Abuubakr. Mzee huyo alitia huruma SI Kidogo, alinywea, akawa macho kayalegeza Kama mbwa mwoga, Ameloa. Akajaribu ainue macho yake amtazame Masu, aibu ikamjaa.
'Nisamehe mwanangu!' akatamka mzee Abuubakr.
'Haya Yupo wapi Malkia wangu?, siku ya tatu hii simpati kwenye simu, SI kawaida yake, Hadi Sasa angekuwa keshafanya mpango tuwasiliane. Nataka majibu haraka iwezekanavyo, sina muda wa kupoteza, na usijaribu kuleta ujuaji.'
'Nitakueleza. Nakuomba tu, usinidhuru mwanangu.' Sheikh Abuubakr alizungumza kwa sauti iliyosheni kitetemeshi.
'Hilo wewe ndio mwenye maamuzi nalo mzee, tupe ukweli, na sisi tuendelee na shughuli zingine.' Yusuf akachomekea.
'Mwamvita Yuko Oman kwa mzee Kisiki. Mtaa wa Umm Al Ghawarif, Nyumba namba 27890.. Halfani Nassor residence.' Sheikh akaitoa Siri.
'Uufunge mdomo wako, sio nisikie Tena umemjulisha huyo mpuuzi mwenzako Kama tuna habari zake,hakika sitakuacha Salama baba mkwe!' Masu akamweleza Sheikh Abuubakr, halafu akamgeukia Askari.
'Waitwa Nani Afande?'
'Haji, Haji Hamduni' Mjomba alijibu haraka haraka Kama anayeomba po!
'Umemsikia mzee Abuubakr mwenyewe akikiri kuwa alitaka kutubambika kesi ilhali yeye mwenyewe ndio kamwoza bintiye kwa huyo mzee mwenzie, Kisiki. Sasa nisisikie Tena kuwa mnanifuatilia Mimi. Haki ya mama naapa, nitakukata pua. Hao wenzako wataamka Kati ya saa moja hivi Hadi mawili. Waambie wasinitafute. Imeshaisha hii habari, sawa?'
'Sawa, Afande!'
'Mimi sio Afande wewe, jiangalie.' Masu akatamka kwa bezo.
Wakamkabidhi bunduki ile, nao wakatoka zao, kwa mbali wakimuona mamkwe akiwatazama walipokuwa wanapotelea getini.

***
Mzee Kisiki, mtu dhalili aliwasha runinga na kuweka picha chafu. Akamkurubia Mwamvita na kuanza kumpapasa. Mwamvita machozi yakatengeneza mifereji miwili mashavuni mwake. Uvumilivu ulipomshinda, akaangua kilio Cha mtoto mdogo. Wakati wote hayo yakiendelea, wakeze Kisiki walikuwa hapo, mmoja akirekodi huo uchafu aliotaka kuufanya mzee Kisiki kwa Mwamvita.
'Nini unalia Sasa mke wangu Mwamvita, Nini kinakuliza?' mzee Kisiki akajifanya anauliza kwa mahaba. Kuwa eti Sasa anambembeleza mpenziwe.
'Naumwa, tumbo linaniuma sana mume wangu.' Mwamvita akajibu huku mzee huyo akijifanya kumfuta machozi.
'Bado Kidogo nitajifungua, nivumilie Hadi hapo, kwa Sasa sitakufurahisha mume wangu.!'
'Ah, hapo ndio Unataka kunichafua roho yangu, na hizi hamu zangu kwako nazifanyaje Sasa? Halafu siku hizi hakuna hakika sana Mambo ya uzazi yanavyosumbua, ukafa wakati wa kuzaa Mimi nitalala na maiti?' kauli hiyo ikamkata maini mwamvita, SI yeye pekee aliyeshitushwa na kauli hiyo, wakeze wengine pia walishituka mno.
Kauli hiyo, ikamfadhaisha Sana Mwamvita na kuushitua moyo wake. Mapigo ya moyo yakabadilika, yakatoka kwenye mdundo wa kawaida, sasa yakawa Kama yanakimbia mbio za meta Mia. Mara, hee! Mwamvita kalegeza macho, mwili ukanyong'onyea, asingekuwa Aneth kaona Hali hiyo, Mwamvita angepigiza kichwa chake kwenye marumaru iwe historia. Alimwahi na kumdaka, wakati mzee Kisiki alishangaa Nini kimetokea.

Mwamvita alizimia. Aneth akamuomba Kisiki amtoe nje kwenye upepo kumpepea. Kisiki akamruhusu, na Kama vile hakikutokea kitu, akamvuta Eva mkono, akamvua nguo kwa staili ya kuichana. Mzee huyo bila kujali Nini kimetokea kwa Mwamvita akaendelea kumbaka mkewe Eva, huku Halima akirekodi kitendo hicho. Huo ndio uchafu aliojaa mzee Kisiki. Ukichaa aliousema Aneth. Kwa mzee Kisiki, hiyo kwake Ilikuwa peponi. Aliamua kujitengenezea pepo yake hapa hapa duniani. Ya Nini kusubiri wale mahurulain wa peponi, wenye macho yenye haya, makubwa, ya kurembuka, na ya mahaba, macho ya mfano wa lulu, mazuri, ya kuvutia, ikiwa hapa hapa angeweza kujipatia. Tena wasichana wabichi waliokwiva? Na kusema Kweli, Kisiki hakuwachukua mabinti alimradi, alijua kuwachagua wale wenye mvuto na sifa kama za mahurulain. Alijua kwa maisha yake maovu, pepo asingeingia kamwe, ndio chanzo Cha kujijengea ngome hii, na kujitafutia mabinti mfano ya mahurulaini. Pesa zake akizitumia Kama silaha ya kujilinda. Polisi ya Salalah Ilikuwa na habari ya vitendo vyake, polisi ya Zanzibar pia, Dubai na kwingineko alikowekeza mzee huyo. Ajabu alisifika Sana na kusujudiwa na baadhi ya watendaji wa idara hizo. Akaandikwa kwenye magazeti kwa misaada aliyotoa kwa taasisi mbalimbali maeneo tofauti tofauti. Mtu mwema, mcha Mungu, kanali mstaafu aliyetukuka!

Mwamvita alilala nusu kaputi kwa masaa mawili. Alipoamka, alikuwa amechoka Sana. Mathalani, alishindwa hata kusimama mwenyewe na kumlazimu Aneth kumuegamisha kwenye bega lake ndio waingie ndani. Usiku huo, hakuonana Tena na mzee Kisiki. Kesho yake pia, hakumuona mzee huyo. Akafurahi, maana Hakuna kitu Mwamvita aliogopa Kama mzee huyo kutaka kumwingilia. Alihisi lingekuwa kosa kubwa Sana kumtenda mwanae aliyekuwa tumboni mwake. Alihisi angemnajisi kwa kitendo hicho. Siku ya pili pia ikapita. Alikuwa yuashinda ndani na kila alipopata nafasi, alitumia kumuomba Mungu amwepushe na mikono ya mzee Kisiki. Hakuruhusiwa kutoka nje ya geti. Mwamvita angeamka, azurure ndani ya fensi ile akiota ndoto za mchana. Kuna wakati aliota ameota mabawa halafu amepepea Kama kipepeo na kutoka ndani ya fensi ile ndefu na kutua zake Zanzibar. Halafu Kuna wakati pia aliota Masu ameingia Oman na kumtandika ngumi ya pua mzee Kisiki halafu kuwaokoa yeye na wale wake wenza. Wakati mwingine, aliota Mungu amejibu maombi, amemtandika radi mzee Kisiki amepooza mwili. Aliendelea kuota na kuota, akaendelea kuomba na kuomba.

***
Alfajiri Sana, Issa aliamka kwa ajili ya swala. Pembeni yake alikuwa Molio kalala kama mtoto mdogo. Issa akamtazama msichana huyo na kutabasamu. Alimpenda. Akajiahidi moyoni mwake. Lazima, lazima amtoe huko kifungoni. Aishi naye Kama mkewe halali. Akatandika chini kizulia chake Kidogo ambacho Mara nyingi alitembea nacho kwa ajili ya kufanyia ibada. Akasujudu na kusali. Alipomaliza, akatoka Hadi jikoni, akapasha Moto slesi za mikate, akachemsha maziwa, akachukua box la cornflakes, akaweka kwenye kisinia na kwenda nacho chumbani. Huko akamkuta Molio mrembo, Yupo macho sema kajilaza tu kitandani.
'Ohoo, ushaamka babe!'
Molio akajinyoosha hapo, akaunyoosha mkono na kumshika begani Issa aliyekuwa Sasa kaketi pale kitandani.
'Umeamka mapema Sana mpenzi, nilikuwa nataka kupiga yowe la kuomba msaada kwa majirani'
'Msaada gani?' Issa akamhoji
'Kama wamenionea mpenzi wangu mzuri, mweupe mwenye kamzuzu kidevuni. Mrefu na mwenye kujua kuninyoosha chumbani'
'Hahaha, chizi Kweli wewe, ungewaambia hivyo majirani?'
'Ah wapi, niwaambie waanze kukuwinda uwanyooshe, aku!' Molio akatamka hayo huku akibetua mabega yake kukana.
Issa akamsogelea na kumbusu Molio shavuni.
'Nimekuandalia breakfast maridhawa. Haya kaa vizuri nikuone unavyokula breakfast yako'. Issa akamweleza Molio.
Kama alivyofanya awali, Molio akayabetua mabega yake kukataa.
'Nataka breakfast wewe kwanza.'
Issa akaondoa sinia kitandani na kuliweka juu ya meza. Akamrukia Molio kitandani.
'Umekuwa na tabia mbaya Sana. Nataka nikufunze adabu.'
'Ndiyo mwalimu, nataka unichape viboko nikome' Molio akatamka kwa sauti ya kumtoa nyoka pangoni. Ukafuatia mtanange wa hatari, mwanafunzi akachezea viboko. Akashika adabu yake.. Halafu wakapata breakfast. Issa Musa akaona huu waweza kuwa muda mwafaka wa kuzungumza na Molio juu ya mpango wake.
'Mpenzi, nimekuwa natafakari Sana siku za karibuni. Sitaki Mimi na wewe tukae mbali. Nataka kukuoa Molio'
'Asante mpenzi, lakini usinambie kuachana na Entry.!'
'Halafu mpenzi unajua sijajua hasa kwa Nini huwezi kuacha kundi Hilo?'
'Kwa sababu mpenzi, nilishajaribu Mara nyingi na nimekuwa nashindwa. Siku nitakapoamua kuachana nao, hakika nitakufa.'
'Mbona uwe na hakika na Jambo Kama Hilo?' Issa akauliza kwa hamaki.
'Mpenzi, hao watu, Ni hatari Sana, na ili kuhakikisha nakuwa mtumwa wao daima, mwilini mwangu sijui wapi, ila walishaweka microchip ambayo, wakiiamrisha huko waliko, hunipa mateso makubwa. Wakiamua kuniadhibu utanihurumia dear, wakiamua, wanaweza kuniua kwa mateso. Ingekuwa zamani, ningesema nimetupiwa jini wallah!'
'Umefanya vyema kunieleza. Nina hakika Hilo suala naweza kulimudu. Nilisoma na Jamaa mmoja UK, kwa Sasa anafanyia kazi kampuni moja ya kimarekani, inaitwa 'Amchip', ushawahi kuisikia.?'
'Hataa!'
'Hiyo kampuni imeingia ubia na serikali ya Sweden kwa ajili ya kupachika microchip kwa wagonjwa, wazee na watoto, kwa ajili ya kujua taarifa zao za afya na hata kujua walipo ikitokea wamepotea. Nikimpigia simu, Ni fasta, ataweza kutusaidia kujua ilipo na kuiondoa halafu kuiharibu kabisa. Unaonaje Wazo Hilo?'
'Ooh mpenzi, unaweza kufanya Hilo?'
'Nakupenda, naweza kufanya chochote kwa ajili yako mpenzi'. Molio akamrukia na kumkumbatia kwa nguvu Issa. Wakajipata Tena kitandani.
Mara, saa mbili asubuhi ikawakuta bado Wapo kitandani. Wakiwa wamelala fofofo Usingizi.
Simu ya Molio ilipoita, ikawaamsha. Loo! Walikuwa wanachelewa. Wakaingia bafuni kuoga, wakavaa haraka. Wakatoka.
'So nitawasiliana na Yaraslav, tukutane jioni kwa mrejesho. Halafu, kuna yule dada.. Ah, hebu tutamuongelea ukirudi' Issa akaongea. Walikuwa wanashuka ngazi toka orofa ya pili ilipokuwa apartment ya Issa Musa.
Yaraslav, ndio jina la rafikiye waliyesoma wote. Mtaalamu wa masuala ya hizo chip, raia wa Urusi.
'Dada gani, niambie Sasa hivi!' Molio akawaka Moto wa wivu. Habari za wadada na mpenziwe hakutaka kuzisikia.
'Ok,Kuna dada mlimchukua uwanja wa ndege, anaitwa Mwamvita, nilisafiri naye toka Zanzibar, akanambia anakuja huku kwa Shangazi yake aitwaye Amina. Sasa nilikuona ukimchukua,Mara moja nikajua ameshauzwa huyo. Ni mjamzito for God's sake. Nakuomba uhakikishe usalama wake kipenzi.'
'Ahaa, sawa. Nishamfahamu. Usisahau tafadhali kuwasiliana na Yara.'
'Siwezi kusahau, Jambo Hilo Ni la muhimu zaidi kwangu. I love you babe' Issa alimwambia Molio. Tayari walikuwa wameshashuka toka orofani walikokuwa. Issa akielekea kwenye miadi aliyoweka tangu Jana yake, na Molio akienda ofisini,. Jirani na jengo la Halfani Nassor, ndiko kulikuwa na ofisi zao za entry, lakini walisajili ofisi hizo kwa jina la kampuni iliyojishughulisha na usafirishaji mizigo.. 'Transport Asia world-wide'.
______________________________________

Haya Basi mpenzi na shabiki wa KAZI YA MZUNGU, Naomba nikushukuru Sana kwa kwenda nami Hadi hatua hii. Kampani yako Ni muhimu Sana. Shukrani za pekee kwa wale mlio-like na ku-comment na kwako wewe uliyependa Kimya Kimya. Nachojua, Ni kwamba sote tuliosoma KAZI YA MZUNGU Hadi hatua hii, Kuna kitu tumepata.
Bado hatujaijua KAZI YA MZUNGU Ni kazi gani, tunajua Kuna hotel yenye eneo la Siri chini ya ardhi, tunajua Kuna wazungu wanatafuta vijana na kuwapa mafunzo ya kijeshi na kiintelijensia. Hatujui kwa Nini. Tungependa kujua undani wake, sivyo? Lakini pia tungependa kujua hatima ya wahusika wetu Masu na Mwamvita, Molio na Issa.
Basi kaa tayari kwa ujio wa kitabu Cha kazi ya Mzungu kitakachokujia mwishoni mwa mwaka huu/mwanzoni mwa mwaka 2021 tukijaaliwa wote kuwepo.

Napenda pia kutumia fursa hii kukutangazia ujio wa vitabu vyangu viwili, Mateka wa Huba na Tineja. Ni vitabu makini Sana. Napokuandikia, huwa nataka uburudike lakini zaidi, upate kitu kinachokufanya utafakari na kuelimika. Vitakuwa madukani mwezi wa sita 2020. Usikose!

Kitabu Cha Tineja, Ni kitabu ambacho kinazungumzia changamoto zinazokabili matineja. Kinamfaa mzazi mwenye Tineja na matineja wenyewe lakini kinakufaa wewe pia Kama mwanajamii. Kitabu kinachoweza kusomwa na watu wa Rika zote.

'Kitabu Cha mateka wa Huba ni Crime Story(Simulizi ya uhalifu), Kuna upelelezi ndani, mapenzi, ushirikina na msamaha. Imejikita kwenye maisha yanayomzunguka tajiri Baltazar Chomo, billionaire mwenye ushawishi mkubwa lakini ambaye upendo wake kwa mke wa kijana Sanga, aitwaye Maimartha, kijana toka familia maskini, unakuwa mwiba unaomkwamia kooni. Je Nini hatima ya penzi Hilo la hila? Msome David Samson kwenye Mateka wa Huba. Hiki kitabu Ni Moto.'
Maneno ya Mhariri wangu Joseph Kyando.

Endelea kufuatana nami kwa Simulizi mpya inayofuata. 'Siri ya marehemu'

Itapendeza Sana Kama uta- share bandiko hili kwenye magroup yako ya fb, na hata WhatsApp. Pia alika marafiki wajiunge na group letu la Simulizi za King David (Ngocho).
Asante Sana.

2020
David Ngocho Samson
0629077792 (WhatsApp)
FB_IMG_1583317191932.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
dah nikafikir goma linaendelea nimekuja mbio hizo
 
Amani kwenu ndugu zanguni.


Namshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na Pendo. Kwa neema zake, hatimaye nimekamilisha ahadi niliyowaahidi ya kuwaleteeni kitabu cha MATEKA WA HUBA ifikapo June. Nilitarajia kingetoka mwanzoni mwa Mwezi huu lakini si vibaya, bado lengo la kukitoa Mwezi huu limekamilika.


Basi nikuombe uchukue hatua ya kujipatia nakala yako, uburudike, uelimike na pia uwe sehemu ya kuchangia juhudi zangu kama mwandishi wako


Vitabu vinapatikana

Kona ya riwaya Kinondoni B - 0655428085/0784122598


Posta opposite na Sanamu ya Askari( Kwa George) - 0755454152


Kwa mr.Nakale, Meza ya vitabu Katikati ya Azania na Posta benki, Mtaa wa Samora na Makunganya. - 0715451711


Pangoni, mcheki mwalimu Gamba, atakuletea ulipo utachangia nauli kidogo - 0714839430


Joint aka Kiroboto 0717301966 atakuletea ulipo kwa makubaliano maalum juu ya nauli.


Fred 0625569652, atakuletea kwa kuchangia nauli kidogo.


Ununio come and read bookstore 0717978899


Kariakoo 065227777/0653799999


MIKOANI VITAPATIKANA KUANZIA JUMATANO TRH 17/06


ARUSHA 0757690302/0686965223/0656744390 NJE YA JENGO LA KIMAHAMA.


IRINGA -LUTENGANO BOOKSHOP 0736361984/0767361984


MOROGORO - MARCUS MPANGALA 0717226293


KILIMANJARO - Piga simu 0719867477


RUKWA - NIPIGIE KWA NAMBA 0629077792/0744509465


MWANZA - 0689074051


SHINYANGA - 0752571571/0713563703


BEI NI TSH 10,000/=TU



KWA MAWASILIANO ZAIDI 0629077792/0744509465

DAVID NGOCHO SAMSON


SAMBAZA UPENDO, SHARE KWA MARAFIKI WENGI UWEZAVYO NA UBARIKIWE SANA.


FB_IMG_1592108536669.jpg
FB_IMG_1592503261560.jpg
FB_IMG_1592503228240.jpg
 
KAZI YA MZUNGU 19


'Mwanangu ee, mie nitalazimika kwenda zangu huko Oman, sijawahi fika huko, lakini naamini Siwezi kishindwa kitu, elimu tuliyopata kwa Steve Curl, inatosha kwa kila kitu. Sheikh amenifanyia upuuzi Sana, aombe nimkute Salama Malkia.'

'Dah, itabidi iwe hivyo. Vipi, hutahitaji kampani yangu? Nimezipata za chini ya kapeti, yule dingi ni kanali mstaafu na anamiliki genge la uhalifu. Kwa maoni yangu, Ni Vema Zaidi tungechimba kwanza Intel muhimu, lakini dah, muda nao Ni muhimu kuuzingatia. Mchezo ukiisha mapema Ni uhakika kuliko kuchelewa.'

'Kampani yako Ni muhimu, ila nitakuomba itokee hapa. Utakuwa unanijulisha baadhi ya Mambo, hivyo Nikuombe Sana uchukue jukumu la kuchimba habari zozote unazoweza kumudu juu ya mzee Kisiki na genge lake. Hizo zitanirahisishia zoezi langu au vipi mwana?'

'Hapo mzee baba hapo ndio penyewe, unajua, Kama ningebahatika kwenda University, ningeenda kusomea masuala ya inteligensia ya mitandao na computer, ningehack CIA ya Marekani iwe tiketi ya kuajiriwa nao, na Kama wangezingua, ningemcheki hata mchizi kiduku pale Korea kaskazini. Ah,dunia ingelitambua jina la Yusuf Shemdoe, ningekuwa maarufu kuliko bin Laden mzee baba, nakuapia Tena!'

'Hata Sasa nakuaminia Sana mtu wangu. Nakupa miaka hii, mitano, Yusuf Shemdoe litasomeka kwenye Intel za kimataifa. Uhai TU, mwenyezi Mungu atujalie!'

'Amin.'

'Mie Wacha nifanye Taratibu za usafiri leo, ikiwezekana Kesho mapema TU, niingie jijini Salalah Oman. Na, Jana ile baada ya kutoka kwa baba mkwe pale, niliwasiliana na Steve. Yupo zake Miami anakula Bata na Kama kawaida, Mwisho wa mwezi tunaingia kazini. Leo, tunakuwa tumebakiwa na wiki mbili tu. Naomba TU Mungu, hili zoezi likamilike mapema, ili Mambo ya Steve Curl yachukue hatamu. Alikupa hai Sana kwa kiswahili chake broken!'

'Haha, atakuwa alisema, wewe salimia Yeye Yusuf'

'Haha unamfahamu vilivyo, hivyo hivyo mwanangu! Haha!' Masu na Yusuf wakacheka kufuatia igizo Hilo.


***

Mawasiliano Kati ya Issa Musa na Yaraslav yalifanyika Mara baada ya Issa kumaliza miadi yake na wafanyabiashara wenzake waliomsambazia bidhaa. Bahati ikawa upande wao. Yaraslav alikuwa Zanzibar kwa likizo. Kwenye hoteli moja ya kitalii. Safari hotel. Hotel iliyomilikiwa kwa sehemu na Mzungu Steve Curl na mabilionea wengine wawili wa huko Marekani. Kama Una kumbukumbu njema, utakumbuka ile hoteli ambayo ina kumbi za starehe ardhini, sehemu ambayo serikali Haina mkono wake huko. Eneo la Siri, linalolindwa kwa siri pia.


Kujua kwamba Jamaa Yuko Zanzibar, ilimpa Imani Issa kwamba hatimaye, Molio angekuwa wake bila kipingamizi. Akaanza kupanga mipango mahsusi ya wapi, Nini na kwa Nini wataenda wapi kuishi mbali na wahuni wa entry. Akajinyanyulia simu yake na kumtwangia Molio.

Simu ikapokelewa kwa furaha.

'Bee mpenzi. Nambie wangu?'

'POA Sana mpenzi, mawasiliano na Yaraslav tayari'

'Enhee! Kasemaje dear?' Molio akauliza kwa wahka!

'Tutaongea jioni kwa uzuri, ila jua TU, Ni habari njema'

'Ooh, Asante Sana mpenzi, can't wait to hear about it in detail. Mmmmwaah!'


Baada ya habari hiyo, Molio alijikuta mwenye furaha iliyopitiliza. Kila aliyekutana naye alijua tu, dada Molio kafurahi, alisalimia watu kwa uchangamfu, alibusu watoto wadogo waliobebwa mikononi bila ridhaa ya wazazi au walezi. Alitoa fedha kwa ombaomba bila kujali Kama alivyofanya kikawaida. Na Mara kadhaa alijikuta akirukaruka Kama ndama kila alipopata nafasi. Ilikuwa siku njema Sana kwenye maisha yake. Moyoni alijua Mambo yatakuwa bambam. Hatimaye atakuwa huru.



Alipotoka kazini Wazo lake lilikuwa kwenda kwa Issa Musa, akakumbuka habari ya mwamvita, akaazimu kupita kwa mzee Halfani Nassor, aka Kisiki. Alikuwa na taarifa kuwa boss wake huyo alikuwa kaenda Dubai kwenye mradi wa watoto. Hivyo alijua angepata muda mzuri wa kuzungumza na mwamvita kabla ya kwenda kwa Issa.


Alibonyeza kengele ya getini, geti likafunguliwa na mlinzi mwenye asili ya kiarabu. Jina lake Mahmoud. Kijana huyo akamkaribisha ndani kwa tabasamu.

'Ah Molioo, nambie mtu wangu! Umeadimika Sana, Salama?'

'Safi tu Muddy, nimekuja kuwatembelea wakina Malkia!'

'Haha, sawa. Ila hivi Ni kusema mpango wangu ushagaupotezea?'

'Kwani nikikwambiaje Mara ya Mwisho?'

'Ulisema nivute subra!'

'Hewalaa, vuta subra Muddy, Mambo mazuri hayataki haraka.'

'Sawa sawa Molio, ila usichukue milele Sasa!'

'Wala usijali, tuombe uzima TU.

'Naam' Mahmoud akaongea Huku akicheka Kama tineja aliyeangukia mapenzi kwa Mara ya kwanza.


Mradi wa watoto, uliokuwa huko Dubai, Ilikuwa Ni mpango mahsusi wa genge la entry uliohusika na kujenga utamaduni wa genge Hilo ili kuwa la kipekee duniani. Viongozi wa entry walibaini kuwa magenge mengi yalikuwa rahisi kupotezwa na serikali mbalimbali hasa watu wao walipoingia mikononi mwa inteligensia za mataifa babe kwa ujasusi, Hali iliyopelekea kusalitiana na kuanguka kabisa kwa makundi hayo.


Entry ikaja na mpango kabambe wa kukabili Hilo Kama lingetokea. Waliwachukua watoto wenye umri wa miezi sita na kuendelea, wakawaweka kwenye karantini maalum, wakakua bila mahusiano na binadamu wa kawaida isipokuwa majasusi waliopewa kazi hiyo maalum ya kuwakuza watoto hao. Maisha yao, tangu utoto, hawakutakiwa kuwa na hisia za kibinadamu. Waliwakuza kuwa sawa na maroboti. Ukatili, ubandidu, ubahauli, unyama. Watoto hao licha ya kukuzwa kwa namna hiyo, waliwekwa microchips kwenye miili yao ili kuwawekea ulinzi ilipobidi. Maisha yao yaliendeshwa kwa inteligensia bandia. Hawakujua kutumia bongo zao. Kazi yao Ilikuwa moja, kupokea amri na kuitekeleza. Wakawa Ni watu hatari zaidi kukutana nao kwenye mapambano kuliko kukutana na wanyama mwitu.


Molio hakuwa miongoni mwao hao, alikuwa na microchip, sawa, lakini hakuanza kukuzwa na entry akiwa kichanga. Aliingizwa entry akiwa tayari anajua hisia za upendo na hata chuki. Akiwa anaweza kutumia ubongo wake kuchanganua Mambo. Alikuwa na miaka kumi na miwili Alipotekwa na entry, enzi zile, entry ndio Ilikuwa inajijenga, hivyo ilijipatia fedha kwa kila namna, ikiwamo kuteka watoto wa matajiri na kudai fedha ili kuwaachia. Walipomteka Molio, wakati wanatafuta hizo fedha za kumkomboa, wakiwa wameshituliwa na taarifa hiyo, wazazi wa Molio wakachanganyikiwa. Hangaika hangaika yao ikawasababishia ajali mbaya Sana. Wakafariki. Entry hawakuwa na namna ya kupata fedha za Marehemu hao, wakaamua kumuingiza Molio kundini.


Molio alionana na Mwamvita wakaketi peke yao kwa kujitenga. Wakawa wanazungumza.

'Hujambo mdogo wangu?' Molio alimsabahi Mwamvita. Mwamvita machozi yakamdondoka.

'Usilie jamani!' Molio alikuwa na kazi ya kubembeleza.

'Kwa Nini dada? Kwa Nini uliamua kufanya kitendo Cha kikatili hivi?' Mwamvita alimudu kutoa dukuduku lake.

'Najua shangazi hajui hata Kama nipo Oman muda huu. Najua kwa sababu niligundua baadaye kwamba sauti yake na yako ni sawa. Aliyenipigia simu nikiwa Zanzibar ni wewe na Wala SI shangazi. Ona da Mariamu,ona hili tumbo. Mbona hamkusubiri Basi nijifungue kwanza?' Mwamvita aliendelea kulalamika. Kilio chake kikamgusa Molio kihisia. Anaanzaje kumweleza kuwa, hiyo mimba Ni muhimu Sana kwa entry? Kwamba umuhimu wake Mwamvita Ni pamoja na mimba yake? Kwa maana ya mtoto wake alikuwa kachaguliwa awe miongoni mwa kizazi katili cha entry? Molio alihisi machozi yanacheza cheza machoni,lakini asingeruhusu kamwe kudondoka.

'Pole Mwamvita. Lakini Usijali. Kaa ukijua siku si nyingi, Mimi mwenyewe nitakutorosha kutoka humu. Nimekuja nikwambie hilo.' Molio akatamka kwa sauti kavu, Huku akisimama.

'Cha msingi jaribu kumkwepa mzee kwa kadri uwezavyo, Tumia mimba yako Kama kisingizio sawa. Usijali, mwanao atakuelewa!'

'Ni Kweli utanisaidia dada?' Mwamvita akauliza.

'Ndiyo Mwamvita, nitakusaidia kwa sababu Issa ameniomba nifanye hivyo. Nitashirikiana naye kukamilisha hilo.'

'Asante Sana da Mariamu. Nakutegemea. Una kalamu na karatasi hapo?'

'Ya kazi gani Tena Mwamvita?'

'Kama huna naomba uhifadhi namba hii kwenye simu yako. Ukionana na Issa, mwambie ni namba ya Masu. Ataelewa.'

'Masu mpenzio siyo!?' Molio akachomekea. Mwamvita akashituka Kidogo. Hakutaka Mariamu ajue hiyo habari. Hakumwamini. Lakini Sasa, hakuwa na namna.

'Ndiyo da Mariamu' akatamka kwa Haya.

'Usijali, tutamjulisha.'

'Asante Sana'


Molio akaondoka zake. Getini Muddy akabaki anajichekesha Kama kijana anayesumbuliwa na balehe. Molio akaelekea kwa Issa Musa.

David Ngocho Samson

FB_IMG_1583317191932.jpg
 
KAZI YA MZUNGU 19


'Mwanangu ee, mie nitalazimika kwenda zangu huko Oman, sijawahi fika huko, lakini naamini Siwezi kishindwa kitu, elimu tuliyopata kwa Steve Curl, inatosha kwa kila kitu. Sheikh amenifanyia upuuzi Sana, aombe nimkute Salama Malkia.'

'Dah, itabidi iwe hivyo. Vipi, hutahitaji kampani yangu? Nimezipata za chini ya kapeti, yule dingi ni kanali mstaafu na anamiliki genge la uhalifu. Kwa maoni yangu, Ni Vema Zaidi tungechimba kwanza Intel muhimu, lakini dah, muda nao Ni muhimu kuuzingatia. Mchezo ukiisha mapema Ni uhakika kuliko kuchelewa.'

'Kampani yako Ni muhimu, ila nitakuomba itokee hapa. Utakuwa unanijulisha baadhi ya Mambo, hivyo Nikuombe Sana uchukue jukumu la kuchimba habari zozote unazoweza kumudu juu ya mzee Kisiki na genge lake. Hizo zitanirahisishia zoezi langu au vipi mwana?'

'Hapo mzee baba hapo ndio penyewe, unajua, Kama ningebahatika kwenda University, ningeenda kusomea masuala ya inteligensia ya mitandao na computer, ningehack CIA ya Marekani iwe tiketi ya kuajiriwa nao, na Kama wangezingua, ningemcheki hata mchizi kiduku pale Korea kaskazini. Ah,dunia ingelitambua jina la Yusuf Shemdoe, ningekuwa maarufu kuliko bin Laden mzee baba, nakuapia Tena!'

'Hata Sasa nakuaminia Sana mtu wangu. Nakupa miaka hii, mitano, Yusuf Shemdoe litasomeka kwenye Intel za kimataifa. Uhai TU, mwenyezi Mungu atujalie!'

'Amin.'

'Mie Wacha nifanye Taratibu za usafiri leo, ikiwezekana Kesho mapema TU, niingie jijini Salalah Oman. Na, Jana ile baada ya kutoka kwa baba mkwe pale, niliwasiliana na Steve. Yupo zake Miami anakula Bata na Kama kawaida, Mwisho wa mwezi tunaingia kazini. Leo, tunakuwa tumebakiwa na wiki mbili tu. Naomba TU Mungu, hili zoezi likamilike mapema, ili Mambo ya Steve Curl yachukue hatamu. Alikupa hai Sana kwa kiswahili chake broken!'

'Haha, atakuwa alisema, wewe salimia Yeye Yusuf'

'Haha unamfahamu vilivyo, hivyo hivyo mwanangu! Haha!' Masu na Yusuf wakacheka kufuatia igizo Hilo.


***

Mawasiliano Kati ya Issa Musa na Yaraslav yalifanyika Mara baada ya Issa kumaliza miadi yake na wafanyabiashara wenzake waliomsambazia bidhaa. Bahati ikawa upande wao. Yaraslav alikuwa Zanzibar kwa likizo. Kwenye hoteli moja ya kitalii. Safari hotel. Hotel iliyomilikiwa kwa sehemu na Mzungu Steve Curl na mabilionea wengine wawili wa huko Marekani. Kama Una kumbukumbu njema, utakumbuka ile hoteli ambayo ina kumbi za starehe ardhini, sehemu ambayo serikali Haina mkono wake huko. Eneo la Siri, linalolindwa kwa siri pia.


Kujua kwamba Jamaa Yuko Zanzibar, ilimpa Imani Issa kwamba hatimaye, Molio angekuwa wake bila kipingamizi. Akaanza kupanga mipango mahsusi ya wapi, Nini na kwa Nini wataenda wapi kuishi mbali na wahuni wa entry. Akajinyanyulia simu yake na kumtwangia Molio.

Simu ikapokelewa kwa furaha.

'Bee mpenzi. Nambie wangu?'

'POA Sana mpenzi, mawasiliano na Yaraslav tayari'

'Enhee! Kasemaje dear?' Molio akauliza kwa wahka!

'Tutaongea jioni kwa uzuri, ila jua TU, Ni habari njema'

'Ooh, Asante Sana mpenzi, can't wait to hear about it in detail. Mmmmwaah!'


Baada ya habari hiyo, Molio alijikuta mwenye furaha iliyopitiliza. Kila aliyekutana naye alijua tu, dada Molio kafurahi, alisalimia watu kwa uchangamfu, alibusu watoto wadogo waliobebwa mikononi bila ridhaa ya wazazi au walezi. Alitoa fedha kwa ombaomba bila kujali Kama alivyofanya kikawaida. Na Mara kadhaa alijikuta akirukaruka Kama ndama kila alipopata nafasi. Ilikuwa siku njema Sana kwenye maisha yake. Moyoni alijua Mambo yatakuwa bambam. Hatimaye atakuwa huru.



Alipotoka kazini Wazo lake lilikuwa kwenda kwa Issa Musa, akakumbuka habari ya mwamvita, akaazimu kupita kwa mzee Halfani Nassor, aka Kisiki. Alikuwa na taarifa kuwa boss wake huyo alikuwa kaenda Dubai kwenye mradi wa watoto. Hivyo alijua angepata muda mzuri wa kuzungumza na mwamvita kabla ya kwenda kwa Issa.


Alibonyeza kengele ya getini, geti likafunguliwa na mlinzi mwenye asili ya kiarabu. Jina lake Mahmoud. Kijana huyo akamkaribisha ndani kwa tabasamu.

'Ah Molioo, nambie mtu wangu! Umeadimika Sana, Salama?'

'Safi tu Muddy, nimekuja kuwatembelea wakina Malkia!'

'Haha, sawa. Ila hivi Ni kusema mpango wangu ushagaupotezea?'

'Kwani nikikwambiaje Mara ya Mwisho?'

'Ulisema nivute subra!'

'Hewalaa, vuta subra Muddy, Mambo mazuri hayataki haraka.'

'Sawa sawa Molio, ila usichukue milele Sasa!'

'Wala usijali, tuombe uzima TU.

'Naam' Mahmoud akaongea Huku akicheka Kama tineja aliyeangukia mapenzi kwa Mara ya kwanza.


Mradi wa watoto, uliokuwa huko Dubai, Ilikuwa Ni mpango mahsusi wa genge la entry uliohusika na kujenga utamaduni wa genge Hilo ili kuwa la kipekee duniani. Viongozi wa entry walibaini kuwa magenge mengi yalikuwa rahisi kupotezwa na serikali mbalimbali hasa watu wao walipoingia mikononi mwa inteligensia za mataifa babe kwa ujasusi, Hali iliyopelekea kusalitiana na kuanguka kabisa kwa makundi hayo.


Entry ikaja na mpango kabambe wa kukabili Hilo Kama lingetokea. Waliwachukua watoto wenye umri wa miezi sita na kuendelea, wakawaweka kwenye karantini maalum, wakakua bila mahusiano na binadamu wa kawaida isipokuwa majasusi waliopewa kazi hiyo maalum ya kuwakuza watoto hao. Maisha yao, tangu utoto, hawakutakiwa kuwa na hisia za kibinadamu. Waliwakuza kuwa sawa na maroboti. Ukatili, ubandidu, ubahauli, unyama. Watoto hao licha ya kukuzwa kwa namna hiyo, waliwekwa microchips kwenye miili yao ili kuwawekea ulinzi ilipobidi. Maisha yao yaliendeshwa kwa inteligensia bandia. Hawakujua kutumia bongo zao. Kazi yao Ilikuwa moja, kupokea amri na kuitekeleza. Wakawa Ni watu hatari zaidi kukutana nao kwenye mapambano kuliko kukutana na wanyama mwitu.


Molio hakuwa miongoni mwao hao, alikuwa na microchip, sawa, lakini hakuanza kukuzwa na entry akiwa kichanga. Aliingizwa entry akiwa tayari anajua hisia za upendo na hata chuki. Akiwa anaweza kutumia ubongo wake kuchanganua Mambo. Alikuwa na miaka kumi na miwili Alipotekwa na entry, enzi zile, entry ndio Ilikuwa inajijenga, hivyo ilijipatia fedha kwa kila namna, ikiwamo kuteka watoto wa matajiri na kudai fedha ili kuwaachia. Walipomteka Molio, wakati wanatafuta hizo fedha za kumkomboa, wakiwa wameshituliwa na taarifa hiyo, wazazi wa Molio wakachanganyikiwa. Hangaika hangaika yao ikawasababishia ajali mbaya Sana. Wakafariki. Entry hawakuwa na namna ya kupata fedha za Marehemu hao, wakaamua kumuingiza Molio kundini.


Molio alionana na Mwamvita wakaketi peke yao kwa kujitenga. Wakawa wanazungumza.

'Hujambo mdogo wangu?' Molio alimsabahi Mwamvita. Mwamvita machozi yakamdondoka.

'Usilie jamani!' Molio alikuwa na kazi ya kubembeleza.

'Kwa Nini dada? Kwa Nini uliamua kufanya kitendo Cha kikatili hivi?' Mwamvita alimudu kutoa dukuduku lake.

'Najua shangazi hajui hata Kama nipo Oman muda huu. Najua kwa sababu niligundua baadaye kwamba sauti yake na yako ni sawa. Aliyenipigia simu nikiwa Zanzibar ni wewe na Wala SI shangazi. Ona da Mariamu,ona hili tumbo. Mbona hamkusubiri Basi nijifungue kwanza?' Mwamvita aliendelea kulalamika. Kilio chake kikamgusa Molio kihisia. Anaanzaje kumweleza kuwa, hiyo mimba Ni muhimu Sana kwa entry? Kwamba umuhimu wake Mwamvita Ni pamoja na mimba yake? Kwa maana ya mtoto wake alikuwa kachaguliwa awe miongoni mwa kizazi katili cha entry? Molio alihisi machozi yanacheza cheza machoni,lakini asingeruhusu kamwe kudondoka.

'Pole Mwamvita. Lakini Usijali. Kaa ukijua siku si nyingi, Mimi mwenyewe nitakutorosha kutoka humu. Nimekuja nikwambie hilo.' Molio akatamka kwa sauti kavu, Huku akisimama.

'Cha msingi jaribu kumkwepa mzee kwa kadri uwezavyo, Tumia mimba yako Kama kisingizio sawa. Usijali, mwanao atakuelewa!'

'Ni Kweli utanisaidia dada?' Mwamvita akauliza.

'Ndiyo Mwamvita, nitakusaidia kwa sababu Issa ameniomba nifanye hivyo. Nitashirikiana naye kukamilisha hilo.'

'Asante Sana da Mariamu. Nakutegemea. Una kalamu na karatasi hapo?'

'Ya kazi gani Tena Mwamvita?'

'Kama huna naomba uhifadhi namba hii kwenye simu yako. Ukionana na Issa, mwambie ni namba ya Masu. Ataelewa.'

'Masu mpenzio siyo!?' Molio akachomekea. Mwamvita akashituka Kidogo. Hakutaka Mariamu ajue hiyo habari. Hakumwamini. Lakini Sasa, hakuwa na namna.

'Ndiyo da Mariamu' akatamka kwa Haya.

'Usijali, tutamjulisha.'

'Asante Sana'


Molio akaondoka zake. Getini Muddy akabaki anajichekesha Kama kijana anayesumbuliwa na balehe. Molio akaelekea kwa Issa Musa.

David Ngocho Samson

View attachment 1484931
Mogambi
Bora weye umekuja kututupia kapunje!!
je utaifikisha mwisho au umetumong'onyolea hilo kimba mojà tu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom