Jomba Wajo
Member
- Apr 6, 2012
- 33
- 17
SIMULIZI ZA JOMBA WAJO
HEKALU LA MAOVU. Sehemu Ya 1.
Pengine ni kwa sababu alizaliwa kipindi cha mwezi mkuu, wakati mbweha na mbwa mwitu wakibweka kuzunguka kibanda cha mama yake kilichojengwa katikati yam situ mnene, msitu wa giza, ndiyo maana Zonda alizaliwa na asili ya uovu ama huenda kulikuwa na kitu kingine zaidi ya hicho. Lakini ajabu inabaki kuwa kwamba, Zonda alizaliwa na nguvu nyingi za ajabu!
Ilikuwa dhahiri kwamba baada ya Mama yake Zonda kumtelekeza mwanaye kwenye huo msitu mnene uliojulikana kama ‘Msitu wa Giza’, Zonda alikulia chini ya malezi ya kichawi ya Alwatani Gwiji, aliyeishi katikatiki yam situ huo. Alifundishwa nyendo zote za kichawi za Alwatan Gwiji na baadaye akagundua nguvu zake za asili za kichawi alizozaliwa nazo zaidi ya zile alizovuna kutoka kwa Alwatani Gwiji, mlezi wake.
Kwa kutumia nguvu zake za asili, Zonda aliweza kunyausha miti na mimea kwa kutumia vidole vyake tu, na wakati mwingine miti ilikauka na kufa kabisa. Aliweza kuwafanya wadudu, ndege na wanyama wamtii kwa kuwaangalia tu kwa aina fulani ya macho.
Alwatani Gwiji na wachawi wenzake walimsaidia na kumpa msukumo wa kuziendeleza nguvu zake hizo za asili. Nia yao ilikuwa ni kuja kumfunza mbinu kongwe za kichawi zilizotumika tangu enzi za zama za mawe na mababu wa mababu zetu. Ni aina ya uchawi wenye nguvu sana kiasi cha kuweza kumdhuru hata kumuua kabisa mtumiaji asiye na uwezo wa asili wa kichawi, ama ambaye hastahili kupewa uwezo huo.
Zonda alianza akujifunza nguvu hizo za kichawi akiwa mdogo mpaka anafikia umri wa kupita baleghe. Ili kuwaridhisha Wazee waliotaka kumfunza na kumrithisa mbinu hizo kongwe za kichawi, Zonda alitakiwa apitie majaribu makubwa na mazito.
Zonda alitakiwa kufunga safari mpaka nje kabisa ya msitu huo wa giza, kwenye jangwa lililoitwa “Jangwa La Wafu.” Alitakiwa aende huko kuutafuta mji wa zamani uliotoweka na kufunikwa na jangwa hilo uliokuwa unajulikana kama Vato. Ndani ya mji huo kulikuwa na masanamu ya ‘Dragon”’ au mijusi mikubwa ya zamani sana iliyokuwa na uwezo wa kupaa kwa mabawa, ambayo alitakiwa akayatafute hadi kuyapata.
Maneno machache ya kunuia yangeweza kuyafanya hayo masanamu kuwa viumbe hai, na Zonda angeyapa maelekezo ya kumbeba na kupaa nayo kurudi tena kwenye ‘Msitu wa Giza.’ Jeshi kubwa la wachawi wakongwe wangakuwa wamekusanyika kwa gwaride la kumtunuku Zonda nguvu hizo adimu za kichawi kupatikana duniani kote.
Baada ya kupokea hizo nguvu za kichawi, Zonda alitakiwa kuongoza mapambano ya kiovu dhidi ya mji ulioitwa Mshikamano, mji uliojengwa na watu wema walioshi kwa amani na upendo. Walitaka kuvamia na kuuangamiza kabisa mji huo, watu na mali zake zote, kisha wauweke chini himaya yao ya kichawi.
Ilikuwa ni kwa cheche ya bahati tu iliyopelekea mipango haiyo hatari ya Alwatani gwiji, Zonga na wachawi wenzao kugundulika kabla ya maangamizi waliyoyapanga hayajaanza kutokea. Aliyegundua mipango hiyo michafu ni mzee mmoja aliyeitwa Yamoto, aliyeishi kwenye ukingo wa Msitu wa Giza.
Mzee yamoto hakuwa mchawi, bali alikuwa na nguvu fulani za kimiujiza zilizomwezesha kuwasiliana na wanyama na ndege. Pia alikuwa akitoa msaada wa kitabibu kwa watu waliohitaji huduma za kiganga. Aliishi peke yake kando ya msitu huo wa Giza, na mara chache sana alitoka nje ya makazi yake kwa kuwa alikuwa akipokea wateja wenye shida mbalimbali karibu muda wote.
Japo mzee Yamoto alifahamika na wenyeji wengi wa mji wa Mshikamano, haikuwa kawaida kwa yeye kuonekana kwenye mji huo mara kwa mara, hivyo alivyoonekana tu siku hiyo kila mtu alihisi kuna jambo lisilo la kawaida lililompeleka pale, hasa alipoomba kuonana na Mtawala wa mji ule.
Kipindi hicho mimi nilikuwa nimeenda kwa ajili ya likizo kupumzika kwenye mji huo mzuri wa kale, Mshikamano., nikifurahia ukarimu wa watu wema wa mji ule.
Nilikuwa katikati ya mji, nikashangazwa na msafara mkubwa wa watu waliokuwa wakimfuata Mzee yamoto aliyeenda akasimama juu ya jukwaa kubwa litumikalo kwa ajili ya mikutano ya mji ule. Watu wengi waliendelea kujaa kuzunguka uwanja huo, nami sikutaka kupitwa.
Umati mzima wa watu ulikuwa umezizima kwa ukimya baada ya mtawala wa ule mji kupanda jukwaani na kuuandaa uma kwa ajili ya kumsikiliza mzee Yamoto kwa yale aliyotaka kuyasema. Nilijisogeza mpaka mbele kabisa ya umati ule karibu na jukwaa ili kuzikwepa kelele zilizokuwa zikiendelea huko nyuma.
Kwa uso mkavu usiyoonyesha chembe yoyote ya furaha, Mzee yamoto alianza kudondosha maelezo yake kuhusu mipanga ya Alwatan Gwiji na wenzake kuvamia mji wa mshikamano na kuuangamiza kwa kutumia Mijusi mikubwa iliyokuwa ikipaa angani, yaani ‘Dragons’. Wenyeji wa mji huo walishtuka sana kana kwamba walikuwa wanayategemea hayo madragoni kutua muda wowote juu yao na kuwaangamiza muda wowote ule.
Mzee yamoto aliwasihi kuwa wajasiri, akisema, “Ndugu zangu, tusihudhunike kwa maovu tuliyopangiwa na adui zetu, tuangalie upande wa pili wa jinsi gani ya kulinda amani na furaha yetu. Kwa bahati nzuri tumefahamu mapema kuhusu kiama chetu tulichoandaliwa na hao wachawi. Asante sana kwa njiwa wangu ambaye aliyasikia mazungumzo kati ya Gwiji na Zonda kisha akaja kunijuza, nami nimekuja kuwapeni taarifa hizo.”
Mzee Yamoto aliujulisha umma. Umati mzima wa watu ulikuwa kimya kwa hofu.
“Tunachotakiwa kufanya ni kumtafuta kijana mmoja jasiri sana, ambaye ataweza kufika kwenye mji uliopotelea kwenye jangwa la wafu, mji wa Valo, kabla ya Zonda anayetumwa na Gwiji na kuyaangamiza kabisa hayo masanamu ya mijusi inayopaa angani kabla Zonda hajafika na kuyaamsha kwa nguvu zake za maajabu.”
Mzee Yamoto alitulia kidogo na kusikilizia kimya cha umati ule mkubwa wa watu.
“Tunahitaji shujaa asiye na woga,” mzee Yamoto aliendelea, “Kijana shujaa ambaye yupo tayari kuyaweka maisha yake hatarini kwa ajili ya kuuokoa mji wetu mzuri wa Mshikamano, na kuokoa maisha yetu wote.”
Mzee yamoto alimaliza kisha akapaaza sauti kwa nguvu,
“ Je, kijana huyo atapatikana katika umati huu?”
Vijana waligeukiana na kutazamana kuona kama kuna aliyekuwa tayari kuipokea changamoto ile. Dakika kadhaa zilipita bila jibu lolote zaidi ya minong’ono ya kujikatia tamaa kutoka kwa watu waliokusanyana pale.
Nikiwa nimesimama mbele kabisa karibu na jukwaa, niliwaangalia wale watu waliosheheni sifa zote nzuri isipokuwa moja tu, ujasiri. Niliona kuna kitu kimoja tu ambacho ningeweza kufanya ili kuwasaidia wenyeji wangu, nacho si kingine bali kulipokea lile jukumu kwa mikono miwili.
Kwa tabasamu pana lililonyanyua matumaini ya wale watu yaliyozama kwenye tope la hofu na wasiwasi, nilinyanyua mkono na kusema,
“Nipo tayari kutoa ushirikiano wangu katika kuokoa mji huu mzuri.”
Mzee yamoto alipepesa macho kuitafuta sauti ya kijasiri iliyotamka maneno yale, na aliponiona aliniambia,
“Safi kijana. Tunatafuta vijana jasiri namna hii. Tengenezeni njia tafadhari kwa shujaa wetu aliyejitolea apate kupita.”
Umati ule ulipasuka katikati na kuachia uwazi mpana kuelekea jukwaani.
“Itabidi tuondoke sasa hivi kuelekea kwenye makazi yangu. Kuna mengi ya kukufahamisha na kujifunza kabla hujalikabili jukumu hili kubwa na hatari.” Alisema kwa furaha Mzee Yamoto wakati akinisubiri nifike alipokuwa amesimama.
Yule mzee aliyekosa subira hakutaka kupoteza wakati kwa kuokoa kila sekunde iliyosalia. Nilipomfikia hakunipa ruhusa hata ya kwenda kuchukua mizigo yangu zaidi ya kuniongoza njia kuelekea kwake.
“Hatuna muda wa kusubiri wakati adui anazidi kujipanga. Hatuwezi kufanya lolte tukiwa hapa mpaka tutakapofika kwenye makazi yangu.”
Alisema wakati tukiondoka kwa haraka kuelekea nyumbani kwake.
**********
Bofya hapa ili uweze kuisoma simulizi yote.