SIMULIZI :Diana wa Kenya

Daudi king

New Member
Jan 12, 2019
1
20
Sehemu ya Kwanza

Wakati naingia ndani ya basi ilikua tayari imefika saa kumi na moja alfajiri, watu hawakua wengi sana ndani ya basi lile, nilitembea taratibu hadi kwenye siti yangu nikiwa nimeshikilia kibegi kidogo mkono wa kulia na mkono wa kushoto nilikua na gazeti la Chomoza, huwa sipendi kusafiri na mizigo mingi sababu ya kuepuka usumbufu wa kuchunga mizigo kila wakati, nilifika hadi katika siti namba 35 na kuangalia ticketi yangu Kisha nikatabasamu, ilikua ni siti ya dirishani ambayo huwa napendelea kukaa, nilifungua buti ya juu ndani ya basi ni kaweka kibegi Kisha nikaketi na kufunga mkanda, nikiwa bado naangaza huku na kule mara niliona koti langi nyeusi likiwa siti ya pembeni yangu nilipolitizama kwa umakini niligundua lilikuwa koti la kike,
Wala si kuonyesha kujali sana, nilifungua gazeti langu na kuanza kujisomea news za kitaifa dakika chache baadae basi lilionekana kujaa ijapokua siti ya pembeni yangu hapakuoneka mtu akija kuketi pale, ilitimu saa 12 kamili, basi likawa linaanza kutoka stendi ndipo jirani yangu ambae alikua amekaa siti ya nyuma kutokana na kuonyesha kwake kujali akaniuliza, "abiria mwenzio yuko wapi ndio tunatoka stendi ivyo" nilibaki kutafuna maneno nisijue namjibu vipi jibu likanijiia "tutamuuliza kondokta" basi yule abiria akawa kimya na kweli basi lilitoka ndani ya stendi na safari ya kuelekea Kenya ikaanza

JE kitatokea nini!?....... Usikose sehemu ya pili hapa
sanchoka_.JPG


Sent using Jamii Forums mobile app
 

ben milazo

JF-Expert Member
Jan 18, 2015
998
2,000
kitakachotokea ni huyo manzi kuamia kwenye hiyo seat ya jamaa afu mwisho wa siku watalala hotel chumba kimoja nakumaliza mchezo mwisho wa siku jmaa anaugua ukimwi anakufa #the end directed by bongomovie
 
Top Bottom