Simulizi: CRAZY IN LOVE 01
Mtunzi: Kalmas Konzo
Simu: 0625 646265
Ilikuwa ni siku mbaya sana kwa Philly Mathew na mama yake. Ilikuwa ni siku ambayo ilikuwa ni ngumu sana kufutika katika fikra za Philly Mathew katika maisha yake yote. Siku ile upepo wa maisha yake uligeuka na kuanza kuvuma kuelekea katika uwanda wa maisha ya tabu na na kila aina ya magumu ya hapa duniani. Kipindi hicho alikuwa ni kijana mdogo wa kidato cha nne.
Philly Mathew alikuwa ni mtoto pekee kwa mama na baba yake mzee Mathew Kamshange. Mzee Mathew alikuwa ni mtu ambaye alikuwa ametunukiwa ukwasi wa kutosha. Alikuwa ni mtu ambaye alikuwa akihodhi vitega uchumi mbalimbali ambavyo vilikuwa vikimwingizia pesa nyingi sana.
Philly Mathew aliishi vema na wazazi wake. Upendo ulitawala katika nyumba kwa kipindi chote ambacho Philly Mathew aliwashuhudia wazazi wao wakiishi pamoja.
Lakini ghafla shetani alipenyeza harufu yake ndani ya ndoa yam zee Mathew Kamshange na mkewe. Mzee Mathew akaanza kuwa na hamu ya kutaka kupata mtoto wa pili lakini ilishindikana. Walijitahidi kila njia lakini haikuwezekana. Inaonekana Mungu alikuwa amewajalia kijana Philly tu katika uzazi wao.
Hali hii ilianza kuyafanya mapenzi ya mzee Mathew Kamshange kupungua kwa mkewe. Hali hii ilimwumiza sana mkewe kwani hakupenda kukosa uzazi wa pili. Alijitahidi kuonyesha upendo wa dhati kwa mumewe lakini hakulitaka hilo. Mke alijitahidi sana kuinusuru ndoa lakini mume ndiyo alizidi kuichochea moto kuelekea katika uharibifu.
Sasa mzee Mathew Kamshange akaamua kutafuta mwanamke nje ya ndoa yake. Haikuwa kazi ngumu kwake kumpata kwa sababu alikuwa na pesa na kawaida pesa ni kama ulimbo kwa wanawake.
Kimada aliyempata mzee Mathew hakuwa na mapenzi ya dhati kwa mzee huyu. Alichotaka ni kumkwangua pesa mzee Mathew. Na kwa kuwa alimwahidi kwamba atamzalia mtoto basi mapenzi ya mzee Mathew Kamshange kwa kimada yule yalizidi kushika kasi. Sasa mzee Mathew akawa hasikii wala haambiliki juu ya mwanamke yule.
Mwanamke yule alimpa masharti mzee Mathew Kamshange kwamba yeye hataki kushiriki mapenzi na mwanamke mwingine. Hivyo basi mzee Mathew achague moja kuwa na yeye au kumwacha mke wake wa ndoa.
Mzee Mathew Kamshange akafanya maamuzi ambayo aliona kwamba yalikuwa ni ya busara kwake.
******
Usiku ule usiosahaulika Mathew anakumbuka mzee wake alikuja pale nyumbani akiwa ameambatana na mwanamke mmoja mrembo sana. Kutoka katika gari la mzee Mathew Kamshange mwanamke yule alianza kushusha mabegi.
“He! Leo tuna mgeni mume wangu? Mbona hukuniambia mapema?” mama Mathew aliuliza.
“Tena afadhali umekuja. Sasa nadhani dakika kumi zitatosha. Baada ya dakika kumi sitaki kuwaona ndani ya nyumba hii wewe pamoja na mwanao!” mzee Mathew Kamshange alimfokea mkewe.
“Unasemaje baba Mathew?” mkewe aliuliza.
“Nimesema hivi sitaki kuwaona wewe na mwanao baada ya dakika kumi. Tena sitaki utoke na chochote humu labda nguo tu kwani vyote hivi ulikuja ulivikuta” mzee Mathew aliongea.
“Mume wangu, uko sawa kweli?” mkewe aliuliza akiwa haamini.
“Kwa hiyo waniona kama nimechanganyikiwa siyo? Sasa kwa taarifa yako nimepata chombo kipya. Huyu mrembo unayemwona hapa ndiye mmiliki wa nyumba hii kuanzia hivi sasa!” mzee Mathew aliongea kwa dharau huku akimkumbatia kimada wake.
Mama Mathew alihisi kama moyo wake ulikuwa unataka kuchomoka. Machozi ya uchungu yalianza kumtoka. Hakuamini kama jambo lile lilikuwa linatokea kweli au ilikuwa ni njozi.
Wakati huo kijana Philly Mathew alikuwa amefika mahali pale mara baada ya kusikia malumbano ya wazazi wake.
“Sasa usiku huu sisi tutaenda wapi mume wangu?” mama Mathew aliuliza kwa huzuni.
“Nani mume wako? Mnazidi kunipotezea muda wangu hapa. Fanyeni haraka muondoke!” mzee Mathew alifoka.
“Baba kwa nini unatufukuza?” Philly Mathew alimwuliza baba yake machozi yakiwa yamlengalenga mara baada yakumwona mama yake akiwa analia.
“Unasemaje wewe punda? Tokeni haraka sana hapa kabla sijawalamba makofi!” mzee Mathew kamshange alifoka huku akichukua chuma fulani katika gari kwa ajili ya kuipondea familia yake.
Philly Mathew alipoona hivyo ilibidi amkokote mama yake mpaka ndani. Huko walianza kukusanya nguo zao huku mama yake Mathew akilia sana. Mathew ilimbidi ajikaze kiume kwa ajili ya kumsaidia mama yake.
“Sasa tutaenda wapi mwanangu na usiku huu? Baba yako mbona anatufanyia hivi?” mama Mathew alilalamika akilia.
“Mama, mwenyezi Mungu atatusaidia. Tuamini kwamba yuko pamoja nasi hivyo atatuongoza na kutulinda!” Philly Mathew aliongea kwa ujasiri.
Mama yake alifarijika sana kwa ujasiri wa kijana wake lakini bado alizidi kuumia moyoni kutokana na unyama na ukatili wa mume wake.
Baada ya muda mzee Mathew Kamshange alienda mpaka kule chumbani ambako Philly Mathew na mama yake walikuwa wakipanga nguo zao.
“Yaani bado hamjatoka tu?” mzee Mathew aliuliza kwa dharau.
“We mzee hebu tulia. Ukiendelea kuongea utumbo wako nitakuvunja shingo yako!” Philly aliamua kumtolea uvivu baba yake.
“Mwanangu usiongee hivyo kwani huyu ni baba yako!” mama yake alimzuia kijana wake asilete vurugu kwa baba yake.
“Baba yangu gani huyu mjaa laana. Yaani wewe mzee ni mchafu uliyelaaniwa. Utamletaje hawara yako ndani ya nyumba ambayo familia yako inaishi. Halafu mbaya zaidi unaifukuza familia yako kwa ajili ya huyo malaya!” Philly aligeuka mbogo.
“Unasemaje wewe mtoto? Naona umekosa adabu!” mzee Mathew aliongea huku akirudi nyuma kidogo maana alihisi huenda mwanawe anaweza kumzidi ubavu.
“Yaani kuanzia leo wewe mzee umetangaza vita na mimi. Mali hizi mmechuma pamoja na mama lakini leo hii unamwona mama yangu hafai. Sasa ninakwambia ama zangu ama zako!”Philly alifoka.
“Unaongea nini wewe! Dua la kuku halimpati mwewe. Umeshika kwenye makali na mimi nimeshika kwenye mpini!” mzee Kamshange alijigamba.
“Sasa safari hii ndiyo utashangaa dua la kuku litakavyompata mwewe. Kwanza potea hapa, usije nifanya nikakutenda kitu cha ajabu sana!” Philly alifoka.
Mzee Mathew ilimbidi atoke mbio mle ndani maana yale macho aliyotazamwa na kijana wake alihisi huenda kijana wake alikuwa akivuta bangi.
Philly aliendelea kumsaidia mama yake kukusanya nguo kwani kwa wakati ule mama yake alikuwa hoi hajiwezi kwa mshtuko aliokuwa ameupata.
“Mama jikaze. Usiwe na hofu, uko na mimi kijana wako. Nitakulinda na hakuna baya lolote litakalokupata!” Philly alimfariji mama yake.
******
ENDELEA