Simulizi: Chumba no 18

Simulizi: Chumba no 18

Don san tan

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2015
Posts
575
Reaction score
443
Simulizi za kusisimua & mapenzi

Simulizi za kusisimua & mapenzi
SIMULIZI; CHUMBA NO 18
MTUNZI; Pascal Pahali
Email;pascalpahali@rocketmail.com
Contact;+255655-123 103
WhatsApp;+255655-123 103
Instagram; santiano del pahali
LIKE ILI NIPOST SIMULIZI NYINGINE

UTANGULIZI
Zilisikika kelele kutoka kwenye chumba kile kilichokuwa kikisomeka kwa utambulisho wa no 18.Watu wengi walishituka kusikia kelele zile na hata baadhi yao kuthubutu kukimbilia kilipokuwepo chumba kile na kuangalia ni nini kilikuwa kikiendelea.Hakuna aliyeweza kuendelea kuwa na furaha baada ya kushuhudia yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chumba kile kilichofahamika kwa jina la chumba no 18.Je nini kilichokuwa kimetokea na kuendelea ndani ya chumba kile no 18.Fuatilia simulizi hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake kujua na pia ikikugusa LIKE & SHARE ili marafiki zako nao waweze kujifunza.

ANZA NAYO
Ni chumba kilichoonekana kuwa na ukimya, utulivu na giza la kutisha ambalo kila mtu ambaye angethubutu kuingia kwenye chumba kile basi asingethubutu kuiona kesho ya maisha yake.Utulivu wa chumba kile uliwapa watu mbalimbali mashaka na kutaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba hicho lakini watu hawa hawakuishia kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba kile lakini walienda mbali kidogo na kutaka kujua ni kiumbe gani ambacho kilikuwa kikiiishi ndani ya chumba kile.

Sawa ndani ya chumba hiki binadamu wanaweza wakaishi lakini kwa ukimya na utulivu wa chumba hiki ndicho kitupacho wasiwasi na kujiamini na kujibu kuwa si wanadamu ambao huishi ndani ya chumba hiki.Hatujawahi kuona moshi wa moto hata siku moja ukifuka kutoka ndani ya chumba hiki.Je binadamu hao wasadikikao huishi ndani ya chumba hiki inamaana wanaishi pasipo kula? Hatujawahi kuona hata siku moja chumba hiki kikifunguliwa.Je binadamu hao wasadikikao huishi ndani ya chumba hiki hawashikwi na haja ambayo huweza kuwalazimu waweze kutoka na kuelekea chooni kwa ajili ya kumaliza haja zao hizo? Lakini si hayo tu yanipayo ushujaa wa kusema waishiyo ndani ya chumba hiki si binadamu lakini hata giza lililopo humu ndani huniongezea ujasiri wa kusema waishiyo ndani ya chumba hiki si binadamu.Tazama haijawahi kuonekana taa au mwanga wa aina yoyote ndani ya chumba hiki.Je binadamu wanaweza kuishi kwa muda mrefu wote huo pasipo mwanga? Alimaliza mtu mmoja aliyekuwa jirani wa chumba kile kutoa mashaka juu ya chumba kile no 18.Baada ya kuulizana sana na kutokupata ukweli na kila mmoja kuogopa kukifungua chumba kile no 18 ili waweze kumaliza utata uliyokuwa ukiwasumbua kwa kutambua ni nini kilichokuwepo ndani ya chumba kile watu wale walitawanyika na kila mmoja kuelekea nyumbani kwake.

Chumba no 18 kiliendelea kuumiza akili za watu wengi waliyokuwa wakitathimini na kutaka kujua ukweli wake.Walikuja watafti mbalimbali, walikuja waandishi wa habari mbalimbali lakini hata wageni kutoka sehemu na nchi mbalimbali waliweza kufika na kukizunguka chumba kile na kukitathimini pia.Kuna baadhi ya wageni waliwiwa kutoa msaada kwenye chumba kile no 18 lakini kwakuwa chumba kile hakikuweza kuonyesha ushirikiano na kufanya kiogopwe na kila aliyeweza kufika mahali pale basi hata wageni wale pia waliondoka pasipo kutoa msaada wowote.Waandishi wa habari waliandika habari za chumba kile no 18 na kufanya chumba kile kipate jina kubwa na habari zake kusikika kwenye masikio ya wengi.Je ni nani awezaye kujitosa na kukifungua chumba kile ili wenye moyo wa kusaidia waweze kukisaidia chumba kile hata kwa kuunganisha taa ndani yake na kuondoa giza nene litandalo ndani ya chumba kile?

Siku moja zilisikika kelele zilizoshindwa kutofautishwa na hii ni kutokana na muingiliano wa kelele zile kutoka kwenye chumba kile no 18.Kuna wakati kelele zile zilikuwa zikisikika kama vilio vya watu, kuna wakati zilisikika kama sauti za watu wakilalamika sana kwa kudai ya kuwa walikuwa wakiumizwa na kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba kile na kuonekana hakuna aliyejali malalamiko na vilio vile.Wengine wakiwa wanakimbia na silaha mikononi, wengine wakiwa wanakimbia huku kiatu kimoja kikiwa mkononi na kingine mguuni walizidi kusogea kilipokuwepo chumba kile.Sauti za kelele zile zilizidi kuongezeka kwa kupenya kwenye ngoma za masikio ya watu waliyokusanyika mahali pale na sasa iliwezekanika kutofautisha kelele zile na hii ni kutokana na kuwa karibu na chumba kile.

Ndani ya kelele zile kulikuwa na sauti za watoto yatima waliyokuwa wakiwalilia wazazi wao waliyokufa kwa sababu mbalimbali.Kuna baadhi ya wazazi wao waliyapoteza maisha yao katika ajali zilizokuwa zimetokea na nyingi ya ajali hizo kusababishwa na walinzi wa chombo hicho ambao wengi walitekwa na rushwa na kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.Lakini pia kuna baadhi ya wazazi wao walipoteza maisha yao kwa kuwa na dukuduku na majeraha ndani ya mioyo yao na majeraha hayo yakisababishwa na ahadi ambazo waliahidiwa wakati wa ujenzi wa chumba hicho lakini mwisho wa siku kutokutekelezewa ahadi hizo.Tazama wengine walishiriki katika ujenzi wa chumba kile no 18 ambapo walitumia vichwa vyao kubeba ndoo za mchanga, maji na hata mawe ili tu kufanikisha ujenzi ule.

Na kuna kipindi wakati chumba kile kinajengwa kuna burudani mbalimbali zilikuwa zikitolewa na hii ili kukusanya watu kutoka sehemu mbalimbali kuja kushiriki ujenzi wa chumba kile.Wakati burudani hiyo ikitolewa tazama wazazi wa watoto wale yatima walifunga vibwebwe na kuinogesha burudani ile kwa kucheza.Lakini sasa wapo wapi waliyoinogesha burudani ile? Wako wapi waliyoshiriki ujenzi wa chumba kile? Wote walikuwa wameshatangulia mbele ya haki na kuwaacha watoto wao kubaki kwenye vilio vya uchungu na kuishia kuogelea dimbwi la machozi yao wenyewe.Chumba no 18 kuwa na huruma na jaribu kusafisha sikio lako ili uweze kusikia vilio vya watoto hawa yatima.

Si watoto yatima pekee waliyokuwa wakilia ndani ya chumba kile no 18 lakini tazama zilisikika sauti za vilio vya wamama wajawazito ambao nao pia walikuwa wakilia kwa uchungu sana hata baadhi yao sauti zao kukata kabisa.Vilio vya wamama wale wajawazito havikumaanisha kuwa tarehe za kujifungua kwao zilifika laah hasha.Kuna baadhi yao hata mimba zao zilikuwa bado ni changa lakini na wao pia walilia vivyo hivyo.Vilio vya wamama wale wajawazito vilimaanisha kutokuandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya kuvipokea viumbe vilivyokuwa ndani ya matumbo yao.Tazama kabla yao kuna wamama wengi walipoteza maisha kwa ubovu wa mazingira ya kuwapokelea viumbe wao.Kumbukumbu ile iliwafanya wamama wale wajawazito kuendelea kupaza sauti za vilio vyao.Ni nani awezaye kunyamazisha vilio vya wamama wale na kuweza kufuta machozi yao yaliyokuwa yakitiririka mashavuni mwao na kutengeneza mifereji ya machozi juu ya mashavu hayo.

Wakati watoto yatima na wamama wajawazito wakiendelea na vilio vyao juu ya mateso makali waliyokuwa wakiyapata ndani ya chumba kile no 18 kuna baadhi ya kelele za malalamiko yalisika kutokea ndani ya chumba kile pia.Je ni nani aliyekuwa akilalamika kutoka ndani ya chumba kile? Ni sauti za vijana zilisikika wakilalamikia ahadi za uongo ndani ya chumba kile.Vijana waliyoonekana kukata tamaa na maisha na hata baadhi yao kuanza kutumia madawa ya kulevya wakidhania yawezekana ile ndiyo ikawa njia pekee ya wao kupotezea maumivu na mawazo waliyokuwa nayo lakini madawa hayo kuendelea kuwapoteza na kuangamiza nguvu ya chumba no 18.Baadhi ya vijana hao baada ya matumizi ya madawa hayo ya kulevya walijikuta kujiingiza kwenye kazi zisizo halali kama wizi, ukabaji na hata ubakaji.Je nani awezaye kuwaponya vijana hawa?

Lakini si vijana hao tu waliyosikika kulalamikia chumba kile lakini pia kuna baadhi ya vijana walionekana kubeba bahasha zao za kaki mikononi na ndani ya bahasha zile kubeba kitu kisichoweza kujulikana kirahisi na hawa pia walipiga kelele na kukilalamikia chumba kile no 18 kwa madai ya kuwa chumba kile kiliwaahidi mambo mazuri mengi lakini makubaliano yao yalikuwa ni kwamba walitakiwa waende kutoa matongotongo yaliyokuwa yameziba kope za macho yao na baada ya kutoa tongotongo hizo ndipo wangeweza kupewa silaha tayari kwa kuingia vitani.Sasa vijana wale walikuwa washatoa tongotongo zile lakini bado chumba no 18 kilishindwa kuwapatia silaha ili vijana wale waweze kuingia kwenye uwanja wa vita.Je ni nini chumba no 18 kilimaanisha? Chumba no 18 naomba ugeuze hiyo shingo yako inayoonekana kuwa ngumu na safisha tongotongo zitatazo ndani ya kope za macho yako ili uweze kutazama vizuri yale yote uliyokuwa umewaahidi watu wako na ikiwezekana anza kuwatekelezea moja baada ya jingine.Naamini kupitia waraka na barua hii utanielewa na kujirekebisha.Nikutakie kila la kheri katika utekelezaji wa ahadi zako.

MWISHO
Huu ndiyo mwisho wa simulizi hii ya CHUMBA NO 18.Ndani ya simulizi hii unakutana na CHUMBA NO 18 kuvaa nafasi ya uhusika huku watoto yatima, wamama wajawazito na vijana kuvaa uhusika usaidizi.Soma fundisho ili uweze kujua ni nini tumefundishwa na simulizi hii na pia tumia akili ili uweze kung’amua na kujua CHUMBA NO 18 ni kitu gani na ikiwezekana comment jibu lako hapo chini ya simulizi hii.

FUNDISHO
Simulizi hii inatoa mafundisho mbalimbali lakini binafsi nipende kuelezea kwa ufupi funzo la UTEKELEZAJI WA AHADI.Ukisoma vizuri na kwa umakini simulizi hii unatambua kuwa CHUMBA NO 18 kiliweza kutoa ahadi nyingi kwa watu wake lakini kushindwa kutekeleza na kushindwa huko kuna sababisha machafuko, vifo na mateso makali kwa waliyoahidiwa ahadi hiyo.Je CHUMBA NO 18 ni kitu gani?
 
Ni chumba kilichoonekana kuwa na
ukimya, utulivu na giza la kutisha ambalo
kila mtu ambaye angethubutu kuingia
kwenye chumba kile basi asingethubutu
kuiona kesho ya maisha yake.Utulivu wa
chumba kile uliwapa watu mbalimbali
mashaka na kutaka kujua ni nini
kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba
hicho lakini watu hawa hawakuishia kutaka
kujua kilichokuwa kikiendelea ndani ya
chumba kile lakini walienda mbali kidogo
na kutaka kujua ni kiumbe gani ambacho
kilikuwa kikiiishi ndani ya chumba kile.
Sawa ndani ya chumba hiki binadamu
wanaweza wakaishi lakini kwa ukimya na
utulivu wa chumba hiki ndicho kitupacho
wasiwasi na kujiamini na kujibu kuwa si
wanadamu ambao huishi ndani ya chumba
hiki.Hatujawahi kuona moshi wa moto hata
siku moja ukifuka kutoka ndani ya chumba
hiki.Je binadamu hao wasadikikao huishi
ndani ya chumba hiki inamaana wanaishi
pasipo kula? Hatujawahi kuona hata siku
moja chumba hiki kikifunguliwa.Je
binadamu hao wasadikikao huishi ndani ya
chumba hiki hawashikwi na haja ambayo
huweza kuwalazimu waweze kutoka na
kuelekea chooni kwa ajili ya kumaliza haja
zao hizo? Lakini si hayo tu yanipayo
ushujaa wa kusema waishiyo ndani ya
chumba hiki si binadamu lakini hata giza
lililopo humu ndani huniongezea ujasiri wa
kusema waishiyo ndani ya chumba hiki si
binadamu.Tazama haijawahi kuonekana taa
au mwanga wa aina yoyote ndani ya
chumba hiki.Je binadamu wanaweza kuishi
kwa muda mrefu wote huo pasipo
mwanga? Alimaliza mtu mmoja aliyekuwa
jirani wa chumba kile kutoa mashaka juu
ya chumba kile no 1.Baada ya kuulizana
sana na kutokupata ukweli na kila mmoja
kuogopa kukifungua chumba kile no 1 ili
waweze kumaliza utata uliyokuwa
ukiwasumbua kwa kutambua ni nini
kilichokuwepo ndani ya chumba kile watu
wale walitawanyika na kila mmoja kuelekea
nyumbani kwake.
Chumba no 1 kiliendelea kuumiza akili za
watu wengi waliyokuwa wakitathimini na
kutaka kujua ukweli wake.Walikuja watafti
mbalimbali, walikuja waandishi wa habari
mbalimbali lakini hata wageni kutoka
sehemu na nchi mbalimbali waliweza
kufika na kukizunguka chumba kile na
kukitathimini pia.Kuna baadhi ya wageni
waliwiwa kutoa msaada kwenye chumba
kile no 1 lakini kwakuwa chumba kile
hakikuweza kuonyesha ushirikiano na
kufanya kiogopwe na kila aliyeweza kufika
mahali pale basi hata wageni wale pia
waliondoka pasipo kutoa msaada
wowote.Waandishi wa habari waliandika
habari za chumba kile no 1 na kufanya
chumba kile kipate jina kubwa na habari
zake kusikika kwenye masikio ya wengi.Je
ni nani awezaye kujitosa na kukifungua
chumba kile ili wenye moyo wa kusaidia
waweze kukisaidia chumba kile hata kwa
kuunganisha taa ndani yake na kuondoa
giza nene litandalo ndani ya chumba kile?
Siku moja zilisikika kelele zilizoshindwa
kutofautishwa na hii ni kutokana na
muingiliano wa kelele zile kutoka kwenye
chumba kile no 1.Kuna wakati kelele zile
zilikuwa zikisikika kama vilio vya watu,
kuna wakati zilisikika kama sauti za watu
wakilalamika sana kwa kudai ya kuwa
walikuwa wakiumizwa na kile kilichokuwa
kikiendelea ndani ya chumba kile na
kuonekana hakuna aliyejali malalamiko na
vilio vile.Wengine wakiwa wanakimbia na
silaha mikononi, wengine wakiwa
wanakimbia huku kiatu kimoja kikiwa
mkononi na kingine mguuni walizidi
kusogea kilipokuwepo chumba kile.Sauti
za kelele zile zilizidi kuongezeka kwa
kupenya kwenye ngoma za masikio ya
watu waliyokusanyika mahali pale na sasa
iliwezekanika kutofautisha kelele zile na hii
ni kutokana na kuwa karibu na chumba
kile.
Ndani ya kelele zile kulikuwa na sauti za
watoto yatima waliyokuwa wakiwalilia
wazazi wao waliyokufa kwa sababu
mbalimbali.Kuna baadhi ya wazazi wao
waliyapoteza maisha yao katika ajali
zilizokuwa zimetokea na nyingi ya ajali
hizo kusababishwa na walinzi wa chombo
hicho ambao wengi walitekwa na rushwa
na kushindwa kutekeleza wajibu wao
ipasavyo.Lakini pia kuna baadhi ya wazazi
wao walipoteza maisha yao kwa kuwa na
dukuduku na majeraha ndani ya mioyo yao
na majeraha hayo yakisababishwa na ahadi
ambazo waliahidiwa wakati wa ujenzi wa
chumba hicho lakini mwisho wa siku
kutokutekelezewa ahadi hizo.Tazama
wengine walishiriki katika ujenzi wa
chumba kile no 1 ambapo walitumia
vichwa vyao kubeba ndoo za mchanga,
maji na hata mawe ili tu kufanikisha ujenzi
ule.
Na kuna kipindi wakati chumba kile
kinajengwa kuna burudani mbalimbali
zilikuwa zikitolewa na hii ili kukusanya
watu kutoka sehemu mbalimbali kuja
kushiriki ujenzi wa chumba kile.Wakati
burudani hiyo ikitolewa tazama wazazi wa
watoto wale yatima walifunga vibwebwe na
kuinogesha burudani ile kwa
kucheza.Lakini sasa wapo wapi
waliyoinogesha burudani ile? Wako wapi
waliyoshiriki ujenzi wa chumba kile? Wote
walikuwa wameshatangulia mbele ya haki
na kuwaacha watoto wao kubaki kwenye
vilio vya uchungu na kuishia kuogelea
dimbwi la machozi yao wenyewe.Chumba
no 1 kuwa na huruma na jaribu kusafisha
sikio lako ili uweze kusikia vilio vya watoto
hawa yatima.
Si watoto yatima pekee waliyokuwa wakilia
ndani ya chumba kile no 1 lakini tazama
zilisikika sauti za vilio vya wamama
wajawazito ambao nao pia walikuwa
wakilia kwa uchungu sana hata baadhi yao
sauti zao kukata kabisa.Vilio vya wamama
wale wajawazito havikumaanisha kuwa
tarehe za kujifungua kwao zilifika laah
hasha.Kuna baadhi yao hata mimba zao
zilikuwa bado ni changa lakini na wao pia
walilia vivyo hivyo.Vilio vya wamama wale
wajawazito vilimaanisha kutokuandaliwa
mazingira mazuri kwa ajili ya kuvipokea
viumbe vilivyokuwa ndani ya matumbo
yao.Tazama kabla yao kuna wamama
wengi walipoteza maisha kwa ubovu wa
mazingira ya kuwapokelea viumbe
wao.Kumbukumbu ile iliwafanya wamama
wale wajawazito kuendelea kupaza sauti za
vilio vyao.Ni nani awezaye kunyamazisha
vilio vya wamama wale na kuweza kufuta
machozi yao yaliyokuwa yakitiririka
mashavuni mwao na kutengeneza mifereji
ya machozi juu ya mashavu hayo.
Wakati watoto yatima na wamama
wajawazito wakiendelea na vilio vyao juu
ya mateso makali waliyokuwa wakiyapata
ndani ya chumba kile no 1 kuna baadhi
ya kelele za malalamiko yalisika kutokea
ndani ya chumba kile pia.Je ni nani
aliyekuwa akilalamika kutoka ndani ya
chumba kile? Ni sauti za vijana zilisikika
wakilalamikia ahadi za uongo ndani ya
chumba kile.Vijana waliyoonekana kukata
tamaa na maisha na hata baadhi yao
kuanza kutumia madawa ya kulevya
wakidhania yawezekana ile ndiyo ikawa
njia pekee ya wao kupotezea maumivu na
mawazo waliyokuwa nayo lakini madawa
hayo kuendelea kuwapoteza na
kuangamiza nguvu ya chumba no
1.Baadhi ya vijana hao baada ya
matumizi ya madawa hayo ya kulevya
walijikuta kujiingiza kwenye kazi zisizo
halali kama wizi, ukabaji na hata ubakaji.Je
nani awezaye kuwaponya vijana hawa?
Lakini si vijana hao tu waliyosikika
kulalamikia chumba kile lakini pia kuna
baadhi ya vijana walionekana kubeba
bahasha zao za kaki mikononi na ndani ya
bahasha zile kubeba kitu kisichoweza
kujulikana kirahisi na hawa pia walipiga
kelele na kukilalamikia chumba kile no 1
kwa madai ya kuwa chumba kile
kiliwaahidi mambo mazuri mengi lakini
makubaliano yao yalikuwa ni kwamba
walitakiwa waende kutoa matongotongo
yaliyokuwa yameziba kope za macho yao
na baada ya kutoa tongotongo hizo ndipo
wangeweza kupewa silaha tayari kwa
kuingia vitani.Sasa vijana wale walikuwa
washatoa tongotongo zile lakini bado
chumba no 1 kilishindwa kuwapatia
silaha ili vijana wale waweze kuingia
kwenye uwanja wa vita.Je ni nini chumba
no 1 kilimaanisha? Chumba no 1
naomba ugeuze hiyo shingo yako
inayoonekana kuwa ngumu na safisha
tongotongo zitatazo ndani ya kope za
macho yako ili uweze kutazama vizuri yale
yote uliyokuwa umewaahidi watu wako na
ikiwezekana anza kuwatekelezea moja
baada ya jingine.Naamini kupitia waraka
na barua hii utanielewa na kujirekebisha.N
ikutakie kila la kheri katika utekelezaji wa
ahadi zako Chumba No 1.
MWISHO
Huu ndiyo mwisho wa simulizi hii ya
CHUMBA NO 1.


Ahsante sana kwa kusoma.
Sent from my Sony Xperia™
Ndefuu halafu haieleweki.
 
bado naendelea kuiscrow, mi ni mvivu wa kusoma, daarhh.... ndefu sana kiaina, jaribuni kufupishaga mambo
 
Kama wewe ni Great thinker utanielewa, lakini kama Elimu ni ya hapa na pale na umo humu ndani ya great thinkers Huwezi kuelewa.... Pole sana wewe unayesema ni Ndefu ni mvivu wa kusoma.. Ndio maana wanasema ukitaka kumficha mwafrika Asikuibie Pesa zako weka katikati ya kitabu. Maana hawana mazoea ya kusoma vitabu hasa Biblia Takatifu na Quorun Tukufu.
 
Poleni Sana enyi mtakao madarakani bila kujiwekea malengo ya kuongoza.... Enyi UKAWA tumieni akili hata za kuazima kutoka CCM kama mlivyofanya uchaguzi ulopita.... Lakini mmeshindwa Lol!
 
Simulizi za kusisimua & mapenzi

Simulizi za kusisimua & mapenzi
SIMULIZI; CHUMBA NO 18
MTUNZI; Pascal Pahali
Email;pascalpahali@rocketmail.com
Contact;+255655-123 103
WhatsApp;+255655-123 103
Instagram; santiano del pahali
LIKE ILI NIPOST SIMULIZI NYINGINE

UTANGULIZI
Zilisikika kelele kutoka kwenye chumba kile kilichokuwa kikisomeka kwa utambulisho wa no 18.Watu wengi walishituka kusikia kelele zile na hata baadhi yao kuthubutu kukimbilia kilipokuwepo chumba kile na kuangalia ni nini kilikuwa kikiendelea.Hakuna aliyeweza kuendelea kuwa na furaha baada ya kushuhudia yale yaliyokuwa yakiendelea ndani ya chumba kile kilichofahamika kwa jina la chumba no 18.Je nini kilichokuwa kimetokea na kuendelea ndani ya chumba kile no 18.Fuatilia simulizi hii kuanzia mwanzo mpaka mwisho wake kujua na pia ikikugusa LIKE & SHARE ili marafiki zako nao waweze kujifunza.

ANZA NAYO
Ni chumba kilichoonekana kuwa na ukimya, utulivu na giza la kutisha ambalo kila mtu ambaye angethubutu kuingia kwenye chumba kile basi asingethubutu kuiona kesho ya maisha yake.Utulivu wa chumba kile uliwapa watu mbalimbali mashaka na kutaka kujua ni nini kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba hicho lakini watu hawa hawakuishia kutaka kujua kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba kile lakini walienda mbali kidogo na kutaka kujua ni kiumbe gani ambacho kilikuwa kikiiishi ndani ya chumba kile.

Sawa ndani ya chumba hiki binadamu wanaweza wakaishi lakini kwa ukimya na utulivu wa chumba hiki ndicho kitupacho wasiwasi na kujiamini na kujibu kuwa si wanadamu ambao huishi ndani ya chumba hiki.Hatujawahi kuona moshi wa moto hata siku moja ukifuka kutoka ndani ya chumba hiki.Je binadamu hao wasadikikao huishi ndani ya chumba hiki inamaana wanaishi pasipo kula? Hatujawahi kuona hata siku moja chumba hiki kikifunguliwa.Je binadamu hao wasadikikao huishi ndani ya chumba hiki hawashikwi na haja ambayo huweza kuwalazimu waweze kutoka na kuelekea chooni kwa ajili ya kumaliza haja zao hizo? Lakini si hayo tu yanipayo ushujaa wa kusema waishiyo ndani ya chumba hiki si binadamu lakini hata giza lililopo humu ndani huniongezea ujasiri wa kusema waishiyo ndani ya chumba hiki si binadamu.Tazama haijawahi kuonekana taa au mwanga wa aina yoyote ndani ya chumba hiki.Je binadamu wanaweza kuishi kwa muda mrefu wote huo pasipo mwanga? Alimaliza mtu mmoja aliyekuwa jirani wa chumba kile kutoa mashaka juu ya chumba kile no 18.Baada ya kuulizana sana na kutokupata ukweli na kila mmoja kuogopa kukifungua chumba kile no 18 ili waweze kumaliza utata uliyokuwa ukiwasumbua kwa kutambua ni nini kilichokuwepo ndani ya chumba kile watu wale walitawanyika na kila mmoja kuelekea nyumbani kwake.

Chumba no 18 kiliendelea kuumiza akili za watu wengi waliyokuwa wakitathimini na kutaka kujua ukweli wake.Walikuja watafti mbalimbali, walikuja waandishi wa habari mbalimbali lakini hata wageni kutoka sehemu na nchi mbalimbali waliweza kufika na kukizunguka chumba kile na kukitathimini pia.Kuna baadhi ya wageni waliwiwa kutoa msaada kwenye chumba kile no 18 lakini kwakuwa chumba kile hakikuweza kuonyesha ushirikiano na kufanya kiogopwe na kila aliyeweza kufika mahali pale basi hata wageni wale pia waliondoka pasipo kutoa msaada wowote.Waandishi wa habari waliandika habari za chumba kile no 18 na kufanya chumba kile kipate jina kubwa na habari zake kusikika kwenye masikio ya wengi.Je ni nani awezaye kujitosa na kukifungua chumba kile ili wenye moyo wa kusaidia waweze kukisaidia chumba kile hata kwa kuunganisha taa ndani yake na kuondoa giza nene litandalo ndani ya chumba kile?

Siku moja zilisikika kelele zilizoshindwa kutofautishwa na hii ni kutokana na muingiliano wa kelele zile kutoka kwenye chumba kile no 18.Kuna wakati kelele zile zilikuwa zikisikika kama vilio vya watu, kuna wakati zilisikika kama sauti za watu wakilalamika sana kwa kudai ya kuwa walikuwa wakiumizwa na kile kilichokuwa kikiendelea ndani ya chumba kile na kuonekana hakuna aliyejali malalamiko na vilio vile.Wengine wakiwa wanakimbia na silaha mikononi, wengine wakiwa wanakimbia huku kiatu kimoja kikiwa mkononi na kingine mguuni walizidi kusogea kilipokuwepo chumba kile.Sauti za kelele zile zilizidi kuongezeka kwa kupenya kwenye ngoma za masikio ya watu waliyokusanyika mahali pale na sasa iliwezekanika kutofautisha kelele zile na hii ni kutokana na kuwa karibu na chumba kile.

Ndani ya kelele zile kulikuwa na sauti za watoto yatima waliyokuwa wakiwalilia wazazi wao waliyokufa kwa sababu mbalimbali.Kuna baadhi ya wazazi wao waliyapoteza maisha yao katika ajali zilizokuwa zimetokea na nyingi ya ajali hizo kusababishwa na walinzi wa chombo hicho ambao wengi walitekwa na rushwa na kushindwa kutekeleza wajibu wao ipasavyo.Lakini pia kuna baadhi ya wazazi wao walipoteza maisha yao kwa kuwa na dukuduku na majeraha ndani ya mioyo yao na majeraha hayo yakisababishwa na ahadi ambazo waliahidiwa wakati wa ujenzi wa chumba hicho lakini mwisho wa siku kutokutekelezewa ahadi hizo.Tazama wengine walishiriki katika ujenzi wa chumba kile no 18 ambapo walitumia vichwa vyao kubeba ndoo za mchanga, maji na hata mawe ili tu kufanikisha ujenzi ule.

Na kuna kipindi wakati chumba kile kinajengwa kuna burudani mbalimbali zilikuwa zikitolewa na hii ili kukusanya watu kutoka sehemu mbalimbali kuja kushiriki ujenzi wa chumba kile.Wakati burudani hiyo ikitolewa tazama wazazi wa watoto wale yatima walifunga vibwebwe na kuinogesha burudani ile kwa kucheza.Lakini sasa wapo wapi waliyoinogesha burudani ile? Wako wapi waliyoshiriki ujenzi wa chumba kile? Wote walikuwa wameshatangulia mbele ya haki na kuwaacha watoto wao kubaki kwenye vilio vya uchungu na kuishia kuogelea dimbwi la machozi yao wenyewe.Chumba no 18 kuwa na huruma na jaribu kusafisha sikio lako ili uweze kusikia vilio vya watoto hawa yatima.

Si watoto yatima pekee waliyokuwa wakilia ndani ya chumba kile no 18 lakini tazama zilisikika sauti za vilio vya wamama wajawazito ambao nao pia walikuwa wakilia kwa uchungu sana hata baadhi yao sauti zao kukata kabisa.Vilio vya wamama wale wajawazito havikumaanisha kuwa tarehe za kujifungua kwao zilifika laah hasha.Kuna baadhi yao hata mimba zao zilikuwa bado ni changa lakini na wao pia walilia vivyo hivyo.Vilio vya wamama wale wajawazito vilimaanisha kutokuandaliwa mazingira mazuri kwa ajili ya kuvipokea viumbe vilivyokuwa ndani ya matumbo yao.Tazama kabla yao kuna wamama wengi walipoteza maisha kwa ubovu wa mazingira ya kuwapokelea viumbe wao.Kumbukumbu ile iliwafanya wamama wale wajawazito kuendelea kupaza sauti za vilio vyao.Ni nani awezaye kunyamazisha vilio vya wamama wale na kuweza kufuta machozi yao yaliyokuwa yakitiririka mashavuni mwao na kutengeneza mifereji ya machozi juu ya mashavu hayo.

Wakati watoto yatima na wamama wajawazito wakiendelea na vilio vyao juu ya mateso makali waliyokuwa wakiyapata ndani ya chumba kile no 18 kuna baadhi ya kelele za malalamiko yalisika kutokea ndani ya chumba kile pia.Je ni nani aliyekuwa akilalamika kutoka ndani ya chumba kile? Ni sauti za vijana zilisikika wakilalamikia ahadi za uongo ndani ya chumba kile.Vijana waliyoonekana kukata tamaa na maisha na hata baadhi yao kuanza kutumia madawa ya kulevya wakidhania yawezekana ile ndiyo ikawa njia pekee ya wao kupotezea maumivu na mawazo waliyokuwa nayo lakini madawa hayo kuendelea kuwapoteza na kuangamiza nguvu ya chumba no 18.Baadhi ya vijana hao baada ya matumizi ya madawa hayo ya kulevya walijikuta kujiingiza kwenye kazi zisizo halali kama wizi, ukabaji na hata ubakaji.Je nani awezaye kuwaponya vijana hawa?

Lakini si vijana hao tu waliyosikika kulalamikia chumba kile lakini pia kuna baadhi ya vijana walionekana kubeba bahasha zao za kaki mikononi na ndani ya bahasha zile kubeba kitu kisichoweza kujulikana kirahisi na hawa pia walipiga kelele na kukilalamikia chumba kile no 18 kwa madai ya kuwa chumba kile kiliwaahidi mambo mazuri mengi lakini makubaliano yao yalikuwa ni kwamba walitakiwa waende kutoa matongotongo yaliyokuwa yameziba kope za macho yao na baada ya kutoa tongotongo hizo ndipo wangeweza kupewa silaha tayari kwa kuingia vitani.Sasa vijana wale walikuwa washatoa tongotongo zile lakini bado chumba no 18 kilishindwa kuwapatia silaha ili vijana wale waweze kuingia kwenye uwanja wa vita.Je ni nini chumba no 18 kilimaanisha? Chumba no 18 naomba ugeuze hiyo shingo yako inayoonekana kuwa ngumu na safisha tongotongo zitatazo ndani ya kope za macho yako ili uweze kutazama vizuri yale yote uliyokuwa umewaahidi watu wako na ikiwezekana anza kuwatekelezea moja baada ya jingine.Naamini kupitia waraka na barua hii utanielewa na kujirekebisha.Nikutakie kila la kheri katika utekelezaji wa ahadi zako.

MWISHO
Huu ndiyo mwisho wa simulizi hii ya CHUMBA NO 18.Ndani ya simulizi hii unakutana na CHUMBA NO 18 kuvaa nafasi ya uhusika huku watoto yatima, wamama wajawazito na vijana kuvaa uhusika usaidizi.Soma fundisho ili uweze kujua ni nini tumefundishwa na simulizi hii na pia tumia akili ili uweze kung’amua na kujua CHUMBA NO 18 ni kitu gani na ikiwezekana comment jibu lako hapo chini ya simulizi hii.

FUNDISHO
Simulizi hii inatoa mafundisho mbalimbali lakini binafsi nipende kuelezea kwa ufupi funzo la UTEKELEZAJI WA AHADI.Ukisoma vizuri na kwa umakini simulizi hii unatambua kuwa CHUMBA NO 18 kiliweza kutoa ahadi nyingi kwa watu wake lakini kushindwa kutekeleza na kushindwa huko kuna sababisha machafuko, vifo na mateso makali kwa waliyoahidiwa ahadi hiyo.Je CHUMBA NO 18 ni kitu gani?
Ipo njema mkuu
 
Back
Top Bottom