Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Hold on Hold on " please ..ngoja nikapige CHAPUTA kwanza
 
lmfao " Mambo ya Zanzibar hayo'.. binti anatunza bikira ya papuchi lakini ya 0712 marinda kwishnehi mpaka uyapige pasi
 
SEHEMU YA 20

MWANZO nilidhani labda swali lake lilikuwa na maana nyingine zaidi ya vile linavyoweza kueleweka.

Lakini nilipoona uso wa daktari yule ukiwa katika hali ya kungoja jibu la swali lile nikatambua hakuwa na maana nyingine zaidi ya vilevile alivyohoji.

“Unamaana gani kusema hivyo?” “Sina maana yoyote zaidi ya kukuonya tabia ya kumwingilia mkeo kinyume na maumbile,” dokta akaniambia, tena alisema huku akiwa amenikazia macho.

Niliendelea kuchanganyikiwa. Mambo niliyokuwa naelezwa na daktari yule yalikuwa yakiniikoroga akili yangu. Kila kitu kilikuwa ni michoro isiyoeleweka.

Sikuwahi kuwa na michezo ya kishenzi kwa mke wangu, kitendo cha kutuhumiwa kumwingilia mke wangu kinyume na maumbile, ilikuwa ni fedheha mbaya sana.

“Sijawahi kufanya huo mchezo mchafu…” nilimwambia kwa ukali kidogo. “Una uhakika?” “Kabisa dokta, sijawahi kujihusisha na tabia za namna hiyo.” “Basi inawezekana kabla ya kukutana kwenu mkeo alipitia hii michezo,” dokta alinileza.

“Kujihususha na mapenzi kinyume na maumbile?” “Ndiyo,” alitikia kwa kwa upole.

Mate mepesi yakanijaa kinywani. Jambo lile lingewezekanaje wakati mimi ndiyo nilikuwa mwanaume wake wa kwanza?

Nilimkuta akiwa mwanamwali, tena bikira, mshamba kwenye ulimwengu wa mapenzi. “Lakini inawezekanaje hilo dokta? Mimi ndiyo nilikuwa mwanaume wa kwanza.

Nilimkuta akiwa mshamba kabisa kitandani.” nikauliza kwa fadhaa nikitaka ufafanuzi na uthibio juu ya alichonieleza.

“Kweli?” “Ndiyo.” niliitikia huku nikimwangalia usoni.

Alifikiria kitu kisha akasema: “Nimekuwa daktari wa wanawake huu mwaka wa 17, mwanamke anapojifungua, hutokea mara kwa mara kutokwa na haja kubwa, lakini kwa mkeo ilikuwa too much, uzoefu unaonesha mtu wa aina hii amekubuhu kwenye tabia za kuingiliwa kinyume na maumbile,” dokta alinipasha.

Nilijisikia vibaya sana, maneno ya Dk. Charles yalinisuta, yakanifanya nijione bwege. Tafsiri rahisi ni kwamba, maisha ya nyuma ya mke wangu yalikuwa na siri kubwa iliyojificha. “lakini usijali Faraji, siyo kesi sana, haya ni mambo ya kawaida tu maishani, ” daktari aliendelea kunitia moyo, kimuonekano ni kama yeye pia alibaini kwamba jambo lile lilikuwa ‘surprise’ kwangu, na alivyoona
 
Sehemu ya 21

“Ndiyo maana nilipoingia hapa manesi hawakunichangamki, kumbe kulikuwa na kasheshe wakati mke wangu anajifungua!”

“Faraji nikwambie mara ngapi hayo ni mambo madogo, hebu achana nayo na jaribu kusahau.

“Siri kubwa ya kuwa na furaha maishani ni kutokukumbuka mambo mabaya ya nyuma…”alisema, kisha akabadili mada.

“Mkeo amejifungua mtoto wa kiume,” aliniambia akifunua funua makablasha yaliyokuwa mezani.

“Kweli?” “Kwa nini nikudanganye?” “Ahsante dokta, ahsante kwa kumsaidia mke wangu.” “Karibu tena Faraji,” alisema huku akinipa mkono wa pongezi.

Alinipeleka kwenye kitanda alicholala mke wangu na mtoto

Nilipofika nilimkumbatia mke wangu na kumpa pole na pongezi ya kunizalia dume la mbegu.

“Ahsante mume wangu, hongera na wewe pia kwa kunipa mimba,” mke wangu naye alinipa pongezi zilizonifanya nijione kidume.

Wakati wote nilimwonesha uso wa tabasamu, sikupenda kabisa malumbano na mke wangu katika kipindi kile cha uzazi.

Hata Dk. Charles aliendelea kunisihi niachane kabisa na mambo yale ambayo kama ningeyaibua pengine yangepelekea ndoa yangu kuwa matatani.

Nilimuitikia na kumuhakikishia amani ya kudumu kati yangu na Nasra, mwanamke mrembo mwenye asili ya Kipemba, ambaye nilichaguliwa na wazazi wangu kama mke.

Tuliruhusiwa kurudi nyumbani, tukiwa na mtoto mzuri wa kiume, niliwataarifu ndugu na jamaa juu ya kupata mtoto, ilikuwa ni furaha kubwa.

Kwa kuwa mke wangu alikuwa akitakiwa kupata huduma za hapa na pale kama kukandwa maji na kuelekezwa mambo mengine juu ya malezi ya mtoto mchanga, ilibidi mama yangu afunge safari kutoka Nguruka aje Dar es salam kwa ajili ya kufanya kazi hiyo.

Baada ya ujio wa mama, nyumba yangu ikazidi kuwa na furaha, mama alimsadia mke wangu katika kila kitu alichohitaji.

Mtoto naye alizidi kukua, na miezi michache badaye tulimpa jina. Tukamwita Mwanda.

Siku zilikwenda, miezi ikayoyoma. Sakata la mke wangu kuingiliwa kinyume na maumbile niliendelea kuliweka kiporo.
 
SEHEMU YA 22

Kama nilivyosema awali sikupenda kuleta ukizani wowote kati yangu na mke wangu hasa katika nyakati zile.

Furaha, vicheko na tabasamu viliendelea kushamiri katika familia yangu, kwa kweli nilikuwa ni moja ya vijana wachache wanaofaidi matunda ya elimu yangu.

Wazungu wana msemo mmoja unaosema: “It is always the very good times of one’s life that normally turns into one’s very bad times in no time…”

Hii ina maana kwamba kama mtu akiwa katika maisha mabovu hakuna kibovu zaidi kitakachomkuta zaidi ya hicho, lakini akiwa kwenye maisha mazuri ndiyo ataona mabadiliko pale hali hiyo itakapotoweka.

Na kwa kawaida maisha mazuri huwa hayadumu. Wakati nasoma chuo kikuu cha Dar es Salaam msemo huu nilikuwa nauelewa sana.

Ajabu katika nyakati zile nilisahau kabisa juu ya ukweli huu. Wakati nikiwa nimesahau kabisa juu ya falsafa hii ghafla amani ndani ya nyumba yangu ikaanza kutoweka.

Mambo yalianza kama masikhara. Kukawa na mikwaruzano ya hapa na pale kati ya mke wangu na mama yangu mzazi, mama yangu alikuwa akimtuhumu mke wangu kwa tabia ya kupenda sana kuchati na simu kuliko mambo muhimu, wakati mke wangu naye alikuwa akimtuhumu mama kwa tabia ya kupenda kulalamika kwa mambo madogo madogo.

Madai yote hayo, yalipoletwa mbele yangu, niliyapuuza, kwakuwa sikuona kama yanamashiko. Sikujua kama nakosea. Na sikujua kama kwa kupuuza migogoro ile ilikuwa ni mwanzo wa kuingia kwenye historia mbaya sana maishani.

Je nini kilitoke?
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…