SEHEMU YA 11
Nilistushwa na mionzi hafifu ya jua la asubuhi ambalo huwa mara nyingi linapenya chumbani kwangu kupitia dirishani.
Pembeni , mke wangu alikuwa bado akikoroma, saa ilionyesha ilikuwa saa mbili asubuhi, nilipiga miayo ya kivivu, nikajiondoa kitandani.
Nilikuwa mtupu, taswira ya penzi la mwanamwali lilikuwa likijitengeneza upya akilini mwangu. Nilitabasamu na kujiona kidume mwenye bahati kubwa maishani.
Kuwa na mke ambaye hajawahi kuguswa na mwanaume ni ushindi mkubwa kwenye dunia ya leo, nilijiambia kimoyomoyo.
Nilisogea kwenye kioo na kusimama wima, nikaona ukoko wa damu ya Mwanamwali iliyogandana kwenye nyeti zangu, nikatabasamu tena huku moyo wangu ukiwa wenye faraja.
Nilipoyarudisha macho kitandani, Mwanamwali alikuwa bado akiuchapa usingizi.
Niliyatembeza macho pale kitandani, sikuwa nimeona kitu kingine nilichotarajia kukiona, nikasogea karibu zaidi.
Naam! hapo nikaona.
Damu ilikuwa imetapakaa kwenye mashuka meupe, nikajipongeza kimoyomoyo kwa kazi nzuri niliyoifanya usiku wa kuamkia siku hiyo.
Kazi ya kufungua bikira ya mwanamwali. ***** Maisha yangu na mke wangu, yalikuwa ni ya furaha, tulipendana na nilimwamini mno. Kama walivyo wanawake wengine wa Kipemba, Nasra alikuwa ni mwanamke mpole, msikivu na mchamungu.
Angalau hata ile aibu iliilipungua. Kwakweli alikuwa na kila kitu ambacho mwanaume yeyote angetaka mkewe awenacho. Wazungu wanasema ‘Wife material’
Ni miezi sita ilikuwa imepita, mjomba Majeed alikwisha rejea kijijini, katika mji wangu tulikuwa tumebakia watatu, yanii mimi, mke wangu, pamoja shemeji yangu Aisha. Huyu ni yule ndugu wa mke wangu.
Nakumbuka siku moja, baada ya kurudi kutoka kazini, kama kawaida yangu huwa napenda kujituliza nyumbani majira ya saa mbili kwa ajili ya kufuatilia taarifa ya habari katika vituo mbalimbali vya runinga.
Wakati huo mke wangu na nduguye walikuwa wakiendelea na matayarisho ya chakula cha usiku.
Nikiwa pale sebuleni, na rimoti mkononi, nikiwa nahamisha stesheni moja hadi nyingine, mara simu ya mke wangu ilianza kuita. Iliita muda mrefu hadi ikakatika.