Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

Simulizi: Bwana Harusi aliyejeruhiwa

SEHEMU YA 16

Jambo alilonieleza mke wangu, ni jambo hilohilo ambalo nilitaka kulijadili mimi na yeye, katika maelezo yake bado nilikuwa na mambo mengi ambayo ningependa kujua, hivyo kwa kuwa mjadala wa jambo lile ulikuwa mezani nikaona hiyo ni njia pekee ya kufahamu chungu na tamu.

“Umemaliza?” nilimuuliza “Ndio mume wangu.” “ Jambo ulilonieleza, ndilo na mimi nilitaka kulizungumzia, kwa kuwa nilianza kulifahamu kabla hujanieleza…” nilisema.

Mke wangu akashituka, niliendelea kuzungumza. “Maadam jambo hilo ni moja basi hebu tulizungumze…” nilipiga funda moja la juisi, nikaendelea.

“Kwanza kabisa ningependa kujua wewe na mwanamuziki, Abdul Ally umefahamiana naye vipi hadi ukafikia kupewa hilo unaloliita dili?” “Ilikuwa ni kama ajali,” alijibu. “Sijakuelewa” “Nilikutana naye supermarket.”

“Eeh!” “Ndio” “Endelea.” “Nilipokuwa naemea mahitaji ndani ya ile supermarket, alinifuata na kunieleza kwamba amevutiwa na mwonekano wangu, hivyo ingekuwa ni vema kama ningeshiriki kwenye video yake mpya anayotarajia kutoa hivi karibuni.

“Awali nilichukulia kama masikhara. Na nilidhani ni janja tu ya wanaume wa mjini ili aweze kunilaghai kimapenzi, lakini nilipokutana naye tena benki akaniwekea milioni moja kwenye akaunti yangu, ndipo nilipoona mtu yule anamaanisha kile anachosema.”

Mke wangu aliniambia. “Alifanya nini?” “Aliniwekea milioni moja” “Ya nini?” nikauliza kwa ukali “ Eti kama motisha ya kutakafari jambo lake”. “Eeh” “Baada ya hapo amekuwa akinipigia mara kwa mara akitaka kujua nimefikia wapi,” “Kwani ulimpa namba yako?” “Ndio” “Endelea kueleza” nilisema kwa ukali “Mara ya mwisho nilimwambia lazima nimshirikishe mume wangu juu ya jambo hilo, lakini leo ameniambia amenitumia milioni tisa kama sehemu ya malipo ya awali ya mkataba wangu, amefanya hivyo bila kujali kama jambo hili litawezekana ama laa,” mke wangu alisema.

Nilishusha pumzi ndefu, kisha nikamuuliza: “Kazi unayotakiwa kufanya kwenye hiyo kampuni ni ipi?”

JE NINI KILITOKEA?
 
SEHEMU YA 17

“Mara ya mwisho nilimwambia lazima nimshirikishe mume wangu juu ya jambo hilo, lakini leo ameniambia amenitumia milioni tisa kama sehemu ya malipo ya awali ya mkataba wangu, amefanya hivyo bila kujali kama jambo hili litawezekana ama laa,” mke wangu alisema.

Nilishusha pumzi ndefu, kisha nikamuuliza: “Kazi unayotakiwa kufanya kwenye hiyo kampuni ni ipi?” “Kushiriki kwenye video zake kama video Queen…” alinijibu.

“Nini!!...” niliuliza kwa jazba nikiwa nimetoa macho. “Sitaki, nasema staki kabisa kusikia huo upuuzi….” nilipayuka kwa ukali hadi cheche za mate zikanitoka. “Umenielewa wewe?”

“Ndio mume wangu nimekuelewa,” mke wangu akaitikia kwa utii. “Eti uwe video queen, khaa! yule mpuuzi amekuchukuliaje? Anadhani wewe ni kiruka njia kama hao wanawake wengine wanaoacha miili yao uchi huku wakishikwashika hovyo,” niliendelea kuunguruma.

Kwa kweli nilikuwa na wivu mkubwa mno dhidi ya mke wangu, sikuwa tayari kuona mwanamke yule anajihusisha na mambo ya kidunia, hususani masuala ya muziki.

Niliamini wanawake wote wanaojihusisha na sanaa za muziki na unenguaji walikuwa ni viumbe waliokubuhu kwa umalaya. “Hivi mke wangu, unajua kama muziki ni haramu kwa mujibu wa dini yetu,”nikamwambia huku nikiwa nimemkazia macho “Najua mume wangu.”

“Sasa kwa nini unataka kujihusisha na huo uovu?” “Nisamehe mume wangu.” “Nisikilize…”nilisema macho yakiwa yamenitoka pima. “Pesa alizokupa huyo baradhuli mrudishie zote, sitaki kabisa kuona upo karibu na huyo mtu…Sawa” “Nimekusikia mume wangu.” “Sio unisikie tu na unielewe.” “Nimekuelewa Faraji,” mke wangu aliendelea kunijibu kwa utii.

Baada ya hapo tukakubaliana ampigie mwanamuziki yule na amweleze juu ya kujiweka mbali naye na kuacha mazoea ya karibu.

Alichukua simu yake na kumpigia Abdul Ally mwanamuziki wa kizazi kipya. Simu iliita bila kupOkelewa, akapiga tena, iliita muda mfupi badaye ikapokelewa na mwanamuziki yule.

“Mume wangu amekataa na hataki kabisa mazoea na mimi, kwa hiyo naomba usitishe mazoea..Nipe akaunti yako nirejeshe fedha zako,”mke wangu alimpasha simuni Abdul Ally.
 
SEHEMU YA 18

“Kuna nini tena baby, kwanini mumeo anakuwa na swaga za kishamba namna hii, anakukoseshaje dili kubwa kama hivi?”Abdul Ally aliongea kwa lafudhi za vijana wa kileo.

Nilijisikia vibaya sana mtu yule kuniita mshamba mbele ya mke wangu, kwa kuwa simu ilikuwa imewekwa ‘loud speker’ niliichukua kisha tukaanza kutupiana maneno na mwanamuziki yule maarufu.

Tulitukanana matusi ya nguoni hadi simu ilipokatika kwa kuishiwa salio, kwa kweli siku hiyo iligeuka na kuwa siku mbaya mno. ***** Masiku yalikatika, angalau amani na furaha ikaendelea kudumu kwenye ndoa yangu. mawasiliano kati ya mke wangu na Abdul Ally yalikufa.

Mke wangu akazidi kuwa mwaminifu, akawa mchamungu, upendo na heshima dhidi yangu ilikuwa haina mafano, urembo wake ukabakia kuwa mali yangu, nilinenepa, dunia yote ikawa yangu. Miezi michache badaye, mke wangu alinasa ujauzito, jambo hilo lilizidisha furaha kubwa katika ndoa yangu.

Nilifuarahi kuona siku moja ningeitwa baba, sikujali ni mtoto gani angezaliwa, kwangu mtoto wa jinsia yeyote nilikuwa tayari kumpokea kwa mikono miwili.

Niliona siku zinakwenda taratibu, shauku ya kupata mtoto ilikuwa kubwa, mapenzi kwa mke wangu yalizidi maradufu.

Sikupenda hata mara moja kuona mwanamke yule anaingia kwenye mkanganyiko wowote katika nyakati zile za kulea mimba. Siku zilienda, waswahili wanasema ‘ndondo si chururu’ Baada ya kusubiri hatimaye miezi tisa ilitimia.

Usiku mmoja mke wangu alipatwa na uchungu, upesi mimi na mdogo wake Aisha tukamwingiza kwenye gari langu na kumwahisha Hospitali ya Regency.

Baada ya kuwasili, manesi walitupokea mbiombio, kwakuwa hali yake ilikuwa mbaya, alipelekwa moja kwa moja leba.

Mimi na Aisha tuliibakia nje kwenye benchi, mbele ya mlango wa kuingilia katika chumba ambacho mke wangu Nasra aliingizwa.

Tulisubiri pale kwa muda mrefu sana, nakumbuka karibu masaa matatu tulikuwa nje ya wodi ile.
 
SEHEMU YA 19

Daktari alishauri tuondoke na turudi kesho yake kwa kuwa uzalishaji wa mke wangu ilikuwa na mizengwe mingi.

Kauli ya daktari ilinitisha, hata hivyo nilipiga moyo konde na kuondoka kuerejea nyumbani. Usiku ule sikulala, moyo ulikuwa ukinidunda, presha ilikuwa juu.

Siku iliyofuatia. Asubuhi na mapema, niliamka nikajiandaa, kisha nikamwaga shemeji yangu Aisha, nikimtaka yeye aje Hospitalini badaye mchana, baada ya kumaliza shughuli zake asubuhi ile.

Niliendesha gari hadi Posta, kwa kuwa magari yalikuwa machache, muda mfupi badaye nilikuwa Regency. Baada ya kufika manesi walinipokea kwa sura zisizokuwa na chembe ya ukarimu wowote.

Mapigo ya moyo yakaanza kunidunda, nikanza kuhisi heunda kuna jambo baya limetokea dhidi ya mke wangu na mtoto. “Vipi hali ya mke wangu?’ nilimuuliza nesi mmoja.

“Daktari Charles Meleka amesema ukifika tu ukamwone ofisini kwake,” badala ya kujibu swali, nesi yule aliniambia kitu kingine kabisa. “Mke wangu ni mzima?” niliuliza kwa wahaka mapigo ya moyo yakinIenda kasi “Kaka hebu kuwa mwelewa,” nesi alizidi kuwa mkali.

Nikaona nisiendelee kurumbana na yule mwanamke, nilichofanya ni kwenda kwenye ofisi ya dokta Charles Meleka.

Baada ya kuingia ndani ya ofisi ile dokta Cherles alikuwa ameketi katika kiti cha kuzunguka huku mezani kwake kukiwa na mafaili kadhaa.

“Hongera Mr Faraji Hussein…” Dr Charles alianza kunipasha baada ya kuingia. “Mkeo kajifungua mtoto wa kiume tena kajifungua salama kabisa….lakini”

Dr Charles Meleka alisema. “Lakini nini?” nikauliza kwa kiherehere. “Kwanini unafanya mapenzi na mkeo kinyume na maumibile?” Dr Charles Meleka aliniuliza kwa ukali. Nikabaki nimepigwa na bumbuwazi.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom