Simuhitaji tena, ipi dawa yake mwanamke huyu?

Simuhitaji tena, ipi dawa yake mwanamke huyu?

Wewe inaonekana humuitaji ila bado unampenda

Sasa kwani akikutext ukauchuna atakuzoeaje ama atawasilianaje na mtu asiyemjibu
Yaani ana Mu entertain kweli. Wanaume wakikulia ngumu Hata hamu ya kumtumia sms huna.
 
Ww ndio tatizo, inaonesha unapenda msg zake, usimjibu au weka app za kublock text na calls zake. Mwambie aje PM yangu
 
Wakuu habarini;

Kama kichwa kinavyojieleza ni ipi dawa ya mwanamke huyu ambaye ni msumbufu kupita kiasi, ni hivi; nilikuwa naye kwenye mahusiano takribani 1 year lakini tuliachana (nilimwacha) kutokana na tabia zake za michepuko ilikuwa mingi japo alilalamika na kuomba msamaha kuwa hatorudia tena.

Niliamua kukatisha (kupunguza kabisa) mawasiliano ili nimsahau lakini mpaka sasa bado nimsumbufu kila mara WhatsApp ananitext na dhahiri kabisa anachohitaji nikurudisha uhusiano na mimi simwitaji tena.

Ushauri nini nikifanye ili asinizoee kabisa au akatishe mawasiliano na mimi maana simwitaji tena.
Hahaha
 
Back
Top Bottom