mrsleo
JF-Expert Member
- Jan 13, 2014
- 2,588
- 3,886
hivi umeoa? kama hujaoa basi subiri ukiingia kwenye ndoa ndo utaelewa, lakini kame umeoa nazani utaelewa tabia za mtu kwenye ndoa na kabla ya ndoa ni tofauti sana, na mtu kabla hajakuoa unaweza kumrekebisha mana anakuwa na shida na wewe kwahiyo atafanya juu chini kukuridhisha lakini mkishaingia kwenye ndoa wanaume wengi huwa wanaona kama vile ndo mwisho wa jeuri ya mwanamke anaamua kufungua makucha. Alafu usijidanganye kwamba kuwambia ndugu au viongozi wa dini ndo kutamfanya abadilike,Hakuwa na tabia hiyo kabla ya kuoana? Kama alikuwa nayo, usingekubali kuolewa. Kama kabadilika, chukua hatua ya kumwambia yeye, then ndugu au viongozi wa dini, ikishindikana basi uamuzi ni wako ufanye nini. At least ukimweleza mtu, atakuelewa.
NEVER mtu anabadilika kwa kutaka mwenyewe, na elewa jambo moja hapa sijaongelea zile tabia nzito ambazo zitakufanya uende kwa watu kutafuta suluhu, hapana ishu hapa ni vile vitabia vidogo vidogo, kama kutompa mwenzio attention na kutomsikiliza mwenzio unataka kila unachosema wewe kwasababu ni mwanaume basi ndio hivyo, yani kwenye maisha yengu mkeo anakuwa hana nafasi ya kutoa wazo, hata ukimshirikisha jambo unataka akubaliane nawewe tu sio na yeye aongezee lake,
mfano mnajenga, lakini unataka kila kitu kiwe vile unataka wewe, mwanamke aki suggest hata sebule basi iwe hivi hutaki, au mnataka kununua gari, utakalo sema wewe ndio hilo mwanamke akitoa wazo lake unamuona hajui kitu, yan inshort inakuwa kila maamuzi utaka yawe ya vile utakavyo wewe ya mwenzio yote unayaona haya maana, sasa hapa ndo nnaposema kwamba mwanaume vitu kama hivi ataviona vidogo ila trust me kwa mwanamke ni msumari unaomchoma pole pole, mana ataanza ku loose confidence kwasababu anajua akitoa wazo lolote litapingwa
