Simuelewi huyu rafiki yangu

Choosen85

JF-Expert Member
Jun 22, 2022
563
1,364
Wakuu mmebarikiwa.

Iko hivi, kuna kazi nliipata mikoa ya Kanda ya Ziwa na nlitegemea kupata pesa nyingi sana ila kwa bahati mbaya mambo yamekwenda tofauti kabisa.

Wakati nafika huku nilikutana na rafiki yangu ni mchungaji nilimuahidi nikipata pesa hizo nitamsupport kifedha kwenye huduma ya Mungu kwa kweli alifurahi, akawa ananipgia simu kama nisipomtafuta na wakati mwingine hata akiwa kwenye maombi nikipiga simu anapokea faster na kunijuza kwamba anaomba.

Sasa nilipompa taarifa ya ile ambayo nilitegemea kuipata kama vile wahusika wamekuwa wababaishaji aisee yule ndugu ame change naweza mtumia sms na asijibu kabisa na wakati kifurushi anacho, maana naweza mtumia sms kama leo halafu unashangaa kesho yake anapiga simu anasema sms nliiona ila nlijisahau tu kujibu na hii siyo kawaida yake.

Hapa nataka kufuta namba zake tu nimpotezee kabisa, binadamu wengi sana tabia zao ni mtu atakuona wa maana sababu kuna maslahi yake kwako nje hapo ni suala la muda tu.

WAKUU MTU WA NAMNA HII SI NI SAHIHI KUMPOTEZEA TU?
 
Nyie madogo miaka hii hamtumii akili, hamfikirii, hata hamtaki hangaisha bongo zenu kutafuta majibu na majawabu. Hili nalo linakushinda kuamua unataka uamliwe? Sasa wewe utakuwa akili yako unaitumia wapi? Ukioa au kuolewa je?
 
Nyie madogo miaka hii hamtumii akili,hamfikirii, hata hamtaki hangaisha bongo zenu kutafuta majibu na majawabu. Hili nalo linakushinda kuamua unataka uamliwe? Sasa wewe utakuwa akili yako unaitumia wapi? Ukioa au kuolewa je?
Tunatumia akili kutafutia mafaranga. Kuomba ushauri wa kutaka maoni ya watu istafsiriwe n kukosa akili au kutokutumia akili punguza ujuaji ule mema ya MUNGU NA YA WANADAMU.
 
Daah nimechoka sana kwa nyuzi zenu hizi Kalyinda hawaondoki Tanzania watakuja na mguu mwingine tena...
 
Huo ndio mfano wa viongozi wetu wa dini wa siku hizi, pesa mbele, just feel free.
 
Me sioni kama kuna shida. Sàsa ambaye anakutafuta kila siku ili tu avune maslahi kutoka kwako, na ambaye anakutafta pale tu anapokua na shida,

NANI NI MNAFIKI?
potezea tu mkuu. Hilo ni kawaida sana. Hata wewe huwezi ukawa unawapigia simu watu woooote kila siku just tu kuamini ipo siku utaomba msaada kutoka kwao. Inachosha bhna.

Me mtu hata kama huwa hatuwasiliani, akinicheck wakat YUKO na shida fresh tu. NDO MAISHA YALIVYO.
 
Back
Top Bottom