nikamwambia nilishakupa ruhusa ufanye mambo yako lakini mdogo mdogo nisijue sasa mbona imekuwa hivi tena, nikamwambia basi kama vipi wewe endelea naye tu isiwe tabu maana jinsi hii nitakuwa nalia kila siku kitu ambacho sikitaki, akalia sana, akampigia huyo bwana wake na kumwambia kuwa hamtaki hapo mbele yangu, nikamwambia hiyo zuga tu lazima uwasiliane naye tu, kiufupi nikaamua kukata mawasilino naye, lakini sasa amekuwa kero, kila wakati ni simu..sms muda wote, sasa sifahamu anachotaka kwangu ni nini wakati anajua siwezi mpa anachotaka, namshangaa na sijamuelewa nimemuambia endelea na maisha yako!