Simuelewi huyu mwanamke

onetime

JF-Expert Member
Feb 2, 2014
331
234
Kwanza nikiri kuwa mimi ni mwanaume ambaye ni muhanga wa nguvu za kiume, na kutokana na tatizo hilo niliabika mara kadhaa huko nyuma hivyo binafsi nikaamua niwe single mpaka nitakapopata ufumbuzi wa tatizo langu.

Nikiwa katika kusubiri huko ndipo nikakutana na huyu dada ambaye tulikuwa marafiki tu mwanzoni lakini baadae akanifungukia kuwa ananipenda na anataka niwe mpenzi wake, mwanzoni sikumtilia maanani lakini baadaye nilikuja kujua kuwa anamaanisha, nilishindwa kukubali kuwa naye kwa kuhofia kumdissapoint ikabidi nimwambie tu ukweli kuwa nina tatizo a b c, alilia sana siku hiyo kisha akanambia nakupenda hivyo hivyo ulivyo, nikaguna tu nikakausha.

Kiuhalisia sikuweza kumtimizia mahitaji yake ya kimwili hivyo nikatumia tu ujasiri nikamwambia najua wewe ni binadamu na hutokaa hivyo siku zote hivyo ukijisikia genye tafuta mtu akukune lakini nisijue maana itaniuma tu kwa vyovyote, akakataa katakata nikajua tu nadanganywa. Baadaye nikafahamu yupo na mtu nikamuuliza akakubali niliumia sana, narudi.
 
nikamwambia nilishakupa ruhusa ufanye mambo yako lakini mdogo mdogo nisijue sasa mbona imekuwa hivi tena, nikamwambia basi kama vipi wewe endelea naye tu isiwe tabu maana jinsi hii nitakuwa nalia kila siku kitu ambacho sikitaki, akalia sana, akampigia huyo bwana wake na kumwambia kuwa hamtaki hapo mbele yangu, nikamwambia hiyo zuga tu lazima uwasiliane naye tu, kiufupi nikaamua kukata mawasilino naye, lakini sasa amekuwa kero, kila wakati ni simu..sms muda wote, sasa sifahamu anachotaka kwangu ni nini wakati anajua siwezi mpa anachotaka, namshangaa na sijamuelewa nimemuambia endelea na maisha yako!
 
Dah! Inahitaji ujasiri kinoma kukiri udhaifu kama huo. Props for that, man.

Huyo mwanamama kwa namna nilivyosoma, ukiendelea na msimamo wako wa kuachana(which is the best option), atatumia udhaifu wako against you. So, jiandae kutukanwa, vijembe, na kutangaziwa. Take heart, my brother.
 
Dah! Inahitaji ujasiri kinoma kukiri udhaifu kama huo. Props for that, man.

Huyo mwanamama kwa namna nilivyosoma, ukiendelea na msimamo wako wa kuachana(which is the best option), atatumia udhaifu wako against you. So, jiandae kutukanwa, vijembe, na kutangaziwa. Take heart, my brother.
hata sijali, mwache aseme tu atakavyo, nahitaji tu uhuru aache kunisumbua lakini ndo haelewi hata kidogo
 
Back
Top Bottom